Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 401 | 402 | (Page 403) | 404 | 405 | .... | 1897 | newer

  0 0

   MAKATIBU wa Kata wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wilaya ya Moshi Vijijini wametishia kubwaga manyanga na kurudisha kadi zao ikiwa Katibu wao wa Wilaya ataendelea na jitihada za kutaka kukigawa chama kwa kumuandaa mtu wake kwa ajili ya kugombea Ubunge mwaka 2015.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti, viongozi hao ngazi ya kata katika wilaya ya Moshi vijijini, walisema migogoro na malumbano ndani ya CCM imekuwa chanzo cha wapinzani kushinda kiurahisi katika Jimbo la Vunjo.  Mmoja wa viongozi wa Makatibu hao ambaye hakutaka kutaja jina lake, alisema, lazima wanachama wa CCM wachague mtu wanayemtaka na siyo viongozi kuwachagulia mgombea.

    Wakizungumza mjini humo,makada hao ambao walikataa kutajwa majina yao kwa sababu za kuepusha malumbano, walidai kuwa  muda mrefu Katibu wao wa Wilaya amekuwa akifanya jitahada za kuhakikisha mtu wake anayemtaka anapita mwaka 2015.

  Mmoja wa viongozi hao ngazi ya kata, alisema Katibu wao wa Wilaya amekuwa hawasikilizi, huku akitumiwa na watu wenye fedha kuwapigia debe wagombea wao wanaowataka hususani katika kuwania ubunge mwakani.

  "Tumekuwa tukimshauri huyu Katibu wetu, lakini hatusikilizi na kuna mtu ambaye mwaka 2010, alikiyumbisha chama na sasa amerudi tena akiwa na mgombea wake na hali ikiendelea hivi chama kitashindwa tena mwakani'', alisema mmoja wa Makatibu Kata

  Alisema kuna kada ambaye anaandaliwa ingawa kwa sasa yupo nje ya wilaya hiyo ili aje kugombea ubunge na kwamba mpango  huo unaratibiwa na watu wenye fedha.

  Aliongeza kuwa wafanyabiashara wasiokitakia mema CCM wanataka wasimamishe mtu ambaye hakubaliki kwa lengo la kukiangusha ili wapinzani waweze kushindwa kiulaini..

  Mmoja wa mwanachana wa CCM, katika jimbo la Vunjo alisema, umefika wakati viuongozi kukaa pembeni na kwaachia wanachama wenyewe waamue kumpitisha mgombea wanayemtaka. Alisema CCM ni chama ambacho kinajali uhuru wa kila mtu, na umefika wakati vijana kupewa kipaumbele katika nafasi za uwakilishi ukiwamo ubunge hapo mwakani.

  Katibu wa CCM  katika wilaya ya Moshi Vijijini, Miriam Kaaya akizungumzia tuhuma hizo, alikanusha madai ya viongozi hao wa Kata na kusema kwamba malalamiko yote yanajadiliwa ndani ya vikao. Alisema hana mgogoro wowote na makada wenzake wa CCM na kwamba siku zote amekuwa akitaka kila mtu anayestahili haki aipate bila mizengwe.

  Alisema hana mpango wa kumbeba mgombea yoyote kwa kuwa muda wa kutafuta wagombea haujafika na kwamba hivi sasa wanashughulika na chaguzi za serikali za mitaa.

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea risala toka kwa Mwenyekiti wa Wazee wa Mkoa wa Dodoma Balozi Job Lusinde wakati wa mkutano na wazee wa mji wa Dodoma leo Oktoba 11, 2014 waliouitisha ili kuzungumza naye maswala kadhaa ya maendeleo.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wazee wa mji wa Dodoma leo Oktoba 11, 2014 waliouitisha ili kuzungumza naye maswala kadhaa ya maendeleo.
  Sehemu ya wazee wakati wa mkutano wao na Rais Kikwete mjini Dodoma leo Oktoba 11, 2014 waliouitisha ili kuzungumza naye maswala kadhaa ya maendeleo.


  0 0
 • 11/04/14--19:47: Article 3


 • 0 0

  BAADA ya matukio ya harusi ya Jumamosi iliyopita natoa onyo ole wake atakayeniomba mchango wa harusi, sitaki utani. Labda kwanza nikueleze jinsi tulivyopata misukosuko sana kwenye uchangiaji wa ile harusi, maana siku hizi hakuna pa kukimbilia, kila asubuhi unaamshwa saa kumi na mbili na meseji kwenye simu;

  “Ndugu rafiki na jamaa wa familia ya Pingapinga inakukumbusha kuwa harusi ya mtoto wao imekaribia hivyo mchango wako unahitajika”, baada ya wiki  meseji huwa kali zaidi;“Siku zinaisha kwa nini hautoi mchango, unajua familia ya Pingapinga ina shughuli ya harusi ya mtoto wao, toa upesi au la usitulaumu.”

  Basi hizi meseji zilikuwa nyingi kuliko zile za kampuni yangu ya simu inayobuni namna ya kunitoa mkwanja kila wiki. Hatimaye nikatoa faini, maana nisiite mchango, maana mchango haulazimishwi.

  Sasa Jumamosi ndiyo ikawa siku ya harusi, kadi nililetewa mapema , nikahakikisha koti langu la kuendea harusini nalicheki vizuri, maana haya makoti yanayokaa kabatini miezi ni muhimu kucheki vizuri maana unaweza kukuta panya kazalia kwenye mfuko halafu wakatimka kutoka  kwenye makazi yao wakati uko katikati ya kucheza mduara wa harusi.

  Kweli tukaingia ukumbini viti vilikuweko swafi, meza zimepambwa kwa maua na MC alitukaribisha kwa maneno mengi yaliyojaa vichekesho visivyochekesha, au vichekesho vingine vimesharudiwa na kila MC hapa mjini halafu akawa analazimisha watu wapige vigelegele! Yote bure watu walikuwa wamenuna maana hakukuwepo na dalili ya hata chupa moja ya kinywaji, ila ahadi kibao zikawa zinatolewa na MC, mara ‘Roli la bia linakuja toka breweries, mara shampeni leo inatoka Ufaransa kwa helikopta.”

  Ghafla wahudumu waliovalia vikofia kichwani wakapitisha sambusa mojamoja kwa kila mtu, wakisindikizwa na MC akituhamasisha tule tufurahi na bwana harusi. Kwa kweli hela yangu ikaanza kuniuma, kwanza nililazimishwa kulipa, halafu sioni chochote hawa jamaa vipi? Wakati ukumbi mzima ukiwa umeendelea kununa utadhani kikao cha msiba, MC akatuambia eti bwana harusi ana machache kabla ya kutuaga kwenda kupumzika na mkewe. Pamoja na kisirani tulikuwa na hamu kumsikia mshenzi huyu anataka kusema nini.

  Bwana harusi akasimama hata suti aliyovaa ilikuwa haijamkaa sawasawa, akakohoa kidogo akaanza, “Asante MC, kwanza naomba nimshukuru Mungu kwa kumuumba mke wangu, kwa hilo Mungu uko juu, kiukweli hapa nimepata mke mtulivu, mpole asiye na makeke, yaani najisikia nina bahati sana.

  “Naomba niwashukuru wakwe zangu kwa kukubali kupokea robo tu ya mahari na kuruhusu ndoa hii ifanyike. Pia nishukuru kwa zawadi zao za kitanda, godoro, kabati na makochi asante sana.  Naomba nimshukuru baba mwenye nyumba wangu kwa kukubali niwe na deni la kodi ya mwaka ili kufanikisha harusi hii, mzee upo juu.

  “Naomba nitoe shukrani kwa bosi wangu kwa kunipa likizo fupi ili nikamilishe shughuli hii, pia wafanyakazi wenzangu kwa zawadi yenu ya jiko la gesi. Namshukuru mke wa kaka yangu kwa kutuazima gauni la harusi, na kaka yangu kwa suti hii niliyovaa. Natoa shukrani kwa mtengeneza keki, nitairudisha keki kwako kesho kama tulivyokubaliana.

  “Nawashukuru wazazi wangu kwa kuja na kikundi cha ngoma toka kijijini, kweli kimeziba pengo la burudani katika harusi hii. Naishukuru kamati ya wazee wa kanisa kwa kufanikisha kumshawishi mke wangu aolewe na mimi, niwape aksante kwa akina mama jirani kwa kuja na sambusa mlizokula toka makwao ili kufanikisha harusi hii, mradi harusi hii ni furaha tupu. “MC wewe ni rafiki yangu nashukuru kwa kukubali tulipane kidogokidogo aksante sanaaaaa

  0 0

   Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za uzalishaji Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Abdullah Makame akimkaribisha mgeni rasmi Katibu Mkuu Afisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Zanzibar Salum Maulid Salum (kati kati) kufungua warsha ya utaarishaji mkakati Itifaki ya soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki. Wakwanza (kushoto) Makamu wa Rais wa Chamber of Commerce Zanzibar Ali Aboud Mzee.
   Katibu Mkuu Afisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Zanzibar Salum Maulid Salum akifungua mkutano huo unaofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resourt Mbweni Wilaya ya Magharibi Zanzibar.
   Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria ufunguzi wa Warsha ya utaarishaji mkakati Itifaki ya soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki wakifuatilia ufunguzi wa mkutano huo Zanzibar Beach Resourt Mbweni.
   Baadhi ya washirki wa warsha ya utaarishaji mkakati Itifaki ya soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki wakimsikiliza Katibu Mkuu Afisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora alipokuwa akifungua warsha hiyo.
   Picha ya pamoja ya washiriki wa warsha hiyo na Mgeni rasmi Katibu Mkuu Afisi ya Rais Ikulu na Utawalaq Bora Salum Maulid Salum (wa katikati) waliokaa.

   Waandishi wa habari wakimuhoji Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Biashara, uwekezaji na sekta za uzalishaji Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Abdullah Makame mara baada ya ufunguzi wa warsha hiyo.
   Dkt. Abdullah Makame akiagana na Katibu Mkuu Afisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Salum Maulid Salum baada ya kufungua warsha hiyo Hoteli ya Zanzibar Beach Resourt, Mbweni.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

  0 0

  12
  Dereva kutoka nchini Ujerumani Rainer Zietlof akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors, Bw.Wayne McIntosh (wa pili toka kulia) wakipata picha ya pamoja na wanahabari.
  Dereva kutoka nchini Ujerumani Rainer Zietlow (katikati) akizungumza na wanahabari kuhusiana na rekodi yake ya kusafiri umbali mrefu Duniani mara baada ya kuwasili nchini Tanzania kwenye Ofisi za Alliance Autos, Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors, Bw.Wayne McIntosh na kushoto ni Meneja Masoko wa CFAO Motors, Tharaia Ahmed.

  DEREVA raia wa Ujerumani Rainer Zietlof yuko mbioni kuvunja rekodi ya dunia ya kuendesha gari kwa kilometa 17,000 kutoka Ulaya hadi Afrika.
  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Zietlof alisema kuwa hiyo itakuwa ni rekodi yake ya tatu baada ya zile za awali alizovunja mwaka 2011 na 2012.

  Awali alivunja rekodi baada ya safari iliyojulikana kama `Panamerica’ambayo ilimchukua kutoka Tierra del Fuego hadi Alaska kwa siku 11 na saa 17 wakati ile ya `Russtralia’ ilimtoa Melbourne, Australia hadi St.Petersburg nchini Urusi ambako alitumia saa 18.

  Zietlof anayetumia gari aina ya VW Touareg V6 TDI alianza rasmi safari yake Septemba 21 mwaka huu huko North Cape nchini Norway na anatarajia kuikamilisha nchini Afrika Kusini, ambako atakuwa ametembea kwa kilometa 17,000. 

  Kwa mujibu wa dereva huyo, safari hiyo ndefu imempitisha katika nchi za Norway, Finland, Sweden, Denmark, Ujerumani, Jamhuri ya Czech, Slovakia, Hungary, Serbia, Bulgaria, Uturuki, Misri, Sudan, Ethiopia, Kenya na sasa Tanzania.
  Dereva huyo alizungumza na wandishi wa habari katika makao makuu ya CFAO Motors yaliyopo barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam, na kusema kuwa atachangia kiasi cha senti 20 za euro kwa kila kilomita, kwa vijiji vya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi (SOS) nchini Tanzania na Zambia.

  Mbali na kuahidi kuvichangia vijiji hivyo, Zietlot pia amesisitiza kuvitembelea vijiji hivyo atakavyo vichangia.Aidha, amelisifia gari hilo kutokana na uwezo wake wa kukabiliana na mazingira tofauti tofauti ya hali ya hewa kama baridi kali na joto pamoja na barabara mbovu.
  Mradi huu wa kuzunguka sehemu mbalimbali za dunia kwa gari hilo umedhaminiwa na makampuni ya Tehama, magari ya Volkswagen ya Ujerumani, Slovakia na Afrika Kusini.Katika safari hiyo Zietlow yuko na wasaidizi wake wawili, Marius Biela ambaye ni mpiga picha na mchukua video; Matthias Prillwitz ambaye ni mzoefu wa mbio za magari nchini Ujerumani.Dereva huyo alianza safari zake za barabarani mwaka 2005 na ameoa na ana mtoto mmoja.
  15
  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors, Bw.Wayne McIntosh (kushoto) akipata picha na Dereva toka nchini Ujerumani Rainer Zietlof
  Meneja Masoko wa CFAO Motors Ltd. Tharaia Ahmed(kushoto) akipata picha na Dereva Rainer Zietlof.
  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors, Bw.Wayne McIntosh akisoma cheti cha rekodi ya dunia alichopewa dereva toka Ujerumani.
  Dereva kutoka nchini Ujerumani Rainer Zietlof (wa kwanza kulia )akiwaelezea jambo wanahabari hawapo pichani Kushoto kwake ni Meneja Masoko wa CFAO Motors Ltd. Tharaia Ahmed
  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors, Bw.Wayne McIntosh akielezea ni kwa namna gani magari yao yako imara kuhimili masafa marefu akitolea mfano gari ya Volkswagen aliyosafiri nayo dereva kutoka nchini Ujerumani Rainer Zietlof.
  Dereva kutoka nchini Ujerumani Rainer Zietlof akioyesha cheti cha rekodi ya dunia mbele ya wanahabari
  Dereva toka nchini Ujerumani Rainer Zietlof akitoa maelekezo ya gari yake aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI
  Dereva toka nchini Ujerumani Rainer Zietlof akitoa maelekezo ya injini ya gari yake aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI aliyosafiri nayo kwenye nchi zaidi ya 19 Duniani.
  Dereva toka nchini Ujerumani Rainer Zietlof akitoa maelekezo ya bodi ya gari yake aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI aliyosafiri nayo kwenye nchi zaidi ya 19 Duniani.
  Dereva Toka Nchini Ujerumani Rainer Zietlof akitoa maelekezo ya sehemu ya kuweka vifaa vya akiba kwenye gari yake aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI
  Dereva Toka Nchini Ujerumani Rainer Zietlof akiendelea kutoa maelekezo ya Gari yake hiyo aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI
  Gari aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI inavyoonekana kwa ndani.

  0 0

  Jumla yaVijana 150 kutoka ndani na nje ya nchi wameudhuria Kongamano la Biashara kwa Vijana lililofanyika jijini Arusha ambapo Benki ya CRDB wakiwa ni miongoni mwa wadhamini wa  kongamani hilo.


  Kongamano hilo lilihudhuriwa na Vijana kutoka katika Vyuo Vikuu vya nchi za Afrika Mashariki na kuandaliwa na Taasisi ya AIESEC ambalo hujihusisha na ubunifu wa vipaji vya uongozi miongoni mwa vijana lililofanyika jijini Arusha hivi karibuni katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Hall CDTI- TENGERU, Arusha ambalo lilihudhuriwa na wanafunzi 150 kutoka nchi tofauti za kimataifa na 150 kutoka vyuo vya elimu ya juu ndani ya Tanzania.


  Benki ya CRDB kama miongoni mwa makampuni yaliyodhamini kongamano hilo, ilialikwa kuweza kutoa elimu juu ya “Teknolojia na Ubunifu” ambapo  Mkurugenzi wa mikakati na ubunifu wa Benki ya CRDB, Bw. Goodluck Nkini aliweza kutoa elimu hiyo kwa wanafunzi walengwa.


   Katika kongamano hilo washiriki walipata nafasi ya kuelemishwa kuhusu huduma za kibenki kwa njia ya kieletroniki zilizotolewa na Mangire Kibanda (Meneja huduma za kibenki kwa njia ya kielektroniki) ambaye alitoa elimu kuhusu huduma za kibenki kwa njia ya simu (SimBanking), kwa njia ya Internet (Internet Banking), mashine za mauzo (Pos), Wakala wa Benki (FahariHuduma).
  Mkurugenzi wa Mikakati na Ubunifu wa Benki ya CRDB, Bw. Goodluck Nkini akitoa mada kuhusu teknolojia  na ubunifu.
  Mkurugenzi wa Mikakati na Ubunifu wa Benki ya CRDB, Bw. Goodluck Nkini akitoa mada.
  Mkurugenzi wa Mikakati na Ubunifu wa Benki ya CRDB, Bw. Goodluck Nkini akijibu maswali ya wanafunzi.
  Ofisa Masoko wa Benki ya CRDB, Alma Ally (kushoto) akifafanua jambo kuhusu akaunti ya Scholar ambayo ni maalumu kwa wanafunzi.
  Baadhi ya wanafunzi wakipata elimu kuhusu huduma za kibenki.
  Meneja wa Huduma za Kibenki za Kieletroniki, Bw. Mangire Kibanda (kulia) akitoa elimu kuhusu huduma za kibenki za kielectroniki kwa njia ya simu (SimBanking), kwa njia ya Internet (Internet Banking), mashine za mauzo (Pos), Wakala wa Benki (FahariHuduma) kwa wanafunzi waliohudhuria kongamano hilo.
  Baadhi ya wanafunzi wakipata elimu kuhusu huduma za kibenki zitolewazo na Benki ya CRDB.
  Wanafunzi kutoka vyuo vya nchi za Afrika Mashariki na Kati wakisikiliza mada kutoka kwa Mkurugenzi wa Mikakati na Ubunifu wa Benki ya CRDB, Bw. Goodluck Nkini (hayupo pichani).
  Ofisa Rasilimali Watu wa Benki ya CRDB, Bw. Petro Kasindya (kulia), akitoa ufafanua kwa walengwa kuhusu mfumo wa Rasilimali Watu wa Benki ya CRDB. 

  0 0

  Fundi wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) akifanyia marekebisho moja ya mabasi ya shirika hilo.
   
   Wakazi wa Dar es Salaam wataanza kupokea huduma zilizoboreshwa zaidi kila watakapotumia mabasi yanayomilikiwa na Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), hii inatokana na mafunzo ya mwezi mmoja yanayotolewa na shirika kwa madereva, makondakta pamoja na wafanyakazi wengine wa shirika hilo.

  Akizungumza wakati wa ziara fupi ya waandishi wa habari katika makao makuu ya UDA jijini Dar es Salaam Jana, Mkuu wa kitengo cha mahusiano ya umma wa UDA, Bw.  George Maziku alisema kuwa miongoni mwa mambo mengine, kampuni yake imejikita katika utoaji wa mafunzo madhubuti kwa wafanyakazi wake ili kuboresha huduma zote zinazotolewa kwa wateja wa UDA.

  “Uongozi wa UDA unalichukulia kwa uzito mkubwa sana suala la usalama. Tumeupitia mtaala wa utoaji elimu kwa wafanyakazi wetu lengo likiwa ni kuboresha usalama na kufanya wateja wetu wafurahie huduma zinazotolewa na shirika. Tunatoa mafunzo haya kwa madereva wetu ili kuinua hali yao ya uzingatiaji wa usalama,” alisema Maziku.  

  Mbali na masuala ya usalama, mkuu huyo wa kitengo cha uhusiano aliahidi uboreshaji wa huduma kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kuwajali wateja, suala ambalo limekua likizua mjadala mkubwa.

  Bw. Maziku alisema kuwa kampuni yake ina mabasi yapatayo 400 jambo linayoifanya UDA kuwa kampuni ya kwanza Tanzania kuwa na magari mengi yanayofanya kazi kwa mkupuo, hivyo kuna uhitaji mkubwa sana wa kuweka viwango thabiti ambavyo vinaweza kuigwa na makampuni mengine.

  “Tunalenga kuwa na mabasi 3000 ifikapo mwakani lakini kikubwa zaidi kabla hata ya kupata idadi hiyo ya mabasi ni kuwapa mafunzo madereva wetu ili wawe na elimu ya kutosha na uzoefu wa kutosha katika sekta ya usafirishaji wa umma.

  “Kwa kulitambua hili, kampuni imeajiri wakufunzi kutoka ndani na nje ya nchi, ili kutoa mafunzo kwa madereva wetu na wafanyakazi wengine wanaojihusisha na usafirishaji, mafundi na wafanyakazi wote (hasa makondakta) katika kuwajali wateja,” alisema.

  Bw. Maziku alisema kuwa mbali na mafunzo hayo, kampuni imekuwa ikifuatilia kwa karibu sana tabia na  mienendo ya madereva na makondakta wake mara kwa mara kwa kuwatumia wasimamizi ambao hupanda mabasi ya kampuni hiyo bila ya makondakta na madereva kupewa taarifa.

  Kwa sasa, mafunzo yaliyokuwa yakitolewa na kampuni hapo awali, yameonyesha kuzaa matunda yaliyotarajiwa kwa kuwabadilisha baadhi ya madereva na makondakta wa kampuni hiyo.

  Hii ilibainika baada ya mkazi wa Dar es Salaam, ambaye amekuwa akitumia huduma za UDA kwa nyakati tofauti, Bw. Andrew Sanga , kukiri kuwa madereva wa UDA wapo tofauti ukilinganisha na madereva wengine wa mabasi ya abiria.

  “Ilikuwa ni adha kubwa kutumia usafiri wa umma kutokana na huduma mbovu ambazo abiria tulikua tukikumbana nazo. Madereva wengi wa abiria hawazingatii suala la usalama barabarani. Wanaendesha hovyo  bila kujali kuwa kuna watumiaji wengine wa barabara. Lakini nina furaha kusema kuwa madereva wa UDA wapo tofauti sana na wenzao,” alifafanua.

  0 0

  DSC_0235

  Katibu Mkuu Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Abdulhamid Mzee akifungua rasmi warsha ya siku moja ya iliyohusisha wadau mbalimbali wa maendeleo, kuangalia malengo ya programu ya maendeleo endelevu (SDGs), iliyoandaliwa na taasisi ya utafiti wa uchumi na jamii (ESRF) iliyofanyika hivi karibuni visiwani Zanzibar. Kulia kwake ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Mkurugenzi wa Idara Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy.

  Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez amepongeza juhudi zinazofanywa na Serikali ya Zanzibar katika kuangalia masuala muhimu yanayohusu muktadha ujao wa kufanikisha uondoaji wa umaskini uliotopea (SDGs) baada ya kukamilika kwa programu ya maendeleo ya milenia (MDGS).

  Alisema kitendo cha serikali kuandaa warsha ya kupashana kuhusu programu hiyo mpya kabla ya mazungumzo na mashirika ya Umoja wa Mataifa ambayo ni washirika wa maendeleo kuhusu SDGs kunaonesha dhamira ya dhati kwa serikali kuendelea kusukuma mbele maendeleo yenye lengo la kunemeesha wananchi.

  Mratibu huyo alisema hayo hivi karibuni katika warsha iliyofungulia na Katibu Mkuu Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Abdulhamid Mzee iliyokusanya wadau mbalimbali wa maendeleo kuangalia malengo ya programu ya maendeleo endelevu (SDGs),iliyoandaliwa na taasisi ya utafiti wa uchumi na jamii (ESRF).

  Warsha hiyo kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Programu wa ESRF Dk. Tausi Kida warsha hiyo ni sehemu ya kuelezana kuhusu mkakati huo mpya wa Umoja wa Mataifa unachukua nafasi ya MDGs na nafasi ya Tanzania katika kutekeleza malengo hayo ya kimataifa.
  DSC_0256
  Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza na wadau mbalimbali wa maendeleo kwenye warsha ya siku moja ya kuangalia malengo ya programu ya maendeleo endelevu (SDGs), iliyoandaliwa na taasisi ya utafiti wa uchumi na jamii (ESRF) iliyofanyika hivi karibuni visiwani Zanzibar. Kushoto kwake ni mgeni rasmi Katibu Mkuu Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Abdulhamid Mzee, Katibu Mtendaji Tume ya Mipango Zanzibar Amina Khamis Shaaban na Mkurugenzi wa Programu kutoka Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF) Dkt Tausi Kida.
   

  Warsha hiyo imefadhiliwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya UNDP, UNAIDS na UNWOMEN.Mratibu huyo wa mashirika ya Umoja wa Mataifa amesema kwamba agenda zilizopangwa kujadiliwa zinaonesha ujasiri wa Tanzania katika kuhakikisha inashiriki kwenye ajenda za dunia kwa kutekeleza nafasi yake katika mipango ya maendeleo na ustawi wa jamii kwa kuzingatia usawa wa jinsia.

  Alisema shughuli inayofanywa sasa ya kuwasilisha malengo hayo kwa majadiliano miongoni mwa wadau mbalimbali kabla ya majadiliano rasmi kati ya mashirika ya Umoja wa mataifa na serikali ni ya maana katika kuongeza uelewa na kuimarishwa kwa mawazo muhimu. 

  Warsha ya kwanza ya aina hiyo ilifanyika Oktoba 27 jijini Dar es Salaam ambapo wadau mbalimbali wakiwemo wanazuoni, wawakilishi wa serikali, taasisi zisizo za kiserikali na wengineo walijadiliana kuhusu SDGs na kama malengo yake yanawezwa kutekelezwa.

  Aidha warsha hiyo ilijadili kama malengo hayo yanawezwa kutumiwa na watunga sera na kuleta tofauti inayotakiwa na kama malengo hayo yanahitaji kuboreshwa zaidi ili kujua kitu cha kufanya na kama umma unaweza kujipanga kutekeleza malengo hayo.
  DSC_0285
  Mkurugenzi wa Idara Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akizungumza kwenye warsha ya siku moja kuhusu Malengo ya Milenia kwa washiriki mbalimbali na kwa kiasi gani Tanzania imeweza kufikia malengo hayo.
  Alvaro alisema agenda hizo zinakwenda vyema na mpango wa Msaada wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa kwa Tanzania (UNDAP) kwa kuwa imejikita katika maeneo muhimu yanayopambana na kutokomeza umaskini na kuwa na maendeleo endelevu.
  Maeneo hayo ni pamoja na malengo ya milenia ambayo hayajatekelezwa kwa ukamilifu, nishati, mabadiliko ya tabia nchi,mazingira na kujenga jamii yenye amani na kujali maendeleo.
  Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika Zanzibar Beach resort, Katibu Mkuu alisema ni vyema wazanzibari wakatumia nafasi hiyo kutengeneza mkakati wa Zanzibar wanayoitaka, Zanzibar yenye maendeleo inayojali haki na yenye amani.
  DSC_0334
  Mkurugenzi wa Programu kutoka Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF) Dkt Tausi Kida akitoa mada juu ya umuhimu wa kutafuta rasilimali za kutosha katika kufikia malengo ya milenia hasa kwa nchini zinazoendelea.
  Aliwataka wana warsha kutumia nafasi hiyo kujipanga vilivyo katika kuhakikisha wanajua kinachotokea duniani katika sekta ya maendeleo na kutumia nafasi hiyo kutengeneza muskabali wa wazanzibari unaoendana na malengo ya dunia ya kutokomeza umaskini na kujenga nchi yenye kujali maslahi ya jamii yenye maendeleo endelevu na amani.
  Alisema mafanikio ya malengo ya milenia yaliyojikita katika kutokomeza umaskini na njaa, kufanikisha elimu ya msingi kuyaleta usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake na kupunguza vifo vya watoto na wanawake wajawazito, kukabiliana na Ukimwi, kuhakikisha mazingira endelevu na kuleta mshikamano wa kimataifa katika maendeleo yanatakiw akuendelezwa.
  Alisema kwa miaka 15 zanzibar imefanya vyema katika programu hizo na kutaka wadau kufikiria kuimarisha na kuangalia kwenye udhaifu ili kuyakamilisha kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
  DSC_0320
  Mhadhiri wa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt Osward Mashindano akifafanua umuhimu wa kuwashirikisha wananchi wa ngazi ya chini kuhusu maswala ya malengo ya milenia ili yaweze kufikiwa kwa urahisi zaidi.
  DSC_0337
  Pichani juu na chini ni wadau mbalimbali wa maendeleo waliohudhuria warsha hiyo ya siku moja ya kujadili na kuangalia malengo ya programu ya maendeleo endelevu (SDGs), iliyoandaliwa na taasisi ya utafiti wa uchumi na jamii (ESRF) na kufadhiliwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya UNDP, UNAIDS na UNWOMEN.
  DSC_0266DSC_0294DSC_0362
  Pichani juu na chini ni washiriki wa warsha hiyo ya siku moja wakichangia hoja wakati wa majadiliano.
  DSC_0379DSC_0388
  Mkurugenzi wa Programu kutoka Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF) Dkt Tausi Kida akijibu moja ya maswali yaliyoulizwa na washiriki wa warsha hiyo.
  DSC_0308 
  Mgeni rasmi Katibu Mkuu Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Abdulhamid Mzee(katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa warsha hiyo.

  0 0

   King Of Swaghili Rapper Gosby leo ame tease mashabiki wake na cover ya single yake mpya kama alivyoahidi, Single hiyo inatarajiwa kutoka leo hii.
   
   Rapper Gosby aka King of Swaghili kutoka Swaghili Nation leo hii anatarajia kuachia ngoma yake mpya "WEMA SEPETU". Ngoma hiyo imerekodiwa ndani ya  studio za Feel Good Music na imetengenezwa kwa ushirikiano wa producers wawili, Jeffrey kutoka Marekani kwa upande wa midundo na Cjamoker kutoka Tanzania kwa upande wa recording, Mixing and Mastering.

  Akiongea na wanahabari Gosby amesema ameamua kushirikisha producers wa nje na wa ndani ya nchi ili kuongeza radha kwenye muziki wake na vilevile kupata uzoefu wa kufanya kazi na watayarishaji tofauti.
   
  “ Muziki wetu unakuwa kwa kasi kubwa, na kama mnavyojua kuwepo kwa mitandao mbalimbali ya kusambaza kazi zetu online inarahisisha sana kazi zetu kufika popote dunia, nadhani ni wakati muafaka sasa tukianza kuangalia soko hili kwa upana zaidi, kuwa na ladha ya bongo na vilevile kuweka ladha ya kimataifa pia"
   
  Akiongea “Wema Sepetu “ Gosby alikuwa na   haya ya kusema
   
  “ Wema Sepetu, dah sijui nianzie wapi ili iwe rahisi kueleweka, anyways.. Wote tunamjua Wema au tumewahi kusikia au kusoma habari kuhusu Wema, Ni former Miss Tanzania, Movies Star, Celebrity wa kike anayezungumzwa kuliko wengine wote ukanda wa Afrika Mashariki, mjasiriamali, Dada Mrembo haswaa!! Wasichana na wanawake wengi wanatamani kuwa Wema Sepetu kwa ujumla au sehemu tu, na huu wimbo umeongelea juu ya msichana au mtoto wa kike ambae labda anafanana na Wema Sepetu .”

  Gosby anaendelea.
  “ Sasa wimbo huu ni special kwa Mawema Sepetu wote ngoja nisimalize utamu, tega sikio leo hii inshallah.....Kwa nini Wema Sepetu mnaweza jiuliza swali hilo, i dont know".

  Kaa tayari kwa kazi hii mpya kutoka kwa Gosby

  0 0  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mwenyekiti wa TPSF, Dkt. Reginard Mengi, wakati alipowasili kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo Novemba 5, 2014 kwa ajili ya kufungua rasmi Kongamano la Kimataifa kuhusu Mitaji Hisa, lililoandaliwa na Taasisi ya Sekta isiyo rasmi ya TPSF.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la Kimataifa kuhusu Mitaji Hisa, lililoandaliwa na Taasisi ya Sekta isiyo rasmi ya TPSF, lililofanyika leo Novemba 5, 2014 kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo waliohudhuri ufunguzi huo wakimsikiliza Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akihutubia.


  0 0  Aliyekuwa MJumbe wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Amon Mpanju ambaye pia ni mwenyekiti wa wa shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania akiwaeleza waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu umuhimu wa Vijana kuwa wazalendo na kulinda amani iliyopo hapa nchini kwa maslahi mapana ya Taifa.

  Frank Mvungi-Maelezo

  Watanzania wametakiwa kuendeleza amani na mashikamano uliopo kwa maslahi ya Kizazi hiki na Kizazi Kijacho kwa kuenzi misingi ya Amani na Uzalendo iliyojengwa na Waasisi wa Taifa hili.

  Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na aliyekuwa Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Amon Mpanju ambaye pia ni mwenyekiti wa wa shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania.

  Nchi ni zaidi ya itikadi na Mihemko ya watu wachache hivyo ni lazima tuwaepuke wote wanaotaka kuvuruga amani na utulivu uliopo alisema Mpanju.

  Akifafanua Mpanju amesema hali iliyojitokeza katika moja ya midahalo iliyofanyika jijini Dar es salaam hivi karibuni ni ya kukemewa na watu wote wanaopenda amani na wazalendo kwa kuwa vitendo hivyo vinaweza kuleta madahara katika jamii hasa kwa makundi maalum kama walemavu,wanawake na wataoto.

  Akizungumzia Katiba inayopendekezwa Mpanju amesema ni vyema Watanzania wakaisoma na kuilewa ili kuepuka upotoshaji unaofanywa na baadhi ya watu kwa maslahi yao binafsi.

  Aliongeza kuwa ni vyema kuepuka kauli zinazoweza kuleta uchochezi katika jamii hasa katika kipindi hichi ambapo baadhi ya watu wamekuwawakitumia mwavuli wa Kutoa elimu kwa wananchi kuhusu Katiba inayopendekezwa na kufanya vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani.

  Pia Mpanju alitoa wito kwa vijana kuwa mstari wa mbele katika kupinga vitendo vyote vinavyoweza kupelekea uvunjifu wa amani hapa nchini kwa kuweka uzalendo mbele na kujali maslahi mapana ya Taifa na si ya Kikundi Fulani cha watu.

  Katika Hatua nyingine Mpanju alikanisha kuhusika na vurugu zilizotokea katika moja ya midahalo hapa jijini Dar es salaam na kudai hahusiki na tukio hilo kwa namna yoyote kama ilivyoripotiwa .

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Qatar aliyemaliza muda wake nchini Tanzania, Mhe. Jassin Mohamed Mubarak Al-Darwish, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Novemba 5, 2014 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi wa nchini yake nchini.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpokea na kumkaribisha Balozi wa Qatar aliyemaliza muda wake nchini Tanzania, Mhe. Jassin Mohamed Mubarak Al-Darwish, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Novemba 5, 2014 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi wa nchini yake nchini.

  0 0


  0 0

   Meneja wa kanda ya Nyanda za juu kusini Bw Ramadhan Sosora akitoa neno la ufunguzi na utambulisho kwa wanahabari.
   Meneja Masoko kutoka Mfuko wa Mafao ya Kustaafu wa GEPF Bw Aloyce Ntukamazina akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi huo kulia kwake ni Afisa masoko katika ofisi ya mbeya Bw Alex William.
   Pichani baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia kwa makini maelezo wakati wa uzinduzi huo.
   Bw Aloyce Ntukamazina akielezea mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 10 toka 2004 – 2014 yaliyopelekea uzinduzi wa ofisi mpya nyanda za juu kusini.
    Uongozi wa Mfuko wa GEPF ukipokea maswali mbalimbali kutoka kwa waandishi wa habari juu ya mipango ya Mfuko wa GEPF katika kupanua wigo zaidi na kufikia watanzania walio wengi.

  Baadhi ya waandishi wa habari walioalikwa wakichukua picha za tukio hilo katika ukumbi wa mikutano wa Mfuko wa GEPF.

  Bw Aloyce Ntukamazina Meneja Masoko wa Mfuko wa GEPF alielezea kuwa sababu kubwa zilipelekea kuzindua ofisi mpya nyanda za juu kusini kwanza ni ukuaji wa kasi wa shughuli za kiuchumi na kibiashara katika mkoa wa Mbeya lakini pia ni mafanikio makubwa ambayo Mfuko umeyapata kwa kipindi cha miaka 10 kutoka 2004 ambapo mfuko ulipata menejimenti yake rasmi hadi 2014.


  Alisema Mfuko umekuwa katika vigezo vyote kwa upande wa wanachama wameongezeka kutoka 16,131 hadi kufikia 76,000, Michango imeongezeka kutoka TZS 5.1 Billioni kwa mwaka hadi TZS 37.29 Billioni na Thamani ya Mfuko imeongezeka kutoka TZS 20.21 Billioni 2004 hadi TZS 245.38 Billioni 2014.


  Ukuaji huu umeonyesha Mfuko una afya njema na unaweza sasa kupanua wigo na kufungua ofisi mpya katika mikoa mingine.  Jambo la pili Bw Ntukamazina alieleza ni ukuaji wa kasi wa mpango wa hiari wa VSRS ambao kwa kipindi kifupi cha miaka mine tangu uanzishwe 2010 umeweza kuwasajili jumla ya wajasiriamali 35,481 ambao kwa kipindi kifupi hicho wamejiwekea akiba ya zaidi ya TZS 5.01 Billioni.  Alisema hii imedhihirisha kwamba mpango huu ni mkombozi kwa watanzania wote na Mfuko ukaona ni vyema sasa usogeze huduma zake karibu kwa watanzania waishio nyanda za juu kusini ili nao waweze kufaidika na mafao yatolewayo.  Mwisho Bw Ntukamazina alitoa wito kwa watanzania wote wajenge utamaduni wa kujiwekea akiba kwani uzee hauepukiki na ipo siku kila mmoja wetu ataishiwa nguvu za kuzalisha mali, lakini pia alisema GEPF kupitia mpango wa VSRS ina mipango madhubuti kuhakikisha kila mtanzania awe mkulima, mama lishe, mjasiriamali, muuza mitumba, mvuvi n.k nao wanalipwa Pensheni kama wengine walio katika ajira rasmi.  0 0

  1Kaimu Mkurugenzi mkuu na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Beatus Chijumba akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye makao makuu ya shirika hilo wakati alipotangaza kampeni ya siku 60 kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kujiuga na Mfuko wa Bima ya Afya katika Halmashauri zipatazo 54 nchini Katikati ni Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti na mwisho ni Ali Othman Mkuu wa kitengo cha Mifumo ya Mawasiliano.2  Kaimu Mkurugenzi mkuu na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Beatus Chijumba akizungumza na waandishi wa habari leo katika makao makuu ya NHIF Bendera Tatu jijini Dar es salaam kuhusu kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko huo, Kutoka kulia ni Ali Othman Mkuu wa kitengo cha Mifumo ya Mawasiliano, Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti na kutoka mkushoto ni  Dr Frank Lekei (Mkurugenzi wa Tiba na masuala ya kiufundi NHIF)3Athman Rehani Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) akifafanua jambo wakati wa mkutano huo , kutoka kulia ni Ali Othman Mkuu wa kitengo cha Mifumo ya Mawasiliano, Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti na Kaimu Mkurugenzi mkuu na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Beatus Chijumba.
  4Kutoka kulia ni Meneja wa CHF Bw. Costantine Makala,  Ali Othman Mkuu wa kitengo cha Mifumo ya Mawasiliano,Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti, Kaimu Mkurugenzi mkuu na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Beatus Chijumba, Athman Rehani Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), Mkurugenzi wa masoko na Utafiti NHIF,Raphael Mwamoto na Dr Frank Lekei (Mkurugenzi wa Tiba na masuala ya kiufundi NHIF).

  0 0

  UZINDUZI wa filamu ya Wape Salamu Zao unatarajia kufanyika siku ya Jumapili tarehe 9 November katika ukumbi Travetine Magomeni, jijini Dar es salaam.

  Uzinduzi huo utambatana na ujio wa sesson 2 kipindi cha Ulimwenguni wa filamu cha TBC 1,kinachoongozwa na Juma Mtetwa katika, kivutio kikubwa ni Jackson Kabirigi ‘Kisate’.

   “Nimepanga kuacha historia katika uzinduzi wa filamu ya Wape Salamu Zao, kuna vitu vingi sana ambavyo sijawahi kuwaonyesha watazamaji hajawahi kuviona kutoka kwangu tarajieni maajabu,”anasema Kabirigi. 

  Uzinduzi huu unasindikizwa na gwiji la muziki wa Taarab Bongo mfalme Mzee Yusuf, ambaye naye ameahidi kufanya show ya kipekee haijawahi kutokea hivi karibuni, na kuimba nyimbo zinazotamba na kufanya vizuri Tanzania. 

  Wasanii nyota wa filamu kutoka Bongo movie watakuwepo wakiwa wamependeza huku zuria jekundu likipamba sehemu ambayo watu watapata nafasi ya kupiga piga katika mapozi, show hiyo ya kufunga mwaka kiingilio ni 8,000/ tu kwa mtu mmoja si ya kukosa.
  0 0  MAKATIBU WAKUU WA WIZARA
   Rais Jakaya Kikwete amefanya uteuzi wa Makatibu Wakuu wa Wizara kwa kuteua Makatibu Wakuu wanne wapya na kuhamisha mmoja, uteuzi uliomuondoa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Charles Pallangyo.
  Pallangyo sasa anakua Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, nafasi ambayo inatafsriwa kuwa adhabu, siku chache baada ya vyombo vya habari ikiwamo FikraPevu kuibua kashfa ya uhaba wa dawa katika hospitali kubwa za serikali.
  Aidha, Rais Kikwete amefanya uteuzi na uhamisho wa Makatibu Tawala wa Mikoa.
  Taarifa iliyotolewa mjini Dodoma jioni ya leo, Jumatano, Novemba 5, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa walioteuliwa ni pamoja na Dkt. Donan Mmbando ambaye anakuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuchukua nafasi ya Pallangyo.

  Katika uteuzi huo Dkt. Yohana Budeba anakuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhandisi Mbogo Futakamba kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Dkt. Adelhelm James Meru ambaye anakuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii na Maliasili.
  Kabla ya uteuzi wake, Dkt Mmbando alikuwa Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Budeba alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Uvuvi na Mifugo, Mhandisi Futakamba alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji na Dkt. Meru alikuwa Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA).
  Aidha, taarifa hiyo imesema kuwa Rais Kikwete amemhamisha Bibi Maimuna Tarishi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii kwenda kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria
  Adoh Steven Mapunda, Mkurugenzi Mtendaji, Manispaa ya Bukoba amepanda na kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Severine Kahitwa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro na Dkt. Faisal Issa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro anahamishiwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza.
  Wakati huo huo, Rais Kikwete amemteua Kanali (Mst) Joseph Simbakalia, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, kuwa Mkurugenzi Mkuu wa EPZA kuchukua nafasi ya Dkt. Meru.
  Uteuzi huo unaanza leo na Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa wataapishwa, Alhamisi, Novemba 6, 2014, Ikulu, Dar es Salaam.

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mhe Samwel William Shelukindo kuwa Balozi na Msaidizi wa Rais Masuala ya Diplomasia leo Ikulu jijini Dar es salaam. Mhe Shelukindo anajaza  nafasi iliyoachwa wazi  na Balozi wa Tanzania nchini Marekani  Mhe Liberata Mulamula, na kabla ya hapo alikuwa Afisa mwandamizi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akumuapisha na kumpa vitendea kazi Mhe Jack Mugendi Zoka kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 6, 2014.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mhe John Vianney Mongella kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera leo Ikulu jijini Dar es salaam. Kabla ya hapo Mhe Mongela alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mhe Halima Omary Denengo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara leo Ikulu jijini Dar es salaam. Kabla ya hapo Mhe Denengo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Dkt Ibrahim Hamisi Msangi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi leo Ikulu jijini Dar es salaam. Kabla ya Hapo Mhe Msengi alikuwa mkuu wa wilaya ya Moshi
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akumuapisha  Dkt Yohana Budeba kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 6, 2014.

  Na Anitha Jonas, MAELEZO Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Profesa Jakaya Mrisho Kikwete leo amewaapisha viongozi kumi na moja aliyowateua, ambao ni Makatibu Wakuu wa Wizara ,Wakuu wa Mikoa,Mabalozi na Makatibu Tawala za Mikoa mbalimbali. Viongozi hao, waliapishwa leo jijini Dar es Salaam katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu na kuhudhuriwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue. 

   Miongoni wa viongozi walioapishwa ni aliyekuwa Mganga Mkuu wa Serikali, ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donald Mmbando, ambapo amesema katika swala la upungufu wa dawa mahospitalini atajitahidi katika bajeti ijayo kujenga hoja na kutetea manunuzi ya dawa. 

   “Serikali ina mpango mbadala wa utoaji wa vifaa vya afya kwani imeandaa mkakati wa kuboresha sekta ya afya ikiwemo kuangalia kuwepo na usawa wa gharama za huduma afya nchini,” alisema. Naye aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Mbogo Futakamba ameapishwa kuwa Katibu wa wizara amesema Wizara ya Maji imefanikiwa katika mpango wa Matokeo Makubwa Sasa(BRN) kwa kufikia 53% kutoka 40% katika kusambaza maji safi maeneo ya vijijini. 

   Aliongeza kwamba Serikali imefanya jitihada mbalimbali katika kuboresha mitambo ya maji Ruvu chini na kujenga visima ili kuwawezesha wakazi wa jijini Dar es Salaam kupata maji ya kutosha. Aidha aliyekuwa Mtumishi Mwandamizi Ofisi ya Rais, Jack Mgendi Zoka ameapishwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada, ambapo ameahidi kwenda kuiwakilisha vyema Tanzania huko na kuisaidia nchi kupata fursa nyingi na kutafuta wahisani wa kuchangia maendeleo katika taifa. Viongozi wengine, waliapishwa ni Jonny Vianney Mongela ambaye ameapishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera,

  Hapo awali alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha, ambapo amesema anaamini ushirikiano mzuri atakaoupata kutoka kwa wananchi ndiyo utakao changia mafanikio makubwa katika mkoa huo,pia kwa kupita uzoefu wake na ataenda kusimamia yote yaliyokwisha kuanzishwa ili kuleta mafanikio zaidi. Naye Bi.Amina Juma Masenza ameapishwa kuwa Mkuu wa Mkoa Iringa , amesema ataenda kuweka msisitizo wa vipao mbele vyote vya taifa katika mkoa wake na pia amesema anaamini kufanya kazi kwa ushirikiano ndio njia ya kuleta mafanikio makubwa katika mkoa huo. 

   Wengine waliaopishwa ni Mkuu wa Mkoa Mtwara Bi.Halima Omari Dendego, ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga amesema changamoto kubwa katika mkoa wake ni kupandisha pato la mkazi wa Mtwara na kupitia miradi mbalimbali iliyopo mkoa huo ikiwemo gesi kupatikana kwa mafanikio, katika swala hilo pamoja kusimamia maswala ya elimu katika mkoa huo. 

  Aidha naye Samuel Shelukindo aliapishwa kuwa Balozi na kupewa wadhifa wa kuwa Mshauri wa Rais masuala ya Kidiplomasia,alisema anamshukuru Rais kwa uteuzi huo na ameahidi kufanya kazi hiyo kwa uadilifu mkubwa huku akingalia maslahi ya taifa kwa ujumla. Katika hafla hiyo Makatibu Tawala walioapishwa ni Addo Mapunda na Charles Amos Pallangyo.older | 1 | .... | 401 | 402 | (Page 403) | 404 | 405 | .... | 1897 | newer