Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46379 articles
Browse latest View live

MKUTANO WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO TASWA WAFANYIKA BAGAMOYO LEO

$
0
0
Mwenyekiti wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys Bw. Ridhiwan Kikwete akifungua mkutano mkuu wa chama cha waandishi wa habari za michezo TASWA unaofanyika kwenye Hoteli ya Kiromo View Bagamoyo mkoani Pwani ambao unajadili mambo mbalimbali ya Maendeleo na changamoto zinazokabili chama hicho. Waandishi wa habari za michezo ambao ni wanachama kutoka vyombo mbalimbali nchini wanahudhuria mkutano huo ambao ni wa siku moja.PICHA NA FULLSHANGWEBLOG.
Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari za michezo TASWA Bw. Juma Pinto akimkaribisha mgeni rasmi ili kufungua mkutano huo leo asubuhi unaofanyika kwenye hoteli ya Kiromo View Bagamoyo.
Katibu wa Chama cha Waandishi wa habari za michezo TASWA Bw. Amir Mhando akizungumza katika mkutano huo, kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa TASWA Maulid Kitenge, Mwenyekiti Juma Pinto, Mgeni rasmi Ridhiwan Kikwete na kushoto ni George John Katibu Msaidizi.
Mtaalam wa SACCOS kutoka Manispaa ya Ilala Bw. Luambano akitoa mada kuweka na kukopa kwa waandishi wa habari wanachama wa TASWA waliohudhuria katika mkutano huo
Kutoka kulia ni waandishi wakongwe Mwina Kaduguda, Mzee Wlly Chiwango na Mzee Salim Said Salim kutoka Zanzibar wakiwa katika mkutano huo.
Kutoka kulia ni Shafii Dauda, Erasto na Ibrahim Masoud wakiwa katika mkutano huo.
Kutoka kulia ni Elizaberth Mayemba , Timzo Kalugira na Crala Alphonce wakifuatilia mada katika mkutano huo.
Kutoka kushoto ni Elius Kambili, Alfred Lucas na Salum Jaba wajumbe wa kamati ya utendaji ya TASWA wakiwa katika mkutano huo.
Kutoka kulia ni Mgaya Kingoba, Salum Jaba, Richard Mwaikenda na Tulo Chambo wakifuatilia mada katika mkutano huo.
Wajumbe mbalimbali wakihudhuria mkutano wa Chama cha Waandishi wa habari za michezo TASWA kwenye hoteli ya Kiromo View mjini nje kidogo ya mji wa Bagamoyo mkoani Pwani .

Kampuni ya Ndege ya Flightlink yakutana na wafanyakazi wake.

$
0
0
 Picha ya pamoja kwa wafanyakazi wote wa Kampuni ya Ndege ya Flightlink.
Wakurugenzi wa Kampuni ya Flightlink wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni waalikwa.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ndege ya Flightlink,Munawer Dhiren akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha usiku iliyokuwa imeandaliwa maalum kwa ajili ya kukutana kwa wafanyakazi wote wa kampuni hiyo pamoja na familia zao ikiwa ni sehemu pia ya kuuaga mwaka iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana.Picha zote na Othman Michuzi.
 Sehemu ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Ndege ya Flightlink pamoja na familia zao wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo,Munawer Dhiren (hayupo pichani) wakati alipokuwa akizungumza nao wakati wa hafla ya chakula cha usiki iliyokuwa imeandaliwa maalum kwa ajili ya kukutana kwa wafanyakazi wote wa kampuni hiyo pamoja na familia zao ikiwa ni sehemu pia ya kuuaga mwaka iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana. 
 Mazungumzo ya hapa na pale kwa wadau wa Kampuni ya Flightlink yakiendelea wakati wa hafla hiyo.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Flightlink wakipozi kwa picha wakati wa hafla ya chakula cha usiki iliyokuwa imeandaliwa maalum kwa ajili ya kukutana kwa wafanyakazi wote wa kampuni hiyo pamoja na familia zao ikiwa ni sehemu pia ya kuuaga mwaka iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana.



 Wakati wa Chakula uliwadia na kila mmoja alipita kuchukua chakula akipendacho.

ARUSHA KUWA MAKAO MAKUU YA CHAMA CHA NGUMI ZA KULIPWA AFRIKA YA MASHARIKI NA KATI (ECAPBA).

$
0
0

 Chama cha Ngumi za Kulipwa Cha Afrika ya Mashariki na Kati (ECAPBA) kimepata nyumbani baada ya Mstahiki Meya wa jiji la Arusha  Mh. Gaudence Lyimo kuomba kihamie Arusha ili kiweze kukaa karibu na “Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, EAC”
Rais wa ECAPBA Onesmo Ngowi alimhakikishia mstahiki meya kuwa ECAPBA itahamishia makao yake makuu katika jiji la Arusha. Kwa sasa ECAPBA ina makao yake makuu katika Halmashauri ya Manispaa ya Moshi.
 Juhudi za Mstahiki Meya Gaudence Lyimo za kukuza michezo na kukuza utalii katika jiji la Arusha ni moja ya sababu zilizomfanya rais wa ECAPBA kuamua kuhamishia makao makuu katika jiji la Arusha.
 Uamuzi huo uliungwa mkono na mmoja wa wanachama wa  ECAPBA bw. Daudi Chikwanje ambaye ndiye Katibu Mkuu wa Chama Cha Ngumi za Kulipwa Cha Malawi!
 Nchi ya Malawi ni mwanachama wa ECAPBA pamoja na Kenya, Zambia, Ethiopia, Burundi, Sudan ya Kusini, DRC, Rwanda, Uganda na Sudan.
 ECAPBA inaratibu ubingwa unaojulikana kama ECAPBF ambao unawapa mabondia wa ukanda huu kuwa mabingwa imara wa ngumi Afrika.

SALAAM ZA 2013 KUTOKA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

MATAYARISHO YA ZANZIBAR KUHAMA ANALOGIA KWENDA DIJITALI

$
0
0

Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar  29/12/2012

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema matangazo ya mfumo wa Analogia yatazimwa rasmi katika Mikoa yote ya Zanzibar ifikapo Februari 28 mwakani ili kupisha mfumo mpya wa matangazo kwa njia ya Dijitali.

Waziri wa habari, utamaduni, utalii, na Michezo Said Ali Mbarouk ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari katika ukumbi wa Habari maelezo kikwajuni mjini Zanzibar kuhusiana na matayarisho ya kuhamia katika mfumo mpya wa matangazo ya Dijitali.

 Amesema Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Kamisheni ya Utangazaji Zanzibar (ZBC) zimeshauriana na kukubaliana kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iingie katika mfumo mpya wa Dijitali kwa awamu ambapo kwa zoni ya Zanzíbar imekubaliwa kuwa February 28 2013 ndio iwe mwisho rasmi wa matangazo ya Analogi.

Waziri Mbarouk amesema Wizara yake haitozima mitambo ya matangazo ya Analogi ifikapo Disemba 31 bali itakachofanya ni kutangaza kwa pamoja matangazo ya Analogi na Digitali kwa mfumo unaojulikana kitaalamu kama SIMU L CAST hadi itakapofika muda rasmi wa kuhama mfumo wa Analogy.

Akizungumzia matayarisho ambayo yamefanywa na Wizara yake katika kuukabili mfumo mpya wa Matangazo ya Dijitali Waziri Mbarouk amesema tayari wamejenga kituo cha usambazaji ishara(signals) katika eneo la Rahaleo kitakachokuwa na kazi ya kupokea na kusambaza ishara na mitambo ya uendeshaji.


Aidha Wizara imetayarisha maeneo matatu Unguja ambayo ni Kizimkazi,Masingini na Nungwi ambapo kwa upande wa Pemba ni Kichunjuu,Mkanjuni na Konde kwa ajili ya kurushia matangazo ya Dijitali.

Matayarisho mengine ni pamoja na kuandaa utaratibu mzuri wa upatikanaji wa Ving’amuzi na maudhui kwa bei nafuu ambapo amesema vitaanza kuuzwa mwishoni mwa mwezi wa Januari mwakani.

Amefahamisha kuwa bei ya Ving’amuzi hivyo itakuwa rahisi kuliko vingamuzi vingine ambapo mwananchi atatakiwa kukinunua kwa Shl.50,000 na kukilipia shl.8,000 kwa mwezi ili kupata huduma ya matangazo hayo.

Amevielezea Ving’amuzi hivyo ambavyo vitakuwa na huduma mbali mbali ikiwemo Mtandao, Video on demand, programme guide, exclusive service yaani mawasiliano ya makundi maalum ambapo pia jumla ya Chaneli 36 za ndani na nje ya nchi zitapatikana kwa uhakika.

Waziri Mbarouk amesema uzinduzi wa mitambo na matangazo ya Dijitali unatarajiwa kufanyika wakati wa sherehe za Mapinduzi Januari 8 mwakani katika maeneo ya Rahaleo mjini Zanzibar.

Mabadiliko ya Mfumo wa matangazo kutoka Analogia kwenda Dijitali yamekuja kufuatia agizo lililotolewa na Shirikisho la Mawasiliano la Afrika Mashariki EACO kuwa Nchi wanachama wa Shirikisho hilo ziwe zimehamia katika mfumo mpya wa Dijitali ifikapo mwaka 2013.
 
 
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR

WAZIRI WA HABARI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI KUHUSU ZANZIBAR KUHAMA ANALOGIA KWENDA DIJITALI

$
0
0
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk akijibu maswali ya waandishi wa habari hawapo pichani kulia ni Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo Bihindi Khamisi Hamadi.
 Mwandishi wa habari Bw.Salum Vuai akiuliza suali kwa Waziri hayupo pichani juu ya upatikanaji wa vinga`muzi  huko katika ukumbi wa habari maelezo mjini Zanzibar.
 -Waziri wa Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali juu ya suala zima la kuuingia katika mfumo wa Digitali huko katika ukumbi wa habari maelezo kikwajuni mjini Zanzibar. 

Jengo linalotarajiwa kufungwa vifaa vya mitambo ya Digitali lililopo Rahaleo mjini Zanzibar.Picha zote na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar 

RAIS KIKWETE AMJULIA HALI PADRI AMBROS MKENDA ALIYEPIGWA RISASI ZANZIBAR

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Padri Ambros Mkenda wa Kanisa Katoliki la Mpendae mjini Zanzibar anayeuguza majeraha katika taasisi ya mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Moi) jijijini Dar es salaam leo Jumamosi Dsemba 29, 2012 kukupigwa risasi sehemu za mdomoni na watu wasiojulikana mapema wiki hii  wakati akisubiri kufunguliwa geti  la nyumbani kwake maeneo Kitomondo Mjini Zanzibar akiwa ndani ya gari aliyokuwa akiendesha akiwa pekee yake. Rais Kikwete amempa Padri Mkenda pole nyingi na kumuombea apate nafuu haraka.
PICHA NA IKULU
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali  Padri Ambros Mkenda wa Kanisa Katoliki la Mpendae mjini Zanzibar anayeuguza majeraha katika taasisi ya mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Moi) jijijini Dar es salaam leo Jumamosi Dsemba 29, 2012 kufuatia kupigwa risasi sehemu za mdomoni na watu wasiojulikana mapema wiki hii  wakati akisubiri kufunguliwa geti  la nyumbani kwake maeneo Kitomondo Mjini Zanzibar akiwa ndani ya gari aliyokuwa akiendesha akiwa pekee yake. Rais Kikwete amempa Padri Mkenda pole nyingi na kumuombea apate nafuu haraka.

Mjengwablog Itakujia Na Sura Mpya Jan 1, 2013!

$
0
0


Ndugu zangu,

Kutokana na maoni ya wadau mbalimbali tunayo furaha kuwatangazia, kuwa Mjengwa Blog itatoka na muonekano mpya ifikapo Januari Mosi 2013.

DJ Topspin arrives in Dar and Club 327 promises to keep prices affordable for New Year’s Eve.

$
0
0
DJ Topspin (Barry Blendiana Jones Gayle) is officially welcomed to Club 327 by the owner Mr. Lawrence Kadri in the Hennessy VIP Suite.
=======    =======  =======

DJ Topspin arrives in Dar and Club 327 promises to keep prices affordable for New Year’s Eve.


It has been a long time since there has been this much anticipation surrounding the arrival of a DJ in Dar es Salaam but Bongo has become a favorite for the American DJ, Topspin, and last night he put his fans at ease announcing his official arrival in country.  Last night after touching down at JNIA, the American, DJ Topspin was taken right away to Club 327 where he was officially welcomed by club owner, Mr. Lawrence Kadri, inside the Hennessy VIP Suite.


Since Club 327’s announcement of DJ Topspin to be the headliner for the day, there has been great anticipation among music lovers in Bongo, as the American DJ is already a favorite in Dar es Salaam since he came over a year ago to celebrate the two-year anniversary of Groove Theory, a once month soulful house music event.  He was also a co-host of the every popular radio show, The Countdown, on Choice FM for two years.


Speaking after arriving, DJ Topspin said he is very excited to be here, as Tanzania is a destination that ranks high on his list of global party spots as he even passed on a New year’s Eve party in the Central American country of Panama this year to return to Dar es Salaam.

On his side, Club 327 owner, Lawrence Kadri welcomed Tanzanians music lovers to come at Club 327 and celebrate the night on the dance floor.


“At Club 327 we are firm believers in originality in the market. That is why we have positioned Club 327 as the place to be for anyone who loves music” said Kadri who also added “Club 327 will not raise our prices on New Year’s Eve, we will remain true to our motto of affordable clubbing, so music fans can be assured that at Club 327 they can bring in the New Year without breaking the bank”. It is common practice for clubs to raise admission as high as 500% on New Year’s Eve in Dar es Salaam. However, Club 327 will not be one of them.


New Year’s Eve festivities kick off at 9pm on the 31st and DJ Topspin is expected to start spinning a little before midnight and continue deep into the morning. 

Ng'ombe Hanenepi Siku Ya Mnada; Ni Wakati Wa Kujiandaa Na Salamu Za Mwaka Mpya!

$
0
0


Ndugu zangu,

... Najiandaa na salamu za Mwaka Mpya kwa ' Wanakijiji wangu' wa Mjengwablog, Kwanza Jamii na marafiki zangu wa FB. Imekuwa ni utamaduni niliojiwekea tangu mwaka 2006 nilipoanzisha Mjengwablog.

Na salamu za Mwaka Mpya hutolewa mara moja tu kila mwaka, Desemba 31, ni kesho. Ni salamu za mwisho kwa mwaka na zenye kutuvusha kwenda kwenye mwaka mpya. Ni tukio muhimu sana.

Najiandaa vipi? Ni kwa kutembea kwa miguu peke yangu japo kwa saa nzima huku nikitafakari. Kisha nitahitaji kula saladi ya matunda na vikombe vya chai ya rangi bila sukari kabla sijaanza kuyaandika niliyoyafikiri. 

Na hata kwa maandalizi hayo haimaanishi kuwa salamu haziwezi kukosa mapungufu, maana, ni kwa vile zinaandikwa na mwanadamu asiyekamilika.

Muhimu ni kutambua, kuwa kwa kila jambo unalotaka kutenda, basi, jitahidi kufanya maandalizi. Na maanandalizi yasifanywe siku ya tukio lenyewe.

Wahenga walisema; ng'ombe hanenepi siku ya mnada!

SALAMU ZA MWAKA MPYA KWA WADAU

$
0
0

Nikiwa na Bloggers Wenzangu Kutoka Kushoto ni Othman Michuzi Wa Mtaa Kwa Mtaa Blog, Katikati ni Mwenyewe Josephat Lukaza wa Lukaza Blog na Kulia Ni John Bukuku wa Full Shangwe Blog Tulipokuwa katika moja ya Kazi zetu Mwezi Desemba Mwaka huu 2012.

IKIWA IMEBAKI SIKU 1 KUMALIZA MWAKA 2012 NAPENDA KUWASHUKURU FAMILIA YANGU, BABA,MAMA,KAKA,DADA ZANGU,NK PAMOJA NA MARAFIKI ZANGU WOTE WA KIKE NA KIUME BILA KUWASAHAU MAADUI ZANGU KWA KUSHIRIKIANA NA MIMI TAKRIBANI MWAKA MZIMA NA KUNIFANYA KUFIKA HAPA NILIPOFIKA LEO KWA MAANA PEKE YANGU NISINGEWEZA. 

 PIA NAPENDA KUOMBA MSAHAMA KWA WALE WOTE NILIOWAKOSEA IWE KWA BAHATI MBAYA AU HATA KWA MAKUSUDI KUWEZA KUNISAMEHE ILI NIWEZE KUMALIZA MWAKA VIZURI NIKIWA NA AMANI YA ROHO. VILEVILE NAPENDA KUWASAMEHE WALE WOTE WALIONIKOSEA IWE KWA BAHATI MBAYA AU MAKUSUDI KABISA.NIMEWASAMEHE KABISA KWA ROHO MOJA.

 LAKINI PIA NIWASHUKURU WATU WOTE AMBAO KUWATAJA HAPA SITAWAMALIZA KILA MMOJA KWA NAFASI YAKE KWA KUWEZA KUWA NAMI KATIKA MWAKA HUU WOTE NA KUWA MOJA YA SEHEMU YA MAFANIKIO YANGU KWA MWAKA HUU UNAOKARIBIA KUMALIZIKA KESHO, KWA UCHACHE NITAWATAJA KAKA ZANGU,BABA NA MAMA YANGU, DADA ZANGU, WAJOMBA NK VILEVILE VERSITY MATE WANGU AMBAO NIMEISHI NAO TAKRIBANI MIAKA 3 CHUONI,WAFANYAKAZI WENZANGU,  BLOGGERS WENZANGU KWA KUSHIRIKIANA NA MIMI KATIKA KAZI HII NA KUHAKIKISHA NAFANYA YALE YOTE YALIYO MEMA MBELE YA JAMII NA KUNIFUNDISHA KAZI NA KUNISHAURI PALE INAPOBIDI, PIA NAPENDA KUWASHUKURU WASOMAJI WA BLOG YANGU KWA MAANA BILA WAO LEO HII SIJUI NINGEKUWA WAPI. 

LAKINI BILA KUWASAHAU WATU HAWA 
Issa Michuzi, Muhidin Sufian, Othman Michuzi, Ahmad Issa Michuzi, John Bukuku,Haki Ngowi,Jestina George, Fredy Tony Njeje, Jane Siame, Magie Hanlon, Hussein Wa Ujanatz, Jennifer Livigha, Andrew Chale, Cathbert Kajuna, Mroki Mroki, Jane John, Dina Ismail, Joachim Mushi, Mahamudy Zubery, Maggid Mjengwa, Annan, Wanafunzi na Wafanyakazi wote wa UDOM kuanzia 2009 hadi 2012 Na Wengine wengi ambao sijawataja Hapa kwa maana ni Wengi Sana Lakini Bila Kumsahau Dada yangu, Aunt Teddy Mapunda Kwa Mchango wao haswa katika kuhakikisha Lukaza Blog inafikia hapa Leo hii. 

Sina Cha Kuwalipa lakini Mungu Atawalipa Zaidi na Zaidi Nasema Mungu Awabariki sana na kuendelea Kushirikiana na Mimi Hususani Katika Mwaka Mpya Ujao 2013 Mungu atubariki na Kutupigania na kutupa Majaaliwa yake tuweze Kuuona Mwaka 2013 na tuendelee kufanya Kazi Pamoja.

Vilevile Napenda kuwashukuru Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL Tanzania), Kampuni ya R&R, Benki ya NMB, Kwa kukubali Kufanya Kazi na Mimi kwa Mwaka mzima hadi 2013, Na Wadau wengine wote ambao nimeweza kushirikiana nao kwa njia moja au nyingine na Pia Napenda Kuchukua Fursa Hii kuwakaribisha Makampuni Mengine na watu wengine pia Kuweza kufanya Kazi na Mimi Pia.

Nachukua Nafasi Hii Pia Kuwatakia Wasomaji, Ndugu zangu, Marafiki Zangu, Maadui zangu Heri ya Mwaka Mpya 2013.

Tafakari ya Leo: Mwaka 2013 tuwe makini katika Kuchagua aina ya Marafiki ambao Watakuwa na Sisi Katika Kila Hali Iwe Shida na Raha na Ambao wanatufundisha Maisha na kutushika mkono pale tunapotaka kutumbukia kwenye Shimo Na Sio kuturudisha Nyuma

Makalla akabidhi Kombe la michuano ya Kawambwa Cup

$
0
0
Nahodha wa timu ya Beach Boys, Mwinyi Ali akionyesha Kombe la ubingwa la michuano ya Kawambwa Cup baada ya  kukabidhiwa na Mgeni rasmi wakati wa Fainali hizo, Naibu Waziri wa Habari, Vijana na Michezo, Amos Makalla. Kushoto ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini,(TFF)  Leodgar Tenga. 
 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa (kulia) akiteta jambo na Naibu Wazir, Habari, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla (katikati) wakati wa Faina za Kawambwa Cup zilizofanyika katika Uwanja wa Mwanakerenge Bagamoyo mkoani Pwani jana. Kushoto ni Rais Shirisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Leodgar Tanga
Kutoka kushoto ni Mbunge wa Tabora Mjini, Ismail Aden Rage, Rais wa Shirisho la mpira wa Miguu nchini (TFF), Leodgar Tenga, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Mbunge wa Bagamoyo ,Dk. Shukuru Kawambwa ambaye ni  mwandaaji wa michuano ya Kawambwa Cup wakishuhudia Fainali ya michuano hiyo iliyofanyika katika Uwanja wa Mwanakerenge Bagamoyo mkoani Pwani

Wakazi wa GOBA na KWEMBE: Msikose leo saa nane mikutano juu ya MAJI

$
0
0


Wakazi wa Kata ya GOBA: 

Tume ya Haki za Binadamu imetangaza/imenukuliwa kwenye vyombo vya habari leo kuwa imeanza kuchunguza na kuchukua hatua juu ya mashtaka niliyowasilisha kuhusu mgogoro wa toka mwaka 2007 unaokwamisha huduma ya MAJI katika mtaa wa Goba. Kwa upande wa Mtaa wa Kulangwa-Kata ya Goba tenki limeshajengwa, ujenzi wa miundombinu mingine unakaribia kuanza ili wananchi wapate maji kupitia mradi wa Madale Kisauke. Ili kuwa na usimamizi bora kuanzia hatua za awali fikeni leo (Desemba 30, 2012) kuanzia saa nane mchana , Mahali: Shule ya Kulangwa kutoa maoni kuhusu Katiba ya Jumuiya ya watumiaji Maji. 

Tume ya Haki za Binadamu a Utawala Bora nayo ikifika muipe ushirikiano tupate ufumbuzi wa kudumu. Pamoja na jumuiya za watumiaji wa maji na kamati za maji kama ufumbuzi wa mpito, suluhisho la kudumu ni Kata nzima ya GOBA kuhudumiwa moja kwa moja na DAWASA na DAWASCO kupata miundombinu inayoendana mijini kwa kuwa Goba si kijijini tena.


Wakazi wa Kata ya Kwembe:

Utekelezaji wa miradi maji kwa ufadhili wa BTC unasonga mbele. Wakati ujenzi wa miundombinu ukiendelea ipo haja ya kuandaa Katiba ya jumuiya ya  watumiaji wa maji ili kuwa na usimamizi endelevu maji yatakapoanza kutoka. Kwa wakazi wa Kata ya Kwembe fikeni ofisi ya serikali ya mtaa leo kuanzia saa nane mchana mtoe maoni yenu.


Hakika Tutafika!

Maslahi ya Umma Kwanza,


John Mnyika,

Mbunge Jimbo la Ubungo

30/12/2012

TUZO HII NI KWA WADAU WOTE WA FULLSHANGWEBLOG NA KUKARIBISHA MWAKA MPYA 2013

$
0
0
Mkurugenzi wa Fullshangweblog.com Bw. John Bukuku kushoto akipokea tuzo hiyo kutoka kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki katika maonyesho ya World Travel Market (WTM)Nchini Uingereza mwezi Oktoba mwaka huu katikati ni Meneja Masoko wa Bodi ya Utaii Tanzania TTB Bw. Geofrey Meena.
.........................................................

Mwaka huu Fullshangwe imefanikiwa kupata Tuzo ya kutangaza utalii wa ndani wa Tanzania kimataifa mwaka 2011 nchini Uingereza inayoitwa TANZANIA TOURISM BOARD WEB TRAVEL MAGAZINE AWARD 2011, Fullshangweblog.com kupitia kwa mkurugenzi wake Bw. John Bukuku ilipokea tuzo hiyo katika maonesho ya utalii ya kimataifa ya dunia World Travel Market (WTM) yaliyofanyikaneo katika eneo la Exel jijini London nchini Uingereza kuanzaia Oktoba 5 mpaka 8 2012, ambapo Fullshangweblog.com ilikuwa moja ya makampuni yaliyoshiriki katika maonyesho hayo katika kupasha habari.

FULLSHANGWEBLOG.COM inaushukuru uongozi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) inayoongozwa na Mkurugenzi Mwendeshaji Dk Aloyce Nzuki, Mkurugenzi wa Masoko Devotha Mdachi , Meneja Masoko Bw. Geofrey Meena na wafanyakazi wote wa bodi hiyo, pamoja na wadau wake wote kwa kutambua mchango wa FULLSHANGWE.BLOG kama web magazine iliofanya kazi nzuri ya kutangaza utalii wa ndani mwaka 2011 na kuitukukia tuzo hiyo, ninawashukuru sana kwani maana ya tuzo hii ni kwamba tunamaliza mwaka 2012 kwa mafanikio.

Kuna baadhi yamambo niliyokumbana nayo katika kazi zangu za kila siku ” Kuna matukio mengi niliwahi kukutana nayo katika shughuli zangu za kutafuta habari mengine yalikuwa ni ya kukatisha tamaa sana, lakini sikukata tamaa niliendelea kukaza buti kadiri mungu alivyonijalia, Lakini mengine yalikuwa ni ya mafanikio yenye kutia moyo.

Katika kazi hii nimekumbana na mambo mengi “Kuna wakati marafiki zangu wa karibu walinikatisha tamaa na kuniuliza kwamba ninafanya nini mbona sieleweki hasa wakati nilipojitambulisha katika mikutano mbalimbali kwamba nawakilisha WWW.FULLSHANGWEBLOG.COM wengi hawakunielewa hata kidogo nini ninachokifanya, hata hivyo niliendelea na juhudi zangu mpaka walipoanza kutambua na kuelewa kwamba nilikuwa nafanya nini”

Siku moja nilisafiri kuelekea nyanda za juu kusini mkoani Iringa nilifika katika wilaya Mufindi Mafinga nilikutana na kisa ambacho pia nilikiripoti kwenye mtandao, kisa hiki kilikuwa hivi. MAPANDA HOTEL WANASEMA LAPTOP COMPUTER INAKULA UMEME KULIKO PASI NA FRIJI! Nimeingia katika hoteli hii ya Mapanda Hotel and Guest House mjini Mafinga ili niweze kupata kifungua kinywa lakini pia niweze kufanya kazi zangu kwenye kompyuta yangu ya mkononi, lakini sikupata kifungua kinywa wala kufanya kazi yoyote, Kilichonipoza ni kutumia Kompyuta yangu (Laptop) Meneja wa Hoteli hiyo ambaye hakutaka kutaja jina lake alinifuata na kuniambia kwamba siwezi kuendelea kutumia kompyuta yangu kwa kuwa inakula sana umeme ni sawa tu na friji au pasi ya umeme, hivyo ningeweza kumaliza umeme wao wa LUKU, nikajaribu kubembeleza lakini meneja huyo alinikatalia kabisa..

Binafsi sikujali sana wala sikukubaliana na hoja yake manake nilijua kwamba umande na umbumbumbu umewajaa kwenye ubongo wao katika teknolojia ya Kompyuta hivyo kwao wao Kompyuta ya mkononi au Laptop ni sawa usiku wa giza, Ikabidi niondoke hapo lakini bahati nzuri nikapata Internet Cafe inayoitwa 3A Traders Internet Cafe hapo nikafanya kazi yangu vizuri kabisa Nawatahadharisha ndugu zangu mnataka kuja na kompyuta zenu hapa Mafinga msijisumbue kwenda hapo Mapanda Hotel kwani yanaweza kuwapata yalionipata mimi.

MATUKIO YA KUKUMBUKWA Kati ya matukio ambayo ni ya kumbukumbu kubwa ni tukio la kuzama kwa September 10, 2011 ambalo mtandao wa Fullshangweblog.com uliripoti kwa ufupi na kuvuta hisia za watembeleaji wengi MELI ya Spice Islander imezama usiku wa kuamkia leo ikiwa safarini kuelekea Pemba ikitokea bandari ya Malindi Unguja. Meli hiyo inasemekana ilikuwa na abiria wapatao 610 ambapo juhudi za kuokoa majeruhi wa ajali hiyo bado zinaendelea hivi sasa. Akizungumzia ajali hiyo, Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu, Issa Haji Ussi amesema tukio hilo limetokea saa 8:30 za usiku. Haji Ussi amesema meli hiyo iliondoka katika Bandari ya Malindi Unguja ikiwa katika hali ya uzima, lakini katikati ya safari ikapata hitilafu na kusababisha kubinuka na hatimaye kuzama kabisa.

Lakini pia tukio linguine lililovuta hisia za watembeleaji wengi lilikuwa ni kifo cha Mwigizaji Maarufu nchini Marehemu Steven Kanumba watu wengi walikuwa wakitembelea mtandao ili kupata taarifa mbalimbali juu ya msiba huo. NINAJISIKIA VIZURI KUWA BLOGGER Nimekuwa nikifurahia kazi yangu na kuipenda sana kwani katika kazi yangu hii ya kupasha habari imenikutanisha na watu wengi maarufu, wasio maarufu lakini ni muhimu katika jamii na wakati mwingine ninaposafiri katika mikoa mbalimbali na vijiji na nje ya nchi, kitu kikubwa kinachonifurahisha ni matukio halisi ninayokutana nayo, kwani nakutana na habari ambazo zinagusa hisia za wasomaji na watembeleaji wa mtandao na pia zinanifanya kujifunza mambo mengi yanayotokea duniani pia napata habari zenye uhalisia wa maisha ya mtanzania na matukio yenye kuvuta hisia kwa wasomaji wetu, jambo ambalo linanifanya nijisikie vyema zaidi ninapopata nafasi ya kupiga picha na kuandika habari za kijamii kutoka vijijini katika mikoa mbalimbali na mataifa mbalimbali hii ni kutokana na mvuto wa picha na habari zenyewe lakini pia ninapata changamoto za kimawazo na jinsi ya kujikwamua katika maisha ya kila siku.

SHUKURANI KWA WADAU Mwisho ninawashukuru wadau wote waliofanikisha hapa kwa njia yoyote ile mafanikio ya mtandao wa FULLSHANGWEBLOG.COMsi kwa juhudi zangu binafsi juhudi binafsi, bali pia ni juhudi za wadau wote ambao tulishirikiana nao na tunaendelea kushirikiana nao kwa moyo wa dhati, ni matumaini yangu kwamba tutaendelea kushirikiana kwa karibu ili tuweze kuendeleza juhudi za kujenga nchini yetu nzuri ya Tanzania na kupasha habari zaidi kadiri tutakavyojaliwa na Mwenyezi Mungu katika mwaka ujao wa 2013

Lakini naomba nitaje baadhi ya taisisi, mashirika na wadau kadhaa waliotusaidia na wanaendelea kutusaidia kwa kututumia habari na matukio mbalimbali, ninatoa shukurani kwa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Idara ya Habari Maelezo, Idara ya Habari Maelezo Zanzibar, Kitengo cha habari Ofisi ya Waziri Mkuu, Kitengo cha Habari Ofisi ya Makamu wa Rais, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB),Kitengo cha habari Ofisi ya Bunge, Vitengo vya habari Katika Wizara mbalimbali, Mashirika, Makampuni binafsi, Idara za serikali na wadau mmoja mmoja waliotusaidia kupata habari mbalimbali muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu.

Nitakuwa siyo mwingi wa fadhila kama sitawashukuru kaka zangu Muhidin Iss Michuzi na Maggid Mjengwa, kaka zangu walionitangulia kwa umri na kazi ya kublogu ninawashukuru kwa ushauri wo ninaoweza kuuita maalumu pia kwa msaada wao katika kunielekeza mambo mengi juu ya uelewa wa kublogu, ambao nimekuwa nikipewa wakati wote, nashukuru sana kaka zangu naomba tuendelee na moyo huohuo na mungu atatutangulia katika yote, Lakini pia niwashukuru mablogger wenzagu Michuzijunior wa Jiachieblog au Ahmed Michuzi kama anavyojulikana, Mroki Mroki, Zainul Nzige, Carthbert Kajuna, Othman Michuzi, Abdalla Mrisho, Josephat Lukaza na Mwanamke blogger mkongwe Mamaa Shamimu Mwasha wote ninawapenda sana.

Mwisho napenda kumshukuru dada yangu, mwandishi wetu na mpiganaji Gladness Mushi wa FULLSHANGWEBLOG.COM mkoani Arusha, ninakushukuru dada yangu kwa kuipigania FULLSHANGWEBLOG na kuitambulisha kwa nguvu mkoani Arusha kutokana na habari nyingi za kijamii ambazo umekuwa ukizituma kutoka huko, tuko pamoja na FULLSHANGWE inakuangalia kwa macho mawili Mungu akubariki sana na uwe na afya njema ili tuendeleze kazi

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AMJULIA HALI PADRI AMBROSE MKENDA ALIYELAZWA MUHIMBILI

$
0
0
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsalimia Padri Ambrose Mkenda, wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mpendae Zanzibar, leo Desemba 30, 2012 aliyelazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) kutokana na majeraha aliyoyapata kwa kujeruhiwa na risasi na watu wasiojulikana wakati akiwa getini akisubiri kuingia nyumbani kwake mjini Zanzibar hivi karibuni. Kulia ni Muuguzi mwangalizi wa mgonjwa huyo, Namsifu Fue.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Padri Ambrose Mkenda, wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mpendae Zanzibar, leo Desemba 30, 2012 aliyelazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) kutokana na majeraha aliyoyapata kwa kujeruhiwa na risasi na watu wasiojulikana wakati akiwa getini akisubiri kuingia nyumbani kwake mjini Zanzibar hivi karibuni. Kulia ni Muuguzi mwangalizi wa mgonjwa huyo, Namsifu Fue. Picha na OMR

RAIS KIKWETE AONGOZA MAZISHI YA MZEE MOHAMED ABOUD MOHAMED

$
0
0

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib  Bilali, Makamu wa Pili wa Rais Wa Znzibar Balozi Seif Iddi, Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika mazishi ya Marehemu Mohamed Aboud Mohamed, aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mstaafu, katika Makaburi ya Ngazija jijini Dar es salam leo Desemba 29, 2012.
ab2. Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akiweka mchanga kaburini wakati wa mazishi ya Marehemu Mohamed Aboud Mohamed, aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mstaafu, katika Makaburi ya Ngazija jijini Dar es salam leo Desemba 29, 2012.

PICHA NA IKULU

msanii wa bongofleva dayna nyage awashukuru wadau na vyiombo vya habari

$
0
0
Mambo vp ndugu zangu. Napenda kuchukua nafasi hii kuwatakia maandalizi mema ya mwaka mpya. Mungu atupe nguvu na neema zaidi ktk mwaka 2013.  

Mwaka 2012 tutaukumbuka kwa mengi yapo mema na mabaya. Naomba nikuombe radh wewe kwa lolote ambalo niliwah kukukosea, nawe kama ulinikosea sina tatizo nawe tangu sasa. pia naomba nitoe shukrani zangu kwa wote waliohusika ktk mafanikio yangu ya kimuziki.  

Naamini wengi mlikuwa mstari wa mbele ktk kunishauri, kunipongeza nahata kunikosoa nilipokosea. Shukrani nying zwafikie radio presenter, dj's,  radio na tv zote tz na  Afrika naamini bla nyinyi kuzicheza nymbo zang Basi nisingefika hapa. Waandaz wa magaazeti mlikuwa mstari wa mbele ktk kuona nafika mbali kwa kuandika habari zangu na kufika hata vjijini. Nachukua fursa kuwashukuru pia. 

Blogs mbalimbali. Mlikuwa mstari wa mbele kwakuandka habari na kupost hata baadh ya show zangu ambazo mmenipa heshma ya kufika mbali zaid na kusikika hata nje ya nch mchango wenu ni mkubwa  japo siwez kuwataja wote. Pia Requester wa media cna cha kuwalipa nawashkuru sana sana na ntabaki kuwaheshmu kwani mmetoa mchango mkubwa sana kwa kuomba nymbo zangu media na zikachezwa Na amini ni mchango mkubwa sana ktk game hasa kwetu wasanii Ntabaki kuwaheshimu na kuwathamini siku zote. Bila kuwasahau wasanii wenzangu walikuwa nami bega kwa bega ktk  kunishauli na kunisaidia kwa chochote.Pia ma dj wa club mbalimbali, mmekuwa chachu ya mzk wangu pale mlipoonesha ushirikiann wenu kwangu. 

Pia Waandaaji wa (show) matamasha  madogo na makubwa nawashukuru sana sana kwa kuniamini na kukubali kufanya kazi na mm Siwasahau maproducers wa video na  Audio  na studio mbalimbali kwa kunifanyia kaz za uhakika na jamii ikanikubali kwa kazi hzo. Wote kwa pamoja naamini sasa ni kama ndugu. Nawaomba muonyeshe tena moyo huwo na mwaka ujao na mingine kwani kaz nzur ni yenye kushirikiana. Msisite kama ntawakosea naomba msisite kunikanya na kunisamehe. Napenda wote na kuwajali. Nawatakia  mwaka mpya.

 Ts me.               Dayna Nyange (mkali wao)

taarifa kwa umma:USITISHAJI WA MATANGAZO YA ANALOJIA NA KWENDA KATIKA MFUMO WA DIJITALI

$
0
0

TAARIFA YA MHE. JANUARY Y. MAKAMBA (MB), NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA KUHUSU USITISHAJI WA MATANGAZO YA ANALOJIA NA KWENDA KATIKA MFUMO WA DIJITALI

Ndugu Wananchi,

Mtakumbuka kuwa hapo tarehe 23 Februari 2012 tuliwatangazia kupitia vyombo vya habari juu ya usitishwaji wa matangazo ya televisheni kwa kutumia teknolojia ya analojia kwenda katika mfumo mpya unaotumia teknolojia ya dijitali.

Napenda kuwaleleza kuwa, maandalizi ya kuzima mitambo ya analojia kuanzia tarehe 31 Desemba 2012 yamekamilika kwa mujibu wa makubaliano ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Hata hivyo, napenda sasa kutoa taarifa kuwa uzimaji wa mitambo ya analojia utafanyika kwa awamu kama ifuatavyo:-

(1) Dar Es Salaam-31 Desemba, 2012;
(2) Dodoma & Tanga- 31 Januari, 2013;
(3) Mwanza-28 Februari, 2013;
(4) Moshi & Arusha-31 Machi, 2013;
(5) Mbeya-30 Aprili, 2013.

Tumeamua kuanza kuzima mitambo hiyo kwa Jiji la Dar es Salaam kwanza ili kutoa fursa kwa makampuni yenye leseni kusimika mitambo ya utangazaji wa dijitali katika mikoa mingine. Makampuni haya yamejipanga kukamilisha usimikaji wa mitambo hiyo katika mikoa minane katika miezi minane ijayo.

Mitambo ya analojia itakayozimwa kesho ni ile iliyopo Kisarawe na Makongo. Vituo ambavyo siku ya tarehe 1 Januari 2013, vitapaswa kuanza kutangaza matangazo kwa mfumo wa dijitali ni TBC1, ITV, EATV, Channel 10, StarTV, DTV, CapitalTV, TumainiTV, ATN, MlimaniTV, C2C, CTN, CloudsTV na Efatha.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inafanya jitihada za kutosha kuhakikisha kwamba makampuni yenye leseni za kusambaza ving’amuzi yanakuwa na ving’amuzi vya kutosha na vingine vimeagizwa ili kukidhi mahitaji ya baadaye na vile vilivyopo sokoni vina ubora unaokubalika.

Vilevile, Serikali kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania itahakikisha kwamba zoezi la uhamaji linafanyika bila usumbufu na kero kwa wananchi. Makampuni yanayouza ving’amuzi yameagizwa yaimarishe huduma kwa wateja wakati wa kuuza ving’amuzi na hata baada ya ununuzi iwapo wananchi watakuwa na matatizo na ving’amuzi.

Zoezi hili la uhamaji ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi yetu. Tutakapokuwa tumekamilisha uhamaji, huduma za mawasiliano na utangazaji zitapanuka na kuwa bora zaidi. Kwa mfano, itawezekana sasa kuangalia televisheni kupitia simu zetu za mikononi. Vilevile, itawezekana, kwa bei nafuu kabisa, kwa mtu mwenye uwezo wa kutengeneza vipindi kukodisha chaneli yake na kutangaza vipindi vyake. Vilevile, bei za mawasiliano na utangazaji zitashuka, na tutakuwa tumepiga hatua kubwa kwenye mapinduzi ya teknolojia duniani, ambayo nchi yetu haiwezi kubaki nyuma.

Ndugu Wananchi,

Serikali kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania itaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu uhamaji huu. Serikali inatarajia kupata ushirikiano wa karibu kutoka kwa wadau wa sekta ya utangazaji na wananchi kwa ujumla katika kipindi cha uzimaji wa mitambo ya utangazaji wa televisheni ili kufanikisha zoezi la uzimaji wa mitambo ya utangazaji ya teknolojia ya analojia.

Uhamaji huu hautahusu televisheni za wananchi zinazopata matangazo kupitia madishi (nyungo) (satellite) au nyaya (cables). Hivyo, wananchi wanaopata matangazo kupitia DStv, Zuku, na nyinginezo wataendelea kupata matangazo yao kama kawaida.

Ndugu Wananchi

Kama kuna mwananchi yoyote ana kero, malalamiko, swali au anahitaji maelekezo kuhusu uhamaji, awasiliane na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kupitia namba 0784-558270; 0784558271 au barua pepe: malalamiko@tcra.go.tz

Ndugu Wananchi,

Nawashukuru kwa kunisikiliza

RAIS WA MAKAPERA TANZANIA ISSA KWISSA MWAIFUGE AJIUZULU UKAPERA AWAGEUKA WENZAKE GHAFLA AOA RASMI LEO

$
0
0
 Rais wa Makapera Tanzania, Issa Kwisa Mwaifuge, leo ameamua kuwageuka wafuasi wake rasmi na kuvunja katiba ya kundi lake na kuamua kuuaga ukapera rasmi na kumuoa Binti mrembo aliyewahi kushiriki shindano kubwa la Miss Tanzania, 2004, Verdiana Kamugisha, ambao kwa pamoja wameamua kumeremeta siku ya leo na kufunga ndoa yao katika Kanisa la Lutheran lililopo mitaa ya Sinza jijini Dar es Salaam. Na hapa ni wakati wakiwa katika sherehe ya ndoa yao inayoendelea muda huu katika Ukumbi wa Msasani Makuni. Picha Zote na www.sufianimafoto.blogspot.com
 Bwana Harusi, Issa Kwisa (kushoto) akisebeneka na Suleiman Semunyu, aliyekuwa akipokea zawadi ya keki kwa niaba ya ITV.
 Maharusi, wakipozi kwa picha na wafanyakazi wa Star Tv, baada ya kuwakabidhi zawadi ya keki.
 Hapa ilikuwa ni muda wa Kwaito..........
 Sehemu ya wageni waalikwa.....
 Wadau kutoka (kulia) ni James Range, Joseph Mpangala na Martine Mauya, wakipozi kwa picha mbele ya kamera ya Sufiaimafoto.
 Baadhi ya wafanyakazi wa ITV ambao ni wafanyakazi wenzake na Bwana Harusi, wakipozi kwa picha, baada ya kukabidhiwa zawadi ya keki na Bwana harusi.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Chanel Ten, wakipozi kwa picha ya pamoja baada ya kupokea zawadi ya Keki.
 Sehemu ya wageni waalikwa,..
Salum Mkambala, akisebeneka kwa staili yake wakati akielekea kupokea zawadi ya keki kwa niaba ya wafanyakazi wenzake wa Chanel Ten.

kampuni ya MSAMA promotions yaTOA MISAADA KWA WATOTO YATIMA

$
0
0

  Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama akimkabidhi sehemu ya msaada wa vyakula Mkurugenzi wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Mwandaliwa, Halima Ramadhani. Mbali ya kukabidhi vyakula hivyo, Msama pia alikabidhi hundi ya sh milioni 1.5 kwa ajili ya kulipia ada za wanafunzi waliofukuzwa shule. Msaada huo  umetokana na mapato ya tamasha la Pasaka, hafla hiyo ilifanyika Mbweni nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama akikabidhi sehemu ya msaada wa vyakula 
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama akikabidhi sehemu ya msaada wa vyakula 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama akikabidhi sehemu ya msaada wa vyakula .
 Baadhi ya watoto wakishusha vyakula viliyotolewa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama
 Baadhi ya watoto wakishusha vyakula viliyotolewa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama
 Baadhi ya watoto wakishusha vyakula viliyotolewa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama
 Baadhi ya watoto wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Mwandaliwa wakiwa katika picha ya pamoja.
Baadhi ya watoto wakishusha vyakula viliyotolewa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama
 Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama akimkabidhi hundi ya sh. milioni 1.5 Mkurugenzi wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Mwandaliwa, Halima Ramadhani kwa ajili ya kulipia ada za wanafunzi waliofukuzwa shule. Mbali ya kukabidhi hundi, Msama alikabidhi msaada wa vyakula mbalimbali vikiwa na thamani ya sh milioni 3 zilizotokana na mapato ya tamasha la Pasaka, hafla hiyo ilifanyika Mbweni nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
 Mkurugenzi wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Mwandaliwa, Halima Ramadhani akimuonesha moja ya vyumba vinavyotumiwa na watoto hao.


Mkurugenzi wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Mwandaliwa, Halima Ramadhani  akizungumza waandishi wa habari kuhusu historia ya kituo chake baada ya kupokea misaada ya vyakula kutoka kwa kampuni ya Msama Promotion ambapo mkurugenzi wake Alex Msama amekabidhi misaada hiyo leo.
 Alex Msama akipata maelezo katika chumba maalum kwa ajili ya watoto kujifunza kushona. 
Dua ya kumshukuru mungu ikisomwa.
Viewing all 46379 articles
Browse latest View live




Latest Images