Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 388 | 389 | (Page 390) | 391 | 392 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mbunge wa Kigamboni Dkt Faustine Ndugulile akiwa Mgeni Rasmi kwenye mkutano wa mabalozi wa CCM kata ya Charambe kilichofanyika kwenye ukumbi wa Dar Live leo asubuhi
    Baadhi ya Mabalozi wa CCM  Kata ya Charambe wakiwa kwenye mkutano wa Mabalozi


  0 0

   
  Mmoja wa maafisa wa TASAF  Hamis kikwate aliyeketi mstari wa mbele akifuatilia kazi ya utambuzi wa kaya maskini katika moja ya walengwa wa mpango huo wilayani Maswa. kazi ya utambuzi wa kaya maskini inaendelea kwa kasi katika maeneo ya wilaya ya Maswa mkoani Simiyu.
  Pichani ni baadhi ya Watoto wakiwa na furaha tupu baada ya kupata maelezo juu ya mpango wa kunusuru kaya maskini wilayani Maswa.
  Baadhi ya walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini wilayani Maswa wakiwa katika picha ya pamoja na mmoja wa maafisa wa TASAF,Hamis Kikwate (mwenye suti nyeusi aliyeketi).
  Walengwa wa mpango wa kunusuru kaya maskini wilayani Maswa wakipewa maelezo ya mpango kabla ya kuorodheshwa .
   Wadodosaji wa taarifa za walengwa wa mpango wa kunusuru kaya maskini wilayani Maswa wakiendelea na kazi hiyo katika moja ya kaya za walengwa wa mpango huo.

  0 0

  Na Beatrice Lyimo- MAELEZO.

  Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo inatarajia kufanya kampeni shirikishi ya ugonjwa wa Surua na Rubella kuanzia tarehe 18 hadi 24 oktoba, 2014.

  Akizungumzia kampeni hiyo itakayofanyika nchini nzima leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Donan Mmbando amesema kuwa itawahusisha watoto wenye umri wa kuanzia miezi 9 hadi miaka 15.

  Amesema kampeni hiyo itaambatana na utoaji wa matone ya Vitamini A, dawa za kutibu na kukinga magonjwa ya Minyoo, Usubi,Matende na Mabusha.

  Dkt. Mmbando amesema kuwa lengo na madhumuni ya kampeni hiyo ni kudhibiti milipuko ya magonjwa ya Surua na Rubella ili kupunguza vifo na madhara yanayosababishwa na magonjwa hayo.

  “Katika kampeni hii tutatoa dawa za kutibu na kukinga magonjwa ya Minyoo, Usubi, Matende na Mabusha katika mikoa 16 yenye maambukizi makubwa ya magonjwa haya”, Amesisitiza Dkt. Mmbando.

  Amefafanua kuwa chanjo ya Surua na Rubella itatoa fursa ya kutoa kinga kwa watoto wengi zaidi ambao hawakupata chanjo hiyo utotoni katika mikoa yenye maambukizi makubwa ya magonjwa hayo ambayo ni Mtwara, Lindi, Tanga , Dar  es salaam,Morogoro, Pwani, Tabora, Manyara, Iringa, Ruvuma, Rukwa, Katavi, Singida, Dodoma na Njombe.

  Akitoa ufafanuzi kuhusu chanjo hizo amesema kuwa chanjo ya Surua na Rubella itatolewa kwa watoto wenye umri wa miezi 9 hadi chini ya miaka 15, matone ya vitamin A kwa watoto wenye umri wa miezi 6 hadi chini ya miaka 5.

  Nyingine ni dawa za minyoo (Mebendazole) zitakazotolewa kwa watoto wenye umri wa miezi 12 hadi chini ya miaka 5 nchi nzima na dawa za kutibu na kukinga minyoo (Albendazole) Usubi, Matende na mabusha au Ngirimaji kwa watu wenye umri wa kuanzia miaka 5 na kuendelea katika mikoa 16 iliyobainishwa.

  Kwa upande wake Meneja Mpango wa Taifa wa Chanjo wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii  Dkt. Dafrosa Lyimo ametoa wito kwa wazazi kuhakikisha kuwa wanawapeleka watoto wao katika vituo vya afya ili waweze kupata chanjo  hiyo.

  Pia ametoa wito kwa mama wajawazito kuhakikisha kuwa wanapata chanjo ya Surua-Rubella ili kuwakinga watoto wao dhidi ya matatizo ya Moyo, mimba kuharibika, kujifungua kabla ya wakati na mtindio wa ubongo yanayotokana na ugonjwa huo.


  0 0

  awashangaa wasanii kutochangamkia mashamba ya Shiwata

  MCHUNGAJI wa Kanisa la KKKT, John Solomoni, ameshangazwa na kitendo cha idadi ndogo ya wasanii kujitokeza katika kununua mashamba ya bei rahisi yanayotolewa na Shirikisho la wasanii Tanzania(SHIWATA( yaliyopo Kijiji cha Ngarambe Wilayani Mkuranga.

  Solomoni  ambaye pia ni Katibu wa kamati ya amani ya viongozi wa Dini mkoa wa Dar es Salaam,aliyasema hayo juzi katika hafla ya kuoneshwa mashamba kwa wasanii hao iliyoendana sambamba na maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

  Alisema kitendo kilichofanywa nawasanii inaonesha ni jinsi gani bado haewajaanza kujitambua katika kutengenezamaisha yao ya mbeleni.
  Alisema kiasi cha shilingi 200,000 kinachotozwa kwa ajili ya msanii kupata ekari moja na nusu ni kidogo sana ukilinganisha na thamani ya ardhi ilivyo sasa lakini anawashangaa kwa nini wasanii wameshindwa kujitokeza kama ilivyotarajiwa.

  “Hapa nimeambiwa shirikisho lina wasanii zaidi ya 8000 wakiwemo wasanii wakubwa wenye majina lakini kwa nini ni 95 tu ndio wanunue mashamba hii ni aibu na kushindwa kujitambua nyie ni kina nani mbele ya jamii,”alisema Mchungaji Solomon.
  .
  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Wilaya ya Mkuranga,Saada Mwaruka, alisema kama Wilaya watawapa ushirikiano wa hali na mali wasanii waliochukua mashamba hayo ikiwemo kuwakopesha pembejeo za kilimo.

  Mwaruka alisema wanataka waone  eneo hilo linakuwa shamba darasa la kuigiwa mfano jambo litakalowaamsha vijana wa Mkuranga nao kujishughulisha na kilimo na kuona kilimo sio kazi ya waliokosa kazi bali ni moja ya njia za kuwainua kiuchumi.

  Naye Mwenyekiti wa Shiwata, Cassim Taalib, alisema  wameamua kubuni mbinu hiyo ili kuwaondoa wasanii wa nchi hii katika umasikini.

  Taalib alisema katika mashamba hayo kuna jumla ya ekari 500 kwa ajili ya kulima huku awali walitangulia kagawa eneo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba robo ekari kwa kila msanii lililopo maeneo ya Mwanzega huko huko Wilayani Mkuranga ili nao waweze kumiliki nyumba.

  Alisema utaratibu huo ndio ulitumiwa na Mwalimu Nyerere wakati wa kuhamasisha vijiji vya Ujamaa ambako mpaka leo watu wameona matunda yake.

  0 0


  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Kisesa (CCM), Luhaga Mpina akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwandu Itinje wilayani Meatu mkoani Simiyu, waliofika eneo hilo kushuhudia mpambano ulioandaliwa na mbunge huyo wa ngoma za asili ya watu wa kabila la Wasukuma kati ya Malogi Hamsini na Magise Jilunga.
  MBUNGE wa Jimbo la Kisesa(CCM), Luhaga Mpina ameahidi kuendelea kuenzi utamaduni wa ngoma za kabila la wasukuma kwani zimekuwa ni sehemu ya kuimarisha mshikamano miongoni mwa jamii hiyo.

  Mpina alitoa kauli hiyo juzi wakati akifunga mpambano wa ngoma za asili katika Kijiji cha Mwandu Itinje wilayani Meatu mkoani Simiyu uliwakutanisha Malogi Hamsini Mgika na Magise Jilunga Mgalu.

  Hata hivyo katika mpambano huo ulihudhuriwa na watazamaji zaidi elfu nane kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Simiyu ambapo Magise Jilunga aliibuka mshindi baada ya kumbwaga Malogi.

  Akizungumza mara baada ya mpambano huo, Malogi Hamsini alikubali kushindwa na mpinzani wake na kueleza kuridhika na uamuzi uliofanywa na kuomba kukutanishwa tena siku nyingine na mpinzani wake huyo.

  Naye Magisa Jilunga alisema pamoja na kumshinda mpinzani wake lakini alikiri pambano hilo lilikuwa gumu kwake na kuamba nae pia kurudiana ombi ambalo lilikubaliwa na Mbunge wa jimbo hilo.

  Pambano hilo lililodhaminiwa na Mbunge Mpina lilivuta hisia za mashabiki wengi na kuomba kufanyika mara kwa mara kwa pambano hilo kwani linaleta umoja na mshikamano miongoni mwa jamii.

  Mpina aliwazawadia shilingi milioni moja kila mmoja katika mpambano huo na kuahidi kudhamini tena pambano lingine kama hilo baadae mwakani. ZAIDI BOFYA PLAY KUSIKILIZA YALIYOJIRI.

  Wachezaji wa ngoma toka kundi la Malogi Hamsini ambaye ni Mgika wakifanya yao.
  Mbunge wa Jimbo la Kisesa (CCM), Luhaga Mpina akipiga ngoma kuashiria ufunguzi wa mpambano wa ngoma asili kati ya Malogi Hamsini na Magise Jilunga.

  Kiongozi wa Wagika, Malogi Hamsini (kulia) akiwa amesimama barabara kuuanza mpambano ambapo alizidiwa nguvu ya uchawi na Mpinzani wake Magise Jilunga ambaye Mgalu.
  Wachezaji wa kundi la Malogi Hamsini wakionyesha kazi.
  Mara baada ya kuona ameshindwa katika nguvu za kichawi Malogi Hamsini alipandwa na hasira ampazo alizielekeza kweye tunguli zake.
  Na hapo ndipo alipo amua kuziteketeza kwa kuzifumua kwa mateke..... PwachAaA!!
  Wingi wa watu ndiyo pointi za ushindi watu walihama toka kwa Malogi Hamsini na kuelekea kwa Magise Jilunga ambapo kila mmoja alikuwa akipiga ngoma kwa wakati mmoja (yaani kulia na kushoto wapi pananoga?).
  Wananchi wakiwa wameizunguka himaya ya Magise Jilunga.
  Kiongozi wa Wagalu, Magise Jilunga wa pili kutoka kushoto akiwa tayari kulianzisha kwenye mpambano kati yake na Malogi Hamsini ulioandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Kisesa Luhaga Mpina.
  Hatari kama anaporomoka vile...
  Malogi Hamsini alituma nyoka kuja kuharibu ngoma ya Magise Jilunga lakini hakufua dafu.
  Mapanga dizaini....
  Akinamama wakiingia kwenye lango kuu kushuhudia mpambano.
  Michezo ya hatari balaa ni mwendo kugalagala kwenye moto.
  Silaha ya ushindi kwa Magise Jilunga ilikuwa ni kubadilika badilika.
  Si kubadilika tu bali alikuwa na vionjo kama kuoga moto mchana kweupe na kunywa mafuta ya dizeli...tobA!
  Ni balaa mwanawane!!!
  Jamaa aliamua kukizika kichwa kwa dakika kadhaa kiasi cha kusisimua mashabiki!!
  Kiongozi wa Wagalu, Magise Jilunga akipiga ngoma kuusaka ushindi.
  Viongozi wa kada mbalimbali nao wamo.
  Mbunge wa Jimbo la Kisesa (CCM), Luhaga Mpina akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwandu Itinje wilayani Meatu mkoani Simiyu, waliofika eneo hilo kushuhudia mpambano ulioandaliwa na mbunge huyo wa ngoma za asili ya watu wa kabila la Wasukuma kati ya Malogi Hamsini na Magise Jilunga.
  Maelfu waliofika eneo hilo kushuhudia mpambano ulioandaliwa na Mhe. Mbunge, ngoma za asili ya watu wa kabila la Wasukuma kati ya Malogi Hamsini na Magise Jilunga.
  Ni wakati wa jaji Mkuu kutangaza matokeo rasmi:- Mpambano wa ngoma za asili ya watu wa kabila la Wasukuma kati ya Malogi Hamsini na Magise Jilunga.
  "Mshindi ni Magise Jilunga...!!"
   Malogi Hamsini (kushoto) akimpongeza kiroho safi Magise Jilunga mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi....
  Full m-banano.
  Mbunge wa Jimbo la Kisesa (CCM), Luhaga Mpina akiwaaga wananchi wa Jimbo lake mara baada ya kumalizika mpambano.
  Mbunge wa Jimbo la Kisesa (CCM), Luhaga Mpina akiwaamezungukwa na maelfu ya wananchi waliofika eneo la uwanja wa kusanyiko.

  0 0

   Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi. Doroth Mwanyika (kushoto) akibadilishana hati ya mkataba wa ushirikiano wa Mpango wa Mageuzi ya Usimamizi wa Fedha za Umma (PFM) Awamu ya IV waliosaini leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Balozi wa Finland nchini Bi. Sanikka Antila.
   Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi. Doroth Mwanyika (kushoto) akitia saini mkataba wa ushirikiano wa Mpango wa Mageuzi ya Usimamizi wa Fedha za Umma (PFM)  Awamu ya IV kwa niaba ya Serikali ya Tanzania leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Balozi wa Finland nchini Bi. Sanikka Antila. 
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi. Doroth Mwanyika (kushoto) akishukuru Serikali ya Finland kwa ushirikiano mzuri wanaoendelea kuipa Tanzania mpaka sasa na kuahidi kuwa fedha hizo zitatumika katika malengo yaliyokusudiwa. Kulia ni Balozi wa Finland nchini Bi. Sanikka Antila.
   Balozi wa Finland nchini Bi. Sanikka Antila  (kulia)PFM akiongea na waandishi wa habari  (hawapo pichani) na kuipongeza kwa kusimamia fedha za umma na kuwa na uongozi unaosimamia utawala wa kidemokrasia, uchumi imara, ufanisi katika matumizi ya rasilimali zilizopo na hivyo kupunguza umasikini. Hafla hiyo imefanyika leo jijini Dae es salaam wakati wa kusaini mkataba wa ushirikiano wa Mpango wa Mageuzi ya Usimamizi wa Fedha za Umma (PFM)  Awamu ya IV. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi. Doroth Mwanyika.
   Baadhi ya waandishi wa habari  waliohudhuria hafla ya kusaini mkataba wa ushirikiano wa Mpango wa Mageuzi ya Usimamizi wa Fedha za Umma (PFM)  Awamu ya IV kati ya Serikali ya Tanzania na Finland leo jijini Dar es salaam.  (Picha zote na Eleuteri Mangi- MAELEZO).
     Serikali ya Tanzania yapokea zaidi ya Sh. Bilioni 10.
  Na Eleuteri Mangi -MAELEZO
  16/10/2014

  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea Sh. Bilioni 10.1 ambazo ni sawa na EURO milioni 4.8 kutika Serilkali ya Finland ikiwa kwa lengo la ushirikiano wa Mpango wa Mageuzi ya Usimamizi wa Fedha za Umma (PFM)  Awamu ya IV. Mkataba wa makubaliano hayo umesainiwa leo jijini Dar es salaam na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi. Doroth Mwanyika kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Balozi wa Finland nchini Bi. Sanikka Antila. 

  Bi. Doroth amesema kuwa Mpango wa Mageuzi ya Usimamizi wa Fedha za Umma Awamu ya nne ametanguliwa na Awamu ya I hadi III ambapo awamu hizo zimeonesha mafanikio mbalimbali nchini. Mafanikio hayo ni pamoja na ongezeko la ukusanyaji wa mapato kutoka Sh. Bilioni 390 mwaka 2009/2010 hadi zaidi ya Sh. Bilioni 700 kwa mwezi mwaka 2013/2014 na kuboresha mifumo ya kifedha kwa kutumia mifumo ya kielektroniki kwa kulipa moja kwa moja kwenye akaunti husika.

  Bi Doroth metaja mafanikio mengine kuwa ni ubureshwaji wa utendaji watumishi wanaosimamia masuala ya mpango wa PFM kupitia Ofisi ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) na utendaji kazi mzuri wa kamati za Bunge zinazohusika na ufuatiliaji wa matumizi ya Fedha za umma.

  Aidha, Bi. Doroth ameishukuru Serikali ya Finland kwa ushirikiano mzuri wanaoendelea kuipa Tanzania na kuahidi kuwa fedha hizo zitatumika katika malengo yaliyokusudiwa katika kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo kupunguza umasikini nchini.

  Naye Balozi wa Finland nchini Bi. Sanikka Antila amesema kuwa usimamizi mzuri wa fedha za umma (PFM) umeifanya nchi yake kuongeza fedha kwa ajili ya mpango huo. “PFM ni muhimu kwa utawala wa kidemokrasia, uchumi imara, ufanisi katika matumizi ya rasilimali zilizopo na hivyo kupunguza umasikini” alisema Bi. Sanikka.

  Ufanisi wa usimamizi mzuri wa fedha za umma umewezesha ufanisi wa malighafi zilizopo nchini katika kuboresha elimu, kutoa huduma bora za kiafya, kuongeza mazao ya kilimo na kuendeleza utalii.

  Mpango wa PFM upo katika awamu ya nne na ulianza 2012 na unatarajiwa kuishia 2017 ambapo awamu ya I hadi III ilianza 1998 na kumalizika 2012, Finland imekuwa nchi ya sita mhisani katika kusaidia mpango huu wa mageuzi. Nchi nyingine wahisani ni pamoja na Canada, Ujerumani Ireland na Uingereza. 

  0 0

   Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara,Phillip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana wakiwa kwenye kikao cha Halmashauri kuu ya CCM (NEC)  kilichofanyika katika Ukumbi wa White House mjini Dodoma leo.
  Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Halmashauri kuu ya CCM(NEC)  kilichofanyika katika ukumbi wa White House mjini Dodoma leo.
  Sehemu ya Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM (NEC) wakiwa kwenye kikao hicho kilichoongozwa na Mwenyekiti wake,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete (hayupo pichani) kilichofanyika katika ukumbi wa White House mjini Dodoma leo.(picha na Freddy Maro).

  0 0

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga akifafanua jambo wakati wa Kikao kazi cha Maafisa Vijana (hawapo pichani) kilichofanyika leo mjini Tabora,kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana nchini Bw. James Kajugusi.
   Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana nchuni Bw. James Kajugusi akitoa mada kuhusu majukumu ya Maafisa Vijana wakati kikao kazi cha Maafisa Vijana (hawapo pichani) kilichofanyika leo mjini Tabora
   Mkurugenzi wa Ubunifu wa Kampuni ya GODTEC Bw. Aloyce Midelo akielezea namna Kampuni yao inavyosaidia vijana katika kujiari kwa kuanzisha makampuni yao wenyewe.ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga (katikati) na Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi
   Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Elimu kwa Umma wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)  akifafanua namna NHC ilivyo saidia vijana kupitia mradi wa ufyatuaji wa matofali na ujenzi wa nyumba za gharama nafuu.Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga na Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi
   Meneja Miradi wa DSW Tanzania Bw. Avit Buchwa akielezea namna Shirika lao linavyosaidia vijana katika Nyanja ya Afya ya Uzazi. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga na Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi
   Baadhi ya Maafisa Vijana wakifuatilia mada mbalimbali kutoka kwa wawezeshaji (hawapo pichani)Picha na Frank Shija, WHVUM .

  0 0

   Meneja Mradi wa huduma kamilifu  kwa kinamama baada ya kuharibika kwa mimba Ngitoria Lemonduli akielezea malengo ya mradi huo mpya uliozinduliwa leo tarehe 16 Oktoba Hoteli ya Mnsons Shangani, Mjini Zanzibar.
   Mkuu wa Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya Zanzibar Dkt. Haji Mwita Haji akizindua Mradi mpya wa huduma kamilifu baada ya mimba kuharibika katika Hoteli ya Masons Shangani, Mjini Zanzibar.
   Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Marie Stopes Tanzania ambae ni Mkurugenzi Rasilimali watu na Utawala Bi Elly Reweta akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi na kufunga mafunzo kwa wahudumu wa Afya Zanzibar.
   Mgeni rasmi katika uzinduzi wa Mradi huo Mkuu wa Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya Zanzibar Dkt. Haji Mwita Haji akimkabidhi cheti mmoja wa washiriki wa mafunzo ya wiki mbili ya huduma kamilifu baada ya kuharibika kwa mimba ambayo yalidhaminiwa na  Shirika lisilo la Kiserikali la Marie Stopes Tanzania.
   Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Dkta Haji Mwita Haji akizungumza na washiriki wa mafunzo na wageni waalikwa katika uzinduzi wa mradi wa huduma kamilifu baada ya mimba kuharibika.
   Baadhi ya waalikwa na washiriki wa mafunzo ya wiki mbili ya huduma za akinamama baada ya kuharibika kwa mimba wakimsikiliza mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi huo.
  Daktari dhamana Kanda ya Unguja Dkt. Fadhil Mohd Abdalla akitoa shukrani kwa Shirika la Marie Stopes baada ya kudhamini mafunzo ya wiki mbili ya kuwajengea uwezo watoa huduma ya afya 20 wa mradi wa huduma kamilifu kwa kinamama baada ya kuharibika kwa mimba. (Picha na Makame Mshenga- Maelezo Zanzibar).

  0 0

   President Drk Jakaya Mrisho Kikwete welcomes UN Special Envoy fir the Great Lakes Region H.E Mr Said Djinnit at Dodoma State lodge. The Two leaders then held talks concerning the current situation in the Great Lakes Region. H.E Mr. Said Djinnit,  an Algerian diplomat, was appointed as a UN Special Envoy for the Great Lakes Region on 17th July, 2014 succeeding Mrs. Mary Robinson who was appointed as a UN Special Envoy for Climate Change.
   President DR.Jakaya Mrisho Kikwete poses for a photo with the UN Special Envoy for Great Lakes Region Mr.Said Djinnit (left) together with Mr. Alvaro Rodrigues who Resident Coordinator for the UN System in Tanzania(right) at Dodoma State lodge.
  President Drk Jakaya Mrisho Kikwete in talks with the  UN Special Envoy fir the Great Lakes Region H.E Mr Said Djinnit at Dodoma State lodge.
  Photos by Fred Maro

  0 0

   Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. George Simbachawene akizungumza na viongozi na watendaji wa Manispaa tatu za Jiji la Dar es Salaam kuhusu maagizo ya namna ya kusimamia maeneo ya wazi. Pia, ametoa siku 14 kuanzia jana Alhamisi kwa Manispaa hizo kubomoa maeneo ya wazi yaliyovamiwa ambayo yalikwishatolewa Ilani. Aidha, Naibu Waziri ametoa siku 30 kwa Manispaa ya Kinondoni kuwasilisha ofisini  kwake utaratibu wa namna ya kusafisha fukwe. 
   Watendaji wa Manispaa zote tatu za Jiji la Dar es Salaam pamoja na wataalam wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. George Simbachawene kuhusu namna yak usimamia maeneo ya wazi  jijini Dar. 
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. George Simbachawene (katikati) akitoa maagizo ya usimamizi wa maeneo ya wazi jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meya wa Manispaa ya Temeke Bw. Maabad Hoja na Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Bw. Khery Kessy.(Picha zote na Rehema Isango)

  0 0


  0 0  0 0

   Meneja wa Msanii wa Kimataifa T.I anayetarajiwa kuwasili chini , kwa ajiri ya kutumbuiza kwenye Tamasha la Fiesta 2014 hapo kesho katika viwanja vya Lidaz Club jijini Dar, Jonson Geter wa kwanza kushoto akifafanua jambo moja ya swali lililoulizwa na mmoja  wasanii walioshiriki kwenye semina ya fursa ndogo ya Wasanii na wadau wa muziki iliyofanyika kwenye ukumbi wa Litle Theather,jijini Dar,Pichani kulia ni Prodyuza  mahiri wa Muziki wa hapa nchini anayemiliki studioo yake ya Bongo Records,P-Funk Majani.

  Aidha Uongozi wa msanii huyo T.I leo umeshiriki  kwenye semina ya fursa Ndogo ya wasanii na wadau wa muziki iliofanyika kwenye ukumbi wa Little Theather ,jijini Dar kuzungumzia Fursa zilizoko katika biashara ya Muziki, Mada iliyoongelewa ni namna ya kujiongeza kwa kuangalia fursa za mbalimbalizi zilizomo kwenye tasnia hiyo na wakati msanii anapokuwa kwenye kilele cha mafanikio.  Fursa 2014 inakaulimbiu ya Jitathmini Jiamini Jiongeze.
  Sehemu ya meza kuu iliyoshiriki semina ya fursa Ndogo ya wasanii na wadau wa muziki iliofanyika kwenye ukumbi wa Little Theather ,jijini Dar kuzungumzia Fursa zilizoko katika biashara ya Muziki, Mada iliyoongelewa ni namna ya kujiongeza kwa kuangalia fursa za mbalimbalizi zilizomo kwenye tasnia hiyo na wakati msanii anapokuwa kwenye kilele cha mafanikio.  Fursa 2014 inakaulimbiu ya Jitathmini Jiamini Jiongeze.
  Mwimbaji wa bendi ya muziki wa dansi ya Skylight Band,Annet Kushaba akiuliza swali kwa uongozi wa msanii T.I kutoka nchini Marekani,kwenye fursa Ndogo ya wasanii na wadau wa muziki iliofanyika kwenye ukumbi wa Little Theather ,jijini Dar kuzungumzia Fursa zilizoko katika biashara ya Muziki, Mada iliyoongelewa ni namna ya kujiongeza kwa kuangalia fursa za mbalimbalizi zilizomo kwenye tasnia hiyo na wakati msanii anapokuwa kwenye kilele cha mafanikio.  Fursa 2014 inakaulimbiu ya Jitathmini Jiamini Jiongeze. 

   Msanii wa muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongofleva atambulikae kwa jina la kisanii la  CPWA akiuliza swali kwenye semina ya fursa ndogo iliofanyika leo jjini dar.

   Msanii wa bongofleva ajulikanae kwa jinal a Witness akiuliza swali kwa uongozi wa msanii T.I kutoka nchini Marekani,kwenye fursa Ndogo ya wasanii na wadau wa muziki iliofanyika kwenye ukumbi wa Little Theather ,jijini Dar kuzungumzia Fursa zilizoko katika biashara ya Muziki, Mada iliyoongelewa ni namna ya kujiongeza kwa kuangalia fursa za mbalimbalizi zilizomo kwenye tasnia hiyo na wakati msanii anapokuwa kwenye kilele cha mafanikio.  Fursa 2014 inakaulimbiu ya Jitathmini Jiamini Jiongeze.  
   Baadhi ya wapenzi na wadau wa muziki walioshiriki senina ya fursa wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo.
   Baadhi ya wapenzi na wadau wa muziki walishiriki pia.Kulia ni Msanii kutoka kampuni ya NO Fake Zone Linah na Rechael kutoka THT.

  0 0


   Meneja wa Mkoa wa Tabora Bw. Erasto Chilambo,  akimpa maelezo ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu Mkuu wa Mawasiliano na Huduma kwa Jamii Bi Susan Omari alipotembelea mradi huo ulioko eneo la Isikizya Wilayani Uyui jana. (Picha kwa hisani ya Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Jamii cha Shirika la Nyumba la Taifa)

   Mwonekanao wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC eneo la Isikizya Mkoani Tabora.

   Meneja wa Mkoa wa Tabora Bw. Erasto Chilambo akiendelea kutoa maelezo ya mradi kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Bi Susan Omari

   Nyumba 38 zilizojengwa karibu kabisa na Makao Makuu ya Wilaya ya Uyui eneo la Isikizya. Nyumba zingine 12 zimejengwa upande wa pili wa barabara eneo la Isikizya.


   Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa NHC, Bi Susan Omari akitoa maelekezo kwa Meneja wa Mkoa wa Tabora Bw. Chilambo

   Msimamizi wa mradi wa NHC isikizya Bw. Tokimu Mondo akitoa maelezo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu eneo la Isikizya jana.

   Sehemu ya nyumba zilizojengwa katika mradi wa nyumba za gharama nafuu eneo la Isikizya Wilayani Uyui zinavyoonekana.

   Meneja wa Mkoa wa Tabora Bw. Chilambo akitoa maelezo kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii Bi. Susan Omari yanayohusu viwanja vya Shirika vilivyoko eneo la Itetemia Manispaa ya Tabora.

   Meneja wa Mkoa wa Tabora Bw. Erasto Chilambo akielezea hatua mbalimbali zilifikiwa na Mkoa huo za kutengeneza nyumba za Shirika. Hili ni mojawapo ya jengo la Hoteli ya Golden Eagle baada ya kufanyiwa matengenezo.

   Sehemu ya mtaa wa Jamhuri/Shule wenye nyumba zilizofanyiwa matengenezo makubwa na NHC Mkoa wa Tabora

   Mojawapo wa jengo lililofanyiwa matengenezo na NHC Mkoa wa Tabora linavyoonekana kwa sasa

  Sehemu ya Maafisa Vijana wakisikiliza mada iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii wa NHC, Bi Susan Omari (hayuko pichani) alipoelezea mpango wa NHC wa kugawa mashine kwa ajili ya kusaidia vijana kwenye Halmashauri zote za Wilaya hapa nchini. Jumla ya mashine 656 zimeshambazwa kwa ajili hiyo.

   Washiriki wa semina iliyotolewa na NHC wakisikiliza mada kwa makini

   Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii wa NHC, Bi Susan Omari akitoa mada juu ya mpango wa NHC wa kusaidia vijana mashine za kufyatulia matofali katika Halmashauri zote za  Wilayanchini.
  Mmoja wa washiriki wa semina hiyo akilishukuru Shirika la Nyumba la Taifa kwa uamuzi wake wa kizalendo wa kusaidia vijana mashine ili waweze kujiajiri alipochangia mada iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii wa NHC.
  Katibu  Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, , Bibi Sihaba Nkinga akitoa maelezo wakati wa semina iliyotolewa na NHC mjini Tabora jana.

  0 0

  Mbunge wa Arumeru Magharibi,mkoani Arusha,Godluck Ole Medeye(kushoto) akitoa vifaa vya michezo kwa kiongozi wa timu ya Kitongoji cha Kazamoyo,Kata ya Bwawani kwaajili kuibua vipaji.
  Mbunge wa Arumeru Magharibi,mkoani Arusha,Godluck Ole Medeye(kushoto) akitoa vifaa vya michezo kwa kiongozi wa timu ya Kitongoji cha Nyamagana ,Kata ya Bwawani kwaajili kuibua vipaji.
  Mbunge wa Arumeru Magharibi,mkoani Arusha,Godluck Ole Medeye(kushoto) akitoa vifaa vya michezo kwa kiongozi wa timu ya Kitongoji cha Kazamoyo,Kata ya Bwawani kwaajili kuibua vipaji.

  Mbunge wa Arumeru Magharibi,mkoani Arusha,Godluck Ole Medeye(kulia) akitoa msaada wa mabati kwa wananchi waliothiriwa na mafuriko jimboni kwake.

  Katibu wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Nduruma,Ally Sululu(kulia)akipokea kiasi cha Sh.500,000 kutoka kwa Mbunge wa Arumeru Magharibi,mkoani Arusha,Godluck Ole Medeye alizoahidi kwaajili ya ukarabati wa Caravati la Kijiji hicho.

  Mbunge wa Arumeru Magharibi,mkoani Arusha,Godluck Ole Medeye(kulia) akikagua caravati linalowaondolea kero ya mawasiliano ,habari picha kwa  woindeshwww.woindeshizza.blogspot.comzza blog  0 0

  DSC_0043
  Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al Amin Yusuph akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mtungi kuzungumza na washiriki 31 wa mtandao wa redio jamii Tanzania (COMNETA) unaotekeleza mradi wa demokrasia na amani (DEP) kuelekea uchaguzi mkuu 2015 wanaohudhuria warsha ya siku nne inayoendelea mjini Dodoma.

  =======  =======  =======
  MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi amezitaka Redio za Jamii kutokubali kutumiwa na vyama vya siasa vinavyotumia unyonge wa watanzania kiuchumi kujinufaisha kisiasa.

  Alisema kwa kufanya maamuzi ya kutotumiwa na vyama vya siasa kutasaidia kuepusha migogoro inayochochewa na taarifa za kishabiki za vyamja vya siasa.
  Jaji Mutungi alisema hayo wakati akichangia mada tatu zinazohusu Sheria ya Gharama za Uchaguzi 2010, Sheria ya Vyama vya Siasa na Kanuni za Maadili ya vyama vya Siasa zilizotolewa kwa viongozi na wamiliki wa redio jamii nchini katika warsha inayoendelea mjini hapa.

  Aliwataka washiriki wa warsha hiyo ya siku nne inayohusu utekelezaji wa mradi wa kuendeleza majadiliano kwa njia ya amani kwa lengo la kukuza demokrasia nchini,kutambua kuwa baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakitumia unyonge wa kielimu na uchumi wa watanzania kuwaahidi mambo yasiyotekelezeka jambo ambalo amesema ni matumizi mabaya ya uhuru wa taasisi.
  DSC_0073
  Msaajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mtungi akizungumza na wadau wanaohudhuria warsha ya siku nne ya kutekeleza mradi wa uchaguzi unaolenga kuboresha Demokrasia na Amani nchini (DEP) kuelekea uchaguzi mkuu ujao unaofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo (UNDP) inayoendelea mjini Dodoma. Kushoto ni Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa shirika la kimataifa la sayansi, elimu na utamaduni (UNESCO) Bwana Al Amin Yusuph na Katikati ni Msajili msaidizi kutoka ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Bw. Ibrahim Sapi Mkwawa.

  Alisema vyombo vya habari vya jamii bado visafi na vina nafasi kubwa kubadilisha mitazamo ya utamaduni wa siasa chafu iliyojengeka kuwa maendeleo ni kupata uongozi wa siasa, tena kwa kauli za uwongo na kujenga chuki. “Maendeleo ni kuchagua kiongozi ambaye ni mwadilifu, mwenye uchungu na taifa na yuko tayari kuitunza amani tuliyoirithi baada ya kupata uhuru wa nchi.” alisema Jaji Mutungi.

  Mada hizo ziliwasilishwa na Wasaidizi wa Msajili wa Vyama vya Siasa Ibrahim Sapi Mkwawa, Sisty Leonard Nyahoza na Ofisa Sheria Mwandamizi Piencia Etanga kutoka ofisi ya Msajili wa Vyama Vingi vya Siasa.
  Msajili wa Vyama Vingi amesema, kwa kuwa Redio Jamii ndiyo zinazowafikia watanzania wenye maisha ya kawaida walio wengi vijijini na ndio wanaofuatwa na wanasiasa wa namna hiyo ili wawaunge mkono nia zao bila kujali maslahi ya wananchi.
  DSC_0246
  Wadau wa mradi wa uchaguzi wakifurahi jambo wakati Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mtungi (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao.
   
  Amezitaka redio jamii kuunganisha nguvu ya pamoja na wadau wakuu wa mradi wa uchaguzi kwa kuwaelimisha wananchi, kusema ukweli bila woga kitu chenye manufaa kwa umma hasa kuhusu wanasiasa matajiri kutumia raslimali zao katika kutafuta kura hali ambayo imeliingiza taifa katika wimbi la rushwa na umaskini wa kupindukia.
  Alisisitiza kuwa siasa ni ushindani na kushinda hivyo zisirubuniwe kirahisi kwa pesa ambazo sio msingi wa maendeleo.
  “Pesa sio msingi wa maendeleo, msikubali kurubuniwa wala kununuliwa na wachache wanaotumia nguvu ya pesa. Silaha kubwa ni kuunganisha nguvu na vyombo vya habari jamii tutafanikiwa kulijenga taifa.”
  Wakati huo huo ofisi ya Msajili wa Vyama Vingi imekuwa ikikabiliwa na matatizo kutokana na udhaifu wa sheria ambao wanasiasa wamekuwa wakiutumia kwa kutoa lugha chafu na za uchochezi ili waweze kuungwa mkono bila kujali maslahi ya taifa.
  DSC_0094
  Msajili msaidizi kutoka ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Bw. Ibrahim Sapi Mkwawa, akiwasilisha mada ya Sheria ya gharama za uchaguzi ya mwaka 2010 kwa wadau wanaotekeleza mradi wa uchaguzi unaolenga kuboresha demokrasia na amani nchini (DEP) katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu ujao, unaofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo (UNDP) kwenye warsha ya siku nne inayoendelea mjini Dodoma. Kutoka kulia meza kuu ni ........Sisty Leonard Nyahoza, Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji John Mkwawa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini (RPP), Jaji Francis Mtungi wakisikiliza kwa umakini mada zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye warsha hiyo.
  Mada nyingine iliyotolewa katika mkutano huo wa siku nne uliofadhiliwa kwa ushirikiano wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya UNDP na UNESCO iliyofanyika katika Ukumbi wa Waziri Mkuu mjini Dodoma ni Jinsia na Kuhusisha Makundi Maalum Katika Uchaguzi 2015 na Margareth Rugambwa kutoka Shirika la Umoja wa Kimataifa linaloshughulikia Kuwapatia Uwezo Wanawake (UN Women).
  Katika semina hiyo washiriki wameazimia kutumia redio jamii katika kufanikisha mawasiliano baina ya wananchi na vyombo vinavyosimamia masuala ya uchaguzi na siasa.
  DSC_0133
  Msajili Msaidizi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Sisty Leonard Nyahoza, akiwasilisha mada ya Sheria ya Vyama vya Siasa kwa wadau wa warsha ya mradi wa uchaguzi unaolenga kuboresha Demokrasia na Amani nchini (DEP) kuelekea uchaguzi mkuu mwakani inayoendelea mjini Dodoma kwenye ukumbi wa mikutano ofisi ya Waziri Mkuu.
  DSC_0124
  Sehemu ya washiriki wa warsha ya siku nne kwa wadau wa mradi wa uchaguzi 2015 unaolenga kuboresha demokrasia amani nchini (DEP)katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu ujao, unaofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo (UNDP) iliyoenda sambamba na mkutano wa tano wa Mtandao wa vyombo vya habari vya Kijamii nchini (COMNETA).
  DSC_0139
  Afisa Sheria Mwandamizi Piencia Etanga kutoka ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa akiwasilisha mada ya Kanuni za Maadili ya vyama vya Siasa zilizotolewa kwa viongozi na wamiliki wa redio jamii nchini katika warsha inayoendelea mjini Dodoma.
  DSC_0002
  Msajili msaidizi wa Vyama vya Siasa nchini (RPP), Jaji Francis Mtungi (kulia) akiteta jambo na mmoja wa wasaidizi wa ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Bw. Ibrahim Sapi Mkwawa (kushoto) kwenye washa ya siku nne ya wadau wa utekelezaji wa mradi wa uchaguzi unaolenga kuboresha demokrasia na amani nchini (DEP) kuelekea uchaguzi mkuu ujao inayofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maendeleo (UNDP).
  DSC_0028
  Mratibu wa Mradi wa kuboresha Demokrasia na Amani (DEP) kutoka ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Bi. Beatrice Stephano, akielezea utekelezaji wa mradi huo unaoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini chini ya ufadhili wa UNDP kwa wadau wa redio za jamii nchini.
  DSC_0015
  Katibu wa mtandao wa redio za jamii nchini (COMNETA), Bw. Abbas Mwakalinga (kushoto) akiteta jambo na Mwenyekiti wa COMNETA ambaye pia ni Mkurugenzi wa Redio ya Jamii FADECO ya wilayani Karagwe, Bw.Joseph Sekiku wakati wa warsha hiyo.
  DSC_0225
  Meneja wa Pambazuko FM Radio ya Ifakara, Bw. Joseph Kamata akihoji swala kwa wa wasilishaji mada kwenye warsha hiyo inayoendelea mjini Dodoma.
  DSC_0127
  Kutoka kushoto ni Mshauri wa UNESCO na Mlezi wa mtandao wa redio jamii (COMNETA), Balozi mstaafu Mh. Celestine Liundi, Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu pamoja na Afisa Habari na Mahusiano Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Bi. Salha Ali wakifuatilia kwa umakini mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa.
  DSC_0199
  Msajili wa Vyama vya Siasa nchini (RPP), Jaji Francis Mtungi akibadilishana mawazo na baadhi ya washiriki wa warsha ya siku nne inayoendelea mjini Dodoma kwenye ukumbi wa mikutano ofisi ya Waziri Mkuu.
  DSC_0186
  Mshauri wa UNESCO na Mlezi wa COMNETA, Balozi mstaafu Mh. Celestine Liundi (kulia) akibadilishana mawazo na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al Amin Yusuph wakati wakielekea kupiga picha ya pamoja na washiriki wa warsha hiyo.
  DSC_0168
  Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mtungi akifurahi jambo na rafiki yake wa siku nyingi Reportuer wa warsha ya wadau wanaotekeleza mradi wa uchaguzi inayoendelea mjini Dodoma Mchungaji Privatus Karugendo.
  DSC_0172
  Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mtungi, wakufunzi, wafanyakazi wa ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa wakiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki.
  DSC_0176

  0 0

  Mratibu wa Uhakiki wa Ubora wa Elimu kutoka Shirika la Kijamii la Masuala ya Elimu (Haki Elimu), Robert Mihayo akitoa mada kuhusu Ubora wa Elimu Tanzania wakati wa semina ya maadhimisho ya Siku ya Walimu Duniani iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Semina hiyo iliandaliwa na TENMET kwa kushirikiana na Chama Cha Walimu Tanzania (CWT).
  Mratibu wa Uhakiki wa Ubora wa Elimu kutoka Shirika la Kijamii la Masuala ya Elimu (Haki Elimu), Robert Mihayo akitoa mada kuhusu Ubora wa Elimu Tanzania wakati wa semina ya maadhimisho ya Siku ya Walimu Duniani iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Semina hiyo iliandaliwa na TEN/MET kwa kushirikiana na Chama Cha Walimu Tanzania (CWT).
  Ofisa Mradi wa TEN/MET, Alistidia Kamugisha (kulia), Meneja wa Fedha na Utawala (TEN/MET), Beatrice Malya (katikati) na Mratibu wa TEN/MET, Cathleene Sekwao. 
  Baadhi ya washiriki wa semina hiyo.
  Baadhi ya washiriki wa semina hiyo.
  Neema Kitundu kutoka National Coordinator Fawetz.
  Neema Kitundu kutoka National Coordinator Fawetz.
  Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Ukaguzi wa Shule Wizara ya Elimu ya Ufundi ya Ufundi, Dk. Edicome Cornel Shirima akitoa mada katika semina hiyo.
  Mkurugenzi Mafunzo ya Ualimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bakari Issa akitoa mada katika semina hiyo.
  Peter Mlimahadala kutoka Chama cha Walimu Tanzania akichangia mada katika semina hiyo. 
   Mratibu wa TEN/MET, Anthony Mwakibinga.

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika(MISATAN) Bwana Andrew Marawiti  akizungumza jambo wakati akifungua kongamano na maafisa habari wa taasisi za serikali zilizofanyika jana jijini Dar es Salaam.

  Maafisa habari mbalimbali kutoka wizara na mihimili tofauti ya nchi, jana walikutana katika hoteli ya JB Belmont hapa Dar es Salaam kujadili changamoto wanazo kumbana nazo wakati kwa kutoa taarifa kwa wananchi.

  Kongamano hilo linafuatia matokeo ya utafiti wa upatikanaji taarifa kwenye taasisi za umma uliofanywa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) nakuzinduliwa rasmi siku ya tarehe 28 Septemba, ambayo pia ni Siku ya Kimataifa ya Haki ya Kupata Taarifa.


  Miongoni mwa taasisi zilizoshiriki katika kongamano hilo ni Bunge, Mahakama, Wizara ya Katiba na Sheria, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Wizara ya Nishati na Madini, Idara ya Habari Maelezo, Mamlaka ya Taifa ya Vitambulisho (NIDA) na Idara ya Taifa ya Takwimu. Wizara za Afya na Mambo ya Nje hazikuweza kuwakilishwa licha ya kupata mwaliko. 

   Mwanasheria kutoka Taasisi Kitaifa ya Msaada wa Kisheria (National Organization of Legal Assistance-nola)  Bwana James Malenga akisisitiza jambo alipokuwa anawasilisha mada yake kwenye kongamano hilo la maafisa habari wa taasisi za kiserikali lililoandaliwa na Misa-Tanzania.
  Afisa Habari na Utafiti wa Misa-TanzaniaBwana Sengiyumva Gasirigwa akitoa ufafanuzi kwenye mada aliyokuwa anaiwasilisha kwenye kongamano la maafisa habari wa taasisi za kiserikali(hawapo picha)  
  Mfanyakazi wa  Misa-TanzaniaBwana Idrisa Abdallah akizungumzia adha anazozipata anapokuwa anakwenda taasisi na idara mbalimbali za serikali kupeleka barua ama maombi ya taarifa.
  Afisa habari wa Mahakama Bi. Mary C. Gwera akizungumza  jinsi ofisi yake ilivyopokea Tuzo ya Kufuli na ambavyo imekuwa chachu ya mabadiliko katika kutoa taarifa kwa umma.
  Afisa Mwandamizi wa habari kutoka Idara ya Habari Maelezo Bwana Abraham Nyantori akielezea changamoto za utoaji taarifa katika taasisi na idara za serikali.   Maafisa habari wakifuatilia kwa umakini mada ya Umuhimu wa Kutoa/Kupata Taarifa serikalini kutoka kwa mwanasheria wa kujitegemea Bwana James Marenga.
  Kaimu Mkurugenzi wa Misa-Tanzania Bwana Andrew Marawiti  akitoa shukrani wa wageni waliofika kwenye kongamano hilo.


older | 1 | .... | 388 | 389 | (Page 390) | 391 | 392 | .... | 1897 | newer