Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 416 | 417 | (Page 418) | 419 | 420 | .... | 1898 | newer

  0 0

  IMG_0216
  Mbunge wa jimbo la Singida mjini Mhe. Mohammed Gulam Dewji akisalimiana na wapiga kura kura wake na wananchi wa jimbo la Singida mjini mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Kibaoni tayari kuzindua kampeni za CCM uchaguzi wa serikali za mitaa katika jimbo la Singida Mjini.(Picha na Geofrey Mwakibete wa MOblog).
  IMG_0223
  Mbunge wa Singida MO Dewji akipata mapokezi kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni zilizofanyika Kibaoni mjini Singida.
  IMG_0182
  Baadhi ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) waliohudhuria uzinduzi huo wakimsikiliza Mbunge wao.


  IMG_0167
  Mbunge wa jimbo la Singida mjini Mhe. Mohammed Dewji akimnadi mgombe wa nafasi ya m/kiti wa mtaaa Kibaoni Timotheo Ruben John kwenye uzinduzi wa kampeni za CCM uchaguzi wa serikali za mitaa katika jimbo la Singida Mjini.
  IMG_0172
  Mbunge wa jimbo la Singda mjini mhe. Mohammed Dewji akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni za CCM uliofanyika katika viwanja vya soko la zamani la kitongoji mjini hapa.
  IMG_0202
  Mjumbe wa halmashauri kuu CCM (NEC) taifa manispaa ya Singida, Hassan Philip Mazala, akitoa nasaha zake kwenye uzinduzi wa kampeni za CCM zilizofanyika Kibaoni mjini hapa.
  IMG_0186
  Mgombea wa nafasi ya uwenyekiti wa mtaa wa Kibaoni Timotheo Ruben John akiomba kura kwa ajili ya nafasi hiyo, Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM (NEC) taifa jimbo la Singida mjini Hassan Mazala akifurahia jambo wakati wa uzinduzi wa kampeni za CCM zilizofanyika jana.

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa pili kulia mbele) na Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Benedict Missani (wa tatu kushoto mbele), wakiwaongoza wafanyakazi wa Airtel Tanzania na wanafunzi kwenye matembezi ya hisani yenye lengo la kuchangisha pesa kiasi cha shilingi milioni 10, kwa ajili ya kuendelea kuboresha Shule ya Msingi Kumbukumbu , yaliyoanzia katika Makao Makuu ya Airtel , Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kupitia Bongoyo, Haile Selasie na kuishia shuleni hapo Block 41, jijini Dar es Salaam jana. 
   Wafanyakazi wa Tanzania na wanafunzi wakiwa  kwenye matembezi ya hisani yenye lengo la kuchangisha pesa kiasi cha shilingi milioni 10, kwa ajili ya kuendelea kuboresha Shule ya Msingi Kumbukumbu , yaliyoanzia katika Makao Makuu ya Airtel, Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kupitia Bongoyo, Haile Selasie na kuishia shuleni hapo Block 41, jijini Dar es Salaam jana.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa pili kushoto) akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Benedict Missani, funguo za kisima kipya cha maji safi kilichojengwa  kwa hisani ya Airtel kwa kushirikiana na Wafanyakazi wake,  katika Shule ya Msingi Kumbukumbu, wakati wa hafla iliyofanyika shuleni hapo eneo la Block 41 jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Malya (kushoto), Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Priscilla Moshi (wa tatu kushoto), na Mwenyekiti wa Shule hiyo, Mwemba Mwilima.
   Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Benedict Missani (kulia) akifungua ili kukagua kisima kipya cha maji safi kilichojengwa  kwa hisani ya Airtel kwa kushirikiana na Wafanyakazi wake,  katika Shule ya Msingi Kumbukumbu, baada ya kukabidhiwa rasmi na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa pili kushoto), wakati wa hafla iliyofanyika shuleni hapo eneo la Block 41 jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Malya (kushoto) na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Priscilla Moshi (wa tatu kushoto).
  Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso akifungulia maji ya bomba kama ishara ya uzinduzi rasmi wa  kisima kipya cha maji safi kilichojengwa  kwa hisani ya Airtel kwa kushirikiana na Wafanyakazi wake,  katika Shule ya Msingi Kumbukumbu, wakati wa hafla iliyofanyika shuleni hapo eneo la Block 41 jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Benedict Missani (wa tatu kushoto) na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Priscilla Moshi (wa nne kushoto).


  Airtel yakabithi kisima cha maji kwa shule ya msingi Kumbukumbu Dar
  ·         Yaendesha matembezi yahisani kuendelea kuboresha mazingira ya shule
  ·         Zaidi ya shilingi milioni 10 kukusanywa
  Dar es salaam Novemba 30, 2014 Kampuni ya Airtel leo imeendesha matembezi ya hisani ili kuchangisha  pesa kwajili ya kuendelea kuboresha shule ya msingi kumbukumbu iliyopo jijini Dar es salaam 
  Matembezi yenye lengo la kupata pesa ili kufanya ukarabati wa darasa la watoto na kununua viti na meza za kukalia yameetimishwa kwa uzinduzi wa kisima cha maji kilichojengwa kwa hisani ya Airtel kwa kushirikiana na wafanyakazi wake ili kukabiliana na tatizo la maji shule hapo
  Akiongea wakati wa kuzindua kisima hicho mgeni rasmi , Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Benedict Missani kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya jamii  jinsia na watoto Mh. Sophia Simba alisema”  naunga mkono juhudi zilizofanywa na Airtel katika kuendelea kuboresha mazingara ya utoaji elimu shuleni hapa. Nimefurai kuona kuwa Airtel haikuridhika na ujenzi wa kisima hii tu bali wameamua kuchua hatua nyingine ya kushirikisha wadau mbalimbali katika kutatua changamoto walizoziona shuleni hapa.
  Leo tumetembe kwa pamoja ili kuweza kuchangisha kiasi cha shilingi milioni 10 zikazowesha kazi ya kuendelea kuboresha mazingara ya shule hii kuendelea. 
  Serikali inaunga mkono dhamira hii na jitihada hizi zinazoenda sambamba na kauli mbili yetu ya Matokeo makubwa sasa  na kuhakikisha tunaboresha maeneo muhimu hususani elimu kwani vijana hao ndio nguvukazi na taifa la kesho. Natoa wito kwa mashirika mengine watu binafsi na taasisi mbalimbali kujitokeza na kuchangia katika shughuli za jamii ili kukubiliana na changamoto tulizo nazo sasa.
  Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso alisema” nawashukuru wafanyakazi wa Airtel na kila moja aliyeshiriki hapa kwa kujitoa katika kusaidia jamii, sisi Airtel tumejipanga kutimiza dhamira yetu ya kuchangia katika kuhakiksha tunachangia katika sekta ya elimu kwa kuendelea kutoa vitabu na kuboresha mazingira ya shule. Kupitia mradi wa Airtel Shule yetu tumeweza kuzifika shule nyingi kwa kuwapatia nyenzo muhimu katika elimu na leo tumewafikia shule ya msingi kumbukumbu tukiwa na lengo na kuendelea kuboresha sekta ya elimu.
  Mpango huu wa Airtel Tunakujali ni endelevu bado tutakuwa  shughuli nyingi zaidi na shule nyingi zikipokea misaada hivyo tunawaomba wadau mbalimbali kuendelea kushirikiana nasi.
  Kwa upande wake mfanyakazi wa Airtel Bi Veneranda Boniface Alisema amejisikia furaha kutumia jumamosi yake kutembea kwaajili yakusaidia jamii, hii ni sehemu pia ya mazoezi lakini zaidi ni njia pekee ya kuniwezesha mimi kwa nafasi yangu katika jamii kushiriki kuchangia.
  Matembezi hayo ya hisani yalianzia katika makao makuu ya Airtel yaliyoko Moroco Dar esaalam na kwenda njia ya Alihasan Mwinyi, kupitia Kaunda, Bongoyo , haileselaile , Ali hassani Mwinyi na kuishia katika shule ya msingi Kumbukumbu.

  0 0

  Kampuni ya African Barick Gold (ABG) inayo furaha kutangaza kuwa imebadili jina lake na sasa na itatambulika kama Acacia Mining plc. Mabadiliko haya ni sehemu ya jitihada kubwa za kubadilisha mtazamo na mkakati wake mpya wa kazi yetu kubwa katika uchimbaji wa madini. Mabadiliko haya yamekuja baada ya wanahisa wa kampuni kukubaliana na kupiga kura ya kupitisha maamuzi haya jana tarehe 26 mwezi Novemba mwaka 2014.

  Acacia ni mti ambao ndiyo chimbuko la jina letu jipya, ni mti unaonekana kuwa ni nembo ya mandhari ya Afrika na unaweka msisitizo kwenye malengo yetu ya kiuwekezaji Afrika. Zaidi ya hayo, tutaendelea kutumia nembo ya Afrika kwenye alama zetu zote ili kusisitiza kujikita kwetu kwenye bara la Afrika. Mfuko wetu wa Maendeleo ya Jamii wa ABG sasa utajulikana kama Mfuko wa Maendeleo ya Jamii wa Acacia.

  Akizungumza kuhusu habari ya mabadiliko haya, Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Acacia Mining, Brad Gordon amesema:

  “Bila shaka mti wa Acacia (kwa Kishwahili “Mgunga”) ni mti unaojulikana kuwa ni sehemu ya utambulisho wa mandhari ya Afrika.Kwa mikakati yetu  mipya, tutajenga biashara endelevu na yenye mafanikio makubwa nchini Tanzania na barani kote Afrika. Kama mti wenyewe wa Acacia ulivyo enea.  Tunaamini kuwa mlinganisho wetu huu na mti wa Acacia ni madhubuti na tutaweza kustahimili mazingira magumu yoyote tutakayokumbana nayo.

  Tunataka kuweka wazi kuwa mabadiliko haya ya jina hayana maana kuwa ni njia ya kukwepa  wajibu waliokuwa nao ABG kama vile kulipa kodi, bali ni kuakisi hatua na mkakati wetu mpya wa biashara. Vilevile  mabadiliko haya, hayataathiri ajira zozote na hayabadilishi mfumo wa umiliki wa kampuni. Tutaendelea kuwa wachimbaji wa dhahabu tuliojitegemea na tulio orodheshwa kwenye masoko yote ya hisa ya London na Dar es Salaam.  Hakutakuwa na mabadiliko yoyote ya mikataba ya ajira au makubaliano (mapatano) na masharti ya ajira katika migodi yetu kufuatia mabadiliko ya jina la Kampuni."

  Kufuatia jitihada hizi za kubadilisha jina la kampuni, alama zetu kwenye  masoko ya hisa pia zimebadilika kutoka ABG na kuwa ACA katika masoko ya hisa ya London (LSE) na Dar es Salaam (DSE).

  Kampuni ya uchimbaji wa madini ya Acacia iko kwenye safari kutengeneza biashara itakayo kuwa kinara  katika bara la Afrika kwa kipindi cha miaka mitano ijayo. Ni muhimu jina hili liakisi hayo kwa usahihi.  Ubadilishaji wa jina ni hatua muhimu ya kuwaleta wadau wetu pamoja kwa lengo la kuunga mkono  utambulisho huu mpya wa kampuni.

  Kampuni ya Acacia itaendelea kuwekeza na kufanya kazi kwa karibu na jamii zinazozunguka migodi yetu kupitia miradi iliyopo na miradi/mipango mipya. Tutaendelea kuwa miongoni mwa wachangiaji wakubwa wa uchumi nchini Tanzania na tutaendelea kuzingatia viwango vya juu kabisa vya ubora katika biashara yetu na pia kuendeleza uchimbaji huku usalama ukiwa kipaumbele chetu muhimu.

  0 0

  Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Watatu kushoto) akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Bandari ya Kasanga, Bw. Mponjoli Thompson Mwamafupa (Kulia) mara walipowasili katika bandari hiyo kujionea shughuli mbalimbali za maendeleo bandari hapo.
  Mkuu wa Bandari ya Kasanga, Bw. Mponjoli Thompson Mwamafupa (Kushoto) akiwaongoza wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango kujionea moja ya meli za kigeni zinazotia nanga katika bandari hiyo. Meli hiyo ni MV Rwegura kutoka nchini Burundi.
  Mkuu wa Bandari ya Kasanga, Bw. Mponjoli Thompson Mwamafupa (Kushoto) akiongea na wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango kuhusu namna ya kuhudumia meli kutoka nje ya nchi.

  Na Saidi Mkabakuli, Sumbawanga

  Serikali imeazimia kuanza kuiboresha bandari ya kimkakati ya Kasanga inayohudumia nchi za Burundi, Rwanda na Kongo iliyopo katika Ziwa Tanganyika, mkoani Rukwa.

  Ahadi hiyo imetolewa na Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri wakati walipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya miundombinu katika Bandari ya Kasanga.

  Bibi Mwanri alisema kuwa serikali kupitia Mamlaka ya Bandari Tanzania imepanga kuboresha bandari zote ili kuwa malango kuu la biashara kwa soko la ndani na kwa nchi jirani ili kuongeza uwezo wa kuhudumia shehena kwa ufanisi.

  “Tumedhamiria kuendelea kuboresha miundombinu ya bandari hususan miradi iliyoibuliwa katika Programu ya Matokeo Makubwa Sasa ikiwemo Bandari ya Kasanga ili kuweza kukidhi mahitaji ya utoaji wa huduma katika eneo hili,” alisema.

  Bibi Mwanri aliongeza kuwa serikali pia imejipanga kuendelea kuboresha miundombinu na ununuzi wa vifaa mbalimbali vya kuhudumia shehena katika bandari za Dar es Salaam, Tanga, Mtwara, Kasanga na Kigoma na kukamilisha maandalizi ya ujenzi wa bandari mpya za Mwambani (Tanga), Mbegani (Bagamoyo) na Bandari Kavu ya Kisarawe.

  Akizungumza na ugeni huo, Msimamizi Mkuu wa Bandari ya Kasanga, Bw. Mponjoli Thompson Mwamafupa alisema kuwa Bandari hiyo ina fursa nyingi katika kuhudumia shehena na abiria wanaopitia bandarini hapo.

  “Bandari yetu ina fursa kubwa za kibiashara kwani tuna wateja wengi kutoka ndani na nje ya nchi wanaotumia bandari yetu kupitishia bidhaa zao, pamoja na abiria wanaosafiri kwenda nje na ndani ya Tanzania,” alisema.

  Kwa mujibu wa Mpango wa Maendeleo kwa mwaka ujao wa fedha Serikali imedhamiria kuboresha mazingira yatakayowezesha sekta binafsi kuwekeza katika kujenga miuondombinu na kuboresha usafirishaji wa mizigo katika bandari zote nchini.

  Pia, Mpango huo unaweka bayana kuendeleza na ukarabati na ununuzi wa vyombo vya usafiri na usafirishaji katika maziwa.

  0 0

   Sehemu ya mashuhuda wa tukio la kuanguka mti mkubwa katika barabara ya Sea View,Upanga jijini Dar es Salaam.Baadhi ya mashuhuda waliokuwepo kwenye tukio hilo wameeleza kuwa kuwa chanzo cha kuanguka kwa mti huo ni ukongwe wa mti huo.
   Sehemu ya magari yaliyoangukiwa na Mti huo mchana huu.
   Muonekano wa Mti huo.
   Mti huo ukiwa umeangukia ukuta.
   Baadhi ya wamiliki wa magari hayo wakijadiliana mara baada ya magari yao kuangukiwa na mti huo.
   Pichani ni viti ambavyo vilikuwa vimekaliwa na watu ambao walinusurika.
  Hawa ndio waliokuwa wamekaa kwenye hivyo viti.

  0 0

  Mtafiti mafunzo, usambazaji na teknolojia kutoka taasisi ya utafiti wa zao la Kahawa (TACri),Jeremia Magesa (kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Kahawa Kajiru Kisenge wakifuatilia mawasilisho yaliyokuwa yakifanywa na mwakilishi wa Cafe Africa ,Catherine Mwangata(Hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa mtaala endelevu wa kitaifa juu ya zao la Kahawa nchini.
  Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Bodi ya Kahawa Tanzania(TCB) Astery Bitegeko akipitia mambo kadhaa yaliyokuwa yakiwasilishwa wakati wa uzinduzi wa mtaala endelevu wa kitaifa juu ya zao la Kahawa ,uzinduzi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano ya Bodi ya TCB,kulia kwake ni afisa utumishi wa TCB,Moses Chimwinga.
  Wawakilishi wa Cafe Africa,Catherine Mwangata(Coutry Manager)  na Wiliam Wakuganda(Special Advisor) wakifuatilia mjadala wakati wa uzinduzi wa mtaala endelevu wa kitaifa juu ya zao la Kahawa ,uzinduzi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano ya Bodi ya TCB.
  Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Bodi ya Kahawa Tanzania(TCB) Alhaj ,Dk Juma Ngasongwa(shoto) akiwa na Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Kahawa Tanzania(TCB0 Adolf Kumburu wakifuatilia kwa makini maelezo ya mwakilishi wa Cafe Africa hayupo pichani.
  Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Bodi ya Kahawa Tanzania(TCB) Alhaj Dk Juma Ngasongwa akichangia wakati wa uzinduzi wa mtaala endelevu wa kitaifa juu ya zao la Kahawa.
  Mtafiti mafunzo, usambazaji na teknolojia kutoka taasisi ya utafiti wa zao la Kahawa (TACri),Jeremia Magesa akichangia jambo wakati wa uzinduzi wa mtaala endelevu wa kitaifa juu ya zao la Kahawa.
  Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Kahawa Tanzania(TCB) Adolf Kumburu akitoa neno wakati wa uzinduzi wa mtaala endelevu wa kitaifa juu ya zao la Kahawa ,uzinduzi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano ya Bodi ya TCB.
  Mwakilishi wa Cafe Africa nchini Tanzania ,Catherine Mwangata akifafanua jambo wakati akiwasilisha mtaala endelevu wa kitaifa juu ya zao la Kahawa uliozinduliwa na Bodi ya Kahawa nchini (TCB). Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya Kaskazini.

  0 0

     Baadhi ya Wanafunzi kutoka shule mbalimbali  wakiongozwa na Brass band yaJeshi la Polisi,wakiwa kwenye uzinduzi wa matembezi ya maadhimisho  ya siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya Wanawake na watoto yaliyofanyika katika viwanja vya Oysterbay Polisi,leo Jijin Dar.
   Baadhi ya Askari Jamii wakiwa kwenye uzinduzi wa matembezi ya maadhimisho  ya siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya Wanawake na watoto yaliyofanyika katika viwanja vya Oysterbay Polisi,leo Jijin Dar.
    Baadhi ya Wanafunzi kutoka shule mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi wa matembezi ya maadhimisho  ya siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya Wanawake na watoto yaliyofanyika katika viwanja vya Oysterbay Polisi,leo Jijin Dar.
  Baadhi ya Maofisa wa Polisi wakisubiri  kupokea matembezi ya uzinduzi wa maadhimisho  ya siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya Wanawake na watoto yaliyofanyika katika viwanja vya Oysterbay Polisi,leo Jijin Dar.

  0 0

  Na Mwandishi Wetu

  MAKAMU wa Rais, Dk.Mohammed Gharib Bilal (pichani) Desemba 2 anatarajiwa Kuwa mgeni rasmi katika sherehe za uwekwaji wa jiwe la Msingi la Chuo Kikuu Cha Bagamoyo(UB), zitakazofanyika Kijijini Kiromo,Bagamoyo Mkoani Pwani.

  Akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake Mikocheni Dar es Salaam Ofisa Habari wa (UB), Happiness Katabazi alisema sherehe hizo zitafanyika Kijijini Kilomo Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani na kwamba uwekwaji wa jiwe hilo ni ufunguzi rasmi wa ujenzi wa Chuo Kikuu Cha Bagamoyo Katika Kijiji hicho ambao utaanza mapema Januari Mwaka 2015.

  Katabazi alisema Dk. Bilal ndiye atakuwa mgeni rasmi katika sherehe hiyo ya kihistoria katika Wilaya ya Bagamoyo kwasababu Somo la Historia linatufundisha kuwa mji wa Bagamoyo ilikuwa ukikaliwa na watumwa.

  " Sasa sisi UB tunaitambua hiyo historia na ndiyo maana tukaamua kuanzisha Chuo Kikuu ambacho tumekipa jina la Bagamoyo.Na kwakuwa kupitia Mji wa Bagamoyo tulikuwa watumwa, basi sasa kupitia UB ambayo inajenga makazi yake ya kudumu katika mji huo, binadamu wote watakuwa huru kwasababu tutapata elimu" alisema Katabazi.

  Alisema UB ambayo ilianzishwa rasmi mwaka 2011 ambayo ina makazi yake yake ya muda ,Mikocheni ,Dar es Salaam na kwamba ujenzi wa Makazi ya kudumu ya UB kijijini Kilomo , utasaidia kukuza shughuli za uchumi, wananchi wa eneo hilo kupata huduma ya elimu ya ngazi ya Chuo Kikuu kwa ukaribu.

  Aidha aliwaomba wananchi Wilaya Bagamoyo na Mkoa wa Pwani kwa ujumla kujitokeza kwa Wingi Katika sherehe hiyo. UB ilianzishwa rasmi Mwaka 2011.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mkuu wa mkoa wa Njombe, Dkt. Rehema Nchimbi, kwa pamoja wakisimama kupokea maandamano wakati wa sherehe za Maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani iliyofanyika leo Desemba 1, 2014 Kitaifa kwenye Uwanja wa Sabasaba Mkoani Njombe
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Sabasaba Mkoani Njombe leo, Desemba 2014.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Sabasaba Mkoani Njombe leo, Desemba 2014. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Wa pili kulia ni katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar Dkt Omar Dadi Shajak, Kushoto Mkurugenzi wa Mazingira Offisi ya Makamu wa Rais Dkt Julius Ningu, Nyuma KUlia MKurugenzi Msaidizi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais ambae pia ni Mtaalamu wa Mabadiliko ya Taibia Nchi wakifuatilia hotuba ya  Ufunguzi wa mkutano wa 20 wa Dunia wa Mabadiliko ya Tabia Nchi MJini Lima Nchini Peru.
  Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia  sehemu nyingine ya ufunguzi wa chombo cha utekelezaji SBI katika mkutano wa 20 wa Dunia wa Mabadiliko ya Tabia nchi ulioanza rasmi leo Mjini Lima, Peru.
  Picha na Evelyn Mkokoi wa Ofisi ya Makamu wa Rais


  0 0

  Pictured here: Idris and Macky2. Last night (Sunday, 30 November) four big Brother Hotshots Housemates were evicted, Sheillah from Botswana, Trezegah from Mozambique, Goitse from Botswana and Ellah from Uganda.  Africa’s biggest reality show Big Brother Hotshots, produced for M-Net’s AfricaMagic, is being screened live 24/7 on DStv 197/198. For more information log on towww.bigbrotherafrica.com 
  -------------------------------------------------------
  Sheillah, Trezagah, Ellah & Goitse fell just one week short of a shot at the USD 300 000 prize on Big Brother Hotshots as they were sent home in a heart-stopping quadruple eviction on Sunday night. Their departure means that 8 housemates are left in the game – and one of them must be named as the winner next Sunday!

  Viewers must now choose between, in alphabetical order, Butterphly (Zimbabwe); Idris (Tanzania); JJ (Zimbabwe); M'am Bea (Ghana); Macky2 (Zambia); Nhlanhla (South Africa); Sipe (Malawi) and Tayo (Nigeria) – and get voting! Next week’s 2-hour live show will start an hour earlier, at 19:00 CAT, to pack all the drama of season 9 into one sizzling episode.

  Macky2 revealed his Head of House ‘add’ decision to the housemates, with Ellah declaring “I knew it” as he’d explained that he’d based his decision on who he felt was a strong competitor. The Ugandan was spared - in the first round of evictions, at least - as IK revealed that Sheillah and Trezagah had been evicted. Joining him on stage, the Motswana said that she’d known ‘something was up’ when she wasn’t nervous for the first time, this week. 

  She declared that her ‘thing’ with Nhlanhla as “very complicated” and that it wasn’t “a relationship”. Trezagah said he felt “so bad” at falling so close to the final and explained that he’d moved during the ‘freeze task’ – the only reason he was up for eviction in the first place – because he thought the task was over, and that he was being pranked again.

  IK went back into the house and revealed that someone else was going to be evicted. He read out two more names – Ellah and Goitse – taking the number of evictees to four. The Ugandan could consider herself particularly unlucky to be sitting on the stage with IK, rather than sipping celebratory champagne inside the house with the finalists, as she never received a single nomination on Monday and was only up for eviction because Macky2 had added her to the list. She showed her annoyance when she told IK that she just wanted to punch Macky2 – though she also said she was proud of him for making a bold decision. Goitse said she was feeling “super awesome” and that she was looking forward to using her newfound fame to help her explore dancing, acting, writing, poetry, presenting “and everything”.
  Five housemates were tied on 1 country vote apiece after Africa voted this week, so the tie-breaker rule came into effect, sending the four contestants with the lowest percentage vote for all countries, home. Since JJ picked up a higher percentage vote, he was spared and sent into the final. Conversely, Tayo picked up the most country votes (4), followed by Idris (3) and Sipe (2).
  Sipe won the StarMeter prize this week on the back of the question: “Which of the Big Brother Hotshots housemates do you think has what it takes to win?”. Big Brother celebrated the work done by the Friends of the Global Fund Africa this week, naming them as winners of the USD 100 000 ONE Africa Award – in keeping with the housemates’ theme for the past week.
                                                                                                                                                        
  Ugandan Reggae & Ragga star Bebe Cool performed ‘Love You Everyday’ and Fally Ipupa almost brought the house down with ‘Original’.
  Voting opened immediately after the show and runs until 06:00 CAT on Sunday. Voters must now choose who of JJ, Tayo, Idris, Butterphly, Macky2, Sipe, Nhlanhla and M'am Bea they want to win Big Brother Hotshots! The more you vote for your favourite housemate, the better their chance of bing named as the winner of Big Brother Hotshots next week. There are four ways to vote the housemate you want to win.

  1.       Via SMS
  2.       Via WeChat
  3.       Via www.bigbrotherafrica.com
  4.       Via the mobisite on your mobile phone

  SMS Voting
  To vote via SMS: Text the keyword ‘Vote’, followed by the name of the housemate to the short code number for your country. For example SMS “Vote Uti” to 22626. SMS's are charged as applicable per specific network tariff. VAS rates apply. Free minutes do not apply. Please note that you can vote 100 times by SMS per mobile number during each voting period.

  The SMS numbers for Tanzania are:
   Tanzania, United Republic of
  Operator             Tariff                     Short Code
  Vodacom             TSH 600                15426
  Tigo                        TSH 600                15426
  Zantel                   TSH 600                15426
  Airtel                     TSH 600                15426

  WeChat Voting
  Voting on WeChat is free. To vote via WeChat on your mobile phone, go to your app store and download the WeChat app. Create your profile, then search for BigBrotherAfrica and add the account. You can then start voting on WeChat, up to 100 times per mobile phone number during a valid voting period.

  Website and mobile site voting
  Voting on the website and on the mobile site is free and you are allowed to vote 100 times per cellphone number on the website and again 100 times per cellphone number on the mobile site during a valid voting period.

  Visit www.bigbrotherafrica.com for more information and for the terms and conditions. Stay in touch with Big Brother Hotshots on social media - follow @bigbroafrica on Twitter, @bigbro_africa on Instagram and on Facebook at facebook.com/bigbrotherafrica.


  Big Brother Hotshots is produced by Endemol South Africa

  0 0

  DSC_0162

  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akimsikiliza kwa makini Mkuu wa kitengo cha watoto walemavu shule ya msingi Buhangija Jumuishi ya mkoani Shinyanga Mwl. Loyce Daudi aliyekuwa akimwelezea changamoto mbalimbali walizonazo shuleni hapo.(Picha na Zainul Mzige).

  Na MOblog, Shinyanga
  SHULE ya watoto wenye ulemavu ya Buhangija Jumuishi inakabiliwa na changamoto kubwa zinazofanya maisha kwa watoto hao kuwa magumu. Miongoni mwa changamoto hizo ni kukosekana kwa huduma za matibabu, walimu wa kutosha na mabweni.

  Hayo yamebainika wakati wa ziara fupi ya Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues. Mkuu wa Kitengo cha watoto walemavu shule ya msingi Buhangija Jumuishi iliyopo mkoani Shinyanga Mwl. Loyce Daudi, ndiye aliyeelezea ugumu uliopo katika shule hiyo yenye wanafunzi 209 wenye ulemavu wa aina mbalimbali.
  DSC_0173
  Mkuu wa kitengo cha watoto walemavu shule ya msingi Buhangija Jumuishi ya mkoani Shinyanga Mwl. Loyce Daudi akimtambulisha Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues aliyefanyia ziara fupi akiwa safarini kuelekea jijini Mwanza akiwa ameambatana na Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias (katikati).

  Alisema shule hiyo yenye walemavu wa aina tatu wa kusikia, ngozi na wasioona inakabiliwa pia na lishe duni ambayo haimpi kijana nafasi ya kuendelea, kwani wanakula mlo wa aina moja na kidogo. Shule hiyo ambayo awali ilikuwa inawapokea wanafunzi wasioona sasa inapokea walemavu wa ngozi kutokana na hofu iliyokuwa inalikumba taifa ya mauaji ya albino.

  Aidha mwalimu huyo alisema kwamba wameiomba serikali kuwa na muuguzi na daktari katika makazi hayo lakini mpaka sasa hawajapatiwa kutokana na wao wenyewe kutokuwa na uwezo wa kuwalipa. Alisema kutokana na rika mbalimbali na tatizo la walemavu wa ngozi shule hiyo ambayo sasa imegeuzwa kuwa makazi inastahili kuwa na daktari na mabweni yaongezwe.

  DSC_0191
  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues ( wa pili kushoto) akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Buhangija Jumuishi ya mkoani Shinyanga (hawapo pichani) alipofanya ziara fupi akiwa safarini kuelekea jijini Mwanza akiwa ameambatana na Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias (wa pili kulia). Kulia ni Mkuu wa kitengo cha watoto walemavu shule ya msingi Buhangija Jumuishi ya mkoani Shinyanga Mwl. Loyce Daudi.

  Aidha mwalimu alisema walimu kwa ajili ya viziwi hawatoshi.
  Naye Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues, amesema ameyaona mazingira hayo na kuahidi kushirikiana na marafiki na mamlaka nyingine kuboresha mazingira ya kituo hicho.
  Alisema kwamba amefurahishwa kuwapo katika kituo hicho na kuona namna wanavyoweza kusaidia sehemu hiyo ya jamii kutojisikia upweke.

  Akizungumza na watoto hao walimwambia kwamba wana changamoto ya nguo, vitanda, vitabu na mahitaji mengine ya lazima kama watoto na wanafunzi.
  DSC_0177
  Baadhi ya watoto wanaosoma shule ya msingi Buhangija Jumuishi ya mkoani Shinyanga wakimsikiliza Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (hayupo pichani).
  DSC_0201
  DSC_0222
  Mwanafunzi wa kidato cha pili shule ya sekondari Loreto mkoani Shinyanga Beatrice Leme anayelelewa kwenye kituo hicho kutokana na kukithiri kwa mauaji ya walemavu wa ngozi mkoani humo akimwelezea changamoto mbalimbali zinazowakabili kwa niaba ya wanafunzi wenzake Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues aliyefanya ziara fupi shuleni hapo.
  DSC_0233
  Mwanafunzi wa darasa la sita shule ya msingi Buhangija Jumuishi ya mkoani Shinyanga, Daniel Limbu akizungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues kwa niaba ya wanafunzi wenzake.
  DSC_0256
  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues, Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias pamoja na Mkuu wa Kitengo cha watoto walemavu shule ya msingi Buhangija Jumuishi ya mkoani Shinyanga Mwl. Loyce Daudi wakifurahi pamoja na watoto wenye ulemavu wa ngozi katika shule hiyo.
  DSC_0257
  DSC_0301
  Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto wenye ulemavu wa ngozi wanaolelewa kwenye kituo hicho ambacho ni salama kwao kutokana na hofu iliyokuwa inalikumba taifa ya mauaji ya albino.
  DSC_0274
  Baadhi ya majengo ya mabweni ya shule ya msingi Buhangija ya wilayani Shinyanga.
  DSC_0306
  Baadhi ya watoto wenye ulemavu wa ngozi wakicheza mpira kwenye mazingira salama shuleni hapo kutokana na hofu iliyokuwa inalikumba taifa ya mauaji ya albino.
  DSC_0308
  Mkuu wa Kitengo cha watoto walemavu shule ya msingi Buhangija Jumuishi iliyopo mkoani Shinyanga Mwl. Loyce Daudi akimtambulisha mtoto Erick mwenye ulemavu wa ngozi kwa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (kushoto) aliyefanya ziara fupi kwenye kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu (mahitaji maalum).
  DSC_0322
  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akimsuka kwenye bembea mmoja wa watoto wenye ulemavu wa ngozi Zawadi Deus anayesoma shule ya msingi Buhangija Jumuishi iliyopo mkoani Shinyanga wakati wa michezo alipofanya ziara fupi shuleni hapo.
  DSC_0358
  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akisaini kitabu cha wageni wakati akijiandaa kuondoka shuleni hapo baada ya kuhitimisha ziara yake fupi. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha watoto walemavu shule ya msingi Buhangija Jumuishi iliyopo mkoani Shinyanga Mwl. Loyce Daudi.

  0 0  0 0


  0 0
  0 0

  SHIRIKA LA USAFIRI DAR ES SALAAM (UDA)
   
  SHIRIKA la Usafiri Dar es Salaam (UDA) linawatangazia Watanzania wote hususan wakazi wa jiji la Dar es Salaam kwamba linahitaji kuajiri madereva  kwa ajili ya kuendesha mabasi yake hapa jijini.
   
  SIFA ZA WAOMBAJI
  Waombaji wa kazi ya udereva wanatakiwa kuwa na umri wa kuanzia miaka 30-55, ujuzi wa udereva wa mabasi kutoka katika vyuo vya VETA, NIT, au chuo kingine kinachotambulika na Mamlaka ya Elimu ya Ufundi nchini (NECTA). Pia wanapaswa kuwa na leseni ya udereva daraja C Kavu (Class C Plain) na daraja C1(Class C1) , rekodi nzuri ya utendaji na afya njema.
   
  NAMNA YA KUOMBA
  Waombaji wote walete barua zao za maombi wakiambatanisha na barua za udhamini, walete barua hizo kwa mkono katika Ofisi ya Afisa Rasilimali watu na Utawala, Makao Makuu ya UDA, KAMATA COMPLEX, mahali zilipokuwa ofisi za mabasi ya SCANDINAVIA.
   
  Wanawake wanyesifa wanahimizwa zaidi.
  KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA NAMBA 255222127421, 0766777754, 0766777753 ,0754776700, 0715776500,0712000037 au wasiliana kwa barua pepe info@uda.co.tz,uda@umojainvestments.com au kwa sanduku la posta
  Shirika la Usafiri Dar Es Salaam (UDA)
  S.L.P 872
  Dar Es Salaam,Tanzania
  LIMETOLEWA NA OFISI YA MAHUSIANO YA UMMA UDA
  DESEMBA 01, 2014.

  0 0

   Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Ponsiano Nyami akizungumza na wanamichezo wa Bandari.
  Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA ambaye pia ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Bw. Peter Gawile akizungumza na wanamichezo wa Bandari.
   Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Ponsiano Nyami akiikagua timu ya Bandari ya Dar es Salaam kabla ya kuwavaa Bandari Mtwara.

  Mchezo wa bao baina ya Makao Makuu na Bandari ya Mtwara.
   Timu ya kuvuta kamba kutoka Bandari ya Dar es Salaam wakimenyana na wenzao wa Bandari Mtwara.
   Timu ya kuvuta kamba kutoka Bandari Mtwara wakimenyana na wenzao wa Bandari ya Dar es Salaam.
   Timu kutoka Bandari za Maziwa ikiingia uwanjani.
   Timu ya Makao Makuu.
   Kikosi cha Bandari ya Dar es Salaam wakijipanga kwa ufunguzi.
   Mashabiki wakiwa uwanjani.
   Kikosi kazi cha Bandari ya Mtwara kabla ya kuwavaa Bandari ya Dar es Salaam.
   Maafisa wa huduma ya kwanza kazini.
   Timu ya netball kutoka Bandari ya Mtwara.
  Timu ya netball kutoka Makao Makuu.


  0 0

   Mdau wa Globu ya jamii,Daniel Chongolo
  leo anasherehekea siku yake adhimu ya kuzaliwa, Anasema Sifa na Utukufu anazirudisha kwa Mungu maana yeye ndiye ajuae sababu ya kumuacha hadi hii leo na hakuna alicho mpa. Pia anashukuru Wazazi hasa mama yake, familia yake ikiongozwa na mkewe pamoja na watoto wao. 

  Globu ya jamii inamtakia afya njema na kila lakheri katika siku yake hii muhimu kwake.

  0 0

  Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mpanda kujionea shughuli mbalimbali za maendeleo uwanjani hapo.
  Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) akizungumza na Meneja wa Uwanja wa ndege wa Mpanda, Mkoani Katavi Bw. Seneti Lyatuu (Kulia). Anayefuatilia mazungumzo ni Bw. Omary Abdallah ambaye Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na Ufuatiliaji (Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango).

  Na Saidi Mkabakuli, Mpanda

  Kufuatia kukamilika kwa ukarabati na upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda, mkoani Katavi, Serikali imewaasa watumiaji wa uwanja huo kutunza miundombino ya uwanja huo ili kuweza kuhudumia wakazi na wageni wapitao uwanjani hapo kwa muda mrefu.

  Wito huo umetolewa na Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri wakati walipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya miundombinu katika Uwanja wa Ndege wa Mpanda, mkoani Katavi.

  Bibi Mwanri alisema kuwa serikali kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege imekamilisha kazi ya kuufanya uwanja huo uwe wa kiwango kizuri tayari kwa kutumika kwa ndege za binafsi na biashara, hivyo uongozi wa uwanja huo hawana budi ya kuhakikisha miundombinu ya uwanja huo inatunzwa ipasavyo.

  “Kama munavyofahamu Serikali imekuwa ikiwekeza sana katika uendelezaji wa miundombinu ya usafiri nchini hasa kuendelea kuboresha miundombinu ya usafiri wa anga ili kuongeza ufanisi na kuendelea na kazi ya ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege katika maeneo ya kimkakati, hivyo kuna haja ya kuunga mkono jitihada hizi za Serikali,” aliasa Bibi Mwanri.

  Akitoa taarifa ya uendelezaji uwanja huo kwa msafara wa timu ya ukaguzi, Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda, Bw Seneti Lyatuu alisema uwanja huo umeboreshwa na hivyo, unaweza kutumika kutua na kuruka ndege za kiwango cha kati na hata zile ndege kubwa zinaweza kutua kwa dharura.

  “Uwanja huu umekarabatiwa na barabara ya kuruka na kutua ndege imerefushwa kwa kiwango cha lami kutoka urefu wa mita 1,500 na upana wa mita 30 hadi kufikia urefu wa mita 1,820 na upana wa mita 30,” alisema Bw. Lyatuu.

  Kwa mujibu wa Meneja huyo, kukamilika kwa uwanja huo kumevutia idadi ya abiria wanaoutumia uwanja huo kutoka abiria 285 mwaka 2009 hadi 2,390 mwaka 2013/14.

  Kwa mujibu wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2011/12 - 2015/16),  Miundombinu ni kipaumbele cha kwanza, hasa uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya nishati, usafirishaji (bandari, reli, barabara na usafiri wa anga), maji (safi, taka na ya uzalishaji) na TEHAMA.

  Serikali imeandaa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12 -2015/16) wa kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. Lengo kuu la Mpango huu ni kufungulia fursa za ukuaji uchumi wa nchi ili kuweka misingi ya ukuaji mpana wa uchumi na unaolenga watu walio masikini zaidi. 

  Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa Miaka Mitano unawianisha katika mfumo mmoja wa mipango mbalimbali ya maendeleo ya kitaifa ili kutoa mwongozo wa utekelezaji na kuipa Serikali fursa na mfumo rasmi wa ufuatiliaji na tathmini wa miradi ya maendeleo kitaifa.

  Lengo la Dira ni  kuibadili Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.  0 0

  MultiChoice Africa, kampuni inayoongoza katika kutoa burudani ya kulipiwa ya dijitali pamoja na IPP Media wamesaini makubaliano yatakayoleta chaneli maarufu zaidi Tanzania, ITV, kuwa sehemu ya jukwaa la DStv.

  Ushirikiano huu wa kusisimua utawapa watazamaji wa Tanzania kote nchini fursa ya kuangalia vipindi vilivyotengenezwa hapa hapa nchini vikiwa na ubora mkubwa kidijitali. Chaneli hii itapatikana kwenye vifurushi vyote vya DStv ikiwemo kifurushi kilichozinduliwa hivi karibuni cha Bomba, Family, Compact, Compact Plus na Premium. 

  Akizungumzia ushirikiano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa ITV Bi Joyce Mhaville alisema: “Tunajivunia sana ushirikiano huu ambao tumekuwa tukiufanyia kazi kwa muda mrefu. Fursa zinazojitokeza kutokana na makubaliano haya yatanufaisha kampuni zote mbili pamoja na kuwanufaisha watazamaji wetu, hasa kwa wakati huu ambao tumehama kutoka katika mfumo wa analojia kuingia dijitali. ITV ina vipindi vyenye ubora vilivyotengenezwa hapa hapa nchini na ambavyo vinawafaa watanzania wakati DStv itatuwezesha kupanua wigo wetu.”

  Akizungumza juu ya hili, Mkurugenzi wa MultiChoice Africa kanda ya Afrika Mashariki Bwn Stephen Isaboke alisema: “MultiChoice imejizatiti kuwapa watazamaji wake chaneli nyingi mbalimbali zikiwepo zinazoonyesha vipindi vya hapa hapa na vile vya nje. 

  Kwa kuwa ITV inakuwa kwa kasi na ina watazamaji wengi, ushirikiano huu utatufaa kwa vile unaongeza vipindi vilivyotengenezwa hapa nchini.  Tutaendelea kuwekeza katika kuwaletea vipindi vyenye utofauti. Kwa kupitia vifurushi vyetu mbalimbali, tunawapa wateja wetu chaneli nyingi kwa bei tofauti ili wawe na uwanja mpana wa kuchagua.”

  Bw Isaboke na Bi Mhavile walionyesha kufurahishwa sana na kujitoa kwao kwa ushirikiano huu. Waliwahamasisha watanzania kununua DStv ili waweze kufurahia ITV na chaneli zingine nzuri.  


older | 1 | .... | 416 | 417 | (Page 418) | 419 | 420 | .... | 1898 | newer