Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 413 | 414 | (Page 415) | 416 | 417 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Diodorus Kamala aliyeongoza jopo la wadau wa sekta ya usafirishaji na wafanyabiashara waliotembelea nchini kuanzia Novemba 22- 29 akizungumza kwenye Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) leo asubuhi, kulia kwake ni Meneja wa Kampuni ya Ujenzi ya BS Solutions. Jopo hilo liko nchini kuangalia fursa za uwekezaji nchini. Ujumbe huo ulitoa mada kuhusu ujenzi wa nyumba kwa kutumia teknolojia rahisi ya kuunganisha na mabati maalumu ambao hutumia muda mfupi na kuwa nafuu kwa gharama. Picha zote za NHC.
  Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Diodorus Kamala aliyeongoza jopo la wadau wa sekta ya usafirishaji na wafanyabiashara waliotembelea nchini kuanzia Novemba 22- 29 akizungumza kwenye Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) leo asubuhi, kulia kwake ni Meneja wa Kampuni ya Ujenzi ya BS Solutions, Ing Jean Noel Galasse. Jopo hilo liko nchini kuangalia fursa za uwekezaji nchini.
  Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Diodorus Kamala aliyeongoza jopo la wadau wa sekta ya usafirishaji na wafanyabiashara waliotembelea nchini kuanzia Novemba 22- 29 akizungumza kwenye Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) leo asubuhi, kulia kwake ni Meneja wa Kampuni ya Ujenzi ya BS Solutions, Ing Jean Noel Galasse. Jopo hilo liko nchini kuangalia fursa za uwekezaji nchini.
  Baadhi ya wadau wa sekta ya usafirishaji na wafanyabiashara waliotembelea nchini wakifuatilia kwa karibu mjadala. Jopo hilo liko nchini kuangalia fursa za uwekezaji nchini.

   Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Jamii wa NHC, Susan Omari (kulia), Akifuatiwa na Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa NHC, Haikamen Mlekio na Mhandisi Mwandamizi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Morgan Nyonyi wakifuatilia majadiliano yaliyokuwa yaiendelea katika mkutano huo.
   Meneja wa Kampuni ya Ujenzi ya BS Solutions, Ing Jean Noel Galasse akifafanua jambo kwenye Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) leo asubuhi, kulia kwake ni Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Diodorus Kamala.
   Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Diodorus Kamala aliyeongoza jopo la wadau wa sekta ya usafirishaji na wafanyabiashara waliotembelea nchini kuanzia Novemba 22- 29 akishukuru kabka ya ujumbe huo kuondoka kuelekea na ziara nyingine leo asubuhi.
  Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Diodorus Kamala aliyeongoza jopo la wadau wa sekta ya usafirishaji na wafanyabiashara waliotembelea nchini kuanzia Novemba 22- 29 akiondoka katika chumba cha mikutano.

  0 0

  SONY DSCMkuu wa Bandari ya Kyela, Bw. Percival Ntetema  akiwakaribishia wakaguzi wa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipofika ofisini kwake.SONY DSCMkuu wa Bandari ya Kyela, Bw. Percival Ntetema  akiwakaribishia wakaguzi wa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipofika ofisini kwake.SONY DSCKiongozi wa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence (Mbele) akiwaongoza wajumbe wa Timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango kupanda boti ili kwenda kushuhudia lango la kuingilia Gati la Bandari ndogo ya Itungi. Itungi ni bandari ya kipekee nchini kujengwa mtoni.SONY DSCMkuu wa Bandari ya Kyela, Bw. Percival Ntetema  (Kulia) akiwaonesha kitu wajumbe wa Timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakati wakishuhudia lango la kuingilia Gati la Bandari ndogo ya Itungi.SONY DSCMkuu wa Bandari ya Kyela, Bw. Percival Ntetema  (Aliyevaa tai) akiwaonesha kitu wajumbe wa Timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo sehemu inapojengwa gati mpya (halionekani) katika Bandari ya Kiwira.SONY DSCWajumbe wa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipata fursa ya kujionea meli pekee inayotoa huduma ya kusafirisha abiria na mizigo (MV Songea) katika Ziwa Nyasa kwa upande wa Tanzania.

  PICHA ZOTE NA SAIDI MKABAKULI
  ……………………………………………………………………..
  Na Saidi Mkabakuli, Kyela.

  Kufuatia adha ya usafiri wa majini inayowakabili wakazi waishio katika fukwe za Ziwa Nyasa, Mamlaka ya Bandari Tanzania kupitia kituo chake cha Kyela ipo mbioni kujenga meli ya abiria na mizigo ili kuwahudumia wakazi hao.

  Hayo yaliwekwa bayana na Mkuu wa Bandari ya Kyela, Bw. Percival Ntetema wakati timu wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Tume ya Mipango ilipotembelea na kukagua bandari za Itungi na Kiwira zilizopo wilaya ya Kyela, mkoani Mbeya.

  Bw. Ntetema alisema kuwa Mamlaka imeshakamilisha mchakato wa manunuzi na tayari imempata mkandarasi M/S Songoro Marine Transport Ltd kwa ajili ya ujenzi wa meli yenye uwezo wa kubeba jumla ya tani 200 za mizigo na abiria 200. “Mamlaka ipo kwenye hatua za mwisho za kuandaa mkataba unaotarajiwa kutiwa saini mwezi ujao  na kazi itaanza mwanzoni mwa mwaka ujao,” alisema.

  Bw. Ntetema aliongeza kuwa mpaka sasa Bandari ya Kyela imeshaanza maandalizi ya kuvuta umeme uliofadhiliwa na Wakala wa Umeme Vijijini pamoja na kuaanza kwa kujenga matishari mawili ili yaweze kurahisisha utoaji wa huduma mara meli hiyo itakapoanza kazi mwishoni mwa mwaka ujao.

  Akizungumza wakati wa ziara hiyo, kiongozi wa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri aliupongeza uongozi wa Mamlaka kwa hatua yake hiyo kwani itaongeza tija ya shughuli za kiuchumi katika kanda hiyo ya Ziwa Nyasa. “Ninaupongeza uongozi wa Mamlaka ya Bandari kwa kuanza mchakato huu utakaofungulia fursa za kiuchumi na maendeleo kwenye ukanda huu, hivyo kuunga mkono jitihada za serikali za kupunguza vikwazo mbalimbali vinavorudisha kasi ya kusaka kupunguza umaskini nchini,” alisema.

  Bibi Mwanri aliongeza kuwa kukamilika kwa mradi huo kutatoa fursa za kuhudumia shehena na abiria kutoka mikoa ya Mbeya, Njombe, na Ruvuma. Pamoja na kuhudumia nchi za jirani ikiwemo Malawi, Msumbiji na Zambia.

  Kwa mujibu wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/2012 – 2015/2016) bandari ni mojawapo ya vipaumbele vitano vya kimkakati vyenye lengo la kufungulia fursa za ukuaji uchumi wa nchi ili kuweka misingi wa uchumi kwa watu walio wengi. 

  Vipaumbele vingine ni Kilimo ambapo lengo kuu likiwa ni kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao ya kilimo ili kujitosheleza kwa chakula na kuwa na ziada ya kuuza nje ya nchi; Maendeleo ya viwanda: Msisitizo umewekwa katika kuvutia, kuanzishwa na kuendeleza viwanda vinavyotumia malighafi zinazopatikana nchini (kama vile viwanda vya nguo, mbolea, saruji, makaa ya mawe, chuma na bidhaa za chuma) na pia sekta ya madini kwa lengo la kuongeza mapato ya Serikali.

  Pamoja na kipaumbele cha Maendeleo ya rasilimali watu na ujuzi: Mpango unahimiza kuwekeza katika elimu (hasa katika elimu ya juu na vyuo vya ufundi) na huduma za afya (kuongeza ubora na upatikanaji wa huduma) katika kujenga nguvu kazi itakayotuletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii; na Utalii, Biashara, na huduma za Fedha ambapo jitihada zimewekwa kwenye uendelezaji uwezo wa kuuza katika masoko ya ndani na nje, kuongeza   idadi ya watalii na matumizi yao wawapo nchini, na kuongeza upatikanaji wa huduma za kifedha.

  0 0

  Miss Ilala 2014 JihanDimack, akiwanawisha mikono watoto yatima wa kituo cha Mwana Orphans Centre kilichopoVingunguti jijini Dar es Salaam katika hafla ya chakula cha mchana iliyofanyika katika hoteli ya Cape Town Fish Market.  (Picha na John Dande)
  Miss Ilala 2014 Jihan Dimack, akiwagawia chakula watoto wanaolelewa na kituo cha kulelea watoto yatima wakituo cha Mwana Orphans Centre kilichopoVingungutijijini Dar es Salaam katikahaflayachakula cha mchanailiyofanyikajuzikatikahoteliya Cape Town Fish Market. 
  Miss Ilala 2014, Jihan Dimack akila chakula pamoja na watoto waishio katika kituo cha kulelea watoto yatima wa kituo cha Mwana Orphans Centre kilichopoVingunguti jijini Dar es Salaam hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Cape Town Fish Market.  
  Miss Ilalawamwaka 2014 Jihan Dimack akimlisha chakula Miskia Nassor, wa kituo cha Mwana Orphans Centre kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam.
  Miss Ilala 2014 Jihan Dimack akiwa amembeba mtoto FatumaYusuph, anaelelewa na kituo cha watoto yatima wa kituo cha Mwana Orphans Centre kilichopoVingunguti jijini Dar es Salaam katika hafla ya chakula cha mchana iliyofanyika katika hoteli ya Cape Town Fish Market. 
  Miss 2014 Jihan Dimack akitoa zawadi kwa watoto wanaolelewa na kituo cha kulelea watoto yatima wa Kituo cha Mwana Orphans Centre kilichopoVingunguti jijini Dar es Salaam hafla hiyo ilifanyika  katika hoteli ya Cape Town Fish Market. 
  Miss Ilalawamwaka 2014 JihanDimack akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watoto wanaolelewa na kituo cha kulelea watoto yatima wa kituo cha Mwana Orphans Centre kilichopoVingunguti jijini Dar es Salaam katika hafla ya chakula cha mchana iliyofanyika juzi katika hoteliya Cape Town Fish Market. 
  Miss Ilala 2014 JihanDimack.akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa hoteli ya Cape Town Fish Market.

  0 0

  DSC_0825

  Maximilian Mapunda kutoka shirika la Afya Duniani (WHO-Country Officer) akiwasilisha mada kwenye kongamano hilo.

  Na Andrew Chale, Bagamoyo
  Pichani ni baadhi ya picha za matukio ya siku ya pili, jana Novemba 25 kwenye kongamano la Kisayansi la 31, '31th Annual Scientific Conference and Annual General Meeting'.. lililoandaliwa na Tanzania Public Health Association (TPHA). Mkutano huo unafanyika mjini hapa Bagamoyo katika Ukumbi wa Stella Maris, Bagamoyo, Pwani Tanzania.

  Kongamano hilo la kisayansi la 31, limeanza Novemba 24 linatarajia kuwa la siku tano na kutarajia kumalizika Novemba 28 ambapo wataalamu wa afya na wadau watajadilina mambo mbalimbali ya afya hapa nchini.
  DSC_0830
  Katibu Mtendaji wa TPHA Taifa, Dk. Oberlin Kisanga akiwasilisha mada maalum kwenye kongamano hilo.
  DSC_0852
  Dk. Ali Mzige mshiriki wa Kongamano la Kisayansi la 31, akiwasilisha mada maalum.
  DSC_0848
  Mwenyekiti wa TPHA Taifa, Dk.Elihuruma Nangawe akitoa ufafanuzi kwenye mada zinazotolewa na wajumbe kwenye kongamano hilo.
  DSC_0856
  Wajumbe wa kongamano hilo wakichangia mada.
  DSC_0857
  Katibu Mtendaji wa TPHA Taifa, Dk. Oberlin Kisanga (kushoto) akifuatilia kwa makini kongamano hlo.

  0 0  0 0


   Ujenzi wa mradi wa maji wa Sengenya ukiwa unaendelea ambapo ukikamilika utasaidia vijiji vitatu wilayani Nanyumbu mkoa wa Mtwara.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupanga mawewakati wa ujenzi wa bwawa la maji la Sengenya ambalo litasaidia vijiji vya Sengenya ,Mara na Nangarinje.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Daktari Mkuu wa Wilaya wilaya ya Nanyumbu Dkt. Ahmad Mhando ambapo Katibu Mkuu wa CCM alitembelea kituo hicho cha afya cha Mangaka.
    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiagana na  Daktari Mkuu wa Wilaya wilaya ya Nanyumbu Dkt. Ahmad Mhando baada ya kukagua  kituo hicho cha afya cha Mangaka.
   Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Katibu wa NEC itikadi na Uenezi Nape Nnauye kutanzama daraja hilo linalounganisha nchi mbili za Tanzania mfumo.
   Shehena ya mbao zilizokamatwa ma TRA Mtambaswala
   Katibu Mkuu wa CCM akiondoka kwenye ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania zilizopo Mtambaswala.


   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia wakina Mama wakifyatua matofali kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya UWT wilaya ya Nanyumbu mkoa wa Mtwara
   Mbunge wa Jimbo la Nanyumbu Dunstan Daniel Mkapa akihutubia wakazi wa Mangaka mji ni na kuelezea utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2010.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mangaka wilaya ya Nanyumbu na kuwataka wananchi hao kujiandikisha kwenye madaftari ya wapiga kura .
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Mangaka  wilaya ya Nanyumbu ambapo aliwaambia CCM ya sasa itakuwa kali kuliko wakati wowote na itaisimamia serikali na kuipongeza inapofanya vizuri na itakapofanya vibaya itasemwa.

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika  Mangaka mjini wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipandisha bendera mara baada ya kufungua shina la wakereketwa Maneme wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara.
   Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia daraja la Umoja lililopo mpakani na Tanzania.
   Daraja la Umoja.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na viongozi wa CCM wa wilaya ya Nanyumbu wakikata utepe kuashiria kufunguliwa kwa jengo la ofisi ya CCM kijiji cha Chungu kata ya Nanyumbu.
   Katibu wa CCM mkoa wa Mtwara Ndugu Shaibu Akwilombe akiwasalimu wananchi wa kata ya Nanyumbu,wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara.
   Wananchi wakimfurahia kumuona mkuu wao mpya wa mkoa
   Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mh. Halima Dendego akiwasalimu wananchi wa kata ya Nanyumbu mkoani Mtwara
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman akimkabidhi kadi ya CCM Ndugu Yasin Seleman maarufu kwa jina la Msouth aliyekuwa mgombea wa nafasi ya uenyekiti kupitia Chadema.
   Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mtwara  Ndugu Mohamed Sinani akihutubia wakazi wa kata ya Nanyumbu kabla hajamkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kianana.

   Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kata ya Nanyumbu ambapo aliwaambia wananchi kuwa serikali lazima irahishe taratibu za kufanya biashara mpakani
  Kila mtu anamsikiliza Kinana kwenye mikutano yake..
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara baada ya kupokea taarifa za chama na serikali juu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2010.

  0 0

  JACKLINE MASANJA A.K.A JACK WA NJIAPANDA ENZI ZA UHAI WAKE.
  Ilikua ni miaka kumi iliyopita (10) mwaka 2004, nikiwa ndio kwanza nimeanza kufanya kazi chini ya kaka yangu Dr Sebastian Ndege na chini ya uangalizi wa karibu sana wa boss Ruge Mutahaba na Boss Joseph Kussaga nilipokutana na wewe mdogo wangu Jackline Masanja kupitia Njiapanda ulipokuwa unatafuta msaada ukiwa mgonjwa sana. 

  Nakumbuka Dr Sebastian Ndege alipokuona tu alikubaliana na mimi kuwa tuache kila mpango tuliokua nao tuweke nguvu zote kwako. Kweli ulikua unaonekana ni mgonjwa, Kwa kutumia nafasi ya Dr Ndege kipindi hiko akiwa ndio anakaribia kumaliza masomo yake ya udaktari na mimi ndio kwanza nikiwa mwaka wa pili wa udaktari tulifanikiwa kuhakikisha kuwa unapata matibabu ya haraka uliyokua unayahitaji sana. 

  Ulikua shujaa sana kukubali kusema kuwa uko tayari Dr Ndege atangaze hali yako mbele ya uma wa WaTanzania na kwa ruhusa yako tukafanya kipindi na wewe huku ukiwa mgonjwa na ukasema kuwa umeathirika na kwa kipindi kile kinga yako ilikua chini sana (CD4 zilikua 4). 

  Wewe ulikua ni watu wa mwanzo kabisa kuja mbele ya umma kuongea kuhusu hali halisi ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI na maradhi ya UKIMWI. Tulikuita shujaa na Muhimbili ulipokua unatibiwa kipindi kile wahudumu wote walikuita Jackie wa Njiapanda (ndio chanzo cha kumuita jina hilo miaka yote hii). Kutokana na juhudi nyingi zilizofanyika ulipona kabisa na ukarudi kwenye hali yako ya kawaida ya kawaida na ukaendelea na maisha yako.

  Kutokana na yote yaliyotokea mimi na Dr Ndege tukaona ni vyema kama tutakuomba ukae na sisi kama Njiapanda na uendelee kutusaidia kwa kuwa Njiapanda ilikua imekua sana na waliokua wanahitaji msaada walikuwa wanaongezeka kila kukicha. Hukusita kukubali na kuanzia miaka hiyo ukawa unatusaidia kushughulika na wote wanaohitaji msaada wa Njiapanda. Ni wengi uliwachukua na kukaa nao kwako ingawa hali yako ya kiuchumi haikua nzuri sana kusema eti wewe ni tajiri.

  Miaka ilienda na ukaendelea kupambana na maisha huku ukiendelea vyema. Nakumbuka vizuri sana sakata la dawa ya Babu wa Loliondo lilipoanza mimi na wewe tulikua hasi na chanya. Mimi nilikua napinga sana kwa kuwa nilikua na sababu za kisayansi na wewe siku zote ulikua unakasirika kwa kuwa ulikua ukiamini kuwa dawa inaponya. Ukaniomba nikuruhusu uende na kweli tukakubaliana tukafanya mchakato na ukaenda. Tukakubaliana kuwa mimi nachohitaji ni kimoja tu nacho ni kukutumia wewe kama somo kwa hiyo tukarekodi kila kitu kabla hujaenda kwa babu na tukafanya kipindi maalum. 

  Ukasema kinga yako ni ngapi na kila kitu wala hukuogopa. Ukaenda Loliondo ukanyweshwa kikombe na ukarudi. Tukafanya kipindi ukasema unaendelea vizuri. Tukaendelea na vipimo na maisha yakaenda. Miezi miwili baadae nakumbuka nilikua nimekaa kliniki nikakuona kwa chini unatembea huku unajikongoja, nikakufuata pamoja na manesi wa pale clinic tukakuchukua tukaendelea na uchunguzi tukagundua kuwa kinga yako imeshuka sana kwa kuwa baada ya kwenda kwa babu hukuendelea na dawa (kinga ilikua 14). 

  Tukaanza kufanya jitihada za kuhakikisha afya yako inarudi kuwa nzuri na kweli ukawa Ok na tukafanya kipindi tena kuhusu kilichotokea. Kama kawaida ukawa shujaa na kusema kila kitu. Kupitia kwako waTanzania wakajifunza mengi kuhusu kikombe cha babu na maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa ujumla. Kupitia wewe Jackline Masanja watu wakafanya maamuzi huku wanajua, ambayo kisayansi ni jambo la maana sana. Jackie mdogo wangu, mimi na Dr Sebastian Ndege kamwe tusingeweza kuifikisha Njiapanda ilipofika bila ya ushujaa wako, bila ya utayari wako wala bila ya uwazi wako. 

  Sio tu kwa kupitia story yako watu wamejifunza mengi kuhusu maambukizi ya virusi vya UKIMWI bali pia mchango wako wa kusaidia Njiapanda na watu wa njiapanda tumeweza kufanya mengi sana. Nakumbuka habari ya wamasai uliileta wewe, habari ya yule msichana aliyelazimishwa kufanya mapenzi na mbwa ilitoka kwako, watoto wa mitaani wanaolazimishwa kufanya mapenzi kinyume cha maumbile pale kariakoo uliifuatilia wewe mpaka ukalala kariakoo usiku kucha kuifuatilia. Ni nyingi sana Jackie.

  Jackie, kwangu mimi na kwa Dr Sebastian Ndege wewe ni mdogo wetu yule yule wa miaka 10 iliyopita. Ulikua unatuita kaka na sisi tukauita mdogo wetu. Nakumbuka hata mambo yalipokua magumu nikgombana na ma boss wangu kina Ruge nilikua nakuomba ukaniombee msamaha maana boss Ruge alikua anakupenda sana kama mdogo wake, nilijua kuwa ukisema tu boss atanisamehe hahahaaaaa…asante sana mdogo wangu kwa kuokoa jahazi mara kwa mara lol.

  Leo hii nimeamua kuandika huu waraka mrefu kwako wewe Jackie kwa kupitia ndugu zangu wa Facebook na platforms nyingine kwa sababu, siku ya jumamosi 22 November 2014 nilipata ujumbe kutoka kwa rafiki yangu na mfanyakazi mwenzangu Geah Habibu kukuhusu wewe mdogo wangu, kwamba mwili wako umekutwa ukiwa umekwishafariki. 

  Sio tu kuwa kifo chako kilikua cha kawaida bali inaonekana umeuawa. Kwa bahati mbaya sana kwa sasa siko nchini kwa hiyo sikuamini na sikuweza kufanya chochote mpaka pale nilipoona picha yako. Kusema ukweli bado sikuamini so nikaongea na Douglas na Amani (watengenezaji wa Njiapanda) wafuatilie hii habari. Mwisho wa siku ni kweli ikaonekana kuwa umeuawa tena kikatili. 

  Nikawasiliana na kaka yangu Dr Sebastian Ndege naye hakuamini. Jumapili ilipofika nikasema nisiseme chochote maana naona bado si kweli (nisamehe mdogo wangu) nikajikaza nikafanya Njiapanda bila kusema chochote. Jana jumatatu ndio Geah akanihakikishia kuwa ni kweli umefariki na baba yako amekutambua na msiba kweli uko.

  Nimelia sana, sijui kwa nini umefanyiwa ukatili huu, siwezi kusema chochote kwa kuwa sijui, lakini kitu kimoja nachoamini na kinachoniuma moyoni mwangu ni kuwa mimi, wewe na Seba tumepambana sana Zaidi ya miaka kumi kuhakikisha unakua ok na afya njema, najiuliza swali yote hiyo ilikua kwa nini? JE NI KWELI KUWA JUHUDI ZOTE HIZO ZILIKUA KUKUTAYARISHA UJE UUWAWE KINYAMA NAMNA HII??

  Mwenyezi Mungu pekee ndie anayejua kilichotokea na ndiye anayejua hukumu ya kila mmoja wetu. Jackie mdogo wangu umeenda, umeacha wadogo zako na familia yako. Mungu akulaze mahali pema peponi mdogo wangu, naamini sasa utapumzika maana umehangaika sana na haya maisha.

  Familia yako naamini Mungu atabariki itakaa salama na yote yatakua heri. Dr Ally Kaduma na clinic nzima ya IDC wanakulilia, Clinic ya watoto na ya watu wazima ya DarDar wanakulilia watamiss unga wako ule wa uji wa watoto uliokua unaleta.

  Clouds Media yooote inakulilia, boss Ruge anakulilia, familia yote ya Njiapanda inakulilia, kina mama Derick na kina brother Gelvas na kaka yako mkubwa kabisa Danny Kiondo wanakulilia.

  Mimi, Dr Ndege, Mishy Singano, Jackie Chengula (tunamwita JACKIE mkubwa kwa kuwa wewe ulikua unajiita Jackie mdogo), Simon Simalenga, Amani Siri, Douglas Pius, Arnold Kayanda (hadi harusi yake ulisimamia), Geah Habib, Regina Mwalekwa, Ruge Mutahaba, Team Njiapanda ya tangu 2003 mpaka ya leo wote tunakulilia mdogo wetu. 

  Kwetu sisi wote wewe bado ni Jackie wa Njiapanda yule wa tangu 2004. Mdogo wetu mwenye upendo na uliyekua tayari kutumia hadithi ya maisha yako kama fundisho kwa wengine. Wewe ni shujaa na kamwe hilo halitokaa libadilike. Sheria itachukua mkondo wake kwa wote waliosababisha kifo chako na Mungu atamhukumu kila mtu kwa jinsi alivyotenda.

  Ninalia sana, ninahuzunika sana ninatamani ningeweza kufanya lolote lakini nimeshindwa ndio maana nikashindwa kukuokoa na hili, Mungu atanisamehe maisha yameniweka mbali na wewe mdogo wangu mpaka mauti yamekukuta. Kibaya Zaidi ni kuwa hata kukuzika sitaweza kwa kuwa niko mbali na nyumbani. Lakini ninaamini huko ulipo utafurahi kufahamu kuwa ninafanya yote haya ninayofanya ili niweze kuwasaidia waTanzania wenzetu vizuri Zaidi nao wawe na afya njema kama nilivyojitahidi kufanya yako iwe.

  Ulale pema peponi mdogo wangu, Jackline Masanja..
  Mungu ibariki familia yako,
  Mungu ibariki Clouds Media Group
  Mungu ibariki Njiapanda

  0 0
 • 11/26/14--04:39: Article 11


 • 0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la Kimataifa la kuchochea mwamko wa nafasi ya mabingwa wa uchunguzi tiba katika kuboresha huduma za tiba. Kongamano hilo linalofanyika katika Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam, limewakutanisha mabingwa wa tiba za afya kutoka nchi mbalimbali za Afrika na nje ya Afrika.
  baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akihutubia katika ufunguzi wa Kongamano hilo leo Novemba 26, 2014.


  0 0

  Wanaharakati kutoka shirika la WiLDAF wakiwa katika maandalizi ya matembezi ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yaliayoanzia viwanja vya Mnazi mmoja na kuishia katika Ukumbi wa Karimjee hapo jana.
  Maandamano ya kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yakipita katika mitaa mbalimbali jijini Dar es Salaam hapo jana
  Maandamano ya kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yakipokelewa na Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Anna Maembe
  Mgeni rasmi katika siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Anna Maembe ambaye alikuwa anamuwakilisha Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akitoa hotuba yake.
  Mratibu wa Kitaifa shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Ndugu Judith Odunga akitoa hotuba yake katika siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.


  0 0

  Na Andrew Chale

  ASIA Idarous Khamsin na Safari  Carnival  wanakuletea usiku wa Khanga Party na Spice Modern Taarab watakaowasha moto wa burudani sambamba na gwiji wa mipasho nchini Khadija Kopa pamoja na Bilal Mashauzi,  Jumamosi ya usiku wa Novemba 29, ndan ya ukumbi wa Safari Carnival, Mikocheni B.

  Kwa mujibu wa  mmoja wa wandaaji wa usiku huo, Asia Idarous Khamsin,  amesema tayari maandalizi yake yamekamilika na amewasihi wadau kujitokeza kwa wingi katika onesho hilo la aina yake  kwa kiingilio cha sh 10,000 na 20,000 kwa V.I.P.

  Asia Idarous Khamsin alisema Usiku wa Khanga, itaanza kuanzia usiku wa saa mbili  na kuendelea huku vazi maalum likiwa ni Khanga.

  "Usiku huu ni maalum kulienzi vazi la khanga, ambalo pia ndilo vazi maalum la usiku huo. Pia watafurahia muziki mzuri kutoka kwa magwiji wa taarab hapa nchini akiwemo Khadija Kopa, Spice Modern taaba na Bilal Mashauzi." alisema Asia Idarous Khamisin  ambapo pia alisisitiza vazi la khanga ni la heshima hasa kwa mwanamke wa Kitanzania hivyo kila mmoja atakapolitengeneza vizuri ama kufunga litamweka malidadi.

  Aidha, alibainisha kuwa, usiku huo pia kutakuwa na  zulia jekundu 'Red Carpet' ambapo watu mbalimbali watapata kupiga picha na mastaa na watu maalufu watakao jitokeza usiku huo.

  Pia alibainisha kuwa, tayari tiketi zimeanza kuuzwa sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam ikiwemo Fabak fashions Mikocheni na Safari Carnival  kwa mawasiliano piga 0754263363 au 0713263363

  0 0

    Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk akizungumza na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Bi. Malika Berak alipomtembelea Ofisini kwake Kikwajuni. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
   Ofisa  Ubalozi wa Ufaransa anaeshughulikia Ushirikiano na Utamaduni Philippe Boncour akisisitiza jambo katika mazungumzo na Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Said Ali Mbarouk (hayupo pichani) Ofisini kwake Kikwajuni
  Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk akimkabidhi zawadi ya kanga Balozi Malika baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Wizarani kwake Kikwajuni. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

  0 0

   Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephrahim Kwesigabo, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu Siku ya Takwimu Afrika itakayo adhimishwa Dar es Salaam kesho. Kulia ni Mtakwimu Mkuu, Adella Ndesengia.
   Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephrahim Kwesigabo, akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari  uliofanyika leo jijini Dar es Salaam kuhusu Siku ya Takwimu Afrika itakayo adhimishwa Dar es Salaam kesho.
  Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephrahim Kwesigabo, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) uliofanyika leo jijini Dar es Salaam kuhusu Siku ya Takwimu Afrika itakayo adhimishwa Dar es Salaam kesho. (PICHA NA VERONICA KAZIMOTO – MAELEZO).


  ========  ======  =======

  Na Veronica Kazimoto - MAELEZO

  26 Novemba, 2014.

  Tanzania itaungana na nchi nyingine barani Afrika katika kuadhimisha Siku ya Takwimu Afrika ambayo itafanyika tarehe 27 Novemba, 2014 katika ukumbi wa mikutano uliopo Jumba la Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza leo na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii Ephraim Kwesigabo wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu amesema lengo la kuadhimisha siku hiyo ni kuongeza ufahamu kuhusu nafasi na mchango wa tasnia ya takwimu katika kuleta maendeleo  ya kiuchumi na kijamii barani Afrika.Kwesigabo amesema kuwa, Kaulimbiu ya Siku ya Takwimu Afrika kwa mwaka 2014 ni “Takwimu Huria kwa Uwajibikaji na Ushirikishwaji wa Wadau wote”.

  “Kaulimbiu ya Siku ya Takwimu Afrika kwa mwaka huu imebeba ujumbe muafaka ambapo kwa kuwa sasa maendeleo ya Afrika yanategemea takwimu huria katika kuongeza uwajibikaji na ushirikishwaji katika kuandaa sera, kupanga na kutathmini mipango mbalimbali ya maendeleo na kufanya maamuzi sahihi, amefafanua Kwesigabo”.

  Takwimu huria ni takwimu na taarifa zinazozalishwa kwa ubora na viwango kutokana na tafiti au taarifa za kiutawala ambazo zinatolewa, kusambazwa na kutumiwa na mtu yeyote bila kikwazo chochote.  Akielezea baadhi ya sifa za takwimu huria Mkurugenzi Kwesigabo amesema ni pamoja na upatikanaji wake kwa urahisi kulingana na mahitaji ya watumiaji, ziwe kamilifu kwa kutoa ujumbe sahihi na unaoeleweka na ziwe katika mfumo  

  utakaomrahisishia mtumiaji kuzitumia kulingana na mahitaji yake pasipo kizuizi chochote.  Sifa nyingine za takwimu huria ni kutokuwa na ubaguzi, zitolewe kwa wakati, na muundo wa uhifadhi wake uwe rahisi ambao unaweza kusomeka katika programu mbalimbali za kompyuta.

  Kwesigabo ameongeza kuwa Serikali ya nchi yoyote inapokuwa na mfumo wa takwimu huria, huwezesha wananchi na wadau wengine kupata taarifa na takwimu zinazozalishwa katika nchi hiyo bila kizuizi chochote. Aidha, huongeza uwazi na ushirikishwaji wa wananchi katika uendeshaji wa shughuli za Serikali.

  Washiriki mbalimbaliwa kutoka katika Wizara, Idara na Taasisi za Serikali, Wadau wa Maendeleo, Vyuo vya Elimu ya Juu, Wanafunzi wa Shule za Sekondari pamoja na Wadau wengine wa takwimu nchini wanatarajia kuhudhuria katika maadhimisho hayo. Maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika hufanyika tarehe 18 Novemba, kila mwaka lakini kwa Tanzania maadhimisho hayo yatafanyika kesho tarehe 27 Novemba, 2014.

  0 0

  Wanaharakati kutoka shirika la Kwieco la mkoani Kilimanjaro wakiwa katika maandalizi ya maadhimisho ya siku 16 za kupingaukatili wa kijinsia.
  Maandamano ya kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yakipita katika mitaa mbalimbali ya mji wa Moshi.


  Mkurugenzui wa shirika la KWIECO ,Elizabeth Minde (mwenye miwani myeusi) akiwa katika maandamano hayo.
  Brass Band ya Chuo cha Polisi ikiongoza maandamano ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa kanda ya kaskazini yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro.
  Maandamano yakiingia katika viwanja vya manyema ambako maandamano hayo yalikomea na kufuatia na burudani mbalimbali sanjari na hotuba toka kwa mgeni rasmi.
  Afisa habari wa shirika la KWIECO ,Veronica Ollomi akitoa maelezo juu ya utendaji kazi wa shirika kwa mgeni rasmi Mtumwa Mwako alipotembelea bana la shirika hilo .
  Afisa habari wa KWIECO ,Veronica Ollomi akitoa zawadi kwa mgeni rasmi Mtumwa Mwako.
  Mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili,mganga mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Mtumwa Mwako akipitia hotuba yake ,shoto kwake ni mwenyekiti wa kamati ya maadhimisho ya siku hiyo ,
  Mkuu wa dawati la jinsia mkoa wa Kilimanjaro ,Mrakibu wa jeshi la Polisi ,Grace Lyimo pia alikuwa miongoni mwa washiriki wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.
  Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ,Elizabeth Mushi akisoma risala mbele ya mgeni rasmi katika maadhimisho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya manyema mjini Moshi.
  Mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa kanda ya kaskazini ,Dk Mtumwa Mwako akitoa hotuba yake katika maadhimisho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Manyema.
  Mratibu wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili kanda ya kaskazini ,Hilary Tesha (katikatika)akijadiliana jambo na baadhi ya washiriki katika maadhimisho hayo katika viwanja vya Manyema mjini Moshi.
  Wanaharakati kutoka mashirika mbalimbali yanayopambana na vitendo vya unyanyasaji pamoja na ukatili wa kijinsia katika mikoa ya Kilimanjaro ,Arusha na Manyara wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi(hayupo pichani.
  NA Dixon Busagaga wa Globu ya jamii kanda ya kaskazini.

  0 0

  SAM_0100
  Mwanzilishi na Mwenyekiti wa kampuni ya Nabaki Afrika Hamish Hamilton akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi rasmi wa tawi kubwa la Arusha uliofanyika hivi karibuni
  SAM_0113
  SAM_0109
  Kulia niTania Hamilton akiwa na mumewe mwenyekiti wa kampuni Nabaki Afrika Hamish Hamilton
  SAM_0123
  Muonekano katika wa ndani
  SAM_0124
  Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo wakibadilishana mawazo wakati katika ufunguzi huo
  SAM_0125
  Vifaa vya ujenzi katika muonekano
  SAM_0128
  Mwanzilishi na Mwenyekiti wa kampuni ya Nabaki Afrika Hamish Hamilton akiwa anampa maelekezo mteja aliyetembelea tawi hilo siku ya ufunguzi hivi karibuni Nabaki Afrika imefungua rasmi tawi kubwa jijini Arusha eneo la njiro nyuma ya petro stationya BP katika jingo la RSA

  Aidha mafanikio hayo yamepatikana baada ya kutoa huduma yake Arusha kwa miaka miwili katika tawi eneo nane nane njiro Arusha,Sambamba na kuzinduzindua tawi hili Nabaki Afrika imesherehekea miaka 20 tangu kuzaliwa kwake hapa Tanzania jijini Dar es saalam

  Katika hatua nyingine Nabaki Afrika imejipanga zaidi katika kuboresha zaidi huduma kwa wateja wake ili kuwawezesha watanzania wote kufanya ujenzi bora na si bora ujenzi

  Kwa upande wake msimamizi mkuu wa tawi hilo Jesse Madauda alisema kuwa watu mbalimbalii wajitokeze katika tawi hilo ili waweze kupata msaada zaidi katika ushauri na bidhaa zenye ubora wa hali ya juukatika ujenzi

  Naye mwanzilishi wa kampuni hiyo Hamish Hamilton alisema changamoto pamoja na mafanikio waliyoyapata kupitia wafanyakazi wa kampuni hiyo kuwa ni watu wakujituma katika kazi

  Pia alisema kuwa kauli mbiu ya kampuni hiyo ni kuwa imejaribiwa imepimwa imeaminiwa na watanzania kwa mda mrefu sasa(Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)

  0 0

   Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Jumanne Sagini akionyesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) Daftari la Wapiga Kura linalotumika kuandikisha wananchi katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Kushoto ni Mratibu wa Uchaguzi huo Bw. Denis Bandisa.

  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Bw. Jumanne Sagini akiongea na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Desemba 14 mwaka huu ambapo amesema hadi sasa maandalizi yote yamekamilika. Kushoto ni Mratibu wa Uchaguzi huo Bw. Denis Bandisa na kulia ni Afisa Mwandamizi wa TAMISEMI Bw. Mohamed Mavura.

   Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Bw. Jumanne Sagini akitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye  Daftari la Wapiga Kura ili waweze kushiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu. Pia Katibu Mkuu huyo amewataka Viongozi wote wanaosimamia uchaguzi huo kuzingatia sheria na kanuni za uchaguzi. Kushoto ni Mratibu wa Uchaguzi huo Bw. Denis Bandisa na kulia ni Afisa Mwandamizi wa TAMISEMI Bw. Mohamed Mavura.
   Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Bw. Jumanne Sagini  akitoa wito kwa Viongozi wa Vyama vya Siasa, Wagombea na Washabiki wao kuendesha kampeni kwa amani, utulivu na ustaarabu bila kukiuka kanuni na taratibu zilizowekwa. Kushoto ni Mratibu wa Uchaguzi huo Bw. Denis Bandisa.
   Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Jumanne Sagini akionyesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Mwaka 2014 ambazo tayari zimesambazwa kwa wadau wote wa uchaguzi huo. Aidha amesema kuwa Kanuni hizo zimewekwa katika Tovuti ya TAMISEMI ambayo ni www.ps@pmoralg.go.tz . Kushoto ni Mratibu wa Uchaguzi huo Bw. Denis Bandisa.
  Mratibu wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kutoka TAMISEMI Bw. Denis Bandisa akifafanua utaratibu wa kumuandikisha Mpiga Kura katika Daftari laWapiga Kura wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Amesema Serikali imetenga Shilingi Bilioni 20 kwa ajili ya Uchaguzi huo. (PICHA NA MAELEZO).

  0 0

   Mchezaji mpya wa Yanga, Emerson Oliveira Neves Roque akiwasalimia mashabiki wake timu hiyo, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere.
    Mchezaji mpya wa Yanga, Emerson Oliveira Neves Roque akiwasalimia kwenye Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere.
    Mchezaji mpya wa Yanga,Emerson Oliveira Neves Roque (katikati) mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere. Kushoto ni Andrey Coutinho

   Mchezaji mpya wa Yanga, Emerson Oliveira Neves Roque (kushoto) akiwasalimia mashabiki wa timu hiyo, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimatifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa na mchezaji mwenzake Andrey Coutinho (katikati).

  Mchezaji mpya wa Yanga, Emerson Oliveira Neves Roque (kulia) akiwa na wadau wa Klabu ya Yanga.
  Maximo akiwasili.

  0 0

   Ndugu wa Marehemu Sebastian Mgimba Philipo Mgimba (katikati) akiwa amebeba msalaba huku pembeni ndugu mwingine akiwa pamoja na picha ya marehemu wakati wa misa fupi ya mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar Es Salaam leo.
  Dada wa Marehemu Sebastian Mgimba, Mariam akiwa na ndugu zake wakati wa sala ya mazishi iliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni leo
   Rafiki wa Marehemu akiweka udongo kwenye kaburi la Marehemu Sebastian Mgimba mara baada ya sala fupi ya mazishi kufanyika
   Baba Mzazi wa Marehemu Sebastian Mgimba, Mzee Mgimba pamoja na Mama wakiwa na shada la maua tayari kwa kuweka juu ya kaburi la Mtoto wao Marehemu Sebastian Mgimba.
   Ndugu wa Marehemu Sebastian Mgimba wakiweka shada la Maua juu ya kaburi la Marehemu Sebastian Mgimba
   Dada wa Marehemu Sebastian Mgimba, Bi Mariam Lukaza akiwa na mumewe Johnson Lukaza wakijiandaa kuweka shada la Maua juu ya Kaburi la Marehemu Sebastian Mgimba katika mazishi yaliyofanyika leo katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar Es Salaam.
  Mama Leoncia Lukaza akijiandaa kuweka Shada la Maua kwa niaba ya familia ya Lukaza katika kaburi la Marehemu Sebastian Mgimba kwenye mazishi ya marehemu Sebastiani Mgimba yaliyofanyika leo katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar Es Salaam.
  Umati wa Watu waliojitokeza kwaajili ya Kumpumzisha Ndugu yetu Sebastian Mgimba katika makaburi ya Kinondoni.Picha na Josephat Lukaza - http://www.josephatlukaza.com
  Marehemu Sebastian Mgimba alifariki dunia tarehe 20 Nov 2014 nchini Malaysia, Marehemu ameacha Mke na mtoto mmoja. Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahala Pema Peponi Amin

  0 0

  ·         Wafanyakazi wa Airtel kutembea ili kukusanya jumla ya zaidi ya milioni 10.
  ·         Wafanyakazi wa Airtel kukarabati darasa na kununa madawati shule ya kumbukumbu.

  Wafanyakazi wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mpango wake maalumu wa “Airtel tunakujali” imeandaa matembezi ya hisani huku ikialika wadau wote wenye wito wa kuchangia elimu kuungamkono jitiada hizo ili kukamilisha lengo la kuikarabati shule ya msingi kumbukumbu iliyopo kinondoni jijini Dar es Saalam.

  Matembezi hayo yanayoandaliwa na wafanyakazi wa Airtel yatashirikisha wadau mbalimbali na yatafanyika siku ya Jumamosi tarahe 29/11/2014 kuanzia saa moja asubuhi katika viwanja vya ofisi ya Airtel Makao makuu Morocco.

  Akiongea kuhusu Matembezi haya Meneja huduma kwa jamii Hawa Bayumi alisema “wafanyakazi wa Airtel nao wameona mapungufu yaliopo shuleni hapo na kuamua kujitosa kwa kutumia sehemu ya kipato chao kuihudumia jamii kwa njia hii, kila mfanyakazi wa airtel ambae amehamasika tayari ameshachangia.

  Na sasa tumeona ni vyema kuishirikisha jamii pia wakiwemo wanafamilia, marafiki na wote wenye wito wa kuchangia elimu kuungana nasi kuhakikisha watoto wanaosoma shule ya kumbukumbu wanasoma katika mazingira mazuri

  “Lengo ni kukusanya zaidi ya shilingi milioni 10 ili kukarabati darasa moja na kununua madawati kwa ajili ya darasa la wanafunzi wa darasa awali”  
  Tutafanya Matembezi ya Kilomita 5 ambapo ni ya wazi ili kila mtanzania aweze kushiriki na kuchangia, pia kutakuwa na Tshirt maalumu zinapatikana katika ofisi ya Airtel Makao Makuu kwa gharama ya shilingi 15,000. Kwa kununua lengo ni kumfanya kila mmoja aweze kuchangia.

  Tunatoa wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza na kuungana nasi katika matembezi haya kwa kununua tshirt hizi maalumu na kwa kujitokeza kutembetea nasi ili kuwezesha vijana wetu ambao ni taifa la kesho kupata elimu bora ,katika mazingira mazuri  na yaliyoboresha zaidi. Aliongeza Hawa

  Airtel chini ya mpango wa”Airtel Tunakujali” unaoendeshwa na wafanyakazi katika vitengo mbalimbali umeshika kasi ambapo kitengo cha huduma kwa wateja kilifanya burudani na kumshirikisha banana zoro na mzee king Kikii na sasa kitengo cha rasilimali watu na ofisi ya mkurugenzi imeandaa matembezi ya hisani lengo likiwa ni kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia maeneo mbalimbali yanayozunguka jamii hususani kwenye elimu ambapo utekelezaji wake unategemea kutafanyika mapema mwakani.

  0 0

   Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Industries Group), mfanyabiashara maarufu Afrika, Alhaji Aliko Dangote akitumia gari kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda chake kikubwa cha saruji katika Kijiji cha Msijute, mkoani Mtwara leo.
   Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Industries Group), mfanyabiashara maarufu Afrika, Alhaji Aliko Dangote (kushoto) akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Dangote nchini, Esther Baruti kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara leo.
   Balozi wa Nigeria nchini, Dk. Ishaya Manjanbu akimlaki Alhaji Dangote.

   Dangote akiwa na Mwakilishi Mkazi wa Kampuni yake hapa nchini, Esther Baruti

  Dangote akikaribishwa na viongozi wa kampuni ya Dil & Sinoma alipowasili eneo la Kiwanda cha simenti cha Dangote.
   Alhaji Dangote akiwa na maofisa wake  katika kikao na viongozi wa kampuni inayojenga kiwanda hicho ya Dil & Sinoma kwa ajili ya kupewa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho ambacho kitakuwa cha tatu kwa ukubwa Afrika.   Waandishi wa habari wakimhoji Dangote kuhusu maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho
                                                                        Alhaji Aliko Dangote
   Alhaji Dangote akiwa kwenye msafara wa magari akikagua maendeleo ya ujenzi ya kiwanda cha saruji Mtwara

   Mwakilishi Mkazi wa Kampuni hiyo ya Dangote hapa nchini, Esther Baruti akiwa na mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni ya Dangote
   Alhaji Dangote akisindikizwa kwenda kupanda ndege kwenda nchini Ethiopia kuendelea na ziara yake.


   Ndege ya bilionea huyo wa Afrika, Alhaji Dangote ikitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara
   Alhaji Aliko Dangote kutoka Nigeria, akilakiwa na Mwakilishi Mkazi wa Dangote nchini, Esther Baruti alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara leo. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

   Ofisa Mnadhimu wa Poilisi Mkoa wa Mtwara, George Salala akiagana na Alhaji Dangote
   Alhaji Dangote akipanda ndege tayari kuondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara
   Mwakilishi Mkazi wa Dangote hapa nchini, Esther Baruti akiondoka baada ya kuagana na Dangote
  Ndege iliyombeba Alhaji Dangote ikipaa.

older | 1 | .... | 413 | 414 | (Page 415) | 416 | 417 | .... | 1897 | newer