Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 386 | 387 | (Page 388) | 389 | 390 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa katika jiwe la msingi wakati wa uzinduzi wa kijiji cha mfano cha vijana Pathfinders Green City katika kata ya Igigwa wilayani Sikonge leo.Rais Kikwete yupo Mkoani Tabora kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo ambapo pia atakuwa mgeni rasmi katika kilele cha mbio za mwenge hapo kesho.watatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bi.Fatma Mwassa na wapili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Bi.Hanifa Selenga.
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya uchakataji asali kutoka kwa mmoja wa vijana waishio katika kijiji cha mfano cha vijana wajasiriamali katika kata ya Igigwa, wilayani Sikonge, Mkoani Tabora leo.
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua baadhi ya madawati yaliyotengenezwa na kikundi cha vijana wajasiriamali katika kijiji cha mfano cha Pathfinders katika kata ya Igigwa, wilayani Sikonge,Mkoani Tabora muda mfupi baada ya kukizindua kijiji hicho.
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua viatu vya ngozi vilivyotengenezwa na vijana wajasiriamali katika kijiji hicho cha mfano
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua viatu vya ngozi vilivyotengenezwa na vijana wajasiriamali katika kijiji hicho cha mfano. Picha na Freddy Maro.

  0 0

  Hivi karibu Msanii Mahiri na Nguli katika tasnia ya filamu nchini Elizabeth Michael almaarufu kama LULU ataibuka na filamu yake Mpya na yenye kusisimua iitwayo "MAPENZI YA MUNGU" ambapo moja kati ya washiriki katika filamu hiyo ni Bi Flora Mtegoha ambae ni Mama Mzazi wa aliyekuwa Msanii Nguli wa Kiume Hapa Bongo Marehemu Steven Kanumba.
  Filamu ya "Mapenzi ya Mungu" ni moja ya filamu ambayo Lulu ameonyesha uwezo wa hali ya na kuthibitisha kuwa ni mmoja kati ya wasanii wa kike hapa Tanzania ambae ana kipaji cha hali ya juu katika kuuvaa uhusika ambapo ana uwezo wa kubadilika badilika kutokana na muongozo anaopewa.
  Filamu ya "Mapenzi ya Mungu" itakuwa Sokoni hivi Karibu Kwa Wauzaji wa Filamu kote Nchini.
  Filamu hii itasambazwa na Kampuni mahiri ya Proin Promotions Ltd.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile ambaye ni kiongozi wa ujumbe kutoka Tanzania na anawakilisha kama Gavana Mbadala (Alternate Governor) pamoja na Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu ambaye pia ni Gavana katika mikutano hii. 

  Katika picha viongozi hao wakiwa wanafanya majumuisho ya majadiliano ya awali na kukubaliana cha kufanya kwa pamoja na viongozi kutoka IMF na WB kuhusiana na hali ya uchumi kwa maana ya sera za fedha na sera za mapato na matumizi.
  Bw.Herve’ Joly ambaye ni Mkurugenzi msaidizi na Mkuu wa idara ya Afrika sehemu ya Mashariki akimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile hayupo katika picha, alipokuwa akitoa msimamo wake kuhusu sera zinazopendekewa na IMF na WB.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile alipokuwa akitoa msimamo wake kuhusu sera zinazopendekewa na IMF na WB.

  Dr. Servacius Likwelile Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali akiwa pamoja na ujumbe kutoka Tanzania.Wakichukua mapendekezo kutoka kwa viongozi wa IMF na WB hawapo kwenye picha. 

  Kutoka kushoto ni Gavana wa Benki kuu ya Tanzania akiwa amefuatana na Bi. Natujwa Mwamba Naibu Gavana wa Benki kuu ya Tanzania na kutoka kulia ni Bw. Philip Mpango Katibu Mtendaji tume ya Mipango akifuatiwa na Msaidizi wa kamishna sera Bw. Shogholo Msangi na wa mwisho ni Kamishna wa Bajeti Bw. John Cheyo na walioketi nyuma wote ni wajumbe kutoka Tanzania.

  0 0

   
   Afisa Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. Jumanne Mbepo (kulia) akimkabidhi hundi ya shilingi milioni 15 ili kudhamini mbio za Rock City Marathon 2014 Mratibu wa mbio hizo Bw. Mathew Kasonta (kushoto) katika hafla ya kukabidhi hundi hiyo na kutangaza rasmi zawadi zitakazotolewa katika mbio hizo iliyofanyika jijini Dar es Salaam Jana. Mbio hizo zitafanyika mkoani Mwanza, katika uwanja wa CCM Kirumba tarehe 26 mwezi Oktoba mwaka huu. NSSF ikiwa kama mdamini mkuu wa mbio hizo.
   Mratibu wa mbio za Rock City Marathon 2014 kutoka Capital Plus International (CPI), Bw. Mathew Kasonta (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 15 iliyotolewa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),kudhamini mbio za Rock City Marathon 2014 na kutangaza rasmi zawadi zitakazotolewa katika mbio hizo jijini Dar es Salaam jana. Mbio hizo zitafanyika mkoani Mwanza, katika uwanja wa CCM Kirumba tarehe 26 mwezi Oktoba mwaka huu. NSSF ikiwa kama mdamini mkuu wa mbio hizo. Wakishuhudia katikati ni Afisa Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. Jumanne Mbepo na Afisa Uhusiano wa NSSF, Bi. Anna Nguzo (Kulia).
   Afisa Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. Jumanne Mbepo (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 15 kudhamini mbio za Rock City Marathon 2014 na kutangaza rasmi zawadi zitakazotolewa katika mbio hizo jijini Dar es Salaam jana. Mbio hizo zitafanyika mkoani Mwanza, katika uwanja wa CCM Kirumba tarehe 26 mwezi Oktoba mwaka huu. NSSF ikiwa kama mdamini mkuu wa mbio hizo. Wakishuhudia kushoto ni Mratibu wa mbio kutoka Capital Plus International (CPI), Bw. Mathew Kasonta na Afisa Uhusiano wa NSSF, Bi.. Anna Nguzo (Kushoto).
  =========  =======  ========
  NSSF yanogesha mbio za Rock City 2014
  • · Zawadi nono zatangatazwa kwa washindi

  Zawadi za washindi wa mbio za Rock City zitakazofanyika katika mkoa wa Mwanza tarehe 26 mwezi huu zimetangazwa jana huku mdhamini mkuu wa mbio hizo, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) likitoa shilingi milioni 15 kuboresha mbio hizo.

  Akizungumza wakati wa makabidhiano ya hundi ya shilingi milioni 15 kwa waratibu wa mbio hizo, Capital Plus International Limited, Afisa uhusiano wa NSSF, Bw. Jumanne Mbepo amesema kuwa NSSF imeendelea kudhamini mbio hizi kwa mwaka wa sita mfululizo kutokana na kuona maboresho yanayofanyika katika mbio hizo kila mwaka.

  “Mbio hizi zitaambatana na kutoa elimu kwa wakulima na wachimbaji wadogowadogo wa madini katika kanda ya ziwa, juu ya umuhimu wa kujiunga na mfuko wa NSSF ili waweze kunufaika na huduma zitolewazo na shirika kama vile mkopo, bima ya afya pamoja na mafao mbalimbali,” Alisema Bw. Mbepo.

  Mratibu wa mbio hizo, Bw. Matthew Kasonta amesema kuwa udhamini huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kufanikisha maandalizi ya mbio hizo na kuleta maboresho makubwa katika mbio za mwaka huu. Amesema kuwa maboresho hayo ni pamoja na kuwepo kwa mbio fupi zitakazo jumuisha vijana kutoka katika shule za sekondari na wale waliopo shule za msingi madarasa ya juu.

  “Baada ya kupata udhamini huu, tunafaraja ya kutaja zawadi watakazopatiwa washindi. Kwa mbio za Kilomita 21, jumla ya shilingi milioni saba na laki moja zimetengwa kwa ajili ya washindi. Washindi wa kwanza watazawadiwa Tsh 1.5m/- huku washindi wa pili watapata laki tisa na washindi wa tatu watapata laki saba kila mmoja.

  Kwa mbio za kilomita tano, zaidi ya shilingi laki nne zimetengwa kwa ajili ya washindi. Jumla ya shilingi laki tatu na arobaini zimetengwa kwa ajili ya washindi wa mbio za kilomita 3 na shilingi laki mbili imetengwa kama zawadi kwa ajili ya mbio za watoto za kilomita mbili.” 

  Bw. Kasonta amesema kuwa kwa mbio fupi ambazo zimeanzishwa mwaka huu (mita 100, mita 400 na mita 1,500) jumla ya shilingi laki nne na themanini pesa taslimu zimetengwa kwa ajili ya washindi huku washindi wote wa kwanza (wa kike na kiume) watapata king’amuzi cha Continental Decoders.

  Bw. Kasonta aliwataja wadhamini waliofanyikisha mbio hizo kuwa ni Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), TSN Group kupitia kinywaji chake cha Chilly Willy, pamoja na African Barrick Gold, IPTL, Air Tanzania, New Mwanza Hotel, Nyanza Bottling, Sahara Media Group, Continental decoders, New Africa Hotel, PPF, Tanapa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).

   “Nawasihi watu waendelee kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za usajili katika ofisi za kampuni ya Capital Plus International Limited (CPI) jengo la ATC ghorofa ya tatu jijini Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Mwanza, Ofisi zote za wilaya za Michezo na Utamaduni mkoani Mwanza na Uwanja wa Nyamagana,” alisema Bw. Kasonta.

  0 0

  Afisa wa Kanda ya Afrika wa ICAO Papa Issa Mbengue (kushoto)akisisitiza jambo juu ya mfumo mpya wa shirika la Kimataifa la usafiri wa Anga (ICAO) lenye kulenga ufanisi wa wataalamu wa kuongoza ndege ,vyombo vya usafiri wa anga pamoja na mitambo ya kuongonzea ndege wakati wa Kongamano la mafunzo ya ufanisi wa masuala ya uongozaji wa ndege linalofanyika kwa siku tatu katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam kwa udhamini wa Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wanaomsikiliza ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Charles Chacha(watatu kutoka kulia) Kaimu Mkurugenzi Idara ya Huduma za Uongozaji ndege Said Onga (Kulia) Meneja mratibu wa safari za ndege Afrika Frederic Legrand. (wapilia kutoka kulia) na Makamu wa rais wa airspace and airlines Servises Airbus ya Ufaransa Don Facpues Ould.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Charles Chacha(kushoto) akiongea wakati wa uzinduzi wa kongamano la mafunzo ya mfumo mpya wa shirika la Kimataifa la usafiri wa Anga (ICAO) lenye kulenga ufanisi wa wataalamu wa kuongoza ndege ,vyombo vya usafiri wa anga pamoja na mitambo ya kuongonzea ndege katikati ni Meneja mratibu wa safari za ndege Afrika Frederic Legrand, Kongamano hilo linazihusisha nchi za Afrika linafanyika hapa nchini kwa siku tatu kuanzia leo katika hateli ya Serena jijini Dar es Salaam. Kaimu Mkurugenzi Idara ya Huduma za Uongozaji ndege Said Onga (Kulia)
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Charles Chacha akimsikiliza kwa makini Meneja mratibu wa safari za ndege Afrika Frederic Legrand(African Flight Proceducare Manager) wakati alipokuwa akizungumza kwenye kongamano la mafunzo ya mfumo mpya wa shirika la Kimataifa la usafiri wa Anga (ICAO) lenye ufanisi wa wataalamu wa kuongoza ndege ,vyombo vya usafiri wa anga pamoja na mitambo ya kuongonzea ndege.Kongamano hilo la siku tatu katika hateli ya Serena jijini Dar es Salaam kwa udhamini wa TCAA.
  Baadhi ya washiriki wa kongamano la mafunzo ya mfumo mpya wa shirika la Kimataifa la usafiri wa Anga (ICAO) lenye ufanisi wa wataalamu wa kuongoza ndege ,vyombo vya usafiri wa anga pamoja na mitambo ya kuongonzea ndege,wakifuatilia moja ya mada zilizokuwa zikitolewa hapo kongamano hilo limedhaminiwa na TCAA.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Charles Chacha (kulia)akisalimiana na Makamu wa rais wa airspace and airlines Servises Airbus ya Ufaransa Don Facpues Ould, baada ya kufungua kongamano la mafunzo ya mfumo mpya wa shirika la Kimataifa la usafiri wa Anga (ICAO) lenye ufanisi wa kulenga wataalamu wa kuongoza ndege ,vyombo vya usafiri wa anga pamoja na mitambo ya kuongonzea ndege.Kongamano hilo linafanyika kwa siku tatu kuanzia leo katika hateli ya Serena jijini Dar es Salaam.Katikati ni Meneja mratibu wa safari za ndege Afrika Frederic Legrand.(African Flight Proceducare Manager)
  Washiriki wa kongamano lamafunzo ya mfumo mpya wa shirika la kimataifa la usafiri wa anga (ICAO)kutoka nchi za Nigeria,Mali,Ivort coast,Senager,Rwanda,Cape Verde,Gabon na Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa Kongamano hilo la siku tatu linalofabnyika kwenye hoteli ya serena jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola, marehemu Dkt. William Shija, wakati wa shughuli za maziko yaliyofanyika Kijijini kwake, Nyampande Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza, jana Oktoba 13, 2014.
  Spika wa Bunge la Jamhuri, Mhe. Anne Makinda, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola, marehemu Dkt. William Shija, wakati wa shughuli za maziko yaliyofanyika Kijijini kwake, Nyampande Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza, jana Oktoba 13, 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola, marehemu Dkt. William Shija, wakati wa shughuli za maziko yaliyofanyika Kijijini kwake, Nyampande Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza, jana Oktoba 13, 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola, marehemu Dkt. William Shija, wakati wa shughuli za maziko yaliyofanyika Kijijini kwake, Nyampande Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza, jana Oktoba 13, 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika Kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola, marehemu Dkt. William Shija, wakati wa shughuli za maziko zilizofanyika Kijijini kwa marehemu, Nyampande Wialaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza jana, Oktoba 13, 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bialal, akiwafariji wanafamilia wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola, marehemu Dkt. William Shija, wakati wa shughuli za maziko zilizofanyika Kijiji ch Nyampande Wilaya ya Sengerema, Mkoa wa Mwanza jana, Oktoba 13, 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakijumuika na waombolezaji wakati wa shughuli za maziko zilizofanyika nyumbani kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola, marehemu Dkt. William Shija, Kijiji cha Nyampande Wilaya ya Sengerema, jana Oktoba 13, 2014. Picha na OMR

  0 0
 • 10/14/14--06:48: TAARIFA YA MSIBA
 • Menejimenti ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) inasikitika kutangaza kifo cha mfanyakazi mwenzao Bw. Amin Elias Mbaga aliyekuwa Meneja Uhusino kilichotokea tarehe 13.10.2014 katika Hospitali ya Regency jijini Dar es Salaam. Mipango ya Mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Sinza Kumekucha.

  Ibada ya kumuombea marehemu itafanyika tarehe 15/10/2014 katika Kanisa la KKKT Sinza Kumekucha kuanzia saa saba mchana na baada ya ibada safari ya kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Same kwa maziko itaanza.

  Maziko yanatarajia kufanyika katika kijiji cha Muhezi Mwembe Mlimali Same siku ya Alhamisi tarehe 16/10/2014.

   Amin tulikupenda lakini Mungu amekupenda zaidi pumzika kwa Amani. 

  Amen.

  Imetolewa na menejimenti ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL)

  0 0

  Kiongozi wa mbio za mwenge 2014 Rachel Kassandra akikabidhi mwenge wa Uhuru kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa maadhimisho ya kilele cha mbio za mwenge ulius na kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere zilizofanyika katika uwanja wa michezo wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora leo.Kulia ni Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na michezo Dkt.Fenela Mkangara. 

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mwenge wa Uhuru wakati wa maadhimisho ya kilele cha mbio za mwenge ziizofanyika mkoani Tabora leo.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mbio za mwenge mwaka huu wakati wa maadhimisho ya kilele cha mbio hizo zilizofanyika katika uwanja wa michezo wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora leo.
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa kilele cha mbio za mwenge 2014 ziilizofanyika katika uwanja wa michezo wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora leo(picha na Freddy Maro)


  0 0  0 0


  Utangulizi.

  Fleva Inc Film Academy ni taasisi inayojihusisha na shughuli za ukuzaji wa  sanaa nchini hasa kwa  yale masuala yanayohusu tasnia ya filamu hapa Tanzania, ni taasisi inayofanya kazi na kutoa mafunzo ya uigizaji, uongozaji wa filamu au tamthilia,matangazo ya biashara , uandishi wa michezo  ya kuigiza ya jukwaani,uhariri wa filamu pamoja na utayarisahji wa Filamu kwa ujumla. 

  Fleva Inc Film Academy ni taasisi inayotambulika na mamlaka inayosimamia shughuli za sanaa na inapatikana  Manispaa ya Temeke hapa  Mjini  Dar es Salaam.

  Malengo ya Fleva Inc Film Academy.
  Fleva Inc Film Academy ina malengo na madhumuni yafuatayo;
  (a)                Kutoa Mafunzo yanayohusu tasnia ya filamu yenye ubora unaondana na mabadiliko ya ukuaji teknolojia duniani kote.hasa kwa fani  za uigizaji michezo ya kuigiza na filamu, Kutoa mafunzo ya  kuhariri filamu, michezo ya kuigiza pamoja na tamthilia .
  (b)               Kushirikiana na serikali,asasi zisizo za serikali,vikundi vya kijamii katika mambo mbalimbali yatayoweza kuleta mabadiliko ya kimaendeleo kwa Wasanii wa Tanzania na jamii kwa ujumla.

  Ndugu Waandishi kama tunavyofahamu tasnia ya filamu nchini imepitia hatua mbalimbali katika ukuaji wake ili kufikia maendeleo yanayoonekana sasa. Lakini jitihada hizi zimefanywa na kada mbalimbali za kisekta zikijumlisha serikali na taasisi zake pamoja na Wadau na Wabia  mbalimbali pamoja na Wasanii wenyewe wakishirikiana na taasisi zao.

  Lakini pamoja na changamoto nyingi zilizopatikana katika maendeleo ya tasnia ya filamu hapa nchini na sanaa nyinginezo kwa ujumla bado serikali yetu inayoongozwa na  Mheshimiwa  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete imejaribu kufanya maboresho na au utungaji wa sheria na kanuni kadhaa zitazowezesha kutoa miongozo iliyo  sahihi  katika kulinda , kutetea, kusimamia na ukuzaji wa tasnia za sanaa za ufundi, sanaa za maonesho, filamu na muziki.

  Baadhi ya sheria hizo ni za hakimiliki na hakishiriki ya 1999 inayosimamia haki bunifu za Wasanii, sheria ya TRA ya mwaka 2014 inayosimamia kodi za mauzo ya kazi za filamu na muziki pamoja na sheria namba ya 4 ya mwaka 1976 inayosimamia michezo ya kuigiza ambazo kanuni zake zilizinduliwa  mwaka 2011 Mjini Musoma.  Pamoja na jitihada hizo kufanyika bado sekta ya sanaa haikupewa uzito unaostahili kwa sababu ilionekana si eneo ambalo linaweza kuwa na mchango katika pato la Taifa letu, yaani sanaa ilionekana ni kiburudisho kwa watu Fulani na umuhimu wake ulikuwa katika matukio na hafla maalumu.

  Ndugu Waandishi, nachukua fursa hii kuipongeza Wizara ya Habari, Utamaduni Vijana na Michezo, Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Fedha  na taasisi zao ambazo zimepewa majukumu ya  kusimamia kazi za Wasanii kwa namna moja au tofauti, zikiwemo,BASATA, COSOTA,TRA na  Bodi ya Filamu Tanzania na matunda ya majukumu yao yanaonekana.   

  Pamoja na jitihada hizo za awali Naipongeza Serikali ya Mh Rais Dkt Mrisho Jakaya Kikwete kuanzisha mchakato wa kuandikwa kwa katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo katika mchakato huo makundi mbali mbali ya kijamii yalishirikishwa kuanzia hatua ya Mwanzo mpaka katika uundwaji wa Bunge Maalum la Katiba, Kutokana na hilo sisi tunaofanya kazi katika sekta ya Sanaa tuliwakilishwa na Ndg Paul Mtenda ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Waongozaji wa Filamu na Michezo ya kuigiza Tanzania(TAFIDA).
  Ndugu Waandishi wa Habari mchakato wa Bunge Maalum la Katiba na majukumu yake yamekamilisha historia muhimu kwa Taifa la Tanzania ambapo tarehe 8/10/2014  katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma  Mwenyekiti wa Bunge hilo maalumu Mh Samuel Sita  na kamati zake walimkabidhi rasmi  KATIBA INAYOPENDEKEZWA kwa Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete.   

  Ndugu Waandishi, mimi ni mmoja kati ya Walioalikwa na Bunge kuhudhuria sherehe hizo nikiwa Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wahariri wa Filamu na Michezo ya Kuigiza Tanzania (TAFEA) na Mkurugenzi Mkuu wa taasisi ya  Fleva Inc Film Academy na nikiwa Katibu Mstaafu wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), nimeipitia Katiba inayopendekezwa na hasa vifungu vinavyohusu maslahi na haki za Wasanii Tanzania.
  Kutokana na hilo nalipongeza Bunge Maalumu Katiba kwa kazi nzito walioifanya na hasa kuthamini na kuyapa umuhimu madai ya Wasanii wa Tanzania kwa kuingiza mambo ya msingi yanayohusu sekta ya Sanaa na hasa katika ulinzi wa haki bunifu za kazi za Wasanii, usimamizi na uendelezaji wa sekta ya Sanaa,utafiti  na taaluma kwa ujumla  ambazo zimeorodheswa katika Sura ya tano kifungu namba 59(1 -3) na 3(a) – (f) ukurasa 47 – 48.

  Ndugu Waandishi,Pamoja na mazuri yaliyoorodheshwa katika vifungu hivyo bado kuna changamoto kubwa inayoikabili sekta sanaa hasa muziki na filam, nalo ni tatizo la bei katika soko la filamu limekua si lenye kueleweka, katika hili naweza kusema kuwa thamani ya kazi za msanii wa filamu na muziki bado hazijatazamwa inavyostaahili na hasa tukizingatia kwamba tunafanya kazi kubwa katika mazingira magumu lakini bado tatizo la  bei ya zao letu haijatazamwa kwa kina.

  Kwa sababu kama Wavuvi, Wafugaji, na Wakulima watakua na mizania ya bei ya mazao yao kama ilivyotajwa katika Katiba Inayopendekezwa Sasa Sura 3 (13)(2)d ukurasa 10-11,  kwa nini pia katika zao la filamu pasiwepo na utaratibu wa bei elekezi kama ilivyo katika bidhaa za mafuta na sasa kwa wafugaji,Wakulima na wavuvi?. Lakini jambo hili halijachelewa kwa sababu zipo mamlaka zinazoweza kukaana Wadau wake ili kuliongelea na kulipatia ufumbuzi.


   Hivyo basi naziomba taasisi za BASATA, COSOTA, Bodi ya Filamu na Mashirikisho husika kulitazama kwa kina kama wanataka kuleta mapinduzi ya kiuchumi kwa Wasanii wenyewe ili wawezekulipia kodi kadhaa zinazowakabili.

  Mwisho napenda kuwashawishi Wasanii wa Tanzania kuchukua hatua madhubuti katika kutafuta fursa mbalimbali za kuiendeleza tasnia ya Filamu na Sanaa kwa ujumla lakini pia kuipitia katiba hii inayopendekezwa ili Waielewe na kujua yaliyomo ndani kuliko kupiga kelele ambazo majibu yake tayari yamepatiwa ufumbuzi.  

  Lakini pamoja na hayo ili kuleta tija na matokeo chanya ya Katiba hii INAYOPENDEKEZWAitapokuwa tayari na tunaiomba Serikali na hasa mamlaka zinazosimamia sekta za sanaa kuhakikisha inasimamia taratibu zote zinazoelekeza wajibu wa Wasanii na Watendaji wake ili kufanikisha malengo.

  Hongera Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  Hongera Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba

  Nawatakia kazi njema  PAMOJA  TUILINDE  NA  KUIENDELEZA  TASNIA  YA  FIAMU TANZANIA.


  WILSON R. MAKUBI
  MKURUGENZI  MKUU
  FLEVA INC FILM ACADEMY
  0715 316  796, 0798 298 870

  0 0

   Rais Jakaya Kikwete akimpa cheti cha uraia wa Tanzania, Loveness Ruhaga (kulia) aliyekuwa Mkimbizi kutoka nchini Burundi katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Tabora leo. Rais Kikwete alitoa vyeti vya uraia kwa wakimbizi 162,156 na kuwatangazia kuwa sasa wamekuwa raia halali wa Tanzania hivyo wahakikishe wanafuata sheria zote za nchi na waepuke kufanya vurugu za aina yoyote kwani wakikiuka masharti hayo waweza kunyanganywa uraia huo. Wakimbizi hao walioingia nchini tangu mwaka 1972 walionyesha furaha kwa kuimba na kucheza vyimbo mbalimbali. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe.  
   Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole (kushoto) akimuonesha Rais Jakaya Kikwete (kulia) mchoro unaoonesha jinsi wakimbizi wa Burundi walivyoingia nchini wakati walipokuwa wanatoka nchini kwao mwaka 1972. Rais Kikwete alitoa vyeti vya uraia kwa wakimbizi 162,156 waliokuwa raia wa Burundi katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkoa wa Tabora leo. Katikati ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe.

   Rais Jakaya Kikwete akizungumza baada ya kuwapa vyeti vya uraia wa Tanzania, waliokuwa wakimbizi 162,156 kutoka nchini Burundi walioingia nchini tangu mwaka 1972. Tukio la utoaji wa vyeti hivyo lilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora mjini humo leo. Raia Kikwete katika hotuba yake aliwataka raia hao wapya kuwa waadilifu na kufuata sheria zote za nchi. Wanne kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil na kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi nchini, Harrison Mseke.  
   Msoma risala ambaye ni mwakilishi wa raia wapya 162,156 nchini ambao walikuwa wakimbizi kutoka nchini Burundi, Dafroza Baragwimba akiisoma risala yao mbele ya Rais Jakaya Kikwete (watatu kulia) wakati ya hafla ya utoaji wa vyeti kwa raia hao. Rais Kikwete alitoa uraia kwa wakimbizi hao na kuwataka wawe waadilifu na kufuata sheria zote za nchi. Wanne kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. 
  Rais Jakaya Kikwete (wasita kushoto waliokaa), mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa nchini, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (watano kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke (watatu kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa (wasita kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya raia wapya 162,156 wa Tanzania (nyuma waliosimama) baada ya kupewa vyeti vya uraia na Rais Kikwete katika hafla iliyofanyika  katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini humo.  Picha zote na Felix Mwagara, wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


  0 0

  Mgeni rasmi,Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Leornad Thadeo  akifungua bonanza la NGUVU YA KODI lililofanyika katika Viwanja vya chuo cha ustawi wa jamii katika siku ya kumbukumbu ya kuadhimisha miaka kumi na tano (15) tangu hayati  baba wa taifa Mwalimu Julius K Nyerere alipofariki  Dunia  Jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo limemkumbuka Baba wa Taifa kwa kutoa Elimu na maelezo ya kutosha juu ya Kodi na Nguvu yake katika kuchangia maendeleo ya Taifa letu na Kukuza uchumi.
   Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Leornad Thadeo (kushoto) akiwa na Mratibu wa Shirika La Activista Ein Ahimidiwe wakati akimkaribisha kusaini katika ubao wa saini
   Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Leornad Thadeo akisai ubao kuungana na Activista pamoja na Action Aid Tanzania katika upingaji wa watu kuto kulipa kodi
  Mkurugenzi wa Fedha wa TRA Bw.Salehe B Msholo ambaye alikuwa mgeni Rasmi katika bonanza akitia Saini yake katika ubao wa saini katika uwanja wa ustawi wa jamii siku ya kumbukumbu ya kuadhimisha miaka kumi na tano (15) tangu hayati  baba wa taifa Mwalimu Julius K Nyerere alipo fariki Dunia  Jijini Dar es Salaam 
   LRP Coordnator&Partnership Develop[ment manager Jovina Nawenzala Akitia saini katika ubao wa saini ili kuunga mkono wanafunzi wanaopinga  kutokulipa  kodi kwa baadhi ya wawekezaji na wengine kuwekewa punguzo la kodi.
  Bi. Jovina Nawenzala akitoa ufafanuzi wa kina kuhusu shirika la kimataifa lisilo la kiserikali la Action Aid na kazi zake katika siku ya kumbukumbu ya kuadhimisha miaka kumi na tano (15) tangu hayati  baba wa taifa Mwalimu Julius K Nyerere alipo fariki Dunia 
  Mabango mbalimbali yakiwa na  na ujumbe tofauti katika maadhimisho ya kumbukumbu ya kuadhimisha miaka kumi na tano (15) tangu hayati  baba wa taifa Mwalimu Julius K Nyerere alipofariki Dunia 
   Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la maendeleo la kabenzo Tanzania john A Sekamba Kulia akiwa na Jerry Kerenge katika bonanza hilo
   
  Watumbalimbali walio ungana na kuweza kuweka saini katika ubao ilikuweza kukumbusha  watu kulipa kodi ndio maendeleo ya nchi yetu
  Vikombe vikiwa mezani vikisubiri mshindi katika mpira wa miguu pamoja na mpira wa pete kwa mshindi wa kwanza kwa upande wa vyuo na shule za sekondari
  Mechi kati ya chuo cha ustawi wa jamii wakiwa wanapambana vikali na chuo cha kumbukumbu ya mwalimu Nyerere
   Wanatimu kwa upande wa vyuo walioshinda  na kuondoka na kikombe kwa mshindi wa kwanza ni chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere 
  Mlinda mlango wa timu ya shule ya sekondari oysterbay  akiupangua Mkwaju wa penati na kuipelekea timu yake kuwa mshindi na kutinga nusu fainali
   Baadhi ya Timu shiriki katika mashindano yaliyo andaliwa na Action Aid na Activista Tanzania 
  Mchezo wa kuvuta kamba nao haukuwa mbali hizi ni baadhi ya timu chache shiriki
  wanafunzi mbalimbali wakijiandaa kukimbia mbio za urefu wa mita miamoja
   Mshindi wa mbio za mita Miamoja (100)kwa wanafunzi wa kiume Japhet Mwandimo kutoka shule ya sekondari Kibasila
    Mshindi wa mbio za mita Miamoja (100) mwanafunzi kwa wasichana Salome Saimon akisai jina lake baada ya kuibuka mshindi
  Timu ya washindi wa mchezo wa mpira wa pete katika bonanza hilo katika shule ya sekondari wakiwa katika picha ya pamoja
  Mgeni Rasmi Akimkabidhi Mwakilishi wa mshindi wa pili katika mchezo wa mpira wa pete kutoka chuo cha ufundi Veta akipokea medani kwa niaba ya Timu
   Mshindi wa mbio za Ndimu Akipokea Medali Ya ushindi wa Mbio hizo katika Bonanza kutoka kwa mgeni rasmi
   Mkurugenzi wa Fedha wa TRA Bw.Salehe B Msholo ambaye ndiye Mgeni Rasmi akifunga Bonanza lililofanyika siku ya kumbukumbu ya kuadhimisha miaka kumi na tano (15) tangu hayati  baba wa taifa Mwalimu Julius K Nyerere alipo fariki Dunia  Jijini Dar es Salaam 
   Picha za pamoja waalimu wafanyakazi wa mashirika wanafunzi pamoja na Mgeni Rasmi
  Baadhi ya wanafunzi walio weza kuhudhuria bonanza hilo 
    kikundi cha burudani kikiwa kipo jukwaani kwaajiri ya kusherehesha katika bonanza lililo andaliwa na Action Aid Tanzania .


  0 0

  3
  Meneja wa mradi wa CIRDA kutoka UNDP, Bonizella Biagini akizungumza wakati akitambulisha maofisa waliokuwepo katika uzinduzi wa warsha ya siku tatu ya kimataifa ya ukusanyaji na matumizi ya taarifa ya hali ya hewa kwa nchi 12 duniani. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa mataifa la Mipango ya maendeleo duniani (UNDP) Phillippe Poinsot, Mwakilishi wa Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Binilith Mahenge, Bw. Richard Muyungi.

  MATAIFA 11 ikiwemo Tanzania yanakutana jijini Dar kwa mafunzo ya siku tatu yanayohusu utengenezaji wa mifumo bora ya upatikanaji wa taarifa za hali ya hewa,uchakataji wake na matumizi ya taarifa hizo kwa wananchi wa kawaida na watunga sera ili kuwa na uhakika na Mipango ya maendeleo.

  Mataifa hayo ni yale yalioyopo katika mradi wa Multi Country Support Programme to Strengthen Climate Information Systems in Africa (CIRDA).
  Nchi zinazohusika katika mpango huu pamoja na wenyeji Tanzania ni Benin, Burkina Faso, Ethiopia, the Gambia Liberia, Malawi, Sierra Leone, Sao Tome and Principe,Uganda na Zambia.

  Mpango wa CIRDA unafadhiliwa na Global Environment Facility (GEF) na Least Developed Country Fund (LDCF) ukilenga kuwezesha utumiaji wa teknolojia mpya miongoni mwa wakulima, watunga sera na sekta binafsi ili kuweza kufanya maamuzi sahihi kwa kuzingatia taarifa sahihi za hali ya hewa.

  Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkazi wa UNDP,Phillippe Poinsot Mpango wa CIRDA, ambao ni mfano wa kuigwa kwa juhudi za mataifa ya Afrika ya kuwa na ubadilishanaji wa maarifa na taarifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, huzingatia uhusishaji wa sekta binafsi, matumizi ya simu na takwimu za kilimo (agricultural index insurance).
  DSC_0083
  Akifungua mafunzo hayo, kwa niaba ya waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa rais, mazingira Binilith Mahenge, Ofisa anayeshughulikia mradi huo nchini Richard Muyungi alisema mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka ambapo dunia nzima iko katika changamoto kubwa ya mabadiliko ya tabianchi.

  Alisema Mafunzo hayo ambayo yanazinduliwa nchini yatajenga uwezo wa wataalamu wa kubadilishana maarifa ili kuona kwamba wananchi wanafaidika na utaalamu uliopo.
  Alisema Tanzania ikiwa inategemea zaidi wakulima katika uchumi wake ufikishaji wa taarifa za hali ya hewa katika ngazi za chini na kwa usahihi ni muhimu.

  Alisema program ya CIRDA ni mwenedelezo wa juhudi za serikali ya Tanzania katika kushirikiana na mataifa mengine, kuimarisha mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, kw akuongeza uwezo na weledi miongoni mwa wananchi wake na wadau wa hali ya hewa.
  Kutokana na hali hiyo Muyungi, alisema Tanzania inafuraha kufanyakazi na UNDP kwa lengo la kuhakikisha kwamba taarifa za hali ya hewa na hadhari ya awali ya uwapo wa majanga zinawafikia wananchi na zinatumika kwa ajili ya maendeleo ya taifa.
  1
  Ndugu Abbas Kitogo Afisa Miradi ya Mabadiliko Tabia nchi kutoka UNDP akijitambulisha kwa washiriki wa warsha.


  Kwa mujibu wa Muyungi Tanzania inashirikiana na UNDP kuboresha upatikanaji wa takwimu zinazotakiwa za hali ya hewa ili kupunguza madhara ya mabadiliko ya hali ya hewani katika sekta za maendeleo. Warsha hiyo inayofanyika katika hoteli ya Whitesands imelenga kutoa na kubadilishana utaalamu wa namna ya kuhudumia wananchi kupitia data zinazotolewa na mamlaka za hali ya hewa na taasisi za kukabiliana na majanga.

  Akisisitiza umuhimu wa mafunzo hayo Mkurugenzi Mkazi wa UNDP Philippe Poinsot ambaye alimwakilisha mratibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini,Alvaro Rodrigues alisema uzinduzi wa programu hiyo umelenga kuimarisha upatikanaji wa taarifa za hali ya hewa na hadhari za awali za majanga kwa manufaa ya wananchi wa mataifa hayo.

  Naye meneja wa CIRDA, Bonizella Biagini, alisema watengeneza sera, wakulima na wananchi wa Afrika wanahitaji takwimu za hali ya hewa za kisasa na zinazotolewa kisayansi kwa kasi na kwa namna wanavyoweza kuzitafsiri iliwaweze kufanya mipango yao ya muda mrefu ya maendeleo.
  8
  Mwakilishi wa Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Binilith Mahenge, Bw. Richard Muyungi akifungua mafunzo hayo ya siku tatu kwa wataalamu wa hali ya hewa, mabadiliko ya tabia nchi na wanaojihuisha na majanga kutoka nchi 12 ikiwemo Tanzania katika mpango wa CIRDA.

  CIRDA ni mpango wa kiutafiti wa mfumo wa hali ya hewa na mabadiliko yake unaozingatia upatikanaji wa data za hali ya hewa na kuzifikisha maeneo husika kwa matumizi kwa wakati.
  Mradi huo umelenga kuhakikisha wakulima, watunga sera na sekta binafsi wanafanya maamuzi kwa kuzingatia taarifa za hali ya hewa kutokana na mabadiliko makubwa yaliyopo sasa.

  Mabadlikiko ya tabia nchi yamefanya nchi nyingi kukumbwa na hali ya hewa mbaya kwa maana ya kuvuruga uasili wa mazingira na kusababisha adha katika kilimo na uvuvi.
  Mafunzo hayo yamelenga kuangalia teknolojia iliyopo sasa na namna ya kutumia teknolojia hiyo kutoa tija katika kutengeneza na kutathmini taarifa za hali ya hewa kwa lengo la kuimarisha mipango ya maendeleo ya taifa.
  DSC_0016
  Mkurugenzi mkazi wa UNDP Philippe Poinsot akihutubia katika warsha hiyo.
  Mapema mwakilishi wa UNDP Tanzania alisema Tanzania ni mojawapo ya nchi ambazo zinaathiriwa na mabadiliko ya hali ya hewa na mafunzo yatasaidia kuepuka adha za mabadiliko ya hali ya hewa kwa wananchi vijijini hasa kwa kuzingatia kwamba wananchi wake wengi wanategemea kilimo.
  Alisema kukosekana kwa taarifa za hali ya hewa kunafanya wananchi waliopo vijijini kutokuwa na uhakika na maendeleo yao na kuwa katika hatari ya kuyumbishwa na majanga mbalimbali.
  Alishukuru kwamba wataalamu wa kimataifa wanafanyakazi na serikali ya Tanzania kwa lengo la kuhakikisha kwamba taarifa za hali ya hewa zinapatikana na kutumiwa kusaidia mipango endelevu. (1) Ndugu Abas Kitogo Afisa Miradi ya Mabadiliko Tabia Nchi kutoka UNDP Akijitambulisha kwa washiriki wa warsha.
  DSC_0024
  Washiriki wa warsha hiyo wakisikiliza mada kwa makini.
  DSC_0026
  4
  Ndugu Pascal F.Waniha mwakilishi wa mkurugenzi wa mamlaka ya hali ya hewa akitoa mada wakati warsha hiyo.
  9
  Meza kuu wakipiga makofi.
  DSC_0143
  Mmoja wa watoa mada Jeremy Usher kutoka CIRDA akiwasilisha mada kuhusu umuhimu wa takwimu na uangaliaji wa mifumo katika dunia inayokabiliwa na mabadiliko ya tabia nchi.
  6
  Sehemu ya washiriki kutoka nchi kumi na moja zinazoendelea kiuchumi wakifuatilia warsha.
  2
  Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi ndugu Richard Muyungi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais.

  0 0

  DSC01247
  Mkuu wa shule ya msingi Ikungi mchanganyiko wilaya ya Ikungi, Mwl. Olivary Kamilly, akitoa taarifa yake kwenye kilele cha mahafali ya 63 yaliyofanyika kwenye viwanja vya shule hiyo kongwe iliyoanzishwa mwaka 1944.

  Na Nathaniel Limu, Ikungi
  MWENYEKITI wa halmashauri ya wilaya Ikungi mkoani SIngida, Celestine Yunde, amewaagiza maafisa mipango kushirikisha viongozi wa taasisi zenye mahitaji maalumu wakati wa kuandaa bajeti. Mwenyekiti Yunde ametoa wito huo wakati akizungumza kwenye mahafali ya 63 ya wahitimu wa darasa la saba shule ya msingi Ikungi mchanganyiko.

   Alisema hatua hiyo itawajengea mazingira mazuri maafisa kutambua ukubwa wa bajeti katika taasisi husika. Akifafanua,Yunde alisema shule ya msingi Ikungi Mchanganyiko, ni taasisi maalum kwa madi kwamba inayo wanafunzi wenye ulemavu mbali mbali na wasio walemavu ambao baadhi wametoka nje ya mkoa.

  “Wanafunzi wenye ulemavu mbali mbali , ni wanafunzi ambao mahitaji yao mengi ni ya gharama kubwa.Ukiachilia mbali gharama za nauli wanakotoka,karibu kila kundi lina mahitaji maalum na ni ghali", alifafanua Yunde. Alisema wanafunzi hao walemavu wanaishi kwenye mabweni, mahitaji yao ni ya gharama kubwa na hivyo halmashauri inayo jukumu la kushirikisha viongozi wa shule hiyo,wakati wa kuandaa bajeti itakayokidhi mahitaji.
  DSC01266
  Mgeni rasmi katika mahafali ya 63 ya shule ya msingi Ikungi mchanganyiko, Celestine Yunde, akimkabidhi cheti mmoja wa wahitimu wa darasa la saba (mwenye ulemavu wa macho).
  DSC01273
  Baadhi ya wahitimu wa darasa shule ya msingi Ikungi mchanganyiko wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, wakiwa wamepozi na vyeti vyao vya kumaliza elimu ya msingi.
  DSC01263
  Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi,Celestine Yunde, akizungumza kwenye mahafali ya 63 ya shule ya msingi Ikungi mchanganyiko yaliyofanyika kwenye viwanja vya shule hiyo.
  “Naahidi mwezi huu tarehe 29, nitaleta shuleni hapa madiwani wote wa halmashauri yetu. Nataka madiwani hawa waje wajionee wenyewe uhitaji mkubwa wa fedha kwa ajili ya kugharamia uendeshaji wa shule hii yenye walemavu mbalimbali, wengine wanaandikia miguu badala ya mikono”,alisema.
  Katika hatua nyingine, mwenyekiti huyo aliupongeza uongozi wa shule hiyo kwa ubunifu wake uliopelekea shule kupewa kompyuta 10 na printa moja, na mamlaka ya mawasiliano Tanzania.
  “Katika taarifa yenu, mmesema shule ilishiriki shindano lililoendeshwa na mamalaka ya mawasiliano Tanzania, na kati ya zaidi ya shule 3,000 nchini zilizoshoriki shindano hilo,ninyi ni miongoni mwa shule nne tu, zilizofanikiwa kushinda. Hongereni sana na hasa pongezi hizi zimwendee mkuu wa shule, Olivary Kamily”,alisema mwenyekiti huyo.
  Kwa mujibu wa wakuu wa shule hiyo Kamilly, msaada huo wa kompyuta, unaambatana na kufungiwa mtandao wa huduma ya intaneti kwa mwaka mmoja. Pia itazinduliwa website ya shule.
  Jumla ya wanafunzi 165 walioanza shule mwaka 2008, 85 wamehitimu kati yao wavulana 25 na wasichana 60.
  DSC01278
  DSC01287
  Baadhi ya wazazi wa wahitimu wa darasa la saba shule ya msingi Ikungi mchanganyiko,wakishiriki burudani na wanafunzi waliomaliza elimu ya msingi.
  DSC01300
  Bango la shule ya msingi Ikungi mchanganyiko wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida.(Picha na Nthaniel Limu).

  0 0

  Jezi Zilizodhaminiwa na Binslum
  Jezi zilizodhaminiwa na Binslum
  Group la Kandanda katika Mtandao wa Facebook tarehe 25/10/2014 litakuwa likitimiza miaka 4 tangu kuanzishwa ndani ya facebook.

  Kuadhmisha siku hiyo, Members wa Kundi hilo wametengeza timu ambazo ni #TeamDizomoja na #TeamIsmail, ambazo zitachuana siku hiyo katika viwanja vya TCC Sigara-Chang’ombe.
  Timu hizo zote mbili zimekuwa na maandalizi ya Takribani Miezi miwili sasa, na usajili ulishafungwa tarehe 11/10/2014.Dizo-Moja-na-ISmail-Banner
  Sherehe hizo zinatarajiwa kuanza saa 3 Asubuhi ikifuatiwa na Offline Socializition yamembers wa kundi hilo ambao hutumia 24/7 kujadili masuala ya soka katika Facebook.

  Kamati ya maandalizi inawakaribisha wanakandanda wote kwa makabila (Timu) tofauti popote mlipo katika viwanja hivyo vya TCC Sigara, usisahau Jezi yako tuu! Ndicho kitambulisho cha Kabila zetu

  0 0

   Pichani (wa tatu kulia),Meneja Matekelezo Mfuko wa Pensheni wa LAPF,Bwa.Victor Kikoti akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani),mapema leo katika ofisi zao zilizopo jengo la Millenium Tower,Kijitonyama jijini Dar,kuhusiana na kufanyika kwa mkutano wao wa 7 wa mwaka wa wadau kuanzia Oktoba 23 mpaka 24, 2014.

  Mkutano huo utafanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano (AICC),jijini Arusha.Bwa.Victor amesema kuwa kauli mbiu ya mkutano huo ni '' kusherehekea miaka 70 ya ukuaji na huduma bora kwa Wanachama''. '' Kauli mbiu hii imefikiwa baada ya mfuko kutimiza miaka 70 tangu ulipoanzishwa mwaka 1944,ambapo Wadau wa mkutano huo watajadili kwa kina juu ya huduma za LAPF kwa miaka 70iliyopita pamoja na kushiriki mafanikio ya mfuko kwa pamoja.

  Matekelezo Mfuko wa Pensheniwa LAPF,Bwa.Victor Kikoti amesema kuwa,Mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwaWAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh.Hawa Ghasia
   
  Pichani kulia ni Meneja Mkoa Bwa.Ramadhani Mkeyange,Meneja Takwimu,Tathmini na Hadhari Bwa.Abubakar Ndwata pamoja na Meneja wa Kanda ya Dar,Bi.Amina Kassim
   Meneja Takwimu,Tathmini na Hadhari Bwa.Abubakar Ndwata,akifafanua moja ya swali aliloulizwa na Waandishi wa Habari kuwa mfuko wa LAPF unaendelea kujivunia mafanikio ya kuwa mfuko unaokuwa kwa kasi hapa nchini pamoja na kuwa bora kwa miaka mitano mfululi kwenye suala zima la uwajibikaji na utunzaji wa vitabu.

  Amesema kuwa mfuko pia utazindua logo mpya  inayotumika,ambayo  inaashiria ukuaji wa mfuko huo na dhamira yao ya kuendelea  kukua zaidi  na kuboresha huduma kwa wanachama wao,ameongeza kusema kuwa mfuko huo utatoa fursa  mpya ya mkopo wa elimu kwa wanachama wake ilivyozinduliwa mwezi Agosti mwaka huu.
  Pichani ni baadhi ya wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo wa LAPF.

  0 0

  Mganga Mkuu wa Zahanati ya Makuburi, Manispaa ya Kinondoni, Dkt. Stella Kivugo (kulia), akijaribu kufungua bomba la maji, baada ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Makaburi, Bw. James Ngoitanie (wa nne kushoto), kukata utepe kuzindua kisima cha maji kilichojengwa kwa hisani ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wengine ni watendaji wa Mtaa wa mwongozo. (Na Mpigapicha Wetu)
   Mwenyekiti wa Mtaa wa Mwongozo, Dar es Salaam, Bw. James Ngoitanile (wa nne kushoto), akifurahia kwa kuonesha mkasi juu baada ya kukata utepe kuzindua rasmi kisima cha maji safi, kilichojengwa kwa hisani ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), katika Zahanati ya Makuburi, Manispaa ya Kinondoni. Kulia ni Mganga Mkuu wa Zahanati hiyo, Dkt. Stella Kivugo na Meneja Mauzo wa TBL Kinondoni, Bw. Joseph Nicholaus (wa pili kulia).

  Mwenyekiti wa Mtaa wa Mwongozo, Bw. James Ngoitanile, akimtwisha ndoo ya maji Mjumbe wa Shina, Bi. Zubeda Samata, baada ya kuzindua bomba la maji safi lilijengwa kwa Hisani ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), katika Zahanati ya Makuburi, Dar es Saaam.   Mwenyekiti wa Mtaa wa Mwongozo, Dar es Salaam, Bw. James Ngoitanile (wa nne kushoto), akifurahia kwa kuonesha mkasi juu baada ya kukata utepe kuzindua rasmi kisima cha maji safi, kilichojengwa kwa hisani ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), katika Zahanati ya Makuburi, Manispaa ya Kinondoni mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mganga Mkuu wa Zahanati hiyo, Dkt. Stella Kivugo na Meneja Mauzo wa TBL Kinondoni, Bw. Joseph Nicholaus (wa pili kulia).

   Mwenyekiti wa Mtaa wa Makaburi, Bw. James Ngoitanie (wa nne kushoto), akifungua koki ya maji baada ya kukata utepe kuzindua kisima cha maji kilichojengwa kwa hisani ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Uhusiano wa TBL, Bi. Doris Malulu, Mganga Mkuu wa Zahanati ya Makuburi, Manispaa ya Kinondoni, Dkt. Stella Kivugo, Meneja Mauzo wa TBL Kinondoni, Bw. Joseph Nicholaus (wa tatu kulia)  na watendaji wa Mtaa wa mwongozo. (Na Mpigapicha Wetu)
   Mwenyekiti wa Mtaa wa Mwongozo, Bw. James Ngoitanile, akimtwisha ndoo ya maji Mjumbe wa Shina, Bi. Zubeda Samata, baada ya kuzindua bomba la maji safi lilijengwa kwa Hisani ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), katika Zahanati ya Makuburi, Dar es Saaam.

  0 0
 • 10/15/14--02:50: KIBONZO CHA NATHAN MPANGALA


 • 0 0

  Stori: Ojuku Abraham
  SHIRIKA la Ndege la Fast Jet linalotoa huduma ya usafiri wa anga katika baadhi ya mikoa ya Tanzania na nje ya nchi, limelalamikiwa na wateja wake mbalimbali kutokana na jinsi linavyofanya kazi, Risasi Jumatano lina habari kamili.
  Wafanyakazi wa Shirika la ndege la Fast Jet.
  Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili, baadhi ya wateja hao wamesema kuwa, matangazo ya kila siku kuwa shirika hilo linatoa huduma ya usafiri wa anga kwa bei nafuu ni usanii, kwani tiketi…
  Stori: Ojuku AbrahamSHIRIKA la Ndege la Fast Jet linalotoa huduma ya usafiri wa anga katika baadhi ya mikoa ya Tanzania na nje ya nchi, limelalamikiwa na wateja wake mbalimbali kutokana na jinsi linavyofanya kazi, Risasi Jumatano lina habari kamili.
  Wafanyakazi wa Shirika la ndege la Fast Jet.
  Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili, baadhi ya wateja hao wamesema kuwa, matangazo ya kila siku kuwa shirika hilo linatoa huduma ya usafiri wa anga kwa bei nafuu ni usanii, kwani tiketi zinazouzwa kwa bei hizo ndogo, daima huelezwa kuwa zimekwisha.

  “Wanatangaza kuna tiketi za shilingi 32,000, ni uongo, mimi binafsi nimewahi kuulizia hizi tiketi mara kadhaa, lakini kila nikiomba ninaambiwa zimeisha na hata ndani ya ndege sijawahi kukutana na msafiri mwenye tiketi ya bei hizo,” alisema Samuel Kuntu, mkazi wa jijini Mwanza.

  Aliongeza yeye amewahi kusafiri mara kadhaa na ndege za Fast Jet, lakini amegundua upungufu mkubwa wa shirika hilo, ikiwemo nauli kubwa tofauti na inavyotangazwa kwenye vyombo vya habari. “Jana (Jumapili iliyopita) nilikuja na ndege hii na nimelipia shilingi laki nne kwa safari ya Dar, bei hii ni kubwa, nadhani ATCL ndilo shirika lenye bei rahisi, lakini si hawa,” alisema Kuntu ambaye alionekana kujua mengi kuhusu Fast Jet.
  Abiria wakishuka kutoka kwenye ndege ya Fast Jet.
  Alisema shirika hilo la ndege lina utaratibu unaomuumiza mteja hasa pale anapoahirisha safari au kuchelewa ndege, tofauti na mashirika mengine kama Precision Air na Air Tanzania.

  “Inapotokea abiria amechelewa ndege (no-show), Fast Jet humtaka alipe tiketi nyingine na kulipa asilimia 100, wakati mashirika mengine humtoza faini abiria ambaye amechelewa ndege kwa asilimia 25 ya bei aliyonunulia tiketi kisha kumpangia siku nyingine ya safari.

  “Wakati mwingine wanaahirisha safari au ndege kuchelewa lakini mteja hafidiwi kwa chochote, ila mteja akichelewa, harudishiwi hata shilingi wala kupangiwa siku nyingine, alisema mfanyabiashara huyo anayesafiri mara kwa mara kati ya Mwanza na Dar es Salaam.

  Msafiri mwingine , Sunday Shomari ambaye alisafiri na ndege hiyo akitokea Arusha kwenda Dar es Salaam, alisema alisahau simu yake ya mkononi ya gharama kubwa pamoja na Ipad yake ndani ya ndege hiyo, lakini muda mchache baada ya kurejea hakupata vitu vyake.

  “Nilikuwa na mke na watoto tunatoka Arusha, tulipofika Dar es Salaam tukashuka na kuvisahau vitu hivyo kwa bahati mbaya, tulipofika nje mke wangu akaniuliza simu yako ipo wapi? Nikakumbuka nimeisahau ndani ya ndege, nikarudi uwanjani na kuwaomba walinzi wanisaidie niende nikachukue simu yangu.
  Marubani wa ndege ya Fast Jet wakiwa mzigoni.
  “Wakaniambia wao hawana mamlaka ya kuingia ndani ya ndege ile, badala yake wakanisaidia kuwaambia wafanyakazi wa ndege kuwa waniangalizie vitu vyangu pale nilipokaa, lakini jambo la ajabu eti wakadai hawakuviona, wakati mimi nilikuwa msafiri wa mwisho kushuka kwenye ndege, ina maana hakukuwa na mwingine baada ya mimi kushuka ambaye ningeweza kusema l ndiye aliyechukua vile vitu,” alisema Shomari ambaye ni mtangazaji wa zamani wa ITV na Radio One, kwa sasa anafanya kazi Sauti ya Amerika (Voa) jijini Washington, Marekani.

  Abiria mwingine aliyekataa jina lake kutajwa gazetini, alisema mshangao mwingine kwenye ndege za shirika hilo ni kuuziwa vitu ambavyo katika mashirika mengine, wasafiri hupewa bure akitolea mfano soda, bia na viburudisho vingine.

  Mwandishi wa habari hizi alifika katika ofisi za Fast Jet zilizopo Barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam kwa lengo la kutaka maelezo ya uongozi kuhusu tuhuma hizo, lakini walinzi walimzuia kuingia ndani na kutakiwa kuchukua anuani ya barua pepe ya msemaji wake, kwa maelezo kwamba ndiye angeweza kumsaidia kwa mambo ya kihabari.

  Mwandishi aliandika madai yote na kuyatuma kwenye anuani hiyo akitaka kuonana na uongozi kwa ajili ya kujibu maswali kadhaa, lakini afisa uhusiano aliyejibu ujumbe huo, Lucy Mbogoro, baadaye alilitaka gazeti hili kuandika maswali hayo na kuyatuma, sambamba na nakala ya sura ya mbele ya gazeti.

  Lakini hata baada ya kutuma maswali hayo kama ilivyotakiwa, Fasjet wameshindwa kutoa majibu na Lucy alipopigiwa simu na kuulizwa, alidai anayehusika na majibu hayo ametingwa na kazi.Hata hivyo, gazeti hili bado linafuatilia kwa karibu ili kupata majibu ya maswali hayo.


  0 0

   Meneja Biashara wa Bayport Tanzania, Thabit Mndeme kushoto; na Meneja Masoko na Mawasiliano (katikati), Ngula Cheyo waki zinduwa Mkopo wa Bidhaa, Bayport Head office Daressalaam.
  =====  =====  =====
  TAASISI ya kifedha ya Bayport Tanzania, leo imezindua huduma mpya ijulikanayo kama Mikopo ya Bidhaa ikiwa na lengo la kurahisha utendaji kazi wa watumishi wa umma na wafanyakazi wote wa kampuni zilizoidhinishwa na Bayport.

  Uzinduzi huo uliofanyika jana, umeonyesha matumaini mapya ya Watanzania wanaosumbukia usafiri katika vituo vyao vya kazi, hususan maeneo ya mikoani ambako mara kadhaa kumesikika malalamiko ya maisha magumu ya watumishi wa umma.

  Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Meneja Biashara wa Bayport Tanzania, Thabit Mndeme, alisema kwamba  ni wakati wa kukuza uchumi wan chi kwa kuhakikisha kuwa watu wote wanafanya kazi kwa bidii na shauku yote.

  Alisema wapo watumishi ambao wanaishi kwa tabu kutokana na changamoto ya usafiri na mahitaji mengine ya kijamii, hivyo kwa kupatikana hudumaa mpya ya kukopeshwa pikipiki bodaboda ni jambo zuri kwao.

  ‘’Bayport tumekaa na kuangalia namna gani Watanzania wataendelea kufanya kazi kwa moyo na kukuza uchumi wetu, tukaona sambamba na kuwakopesha fedha kama tunavyofanya, pia tuwakopeshe bidhaa kama vile Boxer, Toyo na Lifan.

  ‘’Zote hizi zitakuwa kwenye mpangilio mzuri sambamba na kuzikatia huduma ya bima, kuzifanyia servise mara tatu bure, garantii ya mwaka mmoja, huku mkopaji akitakiwa kulipa kwa miezi 36 sawa na miaka mitatu,’’alisema Mndeme.

  Naye Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Tanzania, Ngula Cheyo, alisema kuwa mikopo hiyo mipya itapatikana kwa masaa 24, huku ikipatikana pia kwa mikoa yote na wilaya zote kwenye ofisi za Bayport Tanzania.

  ‘’Tunawaomba watu waendelee kuiunga mkono Bayport kwa kuhakikisha kuwa wanachangamkia fursa hii ya mikopo ya bidhaa ambayo tumeianzisha ili kuwafanya watumishi wa umma na wafanyakazi wengine warahisishiwe utendaji wao wa kazi,’’ alisema Cheyo.
   

older | 1 | .... | 386 | 387 | (Page 388) | 389 | 390 | .... | 1898 | newer