Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 414 | 415 | (Page 416) | 417 | 418 | .... | 1898 | newer

  0 0
 • 11/26/14--20:18: Article 11
 •  
   Shop & Brunch Event
  Saturday 29 November 2104
  Thai Village, Masaki, Dar Es Salaam.
  Time: 10am-6pm
  Entrance is Free
  Welcome Champange on the House & Music
  Invite Family & Friends as you feast & shop.
  See U there!!!

  Karibuni mfanye shopping Thai Village Jumamosi ijayo 29 November 2014.
  Muda: Saa Nne asubuhi mpaka saa kumi na mbili jioni
  Kutakuwa na vitu mbali mbali kama vile nguo, viatu, vitabu nk. Pamoja na hayo kutakuwa na glass of Champange kwa kila antakae hudhuria pamoja na muziki.
  Karibuni.

  0 0

  Mgeni Rasmi Waziri wa Maendeleao ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (MB) akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Mradi wa Ufugaji wa Samaki ndani ya Ziwa Viktoria Kiteule cha Bulamba kwa kutumia teknolojia mpya ya vizimba (Cages). Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Tarime Mhe.John Henjewele, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mara. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Raphael M. Muhuga.
  Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani akipandikiza vifaranga vya samaki ndani ya Ziwa Victoria, mradi unaotekelezwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Wilaya ya Bunda, Kiteule cha Bulamba kwa kutumia teknolojia mpya hapa nchini ya kuzalisha samaki kwenye vizimba.
  Picha ya vizimba ambavyo ufugaji wa samaki umeanza mara baada ya Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi kuzindua mradi huo na kupandikiza vifaranga vya samaki. Mradi unatekeleza na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Wilaya ya Bunda, Kiteule cha Bulamba kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Economic Social Research Foundation (ESRF), Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Ufugaji wa samaki kwa kutumia teknolojia ya vizimba ndani ya Ziwa Victoria, umekuwa ukitekelezwa pia na wenzetu wa Kenya na Uganda ambao wamepiga hatua kubwa.


  0 0

   Mkurugenzi wa kwaya ya ‘Family Singers’ Daniel Misheto (kulia). 

  WAZIRI MKUU, Mizengo Pinda ametajwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa albamu ‘Usilie’ ambayo itapatikana kwenye DVD Desemba 7, mwaka huu.

  Akizungumza Dar es Salaam jana kwenye mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa kwaya ya ‘Family Singers’ Daniel Misheto, alisema hafla hiyo itafanyika kwenye Ukumbi wa PTA uliopo Uwanja wa Sabasaba, Dar es Salaam. Mbali ya uzinduzi huo Misheto alisema pia wasanii mbalimbali wa filamu watanogesha siku hiyo.
   Aliwataja waimbaji wa injili ambao watakuwepo siku hiyo kuwa ni Leah Mudy, AIC (T) Vijana Chang’ombe, Accasia Singers, Papson Mastaki kutoka Kenya na Frank Hume kutoka Boston nchini Marekani watatumbuiza.
  Uzinduzi huu umeratibiwa na Misheto Promotion, ambapo kabla ya uzinduzi huo kutafanyika huduma za bila malipo za kiafya na kitabibu kutoka kwa madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali, ambayo yamekuwa yakiikabili jamii.

  Misheto ameyataja magonjwa hayo kuwa ni moyo, figo, kisukari na mengineyo ambapo huduma hiyo itatolewa na madaktari bingwa nchini. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
  “Huduma hii itaanza saa mbili asubuhi na itatolewa bure, ikiwemo ushauri na kwa wale ambao wataweza kutibika watatibiwa, ila ambao watakuwa kesi zao zimekuwa ni kubwa zaidi watapewa ushauri wa bure wa kuendelea na matibabu katika hospitali kubwa na hakutakuwa na kiingilio," alisema Misheto.

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Newala Kepteni Goerge Mkuchika wakati wa mapokezi wilayani Newala.
   Wafanyakazi wakibangua korosho kwenye kiwanda cha Micronix Newala ambacho kilitembelewa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye yupo kwenye ziara ya kujenga na kuimarisha chama mkoani Mtwara
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuchagua korosho na kuzitenga kutokana na ubora wa madaraja kwenye kiwanda cha Micronix kilichopo Newala mkoani Mtwara.

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kulia)akishiriki kusuka nondo pamoja na mbunge wa Jimbo la Newala Kepteni George Mkuchika kwenye ujenzi wa tenk la maji Kilidu wilayani Newala mkoa wa Mtwara.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua kituo cha afya cha Mkwedu wilayani Newala ikiwa sehemu ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM.
   Jengo la Kituo cha Afya Mkwedu wilaya ya Newala.

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Newala kwenye viwanja vya Mahakama ya Mwanzo ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa Serikali lazima itafute namna ya kuhakikisha uzalishaji wa korosho wote unafanyika nchini kwa kujenga viwanda vya kutosha vya korosho.


   Mbunge wa Jimbo la Newala Kepteni George Mkuchika akihutubia wananchi wa Mkwedu mara baada ya Katibu Mkuu wa CCM kutembelea jengo la kituo cha afya cha Mkwedu wilayani Newala
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwaonyesha wananchi wa Mkwedu kadi ya CUF iliyorejeshwa kwake na Hakika Ibrahim ambaye alirudisha kadi hiyo baada ya kuona na kuelewa utekelezaji wa ahadi za CCM unavyokwenda vizuri.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionnyesha kadi juu zilizorudi kutoka upinzani ambapo wanachama hao kutoka upinzani wameahidi kushirikiana na CCM kwa ajili ya kuleta maendeleo yaTengulengu wilayani Newala.

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Tengulengu baada ya kufungua shina la wakereketwa Tengulengu.
   Kikundi cha Kwaya ya CCM Newala kikitoa burudani kabla ya Viongozi kuhutubia kwenye viwanja vya Mahakama Newala
   Mkuu wa Wilaya ya Newala Ndugu Christopher Magala akiwasalamu wananchi wa Newala mjini wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya mahakama ya mwanzo na mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
   Mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego akiwasalimu wakazi wa Newala ambapo aliahidi kushirikiana nao vizuri
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Newala ambapo aliwaambia vyama vingi vya siasa hawajui walifanyalo na wamekuwa wakifanya shughuli za kiharakati zaidi kuliko siasa na kuwataka wananchi wa Newala waendelee kukiunga mkono chama chenye mfumo madhubuti cha CCM.
   Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Newala Ndugu  Adam Lawi Nangwanda Sijaona  akitangaza rasmi kurejea CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya mahakama Newala.
    Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Newala Ndugu  Adam Lawi Nangwanda Sijaona akivua nguo za Chadema mbele ya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Ndugu Nape Nnauye.
   Wananchi wakishangilia kurejea kwa  Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Newala Ndugu  Adam Lawi Nangwanda Sijaona kwenye mkutano wa hadhara uuliofanyika kwenye viwanja vya Mahakama ya mwanzo Newala
    Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Newala Ndugu  Adam Lawi Nangwanda Sijaona akiwa amekabidhi kadi yake na ya mkewe kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana .
   Mbunge wa Jimbo la Newala Kepteni George Mkuchika akihutubia wakazi wa Newala mjini ambapo alielezea maendeleo ya utekelezaji wa ahadi za CCM kwenye jimbo lake na pia alitaka wakaguzi watumwe jimboni kwake kuja kukagua ulaji unaoendelea kiasi cha kuwakandamiza wakulima wa korosho wilayani Newala.
   Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana akikadidhi pikipiki kwa vijana wa Newala ,pikipiki hizo ni mradi wa CCM wilaya ya Newala kuwakopesha vijana ziwasaidie kwenye shughuli zao za kila siku zikiwemo za boda boda.


  0 0
 • 11/27/14--00:00: Article 7
 • vacancies

  Basically, professionals with this background:
  Required Skills and Experience
  Education:
  At least a Master’s Degree in Business Administration, Finance, Banking or related areas, plus preferably a Bachelor Degree in engineering, finance or economics.

  Experience:
  Preferably a minimum of 5 years of relevant experience;
  Ability to build partnerships and deliver results that meet the needs and long-term interest of clients within and outside the institution;
  Demonstrated experience in preparation of project financial analysis and creation/evaluation of advanced and complex Ms Excel spread sheet financial models;

  Demonstrated experience with private equity/venture investments, credit and risk assessment, with solid financial modelling and risk assessment skills. Project financing experience in the private sector is a plus;
  Demonstrated experience in preliminary evaluation of project proposals for assessing their feasibility for private sector funding and/or technical support by LFI.
  Here is the link with more information

  0 0


  VIWANJA HIVI VIPO KIGAMBONI,KATA YA PEMBA MNAZI,MTAA WA MUHIMBILI (TUNDWI CENTER),VIPO UMBALI WA MITA 600 - 700 KUTOKA BARABARA KUU,NI VIWANJA VILIVYOPIMWA.

  ENEO  LA SHULE NI KWA AJILI YA CHEKECHEA,PRIMARY PAMOJA NA SEKONDARI ,UKUBWA WA ENEO HILO NI  35,022 SQM.
   
  KWA MAELEZO ZAIDI JUU YA VIWANJA HIVYO,WASILIANA NA NDG. JAMES MPAYO KWA NAMBA HIZO HAPO CHINI.
  0784 207877 NA 0754 780878
  PIA UNAWEZA KUMTUMIA EMAIL: 
  JMPAYO@OVI.COM

  0 0

  Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali Mhe Zitto Kabwe akisoma Ripoti ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu akauti ya ESCROW Bungeni Mjini Dodoma leo.
  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Anne Makinda akifafanua jambo wakati akiendesha Bunge hilo leo mjini Dodoma.
  Baadhi ya wahudumu wa Bunge wakigawa Ripoti ya CAG kuhusu akauti ya ESCROW kwa Wabunge
  Waheshimiwa Wabunge wakipitia ripoti ya CAG kwa makini wakati ikisomwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Mhe Zitto Kabwe.

   Mhe Said Arfi akimpongeza Mhe.Zitto Kabwe ,mara Baada ya kumaliza kusoma ripoti ya CAG
  Wabunge wakiwa wamesimama kuashiria kuunga mkono mara baada ya Mhe.Zitto Kabwe kumaliza kusoma ripoti ya CAG BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Lazaro Nyalandu unveils the foundation stone of the Lake Manyara hot springs boardwalk way yesterday.
  Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Lazaro Nyalandu (2nd left) cut off ribbon to officially launch Lake Manyara hot springs boardwalk way and hippo pool view point in Lake Manyara. Others in the picture from left are Manyara Regional Commissioner Hon. Elaston Mbwilo; Director General of TANAPA Allan Kijazi and the Chairman of the Parliamentary Committee on Lands, Natural Resources and Environment Hon. James Lembeli.

  Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Lazaro Nyalandu has commended a remarkable initiative by Tanzania National Parks in introducing new tourism products at Lake Manyara National Park. Nyalandu said this during the official launching of the hot springs boardwalk way and hippo pool viewpoint projects at the park yesterday. Nyalandu said that the two projects will add value to the tourism sector by increasing the number of tourist arrivals in the country and urged other stakeholders to be innovative in introducing products that will attract more tourists.

  The Manyara boardwalk way and hippo pool viewpoint projects worth about 200 millions were initiated to counter the decreased trend of tourist numbers in the park following the flashfloods hit the park in March 2013 which damaged most of tourist infrastructures.

  The first ever tourism product in the national parks, the boardwalk way is featured with 1.5 meters wide impressive wooden structure, creating a 300 meters long trail standing 1.5 meters above ground winding up in an observation platform that is 15 meters long and 2.5 meters wide. The trail meanders through the hot springs and lakeshore around a marsh and finally into the lake. The boardwalk will give visitors a unique view and wonderful photo opportunities at every turn of the boardwalk trail.

  Hot springs boardwalk way is designed to simply give people a nice place to walk along the numerous hot springs and be close to the attractions and enjoy the wide view of the lake.

  Visitors will use the facilities boardwalk way for free and have opportunity of walking around 600 meters on a return trip to the lakeshore and over the hot springs. Educational signage with entertaining themes will be erected in key locations to allow visitors’ easy reading and understanding of the nature and the resources found in the area. These signs will educate visitors about the ecology and adaptation of plants and animals to the area. Moreover, it will explain the fragility of the ecosystem and why it is so important to use the boardwalks to avoid, as much as possible, disturbing the environment.

  Moreover, the viewpoint is a freestanding wooden platform rising by 8 feet above the ground measuring 56 feet in length and 5 feet in width. It is about 8 km away from main gate. Standing at the top of the viewing platform enables the viewer a spectacular view of the marshland and its inhabitants – waterfowl, hippo, buffalo and wildebeest – from a point of vantage while affording the visitor a high sense of security.  0 0

  Mkurugenzi Mkuu  wa TFDA , Bw. Hiiti B. Sillo akitoa hotuba ya TFDA kukubali kujiunga na Umoja wa Nchi za Asia katika Udhibiti wa Vifaa Tiba na Vitendanishi (Asian Harmonization Working Party on medical devices and diagnostics - AHWP) wakati wa mkutano wa mwaka wa AHWP uliofanyika Seoul, Korea Kusini kuanzia tarehe 17 - 21 Novemba 2014. Tanzania imekubaliwa rasmi kuwa mwanachama 24 wa AHWP  ikiwa  ni  nchi  ya pili Barani Afrika kujiunga  na  umoja huo baada  ya Afrika Kusini.
   Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bw. Hiiti B. Sillo akiwa na Mwenyekiti wa umoja huo Dkt. Saleh Al –Tayyar  kutoka Saudi Arabia baada ya kukabidhiwa mwongozo rasmi TFDA wa kuimarisha mfumo wa udhibiti wa vifaa tiba na vitendanishi kama mwanachama mpya wa umoja huo.

  Mwenyekiti  wa AHWP , Dkt. Saleh Al –Tayyar  kutoka Saudi Arabia akiwapongeza Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bw. Hiiti B. Sillo na Meneja wa Udhibiti wa Vifaa Tiba, TFDA, Bi. Agnes Sitta Kijo, baada ya Tanzania kujiunga rasmi kuwa mjumbe wa Umoja wa Wadhibiti wa Vifaa Tiba katika nchi za Asia (AHWP).
   Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bw. Hiiti B. Sillo akisalimiana  na Waziri  anayesimamia Usalama wa Chakula na Dawa nchini Korea na kati yao ni Mwenyekiti wa AHWP  Dkt. Saleh Al –Tayyar .
  0 0


  0 0

    Wafuasi wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda wakiwa nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo huku wakipaza sauti baada Sheikh Ponda kushinda rufaa ya kupinga hukumu ilitolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya kuvamia na kujimilikisha kwa nguvu kiwanja cha Markaz Chang’ombe jijini Dar es Salaam. Hukumu hiyo ilitolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Victoria Nongwa, Mei 9, 2013. (Picha na Francis Dande)
   Wafuasi wa Sheikh Ponda.
   Wafuasi wa Sheikh Ponda Issa wakitoka Mahakamani.
  Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda (wa pili kushoto) akitoka katika chumba cha Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kushinda rufaa ya kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya kuvamia na kujimilikisha kwa nguvu kiwanja cha Markaz Chang’ombe jijini Dar es Salaam.


  Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda akiwa chini ya ulinzi wa askari wa Magereza wakati  akitoka Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

  Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda akitoka katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam baada ya kushinda rufaa ya kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya kuvamia na kujimilikisha kwa nguvu kiwanja cha Markaz Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
   Wafuasi wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda wakiwa nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam huku wakipaza sauti baada ya kushinda kesi iliyokuwa ikimakabili.
   Wafuasi wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda wakiwa nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam huku wakipaza sauti baada ya Sheikh Ponda kushinda kesi iliyokuwa ikimakabili.
    Wafuasi wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda wakiwa nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam huku wakipaza sauti baada ya Sheikh Ponda kushinda kesi iliyokuwa ikimakabili.
  Wafuasi wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda wakiwa nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam huku wakipaza sauti baada ya Sheikh Ponda kushinda kesi iliyokuwa ikimkabili.
  Mfuasi wa  Sheikha Ponda akitoka Mahakamani.

   Ulinzi ukiwa umeimarishwa nje ya Mahakama Kuu Dar es Salaam wakati wa kesi ya Ponda.
    Wafuasi wa Sheikh Ponda Issa wakiwa wamelizunguka basi la Magereza alilokuwa amepanda Sheikh Ponda wakati akielekea mahabusu ya gereza la Keko.
    Wafuasi wa Sheikh Ponda Issa wakilifukuza basi la Magereza alilokuwa amepanda Sheikh Ponda wakati akielekea mahabusu ya gereza la Keko.
    Wafuasi wa Sheikh Ponda Issa wakitoka Mahakamani.
   Gari la Polisi.
   Wafuasi wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda wakiwa nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam huku wakipaza sauti.


  0 0

   Waziri wa Fedha wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Omar Yussuf Mzee akifungua maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam” na kuwashirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi  chini ya kauli mbiu isemayo “ Takwimu Huria kwa uwajibikaji na ushirikishwaji wa wadau wote.
    Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Mohammed Hafidh akisisitiza jambo kuhusu athari, madhara  na  ya  matumizi ya takwimu zisizo sahihi.
    Baadhi ya wadau mbalimbali na wataalam wa takwimu waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika wakifuatilia masuala mbalimbali  leo jijini Dar es salaam.
   Mwakilishi kutoka nchi washirika wa maendeleo Bw. Jacques Morisset (kushoto)  akizungumza na wadau mbalimbali kuhusu mchango wa matumizi ya takwimu sahihi katika maendeleo ya taifa lolote wakati wa maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika leo jijini Dar es salaam.

   Msanii Stara Thomas (kulia) akiwa na waimbaji wenzake akiwasilisha ujumbe wa matumizi ya takwimu sahihi kupitia wimbo maalum wakati wa maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyowashirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi  chini.
   Waziri wa Ferdha wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Omar Yussuf Mzee (wa nne kutoka kulia mbele) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji na watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu mara baada ya kufungua maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika leo jijini Dar es salaam.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
  Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Aldegunda Kombo akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi hiyo kuhusu matumizi ya takwimu sahihi katika kupanga shughuli za maendeleo  nchini wakati wa maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.

  ========= ======  ======

  Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
  27/11/2014, Dar es salaam.

  SERIKALI kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu imesema kuwa itaendelea kuwapatia wananchi takwimu sahihi zinazohusu sekta mbalimbali ili kuwajengea uwezo wa kushiriki katika ngazi za maamuzi na masuala mbalimbali nchini.

  Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Fedha wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  Omar Yussuf  Mzee wakati akifungua rasmi maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yanaoongozwa na kauli mbiu isemayo Takwimu Huria kwa uwajibikaji na ushirikishwaji wa wadau wote.

  Amesema upatikanaji wa taarifa na  takwimu sahihi kwa wananchi unaongeza ushiriki wao katika maamuzi na kuwajengea uwezo wa kutathmini utendaji wa Serikali katika masuala mbalimbali yakiwemo mapato na matumizi.

  Amesema Ofisi ya Taifa ya Takwimu itaendelea kuhakikisha kuwa takwimu mbalimbali zinapatikana kwa urahisi kupitia mtandao, machapisho na mifumo rahisi ili kuwawezesha wananchi na wadau mbalimbali kuzipata pindi wanapozihitaji.

  “ Maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika mwaka huu yanaongozwa na kauli Mbiu isemayo Takwimu Huria kwa uwajibikaji na ushirikishwaji wa wadau wote ambayo inalenga kurahisisha upatikanaji wa takwimu sahihi kwa urahisi na kumwezesha mtumiaji kuzipata bila kizuizi chochote” Amesema.

  Amefafanua  kuwa upatikanaji wa takwimu huria unawawezesha wananchi kujua sababu zinazoifanya serikali kutekeleza maamuzi mbalimbali, kuongeza uwajibikaji na kuwawezesha kupima matokeo ya sera za Serikali, kutathimini matumizi ya Serikali na kushiriki katika midahalo mbalimbali ya kitaifa.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Aldegunda Kombo akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi hiyo amesema kuwa maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika mwaka huu yameweka msisitizo katika kuweka miundombinu ya kuwarahisishia wadau kupata takwimu sahihi kwa wakati.

  Amesema maadhimisho hayo licha ya kujadili masuala mbalimbali yanajikita katika kuweka msukumo wa kuhakikisha kuwa takwimu sahihi zinawafikia wananchi na wadau mbalimbali wa maendeleo bila vikwazo vyovyote ili kuongeza uwazi wa utendaji wa shughuli za serikali serikali.

  Naye mwakilishi kutoka nchi washirika wa maendeleo Bw.Jacques Morisset akizungumza wakati wa maadhimisho hayo ameeleza kuwa takwimu sahihi ni ufunguo wa maendeleo kwa nchi yoyote duniani.

  Amesema kuwa upatikanaji wa taarifa mbalimbali unawawezesha wananchi kutambua na kupima kiwango cha maendeleo ya nchi yao katika masuala mbalimbali yanayogusa maisha yao ya kila siku yakiwemo ya matumizi ya rasilimali, Elimu, ukuaji wa uchumi, shughuli za kilimo na sekta ya viwanda na Biashara.


  0 0

   
   Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), Bw John Samangu (kushoto) akikata utepe kuzindua rasmi albamu ya kwanza kutolewa na ya kwaya ya Kanisa la Kigango cha Mtakatifu Rita wa Kashia ijulikanayo kama ‘Msifuni Bwana’ jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Wanaoshuhudia ni mwenyekiti wa Kigango cha Mt. Rita Bw. Frederick Msumali(kushoto) na waumini wengine.
   Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), Bw. John Samangu, akionyesha moja ya DVD wakati wa uzinduzi wa albamu ya kwaya ya Kigango cha kanisa la Mtakatifu Rita wa Kashia iitwayo ‘Msifuni Bwana’ jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Wanaoshuhudia ni Padre Xavery Kassase, Paroko Msaidizi wa Parokia ya Kanisa Katoliki la Mavurunza (kulia) na Mwenyekiti wa Kigango cha Mt. Rita Bw. Frederick Msumali(kushoto).

  Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), Bw John Samangu (kulia), akifungua moja ya kanda za albamu ya ‘Msifuni Bwana’ ya kwaya ya Kanisa la Kigango cha Mtakatifu Rita wa Kashia jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Anayeshuhudia ni mwenyekiti wa Kigango cha Mt. Rita Bw. Frederick Msumali (kushoto). 

  JAMII imeombwa kusaidia kuinua muziki wa injili unaofanywa na madhehebu mbalimbali ya dini ya nchini ili kusaidia kukuza maadili mema miongoni mwa wanajamii.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi wa albamu ya kwanza kuwahi kutambulishwa na kwaya ya kigango cha kanisa la Mtakatifu Rita wa Kashia jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), Bw. John Samangu, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo, alisema kuwa albamu hiyo inayobeba jina la ‘Msifuni Bwana’ itasaidia kukuza maadili mema katika jamii, kwani nyimbo nyingi katika albamu hiyo zimebeba ujumbe mzuri.

  Bw. Samangu alikuwa mtu wa kwanza kununua nakala tatu za DVD na albamu hiyo ambayo ni ya kwanza kuwahi kutambulishwa na kwaya ya kigango cha kanisa la Mtakatifu Rita wa Cascia tangu kuanzishwa kwake mwaka 2010.
    
  Alisema kutokana na hali iliyopo sasa ya kuporomoka kwa maadili katika jamii, kuna umuhimu mkubwa wa taasisi kama makanisa kuhimiza watu kubadili tabia zao ili ziwe nzuri na zenye kupendeza. Alisema muziki wa injili ni miongoni mwa njia za kufikisha ujumbe utakaokuwa na athari chanya kwa walengwa wengi zaidi.

  “Naisihi kwaya ya kigango cha kanisa la Mtakatifu Rita wa Kashia kuendelea kusambaza neno la Mungu, kwani kwa kupitia muziki pekee, idadi kubwa ya watu inaweza kufikiwa. Hii itasaidia jamii kubadilika na kuwa katika mlengo ulio sahihi,” alisema Bw. Samangu.

  Kwa upande wake, Paroko Msaidizi wa Parokia ya kanisa la Mavurunza, Padri Xavery Kassase, alisifu kitendo cha kwaya hiyo kutafsiri nyimbo zote katika albamu hiyo kwa kutumia lugha mbalimbali. Alisema kitendo icho kitasaidia albamu hiyo kuwafikia wasikilizaji wengi zaidi hata nje ya mipaka ya Tanzania.

  “Kwa kuzitafsiri nyimbo kwenye lugha mbalimbali, inamaanisha kuwa mtaweza kusambaza albamu yenu nje ya nchi na hata kutumia mitandao ya kijamii kama YouTube ili watu wengi zaidi waweze kusikiliza na kuelewa ujumbe mzuri unaopatikana katika nyimbo hizi.  

  Naiomba kwaya isiridhike na mafanikio waliyoyapata hadi kufikia sasa badala yake waendelee kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha kuwa inakuwa miongoni mwa kwaya bora zaidi nchini Tanzania,” alisema Padri Kassase.

  Mbali na hilo, Padri Kassase aliwaomba watu wauunge mkono muziki wa injili kwani unabeba ujumbe wenye mafundisho yanayohimiza maadili mema katika jamii badala ya kushabikia nyimbo zinazoshabikia mambo maovu.


  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisaidia kubeba gunia la korosho kwenye ghala la korosho la TANECU ,Tandahimba mkoani Mtwara.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipita juu ya magunia ya Korosho alipotembelea ghala la korosho la TANECU ikiwa sehemu ya ziara yake ya kujenga na kuimarisha Chama mkoani Mtwara .
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Tandahimba ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa zao la korosho lina hadithi nyingi sana na njia pekee ya kuleta ukombozi kwa mkulima ni kujenga kwa viwanda vya kutosha vya kubangulia Korosho nchini.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Tandahimba ambapo aliwaambia wasihadaike na wapinzani ambao muda wao wa ujana wameutumia wakiwa CCM na uzeeni kuingia upinzani na kuanza kuhadaa watu walioishi kwa amani kwa muda mrefu.

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia moja ya nyumbailiyo ezuliwa paa na mvua yenye upepo mkali iliyonyesha jana jioni katika Kata ya Nanyanga Ndugu Saidi Mnambenga ambaye  ni mlemavu wa macho.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wajumbe wa kikao cha halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Tandahimba, uliofanyika Mahuta wilayani Tandahimba,Mtwara.

  0 0

  Shirika lisilokuwa la kiserikali linalojihusisha na uhifadhi wa mazingira na wanyama pori la World Wide Fund for Nature (WWF), limejiunga katika jitihada za kitaifa na kimaifa za kupambana na ujangili nchini ambapo pamoja na mambo mengine limetoa mabango yanayotahadharisha wananchi na wageni waingiao na watokao Tanzania kutojihusisha na shughuli yoyote inayohusiana na ujangili wa wanyama.

  Akikabidhi vifaa hivyo Novemba 27, 2014 jijini Dar es Salaam kwa Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wa jijini Dar es salaam ,Bw.Moses Malaki,Mkurugenzi wa WWF Tanzania Bw. Bell'Aube Houinato,aliwataka jumii ya za ndani na za kimataifa kuhakikisha zinaongeza jitihada ili kuhifadhi rasilimali hizo kwa manufaa ya sasa na kizazi kijacho.

  " Jukumu la kumaliza kadhia hii ya biashara haramu ya nyara za umma ni la wote si la serikali pekee au WWF bali umma mzima wa Tanzania na kimataifa,hivyo kila mmoja kwa sehemu yake na eneo lake awajibike ipasavyo",alisema Bw.Houinato.

  Aidha,aliongeza kuwa ni jukumu la kila mmoja wetu kuhakikisha vyombo vinavyohusika na ulinzi na uangalizi wa rasilimali zetu vinajengewa uwezo wa kimaarifa na kivifaa ili kuhakikisha vyombo vyote vinatimiza wajibu wake kwa tija kubwa.

  Kwa miaka ya hivi karibuni nchini Tanzania,kumeibuka tatizo la ujangili ambapo mauaji a Tembo na Faru yameongezeka huku jitihada za kimataifa na kitaifa zikiwa zinaonekana kulegelega jambo lililozishtua jamii za kimataifa hivyo kujiunga na kuongeza bidii katika vita hiyo.
   Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wa jijini Dar es salaam ,Bw.Moses Malaki (kulia), akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), wakati wa hafla ya kukabidhiwa mabango yanayotahadharisha wananchi na wageni waingiao na watokao Tanzania kutojihusisha na shughuli yoyote inayohusiana na ujangili wa wanyama (kushoto), Mkurugenzi wa WWF Tanzania Bw. Bell'Aube Houinato.PICHA NA PHILEMON SOLOMON
   Mkurugenzi wa WWF Tanzania Bw. Bell'Aube Houinato akisisitiza jambo kuhusiana na vyombo vinavyohusika na ulinzi na uangalizi wa rasilimali za nchi.
   Waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wa jijini Dar es salaam ,Bw.Moses Malaki (meza kuu kulia), wakati wa hafla hiyo.
   Mkurugenzi wa WWF Tanzania Bw. Bell'Aube Houinato (kulia), akimkabidhi Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wa jijini Dar es salaam ,Bw.Moses Malaki moja ya mabango hayo.
   Muonekano wa moja ya mabango hayo yenye luga tatu ambayo yatawekwa sehemu mbalimbali ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wa jijini Dar es salaam.


  0 0  0 0  SERIKALI Kuu kwa kushirikiana na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya Handeni na Mkoa mzima wa Tanga, wameombwa kuingilia kati mgogoro mzito wa ardhi katika kijiji cha Komsala, wilayani Handeni, ili kuepusha hatari inayoweza kutokea, ikiwamo vita ya wenyewe kwa wenyewe.

  Hayo yamesemwa juzi na wananchi wa kijiji hicho katika mkutano ulioandaliwa na taasisi ya Handeni Kwetu Foundation inayofanya ziara katika maeneo mbalimbali, hususan ya wilaya ya Handeni, mkoani Tanga, baada ya kuzinduliwa Mei 8 mwaka huu.

  Wakizungumza kwa uchungu mkubwa, wananchi hao walisema kuwa hali ni mbaya, maana kijiji chao kimeendelea kutekwa na kubaki eneo dogo lililoanza kuibua chuki za wazi kwa wananchi.

  Mzee aliyejitambulisha kwa jina la Alhaj Ally Yasin Ling’ande, alisema kiuhalisia hakuna kijiji cha Komsala, kwakuwa hawana eneo la ardhi, hasa baada ya wilaya Korogwe kuingia kwenye eneo lao kwa kufikia hata kujenga mnada wa ng’ombe.

  “Ukiaangalia usawa palipojengwa mnada, utaamini kuwa hata kwenye shule ya Msingi Komsala pia patakuwa ni eneo la Korogwe, ingawa si sahihi kulinganaa na ramani ya mwaka 1978, jambo linaloonyesha kuwa huu ni mzozo utakaoweza kumwaga damu,” alisema.

  Naye William Seif alisema mbali na mipaka hiyo kuwa tata, pia kumekuwa na idadi kubwa ya wageni kumiliki heka zaidi ya 130 na bado wanaingia kwa wenye heka tatu wakiamini kuwa uwezo wao kifedha unawafanya wamudu kesi zinazoendeshwa kwenye mabaraza ya Kata na wao kupata haki.

  “Masikini akionewa anakimbilia kwenye Bazara la Kata, lakini huko kumekuwa na danadana nyingi, ukizingatia kuwa siku zote mkono mtupu haulambwi, ndio maana tunaoimba serikali ya wilaya ya Handeni, mkoa na wadau wengine wa ardhi kuja kujionea bomu hili linalosubiriwa kuripuka hapa kwetu,” alisema.

  Mwananchi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Bashiri Wabu, alisema kuwa ardhi katika kijiji chao imeuzwa kiholela kwa watu wenye nazo bila kufuata sheria za ardhi, ikiwamo ya kuandaa mkutano wa wananchi wote.

  “Kuna watu hawana maeneo kabisa ya kulima, wakati watu wachache wanamiliki maeneo makubwa ambayo hata kuyalima yote hawana uwezo huo, jambo linalokera na kuudhi mno kila tunapoliangalia suala hili katika kijiji chetu,” alisema Wabu, akiungwa mkono pia na Hemed Ngona, Kombo Twaha, wakisisitiza kuwa sheria za ardhi na utawala bora hazifuatwi katika kijiji chao.

  Katika mkutano huo ulioanza saa 9 alasiri na kumalizika saa 12 jioni, ulihudhuriwa na watu wengi, huku idadi kubwa ikiegemea katika kero ya ardhi na mipaka.

  Aidha Mwenyekiti wa kijiji cha Komsala anayemaliza muda wake, Mwanaidi Said, alisema kero kubwa katika kijiji hicho ni mipaka iliyoshindwa kutatuliwa na viongozi wa juu, licha ya kupeleka malalamiko yao mara kadhaa.

  “Kijiji cha Komsala sasa ni kama kitongoji tu, maana kimechotwa katika pembe zote na ndio maana hata wenzetu wa Korogwe wamekuja kujenga mnada wa ng’ombe kwa madai kuwa ni kwao, jambo ambalo hata mwenyekiti atakayefuata litamuumiza kichwa,” alisema na kuwafanya wananchi wapatwe na hofu.

  Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo aliyetumia muda huo kuaga wananchi wake, sekeseke la mipaka limeshindwa kutatuliwa, huku akiwataka viongozi kulipa kipaumbele kabla ya matatizo hayajakikumba kijiji chao pale wananchi hao watakapotafuta haki yao.

  Naye Msemaji Mkuu wa taasisi hiyo, Kambi Mbwana, aliwashukuru viongozi wa serikali ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kwa kuwapa ushirikiano, ikiwamo kuruhusu kutembelea katika vijiji mbalimbali kutoa elimu ya uraia na kuhamasisha utawala bora.

  “Naomba niwatoe hofu Watanzania wote kuwa mikutano hii ya hadhara hairatibiwi na chama chochote cha siasa, hivyo tunaomba tushirikiane kwa ajili ya kufanikisha maendeleo, hasa kama wananchi watahudhuria mikutano wanapoitwa na viongozi wao,” alisema.

  Ziara ya Handeni Kwetu Foundation ilianzia Kata ya Misima, ambapo wananchi wengi wameiunga mkono taasisi hiyo yenye lengo la kuwakomboa wananchi kwa kutoa elimu na kuhamasisha maendeleo ya jamii.

  0 0

   Balozi wa Tanzania Nchini Ubelgiji Dkt. Diodorus B. Kamala akielezea lengo la ujio wa wawekezaji kutoka Ubelgiji kuja kuwekeza nchini Tanzania alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kufuatia ujio wa wawekezaji wa nchi hiyo Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar
   Waziri wa Miundombinu na Mawasilino Juma Duni Haji akiwa na watendaji wake wakuu wakimsikiliza Meneja mauzo  wa Kampuni ya ujenzi ya Anglo Belgian Corporation ya Ubelgiji walipofanya mazungumzo Ofisini kwake Kisauni. 
   Wamiliki wa makampuni  toka Ubelgiji wakimsikiliza Mkurugenzi Uenezi wa Mamlaka ya Uendelezaji  Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA) Bi. Nasria Mohd Nassor (hayupo pichani)  walipofika ofisini kwake Maruhubi Mjini Zanzibar.
   Afisa Mipango wa Shirika la Bandari Zanzibar   Ali Haji akizungumza na wamiliki wa makampuni  kutoka Ubelgiji walipotembelea bandari ya Malindi  mjini Zanzibar .
   Waziri wa Fedha Omar Yussuf Mzee akizungumza na ujumbe wa Wafanyabiashara  wa Makamupuni ya uwekezaji kutoka Ubelgiji walipomtembelea Ofisini kwake  Vuga Mjini Zanzibar.
  Picha ya pamoja ya wawekezaji kutoka nchini Ubelgiji na viongozi  wa Mamlaka ya Uendelezaji Vitega Uchumi Zanzibar  (ZIPA).(Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

  0 0

  MSANII wa vichekesho (komedy) kutoka Nigeria,Okopcha Bright Onyekere maarufu kama Basket Mouth amewasifu wasanii wa Tanzania kwa juhudi wanazofanya kuelimisha jamii kutumia vipaji vyao.

  Akizungumza Dar es Salaam jana baada ya kuwasili kutoka Nigeria kwa ajili ya onesho maalum kushirikiana na wasanii wa Tanzania juzi Dar es Salaam alisema kutoka aanze sanaa ya vichekesho miaka 16 iliyopita amekuwa akipata sifa za wasanii wa Tanzania wakiwika katika fani za muziki, sanaa za filamu, michezo ya kuigiza na vichekesho.

  Onyekere aliyetamba nchini Nigeria na Bara la Afrika katika fani hiyo amekuja kufanya onesho moja lililopangwa kufanyika jana hoteli ya Golden Tulip, aliongeza kuwa sanaa ni utajiri mkubwa kama vipaji walivyopewa vitatumika ipasavyo na kutawala jukwaa .

  Mkurugenzi wa Kampuni ya Vuvuzela, Evans Bukuku alisema lengo la kumleta msanii huyo wa komedy ni kuimarisha sanaa ya vichekesho kwa wasanii chipukizi wa Tanzania ambao wanahitaji kuandaliwa kwa soko hilo nchini na nje ya nchi.

  Alisema Kampuni ya Vuvuzela imejitolea kusaidia wasanii wa vichekesho nchini na kuwafundisha namna watakavyoweza kuendeleza fani hiyo kazi iliyoanza miaka minne iliyopita kampuni ilipoanzishwa.

  Bukuku alisema kila mwisho wa mwezi kuna onesho maalum ambalo hutumika kuonesha vipaji vya wasanii wa vichekesho na jinsi msanii anavyoweza kutawala jukwaa kuwaburudisha watazamaji.

  Alisema kampuni yake inatarajia kufanya maonesho kama hayo mikoa mbalimbali ya Tanzania kuibua wasanii wengine wenye uwezio katika fani hiyo.

  Mkurugenzi Bukuku alisema katika onesho la karibuni Watanzania walikongwa nyoyo zao pale wasanii wa Tanzania washirikiana na wasanii wa vichekesho kutoka Kenya ambaye ni Mdomo Baggy na Dick Omondi kutoka Uganda anayejulikana kama Uncle Bob kufanya onesho kali nchini.

  Bukuku aliwashukuru wadhamini waliojitokeza kusaidia kufanyika kwa onesho hilo ambao ni Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA),Hoteli ya  Golden Tulip, Gazeti la Mwananchi Communications, Clouds Media Group, Ultimate security, Simu TV, Prime Advertising, Dar insites, Advertising Dar, Bongo 5, Eventlites, Hugo Domingo na Michuzi Blog.

  0 0

  Na Eleuteri Mangi- Dodoma
  28/11/2014.
   
  Serikali imesema kuwa VICOBA ni taasisi binafsi inayomilikiwa na wananchi wenyewe vikiwa ni miongoni mwa tasisi ndogo za kifedha ambazo ni za kibinafsi na huanzishwa, kuendeshwa na kusimamiwa ama kijijini, kitongojini na hata kwenye kata.

  Hayo yamebainishwa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Rungwe Magharibi Prof. David Mwakyusa (CCM) ambaye alitaka kujua kama Serikali inatambua VICOBA  kama mkombozi wa wanyonge.

  Mwigulu amefafanua kuwa taasisi hizo zimo kwenye sekta ya fedha isiyorasmi na zinatoa huduma za kifedha mijini na vijijini.

   “Uwepo wa taasisi hizi, umewezesha kufikisha huduma za kifedha kwa wananchi waliombali na huduma za sekta rasmi ya fedha na hivyo kuwa mkombozi wa wanyonge” alisema mwigulu.

  Aidha, kwa kutambua suala hilo, ili kusaidia na kuimarisha taasisi hizo, Mwigulu amesema kuwa Serikali baada ya kupata ushauri kutoka kwa Mshauri Mwelekezi wa masuala ya uchumi na tafiti za kijamii, inafanya mapitio ya Sera ya Taifa ya Taasisi ndogo za huduma ya fedha ya mwaka 2000 ili kuihuisha iweze kukabili na kuzingatia mabadiliko na maendeleo yanayojitokeza katika sekta hiyo.

  Vilevile Mwigulu amesema kuwa Serikali inakamilisha uhuishaji wa sera ya taasisi ndogo ndogo za kifedha ambapo hatua inayofuata ni kuandaa mapendekezo ya muswada ambayo yatapelekwa Baraza la Mawaziri mara baada ya kupata idhini na maelekezo ya Baraza hilo na muswada huo utafikishwa bungeni.

  Taasisi ya VICOBA ilianzishwa nchini mwanzoni mwa miaka ya 2000, ambapo imekuwa na manufaa kwa wananchi wengi wenye kipato cha chini hususan wanawake waishio vijijini wamefanikiwa kuboresha kipato chao na maisha yao kwa ujumla kwa kujiunga na taasisi hiyo.

older | 1 | .... | 414 | 415 | (Page 416) | 417 | 418 | .... | 1898 | newer