Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46366 articles
Browse latest View live

WACHINA WAVUTIWA NA KASI YA UKUAJI WA UCHUMI

$
0
0
Naibu Katibu Mtendaji (Uchumi Jumla), Prof. Longinus Rutasitara (Wapili kushoto) akizungumza na Ugeni kutoka Tume ya Mipango na Maendeleo ya China wakati walipofanya ziara nchini. Kushoto ni Naibu Katibu Mtendaji (Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Kiuchumi), Bw. Paul Sangawe.
Naibu Katibu Mtendaji (Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Kiuchumi), Bw. Paul Sangawe akizungumza wakati wa ziara hiyo. Kushoto ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri.


Na Saidi Mkabakuli

Ugeni kutoka Tume ya Mipango na Maendeleo ya China imevutiwa na kasi ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania hali inayochochewa na mipango thabiti ya kuvutia uwekezaji hasa kwenye Maeneo Maalum ya Kiuchumi (SEZs).

Akizungumza wakati wa kikao cha pamoja na viongozi wa Tume ya Mipango ya Tanzania, Kiongozi wa Msafara huo, Bw. Wang Jianjun ambaye ni Naibu Mkurugenzi Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, alisema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi chache barani Afrika zenye fursa kubwa ya kufikia maendeleo na kuweza kuondoka kwenye kundi la nchi maskini ndani ya kipindi kifupi kijacho.

Bw. Jianjun aliongeza “ili kuweza kufikia maendeleo ya haraka zaidi, Tanzania inapaswa kuwekeza katika viwanda ili kuongeza tija katika uzalishaji na kuongeza thamani bidhaa zake ili kuvutia masoko toka nje ya nchi.”

Akizungumza wakati wa kuwakaribisha wageni hao, Naibu Katibu Mtendaji anayeshughulikia Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Kiuchumi, Bw. Paul Sangawe, amesema kuwa Tanzania imedhamiria kuwa nchi ya viwanda ndani ya muda mfupi ujao.

“Tumedhamiria kuwekeza nguvu zetu kwenye uwekezaji katika viwanda; katika Mpango wa Pili wa Maendeleo, nguvu kubwa tunaiweka katika maendeleo ya viwanda ili kuweza kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025,” alisema Bw. Sangawe.

Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 imedhamiria kuifikisha Tanzania kuwa nchi yenye hadhi ya kipato cha kati na kuondokana na umaskini kufikia mwaka 2025.

MEGATRADE INVESTIMENT LTD YAIBEBA POLISI KILIMANJARO.

$
0
0
Mwakilishi wa Mauzo wa Kampuni ya Megatrade Investment Ltd,Roselian Laizer akimkabidhi jezi kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Moita Koka kwa ajili ya timu ya Polisi Kilimanjaro inayoshiriki ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa.kulia ni Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya jinai (RCO) ,Ramadhani Ng'anzi.
Mwakilishi wa Mauzo wa Kampuni ya Megatrade Investment Ltd,Roselian Laizer akimkabidhi Hundi ya kiasi cha shilingi milioni moja Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Moita Koka kwa ajili ya timu ya Polisi Kilimanjaro inayoshiriki ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa.kulia ni Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya jinai (RCO) ,Ramadhani Ng'anzi akishuhudia makabidhiano hayo.
Mwakilishi wa Mauzo wa Kampuni ya Megatrade Investment Ltd,Roselian Laizer akikabidhi Mpira kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Moita Koka kwa ajili ya timu ya Polisi Kilimanjaro inayoshiriki ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa.kulia ni Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya jinai (RCO) ,Ramadhani Ng'anzi akishuhudia makabidhiano hayo.
Mwakilishi wa Mauzo wa Kampuni ya Megatrade Investment Ltd,Roselian Laizer akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa vya michezo pamoja na Hundi kwa uongozi wa jeshi la polisi mkoa wa Kilimanjaro kwa ajili ya maandalizi ya timu ya Polisi Kilimanjaro inayoshiriki ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa.
Baadhi ya viongozi wa timu ya Polisi Kilimanjaro na wawakilishi wa Kampuni ya Megatrade wakishuhudia makabidhiano hayo.
Kaimu kamanda mkoa wa Kilimanjaro Moita Koka akizungumza mara baada ya kukabidhiwa msaada wa jezi pamoja na fedha toka kampuni ya Megatrade Investment ya jijini Arusha.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Moita Koka akikabidhi vifaa kwa nahoda wa timu ya Polisi ,Abdalah Amir mara baada ya kukabidhiwa na kampuni ya Megatrade Investment ya jijini Arusha.Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya kaskazini.

Vijiji 1,800 kupata mawasiliano ya simu mwakani

$
0
0
 Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia January Makamba  (Kulia) akizungumza katika mkutano wa wadau wa teknolojia ya Tehama (Capacity Africa 2014) ambapo amesema serikali itaondoa tatizo la mawasiliano nchini na huku ikitarajia kusambaza huduma hiyo kwa vijiji  1,800 ifikapo mwakani na vijiji 4,000 ikikapo mwaka 2017. Kushoto kwa Naibu Waziri Makamba ni  mkurugenzi wa kampuni ya Seacom Byron Clatterbuck na Mwakilishi wa kampuni ya internet solution Prenesh Padayachee.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Six Telecoms, Rashid Shamte akifafanua jambo kuhusiana na maendelea ya teknolojia ya Tehama nchini. Kampuni hiyo ni moja ya wadhamini wa mkutano huo unaofanyika nchini kwa mara ya pili.  Kulia ni Ofisa Biashara mkuu wa kampuni hiyo, Tinashe Bgoya.
 Ofisa Biashara mkuu wa kampuni ya Six Telecoms, Tinashe Bgoya (kushoto) akizungumzia maendeleo ya maendelea ya teknolojia ya Tehama nchini. Kulia ni Saidi Mohmed Alli ambaye ni Mkuu wa kitengo cha ‘Data’ cha kampuni hiyo.
 Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota (Kushoto) akifafanua jambo katika mkutano wa wadau wa mawasiliano ya Tehama ujulikanao kwa jina la Capacity Africa. kampuni hiyo ni moja wa wadhamini wa mkutano huo. Kulia ni Mwakilishi wa kampuni ya internet solution Prenesh Padayachee.
 
========  =====  ===== =======
Dar es Salaam. Jumla ya vijini 1,800 vinatarajia kupatiwa mawasiliano ya simu ya na teknolojia ya mawasiliano ya habari na mawasiliano (Tehama ) ifikapo mwakani.
 
Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa wadau wa Tehama wa Africa (Capacity Africa), Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia January Makamba alisema kuwa mpango huo upo katika hatua za mwisho na ifikapo mwaka 2017, jumla ya vijiji 4,000 zitakuwa vimepatiwa huduma hiyo.
 
Makama alisema kuwa serikali ipo katika hatua za mwisho kuzungumza na kampuni  ya simu kutoka Vietnam ijulikanayo kwa jina la Viettel na hivi karibuni wanatarajia kuzindua rasmi mpango huo.Alisema kuwa kuna vijiji mbali mbali Tanzania havina kabisa mawasiliano na jukumu la serikali kuhakikisha kuwa tatizo hilo linatatuliwa. 

Kwa mujibu wa Makamba sekta ya mawasiliano inazidi kukuwa na serikali imeweka mpango maalum kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma hiyo tena kwa ubora wa hali ya juu.Alisema kuwa sekta hiyo ina changamoto nyingi kutokana na kupanuka kwa teknolojia ya mawasiliano na tayari serikali imechukua hatua kukabiliana na tatizo hilo hasa baada ya kukamilika kwa hatua ya tatu ya mkongo wa Taifa wa mawasiliano.
 
“Mpaka sasa ni mkoa wa Simiyu tu haujafikiwa na mkongo wa taifa na hiyo imetokana na kugawanywa kwa mkoa wa Shinyanga, hata hivyo mikakati inafanyika ili kuhakikisha mkoa huo unapata huduma hiyo na kuanza kufurahia huduma ya Tehama,” alisema Makamba.Naye Mkurugenzi wa kampuni ya Six Telecoms, Rashid Shamte alisema kuwa anaamini kuwa kukamilika kwa mkongo wa Taifa kutanufaisisha nchi jirani ambazo hazina bahari.
 
Shamte ambaye kampuni yake ilidhamini mkutano wa mwaka 2012 alisema kuwa wanafuraha kubwa kuona nchi inafanya juhudi za kutatua tatizo la mawasiliano vijijini na nchi takribani nane zinazoizunguka Tanzania.
 
Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota alisema kampuni yao imeanzisha kitengo cha mtandao wa internet ambacho kitatoa huduma hiyo kwa bei nafuu.
 
“Lengo letu kubwa ni kurahisisha mawasiliano, hivyo tunawahikikishia kuwa watu wote wanaoishi vijijini watapata huduma hii kwa bei nafuu,”  alisema Ngota.

Halmashauri za majiji na manispaa zahimimizwa kutunza na kuhifadhi miradi yote ya maendeleo.

$
0
0
  NDG. ZUBERI M. SAMATABA, KAIMU KATIBU MKUU- OWM-TAMISEMI AKIFUNGUA MKUTANO HUO WA SIKU TATU.
 MR. ONOUR OZLY- MWAKILISHI WA BENKI YA DUNIA, ALIPOKUWA AKITOA MALEZO MAFUPI KUHUSU LENGO LA MKUTANO HUO.
 JANE JACOB- MWAKILISHI WA DANIDA ALIPOKUWA AKITOA SALAM ZA DANIDA KATIKA KIKAO CHICHO.
 WASHIRIKI WA MKUTANO HUO WAKIFURAHIA JAMBO WAKATI WA MKUTANO HUO.
 MHANDISI EZEKIELI MAGOTI KUNYALANYALA, AKIWASILISHA MADA KATIKA KIKAO HICHO.
=========  ==========  =======
Na: Atley Kuni- Afisa habari  Mwanza.
 
Halmashauri za majiji na manispaa zimehimizwa kutunza na kuhifadhi miradi yote ya maendeleo inayo tekelezwa katika maeneo yao na kuhakikisha inadumu kwa manufaa ya kizazi cha leo na kijacho.
 
Kauli hiyo imetolewa mapena hivi leo na Zuberi Samataba, Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) katika hoteli ya Gold Crest Jijini Mwanza wakati wa kikao cha pamoja baina ya TAMISEMI, Benki ya Dunia (World Bank) DANIDA na watendaji kutoka halmashauri zinazo tekeleza miradi ya Tanzania Strategic Cities Project (TSCP).
 
Samataba, amesema, kuna haja kwa kila halmashauri kuhakikisha inatunza miradi yote ambayo inafadhiliwa na wahisani hata baada ya wahisani kumaliza muda wao na kuondoka  kasha  miradi hiyo mikononi mwa Halmashauri. "Nivema mkawa  mnatenga fedha kwa ajili yakuhudumia miradi inayo anzishwa na wafadhili kwa ajili ya ukarabati na kuimarisha  ili iendelee kudumu kwa muda mrefu hata baada ya miradi hiyo kuisha muda wake na wafadhili kuicha mikononi mwetu".
 
Katika hatua nyingine  amewaagiza watendaji hao kutoa taarifa kwa wakati ili kujenga imani kwa wafadhili wanao toa fedha zao kwa ajili ya miradi mbali mbali ya maendeleo wanayo ifadhili, "Wenzetu suala la mrejesho ni muhimu sana lakini zaidi sana mrejesho kwa wakati,  kwani  ni kama wanasheria wanavyo amini kuwa HAKI ILIYO CHELEWESHWA NI HAKI ILIYO NYIMWA". 
 
 kwa mantiki hiyo kutoa taarifa kwa wakati ni suala muhimu sana,  vinginevyo au kinyume chake nikuwafanya wafadhili kupoteza imani kwa wanao wafadhili kwenye miradi amesema na kuongeza kuwa kwakuwa serikaliinaondoka kwenye utendaji wa kawaida na kuelekea kwenye utendaji wa upimaji ufanisi kwa matokeo (Performance for Result ) hivyo moja ya kigezo muhimu kitakachotumika ni kupima matokeo ni uwasilishaji wa taarifa kwa wakati.
 
Kikao hicho cha siku tatu kina wakutanisha Watendaji kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Halmashauri Jiji la Mwanza , Manispaa ya Ilemela, Manispaaya Kigoma Ujiji, Manispaa ya Dodoma, (CDA), Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Halmashauri ya mikindani Mtwara, Jiji la Tanga, Jiji la Arusha pamoja na wawakilishi wa DANIDA sambamba na  World Bank.

Kova akanusha utekaji wa watoto Dar es Salaam

$
0
0


Hussein Makame-MAELEZO
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limekanusha vikali uvumi unaoendelea kuzushwa jijini Dar es Salaam kuhusu utekeaji nyara wa watoto wadogo wanaosoma shule za jiji hilo na kuwataka wananchi kuupuuza.

Akizungmza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema kuwa mpaka sasa jeshi hilo halina taarifa yoyote ya mtoto kutekwa au kufanyiwa madhara yoyote kwa mtindo wa utekaji nyara.

“Jeshi la Polisi limegundua kwamba huu ni uvumi ambao haujulikani chanzo chake hivyo wananchi wanaombwa kuachana nao na kuupuza kwani unaleta hofu katika jamii bila sababu za msingi” alisema Kova.

Alisema kuwa pia uvumi huo umeanza kuleta usumbufu ambapo mnamo Oktoba 3 mwaka huu saa 3:00 asubuhi huko Vingunguti, mtu mmoja aitwaye Prosper Makame (34) akiwa na mkewe Marystella Munis (30) walipata usumbufu unaotokana na uvumi huo.

Kamishna Kova aliongeza kuwa watu hao ambao ni wafanyabiashara wa vyombo vya nyumbani walifika maeneo ya shule ya msingi Kombo iliyopo Vingunguti kwa ajili ya biashara zao, wakiwa na gari aina ya Noah yenye namba  T252 DAY, ghafla walizingirwa na watu wakidaiwa wanateka wanafunzi.

“Pia mnamo Oktoba 13, 2014 majira ya saa 4:00 asubuhi huko katika kituo cha Polisi Tabata uliibuka uvumi kuwa gari namba T548 BUN aina ya Noah rangi nyeusi ambayo ni mali ya askari polisi A/INSP Ester wa kikosi cha usalama barabarani, ilivumishwa kwamba ndani ya gari hiyo kuna vichwa vitano vya watoto wa shule ya msingi Mtambani na kusababisha wazazi wenye watoto wanaosoma shule hiyo kukusanyika kituoni hapo ili kushuhudia na kuona vichwa hivyo” alisema Kamishna Kova na kuongeza:


“Na ndipo Mkuu wa kituo hicho  cha Polisi aliamuru gari hilo lifunguliwe na kuwathibitishia wananchi kuwa habari hizo ni za uongo na uvumi”
Kutokana na tukio hilo jeshi hilo lilifanya uchunguzi na kumkamata mtu mmoja Gilbert Stanley (32) mhehe mkulima na mkazi wa Tabata alipohojiwa alikiri kueneza habari hizo na kudai yeye aliambiwa na mtu ambaye hakumkumbuka.

Hivyo, Kamishna Kova alisisitiza kuwa uvumi wa kuwepo kwa kikundi cha wahalifu wanaowateka watoto wanafunzi si wa kweli hata kidogo na hivyo wananchi wanatakiwa kuepukana na taarifa hizo kwani zinaweza kusababisha uvunjifu wa amani.

Katika hatua nyingine, Kamishna Kova alithibitisha kutokea kwa vifo vya watu watano na wengine 16 kujeruhiwa katika ajali ya moto iliyotokea Oktoba 13 mwaka huu majira ya saa 5:00 usiku huko kwenye mzunguko wa Mbagala Charambe baada ya lori aina ya Scania  T347 BXG lilipoanguka likiwa na mafuta aina ya petrol lita 38,000.

Aliwataja waliofariki kuwa ni Masoud Masoud mkazi wa Charambe, Hassani Mohamed mkazi wa Mbagala Kibangulile, Mohamed Ismail, Ramadhani Halfan na Maulidi Rajabu wote ni wakazi wa Mbagala Charambe.

Alisema kuwa majeruhi wamelazwa kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili na hospitali ya wilaya ya Temeke wakiendelea na matibabu huku ajali hiyo pia ikisababisha nyumba ya kulala wageni iitwayo United kuungua moto na kuteketea kwa pikipiki saba za bodaboda zilizokuwa zimeegeshwa karibu na aneo hilo, maduka matano yenye bidhaa zenye thamani ya shilingi Milioni 197 yaliungua moto.

Kamishna Kova aliwataka wananchi kuacha tabia ya kukimbilia kwenye ajali za magari ya mafuta kwani ni hatari kwa maisha yao kwani watu wengi waliojeruhiwa walikuwa wakichota mafuta yaliyomwagika kutokanana ajali hiyo.

Katika tukio lingine,Kamishna Kova alisema kuwa Jeshi hilo limefanikiwa kumkamata jambazi sugu aitwaye Paulo Thamas Milanzi maarufu Chinga  (35) mmakonde mkazi wa  Chanika ambaye baada ya majibizano ya risasi jambazi hilo lilijeruhiwa na kufikshwa hospitali ya muhimbili kwa matibabu ingawa baadaye alifariki dunia.

Alisema jambazi hilo lilikuwa likitafutwa na polisi kutokan na kuhusika kwenye matuio ya mauaji na wizi ikiwemo tukio la kuuawa kwa Afisa Mwandamizi wa Usalama wa Taifa, Sylivabus Adrian Mzeru Aprili 29 mwaka huu liliotokea Uwanja wa Ndege.

Aliongeza kuwa jambazi lilikamatwa na bastola aina ya Star ambapo majambazi wenzake walikamatwa na sasa wako gerezani, hivyo ameitahadharisha jamii iachane na uhalifu kwani hauna manufaa yoyote.

MAKAMU WA RAIS DKT. MOHAMMED GHARIB BILAL AZINDUA RASMI UKUMBI WA MIKUTANO WA MWADHAMA LAUREAN KADINALI RUGAMBWA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania Mhashamu Askofu Tarcius Ngalekumtwa, wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Mwadhama Laurean Kadinali Rugambwa Oysterbay jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuhudhuria hafla ya makabidhiano ya ukumbi huo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Askofu wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Mwadhama Polycap Kadinali Pengo kwa pamoja wakikata utepe kuzindua rasmi ukumbi wa Mwadhama Laurean Kadinali Rugambwa Oysterbay jijini                        Dar es salaam
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua pazia kuzindua rasm ukumbi wa Mwadhama Laurean Kadinali Rugambwa Oysterbay jijini Dar es salaam
Muonekano wa nje wa ukumbi wa Mwadhama Laurean Kadinali Rugambwa Oysterbay jijini Dar es salaam

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YAZINDUA RASMI USAMBAZAJI WA MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2012.

$
0
0
 Baadhi ya washiriki wa Semina ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 wakifuatilia masuala mbalimbali leo mkoani Pwani.
 Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi 2012 Hajjat Amina Said Mrisho akimkabidhi machapisho ya Sensa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Bi. Mwantumu Mahiza (aliyekaa) akizindua rasmi Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 leo mkoani Pwani.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Bi. Mwantumu Mahiza (aliyekaa) akizindua rasmi Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 leo mkoani Pwani. Nyuma yake  ni viongozi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Dkt. Albina Chuwa (kushoto).
 Baadhi ya washiriki wa Semina ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 wakiangalia moja ya ramani  inayoonyesha takwimu ya Mgawanyo wa Watu kwa umri na Jinsi na taarifa za Msingi za Kidemografia, Kijamii na Kiuchumi.
Washiriki wa Semina ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 wakiangalia moja ya ramani  inayoonyesha takwimu ya Mgawanyo wa Watu kwa umri na Jinsi na taarifa za Msingi za Kidemografia, Kijamii na Kiuchumi.

 Washiriki wa Semina ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 wakiwa katika picha ya pamoja.


 Picha na Habari na 
Aron Msigwa–MAELEZO
Ofisi ya Taifa ya Takwimu imezindua rasmi usambazaji wa matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi  ya mwaka 2012 na kuwataka wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa wilaya na mikoa kote nchini kuanza kutumia na kuhamasisha matumizi ya takwimu rasmi zilizotolewa na ofisi hiyo katika kupanga mipango ya maendeleo.

Hayo yamebainishwa leo mkoani Pwani na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa wakati akiwakaribisha viongozi, watendaji na wadau mbalimbali wa mkoa wa Pwani waliohudhuria semina ya usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012.

Amesema Tanzania ina takwimu bora kutokana na kazi kubwa iliyofanywa  na Ofisi yake kwa kushirikiana na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  kuandaa na kukamilisha taarifa za matokeo ya Sensa yakiwemo machapisho matatu yanayohusu Idadi ya Watu katika ngazi ya Utawala, chapisho la Mgawanyo wa Watu kwa umri na Jinsi na chapisho la Taarifa za Msingi za Kidemografia, Kijamii na Kiuchumi.

Dkt. Chuwa ameeleza kuwa Ofisi ya Taifa ya Takwimu inaendelea na mikakati mbalimbali ya kuhamasisha matumizi ya takwimu za matokeo ya Sensa katika ngazi ya mkoa, wilaya na vijiji ili ziweze kutumika katika kupanga mipango ya maendeleo.

Ameeleza kuwa takwimu zitakazowasilishwa katika maeneo mbalimbali katinga ngazi ya kijiji, wilaya na mikoa ukiwemo mkoa wa Pwani ambao umezindua rasmi shughuli hiyo ya usambazaji wa matokeo zitahusu Umri, Jinsi na Viashiria muhimu vya umri katika makundi, hali ya ndoa, hali ya uyatima na vifaa vilivyotumika katika ujenzi wa nyumba .

Amesema lengo la usambazaji wa takwimu hizo ni kueleza hali halisi ya mafanikio ya mikoa katika Nyanja za uchumi, umasikini, elimu na afya ili kuwezesha uboreshaji wa maeneo ambayo hayafanyi vizuri.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Bi. Mwantumu Mahiza akizindua rasmi Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 kwa ngazi ya vijiji, Wilaya na mikoa ameeleza kuwa usambazaji wa matokeo hayo  utawasaidia na kuwarahisishia viongozi wa maeneo mbalimbali kupanga Bajeti  na mipango ya maendeleo.

Amesema matumizi ya takwimu sahihi yatawezesha upelekaji wa huduma za jamii zikiwemo shule, hospitali, ujenzi wa masoko, huduma za maji na kuirahisishia serikali kuwafikishia wananchi huduma hizo kutokana na takwimu zilizoainishwa katika maeneo husika na kuiepusha serikali kuwekeza fedha nyingi katika miradi ambayo haiendani na idadi ya watu katika eneo husika.

Ameongeza kuwa matumizi ya takwimu hizo kuanzia ngazi ya familia hadi taifa yatasaidia kupunguza na kuondoa migogoro ya ardhi hususani kurahisisha suala la umiliki na mgawanyo wa ardhi kulingana na idadi ya watu na huduma. 

Bi.Mahiza ametoa wito kwa viongozi mbalimbali wa serikali na madhehebu ya dini kote nchini kuwahamasisha wananchi kutumia takwimu zitakazosambazwa katika maeneo mbalimbali nchini. 

Naye mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu Duniani (UNFPA) nchini Tanzania Bw.Colins Opiyo akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo amesema kuwa UNFPA itaendelea kushirikiana na Tanzania ili kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa na takwimu sahihi.

Amesema kuwa ili takwimu ziwe sahihi lazima ziendane na uhalisia wa eneo husika, zitolewe katika muda maalum , zikidhi vigezo vilivyowekwa kimataifa na kutafsiriwa kulingana na shughuli za kiuchumi za wananchi wa Tanzania wakiwemo wakulima, wafugaji na wafanyabiashara.


Wadhamini waanza kujitokeza Mbio za Uhuru Marathon

$
0
0
Meneja wa Kinywaji cha Grand Malt,Mama Consolata Adam (katikati) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi Milioni 35 kwa Mratibu wa Mbio za Uhuru Marathon,Innocent Melleck (kulia) wakati wa hafla fupi ya makabidhiano hayo iliyofanyika leo jijini Dar.Kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Shirikisho la Riadhaa Tanzania (RT), Tullo Chambo.
 Meneja wa Kinywaji cha Grand Malt,Mama Consolata Adam akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) wakati wa kutanganza udhamini wa mbio fupi (half marathon) katika Mbio za Uhuru Marathon zinazotarajia kufanyika Desemba 7,2014 jijini Dar es Salaam.Grand Malt imetoa kiasi cha Milioni 35 ili kufanikisha mbio hizo.
 Mratibu wa Mbio za Uhuru Marathon,Innocent Melleck (kulia) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) wakati akitoa shukrani zake kwa Kampuni ya TBL kupitia kinywaji chake cha Grand Malt kwa udhami huo walioutao katika mbio hizo.Katikati ni Meneja wa Kinywaji cha Grand Malt,Mama Consolata Adam na Kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Shirikisho la Riadhaa Tanzania (RT), Tullo Chambo.

MFUKO WA PENSHENI WA LAPF KUFANYA MKUTANO WA 7 WA MWAKA WA WADAU JIJINI ARUSHA OKTOBA 23-24,2014

Bayport Tanzania yazindua huduma mpya ya Mikopo ya bidhaa

$
0
0


 Meneja wa Masoko na mawasiliano wa taasisi ya kifedha ya Bayport Tanzania, Ngula Cheyo (wa kwanza kushoto),  akiwa kwenye picha ya pamoja na Meneja masoko wa Fair Deal Auto (pvt) Limited, wasambazaji wa pikipiki aina ya Boxer na Bajaji, Saimon Paul  pamoja na  Meneja Bishara wa Bayport, Thabit Mndeme (kulia),  wakati wa utambulisho wa kuzindua huduma hiyo ya Mikopo ya bidhaa.


 Meneja wa Masoko na mawasiliano wa taasisi ya kifedha ya Bayport Tanzania, Ngula Cheyo (wa kwanza kushoto),  akifuatiwa na Meneja masoko wa Toyo,  Drima Makachwa (katikati)  pamoja na  Meneja Bishara wa Bayport, Thabit Mndeme (kulia), kwenye uzinduzi huo.


Meneja wa Masoko na mawasiliano wa taasisi ya kifedha ya Bayport Tanzania, Ngula Cheyo (katikati) akiongea na wandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa utambulisho wa huduma ya Mikopo ya bidhaa. Picha zote na Andrew Chale.

=========== ======= ======


Taasisi ya kifedha ya Bayport Tanzania  mapema leo Oktoba 15, 2014 imezindua huduma mpya ijulikanayo kama Mikopo ya bidhaa ikiwa na lengo la kurahisisha utendaji kazi wa watumishi wa umma na wafanyakazi wote wa kampuni zilizoidhinishwa na Bayport. 


Uzinduzi  huo ulifanyika katika ofisi za makao makuu ya Bayport, maeneo ya Moroco jijini Dar es Salaam mbele ya wandishi wa vyombo mbalimbali vya habari  umeonyesha matumaini mapya ya watanzania wanaosumbukia usafiri katika vituo vyao vya kazi, hususani maeneo ya mikoani ambako mara kadhaa kumesikika malalamiko ya maisha magumu kwa watumishi wa umma. 


Akizungumza juu ya tukio hilo, Meneja Bishara wa taasisi hiyo Thabit Mndeme alisema kwamba ni wakati wa kukuza uchumi wa nchi kuhakikisha kuwa watu wanafanya kazi kwa bidii na shauku.
Alisema wapo watumishi ambao wanaishi kwa tabu kutokana na changamoto ya usafiri na mahitaji mengine ya kijamii ,hivyo kutokana na huduma hiyo mpya ya kukopeshwa pikipiki ,boda boda itasaidia kwa kiasi chake. 


Pia alisema Bay port imekaa kuangalia namna ganib watanzania wataendelea kufanya kazi kwa moyo na kukuza uchumi ambao uko sambamba na kuwakopesha  fedha kama wanavyofanya kwa sasa na kuamua kuwakopesha tena na bidhaa za usafiri. 


Naye Meneja wa Masoko na mawasiliano wa taasisi hiyo Ngula Cheyo alisema kuwa mikopo mipya kwa sasa inapatikana kwa masaa 24, huku ikipatikana pia kwa mikoa na wilaya zote kwenye ofisi za Bayport zaidi ya 80, nchini. 


Bayport ni Taasisi ya kifedha isiyo ya kibenki inayoongoza katita utowaji wa mikopo barani Africa na Amerika ya kusini .imeanzishwa mwaka 2001, na umiliki wake ukiwa Mauritius.

RAIS KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU CCM MJINI DODOMA JIONI HII

$
0
0
 Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu  ya Halmashauri Kuu ya Taifa CCM kwenye ukumbi wa NEC,CCM Makao Makuu Dodoma.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisoma taarifa fupi ya ufunguzi wa kikao kwenye ukumbi wa NEC mjini Dodoma.
 Katibu wa NEC Uchumi na Fedha Bi.Zakia Meghji akizungumza na Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Mohamed Seif Khatib wakibadilishana mawazo muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa mjini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Ndugu Mwigulu Nchemba akizungumza na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye katika ukumbi wa NEC kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM mjini Dodoma.

Kampuni ya TTCL yaanzisha kituo cha interneti 'IP Pop'

$
0
0
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba (kulia) akizungumza na wanahabari mara baada ya mkutano wa wadau wa mawasiliano Afrika ikiwemo kampuni ya TTCL. Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba (kulia) akizungumza na wanahabari mara baada ya mkutano wa wadau wa mawasiliano Afrika ikiwemo kampuni ya TTCL.Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba akizungumza katika mdahalo wa wadau wa mawasiliano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.  
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba akizungumza katika mdahalo wa wadau wa mawasiliano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba akizungumza katika mdahalo wa wadau wa mawasiliano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba akizungumza katika mdahalo wa wadau wa mawasiliano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.Kampuni ya TTCL yaanzisha kituo cha interneti 'IP Pop' Kampuni ya TTCL yaanzisha kituo cha interneti 'IP Pop'Ofisa Mkuu Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota (kushoto) akizungumza na wanahabari mara baada ya mkutano wa wadau wa mawasiliano Afrika ikiwemo kampuni ya TTCL. 
Ofisa Mkuu Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota (kushoto) akizungumza na wanahabari mara baada ya mkutano wa wadau wa mawasiliano Afrika ikiwemo kampuni ya TTCL.Ofisa Mkuu Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota (kushoto) akizungumza katika mdahalo wa wadau wa mawasiliano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Ofisa Mkuu Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota (kushoto) akizungumza katika mdahalo wa wadau wa mawasiliano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Kampuni ya TTCL yaanzisha kituo cha interneti 'IP Pop' Kampuni ya TTCL yaanzisha kituo cha interneti 'IP Pop'.Ofisa Mratibu wa Ufundi wa TTCL, Mhandisi Anifa Chingumbe (kushoto) akimwelezea. 
Ofisa Mratibu wa Ufundi wa TTCL, Mhandisi Anifa Chingumbe (kushoto) akimwelezea.Baadhi ya wadau washiriki katika mkutano wa wadau wa mawasiliano Afrika ikiwemo kampuni ya TTCL wakifuatilia mkutano huo. Baadhi ya wadau washiriki katika mkutano wa wadau wa mawasiliano Afrika ikiwemo kampuni ya TTCL wakifuatilia mkutano huo.


KAMPUNI ya Simu nchini Tanzania (TTCL) imeanzisha kituo cha kuuzia huduma za interneti 'IP Pop -Internet Protocol Point of Presence' nchini ikiwa ni jitihada za kuboresha huduma za mawasiliano zaidi. Huduma kama hii awali ilikuwa ikinunuliwa nje hasa makampuni anuai yanayotoa huduma hizo barani ulaya. 

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Ofisa Mkuu Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota alipokuwa akizungumza na wanahabari katika mkutano wa wadau anuai wa mawasiliano kutoka nchi za Afrika Mashariki na baadhi za mataifa ya Afrika unaofanyika Tanzania. Ngota alisema kampuni ya TTCL imekuwa na mchango mkubwa wa kusimamia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ili kuwawezesha Watanzania na hata nchi jirani kupata mawasiliano mazuri kutoka katika nchi zao hadi katika nchi za ulaya.

 "...Kuna juhudi mbalimbali TTCL tunafanya ili kuongeza fursa kwenye mawasiliano ambapo kwa sasa tumefungua kituo cha kuuzia interneti hapa nchini, kinaitwa IP Pop (Internet Protocol Point of Presence). Awali interneti tulikuwa tunaenda kununulia London kwenye makampuni mbalimbali sasa hivi tumeanzisha kituo chetu cha kununulia intaneti hapa hapa nchini...Kwa hiyo tunawakaribisha watumiaji wa interneti kuja kununua huduma hizi kwetu," alisema Ngota. 

Akizungumzia mkutano huo, Ngota alisema wadau wa mawasiliano Afrika ikiwemo TTCL imejipanga vizuri kutumia fursa ambazo zinaweza kupatikana nchini na nje ya nchi ili kuendeleza sekta ya mawasiliano. "...Unapopiga simu lazima uende hadi nchi za nje kupata ile njia alafu ndo unarudi ulipo Afrika sasa hivi tunaangalia namna gani tutajikwamua na huduma kama hizo kuzipata hapa hapa Afrika..." alisema ofisa huyo wa TTCL. 

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba akizungumzia mkutano huo alisema mkutano huo ni muhimu kwani wadau wa mawasiliano wamekutana kujadili maendeleo ya sekta ya mawasiliano, hasa katika ukanda wa afrika mashariki na afrika kwa ujumla. Alisema Tanzania inategemewa sana na nchi karibia saba ambazo zipo pembezoni mwa bahari kupitia huduma ya mkongo wake wa mawasiliano. 

"Mkongo wa mawasiliano wa kimataifa umetua katika bahari yetu na sisi tunauza huduma hiyo kwa nchi nyingine...Tumeupeleka hadi kwenye mipaka ya majirani zetu kama Rwanda, Burundi, Malawi, Zambia na wengineo ambao hawana mawasiliano." Makamba alisema mpango wa Serikali ni kuhakikisha kila Mtanzania anapata mawasiliano mazuri na yalio bora maana hiyo ni haki yake. Sera na kanuni za Serikali ni kuhakikisha hilo linafanikiwa. Aliongeza kuwa kwa kulitambua hilo Serikali imewekeza kiasi kikubwa cha fedha kujenga mkongo wa taifa wa mawasiliano.

 "..Na sasa tunaingia kwenye awamu ya tatu ya upanuzi wa mkongo huo ikiwa ni sambamba na uboreshaji wa mawasiliano, ili ufike kila wilaya nchini, Watanzania wengi maeneo ya vijijini bado hawana mawasiliano, sehemu nyingine hakuna mawasiliano kabisa au pengine yapo lakini si mazuri. Aidha alibainisha kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2015 maeneo yote ambayo hayana mawasiliano yanapata mawasiliano, hii ni pamoja na kukaribisha makampuni mapya yaweze kuwekeza katika sekta hii ili uwepo ushindani kwamba kama kuna maeneo kampuni fulani haitaki kwenda basi nyingine ziende huko.

 "...Mkongo wa taifa wa mawasiliano ni biashara na majirani zetu wanategemea na wananunua huduma hiyo kutoka kwetu. Tunachokifanya ni kuiimarisha kampuni ya TTCL hadi sasa wanafanya kazi nzuri sana wana wadau na washirika wengi toka nchi jirani ambapo wanafanya nao biashara. Kazi ya Serikali ni kuiwezesha ili biashara hiyo iwe kubwa zaidi," alisema Makamba. *Imeandaliwa na www.thehabari.com

masuala mbalimbali yanayohusu uchumi wa Tanzania yajadiliwa

$
0
0
 Baadhi ya viongozi wa Wizara ya fedha wakifuatilia kwa makini mkutano uliokuwa ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali  Dr. Servacius Likwelile, ambapo ujumbe kutoka Tanzania ulikutana na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Phippe Dongier hawapo kwenye picha kwa madhumuni ya kujadili masuala mbalimbali yanayohusu uchumi wa Tanzania. 

Kutoka kushoto ni Bw. John Cheyo ambaye ni Kamishna wa Bajeti, anayefuata ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar Bi Amina na wa kushoto kwake ni Bw. Said Magonya ambaye ni Kamishna wa Fedha za nje Wizara ya Fedha.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali  Dr. Servacius Likwelile alipokuwa akitoa msimamo wake kuhusu sera zinazopendekewa na Benki ya Dunia  kwa mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia kwa Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Phippe Dongier.
 Dr. Servacius LikwelileKatibu Mkuu wa Wizara ya Fedha  na Mlipaji Mkuu wa serikali  akiwa pamoja na ujumbe kutoka Tanzania. Kutoka kulia ni Gavana wa Benki kuu ya Tanzania na kutoka kushoto ni  Bi. Natu Mwamba Naibu Gavana wa Benki kuu ya Tanzania wakimsikiliza kwa makini Bw. Phippe Dongier ambaye ni mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia kwa Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi hayupo kwenye picha, alipokuwa akijibu hoja zilizowekwa mezani.
Bw. Phippe Dongier ambaye ni mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia kwa Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi alipokuwa akijibu hoja zilizotolewa na Dr. Servacius LikwelileKatibu Mkuu wa Wizara ya Fedha  na Mlipaji Mkuu wa serikali  na kuahidi kuzifanyia kazi.
Picha zote na Ingiahedi Mduma – Washington DC.

ELIMU YA URAIA NA UPIGAJI KURA HAIPASWI KUWA NA UTASHI WA KISIASA WALA UPENDELEO

$
0
0
DSC_0087
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa shirika la kimataifa la sayansi, elimu na utamaduni (UNESCO) Bwana Al Amin Yusuph akielezea madhumuni ya warsha ya wadau wa mradi wa uchaguzi 2015 unaolenga kuboresha demokrasia amani nchini katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu ujao, unaofadhiliwa na Shirika La Kimataifa la Maendeleo (UNDP) ulioenda sambamba na mkutano wa tano wa Mtandao wa vyombo vya habari vya Kijamii nchini (COMNETA).

Uchaguzi huru na wa haki utafanikiwa iwapo wananchi watapewa elimu sahihi ya uraia na upigaji kura itakayohamasisha wapiga kura kufanya maamuzi sahihi wakati wa uchaguzi. Hayo yamesemwa na Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji John Mkwawa kwenye washa ya siku nne ya wadau wa utekelezaji wa mradi wa uchaguzi unaolenga kuboresha demokrasia na amani nchini kuelekea uchaguzi mkuu ujao .

Kamishina alisema elimu ya uraia ni muhimu kwa wananchi ili kuwahamasisha ushiriki wao katika demokrasia na kwamba haipaswi kuwa na utashi wa kisiasa au upendeleo kwa chama chochote cha siasa.

Akitoa mada katika warsha hiyo inayofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maendeleo (UNDP) Jaji Mkwawa alisema katika kutoa elimu hiyo wanahabari hawana budi pia kuzingatia miongozo iliyowekwa ya kutofungamana upande wowote kisiasa na kutoa habari kwa usahihi kuhakikisha kwamba makundi yote yanapewa fursa na haki sawa.
DSC_0124
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo (UNDP) Godfrey Mulisa akisoma risala ya ufunguzi wa warsha hiyo kwa niaba ya Philippe Poinsot inayoendelea kwenye ukumbi wa mikutano ofisi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma.

“Pamoja na changamoto zinazozikabili redio jamii, zina mchango mkubwa katika mchakato wa uchaguzi kwa sababu idadi kubwa ya Watanzania hawajui kusoma na kuandika hivyo kutegemea redio. Kwa misingi hiyo ni vyema kwa waandishi wa habari wa redio jamii kusaini mwongozo wa maadili ambayo yataonyesha utekelezaji wao kwa kutopendelea chama chochote cha siasa au mgombea yoyote yule ”.

Amependekeza pia umuhimu wa kuielewa jamii inayolengwa wakati wa kutayarisha vipindi vya elimu ya uraia na utekelezaji ili taarifa zinazotolewa kwao zikidhi matakwa ya sehemu hiyo. Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji John Mkwawa ametoa mfano wa kuilewa jamii kuwa ni pamoja na kufahamu sababu zinazowafanya wananchi wasijitokeze kwa wingi katika upigaji kura iwapo kunasababishwa na ukosefu wa taarifa muhimu na sahihi, kukosa motisha ya kupiga kura, utashi na kutokuwepo kwa ushindani katika kugombea.

“Katika uchaguzi mkuu mwaka 2010 watu wachache sana walijitokeza kupiga kura pamoja na jitihada zote za kuhamasisha na kuelimisha upigaji kura, na baadhi ya sababu ni kwamba kupiga kura hakutampa faida yoyote mpiga kura, au kupiga kura hakutaleta mabadiliko yoyote na kutouamini mfumo mzima wa uchaguzi”.
DSC_0005
Mwenyekiti wa mtandao wa vyombo vya habari vya kijamii Tanzania (COMNETA) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Redio ya Jamii FADECO wilayani Karagwe, Bw.Joseph Sekiku akieleza kwa ufupi maendeleo ya COMNETA wakati wa sherehe za ufunguzi za mkutano wa tano wa Mtandao wa vyombo vya habari vya Kijamii nchini (COMNETA) unaofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma.


Masuala mengine yanayopaswa kufahamika ni sehemu wanakoishi walengwa ili kubaini iwapo kuna miundombinu ya kutosha hususan kiwango cha elimu na uelewa wao katika masuala ya uchaguzi ili kurahisisha utekelezaji wa mradi husika.

Amezishauri redio za jamii pia kuelewa ni mabadiliko gani yametokea katika uongozi wa uchaguzi, kanuni na maelekezo ya uchaguzi na sababu mbalimbali zinazotakiwa kuwafahamisha walengwa wa makundi mbalimbali wakiwemo wanawake, watu wenye ulemavu, vijana na makundi maalum hususan wazawa, wachungaji, watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi na Watu wenye ulemavu wa ngozi ili waweze kushiriki kikamilifu katika uchaguzi.
Wakati huo huo Godfrey Mulisa akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkazi wa UNDP Philippe Poinsot alikumbusha baadhi ya masuala muhimu yanayotakiwa kufanyinywa na redio za jamii katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2015.
DSC_0169
Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji John J. Mkwawa, akitoa mada kwa wadau wa utekelezaji wa mradi wa uchaguzi unaolenga kuboresha demokrasia amani nchini (DEP) katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu ujao, unaofadhiliwa na Shirika La Kimataifa la Maendeleo (UNDP) ) katika warsha ya siku nne inayoendelea mjiji Dodoma. Kutoka kulia ni Afisa Habari na Mahusiano Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Bi. Salha Ali, Bi. Margaret Rugambwa mtalaam wa masuala ya jinsia na jamii kutoka UN Women na Mgeni rasmi Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo (UNDP) Godfrey Mulisa ambaye pia ni Mtaalam wa masuala ya utawala bora kutoka UNDP.
Ameyataja masuala hayo kuwa ni kuibua mapema maovu mbalimbali yanayohusiana na uchaguzi yanayoweza kujitokea ili yarekebishwe mapema, ukiukwaji wowote wa upigaji kura utakaoenda kinyume cha sheria, kuhamasisha watu wenye sifa za kupiga kura wajitokeze kwa wingi na kutoa ulingo kwa vyama vya siasa kuelezea sera za vyama vyao vya siasa kwa wapiga kura wao.
Mambo mengine ni kuibua matukio yanayohatarisha amani na utulivu, kuwaelezea wapiga kura kwa ufasaha na lugha rahisi sheria za uchaguzi, kuwaeleza wananchi umuhimu wa kupiga kura na masuala muhimu yanayowahusu hususan wazee, wanawake, maskini na wasiofikiwa kwa urahisi.
Mulisa pia amezitaka redio za jamii kuendesha mijadala kwa kuwashirikisha wananchi na vyama visivyo vya kiserikali, kuhoji miradi ya maendeleo ya taifa na kuchangia taarifa endelevu kwa maendeleo.
Akielezea madhumuni ya warsha ya wadau wa mradi wa uchaguzi 2015, Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa shirika la kimataifa la sayansi, elimu na utamaduni (UNESCO) Al Amin Yusuph, alisema kukutana kwa wadau wakubwa wa uchaguzi kunalenga kukumbushana majukumu yaliyoko katika uchaguzi hususan kujisajili kwa wapiga kura kutokana na mchango mkubwa wa redio jamii katika kufikisha ujumbe, kuwa na dhamana, kuwahamasisha na kuwaelimisha jamii na pia kuboresha sera za mtandao wa redio jamii nchini.
DSC_0282
Sehemu ya washiriki wa redio mbalimbali za jamii nchini wakifuatilia kwa umakini mada zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye warsha hiyo inayoendelea mjini Dodoma.
“ Matatizo ya vitambulisho vipya elimu ni muhimu, kuhamasisha mchakato wa demokrasia wananchi ambao uweo wao sio mkubwa kuwafikia hususan wanawake ambao wanakosa fursa za kupiga kura na hawana nyenzo za kupata habari, vijana nao hawapendi kujisajili na kupiga kura na vile vile kuna vijana waliofikia umri wa kupiga kura, wote hawa wanahitaji elimu”.
Warsha hiyo ya siku nne imeandaliwa kwa ushirikiano wa wadau wakubwa wa mradi huo wa DEP ambao ni UNESCO, Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa (RPP), NEC na ZEC.
Warsha hiyo pia inawashirikisha washiriki 31 wa mtandao wa redio jamii Tanzania (COMNETA) unaotekeleza mradi wa demokrasia na amani kuelekea uchaguzi mkuu 2015 unaofadhiliwa na mfuko wa mashirika ya maendeleo 10 ambayo ni Canada, Uingereza (DFID), Denmark, Umoja wa Ulaya na Finland. Nyingine ni Ireland, Norway, Sweden, Switzerland na mfuko wa Umoja wa Mataifa.
DSC_0251
DSC_0214
Makamu wa Msajili wa vyama vya siasa nchini, Bw. Ibrahim Sapi Mkwawa, akitoa salamu kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa inayoratibu mradi wa uchaguzi unaolenga kuboresha demokrasia amani nchini (DEP) katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu ujao, unaofadhiliwa na Shirika La Kimataifa la Maendeleo (UNDP) ) katika warsha ya siku nne inayoendelea mjiji Dodoma.
DSC_0063
Mtaalamu wa masuala ya uchaguzi kutoka UNDP, William Hogan akiwasalimia washiriki wa warsha hiyo.
DSC_0119
Baadhi ya maafisa kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye warsha hiyo inayoendelea mjini Dodoma.
DSC_0202
Afisa Habari na Mahusiano Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Bi. Salha Ali, akielezea mahusiano ya tume yake na vyombo vya habari vya jamii visiwani Zanzibar.
DSC_0219
Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu akihoji swali kwa watoa mada wakati wa warsha hiyo ya siku nne inayoendelea mjini Dodoma.
DSC_0259
Makamu Mwenyekiti wa COMNETA ambaye pia ni Meneja wa Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Telecentre Sengerema FM mkoani Mwanza Bw. Felician Ncheye akitoa maoni yake wakati wa kujadili mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye warsha hiyo.
DSC_0320
Nuru H. Chuo kutoka Tandabui Health Access Tanzania/Afya Radio Mwanza akishiriki kuchangia maoni kwenye vikundi kazi.
DSC_0302
Washiriki wakijadiliana kwenye vikundi kazi.
DSC_0348
Khadija Aboud kutoka Zanzibar Youth Organization Network (ZAYONET) akiwasilisha kazi ya kikundi wakati wa warsha hiyo ya siku nne inayoendelea mjini Dodoma.

MTEMVU AZINDUA OFISI ZA UWT-CCM KATA YA VITUKA, TEMEKE

$
0
0
  Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu (katikati), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Ofisi ya wanachama wa (UWT) wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dar es Salaam leo (kushoto ni) Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania Kata ya Vituka Temeke Dar es Salaam na wanachama wengine  .
Mtemvu na viongozi wengine wa UWT, wakishangilia baada uzinduzi wa ofisi hizo kufanyika
Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu na Diwani wa Viti Maalum wa Temeke, Mariam Mtemvu wakitia saini kwenye vitabu vya wageni katika ofisi hizo.
 Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu (kulia), akisaliliana na wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mara alipo wasili katika Ofisi ya Kata ya   Vituka Dar es Salaam leo

Mtemvu akiwa na wafuasi wa CCM wakielekea kwenye mkutano wa hadhara katika Kata ya Vituka
Mtemvu akisalimiana na wananchi

Mtemvu, Mariam Mtemvu na Mwenyekiti wa UWT Kata ya Vituka, Suzana Mdete wakiwapungia mikono wananchi
Baadhi ya wafuasi wa CCM wakiwa katika mkutano huo
Wananchi wakisikiliza kwa makini hotuba ya  Mbunge wa Jimbo la Temeke, Mtemvu
Msaidizi Mkuu wa Mbunge wa Temeke, Ally Mehalla akitambulishwa kwa wananchi wakati wa mkutano huo.
Timu ya soka wakiwa katika mkkutano huo
Mtemvu akitoa zawadi kwa msanii Haassn Mapenje  aliyekuwa akitumbuiza kwa sarakasi katika mkutano huo
Msanii Hassan Mkenjula akifanya mambo yake katika mkutano huo
Mbunge akimpongeza msanii Hassan Mkenjula
Mtemvu akisalimiana na mmoja wa wananchama wa CCM
Mdete akifungua mkutano huo wa hadhara
Mwanachama wa Chadema Husna Dole  akishangilia kwa furaha baada ya kukabidhi kadi ya chama hicho na kutangaza kujiunga na CCM katika mkutano huo
Husna akikabidhi kadi kwa Mtemvu
Mtemvu akimvisha fulana ya CCM Husna
Mtemvu akimkabidhi kadi ya CCM Husna

Mtemvu akisalimiana na wananchi baada ya mkutano kumalizika. PICHA ZOTE NA KHAMIS MUSSA


Mwili wa Marehemu Amin Elias Mbaga Waagwa Dar

$
0
0
]Mwili wa marehemu Amin Elias Mbaga aliyekuwa mfanyakazi wa Kampuni ya TTCL ukiwasili Kanisa la KKKT Sinza, jijini Dar es Salaam tayari kwa ibada ya kumuombea marehemu. 
Mwili wa marehemu Amin Elias Mbaga aliyekuwa mfanyakazi wa Kampuni ya TTCL ukiwasili Kanisa la KKKT Sinza, jijini Dar es Salaam tayari kwa ibada ya kumuombea marehemuMwili wa marehemu Amin Elias Mbaga aliyekuwa mfanyakazi wa Kampuni ya TTCL ukiingizwa kanisani. Mwili wa marehemu Amin Elias Mbaga aliyekuwa mfanyakazi wa Kampuni ya TTCL ukiingizwa kanisani.Mwili wa marehemu Amin Elias Mbaga aliyekuwa mfanyakazi wa Kampuni ya TTCL ukiingizwa kanisani. Mwili wa marehemu Amin Elias Mbaga aliyekuwa mfanyakazi wa Kampuni ya TTCL ukiingizwa kanisani.Mke na Watoto wa Marehemu Amin Elias Mbaga wakiwa katika ibada hiyo. Mke na Watoto wa Marehemu Amin Elias Mbaga wakiwa katika ibada hiyoWanafamilia na familia ya Marehemu Amin Elias Mbaga wakishiriki misa ya kumuombea aliyekuwa mfanyakazi mwenzao, marehemu Amin Elias Mbaga. Mwili wa marehemu umesafirishwa jana kuelekea Kilimanjaro kwa mazishi. Wanafamilia
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya wafanyakazi wote wa TTCL mara baada ya ibada hiyo iliyofanyika Kanisa la KKKT Sinza, jijini Dar es Salaam. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya wafanyakazi wote wa TTCL mara baada ya ibada hiyo iliyofanyika Kanisa la KKKT Sinza, jijini Dar es Salaam.[/caption][caption id="attachment_52127" align="aligncenter" width="640"]Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) akiwafariji wanafamilia ya marehemu Amin Elias Mbaga. Mwili wa marehemu umesafirishwa jana kuelekea Kilimanjaro kwa mazishi. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) akiwafariji wanafamilia ya marehemu Amin Elias Mbaga. Mwili wa marehemu umesafirishwa jana kuelekea Kilimanjaro kwa mazishi.[/caption][caption id="attachment_52131" align="aligncenter" width="640"]Baadhi ya ndugu, jamaa, marafiki na wafanyakazi wa kampuni ya TTCL wakishiriki misa ya kumuombea aliyekuwa mfanyakazi mwenzao, marehemu Amin Elias Mbaga. Mwili wa marehemu umesafirishwa jana kuelekea Kilimanjaro kwa mazishi. Baadhi ya ndugu, jamaa, marafiki na wafanyakazi wa kampuni ya TTCL wakishiriki misa ya kumuombea aliyekuwa mfanyakazi mwenzao, marehemu Amin Elias Mbaga. Mwili wa marehemu umesafirishwa jana kuelekea Kilimanjaro kwa mazishi.[/caption][caption id="attachment_52126" align="aligncenter" width="451"]Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya wafanyakazi wote wa TTCL mara baada ya ibada hiyo iliyofanyika Kanisa la KKKT Sinza, jijini Dar es Salaam. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya wafanyakazi wote wa TTCL mara baada ya ibada hiyo iliyofanyika Kanisa la KKKT Sinza, jijini Dar es Salaam.[/caption][caption id="attachment_52136" align="aligncenter" width="401"]Baadhi ya wafanyakazi na viongozi wa Kampuni ya TTCL, pamoja na jamaa wengine waliowahi kufanya kazi na marehemu wakiwafariji ndugu, jamaa, marafiki wa familia ya marehemu Amin Elias Mbaga. Baadhi ya wafanyakazi na viongozi wa Kampuni ya TTCL, pamoja na jamaa wengine waliowahi kufanya kazi na marehemu wakiwafariji ndugu, jamaa, marafiki wa familia ya marehemu Amin Elias Mbaga.[/caption][caption id="attachment_52137" align="aligncenter" width="640"]Baadhi ya wafanyakazi na viongozi wa Kampuni ya TTCL wakiwa katika ibada ya kumuombea marehemu Amin Elias Mbaga aliyekuwa mfanyakazi mwenzao ibada hiyo ilifanyika Kanisa la KKKT Sinza, jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wafanyakazi na viongozi wa Kampuni ya TTCL wakiwa katika ibada ya kumuombea marehemu Amin Elias Mbaga aliyekuwa mfanyakazi mwenzao ibada hiyo ilifanyika Kanisa la KKKT Sinza, jijini Dar es Salaam.[/caption]ilia na familia ya Marehemu Amin Elias Mbaga wakishiriki misa ya kumuombea aliyekuwa mfanyakazi mwenzao, marehemu Amin Elias Mbaga. Mwili wa marehemu umesafirishwa jana kuelekea Kilimanjaro kwa mazishi.Baadhi ya ndugu, jamaa, marafiki na wafanyakazi wa kampuni ya TTCL wakishiriki misa ya kumuombea aliyekuwa mfanyakazi mwenzao, marehemu Amin Elias Mbaga. Mwili wa marehemu umesafirishwa jana kuelekea Kilimanjaro kwa mazishi. Baadhi ya ndugu, jamaa, marafiki na wafanyakazi wa kampuni ya TTCL wakishiriki misa ya kumuombea aliyekuwa mfanyakazi mwenzao, marehemu Amin Elias Mbaga. Mwili wa marehemu umesafirishwa jana kuelekea Kilimanjaro kwa mazishi.[/caption][caption id="attachment_52124" align="aligncenter" width="620"]Mwili wa marehemu Amin Elias Mbaga aliyekuwa mfanyakazi wa Kampuni ya TTCL ikiombewa kabla ya kusafirishwa kuelekea Mkoani Kilimanjaro kwa mazishi. Mwili wa marehemu Amin Elias Mbaga aliyekuwa mfanyakazi wa Kampuni ya TTCL ikiombewa kabla ya kusafirishwa kuelekea Mkoani Kilimanjaro kwa mazishi.[/caption]

SLIMMING JUICY YA KUONDOA KITAMBI NA KUPUNGUZA MAFUTA MWILINI.

$
0
0
 Neema   Herbalist  ni   wauzaji  wa  dawa  mbalimbali  za  asili  nchini  Tanzania. Tunapenda  kuwatangazia  wateja  wetu  kuwa  sasa  tunayo    SLIMMING  JUICY  HERBAL  inayo  ondoa  kitambi  na  kupunguza   mafuta   mwilini. 

 Ni  dawa  ya asili  kabisa  ( Pure  Herbal )  ambayo  haijachanganywa  na  kemikali  yoyote  na  inaondoa  kitambi  na  kumaliza  mafuta  yote  mwilini.


JINSI  INAVYO  FANYA  KAZI.
Dawa  hii  inafanya  kazi  mbalimbali  ndani  ya  mwili  wa  mwanadamu  ambazo  ni  pamoja  na  :
i.                     Kutoa sumu  mwilini   zitokanazo  na  kemikali mbalimbali
ii.                    Kuzibua  mirij  ( To  Clear  Arteries )
iii.                  Kusafisha  damu
iv.                  Kuondoa  mafuta  ndani  ya  damu,
v.                   Kuyeyusha mafuta  mwilini  pamoja  na  faida nyingine  nyingi.
BEI  YA  DAWA:
Dawa  hii  inapatikana  kwa  gharama  ya  shilingi  ELFU  HAMSINI  TU.
MAHALI  ZILIPO  OFISI  ZETU :
Tunapatikana  jijini  Dar  Es  salaam  katika  eneo  la  Changanyikeni karibu  na  CHUO  CHA  TAKWIMU  mbele  ya  Chuo  Kikuu  Cha  Dar  Es  salaam.
MAWASILIANO  YETU :  Wasiliana  nasi  kwa  simu  0766538384.
Kwa  taarifa  zaidi  kuhusu  huduma  zetu, tembelea ;

27 wateuliwa kuwa makatibu wa CCM wilaya

$
0
0
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Ndugu Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa NEC mjini Dodoma.

SNV AND FINCA TANZANIA LAUNCHES A PROJECT TO IMPROVE 20,500 YOUTH LIVES.

$
0
0
  Project Manager for OYE-Tanzania, Mozambique and Rwanda, Mr Roy Van Der Drift stress a point to members of press during the launch of SNV and FINCA partnership on OYE project. On his right is Awadh Milas, OYE Program Leader-Youth Skills Development, and from left are Mr Ed Greenwood, FINCA Chief Executive Officer and Head of Retail for FINCA Tanzania, Gershom Mpangalah.
   Head of Retail for FINCA Tanzania, Gershom Mpangalah, stresses a point to the media during today’s press conference on the launch of SNV-FINCA Partnership on OYE Project. Looking on from far left are Awadh Milas, OYE Program Leader-Youth Skills Development, Project Manager for OYE-Tanzania, Mozambique and Rwanda, Mr Roy Van Der Drift and Ed Greenwood, FINCA Chief Executive Officer.
  Awadh Milas, OYE Program Leader-Youth Skills Development speaking to the members of the press during the launch of SNV and FINCA partnership on OYE project. Looking on from his right are Project Manager for OYE-Tanzania, Mozambique and Rwanda, Mr Roy Van Der Drift, Mr Ed Greenwood, FINCA Chief Executive Officer and Head of Retail for FINCA Tanzania, Gershom Mpangalah

    Some of the youth beneficiaries of OYE project phase one

The Netherlands Development Organisation SNV, in partnership with the MasterCard Foundation today has launched its new partnership with FINCA Tanzania dubbed The Opportunities for Youth Employment (OYE) project aimed to improve the livelihoods of 20,500 rural, out-of-school youth.

Speaking during the launch, Project Manager for OYE-Tanzania, Mozambique and Rwanda, Mr Roy Van Der Drift said their partnership with FINCA Tanzania is for the implementation of a five-year OYE project in Tanzania, Mozambique and Rwanda countries through connecting skilled youth with labour market opportunities and contributing to the establishment of new youth-led enterprises.

“Our Partnership with FNCA Tanzania is purposely designed to implement our OYE-Project which intends to harnesses the motivation, energy and passion of rural youth to innovate and transform existing markets and to create new ones’ said Mr Drift.

The SNV -FINCA Tanzania partnership aims to facilitate the access to financial services, advise on appropriate financial products and also compliment the Business Development training in areas of trainings that responds to youth own aspirations and the needs of local Agriculture and Renewable Energy markets. 

"Small and Medium enterprises, if developed, can play an important role in this endeavor. This project will ease unemployment by creating jobs for the youth and the fastest-growing segments of the poor and unemployed in rural areas" said Awadh Milas, Project Leader/Advisor OYE Agriculture.  

The project, now on its second year have already trained 1300 youth in agribusiness skills and renewable energy technologies whereas now it aims to reach 900 youth and train them on business development.

‘FINCA operates in almost 17 region in the country, and we are sure by this project we will be able to reach more youth and work together in promoting youth led enterprises and their access to financial services in order to realize their business ambitions” says Ed Greenwood, FINCA Chief Executive Officer.

SNV through the OYE project reinforces the employability and business skills of youth, making them more reliable to handle finance, while mentoring and coaching them to develop and establish their own enterprises.

MWANRI: ZINGATIENI WELEDI WAKATI WA KUANDAA MAANDIKO YA MIRADI

$
0
0
 Kaimu Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (aliyesimama) akizungumza na baadhi ya viongozi waandamizi wizara za viwanda na biashara, fedha, uchukuzi, nishati na madini pamoja na viongozi waandamizi kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Zanzibar. 
 Bibi Maryam Khamis (Wapili kulia) Mtaalam wa uchumi kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Zanzibar akizungumza katika kikao hicho.
 Pichani ni baadhi ya viongozi waliohudhuria Kikao hicho. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA), Dkt. Adelhelm Meru.
Mmoja wa wajumbe wa kikao hicho, Bw. Aunyisa Meena kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara akichangia mada.

Na Saidi Mkabakuli
Wapanga mipango nchini wameaswa kuzingatia weledi wakati wa kuandaa maandiko ya miradi yanayowasilishwa kwa wafadhili ili kuongeza ushindani dhidi ya nchi nyingine wakati wa uwasilishaji wa maombi ya kupatiwa ufadhili wa miradi ya maendeleo.

Wito huo umetolewa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri wakati alipofanya mazungumzo na viongozi waandamizi kutoka wizara za viwanda na biashara, fedha, uchukuzi, nishati na madini pamoja na viongozi waandamizi kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Zanzibar.

Bibi Mwanri alisema kuwa kuna ushindani mkubwa kwa nchi zinazoomba ufadhili wa miradi ya maendeleo hivyo uandishi wa maandiko yenye kuzingatia weledi na viwango vya kimataifa ni msingi katika kuongeza ushindani na kuweza kuwashawishi wafadhili kuvutiwa na miradi husika.

“Katika kukabiliana na ushindani hatuna budi kujikita katika weledi na kuandika maandiko yenye kuweza kuvutia wafadhili ili waweze kuja kuwekeza nchini kwetu, ili tuweze kutimiza ndoto zetu za kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye uchumi wa kati kufikia mwaka 2025” alisema Bibi Mwanri.

Mwezi Juni mwaka 2011, Serikali iliandaa Mpango wa Kwanza wa Maeneleo (2011/12 – 2015/16) kwa lengo la kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 ambapo Mpango huu ulihitaji takribani trilioni 40 ili kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo kwa kipindi cha miaka mitano. 

Kwa mujibu wa Mpango huo, vyanzo vya utekelezaji wake ni  pamoja na Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP);  uwekezaji wa kigeni; Hati Fungani kwa Waishio Ughaibuni; Hatifungani za ndani; Hati Fungani katika Masoko ya Nje; Mifuko ya Pensheni na hifadhi ya jamii; na makubaliano ya ushirikiano wa kiuchumi wa nchi zinazoendelea.
Viewing all 46366 articles
Browse latest View live




Latest Images