Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 418 | 419 | (Page 420) | 421 | 422 | .... | 1904 | newer

  0 0

   Ujumbe wa Watalaamu wa masuala wa ICT, Ulinzi na Ujenzi kutoka Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) uko kwenye ziara ya mafunzo ( Study tour ) katika Mamlaka ya Bandari Ghana (GPHA) ili kubadilishana utaalamu wa namna ya kuongeza ufanisi wa utekelezaji na kuimarisha Ulinzi wa Bandari, ujumbe wa TPA unaongozwa na Ndg. Phares Magesa Mkurugenzi wa ICT - TPA .

  Kwa sasa TPA inatekeleza miradi kadhaa ya kuongeza ufanisi kwa kutumia ICT, kuboresha  Ulinzi kwa kufunga Mitambo ya kielektroniki na kuongeza vifaa na maeneo ya operations ikiwa ni pamoja na upanuzi wa bandari za Dar, Mtwara na Ujenzi wa bandari mpya Bagamoyo na Mwambani Tanga.
   Ujumbe wa TPA ukiongozwa na Ndg. Magesa wakiwa kwenye mazungumzo na wenyeji wao kutoka Mamlaka ya Bandari ya Ghana kufanya majumuisho ya ziara .
    Watalaamu wa TPA wakiwa kwenye chumba Chenye vifaa vya kielektroniki Cha kuangalia matukio ya kuilinzi na ki usalama katika Bandari ya Tema
  Watalaamu wa TPA toka idara za Ujenzi, TEHAMA na Ulinzi wakiangalia Ujenzi wa Magati manne ya kisasa katika Bandari ya Tema , Ghana
  Watalaamu wa TPA wakiangalia lango la kuingia bandarini ambazo lina vifaa maalumu vya ki electronic vya kutambua magari, makasha na dereva bila kusimamia.


  0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Injinia Binilith Satano Mahenge  (wa kwanza kushoto) na Naibu Waziri  Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu (wa pili kushoto), wakisikiliza kwa makini ripoti ya maoni inayohusu mabadiliko ya Tabianchi itakayowasilishwa huko Peru hivi karibuni ,ikitolewa na  Uester Kibona ambaye ni mwenyekiti wa Asasi isiyo ya Kiserikali inayojihusisha na Mabadiliko ya Tabianchi na Mazingira  (FORUM CC).
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Injinia Binilith Satano Mahenge (wa kwanza kushoto), akipokea ripoti ya maoni inayohusu mabadiliko ya Tabianchi kutoka kwa Uester Kibona ambaye ni mwenyekiti wa Asasi isiyo ya Kiserikali inayojihusisha na Mabadiliko ya Tabianchi na Mazingira (FORUM CC).
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira Mheshimiwa Dkt. Injinia Binilith Satano Mahenge (wa kwanza kushoto) pamoja na  Naibu Waziri  Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu (wa tatu kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi kutoka Asasi isiyo ya kiserikali inayojihusisha na Mabadiliko ya Tabianchi na Mazingira  (FORUM CC).

  0 0
 • 12/04/14--00:23: THE NIGHT OF KINGS DAR LIVE

 • Anza kuzichanga sasa, jiji zima kuhamia Mbagala Dar Live!

  0 0

  Maandamano ya washiriki wa hafla ya Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP. Maandamano ya washiriki wa hafla ya Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP.Msanii Christian Bella akiwatumbuiza washiriki katika Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP jijini Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yameandaliwa na TGNP Mtandao. Msanii Christian Bella akiwatumbuiza washiriki katika Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP jijini Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yameandaliwa na TGNP Mtandao.Mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP, Katibu Mtendaji Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora –Tanzania, Bi. Mary Massay akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa eneo la kula kiapo kwa washiriki kupinga ukatili. Mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP, Katibu Mtendaji Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora –Tanzania, Bi. Mary Massay akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa eneo la kula kiapo kwa washiriki kupinga ukatili.Mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP, Katibu Mtendaji Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora –Tanzania, Bi. Mary Massay akizindua eneo la kula kiapo kwa washiriki kupinga ukatili. Mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP, Katibu Mtendaji Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora –Tanzania, Bi. Mary Massay akizindua eneo la kula kiapo kwa washiriki kupinga ukatili.Mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP, Katibu Mtendaji Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora –Tanzania, Bi. Mary Massay akiweka saini kama ishara ya kukubali kupiga vita ukatili. Mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP, Katibu Mtendaji Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora –Tanzania, Bi. Mary Massay akiweka saini kama ishara ya kukubali kupiga vita ukatili.
  Mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP, Katibu Mtendaji Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora –Tanzania, Bi. Mary Massay akiweka saini kama ishara ya kukubali kupiga vita ukatili. Mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP, Katibu Mtendaji Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora –Tanzania, Bi. Mary Massay akiweka saini kama ishara ya kukubali kupiga vita ukatili.Mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP, Katibu Mtendaji Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora –Tanzania, Bi. Mary Massay akizungumza. 
  Mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP, Katibu Mtendaji Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora –Tanzania, Bi. Mary Massay akizungumzaKaimu Mkurugenzi wa TGNP Mtandao, Bi. Lilian Liundi akizungumza katika Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP. Kaimu Mkurugenzi wa TGNP Mtandao, Bi. Lilian Liundi akizungumza katika Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP.[/caption] [caption id="attachment_53707" align="aligncenter" width="640"]Kaimu Mkurugenzi wa TGNP Mtandao, Bi. Lilian Liundi akizungumza katika Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP. Kaimu Mkurugenzi wa TGNP Mtandao, Bi. Lilian Liundi akizungumza katika Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP.[/caption] [caption id="attachment_53712" align="aligncenter" width="640"]Maandamano ya washiriki wa hafla ya Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP. Maandamano ya washiriki wa hafla ya Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP.[/caption] [caption id="attachment_53710" align="aligncenter" width="640"]Maandamano ya washiriki wa hafla ya Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP. Maandamano ya washiriki wa hafla ya Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP.[/caption] [caption id="attachment_53709" align="aligncenter" width="640"]Mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP, Katibu Mtendaji Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora –Tanzania, Bi. Mary Massay na Kaimu Mkurugenzi wa TGNP Mtandao, Bi. Lilian Liundi pamoja na meza kuu wakipokea maandamano ya washiriki hao kabla ya kuanza kwa Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP. Mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP, Katibu Mtendaji Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora –Tanzania, Bi. Mary Massay na Kaimu Mkurugenzi wa TGNP Mtandao, Bi. Lilian Liundi pamoja na meza kuu wakipokea maandamano ya washiriki hao kabla ya kuanza kwa Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP.[/caption] [caption id="attachment_53708" align="aligncenter" width="640"]Baadhi ya washiriki katika hafla ya Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP, wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa katika hafla hiyo. Baadhi ya washiriki katika hafla ya Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP, wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa katika hafla hiyo.[/caption] [caption id="attachment_53705" align="aligncenter" width="640"]Baadhi ya washiriki katika hafla ya Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP, wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa katika hafla hiyo. Baadhi ya washiriki katika hafla ya Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP, wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa katika hafla hiyo.[/caption] [caption id="attachment_53700" align="aligncenter" width="640"]Baadhi ya washiriki katika hafla ya Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP, wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa katika hafla hiyo. Baadhi ya washiriki katika hafla ya Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP, wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa katika hafla hiyo.[/caption] [caption id="attachment_53704" align="aligncenter" width="640"]Moja ya vikundi vya sanaa vikuwaburudisha washiriki wa Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP jijini Dar es Salaam. Moja ya vikundi vya sanaa vikuwaburudisha washiriki wa Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_53703" align="aligncenter" width="640"]Mada mbalimbali zikiwasilishwa katika Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP, Katibu Mtendaji Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora –Tanzania, Bi. Mary Massay akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa eneo la kula kiapo kwa washiriki kupinga ukatili. Mada mbalimbali zikiwasilishwa katika Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP, Katibu Mtendaji Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora –Tanzania, Bi. Mary Massay akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa eneo la kula kiapo kwa washiriki kupinga ukatili.[/caption] [caption id="attachment_53702" align="aligncenter" width="640"]Mada mbalimbali zikiwasilishwa katika Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP, Katibu Mtendaji Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora –Tanzania, Bi. Mary Massay akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa eneo la kula kiapo kwa washiriki kupinga ukatili. Mada mbalimbali zikiwasilishwa katika Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP, Katibu Mtendaji Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora –Tanzania, Bi. Mary Massay akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa eneo la kula kiapo kwa washiriki kupinga ukatili.[/caption] [caption id="attachment_53701" align="aligncenter" width="640"]Baadhi ya washiriki katika hafla ya Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP, wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa katika hafla hiyo. Baadhi ya washiriki katika hafla ya Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP, wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa katika hafla hiyo.[/caption] [caption id="attachment_53686" align="aligncenter" width="640"]Msanii Christian Bella (katikati) akiwatumbuiza washiriki katika Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP jijini Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yameandaliwa na TGNP Mtandao. Msanii Christian Bella (katikati) akiwatumbuiza washiriki katika Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP jijini Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yameandaliwa na TGNP Mtandao.[/caption] [caption id="attachment_53687" align="aligncenter" width="640"]Msanii Christian Bella (kushoto) akicheza na MC Scholar kutoka TGNP katika Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP jijini Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yameandaliwa na TGNP Mtandao. Msanii Christian Bella (kushoto) akicheza na MC Scholar kutoka TGNP katika Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP jijini Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yameandaliwa na TGNP Mtandao.[/caption] [caption id="attachment_53688" align="aligncenter" width="480"]Msanii Christian Bella (kushoto) akicheza na MC Scholar kutoka TGNP katika Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP jijini Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yameandaliwa na TGNP Mtandao. Msanii Christian Bella (kushoto) akicheza na MC Scholar kutoka TGNP katika Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP jijini Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yameandaliwa na TGNP Mtandao.[/caption] [caption id="attachment_53690" align="aligncenter" width="640"]Moja ya vikundi vya maigizo vikuwaburudisha washiriki wa Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP jijini Dar es Salaam. Moja ya vikundi vya maigizo vikuwaburudisha washiriki wa Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_53685" align="aligncenter" width="640"]Msanii Christian Bella akiwatumbuiza washiriki katika Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP jijini Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yameandaliwa na TGNP Mtandao. Msanii Christian Bella akiwatumbuiza washiriki katika Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP jijini Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yameandaliwa na TGNP Mtandao.[/caption] [caption id="attachment_53698" align="aligncenter" width="480"]Burudani kwa washiriki.... 
  Burudani kwa washiriki...Msanii Christian Bella (kushoto) akicheza na MC Scholar kutoka TGNP katika Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP jijini Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yameandaliwa na TGNP Mtandao. Msanii Christian Bella (kushoto) akicheza na MC Scholar kutoka TGNP katika Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP jijini Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yameandaliwa na TGNP Mtandao.Msanii Christian Bella akiwatumbuiza washiriki katika Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP jijini Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yameandaliwa na TGNP Mtandao. 
  Msanii Christian Bella akiwatumbuiza washiriki katika Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia TGNP jijini Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yameandaliwa na TGNP Mtandao.

  0 0

  Mkurugenzi wa Shirika la Utunzaji wa Mazingira WWF Tanzania Bw. Bell’Aube Houinato akielezea malengo ya Shirika hilo, ambayo pamoja na mambo mengine ni kuhakikisha ulinzi wa viumbe hai na misitu izingatiwe ili kulinda mazingira na kuinua uchumi wa taifa.
  Meneja Uhifadhi wa Shirika la Utunzaji wa Mazingira WWF Tanzania, Dr. Amani Ngusaru ,akizungumza na wahariri na waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari mbalimbali katika semina ilioandaliwa na (WWF) iliofanyika Disemba 2-3, 2014 mkoani Morogoro juu ya utunzaji wa mazingira ili kuleta uwiano sawa wa rasilimali zinazopatikana maeneo mbalimbali nchini.  0 0

  Nianze kuliandikia hili kwa kuonyesha furaha yangu kuwa huwenda sasa kumekua na uelewa juu ya maswala ya usalama mitandao. Nalisema hili kutokana na uhalisia kwamba Jana nilipata maswali kutoka kwa watu wengi sana huku nikipata jumbe nyingi zilizofanana zikielezea juu ya tukio la benk ya NBC kuingiliwa na wadukuzi.

  Wengi walinitaka pia nielezee huku nikiulizwa mbona hakuna nilichozungumza. Nilifarijika sana kwani muda uliopita wengi hawakua wakihoji juu ya maswala ya udukuzi pamoja na usalama mitandao na huwenda hii ilitokana na kutokua na uelewa wa maswala husika.

  NINI HASA KILITOKEA?

  Kwanza kabisa Kulikua na Itlafu ya Umeme ambayo ilisababisha baadhi ya Mashine kuzima.

  Pili, Kulitokea Tahadhari ya Moto iliyosababisha wafanyakazi kuchuukua tahadhari ya kutoka nje.

  Na Tatu, Mifumo ya Mobile banking (Inayotoa huduma za miamala kupitia simu za kiganjani) kushindwa kufanya kazi yake ipasavyo iliyo sababisha kutoa kiwango kisicho sawa kwa waliokua wakiangalia salio.

  Matukio haya matatu yaliunganishwa na kutengeneza taarifa moja iliyo sambazwa kua kuna mdukuzi aliingilia banki ya NBC na kusababisha mifumo kutofanya kazi na hatimae kuhamisha kiasi kikubwa  cha pesa. Kitu ambapo kilipelekea wafanya kazi kutoka nje ili uchunguzi zaidi uweze kufanywa.

  Na anaepata taarifa anapo angalia salio anaona kunatatizo katika kiasi chake na kuamini jumbe ile. Panapotoka ufafanuzi wa taarifa hii wengi bado wanahoji bado kuna shaka niendelee kutoa ufafanuzi nini hasa kinaweza kikawa kimesababisha?


  0 0

  Umoja wa wamiliki magari ya mizigo TATOA umewapa pole wamiliki wa magari, madereva na wafanya biashara wanaosafirisha mizigo kuelekea Kongo DRC kufuatia ajali ya moto iliyotokea takribani wiki mbili zilizopita katika Yadi ya Whiski iliyoko jirani na mpaka wa Kasumbalesa katika nchi ya Demokrasia ya watu wa Kongo na kusababisha vifo na uharibifu wa mali.  

  ‘TATOA inatoa pole kwa familia na waathirika wote wa janga hili la moto kutoka nchi za Tanzania, Zambia, Zimbabwe, Congo na Afrika Kusini, na pia kipekee TATOA inapenda kutoa shukrani kwa serikali ya Congo kwa juhudi zao za kuhakikisha hali ya amani boda na kazi kuendelea pamoja na taratibu mpya za kiusalama walizochukua’ alisema msemaji wa TATOA, Bwana Elias Lukumay. 

  Akielezea chanzo cha moto huo, bwana Lukumay alisema taarifa za awali zinaonyesha mlipuko huo ulitokea baada ya gari la mafuta  kukwaruza gari jingine hivyo kupata nyufa katika Tanki lake la mafuta  hali iliyosabababisha mafuta kuvuja na kutapakaa katika eneo la Yadi na baadaye kushika moto.

  ‘Tatizo la msingi ni kuwa yadi ya Whiski haikuwa na vifaa vya kupambana na moto, na hivyo tunaziomba serikali zetu zinazosimamia vituo vya mipakani kujifunza kutokea kwenye tatizo hili na hivyo kuchukua hatua stahiki kuboresha huduma kwenye yadi hizo’ alisisitiza Lukumay.

  Bwana Lukumay pia alisema TATOA imetuma timu ya wataalam kwenda Lubumbashi kuangalia upana wa maafa, huku pia IKITOA wito kwa makampuni mwanachama wa TATOA kutoa taarifa kuhusiana na maafa waliyoyapata.

  TATOA, ingependa kuona inapata ushirikiano wa karibu kutoka upande wa serikali, ili kwa pamoja tujipange na tuweze kufanya maandalizi ili janga kama hili lisije tokea kwenye boda zetu zote siku zijazo’ alisema Lukumay.

  TATOA pia imeiomba mamlaka ya barabara Tanzania (TANROADS) kupunguza usumbufu usio wa lazima kwa malori katika maeneo ya mizani hasa katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka ambapo bandari yetu imejaa mizigo mingi ya nchi jirani.  0 0


  0 0

  1

  WaziriMkuu, MizengoPinda akisalimiana na Mbunifu wa kimataifa wa Mavazi, Sheria Ngowi alipotembelewa jana nyumbani kwake Masaki jijini Dar esSalaam. (Picha Zote: AtuzaNkurlu-SheriaNgowi Brand).
  2
  Mbunifu wa kimataifa wa Mavazi, Sheria Ngowi akimuonesha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda baadhi ya vitambaa vya kisasa vya suti ambavyo vitatuka Kumtengenezea Waziri Mkuu jana jijini Dar es Salaam.
  3
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiangalia na kuchagua aina ya vitambaa vya suti amabvyo vitatumika kutengenza baadhi ya Suti Zake alipotembelewa na Mbunifu wa Kimataifa wa Mavazi, Sheria Ngowi jana jijini Dar es Salaam.(Picha Zote: Atuza Nkurlu-Sheria Ngowi Brand).

  0 0

  Baada ya kukosekana mvua kwa muda mrefu katika maeneo yanayozunguka Mlima Kilimanjaro kutokana na uharibifu wa mazingira ikiwa ni pamoja na ukataji wa mitim, hali ya zamani imeanza kurejea.
  Kurejea kwa hali hiyo kumetokana na jitihada za mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama pamoja na Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) ,kushiriki katika utunzaji wa mazingira kwa kuzuia wananchi walioishi jirani na maeneo yanayozunguka mlima Kilimanjaro kuingia katika eneo la nusu maili kufanya uharibifu katika misitu ya asili,Mito iliyokuwa imekauka sasa imeanza kutirisha maji kama ilivyokuwa zamani.
  Kina mama ambao awali walilazimika kuingia ndani ya Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) kwa ajili ya ukatajai wa majani kwa ajili ya mifugo yao ,sasa hivi hali ni tofauti wamekuwa wakikata majani waliyootesha wenyewe na kustawi kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika maene hayo ,na sasa hawaingii tena katika hifadhi ya taifa ya mlima Kilimanjaro kukata majani.
  Majani kwa ajili ya mifugo kwa sasa yanapatikana na hata afya sasa imeanza kurejea tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
  Mmoja wa wafugaji Ludovick Meela Serik akifurahia hali ya upatikanaji wa majani kwa ajili ya mifugo yake ilivyo sasa.
  Kina mama ambao wamekuwa wakijishughulisha na kilimo cha Mboga mboga wamekuwa wakifanya biashara vizuri kutokana na upatikanaji wa mboga ambazo kwa sasa zimekuwa zikipatikana kwa wingi tofauti na hapo awali ambapo wamekuwa wakisafirisha mboga hizo hadi nchi jirani ya Kenya.
  Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la FLORESTA Bw. Richard Mhina akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) namna ambavyo shirika lake lilivyo saidia vikundi mbalimbali katika kampeni za utunzaji Mazngira kwa kuotesha miti pamoja na uanzishwaji wa vitalu vya miti.
  Na Dixon Busagaga wa Globu 
  ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  0 0

  Kada wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro,Olivia Sanare (Mwenye kofia) akiwa amesaidiwa na vijana wenzake wa CCM kubeba zawadi mbalimbali kwa ajili ya watoto  yatima na wale waishio katika mazingira magumu wa kituo cha Kili Center.
  Kada wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro,Olivia Sanare akikabidhi zawadi kwa watoto wa kituo cha Kili Center ikiwa ni sehemu ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.
  Makada mbalimbali wa CCM mkoa wa Kilimanjaro wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wa kituo cha Kili Center baada ya kumsindikiza mwenzao Olivia Sanare aliyekuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.
  Kada wa CCM,Olivia Sanare akizungumza na watoto waishio katika mazingira magumu wa kituo cha Kili Center alipotembelea kituo hicho kutoa zawadi kwa watoto wa kituo hicho.
  Watoto wa kituo cha Kili Center wakimuimba wimbo wa Birthday,kada wa CCM mkoa wa Kilimanjaro Olivia Sanare aliyevaa kofia. 
  Kada wa CCM ,Olivia akisakata Kwaito na watoto wa kituo cha Kili Center.
  Watoto wa kituo cha Kili Center wakitoa burudani ya Kuch kuch Hota Hae kwa wageni waliowatembelea  kituoni hapo.
  Kada  wa CCM ,Olivia akila chakula pamoja na watoto wa kituo cha Kili Center ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu yake ya siku ya kuzaliwa.
  Olivia akiwa amebeba watoto katika kituo cha Kili Center mara baada ya kuwatembelea na kuwapatia zawadi.Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya kaskazini,

  0 0

  Watanzania wana matarajio mengi kuhusu maisha yao ya baadaye
  Wananchi wanamatumaini kuwa nchi itakuwa yenye uchumi wa kati ifikapo 2025

  4 Desemba 2014, Dar es Salaam: Zaidi ya nusu ya wananchi (54%) wanafikiri kuwa maisha yao yatakuwa bora zaidi ifikapo mwaka 2025. Huu ndio mtazamo wa wananchi wakio katika makundi yote- vijana kwa wazee, wanaume kwa wanawake, na wakazi wa vijijini na mijini. Mtazamo huu ni tofauti kabisa na ule wa nchi za Marekani na Ulaya ambapo karibu wananchi saba kati ya kumi (65%) wanafikiri kuwa watoto wao watakuwa na hali mbaya zaidi kifedha kuliko walivyo wao sasa.

  Matokeo haya yametolewa na Twaweza na Society for International Development (SID) kwenye muhtasari wa utafiti wenye jina la Tanzania ifikapo mwaka 2025: Je, Watanzania wana matarajio gani na maisha yao ya baadaye? Muhtasari umetokana na takwimu za Sauti za Wananchi, utafiti wa kwanza barani Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaofanyika kwa njia ya simu za mkononi. Utafiti huu hufanyika katika maeneo yote Tanzania Bara (Zanzibar haimo kwenye matokeo haya). Matokeo haya yametokana na takwimu zilizokusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,408 mwezi Agosti 2014.

  Wakiangalia nchi kwa ujumla, wananchi wawili kati ya watatu wanaamini kuwa Tanzania itakuwa mahali pazuri pa kuishi mwaka 2025. Wananchi makundi yote bila kujali hali zao za kiuchumi wanaamini hivyo; mathalan, wananchi wenye kipato kikubwa 64% na wananchi maskini 68% wana matumaini na siku zijazo. Watanzania wana matumaini na akiba tuliyonayo kwa ajili ya nchi.

  Hata hivyo, baadhi ya wananchi bado wana wasiwasi. Karibu mwananchi mmoja kati ya watano (18%) wanahofia maisha yako yatakuwa mabaya zaidi mwaka 2025 kuliko yalivyo leo, na wapo wengine wanaodhani nchi itakuwa mahali pabaya pa kuishi mwaka 2025. Hapa kuna baadhi ya tofauti kati ya matajiri na maskini, mwananchi mmoja kati ya wanne katika kundi la matajiri (25%) na mmoja kati ya watano katika kundi la maskini (18%) hawana matumaini kuhusu siku zijazo.

  Haijalishi mtazamo gani wananchi wanao, bado wanaamini kuwa matokeo na mustakabali wa Tanzania uko mikononi mwa Watanzania. Wananchi tisa kati ya kumi wanaamini kuwa viongozi wa Tanzania (54%) au wananchi (37%) watakuwa na udhibiti zaidi wa maamuzi ya nchi yao. Linapokuja suala la maisha yao wenyewe, wananchi wanaamini jitihada zao wenyewe kuwa ndizo zitazobadilisha maisha yao; wananchi sita kati ya kumi wanafikiri kuwa wao wenyewe ndio wenye ushawishi zaidi juu ya hatma yao ya baadaye. Hata hivyo, wakati mwananchi mmoja kati ya watano anaamini kuwa Serikali itakuwa na ushawishi mkubwa juu ya ustawi wa maisha yao ya baadaye, hakuna mwananchi wa mjini aliyetaja Serikali kama ina ushawishi muhimu. Mbali na wao wenyewe, wahojiwa wa mijini walitaja familia zao (20%) na marafiki au wenzao (19%) kuwa wenye ushawishi juu ya maisha yao ya baadaye.

  Ukiangalia kila jambo moja baada ya jingine, karibu wananchi watatu kati ya wanne (72%) wanaamini kuwa Tanzania itakuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo 2025. Wananchi saba kati ya kumi (68%) pia wanafikiri kutakuwa na Rais mwanamke ifikapo mwaka 2025, na wananchi sita kati ya kumi (64%) wanatabiri kukua kwa uzalishaji wa viwanda na kupungua kwa kilimo. Kwa upande mwingine, wananchi wengi wanatabiri kutokea migogoro ya kidini (62%) na nusu yao (51%) wanatarajia kugawanyika kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Chochote kitakachotokea huko mbeleni, wananchi wanaona mabadiliko makubwa, wananchi sita kati ya kumi wanatabiri kuwa upinzani utashinda urais, na tembo watapotea kabisa ifikapo 2025. Jambo la kushangaza, matukio mawili yenye uwezekano mdogo kutokea ni Tanzania kufuzu kushiriki mashindano ya Kombe la Dunia (38% ) na kuanzishwa kwa Shirikisho la Afrika Mashariki chini ya Rais mmoja (34%).

  Mambo muhimu wanayotaka wananchi kwa siku zijazo ni maboresho kwenye huduma za kijamii (28% wanaona ni kipaumbele chao muhimu) na ukuaji wa uchumi (16% wanaona ni kipaumbele muhimu).

  Aidan Eyakuze, Mkurugenzi wa shirika la Society for International Development, alitoa maoni yake kwenye matokeo haya "Watanzania kwa kiasi kikubwa wana matumaini na maisha yao binafsi ya baadaye, hasa ikilinganishwa na wenzao kutoka nchi zenye maendeleo makubwa kiuchumi, Marekani na Ulaya. Matumaini haya na mtazamo chanya ni mtaji mkubwa. Vinaimarisha uwezo wa nchi kusonga mbele kwa kujiamini na pia inaweka mzigo kwa kila mmoja wetu kuhakikisha kuwa tunafikia malengo ya mafanikio kwa nchi yetu."

  Rakesh Rajani, Mkuu wa Twaweza, alisema "Katika kipindi cha mabadiliko muhimu ya kitaifa na ya kimataifa, wananchi wa matabaka yote kiuchumi, maeneo na jinsia zote, wana matumaini kuhusu kile kilichopo siku za mbeleni nchini Tanzania. Changamoto kwa Serikali ya Tanzania, wasomi wa ndani pamoja na wananchi wenyewe, ni kuhakikisha kuwa matumaini haya yanaendelezwa kupitia utungaji sera na utekelezaji wenye ufanisi, kuhimiza maendeleo yenye usawa na kujenga mshikamano wa kijamii, ili matarajio ya wananchi ya maisha bora siku zijazo yafikiwe."

  0 0

   Mashabiki wakiwa uwanjani Nangwanda Sijaona wakifatilia mechi ya soka kati ya Mtwara na Maziwa.
   Matalena Muhagama mkimbiaji kutoka Bandari ya Dar es Salaam akiwa mbele ya wakimbiaji wengine wakati wa michezo ya Bandari ‘Inter-Ports Games’ inayoendelea mjini Mtwara.
   Suleiman Mwalilo a.k.a Kingsley kutoka Bandari ya Dar es Salaam akikata upepo katika michezo ya Bandari ‘Inter-Ports Games’
   Damian Mkobokwa wa timu ya Makao Makuu na wenzake wakianza mchezo wa kupokezana vijiti.
   Mrusha mkuki Ally Mnubi kutoka Bandari ya Dar es Salaam akijiandaa kurusha mkuki.

   Mrusha mkuki, Mathias Shija kutoka Bandari za Maziwa akijaribu kete yake katika mchezo huo.
   Mrusha mkuki kutoka Bandari Dar es Salaam akijaribu kete yake katika mchezo huo.

   Wachezaji wa timu za Bandari Maziwa na Mtwara wakiwa katika mtanange ambao ulivuta hisia za mashabiki wa mjini Mtwara

  0 0

  Bw. Peragius  Cosmas mwanafunzi aliyehitimu shahada ya Uhasibu na kupata  GPA 4.91 akipokea cheti cha pongezi kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha CBE Prof.Emanuel Mjema.
  Bi. May Issa  mwanafunzi aliyehitimu shahada ya kwanza ya Usimamizi wa manunuzi  na kupata  GPA 4.92 Akipokea cheti cha pongezi kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha CBE Prof.Emanuel Mjema.

  Kwa kile ambacho kimeonekana ni tishio kwa chuo cha Elimu ya Biashara (CBE)  wanafunzi hawa  kutoka kampasi ya Dodoma  wameweza kupata ufaulu mkubwa katika masomo yao.

   Bi. May Issa  Mwanafunzi  aliyehitimu shahada yake ya kwanza ya Usimamizi wa  Manunuzi  katika mahafali ya 49 ya chuo cha Elimu ya Biashara CBE Dodoma mwaka 2014 ametangazwa  kuwa mwanafunzi wa kwanza aliyeongoza kwa ufaulu kwa kupata GPA ya  4.92. ambapo  aliweza kupata alama  A  28 , alama  B+ tatu  na  alama  B  moja  kati ya masomo  32  ya shahada yake ya kwanza  ya  Usimamizi wa manunuzi akifuatiwa na  Bw. Peragius Cosmas  aliyepata GPA ya 4.91.

   Kwa upande  wake Mwanafunzi mwingine  Bw, Peragius Cosmas  aliye kuwa akisoma Shahada ya kwanza ya Uhasibu   yeye pia alionyesha maajabu kwa kuweza kupata GPA ya  4.91  ambapo aliweza kupata alama  A  29 na  alama  B+ tatu    kati ya masomo  32  ya shahada yake ya kwanza  ya  uhasibu.

  Hivi  karibuni katika Chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM)  pia tulishuhudia  Msichana   Doreen Kabuche aki ]ongoza kwa ufaulu UDSM kwa kuwa  Mhitimu bora wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2014, Doreen Kabuche alitangazwa kuwa kinara kwa ufaulu kwa kupata alama A 32 na B+ sita kati ya masomo 38 ya shahada ya Takwimu Bima (Actuarial Science). Kwa alama hizo, Doreen alipata wastani wa alama za ufaulu (GPA) 4.8 na kuacha alama ya 0.2 ili kufikia kiwango cha juu kabisa cha ufaulu cha alama tano.   Bi. May  Issa akionekana mwenye furaha siku ya mahafali  ya 49 iliyofanyika hivi karibuni katika chuo cha Elimu ya biashara kampasi  ya Dodoma.
  Bw. Peragius Cosmas akionekamna mwenye furaha  katika mahafali ya  49 ya  chuo cha CBE iliyofanyika hivi karibuni katika  Chuo cha Elimu ya Biashara kampasi ya Dodoma.
    Rais mstaafu wa Serikali ya Wanafunzi CBE  kampasi ya Dodoma 2013/2014 Bw. Remidius Emmanuel (kulia) akimpongeza  Bi. May  Issa kwa kufanya vizuri katika  masomo yake  kwa kipindi chote cha masomo yake.  0 0

   Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Stephen Kilindo,(kushoto), akimkabidhi Kamanda Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Mohammed Mpinga. Ripoti ya Upimaji wa afya za madereva, wakati wa Wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani iliyofanyika Novemba 22 hadi 28 katika vituo vya mikese, mkoaniMorogoro. Makabidhiano hayo yalifanyika Dar es Salaam juzi.
    Kamanda Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Mohammed Mpinga. akitoa shukrani kwa TBL baada ya kukabidhiwa  Ripoti ya Upimaji wa afya za madereva,
   Mganga Mkuu wa Polisi akisoma ripoti hiyo.

  0 0


  0 0

  Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji Huduma za Usafi wa nchi kavu na Majini, Dk Oscar Kikoyo akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es salaam leo kuhusu ya hali ya usafiri kipindi cha siku kuu za Krismas na mwaka mpya ambapo ametahadharishja abiria kuto kukubali kutozwa nauri za juu na pindi ikitokea hivyo Sumatra ipewe taarifa haraka.  Soma taarifa kamili hapa chini. Source Father Kidevu Blog.

  NAURI HALALI ZA MABASI YA MIKOANI

  0 0

   Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (kushoto) akisaini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu kwa serikali ya Tanzania kwa niaba ya Serikali ya Tanzania leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Saudia Mhandisi Hassan Al-Attas.
   Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (kushoto) akibadilishana hati ya  mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu kwa serikali ya Tanzania waliosaini kwa niaba ya Serikali ya Tanzania leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Saudia Mhandisi Hassan Al-Attas.
   Baadhi ya waandishi wa habari na watumishi wa wizara ya Fedha pamoja na wawakilishi wa Serikali ya Saudi Arabia wakiwashuhudia Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Saudia Mhandisi Hassan Al-Attas wakisaini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu kwa serikali ya Tanzania leo jijini Dar es salaam.(Picha zote na Eleuteri Mangi- Maelezo)
   
  Eleuteri Mangi- MAELEZO
  04/12/2014
  Serikali ya Tanzania imesainiana  mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa zaidi ya  shilingi bilioni 45.2 na Shirika la Maendeleo la Saudia kwa lengo la kuboresha miradi wa maji kwa wilaya ya Same, Mwanga na ujenzi na ukarabati wa barabara Visiwani Zanzibar.

  Mkataba huo umesainiwa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Saudia Mhandisi Hassan Al-Attas.

  Akiongea na waandishi wa habari katika hafla hiyo, Waziri Saada alisema kuwa kati ya mkopo huo shilingi bilioni 41.25 ambazo ni sawa na Dola za Kimarekani milioni 25 zitagharimia mradi wa maji katika wilaya za Same na Mwanga na  shilingi bilioni 3.96 kwa ajili ya maradi wa barabara Pemba, visiwani Zanzibar.

  Waziri Saada alilishukuru Shirika la Maendeleo la Saudia kwa jitihada zao za kuisaidia Serikali ya Tanzania katika kautatua tatizo la maji wilaya za Same na Mwanga pamoja na uboreshaji wa barabara katika visiwa vya Pemba.
   
  Aidha, mradi wa maji wa Same- Mwanga utagharimu Dola za Kimarekani milioni 110.34 ambazo benki ya BADEA, Shirika la Maendeleo Kuweit, OPEC na mashirika mengine wamekubali kukamilisha sehemu ya fedha iliyobakia.

  Mradi wa maji wa Same- Mwanga baada ya kukamilika utasaidia kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji vijijini amabapo utasaida kuboresha hali ya maisha wa wananchi wa maeneo hayo, upatikanaji nwa maji safi na salama kwa maendeleo ya afya za wakazi hao na kuboresha uchumi wao kwa kutumia muda mwingi kwa shuighuli za uzalishaji mali badala ya kutumia muda mwingi kutafuta maji.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Saudia Mhandisi Hassan Al-Attas amesema kuwa makataba waliosaini leo unaonesha kuwa Saudi Arabia iko mstari wa mbele katika kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Tanzania katika kukuza uchumi wake kwa kuzingatia mahusiano mazuri yaliyopo kati ya nchi hizo.

  Hafla hiyo ilihudhuriwa waandishi wa habari na baadhi ya watumishi wa wizara ya Fedha na wawakilishi wa Serikali ya Saudi Arabia.
  Mwisho

  0 0

   Makamu wa Rais wa Bunge la Ulaya (EP), Rainer Wieland akizungumza jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar, Salum Mwalimu na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (BAVICHA), Patrobas Katambi. Ujumbe wa CHADEMA ukiongozwa na mwanadiplomasia mahiri Profesa Abdalla Safari, uko nchini Ubelgiji kwa ziara ya kikazi kufuatia mwaliko wa bunge hilo.
  Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Profesa Safari Abdalla akisalimiana na Makamu wa Rais wa Bunge la Ulaya (EP) Rainer Wieland wakati ujumbe wa CHADEMA ulioko nchini Ubelgiji, ulipofika ofisi za bunge hilo mjini Brussels kwa ajili ya ziara ya kikazi. Wengine kutoka kulia ni Mwenyekiti wa BAVICHA, Patrobas Katambi, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu, Katibu Mkuu wa BAWACHA, Grace Tendega na Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri John Mrema.
   Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demoikrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Profesa Abdalla Safari na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar, Salum Mwalimu wakiwa kwenye mazungumzo na Makamu wa Rais wa Bunge la Ulaya (EP), Rainer Wieland, wakati ujumbe wa CHADEMA ulipofika Ofisi za EP kuanza ziara ya kikazi kufuatia mwaliko wa bunge hilo.
  Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Profesa Abdalla Jumbe Safari akiwa na Makamu wa Rais wa Bunge la Ulaya (EP), Rainer Wieland, walipokutana jana mjini Brussels, Ubelgiji kwa mazungumzo, ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi ya ujumbe wa CHADEMA kufuatia mwaliko wa bunge hilo.

  0 0

   Mratibu wa mafunzo ya mfumo wa ukusanyaji taarifa za Afya (D.H.I.S) Suleiman Salum  Ali  akieleza mafanikio  ya mafunzo hayo  yaliyofanyika Hoteli ya Double Tree Nungwi, wa kwanza (kulia) ni Profesa Kristin Braa kutoka Chuo Kikuu cha Oslo ambao ni waandaaji wa mafunzo hayo kwa kushirikiana  na Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Wizara ya Afya Zanzibar. (kati) ni Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo aliefunga mafunzo hayo. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo zanzibar)
   Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akimkabidhi cheti mmoja ya washiriki wa mafunzo ya D.H.I.S  Osama Al Zubair  kutoka Sudan wakati wa kufunga mafunzo hayo katika Hoteli ya Double Tree Nungwi, Kaskazini Unguja.
   Mgeni rasmi katika ufungaji wa mafunzo ya D.H.I.S Mahmoud Thabit Kombo akiwahutubia washiriki wa mafunzo hayo kutoka Nchi za Afrika, Marekani, Ujerumani na Mashirika wahisani katika Hoteli ya Double Tree Nungwi.
   Washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo alipokuwa akiyafunga mafunzo ya siku 10 yaliyofanyika Hoteli ya Double Tree Nungwi.
   Mratibu wa mafunzo ya mfumo wa ukusanyaji taarifa za Afya Suleiman Salum Ali akizungumza na waandishi wa Habari walioshiriki ufungaji wa mafunzo hayo katika Hoteli ya Double Tree Nungwi.
   Picha ya pamoja ya washiriki wa mafunzo ya mfumo wa ukusanyaji taarifa za Afya (D.H.I.S) wakiwa na mgeni rasmi katika kufunga mafunzo hayo Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo katika Hoteli ya Double Tree Nungwi. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo zanzibar).

older | 1 | .... | 418 | 419 | (Page 420) | 421 | 422 | .... | 1904 | newer