Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

HOSPITALI YA KAIRUKI YAPATA TUZO YA UBORESHAJI VIWANGO VYA HUDUMA YA AFYA

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Hospital ya Kairuki, Dk. Asser Mchomvu akiwa amebeba tuzo aliyokabidhiwa na na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal (katikati). Kushoto ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Seif Rashid.
Picha ya pamoja.

Na Mwandishi Wetu 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, ameukabidhi uongozi wa Hospitali ya Kairuki (KH) tuzo ya waliofanya vizuri katika vigezo mbalimbali vya uboreshaji viwango vya huduma ya Afya katika mkutano wa 4 wa kitaifa kuhusu uboreshaji Viwango vya huduma ya Afya uliofanyika wiki iliyopita (Octoba 31-2014) katika ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mkuu wa Hospital ya Kairuki, Dk. Asser Mchomvu alisema sifa ya mafanikio yao mpaka wakapata tuzo hiyo yanatokana na mafunzo  kwa wafanyakazi wa Hospital wapatao 20 yaliyoendeshwa na Wizara ya afya ikishirikiana na Jhpiego,CDC na PEPFAR.

Dk. Mchomvu aliongeza kuwa mafunzo kuendelea kutolewa na wakufunzi wa ndani (inhouse training), kuundwa kwa timu maalum ya ndani kwa ajili kufanya ukaguzi wa kushtukiza ndani na utayari wa KH kushirikia katika zoezi la udhibiti na uzuiaji wa maambukizi.

Aidha, Dk. Mchomvu alieleza kuwa siri nyingine ni ushirikiano mzuri baina ya manegimenti ya KH na timu ya wakaguzi toka wizara ya Afya katika kutekeleza maagizo na mapendekezo na kuyafanyia kazi.

“Kwa upande wetu maeneo yaliyofanya vizuri katika zoezi ili ni pamoja na mashine bora za kuuwa vijidudu (sterilization unit) na eneo zima katika kitengo hicho, eneo la kuifadhi/ kutenganisha na usafirishaji wa taka hatarishi, taka mbichi na taka mchanganyiko pia chumba cha upasuaji kufuata taratibu stahiki za kimataifa katika kuzithibiti maambukizi,” alisema Dk. Mchomvu.

Aliongeza kuwa wakati huohuo KH imezindua kampeni maalum za muda mrefu katika kuchunguza na kutibu magonjwa yasiyoambukiza, mfano saratani ya matiti, saratani ya shingo ya kizazi na saratani ya tezi dume (prostate). Saratani hizi ndizo zinazoongoza kwa  hapa nchini.
Moja ya mashine za kisasa za kupima saratani ya matiti katika Hospitali ya Kairuki.

“Lakini pia KH imezidi kuboresha huduma katika vitengo vya macho, sikio, pua na  koo kwa kupata mitambo ya kisasa katika nyanja hizo,” alisema Dk. Mchomvu.Aliongeza kwa kusema kuwa KH imezindua wodi mpya ya kisasa hasa kwa ajili ya wanachama  wa mfuko wa Bima ya taifa ya afya. (NHIF) na wodi maalum ya watoto.

Wengine waliotunukiwa tuzo hizo za uboreshaji wa huduma za afya ni Hospitali ya Bugando-Mwanza pamoja na Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC). 

Tuzo hizo zilitolewa na Wizara ya Afya wakishirikiana na Kituo cha Kudhibiti Maradhi cha Marekani (CDC) na Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR).

MSAMA AUCTION MART KWA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI WAKAMATA VIFAA MBALIMBALI VYA KUDURUFU KAZI ZA WASANII

$
0
0
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani), moja kati ya mashine 4 za  kurudufu CD  feki zilizokamatwa katika eneo la Kimara jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Ofisa wa Polisi, D/SSGT Daniel Gingo.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani), wino unaotumika kunakshia makasha ya CD feki wanazozitengeneza
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani), baadhi ya CD feki zilizokamatwa


=========  =======  =======  =======
KAMPUNI ya Udalali ya Msama Auction Mart ya jijini Dar es Salaam chini ya Mkurugenzi wake Alex Msama ikishirikiana na Jeshi la Polisi Kituo cha Urafiki na Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, imekamata kompyuta za kufyatua kazi feki za wasanii zenye thamani ya mil18.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart, Alex Msama, alisema mitambo hiyo imekamatwa kwa ushirikiano mkubwa kati ya pande hizo tatu pamoja na sapoti ya wasamaria wema. Alisema kopyuta, mashine na kazi feki zenye thamani ya mamilioni ya fedha, zimekamatwa eneo la Kimara-Machungwani, jijini Dar es Salaam na mtuhumiwa huyo amefikishwa katika kituo cha Polisi kwa ajili ya mchakato wa kiheria wa kufikishwa mahakamani. 

Msama alisema akiwa mdau wa masuala ya burudani kupitia kampuni yake ya Msama Promotions Ltd ambayo imekuwa ikiratibu matamasha ya Muziki wa Injili, amekuwa akiguswa na kitendo wanjanja wachache kunufaika na jasho la kazi ya wengine.Alisema wizi wa kazi za wasanii mbalimbali umekuwa kikwazo cha mafanikio ya wahusika ambao licha ya kuifanya kazi hiyo kwa muda mrefu, wameshindwa kupiga hatua kiuchumi kutokana na wajanja hao kuingiza kazi feki mtaani ambazo huuzwa kwa bei ya kutupa.

Msama alisema kazi hiyo ngumu ambayo imekuwa ikifanywa na kampuni yake kwa kushirikiana na wadau wengine, anashukuru kwamba kadiri siku zinavyosogea wengi wamezidi kukamatwa kutokana na ushirikiano ambao wamekuwa wakipewa.“Msama Auction Mart tunachukua nafasi hii kulipongeza Jeshi la Polisi hasa Kituo cha Ubungo ambacho wamekuwa msaada mkubwa kwetu katika vita hii ya kupambana na
wezi wa kazi za wasanii,” alisema Msama.

Aliongeza, kwa ushirikiano mkubwa wa Jeshi la Polisi na Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, anashukuru kazi hiyo imekuwa ikisonga mbele kwa kazi feki kuzidi kukamatwa katika maeneo mbalimbali ya nchi katika kulinda maslahi ya wasanii.Alisema tangu kuanza kwa kazi hiyo ngumu ya kukabiliana na wizi wa kazi za wasanii, kampuni yake imekamata vifaa mbalimbali vya kukamilisha kazi hiyo na kazi zenye jumla
ya shilingi bil.12.

Msama alisema kampuni yake imejitwika jukumu hilo zito kwa lengo la kuona wasanii wa Tanzania wananufaika na ubora wa kazi zao katika kuendesha maisha yao kwamba kupitia vipaji vyao, wahusika waweze kujiajiri.Alisema, katika mazingira ya sasa ambapo jasho la wasanii linaishia mikononi mwa wajanja wachache ambao wamekuwa wakichakachua kazi, kamwe wasani hawawezi kupata kipato cha kutosha kuboresha maisha yao.

Msama ametoa wito pia kwa wasamaria wema sio tu kutoa taarifa kwa kampuni yake au Jeshi la Polisi za kuwafichua wanaojihusisha na uchakachuaji wa kazi za wasanii,  pia kuacha kununua kazi feki japo huuzwa kwa bei ya kutupa.Baadhi ya wananchi walioshuhudia baadhi ya vifaa na kazi feki, kwa nyakati tofauti wameipongeza kampuni ya Msama Auction Mart kwa kazi hiyo ngumu kwa maslahi
ya wasanii.

Kelvin Living na Iddy Abbas wa Mabibo, kwa nyakati tofauti, wameomba kazi hiyo iwe endelevu kwa sababu wajanja hao wachache wanachangia wasanii kukosa maslahi mazuri kupitia vipaji vyao.

MAFUNZO YA ELIMU YA UJASIRIAMALI KWA WASHIRIKI WA SHINDANO LA MASHUJAA WA KESHO MKOANI MTWARA YAMALIZIKA

$
0
0
Mafunzo ya elimu na ujasiriamali kwa washiriki wa shindano la Mashujaa wa  Kesho yanayoratibiwa na kampuni ya Statoil Tanzania, yenye lengo la kumjenga  kijana kuwa mjasiriamali yamekamilika hivi karibuni.

Akibainisha aina ya mafunzo ya ujasiriamali waliyopata vijana hao, Erick
Mchome Afisa Mahusiano wa Statoil-Tanzania amesema kuwa
Mafunzo waliyopata vijana hao yamelenga kuwawezesha vijana kuandika mpango wa biashara ikiwa ni hatua ya awali katika harakati za ujasiriamali.

Pamoja na hilo vijana pia wamefundishwa kujenga uwezo wa kujieleza kwani sifa moja ya mjasiriamali ni kujiamini na kuweza kusimama mbele ya wateja kunadi biashara yake. ‘’ Tumekuwa na siku nne nzuri za mafunzo na ni imani yetu kuwa vijana hawa hamsini na ziaidi watakuwa chachu ya mafanikio kwa vijana wenzao kwani mafunzo haya yamewatoa kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine,’’ alisema Mchome.

Sambamba na hayo vijana hao ambao walifikia idadi ya hamsini na zaidi wamefundishwa namna ya kujijenga kama wajasiriamali ikiwa ni pamoja na namna za kutafuta mtaji, kupanga mapato na matumizi na pia kutenga faida kwa kila biashara watakayofanya. Lengo la mfunzo haya ni kuchochea ari ya ujasiriamali kwa vijana ambao wameshiriki na kuingia awamu ya pili ya shindano la mashujaa wa kesho. 

Kwa upande vijana waliochaguliwa kuingia hii awamu ya pili wao wamesema kuwa elimu waliyoipata imewafungua macho na kupanua mawazo sana. Majadiliano yamewaonyesha wazi kwamba kuna fursa nyingi sana nje ya kuajiriwa.

“Nawashukuru Statoil-Tanzania pamoja na wasimamizi wa mafunzo haya kwani elimu tuliyopata hapa ni msingi mkubwa kwa sisi kuwa wajasiriamali, kufanya biashara zetu ilitukamate fursa za biashara ambazo zipo mbele yetu. Kuna njia nyingi sana za kutafuta maisha ”, Alisema Ally Seleman mshiriki wa shindano la Mashujaa wa Kesho.

Mafunzo ya elimu ya biashara na ujasiriamli yalianza toka tarehe 27 Oktoba
2014 na kuendelea kwa siku nne.Mara baada ya mafunzo hayo kukamilika vijana wamepewa siku 12 za kuaandika mawazo ya biashara na kuyakusanya siku ya jumatano ya tarehe 12 mwezi Novemba ili kuweza kuingia katika awamu ya pili ya mchakato wa kupata washindi wa shindano hili la Mashujaa wa kesho.

Shindano la mashujaa wa kesho lilizinduliwa mnamo mapema mwezi Septemba na linatarajiwa kufika kilele mwanzoni mwa mwezi Desemba ambapo mshindi atajinyakulia kitita cha dola za kimarekani elfu tano kutoka kampuni ya Statoil.

KINYWAJI CHA SHUDA COCKTAILS CHAZINDULIWA JIJINI DAR

$
0
0
Kampuni ya A&K HOLDINGS LTD mwishoni mwa wiki iliyopita ilizinduz kinyaji cha Shuda Cocktails hafla iliyofanyika Novemba 1, 2014 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, kinywaji hicho kimetengenezwa kwa ufanisi na kuchanganywa katika vipimo maalum ili kupata bidhaa zenye ladha nzuri zinazolenga na kukubalika na matabaka yote ya wanywaji au watuamiaji wa vileo. Ujazo wake ni 700ml. Bidhaa hii inazalishwa nchini Uingereza.

Meneja Masoko ya Kinywaji cha Shuda Cocktails, Bernadetha Daudi akiongea katika uzinduzi wa kinywaji huo mwishoni mwa wiki iliyopita Nobemba 1, 2014 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Kampuni ya A&K HOLDINGS LTD ambao ni wasambazaji wa kinywaji cha Shuda Cocktails akiongea katika uzinduzi wa kinywaji hicho, halfa iliyofanyika  mwishoni mwa wiki iliyopita Novemba 1, 2014 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Shuda Cocktails zipo katika ladha nne kwa sasa: Woo Woo, Pina Colada, Mojito na On the Beach. bei ya rejareja ni Tsh 12,000 kwa chupa.
Mabinti waliokipamba kinywaji cha Shuda Cocktails.
Balozi wa Kinywaji hicho, Lemtuz akiwa na mabinti wakikipamba kinywaji cha Shuda Cocktails.
Kwa sasa zinapatikana katika supermarket zote hapa Dar es salaam, kumbi za starehe na bar kwenye kila kiunga cha Dar es salaam. Hivi karibuni, Shuda Cocktails zitapatikana mikoani pia.
Ofisi zetu zipo Masaki, Kahama Rd mkabala na Mafian Lounge ya zamani.
Ili kupata maelezo zaidi kuhusiana na shuda Cocktails tembelea tovuti yetu www.shudacocktails.tz.co na facebook kupitia Shuda Cocktails Tanzania
Tunapatikana pia kupitia namba +255 717923963 na 0717 528216.
Kila aina ya Shuda ina viungo tofauti kama ifuatavyo:
Shuda Woo Woo; Cranberry juice, peach schnapps and Vodka
Shuda PinaColada: Pineapple juice, banana, Coconut milk and rum
Shuda On the Beach: Peach schnapps, orange juice, vodka
Shuda Mojito; Lime juice, club soda, mint and rum
Furaha ya kinywaji cha Shuda Cocktails.
Marafiki walipokutana pamoja.
Wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi wa kinywaji cha Shuda Cocktails.
Wengine waliamua kuweka kumbukumbu.
Bongo movie nao walikuwepo.
Ukodak ulihusika toka #KajunasonStudio ya Kajunason Blog.
Mtaalam King Maluu akionyesha umahili wake wa kuitandika mdomo wa bata.
Kila mmoja alitaka kupiga picha na Msanii Diamond Platinumz.
Haya mimi pia Mmiliki wa Kajunason Blog niliweza kupata ukodak na Msanii Diamond.
Warembo nao walikuwepo kushuhudia uzinduzi huo.
Khadija Mwanamboka na Shamim Mwasha nao waliwakilisha.
Warembo wakifurahia ukodak toka #KajunasonStudio ya Kajunason Blog. Picha zote na Cathbert wa Kajunason Blog.

BENKI YA UWEKEZAJI YA ULAYA (E.I.B), YAIPIGA JEKI BENKI YA CRDB

$
0
0
Mwakilishi wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya, Nikolaos Milianitis (kulia) akisaini mkataba wa mkopo wa sh. bilioni 43 na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei baada ya Benki hiyo kwa ajili ya kuwakopesha wafanyabiashara Wadogo na Wakati. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Wa pili kushoto anayeshuhudia ni Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima. Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi wa Benki ya CRDB, Martin Mmari na Wa pili kulia ni, Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya, Eric Beaume.
Mwakilishi wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya, Nikolaos Milianitis (kulia) akibadilishana hati na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei baada ya benki hiyo kusaini mkopo wa billion 43 na benki ya CRDB kwa ajili ya kuwakopesha wafanyabiashara Wadogo na Wakati. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Katikati anayeshuhudia ni Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima. 
Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima akiwasili ukumbini wakati wa hafla ya utiaji saini wa mkataba wa mkopo wa sh. Bilioni 43 kutoka Benki ya Uwekezaji Ulaya. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi CRDB, Martin Mmari na (katikati) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei na kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa.


Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (wa pili kushoto), Meneja Mahusiano wa Benki ya CRDBGodwin Semunyu (wa pili kulia) wakiwa katika hafla ya uwekaji saini wa mkataba wa mkpo wa sh. bilioni 43 na Benki ya Uwekezaji Ulaya.
Maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika picha ya pamoja.
Mwakilishi wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya, Nikolaos Milianitis (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.
Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya, Eric Beaume (kulia) akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya, Nikolaos Milianitis (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (wa pili kushoto) na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo.

Baadhi ya maofisa wa Benki ya CRDB pamoja na wadau wengine.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji saini mkataba wa mkopo wa sh. bilioni 43 kutoka Benki ya Uwekezaji Ulaya.
Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akizungumza katika hafla hiyo.
Mwakilishi wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya, Nikolaos Milianitis akizungumza katika hafla hiyo.
Baadhi ya maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika hafla hiyo.
Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima (kushoto) akiwa na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya, Eric Beaume.  
Meza Kuu.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka akifuatilia kwa makini hafla ya uwekaji saini wa mkataba wa mkopo wa sh. Bilioni 43 na Benki ya Uwekezaji Ulaya.
Mwenyekiti wa Bodi ya CRDB, Martin Mmari akizungumza katika hafla hiyo.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima akitoa hotuba yake wakati wa hafla hiyo.

Na Mwandishi Wetu

BENKI ya CRDB imesaini mkataba wa mkopo wa sh. bilioni 43 baina ya benki ya uwekezaji Ulaya (E.I.B) kwa ajili ya kuwakopesha na kuwasaidia wafanyabiashara wanaofanya shughuli za kukuza uchumi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk. Charles Kimei alisema benki yake kwa kushirikiana na EIB imeamuwa kusaidia jamii nchini hivyo mkataba huo ni mwanzo wa ushirikiano endelevu utakaohamasisha upatikanaji wa ajira.

Alisema kufanyakazi na benki ya EIB kutasaidia kukuza biashara katika maeneo muhimu kama uvuvi, usindikaji wa chakula, usafiri, biashara pamoja na huduma zote za kiuchumi.

“Mimi kama kiongozi wa CRDB Tanzania ninamamlaka ya kusaidia hizi sehemu za soko na kuongeza jitihada za kumaliza umaskini, pia kuongeza shughuli za kiuchumi za wateja wetu ili kufikia lengo la kuongeza mapato katika benki yetu,” alisema Kimei.

 Kwa upande wake Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima alisema mkataba huo pia una lengo la kuisaidia benki ya CRDB katika kuendesha shughuli zake mbalimbali.

Alisema ni jambo la faraja kuona benki kama EIB imekubali kuiamini CRDB na kuipa mkopo wa kiasi kikubwa cha pesa kwa ajili ya kuwasaidia wafanyabiashara.

“Tunachokiamini kuwa hii benki kutoka Ulaya siyo benki ndogo ni kati ya benki kubwa zilizopo hapa duniani, sasa kama wamekuja hapa kwetu na wakaonyesha nia njema ya kutusaidia endapo watabaini kuwa pesa zao azitatumika kwa malengo yaliyokusudiwa watavunjika moyo,” alisema.

Mh. Suluhu akutana na balozi wa Norway Nchini,afanya mazungumzo na Mchungaji Stella Matte

$
0
0
Barozi wa Norway Nchini Tanzania Anne - Marie Kaarstad akizungumza na waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano Mheshimiwa Samia Suluhu (kulia), alipomtembelea Ofisini kwake, mtaa wa Ruthuli jijini Dar es Salaam leo.
Anne Kristin Hermansen (kushoto),akiwa pamoja na Elisabeth Schwale wakisikiliza mazungumzo baina ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano Mheshimiwa Samia Suluhu na Barozi wa Norway Nnchini Tanzania Anne - Marie Kaarstad (hawapo pichani) walipomtembelea ofisini hapo leo.
Mchungaji Stella Matte akitoa shukrani kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano Mheshimiwa Samia Suluhu (kulia), kwa kuhudhulia semina waliyoandaa iliyohusu maswala ya uongozi, alipomtembelea ofisini kwake leo mtaa wa Ruthuli jijini Dar es Salaam.

Breaking Newwzzzzzz: Kaimu MKurugenzi WA TPDC na Mwenyekiti wake wa Bodi watupwa rumande kufuatia kushindwa kuwasilisha mikataba 26 kwa PAC.

$
0
0
Taarifa zilizotufikia hivi punde ndani ya chumba cha habari cha Globu ya Jamii,kinaleleza kuwa kaimu Mkurugenzi wa TPDC,Bwa.James Andilile na Mwenyekiti wake wa bodi Bwa.Michael Mwanda wamepelekwa rumande kwa kosa la kutowasilisha mikataba 26 kwa kamati ya bunge la  hesabu za mashirika ya umma PAC,kamati imeagiza wapelekwe huko na hatua zichukuliwe dhidi yao.

Kikosi kazi cha Globu ya Jamii kipo kazini kuifuatilia taarifa hii,hivyo tuendelea kupitia pitia hapa jamvini kupata Updates.

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DR. JAKAYA KIKWETE AFUNGUWA MKUTANO MKUU WA 12 WA SHIRIKISHO LA TAASISI ZA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA KWA NCHI ZA SADC

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Angel Magati ambaye aliimba wimbo maalum wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia Mkutano wa 12 wa Shirikisho la Taasisi za Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwa nchi za SADC (Southern African Forum Against Corruption) ulioanza leo ukitarajiwa kumalizika Ijumaa ya tarehe 07/11/2014 Katika Hoteli ya Malaika jijini Mwanza.
  Sehemu ya wadau toka nchi mbalimbali barani Afrika wameshiriki Mkutano wa 12 wa Shirikisho la Taasisi za Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwa nchi za SADC (Southern African Forum Against Corruption) ulioanza leo ukitarajiwa kumalizika Ijumaa ya tarehe 07/11/2014 Katika Hoteli ya Malaika jijini Mwanza.
 Kutoka kushoto ni Mbunge wa Sengerema William Ngeleja, Meya wa Manispaa ya Ilemela Henry Matata, Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga na Mkuu wa wilaya ya Ilemela Amina Masenza wakisikiliza kwa umakini yanayojiri ndani ya Mkutano wa 12 wa Shirikisho la Taasisi za Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwa nchi za SADC (Southern African Forum Against Corruption) ulioanza leo ukitarajiwa kumalizika Ijumaa ya tarehe 07/11/2014 Katika Hoteli ya Malaika jijini Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Utawala Bora Kapt.George Mkuchika katika Mkutano wa 12 wa Shirikisho la Taasisi za Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwa nchi za SADC (Southern African Forum Against Corruption) ulioanza leo ukitarajiwa kumalizika Ijumaa ya tarehe 07/11/2014 Katika Hoteli ya Malaika jijini Mwanza.PICHA NA IKULU.

TOYOTA TANZANIA YAWATUNUKU WAFANYAKAZI WAKE BORA, MMOJA ALAMBA TIKETI YA KWENDA JAPAN

$
0
0
Meneja wa Karakana wa Kampuni ya Toyota Tanzania Ltd, Josee Alverace (kushoto) na Mwenyekiti wa Toyota Tanzania, Mahmoud Karimjee (katikati) wakimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa jumla, Maria Robi wa Toyota Mwanza, wakati wa hafla maalum ya 12 ya kuwapongeza na kuwatunukia wafanyakazi bora wa mwaka 2014 wa Kampuni hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Ofisi za Toyota zilizopo Barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam. 
Washindi wakipokea zawadi zao...wakati wa hafla hiyo....
Mgeni rasmi, Eng. Prisca Mkama, akimkabidhi zawadi ya mshindi Peter Louce, wakati wa hafla maalum ya kuwapongeza na kuwatunukia wafanyakazi bora wa mwaka 2014 wa Kampuni hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Ofisi za Toyota zilizopo Barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Toyota Tanzania, Mahmoud Karimjee.
Mwenyekiti wa Toyota Tanzania, Mahmoud Karimjee (kushoto) na mgeni rasmi Eng. Prisca Mkama, wakipozi kwa picha na mshindi Anna Mzuri
Washindi wakipokea Tuzo zao...wakati wa hafla hiyo..
Zawadi kwa Maganga (katikati) .
Ma Mc's wakijiandaa kupagawisha....
Baadhi ya wafanyakazi wakiwa katika hafla hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wakiwa katika hafla hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wakiwa katika hafla hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wakiwa katika hafla hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wakiwa katika hafla hiyo.
Kutoka (kulia) Mapunda, Maganga na Naniliu wakishuhudia kilichokuwa kikiendelea jukwaani.
Wafanyakazi hao walianza shughuli yao hiyo kwa dua maalum...
Baadhi ya wafanyakazi wakiwa katika hafla hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wakiwa katika hafla hiyo, mezani ni magari ya mfano...

Pia wafanyakazi hao walishindana kuvuta kamba kati ya Madereva wa Kampuni na wa spea...., Madereva waliburuzwa hadi gereji wakashikishwa spana....
Mabosi wakifurahia shooo.....
Wafanyakazi hao walitoa burudani ya maigizo, (pichani) ni Mkufya na Bi shosti wakiigiza...
Hapa ni Bosi Naniliu akiingilia kati mtafaruku uliojitokeza baina ya mhudumu wa Ofini yake na mteja......
Hapa ni Bosi Naniliu akiingilia kati mtafaruku uliojitokeza baina ya mhudumu wa Ofini yake na mteja....
Mkufya akiendelea kukonga nyoyo za wafanyakazi wenzake...
Wafanyakazi wakifurahia shoo......
Burudani ya ngoma ya asili ya kabila la Wahehe.....
Burudani ya ngoma ya asili ya kabila la Wahehe.....
Msema chochote, Galinoma, akisherehesha huku akifafanua kuhusu moja ya silaha iliyotumika na wahehe kumtwanga Mjerumani enzi za ukoloni..
Hawa ni miongoni mwa washiriki katika kinyang'anyiro hicho cha kuwania tuzo ya mfanyakazi bora, ambapo utaratibu huo wa kuwatunuku na kuwapongeza wafanyakazi bora wa kampuni hiyo ulianza rasmi mwaka 2002, na sasa umetimiza miaka 12.
Fashion Show......

Fashion Show....
Baadhi ya wafanyakazi wakiwa katika hafla hiyo.
Washiriki wa shoo wakipiga picha ya pamoja....
Baadhi ya wafanyakazi wakiwa katika hafla hiyo.
Mgeni rasmi Eng. Prisca Mkama, akizungumza ......
Mjomba akipongezwa wakati akielekea jukwaani kupokea zawadi yake....
Burudani....
Huyu si Aisha Madinda, bali ni mfanyakazi wa Toyota Tanzania, akionyesha umahiri wake wa kunengua wakati wa hafla hiyo...
Baada ya shoo hiyo waliaga kama hivi....
Zawadi kwa wasanii wote walioshiriki kutoa burudani.....
Muda wa maakuli full kujisevia uliwadia.......
Pozi la picha 
Pozi la picha 
Pozi la picha...........

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO YA MSIBA WA RAIS WA ZAMBIA, MICHAEL CHILUFYA SATA

$
0
0
Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Rais wa Zambia, Michael Chilufya Sata, wakati alipofika nyumbani kwa Balozi wa Zambia nchini Tanzania, Judith Kapijimpanga, jijini Dar es Salaam, leo Novemba 3, 2014.
Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Balozi wa Zambia nchini Tanzania, Judith Kapijimpanga, baada ya kusaini kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Rais wa Zambia, Michael Chilufya Sata, nyumbani kwa, Balozi huyo jijini Dar es Salaam, leo Novemba 3, 2014. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Afrika Kusini awasili nchini kwa ziara ya siku moja

$
0
0
Makamu wa Rais wa  Afrika Kusini, Mhe. Matamela Cyril Ramaphosa akiteremka katika ndege mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius  Nyerere Jijini  Dar es Salaam.  Mhe. Ramaphosa yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku moja ambapo pamoja na mambo mengine atazungumza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,  Mahusiano , Mhe. Stephen Wasira kwa pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dkt.  Mahadhi Juma Maalim (Mb), na Bi. Zuhura Bundala, Kaimu Mkurugenzi   wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakati wa mapokezi ya  Makamu wa Rais wa Afrika Kusini.  
Mhe. Ramaphosa akilakiwa na Mhe. Wasira mara baada ya kuwasili.

WAZIRI NYALANDU ATOA WITO KWA VIONGOZI WA DINI KUHUSU KUKEMEA UJANGILI NCHINI

$
0
0
Na Anitha Jonas – Maelezo.

03 Novemba, 2014.

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu ametoa wito kwa Viongozi wa dini wote nchini kupaza sauti kwa pamoja kukemea vitendo vya Ujangili pamoja na Uharibifu wa mazingira nchini.

Wito huo ameutoa leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua mkutano wa viongozi wa dini unaolenga kuwaelimisha viongozi hao kutoa elimu kwa waumini wao juu ya kupinga suala la ujangili na kuwasihi juu ya utunzaji wa mazingira.

Mhe. Nyalando alisema kuwa, vitendo vya ujangili vikiendelea vinaweza kuleta athari kubwa nchini ikiwa ni pamoja na uharibifu wa mazingira na kuharibu sekta ya utalii kwa Mbuga za wanyama.

“Serikali imeamua  kwamba,  mtu yoyote anayefanya vitendo vya kijangili akijisalimisha na kukabidhi silaha yake atasamehewa,” Alisema Mhe. Nyalando

Aliwasihi akina mama wanaojua waume zao wanaojihusisha na vitendo vya ujangili kuacha na kujisalimisha Wizarani.

Naye Sheikh Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Sheikh Alhaj Mussa Salum ameonyesha ushirikiano na kuunga mkono utoaji wa elimu hiyo kwa waumini kwani hata Quran Tukufu  inahubiri juu ya haki za wanyama, hivyo ukatili juu ya wanyama sio jambo zuri mbele za Mungu.

“Dhuluma inayofanyika kwa wanyama ni dhambi kwani Quran inasema fanyeni wema kwani mwenyezi Mungu anapenda wema” Alisema Sheikh Mussa.

Kwa upande wake Askofu wa Jimbo la Iringa Baraza ka Maaskofu Tanzania (TEC), Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa  alisema kuwa rasilimali zote zilizopo nchini ni Baraka, hivyo zinapaswa kutunzwa na kuepuka suala la ubinafsi kwa kutaka kuzitumia zote kwa haraka na kuzimaliza.

“Tufikirie na kizazi kijacho kitahitaji kunufaika na rasilimali asilia hizi, mfano miti inayochukua muda mrefu kuota pamoja wanyama wa porini”,alisema Askofu Ngalalekumtwa.

Naye mdau wa maendeleo nchini Dkt. Regnald Mengi alisema kwamba, viongozi wa dini wana nguvu kubwa katika jamii, kwani chochote wanachokisema kwa waumini wao ni rahisi kwa waumini hao kukifuata kwani wanaamini chochote kinachosemwa nao ni maagizo ya Mungu.

Mkutano huo ulihusisha viuongozi mbalimbali wa kidini wakiwemo Maaskofu, Masheikh pamoja, Wadau wa maendeleo wa UNDP pamoja na Mashirika mbalinmbali ya Wanyamapori yakiwemo TANAPA, TAWIRI, FZC, AWF, WWF, ICCF ambao wenyeji wa mkutano huo.

Usajili wa wanaridha Uhuru marathon Tanzania kuanza rasmi kesho

$
0
0
Katibu wa Kamati ya maandalizi ya mbio za Uhuru wa Tanzania (Uhuru Marathon ),Innocent Melleck akionyesha fomu ya 3km ambayo itatumiwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Jakaya Kikwete kwenye kushiriki mbio hizo na fomu hizo zinatarajiwa kuanza kuuzwa rasmi kesho katika vituo 13 jijini Dar Es Salaam na jumanne kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma ambapo spika Anna Makinda ataongoza wabunge kuchukua fomu za kuishiriki.
Katibu wa Kamati ya maandalizi ya mbio za Uhuru wa Tanzania (Uhuru Marathon ),Innocent Melleck akizungumza na waandishi wa habari (hwapo pichani) jijini Dar Es Salaam juu ya maandalizi ya mbio hizo ambapo fomu za ushiriki zinatarajiwa kuanza kuuzwa rasmi kesho katika vituo 13 jijini Dar Es Salaam na jumanne kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma ambapo spika Anna Makinda ataongoza wabunge kuchukua fomu za kuishiriki.Kushoto ni mdau wa riadha,bwana Mroki Mroki.


USAJILI kwa watu wanaotaka kushiriki mbio ndefu za Uhuru, maarufu kama Uhuru Marathon, zinazotarajiwa kufanyika Desemba 7, mwaka huu jijini Dar es Salaam umeanza rasmi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa Kamati ya mbio hizo, Innocent Melleck alisema, mara baada ya Dar es Salaam fomu za usajili zinatarajiwa kutolewa Dodoma kuanzia wiki ijayo.

“Tunapenda kutangaza rasmi kwamba usajili kwa ajili ya mbio hizo umeanza rasmi katika Mkoa wa Dar es Salaam, ambapo kuna vituo zaidi ya 13 vilivyofunguliwa katika maeneo mbalimbali.

“Pia siku ya Jumanne na Jumatano wiki ijayo fomu hizo zitatolewa rasmi katika Viwanja vya Bunge, Dodoma ambapo Spika Anne Makinda ndiye anayetarajiwa kuongoza katika kujisajili.
Vituo vitakavyokuwa vikiuza fomu za ushiriki ni 1.Triple seven Mikocheni.2.maduka ya TSN,Uchumi supermarkets,Uwanja wa Leaderds Club,Ofisi za Rt Taifa,Standi kuu ya mabasi moshi mjini,Arusha na katika tovuti ya WWW.UHURUMARATHON.COM au kwa kupiga simu 0688108384

Mwaka huu pia kutakuwa na usajili wa vikundi mbalimbali na makampuni ambapo watashiriki kama vikundi ikiwa ni kuonyesha uzalendo wao.

Kwa taarifa hii napenda kuwaomba makampuni,mshirika binafsi na watu mbalimbali ambao wamekuwa wakiulizia kwa wingi kutaka kushiriki mbio za mwaka huu kuwa sasa wanaweza kuchukua fomu na kujaza na kurejesha mapema ili kuondoa usumbufu mkubwa unaoweza kujitokeza,Mwaka jana kulukuwa na msoongamano mkubwa sana sasa mwaka huu ni vyema tukachua fomu mapema ili kuepukana na usumbufu wa foleni kipindi cha mwisho alisema Melleck.

“Kingine mtu anayetaka kushiriki anaweza pia kujisali kwa njia ya mtandao wa internet na tunafanya utaratibu maalumu wa kuhakikisha pia yoyote anayetaka anaweza kujisaili kwa njia ya simu, “alisema.

Melleck alisema, katika usajili huo, fomu zitakazotolewa kwa mshiriki wa kilomita 3 atalipa Sh 50,000 yule wa kilomita 5 Sh 5,000 na washiriki wa kilomita 21 watalipia Sh 10,000.Mbio za mwaka huu pia zinatarajia kuhusisha shule za sekondari na msingi 25 ambazo zitashiriki katika mbio za kilometa 5

“Pia tunapenda kuchukua fursa hii kuziomba kampuni au taasisi mbalimbali zinazotaka kudhamini mbio hizo zijitokeze na kufanya hivyo, kwani nafasi bado ipo na tukumbuke bila amani hakuna chochote kinachoweza kuendelea, hivyo hata wao pia wanatakiwa kuipigania amani kwa nguvu zote.”

Mbio hizo zinatarajiwa kushirikisha wanariadha kadhaa maarufu duniani.

PAUL MAKONDA APINGA VIKALI KUHUSIKA NA FUJO ZA MDAHALO.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA WAJUMBE WA ILIYOKUWA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA, SERENA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na kuzungumza na aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Mwesiga Baregu, walipokutana katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo Novemba 3, 2014 baada ya kuzindua rasmi utoaji wa huduma kwa walemavu wa kusikia (Viziwi) uzinduzi huo umefanyika leo Novemba 3, 2014 kwenye Viwanja vya Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, chini ya usimamizi wa Taasisi ya Starkey Hearing ya nchini Marekani. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na waliokuwa wajumbe wa Tume ya Katiba mpya, kutoka (kushoto) ni Humphrey Polepole, Mwenyekiti wa Mfuko wa Mwalimu Nyerere, Julius Butiku na Prof. Mwesiga Baregu, baada ya kuzindua rasmi utoaji wa huduma kwa walemavu wa kusikia (Viziwi) uzinduzi huo umefanyika leo Novemba 3, 2014 kwenye Viwanja vya Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, chini ya usimamizi wa Taasisi ya Starkey Hearing ya nchini Marekani. Picha na OMR

USED CARS BUYERS SEMINAR

$
0
0


 GET YOURSELF TRAINED ON HOW TO BUY A USED CAR RIGHT FROM JAPAN THROUGH SAMURAI JAPAN TRADING.  MR SHIMBUTSU - A CONSULTANT IN CAR SELLING BUSINESS FROM JAPAN WILL BE OFFERING FREE SEMINARS EVERY SATURDAY FOR THE MONTH OF NOVEMBER 2014.

TIME: 3 TO 4 PM

VENUE: SAMURAI JAPAN TRADING OFFICES MAKTABA COMPLEX 3 RD FLOOR BIBI TITI MOHAMED ROAD



'' GET A CHANCE TO EXPAND YOUR KNOWLEDGE FOR FREE''

MAKAMU WA RAIS WA BENKI YA DUNIA BW. KYLE PETERS ATEMBELEA WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI UNAOETEKELEZWA NA TASAF KATIKA WILAYANI BAGAMOYO.

$
0
0

    Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kyle Peters akiwahutubia wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya masikini katika kijiji cha Buma wilayani Bagamoyo.
    Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ladislaus Mwamanga (aliyesimama) akitoa ufafanuzi wa masuala ya mpango wa kunusuru kaya masikini kwa walengwa (hawapo pichani) wakati wa ziara ya Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kyle Peters.
0Baadhi ya wanuafaika wa mpango wa kunusuru kaya masikini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii – TASAF katika kijiji cha Buma wilyani Bagamoyo wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kyle Peters na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ladislaus Mwamanga.
    Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Ahmed Kipozi akimkaribisha Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kyle Peters alipotembelea miradi ya TASAF wilayani humo. Kushoto kwake Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ladislaus Mwamanga.

 Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Bwana Kyle Peters amefanya ziara katika kijiji cha Buma wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani ambako ameshuhudia walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na TASAF na kuridhishwa kwake na namna mpango huo ulivyowanufaisha walengwa ambao wameanza kuondokana na umaskini.

Akiwa kijijini hapo Bwana Peters alitembelea moja ya nyumba iliyoboreshwa na mmoja wa walengwa wa Mpango wa Kunusuru kaya maskini Bwana Bakari Rajabu Bakari ambaye kwa kutumia fedha za ruzuku kupitia Mpango wa kunusuru kaya maskini ameweza kuboresha maisha yake ikiwa ni pamoja na kununua Luninga(TV) huku akimudu pia kusomesha watoto wake.

Bwana Peters amesema utekelezaji wa Mpango huo umeanza kuonyesha mafanikio nchini TANZANIA  jambo ambalo litatumiwa na Benki ya Dunia kuendelea kuufadhili huku mfano huo ukisambazwa katika nchi nyingine ili kazi ya kuutokomeza umaskini iwe na mafanikio.

Akizungumza katika ziara hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga amesema mafanikio ya utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya maskini yanatokana na taasisi yake kuamini na kutekeleza majukumu yake kwa uwazi na kuwashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo walengwa katika hatua za utekelezaji wake.

Zifuatazo hapo chini ni baadhi ya picha za ziara ya makau huyo wa Rais wa Benki ya Dunia katika kijiji cha Buma wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.
    Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kyle Peters akiangalia kitambulisho cha afya ya jamii kutoka kwa mlengwa wa mpango wa kunusuru kaya masikini katika kijiji cha Bumba wilaya ya Bagamoyo.
    Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ladislaus Mwamanga akifafanua jambo kwa Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kyle Peters alipotembelea shamba la mananasi la mmoja wa walengwa wa PSSN Bakari Rajabu Bakari mwenye kofia nyeupe
    Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kyle Peters akiangalia miche ya machungwa iliyooteshwa na mmoja wa walengwa wa mpango wa kunusuru kaya masikini PSSN katika kijiji cha BUMA wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani
    Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kyle Peters akiangalia miche ya machungwa iliyooteshwa na mmoja wa walengwa wa mpango wa kunusuru kaya masikini PSSN katika kijiji cha BUMA wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani
    Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kyle Peters akipokea zawadi ya nanasi kutoka kwa Bakari Rajabu Bakari ambaye ametumia sehemu ya fedha za mpango wa kunusuru kaya masikini kuendeleza shughuli za kilimo cha mananasi

TBC KUONESHA LIVE JK AKIONGEA NA WAZEE WA DODOMA WAKATI WOWOTE KUANZIA SASA

$
0
0
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Profesa Jakaya Mrisho Kikwete mchana huu ataanza kuzungumza na Wazee wa Dodoma  katika ukumbi wa Kilimani mjini Dodoma wakati wowote kuanzaia sasa. Usikose kuangalia mazungumzo hayo yatayooneshwa moja kwa moja na TBC One pamoja na mtandao wa
www.ikulu.go.tz

IMETOLEWA NA KITENGO CHA 
MAWASILIANO YA RAIS IKULU,

NOVEMBA 4, 2014

Zanchick watoa msaada wa chanjo 600,000 kwa wafugaji kuku Zanzibar

$
0
0
Mkurugenzi wa Kampuni inayojishughulisha na uboreshaji wa kuku Zanzibar(Zanchick) Bw.Issa Khasim Issa akikabidhi chanjo 600,000 zenye thamani ya Tshs 9,000,000 kwa Naibu katibu katika kitengo cha kutoa huduma kwa wanyama kutoka Wizara ya Ufugaji na Uvuvi Zanzibar, Dr.Omar Ali Amir kwa ajili ya kuwalinda kuku na ugonjwa wa Mdondo, anayeshuhudia kulia Mkurugenzi katika kitengo cha kutoa huduma kwa wanyama kutoka Wizara ya Ufugaji na Uvuvi Zanzibar, Dr.Yusuf Hajj Khamis.

Kampuni inayojishughulisha na uboreshaji wa kuku Zanzibar, Zanchick, leo imetoa chanjo 600,000 zilizo na thamani ya Tshs 9,000,000 kwa wafugaji kuku kwa ajili ya kuwalinda kuku wao na ugonjwa wa Mdondo. Utoaji wa chanjo hizo ulifanyika kwa msaada wa wizara ya Ufugaji na Uvuvi Zanzibar ambao wata ratibu na kusimamia zoezi zima.

Meneja wa Uendeshaji, kutoka Zanchick, Bwana Christopher Kontonasios alisema: “Tunashukuru Wizara ya Ufugaji na Uvuvi kwa kuwa washiriki wakubwa katika kuratibu zoezi hili na tunataraji serikali itazidi kuwasaidia wazalishaji kuku wa kawaida, kwa kuondoa kodi ya kuagiza chakula cha kuku, jambo ambalo litawaruhusu wazalishaji wa kawaida kupata chakula bora cha kuku chenye bei nafuu.

Hii ndio njia pekee ya kuwawezesha wakulima wa kawaida kuendeleza ufugaji wa kuku, kwa kiwango cha hali ya juu, na pia kuwaruhusu kukidhi biashara zenye faida.

Mkurugenzi katika kitengo cha kutoa huduma kwa wanyama kutoka Wizara ya Ufugaji na Uvuvi Zanzibar, Dr.Yusuf Hajj Khamis alisema, “Tunafarijika na juhudi za Zanchick katika kuboresha uzalishaji wa kuku Zanzibar, hii ni hatua kubwa kwa wafugaji wa kawaida. Tunatarajia kuongeza juhudi katika kushirikiana kukuza viwango na jitihada za ufugaji kuku kisiwani hapa."

Kirusi cha ugonjwa wa Mdondo kwa ujumla hakisababishi madhara yoyote kwa afya ya binadamu, lakini kina uwezo wa kuleta maafa makubwa kwa wafugaji wa kawaida, kwa kumaliza kiasi kikubwa cha kuku na hatimaye kuangamiza biashara yao.

Msaada huu mkubwa na muhimu ni katika juhudi za Zanchick kufanya kazi na wafugaji wa kawaida ili kuongeza, kuboresha na kunadi uzalishaji wa kuku Zanzibar.

MBUNGE JAMES MBATIA ACHANGISHA FEDHA KUNUSURU ELIMU JIMBO LA VUNJO.

$
0
0
Wanafunzi wanao fanya mitihani ya kidato cha nne katika shule ya sekondari Bishop Moshi iliyoko Vunjo.
Wanafunzi wa kidato cha tatu shule ya sekondari Bishop Moshi wakitoa burudani ya nyimbo wakati wa harambee ya kuchangia Bweni la wavulana.
Mkuu wa shule ya sekondari Boshop Moshi,Sophia Mushi akisoma risala mbele ya mgeni ,Mbunge wa kuteuliwa James Mbatia.
Mbunge wa kuteuliwa akizungumza wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa Bweni ;a wavulana katika shule ya sekondari Bishop Moshi.
Mbunge Mbatia akichangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Bweni.
Wanafunzi wa kidato cha nne katika shule hiyo walichangia mifuko mitatu ya Sementi ambayo walikabidhi kwa mgeni rasmi Mbunge Mbatia.
Wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yao wakipewa zawadi wakati wa hafla hiyo ya harambee ya kuchangia ujenzi wa Bweni.
Mbunge Mbatia akitangaza kiasi cha mchango wake katika ujenzi wa Bweni ambapo alitangaza kutoa kiasi cha shilingi milioni 10 ,pembeni yake ni mkuu wa shule hiyo Sophia Mushi akifurahi .
Wanafunzi wa kidato cha nne wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi,Mbunge Mbatia.Na Dixon Busagaga wa Globu ya jamii kanda ya kaskazini.
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images