Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live

TASAF YAENDESHA MAFUNZO KWA WAWEZESHAJI WA UTAMBUZI WA KAYA MASKINI KATIKA WILAYA YA MUFINDI MKOANI IRINGA.

0
0
 Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF unaendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo wawezeshaji wa utambuzi wa kaya maskini katika halmashauri kadhaa nchini. Zoezi hilo ni mwendelezo wa jitihada za TASAF za kunusuru kaya maskini nchini zoezi lililoanza mwaka uliopita kwa awamu katika maeneo mbalimbali nchini.

Miongoni mwa halmashauri ambako mafunzo hayo yanafanyika ni wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa ambako wawezeshaji hao watashiriki katika kuwapa mafunzo wadodosaji watakaofanya kazi ya tathmini itakayowezesha kutambua kaya maskini katika vijiji vipatavyo 94.
Zifuatazo ni picha za washiriki wa mafunzo hayo yanayoendeshwa na TASAF.
 Baadhi ya washiriki wa warsha ya utambuzi wa kaya maskini inayoendeshwa na TASAF.
 Baadhi ya washiriki wa warsha ya utambuzi wa kaya maskini katika eneo la utekelezaji la wilaya ya Mufindi wakimskiliza mwezeshaji wa warsha (hayupo pichani).
 Mmoja wa wawezeshaji katika warsha ya kuwajengea uelewa wawezeshaji ngazi ya halmashauri ya wilaya ya Mufindi akiwasilisha mada.
 Mtaalamu wa ushauri wa TASAF katika halmashauri ya wilaya ya Mufindi ,Lawrence Mwakitalu akitoa mada kwenye warsha ya kuwajengea uelewa wawezeshaji wa ngazi ya halmashauri ya wilaya ya Mufindi.
washiriki wa warsha ya utambuzi wa kaya maskini katika wilaya ya Mufindi mkoani Iirnga wakimsikiliza mwezeshaji wa warsha hayupo pichani.

Top 10 Reasons to drink ARGI+

0
0



Top 10 Reasons to drink ARGI+

In summary, what are the benefits of taking ARGI+?

1. Is a marvelous daily supplement that supports better health throughout many systems of the body, delivering optimal performance.
2. Supports the immune system. Nitric oxide derived from L-Arginine, is used by white blood cells to attack bacterial etc. as it is toxic to them and makes these immune cells more lethal.
3. Helps maintain a healthy blood pressure and cardiovascular system.
4. Aids bone and tissue growth and repair, so is particularly appropriate after fractures and soft tissue injury.
5. The nitric oxide formed, permits greater blood flow and may improve sexual function.
6. Increases muscle mass and strength, whilst reducing the amount of fatty tissue. A welcome benefit for sports men and women.
7. The pomegranate and fruit components are a rich source of antioxidants, needed to fight the damaging effects of free radicals.
8. Contains an extract of red wine, which helps to reduce blood cholesterol levels.
9. Affects insulin sensitivity so is particularly useful in maintaining blood glucose control.
10. Acts to release anti-ageing hormones. Who wants to look older than their years?

What Vitamins are in ARGI+?

1. Vitamin C-for immune system, a healthy nervous system, concentration sleep and healthy bones and skin.
2. Vitamin K2 ? for bone formation, blood clotting, healing and vitality.
3. Vitamin B6 for immune system, a healthy nervous system brain, muscles, oxygen transportation, protein, fat and carbohydrate metabolism.
4. Vitamin D3 ? for the immune system, bones, a healthy nervous system and positive mood.
5. Vitamin B9- for new cells, brain, nerves and growth.

WITH SO MANY HEALTH BENEFITS, IT?S NO WONDER L-ARGININE IS GENERATING SO MUCH EXCITEMENT AT ONLY TSH 132,000. CALL 0786139316/0769888605 FOR MORE INFORMATION.

WAFANYAKAZI WA BENKI YA CRDB WASHEREHEKEA SIKU YA FAMILIA

0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akifafanua jambo wakati wa Sherehe za Siku ya Familia iliyofanyika katika hoteli ya Kunduchi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei (wa pili kulia mstari wa nyuma) na Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali Watu wa benki hiyo, Dorah Ngaliga wakiwa katika picha ya pamoja na watoto waliohudhuria tamasha la ‘Family Day’ lililowashirikisha wafanyakazi wa benki hiyo pamoja na familia zao. Tamasha hilo lilifanyika Kunduchi Wet 'N' Wild Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei  Naibu Mkurugenzi wa Benki ya CRDB.
Wafanyakazi wa benki ya CRDB.
Wafanyakazi wakiwa picha ya pamoja.
Vikombe vya washindi walioshinda katika michezo mbalimbali.
Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali Watu, Dolah Ngaliga akizungumza katika sherehe hizo. Kushoto ni Dk. Kimei.
Dk. Kimei akivishwa nishani.
Maofisa wa Benki ya CRDB wakifurahia jambo.
Dk. Kimei akifurahia nishani aliyotunzwa kwa kuwajali wafanyakazi kupitia Family Day.
Washindi wa kwanza katika mchezo wa Soka wakiwa katika picha ya pamoja na Dk. Kimei.
Shabani Badi akipokea kikombe kutoka kwa Dk. Charles Kimei baada ya kuwa washindi wa kwanza katika mchezo wa soka.
Washindi wa pili.
Picha ya pamoja.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB pamoja na familia zao wakiingia katika hoteli ya Kunduchi wakati wa sherehe za siku ya familia.
Michezo mbalimbali ikiendelea.

Wafanya kazi wa benki ya CRDB wakiwa pamoja na familia zao katika mchezo wa Soka wakati wa Tamasha la Family Day lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Watoto wakicheza michezo wakati wa sherehe za siku ya familia
Watoto wakiendesha treni.
Michezo katika maji.
Watoto wakicheza mpira wa kikapu.
Watoto wakichorwa michoro mbalimbali.
Husna Idd akipokea zawadi za madaftari baada ya kushinda katika kucheza muziki.
Husna Idd akionyesha kipaji cha kucheza muziki.

RATIBA YA KUAGA MWILI LEO NA MAZISHI YA ROBERT VICTOR LENGEJU

0
0

Familia ya Lengeju wa Kipera Mkoani Morogoro na Dar es Salaam inapenda kuwatangazia ndugu jamaa na marafiki wote wa marehemu ROBERT VICTOR LENGEJU na Familia ya LENGEJU kuwa kijana wao mpenda aliyefikwa na umauti Novemba 10, 2014 katika Hospitali ya TMJ baada ya kuugua kwa muda mfupi anataraji kuzikwa kesho Alhamisi nyumbani kwao Kijiji cha Kipera, Kata na Tarafa ya Mlali Wilayani Mvomero mkoa wa Morogoro.

Kipera ipo mbele kidogo ya Chuo Kikuu cha Mzumbe.

Mwili wa marehemu ROBERT LENGEJU, utaagwa leo kuanzaia saa 6:00 mchana baada ya Misa katika Kanisa Katoliki Msimbazi Dar es Salaam na baade jioni kusafirishwa hadi Morogoro.

Kesho Novemba 13 2014, kuanzia saa 5:00 Asubuhi taratibu za mazishi zitaanza nyumbani kwao KIPERA kwa misa takatifu na maziko.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.

KINUKAMORI WAOMBA DOLA 30,000 KUTENGENEZA AJIRA KWA WATU 300

0
0
DSC_0218
Mkurugenzi Mtendaji wa EWP na Mkurugenzi wa Kinukamori Enterprises, Bw. Alpha Phares Moshi (wa pili kushoto) akimkaribisha Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la maendeleo UNDP, Alvaro Rodriguez alipowasili kwenye Taasisi isiyo ya kiserikali inayo shughulika na uhifadhi wa mazingira eneo la Kinukamori, Marangu mkoani Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na UNDP huku akiwa amembatana na Mratibu wa Kitaifa miradi ya COMPACT mkoani Kilimanjaro, Victoria Nderumaki (wa tatu kulia) pamoja na Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu (wa pili kushoto).

Na mwandishi wetu, Moshi
Taasisi isiyo ya kiserikali inayo shughulika na uhifadhi wa mazingira eneo la Kinukamori, Marangu mkoani Kilimanjaro Executive Wilderness Program (EWP) inatafuta dola za marekani 30,000 kwa ajili ya kuendesha program tatu zenye kutengeneza ajira, ujasirimali, utunzaji wa mazingira na mvuto kwa watalii wanaokwenda kupanda mlima Kilimanjaro.
Kauli hiyo wameitoa kwa Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la maendeleo UNDP, Alvaro Rodriguez wakati alipofanya ziara mkoani Kilimanjaro kuangalia miradi inayofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

Uongozi wa EWP and Kinukamori Enterprises katika taarifa yao kwa Mratibu huyo, iliyosomwa na Mshauri wao wa fedha Grace Shayo wamesema pamoja na nia yao ya kuhakikisha maporomoko ya Kinukamori yanaendelea, kwanza kama taasisi na pili kama mradi wa kuhifadhi mazingira ya Mlima Kilimanjaro ambao ni sehemu ya urithi wa dunia, wakishirikiana na KINAPA wamefikiria miradi kadhaa ambayo ikienda kwa pamoja itaendeleza eneo hilo.

Wamesema fedha hizo zitatumika kutoa elimu ya ujasirimali kwa vijana 300 wanaoishi katika jamii ya Marangu ambao hutoa huduma mbalimbali kwa wenyeji na pia wageni wakiwemo watalii. Kundi hilo linalotakiwa kupewa mafunzo ni pamoja na wapagazi 50, waendesha pikipiki 100, wachuuzi 100 na walima mboga 50.

DSC_0221
Mshauri wa fedha wa EWP na Kinukamori Enterprises, Grace Shayo akisalimiana na Mratibu miradi ya UNDP Kitaifa, Nehemia Mususuri aliyembata na Bw. Alvaro Rodriguez. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa EWP na Mkurugenzi wa Kinukamori Enterprises, Bw. Alpha Phares Moshi.

Pia fedha hizo zitatumika kwa ajili ya kuanzisha na kutoa huduma ya chakula kwa wanaopanda mlima Kilimanjaro kwa lengo la kupunguza uchafu katika mlima huo na wakati huo huo kuongeza ajira kwa vijana. Aidha fedha hizo zitatumika kuanzisha kituo cha mazoezi kwa ajili ya wageni wanaotaka kupanda mlima Kilimanjaro kujizoesha na hali ya eneo hilo kabla ya kupanda mlima. Grace alisema shughuli zote hizo zimelenga vijana kuwa na maeneo ya kudumu yenye ajira endelevu.

Pamoja na kutoa ombi la kusaidiwa kupata fedha hizo, wameshukuru pia kwa misaada iliyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) kwa kupitia COMPACT.Wamesema kama si misaada hiyo eneo hilo ambalo lina historia ya kuharibiwa kwa mazingira yake lisingekuwa linavutia na kutoa ajira kama ilivyo sasa.

Eneo hilo limeboreka mazingira baada ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo ya EWP kazi iliyofanywa na Bw. Alpha Phares Moshi ambaye kwa sasa ndiye Mkurugenzi Mtendaji wa EWP na Mkurugenzi wa Kinukamori Enterprises ambapo kwa kushirikiana na KINAPA na COMPACT vijana walipewa elimu iliyowezesha kutengenezwa kwa mradi wa kuhifadhi mazingira ya mto Una wenye maporomoko ya Kinukamori.
DSC_0231
Bw. Alvaro Rodriguez akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye mradi huo.

Vijana hao ambao ndio wanaoishi katika mteremko wa mlima Kilimanjaro walianza shughuli hizo mwaka 1997 na kuanza kufikiria kuyatengeneza maporomoko ya Kinukamori kama chanzo cha kivutio katika juhudi za kuhifadhi mto Una.

Walisema kwa kuzingatia madhumuni ya kuanzishwa kwa mradi huo vijana na wanawake walianza kurejesha hali ya mazingira kwa kuyaweka bora na kudhibiti uharibifu wa ikolojia.
Kutokana na juhudi hizo miti zaidi ya 5000 mingi ikiwa ya asili ilipandwa kandoni mwa mto na sasa miti hiyo inatumika kutoa mafunzo na kurejesha hali ya upatikanaji wa maji ya kutosha kwa ajili ya wananchi wa Marangu.

Aidha wanyama na ndege waliokuwa wametoweka kutokana na uharibifu wa mazingira uliokuwepo kwanza wameshaanza kurejea eneo hilo.
Pamoja na mafanikio hayo EWP wanakabiliwa na changamoto kubwa hasa ukubwa wa eneo la shughuli zao ambalo ni ndogo na sasa wanataka kusaidiwa kufika hadi maeneo ya chemchem ya Soko iliyopo Kahe.
DSC_0262
Mshauri wa fedha wa EWP na Kinukamori Enterprises, Grace Shayo akisoma taarifa ya taasisi yao kwa Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la maendeleo UNDP, Alvaro Rodriguez.

Aidha wamesema wanakabiliwa na tatizo la fedha na hasa kushawishi vijana kujikita zaidi katika masuala ya uhifadhi wa mazingira na utalii wa kitamaduni. Naye Mwakilishi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa pamoja na kuwapongeza EWP kwa kufanikisha kurejesha mazingira katika hali ya kawaida katika eneo hilo amesema kwamba wataendelea kushirikiana nao kuhakikisha kwamba shughuli za hapo zinahifadhi mazingira na kutoa ajira kwa vijana.

Alisema duniani nzima kwa sasa inakabiliwa na tatizo la ajira kwa vijana ambao kutokana na kukosekana kwa ajira wanatopea katika ulevi na hivyo kuhatarisha nguvu kazi hiyo muhimu.
Alisema hata Tanzania pamoja na kuanza kufikiria kuwa na uchumi wa gesi, hatua hiyo itachukua muda lakini kuna haja ya vijana wanaomaliza shule wakawajibika katika miradi mbalimbali ya uhifadhi na maendeleo ya kiuchumi.
DSC_0271
Mshauri wa fedha wa EWP na Kinukamori Enterprises, Grace Shayo akikabidhi taarifa ya taasisi hiyo kwa Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la maendeleo UNDP, Alvaro Rodriguez aliyetembelea mradi wao na kujionea maendeleo yao.

Mwakilishi huyo pamoja na kutotoa ahadi katika ombi la taasisi hiyo amesema kwamba wataangalia nini cha kufanya kwani alifika eneo hilo kujifunza na kuona maendeleo kwani ana miezi miwili tu toka ameingia nchini kuwakilisha mashirika ya Umoja wa Mataifa.Alisema amefurahishwa na maendeleo yaliyopo na hasa kwa kuzingatia kwamba kulikuwa na tatizo la raslimali kufanya shughuli hiyo.

Alisema anatambua changamoto zilizopo cha ongezeko la watu, tatizo la ajira kwa vijana na mabadiliko ya tabia nchi na kwamba wataendelea kushirikiana na taasisi hiyo kuona kwamba changamoto hizo zinakabiliwa na kufutwa.
DSC_0228
Bango linaloonyesha tarehe ya kuzinduliwa kwa mradio huo wa COMPACT unaofadhiliwa na UNDP.
DSC_0455
Baadhi ya sheria zilizowekwa kwenye maporomoko ya maji ya Kinukamori yaliyopo Marangu mkoani Kilimanjaro.
DSC_0238
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu akiwa amefuatana na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la maendeleo UNDP, Alvaro Rodriguez kutembelea mazingira ya taasisi hiyo pamoja na vivutio vya kitalii vilivyomo kwenye Maporomoko ya maji ya Kinukamori yaliyopo Marangu mkoani Kilimanjaro.
DSC_0276
Pichani juu na chini ni mtoa maelezo kwa watalii (Guide) wa EWP na Kinukamori Enterprises, Pascal Cosma akitoa maelezo ya sehemu ya utamaduni wa Kabila la Kichaga kwa Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la maendeleo UNDP, Alvaro Rodriguez aliyembatana na ujumbe wake kutembelea miradi mbalimbali inayofadhiliwa na UNDP.
DSC_0280
DSC_0285
DSC_0283
Sanamu la aliyekuwa Chifu wa kabila la Wachaga Chifu Thomas Marealle lilipo kwenye taasisi hiyo.
DSC_0293
Pichani juu na chini ni mtoa maelezo kwa watalii (Guide) wa EWP na Kinukamori Enterprises, Pascal Cosma akiendelea kutoa maelezo ya tamaduni mbalimbali za kabila la wachaga ikiwemo na sanamu mbalimbali zilizowekwa kwenye taasisi hiyo.
DSC_0295

SHIWATA YALIA KUMPOTEZA AMIGOLAS

0
0
MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA)unaungana na watanzania kuomboleza kifo cha mwanamuziki maarufu Hamisi Kayumbu 'Amigolas' aliyefariki Jumapili na kuzikwa Jumatatu iliyopita katika makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema jana Dar es Salaam kuwa marehemu Amigolas atakumbukwa kwa mengi aliyoyafanya akiwa mwanachama wa mtandao huo alishiriki kutafuta eneo la makazi ya wasanii ya kijiji cha Mwanzega na shamba la wasanii lililopo Ngarambe wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.

Alisema alikuwa kiongozi wa mstari wa mbele pale  alipowahamamisha wanamuziki wenzake kujiunga SHIWATA kutoka bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta'akiwemo Luiza Mbutu,marehemu Abuu Semhando na wengine.

Marehemu Amigolas alifariki kwa ugonjwa wa moyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (M.N.H) alipokuwa amelazwa kwa siku tano kabla mauti kumkuta Jumamosi saa tano usiku.

Mkurugenzi wa African Stars 'Twanga Pepeta', Asha Baraka aliyekuwa mwajiri wake kabla ya kuhamia bendi ya JKT Ruvu alisema marehemu alikuwa mwanamuzi aliyejituma na kufanya kazi kwa juhudi zote kutoka ajiunge na bendi hiyo mwaka 1997.

Hivi karibuni SHIWATA imepoteza wanachama wake maarufu waliofariki akiwemo Abuu Semhando,Amina Ngaluma na Muhidin Gurumo.

Marehemu Amigolas alizikwa na umati mkubwa wa waombolezaji kwenye makaburi ya Kisutu Jumatatu saa 10 jioni. Ameacha wajane wawili na watoto wanne. Mungu ilaze roho marehemu mahali pema peponi. Amen.

ZAIDI YA WANARIADHA ELFU KUMI NA TANO KUSHIRIKI UHURUMARATHON 2014

0
0
ZAIDI ya wanariadha 15,000 kutoka ndani na nje wanatarajiwa kuthibitisha kushiriki katika mbio za Uhuru Marathon ambazo zinatarajiwa kufanyika Desemba 7 kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Mratibu wa mbio hizo, Innocent Melleck, alisema kuwa maandalizi yako katika hatua za mwisho huku akimtaja Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, anatarajiwa kuongoa mbio hizo.

Melleck pia alikabidhi ada ya Sh. Milioni mbili kwa Chama cha Raidha Tanzania (RT) na Sh. Milioni moja kwa wenyeji Chama cha Raidha Mkoa wa Dar es Salaam (DAAA), ili kupata kibali cha kuendesha mbio hizo.

Mratibu huyo alisema kuwa fomu kwa ajili ya kushiriki mbio hizo zimeanza kutolewa jana na jijini zinapatikana katika maduka yote ya TSN, huku pia zikitolewa kwenye mikoa ya Arusha, Moshi mkoani Kilimanjaro na Leaders.

“Tunawashukuru wadau wote walioshiriki katika kujiandaa kushiriki mbio hizo hasa klabu za jogging ambazo zinahamasisha wanariadha kushiriki mbio hizo zenye kuhamasisha Amani, ushirikiano na mshikamano,” alisema Melleck.

Katibu Mkuu wa RT, Suleiman Nyambui, alisema kuwa chama kimeialika mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani, nchi za Afrika Mashariki na mataifa mengine ambayo yako tayari kushiriki mbio hizo zitakazofanyika sambamba na sherehe za Uhuru wa Tanzania.

Nyambui alisema kuwa wanariadha wamejiandaa kuonyesha vipaji vyao na wanaamini yataendelea kukuza vipaji vyao kulitangaza jina la Tanzania. Naye Mjumbe wa DAAA, Tullo Chambo, alisema kwamba chama kimeshiriki kuanzia hatua ya awali na wanawahakikishia wadau kuwa mbio za mwaka huu zitakuwa na mafanikio. Chambo alisema kuwa wanazipongeza klabu na makundi yote yanayoendelea kujiandaa kushiriki mbio hizo na kila kitu kitafanyika kwa kufuata taratibu za kiufundi.

Melleck alitoa rai kwa makampuni na mashirika pia watu binafsi kujitokeza kwa wingi ili kuweza kudhamini mbio hizi kwani bado nafasi ipo kwa wale wote wenye nia ya kudhamini kwa mwaka huu.

Mbio za Uhurumarathon kwa mwaka huu zinadhaminiwa na Kampuni ya Bia nchini TBL kupitia kinywaji chake Grandmalt,Maji ya Uhui,Azam Tv,Tbc 1,Mwananchi Communications Ltd,Magazeti ya Uhuru,Jambo Leo,Michuzi media,CxC Africa,Kitwe General Traders,Samsung,Cokacola,Tindwa Mediacal Service,Gazeti la TABIBU,Konyagi,na TSN SUPERMARKETS.
Mratibu wa mbio za Uhuru Marathon 2014,Innocent Melleck (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar Es Salaam leo juu ya maandalizi ya mbio hizo kwa mwaka huu ambapo zinataji kufanyika Desemba 7,2014.Kulia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha nchini,Sulemani Nyambui na kushoto ni Mjumbe wa Chama cha Riadha mkoa wa Dar es Salaam,Tullo Chambo
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha nchini,Sulemani Nyambui akizungumzia namna mbio hizo zitakavyokuwa ikiwa ni pamoja na njia zitakazokuwa zikitumika kwa washiriki wa mbio ndefu.Kulia ni Mratibu wa mbio za Uhuru Marathon 2014,Innocent Melleck na kushoto ni Mjumbe wa Chama cha Riadha mkoa wa Dar es Salaam,Tullo Chambo.
Mratibu wa mbio za Uhuru Marathon 2014,Innocent Melleck akionyesha moja ya fomu za kujiunga na mbio hizo wakati akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar Es Salaam leo juu ya maandalizi ya mbio hizo kwa mwaka huu ambazo zinataji kufanyika Desemba 7,2014,huku Mgeni rasmi akitazamiwa kuwa ni Rais Jakaya Mrisho Kikwete huku Zaidi ya wanariadha elfu kumi na tano kukadiriwa kushiriki kwa mara ya kwanza.kushoto ni Mjumbe wa Chama cha Riadha mkoa wa Dar es Salaam,Tullo Chambo
Mratibu wa mbio za Uhuru Marathon 2014,Innocent Melleck akiendelea kuongea na vyombo vya habari.
Kutoka kwenye Kamera: anaonekana Mjumbe wa Chama cha Riadha mkoa wa Dar es Salaam,Tullo Chambo akizungumza machache.
Mratibu wa mbio za Uhuru Marathon 2014,Innocent Melleck (katikati) akikabidhi ada ya Sh. Milioni mbili kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Raidha Tanzania (RT),Suleiman Nyambui (kulia) huku Mjumbe wa Chama cha Riadha mkoa wa Dar es Salaam,Tullo Chambo akizungumza machache akishuhudia.
Mratibu wa mbio za Uhuru Marathon 2014,Innocent Melleck akikabidhi ada ya Sh. Milioni moja kwa Mjumbe wa Chama cha Riadha mkoa wa Dar es Salaam,Tullo Chambo.

MDAU ALALAMIKIA KUCHELEWESHWA UTOLEWAJI WA VYETI VETA.

0
0

Lalamiko langu kubwa ni kuhusu VETA kumekuwa na tatizo la ucheleweshaji wa vyeti pindi wahitimu wanapomaliza course zao siju ni kwanini? 

Tukiangaliwa vyuo vingi vinavyomilikiwa na serikali wanafunzi wanapomaliza shule yao na matokeo yao yakatoka uwa wanapewa result
slip inayoonyesha kuwa huyu mtu amemaliza course fulani na ameshinda wakati anasubili cheti chake na cheti hakichelewi sana kutoka kama ilivyo kwa VETA kitu ambacho ni tofauti na VETA.

Mwanafunzi anapomaliza course yake na matokeo yakatoka amefauru anasubili cheti karibu mwaka mzima sasa huyo mwanafunzi au mhitimu kama anatafuta kazi ataipataje bila cheti? au atafanyaje maombi katika vyuo vingine kwa ajili ya kujiendeleza? Jamani tunaomba milifanyie kazi maana sio kawaida kabisa ni uonevu hasa kwa vyuo vya mikoani kazi zenyewe zimekuwa ngumu bila cheti cha uhakika sio rahisi kupata kazi.
TUNAOMBA WAHUSIKA WALIFANYIE KAZI
Nimewasilisha

Mwenyekiti wa Chadema aunguruma mikoa ya KIGOMA na KATAVI

0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kazuramimba mkoani Kigoma, katika mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM juzi.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Zanzibar), Salumu Mwalimu akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kazuramimba mkoani Kigoma, katika mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM juzi.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akiwakabidhi kadi za Chadema waliokuwa viongozi wa CCM wa serikali ya kijiji cha Kapalamsenga katija jimbo la Mpanda Vijijini, baada ya kujiunga na Chadema katika mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM juzi.
Badhii ya waliokuwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa serikali ya kijiji cha Kapalamsenga katika jimbo la Mpanda Vijijini, wakimkabidhi kadi za CCM Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, walipoamua kujiunga na Chadema, baada ya mkutano wa Oparesheni Delete CCM, uliofanyika kijijini Hapo juzi.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akisalimiana na Bi. Mariamu Ramadhani (86), baada ya kuwasili katika kijiji cha Kapalamsenga mkoani Katavi, ambako alihutubia mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM juzi.

Nishati na Madini yatakiwa kushirikisha jamii kwenye uanzishaji wa miradi

0
0
Mtaalam Mwelekezi kutoka Kampuni ya Petrogas Bw. Tom Mitro (kushoto) akielekeza namna ya kuandaa mapendekezo ya miradi ( project proposals) mbele ya washiriki wa mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki kutoka Wizara ya Nishati na Madini wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zinawasilishwa na Bw. Tim Mitro kutoka kampuni ya Petrogas (hayupo pichani).
Mtaalam Mwelekezi kutoka Kampuni ya Petrogas Bw. Tom Mitro akisisitiza jambo wakati wa mafunzo hayo.

Na Greyson Mwase, Bagamoyo

Wataalamu wa Nishati na Madini wametakiwa kushirikisha jamii inayozunguka miradi inayoanzishwa ili kuzuia migogoro inayoweza kutokea kutokana na wananchi kukosa uelewa na miradi mipya.

Wito huo umetolewa na mtaalamu kutoka kampuni ya Petrogas Bw. Tom Mitro katika mafunzo ya jinsi ya kuandaa mapendekezo ya miradi, sera pamoja na utekelezaji wake yanayoendelea mjini Bagamoyo. Mafunzo hayo yalishirikisha wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi (TDGC).

Bw. Mitro alisema kuwa katika nchi nyingi za Afrika hususan zenye rasilimali nyingi kumekuwepo na migogoro mikubwa katika uanzishwaji wa miradi kutokana na jamii kutoshirikishwa kabla ya kuanzishwa kwa miradi.

Alisema katika hatua za awali za maandalizi ya miradi, wadau mbalimbali muhimu wamekuwa wakishirikishwa ikiwa ni pamoja na taasisi za kifedha, serikali, wanasiasa, wahisani huku kundi la jamii inayozunguka miradi husika likisahauliwa kabisa.

Akielezea athari za kutowashirikisha jamii inayozunguka miradi Bw. Mitro alisema kuwa ni pamoja na migogoro inayopelekea kukwama kwa miradi hali inayopelekea miradi kutokamilika kwa wakati.

“ Wananchi wengi wanapokosa uelewa wa miradi yenye manufaa kwa taifa, matokeo yake ni kuipinga hali inayopelekea kukwama kwa miradi hiyo.” Alisema Bw. Mitro. Bw. Mitro alisema kuwa jamii inayozunguka miradi pamoja na asasi za kiraia zina umuhimu mkubwa sana katika ushirikishwaji katika uanzishaji wa miradi kwani ndio walinzi wa miradi husika hususan miundombinu yake.

Akilelezea jinsi jamii inayozunguka miradi inavyoweza kushirikishwa Bw. Mitro alieleza kuwa ni pamoja na mikutano ya mara kwa mara na wananchi ikiwa ni pamoja na wawakilishi wao na kusisitiza kuwa wanaposhirikishwa katika kila hatua ya mradi wanakuwa mabalozi kwa wananchi wenzao.

Aliongeza kuwa ushirikishwaji wa jamii unaifanya jamii kuwa sehemu ya umiliki wa miradi na kulinda miundombinu yake.

Mafunzo hayo yameandaliwa na mradi unaohusika na kuwajengea uwezo wataalamu wa nishati na tasnia ya uziduaji (CADESE; Capacity Development  in the Energy Sector & Extractive Industries) lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wataalamu kutoka sekta za nishati na madini katika uandaaji wa mapendekezo ya miradi mbalimbali ( project proposals) na sera na hivyo kuepusha gharama ya kutumia wataalamu kutoka nje na kukuza umiliki.

Mafunzo hayo yatakayochukua wiki tatu yatashirikisha washiriki 60 ambapo kila kundi la washiriki 20 litajifunza kwa muda wa wiki moja. Kundi la kwanza litajifunza juu ya uandaaji wa mapendekezo ya miradi na kufanya tathmini yake ( project proposals preparations and evaluations ), kundi la pili litajifunza juu ya uandaaji wa sera na kundi la tatu litajifunza juu ya usimamizi wa miradi.

Mradi wa CADESE unaofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Maendeleo (UNDP) ulianzishwa mwaka huu unatekelezwa na Wizara ya Nishati na Madini kwa kushirikiana na wadau wengine kama vile Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Taasisi ya Uogozi na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF).

WATU WATANO WADAIWA KUPOTEZA MAISHA NA WENGINE KUJERUHIWA VIBAYA KUFUATIA AJALI YA BASI LA WIBONELA KUPINDUKA MJINI KAHAMA LEO

0
0


 Basi la Wibonela linalofanya safari zake kahama Dar limeua watu zaidi ya watano na kujeruhi wengi leo asubuhi eneo la Fantom Kahama. Chanzo ni mwendo kasi uliomshinda dereva wa basi hilo kukata kona ya kuingia barabara kuu hivyo kuruka nje na kusababisha basi hilo kupinduka. Na pia kibaka aliyekuwa anapekua na kuchomoa fedha na Vitu kwa majeruhi wa ajali hiyo amepigwa na kuchomwa moto hadi kufikia na watu wenye hasira kali. Mpaka sasa haijajulikana majeruhi ni wangapi na waliokufa ni wangapi.

MWILI WA MAREHEMU ROBERT LENGEJU WAAGWA JIJINI DAR ES SALAAM KUZIKWA KESHO KIPERA MOROGORO.

0
0
Hili ndilo sanduku lililouhifadhi mwili wa Mwandishi/Mchambuzi wa Jukwaa Maalumu la MWALE WA DEMOKRASIA katika Gazeti la Raia Tanzania (Gazeti dada la Raia Mwema), kila Alhamisi. Mwili wa shujaa huyo wa Demokrasia uliswaliwa katika Kanisa Katoliki M<simbazi Jijini Dar es Salaam leo. 

Watu mbalimbali walihudhuria katika misa hiyo ya kumsindikiza Lengeju katika safari yake ya mwisho kabla ya maziko yatakayo fanyika kesho (Novemba 13,2014) Kijijini kwako Kipera, Kata na Tarafa ya Mlali, Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro. Na Mroki Mroki-Father Kidevu Blog.
wanakwaya wakiimba katika misa hiyo.
wanafamilia wakiwa Kanisani katika misa.
Wanafamilia, ndugu jamaa na marafiki wakiwa katika misa hiyo leo.
 Kaka wa Marehemu Charles Lengeju akiwa amebeba msalaba wa marehemu.
Gari lililobeba mwili wa marehemu Robert Lengeju likiwa tayari kwa safari ya Kipera Mkoani Morogoro. 

 Ndugu wa marehemu Robert Lengeju wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa mdogo wao.
Heshima za mwisho ziliendelea kutolewa na ndugu jamaa na marafiki.
Godfrey Dililunga kutoka kampuni ya Raia Mwema wachapaji wa gazeti la Raia Mwema na Raia Tanzania akitoa heshima za mwandishi huyo wa Makala za Mwale wa Demokrasia katika gazeti lao.
Mhariri wa Raia Mwema, Ezekiel Kamwaga akitoa heshima kwa mwili wa marehemu.
Waombolezaji wakipita kutoka heshima za mwisho.
Mkuu wa Mkoa wa Mstaafu, Isdore Shirima nae alikuwepo kutoa heshima za mwisho kwa Lengeju.
Waombolezaji

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AIWAKILISHA TANZANIA KWENYE MAZISHI YA RAIS SATA WA ZAMBIA

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Rais wa Zambia Marehemu Michael Chilufya Sata Ikulu mjini Lusaka Zambia jana Novemba 11,2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal wa kwanza (kushoto) akiwa na Rais Mstaafu wa Zambia Mhe. Rupia Banda, Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta, Rais wa Msumbiji Mhe. Ermando Guebuza na Kaimu Rais wa Zambia Dkt. Guy Scott kwenye Misa Maalum ya kuaga mwili wa Rais Michael Sata iliyofanyika jana Novemba 11,2014 kwenye Uwanja wa Taifa mjini Lusaka Zambia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akizungumza na Katibu Mkuu wa Chama cha Tawala cha PF Mhe. A.B. Chikwanda kwenye Viwanja vya Ubalozini katika Makaburi ya Viongozi wa Kitaifa wakati mazishi ya Rais wa Zambia Marehemu Michael Chilufya Sata yaliyofanyika jana Novemba 11,2014 kwenye uwanja wa Taifa mjini Lusaka Zambia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimfariji Rais mstaafu wa kwanza Zambia Dkt. Keneth Kaunda mara baada ya kumalizika maziko ya Rais wa Zambia Marehemu Michael Chilufya Sata kwenye Viwanja vya Ubalozini katika Makaburi ya Viongozi wa Kitaifa yaliyofanyika jana Novemba 11,2014 mjini Lusaka Zambia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimfariji Rais mstaafu wa Zambia Mhe. Ruphia Banda baada ya kumalizika mazishi ya Rais wa Zambia Marehemu Michael Chilufya Sata kwenye Viwanja vya Ubalozini katika Makaburi ya Viongozi wa Kitaifa yaliyofanyika jana Novemba 11,2014. katikati Rais mstaafu wa kwanza wa Zambia Dkt. Keneth Kaunda. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisaini kitabu cha maombolezo ya Rais wa Zambia Marehemu Michael Chilufya Sata kwenye Viwanja vya Ubalozini katika Makaburi ya Viongozi wa Kitaifa yaliyofanyika jana Novemba 11,2014. (Picha na OMR)

DR MWAKA SPORTS XTRA NDONDO CUP TEMEKE MARKET NA BLACK SIX MECHI YALALA

0
0

Michuano ya DR MWAKA SPORTS XTRA NDONDO CUP imeendelea leo kwenye uwanja wa Bandari maeneo ya Tandika Mwembe Yanga kwa kuzikutanisha timu za TEMEKE MARKET na BLACK SIX ya Buguruni,mchezo huo umemalizika kwa timu hizo kushindwa kumpata mshindi baada ya kufungana bao 1-1 baada ya dakika tisini,na pia ilipofika changamoto ya mikwaju ya penati timu zote zilitumbukiza mikwaju yote mitano kimiani na kupelekea mwamuzi wa mchezo huo kuuvunja baada ya giza kuingia. Mchezo huo sasa utarudiwa siku ya jumanne ya tarehe 18/11/2014 kwenye uwanja huo huo wa Bandari. Robo Fainali ya tatu inaytaraji kupigwa kesho kwenye uwanja huo huo wa Bandari kati ya Burudani FC ya Temeke Mikoroshini dhidi ya Kiluvya UTD kutoka mkoani Pwani. 1Mashabiki wakishuhudia mtanange wa TEMEKE MARKET na BLACK SIX ya Buguruni kwenye DR MWAKA SPORTS XTRA NDONDO CUP. 2Mpambano ulipigwa kwenye dimba la Bandari maeneo ya Tandika Mwembe Yanga..... 3
ssssssssssssssssssssssssssssss 4ssssssssssssssssssssssssss 5sssssssssssssssssssss 6sssssssssssssssssssssssssssssss 7ssssssssssssssssssssssss 89CaptureMshambuliaji wa zamani Yanga na Singida Utd Kipanya Malapa ( Kulia ) alikuwepo pia kuipa sapoti timu yake ya Black Six... GAZA Kiungo wa zamni wa Simba Gerorge Lucas 'GAZZA' anayeonyeshwa na mshale pia alikuwepo

TAASISI YA STARKEY HEARING FOUNDATION YAKABIDHI MADARASA MATATU SHULE YA MSINGI YA LOIBORSOIT

0
0
1Mwanzilishi wa Taasisi ya Starkey Hearing Foundation, Bill Austin pamoja na Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka wakifunua kitambaa kuashiria ufunguzi rasmi wa majengo matatu ya shule ya Msingi ya Loiborsoit yaliyojengwa na mwanzilishi huyo kwa ajili ya jamii ya Kimasai katika sherehe zilizofanyika eneo hilo wilayani Simanjiro mkoa wa Manyara jana.David na steven.23Mwanzilishi wa Taasisi ya Starkey Hearing Foundation, Bill Austin akipima sikio kwa mmoja wa watoto waliohudhuria kliniki iliyokwenda sambamba na ufunguzi rasmi wa majengo matatu ya shule ya Msingi ya Loiborsoit yaliyojengwa na mwanzilishi huyo kwa ajili ya jamii ya Kimasai katika sherehe zilizofanyika eneo hilo wilayani Simanjiro mkoa wa Manyara jana.
4Mwanzilishi wa Taasisi ya Starkey Hearing Foundation, Bill Austin pamoja na Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka wakifunua kitambaa kuashiria ufunguzi rasmi wa majengo matatu ya shule ya Msingi ya Loiborsoit yaliyojengwa na mwanzilishi huyo kwa ajili ya jamii ya Kimasai katika sherehe zilizofanyika eneo hilo wilayani Simanjiro mkoa wa Manyara jana.
5Mwanzilishi wa Taasisi ya Starkey Hearing Foundation, Bill Austin pamoja na mkewe, Tani wakipokelewa na wanakikiji wa Loiborsoit kwenye ufunguzi rasmi wa majengo matatu ya shule ya Msingi ya Loiborsoit yaliyojengwa na mwanzilishi huyo kwa ajili ya jamii ya Kimasai katika sherehe zilizofanyika eneo hilo wilayani Simanjiro mkoa wa Manyara jana.Kulia ni David Furnish mmoja wa wageni maarufu aliyehudhuria hafla hiyo.Yohana shinini.

7Wanafunzi wa darasa la kwanza wa Shule ya Msingi Loborsoit iliyopo Simanjiro wakiwa darasani huku timu ya Taasisi ya Starkey Hearing Foundation wakiwa nyuma yao wakati wa kukabidhiwa majengo hayo katika sherehe iliyofanyika Wilayani Simanjirojana..
911a
unnamed1Wakiwa katika picha ya pamoja unnamed2Wakurugenzi wa Kampuni ya Montage Nesto Mapunda na Teddy Mapunda wakiwa katika picha ya pamoja unnamed3Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Teddy Mapunda akishuka kwenye helkopeta iliyowachukua wakuu wa taasisi ya Starkey Hearing Foundation

WAZIRI MUHONGO AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA MCC

0
0
8
9Makamu wa Rais wa Mfuko wa Changamoto za Millenia (MCC) Kamran Khan ( wa kwanza kushoto ) akimweleza jambo Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (wa kwanza kulia) anayesikiliza katikati ni Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress mara baada ya kikao hicho.
11Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospter Muhongo katikati) katika picha ya pamoja ofisini kwake na Makamu wa Rais wa Mfuko wa Changamoto za Millenia (MCC) Kamran Khan (kushoto) na Balozi wa Marekani nchini , Mark Childress (Kulia)..
……………………………………………………………………
Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amekutana na Makamu wa Rais wa Mfuko wa Changamoto za Millenia (MCC) Kamran Khan na Ujumbe wake akiwemo Balozi wa Marekani nchini Mark Childress, katika kikao kilicholenga kujadili maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa MCC Awamu ya pili na masuala ya kuendeleza sekta ya nishati nchini. 
Kikao hicho kimezihusisha pia taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati na Madini ikiwemo, Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC) pamoja na taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (EWURA). 
 Katika kikao hicho, Profesa Sospeter Muhongo amezitaka taasisi hizo kutekeleza miradi hiyo kwa kasi zikizingatia suala la uwajibikaji, ubunifu, uwazi na kuongeza kuwa, miradi hiyo itatekelezwa bila kuwepo na mazingira ya rushwa , huku akisisitiza ushirikiano baina ya serikali na sekta binafsi katika uendelezaji wa miradi hiyo.
Kwa upande wake Makamu wa Rais wa MCC, Kamran Khan ameahidi kutoa ushirikiano kwa Wizara katika kutekeleza miradi hiyo ambayo inalenga kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa na umeme wa uhakika na wa kutosha. 
Kwa upande wake Balozi wa Marekani nchini Mark Childress amesisitiza suala la kuzingatia muda katika utekelezaji wa miradi hiyo na kuongeza kuwa, hakuna sababu itakayokwamisha miradi hiyo.

msanii wa bongofleva Geez mabovu afariki dunia mjini Iringa usiku huu.

0
0
Msanii wa muziki wa bongofleva (pichani enzi za uhai wake )Ahmed Ally Upete ambaye pia akitambulika kwa jina la kisanii  kama Geez Mabovu,emefariki Dunia mnamo majira ya saa moja usiku wa leo,taarifa zinaeleza kuwa Geez amekutwa na umauti nyumbani kwao mjini Iringa.Taarifa kamili tutawaletea kadiri ya zitakavyokuwa zikiingia,MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMEN

THE RICHEST PEOPLE IN AFRICA: MOHAMMED DEWJI NAMED YOUNGEST BILLIONAIRE IN AFRICA

0
0
DSC_0317-1024x682
24. Mohammed Dewji
Net Worth: $2 BILLION
Industry: Diversified
Country of Citizenship: Tanzania
Age: 39
Number of Jobs Created: 16,800
Mohammed Dewji has seen his net worth rise considerably over the past year as his MeTL group, a conglomerate in 11 countries with interests in trade, FMCG and manufacturing, undergoes significant expansion.

SERIKALI, UN, VYOMBO VYA HABARI KUTOA ELIMU DHIDI YA EBOLA

0
0
001
Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma kutoka Wizara ya Afya na Ustawi ya Jamii, Said Makora (kulia), akielezea jinsi Wizara hiyo inavyopambana kutoa elimu ya ugonjwa wa Ebola kwa wananchi wakati wa kongamano lililoandaliwa na UNESCO, WHO, UNICEF, Wizara ya Afya na Ustawi ya Jamii, uliofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Novemba 11,2014 jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo uliowakutanisha wamiliki wa Redio za kijamii kuwaelimsha Radio za Kijamii za Mikoani ni namna gani wanavyoweza kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi ya jamii ili kutoa taarifa sahihi kwa wananchi kuhusu ugonjwa wa Ebola, Ebola ni nini namna ya kujinga na dalili zake.(kushoto), Kushoto ni Mwenyekiti wa COMNETA ambaye pia ni Mkurugenzi wa Redio FADECO, Sekiku Joseph.(PICHA NA PHILEMON SOLOMON).
=======  ======  =======
SERIKALI , Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) na vyombo vya habari nchini hapa vimekubaliana kufanyakazi kwa pamoja kwa ajili ya kuelimisha watanzania kuhusu ugonjwa hatari wa Ebola. Katika juhudi za kuwekana sawa kuhusu uelimishaji wa umma kuhusu ugonjwa huo, kumefanyika kongamano la mafunzo kwa siku mbili, Chuo Kikuu huria jijini Dar es salaam.Kongamano hilo lilifanyika Novemba 10 na 11. Kongamano hilo liliwashirikisha viongozi wa radio za wananchi zaidi ya 28 kutoka Visiwani na Tanzania Bara.

Katika kongmano hilo kulitengenezwa mikakati mbalimbali yenye kuleta uelewa kwa umma na kuwafanya kuchukua hatua za tahadhari na kuzuia ugonjwa huo usiingie nchini.
002
Mshauri wa Redio Jamii na Mkufunzi kutoka Shirika la Kimataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Mwalimu akiendesha majadiliano kuhusu mikakati endelevu itakayowezesha kuihusisha jamii katika upatikanaji wa taarifa sahihi juu ya ugonjwa wa Ebola wakati wa kongamano hilo lililowakutanisha wamiliki wa radio za kijamii lengo ni kuwaelimsha Radio za Kijamii za Mikoani ili kutoa taarifa zilizo sahihi kwa wananchi kuhusu ugonjwa wa Ebola.

Kwa mujibu wa mmoja wa watu wanaounda kikundi kazi chenye lengo la kukabiliana na ugonjwa huo mafunzo hayo yaliandaliwa na Shirika la sayansi, elimu na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) . Aidha mafunzo hayo yaliwezeshwa kwa pamoja kati ya wizara ya afya na Umoja wa Afya duniani (WHO), na Shirika la kusaidia watoto la UNICEF.


Mafunzo hayo yaliyokuwa na washiriki walikuwa ni pamoja na wanachama wa wanamtandao wa vyombo vya habari Tanzania (COMNETA), yaligusa zaidi redio ambapo 25 kati yake zinaohudumiwa na Umoja wa Mataifa. Wakati lengo kuu ni kuwafanya watanzania waujue ugonjwa huo na kuanza kuchukua hatua za tahadhari, mafunzo yalilenga kushawishi vyombo hivyo kutenga muda mchache kwa ajili ya elimu hiyo ili kuzuia mlipuko wake nchini.
003
Mkurugenzi wa Redio Kwizera ilioko Ngara-Kagera, Damas Missanga akichangia mada yake wakati wa kongamano la kuwaelimsha wamiliki wa Redio za Kijamii za Mikoani ili kutoa taarifa zilizo sahihi kwa wananchi kuhusu ugonjwa wa Ebola.

Katika mafunzo hayo washiriki walidadavua ebola nini na jamii inaweza kujijenga namna gani ili kukabiliana na janga hilo la kidunia. Matumizi ya elimu ya mawasiliano yalitiliwa mkazo hasa kwa kubaini kwamba elimu hiyo ndiyo itakayoweza kutengeneza mkakati wa kuwabadili wengine na hivyo kuzuia kuingia kwake na kusambaa.

Washiriki na wawezeshaji walikubali kufanyakazi ya pamoja na Tume ya taifa inayoratibu mapambano dhidi ya Ebola katika kuelimisha umma kwa kuweka wazi taarifa za ugonjwa huo na namna ya kukabiliana nao.Iliamuriwa kwamba radio hizo za jamii zitatumika kuanzisha midahalo yenye lengo la kuwasilisha taarifa mbalimbali kutoka kwa kikosi kazi cha kukabiliana na ugonjwa huo.
004
Meneja wa Redio jamii FADECO ya wilayani Karagwe, Adelina Lweramula akichangia mada wakati wa kongamani hilo.

Radio hizo ambazo zina changamoto ya aina yake kuanzia zile za wafugaji wa Serengeti ambako mara nyingi nyama ndizo zinazoliwa hadi kwenye jamii mbalimbali na hasa makorido yenye wageni wengi kama Zanzibar. Aidha kongamano hilo limeboresha ushirikiano kati ya vyombo vya habari na serikali za mitaa ili kuendelea kutoa taarifa sahihi na zinazozingatia utamaduni wa eneo husika huku kukiwa na wito wa mabadiliko.

Katika kukabiliana na janga la Ebola na virusi vya Marburg, mafunzo hayo yaliangalia pia umuhimu wa kushirikiana katika kuhakikisha kwamba ugonjwa huo unashughulikiwa na kila mtu na kuondokana na hofu zinazofanya watu wayakimbie maeneo husika. Kumeelezwa ni lazima juhudi za makusudi zichukuliwe ili jamii kuelimishwa na wao kushiriki katika kukabilina na tishio la Ebola hata kwa vijiji ambavyo vipo pembezoni.

Kama alivyosema Dk. Said, Mwenyekiti mwezeshaji kutoka wizara ya afya na ustawi wa jamii alisema anafurahishwa ushirika na wadau umepelekwa hadi katika radio za jamii ambazo ni muhimu sana katika kuimarisha juhudi za kufikia wananchi waliopo pembezoni.
005
Wamiliki wa Redio za Kijamii wakiwa katika mkutano ulioandaliwa na UNESCO, WHO, UNICEF, Wizara ya Afya na Ustawi ya Jamii ili kuwaelimsha wa wamiliki hao kutoa taarifa zilizo sahihi kwa wananchi kuhusu ugonjwa wa Ebola.
006

Article 1

0
0

Viewing all 46201 articles
Browse latest View live




Latest Images