Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 384 | 385 | (Page 386) | 387 | 388 | .... | 1898 | newer

  0 0


   Single Mtambalike 'Richie'.MSANII wa maigizo na filamu nchini Na aliyekuwa Jaji wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) Single Mtambalike maarufu kwa jina la Richie, amefiwa na baba yake mzazi Mzee Mtambalike usiku wa kuamkia leo, Msiba upo Tabata, Dar.Timu Nzima ya Tanzania Movie Talents (TMT) na Kampuni nzima ya Proin Promotions Limited inapenda kutoa pole kwa Rich na familia yake kwa kuondokewa na Mzazi wake. TMT na Proin Promotions inaunga nae katika Kipindi hiki kigumu 

  0 0


  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu zoezi la utoaji wa chanjo ya Matende , Mabusha, dawa za Minyoo, matone ya Vitamini A, na Surua  - Rubella,  litakalofanyika  katika mikoa yote ya Tanzania kuanzia  Oktoba 18 hadi 24, 2014.
   Kaimu Mgaga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Dkt. Hawa Kawawa  akisisitiza umuhimu wa  chanjo ya Surua –Rubella itakayotolewa wakati wa zoezi la chanjo Oktoba 18 hadi 24 na umuhimu wake kwa wanawake walio katika umri wa kuzaa na wajawazito ambapo huwakinga watoto walio tumboni dhidi ya Virusi ambavyo huleta madhara pindi watoto wanapozaliwa.

  Picha na Aron Msigwa - MAELEZO
   
  WAKAZI  DAR WAASWA KUJITOKEZA KWENYE CHANJO YA MATENDE NA SURUA-RUBELLA.

  Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
  10/10/2014. Dar es salaam.

  Wakazi wa jiji la Dar es salaam wametakiwa kushiriki kikamilifu katika zoezi la utoaji wa chanjo ya Matende , Mabusha, dawa za Minyoo, matone ya Vitamini A, na Surua  - Rubella,  litakalofanyika  katika mikoa yote ya Tanzania kuanzia  Oktoba 18 hadi 24, 2014.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki amesema kuwa serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inaendesha zoezi hilo kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) na  Shirika la kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF) kwa lengo la kudhibiti magonjwa yayoweza kuzuilika ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa kuboresha afya za wananchi. 

  Amesema zoezi hilo litawahusisha watoto  wenye umri wa miezi 9 hadi miaka 15 ambao watapatiwa chanjo ya Surua-Rubella, watoto wenye umri wa miezi 6 hadi 59  watapatiwa matone ya Vitamini A huku dawa za minyoo zikitolewa kwa wale walio na umri kunzia mwaka 1 hadi miezi 59 . 

   Ameeleza kuwa zoezi la utoaji wa chanjo ya dawa za Matende na Mabusha litawahusisha wananchi wote walio na umri wa kuanzia miaka 5 hadi 100.

  Bw. Meck Sadiki amefafanua kuwa  katika jiji la Dar es salaam huduma itatolewa katika vituo vya afya pamoja na vituo vya muda vitakavyochaguliwa na viongozi  wa serikali ngazi ya kata ili kukidhi mahitaji na kusogeza huduma ya chanjo karibu na wananchi.

  Aidha, amesema baadhi ya wadau wakiwemo LIONS  CLUB, RED CROSS na viongozi wa dini wamejitolea  kuwahamasisha wananchi katika  maeneo mbalimbali ili waweze kuitikia wito wa kushiriki  katika zoezi hilo muhimu kwa maendeleo ya taifa.
   
  Ametoa wito kwa wananchi hususan wakazi wa jiji la Dar es salaam kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha zoezi hilo litakalofanywa na wataalam wa afya na kusisitiza kuwa chanjo hiyo ni salama na itatolewa bure na Serikali kwa wananchi wote.

  Kwa upande wake Kaimu Mgaga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Dkt. Hawa Kawawa amesema kuwa zoezi hilo  ni salama na lina umuhimu mkubwa kwa afya na maendeleo ya wananchi na kuongeza kuwa litasimamiwa na wataalam wa afya .

  Akizungumzia kuhusu utoaji wa chanjo ya Surua –Rubella amesema kuwa una umuhimu mkubwa kwa wanawake walio katika umri wa kuzaa na wajawazito ambapo huwakinga watoto walio tumboni dhidi ya Virusi ambavyo huleta madhara pindi watoto wanapozaliwa.

  Amesema Virusi hivyo huwa na athari kwa mtoto aliye tumboni kwani humsababishia kuzaliwa akiwa na ngozi yenye vipele, homa, tatizo la mtoto wa jicho, mtindio wa ubongo, ulemavu na tatizo la Moyo.

  Ametoa wito kwa wanachi wote hususan wakazi wa jiji la Dar es salaam kujitokeza kwa wingi ili waweze kupata chanjo zitakazowakinga watu wazima na watoto dhidi ya magonjwa mbalimbali.

  0 0

  Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) laanza kuuza viwanja takribani 444 vyenye jumla ya mita za mraba 465,161 katika eneo la Kiluvya A Halmashauri ya Kisarawe Mkoa wa Pwani.

  Hayo yamesema na Meneja Miradi wa NSSF Bw.Abdallah Mseli  wakati wa ziara ya waandishi wa habari walipotembelea eneo la mradi huo kuona maendeleo ya mradi huo .

   “Eneo hili litakuwa na makazi mapya ya kisasa, litakuwa na huduma muhimu za maji,umeme,barabara na pia kuna maeneo ya kujenga shule, zahanati na maduka ya kisasa ” alisema  Mseli

  Akifafanua zaidi kuhusu mradi huo Mseli amesema fomu za maombi ya kununua viwanja zinapatikana kwa gharama ya shilingi elfu 40,000  katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashuri ya Wilaya ya Kisarawe na Ofisi za NSSF Benjamin Mkapa Pension Towers.

   Akizungumzia bei za viwanja Mseli  alisema kwa kiwanja cha makazi pekee (ujazo wa juu na kati) gharama kwa kila mita ya mraba ni elfu 15,000/- wakati wakati kwa makazi pekee (ujazo wa chini) Mita  moja ya mraba ni 16,000/.

  Kwa upande wa Viwanja kwa ajili ya Makazi na biashara Mseli alibainisha kuwa gharama ya kila mita ya mraba ni elfu 17,000/ na vile vya nyumba za ibada vitauzwa elfu 10,000 kwa kila mita ya mraba.

  Kwa wale watakaohitaji viwanja kwa ajili ya makazi maalum (housing estate) Mseli alibainisha kuwa vitauzwa shilingi elfu 20,000 kwa kila mita ya mraba.

  Naye Meneja uhusiano wa NSSF Bi Eunice Chiume alitoa wito kwa wananchi kutumia fursa hiyo ambayo imetolewa na shirika hilo ikiwa ni sehemu ya mkakati wake wa kusaidia jamii  na kuchangia katika maendeleo ya Taifa.

  Mradi wa NSSF (Serviced plots) uliopo kata ya Kiluvya-A Madukani Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani una eneo lenye ukubwa wa Hekta 90.5 sawa na ekari 223.6 na una jumla ya viwanja 444 vyenye mita za mraba 465,161.

  0 0

    Mkurugenzi wa Mazingira katika Mradi wa Ziwa Tanganyika akiongea katika Warsha inayohusu mradi huo iliyofanyika mjini Bagamoyo
   Mgeni Rasmi ambaye ni Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Richard Muyungi akiongea na wadau waliohudhuria warsha hiyo.
   Sehemu ya Washiriki wa Warsha hiyo wakimsikiliza mgeni Rasmi
  Picha ya pamoja ya Washiriki wa warsha ya siku moja ya uelewa wa Jamii juu ya mradi wa Ziwa Tanganyika iliyofanyika mjini Bagamoyo.

  0 0

   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya Uteuzi wa Makadhi wa Wilaya za Unguja na Pemba.

  Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee Makadhi hao ni Sheikh Ali Haruna Ramadhan-Unguja na Sheikh Abubakar Ali Mohamed-Unguja.

  Wengine ni Mohamed Ramadhan Khamis-Unguja na Sheikh Omar Juma Othman-Pemba. Rais Shein amefanya Uteuzi huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu namba 5 cha Sheria ya Mhakama ya Kadhi Namba 3 ya mwaka 1985 kama ilivyorekebishwa na Sheria namba 4 ya mwaka 2003.

  Uteuzi huo umeanza Septemba 12,2014
  IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

  0 0

   Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Said Ali Mbarouk amewateua Wajumbe watatu kuwa Wajumbe wa Baraza la Taifa la Michezo la Zanzibar.


  Wajumbe hao ni Ndugu Ameir Mohamed Makame kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar. Wengine ni Hassan Kificho kutoka Idara ya Watu wenye Ulemavu na Khamis Abdallah Said kutoka Wadau wa Michezo.

  Uteuzi huo umeanza Octoba 10, 2014
  IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR

  0 0

  MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umeandaa ibada maalum ya kumkumbuka Baba wa taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere itakayofanyika katika mashamba yao yaliyopo kijiji cha Ngarambe, Mkuramga mkoa wa Pawani.

  Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema jana kuwa katika ibada hiyo itaongozwa na Shekhe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Musa Salum kwa upande wa Waislam na Padri John Solomon kwa upande wa Wakristo.

  Taalib alisema katika ibada hiyo Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Mercy Silla na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo wamealikwa kuhudhuria ambayo itakuwa sambamba na ugawaji wa mashamba kwa wanachama ambao wamekubali kulima katika shamba la SHIWATA lenye ekari 500.

  Alisema SHIWATAitaendelea kuenzi fikra za Hayati Mwalimu Nyerere alizowahi kuzifanya na kuziendeleza wakati wa uhai wake ambako wasanii waliitikia mwito kwa kuanzisha kijiji chao cha Mwanzega chenye ukubwawa hekari 300 za makazi ambako mpaka sasa zimejengwa nyumba 66 na nyingine zinajengwa na kukabidhiwa Desemba mwaka huu.

  Alisema SHIWATA yenye wanachama zaidi ya 8,000 imekuwa ikihamasisha wanachama wakewajenge nyumba katika kijiji chao ambacho Serikali imekitambua rasmikwa kukizindua kupitia Mbio za Mwenge wa Uhuru Julai mwaka huu.

  Ofisa Habari wa SHIWATA

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la msingi kuzindua rasmi ujenzi wa barabara ya kilometa 16 kutoka Usagara hadi Kisesa mkoani Mwanza leo.Rais Kikwete yupo mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua daraja la Nyashishi lenye urefu wa mita 67 lililopo katika barabara ya Usagara Kisesa wakati alipokwenda kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara kilometa 16 ya Kisesa hadi Usagara inayojengwa kwa kiwango cha lami leo.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzibdua rasmi daraja la waenda kwa miguu Mabatini Mkoani Mwanza leo.Wapili kushoto ni Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli.
  Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli akimuongoza Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kukagua daraja la waenda kwa miguu huko Mabatini Mkoani Mwanza leo muda mfupi baada ya kulifungua leo.
  Muonekano wa Daraja la waenda kwa miguu liliojengwa Mabatini huko Mwanza lililozinduliwa na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo. (picha na Freddy Maro)

  0 0

  Mke wa Marehemu, Mama Getrude Shija (kushoto), akifuatana na Mama Balozi (Joyce Kallaghe), ndugu, jamaa na marafiki, wakiingia kanisani kushiriki Ibada maalum ya kuuaga Mwili wa Marehemu Dk. William Shija.

  Mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Commonwealth Parliamentary Association (CPA), Dr. William Shija, aliyefariki dunia Jumamosi ya Tarehe 4 Oktoba 2014, umeagwa rasmi jana katika Ibada maalum iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Vincent de Paulo, Osterley, London.

  Ibada hiyo iliyohudhuriwa pia na Balozi wa Tanzania, Uingereza, Mhe. Peter Kallaghe na maafisa wa Ubalozi, ndugu, jamaa na marafiki na wafanyakazi wengine wa ubalozi walikuwepo Kanisani hapo. Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa leo jioni kwa Shirika la ndege la Emirates kwenda Dar es salaam, na hatimaye Sengerema kwa mazishi.

  Mungu aiweke roho ya Marehemu Dk. William Shija mahala pema Peponi ( Amin)
  Mwili wa Marehemu Dk. William Shija ukiingizwa kwenye Kanisa la Mtakatifu Vincent de Paulo kwa Ibada maalum na kuagwa rasmi na ndugu na jamaa wa marehemu.
  Father Mark wa Kanisa Katoliki la Vicent de Paulo, akiongoza Ibada maalum ya kuuga mwili wa marehemu Dk. William Shija Kanisani hapo.
  Mama Balozi Joyce Kallaghe(kushoto), Mke wa Marehemu, mama Getrude Shija, Watoto wa Marehemu, Ndugu na jamaa wa marehemu wakiwa kwenye Ibada ya kuuga Mwili wa Marehemu.
  Mama Balozi Joyce Kallaghe(kushoto), Mke wa Marehemu, mama Getrude Shija, watoto wa Marehemu, Ndugu na jamaa wa marehemu wakiwa kwenye Ibada ya kuuga Mwili wa Marehemu
  Monica William Shija, mtoto wa Marehemu, akiongoza somo moja katika Ibada hiyo maalum ya kuuga Mwili wa Marehemu Dk. William Shija.

  Father Mark akimpa mkono wa pole Mke wa Marehemu, mama Gertude mara baada ya kumalizika kwa Ibada hiyo maalum iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Vincent de Paulo.
  Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Peter Kallaghe akipeana mkono na Father Mark mara baada ya kumalizika kwa Ibada maalum ya kuuga Mwili wa Marehemu Dk. William Shija.
  Balozi wa Tanzania, Uingereza, Mhe. Peter Kallaghe, akijumuika pamoja na familia ya marehemu Dk. William Shija, Ndugu, Jamaa na marafiki waliofika Kanisani hapo kuuaga mwili wa marehemu kwenye Ibada maalum iliyoandaliwa kwenye kwenye Kanisa Katoliki la Mtakatifu Vicent de Paulo, London.

  0 0


  Baraza la waTanzania waishio nchini Marekani (DICOTA) limemaliza mkutano wake wa mwaka Jumapili ya Oktoba 5 jijini Durham jimbo la North Carolina ambao kwa wengi waliohudhuria, wameonyeshwa kuridhishwa nao
  Mwenzangu Mubelwa Bandio, anayo taarifa kamili.

  Hii ni sehemu ya ripoti za Kwanza Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).Hii ilikuwa ripoti ya Oktoba 11, 2014

  0 0

  Attachments area


  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile akiwasilisha mapendekezo yake kwa Bw. Denny H. Kalyalya ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake wa kundi namba 1 la Afrika na Bw. Peter Larose ambaye ndiye anachukua nafasi hiyo.
  Bw. Denny H. Kalyalya ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake wa kundi namba 1 la Afrika na Bw. Peter Larose ambaye ndiye anachukua nafasi hiyo wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile alipokuwa akiwasilisha mapendekezo yake kuhusu hali halisi ya misaada.
  Ujumbe kutoka Tanzania ukimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile alipokuwa akiwasilisha mapendekezo yake kwa Bw. Denny H. Kalyalya ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake wa kundi namba 1 la Afrika na Bw. Peter Larose Mkurugenzi Mtendaji mpya anayeachiwa kiti.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile na Gavana wa Benki kuu ya Tanzania wakiwaangalia kwa mshangao wakurugenzi hao wawili walipokuwa wakiingia (hawapo kwenye picha).habari/picha na Ingiahedi Mduma,Wizara ya Fedha.

  ========  ========  ========
  Katika mkutano muhimu uliofanyika jioni hii hapa mjini Washington DC. Kati ya ujumbe kutoka Tanzania ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile na Bw. Denny H. Kalyalya ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake wa kundi  namba 1 la Afrika pamoja na Bw. Peter Larose ambaye ndiye anachukua nafasi hiyo ulimpatia nafasi nzuri sana Dr. Likwelile kuweza kueleza mambo muhimu ambayo Benki ya Dunia ingepaswa kuyafahamu.

  Katika mawasilisho yake katibu Mkuu huyo aliwaeleza viongozi wa Benki ya Dunia kuwa ,anashukuru kwa ushirikiano mkubwa ambao ameupata kutoka Benki ya Dunia na kusema kuwa hii imeisaidia sana Tanzania katika kupiga hatua kiuchumi. Akiendelea kuzungumza Dr. Likwelile alisema kuwa pamoja na kufanikiwa katika ushirikiano huo kumekuwa na tatizo ambalo lina sababisha kuchelewa kwa utekelezaji wa Bajeti.

  Hili amelieleza kuwa linatokana na masharti ya wafadhili kutaka kwanza mambo yanayohusu IPTL kupatiwa ufumbuzi , kitu ambacho hakikuweko kwenye makubaliano. “ IPTL haina uhusiano na makubaliano ya awali suala hili limeingia katikati hii inaathiri utekelezaji wa kibajeti.”alisema.

  Aidha aliendela kueleza kuwa sera ya Benki ya Dunia inadai kuwa kabila la Kimasai limetengwa na hivyo kutaka baadhi ya miradi isiende sehemu nyingine zaidi ya umasaini, hii nayo ni changamoto nyingine”. Katika mazungumzo hayo ilionekana kweli kuwa kwa kuchelewesha kutoa fedha kwa ajili ya miradi kunachangia sana kurudisha nyuma maendeleo.

  Kwa mapendekezo haya mawili makubwa kama yatafikishwa kwenye ngazi ya juu na yakafanyiwa kazi basi nchi yetu itapiga hatua kama ilivyojipangia.  Wakurugenzi hao waliyapokea mapendekezo hayo kwa mikono miwili na wakaahidi kuyafikisha na kuyafanyia kazi. Hali ya hewa mjini hapa ni ya baridi na manyunyu ya hapa na pale.


  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi jengo la kitega uchumi la mfuko wa pensheni la PPF mjini Mwanza jana jioni.Wengine katika picha kutoka kushoto,ni Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli, Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bwana Wiliam Erio, Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Adam Malima, Mwenyekiti wa Bodi ya PPF Bwana Ramadhani Kija, na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evaristi Ndikilo.
  Jengo la Kitega uchumi la mfuko wa pensheni wa PPF lililozinduliwa rasmi na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mjini Mwanza jana jioni.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bwana William Erio wakiangalia madhari nzuri ya jiji la Mwanza wakiwa katika jengo jipya la kitega uchumi la mfuko wa pensheni wa PPF muda mfupi baada ya kulizindua mjini Mwanza jana jioni.
  Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya PPF Bwana Ramadhani Kija(watatu kushoto), na Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bwana William Erio(kulia) wakimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kuzindua jengo la kitega uchumi la PPF mjini Mwanza jana jioni.
  Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bwana William Erio akitoa maelezo kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ndani ya mgahawa uliopo katika jengo jipya la kitega uchumi la PPF muda mfupi baada ya kulizindua rasmi mjini Mwanza.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na viongozi na wafanyakazi wa Shirika la PPF baada ya kuwa amezindua Jengo la Kitega Uchumi la Shirika hilo katikati ya Jiji la Mwanza jana, Ijumaa, Oktoba 10, 2014. Rais Kikwete yuko katika ziara ya siku tatu ya kikazi Mkoani Mwanza.(picha na Freddy Maro)

  0 0

  Meneja Mwandamizi wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) Kanda ya Magharibi – Tabora Bw. Emmanuel Adina (kushoto) akifafanua jambo kwa Afisa Habari wa kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Jonas Kamaleki alipofanya mahojiahano naye kuhusu Mfuko wa Afya ya Jamii unavyo nufaisha Vijana wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Vijana inayofanyika Kitaifa Mkoani Tabora.
  Afisa Masoko na Elimu kwa Umma wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bibi Catherine Kameka akielezea jambo kuhusu Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwa wananchi walitembelea banda lao wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Vijana yanayofanyika Kitaifa Mkoani Tabora.
  Baadhi ya wananchi wakipata huduma ya upimaji wa Afya inayotolewa bure na Mfuko wa Taifa waBima ya Afya (NHIF) katika Maonyesho ya Wiki ya Vijana yanayoendelea mjini Tabora. 


  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakishiriki kuvuna majani ya chai, katika shamba la Uniliver, eneo la Ngwazi, katika wilaya ya Mufindi mkoani Iringa, leo Oktoba 10, 2014. Kinana yupo katika ziara ya mkoa huo, kukagua na kuhimiza utekelezaji wa ilani ya CCM. (Picha na Bashir Nkoromo).

  0 0

   Vitalu vya miche ya miti vinavyomilikiwa na Umoja wa Vikundi vya Kijamii wilaya ya Mufindi (UVIKIMU)
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kumwagia maji vitalu vya miche ya miti vinavyomilikiwa na Umoja wa Vikundi vya Kijamii wilaya ya Mufindi (UVIKIMU)
   Shamba la chai Ngwazi
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuchuma chai pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwenye shamba la chai Ngwazi wilaya ya Mufindi.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akichuma chai, ambapo alitaka wakulima wadogo pia wasaidiwe ili kufanikisha kilimo ch chai kwani chai ikisimamiwa vizuri itasaidia  kuinua uchumi wa nchi na kumpatia mkulima kipato kizuri.

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kulia),Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu (katikati) na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiwapungia mkono wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya mkutano Nyololo njia panda.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa Jimbo la Mufindi Kusini ambapo aliwaambia anawapongeza wapinzani kwa kukubali Katiba iliyopendekezwa na amesema kama walivyotangaza kuwa watashawishi wapiga kura wasiipigie basi na CCM itawashawishi wapiga kura waipigie .
   Mwenyekiti wa CCM Ndugu Jesca Msambatavangu akihutubia wananchi kwenye kiwanja cha mkutano Nyololo njia panda
   Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini Mendrad Kigola akiwahutubia wananchi wake wa kata ya Nyololo ambapo alisema maji bado hayajapatiwa ufumbuzi zinahitajika zaidi ya milioni 800 kutatua tatizo la maji.
   Hii gari ya aina yake ilikuwa kivutio kwenye mkutano.
   Wananchi wakisikiliza mkutano wakiwa juu ya uzio wa kiwanja cha Nyololo njia panda
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa pamoja na mtoto Meliko Mpevu,na Afisa wa Chama Makao Makuu Edward Mpogolo(watatu kutoka kulia) na wadau wengine wa CCM wilaya ya Mufindi wakifuatilia kwa makini mkutano unavyoendelea.
   Wananchi wakisikiliza kwa makini
   Wananchi wakishangilia hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa jimbo la Mufindi Kusini ambapo aliwaambia tabia ya kufanya kazi kwa mazoea kwa watumishi wengi wa serikali kumechangia sana kushusha nidhamu na kutofanya kazi kwa ufanisi ,Katibu Mkuu pia alisema kuwekwe utaratibu mzuri utakaopunguza malalamiko kwenye utoaji wa vibali vya kuvuna mbao,pia aliwaambia wananchi wa Mufindi kuwa vijiji 46 vitapata umeme ikiwa vijiji 35 vitapata kupitia mradi wa Umeme Vijijini (REA) na 11 vitapata kupitia mradi wa Mwenga Hydro.
   Josephat Sebadi Soda aliyekuwa Katibu wa Chadema kata ya Igowole akitangaza rasmi kurudi CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa mikutano Nyololo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambapo yeye pamoja na wenzake 27 wamerudi na kujiunga na CCM
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea kadi na bendera za Chadem kutoka kwa aliyekuwa Katibu wa Chadema kata ya Igowole  Josephat Sebadi Soda aliyeamua kujiunga na CCM.
   Zaidi ya wanachama wapya 485 wamejiunga na CCM wilaya ya Mufindi.
   Wanachama wapya wakila kiapo.
   Mzee alishindwa kuvumilia na kuamua kuyarudi
   Wasanii wa CCm Band Mufindi wakitoa burudani baada ya mkutano kumalizika.
   Wananchi wakiserebuka pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kumaliza mkutano .
   Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (katikati)na Katibu wa CCM wilaya ya Mufindi Miraji Mtaturu  (kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wasanii wa bendi  ya CCM Band Mufindi.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiangalia kasha la albamu ya bendi ya CCM Mufindi ambayo walizindua albamu inayokwenda kwa jina la ILANI.

  0 0

  Meneja wa POSO Kanda ya Ziwa Bw. Emmanuel Kisamba (kushoto) akitoamaelezo kwa mwananchi aliyetembelea banda la Kampuni ya GODTEC katika viwanja vya Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora ambapo Maonyesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa yanayofanyika mkoani humo kuelekea Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru na Kumbukumbu ya Miaka 15 ya Kifo cha Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Nyerere.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa PAFRI Bw. Boniphace Alex akitoa maelezo namna ya jiko lilotengenezwa na Kampuni yake linavyofanya kazi, kwa vijana waliotembelea banda la Kampuni ya GODTEC katika viwanja vya Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora ambapo Maonyesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa yanayofanyika mkoani humo kuelekea Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru na Kumbukumbu ya Miaka 15 ya Kifo cha Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Nyerere.Katikati ni Afisa Uhusiano wa Bega kwa Bega Microfinance Bibi. Dorcas David Mlapa na Afisa Mtendaji Mkuu wa PAFRI Bw. Boniphace Alex.
  Baadhi ya wafanyakazi wa GODTEC na Bega kwa Bega Microfince wakitoa huduma katika banda lao wakati wa Maonyesho katika viwanja vya Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora ambapo Maonyesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa yanayofanyika mkoani humo kuelekea Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru na Kumbukumbu ya Miaka 15 ya Kifo cha Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Nyerere. Picha na Frank Shija, Tabora

  0 0


  *Aridhishwa na ujenzi wa miundombinu, azindua majengo mapya  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema uamuzi wa Serikali wa kukopa fedha ili kuboresha miundombinu kwenye taasisi za elimu ya juu nchini ulichukuliwa kwa lengo la kujibu tatizo la sasa la wingi wa vijana wanaohitimu kidato cha sita.  Ametoa kauli hiyo jana usiku (Ijumaa, Oktoba 10, 2014) wakati akizungumza na wahadhiri, wakufunzi, wanafunzi na wanajumuiya ya Chuo Kikuu Huria (OUT) mara baada ya kuzindua jengo la ghorofa 10 linalojulikana kama Ghorofa la Elimu ya Masafa ya Huria (Open Distance Learning Tower – ODL Tower) lililogharimu sh. bilioni 3.  Waziri Mkuu ambaye aliwasili jijini Dar es Salaam jana mchana akitokea Morogoro, alitembelea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania ili kukagua utekelezaji wa mradi wa Sayansi na Teknolojia ya Elimu ya Juu (Science and Technology Higher Education Project - STHEP) unaoendeshwa chini ya uhisani wa Benki ya Dunia.  “Mradi huu ni wa miaka mitano ambao ulianza mwaka 2009 na unakamilika mwaka huu. Lengo hasa lilikuwa ni kujenga uwezo wa wataalamu wetu ambao watakuja kufundisha watoto wa kidato cha sita ambao idadi yao inazidi kuongezeka kila mwaka.”  Alisema Serikali iliridhia pia fedha hizo zitumike kujenga miundombinu mipya ya kufundishia pamoja na kukarabati baadhi ya zamani kwani kama miundombinu haipo, kazi ya kufundisha haitakuwepo.  “Tulikubaliana pia fedha hizo zinunue vifaa kwa maana ya kompyuta, vifaa vya maabara pamoja na samani za maktaba na baadhi ya madarasa. Ni fedha za mkopo lakini zimetumika kusaidia Watanzania wote.”  Chini ya uhisani wa mradi huo, Chuo Kikuu Huria kimesomesha wahadhiri 29 kati 12 ni masomo ya Uzamifu na 17 ni masomo ya uzamili. Pia kimejenga Maabara za kompyuta tatu, maktaba ya kuweka watu 224 kwa wakati mmoja, vyumba vya mihadhara (seminar rooms) maabara ya lugha (language lab), ununuzi wa kompyuta na samani.  Mapema akiwa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Waziri Mkuu alikagua majengo mapya ya ghorofa la shule kuu ya elimu, sayansi ya majini (Aquatic Sciences and Technologies), Multi Complex Building ambalo litakuwa na kituo cha wanafunzi, pamoja kuzindua jengo jipya la Uhandisi Migodi na Usindikaji Madini (Mining and Mineral Processing Building) lililopo kwenye Chuo cha Uhandisi na Teknolojia (College of Engineering Technology).  Akitoa taarifa ya miradi yote hiyo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Rwekaza Mukandala alisema katika awamu hii ya kwanza ya mradi wa STHEP, Chuo hicho kilifanikiwa kupata ufadhili wa Dola za Marekani milioni 40.79 (sawa na sh. bilioni 67).  Chini ya mradi huo, Prof. Mukandala alisema chuo kimefanikiwa kuendeleza kimasomo wafanyakazi wake zaidi ya 150, kujenga majengo mapya manane, kusomesha wahadhiri tarajiwa 163 ambapo 63 wamesoma shahada za umahiri (masters) na 67wamepata shahada za uzamivu (Ph.D).  “Tumeweza kununua vifaa mbalimbali vikiwemo vya maabara, kompyuta 864, vitabu zaidi ya 960, na vifaa vya teknolojia, uhandisi na sayansi. Pia tumeweza kupanua madarasa, maabara na ofisi .”  “Tumepata maabara mpya 49 zitakazokuwa zikitumiwa na wanafunzi 3,630 kwa wakati mmoja; madarasa 53 yenye uwezo wa kubeba wanafunzi 4,200 kwa wakati mmoja; ofisi 322 zitakatumiwa na wafanyakazi wasiopungua 600,” aliongeza.


  IMETOLEWA NA:

  OFISI YA WAZIRI MKUU,

  2 MTAA WA MAGOGONI,

  11410 – DAR ES SALAAM.

  JUMAMOSI, OKTOBA 11, 2014

  0 0

   Afisa Mahusiano wa PSPF Coleta Mnyamani kushoto Akimkabidhi Msaada wa Kompyuta Mkuu wa Chuo Kikuu teule cha Marian Father Luke Mbefo  ambapo Kompyuta hizo zitatumika katika Kuhifadhi Nyaraka mbalimbali za Maktaba
   
   Mkuu wa Chuo Kikuu teule cha Marian Father Luke Mbefo  kulia akimshukuru Afisa Mahusiano wa PSPF Bi. Coleta Mnyamani kwa msaada huo
   Mwakirishi wa Shirika la Roho Mtakatifu Father Nicetas Kyara akitoa neno la Shukurani Baada ya kukabidhiwa msaada wa Kompyuta Mbili za kisasa kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF
   Afisa Mahusiano wa PSPF Bi. Coleta Mnyamani akizungumza neno Baada ya kukabidhi Msaada huo
  Afisa wa Fedha kutoka PSPF Bwana Samwel Haule Akizungumza Jambo wakati wa Makabidhiano wa Kompyuta hizo katika Chuo Kikuu teule cha Marian
   Mkuu wa Chuo teule cha Marian Father Luke Mbefo wakiteta Jambo na Afisa Mahusiano wa Pspf Bi Coleta Haule Baada ya Kukabidhi Msaada huo
   Picha ya Pamoja ya Viongozi wa PSPF na Chuo  Kikuu teule cha Marian
  Kulia ni Meneja wa Pwani wa PSPF Msafiri S. Mugaka akimkabidhi Kompyuta 10 Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Ukutubi,Uhifadhi wa Kumbukumbu na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania Dkt. Ally S. Mcharazo kwa niaba ya chuo hicho
  Meneja wa Pwani wa PSPF Msafiri S. Mugaka  akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ukutubi,Uhifadhi wa Kumbukumbu pamoja na wagani waalikwa wakati wa kukabidhi msaada huo wa kompyuta 10 za kisasa
  Rais wa Chuo cha Chuo cha Ukutubi,Uhifadhi wa Kumbukumbu Daudi Joho akitoa neno la Asante Baadhi ya Kukabidhiwa Msaada huo 
  Mbele ni Maofisa wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF
  Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Ukutubi,Uhifadhi wa Kumbukumbu na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania Dkt. Ally S. Mcharazo  akitoa neno la Shukurani
   Baadhi ya wanafunzi wakisoma Vipeperushi vya PSPF
  Wanafunzi wakiwa wanafuatilia kwa makini
  Kila mtu anachukua Kumbukumbu


  Mfuko wa pensheni wa PSPF waendelea kukuza elimu ya Tehama katika vyuo mbalimbali hapa nchini kwa kutoa msaada wa jumla ya kompyuta 12 katika chuo cha Ukutubi Uhifadhi wa Nyaraka Bagamoyo na chuo Teule  ambacho kitakuwa kikiendeshwa chini ya saint augustine's university  (SAUTI) ambapo  kompyuta kumi (10) zimetolewa  katika chuo cha Ukutubi Uhifadhi wa Nyaraka na Mbili zimetolewa katika chuo teule cha cha Mariana university College vyote vilivyopo bagamoyo katika mkoa wa pwani.

  Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo afisa mahusiano wa PSPF Bi. Coletha Mnyamani amesema zoezi hilo limeanza lakin halitaishia hapo kwani ni zoezi endelevu kwani wameamua kusaidia jamii hususani kwa wanafunzi ilikuweza kuwajengea ujuzi katika masomo yao pamoja na kutunza nyaraka zao kisasa na sio katika makaratasi  kama ilivyo kuwa hapo zamani

  Kwaupande wake Meneja wa  Wa PSPF Mkoa wa Pwani  Bw.Msafiri S Mugaka amesema kuwa wameweza kutimiza ahadi waliyo ahidi kwa chuo cha Ukutubi Uhifadhi wa Nyaraka na kuweza kutoa msaada kwa chuo teule cha Mariana university College Hivyo wawaomba wananchi kuiamini na kuendelea kuwa wanafamilia wa mfuko huo wa pensheni

  Naye Mwenyekiti wa Baraza la chuo cha Ukutubi Uhifadhi wa Nyaraka na mkurugenzi wa wa Bodi ya Huduma za Maktaba –Tanzania Ally  Mcharazo kilichopo Bagamoyo wakati akipokea msaada huo kutoka kwa maafisa wa mfuko wa PSPF makao makuu Dar es saalam Amesea wanatoa shukrani kwa Mfuko huo kwani umeweza kuwasogeza katika huduma za kisasa kwa kuwapelekea kompyuta hizo nyaraka zote zitakuwa zikitunzwa katika hali iliyo salama na sio katika hali ya kizamani na kazi kuenda kwa haraka zaidi kwani kompyuta husaidia katika kuokoa muda kazini.

  Pia Bw.Samweli Haule ambaye ni afisa Wa Fedha Wa Mfuko Wa Pensheni wa PSPF Aliweza kutoa maneno ya kuwaasa wanafunzi kwa kuwa makini na wao hawata choka kutoa msaada pindi wanapo kuwa wamekwama ili kuweza kuwaweka wanafunzi wote katika hali ya kisasa zaidi

  Mkuu wa Chuo cha Mariana university College Father Luke Mbefo pia naye aliweza kushukuru Mfuko wa PSPF kwa kuona umuhimu wa kuweza kusaidia upande wa elimu kwa kuchangia kwa aina mbalimbali bila kuchoka na kuchagua rangi wala dini

  Hivyo Mfuko wa Pensheni PSPF Umetoa wito kwa wananchi  pamoja na vyuo mbalimbali kwakuwa wao wapo kwamoyo kwaajili ya wananchi na kuhakikisha kuweza kuikomboa elimu yetu kwa kuipelekea wepesi zaidi katika hali ya udigitali kuachana na analogia,kwani huop ni mwanzo tu mambo mengine yatafuata tena mazuri kutoka PSPFolder | 1 | .... | 384 | 385 | (Page 386) | 387 | 388 | .... | 1898 | newer