Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 398 | 399 | (Page 400) | 401 | 402 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Gerald Guninita akipokea msaada wa mabati 200 kutoka kwa mwakilishi wa PSPF kutoka makao makuu Amelia Rwemamu kwa ajili ya ujenzi wa maabara za sayansi katika shule za sekondari wilayani humo, Makabidhiano yalifanyika juzi katika ofisi za wilaya ya Kilolo
   Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Evalista Kalalu akikabidhiwa mabati 100 kutoka kwa mwakilishi wa PSPF Mkoa wa Iringa, Baraka Jumanne kwa ajili ya chuo cha Ualimu Mufindi(MUTCO) kwa ajili ya ujenzi wa Hostel katika chuo hicho zilizotolewa na PSPF katika makabidhiano yaliyofanyika katika viwanja vya chuo hicho.
  (picha na Denis Mlowe)


  Na Denis Mlowe,Mufindi


  KATIKA kutekeleza maagizo ya Rais Jakaya Kikwete kila shule iwe na maabara tatu ifikapo Novemba mwaka huu Mfuko wa Pensheni ya Watumishi wa Umma (PSPSF) umetoa msaada wa mabati 300 yenye thamani ya zaidi ya Sh Milioni sita katika wilaya za Kilolo na Mufindi, mkoani Iringa kufanikisha ujenzi wa maabara hizo na hosteli kwa chuo cha Ualimu Mufindi.


  Wakati wilaya ya Kilolo imepata bati 200 zitakazotumika kusaidia kukamilisha ujenzi wa maabara unaoendelea  katika shule zake za sekondari, Chuo cha Ualimu Mufundi(MUTCO) kilichopo mjini Mafinga wilayani Mufindi kimepata bati 100 ikiwa ni kutumiza ahadi iliyotolewa na Meneja wa Sheria wa PSPF Abrahamu Siyovelwa aliyotoa May 27 katika mahafali ya chuo hicho.


  Akikabidhi msaada huo kwa mkuu wa wilaya ya Mufindi Monica Kalalu juzi katika viwanja vya Chuo cha Ualimu Mufindi(MUTCO) Afisa Mfawidhi wa PSPF mkoa wa Iringa Baraka Jumanne alisema lengo la msaada huo ni sehemu ya mpango wao katika kusaidia sekta ya elimu nchini na kutekeleza maombi yaliyoombwa na viongozi wa wilaya hizo katika kutekeleza maagizo yaliyotolewa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete kila shule ya sekondari iwe na maabara ifikapo Novemba mwaka huu.


  "PSPF ni shirika la mfuko wa pensheni hivyo faida lazima iifikie jamii hasa katika suala la elimu ya za sekondari na msingi hivyo tumeamua kuwapatia mabati 100 chuo cha Mufindi na wilaya ya Kilolo mabati 200 kutekeleza maombi yao kwa shirika la PSPF kusaidia ujenzi wa maabara na ujenzi wa hostel kwa chuo cha Mutco hivyo leo tunawakabidhi madawati haya mia tatu kwa lengo la kutekeleza ahadi ya shirika.” Alisema Jumanne.


   

  Aidha Jumanne alitoa wito kwa viongozi kuwashawishi wafanyakazi Kilolo  na wanafunzi wa chuo cha Ualimu Mufindi kujiunga mfuko wa pensheni kwa watumishi wa umma wa PSPF kwa huduma bora na mafao bora yakiwemo mafao ya uzeeni,ulemavu,mirathi,mafao ya rambirambi za mazishi, malipo ya wategemezi na malipo ya penshini ya kila mwezi.


  Alitoa faida ya kujiunga na PSPF kwa kuwa kuna baadhi ya mafao mbalimbali yanayotolewa na mfuko  huo yanalenga kuwawezesha watumishi kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili katika utumishi wao kabla na baada ya kustaafu


  Aliongeza kuwa PSPF ina mpango imeweka mahususi wa kuhakikisha unaboresha maisha wa wanachama wake wakiwemo wasio wafanyakazi kwa kuweka akiba isiyo ya hiyari itakayowawezasha kufaidika kwa faida ya maisha yao.


  Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mufindi Monica Kalalu alilishukuru shirika la PSPF kwa msaada huo na kutoa wito kwa wanafunzi na walimu na kuwataka wadau wengine wajitokeze kuisaidia sekta ya elimu hususani ujenzi wa maabara ambao unaendelea nchi nzima kwa sasa

   

  Naye Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Gerald Guninita alisema kuwa msaada huo utazisaidia shule za sekondari za wilaya ya Kilolo katika kukamilisha ujenzi wa maabara na kuwataka pspf wasiishie hapo katika kutoa msaada zaidi katika sekta ya elimu.


  Na Amelia Rweyimamu ambaye ni Muwakilishi wa PSPF makao makuu Dar es salaam, akizungumza wakati wa kukabidhi bati hizo alisema kuwa PSPF inatambua umuhimu wa kuwepo kwa maabara hapa nchini hivyo ofisi yake imeona vyema kushiri katika ujenzi huo kwa kutoa bati hizo.


  Rweyimamu alisema PSPF inatoa mafao mbalimbali ikiwa ni pamoja na fao la uzeeni, fao la ulemavu, fao la kifo, fao la mazishi, fao la wategemezi lisilo na kikomo, fao la kujitoa, fao la uzee, fao la kufukuzwa kazi, na fao la ujasiriamali.


  Aidha aliongeza kuwa PSPF inatoa fao la elimu ambapo mfuko hudhamini mikopo katika bodi ya mikopo ya wanafunzi, lengo kubwa ikiwa ni kujenga uwezo wa kuhudumia wanafunzi wengi katika taaluma mbalimbali ikiwemo pia taaluma ya sayansi, Teknolojia na Afya.


  0 0

  Tone Multimedia Group Kupitia Mtandao wetu wa Mbeya yetu Blog tumeadhimia kuanza kuwasaidia wasanii Chipukizi kutoka Mkoa wa Mbeya na Mikoa mingine ya Jirani kimuziki kwa Kutambulisha kazi zao mbalimbali ili wadau pia mpate kuwafahamu.

  Tunaanza Kumtambulisha kwenu Msanii wa nyimbo za kizazi kipya yaani Bongo Flava kwa jina lake halisi ni Shuku na jina la kisanii anaitwa SJ kijana ambaye yupo chini ya Mdhamini wake Mkuu Jacob Mwaisango ambaye aliona kipaji chake na kuamua kumsaidia kwa Hali na mali mpaka akaingia Studio na kutoa nyimbo kadhaa. Lakini leo Mbeya Yetu Blog Tunawatambulisha kazi hii ya kijana huyu ambaye tumeamua kumdhamini na kumsaidia Muziki wake ufike mbali zaidi.  

  Wimbo wake huu mpya kabisa unaitwa Kumbe Mapenzi.


  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo pinda akizunguma na Watanzania waishio nchini Oman akihitimisha ziara yake nchini humo Oktoba 29, 2014. Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maalim Mahadhi nakushoto ni Balozi wa  Tanzania nchini Oman, Ali Ahmed Saleh.
   Baadhi ya watanzania waishio Oman wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo PInda wakati alipowahutubia kwenye hoteli ya Al Bustan mjini Muscut Oktoba 29, 2014. 
   Baadhi ya watanzania waishio Oman wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo PInda wakati alipowahutubia kwenye hoteli ya Al Bustan mjini Muscut Oktoba 29, 2014.
   Baadhi ya watanzania waishio Oman wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo PInda wakati alipowahutubia kwenye hoteli ya Al Bustan mjini Muscut Oktoba 29, 2014. (Picha na Ofisi yaWaziri Mkuu).

  0 0

  HABARI NJEMA KWA WADAU WOTE WANAOSUMBUKA NA MATATIZO MBALI MBALI KUHUSU NGOZI ZAO KAMA VILE KUUNGUA KWA MIKOROGO,WEUSI WA MACHONI(DARK CYCLE),KUSWEAT KULIKOPITILIZA,MIGUU KUTOA JASHO NA HARUFU..AKCLASSICOSMETICS WAMEAMUA KUCHIMBA NA KUJA NA MAJIBU YA MATATIZO YENU TENA MADINI YASIYO NA MADHARA KABISAAA KWA NGOZI YAKO!!

     WALE WALIOTOKA KUJIFUNGUA NA YALE YOTE YATOKANAYO HATUJAWASAHAU PIA KUANZIA CORSETS,NYWELE(T444Z NA JBCO),WEUSI WA KWAPA NA SHINGO NA OFCOUZ NA USOO KUPIGWA MSASA KIDOGO  UKUNG'ARA KIDOGO BILA KUBADILIKA RANGII!!

     TUPIGIE 0753482909/0713468393.TUPO KINONDONI KWA AMANYANYA NA SINZA KUMEKUCHA,

  BLOG: www.akclassic.blogspot.com
   UNAJUA UNAPOKUWA NA KIKWAPA  CHEUSI CONFIDENCE HUSHUKA KABISA HATA UKIWA FARAGHA!!MATOKEO YAKE MTOTO WA WATU FULL KUSTRESIKA!!SASA #AKCLASSIC WAMELIONA ILO NA SASA WAMEKULETEA BIDHAA INAKWENDA KWA JINA #EXTRACT DEODRANT YAANI HII NI NOUMA!!UTAKUBALI MWENYEWE NDANI YA MUDA MCHACHE KWAPA LIMEIMPROVE VIBAYA!!KARIBUNI
   HIZI HALI PICHA HULETWA NA SABABU TOFAUTI KUNA WALE WA ILE MIKOROGO MIKALI,KUNA HALI YA KUJIFUNGUA LAKINI PIA CHUNUSI SUGU...HALI ZOTE HUFANYA NGOZI KUHARIBIKA KUONEKANA KAMA IMEUNGUA KULETA MAKUNYANZI N.K!AK CLASSIC SAFARI HII TUMEKUJA NA BIDHAA KWA AJILI YA KUTATUA HALI IZO..BIDHAA HIZI NI ORGANIC 100% KUTOKA SWEDEN..TUNA ANTIAGING CREME,MUSK,SERUM NA CLEANSERS MAHUSUSI KWA AJILI YA HILO TATIZO!!MAMBO YAKO #AKCLASSIC
   KASHESHE  NI PALE UNAPOOGOPA KUVAA KIATU FLANI KWA SABABU TU UKIKIVAA JASHO LINAKUTOKA SANA MIGUU NA KUABABISHA HARUFU KALI KIDOGO WAKATI WA KUKIVUA!!SASA #AKCLASSIC WAMELIONA ILO NA SASA JIACHIE DADA/KAKA KWANI TUNA BIDHAA HIYO HAPO #TOSIKUIVA UNAPANGUSA TU MIGUU YAKO MARA MOJA KWA WEEK MAMBO YANAKUWA POA KABISA..UTASKIA HARUFU HATA!!
   WATAALAM WA MAMBO WANASEMA JASHO LINA UMUHIMU WAKO LINAPOTOKA KUMWILI!!LAKINI KUNA ILE HALI YA KUTOKA JASHO KULIKO PITILIZA YAANI KIDOGO TU UMELOWA KAMA UMECHEZEA KOKI YAKHEE!!SASA TUMEKUJA NA HII #ABSOLUTORR HII ITAKUKAUSHA JASHO NA KUKUFANYA UWE MKAVU PASIPO KUWA MADHARA YAANI RAHA MUSTAREHE!!DEODRANT HII UNATUMIA MARA 2 KWA WEEK TENA USIKU!! KARIBU #AKClASSIC KINONDONI KWA MANYANYA AU SINZA KUMEKUCHA..0753482909..UNAWEZA PIA KULETEWA ULIPO!TUPIGIE

  0 0

  Msanii Maarufu nchini Ahmed Olotu 'Mzee Chilo' wa kwanza kulia akimsikiliza mwenyekita wa SHIWATA Cassim Taalib wa pili kushoto  walipokuwa wakigawa mashamba kwa ajili ya wanachama wao
  Watakaohamia kijiji cha wasanii kupewa bustani bure


  MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umetoa bure kwa wanachama wake wanaomiliki nyumba katika kijiji chao cha Mwanzega Mkuranga ya eneo la kulima bustani.

  Mwenyekiti wa SHIWATA,Cassim Taalib aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuwa watakaonufanika na ofa hiyo ni wale watakaohamia katika nyumba zao kabla ya Desemba mwaka huu ambapo mtandao unaadhimisha miaka 10 kutoka uanzishwe.

  Alisema wanachama hao wanatakiwa kufika SHIWATA kugaiwa maeneo hayo ambayo yatalimwa mazao ya muda mfupi (ambayo si ya kudumu) kama vile pilipili,mahindi, matango, pilipili hoho, mananasi, mbogamboga, matikiti maji ambayo hustawi kwa wingi maeneo hayo.

  Katika hatua nyingine SHIWATA imeamua kusafisha shamba la ekari 200 ambazo zimekwisha gaiwa kwa wanachama ambao walijitokeza kulima katika shamba hilo la 500 zinazomilikiwa na mtandao huo kwa ajili ya maandalizi ya kilimo kwanza msimu huu katika kijiji cha Ngarambe, Mkuranga.

  Mwenyekiti Taalib alisema SHIWATA imeingia mkataba na Kampuni ya Willy Enterprises Ltd ya Dar es Salaam kukodisha mtambo wa kusafisha shamba (Buldoza) kwa ajili ya wanachama zaidi ya 100 waliojitokeza kulima.

  Alisema SHIWATA itatumia sh. mil. 22.2 kukodisha buldoza hilo kusafisha shamba la ekari 200 zilizogaiwa kwa wanachama ambapo kila mmoja atalipa gharama ya sh. 111,000 kwa ekari moja.

  Jitihada za kusafisha shamba hilo zinafanywa na SHIWATA ikiwa ni maandalizi ya kufikiwa kwa malengo ya kuanzishwa mtandao huo utakaoadhimisha miaka 10 ya kuanzishwa mwaka 2004.

  Mpaka sasa SHIWATA inao wanachama 8,000 kutoka fani mbalimbali za uigizaji, muziki wa dansi, muziki wa kizazi kipya, taarab, soka, netiboli, vijana na waandishi wa habari.

  Mwanachama wa siku nyingi wa Shiwata Manase Zabron ambaye ni kocha wa mpira wa kikapu nchiniakienda kuoneshwa shamba lake
  Baadhi ya viongozi wa Mtandao wa wasanii Tanzania 'SHIWATA' wakishudia ugawaji wa mashamba kwa wanachama wake juzi Ngarambe Mkulanga Mkoa wa Pwani.

  0 0

   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na kupiga picha ya pamoja na na viongozi wa Bendi ya Msondo ngoma Ikulu jijini Dar es Salaam leo mchana.Viongozi hao walimtembelea Rais Kikwete  kufanya naye mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya tasnia ya muziki nchini. Bendi hiyo kongwe imetimiza miaka 50 mwezi huu. Picha na Freddy Maro


  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo pinda akizunguma na Watanzania waishio nchini Oman akihitimisha ziara yake nchini humo Oktoba 29, 2014. Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maalim Mahadhi nakushoto ni Balozi wa  Tanzania nchini Oman, Ali Ahmed Saleh.
   Baadhi ya watanzania waishio Oman wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo PInda wakati alipowahutubia kwenye hoteli ya Al Bustan mjini Muscut Oktoba 29, 2014. 
   Baadhi ya watanzania waishio Oman wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo PInda wakati alipowahutubia kwenye hoteli ya Al Bustan mjini Muscut Oktoba 29, 2014.
   Baadhi ya watanzania waishio Oman wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo PInda wakati alipowahutubia kwenye hoteli ya Al Bustan mjini Muscut Oktoba 29, 2014. (Picha na Ofisi yaWaziri Mkuu)


  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Kongamano la Maadhimisho ya miaka 10 ya Tume ya utumishi wa Umma lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam .
  Sehemu ya washiriki wa Kongamano la Maadhimiso ya miaka 10 ya tume yaUtumishi wa Umma lililofanyika jijini Dar es Salaam leo
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la Maadhimiso ya miaka 10 ya tume ya Umma lililofanyika jijini Dar es Salaam leo.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa tatu kushoto) pamoja na makatibu wakuu Kiongozi wastaafu Matern Lumbanga(kulia) na Philemon Luhanjo(kushoto).(picha na Freddy Maro)

  0 0

  Hivi karibuni kumezuka taarifa za upotoshwaji zilizotolewa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Serikali ya Tanzania imemteua Bw. Salaah, Mkurugenzi wa Home Shopping Centre, (pichani ) kuwa Konseli wa Heshima (Honorary Consul) kwenye mji wa Guangzhou kwenye Jimbo la Guandong. 

  Watoa taarifa hizo, hawakutoa ushahidi wowote kuthibitisha madai yao zaidi ya kutoa picha mbalimbali za Bw.Salaah kutoka kwenye mitandao mingine ya kijamii.

  Taarifa hizo sio za kweli. 
  Kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za mahusiano ya kidiplomasia ya China, nafasi ya Konseli wa Heshima haitambuliki 'mainland' China.  Kwa maneno mengine hakuna nchi yoyote duniani inayoweza kuteua mtu kuwa Konseli wa Heshima katika eneo lolote la China isipokuwa Hong Kong ambako kuna mamlaka huru za utawala zinazofuata sheria zake.

  Kwa faida ya umma, ni vema kufafanua kwamba Nchi ya China inakubali nchi za Nje kufungua Ubalozi kamili (Embassy) ambao makao yake yanatakiwa kuwepo katika mji Mkuu wa China- Beijing na Konseli Kuu ama kwa lugha iliyozoeleka Ubalozi Mdogo (General Consulate) ambao unaweza kufunguliwa kwenye makao Makuu ya mji wowote ule katika Majimbo ya China.
  Watu wengi wamekuwa wakichanganya Ubalozi Mdogo au Konseli Kuu (General Consulate) na Konseli (Ubalozi) wa Heshima  (Honorary Consulate).   Konseli Kuu (General Consulate) ni sehemu ya Ubalozi (ndio maana wengi huuita Ubalozi Mdogo) ambapo kiongozi wake na maafisa wake wote ni watumishi wa Serikali kutokea Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.  Masharti ya kuwa Mkuu wa Konseli 'General Consulate' lazima uwe Afisa Mwandamizi wa Mambo ya Nje mwenye uzoefu usiopungua miaka 10 ya Utumishi katika Wizara ya Mambo ya Nje.


  Kwa muktadha huo, taarifa kwamba Bw.Salaah ameteuliwa kuwa Balozi wa Heshima wa Tanzania huko Guangzhou sio kweli kwasababu Sheria za China haziruhusu uwepo wa nafasi hiyo.  Aidha, Bw Salaah hawezi kuwa Balozi Mdogo (Consul General) kwa kuwa yeye sio mwajiriwa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.  Hivyo habari zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii sio za kweli na zinalenga kuupotosha umma.


  IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
  WIZARA YA MAMBO YA 

  NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
  OCTOBER 30, 2014

  0 0

   Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira hii leo imekamilisha ziara yake kwa kukagua mgodi wa Buzwagi na kuridhishwa na utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Baraza la Taifa la Hifadhi na usimimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa mgodi huo.

  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh. Ummy Mwalimu akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira. Wa kwanza kulia ni Mh. James Lembeli Mwenyekiti wa Kamati hiyo.
  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Ummy Mwalimu (katikati) akiambatana wajumbe wa Kamati katika ziara ya kukagua bwawa la kuhifadhia maji katika mgodi wa Buzwagi.

  Pichani ni ujenzi wa awamu ya pili wa Kituo cha Afya cha Mwendakulima kinachojengwa na Mgodi wa Buzwagi kwa ajili ya kuwasogezea wananchi huduma bora za afya.

  Baadhi nyumba zitakazotumiwa na waganga na wauguzi wa kituo cha afya cha Mwendakulima pindi kituo hicho kitakapoanza kutumika.

  0 0

   Afisa Mauzo wa Benki ya Exim Tanzania, William Kikoti (wa pili kushoto), akimkaribisha Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Bw. Odilo Majengo (kulia), katika banda la benki hiyo wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Viwango yaliyoandaliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) katika viwanja vya Karemjee jijini Dar es Salaam Jumatano. Waliopo katika banda hilo ni Mkuu wa Matawi wa Benki ya Exim, Bi. Elizabeth Majengoh (kushoto) na wafanyakazi wengine wa benki hiyo
   Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw. Joseph Masikitiko (kushoto), akifurahia jambo wakati akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Matawi wa benki ya Exim, Bi. Elizabeth Majengoh (wa pili kulia), juu ya huduma na bidhaa zitolewazo na benki hiyo, alipotembelea banda la benki hiyo katika Maonyesho ya wiki ya viwango yaliyoandaliwa na TBS na kufanyika katika viwanja vya Karemjee jijini Dar es Salaam Jumatano. Pamoja nao ni Mkuu wa Matawi wa benki hiyo Agnes Kaganda (wakwanza kushoto) na wafanyakazi wengine wa benki hiyo.
   Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw. Joseph Masikitiko (kulia), akiwasalimia wafanyakazi wa Benki ya Exim alipotembelea banda la benki hiyo katika Maonyesho ya Wiki ya Viwango yaliyoandaliwa na TBS na kufanyika katika viwanja vya Karemjee jijini Dar es Salaam Jumatano
  Afisa Mauzo wa Benki ya Exim, Bw. William Kikoti, akifafanua juu ya bidhaa na huduma mbalimbali zitolewazo na benki hiyo kwa baadhi ya washiriki waliohudhuria maonyesho ya wiki ya viwango yaliyoandaliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) katika viwanja vya Karemjee jijini Dar es Salaam Jumatano. Wengine ni wakuu wa watawi wa benki hiyo Bi. Elizabeth Majengoh (wapili kushoto) na Bi. Agnes Kaganda (aliyekaa wakwanza kulia).

  0 0


   Afisa habari wa Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi Stella Vuzo akitoa mada kuu iliyokuwa inahusu malengo ya maendelea ya milenia na kuangalia imefikia wapi kwenye malengo hayo pamoja na kuwaelimisha kuhusu maendeleo endelevu baada ya mwaka 2015(Post 2015 Sustainable Development) iliyotolewa kwa Mtandao wa vijana wa Temeke.

  Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa jana iliandaa Alhamisi ya Burudani kwa ajili ya kujifunza kazi mbalimbali za Umoja wa Mataifa. Kwa kila Alhamis ya mwisho wa mwezi Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa huandaa burudani kwa makundi mbalimbali na kujifunza kazi mbalimbali za Umoja wa Mataifa. Alhamisi ya mwezi wa kumi kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa kilitembelea Mtandao wa Vijana wa temeke na kujadili mambo makuu ya malengo ya Milenia pamoja na kuangalia ni jinsi gani vijana wanashiriki katika shughuri za kimaendeleo katika jamii zao
   Mkutubi - Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa, Bi Harriet Macha akisisitiza jambo kwenye mada kuu iliyokuwa inahusu malengo ya maendelea ya milenia na kuangalia imefikia wapi kwenye malengo hayo pamoja na kuwaelimisha kuhusu maendeleo endelevubaada ya mwaka 2015 (Post 2015 Sustainable Development).
   Mwenyekiti wa Kituo cha Vijana wa Makangalawe, Bwana  Ismael Mnikite akizungumza jambo kuhusu mada husika na kuangalia ni njia  gani zinaweza kuwapelekea vijana kushiriki kwenye shughuli nzima za maendeleo
  Mwenyekiti wa Kituo cha Vijana wa Makangalawe, Bwana  Ismael Mnikite akigawa vipeperushi vya Umoja wa mataifa pamoja na fomu kwa vijana hao wa Temeke.
  Mada ikiendelea
  Katibu wa Mtandao wa Vijana Temeke, Bwana Yusuph Kutengwa akichangia mada
   Omari A. Mketo akichangia
   Ishengoma ambaye ni mlemavu wa macho akieleza faida alizozipata baada ya kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa kutoa mafunzo hayo kwa mtandao wa vijana wa Temeke.

  Baadhi ya vijana wa mtandao wa vijana wa Temeke wakisoma kwa umakini malengo ya milenia wakati kituo cha habari cha umoja wa mataifa walipokuwa wanatoa mada kwa vijana hao
  Picha ya pamoja

  0 0

   
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Sekretarieti,makao makuu ya Chama Ofisi Ndogo Lumumba jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Mtangazaji wa zamani wa Radio Tanzania (RTD) sasa TBC,Ben Hamis Kikoromo maarufu kama Ben Kiko enzi za uhai wake akiwa katika moja ya semina alizohudhuria.

  MTANGAZAJI na mwandishi wa habari mkongwe nchini Ben Kiko amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hosptali ya taifa ya rufaa ya Muhimbili jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

  Ben Kiko ambaye jina lake kamili ni Ben Hamisi Kikoromo alihamishiwa katika hosptali ya Muhimbili kutokea hosptali ya Jeshi ya Milambo ya mkoani Tabora ambako alilazwa kwa ajili ya matibabu ya figo kwa muda wa wiki mbili.

  MUNGU ILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA,
  AMIN
  Mtangazaji wa zamani wa Radio Tanzania (RTD) sasa TBC, Ben Hamis Kikoromo maarufu kama Ben Kikoakizungumza na Mwakilishi wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini Dixon Busagaga alipomtembelea nyumbani kwake eneo la Cheyo mkoani Tabora wakati wa uhai wake.  Mtangazaji wa zamani wa Radio Tanzania Dar es salaam ambayo sasa ni TBC Taifa, Ben Hamis Kikoromo (pichani akiwa ameshika hati ya Tuzo ya Utumishi uliotukuka wa Maisha April 2012) maarufu kama Ben Kiko,   
   atakumbukwa kama mmoja wa watangazaji mahiri ambao walijipatia umaarufu mkubwa ambapo katika enzi za uhai wake alifanya makubwa wakati wa Vita vya Kagera kwa kuleta matukio mbalimbali kutoka uwanja wa vita. Pia aliupaisha sana mkoa wa Tabora alikokuwa akifanyia kazi kwa habari na visa mbalimbali katika kipindi cha RTD cha Majira.

  0 0


   Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC,Rukia Mtingwa wa kwanza kushoto akimkabidhi  hundi yenye thamani ya shilling milioni 116,952,000 Mkurugenzi wa Kituo cha MAA MEDI bwana Furaha Levilal wa kwanza kulia katika uzinduzi wa program maalum ya Vijana.

   Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya  Maendeleo ya Vijana Bwana James kajugusi  akiteta jambo na Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC,Rukia Mtingwa alipokuwa akizindua Programu Maalumu kwa Vijana itakayotolewa Kituo cha MAA MEDI.

   Meneja wa Miradi kutoka kituo cha MAA MEDI bwana Albany James akiongea na waandishi wa habari katika uzinduzi wa programu maalum kwa Vijana iliyozinduliwa jana jijini Dar es Salaam.
   Baadhi ya washiriki walioudhuria uzinduzi huo wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana wakati wa uzinduzi wa Program maalum kwa Vijana iliyoandaliwa na kituo cha MAA MEDI.  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Profesa Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa kituo cha michezo katika eneo la Kidongo Chekundi  jijini Dar es salaam.

  Kituo cha michezo kinajengwa kwa ufadhili wa Klabu ya Sunderland kwa kushirikiana na Symbion Power na Serikali ya Tanzania.

  Shehere hizo zinatarajiwa kesho asubuhi (Jumamosi tarehe 1 Novemba 2014) kuanzia majira ya saa mbili asubuhi.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es salaam na Mwakilishi wa Symbion nchini Julie Foster , sherehe hizo pia zitahudhuriwa na Waziri wa Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella E. Mukangara, Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Sunderland ya Nchini Uingereza Bi. Margaret Byrne na  Afisa Mtendaji Mkuu wa Symbion Power Bw. Paul Hinks

  Taarifa hiyo imeongeza kuwa pamoja na uzinduzi wa ujenzi huo Rais Kikwete atapanda mti kwenye eneo hilo, akisaidiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Sunderland AFC Bi. Byrne, Mkurugenzi wa Biasharawa klabu hiyo Gary Hutchinson, na Afisa Mtendaji Mkuu wa Symbion Power  Bw. Hinks,.

  Klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza ya Barclays, Sunderland AFC inatoa usaidizi wa kiufundi na utendaji katika uendelezaji wa mradi wa mpira wa miguu, ambao ni wa kwanza na wa aina yake nchini humu, utakaohakikisha  maelfu ya vijana wananufaika kutokana na mtazamo wa pamoja wa kuchanganya mpira wa miguu, elimu na ushiriki wa jamii, ili kupata ujuzi na utaalam wa Sunderland AFC.

  0 0

  Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji, Dk Anacleti Kashuliza (wa pili kulia) akiweka saini makubaliano ya ushirikiano kati ya FCDL na TAWOFE katika kuboresha utengenezaji wa samani nchini. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk Mary Nagu (wa kwanza kulia) anayeshuhudia makubaliano hayo.

  KAMPUNI ya Furniture Centre (FCDL), na Shirikisho la Watengenezaji Samani Nchini (TAWOFE), wamesaini makubaliano (MoU) kuongeza ubora wa bidhaa za samani zinazotengenezwa nchini na kuzifanya zipate soko ndani na nje ya nchi.

  Makubaliano haya yamekamilika ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ikiwa ni mwendelezo wa Tathimini iliyofanywa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwa mkoa wa Dar es Salaam na mikoa ya jirani, katika kuiwezesha sekta ya Samani nchini kupitia vikundi na makampuni ya ndani. 

  Tathimini hiyo ya Baraza ya mwaka 2008, ilijikita katika kubaini mahitaji na changamoto zinazoikabili sekta ya samani hapa nchini. Baraza liliweza kuandaa warsha iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali na ambapo matokeo ya tathmini hiyo yaliwasilishwa. Wadau kutoka sekta ya umma na binafsi walishiriki katika mrejesho wa tathmini hiyo na wao pia kuchangia maoni zaidi kwa ajili ya kuiboresha.

  Washirika hao walisaini makubaliano hayo katika  hafla iliyoshuhudiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji wa Uchumi na Uwekezaji), Dk Mary Nagu. Akizungumza katika hafla hiyo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Dk Anacleti Kashuliza, alisema pamoja na kuwepo kwa fursa kubwa ya soko la samani hapa nchini bado ushiriki wa vikundi na makampuni ya ndani katika soko hilo ni mdogo sana kulinganisha na samani zinazoagizwa kutoka  nje ya nchi.

  Alisema tunatoa wito kwa taasisi za Umma na Binafsi  ziunge mkono jitihada hizi kwa kununua samani toka kwa watengenezaji samani  wa ndani na ili kuwapa ushirikiano zaidi utakaowezesha kuimarisha sekta ya samani zitengenezwazo ndani ya nchi. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TAWOFE, Bw Fredrick Waibi, alielezea makubaliano kati ya FCDL na TAWOFE ni mkakati mzuri utaomjengea uwezo fundi seremala kuweza kutengeneza bidhaa zitakazoweza kukubalika kimataifa, kuongeza tija kazini na kupunguza umaskini kati ya mafundi seremala.

  Naye Mkurugenzi Mkuu wa FCDL, Bw Shafik Bhatia, alisema kama wadau muhimu wa samani nchini wameona umuhimu na wanajivunia  kushirikiana na Tawofe katika kuboresha huduma za samani nchini .

  0 0

  Basi la Simba mtoto linalofanya safari zake kati ya Dar na Tanga likiwa limegongana uso kwa uso na Lori la mizigo katikati ya Daraja la Mto Wami mkoani Pwani,dereva wa lori hilo amefariki papo hapo na wengine kujeruhiwa.tutaendelea kupeana taarifa zaidi hapo baadae.
  Baadhi ya wasamaria wema wakijaribu kumchomoa Dereva  wa Lori hilo aliyekuwa amebanwa vibaya,pichani ambalo namba zake za usajili hazikufahamika mara moja.

  0 0  0 0

  DSC_0152

  Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza na waandishi wa habari wa Zanzibar kwenye ofisi ndogo za mashirika ya Umoja wa Mataifa visiwani Zanzibar kuhusiana na mafanikio ya mradi wa kusaidia maendeleo nchini Tanzania (UNDAP) ulioanza mwaka 2011 na sasa ukiwa ukingoni. Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues na kushoto ni Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu.

  Na Mwandishi wetu, Zanzibar
  Zaidi ya watoto 3000 waliokuwa wakikabiliwa na utapiamlo nchini Zanzibar sasa wapo katika hali nzuri baada ya Umoja wa Mataifa (UN)kwa kushirikiana na wadau wengine kufanikisha programu ya kusaidia kukabili utapiamlo mkali kwa watoto hao.

  kauli hiyo imetolewa katika mkutano wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na waandishi wa habari uliofanyika hivi karibuni ambapo UN ilielezea mafanikio ya mradi wa kusaidia maendeleo nchini Tanzania (UNDAP) ulioanza mwaka 2011 na sasa ukiwa ukingoni.

  Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez alisema kwamba Umoja huo ukiadhimisha miaka 69 ya uwepo wake imefurahishwa na maendeleo yaliyopatikana katika maeneo ambayo ilikuwa imejikita kusaidia kukabili umaskini,kuhakikisha utawala bora na kusaidia jamii.

  Alisema pamoja na kuendeleza na juhudi za kukabiliana na utapiamlo katika visiwa vya Pemba pia Umoja huo umefurahishwa na hatua zilizofikia katika kukabiliana na vifo vya mama na mtoto na kusema ni wajibu kuhakikisha watoto hawana matatizo ya utapiamlo kwani wao ndio msingi wa taifa la sasa na lijalo.
  Alisema hata hivyo upo umuhimu wa kuendelea na washirika wengine wa maendeleo kuona kwamba tatizo la utapiamlo la visiwa vya Pemba kwa watoto linamalizwa.
  DSC_0177
  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akielezea kufurahishwa kwake na Serikali Tanzania kwa kupigia hatua katika kutoa ajira nyingi kwa walimu kwenye mkutano huo. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.


  Alisema pamoja na mafanikio hayo Umoja wa Mataifa unaendelea na ujenzi wa uwezo kwa baraza la wawakilishi ili kuhakikisha kwamba baraza hilo linawezesha kuwepo kwa sheria nzuri na bora na zinazotekelezeka ambazo hazikwazi kukua kwa demokrasia na ustawi wa jamii.

  Aidha alisema kwa kuzingatia kwamba mwaka huu mwishoni kuna uchaguzi wa serikali za mitaa na pia uchaguzi mkuu mwakani pamoja na kura ya maoni ya katiba, Umoja huo unaendelea kufanyakazi na Tume ya uchaguzi ya Zanzibar kwa kuiwezesha kitaalamu kuweza kufikisha elimu ya uraia kwa wananchi.
  Aidha katika masuala ya utawala bora Umoja wa Mataifa unashirikiana na taasisi za sheria kwa ajili ya kufanya mabadiliko katika mfumo wa sheria za watoto ili kuwepo na usalama mkubwa kwa watoto hasa kutokana na utamaduni uliopo visiwani kwa sasa.
  Aidha alisema kwamba yamepatikana mafanikio makubwa katika sekta ya tiba na kuzuia maambukizi ya Ukimwi na kuondokana na unyanyapaa.
  DSC_0121
  Mwandishi wa gazeti la Mwananchi Zanzibar, Talib Ussi akiuliza swali kwenye mkutano huo.
  Aliwahimiza waandishi wa habari kuwa daraja la kuelezea mafanikio na pia changamoto zinazotokana na program za Umoja wa mataifa zilizolenga kusaidia maendeleo ya wananchi wa Zanzibar.
  Alisema matokeo ya program ya kusaidia maendeleo ya Tanzania (UNDAP) ndiyo yatakayotumika kutengeneza UNDAP 2 ambayo inatarajiwa kuanza katikati ya mwaka 2016.
  Katika mkutano huo ambapo waandishi walipata nafasi kubwa ya kuuliza masuala yanayohusu shughuli za Umoja wa Mataifa Zanzibar, Bara na duniani kwa ujumla Alvaro alizungumzia pia umuhimu wa Umoja wa Mataifa katika dunia inayobadilika.
  Alisema pamoja na madhumuni ya kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa, baada ya vita kuu ya dunia ya pili mwaka 1945 ya usalama na kujenga uchumi baada ya kuharibiwa na vita yapo palepale, mabadiliko katika utendaji kwa lengo hilo hilo la usalama na maendeleo ni dhahiri.
  Alisema mathalani malengo ya millennia (MDGs) ambayo yalisanifiwa kwa lengo la kuleta maendeleo duniani katika demokrasia, utawala bora na ustawi wa jamii, bado yanatakiwa kuimarishwa kupitia mpango mpya wa maendeleo SDGs wenye lengo la kutokomeza umaskini uliotopea duniani ifikapo mwaka 2030.
  DSC_0060
  Afisa Habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma Ledama akifafanua jambo kwenye mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na mafanikio ya mradi wa kusaidia maendeleo nchini Tanzania (UNDAP) ulioanza mwaka 2011 na sasa ukiwa ukingoni.
  Alisema ni matumaini yake kwamba Tanzania itaendelea kushirikiana na UN katika kuhakikisha kwamba mafanikio katika MDGs yanaendelezwa na pia kukamilisha yale ambayo hayakufikiwa kwa lengo la kutokomeza umaskini uliotopea ifikapo mwaka 2030.
  Alisema mafanikio ya UNDAP kwenye utawala bora, ustawi wa jamii na uondoaji umaskini na ukuaji wa uchumi nchini Tanzania, ni matokeo ya ushirikiano kati yake ya mamlaka mbalimbali nchini Tanzania na kwamba UN itaendelea kushirikiana na mamlaka hizo kuhakikisha maendeleo ya kuwezesha amani na usalama na ukuaji wa uchumi yanapatikana.
  Naye Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma Ledama amesema lengo la kukutana na waandishi wa habari wa Zanzibar lilikuwa kuangalia mafanikio na namna ambavyo program za Umoja wa Mataifa katika visiwa vya Zanzibar zinafanyakazi.
  Alisema kwamba shughuli za Umoja wa Mataifa visiwani humo zinaweza tu kujulikana kwa wananchi kwa kupitia waandishi wa habari ambao wanakuwa wanajua Umoja huo unafanya nini na wapi.
  DSC_0063
  Mkutano kati ya Mashirika ya Umoja wa Mataifa na waandishi wa habari wa Zanzibar ukiendelea.
  DSC_0131
  Mwandishi wa habari wa TBC, Kulthum Ally, akiuliza swali kuhusiana namna Umoja wa Mataifa unavyoweza kuwasaidia Wanawake wa Zanzibar kupata nafasi za uongozi sawa na wanaume.
  DSC_0192
  Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (waliokaa katikati), Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (kulia) pamoja na Meneja wa Baraza la Habari Zanzibar, Suleiman Omar (kushoto) katika picha ya pamoja na waandishi wa habari wa Zanzibar.

older | 1 | .... | 398 | 399 | (Page 400) | 401 | 402 | .... | 1897 | newer