Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46205 articles
Browse latest View live

BONDIA THOMAS MASHALI AJIFUA KUMKABILI MKENYA HENRY WANDERA NOVEMBA MOSI FRENDS CORNE

0
0
Bondia Tomas Mashali  kushoto akijifua wakati wa mazoezi ya kujiandaa kupambana na Bondia Henry Wandera kutoka kenya novemba 1 katika ukumbi wa frends corner manzese, akisimamiwa na Kocha wa Mchezo wa Masumbwi kutoka Sweeden, Juma Ntuve (Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

 BON DIA Thomasi Mashali  yupo katika maandalizi mazito ya kumkabili bondia kutoka kenya Henry Wandera Novemba mosi katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Dar es salaam

akizungumza wakati wa mazoezi yake juzi Mashali amesema kuwa yupo fiti wakati wowote yeye kufanya kazi hivyo aofii ata kiogo mpambano huo na kuwataka mashabiki wake waje waone anavyo mgalagaza vibaya sana siku hiyo mkenya Wandera

mbali na mpambano huo siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi yatakayo wakutanisha Mbayo Ilunga na Fred Sayuni wakati Joseph Mbowe ataoneshana umwamba na Saidy Salum na Ramadhani Johncena ataoneshana ubabe na Baina Mazola

na mipambano mingene mikali zaidi siku hiyo kutakuwa na michezo ya utangulizi zaidi ya nane yenye raundi sita sita

katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na ulinzi wa kutosha kabisa kutokana na kujipanga vizuri katika swala hilo  kingilio ni shilingi, 7000; kwa kila mtu mchezo huu utapambwa na burudani mbalimbali


PSPF YAANDAA CHAKULA CHA JIONI KWA WALIMU MJINI MOROGORO

0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, (Kulia), akiteta jambo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Afande Leonard Paul, wakati wa chakula cha usiku kilichoandaliwa na Mfuko huo kwa baadhi ya wachezaji wa timu ya polisi mkoani Morogoro na wajumbe wa  idara ya utumishi wa walimu wanaohudhuria semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo mkoani Morogoro, Alhamisi Oktoba 23, 2014.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, akisalimiana na baadhi ya wachezaji wa timu ya Polisi Morogoro, Jumatano Oktoba 22, 2014, wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Mfuko huo kwa wachezaji hao na wajumbe wa idara ya utumishi wa walimu, wanaohudhuria semina ya siku moja iliyuoandaliwa na Mfuko huo Mkoani Morogoro
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, akizungumza na wajumbe wa idara ya utumishi wa walimu, wakati wa chakula cha usiku kilichoandaliwa na Mfuko huo mjini Morogoro Oktoba 22, 2014. Wajumbe hao wanatarajiwa kubhudhuria semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo ili kuwaelimisha walimu faida wanazoweza kupata endapo watajiunga na Mfuko huo.

 Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Mwanjaa Seme, akiwasalimia walimu ambao ni wajumbe kutoka idara ya utumishi wa walimu wakati wa chakula cha usiku kilichoandaliwa kwa wajumbe hao wanaohudhuria semina ya siku moja iliyoandaliwa na PSPF, ili kuelezea shughuli mbaklimbali na faida unazoweza kupata unapojiunga na Mfuko huo. Semina hiyo ilifanyika mkoani Morogoro
Msanii Mrisho Mpoto, ambaye pia ni balozi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akiimba sambamba na baadhi ya walimu na maafisa wa Mfuko huo, wakati wa chakula cha usiku kilichoandaliwa na PSPF, kwa wajumbe wa idara ya utumishi wa walimu wanaohudhuria semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo mkoani Morogoro. Picha na Masogange

WAZIRI MKUU AZINDUA JARIDA LA FIRST JIJINI LONDON

0
0
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama Jarida la  First baada ya kukabidhiwa nakala  ya toleo la  jaridai hilo na Muasisi wake, Rupert Goodman  (kulia) kwenye ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza uliopo London. Jarida  hilo limesheheni  makala zenye kuinadi Tanzania na vivutio vyake nje ya nchi
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akizungumza wakati alipozindua toleo la  Jarida la First lenye makala mbalimbali za kuinadi Tanzania na Vivutio vyake nje ya nchi katika hafla iliyofanyika kwenye ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe Peter Kallaghe  na kulia ni Mwanzilishi wa jarida hilo, Rupert Goodman
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akisalimiana na Mwenyekiti na Muasisi wa Kampuni ya Invest Africa ya Uingereza, Bw. Robert Hersov kabla ya mazungumzo yao kwenye hoteli ya Savoy,London Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe Saidi Mwambungu


*Ni Toleo Maalum la Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania
*Linatumika kuitangaza Tanzania kwa watu mashuhuri 

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amezindua jarida la kimataifa la FIRST ambalo limesheheni taarifa za kuitangaza Tanzania kwa wadau wa nchi mbalimbali duniani huku likielezea hatua mbalimbali za ustawi kwa miaka 50 tangu nchi ipate uhuru. 
Uzindusi huo ulifanyika kwenye ofisi za ubalozi wa Tanzania jijini London, Uingereza ambako pia Waziri Mkuu alikabidhiwa nakala ya kwanza ya toleo la sasa ambayo iliwekwa kwenye jalada jekundu la ngozi (leather bound red cover). 

Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri Mkuu alisema Serikali ya Tanzania imepata fursa nzuri ya kujinadi kwa watu maarufu na wafanyabiashara wa kimataifa duniani kupitia jarida hilo na akataka uwekwe utaratibu wa kujinadi kisekta. 

Alimtaka Balozi wa Uingereza, Bw. Peter Kallaghe aweke mkazo na kusimamia suala hilo ili kuhakikisha matoleo yanayofuata yanakuwa ya kisekta zaidi. “Balozi hapa umefanya kazi nzuri sana ya kuinadi nchi yetu, wala usichoke. Tujitahidi sasa kila mwaka waandike kuhusu fursa za uwekezaji kwa miradi ya kisekta kama utalii, nishati, madini na kadhalika,” alisema. 

Waziri Mkuu alimshukuru Mwenyekiti wa taasisi ya First, Bw. Rupert Goodman kwa kazi nzuri aliyoifanya kwa ajili ya Taifa la Tanzania. “Kazi uliyoifanya ni nzuri lakini katika tolea lijalo tuangalie jinsi ya kuitangaza miradi ya uwekezaji ambayo inauzika na iende sekta kwa sekta. Ukisirikiana na Balozo wetu hapa, lazima utapata kitu kizuri,” alisema. 

Mapema, akielezea kuhusu jarida hilo la FIRST, Balozi Kallaghe alisema jarida hilo linasambazwa kwenye mashirika mbalimbali ya ndege kama vile British Airways, Air Astana, Lufthansa, United Airlines, Gulf Air, American Airlines, South African Airways, Korean Airways, Etihad Airways, Qatar Airways na Continental Airlines. 

“Siyo tu kwamba linasambazwa katika mashirika haya ya ndege, bali pia linawekwa kwenye vyumba vya kupumzikia (First Class and Business Class Lounges) abiria wa daraja la kwanza na la pili wa mashirika haya kwenye viwanja vingi vya ndege,” alisema. 

Alisema hili ni toleo la sita ambalo limeandaliwa kwa ushirikiano na ofisi yake (Ubalozi wa Uingereza) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania lakini pia ikilenga kutangaza fursa za uwekezaji lakini pia ikitangaza hatua mbalimbali za maendeleo ambazo nchi hii imepitia.

Uzinduzi huo ulihudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Fedha, Bw. Mwigulu Nchemba; Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Mahadhi Maalim na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Bw. Charles Kitwanga. Wengine ni Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Bw. Said Mwambungu ambao pia wamefuatana na Waziri Mkuu.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, OKTOBA 23, 2014

HYUNDAI presents Heavy Construction Equipment at Oil & Gas Conference.

0
0
 
HYUNDAI Sales Manager, Mr. Alen Nkya (left) clarifies a point to the Deputy Minister for Energy and Minerals of Tanzania, Hon. Stephen Masele and other delegates regarding Construction Equipment and Industrial Vehicles used in oil and gas projects during International Oil & Gas Conference held in Dar es Salaam.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AAGANA NA BALOZI WA BOTSWANA NCHINI TANZANIA IKULU DAR, AKUTANA NA BALOZI WA RWANZA NCHINI TANZANIA

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Balozi wa Botswana nchini Tanzania, anayemaliza muda wake, Oliphant Tuelonyana, aliyefika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Eugene Kayihura, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam jana. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Botswana nchini Tanzania, anayemaliza muda wake, Oliphant Tuelonyana, aliyefika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Eugene Kayihura, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam jana. Picha na OMR

Airtel yatatua changamoto za uhaba wa vitabu vya sayansi Katika shule ya Sekondari Mukulati Mkoani Arusha

0
0
Meneja Mauzo wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel mkoa wa kilimanjaro Paschal Bikomagu kushoto akimkabidhi baadhi ya vitabu vya sayansi kwa Diwani wa kata ya Olkokola Joseph laizer kwa niaba ya shule ya sekondari Mukulati mkoani arusha wakati wa mahafali ya 17 ya kidato cha nne ya shule hiyo.
Makamu mkuu wa shule ya sekondari Mukulati ya mkoani arusha mwalimu Vitalisi Martine akiwakabidhi baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo vitabu vya sayansi vilivyo tolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel wakati wa mahafali ya 17 ya kidato cha nne katika shule hiyo.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel  imeedelea kuungana na serikali katika kusaidia kuboresha maendeleo ya sekta ya elimu  nchini ambapo imetoa vitabu vya ziada na kiada  katika masomo ya sayansi kwa shule ya sekondari mukulati wilayani Arumeru mkoani Arusha

Licha ya Kada ya sayansi kuwa ndio chimbuko kubwa  la wataalamu wengi katika fani mbalimbali bado  inatajwa kutofanya vizuri kutokana na uhaba wa miundombinu na vifaa stahiki ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya kada hiyo. 

Meneja wa Airtel mkoa wa Kilimanjaro  Paschal Mikomagu  akizungumzia mchango wa kampuni hiyo wakati wa mahafali ya 17 ya shule ya sekondari mukulati amesema Airtel kwa kutambua changamoto mbalimbali ndani ya kada ya sayansi nchini ikiwemo uhaba wa vitabu vya kujifunzia  imeamua kuwa na utaratibu wa kugawa vitabu hivyo.  Leo tumehudhuria mahafali  na kuchangia kutatua moja ya kero zinazokumba sekta ya elimu na tuaamini kwa msaada huu wa vitabu vitaongeza ufaulu wa wanafunzi na kusaidia shule kufanya vizuri kitaaluma

Tutaendelea kutimiza dhamira yetu kwa vitengo ya kusaidia kutatua changamoto mbalimbali mashuleni na kuhakikisha tunaboresha uwiano wa vitabu kwa wanafunzi hadi kitabu kimoja kwa mtoto moja au wawili.

Kwa upande wake Diwani wa  kata ya Olkokola Joseph laizer  leo ni sisi Airtel imetoa msaada huu wa vitabu ambavyo vitasaidia shule hapa , lakini zaidi tunawaomba Airtel waendelee kujitolea kushirikiana nasi  na kutufadhili katika ujenzi wa maabara katika shule hii ili kuweza kufikia malengo tuliyowekewa ya kuhakikisha kila shule ya sekondari inajenga maabara kwa ajili ya mafunzo ya ziada

Akiongea mara baada ya kupokea vitabu hivyo MkeeVitalisi Martine mkuu wa shule  kwa msaada huu umeongeza uwiano wa vitabu shule hapa ambapo kwa sasa kitabu kimoja kitatatumika na wanafunzi wawili,  napenda kuwhakikishia vitabu hivi havitakaa kwenye kabati bali vitatumika kwa manufaa yaliyokusudiwa ili atimaye watoto waweze kupata ujuzi kupitia vitabu hivi

Nao baadhi ya wanafunzi walito maoni yao kuhusu mchango huu shule ni hapo ambapo Happy Lyimo alisema natoa shukurani za dhati kwa niaba ya wanafunzi wenzangu kwa Airtel kwa kutupatia mchango wa vitabu vingi vya sayansi. Nimatumaini yangu kuwa vitabu hivi vitasaidia kuinua taaluma kwa wanafunzi na  shule kwa ujumla.

SWEDEN YATOA BIL. 42/- KUSAIDIA MIRADI UN

0
0
DSC_0216
Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mh. Lennarth Hjelmaker akizungumza na waandishi wa habari kwenye hafla ya kutiliana saini makubaliano kati ya nchi ya yake na Umoja wa Mataifa ambapo wametoa fedha kusaidia miradi ya Umoja wa Mataifa kwenye ofisi za ubalozi wa Sweden jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.(Picha na Zainul Mzige MOblog).

SWEDEN imeyapatia mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyopo hapa nchini jumla ya shilingi bilioni 42/- ili kusaidia katika miradi yake ya maendeleo inayofanya nchiini Tanzania. Makubaliano ya fedha hizo yametiwa saini jana kati ya Balozi wa Sweden Lennarth Hjelmaker na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Alvaro Rodriguez.

Fedha hizo ambazo ni sawa na dola milioni 24, zitaelekezwa kwenye miradi ya UNDAP inayoendana na sera za Sweden za kuwezesha masuala ya utawala bora, ustawi wa jamii, wanawake na watoto na usawa wa kijinsia.

Kwa mujibu wa Balozi wa Sweden, fedha hizo zitasaidia utekelezaji wa Mkukuta, Mkuza na Matokeo makubwa sasa (BRN) mipango inayofadhiliwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa . Alisema ni matumaini yake kuwa fedha hizo zitaboresha hali ya kufanya biashara, kuwekeza kwa lengo la kutoa ajira zaidi,kuwezesha uchaguzi huru, kuimarisha huduma za jamii, kuimarisha mipango, uwajibikaji na kuimarisha mawasiliano ya radio kwa ajili ya upashanaji habari vijijini ili kusaidia maamuzi yenye mtazamo mpana zaidi miongoni mwa watu wa vijijini.
IMG_2231
Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mh. Lennarth Hjelmaker (kulia) na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakitiliana saini makubaliano ya msaada wa fedha hizo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam kwenye ofisi za ubalozi huo.

Katika hafla hiyo Balozi wa Sweden alisema pamoja na kutoa fedha hizo kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa, nchi yake itaendelea na makubaliano yaliyofikiwa na serikali ya Tanzania na kuendelea kutoa misaada yake ya kimaendeleo.


Akijibu swali la kwanini wanatoa fedha kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa pekee, na kama wameacha kutoa misaada ya moja kwa moja serikalini, Balozi huyo alisema misaada ya taifa hilo imelenga kupata matokeo yanayotakiwa na kwamba itaendelea kusaidia pia taasisi nyingine zisizo za kiserikali na serikali yenyewe.

Aidha Balozi Lennarth Hjelmåker alisema kwamba Tanzania imekuwa mfano bora kabisa wa mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa kuwezesha ufanisi mkubwa wa miradi ya maendeleo yaliyolenga kuwawezesha watanzania kupiga hatua mbele na kuhakikisha kuwapo kwa amani.
Alisema wanafurahia kusaidia masuala ya utawala bora, kazi kwa vijana, usawa wa kijinsia na kuwapo kwa uchaguzi huru na wenye amani.
DSC_0264
Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mh. Lennarth Hjelmaker (kulia) na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakionyesha hati za makubaliano hayo mara baada ya kutiliana saini.
Sweden imesema itaendelea kusaidia Umoja wa Mataifa nchini hasa inapotekeleza mradi wake wa misaada kwa Tanzania (UNDAP) kama mashirika hayo yalivyokubaliana na serikali ya Tanzania.
Naye Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez, ameishukuru Sweden kwa kuendelea kuwa mdau wa maendeleo.
Tanzania na Umoja wa Mataifa wanatekeleza mradi wa miaka mitano wa UNDAP ambapo mashirika ya UN yaliyopo nchini yanatoa kwa umoja wake huduma stahiki ili kupata Matokeo Makubwa.
DSC_0267
Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mh. Lennarth Hjelmaker (kulia) na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakibadilishana hati hizo za makubaliano hayo.
DSC_0238
Baadhi ya waandishi wa habari na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na Ubalozi wa Sweden waliohudhuria hafla hiyo.
DSC_0242
DSC_0278
Naibu Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Maendeleo kwenye Ubalozi wa Sweden nchini, Maria Van Berlekom, akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za ubalozi huo jana jijini Dar es Salaam.
DSC_0280
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu (kushoto) akimtambulisha Mwandishi wa habari kutoka East Africa Radio Nassa Kingu kwa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati) mara baada ya hafla fupi ya kutiliana saini makubaliano ya fedha hizo baina ya Umoja wa Mataifa na Ubalozi wa Sweden nchini.
DSC_0165
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akiteta jambo na Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mh. Lennarth Hjelmaker mara baada ya Umoja wa Mataifa na Ubalozi wa Sweden kutiliana saini makubaliano ya msaada huo.

Muswada wa Baraza la vijana-John Mnyika

0
0

UTUMISHI YAFANYA KIKAO KAZI KWA VIDEO CONFERENCE NA MIKOA YA SINGIDA,ARUSHA NA DODOMA

0
0
Naibu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB Mkwizu (kulia) akifungua kikao kazi kwa njia ya Ki-elektroniki (video conference)kilichojumuisha Utumishi na Mikoa ya Singida, Arusha, Dodoma na Tume ya Mipango katika ukumbi wa Utumishi mapema leo.
Naibu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB Mkwizu (kulia) akifuatilia mada wakati wa kikao kazi kilichofanyika kwa njia ya Ki-elektroniki (video conference) kati ya Utumishi na Mikoa ya Singida, Arusha, Dodoma na Tume ya Mipango katika ukumbi wa Utumishi mapema leo.
Afisa Utumishi Mwandamizi wa Ofisi ya Rais-Utumishi Bi.Sakina Mwinyimkuu akiwasilisha katika kikao kazi kilichofanyika kwa njia ya Ki-elektroniki (video conference) kati ya Utumishi na Mikoa ya Singida, Arusha, Dodoma na Tume ya Mipango katika ukumbi wa Utumishi mapema leo. Wengine ni viongozi wa Ofisi ya Ris Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakifuatilia mada.
Baadhi ya viongozi na watumishi wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakifuatilia mada wakati wa kikao kazi kilichofanyika kwa njia ya Kielektroniki (video conference) kati ya Utumishi na Mikoa ya Singida, Arusha, Dodoma na Tume ya Mipango katika ukumbi wa Utumishi mapema leo.
Afisa Utumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi Bi.Magreth Ngondya (kushoto) akiwasilisha mada katika kikao kazi kilichofanyika kwa njia Ki- elektroniki (video conference) katika kikao kazi kati ya Utumishi na Mikoa ya Singida, Arusha, Dodoma na Tume ya Mipango katika ukumbi wa Utumishi mapema leo. Wengine ni viongozi wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakifuatilia mada.

2014 CNN – MULTICHOICE JOURNALIST AWARDS SHOWCASES TANZANIA DESPITE FAILURE TO WIN A SINGLE AWARD

0
0
image008
Bento Venâncio, from Jornal Domingo and Brito Simango, from Televisão de Moçambique, posing with Victor Mlunde while holding their Portuguese Language General News Awards.

By Victor Mlunde.

Last Saturday, the world witnessed a historic annual CNN-Multichoice Journalist Award ceremony on the continent, hosted for the first time in our commercial capital, Dar Es Salaam. The choice of Tanzania is not only an unprecedented honor to the great peaceful nation on the continent, but a rare opportunity to showcase Tanzania and open its market to the world.

I congratulate the event organizers and His Excellency the President, Dr Jakaya Mrisho Kikwete, for being the Guest of Honour, for his outstanding economic diplomacy skills and unending efforts in showcasing Tanzania to the world.

As usual, the president’s speech looked at quantity rather than quality, boasting to have more media outlets in the country than neighbors - even with mounting insecurity of media practitioners and existence of Draconian Newspapers Act, 1976 and National Security Act, 1970 which limit press freedom as we approach 2015 general elections, the standard rhetoric maintained that the government will soon table the Freedom of Information and Media Services Bills in parliament, a promise left unattended by the Ministry of Information since begin of his second term in office back in 2006.

Despite government’s slow pace in implementing commitments on free press, we should acknowledge the fact that the head of state is at least committed to transparency and open government more than his predecessors, at least by signing international commitments and protocols on transparency such as the Open Government Partnership, though more work needs to be done in getting Media Freedom Bill and Services Act in place before busy and tense election period comes in.

image009
Categories and winners
The award categories covered economics and business, press freedom, culture, sports, photo journalism, sports reporting and the environment. Others included Portuguese and French stories awards. Winners wrote moving and interesting stories. To mention a few; Bento Venâncio, Jornal Domingo, Mozambique investigated how lack of transparency in procurement of automobiles in Mozambique leads to fraud, Evelyn Watta, a sports reporter from Kenya revealed the value of Senegal’s mythical Wrestling heritage to the West African nation. The most touching of all was Press Freedom Award handed to the wife of jailed Swazi journalist, Bheki Makhubu who is facing sedition for penning columns supporting a state clerk who was charged for trying to put right the system that allowed judicial officers to misuse public cars.

My sincere congratulations should go to the only brave Tanzanian nominee, one Dickson Ng’hily whose Dar traffic jam story was a concern of all Dar commuters; too bad the judges underestimated the significance of his story in pushing authorities in fast growing African cities to expand the road network.
However, a question remains; where were the rest of Tanzanian journalists? it is believed the majority did not submit their work for some reason – probably due to the fact that everyone was very busy reporting on “katiba” stunning headlines “serikali mbili au tatu” instead of simple local stories that could create positive impact in the community! If the awards had a politics category, I am sure we would have beaten the Kenyans and West Africans for our genius in making stunning political headlines.

Yes! We would have defeated our neighbours in Kenya who have outperformed the whole of East Africa in this year’s awards, yet again. In fact it is not the first time; even in the prestigious annual Kili Marathon held in Tanzania’s Kilimanjaro region, Kenyans end up winning more trophies while we the hosts are reduced to mere spectators each year.
415
President Jakaya Kikwete presents the overall ‘CNN MultiChoice African Journalist of the Year’ Award to Joseph Mathenge. Looking on is Mathenge’s son, Geoff Kihato.
Overall winner.

I was personally moved by the story of the overall winner, Joseph Mathenge and his son who convinced father to abandon his private photography tender aimed at raising funds for son’s cancer treatment and instead rushed to the Westgate Mall to capture the very first photos that revealed the images of terror to the whole world.

Way forward
It is high time Tanzanian journalists be proud of their work and confident to present it in future awards, even when unsure of winning. More quantity will help identify quality stories that will make all of us proud.Organizers should also add a social media category to honour and recognize excellent work by social media which uses the internet and citizen journalism to report sensational stories as they happen swifter than the traditional media itself.

On the other hand, award organizers should add a Swahili story category alongside Portuguese and French story awards for it is an African Union (AU) language widely spoken across East and Central Africa. Moreover, I would like to advise CNN to introduce a CNN Swahili language service in East and Central Africa, emulating BBC, Deutsche Welle, Radio France International and VOA in giving local journalists in the broader Swahili speaking East and Central African region to cover and explain local stories to the world.

Victor Mlunde is a Dar es Salaam-based Political and Development Consultant with expertise in media, good governance, elections and conflicts resolution in the Great Lakes region. He can be easily reached through +255 714 289428 and vicmlunde@yahoo.com

MAKAMU WA RAIS DKT. BIALA AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU MSTAAFU WA UBA TANZANIA GENERAL ROBERT MBOMA NA UJUMBE WAKE, IKULU DAR.

0
0
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Ujumbe wa UBA Tanzania ulioongozwa na aliyekuwa Mkurugenzi wake Mkuu mstaafu, General Robert Mbomba, wakati walipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, jana Oktoba 22, 2014.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Ujumbe wa UBA Tanzania ulioongozwa na aliyekuwa Mkurugenzi wake Mkuu mstaafu, General Robert Mbomba (kulia) wakati walipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, jana Oktoba 22, 2014.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa UBA Tanzania, baada ya mazunguzmo yao yaliyofanyika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, jana Oktoba 22, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa UBA Tanzania, General Robert Mboma, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

WAZIRI UMMY MWALIMU ATAKA HALMASHAURI YA KINONDONI KUSIMAMIA SHERIA ZA MAZINGIRA

0
0
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Mhandisi Mussa Natty(kushoto) akizungumza na Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu wakati wa ziara ya kujifunza masuala ya usimamizi wa taka zinazozalishwa katika halmashauri hiyo.
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Mhandisi Mussa Natty (kushoto) akizungumza na Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu wakati wa ziara ya kujifunza masuala ya usimamizi wa taka zinazozalishwa katika halmashauri hiyo.Kulia ni wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na watendaji wa halmashauri hiyo.
 Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu, akizungumza na watendaji wa kata za manispaa ya Kinondoni(hawapo pichani) wakati wa ziara hiyo.Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Mhandisi Mussa Natty.
 Badhi ya watendaji wa kata mbalimbali za manispaa ya Kinondoni wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu, wakati alipotembelea kujifunza masuala ya usimamizi wa taka zinazozalishwa katika halmashauri hiyo.

 Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu (katikati) akiongozwa na Mwenyekiti wa soko la Tandale, Sultan Kiumbo kuingia kwenye ofisi ya soko hilo, wakati alitembelea kujifunza changamoto za mazingira zinazolikabili soko hilo.
 Mwenyekiti wa soko la Tandale, Sultan Kiumbo, akmueleza jambo Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu, wakati alipotembelea soko hilo kujifunza changamoto za mazingira.
 Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu, akisalimiana na mama lishe katika soko la Tandale jijini Dar es Salaam, wakati alipotembelea soko hilo kujifunza changamoto za mazingira.
 Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu, akizugumza na muuza mbogamboga kujua jinis anavyoshughulikia taka anazozalisha kwenye soko la Tandale jijini Dar es Salaam, wakati alipotembelea soko hilo kujifunza changamoto za mazingira.
Mwenyekiti wa soko la Tandale, Sultan Kiumbo, akimuonesha Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu, mabaki ya matunda yalitupwa, wakati alipotembelea soko hilo kujifunza changamoto za mazingira. Picha zote na Hussein Makame-MAELEZO

TASWIRA ZA SIKU YA KWANZA YA ZIARA YA RAIS KIKWETE NA MAMA SALMA KIKWETE NCHINI CHINA

0
0

 Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiwapungia wafanyakazi wa Hoteli ya Diaoyutai ya mjini Beijing mara baada ya kuwasili…
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea ua kutoka kwa mfanyakazi wa Hoteli ya Diaoyutai iliyoko Beijing mara baada ya kuwasili hotelini hapo. Mama Salma ameambatana na mumewe Rais Dkt. Jakaya Kikwete ambaye amewasili nchini China tarehe 21.10.2014 kwa ziara ya kiserikali.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa pamoja na Bwana Yang Hua, Mmoja wa viongozi wakuu wa China National Offshore Oil Corporation (CNOOC), wakisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mwenyekiti wa Shirika hilo Bwana Wang Yilin kwa Rais Dkt. Jakaya Kikwete alipotembelea makao makuu ya Shirika hilo yaliyoko Beijing nchini China tarehe 22.10.2014. Shirika hilo hujishughulisha na utafiti wa mafuta na gesi baharini, uchimbaji na uuzaji wa maliasili hizo.
 Rais Dkt. Jakaya Kikwete na Mwenyekiti wa China National Offshore Oil Corporation Bwana Wang Yilin wakizindua rasmi mtambo mpya wa utafutaji wa mafuta na gesi baharini, Uzinduzi huo ulifanyika kwenye Makao Makuu ya Shirika hilo huko Beijing tarehe 22.10.2014.
 Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiongoza ujumbe wa Tanzania unaozuru nchini China wakiangalia vifaa mbalimbali vinavyotumiwa na Shirika la  CNOOC la China katika kazi ya utafutaji wa mafuta na gesi baharini wakati walipotembelea Makao Makuu ya Shirika hilo huko Beijing tarehe 22.10.2014.
 Rais Dkt. Jakaya Kikwete akishirikiana na Mkewe Mama Salma Kikwete na Professa Li Songshan (kushoto kwa Rais Kikwete), Mwanzilishi wa Kijiji cha Sanaa cha Afrika kuondoa kitambaa ikiwa ni ishara ya kufungua rasmi kijiji hicho kilichopo katika wilaya ya Songzhuang nchini China tarehe 22.10.2014.
 Vifijo baada ya ufunguzi wa Kijiji cha Sanaa cha Afrika kuondoa kitambaa ikiwa ni ishara ya kufungua rasmi kijiji hicho kilichopo katika wilaya ya Songzhuang nchini China tarehe 22.10.2014.
 Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiangalia baadhi ya ngoma za asili ya Afrika zilizokuwa zikipingwa na vijana wa kichina mara baada ya ufunguzi rasmi wa kituo cha sanaa za Afrika huko Songzhuang tarehe 22.10.2014.
 Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiandika kumbukumbu yake katika kitambaa maalum mara baada ya kuzindua rasmi Kijiji cha sanaa za Afrika. Mke wa Rais Mama Salma Kikwete anaonekana wa kwanza kushoto akifuatiwa na Professa Li Singshan. Kulia kwa Rais Kikwete ni Dkt. Han Rong, Mke wa Professa Li na Mwanzilishi mwenza wa Kijiji hicho na wa kwanza kushoto ni Bwana Joseph Kahama.
 Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiandika kumbukumbu yake katika kitambaa maalum mara baada ya kuzindua rasmi Kijiji cha sanaa za Afrika. Mke wa Rais Mama Salma Kikwete anaonekana wa kwanza kushoto akifuatiwa na Professa Li Singshan. Kulia kwa Rais Kikwete ni Dkt. Han Rong, Mke wa Professa Li na Mwanzilishi mwenza wa Kijiji hicho na wa kwanza kushoto ni Bwana Joseph Kahama.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiandika kumbukumbu yake kwenye kijiji cha sanaa za Afrika mara baada ya Rais Dkt. Kikwete kuandika kumbukumbu yake.
Waanzilishi wa Kijiji cha Sanaa za Afrika Professa Li Songshan na Mke wake Dkt. Han Rong wakimkabidhi zawadi ya mchoro wa  Tingatinga Rais Dkt. Jakaya Kikwete na Mke wake mara baada ya ufunguzi rasmi wa kijiji hicho tarehe 22.10.2014. Picha na John Lukuwi

UK TRADE & INVESTMENT LONDON/SOUTH EAST TRADE MISSION TO TANZANIA

0
0
Untitled
David Bilingsby, Head of the UK Trade & Investment (UKTI) London/South East Trade Mission to Tanzania fields questions from journalists during a press conference held yesterday at Serena Hotel. On his left is Bikash Dawahoo, Regional Economics Advisor (Photo courtesy of the British High Commission).

14 UK companies cutting across various sectors e.g. Education and Training, Security, Consultancy, Healthcare amongst others are hoping to penetrate new trade opportunities within Tanzania by taking part in UKTI London and South East trade mission to Tanzania between October 22nd-24th 2014. This is the first, independent visit by UKTI London and South East to Tanzania and East Africa.

Tanzania is fast emerging as a thriving commercial entity with a GDP growth rate of over 7% year upon year. The major city of Dar es Salaam where we will be staying is the centre of most government activity as well as being the major commercial centre with its own deep water port with trading links to the landlocked countries of Malawi, Zambia, Democratic Republic of Congo, Burundi, Rwanda and Uganda.

Tanzania not only has some of the best wildlife in the world but also huge natural resources ranging from gemstones to natural gas. As such, it is fast becoming the regional hub for a number of multinational corporations. This will be an exciting opportunity for UK businesses to see what they can bring to the country.
Untitled 1
Victor Mlunde, Senior Political Advisor at the British High commission explains a point at a press conference held at Serena yesterday. On his left is Bikash Dawahoo, Regional Economics Advisor and David Bilingsby, Head of the UK Trade & Investment (UKTI) London/South East Trade Mission to Tanzania (Photo courtesy of the British High Commission).


As part of the programme which is being organised by UKTI in Tanzania, the delegates will have a first-hand opportunity to meet and speak with local trade associations and their members e.g. the Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) and the Tanzania National Chamber of Commerce and Industry (TNCCI) and the newly set-up British Chamber of Commerce Tanzania (BCCT). They will also have a chance to speak directly with business at a Business to Business event scheduled for Thursday, 23rd October at the Serena Hotel from 1.00 to 4.00pm. We believe this will create a great opportunity for the visiting companies to meet and discuss business directly with business. 

David Billingsby, UKTI International Trade Adviser, who will lead the London delegation, said:
“Having worked in Tanzania before, I know the excellence of the reception these British companies will receive. I am certain that the mission will be successful and the delegates will be saying Asante sana!”
Untitled 2
Bikash Dawahoo, Regional Economics Advisor at the British High Commission, Dar es Salaam explains a point to members of press during a press conference on the UK Trade & Investment (UKTI) London/South East Trade Mission to Tanzania held yesterday at the Serena Hotel in Dar Es Salaam (Photo courtesy of the British High Commission).
The delegation will include the following companies who will then relocate to Kenya for 26th-30th October:

Edward Munyard - Eagle Scientific Carl Gibbard - Concept Smoke Screen Ltd Mike Thompson - tph Machine Tools Sudhir Patel - Velmo International Christine Meade - GSVO Hanaa Chattun - Lacaze Adam Hersi - Haad Logistics Ltd Chris Stephenson & Dan Olal - McKinney Rogers Peter Charnaud & William Charnaud - Scott & Sargeant Woodworking Machinery Umair Munir - MAP IT Services Robert Magembe - InterVAS Limited UK William Rhys-Jones - Cobham Tactical Communications & Surveillance Joy Okwuadigbo - Highbury College Nemish K Mehta - e-tel (uk) ltd
Untitled 3
Some of the local and international business people listen to the Head of the UK Trade & Investment (UKTI) London/South East Trade Mission to Tanzania, David Bilingsby (not in picture) as he clarifies a point to members of press. On extreme right is Fatuma Kweka, Trade Officer at the UK Trade and Investment (UKTI) department at the British High Commission, Dar Es Salaam (Photo courtesy of the British High Commission).
Untitled 4
A cross section of members of press listen keenly to the Head of Head of the UK Trade & Investment (UKTI) London/South East Trade Mission to Tanzania, David Bilingsby (not in picture) as he clarifies a point (Photo courtesy of the British High Commission).

KANUNI ZA SHIRIKISHO LA WANAFUNZI WA VYUO VYA ELIMU YA JUU TANZANIA.

0
0


Rich Mavoko kunogesha shoo ya Instagram Part Zanzibar

0
0
NA ANDREW CHALE.
 
MSANII nyota nchini, Richard Martin maalufu Rich Mavoko anatarajiwa kutumbuiza kwenye shoo kali na ya aina yake ya Instagram Part Zanzibar itayofanyika ndani ya Zanzibar Beach hotel, Novemba Mosi  mwaka huu.
 
Kwa mujibu wa wandaaji wa shoo hiyo kampuni ya Bond Entertainment, kupitia kwa msemaji wa kampuni hiyo Mackson Madoro  alieleza kuwa kila kitu kipo sawa kwa ajili ya tukio hilo  ambayo mpaka sasa wadau na wapenzi wa burudani wakiwemo wa ndani na nje ya Visiwa hivyo wanaisubiria kwa hamu kubwa.
 
“Novemba Mosi ambayo itakuwa siku ya Jumamosi, kwa mara ya kwanza, Msanii Rich Mavoko atapiga shoo ya aina yake katika Instagram Part Zanzibar. Hii itakuwa ni kwa mara ya kwanza tokea kwa msanii huyo atoe wimbo wake wa ‘Pacha wangu’  unayotamba kwa sasa” Alisema Madoro.
Kwa upande wake msimamizi wa shoo, Dhamir  Ramz Jr  alieleza kuwa mbali na msanii huyo kutoa shoo pia kutakuwa na wageni maarufu mbalimbali watakaojumuika kwa pamoja na kupiga piucha  kwenye zulia jekundu na watu watakaoudhulia siku hiyo.
 
“Instagram Part Zanzibar hii si ya kukosa kwani itakuwa na ‘surprise’ za kila aina kutoka kwa watu maarufu watakaopiga picha na wapenzi wa burudani na marafiki watakaojitokeza siku hiyo” alieleza Ramz Jr.Ramz Jr aliongeza kuwa, shoo hiyo inayotarajiwa kuanzia majira ya mchana  mpaka usiku, ni ya watu wote ambapo ulinzi na usalama umezingatiwa kwa kiwango kikubwa na kuwaomba wajitokez kwa wingi huku kiingilio ikiwa ni sh 10,000 kwa kila mmoja.
 
 ambapo pia kutakuwa na zawadi  kkutoka kwa wadhamini kwa watu wa mwanzo watakaoingia kwenye siku hiyo ambayo itakuwa ni ya kihistoria kwa kukutana kwa marafiki na kubadilishana mawazo.Kampuni ya  Bond Entertainment, imekuwa ikijihusisha na masuala ya kuendeleza  tasnia ya sanaa kupitia muziki na wasanii mbalimbali kupitia kazi zao na kuandaa matamasha kwa wasanii wa ndani na nje.
 
“This event aims to entertain and bring together users of the social network INSTAGRAM with emphasis to creating a conducive environment for all instagrammers to meet and exchange their ideas in social networking and bring awareness with regards to the power of the social media in providing information first hand in all issues including social, political and economic platforms. 
 
It is only a once in a life time event to meet your fellow instagrammers  from diffrent parts of the country. Don't miss it!The first  attendants will be presented with a special  gift .. exclusively designed for the event. Be there!!”

SHEREHE ZA MIAKA 50 YA USHIRIKIANO WA KIDIPLOMASIA KATI YA TANZANIA NA CHINA HUKO BEIJING

0
0
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Ndugu Li Yuanchao wakati walipokutana kwenye Sherehe ya kutimiza Miaka 50 ya Uhusiano wa Kidiplomasia baina ya Tanzania na China. Sherehe hizo zilizoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini China na kufanyika jijini Beijing leo
 Makamu wa Rais wa China Ndugu Li Yuanchao akigonganisha  glasi ikiwa ni ishara ya kusherehekea kutimiza miaka 50 ya ushirikiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na China. Sherehe hizo zilifanyika jijini Beijing 
 Rais Dkt. Jakaya Kikwete akigonganisha glasi na  Mama Salma wakisherehekea kutimiza miaka 50 ya ushirikiano wa Kidiplomasia kati ya Tanzania na China.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Ndugu Bernard Membe wakisherehekea kutimiza miaka 50 ya Ushirikiano wa Kidiplomasia baina ya Tanzania na Cina kwa kugonganisha glasi zao huku Mama Salma na Makamu wa Rais wa China Ndugu Li Yuanchao (aliyesimama kulia)  wakishuhudia. Sherehe hizo zilifanyika Beijing nchini China leo. PICHA NA JOHN  LUKUWI

KAMATI YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA MAZINGIRA YATEMBELEA ENEO LA TANGANYIKA PAKERS AMBAPO NHC INATEKELEZA MRADI WA YUMBA WA (KAWE CITY)

0
0
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Felix Maagi akiiongoza Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira wakati ilipotembelea eneo la mradi wa nyumba ambao unatarajiwa kuanza katika uwanja wa kulenga shabaha wa jeshi la wananchi Kunduchi, baada ya makubaliano kati ya jeshi la wananchi na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). 

Kamati hiyo ikiongozwa na mwenyekiti wake na jimbo la Kahama Mbunge Mh. James Lembeli na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka ilitembelea eneo hilo ili kujiridhisha na kujionea hali halisi na kupata maelezo ya kina kabla ya kuanza kutekelezwa kwa mradi huo. Kulia ni Mjube wa Kamati hiyo Mh. Hamud Jumaa na Mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini, kulia ni James Lembeli Mbunge wa Kahama na Mwenyekiti wa kamati hiyo.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM) 2Isaack Peter Mkurugenzi wa Ubunifu Shirika la Nyumba la Taifa NHC akielekeza jambo wakati alipokuwa akionyesha eneo hilo kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka na wajumbe wa kamati hiyo wakati alipotembelea eneo hilo huku Kunduchi.3Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Mazingira na Maliasili Mh. Hery Shekifu akifafania jambo huku Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mh. James Lembeli wakimsikililiza4Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mh. James Lembeli akizungumza jambo wakati kamati hiyo ilipotembelea eneo la kulenga shabaha la jeshi Kunduchi, kulia ni Mama Zakhia Megji Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Nyumba NHC na kushoto ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka5Baadhi ya watendaji na maofisa wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC wakiwa katika picha ya pamoja kwenye uwanja wa Kulenga Shabaha wa jeshi Kunduchi ambao kwa sasa matumizi yake yanabadilisha na kuwa mradi wa nyumba za Shirika la Nyumba la NHC.
7Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi , Maliasili na Mazingira wakishuka kwenye gari mara baada ya kuwasili katika eneo la Tanganyika Pakers ambapo mradi wa Kawe City unatarajiwa kuazishwa na shirika hilo la NHC.8Huu ndiyo uwanja wa Kulenga Shabaha wa jeshi Kunduchi mahali ambapo sasa panaanzishwa mradi wa nyumba za NHC.9Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka akishuka kwenye gari mara baada ya kuwasili katika eneo la Tanganyika Pakers Kawe jijini Dar es salaam leo.10Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira na mbunge wa Kahama Mh. James Lembeli akishuka kwenye gari katika eneo la Tanganyika Pakers mahali ambapo patatekelezwa mradi wa Kawe City unaofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa NHC.12 
Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mh. James Lembeli katikati ni mjumbe wa kamati hiyo na Mbunge wa jimbo la Lushoto Mh. Hery Shekifu 13Isaack Peter Mkurugenzi wa Ubunifu Shirika la Nyumba la Taifa NHC akendelea kutoa maelezo kwa kamati hiyo wakati ilipotembelea katika eneo la Tanganyika Pakers Kawe.14Wajumbe wa kamati hiyo wakipata maelezo kabla ya kuanza ziara yao leo katika makao makuu ya shirika la Nyumba la Taifa NHC Upanga jijini Dar es salaam.15Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mh. James Lembeli akizungumza wakati kamati hiyo ilipokuwa ikipata maelezo ya awali kabla ya kutembelea maeneo yatakapotekelezwa miradi hiyo mikubwa ya makazi , Kushoto ni Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka na kutoka kulia ni Mh. Mary Mwanjelwa mjumbe wa kamati hiyo na mbunge wa viti maalum Mbeya mjini na Mh. Abdulkarim Shah Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo na na Mbunge wa Mafia.17 
Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Nyumba la NHC Mh. Zakhia Megji, Bw. Felix Maagi Kaimu Mkurugenzi wa NHC na Mbunge wa jimbo la Ubungo na mjumbe wa kamati hiyo Mh. John Mnyika ambaye naonekana akitoa mchango wake wakati wa wajumbe hao walipokuwa wakipata taarifa ya awali..

FLAVIANA MATATA FOR THE GLAMOURAI MAGAZINE

0
0
NI MWANAMITINDO FLAVIANA MATATA AFANYAYE KAZI ZAKE NCHINI MAREKANI SAFARI HII KATOKELEZEA KWENYE JARIDA THE GLAMOURAI MAGAZINE AKINADI MAPAMBO image (2)image (3)image (4)image (5)image (6)image (7)image (8)image

WAZIRI MKUU AKARIBISHA WAWEKEZAJI WA POLAND

0
0
*Wengi wajitokeza katika sekta za kilimo, afya, madini, nishati na hoteli
 WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewasili nchini Poland kwa ziara ya siku mbili ya Kiserikali ambayo inalenga kuwavutia wafanyabiashara wa nchi hii waje kuwekeza Tanzania.

Mara baada ya kuwasili jijini Warsaw, akitokea London Uingereza, Waziri Mkuu jana jioni (Alhamisi, Oktoba 23, 2014) alikutana na wafanyabiashara zaidi ya 50 kwenye mkutano uliofanyika kwenye ofisi za Chama cha Wafanyabiashara cha Poland (Polish Chamber of Commerce).

Katika Mkutano huo, Waziri Mkuu aliwaeleza mipango ya Serikali ya kuikwamua Tanzania kiuchumi huku akigusia sekta za kilimo, uvuvi, uchukuzi, miundombinu, madini, nishati na utalii.

“Nia ya ziara yangu fupi lakini yenye malengo mahsusi ni kuamsha mahusiano baina ya nchi zetu mbili lakini zaidi ni kutafuta mbinu za kukuza biashara kati ya Tanzania na Poland. Nataka muione Tanzania kama mahali salama pa kuwekeza mitaji yenu, mahali rafiki pa kuweka mitaji lakini pia mahali pa kufanya biashara ambayo pia itahusisha uwekezaji,” alisema.

Katika mkutano huo Waziri Mkuu alijibu maswali kutoka kwa wafanyabiashara zaidi ya 10 ambao walikuwa na shauku ya kutaka kufahamu ni maeneo yapi zaidi yanayohitaji uwekezaji.

Pia aliishukuru Serikali ya Poland kwa kusaidia ukarabati na uimarishaji wa miundombinu kwenye Chuo cha Maendeleo ya Jamii cha Tengeru, kilichopo Arusha.

Mapema akimkaribisha Waziri Mkuu kuongea na wafanyabiashara hao, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland anayeshughulikia masuala ya Afrika na Mashariki ya Kati, Bibi Katarzyna Kacperczyk alisema nchi hiyo imeanzisha mpango maalum ujulikanao kama “Go Africa” ambao umelenga kukuza mahusiano ya kiuchumi na bara la Afrika.

“Tukiwa ndani ya Jumuiya ya Ulaya, pamoja na hatua kubwa za kiuchumi tunazokwenda nazo, kama Serikali tuliamua kwa dhati kwamba hatuwezi kuwaacha ndugu wetu wa iliyokuwa Ulaya Mashariki kabla ya mageuzi ya kiuchumi duniani... lakini tumeamua kuangalia bara la Afrika kama mdau muhimu wa maendeleo lakini pia kama soko la uhakika kwa bidhaa tunazozalisha,” alisema.

Alisema mpango huo umeanzisha mahsusi ili kuwasaidia wafantabiashara wa Poland kupata taarifa sahihi na haraka kuhusiana na masuala ya ushirikiano na uwekezaji barani humo.

Alisema wameanzisha mpango huo ili kuwahamasisha wenye makampuni barani Afrika waone kuna wenzao wa Poland na waamue kushirikiana katika kulijenga bara la Afrika.

Waziri Mkuu leo atatembelea kampuni ya Rol Brat inayotengeza zana za kisasa za kilimo yakiwemo matrekta na mashine za kuvuna mazao mazao mashambani. Pia atatembelea kampuni ya “Mtynpol” ambayo inahusika na ujenzi wa maghala ya kuhifadhia vyakula na miundombinu yake.

Kesho asubuhi atakutana na Watanzania waishio Poland na baadaye kufanya vikao na baadhi ya wafanyabiashara wa jijini Warsaw.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, OKTOBA 24, 2014
Viewing all 46205 articles
Browse latest View live




Latest Images