Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46379 articles
Browse latest View live

UHURU MARATHON 2014 YADHAMINIWA NA STAR TIMES

$
0
0
Mratibu wa Uhurumarathon Innocent Melleck akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam wakati akielezea juu ya udhamini wa kampuni ya startimes kudhamini kwa kutoa matangazo na vifaa vyenye Zaidi ya shilingi milioni nne na laki tano.Kushoto kwake ni meneja huduma kwa wateja wa startimes Jackson Ngowi

RAIS KIKWETE AMUAPISHA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI PROFESA MUSA JUMA ASSAD LEO

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho kikwete katika picha ya pamoja na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Musa Juma Assad  na wafanyakazi wa ofisi ya CAG  Ikulu jijini Dar es salaam leo
 Rais Jakaya Mrisho kikwete akiwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa  Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Musa Juma Assad na CAG Mstaafu Bw. Ludovick Utouh Ikulu jijini Dar es salaam leo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

CLOUDS FM YASHEREHEKEA KUTIMIZA MIAKA 15 TANGU KUANZISHWA KWAKE.

$
0
0
Mmoja wa Watangazaji machachari wa Clouds FM,Adam Mchomvu akitoa muongozo mfupi kwa baadhi ya Wafanyakazi wenzake waliomzunguka,kuhusiana na ukataji na ulaji wa Ndafu kama ionekavyo pichani,wakati wa hafla ya kutimiza miaka 15 ya kituo cha redio ya Clouds FM,tangu kuanzishwa kwake nchini.Redio hiyo imejizolea umaarufu mkubwa Afrika Mashariki na Kati na Duniani kwa ujumla.

Globu ya Jamii inaitakia kheri na fanaka Clouds FM katika kusherehekea miaka 15 tangu kuzaliwa kwake.
 Ndafu wa shughuli akiwa mezani
 Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi Ruge Mutahaba akilishwa kipande cha Ndafu na mtangazaji wa kipindi cha XXL,Dj Fetty,huku miluzi na shangwe za hapa na pale zikiwa zimetawala mjengoni humo,Mikocheni jijini Dar
 Msanii mkongwe wa Muziki wa kizazi kipya,Prof Jay akilishwa kipande cha ndafu,wakati wa hafla ya muendelezo wa redio hiyo kutimiza miaka 15 tangu kuanzishwa kwake nchini.
 Mkuu wa Vipidi wa Clouds FM,Sebastian Maganga akishukuru jambo kwa baadhi ya Wafanyakazi wenzake mara baada ya kulishwa keki na Mtangazaji wa kipindi cha XXL,Dj Fetty.
 Dj Mkongwe ndani ya Clouds FM,Dj Venture akilishwa keki kwenye hafla hiyo ya kutimizwa miaka 15 ya kituo hicho maarufu cha redio hapa nchini na kwingineko.
 Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa kizazi kipya,Banana Zorro akihojiwa mambo kadhaa kuhusiana na hafla ya muendelezo wa kituo hicho cha redio kutimiza miaka 15 tangu kuanzishwa kwake nchini.

watanzania shime tumpigie kura Idris Sultan ashinde Big Brother Afrika/ Vote Idris Sultan to win Big Brother Africa

$
0
0

Watanzania tuungane na kumchagua mwenzetu Idris Sultan aweze shinda mashindano ya Big Brother Africa.Wiki hii ndio wiki ya mwisho na kinyang'anyori ni kikali kweli .Ila Idris ana nafasi nzuri ya kushinda
tukimpigia kura.Ameweza kuonyesha ni mtu mwenye vipaji lukuki na kuweza kwenda mbali kwa vipaji alivyonavyo

 Mpe kura yako kwa  kupiga

 1.Kura ya bure kupitia mtandao na simu mara 100 bila gharama
yoyote.Unachohitaji ni kuweka namba yako kwenye link ya DSTV na
ku-press Idris mara 100 .Pitia hapa

 haichukui zaidi ya dakika tano

 2.Download  WeChat app kwenye smartphone yako, ongeza ID
BigBrotherAfrica na  piga kura mara 100 bure !

 3.Tuma sms Vote Idris kwenda namba 15426 kupitia mitandao yote
Tanzania.Unaweza fanya hivyo hata kwa mara 100 kwa siku haina noma!

 4.Sehemu nyingine Africa tuma sms Vote Idris kwenda 2783142100414 mara 100

 Asanteni

How to Vote

1.Vote for free up to 100 times on the website and again up to 100
times on the mobile site

     FIRST register here
     https://connect.dstv.com/4.0.863/en-ZA/Login/?returnUrl=http%3A%2F%2Fbigbrotherafrica.dstv.com%2Fvote

     It will take you 5 minutes only to send 100 free votes to Idris
2.Download the WeChat app on your smartphone, add ID BigBrotherAfrica
and vote up to 100 times  FOR FREE !

3.In Tanzania through sms " VOTE Idris" and send to 15426  Vote up to
100 times by SMS (Vodacom,tiGO,Zantel,Airtel).You are charged Tsh 600
only

4.In Rest of Africa sms " VOTE Idris " and send to 2783142100414  Vote
up to 100 times by SMS

Msimu wa pili wa tamthilia Siri ya Mtungi Wazinduliwa, kuonekana TBC

$
0
0
 Mtayarishaji wa tamthilia ya Siri ya Mtungi  Louise Kamin kutoka  Shirika Lisilo la Kiserikali la  Media for Development International Tanzania (MFDI-TZ) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na msimu wa pili na wa mwisho wa tamthilia hiyo. Kutoka kulia kwa Kamin ni Karabani (Muongozaji), Cheche (Muigizaji), Jordan Riber (Muongozaji). Kutoka kushoto ni Goldliver Gordian (cheusi) na David Michael (Duma).
 Cheche akizungumza katika mkutano huo.
 Muongozaji wa tamthilia hiyo, Karabani akisisitiza jambo katika mkutano huo.
Muongozaji , Jordan Riber akifafanua jambo katika mkutano huo.


Msimu wa pili wa tamthilia ya Siri ya Mtungi itazinduliwa rasmi Desemba 7 kupitia televisheni ya Taifa (TBC). Akizungumza jijini leo mtayarishaji wa tamthilia hiyo, Louise Kamin kutoka Shirika Lisilo la Kiserikali la Media for Development International Tanzania (MFDI-TZ) alisema kuwa sehemu ya pili ya tamthilia hii inakamilisha Siri ya Mtungi kufuatia msisimko mkubwa wa msimu wa kwanza. 

Kamin alisema kuwa kukamilika kwa hatua ya pili kunatokana na udhamini mnono wa the John Hopkins University Centre for Communication Programs (JHU CCP) ambao walitoa uongozi wa elimu na mkakati katika tamthilia, taasisi ya Misaada ya Wamarekani kupitia (Usaid), Wizara ya Afya Ustawi wa Jamii na MFDI. Alisema kuwa sehemu hii ndiyo inatoa majibu ya msimu wa kwanza na kuwataka mashabiki watamthilia hii kuangalia TBC kuanza saa 12.30 jioni kupitia TBC. 

“Msimu wa kwanza wa tamthilia ya Siri ya Mtungi uliwavutia watu wengi wa ukanda wa Afrika Mashariki na kuwaachia maswali kibao na hii imetokana na tamthilia kubeba vionjo halisi vya maisha katika jamii na hasa kwa wakazi wa mikoa ya Pwani ya Tanzania,” alisema Kamin. 

Alisema kuwa mapokeo mazuri kutoka kwa watazamaji kuliwapa nafasi ya kuingia katika vipengele saba vya tuzo za M-Net Africa Magic Viewers Choice Awards mwaka 2014 ambavyo ni TV Series, Make Up, Wardrobe, Art Direction, Sound Editor, Acting, and Indigenous Language Series.

 “Msimu wa kwanza ulikuwa hewani katika vipindi vya miaka miwili tangu mwezi Desemba mwaka jana kupitia vituo vya televisheni vya ITV/EATV na baadaye kurushwa hewani kupitia DTV, TV1, MNet Africa Magic, Maisha Magic kabla ya msimu huu kupitia televisheni ya TBC,” alisema. 

Kwa mujibu wa Kamin, mpaka sasa wanajivunia kupata mapokeo mazuri kwenye mitandao ya kijamii na hasa facebook kwa kupata mashabiki 200,000 na kwenye YouTube ambapo tumepata watazamaji zaidi ya 500,000 kwani tamthilia hii imepata umaarufu mkubwa kwa kutazamwa na mashabiki wengi kuliko vipindi mbali mbali vya televisheni hapa nchini na ukanda wa Afrika Mashariki. 

Alisema kuwa Siri ya Mtungi ni hadithi ya Kitanzania ambapo wametumia siku 86 kukamilisha kurekodi. Alisema mbali ya kuwashirikisha waigizaji maarufu kama yvonne Cherie maarufu kwa jina la Monalisa, pia imewashirikisha warembo maarufu kutoka Miss Tanzania kama Richa Adhia na Jokate Mwegelo.  “Tumetoa ajira kwa waigizaji 60 ambao walipatikana baada ya mchujo wa watu 2,500,” alisema.

WAJASIRIAMALI WAELEZEA WALIVYOWEZESHWA NA PROMOSHENI YA SAFARI LAGER WEZESHWA YA TBL

$
0
0
 Jacquline Shija Mazemle, aliyewezeshwa na TBL na kufanikiwa kuanzisha mghahawa maarufu wa FACEBOOK, ulioko karibu na Chuo Kikuu cha Kampala, Gongo la Mboto, Dar es Salaam.
Akiandaa chakula na wenzake Ramadhan Seleman kushoto na Hans Shija
 Akiwahudumia na wateja wa Facebook
 Dorren Asey aliyewezeshwa na TBL kutengeneza mikate, keki na maandazi kupitia kampuni yake ya Dee Bakery,Doreen akiandaa mikate.

 Doreen akiandaa mikate
 Dorren akionyesha mashine ya zamani


 Dorren kulia na msaidizi wake Ali Chares


 Dorren Assei akionesha moja ya majiko ya kuokea mikate
 Hapa ndio Facebook
 Jacquline Shija akielezea kuhusu mafanikio yake baada ya kuwezeshwa na Safari Lager Wezeshwa

UKIMWI OPHANS yawakaribisha kwenye Fundraising Jumamosi hii

GARI INAUZWA

$
0
0
Gari  aina ya Nadia type SU
MWAKA  2001
IMETEMBEA KILOMETER ELFU KUMI TANZANIA
AC INAFANYAKAZ
LIMU ZA SPORTS
INA SECURITY ALARM
INA RATHER SEATS
ENGINE TYPE 3 S
Acc   2000
KWA MAWASILIANO PIGA NAMBA 0783101670
 


WANABIAFRA WASHIRIKI KATIKA UZINDUZI WA MRADI WA KUHAMASISHA MICHEZO KWA VIJANA NA WATOTO

$
0
0
Baraza la Michezo la Taifa (BMT) chini ya udhamini wa taasisi ya UK Sports - Internationa Inspiration iliandaa mafunzo uhamasishaji wa michezo kwa vijana na watoto. Mafunzo hayo yaliyofanyika katika uwanja wa taifa yaliwakutanisha pamoja makatibu tawala pamoja na maafisa michezo toka katika wilaya zote nchini. Mafunzo hayo pia yalifanyika ikiwa ni sehemu ya Mkutano Mkuu wa Mwaka wa wa baraza la Michezo Tanzania uliofanyika katika uwanja wa Taifa wa Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Sihaba Mkinga, wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Makatibu Wakuu na Wenyeviti wa Kamati za Michezo za Mikoa Tanzania, uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. (picha kwa hisani ya Hivi Sasa Blog).

Baada ya mafunzo hayo, sherehe  rasmi ya uzinduzi wa kampeni ya Inspire Tanzania ilifanyika tarehe 20 September, 2014 katika uwanja wa taifa. Sherehe hiyo ilitanguliwa na mazoezi ya mbio za pole pole (jogging) ambayo yaliratibiwa na klabu ya michezo ya Biafra pamoja na vilabu vingine vya jogging katika mkoa wa Dar es Salaam ambavyo Temeke Jogging, Faita, Jogging, Kopa Jogging, n.k.

CHADEMA NA KAMPENI SERIKALI ZA MITAA MKONI RUKWA

$
0
0
 Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar, Salum Mwalimu akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Kisumba, Jimbo la Kalambo, mkoani Rukwa, katika mfululizo wa mikutano ya ziara ya Operesheni Delete CCM katika vijiji vya mkoa huo
 Naibu akikumbatiana na mzee ambaye alikuwa mmoja wa wasikilizaji kwenye mkutano wa Operesheni Delete CCM uliofanyika katika Kijiji cha Samazi, mkoani Rukwa. Mzee huyo ambaye alitokwa na machozi wakati akisikiliza hotuba, alisema kuwa aliguswa sana na maneno ya Mwalimu.
 Naibu Katibu Mkuu akiagana na wananchi wa kijiji cha Kisumba baada ya mkutano huo wa hadhara kijijini hapo.
Naibu Katibu mkuu na msafara wake wakishiriki chakula walichoandaliwa na wenyeji wao katika Kijiji cha Samazi Jimbo la Kalambo, baada ya mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo ikiwa ni mwendelezo wa mikutano mfululizo wa Operesheni Delete CCM mkoani Rukwa.

INTRODUCING NEW TRACK-WEMA NI AKIBA YA JENNIFER MGENDI

BENKI YA CRDB YASAINI MKATABA WA HALI BORA ZA WAFANYAKAZI WAKE

$
0
0
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (katikati) akisaini mkataba wa hali bora za wafanyaka wa benki hiyo na Katibu Mkuu Msaidizi wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Fedha, Viwanda, Biashara, Huduma na Ushauri (TUICO), Shikunzi John.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia) akisaini mkataba wa hali bora za wafanyaka na Katibu Mkuu Msaidizi wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Fedha, Viwanda, Biashara, Huduma na Ushauri (TUICO), Shikunzi John (wa pili kulia).
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (wa pili kulia) na Katibu Mkuu Msaidizi wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Fedha, Viwanda, Biashara, Huduma na Ushauri (TUICO), Shikunzi John, wakibadilishana hati ya Mkataba wa Hali Bora za Wafanyakazi wa benki hiyo na TUICO jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia) na Katibu Mkuu Msaidizi wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Fedha, Viwanda, Biashara, Huduma na Ushauri (TUICO), Shikunzi John, wakibadilishana hati ya Mkataba wa Hali Bora za Wafanyakazi kati ya Chama hicho na Benki ya CRDB jijini Dar es Salaam.   

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza wakati wa uwekaji saini wa Mkataba wa Hali Bora za Wafanyakazi na Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Fedha, Viwanda, Biashara, Huduma na Ushauri (TUICO) uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Dorah Ngaliga na Katibu wa Benki, John Rugambo. 
 Baadhi ya maofisa wa CRDB wakiwa katika mkutano huo.
 Katibu Mkuu Msaidizi wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Fedha, Viwanda, Biashara, Huduma na Ushauri (TUICO),
Shikunzi John akizungumza katika hafla hiyo. Kulia ni
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Dorah Ngaliga, Katibu wa Benki, John Rugambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei.


Na Mwandishi Wetu

BENKI ya CRDB na imetiliana saini mkataba na Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Fedha, Viwanda, Huduma na Biashara (TUICO) wa kuboresha hali bora za wafanyakazi wa benki hiyo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, alisema mafanikio yoyote ya kibiashara hayapatikani kama wafanyakazi ambao ndio wazalishaji hwatakuwa na mazingira yenye maslahi bora na motisha mbalimbali.

Dk. Kimei alisema nia ya CRDB ni kuboresha mahusiano kati ya mwajiri na wafanyakazi, kuboresha mazingiraya utendaji kazi ili kuchochea ufanisi, kurasimisha mahusiano kati ya benki na wafanyakazi kwa kuweka miongozo itakayosaidia kupunguza mifarakano kati ya CRDB na wafanyakazi.

“Mkataba huu ni wa miaka mitatu, utasaidia kuajiri na uthibitishwaji wa wafanyakazi kazini, kushughulikia migogoro ya kikazi, uhamisho wa viongozi wa chama cha wafanyakazi sehemu ya kazi,utaratibu wa likizo ya uzazi, likizo ya ugonjwa, ulipwaji gharama ya usafirishaji mizigo kwa wafanyakazi wanaohamishwa, mazishi ya wazazi wa wafanyakazi, bima na utoaji tuzo,”alisema  
Aidha alisema

UWEZO WA VYUO VIKUU KUCHUKUA WANAFUNZI WA SAYANSI BADO CHANGAMOTO KWA TANZANIA KUTIMIZA MALENGO YA EFA

$
0
0
DSC_0341
Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi nchini Tanzania Mh. Dkt. Shukuru Kawambwa akifungua mkutano wa kimataifa wa kutathmini mafanikio na changamoto za utekelezaji wa malengo ya Mpango wa Kimataifa wa Elimu kwa Wote-EFA uliofanyika jijini Dar Es Salaam ambapo amesema tangu mwaka 2000 Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuelekea kutimiza malengo ya Mpango huo ikiwa ni utashi wa kisiasa na kuwajibika vikisaidiwa na kujitolea kwa wadau wa sekta ya elimu pamoja na washirika wa maendeleo.(Picha na Zainul Mzige wa MOblog).

Tanzania imekuwa moja wapo ya nchi za kutolea mfano miongoni mwa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara katika kutekeleza maazimio ya mpango wa Elimu kwa wote (EFA).Akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa wadau wote wa elimu , Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi nchini Tanzania Mh. Dkt. Shukuru Kawambwa amesema Tanzania Bara na Visiwani imeweza kukaribia kufikia malengo ya mpango huo ikiwa ni pamoja na suala la wastani wa waalimu kwa wanafunzi.

Amesema kwamba kwa shule za msingi Tanzania Bara imefikia wastani wa wanafunzi 47 kwa mwalimu mmoja wakati Visiwani Zanzibar ni wastani wa mwalimu mmoja kwa wanafunzi 27. Mafanikio mengine yaliyopatikana chini ya mpango huo ni kuboresha wastani wa wanafunzi kwa darasa, ambapo kwa Tanzania Bara wastani umetoka kuwa wanafunzi 92 kwa darasa na sasa ni wanafunzi 65 huku Zanzibar wastani ukiwa ni wanafunzi 62 kwa darasa.
DSC_0288
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues akizungumza wakati wa mkutano wa kimataifa wa kutathmini mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika kutekeleza malengo ya Mpango wa Kimataifa wa Elimu kwa Wote –EFA ulioshirikisha wadau wote wa sekta ya elimu uliofanyika jijini Dar Es Salaam. Amesema lengo kuu la mkutano huo ni kuiandaa Tanzania kuweza kushiriki kikamilifu katika mashauriano ya kiserikali baina nchi mbalimbali na kuhakikisha wadau wakuu wa elimu kitaifa wanapata taarifa juu ya mapendekezo ya agenda zitakazoanza mwaka 2015.

Awali Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues amesema ikumbukwe kwamba malengo nane (8) ya EFA yanachangia kufanikisha Malengo Makuu ya Maendeleo ya Millennia (MGDs) yaliyopitishwa mwaka 2000 kati ya nchi 189 na Taasisi za Mendeleo zinazoongoza Duniani.

Bi. Rodrigues amefafanua kuwa tunapoelekea mwaka 2015, Tanzania Bara na Visiwani zimeonyesha juhudi katika kupunguza tofauti kubwa zilizokuwepo kielimu ikiwa ni pamoja na kukabilia na changamoto zilizojitokeza na kuweza kuweka sera, mipango na utawala bora katia Nyanja za fedha , wadau, usimamizi na uwajibikaji.

DSC_0224
Pichani juu na chini ni sehemu ya wadau wa elimu kutoka bara na visiwani wakifuatilia hotuba za viongozi wakati wa mkutano wa kimataifa wa kutathmini mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika kutekeleza malengo ya Mpango wa Kimataifa wa Elimu kwa Wote –EFA.

Katika mkutano huo imeelezwa kwa sasa hakuna tatizo la uwiano wa wanafunzi wa kike na wa kiume kwa kuwa jinsia zote zipo darasani katika uwiano unaoridhisha unaokaribia wastani wa 50/50, lakini pia kigezo kingine ni uwiano wa idadi ya wanafunzi wanaojiunga na sekondari ambapo bado kumeonyesha kuwa na mapungufu hivyo kazi ya ziada inahitajika.

Mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam ulikuwa na nia ya kutoa fursa kwa nchi wahusika kujitathimini zimefikia wapi katika utekelezaji wa malengo waliyojiweke ya Mpango wa Elimu kwa Wote-EFA kwa kipindi cha mwaka 2000 hadi 2015 na kujiwekea mikakati mipya.
DSC_0280DSC_0470DSC_0236DSC_0364DSC_0489
Kamishna wa Elimu kutoka Wizarani, Prof. Eustella Bhalalusesa (wa pili kushoto) akitoa maoni juu changamoto zinazolikabili taifa katika kuleta uwiano kwenye ya sekta elimu.
DSC_0476
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues akishea uzoefu wake katika utekelezaji wa malengo ya EFA baina ya Tanzania na nchi zingine za Afrika.
DSC_0371
DSC_0491
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Maalim Abdallah M. Abdallah (kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues wakati wa mkutano huo. Kushoto ni Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi nchini Tanzania Mh. Dkt. Shukuru Kawambwa.
DSC_0501
Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi nchini Tanzania, Mh. Dkt. Shukuru Kawambwa akifurahi jambo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues baada ya kumalizika kwa mkutano huo.
DSC_0505
Mkurugenzi wa ofisi ya elimu kutoka Shirika la USAID, Bw. David Bruns (kushoto) akibadilishana mawazo na Waziri Kawambwa (katikati) na Bi. Zulmira Rodrigues.
DSC_0512
Afisa Miradi Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO, Myoung Su Ko akiteta jambo na Afisa mipango ya Elimu wa Shirika la UNESCO, Bi. Jennifer Kotta.
DSC_0457
Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi nchini Tanzania Mh. Dkt. Shukuru Kawambwa, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na nafasi ya Tanzania ilipofikia tangu 2000-2015 katika utelekezaji wa malengo ya EFA.
DSC_0429
Afisa mipango ya Elimu wa Shirika la UNESCO, Bi. Jennifer Kotta akizungumza na waandishi wa habari juu ya umuhimu wa mkutano huo baina ya UNESCO na Wizara katika kutathmini utelekezaji wa malengo ya EFA katika kipindi cha miaka 15 na kutoa nafasi ya kujipanga kwa awamu nyingine itakayoanza 2015-2030.KAWAIDA

Bodi ya Filamu Tanzania yaifagilia tamthilia ya Siri ya Mtungi

$
0
0

Bodi ya Filamu Tanzania imewataka waandaaji wengine wa fani hiyo kuiga mfano wa waandaaji wa tamthilia ya Siri ya Mtungi, Shirika Lisilo la Kiserikali (NGO ya Media for Development International Tanzania (MFDI-TZ) kwa kutoa filamu yenye mafundisho mbali ya kuburudisha.
 
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fissoo kupitia kwa mwakilishi wake, Beatrice Sumari kwenye ukumbi wa Cinemax Century wakati wa uzinduzi rasmi uliowashirikisha wadau wa fani hiyo, wadhamini na waandaaji.
 
Sumari alisema kuwa Tamthilia ya Siri ya Mtungi Msimu wa Pili mbali ya kuburudisha, pia imetoa ajira kwa Watanzania wengi, pia imeleta changamoto kuhusiana na mabadiliko ya tabia kwa jamii.“Filamu imetengenezwa kwa ubora wa hali ya juu, hii ni fursa kwa wadau wa fani hiyo kuiga MFDI-Tanzania kwa kuleta katika jamii filamu yenye ubora huu, naomba wengine wafuate nyayo zao,” alisema  Sumari.
 
“Filamu hiyo ina ubora  wa picha, sauti, maudhui na mfuatano wa matukio wa kipekee na kuleta burudani ya aina yake.. ni tamthilia ambayo ukianza kuangalia, hauta kinai na kuwa na hamu ya kufuatilia kile kinachofuata,” alisema.Afisa kutoka Taasisi ya Misaada ya Wamarekani kupitia (Usaid), Ana Bodipo alisema kuwa wanajisikia furaha kudhamini tamthilia hiyo ambayo imezungumzia maisha halisi ya Mtanzania.
 
Bodipo alisema kuwa alisema kuwa tamthilia hiyo inaelekeza jamii kuhusiana na ugonjwa hatari wa Ukimwi na kwa wao ni moja ya nyenzo ya kushiriki katika masuala ya afya katika maeneo mbalimbali nchini.
 
“Matukio mengi katika tamthilia hii yana akisi taswira ya kweli katika jamii na na kuwafanya wafuatiliaji kupata somo halisi kutokana na changamoto mbalimbali,” alisema Bodipo.Mtayarishaji wa tamthilia hiyo, Louise Kamin kutoka taasisi ya Media for Development International Tanzania (MFDI-TZ) alisema kuwa wamefuraishwa na mapokeo ya tamthilia hiyo pamoja na kuhitimisha na kufichua kilichopo katika mtungini.
 
alisema kuwa sehemu ya pili ya tamthilia hii inakamilisha Siri ya Mtungi kufuatia msisimko mkubwa wa msimu wa kwanza.Kamin alisema kuwa kukamilika kwa hatua ya pili kunatokana na udhamini mnono wa the John Hopkins University Centre for Communication Programs (JHU CCP) ambao walitoa uongozi wa elimu na mkakati katika tamthilia, taasisi ya Misaada ya Wamarekani kupitia (Usaid), Wizara ya Afya Ustawi wa Jamii na MFDI.

MATUKIO PICHANI

$
0
0
 Picha ya pamoja
 Naibu Mtendaji Mkuu wa Benki M, Bi. Jacqueline Woiso (kushoto), akijaribu kumvika Joho la Heshima, Mwakilishi wa Kampuni ya Tanga Fresh, Bw. Douglas Kakere, wakati wa chakula cha usiku kupongeza makampuni 100 ya kati, Dar es Salaam juzi.
  Naibu Mtendaji Mkuu wa Benki M, Bi. Jacqueline Woiso (wa tatu kushoto), akikadhi Tuzo maalumu kwa mwakilishi wa Kampuni ya Tanga Fresh, Bw. Douglas Makere, baada ya kumvika Joho la heshima kutambua mchango wa kampuni hiyo, wakati wa chakula cha usiku kilichoandaliwa kwa ajili ya kuyapongeza makampuni 100 ya kati, Dar es Salaam juzi. Kulia ni Ofisa wa Kampuni hiyo, Bw. Protas Kimario.
 Meneja Biashara wa Benki ya Afrika (BOA), Bw. Solomon Haule (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari, kabla ya kuchezesha mchezo wa bahati nasibu kwa wateja wa benki hiyo, Dar es Salaam jana. Wengine ni Mkuu wa Mawasiliano, Bw. Willington Munyanga na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha, Bw. Bakari Maggid (kulia).

MAHAKAMA YA TANZANIA YAKUTANA NA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI (JUDICIAR MEDIA FORUM) KUJADILI JUU YA MISINGI BORA YA UPASHANAJI HABARI KATIKA UTENDAJI BAINA YA TAASISI HIZO MBILI

$
0
0
Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania (wa nne kushoto), Mhe. Shaaban Lila, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania (wa pili kulia), Bw. Kajubi Mukajanga, Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Mhe. Jaji Mstaafu, Thomas Mihayo, Rais wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) (wa tatu kushoto), Prof. Mugongo Fimbo (wa pili kulia) na Msajili wa ICTR (wa kwanza kulia) wakiwa  katika picha ya pamoja na baadhi ya Wahariri. Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na Baraza la Habari Tanzania (MCT)  wameandaa Mkutano huu kwa Mara ya kwanza, lengo likiwa ni kubaini matatizo baina ya pande zote mbili na kutoka na mapendekezo ili kuboresha utendaji kazi. (Picha na Mary Gwera, Mahakama).
 Mhe. Jaji Mstaafu Thomas MIHAYO, Rais wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) akitoa neno katika Mkutano Kati ya Mahakama na Vyombo vya Habari, 'Judiciary Media Forum' unaofanyika Leo katika UKUMBI wa mikutano wa Julius Nyerere International Convention Centre. (JNICC).
 Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania (wa kwanza kushoto), Mhe. Jaji Mstaafu, Thomas MIHAYO, Rais wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) wa pili kushoto, Mhe. Shaaban Lila, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania (wa  tatu kulia) na baadhi ya Majaji na wageni waalikwa wa Mkutano huo wakifuatilia mjadala katika Mkutano huo, ambao umelenga kujenga uhusiano katika utendaji kazi wa Mahakama pamoja na Vyombo vya Habari.
 Baadhi ya Wahe. Majaji wakiwa katika Mkutano huo uliofanyika katika UKUMBI wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Nyerere (JNICC)
 Baadhi ya WAHARIRI wa Vyombo vya Habari wakiwa katika  Mkutano huo leo.

MAZISHI YA MRAKIBU WA POLISI CAPT.KIDAI SENZALA ALIYEFARIKI KATIKA AJALI YA HELKOPTA DAR ES SALAAM

$
0
0
Maafisa wa Polisi wakiwa wamebeba sanduku lililohifadhi mwili wa Marehemu Capt. Kidai Senzala Kalise aliyefariki Novemba 29 mwaka huu katika ajali ya Helkopta iliyotokea Kipunguni B-Moshi Bar Dar es Salaam wakielekea katika makaburi ya familia huko Gonja Maore Wilaya ya Same mkoa wa Kilimanjaro Desemba 1, 2014.

Marehemu Kidai alikuwa Mrakibu wa Polisi na alizikwa kwa heshima zote za Kipolisi ikiwa ni kupigiwa mizinga na saluti mbalimbali za kipolisi kabla na baada ya maziko yake. 

Helkopta aina ya Robertson R44 iliyo tolewa msaada kutoka kwa Taasisi ya Howard G. Foundation inayomilikiwa na mfanyabiashara mashuhuri nchini Marekani Bw. Warren Buffet  ililetwa nchini kwa lengo la kukabiliana na vitendo vya ujangili na kupokelewa nchini na Waziri wa Maliasili na Utalii June 14, 2014 jijini Dar es Salaam na kuikabidhi kwa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) ilipata ajali majira ya saa nne asubuhi baada ya upata hitilafu katika injini yake na kupoteza maisha ya Mrakibu wa Polisi Capt. Kidai Senzala Kaluse, Mkaguzi wa Polisi Capt. Simba Musa Simba,  Konstebo wa Polisi, Josso Selestine na Capt. Joseph Khalfan wa Malisasili aliyezikwa Arusha.SOURCE: Father Kidevu Blog
Maofisa wa Polisi wakijiandaa kulibeba jeneza la Marehemu Capt Kidai.
 Maofisa wa Polisi wakiwa wamebeba sanduku la Mrakibu wa Polisi-Capt. Kidai.
 Heshima za Kihjeshi zikitolewa kabla ya jeneza kushushwa kaburini na kupigiwa mizinga.
 Heshima zikiendelea...

 Wanafamilia wakiwa katika gari lililobeba mwili wa mpendwa wao Capt. Kidai Senzala.
Ndugu wa marehemu akiwepo mkewe, mama yake mzazi marehemu, dada zake na ndugu wengine wakitafakari kazi ya Mungu baada ya kufanyika kwa mazishi ya Capt. Kidai Senzala.

CHEREKO LA USIKU WA SUMAI, BONGE LA PARTY LA SEND OFF LAFANYIKA JEMBE BEACH MWANZA.

$
0
0
Sumai Kazi (with white dress) akiwa na dada ake wakiingia eneo la ukumbi kwa kutumia boat maalum ili kujumuika na ndugu jamaa na marafiki waliofika Jembe Beach kushuhudia Send Of Party yake.
Wakishuka kwa kutumia ghati tayari kuingia ukumbini.
Sumai (L) akiwa na dadayake (R) sanjari body guard wake. 
Sumai's Night.
Body guard namba moja.
Mazingira ya juu ukumbi wa bustani tulivu ya Jembe Beach Mwanza mahali ambako kulifanyika Usiku wa Sumai.
Sumai akiwakabidhi keki wazazi wake Mr& Mrs Kazi.
Sumai akikabidhi keki familia ya upande wa Bwana Harusi mtarajiwa.
Kitu cha udrinki wa milipuko....kilihusishwa kama sehemu ya ufunguzi wa sherehe na kusherehekea usiku wa Sumai.
Sumai akitosti na familia ya wakwe zake.
Sumai akimkumbatia shangazi yake.
Sumai akimvisha zawadi mumewe mtarajiwa Jully Ilunga Mbwebwe mara baada ya kumtambulisha kwenye hafla maalum iliyofanyika katika bustani yenye maadhari ya mvuto wa kipekee ya Jembe Beach aka Jembe ni Jembe jijini Mwanza.
Sumai Kazi akiwa na mumewe mtarajiwa Jully Ilunga Mbwebwe ambaye wapambe wake wanamuita Weston Grand Packeboo.
Familia ya ndugu na jamaa wa Jully Iluga Mbwebwe walikuwa na zawadi maalum kwa Sumai, na hapa walimkabidhi vito vya thamani na kumvisha.
Misosi tyme.
Apple thing.
Pacho Mwamba ni msemaji wa Familia na hapa akiungana na wageni kupata chakula.
Wakijinafasi.
Hapo vipi....!!?
Sister Sisters kutoka kushoto ni Sis-Kanengo, Sis-Matata na Kebby. 
Utamaduni wa Mwafrika kanga muhimu kuhusika.
Mambo ya vidole juu kwa akinamama na akinadada.
Sumai hapa alioga fedha mpaka baaasi.
Mama ni Mama.
Mr & Mrs Kazi wakizawadiwa kwa kuzaa chema.
Mizawadi mpwachaa!!
Kapu la mama.....hilooooo!!!
Mijihela....!!
Shavu....!!
Mkono wa kheri.
Hapa zilimwagika dorali kama gunia saba hivi....
Zawadi za Sumai kwa Baba na Mama.
Kamati ikiwasilisha mchango wake kama sehemu ya zawadi.
Kisha ikajitambulisha.
Bye Bye...!!
Dance la Bwana harusi mtarajiwa na nduguze lilikuwa nowmer siunajua tena wakongomani na masebene walisebenuka ile kisawasawa....!!
Mc G.Sengo (L) na Pacho mwanamuziki wa Fm Academia Patchou Mwamba.
Kisha ngoma juu ya ngoma.
PICHA NA GSENGO

TANZANIA YAUNGANA NA MATAIFA MENGINE KUADHIMISHA MIAKA 70 YA USAFIRI WA ANGA DUNIANI.

$
0
0
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Anga Tanzania (TCAA) Bw. Charles Chacha akiongea na waandishi wa habari kuhusu hali ya usalama wa anga Tanzania na namna Tanzania ilivyofanikiwa kupunguza idadi ya ajali za ndege.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaaban Mwinjaka akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu maadhimisho ya miaka 70 ya Usafiri wa anga duniani yanayoendelea nchini na namna Serikali kupitia Mamlaka ya Anga Tanzania (TCAA) ilivyojipanga kuhakikisha usalama wa ndege na abiria wanaotumia anga la Tanzania.
 Afisa mwongoza ndege wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere  Bi. Mossy Kitangita akiwahamasisha baadhi ya vijana na wanafunzi waliotembelea banda la maonesho la kitengo cha kuongozea ndege (hawapo pichani) kusoma masomo ya Sayansi ili waweze kupata fursa ya kujiunga na fani ya uongozaji wa ndege ndani na nje ya nchi.
 Afisa mwongoza ndege wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere  Bi. Mossy Kitangita (kulia) akimweleza Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaaban Mwinjaka  namna kitengo cha uongozaji wa ndege katika uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kinavyofanya kazi na changamoto wanazokabiliana nazo.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaaban Mwinjaka (Kushoto) akimuuliza swali Bw. Nyello Abeid, mkufunzi wa Chuo cha Usafiri wa Anga nchini kuhusu  alipotembelea banda la maonesho la chuo hicho leo jijini Dar es salaam wakati wa maadhimisho ya miaka 70 ya Usafiri wa anga duniani yanayoendelea nchini.
 Meneja wa Huduma za Hali ya Hewa kwa Usafiri wa Anga kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Bw. John Mayunga akifafanua utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka ya Hali ya Hewa katika usafiri wa anga.
  Mkuu wa masuala ya Ulinzi na Usalama katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Bw. Ole Laputi (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya wananchi waliotembelea banda la maonesho la idara hiyo kuhusu baadhi ya vimiminika visivyoruhusiwa kwa abiria wanaotumia usafiri wa anga.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaaban Mwinjaka (Kushoto) akitembelea banda la maonesho la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege kuona  utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa miundombinu na viwanja vya ndege  katika maeneo mbalimbali nchini.
Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.

KIWANJA CHA NDEGE CHA KIGOMA KUTANULIWA

$
0
0
SONY DSCKaimu Meneja wa Kiwanja cha Ndege Kigoma, Bw. Joseph Nyahende (Aliyenyanyua mikono) akitoa maelezo juu ya sehemu zitakazoendelezwa kwa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.SONY DSCKiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) akiangalia tabaka za udongo uliotumika katika kujengea Kiwanja cha Ndege Kigoma. Anayemuonesha ni Kaimu Meneja wa Kiwanja cha Ndege Kigoma, Bw. Joseph Nyahende (Kulia).
SONY DSCMeneja Mradi wa Utanuzi wa Kiwanja cha Ndege Kigoma, Mhandisi Neema Mwasha (Wapili kulia) akionesha eneo likaloboreshwa katika Mradi wa Utanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kigoma.

………………………………………………………………………………………
Na Saidi Mkabakuli, Kigoma
Serikali imeazimia kuanza kufanya utanuzi wa Kiwanja cha Ndege Kigoma ili kuweza kukidhi mahitaji yanaongeza siku baada ya siku ya kiwanja hicho.
Azma imetolewa na Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri wakati walipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya miundombinu katika Uwanja wa Ndege wa Kigoma.
Bibi Mwanri alisema kuwa serikali kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini ipo kwenye mkakati wa kuuendeleza uwanja huo ili uwe wa kiwango kizuri kwa kuhudumia watumiaji wa wa kiwanja hicho.
“Kama munavyokumbuka Serikali katika mwaka ujao wa fedha imepanga kuendeleza na kuboresha miundombinu ya usafiri wa anga ili kuongeza ufanisi; na kuendelea na kazi ya ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege katika maeneo ya kimkakati ikiwamo Kiwanja cha Ndege cha Kigoma,” alisema.
Kwa mujibu wa Bibi Mwanri, uendelezaji wa Kiwanja hicho utajumuisha ujenzi wa jengo la abiria pamoja na miundombinu yake (maegesho ya ndege, maegesho ya magari na barabara ya kuingia na kutoka) na kurefusha barabara ya kuruka na kutua ndege.
Akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya uwanja huo, Meneja Mradi wa Utanuzi wa Kiwanja cha Kigoma, Mhandisi Neema Mwasha alisema kuwa mpaka sasa Mamlaka ya Usimamizi wa Viwanja vya Ndege nchini imekamilisha taratibu za kumpata mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa uzio wa usalama na eneo la maegesho ya ndege.
“Kwa sasa tunaendelea na kazi ya utayarishaji wa makabrasha ya zabuni kwa ajili ya kazi za ujenzi wa barabara ya kuingia kiwanjani, maegesho ya magari, na usanifu wa kina kwa ajili ya upanuzi wa maegesho ya ndege pamoja na usimikaji wa taa na mitambo ya kuongozea ndege,” alisema.
Mhandisi Neema aliongeza kuwa wapo kwenye mchakato wa kumpata Mhandisi Mshauri wa kufanya usanifu wa jengo la abiria uwanjani hapo.
Naye Kaimu Meneja wa Kiwanja cha Ndege Kigoma, Bw. Joseph Nyahende alisema kuwa katika kuhakikisha kazi hiyo inafanyika kwa wakati, Mamlaka ya Usimamizi wa Viwanja vya Ndege nchini kwa kushirikiana na Mkoa wa Kigoma vimeainisha na kufanyia tathmini eneo litakalotumika kwa ajili ya kazi hiyo.
Viewing all 46379 articles
Browse latest View live




Latest Images