Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar apokelewa kwa shangwe

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeo (CHADEMA) - Zanzibar,Bw. Salumu Mwalimu (kulia) akikabidhiwa vifaa vya ofisi kutoka kwa mtangulizi wake,Bw. Hamad Yusuf (kushoto) wakati wa hafla ya kumkaribisha iliyofanyika kwenye ofisi za chama hicho Daraja bovu mjini,Zanzibar jana.Katikati ni Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeo (CHADEMA) - Zanzibar,Bw. Salumu Mwalimu akiongea kwenye mkutano wa ndani baada ya kuwasili kwenye ofisi za chama hicho Daraja bovu mjini Zanzibar jana.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa akiongea na wanachama na viongozi wa Chadema jana
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeo (CHADEMA) - Zanzibar,Bw. Salumu Mwalimu akipokewa na viongozi wa chama hicho baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Zanzibar akifuatana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk.Wilbrod Slaa (kulia) na viongozi wengine wa chama hicho jana.
Sehemu ya Wanachama na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeo (CHADEMA) wakiwa kwenye mapokezi ya Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Salumu Mwalimu baada ya kuwasili kwenye ofisi hiyo Darajabovu mjini Zanzibar jana.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa akiteta jambo na Manaibu wake,Mh. John Mnyika - Bara (kushoto) na Salumu Mwalimu - Zanzibar (kulia) kwenye mkutano na wanachama na viongozi wa chama hicho jana.
Wanachama na wapenzi wa Chadema wakimsikiliza Dk.Slaa alipozungumza nao kwenye ofisi za chama hicho huko Darajabovu mjini Zanzibar jana.

MAADHIMISHO SIKU YA POSTA DUNIANI YAFANA JIJINI DAR LEO

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Mkoma, akizungumza katika mkutano huo.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano,  Sayansi na Teknolojia, Profesa Patrick Makungu akihutubia katika uzinduzi huo. 
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano,  Sayansi na Teknolojia, Profesa Patrick Makungu (kushoto), akimkabidhi zawadi Mwalimu  Lucy Mshomi wa Shule ya Wasichana ya Kifungiro kutokana na mchango mkubwa kwa wanafunzi wao. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Posta, Deus Mndeme.


WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya St Mary's ya Mazinde Juu iliyopo mkoani Tanga wameibuka vinara wa shindano la uandishi wa barua lililoshirikisha wanafunzi wa shule mbalimbali nchini katika kuadhimisha siku ya posta duniani.

Shindano hilo la uandishi wa barua  limeratibiwa na Shirika la Posta Tanzania kwa kushirikiana na umoja wa posta duniani.
Akizungumza  Dar es saalam leo katika hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya posta duniani, Mkurugenzi Mkuu wa Posta nchini,  Deus Mdeme  alitoa pongezi kwa washindi hao na walimu wao kwa kufanikiwa kuibuka videdea ambapo mshindi wa kwanza ataiwakilisha Tanzania katika mashindano ya barua ya kimataifa yatakayofanyika baadaye mwaka huu nchini Uswisi.

"Madhumuni ya shindano hili ni kuwajengea uwezo vijana ambao hawajazidi miaka 15'' alisema Mdeme.

 Katika Shindano hilo la uandishi wa barua jumla ya washindi kumi walipatikana, huku St Mary Mazinde juu wakiibuka videdea kwa kutoa washindi wawili huku mshindi wa pili akitoka Shule ya Sekondari ya Lufingilo mkoani humo ambapo walikabidhiwa vyeti na zawadi mbalimbali.

Aidha katika kuadhimisha siku hiyo ya posta duniani, yenye kauli mbiu isemayo posta inachukua nafasi yake katika mageuzi ya sekta ya mawasiliano imeadhimishwa kwa kuelezea malengo na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Posta Tanzania.

Wakati huo huo Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Patrick Makungu kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo, Profesa Makame Mbarawa, alielezea mafanikio na changamoto mbalimbali zinazoikabili Sekta ya Posta Tanzania katika kufanikisha malengo yake.

Vilevile alitumia nafasi hiyo kuhamasisha wanafunzi wengi zaidi kushiriki katika shindano hilo linaloandaliwa na umoja wa posta duniani na kuwataka wadau wa posta nchini kushirikiana na shirika hilo ili likue na kutoa huduma kwa jamii baada ya kubadilisha ufumo wa utoaji huduza zake kwa kutumia zaida Tehama.

GREEN WASTE PRO LTD YAKABIDHI MAKASHA YA KUHIFADHIA TAKA SHULE YA MSINGI BUNGE

$
0
0
DSC_0093
Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Bunge Bi. Khadija Telela, akizungumza na Meneja wa uendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena aliyeambata na Afisa Rasilimali watu wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Naima Mpili (kulia) waliofika shuleni hapo kukabidhi rasmi makasha ya kuhifadhia taka.

KAMPUNI ya Usafi ya Green Waste Pro imetimiza ahadi yake ya kuipatia shule ya Msingi Bunge makasha ya kuhifadhia taka na vifaa vya usafi wa mazingira iliyoitoa mwaka jana.Mwaka jana wakati wanafanya shughuli ya kupaka rangi shule hiyo,kampuni hiyo ilifurahishwa na mazingira ya shule jinsi yanavyotunzwa kiasi cha kufanya maamuzi ya kuwapelekea vifaa vya mazingira na hasa makasha ya kuhifadhia taka.

Kwa mujibu wa Afisa uendeshaji wa kampuni hiyo Abdallah Mbena,ambaye ndiye aliyekabidhi makasha hayo,maamuzi ya kuwapatia makasha yametokana na jinsi klabu ya mazingira ya shule hiyo na mwalimu wao anavyochakarika katika kuhakikisha usafi wa mazingira katika shule hiyo.
Mbena alisema kwamba wamefarijika sana na juhudi zinazofanywa na mwalimu na wanafunzi wake katika kuhakikisha kwamba wanatunza mazingira.
DSC_0076
Meneja wa uendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena, akielezea nia ya kampuni yake kuendelea kusaidia shughuli mbalimbali za mazingira katika shule hiyo kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Bunge Bi. Khadija Telela (kushoto).

Pamoja na sababu za wanafunzi hao na mwalimu wao katika kutoa kipaumbele mazingira, kuwa chanzo cha kutolewa kwa makasha hayo, sababu nyingine iliyozingatiwa ni kuwa shule hiyo ipo katika kata ya Kivukoni ambapo kampuni hiyo inazabuni ya kufanya usafi.
Amesema wana mpango wa kuwapatia vifaa vya aina hiyo kwa shule nyingine zinazofanya vyema kwenye usafi wa mazingira ila kwa sasa wameanza na shule ya Bunge.

Mwalimu wa mazingira wa shule hiyo, Frida Madanganya ameshukuru kampuni hiyo kwa kuendelea kuwasaidia na anawategemea wataendelea zaidi kuhakikisha kwamba shule hiyo inakuwa namba moja kwa utunzaji wa mazingira. Naye Mwalimu Mkuu Khadija Telela alisema shule yake ina changamoto kubwa hasa maji ya Dawasco kwani maji yao ni yachumvi kwa kisima walichochimba. Alisema maji hayo yana chumvi lakini juhudi zinaendelea kupata maji ya Dawasco.


Aidha aliwataka wanafunzi waliosoma hapo kuikumbuka shule hiyo kwani wengi wana uwezo wa kuifanya iendelee kuwika.
DSC_0058
Mwalimu wa klabu ya mazingira wa shule ya msingi Bunge, Mwalimu Frida Madanganya akiwatembeza kukagua mazingira ya maeneo mbalimbali ya shule hiyo Meneja wa uendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena aliyeambatana na Afisa Rasilimali watu wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Naima Mpili kabla ya kukabidhi makasha hayo.
DSC_0046
Mwalimu wa klabu ya mazingira wa shule ya msingi Bunge, Mwl. Frida Madanganya akimtambulisha Meneja wa uendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena kwa wanachama wa klabu ya mazingira wa shule hiyo wakati wa hafla ya kukabidhi makasha ya kuhifadhia taka.
DSC_0053
Meneja wa uendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena akizungumza na wanafunzi wa klabu ya mazingira shule ya msingi Bunge na kuwahamasisha kuendelea kutunza mazingira yao na hata majumbani pia ili wawe mabalozi wazuri wa mazingira.
DSC_0024
Kaka Mkuu wa shule ya msingi Bunge na mwenyekiti wa klabu ya mazingira shuleni hapo Joseph Zakayo (kulia) akitoa shukrani kwa kampuni ya Green Waste Pro Ltd kwa kutoa msaada huo wa makasha matatu ya kuhifadhia taka. Kushoto ni Mwalimu wa klabu ya mazingira wa shule ya msingi Bunge, Mwl. Frida Madanganya akifuatiwa na Meneja wa uendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena aliyeambatana na Afisa Rasilimali watu wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Naima Mpili.
DSC_0062
Meneja wa uendeshaji wa kampuni ya usafi ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena akikabidhi rasmi moja kati ya makasha matatu ya kuhifadhia taka yaliyotolewa na kampuni hiyo kwa Mwalimu wa klabu ya mazingira wa shule ya msingi Bunge, Mwl. Frida Madanganya. Kulia ni Afisa Rasilimali watu wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Naima Mpili.
DSC_0003
Baadhi ya michoro iliyopo kwenye majengo ya shule ya msingi Bunge yanayohamasisha utunzaji wa mazingira kwa wanafunzi wa shule hiyo.
DSC_0102
Wanafunzi wa klabu ya mazingira shule ya msingi Bunge wakiagana na Meneja wa uendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena aliyeambatana na Afisa Rasilimali watu wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Naima Mpili.

Wizara ya Fedha ya kutana na uongozi wa Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC)

$
0
0

Dr. Servacius Likwelile Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali wakiwa pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakiusikiliza kwa makini ujumbe wa Mfuko wa Changamoto za Milenia. 4a 
Ujumbe wa Tanzania ukiwa katika kikao cha majadiliano pamoja na uongozi wa mfuko wa changamoto za Milenia Mjini Washington Dc.Balozi wa Tanzania nchini Marekani – Washington Mhe.Liberata Mulamula pamoja na aliyekuwa Balozi wa zamani wa ubalozi huo Bw. Ombeni Sefue wote walikuwepo katika mjadala huo.
5a 
Viongozi wa Mfuko wa Changamoto za Milenia wakimfurahia Katibu   Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue baada ya kumuona tena na kufurahi kwamba amekuja kujumuika na Watanzania wenzake katika kutafuta fedha za kuinua uchumi wa Tanzania.
6a 
Makamu wa Rais wa shughuli za operesheni za mfuko wa Changamoto za Milenia, Bw. Kamran Khan wa katikati akitoa maelezo na msimamo wa mfuko huo. Waliomzunguka ni wasaidiki wake ambao anafanya nao kazi kwa karibu..
7a 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr.Servacius Likwelile, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Balozi Liberata Mulamula pamoja na Bw. Laston Msongole ambaye ni Mtendaji Mkuu wa mfuko wa milenia wa awamu ya pili wakiusikiliza kwa makini ujumbe wa Mfuko wa Changamoto za Milenia na kutoa mawazo yao.
Picha zote na Ingiahedi Mduma- Wizara ya Fedha.
1a
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile akifurahia jambo na Mkuu wa mambo ya uchumi wa Mfuko wa changamoto za milenia. Wakiwa pamoja na Kamishna wa Fedha za Nje Bw. Saidi Ngosha Magonya.
2a 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile akifurahia jambo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue. Wakishuhudiwa na Bw. Abbas Abeid Missana Mwambata wa uhamiaji Ubalozi wa Marekani wakwanza kutoka kulia na Bw. Laston Msongole ambaye ni Mtendaji Mkuu wa mfuko wa milenia wa awamu ya pili wa mwisho kutoka kulia.

FLAVIANA MATATA KWA KATE SPADE

$
0
0
MWANAMITINDO FLAVIANA MATATA AKIWA KAZINI KATIKA KUTANGAZA BRAND NA DESIGNS ZA KAMPENI YA KATE SPADE SATURDAY photo 1photo 2photo 3photo 4photo 5f

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA YATINGA MUFINDI.

$
0
0
 
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akiwapungia mkono wananchi wa Mafinga wakati akiwasili kwenye uwanja wa Mashujaa .
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana na Bi.Mwigavillo Ngole ambaye amesafiri mwendo mrefu kuja kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM
 Wazee wa Kimila wakiwa uwanjani kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambapo walimpa Uchifu na kumtambua kwa jina la  Galiendela Matuga .
 Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mufindi Johanes Kaguo akifungua mkutano na kuhutubia wananchi wa Mafinga ambapo alielezea kero mbali mbali zinazowakabili wananchi wa Mafinga kwa Katibu Mkuu wa CCM.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mafinga na kuwaambia kuwa Mafinga hamna upinzani ila kuna manung'ung'uniko ya wananchi ambao hawapati taarifa za kina kuhusu masula yanayohusu ugawaji na upatikanaji wa vibali vya mbao.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu akihutubia wananchi wa Mafinga kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa
 Umati wa watu waliofurika kwenye uwanja wa Mashujaa Mafinga kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana

 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Mafinga wilaya ya Mufindi ambapo aliwaambia viongozi kuwa mstari wa mbele kusimamia haki na wajiepushe kuingia kwenye mambo ambayo yatasababisha kushindwa kuwatetea wananchi wao.
 Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mahamoud Mgimwa akihutubia wananchi wa Mafinga kwenye uwanja wa Mashujaa ambapo alisema waombaji wa vibali ni wengi kuliko uwezo wa serikali hivyo umeanzishwa utaratibu wa kila aliyepata kibali asiombe mara ya pili.
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akipitia taarifa mbali mbali zinazohusu wilaya ya Mufindi
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi hao ambapo aliwatajia vijiji vitakavyopata umeme ,maji na umuhimu wa kujiandikisha kwenye mfuko wa afya ya jamii.
 Wananchi wakifuatilia mkutano
 Kila mtu alikaa alipoweza kumuona Katibu Mkuu wa CCM Ndugu abdulrahman Kinana.
 Watu walikuwa mpaka kwenye ukuta wa uwanja wa Mashujaa kumsikiliza Kinana
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akimkabidhi kadi ya uanachama wa CCM Bi.Leah Msese ,zaidi ya watu 400 wamejiunga na CCM Mafinga.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Bi. Christiana Kiando wa kijiji cha Sao Hill baada ya kumaliza mkutano wa hadhara.

Nakaaya Ashusha Kitu Kipya Sokoni, Ni Katika Albam ya Blessing

$
0
0
Nakaaya Ashusha Kitu Kipya Sokoni, Ni Katika Albam Blessing Nakaaya Ashusha Kitu Kipya Sokoni, Ni Katika Albam Blessing.Nakaaya Ashusha Kitu Kipya Sokoni, Ni Katika Albam Blessing Nakaaya Ashusha Kitu Kipya Sokoni, Ni Katika Albam Blessing.Nakaaya Ashusha Kitu Kipya Sokoni, Ni Katika Albam Blessing Nakaaya Ashusha Kitu Kipya Sokoni, Ni Katika Albam BlessingNakaaya Ashusha Kitu Kipya Sokoni, Ni Katika Albam Blessing MSANII wa muziki wa kizazi kipya Nakaaya Sumari hivi karibuni alikonga nyoyo za mashabiki wake kwa kuzindua albam mpya iendayo kwa jina la Blessing yenye nyimbo kumi na mbili (12). Albam hiyo ambayo ni albam yake ya pili ilizinduliwa jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashabiki wa muziki wake kutoka mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro. Huku akiungwa mkono na wasanii wenzake kutoka hapa hapa nchini na nje ya nchi.

 Uzinduzi huo ulipambwa na burudani kabambe kutoka kwa Hisia, G Nako, Jambo squad wote kutoka Arusha, Naaziz kutoka Kenya, na Nakaaya mwenyewe  yote.hiyonikumpasapotimsaniimwanzao. Akizungumza kwa furaha mwanadada Nakaaya Sumari alisema kuwa anawashukuru sana wote waliokuja kumuunga mkono katika uzinduzi wake. “Nawashukuru sana mashabiki wangu kwa kunipa sapoti ya nguvu kwani wa lijitokeza kwa wingi, nimefurahi sana kwani huu ni mwanzo mzuri,” alisema Nakaaya. 

 “Albam hii imebebwa na wimbo wa Blessing ambao ni maalum kwa mwanangu kipenzi kwani yeye ni Baraka kwangu hata napokua mbali naye bado nakua na matumaini na faraja,” Nakaaya aliongeza kwa msisitizo. Albam ya Blessing ipo sokoni sasa na inanyimbo nzuri za kuelimisha, kuburudisha na kuliwaza kama vile Utu uzima dawa, Temana na watu, Blessing, Beautiful, I am an African, Sister sister, Ngufurie, na Mwanamke shujaa, kubwa ni kumpa sapoti kwa kununua albam hii.

LORRAINE ATUA NCHINI APONGEZA WATANZANIA

$
0
0
Lorraine akiwasili muda
Lorraine Clement akipungia watu waliofika kumlaki , alipokuwa akiwasili uwanja wa ndege JNI, alipokuwa akitokea nchini, Thailand, kushiriki mashindano ya Miss Grand International 2014, ambapo Lorraine aliibuka nafasi ya 20 bora.

Na Andrerw Chale
MWANADADA Lorraine Clement aliyeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya urembo ya kimataifa ya Miss Grand International 2014, na kufanikiwa kushika nafasi ya 20 bora katika shindano lililofanyika mjini, Bangkok, Thailand, ametua nchini jana Oktoba 9 majira ya saa 10 jioni na kuwashukuru watanzania kwa kumuunga mkono.

Akizungumza na wandishi wa habari muda mfupi alipowasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Jijini Dar es Salaam, Lorraine aliwashukuru wadau mbalimbali kwa kufanikisha ushiriki wake kwenye mashindano hayo makubwa duniani, ikiwemo kampuni ya Redline Communication Ltd, Iliyofanikisha mshiriki huyo kushiriki kwa mwaka huu.
“Pongezi kwa wadau wote mliofanikisha mimi kupeperusha vyema bendera ya Tanzania. Millen Magese kupitia kampuni yake ya MMG, Jacqueline Kibacha, Doreen Mashika, Husna Tandika na wengine wengi.
Lorraine Clement akishukuru
Lorraine Clement akishukuru Mungu, alipokuwa akiwasili uwanja wa ndege JNI, alipokuwa akitokea nchini, Thailand, kushiriki mashindano ya Miss Grand International 2014, ambapo Lorraine aliibuka nafasi ya 20 bora.

Katika mapokezi hayo, Lorraine alilakiwa pia na wazazi wake pamoja na mtendaji Mkuu wa Redline Communication, Abubakar Faraji ‘Abu’ na wadau wengine walijitokeza uwanjani hapo.Kwa upande wake, Mama Mzazi wa Lorraine, Paula David aliwashukuru watanzania kwa kumpigia kura mwanae na kupeperusha vyema bendera ya Tanzania.Hii ni kwa mara kwanza, mtanzania huyo anashiriki shindano hilo ambalo kwa hapa nchini linaendeshwa na kampuni ya Redline Communication Ltd, ambapo mshiriki wake huitwa ‘Miss Grand Tanzania’, kwa mwaka huu, Lorraine alikuwa ni mshindi wa pili kwenye shindano la Tanzania Top Models 2013.

Aidha, Katika shindano hilo, mwanadada, Daryanne Lees kutoka nchi ya Cuba, ndiye aliyetwaa taji hilo kwa mwaka huu. Wengine ni Miss Ethiopia, Hiwot Mamo na Miss Canada, Kathryn Kohut. Shindano hilo la Miss Grand International, kwa sasa ni msimu wa pili likifanyika nchini Thailand, tokea kuanzisha mwaka 2013. Mshindi wa mwaka huu, ameweza kunyakua kitita taslimu cha dola za kimarekani 40,000, pamoja na thamani za ndani.
Lorraine na meneja wake Abubar Faraj
Lorraine akilakiwa na meneja wake Abubakar Faraji.
Lorrainea kiwa na familia yake na mama yake (kulia)
Lorrainea kiwa na familia yake na mama yake (kulia).

MWENYEKITI WA CHADEMA ATAMBUA JUHUDI ZA KINANA

LEO NI SIKU YA MWISHO: Piga kura uboreshe maisha ya watu wenye ulemavu wa ngozi

$
0
0
Untitled
Shirika linalojibidisha na kutetea na kulinda watu wenye ulemavu wa ngozi nchini Under the Same Sun, (UTSS) limeteuliwa kushindania Tuzo ya Haki za Binadamu ijulikanayo kama “Tulip” itolewayo nchini Uholanzi. Iwapo UTSS watashinda tuzo hiyo, ni dhahiri kwamba kutakuwa na mapinduzi makubwa katika uboreshaji wa maisha ya watu wenye ulemavu wa ngozi. Shiriki kwa kupiga kura ili UTSS washinde Tuzo hii na kulinda ndugu zetu wenye Ulemavu wa Ngozi Tanzania kwa kupiga kura hapa chini na kusambambaza tarifa hizi kwa taasisi na watu mbalimbali.
Kwa kupiga kura hiyo bofya hapa

KAAZI KWELI KWELI

Mkutano wa kundi namba 1 la nchi za Afrika- Benki ya Dunia waendelea leo

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile akifuatilia kwa makini mkutano wa kundi namba 1 la nchi za Afrika- Benki ya Dunia ambao umefanyika leo hapa mjini Washington DC.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile akisoma nyaraka za mkutano wa kundi namba 1 la nchi za Afrika- Benki ya Dunia ambao umefanyika leo hapa mjini Washington DC.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile akisoma nyaraka za mkutano wa kundi namba 1 la nchi za Afrika- Benki ya Dunia ambao umefanyika leo hapa mjini Washington DC. Aliye kaa nyuma yake ni Kamishna wa Fedha za Nje Bw. Saidi Ngosha Magonya.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile akisoma nyaraka za mkutano wa kundi namba 1 la nchi za Afrika- Benki ya Dunia ambao umefanyika leo hapa mjini Washington DC. Picha zote na Ingiahedi Mduma- Wizara ya Fedha.

========   ==========
Mkutano wa kundi namba 1 la nchi za Afrika hufanyika kila mwaka wakati wa mikutani ya Benki ya Dunia na IMF na unahusisha kundi la nchi za Benki ya Dunia ambazo zinapata mikopo nafuu kutoka IDA. IDA ni shirika au mfuko wa maendeleo kwa ajili ya kutoa mikopo nafuu kwa nchi zinazoendelea kwa kundi la Benki ya Dunia.

Katika mikutano hii wanazungumzia zaidi masuala ya sera za kibenki na mambo ya utawala kama vile ajira , uchaguzi wa wenyeviti wa mikutano hiyo na kamati mbalimbali. Mkutano huo unaudhuriwa na Mawaziri wa Fedha. Kwa mwaka 2014 -16 Mwenyekiti atakuwa Waziri wa Fedha kutoka Ethiopia na Makamu wake anatoka Gambia. Viongozi hawa wataongoza mpaka mwaka 2016. Mwaziri wa Fedha ni Magavana na Matibu wakuu ni MaGavana mbadala, hivi ni vyeo vya uwakilishi kattika Benki ya Dunia.

Akiongea katika mkutano huo mwenyekiti aliyemaliza muda wake alisema kuwa”tumepata Mkurugenzi Mtendaji mpya wa kundi la kwanza la nchi za Afrika ambaye anatoka visiwa vya Shelisheli na Mbadala wake anatoka Zimbabwe “ alisema.

Akiendelea kuzungumza katika mkutano huo aliwaambia wajumbe kuwa anayemaliza muda wake anatoka Zambia na kuwa Viongozi hawa wanachaguliwa kwa kupigiwa kura na kila nchi. “Hawa watakuwa watendaji moja kwa moja kuanzia sasa na nafasi hizi zinapatikana kwa mzunguko.”alisisitiza.

Vilevile katika kundi hilo kutakuwa na kamati ya maendeleo ambayo itakuwa na mwenyekiti ambaye atatoka Uganda na wajumbe watatoka Tanzania, Namibia pamoja na Sierralion.

Jambo lingune ambalo limeongelewa kwenye mkutano huo muhimu ni kwamba Benki itaendelea kutoa misaada ya fedha kwa nchi zinazoendelea toka kwenye mfuko wa IDA kwa kuzingatia vipaumbele vya nchi husika.

Vilevile walisisistiza suala la gonjwa la EBOLA. Walielezea kuwa wataendelea kusaidia kupeleka misaada kwa nchi zinazokabiliwa na hilo tatizo. Pia Benki ya Dunia itaendelea kupeleka wafanyakazi kujifunza jinsi Benki ya Dunia inavyofanya kazi na kusisitiza kuwa ni muhimu kuchagua watu wazuri ambao wana uwezo ili wanaporudi nchini kwao waweze kutumia ujuzi wanao upata.

Mwisho walimalizia kwa kusema kuwa Benki itaendelea kusaidia jitihada ambazo zinalenga matokeo makubwa sasa kwani hata wao wanafanya kazi kwa kuzingatia matwakwa ya BRN. Hivyo wanatagemea fedha zinazotolewa zitafanikisha kuwa na matokeo makubwa sasa. Hali ya hewa mjini hapa ni baridi kiasi.

Halmashauri ya Geita kupata wastani wa Dola za Marekani milioni 1.8 kutoka GGM

$
0
0

Na Greyson Mwase, Dar es Salaam.

Halmashauri ya Geita  itaanza kupata  wastani wa  Dola za Marekani milioni 1.8 kwa mwaka  kutoka Mgodi wa  Dhahabu wa  Geita (GGM) baada ya kusainiwa rasmi kwa marekebisho ya mkataba  baina ya kampuni hiyo na Serikali.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo  kabla ya kutiliana saini marekebisho ya mkataba huo  ambao uliosainiwa  awali mwaka 1999. Awali, Halmashauri hiyo ilikuwa ikipata  ushuru wa huduma wa  Dola za Marekani  200,000 kila mwaka badala ya kulipwa  asilimia 0.3 ya mapato ghafi ya kila mwaka  kama sheria ya fedha ya serikali za mitaa ya mwaka 1982 inavyotaka.

Kwa kuzingatia kiwango cha mapato ghafi  ya mgodi wa Geita kwa mwaka yanayopatikana hivi sasa,  Halmashauri ya Geita itakuwa na uhakika wa kupata  kiasi kisichopungua  Dola za Marekani  milioni 1.8 kwa mwaka.

Kwa mujibu wa makubaliano  yaliyofikiwa  kati ya Serikali  na wamiliki wa mgodi huo, malipo hayo yataanza kulipwa  rasmi kuanzia tarehe 01 Julai, 2014.
Profesa Muhongo alisema kuwa fedha hizi ni nyingi mno  na kuwataka  wananchi wa Geita kujiandaa kwa ajili ya maendeleo ya miundombinu  pamoja na huduma za jamii  zitakazopelekea uchumi wake kukua kwa kasi.

Profesa Muhongo alisisitiza kuwa ni vyema makabidhiano ya  fedha hizo kwa njia ya hundi yakafanyika kwa uwazi mbele  ya wananchi ili kupunguza malalamiko, ikiwa ni pamoja na kuongeza imani kati ya wananchi na migodi.

Aidha, aliwataka Viongozi wa Halmashauri hiyo,   kusimamia vyema fedha hizo kwa kuhakikisha kuwa zinachangia katika shughuli za maendeleo badala ya kutumika katika matumizi yasiyo ya lazima na tija katika jamii, hususani kulipana posho  za vikao na safari.

“ Kwa mazingira ya sasa, mji wa Geita hauna sababu ya kukosa maji, barabara bora, vituo  vya afya, ni imani yangu kuwa fedha hizi zitachangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa uchumi wa Geita iwapo zitasimamiwa ipasavyo,” alisema.

Maeneo mengine yaliyofanyiwa  marekebisho  kwenye mkataba wa awali  uliosainiwa mwaka 1999 ni kupandisha kiwango  cha malipo ya mrabaha kutoka asilimia  tatu ya mapato baada ya kuondoa gharama za uchakataji madini na kufikia asilimia nne ya mapato ghafi.

Eneo jingine lililofanyiwa marekebisho ni kufuta kipengele kilichokuwa kinatoa nyongeza ya asilimia 15 kwenye mtaji wa uwekezaji ambao haujarejeshwa. Kuendelea kuwepo kwa kipengele hiki kwenye mkataba, kungeipunguzia serikali  kodi ya mapato.

NEW Video : Pam Daffa - Nimempata (Official Video) Ft. Mesen Selekta

Wadau wa Vijana washiriki mdahalo katika Wiki ya Vijana mkoani Tabora

$
0
0
Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Steven Kissuiakizungumza katika mdahalo wa vijana leo mkoani Tabora ambapo mdahalo huo umefanyika ikiwa ni kuadhimisha Wiki ya Vijana ambayo kitaifa inafanyika mkoani hapa.
Mchumi Mkuu Sekretariat ya Mkoa wa Tabora Bw.Nicholas Kileka akitoa mada kuhusu ijue Tabora leo mkoani humo wakati wa mdahalo uliohusisha vijana mbalimbali wanaoshiriki maadhimisho ya Wiki ya Vijana ambayo kitaifa yanafanyika mkoani humo.
Afisa Vijana Mwandamizi kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Florent Karist akitoa mada kuhusu maudhui ya Wiki ya Vijana leo mkoani humo wakati wa mdahalo uliohusisha vijana mbalimbali wanaoshiriki maadhimisho ya Wiki ya Vijana ambayo kitaifa yanafanyika mkoani humo.


WAZIRI MKUU AVUTIWA NA KASI YA MABADILIKO SOKOINE

$
0
0
*Maprofesa waomba kuongezewa muda wa kustaafu

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema amevutiwa na kasi ya mabadiliko katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) na hasa uanzishwaji wa kozi mpya zinazolenga uongezaji thamani wa mazao ya kilimo (Agri-processing).

Ametoa kauli hiyo jana jioni (Alhamisi, Oktoba 9, 2014) wakati akizungumza na wahadhiri, wakufunzi, wanafunzi na wanajumuiya ya SUA mara baada ya kutembelea chuo hicho na kukagua utekelezaji wa mradi wa Sayansi na Teknolojia ya Elimu ya Juu (Science and Technology Higher Education Project - STHEP).

“Nimefurahia sana hili suala la Agri-processing kwa sababu hivi tuna mzigo mkubwa unaoisumbua Serikali nao ni namna ya kununua mazao ya wakulima. Tuna ziada ya tani milioni 1.5 za mahindi na tani laki nane za mpunga wakati uwezo wa NFRA ni kununua tani 240,000 tu. Haya ni matokeo ya wahitimu waliotoka SUA na kupelekwa wilayani na vijijini wakahimiza kilimo bora kwa wananchi,” alifafanua.

Waziri Mkuu ambaye aliwasili Morogoro jana mchana akitokea Dodoma, alifanya ziara ya siku kwa kutembelea Chuo Kikuu hicho pamoja na kiwanda cha kutengeneza nguo cha 21stCentury.

Akiwa chuoni hapo, Waziri Mkuu alikagua majengo matatu yaliyojengwa chini ya mradi wa STHEP na kuzindua mawili kati ya hayo, alitembelea maabara za upimaji ubora wa vyakula na kisha kuzungumza na wanaSUA.

Akizungumza na wanajumuiya hao, Waziri Mkuu aliwataka wawe ni viongozi wa mfano kwa kumiliki walau ekari moja ya shamba, walime au kuweka mifugo ili yale wanayofundisha darasani yaonekane kwa vitendo katika mashamba hayo.

“Tatizo la sasa hivi miongoni mwa wasomi wengi ni kudhani kwamba kazi ya kilimo ni ya watu wa hali ya chini lakini wakifika mezani wao ndiyo wa kwanza kudai ubwabwa na kuku. Sisi wenye upeo ndiyo tunapaswa tuonyeshe njia na mashamba au mifugo yetu yawe ni ya mfano kwa wengine,” alisema.

Mapema,akiwasilisha taarifa ya mradi wa STHEP, Profesa Gerald Monella alisema mradi huo wenye thamani ya dola za Marekani milioni 7.48 (sawa na sh. milioni 12.5/-) umekisaidia chuo hicho kupata majengo manne yenye kati ya ghorofa moja na mbili, ambayo yameongeza nafasi za kufundishia wanafunzi, vyumba vya maabara na vifaa vyake, kuanzisha mitaala miwili pamoja na kusomesha walimu 21.

Kwa kutumia majengo hayo, Chuo kinaweza kufundisha wanafunzi 807 kwa wakati mmoja ambayo ni sawa na wanafunzi 10,565 kwa wiki moja. Chuo hicho pia kimeweza kupata vifaa vya maabara vyenye thamani ya dola za marekani milioni 1.71 ambavyo vimenunuliwa na kufungwa kwenye maabara hizo.

“Kwa upande wa elimu ya juu, mradi umeweza kusomesha walimu 21, miongoni mwao 11 wakiwa ni wa shahada ya uzamivu (PhD) na 10 ni wa shahada za uzamili (Masters’).

Aliiomba Serikali iongeze muda wa kustaafu kwa wahadhiri wa vyuo vikuu kwani wanapozeeka ndiyo wanapata muda wa kufanya tafiti zaidi. “Fani nyingie watumishi wanastaafu wakiwa na miaka 60 au zaidi, nasi tunaomba tuongezewe muda badala ya kutumia mfumo wa sasa wa kuongezewa miaka miwili miwili halafu mmoja,” alisema.

Naye, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho, Mama Kate Kamba wakati akitoa salamu za shukrani kwa Waziri Mkuu, alisema Serikali iangalie uwezekano wa kuongeza bajeti ya Chuo kwani kinahitaji fedha zaidi kwa ajili ya kufanya tafiti na kuboresha miundombinu.

“Tunahitaji fedha za kufanya tafiti zaidi, fedha za kuboresha miundombinu ya kufundishia ili tuweze kwenda sambamba na azma ya Serikali ya kuimarisha viwanda vya usindikaji mazao ya kilimo, uvuvi na mifugo,” alisema.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
11410 – DAR ES SALAAM.
IJUMAA, OKTOBA 10, 2014

WAZIRI MKUU AKAGUA TIMU ZA VIONGOZI WA DINI

$
0
0
 *Ataka Watanzania wajitokeze kwa wingi Oktoba 12

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewataka Watanzania wajitokeze kwa wingi kushangilia mechi ya viongozi wa dini wa mkoa wa Dar es Salaam itakayochezwa Jumapili, Oktoba 12, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Ametoa kauli hiyo leo asubuhi (Ijumaa, Oktoba 10, 2014) wakati akizungumza na wachezaji wa timu za AMANI na MSHIKAMANO zinazoundwa na Masheikh, Maaskofu, Maimamu na Wachungaji kutoka madhehebu mbalimbali ya mkoa wa Dar es Salaam ambao wamepiga kambi mjini Morogoro.

“Hii haijapata kutokea… katika hali ya kawaida mkusanyiko kama huu siyo rahisi na katika nchi nyingine kupata mjumuiko kama huu haiwezekani,” alisema wakati akiongea nao kwenye viwanja vya michezo vya taasisi ya Highlands Baptist Mission iliyoko Kigurunyembe, Morogoro.

Alisema uamuzi wa viongozi wa dini kukaa pamoja na kucheza mechi hiyo ni kutaka kuonyesha dhamira ya kweli ya kufanya mshikamano na amani kuwa ajenda ya kudumu kwa Taifa hili.

“Mimi ninaamini kinachotuunganisha siyo dini bali ni kutambua kwamba sisi sote tumeumbwa na Mungu… sisi sote ni bin-adam. Dini ni milango tu ya kutusaidia tufike kule ambako Mwenyezi Mungu anataka tuende,” alisema.

“Ukichukulia mfano wa wakristo, kuna madhehebu mengi. Kwa hiyo hawa wakigombana tayari ni tatizo. Hivyo uamuzi wa kuwachanganya katika timu ni jambo zuri, ni kudumisha umoja, amani na mshikamano,” aliongeza.

“Hii ni hatua ya kwanza kinachofuata sasa ni kuwa na One Destiny, One People, One Nation,” akimaanisha kuwa na Lengo Moja, Watu Wamoja na Taifa Moja. Alisema hiyo ni kama sura ya kwanza imefunguliwa hivyo, hawana budi kuendelea mbele.

Mapema, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Saleem alimweleza Waziri Mkuu kwamba timu hizo ziko kambini hapo tangu Jumatano, Mei 8, 2014. Alisema leo baada ya mazoezi watakwenda kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mikumi na kurejea kambini Morogoro. Wanatarajia kurejea jijini Dar es Salaam kesho (Jumamosi) tayari kwa pambano lao la Jumapili, Oktoba 12, 2014.

Waziri Mkuu ambaye aliwasili Morogoro jana mchana akitokea Dodoma, alifanya ziara ya siku kwa kutembelea Chuo Kikuu cha Sokoine na leo atatembelea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu Huria kukagua miradi kama hiyo.

 (mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
11410 – DAR ES SALAAM.
IJUMAA, OKTOBA 10, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI HAFLA YA CHAKULA CHA JIONI CHA HISANI KUCHANGIA MFUKO WA KAMPENI WA JITOLEE KWA AJILI YA KINAMAMA WA AFRIKA, JIJINI DAR.

$
0
0
 Makamua wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya Chakula cha Hisani kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Kampeni ya Jitolee kwa ajili ya Akinamama wa Afrika, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jana usiku Oktoba 9, 2014 jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Mkurugenzi Mtendaji wa Push Mobile, Freddie Manento, wakati wa hafla ya Chakula cha Hisani kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Kampeni ya Jitolee kwa ajili ya Akinamama wa Afrika, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, jana usiku Oktoba 9, 2014.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Mkurugenzi Mtendaji wa ITV na Redio One, Joyce Mhavile, wakati wa hafla ya Chakula cha Hisani kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Kampeni ya Jitolee kwa ajili ya Akinamama wa Afrika, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, jana usiku Oktoba 9, 2014.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Meneja Masoko Msaidizi wa Kampuni ya TOYOTA Tanzania, Eliavera Timoth, wakati wa hafla ya Chakula cha Hisani kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Kampeni ya Jitolee kwa ajili ya Akinamama wa Afrika, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, jana usiku Oktoba 9, 2014.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa meza kuu na baadhi ya viongozi wakati wa hafla hiyo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa  mradi wa Uzazi Uzima, Dkt. Benatus Sambili (wa pili kushoto) wakati alipokuwa akielezeewa kuhusu miradi inayosimamiwa na Amref Afrika, katika hafla ya Chakula cha Hisani kilichoandaliwa kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana usiku kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Kampeni ya Jitolee kwa ajili ya Akinamama wa Afrika.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa  Mpango wa Kujenga Uwezo katika mradi wa Uzazi Uzima wa Amref, Dkt. Pius Chaya (kushoto) wakati alipokuwa akielezeewa kuhusu miradi inayosimamiwa na Amref Afrika, katika hafla ya Chakula cha Hisani kilichoandaliwa kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana usiku kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Kampeni ya Jitolee kwa ajili ya Akinamama wa Afrika. Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Amref Health Afrika, Dkt. Festus Ilako
  Baadhi ya wadau, wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo. 14 na 15: Baadhi ya kinamama wakiserebuka kucheza muziki maalum unaomtukuza mama, wakati wa hafla hiyo.
 

JAMBAZI SUGU LILILOKUA LIKIUWA WANAWAKE ARUSHA LAUWAWA NA POLISI WANANCHI WASHANGILIA

$
0
0
picha ya juu na chini  wananchi wa jiji la Arusha  waliojitokeza kuuangalia mwili wa  jambazi huyo atari aliowawa na polisi usiku wa kuamkia leo.
 wananchi wakiendelea kushuhudia mwili wa jambazi hilo nje ya jengo la makao makuu ya polisi mkoani Arusha.


 baadhi ya vitu vilivyokutwa kwa jambazi hilo zikiwemo silaha mbalimbali
 kamanda wa polisi akionyesha moja ya kifaa cha kufanyia tageti kabla ya kupiga kijulikanacho kwa jina la Glock Fab Defence moja ambacho jambazi hilo lilikuwa likitumia.

Jambazi mmoja aliefahamika kwa jina la Ramathan Abudallah  alimaarufu kwa jina la Ramadhani Ndonga (37) mkazi wa  Moivo  ameuwawa baada ya kupigwa risasi katika majibizano na askari  wa jeshi la polisi.

Akizungumzia tukio hilo kamanda wa polisi mkoani Arusha Liberatus Sabas Alisema kuwa tukio hilo limetokea October 10  mwaka huu majira ya saa nane na dakika nne usiku   katika  kijiji cha  Moivo  kilichopo ndani ya kitongoji cha  Enaboishu wilayani Arumeru.

Alisema kuwa marehemu  Ramadhan Abdallh  aliuwa anatafutwa kwa muda mrefu na jeshi la polisi kwa kuhusika na matukio mbalimbali ya uhalifu ambayo yameshawahi kutokea ndani ya  mkoa huu pamoja na katika maeneo mbalimbali ya nchi hiii.

Alibainisha  kuwa kuuwawa kwa jambazi hili kumetokana na  juhudi na kutumia mbinu za kisasa za kiyupelelezi na kufika  nyumbani kwa mtuhumiwa (marehemu) ambapo askari polisi walimwamuru  ajisalimishe lakini alikaidi amri na kuanza kuwarushia risasi hali ambayo ilisababisha askari kujibu mashambulizi na kumsababishia  umauti kumfika.

“Mara baada yakupiga jambazi huyo polisi walianza kumpekuwa  mwili wa marehemu na alipatiana akiwa ba bastola aina ya Glock 19 yenye namba RLU976 iliotengenezwa nchini Austria ikiwa na magazine yenye risasi (14) ambapo alikuwa ameishika mkononi pamoja na maganda matano yarisasi  na  mbali na hapo polisi pia  walifanya upekuzi katika chumba cha jambazi hilo na kukuta magazine ingine moja yenye risasi (15) na magazine zingine mbili zenye uwezo wa kubeba risasi thelathini kila moja ,Radio call moja  yeye nembo ya ITSS/UNICTR  pamoja na pikipiki aina ya toyo power king rangi nyekundu yenye namba za usajili T507 BSU  pamoja na kofia ngumu”alisema Sabas

Aidha alibainisha kuwa  pia katika upekuzi huo wa ndani ya nyumba ya jambazi hilo pia walifanikiwa kupata pingu moja ,plate namba ingine ya pikipiki yenye namba za usajili T 805 CVD  ambapo alibainisha kuwa jambazi hili lilikuwa likibadilisha plate namba ya pikipiki kila mara  pamoja na  chomba maalumu cha kuwekea magazine pamoja na kufanyia tageti kabla yakupiga risasi (Glock Fab Defence moja),kifaa cha kusafishia bastola pamoja na koti kubwa jeusi.

Kamanda Sabas alitaja baadhi ya matukio ambayo jambazi hili lilishayafanya  kuwa ni pamoja na tukio  lililotekea Augast 6  majira ya saa tatu na nusu usiku maeneo ya kwa iddi ambapo mtuhumiwa  akiwa na mwenzake ambaye ajakamatwa walimpiga risasi ya shingo mwanamke aliyefahamika kwa jina la Shamimu Rashid aliyekuwa mkazi wa sakina wakati akijiandaa kuingina nyumbani kwake  ,hu ku tukio lingine likiwa limetokea Augast 21 saa 19:00 maeneo yaoasiti ambapo jambazi huyo akiwa na mwenzake kwenye pikipiki walimjeruhi kwa kumpiga risasi yam domo na kutokea kichwani  mototo aitwaye Christen NIckson mwenye umri wa miaka mitatu na nusu na kisha kufanikiwa kumpora TSH 2000 na baadae majeruhi kufariki dunia akiwa anapatiwa matibabu.

Kamanda sabas alitumia nafasi hiyo kuwapongeza askari wake kwa kufanya kazi nzuri pamoja na kuwahaidi wananchi kuendelea kufanya uchunguzi na kuwabaini wahalifu wote na kuwachukulia sheria kali.

“arusha sio sehemu ya kuifadhi wahalifu ivyo tutajitaidi kwa hali na mali kuhakikisha tunawamaliza majambazi wote pamoja na wahalifu wote na napenda kuwaaambia wahalifu waache mapema maana sasa ivi tumejipanga vilivyo ,pia napenda kuchukuwa nafasi hii kuwaomba wananchi pia waendelee kuwafichua wahalifu  popote pale ili tuwaangamize kabisa”alisema Sabas

Mmoja wa wananchi ambaye alijitokeza kushuhudia maiti ya jambazi hilo Aliyejitambulisha kwa jina la Alaija Saro akiongea na libeneke blog hili alilipongeza jeshi  la polisi kwa kuweza kumuangamiza jambazi hilo kwani limekuwa likiwatia mashaka watu wengi na kuwanyima raha kwa jinsi walivyokuwa wanauwa watu.

habari picha kwa hisani ya woindeshizza blog

Benki ya CRDB yaadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja

$
0
0
Meneja  wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyu (kushoto) akiwa na Meneja wa tawi la Meru, Loiyce Kapaliswa wakimkabidhi msaada Mwenyekiti wa Kituo cha kusaidia Wazee Arusha, Mzee Ngonyani  ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma  Wateja. Kulia ni Ofisa wa Benki ya CRDB, Pamela.

Wafanyakazi wa benki ya CRDB tawi la moshi. Wakikata keki kama maadhimo ya Wiki ya Wateja wa Benki ya CRDB.


Meneja Uhusiano wa Akaunti ya Tanzaniteya Benki ya CRDB, Lucy Naivasha  akiwapa Champagnewateja wa Benki hiyo wa tawi la UDSM wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Wateja.
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Babati, Ronald Paul (kushoto) akibadilishana mawazo na wateja.


Meneja wa tawi la Usa iver Jeneffer Tondi kigonga cheers na wateja katika maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa Wateja.

Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images