Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 415 | 416 | (Page 417) | 418 | 419 | .... | 1897 | newer

  0 0


  0 0


  Na Andrew Chale

  USIKU maalum wa kuenzi vazi la Khanga na magwiji wa taarab nchini 'Usiku wa Khanga Party na Spice Modern Taarab' unapotarajia kulindima usiku wa leo Novemba 29 ndani ya Ukumbi wa Safari Carnival, Mikocheni B, karibu na daraja la Kawe, na kusindikizwa na gwiji wa mipasho Khadija Kopa pamoja na Bilal Mashauzi. 

  Kwa mujibu wa Mama wa Mitindo Bi. Asia Idarous Khamsin amebainisha kuwa kwa ushirikiano wa Fabak Fashions na Safari Carnival wameandaa usiku huo maalum kuenzi vazi la Khanga.

  "Usiku wa Khanga Party na Spice Modern Taarab ni maalum kuenzi vazi hili la khanga ambapo pia watu wote watakaofika watavaa vazi maalum la khanga. Hivyo wadau wajitokeze kwa wingi kwa kiingilio cha sh 10,000 na 20,000 kwa V.I.P." alisema Asia Idarous Khamisin.

  Aidha, alisema wadau watafurahia muziki mzuri kutoka kwa magwiji wa taarab hapa nchini akiwemo Khadija Kopa, Spice Modern taaba na Bilal Mashauzi.

  Amesema  leo usiku  pia kutakuwa na zulia jekundu  (Red Carpet)  ambapo watu mbalimbali watapata kupiga picha na mastaa na watu maarufu watakaojitokeza, ambao pia The Legend Dj John Dilinga wa nIsumba Lounge atasimamia muziki Old School.
  Pia alibainisha kuwa, tayari tiketi zimeanza kuuzwa sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam ikiwemo Fabak fashions Mikocheni na Safari Carnival.

  0 0

  Mnara wa Kumbukumbu ya Mwanajeshi wa Tanzania , Hamad Mzee aliyeuawa na ndege ya kivita ya wareno baada ya kuzitungua ndege mbili za kivita mwaka  1972 katika Kijiji cha Kitaya mpakani mwa Msumbiji na Tanzania wakati wa mapambano ya kuikomboa Msumbiji

   Kinana akitoa heshima katika mnara wa kumbukumbu shujaa Hamad Mzee katika Kijiji cha Kitaya, Mtwara Vijijini
   Wananchi wakishangilia wakati wa mkutano wa hadhara katika Kata ya Kitaya
   Ngoma ya asili ikitumbuiza wakati wa mkutano huo
   Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano huo


  Kinana akihutubia katika mkutano huo
   Kinana akipanda katika moja ya pikipiki 10 zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia kwa makatibu Kata wa CCM Wilaya ya Mtwara Vijijini katika mkutano wa hadhara wa katika Kata ya Kitaya.
  Kinana akimkabidhi kadi ya CCM mmoja wa wanachama wapya wa chama hicho katika mkutano huo.
   Watoto wakiwa na vipeperushi vya picha ya Kinana wakati wa mapokezi yake katika Kijiji cha Kibaoni
   Kinana akikunjua bendera wakati wa uzinduzi wa Tawi la CCM la Vijana akatika Kijiji cha Nanyamba
   Kinana akitoka kukagua mradi wa maji katika Kata ya Nanyamba Mtwara Vijijini
   Vijana wakicheza ngoma ya madudu katika mkutano uliofanyika katika Kata ya Nanyamba

   Kinana akikagua ujenzi wa Kituo cha Afya cha Nanguruwe kinachotarajiwa kuwa hospitali ya wilaya Mtwara Vijijini
  Kinana akishiriki katika ujenzi wa Kituo cha Afya cha Nanguruwe
   Wananachi wakimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipowasili Wilaya ya Mtwara Vijijini, wakati wa ziara yake ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG


   Kinana akizungumza wakati wa mapokezi katika Kijiji cha Kibaoni, Mtwara Vijijini leo.
   Kinana akihutubia katika mkutano uliofanyika Katika Kijiji cha Nanguruwe, Wilaya Mtwara Vijijini
   Mzee Ismail Lumbeya (95), akisikiliza kwa makini wakati Kinana akihutubia katika mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Nanguruwe

  0 0

   Mkurugnezi Mtendaji wa Kampuni ya Kitanzania ya  MaxCom Africa, inayotoa huduma za Max Malipo,  Juma Rajabu  na Mwakilishi wa Manispaa ya Kinondoni, Richard Chagula wakikata utepe kuzindua muonekano mpya wa huduma ya Max Malipo, katika hafla iliyokutanisha uongozi wa kampuni hiyo ya Jukwaa la Wahariri, leo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
   Mkurugnezi Mtendaji wa MaxCom Africa, watoaji wa huduma za Max Malipo, Juma Rajabu akizindua muonekano mpya wa huduma ya Max Malipo itakavyokuwa sasa kwenye ofisi za mawaakala wake.
   Mkurugnezi Mtendaji wa Kampuni ya Max Com Africa, watoaji huduma za Max Malipo, Juma Rajabu akimkabidhi mfano wa hundi ya sh. milioni 10, kwa Mwakilishi wa Manispaa ya Kinondoni, Richard Chagula, kuashiria kampuni hiyo kutoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya ujenzi wa maabara katika shule zilizomo katika Manispaa hiyo, wakati wa hafla ya kampuni hiyo kutimiza miaka mitano ambapo uongozi ulikutana na wadau wakiwemo Jukwaa la Wahariri katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo.

  0 0

   Ajali ya Helicopter ya Maliasili na Utalii imegharimu maisha ya marubani 3 wa Jeshi la Polisi Tanzania. Sp Kidai Kaluse, Insp.Simba Must Simba, Pc. Josso Selestine, Na rubani mmoja Capt. Khalfan,Ajali  hiyo imetokea huko Kipunguni B Moshi Bar,Ukonga-Ilala jijini Dar es Salaam. Chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikaa mpaka sasa.
   Sehemu ya mabaki ya Helikopta baada ya kuanguka
   Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova
  akifafanua jambo mbele ya Vyombo vya habari katika eneo la ajali,kufuatia kutokea kwa ajali hiyo iliyopelekea vifo vya watu wanne
   Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaa,Mh.Sadick Meck Sadick akizungumza mbele ya Vyombo vya habari katika eneo la ajali,kufuatia kutokea kwa ajali hiyo iliyopelekea vifo vya watu wanne
   Baadhi ya Wataalamu wakifanya uchunguzi wa chanzo cha ajali hiyo ya Helikopta.
   Baadhi ya Watu wakishuhudia mabaki ya helikopta hiyo iliyopata ajali maeneo ya Kipunguni B Moshi Bar,Ilala jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Utamaduni, Michezo, Habari na Vijana Dkt. Kissui S. Kissui akifungua Rasmi Kongamano la Ulingo wa Maendeleo ya Biashara na Uchumi Karakana ya wajasiliamali uliofanyika Wazo Hill Tegeta, Katika Hotuba yake aliwapongeza PSPF kwa kujitoa kuwasaidia wajasiliamali kuwekeza kupitia Fao lao la Ujasiliamali na Kujiunga katika mfuko wa uchangiaji wa Hiari wa PSS, Pia aliwapongeza Haiba Foundation kwa kuwasaidia wajasiliamali wadogo wadogo na Mwisho alitoa somo maalum kwa ajili ya kuwasaidia wajasiliamali jinsi ya kupata Kipato na kujua matumizi mazuri ya Fedha.
   Afisa Masoko kutoka PSPF Eliachi Remmy akitoa maelezo ya Kina juu ya Mfuko wa Uchangiaji wa Hiari wa PSS ambapo alisema kuwa mfuko huu ni Ruhusa kuwa mwanachama ukiwa raia au asiye raia wa Tanzania na anayefanya kazi nje au ndani ya nchi pia kujiunga katika mfuko huu wa PSS ni Bure kabisa. Aliongeza kuwa kama Mjasiliamali mfuko huu ni muhimu kwake kwa kuwa anaweza kulipia kirahisi kabisa hata kupitia mitandao yote ya simu. Pia alizungumzia kwa kina Mafai mbalimbali yanayopatikana PSPF kupitia Mpango wa Hiari ikiwa ni pamoja Fao la Elimu, Fao la Ujasiliamali,Fao la Uzeeni, Fao la kifo na Fao la Ugonjwa/ Ulemavu Mwisho aliwasisitiza wajasiliamali kujuinga na mfuko huo wa PSS na kuwaeleza juu ya Mkopo wa Nyumba.

   


   Washiriki ambao ni wajasiliamali katika mambo Mbalimbali wakiwepo wauza Ubuyu, Karumati, Mkaa, Kuku, Magenge ya Mboga, Matunda, Maziwa, Chips, Mgahawa, na mengine mbali mbali wakiwa wanafuatilia kwa Makini Kongamano la Ulingo wa Maendeleo ya Biashara na Uchumi Karakana ya Wajasiliamali  Wazo Hill Tegeta .

   Afisa Masoko kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Michael Leon Kazimili akizungumza kwa kina Faida za Kuwekeza PSS pia alitoa tofauti kati ya Kuwekeza PSPF na katika mabenki na kusisitiza kuwa kuna faida kubwa kama mtu akiwekeza katika Mifuko ya Jamii hasa PSPF kwamba kuna faida kubwa ya asilimia 6% kama ukiwekeza PSPF, Pia alizungumzia mkopo wa nyumba ambapo alisema kwamba Mwanachama wa PSPF awe ni wa Kuchangia kwa Lazima au kwa Hiari atapata Mkopo wa Nyumba na atalipia kwa muda wa Miaka 25 kwa kuzingatia Taratibu za Mfuko.
   Mwenyekiti wa  Karakana ya Haiba Foundation Mzee Adam Kaira akitoa utangulizi kwa wajasiliamali ambapo alitoa mwelekeo wa Haiba Foundation pia alieleza kuwa kuna mpango wa kuanzisha Benki ambayo itawasaidia wajasiliamali aliongeza kuwa mpaka sasa Haiba Foudation imefanikiwa kuwa na vikundi 75 ambavyo vinafanya vizuri, Pia aliongezea kuwa wajasiliamali wanaweza kupata Mkopo kuanzia Tsh 400,000 hadi 1,000,000 na kuna wanachama walishapata, mwisho alizungumzia juu ya wajasiliamali kuwekeza katika Mfuko wa Uchangiaji wa Hiari wa PSS ambapo utawasaidia zaidi katika kuboresha maisha yake.
   Mkurugenzi wa Haiba Foundation Adam Ngamage akitoa mada juu ya Haiba ya Ujasiliamali ambapo alisisitiza Jinsi gani Mjasiliamali anaweza kubadili mwenendo wake wa kuwa mfanyabiashara mzuri na mbinu mbali mbali za kufanya Biashara yake iweze kwenda mbele bila kukwama Mwisho alizungumzia umuhimu wa kuwekeza kupitia Mfuko wa Pensheni wa PSPF
   Mkurugenzi Mtendaji wa Twiga-Kuku Gren Mushi Maarufu kwa Mama Kuku akizungumzia ujasiliamali lakini hasa huu wa ufugaji wa Kuku ambapo yeye ni mzoefu wa muda mrefu na ameanza tangu miaka ya 1970, alizungumzia jinsi gani wajasiliamali ambavyo wanaweza kusaidiana katika njia mbalimbali, aliongeza amesisitiza Biashara ya kuku sasa inakuwa sana na amesema kuna mpango wa kuanzisha Jokofu ya kuuzia kuku ambayo yatakuwa katika maeneo mbalimbali yakiuza kuku kwa vipande ili kila mwananchi anayehitaji kuku apate kitoweo hicho. Mwisho aliwashukuru kwa Dhati PSPF kwa moyo wao wa Dhati
   Muwezeshaji wa Kongamano hilo  kutoka Haiba Foundation Chonya Libe akiendelea kutoa Mwongozo .
   Afisa Masoko kutoka Mfuko wa PSPF David M. Mgaka akiwagawia Fomu za Mpango wa Uchangiaji wa Hiari PSS wajasiliamali wote waliofika katika Kongamano hilo.
   
  Maafisa kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF wakifuatilia kwa makini Kongamano hilo la Wajasiliamali
  Baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa Makini Kongamano hilo
   Baadhi ya Washiriki wakijiunga na Mfuko wa kuchangia kwa Hiari wa PSS


  0 0

  Rais Kikwete akizungumza na Wanahabari kwenye ukumbi maalum wa mikutano,Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jiini Dar,mara tu baada ya kuwasili jiioni hii akitokea nchini Marekani kwa matibabu.

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimshukuru  Mama Maria Nyerere baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Majeshi Jenerali davis Mwamunyange baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiongea na Mama Maria Nyerere aliyefika kuwapokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na waandishi wa habari na viongozi mbalimbali waliokuja kumlaki baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea mashada ya maua kutoka kwa wafanyakazi wa Ikulu waliojitokeza kumpokea mara baada ya kuwasili Ikulu akitokea nchini Marekani kwenye matibabu. Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue aliyeongoza mapokezi hayo ya Ikulu 
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea kadi ya pole toka kwa mjukuu wake Aziza Ridhiwani Kikwete mara baada ya kuwasili Ikulu.


  0 0

  Mrakibu wa Polisi-Captain Kidai Senzala Kaluse enzi za uhai wake. 

  Familia ya Mzee Senzala Kaluse wa Kimara Mwisho Dar es Salaam, inasikitika kutangaza kifo cha mtoto wao KIDAI SENZALA KALUSE kilichotokea Novemba 29, 2014 Saa 4 asubuhi kwa ajali ya Helkopta huko Kipunguni B, Moshi Bar Dar es Salaam.

  Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa baba yake Mzee Kaluse, Kimara Mwisho. Habari ziwafikie, Ukoo wote wa Warutu, Ukoo wa Kaluse, Ukoo wa Mroki, Familia yote ya Timothy Nathan, Ukoo wa Kajiru na Taluka, Wakamba wote wa Ugweno Msangeni, Bibi wa Marehemu Mary Nathan wa Kinyenze- Morogoro, Familia ya Tarimo ya Ukonga Mombasa, Omary Msuya wa Moshi, Abdalh Mgonja wa Gonja Maore, Hosea wa Arusha.

  Taarifa pia ziwafike maofisa wa Jeshi la Polisi Tanzania, Askari wa Kikosi cha Polisi Anga, Ndugu, Jamaa na Marafiki popote pale walipo.

  Misa ya kuaga Mwili wa Marehemu itafanyika mnyumbani kwao kuanzia Saa 6:00 kabla ya safari ya kuelekea Gonja Maore, Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro kuanza na mazishi yatafanyika Jumatatu Kijijini Kwao Gonja Maore.  

  Mawasiliano zaidi: Mroki Mroki- +255 717002303. 
   MATAYO 5: 4 HERI WENYE HUZUNI; MAANA WAO WATAFARIJIKA

  0 0

   Mkufunzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wafamiasia wa vituo vya afya Zanzibar Ali Shaaban akitoa neno la shukrani kwa wanafunzi wake (hawapo pichani) wakati wa kuyafunga mafunzo hayo katika Hoteli ya Masons, Shangani Mjini Zanzibar.
   Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya wafamasia wakifuatilia ufungaji wa mafunzo yao yaliyochukua sita tano katika Hoteli ya Mazsons, Shangani.
   Mkurugenzi bohari kuu ya dawa Zanzibar Zahran Ali akimkabidhi cheti kwa mfamasia Issa Ahmada kutoka kituo cha afya cha Jambiani baada ya kumaliza mafunzo yaliyofanyika Hoteli ya Mazsons, Shangani.
   Mkurugenzi wa Bohari kuu ya dawa Zanzibar Zahrani Ali akizungumza na washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wafamasia wakati wa kuyafunga mafunzo hayo katika Hoteli ya Mzsons, Shangani.
  Picha ya pamoja ya washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wafamasia na wakufunzi wao baada ya kumaliza mafunzo yao katika Hoteli ya Mazsons, Shangani.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wa tatu kutoka (kushoto) Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto, (kushoto kwake) Makamu wa Rais kwanza wa Burundi, (kulia kwake) wakijumuika kwa pamoja na viongozi  wengine wakionyesha Taarifa ya pamoja waliyoisaini kuhusu majadiliano ya kuimarisha Miundombinu kwa nchi wanachama wa  Jumuiya ya Afrika Mashariki, katika mkutano wa 3 wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Miundombinu, uliofanyika kwenye Ukumbi wa KICC, jijini Nairobi jana Novemba 29, 2014. Picha na OMR.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza katika mkutano wa 3 tatu wa wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu miundombinu, uliofanyika katika ukumbi wa KICC jijini Nairobi jana Novemba 29, 2014. Picha na OMR.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya viongozi wakati  wakitoka kwenye Ukumbi wa mikutano wa KICC, baada ya kushiriki katika mkutano wa 3 wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Miundombinu uliofanyika jijini Nairobu, Kenya jana Novemba 29, 2014.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi 
  wengine walioshiriki katika mkutano huo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kifurahia jambo na Makamu wa Rais wa  Kenya William Ruto na Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, wakati wakiondoka katika viwanja vya Ukumbi wa mikutano wa KICC, baada ya kushiriki kwenye mkutano wa 3 wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Miundombinu, uliofanyika jijini Nairobi, Kenya jana Novemba 29, 2014. Picha na OMR


  MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI (EAC) KUHUSU MIUNDOMBINU JIJINI NAIROBI, KENYA
  Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal jana Novemba 29, 2014 aliiwakilisha Tanzania katika mkutano wa siku moja wa Wakuu wa Nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Nairobi, Kenya. Mkutano huo, kwa mujibu wa utaratibu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, unafanyika kila baada ya miaka miwili na lengo lake kuu ni kufanya tathmini juu ya miradi ya miundombinu inayoshirikisha nchi washirika, sambamba na kutazama fursa ya kutanua miundombinu mipya katika nchi hizi kwa lengo la kukuza uchumi wa pamoja kwa nchi za Afrika Mashariki.
  Tathmini hii ya Miundombinu inafanyika kwa kuwa mataifa ya Afrika Mashariki yanatambua umuhimu wa kuwa na miundombinu bora katika nchi hizi ili kuharakisha ukuaji wa uchumi, sambamba na kutanua mtengamano wa nchi hizi na hivyo kuwafanya wananchi wanaoishi ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuzidi kuwa wamoja.
  Mkutano wa jana uliongozwa na Kaimu Rais wa Kenya Mheshimiwa William Ruto na kuhudhuriwa na Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Bilal, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Burundi, Waziri Mkuu wa Rwanda pamoja na Waziri wa Afrika Mashariki wa Uganda. Viongozi wengine waliopata nafasi ya kuhudhuria mkutano huo ni pamoja na Mheshimiwa Balozi Richard Sezibera, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Waziri wa Wizara hiyo kutoka Tanzania, Mheshimkiwa Samwel Sitta, Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Dkt. Donald Kaberuka, Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Ukanda wa Afrika, Bwana Makhtar Diop, Katibu Mtendaji wa UNCTAD, Dkt. Mukhisa Kituyi na Baalozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Balozi Filiberto Sebregondi. Pia mkutano huo ulihudhuriwa na wawakilishi wa nchi za China, Marekani, Japan na nyinginezo ambazo ni wadau wakubwa wa ujenzi wa miundombinu katika nchi za Afrika Mashariki.
  Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Kaimu Rais wa Kenya, William Ruto alifafanua juu ya umuhimu wa kuhakikisha Afrika Mashariki inaunganishwa kwa miundombinu imara ili kukuza uchumi na akapongeza jitihada mbalimbali zinazofanyika katika kufanikisha azma hiyo huku pia akiomba nchi wanachama wa Afrika Mashariki kuendelea kuungana katika kutekeleza miradi ya miundombinu na kujitahidi kutafuta fedha kwa ajili ya kukamilisha miradi hiyo.
  Mkutano huu pia uliambatana na kupokea ripoti ya utekelezaji wa maagizo ya Wakuu wa Nchi za EAC kuhusu Miundombinu kutoka kwa Mawaziri wa Nchi za Jumuiya.  Wakuu wa Nchi katika Mkutano huu walipokea taarifa ya utekelezaji wa maagizo waliyoyatoa katika mkutano wa pili uliofanyika mwezi Novemba, 2012 na kuidhinisha miradi 72 ya miundombinu ya kipaumbele ya Barabara, Reli, Nishati na Bandari.
  Kwa upande wa utekelezaji; miradi 16 imekamilika, 39 inaendelea kutekelezwa na 17 ipo katika hatua za awali za kutafutiwa fedha kwa ajili ya utekelezaji wake.
  Kwa upande wa Tanzania miradi minne imekamilika ambayo ni Umeme katika mji wa Kibondo, mradi wa barabara ya Mbezi-Shule-Tangibovu-Makutano ya Nelson Mandela na barabara ya Tabata. Barabara nyingine iliyokamilika ni Nyangunge – Musoma – Sirari na sehemu ya Simiyu - Musoma inayounganisha Kenya na Tanzania huko ujenzi unaendelea.
  Akizungumza katika Mkutano huo Makamu wa Rais amezitaka nchi wanachama kuharakisha utekelezaji wa miradi ya Miundombinu ili kusaidia utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja, ambayo inalenga kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na abiria. “Tusiishie kubakiza mipango hii katika karatasi, tusiishie kuzungumza tu bali huu ni wakati wa kuhakikisha tunarahisisha ufanyaji biashara katika nchi zetu na kupunguza vikwazo visivyo vya lazima,” alisema Mheshimiwa Makamu wa Rais.
  Katika mkutano huo, Mheshimiwa Makamu wa Rais pia aliambatana na Mheshimiwa Dkt. Mahadhi J. Maalim, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara wa Zanzibar, Mheshimiwa Nassor Ahmed Mazrui. Mheshimiwa Makamu wa Rais na msafara wake tayari wamerejea nyumbani Tanzania ambapo kesho anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, maadhimisho yanayofanyika Kitaifa Mkoani Njombe.
  Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
  Novemba 30, 2014

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuini ya Ushushaji Mizigo Bandarini Tanzania International Cpontainer Termi nal (Ticts) Paul Wallace akipeana mikono na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mivinjeni baaada ya kuwakabidhi msaada wa vitabu.
  Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuini ya Ushushaji Mizigo Bandarini Tanzania International Container Terminal (Ticts) Paul Wallace akiwakabidhi Vitabu wanafunzi wa Shule ya msingi Mivinjeni .
  Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Ushushaji Mizigo Bandarini Tanzania International Container Terminal (Ticts), Paul Wallace (kushoto) akimkabidhi Moja ya Vitabu walivyokabidhi kwa Mwalimu Mkuu ya Shule ya Msingi Mivinjeni Dar es Salaam, Sabas Selestian juzi wapili (kulia) ni Diwani wa Kurasini, Wilfred Kimath na Mwenyekiti wa Bodi shule hiyo, Elijius Anold.

  0 0

  MWANAMUZIKI wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Nasib Abdul, Diamond Platinum  anashindana na aliekuwa mpenzi wake Wema Sepetu katika kuwania Tuzo ya Mtu mwenye ushawishi mkubwa katika mitindo. 

  Tuzo hiyo zitatolewa kwenye Onesho la Mavazi la Swahili Fashion 2014 linaloandaliwa na Kampuni ya 361 Degrees na zitatolewa siku ya mwisho katika onesho la Swahili Fashion Week litakaloanza Desemba 5 hadi 7 mwaka huu.

  Katika shindano hilo wanaoshindana wengine ni pamoja na Mwamvita Makamba            ambae namba yake ya kupigiwa kura ni SFW SY 01, Diamond Platnumz       SFW SY 02, Millen Magesse   SFW SY 03, Mohamed Dewji  SFW SY 04 na Wema Sepetu           SFW SY 05.

  Pia Diamond anashindana katika kipengele cha wanaume wenye kuongoza huku namba yake ya ushiriki ikiwa ni SFW SMP 01 na anaochuana nao katika kipengele hicho ni pamoja na Luca Neghesti        SFW SMP 01,  Baraka Shelukindo       SFW SMP 03, Noel Ndale        SFW SMP, Rio Paul      SFW SMP 05 na           Juma Juxx        SFW SMP 06

  Akizungumza na waandishi wa habari mratibu wa tuzo hizo, Haruna Ibrahim alisema kuwa kwa mwaka huu kuna ushindani mkubwa katika kila kipengele. Aliongeza kuwa Meneja wa Msanii Wema Sepetu, Martin Kadinda nae anawania kipengele cha Mbunifu bora wa mchango katika tasnia hiyo ambapo anashindana na  akina PSJ Couture    SFW MWD 01.

  Martin Kadinda.          SFW MWD 02 Mtani Nyamakababi    SFW MWD 03, Manju Msitta  SFW MD 04 na Gabriel Mollel  SFW MWD 05.

  Aliongeza kuwa pia kwenye kipengele cha mbunifu wa mavazi bora wa mwaka wanaoshindania Kadinda anashindana akiwa anaumana na akina Gabriel Mollel        SFW ID 02, An Nisa Abayas     SFW ID 03, Eve Collections            SFW ID 04

  Alisema kuwa kwa upande wa Baileys, mwanamitindo bora wa kike kwa mwaka huu wanaoshindana ni             Jamilla Nyangassa      ambae namba yake ya kupigiwa kura ni SFW FM 01, Gyver Meena            SFW FM 02,  Jihan Dimachk      SFW FM 03, Neema Kilango   SFW FM 04,     Joceline Maro, SFW FM 05, Lethina Christopher            SFW FM 06.

  Kwa upande wa wanamitindo bora wa kiume wanaoshindania tuzo hizo ni pamoja na Danny  David        SFW MM 01, Victor Casmir SFW MM 02,          Dietrich luhanga         SFW MM 03,  Ally Daxx          SFW MM 04.
  Haruna aliongeza kuwa kwa upande wa Tuzo za Mwanamitido bora wa mwaka kwa Afrika Mashariki wanaoshindaniwa ni pamoja na Vivian Mutesi (UGANDA)    SFW EAM, Sharon Mirembe Sanya (UGANDA)          SFW EAM 02, Christina Masese (KENYA)   SFW EAM 03, Ajuma Nasenyana (KENYA)      SFW EAM 04                                                                                      

   Aliongeza kuwa kwa upande wa Tuzo ya Mbunifu wa mwaka wanaoshindania ni pamoja na Kiki's Fashion    SFW DY 01, Jamilla Vera Swai            SFW DY 02, Ailinda Sawe        SFW DY 03,An Nisa AbayasSFW DY 04, Manju Msita        SFW DY 05, Lucky Creations   SFW DY 06
  Pia aliongeza kuwa kutakuwa na tuzo ya mwaka kwa mtaalamu wa urembo na nywele na wanaoshindaniwa ni pamoja na Rehema Samo      SFW HMA 01, Asila Makeup   SFW HMA 02, Glambox          SFW HMA 03, Lavie Makeup Studio            SFW HMA 04.

  Pia wanaoshiriki katika kipengele cha kushindani tuzo ya vidani ni The Mabinti Center     SFW AD 01, Enjipai Jewelleries      SFW  AD 02, Florinyah Designs           SFW AD 03, Sairiamu  SFW AD 04, Linda August        SFW AD 05 na Nyumbani DesignsSFW AD 06.

  Watakaoshindania tuzo katika kipengele cha mbunifu wa Afrika Mashariki wanaoshindania ni pamoja na             Martha Jabo (Uganda)            SFW EAD 0, Afrostreet Kollektions (Kenya)    SFW EAD 02, Arapapa by Santa Anzo (Uganda)            SFW EAD 03, Akinyi Odongo (Kenya)  SFW EAD, Kiko Romeo (Kenya)           SFW EAD 05 na Mille Colliness (Rwanda)        SFW EAD 06.

  Swahili Fashion Week na Tuzo za mwaka 2014 zinaandaliwa na 361 Degrees kwa usaidizi wa Hotel Sea Cliff, Sea Cliff Court, chini ya udhamini wa EATV, East Africa Radio, Baileys, Mercedes-Benz,  2M Media, Tanzania Printers LTD and Syscorp Media na Basata.

  0 0

  Mgeni rasma ambaye ni DR kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana DR. Natalius Kapilima akikata utepe kuashilia kugawa zawadi mbalimbali kwa wagojwa wa saratani waliolazwa katika hospital ya ocean road wengine kushoto ni Mkurugenzi wa TTCF. Lutgard Kagaruki na wa tatu kulia ni Mratibu wa kampeni ya manusura wa saratani ya Tezi Dume na Mwanzilishi wa Tanzania 50 Plus Campagn Dr Emanuel Kandusi
  DR kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana DR. Natalius Kapilima kulia akimkabizi zawadi mgojwa wa saratani Idd Muhode ambaye amelazwa katika hospitali ya ocean road
  Baadhi ya wadau mbalimbali wa kujitolea kutoka Tanzania 50 plus campaign wakiwa katika picvha ya pamoja baada ya kutoa misaada mbalimbali kwa wagojwa wa saratani katika hospital ya Ocean Road.

  DR kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana DR. Natalius Kapilima akipokea zawadi za wagojwa zilizoenda kugawiwa katika hospitali ta Ocean Road kutoka kwa
  Mratibu wa kampeni ya manusura wa saratani ya Tezi Dume na Mwanzilishi wa Tanzania 50 Plus Campagn Dr Emanuel Kandusi mwingine ni
  Mkurugenzi wa TTCF. Lutgard Kagaruki walipokwenda kutoa misaada mbalimbali kwa wagojwa
  vitu mbalimbalio vikipakiwa kwenye mfuko kwa ajili ya kugawa kwa wagojwa
  vifurushi vikiwa tayali kwa kugawiwa kwa wagojwa wa saratani katika hospitali ya ocean road

  Mratibu wa kampeni ya manusura wa saratani ya Tezi Dume na Mwanzilishi wa Tanzania 50 Plus Campagn Dr Emanuel Kandusi kulia akimkabizi zawadi mgojwa Said Kassam aliyelazwa katika hospital ya Ocean Road

  0 0

  Dr Nelson Ishengoma akiwa katika pozi mara baada ya kutunukiwa shahada yake ya udaktari katika Mahafali ya Tano ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) yaliyofanyika jana katika viwanja vya Chimwaga vilivyopo Chuoni hapo.
   Hongera sana Mwalimu wangu na sasa Mwanzo wa Jina linaanza na Dr. Sio kazi rahisi lakini Mungu ameweza kukusimamia na kukuongoza. Nakuombea kwa Mungu ufanikiwe zaidi na zaidi. Kutoka Kwa Mwanafunzi wako  Josephat Lukaza

  0 0

  kansolele
  Inaniwia vingumu sana kutoa shukrani kwa mtu mmoja mmoja au makundi kutokana na ushirikiano wenu katika kipindi kigumu cha msiba na mazishi ya mpendwa mume wangu na mwenyekiti wa Dorka catering na Dorka group of company Marehemu Dr kephas kansolele Ntevi kwaniaba ya familia yangu .

  Ninapenda kutoa shukrani za dhati kwa wote walio shiriki kwa njia moja au nyingine kwa kipindi chote cha msiba wa mume wangu.Kiukweli tulipatwa na kigugumizi ambacho hakisemeki Ingawa nyote mnastahili kushukuriwa lakini ningependa kutoa shukrani zangu za peke kushukuru madaktari wa Muhimbili na manesi kwenye kitengo cha I.C.U , Dr Kalianyama mlifanya kazi usiku na mchana kuokoa maisha ya mume wangu lakini mungu alimpenda zaidi, kanisa la Good News Mission Tanzania Pastor kiongozi Jeong na ma pastor na waumini wote hamkuchoka kutuombea na bado mnatuombea tuna shukuru sana, Service Provider wezangu kiukweli mmenionyesha upendo ambao hausemeki, Marafiki zangu na wa familia mlikua na sisi usiku na mchana hamkutuacha, Networks wote waliokua wana shirikiana na mume wangu .

  Blogs mbalimbali, majirani zetu wa mwenge na Bahari beach , Familia ya Ntevi, Familia ya Wakaombwe na ya Mzee Massau tunapenda kuwashkuru wote kwa upendo na faraja zenu, Sina maneno mazuri ya kuonyesha shukurani zetu za dhati kwa niaba yangu na wanangu, tunaomba mpokee shukurani zetu mwenyezi mungu awaongezee pale mlipo toa. 

  Tutakua na Ibada ya shukurani nyumbani kwa marehemu kunduchi njia panda ya madini.
  Ratiba itakua kama ifuatavyo

  Tarehe ::5/12/2014 mkesha Ibada na dinner (BBQ Night)
  Tarehe ::6/12/2014 kuanzia saa 2 asubuhi wageni kuwasili na saa nne (BRUNCH) Hadi saa tano mchungani wa Good News mission atapowasili na saa tano na nusu ibada neno la shukrani ya familia
  kwa mawasiliano ::+255718 661 705 / +255717 056 598
  Bwana ametoa na ametwaa
  Wote mnakaribishwa kushirikiana na sisi kumtolea mungu shukrani

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa mjini Mtwara katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye  viwanja vya Mashujaa mjini humo akihitimisha ziara yake ya siku 16 aliyoifanya katika mikoa ya Lindi na Mtwara akikagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 inayotekelezwa na serikali kwa kushirikiana na wananchi wenyewe na kuhimiza uhai wa chama cha Mapinduzi CCM, Katika ziara hiyo Katibu mkuu huyo aliongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi.

   Katika Mkutano huo Kinana amempa wiki mbili Waziri wa Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe kutoa maelezo kwanini bidhaa mbalimbali hazisafirishwi kwenda nje kupitia bandari ya Mtwara, Lakini pia Kinana amewaagiza Waziri wa Nishati na Madini kutoa maelezo ni kwanini wawekezaji wenye kampuni zinazofanya shughuli zao mtwara wanalipia kodi zao jijini Dar es salaam badala ya kulipia mkoani Mtwara ambako wanafanya shughuli zao, Pia waziri wa Ofisi ya Mkamu wa Rais Mazingira amepewa mwezi mmoja kuhakikisha dampo la taka za sumu zinazotupwa na wachimbaji wa gesi na viwanda kuacha mara moja kwa sababu zinahatarisha maisha ya wakazi wa Mtwara.

  Mwisho akaagiza Ofisi ya Waziri Mkuu kutoa kibali cha kugawa viwanja katika manispaa ya Mtwara kwani viwanja vimeshapimwa, Fedha za kulipa fidia zipo ila kibali kutoka ofisi ya Waziri mkuu ndiyo kimkwama kwa muda wa mwaka mmoja sasa.
    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mashujaa mjini Mtwara.
   Wananchi wakinyoosha mikono yao juu kufurahia hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipokuwa akiwahutubia.
   Mbunge wa jimbo la Mtwara mjini Mh. Hasnein Murji akiwahutubia wapiga kura wake ambao walifurahia sana hotuba yake kwenye viwanja vya Mashujaa mjini Mtwara.
   Umati wa wananchi ukiwa umefurika katika mkutano huo.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MTWARA)
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa na viongozi mbalimbali katika meza kuu wakati wa mkutano huo.
   Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiwahutubia wananchi katika mkutano huo.
   Ndugu Abdulrahman Kinana na Nape nnauye wakiingia katika uwanja wa mkutano.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangali vikundi vya ngoma mara baada ya kuwasili katika mkutano wa hadhara.

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa tatu kutoka kulia Nape Nnauye na viongozi wa mkoa wa Mtwara wakiwasili katika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Mashujaa mjini Mtwara leo.

  0 0

  DSC_0202

  Afisa Ardhi na Mazingira wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala (Kahama), Zablon Donge, akifungua rasmi warsha ya siku tatu ya wadau wa mapambano dhidi ya UKIMWI kwa niaba ya Mkurugenzi wa wilaya hiyo, iliyofanyika Kata ya Segese wilayani Kahama mkoani Shinyanga. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues pamoja na Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias.

  Na Mwandishi Wetu, Kahama.
  MKURUGENZI Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues ametaka jamii kujumuisha suala la utamaduni katika kupambana na maambukizi mapya ya Ukimwi.

  Alisema hayo kwenye warsha ya siku tatu ya wadau wa mapambano dhidi ya UKIMWI inayofanyika Kata ya Segese wilayani Kahama mkoani Shinyanga. Alisema katika ufunguzi huo kwamba kwa miaka mingi pamoja na kuwepo kwa elimu ya UKIMWI, kumekosekana mabadiliko yanayotakiwa kukabili maambukizi mapya.

  Alisema UNESCO iliangalia tatizo hili na kubaini kwamba kutobadilika kwa hali kumetokana na kutounganishwa kwa kipengele cha mila ambacho ndicho kinachofanya kuwepo na mazingira rafiki ya kupashana habari.
  DSC_0151
  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akizungumza na washiriki wakati wa uzinduzi wa program ya utamaduni kukabili UKIMWI itakayoendeshwa na shirika lake.


  Warsha hiyo ya Siku tatu imelenga katika kuhamasisha jamii, Shule, Asasi, Taasii za Dini na Serikali katika utoaji wa Elimu sahihi ya huduma rafiki za Afya ya Uzazi, VVU/UKIMWI, ujinsia na maadili ya Afya kwa vijana balehe na vijana.

  Amesema mpaka sasa utoaji wa elimu ya afya, ueleweshaji wa ugonjwa haujafanya mabadilikoya kutosha kutokana na ukweli kuwa katika utekelezaji wa kampeni masuala ya utamaduni na uwasilishaji wa taarifa haukuwa umezingatiwa.

  Alisema wakati Kahama (Msalala) kwa sasa kiwango cha maambukizi ni asilimia 5.9, Juhudi zinatakiwa kufanywa katika kuhakikisha kwamba elimu inayotolewa inahusishwa na masuala ya kitamaduni ili kubadilisha maisha ya wakazi. Alisema katika mapambano ya maambukizi mapya mila na utamaduni zinaweza kabisa kusaidia kukabiliana na maambukizi ya UKIMWI.
  DSC_0348
  Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias akielezea madhumuni ya warsha hiyo ya siku tatu iliyojumuisha makundi mbalimbali ikiwemo Waganga wa jadi, wakunga wa jadi, viongozi wa dini, viongozi wa vijiji na kata, walimu, wataalamu wa afya na elimu na Asasi zisizokuwa za kiserikali.

  Alisema program inayoangaliwa sasa ni ile iliyoleta mafanikio katika nchi kadhaa za Afrika ikiwamo Msumbiji na hivyo wanaona waijaribu Tanzania katika wilaya sita ikiwemo Kahama na hasa halmashauri ya wilaya ya Msalala.

  Alisema pamoja na watu wengi kutibiwa na waganga wa kienyeji ni vyema watengeneza sera na watu wengine kutambua umuhimu wao ili kwa kupitia mila waweze kuwafunua watu akili na kujikinga na maambukizi ya UKIMWI. Alisema anaamini kuwa mila na tamaduni zikitumika vyema na hata matibabu zitasaidia kuokoa maisha ya wengi na pia kuzuia maambukizi mapya.

  Alisema maambukizi mapya ni tatizo kwa sasa hasa ikizingatiwa kwamba wananchi wengi wanajua uwapo wa UKIMWI lakini ufahamu ni mdogo kwa kuwa katika kufundisha watu hawakupewa elimu ya kutosha inayoambatana na kuangalia mila na desturi njema za afya zilizopo.
  DSC_0366
  Afisa afya mkuu kitengo cha elimu ya afya kwa umma-programu ya afya mashuleni kutoka Wizara ya afya na ustawi wa jamii, Avit Maro akielezea jambo kwa washiriki kuhusiana na masuala ya afya ya uzazi wakati wa warsha ya siku tatu ya wadau wa mapambano dhidi ya UKIMWI iliyofanyika Kata ya Segese wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

  Alisema ni vyema wananchi wakatumia mali asili waliyonayo kufundishana juu ya kukabiliana na maambukizi mapya ya UKIMWI. Alisema UNESCO imeamua kuanzisha programu maalumu ya kutumia mila na desturi kukabili UKIMWI kama njia nyingine ya kuoanisha nguvu katika mapambano dhidi ya maambukizi mapya.

  Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala (Kahama), Zablon Donge alishukuru UNESCO kwa kuanzisha program ya kujifunza namna ya kukabiliana na maambukizi mapya ya UKIMWI.
  Alisema ukiwa na halmashauri ya wagonjwa huwezi kuwa na halmashauri kwa kuwa shughuli za kiuchumi na kijamii kushindikana kutekelezwa, na kusema kuja kwa UNESCO ni msaada mkubwa.

  Warsha hiyo imejumisha makundi mbalimbali ikiwemo Waganga wa jadi, wakunga wa jadi, viongozi wa dini, viongozi wa vijiji na kata, walimu, wataalamu wa afya na elimu na Asasi zisizokuwa za kiserikali.
  DSC_0384
  Mkurugenzi msaidizi masuala mtambuka kutoka Wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi, Dkt. Laetitia Sayi akifafanua jambo jinsi wizara yake inavyoshirikisha jamii katika utoaji wa elimu mashuleni hususani afya ya uzazi, VVU/UKIMWI huku ikishirikiana na wadau wao wa karibu UNESCO.
  DSC_0269
  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues, akiendesha warsha hiyo kwa njia ya majadiliano na washiriki juu ya dhana na maana ya balehe, vijana balehe na vijana sambamba na maana ya mimba na ndoa za utotoni.
  DSC_0368
  Pichani juu na chini ni sehemu ya washiriki hao wakifuatilia majadiliano kwenye warsha hiyo ya siku tatu iliyofanyika Kata ya Segese wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
  DSC_0063
  DSC_0257
  Pichani juu na chini ni baadhi ya washiriki wakichangia maoni wakati majadiliano ya kutafuta suluhu ya kupunguza maambukizi mapya ya VVU/UKIMWI, mimba na ndoa za utotoni kwenye jamii zao.
  DSC_0264
  DSC_0096
  Sehemu ya washiriki warsha hiyo kwenye vikundi kazi wakianisha na kubainisha matatizo yanayowakabili vijana balehe na vijana katika jamii zao huku wakiongozwa na Mkurugenzi msaidizi masuala mtambuka kutoka Wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi, Dkt Laetitia Sayi (kushoto).
  DSC_0091
  Mshiriki akiwasilisha kazi za vikundi baada ya majadiliano.
  DSC_0061
  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akifafanua baadhi ya changamoto zilizoanishwa kwenye vikundi kazi na washiriki wakati wa warsha hiyo ya siku tatu.

  0 0
 • 11/30/14--21:10: Article 9


 • 0 0

   Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Emmanuel Humba akisalimiana na wafanyakazi wa mfuko wakati wa hafla ya kumuaga ambapo Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (Tughe) tawi la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), kimemkabidhi zawadi ya sh. milioni 10 aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa mfuko huo, Emmanuel Humba kutokana na kuthamini mchango wake kabla hajastaafu.
  Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (Tughe) tawi la NHIF, Gabriel Ishole (kushoto) akimkabidhi tuzo maalumu Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Emmanuel Humba kutokana na kuthamini mchango wake kabla hajastaafu. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
   Emmanuel Humba akimkabidhi mke wake tuzo maalumu aliyopewa na wafanyakazi wa NHIF baada ya kustaafu.
  Champagne zikifunguliawa.
  Furaha ilitawala ukumbini.
   Cheers kwa afya.
   Kaimu Mkurugenzi Mktendaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Khamis Mdee akigonganisha glasi na Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa mfuko huo, Emmanuel Humba.
   Wafanyakazi wakigonganisha glasi kwa furaha.
  Kila mtu alikuwa na furaha.
   Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa mfuko huo, Emmanuel Humba (kushoto) akigonganisha glasi na wafanyakazi wa mfuko huo.

  Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa mfuko huo, Emmanuel Humba (kulia) akigonganisha glasi na wafanyakazi wa NHIF.
   Ofisa Elimu kwa Umma wa NHIF, Grace Michael (kushoto) akigonganisha glasi na Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa mfuko huo, Emmanuel Humba.
   Wafanyakazi wakifurahi kuagana na Mkurugenzi wao.
   Wafanyakazi wa NHIF wakicheza kwaito
   Kwaito ilipamba moto.
   Kila mtu alionyesha kipaji cjake.

   Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa mfuko huo, Emmanuel Humba akisakata rhumba.
  Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa mfuko huo, Emmanuel Humba akisakata rhumba.
   Wadau wa NHIF wakitafakari


   Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa mfuko huo, Emmanuel Humba akipata chakula cha jioni.
   Mke wa Mkurugenzi Mtendaji mstaafu akipata chakula.
   Katibu wa Tughe tawi la NHIF, Gaudensi Kandyango akipata
  Maofisa wa NHIF wakipata chakula cha jioni.
   Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Emmanuel Humba akitoa neno la shukrani wakati wa hafla hiyo.
   Wafanyakazi wakimtakia mkono wa pongeza Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Emmanuel Humba kwa kazi nzuri aliyofanya kabla hajastaafu. 
  Wafanyakazi wa NHIF wakicheza muziki.
  Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (Tughe) tawi la NHIF, Gabriel Ishole (kushoto) akimkabidhi risiti ya ya Benki ya thamani ya shs. milioni 10 zilizotokana na michango ya wafanyakazi kwa upendo wao kwa Mkurugenzi wao mstaafu, Emmanuel Humba.
   Wafanyakazi wa NHIF wakimpa cheti maalumu kwa kutambua mchango wake.
  Kamati ya maandalizi ikiwa katika picha ya pamoja.
  Kaimu Mkurugenzi Mktendaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Khamis Mdee (kushoto) akimkabidhi zawadi ya picha kumbukumbu Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa NHIF, Emmanuel Humba.
   Kaimu Mkurugenzi Mktendaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Khamis Mdee (kushoto) akimkabidhi picha ya kumbukumbu  Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Emmanuel Humba.
  Pokea picha ya kumbukumbu.
  Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa NHIF akipokea zawadi.
  Picha ya pamoja.
  Wafanyakazi wa NHIF wakiwa na zawadi kwa ajili ya kukabidhi mke wa Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa NHIF.
  Pokea zawadi mama.
  Mke wa Mkurugenzi mstaafu wa NHIF akishukuru kwa zawadi alizopewa na wafanyakazi wa Mfuko huo kutokana na kuthamini mchango wa Mkurugenzi wa NHIF, Emmanuel Humba.
  Wafanyakazi wa NHIF wakiwa na furaha.
  Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa mfuko huo, Emmanuel Humba na mke wake wakifurahia jambo.

older | 1 | .... | 415 | 416 | (Page 417) | 418 | 419 | .... | 1897 | newer