Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

TAARIFA KUTOKA JENZI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ)

$
0
0

JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO

Simu ya Upepo   : “N G O M E”            Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo : DSM  22150463       Sanduku la Posta 9203,
Telex                     : 41051                        DAR ES SALAAM, 20 Octoba, 2014
Tele Fax                : 2153426
Barua pepe       : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti                  : www.tpdf.mil.tz
                  
Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linatoa taarifa kwa wananchi wote kuwa ni kosa kisheria kumiliki au kuvaa sare za JWTZ kwa mtu yeyote asiyehusika.
          Aidha,  kumeonekana matukio kadhaa ya baadhi ya vikundi, ama mtu mmoja mmoja kumiliki au kuvaa sare za JWTZ.  Inakumbushwa kuwa kwa yeyote atakayeonekana amevaa ama kumiliki sare hizo sheria itachukua mkondo wake. 

  
Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na  Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0783 - 309963

GAIDI MKUU WA ULIPUAJI WA MABOMU AWAWA ARUSHA NA POLISI

$
0
0

Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha,Liberatus Sabas
 

Kiongozi wa  matukio ya ulipuaji wa mabomu na umwagiaji tindikali viongozi wa dini aliyejulikana kwa jina la Yahaya Hassani Omary ameuwawa na jeshi la polisi wakati alivyokuwa akijaribu kukimbia.



Akithitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoani Arusha  Liberatus Sabas  Alisema kuwa tukio hilo limetokea  October 19 majira ya saa tano na nusu  katika barabara ya babati mkoani Arusha wakati alipokuwa akijaribu kuwakimbia polisi.



Alisema kuwa mtuhumiwa huyo wa ugaidi alishikiliwa wiki mbili zilizopita  huko mkoani Morogoro  mara baada ya kutafutwa kwa muda mrefu na hapo jana alikuwa akipelekwa wilayani kondoa mkoani Dodoma  kwa ajili ya kwenda kuonyesha sehemu ambazo alikuwa ameficha mabomu mengine.

"mtuhumiwa huyu alikuwa anasakwa kwa muda mrefu bila mafanikio kwani alikuwa akai sehemu moja ila jeshi la polisi huko mkoani morogoro lilimkamata wiki mbili zilizopita na baada ya kufanyia mahojiano alisema ameficha mabomu mengine huko kondoa na jana alikuwakipelekwa kuonyesha ndipo alipotumia trikizake ambazo amefundishwa za ugaidi kwa kupiga gudo na kutaka kuwakimbia askari ndio akapigwa risasi mbili"alisema Sabas



Alitoa wito kwa wananchi kuendelea kuwafichua waovu  ili kuwaza kuteketeza matukio ya uhalifu
habari kwa hisani ya woindeshizza blog

REDIO 5 WAWAKUTANISHA WANASALAMU KUTOKA MIKOA ZAIDI YA 21,WAFANYA ZIARA KUWAONA WAGONJWA MT.MERU

$
0
0
SAM_0706Baadhi ya Wanasalamu wa kituo cha Redio 5 chenye makao yake makuu njiro jijini Arusha wakikabidhi sehemu ya msaada wao kwa uongozi wa hospitali ya mkoa Mt.meru jana,kulia ni mratibu wa salamu kupitia kipindi cha usiku wa moto Yacob Simba kushoto ni Sista Shubi Mjawizi,anayefatia ni Sista Merry Stalla
SAM_0705Yacob Simba akiongea na baadhi ya wanasalamu katika viwanja vya hospitali ya Mt.Meru anayefatia ni Godfrey Thomas ambao ni waratibu wa shughuli hiyo kupitia kituo cha Redio 5 katika kipindi usiku wa moto kinachorushwa kwanzia saa saba usiku hadi kumi na moja alfajiri kwa wiki nzima
SAM_0710Yacob Simba akikabidhi ndoo ya mafuta  kwa uongozi wa hospitali ya Mt.Meru jana baadaa ya wanasalamu kutoka mikoa zaidi 21 kufika hospitalini hapo kuwafariji wagonjwa
SAM_0696
Vicky Mwakoyo ambaye ni Creative Meneja wa kampuni ya  Tan Communication Media inayomiliki kituo cha Radio 5 Arusha,katikati ni Yacob Simba  na Godfrey Thomas wakiwa wanajadili jambo
SAM_0690Kulia ni Lucy Bongole ambaye ni mwanasalamu wakiwa wanajadiliana na wenzake katika viwanja vya hospitali ya Mt.Meru katikati ni Zuhura Mbise maarufu kwa jina la mama Sosy,kushoto ni Sister Monduly
SAM_0691Wanasalamu wakiwa wanajadiliana
SAM_0692Sehemu ya msaada uliotolewa na wanasalamu kwa wagonjwa hospitali ya Mt.Meru jijini Arusha.
SAM_0703Kushoto Mtangazaji maarufu wa Redio 5 kupitia kipindi chake cha  love cuts kinachorushwa jumatatu hadi ijumaa saa nne  hadi saa saba usiku Semio Sonyo  akiwa na mtangazaji machachari aliyejizolea umaarufu mkubwa kupitia kipindi chake cha usiku wa Moto kinachorushwa kwanzia saa saba usiku hadi kumi na moja alfajiri kwa wiki nzima  Godfrey Thomas aka GT wakifurahia jambo
SAM_0715Nesi wa hospitali ya Mt.Meru Sista Merry Stella akitoa neno la shukrani kwa wanasalamu waliofika kuwatembela wagonjwa hospitalini hapo ambapo amewataka watu na mashirika mbalimbali kuiga mfano huo kwa kuwa mahitaji ya wagonjwa ni makubwa
SAM_0721Muonekano katika hospitali ya Mt.Meru jijini Arusha
SAM_0794Wanasalamu wakiwa wamevalia T-sheti za Redio 5
SAM_0776Wapili kulia ni mmiliki wa jamiiblog Pamela Mollel wakwanza kushoto ni Godfrey Thomas aka GT wakiwa katika picha na baadhi ya wanasalamu jana zoezi hilo liliratibiwa na kituo cha Redio 5 kupitia kipindi cha usiku wa moto
SAM_0728Baadhi ya wanasalamu wakisubiria kuingia katika wodi mbalimbali kuwajulia hali wagonjwa hospitalini hapo
SAM_0730"Pole mama Mungu atakuponya"hayo ni maneno ya wanasalamu
SAM_0734Yacob Simba mtangazaji wa Redio 5 akiwa anamjulia hali mama mgonjwa katika wodi ya wanawake
SAM_0741Mwanasalamu mkongwe kutoka Arusha Baba Ali Mbondei(aliyevalia tisheti ya Redio 5)akiwa na wanasalamu wenzake wakimjulia hali mgonjwa katika wodi ya wanaume
SAM_0742Wanasalamu wakiwa wanasoma dua kwa mgonjwa wodi ya wanaume katika hospitali ya Mt.Meru jijini Arusha
SAM_0746Wanasalamu wakiwa wanaingia wodi ya saba kuwaona wagonjwa
SAM_0752Godfrey Thomas  aka GT katikati akiwa amepozi na mashabiki wake ambao ni wanasalamu kupitia kipindi cha usiku wa moto cha kituo cha Redio 5 jijini Arusha
SAM_0749
Wanasalamu kutoka mikoa mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja katika viwanja vya hospitali ya Mt.Meru mara baada ya kufanya ziara ya kuwatembelea wagonjwa (Habari Picha na Pamela wa Jamiiblog)

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGA MKUTANO MKUU WA WANACCM WILAYA YA ILALA JIJINI DAR

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wanachama wa CCM, wakati alipokuwa akifunga mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ilala, uliofanyika jana Oktoba 19, 2014 kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na baadhi ya viongozi wa CCM Wilaya ya Ilala kuimba wimbo maalum wa Chama wakati Dkt. Bilal, alipokuwa akifunga rasmi Mkutano mkuu wa CCM wa Wilaya hiyo jana Oktoba 19, 2014 kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wanachama wa CCM Wilaya ya Ilala, wakiimba na kushangilia kwa furaha wakati walipokuwa wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia alipokuwa akifunga rasmi Mkutano Mkuu wa wanachama wa CCM Wilaya ya Ilala.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Wanachama wa CCM wakati akiondoka kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, jana Oktoba 19, 2014 baada ya kufunga rasmi Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Ilala. Picha na OMR

Chibuku Super yadhamini Uhuru Marathon 2014

$
0
0
Mratibu wa Mbio za Uhuru Marathon,Innocent Melleck (kulia) akizungumza na waandishi wa habari katika dhifa ya kukabidhiwa hundi ya shilingi milioni sita kwaajili ya udhamini wa mbio hizo,ambapo wamedhamini mbio za km 5. kushoto ni meneja usambazaji na mauzo wa Darbrew,Fred Kazindogo.

KAMPUNI ya Bia za asili ya Darbrew (TBL) kupitia bia yake ya asili ya Chibuku super imetangaza kudhamini mashindano ya mbio ndefu za Uhuru ‘Uhuru Marathon’ kwa kiasi cha Sh.  milioni 6.

Akitangaza udhamini huo jana jijini Dar es Salaam, Meneja mauzo na usambazaji wa Darbrew Fred Kazindogo, alisema, wameona ni vyema kudhamini mbio hizo kwa sababu zina lengo la kuimarisha umoja, amani na mshikamano miongoni mwa Watanzania.

Telecom executive launches Leadership book

$
0
0
A Tanzanian based telecommunications executive , Norman Moyo , CEO of Helios Towers Tanzania launched his first leadership book  called Rumble in the Jungle , Leadership from an African perspective . The launch which was attended by more than 300 of some of the top corporate and civic leaders in Tanzania was officiated by the Minister of Communications , Science and Telecommunications .

In his remarks the minister thanked Mr Moyo for being a bold and exemplary business leader who has taken this unchanted route of sharing his Pan African experience with other leaders . He further highlighted commented that “the challenges of leadership in corporate , social and public institutions across the continent is a subject of great debate at many different forums regionally and globally . The call for good leadership is a call which has been getting louder and louder by the day here in Tanzania and across the continent . I am very encouraged to see a new crop of Pan African business leaders beginning to engage in being part of their destiny”  

The minister went on to read a quote from His Excellency former President Benjamin Mkapa , who sent a congratulatory letter to Mr Moyo after reading his leadership book . Mr Mkapa wrote  “There is a lot of talk at African Leaders meetings and academic forums about the Africa we want in the next fifty years. Little is however described, let alone published, about HOW we are to get there. Indeed there is little exposition about the obstacles on the way forward. Your book strives to fill this important gap.” 

“I have appreciated it in particular because it has identified the one factor holding back African development and transformation, namely LEADERSHIP. There is a crying need on all African development fronts for a transformative Leadership – leadership with Conviction ,Vision, Mission and Driving Capacity.”

Speaking also at the book launch at Hyatt , Former Tanzanian Ambassador to the United States , Ambassador Mwanaidi Maarjar, congratulated Mr Moyo and highlighted that “This event for me marks the birth of a new idea, a renaissance, a new chapter in the Pan African agenda. Your corporate journey across all the 4 corners of the continent, starting in Southern, West, Central, North and East Africa has exposed you to a very unique view of the continent very few of us has seen. 

But most importantly it seems to have been a great source of inspiration for you particularly the untapped potential the continent possess. I can not over agree with you that the number one biggest economic driver for this continent is not its oil, gas, gold, diamonds but LEADERSHIP. This is not a new idea to any of us here but you have simply taken the conversation out of the intellectual realm of debates , and endless 50 year programs with realist and proven execution strategy.”

The book is targeted to be marketed across the whole continent and reputed to create a new set of conversations in the continent.  It is primarily targeting middle to senior managers in corporates and also senior civil servants , ministers and presidents across the continent. The launch was followed by an unprecedented purchase of the books  including personalized autographs  by the author .  A number of CEOs purchased books for their organisations after a moving speech from the author himself.

RATIBA YA MAANDALIZI YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA NDANI YA CHAMA CHA CCM

NHC Yatumia shilingi milioni 731,360,000/= kusaidia miradi ya vijana nchini

$
0
0
Na Jonas Kamaleki

NHC Yatumia shilingi milioni 731,360,000/= kusaidia miradi ya vijana nchini
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limetumia jumla ya shilingi milioni 731,360,000/= kusaidia miradi ya vijana ya kufyatua tofali nchini.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kitengo cha Huduma na Mawasiliano wa NHC, Bi Suzan Omari wakati wa Kikao kazi cha Maafisa Vijana kilichofanyika hivi karibuni mkoani Tabora.

Bibi Suzan amefafanua kuwa fedha hizo  zinahusisha ununuzi wa mashine uliyogharimu shilingi 297,000,000/=, mafunzo ya wakufunzi yaliyogharimu shilingi 47,000,000/= na  uwezeshaji mtaji wa kuanzia kazi za vikundi vya vijana kufyatua matofali shilingi 81,500,000/=.

Ameongeza kuwa matumizi mengine kuwa ni usambazaji wa mashine uliyogharimu shilingi 30,000,000/=, uhakiki wa ubora wa mashine uliofanywa na wataalamu kutoka VETA shilingi 6,400,000/=, fedha za kununulia vifaa vya mafunzo katika kila halmashauri vilivyogharimu shilingi 130,400,000 na posho ya wakufunzi wa VETA ni shilingi 139,060,000/=.

Bi Suzan amewataka vijana kote nchini kutumia fursa hii kwa ajli ya maendeleo yao ikiwemo na kuondokana na tatizo la kukukosa ajira. Amayetaka mashirka mengine nchini kuiga mfano wa NHC ili kunusuru nguvu kazi hii kubwa. 

Kwa upande mwingine, Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC, Bw, Muungano Saguya amesema kuwa wadau zikiwemo Halmashauri, Maafisa Vijana wa Mikoa na wilaya kwa kushirkiiana na mamameneja wa mikoa wa NHC wathamini mradi huu kwa kufuatilia ufanisi wake ili mradi huo uwe endelevu.

Ameongeza kuwa mradiukiwa endelevuna kusaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana, bajeti itaongezeka kwa mwaka wa fedhaujao ilikusaidia zaidi mradi huo kwa vijana.

Naye  Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa Mkoa wa Tabora, Bw. Erasto Chilambo amesema maafisa vijana wawaunganishe vijana katik a vikundi ili watumie fursa hii kujiendeleza na kuacha kubweteka na kulalamika kwa kukosa ajira. Aliongeza kuwa vijana  wasiwe sehemu ya tatizo la ajira bali wawe  watatuzi wa changamoto inayowakabili ya kukosa ajira.

Kikao hiki ni kikao cha kuwakumbusha maafisa vijana majukumu yao  kuwasaidia kupata uzoefu toka kwa wenzao. Kimeandaliwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

WAKULIMA WA ZAO LA SHAYIRI WATEMBELEA KIWANDA CHA KIMEA CHA TBL MOSHI

$
0
0
MENEJA wa Kiwanda cha Kimea – Moshi, Vitus Mhus akiwaonyesha hatua ya kwanza ya zao la Shayiri linalotumika kutengenezea kimea mahali linapopokelewa kabla ya kuanza kuingizwa kiwandani.Wakulima hao kutoka Vyama Nane vya Ushirika vya wilaya ya Karatu na Monduli mkoani Arusha walitembelea kiwandani hapo hapo juzi ili kujifunza na kujionea zao wanalolima linaandaliwa vipi hadi kutengeneza KimeaWakulima wa zao la Shayiri kutoka Vyama Nane vya Ushirka vya wilaya ya Karatu na Monduli mkoani Arusha wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kusikiliza maelezo namna ya kulima Shayiri yenye ubora kutoka kwa Meneja  Mradi Kilimo cha Shayiri Dk. Basson Bennie. Wakulima hao walifurahia ziara iliyofanywa kwenye Kiwanda cha kuzalisha Kimea kilichopo mjini Moshi ambapo waliahidi kulima Shayiri yenye ubora zaidi katika msimu ujao.Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Bia nchini (TBL), Edith Mushi akiwapa maendelekezo wakulima wa zao la Shayiri waliotembelea Kiwanda cha kuzalisha Kimea mjini Moshi namna ya kutembelea ndani ya kiwanda ili wajionee namna Shayiri inavyozalishwa na kuwa Kimea.Wakulima hao wanatoka kwenye vyama Nane vya Ushirika vilivypo wilaya ya Karatu na Monduli mkjoani ArushaMeneja wa Kiwanda cha Kimea-  Moshi Vitus Mhusi akiwaonyesha wakulima wa Shayiri waliofanya ziara ya kutembelea kiwanda hicho namna uchafu unavyochambuliwa kutoka kwenye Shayiri wanayolima mashambani, ambapo aliwaomba kujitahidi kuhakikisha inakuwa safi wakati wa mavuno.Pichani ni Meneja wa Kiwanda cha Kimea kilichopo mjini Moshi akiwaonesha wakulika kutoka Vyama vya Ushirika Nane vya Wilaya ya Karatu na Monduli wanaolima Shayiri namna ambavyo uzalishaji wa kimea unavyofanyika, wakati wa ziara yao.Meneja wa Kiwanda cha Kimea kilichopo Moshi, Vitus Mhusi akiwaonyesha wakulima wa Shayiri namna Kimea kinavyozalishwa wakati wa ziara yao kiwandani hapo. Vingozi hao wa Vyama vya Ushirika Nane kutoka wiayani Monduli na Karatu mkoani Arusha walitembelea kiwandani hapo kwa leng la kujifunza zaidi namna ya kulima zao la Shayiri lenye ubora zaidi na hata kufikia mahitaji ya kiwanda ya Tani 12,000

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA 14 WA WATAALAM WA HUDUMA ZA HABARI NA MAKTABA ZA AFYA AFRIKA (AHILA) JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0
01
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati akifungua rasmi Mkutano wa 14 wa Wataalam wa Huduma za Habari na Maktaba za Afya Afrika (AHILA) uliofanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 20, 2014. Picha na OMR 
02
03
Baadhi ya wadau wa mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akiwahutubia  alipokuwa akifungua rasmi Mkutano wa 14 wa Wataalam wa Huduma za Habari na Maktaba za Afya Afrika (AHILA) uliofanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 20, 2014. Picha na OMR
03B
Baadhi ya wadau wa mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akiwahutubia  alipokuwa akifungua rasmi Mkutano wa 14 wa Wataalam wa Huduma za Habari na Maktaba za Afya Afrika (AHILA) uliofanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 20, 2014. Picha na OMR
04
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene, akizungumza kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kufungua Mkutano wa 14 wa Wataalam wa Huduma za Habari na Maktaba za Afya Afrika (AHILA) uliofanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 20, 2014. Picha na OMR
05
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo, mshiriki wa mkutano huo kutoka nchini Zimbabwe, aliyepokea kwa niaba ya Gilchriste Ndongwe,  wakati wa ufunguzi  rasmi wa Mkutano wa 14 wa Wataalam wa Huduma za Habari na Maktaba za Afya Afrika (AHILA) uliofanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 20, 2014. Picha na OMR
06
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo, mshiriki wa mkutano huo kutoka nchini Tanzania, Montea Chipungahelo,  wakati wa ufunguzi  rasmi wa Mkutano wa 14 wa Wataalam wa Huduma za Habari na Maktaba za Afya Afrika (AHILA) uliofanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 20, 2014. Picha na OMR
07
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo, mshiriki wa mkutano huo kutoka nchini Nigeria, aliyepokea kwa niaba ya Samuel Bello,  wakati wa ufunguzi  rasmi wa Mkutano wa 14 wa Wataalam wa Huduma za Habari na Maktaba za Afya Afrika (AHILA) uliofanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 20, 2014. Picha na OMR
10B
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Mkutano huo baada ya ufunguzi rasmi. Picha na OMR
10
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene na baadhi ya waratibu wa mkutano huo wakati akiondoka eneo hilo baada ya kufungua rasmi mkutano huo leo . Picha na OMR

UKAGUZI WA BARABARA YA TUNDUMA - SUMBAWANGA

$
0
0
 Kaimu Meneja wa wakala wa Barabara Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Masuka Nkina (wa kwanza kulia mwenye shati jeupe) akitoa maelezo juu ya utendaji kazi wa mizani ya Nkangamo katika barabara ya Tunduma – Laela- Sumbawanga. Utendaji wa mizani hiyo ni kwa kutumia kompyuta ambapo mteja anachapishiwa risiti yake hapo hapo inayoonyesha taarifa zake zote. Kama mzigo utakuwa umezidi pia risiti hiyo itaonyesha faini anayotakiwa kulia.
 Mhandisi Julius Isoka ambaye ni Mhandisi Mshauri wa Barabara ya  Tunduma- Sumbawanga kutoka kampuni ya Nicholous Odweyer akiwaelezea timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ambao wanatembelea barabara hiyo jinsi ambavyo daraja linasukwa kutoka chini mpaka juu.  Barabara hii inajengwa kwa ufadhili wa Watu wa Marekani chini ya Mradi wa Milleniam Challenge (MCC).
 Daraja la Kashahanzi moja ya daraja kubwa na linalojengwa kwa umahiri mkubwa katika barabara ya Tunduma  –Sumbawanga.  PICHA ZOTE NA JOYCE MKINGA

Benki ya Exim yaahidi kuunga mkono juhudi za serikali kuboresha hali ya magereza nchini

$
0
0
Wafanyakazi wa Benki ya Exim tawi la Mwanza na wawakilishi wa gereza la Butimba wakiwa katika picha ya pamoja, muda mfupi baada ya Benki hiyo kukabidhi vifaa vya usafi  kwa gereza la Butimba lililopo jijini Mwanza hivi karibuni. Mchango huo ni sehemu ya shughuli za kibenki za kijamii lakini pia ukilenga kusaidia wafungwa kubadili tabia.

Exim Bank imeahidi kuendelea kusaidia juhudi za serikali katika kuboresha hali ya magereza nchini, ikiwa ni sehemu ya shughuli zake za kibenki za kijamii. Benki iyo imekabidhi vifaa vya usafi kwa wanawake wanaotumikia vifungo katika gereza la Butimba jijini Mwanza, hatua inayolenga kuwasaidia na kuwaelimisha wanawake hao kubadili tabia.

Akizungumza katika hafla fupi iliyofanyika katika gereza la Butimba jijini Mwanza hapo jana, Mkuu wa Matawi wa Benki ya Exim Mwanza, Bw. Justus Mukuras alisema mchango huo utawasaidia kwa kiasi kikubwa wafungwa walio katika gereza hilo. Alisema mbali na mchango wa vifaa hivyo, benki hiyo iliajiri mwanasaikolojia ambaye alizungumza na wanawake hao na kuwapa faraja pamoja na kuwafundisha mbinu mbalimbali za maisha. Lengo likiwa kuwafanya kuwa mfano bora katika jamii zao pindi watakaporudi uraiani.

 “Hii ni sehemu ya shughuli zetu za kijamii na hatulengi kuishia hapa, hizi ni jitihada endelevu zilizo chini ya kampeni ya benki yetu ya kusaidia wafungwa wa kike nchini. “Pamoja na mambo mengine, kampeni hiyo inalenga kuwafundisha wafungwa mbinu mbalimbali za maisha na kuwafanya wawe watu bora zaidi. Tutaendelea kuwasaidia vifaa vya usafi pamoja na vifaa vingine kwa watoto wanaoishi na mama zao katika magereza,” alisema Bw. Mukuras.

Wafungwa wengi nchini wanakabiliwa na uhaba wa vifaa vya usafi pamoja na vyakula; hii inatokana na idadi kubwa ya wafungwa katika magereza hali inayopelekea mlipuko wa magonjwa.

 “Sisi kama benki tungependa kutekeleza jukumu letu la kusaidia jamii hususani wanawake wanaotumikia vifungo katika magereza pamoja na watoto wanaoishi na mama zao katika magereza hayo kwani baadhi yao wanakabiliwa na upungufu wa virutubisho na afya duni. Ukipata nafasi ya kuingia katika magereza ndipo utakapobaini idadi ya matatizo wanayokumbana nayo,” aliongeza Bw. Mukuras.

Tamasha la Handeni Kwetu lawapigia magoti wadhamini

$
0
0
 
WADAU wa mambo ya utamaduni yakiwamo mashirika, makampuni na watu mbalimbali wameombwa kujitokeza kuliwezesha tamasha la Handeni Kwetu 2014, lililopangwa kufanyika Desemba 13 mwaka huu wilayani Handeni, mkoani Tanga.

Tamasha hilo linafanyika huku mwaka jana likiwezeshwa kwa kiasi kikubwa na Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa ushirikiano na wadau mbalimbali walioliwezesha tamasha hilo kwa mara ya kwanza katika Historia ya Mkoa wa Tanga.

Akizungumza mjini hapa, Mratibu Mkuu wa Tamasha hilo, Kambi Mbwana, alisema kuwa wadhamini wakijitokeza kwa wingi kutaongeza chachu ya maendeleo ya nchi, sanjari na sanaa ya utamaduni inayotakiwa kuungwa mkono na watu wengi.

Alisema kuwa kitendo cha wadhamini kuendelea kuliunga mkono Tamasha hilo kutachangia kwa kiasi kikubwa kuinua uchumi wa nchi pamoja na kutangaza utamaduni wa Mtanzania.

“Mwaka jana wadau wengi walijitokeza kuliwezesha tamasha la Handeni, wakiwamo NSSF, hivyo tunaomba msimu huu pia tuendelee kushirikiana kuliwezesha Tamasha la Handeni Kwetu litakalofanyika Desemba 13 mwaka huu, Handeni Mjini.

“Hadi wakati huu, walioonyesha nia ya kulisaidia tamasha la Handeni Kwetu 2014 ni pamoja na SmartMind & Partners iliyopo chini ya Anesa Co. Ltd kwa kupitia kitabu chao cha Ni Wakati wako wa Kung’aa, Phed Trans, chini ya Yusuphed Mhandeni, Handeni Kwetu Foundation, Wait & Watch Film Company Ltd, Qs Mhonda J Apex Group of Companies Ltd na Skyblue Security and Risk Mgt Ltd,” alisema Mbwana.
 
Tamasha la Handeni Kwetu ni miongoni mwa matukio makubwa ya kiburudani mkoani Tanga, ambako zaidi ya watu 500 walihudhuria tamasha hilo ambalo kwa mwaka huu mipango kabambe ya kuhakikisha kuwa linafanyika kwa mafanikio.

Dk Lyatonga Mrema akihutubia mkutano wa hadhara jimboni kwake vunjo

$
0
0
 Mbunge wa jimbo la Vunjo na Mwenyekiti wa chama cha TLP,Dk.Augustine Lyatonga Mrema akihutubia mkutano wake wa hadhara jimboni kwake  jana kwa ajili ya kuhamasisha uchaguzi wa serikali za mitaa na pia kuelezea utekelezaji wa miradi ya Maendeleo,aidha katika jimbo hilo la Vunjo kumekuwepo na Mvutano mkubwa kwa vyama vya CCM,Innocent Shirima na Mh.James Mbatia wa NCCR-Mageuzi.

Rais Kikwete aanza ziara rasmi ya China leo

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagwa na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange na IGP Ernest Mangu wakati akiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo tayari kuanza  ziara rasmi ya siku sita katika Jamhuri ya
Watu wa China kwa mwaliko wa Rais Xi Jinping.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Raymond Mushi wakati akiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo tayari kuanza  ziara rasmi ya siku sita katika Jamhuri ya Watu wa China kwa mwaliko
wa Rais Xi Jinping.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagwa na maafisa wa Ubalozi wa China nchini Tanzanioa  wakati akiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo tayari kuanza  ziara rasmi ya siku sita katika Jamhuri ya Watu wa China kwa mwaliko wa Rais Xi Jinping. PICHA NA IKULU


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete leo, Jumanne, Oktoba 21, 2014, anaanza ziara rasmi ya siku
sita katika Jamhuri ya Watu wa China kwa mwaliko wa Rais Xi Jinping,
ikiwa ni ziara yake ya pili nchini humo akiwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano.

Baada ya China, Rais Kikwete atafanya ziara rasmi ya siku tatu nchini
Vietnam kwa mwaliko wa Rais wa nchi hiyo.

Wakati wa ziara yake nchini China, Rais Kikwete ambaye aliondoka
nchini usiku wa jana, Jumatatu, Oktoba 20, 2014, atatembelea majimbo
matatu ya nchi hiyo, atafanya mazungumzo na viongozi wakuu wa China,
atashuhudia utiaji saini mikataba muhimu ya shughuli za maendeleo,
atatunukiwa shahada za heshima na atashiriki katika sherehe za miaka
50 tokea kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya Tanzania na
China.

Rais Kikwete amepangiwa kukutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji
wake, Rais Xi Jinping; Waziri Mkuu Mheshimiwa Li Keqiang pamoja na
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Watu wa China, Mheshimiwa Zhang Dejiang.

Rais Kikwete pia atashuhudia utiaji saini wa mikataba ya miradi ya
maendeleo ya Tanzania ambayo inasaidiwa ama inagharimiwa na fedha
kutoka China na pia atakutana kwa mazungumzo na wakuu wa taasisi
muhimu zinazogharimia baadhi ya miradi mikubwa ya maendeleo katika
Tanzania zikiwamo China-Africa Development Fund (CADB) na China
Development Bank (CDB).

Akiwa Beijing, Rais Kikwete atakutana na Mabalozi wa Afrika
wanaoziwakilisha nchi zao katika China, atafungua Mkutano wa Tatu wa
Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na China na atazindua rasmi
Kijiji cha Kiafrika.

Aidha, Rais Kikwete atatunukiwa uprofesa wa heshima na Chuo Kikuu cha
Kilimo cha China cha China Agricultural University na Chuo Kikuu cha
East China Normal University na pia atakuwa mwenyeji wa hafla maalum
ya kusherehekea miaka 50 ya uhusiano wa kibalozi kati ya Tanzania na
China. Uhusiano huo ulitimiza miaka 50, Aprili 26, mwaka huu, siku
ambako Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia ilitimiza miaka 50 ya
kuzaliwa kwake.

Baada ya kumaliza ziara yake Beijing, Rais Kikwete atatembelea Jimbo
la Jinan ambako atashuhudia maonyesho rasmi ya kijeshi ya Jeshi la
Ukombozi la Wananchi wa China la Chinese People’s Liberation Army
(PLA) lililoandaliwa rasmi kwa heshima yake. Hiyo itakuwa mara ya
kwanza katika historia kwa heshima ya namna hiyo kutolewa kwa kiongozi
wa nchi yoyote duniani, nje ya China.

Akiwa Jimbo la Jinan, Rais Kikwete pia atakutana na viongozi wa Jimbo
hilo na pia atakutana kwa mazungumzo na madaktari wa Kichina ambao
wamefanya kazi katika Tanzania katika miaka 50 iliyopita.

Baada ya Jimbo la Jinan, Rais Kikwete atakwenda  Jimbo la Shenzhen
ambako atatembelea makao makuu ya taasisi na makampuni makubwa ya
China ya Shenzhen Economic Zones Authority, China Merchants Holdings
International (CMHI), Huawei na ZTE. Shenzhen ndiko Watanzania wengi
wanaonunua bidhaa kutoka China hufanyia biashara zao.

Mara ya mwisho, Rais Kikwete alitembelea China mwaka 2008 wakati
alipoliwakilisha Bara la Afrika katika Mkutano wa Kwanza wa
China-Afrika katika nafasi yake wakati huo kama Mwenyekiti wa Umoja wa
Afrika (AU).

Imetolewa na;

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu – Dar es Salaam.

21 Oktoba,2014

Airtel yazindua wiki ya Rasilimali watu

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Airtel  Tanzania Bwn Sunil Colaso akiongea na wafanyazi wakati wa uzinduzi wa wiki ya Rasimali watu uliofanyika katika Ofisi za makao makuu ya  Airtel ambapo wafanyakazi watapata fulsa ya kupata elimu juu ya sera kuhusu mafao mbalimbali na haki yao
za kimsingi  na huduma nyinginezo zinazotolewa na kusimamiwa na kitengo cha Rasilimali  watu, hafla ya uzinduzi huo imefanyika katika ofisi za Airtel Moroko leo
 Baadhi ya wafanyakazi wa kitengo cha rasilimali watu cha Airtel Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja  wakati wa uzinduzi wa wiki ya Rasilimali watu iliyozinduliwa  rasmi jana katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar es saalam.
 Meneja Uajiri na vipaji wa Airtel Bi Gabriella Kaisi akiongea wakati wa uzinduzi wa wiki ya Rasilimali watu iliyozinduliwa  rasmi jana katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar es saalam, Pichani ni  manej katika kitengo cha rasilimali watu Airtel
 wafanyakazi wa Airtel wakifatilia uzinduzi wa  uzinduzi wa wiki ya Rasilimali watu iliyozinduliwa  rasmi jana katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar es saalam


 Meneja Rasilimali watu Airtel Bi Sophia Melamari akiongea wakati wa uzinduzi wa wiki ya Rasimali watu uliofanyika katika Ofisi za makao makuu ya  Airtel ambapo wafanyakazi watapata fulsa ya kupata elimu juu ya sera kuhusu mafao mbalimbali na haki yao za kimsingi  na huduma nyinginezo zinazotolewa na kusimamiwa na kitengo cha Rasilimali  watu, hafla ya uzinduzi huo imefanyika katika ofisi za Airtel Moroko leo
 Mkurugenzi wa Kitengo cha Rasilimali watu Airtel  Tanzania Patric Foya akiongea wakati wa zinduzi wa wiki ya Rasimali watu uliofanyika  katika Ofisi za makao makuu ya  Airtel ambapo wafanyakazi watapata fulsa ya kupata elimu juu ya sera kuhusu mafao mbalimbali na haki yao za kimsingi  na huduma nyinginezo zinazotolewa na kusimamiwa na kitengo cha Rasilimali  watu, hafla ya uzinduzi huo imefanyika katika ofisi za Airtel Moroko leo
 Mchekeshaji na mshereheshaji  maarufu kama MC Pilipili  akitoa burdani kwa wafanyakazi wa Airtel wakati wa uzinduzi wa wiki ya Rasimali watu iliyozinduliwa mahususi kwa wafanyakazi wa Airtel kupata elimu juu ya sera na huduma mbalimbali zinazotolewa na kusimamiwa na Kitengo cha Rasilimali watu, hafla ya uzinduzi huo imefanyika katika ofisi za Airtel Moroko leo
 Wafanyakazi wa Airtel wakifurahia burdani toka kwa Mchekeshaji na mshereheshaji  maarufu kama MC Pilipili  wakati wa uzinduzi wa wiki ya Rasimali watu iliyozinduliwa mahususi kwa wafanyakazi wa Airtel kupata elimu juu ya sera na huduma mbalimbali zinazotolewa na kusimamiwa na Kitengo cha Rasilimali watu, hafla ya uzinduzi huo imefanyika katika ofisi za Airtel Moroko leo.

TANZANIA YAJIVUNIA KUFIKIA MALENGO YA MILENIA KATIKA AFYA, ELIMU

$
0
0
DSC_0564
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, John Haule (kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wiki ya Umoja wa Mataifa inayotarajiwa kuanza kuadhimishwa Ijumaa wiki hii (kushoto) ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.

KATIBU MKUU wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, John Haule amesema serikali ya Tanzania imefikia kwa kiwango kikubwa baadhi ya malengo ya milenia ya afya na elimu. MOblog Tanzania inaripoti.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na MOblog Tanzania ofisini kwake jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza mkutano na wanahabari juu ya wiki ya Umoja wa Mataifa inayotarajiwa kuanza Ijumaa wiki hii, Haule amesema Tanzania imeyafikia kwa kiwango kikubwa malengo ya milenia katika afya na elimu.

 “Serikali ya awamu nne kwa kiwango kikubwa imefikia baadhi ya malengo ya milenia hasa katika elimu na afya kwa kujenga shule za msingi na sekondari katika kila kata na vituo vya afya nchi nzima,” amesema Haule.
Amesema kwamba Serikali ya Tanzania itaendelea kushirikiana kwa karibu na Umoja wa Mataifa katika kufikia maendeleo katika kila nyanja duniani.

Aliongeza kwamba ni muhimu nchi zote duniani kuendelea kushirikiana kwa pamoja ili kuhakikisha maendeleo yanayopatikana yanapatikana kwa pamoja na hakuna nchi inayoachwa nyuma. Haule alisisitiza kwamba katika kuadhimisha wiki ya Umoja wa Mataifa serikali itaendelea kutoa ufafanuzi kwa wananchi umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika kila jambo linalofanya na Umoja wa Mataifa.

“Umoja wa Mataifa unatimiza miaka 69 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1945 mafanikio mengi yamepatikana na changamoto bado zipo nyingi lakini nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa wataendelea kushirikiana na umoja huu kutimiza lengo kuu la maendeleo dunia nzima,” alifafanua
DSC_0574
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, John Haule akiteta jambo na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.

Amesema kwamba katika mpango mkakati wa Umoja wa Mataifa juu ya malengo mapya ya kuanzia mwaka 2015-2030 serikali imejipanga kuhakikisha malengo hayo yanafikiwa kwa kiwango kikubwa.

Kwa upande wake, Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, amesema kwamba Umoja wa Mataifa itaendelea kushirikiana na nchi zote wanachama ikiwemo Tanzania katika harakati za kuondoa umaskini.

“Malengo ya milennia yamefanya nchi nyingi wanachama kufanya kazi kwa bidii katika kupunguza umaskini wa kipato, fursa ya elimu na upatikanaji wa matibabu kwa njia nafuu kwa maelfu ya watu duniani,” Aliongeza kwamba katika kauli mbiu ya Umoja wa Mataifa ya kuhakikisha kwamba hakuna mtu anayeachwa nyuma katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii inalenga kuwakutanisha pamoja nchi zote katika kila hatua ya maendeleo dunia nzima.

Rodriguez amesema kwamba Umoja wa Mataifa na malengo yake ni kuhakikisha usawa wa kiuchumi na kijamii unafikiwa katika jamii pana iliyo huru kwa kumshirikisha kila mtu katika maamuzi ya maendeleo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais akutana na Wabunge wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira Mhe. Dkt. Injinia Binilith Satano Mahenge (aliyesimama), akizungumza na Wabunge wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, kuhusu Utekelezaji wa Sheria ya Mazingira katika Migodi ya Bulyankulu, North Mara, Geita na Buzwagi, wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Ummy Mwalimu, akiwa pamoja na Mbunge wa Mafia, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe. Abdulkarim Hassan Shaha(wa pili kulia).
 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Ndg. Sazi Salula (wa katikati), akiwa pamoja na Naibu Katibu Mkuu Inginia Anjelina Madete (wa kwanza kushoto) wakifuatilia kwa makini hotuba inayotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Muheshimiwa Dkt. Injinia Binilith Satano Mahenge (hayupo pichani).
 Baadhi ya Wabunge wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira,wakifuatilia hotuba inayotolewa na  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Muheshimiwa Dkt. Injinia Binilith Satano Mahenge (hayupo pichani).
 

SIKU YA MSANII KUFANYIKA JUMAMOSI IJAYO MLIMANI CITY JIJINI DAR-ES-SALAAM.

$
0
0
 Ofisa Uhusiano wa Siku ya Msanii Tanzania (SYM), Bw. Peter Mwendapole akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Siku ya Msanii Tanzania itakayofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City siku ya tarehe 25 Oktoba, 2014 jijini Dar es Salaam.
Mwimbaji wa muziki wa taarabu, Bi.  Isha Ramadhan maarufu kama Mashauzi akiongea na waandishi wa habari kuhusu Siku ya Msanii Tanzania itakayofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City siku ya tarehe 25 Oktoba, 2014 jijini Dar es Salaam.
 
PICHA ZOTE NA MAGRETH KINABO, MAELEZO)
 
 
Na Beatrice Lyimo- Maelezo.

20/10/2014.

KAMATI ya Siku ya Msanii Tanzania (SYM) imetangaza rasmi majina ya wasanii watakaotumbuiza katika maadhimisho ya siku hiyo itakayofanyika Oktoba 25 mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City uliopo jijini Dar Es Salaam.

Akizingumza na waandishi wa habari leo jijini Dar Es Salaam, Ofisa Uhusiano wa SYM,  Bw. Peter Mwendapole amesema kuwa, kutokana na siku hiyo kuwa ni ya Sanaa zote, Kamati imeangalia uwakilishi wa sanaa za aina mbalimbali ili ziweze kuwakilisha siku hiyo katika historia ya Tanzania.

“Leo tungependa kuwatangaza Wasanii watatu wa Bendi ya Kilimanjaro Wana Njenje wenye vionjo vya Tanzania na Wawakilishi wa kundi la Wanamuziki wakongwe”, alisema Mwendapole.

Mwendapole alisema kuwa, kwa upande wa sanaa kuatkuwa na msanii maarufu kama Isha Mashauzi ambaye atawakilisha fani ya muziki wa jukwaani na upande wa Taarabu, kwani msanii huyo ameweza kufanya mapinduzi makubwa kwenye muziki wa taarabu pamoja na kuweka vionjo mbalimbali vya dansi, asili na taarabu.

Aliongeza kuwa, kutakuwa na kikundi cha sanaa kijulikanacho kama Ako Mpiruka Sound, bendi ya muziki, kikundi cha ngoma, kikundi cha sarakasi, wacheza Yoga na pia kutakuwa na shoo ya muziki wa dansi pamoja na dansi za mitaani.

Amebainisha kuwa, vijana wanaocheza muziki mitaani wakiwezeshwa wanaweza kujiajiri na kupunguza idadi kubwa ya watu ambao hawana ajira.“Siku ya msanii tunataka kuonyesha jinsi gani wanenguaji wana uwezo wa kucheza bila ya kuonyesha maungo yao”, alisisitiza Mwendapole.

Akifafanua kuhusu kiingilio cha siku hiyo ya msanii alisema kuwa, kiingilio hicho kitakuwa ni shilingi 70,000 kwa VIP na 50,000 kwa viti vya kawaida.Siku ya msanii inaandaliwa na kampuni Haak Neel Production (T) Ltd kwa kushirikiana na Baraza la Sanaaa la Taifa (BASATA) na kudhaminiwa na New Habari (2006) LTD kupitia magazeti ya Bingwa, Dimba, The African, na Mtanzania.

Wadhamini wengine wa SYM pamoja na PSPF, Azam Media, EFM, Magic FM, Clouds FM, Channel Ten, CXC, Ledger Plaza Hotel pamoja na Proin Tanzania.

Lundenga azungumzia sakata la umri wa Miss Tanzania 2014

$
0
0
 Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga (kati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya sakata la umri halali wa Mrembo alietwaa taji hilo Mwaka huu, Sitti Abbas Mtemvu (kushoto),katika mkutano huo Lundenga alitolea ufafanuzi swala la umri wa Mrembo huyo kulingana na vilelezo alivyopewa na mrembo huyo wakati akijiunga na mashindano hayo 

"Katika mashindano ya yetu,Washiriki wote hujaza fomu maalum zilizoandaliwa na Kamati ya Miss Tanzania,katika fomu alizojaza mrembo wa Miss Tanzania 2014 Sitty Abbas Mtemvu amejaza tarehe yake ya kuzaliwa ambayo ni Mei 31,1991 na hivyo kuwa ni sahihi kushiriki mashindano yetu" Alisema Lundenga mbele ya wanahabari hao.

Lundenga aliendelea kusema kuwa Mashindano ya Miss Tanzania hayaruhusu mshiriki yeyote mwenye mtoto kushiri,hivyo katika swala la Sitti Mtemvu kuwa ana mtoto,hilo kalina ukweli wowote bali ni uvumi tu wa kwenye mitandao ya kijamii baada ya Mrembo huyo kuonekana akiwa katika picha na mtoto alieomba kupiga nae.
 Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga akionyesha nakala ya cheti cha kuzaliwa cha Mrembo Sitti Mtemvu alicholetewa na wakazazi wake.
 Nakala halisi ya Cheti hicho inayoonyesha Mrembo huyo amezaliwa Mei 31,1991.
Miss Tanzania 2014,Sitti Abbas Mtemvu akizungumza machache na waandishi wa habari. video ya alichokisema Miss Tanzania itawajia muda si mrefu.
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images