Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live

PRESIDENT KIKWETE AWARDED HONORARY PROFESSORSHIP BY CHINA AGRICULTURAL UNIVERSITY

0
0
President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete being awarded Honorary Professorship at the China Agricultural University in Beijing this evening. On the left is Chair of the University Council Jiang Peimin and on the right is the University’s President Professor KE Bingsheng.
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete delivers his speech shortly after he was awarded Honorary Professorship at the China Agricultural University in Beijing this evening. President Kikwete is in China for a working visit at the invitation of the China President Xi Jinping(photos by Freddy Maro).
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete tour the greenhouse shortly after he arrived at China Agricultural University this afternoon. President Kikwete later addressed the University students and lecturers on the agricultural development in Tanzania before being conferred Honorary Professorship.


TAZAMA MSANII TI ALIVYOKAMUA NA KUWAKUNA VILIVYO MASHABIKI WAKE KATIKA TAMASHA LA FIESTA 2014

0
0

Wajumbe wa idara ya utumishi wa walimu watembelea nyumba za PSPF zilizopo eneo la Lukobe mjini Morogoro.

0
0
 Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Neema Muro, (Kushoto), akizungumza na baadhi ya wajumbe wa idara ya utumishi wa walimu, kwenye eneo la mradi wa nyumba za Mfuko huo eneo la Lukobe mjini Morogoro mwishoni mwa wiki. Wajumbe hao walifanya ziara hiyo mara baada yab kuhudhuria semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo kwa lengo la kuwaelimisha juu ya faida mwanachama anazoweza kupata anapojiunga na Mfuko huo.
 Mkurugenzi wa uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Neema Muro, (Kushoto), akiwapa maelezo, baadhi ya wajumbe wa tume ya utumishi wa walimu, kuhusu mradi wa nyumba za Mfuko huo, zilizoko eneo la Lukobe mjini Morogoro, mwishoni mwa wiki.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi, (Mwenye T-Shirt), akiwapa maelezo wajumbe wa idara ya utumishi wa walimu, kuhusu nyumba za Mfuko huo zilizoko eneo la Lukobe mjini Morogoro, mwishoni mwa wiki mara baada ya kuhudhuria semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo mjini humo.

Article 10

0
0

WIZARA YA MALIASILI YABARIKI KUANZISHWA KWA MFUKO WA KULINDA MLIMA KILIMANJARO NA MLIMA MERU.

0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu akizungumza wakati wa kikao kilicho shirikisha Kamati ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Mazingira,Wabunge katika majimbo ya mikoa ya Arusha na Kilimanjaro,Wakuu wa wilaya zinazopakana na mlima Kilimanjaro na mlima Meru,TANAPA na Idara ya Misitu,(kulia)ni kaimu mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Ibrahim Msengi.
Naibu waziri wa TAMISEMI ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Siha ,akichangia wakati wa kikao cha kuanzishwa kwa mchakato wa uanzishwaji mfumo wa kiikolojia wa mlima Kilimanjaro na Mlima Meru ambao utalinda milima yote miwili.
Makamau mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Mazingira,Abdulkarim Shah akizungumza katika kikao hicho kimetokana na wabunge wa mkoa wa Kilimanjaro kuomba kuanzishwa kwa mfuko wa kulinda mlima Kilimanjaro.
Baadhi ya washiriki wa kikao hicho kilichofanyika katika Hotel ya Sal salnero wakifuatilia michango mbalimbali iliyokuwa ikitolewa katika kikao hicho.
Mbunge wa Jimbo la Vunjo ,Agustino Mrema akichangia hoja katika kikao hicho.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassar akichangia katika uanzishwaji wa mfuko huo.
Katibu wa Mbunge wa Moshi mjini,Basil Lema akichangia jambo katika kikao hicho akiwa amemwakilisha Mbunge Philemoni Ndesamburo.
Baadhi ya washiriki katika kikao hicho.
Kaimu mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Moshi Ibrahimu Msengi akichangia katika uanzishwaji wa mfuko wa kulinda mlima Kilimanjaro na mlima Meru.
Mkuu wa wilaya ya Rombo Elinasi Palangyo akizungumza katika kikao hicho,wilaya ya Rombo ni moja ya wilaya ambazo zinapakana na mlima Kilimanjaro.
Mkuu wa wilaya ya Siha Dk ,Charles Mlingwa akizungumza katika kikao hicho,wilaya ya Siha ni moja ya wilaya ambazo zinapakana na mlima Kilimanjaro.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga akizungumza katika kikao hicho,wilaya ya Hai ni moja ya wilaya ambazo zinapakana na mlima Kilimanjaro.
Mbunge wa Arumeru Mashariki ,Joshua Nassar,akiwa pamoja na Mbunge Suzan Kiwanga na katibu wa Mbunge wa jimbo la Moshi mjini ,Basil Lema.
Mkurugenzi wa Wakala wa Misitu (TFS) Juma Mgoo akieleza namna ambavyo mfuko huo utasaidia katika kuimarisha ulinzi wa rasilimali ya misitu.
Mhifadhi mkuu wa hifadhi ya Arusha(ANAPA) Betrita Loibook akichangia katika kikao hicho.
Mhifadhi ,idara ya ujirani mwema ,Theodora Batiho akichangia jambo katika kikao hicho.
Washiriki wa kikao hicho wakifuatilia majadiliano.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu akihitimisha kikao cha majadiliano juu ya kuanzishwa kwa mfuko wa kulinda mlima Kilimanjaro na Mlima Meru.Na Dixon Busagaga wa Globu ya jamii kanda ya kaskazini.

MOI yajiimarisha katika utoaji huduma muhimu za Tiba na Upasuaji

0
0
 Afisa Uhusiano wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Bw. Patrick Mvungi akieleza kwa vyombo vya habari(hawapo pichani) kuhusu mafanikio ya Taasisi hiyo ikiwemo kufanikiwa kwa zaidi ya asilimia 95 ya kutoa huduma muhimu za Tiba na Upasuaji kwa wagonjwa wanaopokelewa na hivyo kupunguza vifo na rufaa za kuwapeleka wagonjwa nje ya nchi,wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar ea Salaam. Kushoto ni Meneja Ustawi wa Jamii na Uhusiano wa Taasisi hiyo Bw. Almas Jumaa.
Meneja Ustawi wa Jamii na Uhusiano wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Bw. Almas Jumaa akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi Taasisi hiyo ilivyoendelea kuwa nguzo Muhimu katika kuokoa maisha ya watanzania ambapo upasuaji wa kitaalam wa mgongo umeendelea kufanyika na kufanikiwa kwa zaidi ya asilimia 99 na kusaidia kuwaondoa wagonjwa wenye tatizo hilo katika hatari ya kupotea uhai.Kulia ni Afisa Uhusiano wa Taasisi hiyo Bw. Patrick Mvungi.PICHA NA MAELEZO.
=======  ========  =======

Na Hassan Silayo-MAELEZO

Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) imeendelea kuwa nguzo muhimu nchini katika utoaji wa huduma za tiba na upasuaji. Hayo yamesemwa na Afisa Uhusiano wa Taasisi hiyo Bw. Patrick Mvungi wakati wa Mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.

Patrick amesema kuwa MOI imesaidia kuokoa zaidi ya asilimia 95 ya watanzania ambao kwa namna moja au nyingine wangeweza kupoteza maisha yao au kupata  ulemavu wa kudumu kutokana na ajali.

“MOI kwa kiasi kikubwa imefanikiwa kuokoa maisha ya watanzania kwa zaidi ya asilimia 95 kutokana na kutoa huduma muhimu ya za tiba na upasuaji wa wagonjwa wanaopokelewa na hivyo kupunguza vifo na rufaa za kuwapeleka wagonjwa nje ya nchi” alisema Mvungi.

Akizungumzia kuhusu upasuaji wa kitaalam wa mgongo (specialized Spine Surgeries) Mvungi alisema kuwa Taasisi hiyo imeendelea kufanya na zaidi ya asilimia 99 ya wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wamepona na kurudi katika hali zao za kawaida. Naye Meneja Ustawi wa Jamii na Uhusiano wa Taasisi Taasisi hiyo Bw. Almas Jumaa alisema kuwa zaidi ya wagonjwa 1,256 ya wagonjwa wa upasuaji mkubwa wa nyonga walipasuliwa salama na zaidi ya asilimia 95 ya wagonjwa hao wamepona kabisa.

Pia Almas alisema kuwa pia Taasisi imeendelea kutoa matibabu ya magonjwa ya ubongo yaliyokuwa yanahitaji upasuaji yamefanikiwa kufanyika kwa zaidi ya asilimia 80 na wagonjwa waliokuwa na matatizo hayo wamepona na kuondolewa kwenye hatari ya kupoteza uhai.

Taasisi ya MOI imewataka watanzania kuitumia Taasisi hiyo na kuacha kufuata matibabu nje ya nchi kwa gharama kubwa tofauti na kama wangepata huduma hizo hapa nchini kwa gharama nafuu.
 

Article 7

0
0

Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kuanza.

0
0
 Makamu Mwenyekiti wa  Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), pia  na Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Hamid   Mahamoud Hamid(kushoto) akisoma taarifa kuhusu kuanza kwa shughuli za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dares Salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa NEC.Kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi Julias Malaba.
Baadhi  ya Watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na waandishi  wa habari kuhusu  taarifa kuhusu kuanza kwa shughuli za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dares Salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa NEC.Kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi Julias Malaba.
 Makamu Mwenyekiti wa  Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), pia  na Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Hamid   Mahamoud Hamid(kushoto)  akitoa ufafanuzi baada kusoma taarifa kuhusu kuanza kwa shughuli za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dares Salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa NEC.Kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi Julias Malaba.
 Makamu Mwenyekiti wa  Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), pia  na Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Hamid   Mahamoud Hamid(kushoto)  akijadiliana  jambo na Mkurugenzi wa Uchaguzi,  Julias Malaba (kulia) baada kusoma taarifa kuhusu kuanza kwa shughuli za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dares Salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa NEC.
Baadhi ya Watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) wakifuatilia mkutano huo.picha zote na Magreth Kinabo- Maelezo.

RAIS KIKWETE AKUTANA NA UONGOZI WA MAKAMPUNI YA CHINA YANAYOTAKA KUWEKEZA KATIKA UJENZI WA RELI NCHINI TANZANIA

0
0
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiangalia ramani ya Tanzania inayoonyesha mchoro wa reli ya Kati inayotarajiwa kujengwa upya na kwa viwango vya kisasa wakati alipokutana na uongozi wa juu wa makampuni ya China yakiongozwa na China Railway Group Ltd. Makampuni mengine ni SINOSURE, Exim Bank, China Development Bank na China Agriculture Development Bank. Rais Dkt. Kikwete yuko nchini China kwa ziara rasmi ya kikazi (State Visit).
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akifanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya China Railway Group Limited Bwana Li Changjin na msafara wake kuhusu mpango wa serikali ya Tanzania wa kujenga reli mpya na ya viwango vya kisasa kutoka Dar Es Salaam hadi Kigoma, Tabora kwenda Mwanza, Kaliua kwenda Mpanda hadi Ziwa Tanganyika. Mazungumzo hayo yalifanyika huko Beijing tarehe 24.10.2014.PICHA NA JOHN LUKUWI.

Ukarabati na Upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda wakamilika

0
0
 Meneja wa Uwanja wa ndege wa Mpanda,  Mkoa wa Katavi Seneti Lyatuu akiwaonesha timu ya ukaguzi wa miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mpanda. Nyuma yake (mwenye suti nyeusi) ni Mhandisi Caroline Mntambo kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndenge Tanzania, Makao Makuu, Dar es Salaam.
  Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda  Bw.  Seneti Lyatuu akifafanua jambo wakati timu ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipotembelea kiwanja hicho.
  Timu ya ukaguzi ikitazama barabara ya kutua na kurukia ndege katika uwanja wa ndege wa Mpanda
 Barabara ya kutua na kurukia ndege katika uwanja wa ndege wa Mpanda, mkoani Katavi
Mhandisi Caroline Mntambo (mwenye suti nyeusi) akifafanua jambo kwa timu ya wakaguzi kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Uwanja wa ndege wa Mpanda umekarabatiwa na kupanuliwa hivyo , kuwa  katika hali nzuri kwa matumizi ya ndege zote za binafsi na biashara.PICHA NA JOYCE MKINGA.
 
Na Mwandishi wetu, Mpanda.
Serikali imekamilisha ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mpanda, mkoa wa Katavi na hivyo kuufanya uwe wa kiwango kizuri tayari kwa kutumika kwa ndege za binafsi na biashara. Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda, Bw Seneti Lyatuu alisema uwanja huo umeboreshwa na hivyo, unaweza kutumika kutua na kuruka ndege za kiwango cha kati na hata zile ndege kubwa zinaweza kutua kwa dharura.

Aliiambia timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango iliyotembelea uwanja huo mwishoni mwa wiki kuwa uwanja huo umeongeza idadi ya wasafiri mara dufu kutokana na ukarabati na upanuzi uliofanyika. Meneja wa Uwanja huo alisema idadi ya abiria imeongezeka kutoka abiria 285 mwaka 2009 hadi 2,390 mwaka 2013/14. Bw. Lyatuu alisema kuwa uwanja huo umekarabatiwa na barabara ya kuruka na kutua ndege imerefushwa kwa kiwango cha lami kutoka urefu wa mita 1,500 na upana wa mita 30 hadi kufikia urefu wa mita 1,820 na upana wa mita 30.

Alisema maeneo mengine yaliyokarabatiwa ni pamoja na kujenga uzio na mifereji ya kupitishia maji ya mvua.“Kwa sasa kiwanja kipo vizuri na ndege za aina zote zinaweza kutua hapa uwanjani hivyo, tunawakaribishwa wadau wote kuutumia uwanja huu” alisema Bw Lyatuu. Eng. Caroline Mntambo kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Makao Makuu Dar es Salaam alisema kuwa tayari wamealika mashirika ya ndege yanayofanya biashara hapa nchini kuanzisha safari katika uwanja huo. Mashirika hayo ni pamoja na ATC, Precision Air, Fast jet   nk.

Eng Mntambo alisema kwa sasa shirika la ndege la Auric Air tayari limeanzisha safari za kwenda Mpanda ambapo linasafirisha abiria kutoka Dar- Mpanda – Mwanza mara tatu kwa wiki.Alisema ndege zingine zinazotua uwanjani hapo kwa sasa ni pamoja na za UNHCR, ndege za kukodi na ndege za serikali.

SERIKALI YAWEKA TARATIBU ZA KUZINGATIA ILI KUHAKIKISHA KUNAKUWA NA WAMILIKI HALALI WA LAINI ZA SIMU.

0
0
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO.
 
Mwanadamu ameumbwa na kuzaliwa akiwa na asili ya kuwa na uwezo na upeo unaomuwezesha kuwasiliana baina ya mtu na mtu kunzia ngazi ya familia, jamii inayomzunguka, taifa na hatimaye ulimwengu mzima.

Akiwa na mamlaka ya kutumia mawasiliano katika maisha yake ya kila siku, mwanadamu anayatumia mawasiliano hayo kama mchakato wa kuhamisha na kupashana taarifa ama habari kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa nyakati tofauti tofauti.

Mchakato huo wa mawasiliano unaweza kuwa ni mwingiliano unaohusisha ishara kati ya angalau wakala wawili walio na mkusanyiko wa ishara na sheria za elimu ishara.Kwa mantiki hiyo, mwanadamu anatumia mawasiliano kwa kupasha au kubadilishana mawazo, maoni, au habari kwa kunena, maandishi, au ishara.

Historia inasema, mawasiliano yamekuwepo tangu kuwepo mwanadamu hatua inayoleta mantiki kuwa mawasiliano yamekuwa kongwe kama jamii ilivyo kwani yamekuwepo tokea enzi za mababu.Mwanadamu anatumia mawasiliano katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku kulingana na wakati husika.
 
Ndani ya mchakato wa kuhabarisha, habari husika hupakiwa, kutumwa na kupashwa na anayetuma kwa anayepokea kupitia kwa njia maalum kulingana na mahali na wakati husika.

Mawasiliano yakishatumwa, anayepokea hupakua ujumbe ule na kumpatia aliyetuma jibu ama majibu ya alichotaka kujulishwa ambapo mawasiliano yanahitaji anyetuma ujumbe na anayepokea wapate mrejesho unaoonesha kumekuwa na mawasiliano sahihi kulingana na mtoa ujumbe.

Ili kuwa na mawasiliano yenye tija katika jamii, njia zinazohusika na kusikia, kama vile unenaji, wimbo, na toni ya sauti, na zile zisizohusisha kusikia, kama vile miondoko ya mwili, lugha ishara, kugusa, kuwasiliana kwa macho, na kuandika.

Njia hizi husaidia jamii kupata ujumbe kwa kutumia ishara husika ambazo zinatarajiwa kuwa ni za kiungwana na zinazojali maadili ya kijamii na hivyo kuwa na taifa linalojitofautisha na mataifa mengine.

Mawasilano haya yanaweza kufikishwa kwa kutumia njia ya mdomo ama mazungumzo ya ana kwa ana, njia ya simu, radio, televisheni, intaneti na mitandao ya kijamii ambayo imekuwa ni njia ya haraka ya kupashana habari mbalimbali miongoni mwa jamii.

Kwa kwa suala la mawasiliano lilivyo nyeti kwa taifa, Serikali imetambua umuhimu huo na kutoa tahadhari kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano, wananchi na umma kwa ujumla kwa kuwatahadhari watumiaji hao wa huduma hiyo nchini.

Matumizi mabaya ya mawasiliano na udanganyifu katika usajili wa namba za simu za mkononi imeonekana kuwa ni tatizo nchini ambapo hivi karibuni Serikali iliwatahadharisha wananchi kuhusu suala hilo na kuonya kuwa kutumia simu isiyosajiliwa ama kusajiliwa kwa kutumia taarifa za udanganyifu ni kosa la jinai.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Meneja mawasiliano wa  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)  Innocent Mungy alisema  kuwa kumekuwepo na watu wachache miongoni mwa jamii wanaotumia mawasiliano pasipo kuzingatia sheria na kanuni zilizowekwa nchini.

Ikizingatiwa TCRA ni chombo cha Serikali kilichopewa jukumu la kusimamia masuala ya mawasiiliano nchini, Mamlaka hiyo ilianzishwa kwa sheria. 12 ya mwaka 2003 kusimamia Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta nchini.

Ili kuendana na wakati, mwaka 2010, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha Sheria la Mawasiliano ya Elektroniki na Posta (EPOCA) kusimamia, pamoja na mambo mengine, uuzaji, usajili na matumizi ya laini za simu za mkononi nchini.

Kwa kuwa TCRA jukumu lake ni kusimamia mwasiliano nchini, imekuwa mstari wa mbele mara zote kuwatahadharisha na kuwakumbusha wananchi kwa ujumla waitambue sheria hiyo ambayo imeainisha makosa yanayotokana na kukiuka vipengele vya sheria ya mawasiliano.

Miongoni mwa makosa hayo ni pamoja na kuuza au kusambaza laini ya simu bila kibali cha mtoa huduma za simu na kuwa na leseni kutoka TCRA na kutumia laini ya simu ambayo haikusajiliwa.

Makosa mengine ni kutoandikisha taarifa sahihi za laini husika kabla ya kuitoa au kuiuza, kutoa taarifa ya uwongo au maelezo yasiyo sahihi wakati wa kusajili laini ya simu na kuchakachua simu ya mkononi au laini ya simu.

Mnamo Mei 30, 2013 Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Prof. John Nkoma kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari aliwataka watumiaji wa simu za mkononi na wananchi kwa ujumla wa waunge mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ili kufanikisha usajili wa namba za simu kwa ajili ya kudumisha na kuendeleza amani na usalama na kuharakisha maendeleo ya sekta ya mawasiliano na ya Taifa kwa ujumla.

Zoezi la kusajili laini za simu, lilikuwa na nia jema ambalo lilimtaka mteja mtarajiwa  kusajili laini ya simu kwa kutoa taarifa sahihikwa  kuonesha mojawapo ya vitambulisho halisi vyenye picha yake ikiwemo hati ya kusafiria (Passport), kitambulisho cha kazi, leseni ya udereva, kadi ya usajili wa mpiga kura, barua ya utambulisho kutoka Serikali za Mitaa ikiwa na picha, kitambulisho cha Taifa, kitambulisho cha SACCOs au kadi ya benki yenye picha ya mhusika halisi anayetaka kusajili laini ya simu.

Haya yote Serikali imeyaweka ili kuzingatia na kuhakikisha kunakuwa na wamiliki halali wa laini za simu ili kurahisisha mawasiliano miongoni mwa jamii.

Kwa kuwa binadamu ni mrahisi kuelewa na ni rahisi pia kusahau, Serikali imweweka sheria ambayo iawakumbusha watumiaji wote wa mawasiliano kuwa  yeyote atayekiuka Sheria hiyo ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010, kifungu cha 131, sheria hiyo imeainisha kuwa ni kosa la jinai kutumia au kuwezesha kutumika namba ya simu isiyosajiliwa kihalali.

Kutokana na kosa hilo, atakayebainika anatumia laini ambayo haijasajiliwa atakumbana na adhabu ya faini ya shilingi 500,000 au kifungo cha miezi mitatu ambayo itatolewa kwa yeyote atakayekiuka sheria hiyo.

Tahadhari zote hiyo inalenga na kuwashauri watumiaji wa simu za mkononi na wananchi kwa ujumla wawe tayari kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ili kufanikisha usajili wa namba za simu kwa ajili ya kudumisha na kuendeleza amani na usalama na kuharakisha maendeleo ya sekta ya mawasiliano na ya Taifa kwa ujumla.

Ni jukumu la letu sote kama wananchi kuzingatia matumizi sahihi ya mawasiliano kwa maslahi mapana yenye tija kwa umma na Taifa.

Aidha, Katika vikao vya pamoja na wadau wa mawasiliano nchini vilivyofanyika  Aprili 04 na Aprili 11, 2013, Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania na makampuni yanayotoa huduma za simu za mkononi walikubaliana juu ya hatua za kumaliza kabisa tatizo la usajili wa namba za simu na utaratibu wa kufungia namba zote za simu ambazo hazikusajiliwa.
 
Vikao hivyo vyote viliwahusisha  TCRA kwa upande wa Serikali, Watendaji Wakuu na wawakilishi wa mitandao ya Airtel, BOL, MIC (TIGO), Sasatel, TTCL, Vodacom na Zantel nchini.
 
Kwa mujibu wa kifungu cha 130 cha sheria ya Mawasiliano ya Elektroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010, sheria haijambana mtumiaji wa huduma tu, kwa upande mwingine imewataka wauzaji au wanaotoa kwa namna yoyote ile namba za simu bila kuzisajili ambapo akibainika atakuwa ametenda kosa la jinai.

Sheria imeainisha kuwa adhabu ya kutenda kosa hilo ni kulipa faini ya shilingi 3,000,000 au kifungo cha miezi 12 au adhabu zote zinaweza kutekelezwa kwa pamoja.
Ili kuhakikisha mawasiliano nchini yamekuwa yenye tija na yamekuwa kichocheo cha maendeleo, Serikali iliona kuna haja na sababu za msingi za kuanzisha utaratibu wa kusajili namba za simu na kupata taarifa sahihi za watumiaji wake.
Lengo mahususi likiwa kuwalinda watumiaji na jamii kutokana na matumizi mabaya ya huduma za mawasiliano, kuimarisha usalama wa taifa pamoja na kuwawezesha watoa huduma za mawasiliano kuwafahamu vizuri wateja wao na kuwahudumia ipasavyo kadiri ya mahitaji yao.

Zaidi ya hapo, Serikali pamoja na makampuni yanayotoa huduma ya mawasiliano waliona ni vema kuwezesha kuwatambua watumiaji wa huduma za ziada za simu, kama huduma za kibenki, kutuma na kupokea fedha, kufanya malipo mbalimbali kwa kutumia simu kwa mfano kulipia huduma za maji, umeme na vipindi vya televisheni vya kulipia.

Licha ya mawasiliano kuwa na mabadiliko kadiri ambavyo wakati umepita, teknolojia imeendelea kukua na kuibua aina mpya na mawazo kuhusu mawasiliano.

Maendeleo haya ya kiteknolojia yalibadilisha jinsi mawasiliano yanavyofanyika ambapo watafiti wamegawanya mawasiliano jinsi yalivyobadilika katika hatua tatu.

Mabadiliko ya mwanzo katika Mawasiliano yalibainisha kuwa maandishi na michoro ndiyo yalianza kutumika kuwasiliana.

Maandishi hayo yaliandikwa kwenye mawe, ambayo yalikuwa mazito mno kuhamishwa. Wakati huo, mawasiliano katika maandishi hayangeweza kubebwa, ingawa yalikuwepo.

Mabadiliko ya pili katika Mawasilianoyalihusisha maandishi ambayo yalianza kutumiwa kwenye karatasi, mavunjo, udongo na nta.

Herufi za alfabeti zilibuniwa, hivyo kuruhusu mfanano wa lugha katika maeneo makubwa, ilikuwa ni hatua kubwa baada ya muda, Mjerumani Johannes Gutenberg aliyeishi kati ya miaka ya 1398-1468, mwaka 1439 alikuwa mtu wa kwanza duniani kutumia mashine ya kuchapisha magazeti chini ya shirika aliloliita Gutenberg lililojihusisha na uchapishaji ili kurahisisha mawasiliano.

Ili kuhabarisha watu, shirika la Gutenberg lilitayarisha kitabu cha kwanza cha kuchapishwa kwa kutumia mashine yake ambapo maandiko haya yaliweza kusafirishwa kwa watu wengine duniani ili wayaone ambayo sasa mawasiliano hayo ya maandishi yanaweza kuhifadhiwa na kubebwa ikiwemo magazeti na vitabu.

Mabadiliko ya tatu ya Mawasiliano yalihusisha taarifa ambayo inaweza kuhamishwa kupitia mawimbi na ishara za kielektroniki ambayo duniani ndio hatua ya juu iliyopo ambapo mwanadamu anajivuni mabadiliko ya sayansi na teknolojia.

Kwa kuwa Tanzania ni miongoni mwa mataifa ya dunia ya leo imefikia kiwango cha watu wake kuweza kupata taarifa na kuhamishwa kupitia mawimbi, na ishara za kielektroniki zilizofikiwa kisayansi duniani, Serikali imeona ni vema iendelee kutoa tahadhari kwa watu wake ili wawe salama wakati wote.

Yanapotokea mafanikio katika jamii, wapo wanaotokea kuhujumu mafanikio hayo ndio maana Serikali kwa kuwajali watu wake imewasisitiza wananchi kujihadhari na utapeli unaoweza kufanywa kupitia simu za mkononi na mtandao wa intaneti.

Tahadhari hiyo iliyotolewa na Serikali inasisitiza kutokutekeleza maagizo yoyote yanayohusu fedha kwa ujumbe wa maandishi hata kama yanatoka kwa mtu unayemfahamu, mmliki wa simu kutumia namba ya siri ambayo sio rahisi mtu mwingine kukisia na kutokutoa namba za siri za anazotumia mmiliki wa simu katika masuala yanqayohusu miamala ya kifedha.

Tahadhari nyingine ni kutokutekeleza maagizo yoyote kutokana na ujumbe wa simu za mkononi unaomtaka mtumiaji wa simu kutuma fedha kutoka namba ambayo mtumiaji wake unamfahamu na ambao unakueleza kuwa simu yake inahitilafu, hivyo hawezi kuongea, usitekeleze maagizo hayo.

Zaidi ya hayo, mtumiaji wa simu anatakiwa kutumia namba ya siri ambayo sio rahisi mtu mwingine kuikisia, kutokutoa namba za siri anazotumia mteja wa simu na kuhakikisha namba ya mtu unayemtumia pesa au salio kabala ya kutuma.

Aidha, mmliki wa simu akipoteza simu yake au laini anapaswa kutoa taarifa kwa mtoa huduma aliyeko karibu nae na aende polisi mara moja kutoa taarifa hiyo.

Endapo mteja asipopata ushirikianaoa wa kutosha kwa mtoa huduma aliyeko karibu yake, mteja anapaswa kuwasilisha malalamiko hayo kwa TCRA.

Njia sahihi za kufikisha malalamiko ni pamoja na kuyatuma kwa kuandika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, S. L. P. 474 Dar es salaam ama kufika ofisi za TCRA makao makuu Dar es salaam au ofisi za kanda na Zanzibar.

Namana nyingine ni kupiga simu namba 0784558270 au 0784558271 na kwa barua pepe malalamiko@tcra.go.tzau complaints@tcra.go.tz.

Pamoja na baadhi ya tahadhari hizo, Serikali inaendelea kuweka mazingira mazuri kwenye Sekta ya Mawasiliano ambayo yameonesha inaendelea kukua nchini na imekuwa na matokeo makubwa.

Kadiri siku zinavyokwenda, kumekuwa na idadi ya kubwa ya watumiaji wa huduma za mawasiliano nchini.
Idadi hiyo  imeendelea kuongezeka kutoka laini za simu za kiganjani milioni 2.96 mwaka 2005 hadi kufikia milioni 27.45 mwezi Desemba 2013 ambapo watumiaji wa mfumo wa intaneti nao wameongezeka kutoka milioni 3.56 mwaka 2008 hadi kufikia milioni 9.3 mwezi Desemba 2013.

Vilevile, mawasiliano nchini yanavyozidi kuongezeka, kumekuwa na ongezeko kubwa la huduma kupitia mawasiliano ya simu za kiganjani ambapo huduma za kifedha zinazotolewa kwa watumiaji wa simu hizo zimeongezeka pia.

Katika kudhihirisha hilo, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mnyaa Mbarawa (Mb), katika hotuba yake wakati akiwasilisha Bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2014/2015 mwezi Mei mwaka huu alisema kuwa huduma zilizoongezeka ni pamoja na miamala ya kifedha ambayo ina watumiaji wapatao 12,330,962 na ununuzi wa huduma na bidhaa kwa kutumia miamala ya kibenki.
“Hivi sasa, wananchi wanaweza kufanya malipo ya huduma mbalimbali wanazozitumia kupitia simu za kiganjani” alisema Prof. Mbarawa.

“Katika kipindi cha Julai, 2013 hadi Aprili, 2014 kuna jumla ya miamala 972, 641,605 yenye thamani inayofikia shilingi Trilioni 28.3 imefanyika”, aliongeza Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa alisisitiza kuwa maendeleo hayo yamesaidia kuokoa muda wa wananchi na kupunguza msongamano sehemu za kulipia na kupata huduma hizo wanazohitaji kwa wakati bila usumbufu wowote.

Maendeleo hayo ndiyo yanayoisukuma Serikali kupitia TCRA kujiwekea malengo katika mwaka wa fedha 2014/2015 ambayo itatekeleza kwa kufanya tathmini ya gharama za huduma za simu za mkononi na kufanya utafiti kuhusu utoaji wa huduma za intaneti na matumizi ya masafa yanayowezesha mawasiliano ya intaneti (Broadband) ili yaboreshwe na kufikia wanachi wengi zaidi na kupata mawasiliano yenye tija manufaakwa taifa.

Aidha, alipokuwa akihitimisha hotuba yake, Prof. Mbarawa aliyashukuru makampuni ya simu za kiganjani kwa kuwa tayari katika kushughulikia changamoto za mawasiliano katika maeneo yasiyo na mawasiliano hapa nchini.

Mbali na huduma ya mawasiliano, Prof. Mbarawa alisema kuwa makampuni hayo ya simu nchini yamekuwa tayari katika kuchangia maendeleo na upatikanaji wa huduma za jamii zenye tija kwa wananchi.

Makampuni hayo yameonesha nia ya dhati na kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii kama vile uchangiaji wa damu salama, ujenzi wa vituo vya afya, ununuzi wa vitabu vya ziada na kiada vinavyotumika mashuleni na vyuoni, ununuzi wa madawati na ujenzi wa madarasa.

Tukiwa kwenye ulimwengu wa utandawazi, kama nchi ni vema kusimamia maadili ya Kitanzania na utamaduni wetu mwema unayoipambanua nchi yetu na mataifa mengine kwa kuzingatia misingi ya utaifa wetu.

Tuyatumia mawasiliano kama sekta muhimu nchini ili taifa lifikie malengo yake ya kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Maenedleo hayo hayawezi kufikiwa kama Watanzania wote kwa umoja wao, nchi na mashirika ambayo ni washirika wa maendeleo, watatumia vibaya mwasiliano kwa lengo la kubomoa badala ya kujenga.

Hima hima TCRA, jukumu mlilopewa na taifa la kusimamia mawasiliano ni nyeti, juhudi zenu zisonge mbele ili watumiaji visivyo wa mawsiliano wachukuliwe kuwa ni wahujumu maendeleo ya taifa letu.

Ni suala la kiungwana na la kisheria kwa watumiaji wa simu za kiganjani kusajili namba zao za simu mbapo TCRA mara zote inawahimiza kusajili laini zao za simu.

Ili kujihakikishia kuwa laini yako ya simu imesajiliwa ni vema mtumiaji wa simu husika kuthibitisha na kijiridhisha kama usajili wake upo sahihi kwa kupiga *106# kwenye simu yako.
 
Uhakiki huo unahusisha watumiaji wa huduma ya mawasiliano kupitia mfumo wa makampuni ya Vodacom, Airtel, Tigo na Zantel, SASATEL na TTCL Mobile, na watasikiliza maelekezo.

Taarifa utakayoipata inatakiwa kutaja jina lako kama mtumiaji halali wa namba husika, na iwapo utapata jibu tofauti, tafadhali fika kwenye ofisi ya mtoa huduma wako au wakala wake ili kurekebisha kasoro hizo.

Watumiaji wa simu za mkononi na wananchi wanashauriwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ili kufanikisha usajili wa namba za simu kwa ajili ya kudumisha na kuendeleza amani na usalama na kuharakisha maendeleo ya sekta na ya Taifa kwa ujumla.

INTRODUCING Julio ft Chege - Special For You (Official video HD)

0
0

CBE YATOA MAFUNZO MAALUM KWA WAJASIRIAMALI WA JIJINI DAR-ES-SALAAM.

0
0
 Mfanyakazi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Bi. Mariam Tambwe akimkaribisha mgeni rasmi ambaye pia ni Mkuu wa Chuo hicho kwa ajili ya kufanya ufunguzi rasmi wa mafun z ohayo na kutowapa wajasiriamali maneno ya busara katika mafunzo ya siku mbili (24-25 Oktoba, 2014) chuoni hapo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) cha jijini Dar es Salaam, Profesa Emmanuel Mjema akifungua rasmi mafunzo maalum kwa Wajasiriamali (hawako pichani) walioko katika mafunzo ya siku mbili (24-25 Oktoba, 2014) chuo hapo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho jijini Dar es Salaam.
 Mwezeshaji wa mafunzo ya Ujasiriamali wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Bw. Ndingo Mwakyusa akiwapa elimu wajasiriamali waliohudhuria mafunzo ya siku mbili (24-25 Oktoba, 2014) chuoni hapo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho jijini Dar es Salaam.
 Mwezeshaji wa mafunzo ya Ujasiriamali wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Bi. Suma Nelson Mwansasu akiwapa elimu wajasiriamali waliohudhuria mafunzo ya siku mbili (24-25 Oktoba, 2014) chuoni hapo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Wajasiriamali waliohudhuria mafunzo ya siku mbili (24-25 Oktoba, 2014)wakifuatilia kwa makini elimu ikiyotolewa katika mafunzo hayo chuoni hapo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho jijini Dar es Salaam.(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA, MAELEZO-DSM)





CBE YATOA MAFUNZO MAALUM KWA WAJASIRIAMALI WA JIJINI DAR-ES-SALAAM
 
Na Benedict Liwenga, Maelezo-DSM.
 
24/10/2014.
 
CHUO cha Elimu ya Biashara (CBE) cha jijini Dar es Salaam kimefungua rasmi Mafunzo ya siku mbili ya Ujasiriamali kwa Wajasiriamali wa jijini Dar es Salaam ikiwa ni moja ya sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho.
 
Akifungua rasmi mafunzo hayo leo 24 Oktoba mwaka huu, Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Emmanuel Mjema amesema kuwa, mafunzo hayo kwa wajasiriamali hao itakuwa chachu ya maendeleo kwani yanalenga kutoa elimu ya biashara ili waweze kukokotoa mahesabu na kuongeza faida katika na shughuli zao za kijasiriamali.
 
Profesa Mjema Ameeleza kuwa, ujasiriamali nchini ni sekta muhimu kwani zaidi ya asilimia 85% ya waajiriwa nchini wanatoka katika sekta hiyo, huku asilimia 15% ni ya watumishi wa umma.
 
Amefafanua kuwa, mjasiriamali ni mtu yule ambaye amethubutu kwa kuwekeza rasilimali zake ili aweze kuendeleza kipato chake mwenyewe na kwa kufanya hivyo, anapunguza tatizo la ukosefu wa ajira nchini ambalo limekuwa ni tatizo linalowakabili wajasiriamali wengi.
 
“Nawapongeza sana kwa kazi nzuri mnazozifanya za ujasiriamali, hakika mchango wenu ni mkubwa kwa jamii nchini na unasaidia kupunguza tatizo la ajira nchini mwetu”, alisema Profesa Mjema.
 
Aidha, amewaasa wajasiriamali hao kuzingatia mafunzo hayo kwa kuhakikisha kuwa wanatunza faida na kuweza kukokotoa mahesabu vizuri huku akibainisha kuwa, tatizo linalowakumba baadhi ya wajasiriamali nchini sio tu mtaji, bali ni elimu ya kibiashara ambayo inawawezesha kufanya shughuli hiyo na kupata faida, hivyo amewataka kuzingatia mafunzo hayo na kuyatumia kivitendo katika kuleta maendeleo yao wenyewe na kwa taifa kwa ujumla.
 
“Tafiti zinaonyesha kuwa, wajasiriamali wengi wanaanguka katika biashara zao kwa kukosa elimu ya biashara”, aliongeza Profesa Mjema.Sambamba na mafunzo hayo, chuo hicho kinatarajia kutoa huduma ya vifaa mbalimbali vya hospitalini ikiwa ni sehemu ya mchango wake wa kuisaidia jamii.
 
Nao wawezeshaji wa mafunzo hayo ya ujasiriamali akiwemo Bwana Ndingo Mwakyusa pamoja na Bi. Suma Mwansasu wamesema kuwa mafunzo hayo wanayoyatoa kwa wajasiriamali hao yanahusisha elimu ya biashara ikiwemo mada mbalimbali kwa wajasiriamali hao kuhusu umuhimu wa ujuzi wa ujasiriamali katika ulimwengu wa kibiashara, kutengeneza hulka za kijasiriamali, vigezo muhimu vya kuzingatia katika biashara, vigezo muhimu katika uendeshaji wa biashara na mengineyo.
 
Mafunzo hayo ya ujasiriamali yanatarajiwa kuendelezwa kwa baadhi ya mikoa ya Pwani, Mbeya, Dodoma, Mwanza pamoja na upande wa Zanzibar.

Prof. Tibaijuka: Magonjwa ya Mlipuko yatekelezwe Kimataifa

0
0
Na Anita Jonas-MAELEZO
Umoja wa Mataifa umeshauri  kuchukua  hatua za haraka kwa magongwa ya mlipuko yanayotokea Afrika kama Ebola kwani yanadhiri uchumi wa mataifa husika.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka wakati wa Maadhimisho ya Miaka 69 ya Umoja wa Kimataifa leo Jijini Dar es Salaam.
Prof. Tibaijuka alisema kuwa Umoja wa Mataifa wanatakiwa kuchukua tahadhari ya milipuko ya magonjwa hatarishi na kuyachukulia kama ni magonjwa ya Kidunia kwani yanaathiri mifumo yote ya kimaendeleo.
“Mataifa yaliyoendelea yasingepuuzia mlipuko wa  ugonjwa wa Ebola ulipojitokeza  Afrika  hali  isingekuwa  hatarishi kama ilivyo sasa, hivyo ni rai yangu kwa Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na mataifa husika kuchukua  tahadhari wakati wote ”Alisema Prof. Tibaijuka.
Aidha, Prof. Tibaijuka alisema kuwa kutokana na tatizo la mabadiliko ya tabia nchi kuwa tishio miongoni mwa wengi duniani, wahisani wa maendeleo hawanabudi kusaidia Mataifa mengine ikiwamo utekelezaji wa Mfuko wa Kijani wa Hali ya hewa.
Akizungumzia kuhusu hatua ya Rais Dkt. Jakaya Kikwete kutoa uraia kwa wakimbizi 162,000 kutoka Burundi, Prof. Tibaijuka alisema kuwa Tanzania imeonyesha ulimwengu kuwa suala la mapambano dhidi ya ukimbizi linaweza kufanyiwa kazi na kuwafanya wakimbizi kuishi maisha kama binadamu wengine.
Naye Mratibu muwakilishi wa makazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bw. Alvaro Rodriguez alisema kuwa shirika hilo kwa kushirikiana na serikali na wadau wengine,  wamepanga kusaidia na kuboresha miundombinu ya kiusalama ili kuendeleza amani Duniani kwani bila amani maendeleo ni vigumu kupatikana.
Pia Bw. Rodriguez aliipongeza Tanzania katika kutekeleza Malengo ya Millenia katika sekta ya afya kwa ambapo asilimia 96 ya vituo vyote vya afya nchini vinatoa huduma ya afya ya uzazi kwa mama na mtoto.
Sherehe hizo zimebebwa na kauli mbiu ya “Leave no One Behind” ikiwa na mlengo wa kuleta maendeleo yenye usawa duniani.

President Kikwete accorded rousing karibu, as China's President Xi Jinping formaly welcomes him to Beijing

0
0
 President Xi Jinping of China welcomes President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete to the Great Hall of the People in Beijing this evening during the official formal reception at the climax of the State visit at the invitation of the Chinese leader.

 President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete and the First Lady Mama Salma Kikwete pose for an official photograph with their host China’s President Xi Jinping and his wife China’s First Lady Peng Liyuan shortly after they arrived for an official formal reception at the Great Hall of the People in Beijing this evening.
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete and the First Lady Mama Salma Kikwete pose for an official photograph welcomed by their  host China’s President Xi Jinping and his wife China’s First Lady Peng Liyuan

President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete and his host Chinese President Xi Jinping inspects a guard of honor mounted China’s People Defense force in Beijing this evening during a formal reception at the Great Hall of the people. President Kikwete is on a State Visit to China at the invitation of President Xi Jinping.
 President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete and his host President Xi Jinping waves to the cheering crowd during a formal reception for the President and his delegation held at the Great Hall of the People in Beijing at the climax of his State visit today.




 President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete introduces former OAU/AU Secretary General Salim Ahmed Salim to China’s President Xi Jinping during the formal reception held at the Great Hall of the People in Beijing this evening.Left is the Minister for Foreign Affairs Mr Bernard Membe and second left is CCM Secretary General Abdulrahman Kinana.

China yamwaga neema kubwa kwa Tanzania

Jamhuri ya Watu wa China leo, Ijumaa, Oktoba 24, 2014, imetangaza neema kubwa kwa Tanzania, ikiwa ni pamoja na kutoa dola za Marekani milioni 85 kwa ajili ya shughuli za maendeleo na kuisaidia Tanzania kufanya mageuzi ya viwanda.
Neema hiyo ya China kwa Tanzania imetangazwa na Rais Xi Jinping wa nchi hiyo katika mazungumzo rasmi ya Kiserikali kati yake na ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye yuko katika ziara rasmi ya siku sita katika China.
Mazungumzo hayo kwenye Jumba la The Great Hall of the People yamefanyika baada ya Rais Kikwete kukaribishwa rasmi katika Jamhuri ya Watu wa China kwa kupokelewa na Rais Xi Jinping katika eneo la East Plaza ya Jumba hilo.
Katika mapokezi hayo ya kuvutia na kusisimua, Rais Kikwete amepigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride la ukakamavu la Jeshi la Ukombozi la Wananchi wa China la People’s Liberation Army.
Katika mazungumzo hayo, Rais Xi Jinping alitangaza kuwa China itaipatia Tanzania kiasi cha dola milioni 85 ikiwa ni mchanganyiko wa msaada na mkopo usiokuwa na riba, fedha ambazo Tanzania itaamua yenyewe jinsi gani ya kuzitumia.
“Katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya Tanzania kuboresha maisha ya wananchi wake, napenda kutangaza kuwa Jamhuri ya Watu wa China itatoa kiasi cha RMB milioni 200 ikiwa ni msaada na RMB 200 milioni nyingine zikiwa ni mkopo usiokuwa na riba kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kiasi cha RMB 100 milioni za msaada kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambazo zitatumika kwa kadri Serikali hizo mbili zitakavyoamua,” amesema Rais Jinping.
Rais huyo wa China pia ametangaza kuwa nchi hiyo itaisaidia Tanzania katika uendelezaji wa maeneo ya uwekezaji ya EPZ, uendelezaji wa miundombinu, itaharakisha ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo na itaingia katika shughuli za kutafuta gesi na mafuta katika ukanda wa Bahari ya Hindi katika eneo la Tanzania.
Rais Jinping pia ametangaza kuwa Serikali ya China imefanya uamuzi wa kuikarabati Reli ya Uhuru ya TAZARA inayounganisha Tanzania na Zambia na yenye urefu wa kilomita 1,860 na kusaidia uendeshaji wa reli hiyo. “Ili kutekeleza uamuzi huu kwa haraka, napendekeza kuundwa kwa kamati ya pamoja ya wataalam kuandaa ramani ya namna ya kuitoa reli hiyo katika matatizo yake ya sasa.”
TAZARA ndiyo reli ya kwanza duniani kujengwa na Jamhuri ya Watu wa China ambao utaalamu wake sasa unasakwa na nchi nyingine nyingi duniani.
Rais Jinping pia ametangaza kuwa Serikali yake itatoa nafasi 100 za masomo ya elimu ya juu kwa wanafunzi kutoka Tanzania katika miaka mitano ijayo, itaongeza idadi ya madaktari ambao China inapeleka Tanzania, itahimiza makampuni zaidi ya China kuwekeza katika Uchumi wa Tanzania na kuzishawishi taasisi za kifedha za China kuanzisha shughuli zake katika Tanzania.
Kiongozi huyo wa China pia ametangaza kuwa nchi yake itajenga chuo kikubwa cha mafunzo ya ufundi katika Tanzania na itaendelea kushirikiana na Tanzania katika eneo la uimarishaji wa ulinzi na usalama.

Rais Jinping amesema kuwa urafiki na uhusiano kati ya China na Tanzania ni mfano unaong’ara wa uhusiano mzuri na mwema duniani na kuwa China iko tayari kutoa uzoefu wake wa maendeleo kwa Tanzania bila wasiwasi wowote.
Rais Kikwete amemshukuru sana Rais Jinping na Jamhuri ya Watu wa China kwa misaada yake ambayo baadhi yake haikutarajiwa

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
24 Oktoba, 2014.



Benki ya Exim yasaini mkataba wa mwaka mmoja na Stand United FC

0
0
 Mkuu wa matawi wa Benki ya Exim Kanda ya Ziwa, Bw. Justus Mukurasi (wapili kushoto) akibadilishana mkataba na Mwenyekiti wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Stand United, Bw. Amani Vicent (wapili kulia) wakati wa hafla fupi iliyofanyika mkoani Shinyanga jana. Mkataba huo utaiwezesha benki kuidhamini timu hiyo katika ligi kuu ya mpira wa miguu ya Vodacom (VPL) katika msimu wa 2014/2015. Wakishuhudia wa kwanza kushoto ni Meneja Msaidizi Tawi la Shinyanga, Bw. Hatunga Nicodemus na Katibu wa kamati ya Fedha, Bw. Bakari Salum (Wa kwanza kulia).
 
Benki ya Exim imesaini makubaliano ya kuifadhili timu ya mpira wa miguu ya Stand United FC ya mkoani Shinyanga. Hii ni timu ya kwanza kupata ufadhili toka Benki ya Exim. Ufadhili huo wa mwaka mmoja utaisaidia timu hiyo kushiriki katika ligi kuu soka Tanzania bara kwa msimu wa 2014/2015.

“Makubaliano haya yanaikutanisha Benki ya Exim na mchezo mkubwa kuliko yote Tanzania,” alisema mkuu wa matawi ya Benki ya Exim kanda ya ziwa, Bw. Justus Mukurasi jana katika hafla fupi iliyofanyika mkoani Shinyanga. Aliongeza kuwa hakuna mchezo wenye watazamaji, wafuatiliaji na mashabiki wengi zaidi nchini kama mpira wa miguu.

“Timu ya Stand United inanguvu kubwa ya kuunganisha mashabiki  wa kanda ya ziwa. Hivyo ni jambo stahiki kwa Benki ya Exim kuisaidia timu hii ambayo mashabiki wake ni miongoni mwa wateja wa Benki ya Exim,” alisema Bw. Mukurasi.

Mukurasi aliongeza kuwa pande hizo mbili zilifanikiwa kuingia katika makubaliano ambayo yataiwezesha benki hiyo kuifadhili timu ya Stand United toka Ligi Kuu Tanzania bara ilipoanza.

“Kwetu sisi udhamini tuliofanya sio tu wa nembo, nbali ni ufadhili wa muda mrefu utakaozinufaisha pande zote mbili,” alisema Mukurasi.

”Tunatumai kuwa kila mmoja wetu ataweza kujifunza kutoka kwa mwenzake ili kupata matokeo mazuri kwa pamoja. Exim itasaidia kukuza na kuundeleza mchezo wa soka na hivyo kuiwezesha benki yetu karibu zaidi na wateja wake,” alisema Bw. Mukurasi.

Naye, Mwenyekiti wa Stand United FC, Bw. Aman Vicent alisema kuwa timu yake inayofuraha kubwa kuingia katika makubaliano na Benki ya Exim. “Tunadhamiria kuimarisha uhusiano huu ili kuhakikisha timu yetu inafanya vizuri katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu,” alisema Bw. Vicent.

“Kwa niaba ya Stand United FC, ningependa kuishukuru Benki ya Exim kwa jitiada zao za kusaidia wachezaji wetu na timu kwa ujumla. Tunafanya kazi kubwa kuhakikisha tunainua vipaji vya wachezaji wetu ili na wao waweze kufika mbali zaidi,” aliongeza Bw. Vicent.
 

RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA AONGOZA WAOMBOLEZAJI KATIKA MAZISHI YA MEJA JENERALI HERMAN LUPOGO

0
0
 Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na mkewe wakiweka shada la maua katika kaburi la Meja Jenerali mstaafu, Herman Lupogo wakati wa mazishi yake katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Meja Lupogo alifariki Oktoba 19 katika hospitali ya Jeshi ya Lugalo. 
 Mke wa marehemu akiweka shada la maua.
 Familia ikiweka shada la maua.
 Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akiweka shada la maua.
 Mashada ya maua yakiwekwa.
 Heshima kwa marehemu Meja Jenerali Herman Lupogo.

SHEREHE ZA UN ZAFANA: TANZANIA YATAKA UTEKELEZAJI MFUKO WA GCF

0
0
IMG_2656
Pichani juu na chini ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akimtambulisha mgeni rasmi Waziri wa Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka kwa baadhi ya wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini mara baada ya kuwasili kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 69 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake.
IMG_2657
IMG_2672
Waziri wa Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka akipokea heshima ya wimbo wa taifa kabla ya kuanza rasmi kwa sherehe za maadhimisho miaka 69 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake.
IMG_2703
Waziri wa Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka akikagua gwaride maalum kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 69 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake zilizofanyika leo jijini Dar.
IMG_3040
Mgeni rasmi Waziri wa Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka akisoma risala kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 69 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake yaliyofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar.
IMG_2923
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisoma  ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 69 ya Umoja wa Mataifa zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar.

Mahafali ya Kidato cha nne shule ya sekondari WAMA-NAKAYAMA kufanyika jumapili hii

NAPE AKIHUTUBIA VIJANA WA CCM KUTOKA VYUO VIKUU

0
0
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live




Latest Images