Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live

NYUMBA ZINAPANGISHWA

0
0
 Sehemu ya mbele.

 ENEO:      Nyumba ipo  PUGU-Umbali wa  mita 100  toka  Barabara Kuu ya lami.

               Nyumba  3 za familia zipo ndani  ya  eneo  moja  kila  moja  inajitegemea.

UKUBWA: Kila  moja  ina vyumba  3 vya kulala, jiko, siting room kubwa na daining ya kutosha.
 UMEME:  Kila  moja  inatumia  Mita  ya Luku kwa kujitegemea.  pamoja  na  maji.

 PAKING:  Eneo kubwa kwa zaidi ya magari 5 kwa wakati mmoja.

BEI.  Ni maelewano kuanzia miezi  miezi  6  au zaidi kutegemea hitaji la mteja.

 kwa mawasiliano: 0686-569999

     Wako  katika makazi bora na ya kisasa. 

KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA CCM CHAENDELEA MJINI DODOMA LEO

0
0

 Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipanga makabrasha tayari kuendesha kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ambapo masuala ya kujiendesha kiuchumi na mipango ya maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa yanajadiliwa.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa NEC mjini Dodoma ambapo aliwaeleza juu ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana Oktoba 16, 2014 katika siku ya kwanza ya kikao chake cha siku mbili kinachoendelea mjini Dodoma chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete imejadili na kupitisha Sera ya CCM ya kujitegemea kimapato na kiuchumi. 

MKURUGENZI MKAZI WA UNESCO AMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA LEO

0
0
DSC_0206
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (katikati) akiongoza na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mtungi (kulia) baada ya kuwasili ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi. Kushoto ni Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al Amin Yusuph.
DSC_0209
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi akimkaribisha ofisini kwake Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues alipomtembelea na kufanya naye mazungumzo. Kushoto ni Msajili wa Vyama vya Siasa nchini. Jaji Francis Mtungi na kushoto ni Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al Amin Yusuph na Nyuma kabisa ni Msajili Msaidizi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Sisty Leonard Nyahoza.
DSC_0232
Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Rehema Nchimbi alipomtembelea leo na kufanya nae mazungumzo juu masuala mbalimbali ya maendeleo likiwemo suala la elimu na changamoto zake katika mkoa wa Dodoma.
DSC_0237
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mtungi (wa pili kulia) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi (kushoto), Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues (wa pili kushoto) pamoja na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al Amin Yusuph, Msajili Msaidizi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Sisty Leonard Nyahoza walipomtembelea Mkuu huyo wa mkoa ofisini kwake leo.
DSC_0248
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (wa pili kushoto) akitoa maelezo ya kazi mbalimbali zinazofanywa na shirika lake ikiwemo Mradi wa Micro Science Kits (MSKs) ulioendeshwa kwa miaka minne wa kusaidia ufundishaji wa masomo ya sayansi kwa kufanikisha majaribio ya maabara uliokuwa ukifadhiliwa na Shirika lake na kuendeshwa na Wizara ya Elimu nchini katika shule 180 zilizopo katika wilaya 34 ambao umemalizika hivi karibuni kwa mafanikio makubwa.
DSC_0280
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi katika picha ya pamoja na ugeni huo ofisini kwake mjini Dodoma leo.
DSC_0330
Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues akisisitiza jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi alipokuwa akigana nae mara baada ya mazungumzo ofisini kwake mjini Dodoma.

NAIBU WAZIRI WA AFYA ATOA TARIFA YA UZINDUZI WA CHANJO YA KUZUIA SURUA NA RUBELLA KWA WANDISHI WA HABARI.

0
0
 Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Wizara hiyo Mnazimmoja kuhusu uzinduzi wa chanjo ya kuzuia Surua na Rubella kwa watoto utakaofanyika kesho Oktoba 18 katika kijiji cha Uroa Mkoa Kusini Unguja.
 Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria mkutano wa Naibu Waziri wa Afya uliozungumiza uzinduzi wa chanjo ya kuzuia Surua na Rubella itakayoanza kesho kijiji cha Uroa.
 Mratibu wa chanjo Zanzibar Yussuf Haji Makame akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari namna chanjo hiyo itakavyoendeshwa nchi nzima kwa muda wa wiki moja kuanzia kesho. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

Makala: Rais Kikwete apongeza Kuanzishwa kijiji cha Pathifinder Green City Tabora

0
0

TAMASHA LA FIESTA LAFANA,DAVIDO,ALI KIBA,DIAMOND WAZUA GUMZO KWA MASHABIKI,T.I AWAKUNA WABONGO

0
0
Mmoja wa askari waliokuwa wamepangwa katika suala zima la kusimamia usalama ndani ya tamasha la Fiesta 2014 akihakikisha usalama wa kutosha unakuwepo katika eneo hilo,na watazamaji wanapata burudani iliyokusudiwa kutoka kwa wasanii mbalimbali waliotumbuiza usiku wa kuamkia leo katika tamasha la Fiesta 2014 lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika viwanja vya Lidaz Kinondoni jijini Dar.
Shaa na madansa wake wakilishambulia jukwaa. 
Pichani kulia ni Msanii kutoka nchini Nigeria ajulikanae kwa jina la Kisanii Davido sambamba na Diamond Platnum kwa pamoja wakilishambulia jukwaa la fiesta 2014 usiku wa kuamkia leo.
Msanii kutoka THT,Barnaba akiimba wimbo wake wa Wahalade sambamba na madansa wake kwenye jukwaa la fiesta 2014,katika viwanja vya Lidaz Kinondoni jijini Dar.
Sehemu ya  umati wa watu waliokuwa wakishuhudia yaliyokuwa yakijiri kwenye jukwaa la Fiesta usiku wa kuamkia leo katika viwanja vya Lidaz Kinondoni jijini Dar.
Ilikuwa ni shoo moja nzuri kutoka nyumba ya vipaji ya THT
Pichani msanii Linah (nyeupe) akiwa na skwadi lake mara baada kumaliza kulishambulia jukwaa kwa pamoja.
Anaitwa Ally kiba ambaye inaelezwa kutoka kwa mashabiki  kuwa alifanyo shoo nzuri na iliyowavutia,na kuthibitisha uwezo wake kuwa ni kweli amerejea kwenye kiti chake cha usanii.
  Msanii kutoka nchini Marekani Clifford Haris a.k.a T.I akilishambulia jukwaa la Fiesta vilivyo
 Msanii kutoka nchini Marekani T.I akiwaimbisha mashabiki wake

HILI NDILO TAMKO LA CHADEMA KUHUSU MCHAKATO WA KATIBA MPYA

0
0
MAAZIMIO YA KAMATI KUU YA CHA396300_216970381724652_100002350745009_483378_1721045790_nMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO KUHUSU MCHAKATO WA KATIBA NA KURA YA MAONI KUHUSU KATIBA INAYOPENDEKEZWA
Dar es Salaam, Oktoba 16, 2014
UTANGULIZI
Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) imekutana katika kikao chake cha kawaida na kujadili, pamoja na mambo mengine, mchakato wa Katiba Mpya. Kamati Kuu imepata taarifa ya kina juu ya mchakato ulivyoendeshwa katika hatua mbali mbali wakati wa kutungwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na marekebisho yake na, baadaye, Sheria ya Kura ya Maoni.
 Aidha, Kamati Kuu imepata taarifa ya mchakato ulivyokuwa katika hatua ya kuundwa kwa Tume ya Mabadiliko, kukusanya maoni ya wananchi na kuandaliwa kwa Rasimu ya Kwanza na ya Pili ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Vile vile, Kamati Kuu imepata na kujadili taarifa ya kina juu ya mchakato wa Katiba katika hatua ya uteuzi wa Bunge Maalum na baadaye ndani ya Bunge hilo. Mwisho Kamati Kuu imepata uchambuzi wa kina wa Katiba Inayopendekezwa iliyopitishwa na Bunge Maalum tarehe 2 Oktoba, 2014.
Uchambuzi huo utatolewa kwa vyombo vyote vya habari na kwa wananchi wa Tanzania kama taarifa hapo baadae.
Baada ya mjadala mrefu na wa kina, Kamati Kuu imeridhika kwamba mchakato wa Katiba katika hatua zake zote ulitawaliwa na nia mbaya iliyokuwa na lengo kuu la kuhakikisha kwamba hakuna mabadiliko yoyote ya maana yatakayofanyika kwenye mfumo wa kikatiba na kiutawala ambao umekuwepo katika nchi yetu kwa zaidi ya miaka hamsini.
  • Mchakato wa kutunga Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ulitawaliwa na ubabe na usiri uliohakikisha kwamba mchakato wa Katiba unadhibitiwa na Serikali na Chama cha Mapinduzi;
  • Uteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalum kutoka ‘Kundi la 201’ ulifanywa na Rais Jakaya Kikwete kwa lengo la kuhakikisha wajumbe wengi zaidi wa Kundi hilo wanatoka CCM na washirika wake. Kwa sababu hiyo, zaidi ya asilimia 82 ya wajumbe wa Bunge Maalum kutoka Kundi la 201 walikuwa wanachama wa CCM waliochomekwa katika makundi na taasisi mbali mbali;
  • Sambamba na idadi hiyo ya wajumbe wa Kundi la 201, asilimia 72 ya wajumbe wa Bunge Maalum waliotokana na Kundi la Wabunge na Wawakilishi wa Zanzibar walikuwa wanachama wa CCM;
Katika hatua ya mjadala ndani ya Bunge Maalum, Kamati Kuu imeridhika kwamba mjadala huo ulitawaliwa na ukiukwaji wa wazi wazi wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na Kanuni za Kudumu za Bunge Maalum.
  • Bunge Maalum lilijigeuza ‘Tume’ na kuanza kukusanya upya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya, wakati kazi ilikwisha kufanywa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba;
  • Muda wa kuwasilisha taarifa za Kamati mbali mbali ulifupishwa kutoka dakika sitini hadi dakika ishirini na ule wa kuwasilisha maoni tofauti ulifupishwa kutoka dakika thelathini hadi dakika kumi;
  • Utaratibu wa kupiga kura juu ya Katiba Inayopendekezwa kwa njia ya kifungu kwa kifungu uliondolewa na badala yake kura zilipigwa kwa ujumla ya Sura za Rasimu, yaani kura zilipigwa kwa Sura kumi za mwanzo na baadae kwa Sura tisa mwisho;
  • Wajumbe waliokuwa nje ya Ukumbi wa Bunge, au nje ya Dodoma na hata waliokuwa nje ya nchi kwa sababu mbali mbali kama vile mahujaji na wagonjwa waliruhusiwa kupiga kura ya kupitisha Katiba Inayopendekezwa;
  • Kura za wajumbe waliopinga baadhi ya vifungu vya Katiba Inayopendekezwa na kukubali vifungu vingine zilihesabiwa kuwa kura za kukubali Katiba Inayopendekezwa;
Katika mazingira haya, mambo ya ajabu na yenye kuifedhehesha nchi yetu yaliyotokea ndani ya Bunge Maalum yasingeacha kutokea.
  • Wajumbe Waislamu waliokwenda Makkah kuhiji na ambao uongozi wa Bunge Maalum ulieleza mwanzoni kwamba wangepiga kura kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia hawakupiga kura Ubalozini na haijulikani walipigia wapi kura zao. Aidha, sasa inajulikana kwamba Mahujaji hao – kama ni kweli walifanya hivyo – walipiga kura siku moja kabla ya siku rasmi ya upigaji kura kwenye Bunge Maalum;
  • Licha ya Waheshimiwa Mohamed Raza na Salim Turky – wote wa kutoka Zanzibar – kuharibu kura zao, kura hizo zilizoharibika zilihesabiwa kuwa kura halali za ‘Ndiyo’;
  • Kura za wajumbe waliokufa kama vile Marehemu Shida Salum zilihesabiwa kuwa kura halali za ‘Ndiyo’;
  • ‘Kura za Maruhani’, yaani wajumbe wa UKAWA kutoka Zanzibar na za Wazanzibari wengine waliojitoa na ambao hawajulikani majina yao hadi sasa zilihesabiwa kuwa kura halali za ‘Ndiyo’;
  • Mheshimiwa Maulida Komu wa UKAWA ambaye alitajwa kwenye Gazeti la Serikali lililotangaza majina ya wajumbe wa Bunge Maalum kuwa anatoka Zanzibar aligeuzwa na kuhesabika kuwa anatoka Tanzania Bara, wakati Mheshimiwa Zakia Meghji wa CCM aliyetangazwa kwenye Gazeti la Serikali kuwa anatokea Tanzania Bara alihesabika kuwa anatoka Zanzibar na hivyo kupiga kura ya ‘Ndiyo’ kama Mzanzibari;
  • Kura za partly ‘Hapana’ na partly ‘Ndiyo’ zilizopigwa na wajumbe wanne wa kutoka Zanzibar zilihesabika kuwa ni kura za ‘Ndiyo.’
Kamati Kuu imeridhika kwamba, katika mazingira haya, theluthi mbili ya kura za Zanzibar isingeacha kupatikana. Katika mazingira haya, na kwa kipimo chochote, Kamati Kuu imeridhika kwamba upigaji kura ya kupitisha Katiba Inayopendekezwa ulikuwa batili – na matokeo ya upigaji kura huo – yaani Katiba inayopendekezwa haiwezi kuwa halali.
Na katika mazingira haya, ujasiri unaostahili kupongezwa wa Mwanasheria wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, na wajumbe wengine nane wa Zanzibar waliopiga kura ya wazi ya ‘Hapana’ kuikataa Katiba Inayopendekezwa licha ya shinikizo kubwa, matusi na vitisho vya kila aina, usingeweza kuzuia uharamia huu wa CCM.
Kwa hali hii, Kamati Kuu inaungana na vyama vingine vya siasa vya UKAWA, taasisi kuu za kidini nchini kama vile Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC), Baraza la Kikristo Tanzania (CCT), Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT), Shura ya Maimamu, Baraza Kuu la Taasisi za Kiislamu, n.k. kulaani matukio yote yaliyotokea wakati wa mchakato wa Katiba katika hatua zake zote hadi sasa. Kamati Kuu inapondeza na kuunga mkono taasisi, mashirika na vyama vya siasa pamoja na wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba waliosusia tukio la Rais Kikwete kukabidhiwa Katiba Inayopendekezwa siku ya tarehe 8 Oktoba, 2014.
Aidha, Kamati Kuu inatoa rai kwa taasisi na mashirika yasiyokuwa ya kiraia ambayo tayari yameshaonyesha msimamo wa kuiunga mkono Katiba Inayopendekezwa kujifikiria upya na kujiridhisha kama mashirika yao hayatumiki kuhalalisha mambo haramu ambayo yamefanywa na CCM na washirika wao katika mchakato huu.
Kamati Kuu imeazimia kwamba CHADEMA itaungana na vyama na taasisi zilizotajwa hapa pamoja na umma wa Watanzania wenye nia njema na taifa kuhakikisha kwamba wanashiriki katika kampeni kubwa na ya nchini ili kuhakikisha kwamba Katiba Inayopendekezwa inapigiwa kura ya ‘Hapana’ katika kura ya maoni, ambayo ni hatua ya mwisho ya mchakato wa Katiba.
Katika hili, Kamati Kuu inatoa rai kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuhakikisha kwamba inatekeleza ahadi yake kwa Watanzania kwamba Daftari la Kudumu la Wapiga Kura litaboreshwa kabla ya kufanyika kwa kura ya maoni ili kuhakikisha kwamba kila Mtanzania mwenye haki ya kupiga kura anajiandikisha kwenye Daftari hilo na anapata haki ya kushiriki katika maamuzi ya jambo hili muhimu kwa taifa letu.
Kamati Kuu inawakumbusha Watanzania kujiandaa kutimiza wajibu wao wa kihistoria wa kukataa uchakachuaji wa maoni yao uliofanywa na CCM na washirika wake katika Bunge Maalum. Kukataa uchakachuaji huu kitakuwa ni kitendo cha kizalendo cha kila Mtanzania. Kunyamazia au kuunga mkono uchakachuaji huu itakuwa ni kuisaliti nchi yetu na kuendeleza utawala wa kikandamizaji na wa kifisadi ambao umekuwa janga la taifa letu kwa miaka mingi.
——————————————————-
Dr. Willibrod P. Slaa
KATIBU MKUU

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHUDHURIA SHEREHE YA KUWEKWA WAKHFU ASKOFU MTEULE WA KANISA LA AFRICAN INLAND DAYOSISI YA MWANZA, MCHUNGAJI JOHN BUNANGO, JIJINI MWANZA.

0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana nabaadhi ya viongozi wa dini ya Kikristu, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo, Oktoba 19, 2014, kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za kuwekwa Wakhfu Askofu Mteule wa Kanisa la African Inland Dayosisi ya Mwanza, Mchungaji John Bunango, iliyofanyika jijini humo leo mchana.
 Maaskofu wakimwekea mikono ya Baraka Askofu mwenzao, Askofu Mteule wa Kanisa la African Inland Dayosisi ya Mwanza, Mchungaji John Bunango, wakati akiwekwa Wakhfu katika sherehe zilizofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo, Oktoba 19, 2014
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia waumini wa dini ya Kikristu, waliohudhuria katika Sherehe za kuwekwa Wakhfu Askofu Mteule wa Kanisa la African Inland Dayosisi ya Mwanza, Mchungaji John Bunango, zilizofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, leo Oktoba 19, 2014
 Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza Askofu Mteule wa Kanisa la African Inland Dayosisi ya Mwanza, Mchungaji John Bunango, baada ya kuwekwa Wakhfu katika sherehe zilizofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo Oktoba 19, 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa dini ya Kikristu na wanafamilia ya Askofu  Mteule wa Kanisa la African Inland Dayosisi ya Mwanza, Mchungaji John Bunango, baada ya sherehe za kuwekwa wakhfu zilizofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo, machana.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na  Askofu Mteule wa Kanisa la African Inland Dayosisi ya Mwanza, Mchungaji John Bunango, wakati akiondoka Askofu huyo kuwekwa Wakhfu katika sherehe zilizofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo Oktoba 19, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na  baadhi ya viongozi wa dini ya Kikristu wakati akiondoka kwenye uwanja wa CCM Kirumba, baada ya kuhudhuria sherehe za kuwekwa Wakhfu Askofu Mteule wa Kanisa la African Inland Dayosisi ya Mwanza, Mchungaji John Bunango, leo Oktoba 19, 2014. Picha na OMR

CCM YATOA PONGEZI KWA BUNGE MAALUM LA KATIBA

0
0
 Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ambacho kimemalizika leo mjini Dodoma na kutoka na mazimio ya kupitisha sera ya chama kujiendesha kiuchumi na kuondokana na utegemezi wa ruzuku ya serikali.
 Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Philip Mangula akiandika baadhi ya mambo muhimu ya kufafanua katika suala la maadili ndani ya Chama.
Dk.Asha-Rose Migiro akizungumzia mambo mbali mbali yanayohusiana na siasa na mahusiano ya kimataifa kwenye kikao cha NEC kilichomalizika leo tarehe 17 Oktoba 2014 ,mjini Dodoma

KUPOTELEWA KWA NYARAKA MUHIMU

0
0
Jina: Deo  Mbasa 

Vitu vilivyopotea ni begi lililokuwa na;
1. Laptop aina ya Acer
2. Simu kubwa ya Kirusi aina ya Oysters
3. Vyeti vya masomo
     a) Cheti cha form four - NECTA
     b) Cheti cha form six - NECTA
     c) Cheti cha Chuo (Digrii ya Kwanza ya Elimu Jamii na Ualimu) -UDSM
4. Vitambulisho mbalimbali ikiwemo kitambulisho cha Taifa.

Vyeti na nyaraka zote zinasomeka kwa jina la Deo Mbasa Daudi.

Mahali vilipopotelea ni maeneo ya Ofisi ya Posta Kijitonyama, jirani na TBC.

Taarida imetolewa Polisi Mabatini, Kijitonyama kwa RB Namba KJN/RB/9576/2014.
Tafadhali naomba msaada wenu katika namba hizi.
Mbasa
 0765 191 108 / 0716 646 177

KENYAN FREELANCE PHOTOJOURNALIST JOSEPH MATHENGE NAMED CNN MULTICHOICE AFRICAN JOURNALIST 2014

0
0
President  Dr. Jakaya Mrisho Kikwete presents to Kenyan photojournalist, Joseph Mathenge,  the top prize at this year’s CNN MultiChoice African Journalist 2014 Awards Ceremony held on Satuday night at the Mlimani City Conference hall in Dar es salaam. Looking on is Mathege's son, Geoff Kihato, also a photographer,  who helped his father capture the captivating images of  the Westgate Mall shoppers in Nairobi, Kenya, when the mall was attacked by unidentified gunmen in September 2013.Nico Meyer, CEO MultiChoice Africa congratulates Mathenge as President Kikwete, Mathege's son Geoff Kihato…
President  Dr. Jakaya Mrisho Kikwete presents to Kenyan photojournalist, Joseph Mathenge,  the top prize at this year’s CNN MultiChoice African Journalist 2014 Awards Ceremony held on Satuday night at the Mlimani City Conference hall in Dar es salaam. Looking on is Mathege's son, Geoff Kihato, also a photographer,  who helped his father capture the captivating images of  the Westgate Mall shoppers in Nairobi, Kenya, when the mall was attacked by unidentified gunmen in September 2013.Nico Meyer, CEO MultiChoice Africa congratulates Mathenge as President Kikwete, Mathege's son Geoff Kihato and Deborah Rayner, SVP International Newsgathering TV and Digital, CNN International,  (partially hidden) look on.President Kikwete, Nico Meyer, CEO MultiChoice Africa, Deborah Rayner, SVP International Newsgathering TV and Digital, CNN International, share a group photo with Mathenge and son Geoff  Kihato during the ceremony.


Mathenge was awarded the overall ‘CNN MultiChoice African Journalist of the Year’ Award for his work ‘Images of Terror’, which appeared in Kenyan daily print newspaper The Standard and was chosen from entries spanning 38 nations across the African continent.


Mathenge said: “It’s a great honor, and I’m humbled to receive this award. All finalists who are here deserve this award. I hope it will motivate men, women and children of good will all over the world to fight terrorism. Memories fade with time, but pictures don’t. We felt it necessary to capture each and every moment so that generations to come may see the horror.”

President Kikwete, Nico Meyer, CEO MultiChoice Africa and Deborah Rayner, SVP International Newsgathering TV and Digital, CNN International, presented Mathenge with the Award.
Chairperson of the judging panel, Ferial Haffajee, said: “Joseph Mathenge’s photographs so eloquently captured one of Africa’s toughest 21st Century moments that they were worth a thousand words. That said, the quality of all the winners’ works made the contest a tightly run one.”
Mathenge, winner in the Mohamed Amin Photography category, was among 28 finalists from 10 countries who attended the Awards ceremony as the culmination of a four day programme of workshops, media forums, networking, and sightseeing.

Deborah Rayner, SVP International Newsgathering TV and Digital, CNN International, said: “This evening’s journalists represent the very best in African journalism. By entering these awards, they have proved they have the determination, professionalism and courage to showcase Africa’s stories to the world. I congratulate each and every one.”

Nico Meyer, CEO MultiChoice Africa, said: “Congratulations to all the 2014 winners, we are proud to recognise your excellence in journalism and to reward you for your courage in telling stories that would have otherwise remained untold. We believe the CNN MultiChoice African Journalist Awards has had a profound effect on the African media landscape and as MultiChoice Africa we remain committed to recognising excellence in journalism throughout Africa. We applaud all the nominees and winners for contributing to Africa’s growth and success.”

Imtiaz Patel, Group CEO of MultiChoice South Africa, congratulated all the winners of this year's Awards: “I would like to thank all of the journalists who have entered this competition and in doing so have helped further develop this award as a platform for excellence in journalism.  Your dedication and commitment to tell stories that reflect the reality of our world is very encouraging.  A special congratulation to the winners announced tonight.  Your work echoes a great future for the role of the journalists and serves to further strengthen the role of the media in Africa.  You are indeed all winners and an inspiration to us all – you have made us very proud.”

Now in its 19th year, the Awards are supported by a range of prestigious sponsors:  Coca-Cola; Ecobank; GE Africa; IPP Media, Tanzania; Merck Sharp & Dohme (MSD) and A24 Media.
The overall CNN MultiChoice African Journalist 2014 wins a substantial cash prize, and a visit to CNN Centre in Atlanta, to attend the three week CNN Journalism Fellowship. All finalists receive a cash prize, and iPad Air, with runner-ups receiving an iPad mini.
(Story credit: CNN)

Rais Kikwete ahitimisha Mafunzo ya Wakongo na Atunuku kamisheni kwa watanzani 23

0
0




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya viongozi waliohudhuria sherehe hizo Mkoani Arusha

Rais Kikwete ahitimisha Mafunzo ya Wakongo.
. Atunuku kamisheni kwa watanzani 23

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo ametunuku kamisheni kwa maafisa wapya wa Kitanzania 23 miongoni mwa maafisa 437 wa kundi la 53/13 – Kongo. Kundi hilo liliwajumuisha maafisa wa kitanzania wapatao 23 na wahitimu 414 kutoka Kongo.

Jumla ya wanajeshi 414 kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo  leo wamehitimu mafunzo ya Uafisa katika chuo cha maafisa  (TMA) Monduli baada ya kufanya kozi kwa muda wa mwaka mmoja.

Maafisa hao wanafunzi kutoka Kongo walipata mafunzo hayo pamoja na maafisa watanzania 23 waliohitimu leo na kupata kamisheni ya cheo cha luteni usu baada ya kula kuapa mbele ya Mhe. Rais Dkt Jakaya Kikwete.
Tofauti na kamisheni zingine kwani pamoja na Mhe. Rais Kikwete aliweza kutoa Kamisheni kwa maafisa wapya wapatao 23 .

Aidha, leo hii kitu ambacho ni kigeni vijana kutoka kongo walihitimu pasi kutunukiwa kamisheni kwani kulingana na taratibu maafisa  wa kongo wanapaswa kupewa kamisheni na Rais na wakiwa katika ardhi yao, hivyo wahitimu hao watakapewa kamisheni nchini mwao.

Akitoa shukurani kwa Rais Kikwete wa Tanzania, Rais Joseph Kabila ambaye alishuhudia maafisa wake wakihitimu mafunzo hayo, alisema anawashukuru kwa kukubali kutoa mafunzo kwa maafisa hao.Pia alisema anaamini atakuwa amepata makamanda wazuri watakaosaidia kuimarisha usalama nchini mwao na pia kuondoa maadui wanaohatarisha amani nchini Kongo.

Miongoni mwa viongozi waliohudhuria sherehe hizo Wazri wa Ulinzi na JKT, Mhe. Dkt Hussein Ali Mwimnyi, Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe, Katibu mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Waziri Mkuu Mstaafu na mbunge wa Monduli, Mhe. Edward Lowasa, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Magesa Mlongo, majenerali, majenerali wastaafu, na mabalozi wa kijeshi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.

kwa upande wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Naibu Waziri Mkuu na waziri wa Ulinzi, Alexander Luba Ntambo, na Waziri wa Mambo ya Nje, Raymond Tshibanda N’tungamulongo, Balozi wa Kongo nchini Jean Pierre Juma Alfani, Mkurugenzi wa Idara ya Usalama Kahimbi Delphin na Mkuu wa Mafunzo, ya Kijeshi,  brigedia Jenerali Aguru Mamba Maurice.

Airtel yazindua huduma ya kutuma na kutoa pesa Afrika Mashariki kupitia Airtel money

0
0
Kampuni ya simu za Mkononi ya Bharti Airtel yenye kufanya shughuli zake katika nchi 20 barani Afrika na Asia leo imetangaza mpango wa kuzindua huduma ya kutuma na kupokea pesa Afrika Mashariki. 
Huduma hii ya kwanza barani Afrika itamwezesha Mteja wa Airtel kutuma , kupokea na kutoa pesa kutoka kwenye salio lake la Airtel Money Hatua ya awali ya huduma hii inategemea kuanza tarehe 1 November 2014 kwa kushirikisha nchi za Kenya, Uganda, Tanzania na Rwanda ambapo huduma hii itaweza kupatikana kufatia kibali kutoka benki kuu ya serikali ya Rwanda, Kenya, Tanzania na Uganda cha kuendelea na uzinduzi wa mpango huu. 

Hatua ya pili ya mwendelezo wa mpango huu kwa nchi nyingine za Afrika ambapo Airtel inaendesha biashara yake zinategemea kuanza mwakani. Akiongea wakati wa Mkutano wa Biashara kwa wakuu wa Makampuni katika nchi za Afrika Mashariki uliyofanyika Rwanda, Mkurugenzi na Mkuu wa kitengo cha Airtel Money bw, Chidi Okpala,alisema” hii ni hatua muhimu itakayowawezesha wateja wetu kuondoa vikwazo vya kutuma na kupokesa pesa nje ya mipaka ya nchi zao kiurahisi kuweza kufanya hivyo kwa kupitia huduma ya Airtel Money. 

Huduma hii itatanua wigo, kutoa unafuu na kuleta urahisi kwa wafanyabiashara wadogo kufanya malipo ndani na nje ya mipaka ya nchi za Afrika Mashariki.” Aliongeza kwa kusema “huduma hii pia italeta fulsa za kibiashara, ni wazi kwamba huduma za kifedha kupitia simu ni muhimili mkuu katika ushirikiano wa huduma za kifedha na ndio dhamira ya serikali za Rwanda, Uganda, Kenya na Tanzania katika kuhakikisha inakuza shughuli za kibiashara ndani ya nchi za Afrika Mashariki.” Sambamba na hilo Hatua hii ya kwanza ya uzinduzi wa huduma hii pia itawawezesha wateja wa Benki ya Afrika nchini Kenya na Uganda kutuma na kupokea pesa katika nchi hizi mbili. 

 Huduma ya Airtel money ni huduma ya kifedha kupitia simu ya mkononi iliyo salama na rahisi inayowawezesha wateja kutuma pesa kutoka simu moja kwenda kwenye simu za mitandao yote, pia inamuwezesha mteja kununua muda wa maongezi kwaajili ya simu yake au kwa simu ya mtu mwingine. 

Pia inawawezesha wateja kulipa ankra zao mbalimbali na kutoa pesa katika mashine za (ATM)’s Imekaririwa na jumuiya ya Afrika Masharika kwamba huduma za kifedha kupitia simu za mkononi ni muhimu katika nchi hizi kutokana na urahisi, uharaka na inaokoa muda kwa wateja na wafanyabiashara. Uzinduzi wa huduma za kibunifu kama vile za mikopo, kuweka pesa, na kutoa huduma za bima zinazofanywa kwa kushirikiana na makampuni yanayotoa huduma za kibenki zimeleta mabadiliko chanya na kuongeza kasi ya ushirikiano wa kuvuka mipaka ya nchi.

ZANZIBAR YAZINDUA CHANJO YA SURUA NA RUBELLA.

0
0
 Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Jamala Adam Taib akielezea utaratibu wa kampeni ya chanjo ya Surua na Rubela pamoja na matone ya Vitamin A na dawa za minyoo itakavyoendeshwa katika uzinduzi rasmi wa kampeni hiyo  kitaifa uliofanyika kijiji cha Uroa Mkoa wa Kusini Unguja.
  Wazazi na wanafunzi  wa kijiji cha Uroa waliohudhuria uzinduzi wa kampeni ya chanjo ya Surua na Rubela wakimsikiliza mgenai rasmi katika uzinduzi huo Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo (hayupo pichani) kabla ya uzinduzi wa Chanjo hizo.
 Mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampeni ya chanjo ya Surua na Rubella Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akimpatia mtoto matone ya Vitamine A katika uzinduzi wa chanjo hiyo kitaifa uliofanyika  kijiji cha Uroa.
 Muuguzi wa Kituo cha Afya cha Uroa akimpatia mtoto chanjo ya surua na Rubella kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika kijijini hapo. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

MANGULA, NAPE WAONGOZA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE YA VIJANA WA CCM VYUO VIKUU , LEO

0
0


 Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Philip Mangula akihutubia Vijana wa Vyuo vya Elimu ya juu kwenye kongamano la Vijana  lililofanyika Mlimani City jijini Dar Es Salaam.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia Vijana wa CCM kutoka vyuo Vikuu mbalimbali kwenye Mkutano wa Kuadhimisha Kumbukumbu ya Baba wa Taifa uliofanyika Mlimani City.

 Nasra Khalfani akipokea kadi yake ya uanachama wa CCM
 Vijana wakila kiapo cha uanachama wa CCM
 Justin Mushi akikabidhi kadi yake ya Chadema kwa makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula na kutangaza kujiunga rasmi CCM.
(Picha na Adam Mzee )

 Katibu Mwenezi wa CCM Tawi la Chuo Kikuu Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Rehema Akikweti akisoma salaam za ufunguzi wa mkutano wa Vijana wa Vyuo Vikuu wa CCM kuadhimisha Kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa.


 Sehemu ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu wakisikiliza mada mbali mbali
 Mwenyekiti wa UVCCM tawi la chuo Kikuu cha Dar es Salaam Theodora Malata akisoma risala ya Umoja wa Vijana wa Elimu ya Juu.


 Katibu Mtendaji wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania Ndugu Christopher Ngubiagai akihutubia wakati wa kongamano hilo.
 CCM Oyee!
 Sehemu ya wanafunzi wa Elimu ya Juu wakisikiliza kwa makini mada mbali.
 Wanafunzi wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano Mlimani City kwenye  mkutano wa Vijana wa Vyuo Vikuu wa CCM kuadhimisha Kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa.
 Zeyana Mohamed Haji Katibu Uchumi na Fedha Mkoa wa Vyuo Vikuu Zanzibar akizungumzia kuboreshwa kwa Elimu ambayo itakomboa Watanzania.
 Gulatone Masiga akizungumzia ubora wa Rasimu iliyopendekezwa na BMK dhidi Rasimu ya 2 ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
 Steve Nyerere akizungumza wakati wa mkutano huo ambapo alisema wakati umefika kwa wasanii wa kitanzania kula milo mitatu kutokana na kukumbukwa kwenye Katiba iliyopendekezwa.
 Raymond Mweli kutoka chuo Mzumbe akizungumzia  falsafa za Mwalimu Nyerere juu ya Katiba ya CCM.
 Wanafunzi wakirekodi matukio kwa kutumia simu zao.





UNESCO BADO KURIDHIA UJENZI BWAWA LA STIEGLER’S GORGE KUFUA UMEME

0
0
UNESCO-logo1
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limesema hakuna makubaliano yaliyofikiwa kati yake na mamlaka husika nchini Tanzania za kuwezeshwa kujengwa kwa bwawa la kufua umeme la Stiegler’s Gorge .

Ofisi za Shirika hilo zilizopo jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki wametoa taarifa ya kukanusha maelezo yaliyoandikwa na gazeti la The Guardian (ref:http://www.ippmedia.com/frontend/index.php?l=72984) kwamba yapo maafikiano kuhusu ujenzi wa bwawa hilo.
Eneo la Stiegler’s Gorge lipo katika hifadhi ya Selou ambayo ni sehemu ya urithi wa kimataifa ambapo ujenzi wa miundombinu yoyote yenye athari kubwa katika hifadhi hiyo lazima kuwepo na maridhiano kati yake na mamlaka husika.

Taarifa hiyo imesema taarifa zilizoandikwa na gazeti hilo Oktoba 8, mwaka huu limeshutua shirika hilo. Taarifa hizo zilizokuwa ukurasa wa mbele zilisema kwamba Tanzania itavuna zaidi nishati ya umeme kutokana na maafikiano yake na UNESCO juu ya ujenzi wa wa bwawa hilo.

Katika taarifa yake UNESCO imesema kwamba katika mkutano wa 36 wa kamati ya Urithi wa dunia (WHC) uliofanyika Saint-Petersburg mwaka 2012 na ule wa 37 uliofanyika Phnom Penh, mwaka 2013 na wa mwisho uliofanyika Doha mwaka huu ulieleza wazi mashaka yake juu ya athari ya ujenzi wa bwawa hilo katika hifadhi.

Katika mikutano yote hiyo ilikubalika kwamba mamlaka zinaozohusika nchini kutofanya shughuli zozote za maendeleo ndani na kwenye mipaka ya hifadhi bila kupata kibali cha WHC kwa mujibu wa kifungu 172 cha makubaliano. Aidha kamati hiyo iliitaka mamlaka zinazohusika kutekeleza ushauri uliotolewa na kamati ya pamoja kati ya WHC na Muungano wa ushirikiano wa hifadhi ya asili (IUCN) wa kutengenezwa kwa mkakati kabambe wa menejimenti ya Ekolojia ya Selous.

Aidha inatakiwa kutayarisha menejimenti hiyo kwa kuweka mipaka katika eneo la urithi wa dunia na kuonesha maeneo ambayo yanastahili kuingizwa katika hifadhi.

Pia kufafanua mradi wa Stiegler's Gorge, hatua iliyofikiwa hasa katika maamuzi na kuhakikisha kwamba ufahamu kuhusu athari, gharama, manufaa na namna inavyofaa au kutofaa na pia kuwa na mpango mbadala kama haikuwezekana.

Mambo yote hayo yanatakiwa kuzingatia umuhimu wa eneo hilo kwa jamii ya dunia na hivyo kuangalia vigezo vyote vya maeneo ya urithi . Katika maamuzi hayo pia Kamati ya Urithi ilifurahishwa na nia ya mamlaka husika za Tanzania kuendesha utafiti huo kwa mujibu wa makabaliano na vigezo stahiki ili kuelewa athari zake katika hifadhi hiyo ambayo ni urithi wa kimataifa, korido za mapito ya wanyama na nini kitatokea kwa korido la Selous-Niassa Corridor.

Kwa mujibu wa taarifa ya UNESCO, kamati hiyo ya Urithi wa Dunia (WHC) ilitarajia kupata taarifa za awali Februari Mosi mwakani. Aidha taarifa hiyo ilitakiwa kuwa na muhtasari wa hatua mbalimbali zinazchukuliwa na muda wake kuhusiana na hifadhi ya Selou kujiondoa katika urithi wa dunia ulio katika hatari ya kutoweka.

Imeelezwa kuwa taarifa hiyo ndiyo itakuwa msingi wa majadiliano katika mkutano ujao wa WHC wa 39 utakaofanyika Bonn Ujerumani. Aidha taarifa hiyo imesema kutokana na vitu vyote kutokuwa bado kufanyika msimamo wa UNESCO unabaki kama ulivyo, kwamba hakuna makubaliano yoyote yaliyofikiwa na kinyume na hapo ni kukiuka makubaliano.

FACEBOOK KUTUMIKA KUFUNZA USALAMA BARABARANI

0
0
DSC_0135
Naibu Kamishna wa Polisi na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga (wa pili kushoto) akifurahi jambo na baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini. 

Kushoto ni Mratibu wa Mradi wa kuboresha Demokrasia na Amani (DEP) kutoka ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Bi. Beatrice Stephano, Afisa Mfawidhi Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kanda ya ziwa Mwanza, Bw. Ludovick Ringia (wa pili kulia) nje ya ukumbi wa mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu mara baada ya kuwasili katika warsha ya siku nne ya wadau wa utekelezaji wa mradi wa uchaguzi unaolenga kuboresha Demokrasia na Amani nchini (DEP) kuelekea uchaguzi mkuu ujao iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na kufadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maendeleo (UNDP). (Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).

Naibu Kamishna wa Polisi na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, amekubaliana na haja ya kuanzisha mafunzo katika vyombo vya habari vya kijamii kama facebook ili kutanua uwanja zaidi wa elimu ya usalama barabarani hasa kwa vijana ambao ndio waathirika wakubwa wa ajali.

Aidha amesema Polisi wanafikiriia kuanzisha mfuko wa kielektroniki wa ulipaji wa faini kwa makosa ya barabarani ili kuongeza kasi ya udhibiti na kuondoa tuhuma za rushwa. Kauli hiyo ameitoa mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na wanahabari na watendaji kutoka redio za jamii nchini mjini Dodoma, katika warsha ya siku nne ya wadau wa utekelezaji wa mradi wa uchaguzi unaolenga kuboresha Demokrasia na Amani nchini (DEP) kuelekea uchaguzi mkuu ujao iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na kufadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maendeleo (UNDP).
washa ya siku nne ya wadau wa utekelezaji wa mradi wa uchaguzi unaolenga kuboresha demokrasia na amani nchini kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
DSC_0141
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Unesco , Bw. Al Amin Yusuph, akisalimiana naNaibu Kamishna waPolisi na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, mara baada ya kuwasili kwenye warsha hiyo iliyomalizika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.


Kauli yake hiyo ilifuatia hoja iliyotolewa na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO), Bw. Al Amin Yusuph, ambaye aligusia redio za jamii katika kusambaza habari zenye kulenga kuokoa maisha na mali kwa ajili ya maendeleo ya taifa.

Mpinga ambaye pia ni kamanda wa kikosi cha usalama barabarani alisema katika mada yake kwamba changamoto kubwa ni kutekeleza sera ya kuhakikisha kwamba hakuna kifo wala majeruhi katika ajali za usalama barabarani. 

Akielezea hali halisi ya ajali barabarani huku akikariri takwimu za Benki ya Dunia na Shirika la Afya Duniani (WHO) kamanda Mpinga alisema kwamba utafiti unaonesha katika kila wakazi 100,000 duniani 24 hufa katika ajali za barabarani ambapo vijana na watu maskini ndio wapo katika hatari kubwa zaidi.

Aidha alisema takwimu zaidi kutoka WHO zinasema kwamba watu million 1 na laki tatu hufa kila mwaka duniani hapa kwa ajali huku ikibainisha kwamba asilimia 75 ya watu wanaojeruhiwa na kufa wanatoka katika nchi maskini ambazo hazina magari mengi kama zile zilizoendelea.
DSC_0171
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Unesco , Bw. Al Amin Yusuph (kushoto) akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Naibu Kamishna wa Polisi na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, kutoa mada kwa watendaji wa redio za jamii nchini. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa mtandao wa redio za jamii nchini (COMNETA) ambaye pia ni Meneja wa redio jamii Sengerema FM ya mkoani Mwanza Bw. Felician Ncheye.

Alisema pamoja na takwimu hizo za kutisha za duniani, nchini kwetu pekee watu 4000 hufa kila mwaka kutokana na ajali na mwaka uliopita walikufa watu 4002. Akitoa mada katika mafunzo hayo alisema kwamba ajali nyingi zinazotokea zinasababishwa na binadamu ambapo asilimia 75 za ajali zote husababishwa na makosa ya kibinadamu.

Alisema utafiti unaonesha kwamba makosa hayo chanzo chake ni uzembe, ulevi, mwendo kasi, kutozingatia sheria, uchovu wa madereva na matumizi ya vyombo vya moto. Aidha uzembe wa waendesha pikipiki ndio unabeba asilimia 20 hadi 30 ya ajali zote. Alisema kufunguliwa kwa biashara ya pikipiki kubeba abiria kumewaingiza vijana wengi ambao wengi wao si wataalamu wakikosa sifa ya kuendesha vyombo hivyo vya moto huku wakiwa vinara wa kuvunja sheria barabarani kwa vitendo.
DSC_0212
Naibu Kamishna wa Polisi na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, akiwasilisha mada kwa watendaji wa redio jamii nchini (hawapo pichani) waliokuwa wakihudhuria warsha ya siku nne ya wadau wa utekelezaji wa mradi wa uchaguzi unaolenga kuboresha Demokrasia na Amani nchini (DEP) kuelekea uchaguzi mkuu ujao iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na kufadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maendeleo (UNDP) iliyoamlizika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma. Kushoto ni Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Unesco , Bw. Al Amin Yusuph na Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa mtandao wa redio za jamii nchini (COMNETA) ambaye pia ni Meneja wa redio jamii Sengerema FM ya mkoani Mwanza Bw. Felician Ncheye.
Madereva hao alisema wanaendesha kasi, hawavai kofia ngumu na kubeba abiria kwa mtindo wa mishikaki.

Akifafanua zaidi amesema kwamba pamoja na madereva wa pikipiki kuongoza kwa kuvunja sheria hali za barabara kama kukosekana kwa alama, muundo wa barabara zenyewe, utelezi , uchakavu wa vyombo na hali ya hewa vimekuwa visababishi vya ajali.

Kamanda alitaka vyombo vya habari vya redio za jamii kuelimisha madereva matumizi sahihi ya barabara kwa kuwaita wataalamu kuelezea mambo hayo bila chumvi wala kuharibu nidhamu na maisha .

Alisema mathalani maeneo ya mnadani madereva wamekuwa wakivunja sheria hasa upakiaji wa mizigo isiyozingatia usalama wa abiria waliomo.
Alisema jeshi la polisi limechukua mikakati kadhaa kuwezesha kukabiliana na hali ya usalama barabarani hasa kwa kuanzisha ukamataji wa makosa hatarishi katika usalama wa barabara.

Makosa hayo ni mwendokasi, ulevi, uendeshaji wa hatari na uzidishaji wa abiria alisema faini zinazotolewa zimefanya kupungua kwa ajali kutoka elfu 17 hadi elfu 11. Alisema mikakati mingine ni utoaji wa elimu kwa kupitia vyombo vya habari na kushukuru kwamba elimu hiyo anaona inasaidia. Alisema wanatoa elimu kupitia televisheni , redio na vyombo vya habari vya kijamii.
DSC_0196
Aidha wamekuwa wakishiriki kutoa mafunzo wakishirikiana na wadau wengine.
Pia aliutaja mkakati mwingine ni kuboresha mifumo ya utendaji kwa kuainisha maeneo yanayotokea ajali mara kwa mara, ukusanyaji wa takwimu na kubadili mfumo wa ukaguzi barabarani kwa kuanzisha maeneo maalumu ya kukagulia magari kwa undani.
Pia kunatengenezwa mfumo wa nukta ambapo dereva anapofanya makosa pointi zinaondolewa na zikimalizika anapokonywa leseni.
Kuhusu ulipaji wa faini kupitia benki na njia nyingine za elektroniki alisema zitarahisha utendaji wa polisi na kuondoa tuhuma za rushwa na pia kuwafanya watu kuwa waangalifu zaidi.
Aidha amesema wanatengeneza utaratibu kwa kushirikiana na wadau wengi kutengenezwa kanuni ya ulazima wa madereva kurejea shule kwa mafunzo hasa kutokana na kubadilika mara kwa mara kwa miundombinu ya barabara na teknolojia ya magari.
DSC_0200
Sehemu ya wadau/watendaji wa redio jamii wa utekelezaji wa mradi wa uchaguzi unaolenga kuboresha Demokrasia na Amani nchini (DEP) kuelekea uchaguzi mkuu ujao wakifuatilia kwa umakini mada iliyowasilishwa na Kamanda Mpinga kwenye warsha hiyo.
Hata hivyo alisema pamoja na mikakati hiyo na mingine Jeshi la Polisi linakabiliwa na changamoto zinazoambatana na bajeti ndogo ya kuiwezesha kununulia vifaa vya kazi kama speed radar za kisasa na mifumo muafaka ya kusimamia usalama barabarani ambapo kwa sasa kila tatizo wanasukumiziwa polisi iwe ni taa mbovu za barabarani au mashimo.
Changamoto nyingine ni wananchi wenyewe kukosa utamaduni wa kuheshimu sheria mpaka waone polisi.
Alivitaka vyombo vya redio jamii kufundisha wananchi na wala sio kuchochea wao wazidi kuvunja sheria na kuitoa mfano wa matuta barabarani ambayo yanadaiwa na wananchi na kusema hiyo si dawa bali elimu kwa wananchi kuhusu usalama barabarani na namna ya kudhibiti ajali.
Naye Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Unesco , Bw. Al Amin Yusuph akimkaribisha Kamanda Mpinga azungumze alisema mafunzo hayo yameandaliwa kwa ajili redio za jamii kujiuza kw apamoja katika kuhudumia umma na kujiendeleza.
Alisema redio ndio njia pekee ya kuwafikia watanzania wengi hasa kwa kuzingatia kwamba watumiaji wa vyombo vingine ni wachache hasa kutokana na kukosekana kwa nishati na pia kuwa mbali na maeneo yanayotangaza habari.
DSC_0221
Wasaidizi wa Kamanda Mpinga wakigawa machapisho mbalimbali yanayotoa elimu ya usalama barabarani kwa washiriki wa warsha hiyo iliyomalizika mwishoni mwa juma mjini Dodoma.
DSC_0244
DSC_0240
Reportuer wa warsha ya wadau wanaotekeleza mradi wa uchaguzi iliyomalizikia mwishoni mwa juma mjini Dodoma Mchungaji Privatus Karugendo akihoji suala la baadhi ya watumiaji wa vyombo vya moto wanaotumia simu za viganjani pindi wawapo barabarani kitu ambacho ni hatari kwa usalama wao.
DSC_0268
Baadhi ya machapisho yaliyogawiwa kwa watendaji wa redio jamii nchini yanayotoa elimu ya usalama barabarani.
DSC_0255
Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo wakipitia machapisho hayo yaliyotolewa na Kitengo cha Polisi Usalama Barabarani kwenye warsha hiyo.
DSC_0259
DSC_0287
Naibu Kamishna wa Polisi na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga,akipata picha ya kumbukumbu na Mshiriki wa warsha hiyo Prosper Kwigize.
DSC_0292
Naibu Kamishna wa Polisi na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, akifurahi jambo na Mkurugenzi wa redio jamii Uvinza Fm, Alhaji Ayubu Kalufya.

FILAMU YA MAPENZI YA MUNGU KUINGIA SOKONI WIKI HII...

0
0
Mwezi, Wiki na Sasa siku zimebaki kwa ile Filamu Mpya na ya Kusisimua ya MAPENZI YA MUNGU Kuingia Sokoni ambayo imewakutanisha wasanii mahiri wa hapa hapa Tanzania ambapo Mmoja kati ya Wasanii waliocheza filamu hiyo Ni Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya anayejulikana kama Linah Sanga, kwa Kushirikiana na Elizabeth Michael bila Kumsahau Flora Mtegoha ambae ni Mama Mzazi wa Marehemu Steven Kanumba watakuwa ndani ya filamu Mpya iitwayo MAPENZI YA MUNGU.

Ni Filamu ambayo Kisa chake na Mafunzo yake yanasisimua lakini Pia ni Moja kati ya filamu ambayo kiukweli ina hadhi na vigezo vya kimataifa......Nimefika hapa leo sio kwa Ujanja wangu Bali ni Kwa"Mapenzi ya Mungu..."
Filamu ya "Mapenzi ya Mungu" ni moja ya filamu ambayo Msanii Linah pamoja na Mama Mzazi wa Marehemu Kanumba wameonyesha uwezo wa hali ya juu na kuthibitisha kuwa kweli Sanaa ni Kazi.
Filamu ya "Mapenzi ya Mungu" itakuwa Sokoni Kuanzi Wiki hii Kwa Wauzaji wa Filamu kote Nchini.
Filamu hii itasambazwa na Kampuni mahiri ya Proin Promotions Ltd.

HOTEL ZA DOUBLE TREE BY HILTON TANZANIA WADHAMINI SIKU YA CHAKULA ILIYOFANYIKA KWENYE VIWANJA VYA TANGANYIKA INTERNATIONAL SCHOOLS

0
0
 Hotel Za Double Tree By Hilton Tanzania Tarehe 18.10.2014 walidhamini Siku Ya Maonesho Ya chakula Iliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya Tanganyika International Schools.Akielezea Madhumuni ya kuandaa siku hiyo .

Mkurugenzi wa Mauzo  wa Hotel za Double Tree By Hilton Tanzania Bwana Florenso Kirambata alisema kuwa nia yao kubwa ni kuweza kuyapa fursa makampuni mbali mbali na wajasiliamali wadogo wadogo kuweza kuonyesha uwezo wao na bidhaa wanazotengeneza.

Mr Florenso  akaongeza kuwa zaidi ya wajasiriamali wadogo wadogo 100(mia Moja) na Wakubwa 50(hamsini) walishiriki kwenye maonesho hayo hasa lengo kuu ikiwa ni kuonesha aina mbali mbali za vyakula wanavyozalisha hivyo kuweza kujitangaza na kufahamika.

Pichani Juu Katikati ni Meneja Masoko wa Hotel za Double Tree By Hilton Bwana Florenso Kirambata kushoto ni mpishi mkuu wa Double Tree Hassan na kulia ni Ayman.
 Mpishi Msaidizi wa Hotel ya Double Tree  Awadh(kushoto) Akiwa Anapata maelekezo toka kwa Mpishi mwenzake Ayman namna ya kuandaa na kuchanganya vyakula

  Mpishi mkuu wa Hotel za Double tree Bwana Hassan akitoa maelekezo kwa wasaidizi wake .
 Meneja Masoko wa Hotel za Double Tree By Hilton Bwana Florenso Kirambata akiwa na wapishi wa Hotel za Double Tree wakipata maelekezo kwa mmoja wa washiriki wa Maonesho ya chakula
 Wapish wa Hotel Za Double Tree Wakiangali moja ya Bidhaa Toka kwa mshiriki wa maonesho ya siku ya chakula
 Mwaandaaji mku wa Maonesho hayo wa kwanza Kulia akiwapa maelekezo wapishi wa Hotel za Double Tree 
 Mpishi msaidizi wa Hotel za Double Tree akiwapa maelekezo wateja waliotembelea banda lao namna chakula cha Hot Dog kinavyotengenezwa
 Banda la American Garden Walikuwepo nao kuonyesha Bidhaa zao Tofauti tofauti
 Watu mbali mbali wakiendelea kutembelea mbanda tofauti tofauti  na kujionea bidhaa
 Waudhuriaji wakiendelea kupata vyakula na kufarihia ladha tofauti za vyakula
 Wahudhuriaji pia walipata nafasi ya kubadilishana mawazo
 Wahudhuliaji wakiendelea kupata ladha tofauti za vyakula

BI REHEMA AMEPOTEA KWA YEYOTE ATAKAYEMUONA ANAOMBWA KURIPOTI KITUO CHA POLISI KIGAMBONI U KILICHO KARIBU

0
0
Bi Rehema Salum Msambya pichani juu amepotea tokea tarehe 16/10/2014 maeneo ya Kigamboni - Kisota karibu na Shule ya Sekondari ya Abdu jumbe. 
Siku hiyo alikuwa amevaa Dela Na Skintirt ya Rangi ya Blue. Bi Rehema ana Matatizo ya Akili. Yeyote atakayemuona anaombwa kutoa taarifa katika kituo cha Polisi Kigamboni au kilicho karibu  au Apige simu namba
0712 22 77 22
0753 63 49 67
0712 70 77 87
0713 23 52 94
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live




Latest Images