Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 382 | 383 | (Page 384) | 385 | 386 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Na Anitha Jonas –Maelezo.

  SHIRIKISHO la Muziki Tanzania limetoa pongezi za dhati kwa Bunge Maalum  la Katiba lililokuwa likiongozwa na Mwenyekiti wa Bunge hilo Mhe. Samuel Sitta kwa kuingiza Ibara tatu katika Rasimu ya Katiba inayopendekezwa huko mjini Dodoma.

  Pongezi hizo zilitolewa jana na Rais wa Shirikisho hilo Bw. Addo November alipokuwa akiongea na Waandishi wa habari hapo jana huku akisema kuwa Rasimu Inayopendekezwa imezingatia haki za Wasanii kwa kuingiza Ibara tatu zikiwemo Ibara ya 15, ya 38 (II)  na Ibara ya 56, 3 (e) ambazo Ibara hizo zinalinda kazi za muziki na sanaa zote kwa ujumla.

  Bw. November alieleza kuwa Shirikisho limefurahi kuona kuwa Sheria ya inayohusu masuala ya kazi za sanaa katika nchini imeanza kutekelezwa Kikatiba kama ilivyo katika nchi mbalimbali zikiwemo Marekani, Rwanda na Uingereza.

  “Kwa kubainisha ibara hizi katika Rasimu ya Katiba Inayopendekezwa, zinaonyesha ulindaji wa Hati Miliki (Intellectual property) za Wasanii na kazi zao na hii itasaidia kuboresha maisha ya wasanii  kimapato kwa kupitia  kazi zao kwani Katiba hii itawalinda wasanii Kisheria”, alisema November.

  Aliongeza kuwa Shirikisho limeingia Mkataba na Kampuni ya JB Belmont kwa kuweza kuwapatia wasanii na waandishi wa habari punguzo la bei katika huduma  mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo.

  Aidha, November aliwashauri waandishi wa habari kuunda Shirikisho la Waandishi wa habari la muziki kwani hii itasaidia kupata na kutoa taarifa mbalimbali kwa jamii zinazohusu masuala ya muziki kwa kuaangalia walikotoka na wanakoelekea kimaendeleo.
   
  Naye Meneja Mahusiano wa Kampuni ya JB Belmont, Bi. Gillian Macheche alisema kuwa kutakuwa na punguzo la asilimia 40 kwa huduma mbalimbali ikiwemo kukodi Ukumbi wa Mkutano, Vyumba vya kulala wageni, vyakula na Vinywaji kwa wasanii na waandishi wa habari.

  Kwa upande mwingine Mjumbe wa Shirikisho hilo ambaye pia ni Mwanamuziki mkongwe nchini Bw. Kassim Mapili alitoa shukrani zake za dhati kwa waandishi  wa habari kwa kutoa taarifa kwa umma  juu ya afya yake pamoja na jamii kwa ujumla kwa kumsaidia katika kipindi chote alichokuwa akitibiwa ugonjwa wa Moyo katika Hospitali ya Taifa  Muhimbili.

  0 0

  Mkurugenzi wa Kampuni ya Rino International Agency ambao ni waratibu wakuu wa Mashindano ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga (kulia) akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leo,juu ya onyesho la Redd's Miss Tanzania 2014 linalotarajiwa kufanyika Oktoba 11,2014 katika Ukumbi wa Mlimani City,Jijini Dar.Katikati ni Meneja wa Kinywaji cha Redd's ambao ni Wadhamini Wakuu wa Mashindano hayo,Victoria Kimaro na kushoto ni Meneja Maria Stopes Tanzania,Anna Shanalingigwa.Picha zote na Othman Michuzi.
  Meneja wa Kinywaji cha Redd's ambao ni Wadhamini Wakuu wa Mashindano ya Miss Tanzania,Victoria Kimaro (kushoto) akizungumzia zawadi watakayotoa kwa Washindi watakaopatikana kwenye Shindano hilo la Redd's Miss Tanzania 2014,ambapo mwaka huu mshindi wa kwanza katika kinyang'anyiro hicho atajinyakulia kitita cha sh. Mil. 18 taslim huku washindi wengine wakiendelea kuondoka na zawadi mbali mbali.Katikati ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Rino International Agency ambao ni waratibu wakuu wa Mashindano ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga na kulia ni Meneja wa Hoteli ya JB Belmont,Gillian Macheche pamoja na Afisa Habari wa Miss Tanzania,Hidan Ricco.
  Sehemu ya Wanahabari pamoja na Warembo watakaoshiriki kwenye kinyang'anyiro cha Redd's Miss Tanzania 2014 wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Kampuni ya Rino International Agency ambao ni waratibu wakuu wa Mashindano ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga alipokuwa akizungumza.
  Sehemu ya Warembo watakaoshiriki kwenye kinyang'anyiro cha Redd's Miss Tanzania 2014 
  Warembo watakaoshiriki kwenye kinyang'anyiro cha Redd's Miss Tanzania 2014 wakipata "SELFIE" mwanana kabisa.

  0 0  Na Mwene Said,Globu ya Jamii

  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu,jijini Dar es Salaam, jana iliamuru mashindano ya urembo Tanzania yaliyopangwa kufanyika Oktoba 11, mwaka huu kuendelea baada ya kutupilia mbali maombi ya dharura yaliyowasilishwa na Prashant Patel dhidi ya Hashimu Lundenga ya kuzuia kuendelea kuendesha kinyang'anyiro hicho kwa madai ya kukiuka mkataba wa makubaliano yao.

  Kadhalika mahakama hiyo imesema maombi ya hati ya dharura yaliyowasilishwa na Patel hayana mashiko ya kisheria na kwamba kuzuia kufanyika mashindano hayo ambayo wadhamini mbalimbali wamewekeza fedha zao itasababisha mgangano wa kimaslahi.

  Uamuzi huo ulitolewa jana na Hakimu Mkazi Frank Moshi  baada ya kusikiliza hoja za mawakili wa pande zote mbili kuhusu maombi hayo ya dharura ya kuzuia mashindano hayo kufanyika Oktoba 11, mwaka huu.

  Hakimu Moshi alisema mlalamikaji amefungua kesi mahakamani hapo pamoja na maombi ya hati ya dharura akiitaka mahakama yake kuzuia mashindano kufanyika kutokana na mlalamikiwa kuvunja haki dhidi ya mwanzilishi mwenzake Patel.

  Alisema Patel kupitia hoja za maombi yake, amedai kuwa Lundenga alivunja mkataba huo kwa kufanya mawasiliano moja kwa moja na mawakala bila kumshirikisha.

  Hata hivyo, mahakama bila kuacha shaka imeona hakuna sababu za msingi katika hati hiyo ya kusababisha mashindano hayo yasifanyike na kwamba hayawezi kuathiri kesi ya msingi iliyofunguliwa na mlalamikaji huyo.

  “Mahakama imeona hakuna sababu ya kuzuia mashindano hayo kwa sababu wadhamini na washiriki wametumia gharama zao na kwamba kwa kufanya hivyo kutasababisha mgongano wa kimaslahi” alisema Hakimu Moshi wakati akitupilia mbali hati hiyo ya dharula.

  Akifafanua zaidi alisema hati ya dharura ya mlalamikaji haina mashiko kisheria kwa sababu kesi yake ya msingi ipo mahakamani na kwamba haina uhusiano na mashindano yatakayofanyika Oktoba 11, mwaka huu.

  Mapema juzi, mahakama hiyo ilitupilia mbali pingamizi la awali la Lundenga lililotaka hati hiyo ya dharura kutupilia mbali.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko Vicent Kone
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko Vicent Kone.
  Katibu Tawala Mkoa wa Singida Bw. Liana Hassan.
  Katibu Tawala Mkoa wa Singida Bw. Liana Hassan.
  Jengo la OPD katika Hospitali Mpya ya rufaa ya Mkoa wa Singida.
  Jengo la OPD katika Hospitali Mpya ya rufaa ya Mkoa wa Singida.
  Jengo la utambuzi wa Magonjwa katika Hospitali Mpya ya rufaa ya Mkoa wa Singida.
  Jengo la utambuzi wa Magonjwa katika Hospitali Mpya ya rufaa ya Mkoa wa Singida.

  0 0

  Aina hii Malware inayojulikana kama Tyupkin yaleta maafa katika mashine za ATM. Tyupkin imekua ikisambazwa na kundi la wahalifu mtandao kutokea ulaya mashariki na kusababisha pesa nyingi kuweza kutoka kupitia ATM mashine ambapo tayari wataalam wa usalama mitandao kutoka Kaspersky Lab wakishirikiana karibu na polisi wasio na mipaka “Interpol” wamesha anza oparesheni ya pamoja kutafuta chanzo na ugunduzi katika mashine 50 umebainika hadi sasa.

  0 0

  Kamati ya Waamuzi wa mchezo wa kuvuta kamba ikisubiri kumkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (hayupo pichani) aliyetembelea viwanja vya Jamhuri,Morogoro mapema leo kushuhudia michezo ya kuvuta kamba.
  Mwamuzi wa mchezo wa kamba Bw.Ruvu Kiwanga (kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil alipotembelea viwanja vya Jamhuri, Morogoro mapema leo.

  Na Happiness Shayo,Morogoro

  Timu za kamba za Ikulu, Hazina na Mahakama zimeingia hatua ya nusu fainali kwa kishindo baada ya kuzivuta timu pinzani katika michezo ya SHIMIWI iliyofanyika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro leo.

  Michezo hiyo ya kusisimua iliyovuta mashabiki wengi ilianza majira ya saa moja asubuhi ambapo timu ya kamba ya wanawake ya Ikulu iliivuta timu ya kamba ya wanawake ya Kilimo na kuibuka mshindi kwa kuvuta mivuto yote miwili.

  Mchezo wa pili ulikuwa kati ya timu ya kamba ya wanawake ya Wizara ya Ujenzi na timu ya kamba ya wanawake ya Wizara ya Uchukuzi zilizolazimishana kutoka droo kwa michezo miwili ya kwanza na hatimaye Uchukuzi kuibuka mshindi kwa mvuto mmoja baada ya kuvutana kwa mara ya tatu.

  Katika mchezo mwingine timu ya kamba ya wanawake ya Wizara ya Mambo ya Ndani ililazimishana droo na timu ya wanawake ya RAS Iringa na kulazimu waamuzi kurudia mchezo huo na hatimaye RAS Iringa kuibuka mshindi kwa kuwa na pointi 1-0.

  Mchezo mwingine ulichezwa kati ya timu ya kamba ya wanawake ya TAMISEMI ikiivuta timu ya wanawake ya Mahakama kwa mvuto mmoja.

  Kwa upande wa timu za kamba za wanaume,Ikulu iliibuka mshindi baada ya kuivuta timu ya NFRA huku Uchukuzi ikiibuka mshindi baada ya kuivuta timu ya Afya kwa mivuto yote miwili.

  Timu nyingine zilizoingia dimbani kwa upande wa timu za wanaume ni timu ya kamba ya Mahakama iliyoivuta timu ya Wizara ya Mambo ya Ndani na kuibuka na pointi 2 huku timu ya kamba ya Hazina ikiivuta timu ya kamba ya Maliasili na kuibuka na pointi 2.

  Timu za kamba kwa wanawake na wanaume leo zimetoana katika hatua ya robo fainali ambapo washindi wataingia nusu fainali itakayochezwa hapo kesho.  0 0

  Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo akitoa taarifa ya mfumuko wa bei nchini kwa mwezi Septemba, 2014 leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Meneja wa Takwimu za Ajira na Bei wa Ofisi hiyo Bi. Ruth Minja.
  =======  ======  ======= 
  Na. Aron Msigwa-MAELEZO.
  Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Septemba 2014 umepungua hadi kufikia asilimia 6.6 kutoka asilimia 6.7 iliyokuwepo mwezi Agosti kutokana na kupungua kwa bei ya bidhaa na huduma katika maeneo mbalimbali nchini.
  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraim Kwesigabo amesema kuwa bidhaa za vyakula zikiwemo  mchele, mahindi, ulezi, matunda, Sukari  na vinywaji baridi zimechangia kupungua kwa mfumuko wa bei nchini
  Bidhaa nyingine zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei nchini ni Sare za shule, Simu za mkononi, runinga na viatu huku akibainisha kuwa Fahirisi za bei kwa maana ya kipimo kinachotumika kupima mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zinazotumiwa na kaya nchini zimeongeka na kufikia  149.93 kwa mwezi Septemba 2014 ikilinganishwa na 140.61 za mwezi Septemba mwaka jana.

  Kwa upande wa mfumuko wa bei unaopimwa kwa kipimo cha mwezi ameeleza kuwa umeongezeka kwa asilimia 0.4 kwa mwezi Septemba 2014 ikilinganishwa na asilimia 0.1 za mwezi Agosti  kutokana na kuongezeka kwa Fahirisi ya baadhi ya bidhaa zikiwemo samaki, matunda, mbogamboga, mihogo na vinywaji baridi, mkaa, mazulia na dawa za Binadamu kuwa na mchango mkubwa katika ongezeko la fahirisi.
  Aidha, amesema mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula nyumbani na migahawani umepungua hadi asilimia 8.3 mwezi Septemba 2014 kutoka asilimia 8.5 za mwezi Agosti 2014 na kuongeza kuwa uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma za jamii  kwa mwezi Septemba, 2014  umefikia  shilingi 66 na senti 70.
  Kwa upande wa mfumuko wa bei wa Tanzania na baadhi ya nchi za Afrika Mashariki Bw. Kwesigabo amesema kuwa una mwelekeo unaofanana, Kenya ukipungua na kufikia asilimia 6.6 kwa mwezi Septemba kutoka 8.34 za mwezi Agosti huku Uganda ikiwa na mfumuko wa bei wa asilimia 1.4 mwezi Septemba kutoka asilimia 2.8 za mwezi Agosti.
   

  0 0

   Dr. Servacius Likwelile Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha  na Mlipaji Mkuu wa serikali  akiwa pamoja na ujumbe kutoka Tanzania. Kutoka kushoto ni Kamishna wa Bajeti Bw. John Cheyo akifuatiwa na Bi.Mwanaidi  Mtanda ambaye ni mhasibu mkuu wa Serikali na wa mwisho kutoka kulia ni Balozi Liberata Mulamula.
   Bw.Herve’ Joly ambaye ni Mkurugenzi msaidizi na Mkuu wa idara ya Afrika sehemu ya Mashariki akishauriana na mwenzake baada ya kupokea hoja kutoka kwa Dr. Servacius Likwelile Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali.
   Balozi wa Tanzania nchini Marekani – Washington Mhe.Liberata Mulamula pamoja na Serikali Dr. Servacius Likwelile Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha  wakifurahia pongezi walizopewa na ujumbe wa IMF kuhusu muelekeo mzuri wa uchumi wa Tanzania.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile akielezea mikakati ya nchi ya Tanzania katika kuinua uchumi na kuongeza pato la Taifa kwenye Mkutano uliofanyika leo juu yuliohusu  masuala na fedha na sera ya kiwango cha ubalilishaji fedha.

  Kila mwaka Bodi ya Magavana ya Shirika la Fedha la Kimataifa na kundi la Benki ya Dunia hukutana kwa ajili ya kujadili kazi za Taasisi zinazowahusu. Mikutano hii imeanza tarehe 06 Octoba na itafikia kilele chake hapo tarehe 13, mwezi Octoba, 2014.

  Mikutano hii hufanyika mjini Washington DC kwa miaka miwili mfululizo na kwa mwaka wa tatu hufanyika kwa nchi mwanachama. 

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile ndiye kiongozi wa ujumbe kutoka Tanzania na yeye anawakilisha kama Gavana mbadala (Alternate Governor) pamoja na Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu ambaye pia ni Gavana katika mikutano hii. 

   Mikutano hii inatoa nafasi ya kuweza kujadiliana na Benki ya Dunia pamoja na Shirika la Fedha la Kimataifa kuhusiana na hali ya uchumi kwa maana ya sera za fedha na sera za mapato na matumizi. Nia yao kubwa ni kutaka kusikia mawazo yetu kuhusu jinsi ya kuboresha uchumi ili wawe katika nafasi nzuri ya kuangalia ni wapi wanaweza kutusaidia kuboresha na kuona kwamba nchi yetu inaendelea kufanya vizuri zaidi. 

  Maeneo ambayo yameshajadiliwa ni pamoja sera kuhusu kiasi cha ubadilishaji fedha, mapato ya nchi kwa ujumla na mwendo wa matumizi ya fedha. Hali ya utendaji wa kiuchumi na hali ya matumizi na mapato ya fedha ya Tanzania imeonekana ni ya kuridhisha japo pado kunachangamoto ya ajira. 

   Imetolewa na: 
  Ingiahedi Mduma 
  Msemaji -Wizara ya Fedha 
  Washington D.C 
  7/10/2014


  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wakazi wa Kilolo Mnadani waliojitokeza kumlaki katika ziara yake wilayani Kilolo.

  MBUNGE wa jimbo la Kilolo mkoani Iringa Profesa Peter Msolla akiwasalimia wananchi wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua matofali ya kikundi cha vijana cha Muungano ambacho kina jumla ya vijana arobaini waliopata mafunzo ya kufyatua matofali na ujenzi.
    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongea na wajumbe wa halmashauri kuu ya wilaya ya Kilolo katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kilolo.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kijiji cha Utengule kata ya Ihimbo ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa uchaguzi wa Serikali za mitaa mwezi Desemba CCM itashinda kwa kishindo.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi  wa kijiji cha utengule kata ya Ihimbo wilaya ya Kilolo mkoani Iringa ambapo aliwaambia viongozi wa Kata na Vijiji pamoja na ngazi ya wilaya wafanye mikutano na wananchi wao na waruhusu maswali ilikujua changamoto zinazowakabili wananchi .
   Mwenyekiti wa Kijiji cha Utengule Ndugu Pancras Mkakatu ambaye ni mwanachama wa Chadema akiongea na wananchi mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambapo  alimpongeza sana Katibu Mkuu wa CCm kwa kazi nzuri anayofanya na kueleza kuwa yeye ni CCM ila alitoka tu kwa sababu ya migongano na viongozi wengine wa CCM .
   Zahanati ya Kijiji cha Utengule ambayo imekamilika ilabado haijapata madaktari
   Mwenyekiti wa Kamati ya ujenzi wa shule ya sekondari ya Uwindi Ndugu Charles Kigwile akiuliza swali linalohusu ujenzi wa madarasa ya shule hiyo ambao umesimama.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhiwa mkuki kama ishallah ya kuwa Mtemi wa Wahehe.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwashukuru wananchi wa kijiji cha Utengule kwa kumpa heshima ya kuwa Mtemi kwenye kijiji chao
   Katibu Mkuu wa CCM akiwa kwenye picha ya pamoja na Watemi wenzake wa kijiji cha Utengule.
    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwaaga wananchi waliofurika kwa wingi kwenye mkutano wake.
    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipeana mikono ya kwa heri na wananchi wa kijiji cha Utengule.
   Madarasa ya shule ya msingi Iwindi wilayani Kilolo mkoani Iringa
  Mwalimu Josephine Konga wa Shule ya msingi akimuonyesha  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana uchache wa vyumba vya madarasa katika shule hiyo kiasi kupata shida sana katika kufundisha.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho kikwete na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt.Mohamed Ali Shein wakiwa wameinua juu  Katiba inayopendekezwa katika hafla iliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma Oktoba 08, 2014 Kulia ni Mwenyekiti wa Bunge maalum la Katiba Mhe.Samuel Sitta akifuatiwa na Makamu wake Mhe samia Suluhu Hassan.
   Mwenyekiti wa Bunge maalum la Katiba Mhe.Samuel Sitta akikabidhi  katiba inayopendekezwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho kikwete na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt.Mohamed Ali Shein katika hafla iliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma Oktoba 08, 2014
   

  0 0

  WALE MABINGWA WA COSMETICS ZA UKWELI KUTOKA USA, @AK CLASSIC COSMETICS SAFARI HII WAMEKULETEA BIDHAA ULIZOKUWA UNAZIMISS KUZIPATA HAPA BONGO. PRODUCTS ZA CHUNUSI  HASA (TEATREA PRODUCTS),WALE MNAOSWEAT KUPINDUKIA SAFARII HII HAMJASAHAULIKA,MAMBO YA SHAPE WEAR,DEODRANT ZA KUONDOA WEUSI KWAPANI,BIDHAA YA KUONDOA WEUSI KWENYE MAPAJA HASA BAADA YA KUGUSIANA UKITEMBEA,BIDHAA ZA KUKUZA NYWELE(T444Z & JBCO),BIDHAA ZA KUTOA MIWANI NA WEUSI WA KUUNGUA NA CREME KALI...NA MENGINE MENGIIII!!!
  EM TUPITIE HAPA .

  KWA MAELEZO YA KINA KWA KILA BIDHAA NA TATIZO HUSIKA NA PICHA ZAIDI WATEMBELEE BLOGUNI
  www.akclassic.blogspot.com
   KUWEKA ODA NA KUFIKISHIWA BIDHAA MPAKA ULIPO PIGA  0753-482909/0713-468393.
  WAPO KINONDONI KWA MANYANYA NA SINZA KUMEKUCHA.

  Pata uhondo wao insta@ak_classic_cosmetics

  KARIBUNI SANA.

  0 0

   Afisa Mtendaji Mkuu wa TSN group, Bw.  Farough Baghozah (wapili kushoto)akimkabidhi hundi ya shilingi milioni 13 Mratibu wa Mbio za Rock City Marathon 2014, Bw. Mathew Kasonta (wa kwanza kulia) wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Mbio hizo zitafanyika mkoani Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba tarehe 26 Mwezi huu. Wakishuhudia wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Operesheni wa TSN Group Bi. Pamela Mandari, na Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo Bi. Koiya Kibanga (wa kwanza kushoto). 
   Afisa Mtendaji Mkuu wa TSN group, Bw.  Farough Baghozah  (wapili kulia)akifafanua jambo  kwa waandishi wa habari wakati wa kukabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni 13 iliyotolewa na kampuni hiyo kudhamini mbio za Rock City Marathon 2014 zitakazofanyika mkoani Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba tarehe 26 Mwezi huu. Wakishuhudia kulia ni Mkurugenzi wa Operesheni wa TSN Group Bi. Pamela Mandari, Mratibu wa mbio hizo, Bw. Mathew Kasonta (wapili kushoto) na Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo Bi. Koiya Kibanga (wa kwanza kushoto). 
   Mratibu wa mbio za Rock City Marathon, Bw. Mathew Kasonta, (wa pili kushoto) akiongea na waandishi muda mfupi kaba ya kupokea hundi yenye thamani ya shilingi milioni 13 iliyotolewa na kampuni ya TSN Group kuoitia kinywaji chake cha Chili Willy kama udhamini wa mbio hizo kwa mwaka huu zitakazofanyika mkoani Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba tarehe 26 Mwezi huu. Kushoto kwake ni Afisa Mtendaji Mkuu wa TSN group, Bw.  Farough Baghozah akifuatiwa na Mkurugenzi wa Operesheni wa TSN Group Bi. Pamela Mandari, na kushoto ni Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo Bi. Koiya Kibanga (wa kwanza kushoto). 
  ======  =======   =========
  Ukurasa mpya umefunguliwa katika mbio za Rock City Marathon za mwaka huu ambapo kwa mara ya kwanza tangu mbio hizo zilipoanzishwa miaka mitano iliyopita, mbio fupi sasa zitakuwepo. 

  Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 13 kwa waratibu wa mbio hizo kampuni ya Capital Plus International Limited (CPI), Afisa Mtendaji Mkuu wa TSN Group Bw. Farough Baghozah aliipongeza hatua hiyo, na kusema kuwa kampuni yake inaungana na wadhamini wengine kuunga mkono tukio hilo la kila mwaka sababu ya dhamira yake ya kuibua na kukuza vipaji vya vijana katika riadha na kukuza utalii wa ndani kupitia michezo.

  “Tunayofuraha kuidhamini mashindano ya mwaka huu ambayo sasa yatajumuisha na vijana wadogo ambao wana vipaji vya kukimbia mbio fupi fupi. Hii itawapa vijana wengi nafasi ya kuonyesha vipaji vyao, ambavyo vinaweza kuwa ndiyo fani zao hapo mbeleni,” alisema Bw. Baghozah. 

  Alisema kuwa kampuni yake imekuwa ikiunga mkono jitihada mbali mbali zinazolenga kukuza sekta ya  michezo na burudani nchini Tanzania, ambayo imekuwa ikitengeneza fursa za ajira miongoni mwa vijana walio wengi nchini.
   
  “Hivi karibuni tu, TSN Group iliweza kuwaleta wachezaji wa timu ya Real Madrid ili kucheza na wachezaji wa zamani wa Tanzania wa mpira wa miguu. Hii ililenga katika kuwatia morari wachezaji wetu na vijana kupenda michezo, wakiendelea kuongeza jitihada ili kufanikiwa zaidi katika kile wanachofanya,” alisema.

  Naye mratibu wa tukio hilo, Bw. Mathew Kasonta alisema udhamini huo kutoka TSN Group utasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha mbio hizo za Rock City Marathon 2014, ambapo vipaji katika mchezo wa riadha vitagundulika pamoja na kuyafanya mashindano hayo kuwa chanzo kikubwa zaidi ya kutangaza maeneo mbali mbali ya utalii katika kanda ya ziwa.  

   “Baada ya kupata udhamini toka kwa wadhamini wetu, kamati ya maandilizi ilikaa na kukubaliana kuwa mbio za Rock City za mwaka huu zitajumuisha mbio fupi. Hizi zitajumuisha vijana kutoka katika shule za sekondari na wale waliopo shule za msingi madarasa ya juu. Uamuzi huo ulichukuliwa baada ya kuona kuwa mashindano ya marathon nyingi nchini, hayana mbio fupi ambazo zina vipaji vingi pia,” alisema Kasonta.   

  Alisema mbio hizo fupi zitakuwa ni; kilomita 100, kilomita 400 na kilomita 1500. Mbio hizo zitafanyika baada ya mbio ndefu ya nusu marathoni. Bw. Kasonta alisema fomu za usajili zinapatikana katika ofisi za kampuni ya Capital Plus International Limited (CPI) jengo la ATC ghorofa ya tatu jijini Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Mwanza, Ofisi zote za wilaya za Michezo na Utamaduni mkoani Mwanza, Uwanja wa Nyamagana na pia zinapatikana katika mtandao wa  www.therockcitymarathon.blogspot.com.  

  “Meya wa jiji la Mwanza, Bw. Stanslaus Mabula alifungua usajili kwa kuwa mshiriki wa kwanza kujisajili katika mbio za Rock City Marathon 2014 ambazo zitaanza katika uwanja wa CCM Kirumba tarehe 26 mwezi Oktoba mwaka huu, ambapo ataonyesha uwezo wake katika riadha kwenye mbio za kilometa 5,” alisema. 

  Bw. Kasonta aliwataja wadhamini waliyofanyikisha mbio hizo kuwa ni Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), TSN Group kupitia kinywaji chake cha Chilly Willy, pamoja na African Barrick Gold, IPTL, Air Tanzania, New Mwanza Hotel, Nyanza Bottling, Sahara Media Group, Continental decoders, New Africa Hotel, PPF, Tanapa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) akipokea Katiba Inayopendekezwa toka kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta wakati wa sherehe ya Makabidhiano ya Katiba hiyo iliyofanyika jana 8 Oktoba, 2014 mjini Dodoma.
   Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein (kushoto) akikabidhiwa Katiba Inayopendekezwa toka kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta wakati wa sherehe ya Makabidhiano ya Katiba hiyo iliyofanyika jana 08 Oktoba, 2014 mjini Dodoma.
   Marais wote wa Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakikata utepe kufungua Katiba Inayopendekezwa wakati wa sherehe ya makabidhiano ya Katiba hiyo hapo jana 8 Oktoba, 2014 mjini Dodoma.
  Marais wote wa Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakionyesha juu Katiba Inayopendekezwa ili wananchi waweze kuziona wakati wa sherehe ya makabidhiano ya Katiba hiyo hapo jana 8 Oktoba, 2014 mjini Dodoma.(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA, MAELEZO-DODOMA).
   
  KATIBA INAYOPENDEKEZWA YAKABIDHIWA RASMI KWA WAHESHIMIWA MARAIS WA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR.
   
  Na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma.
   
  09/10/2014.
   
  KATIBA Inayopendekezwa imekabidhiwa rasmi 8 Oktoba, 2014 kwa Waheshimiwa Marais wa Tanzania Bara, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja Rais wa Zanzibar, Mhe. Ali Mohammed Shein.
   
  Akihutubia wakati wa sherehe ya Makabidhiano ya Katiba hiyo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alisema kuwa tukio hilo la kukabidhiwa Katiba Inayopendekezwa ni jambo la kihistoria kwa nchi ya Tanzania na linaashiria kukamilika rasmi kwa kazi ya lililokuwa Bunge Maalum la Katiba lililoanza tarehe 18 Februari mwaka huu.
   
  Mhe. Dkt. Kikwete alisema kuwa ni hatua nyingine ya kihistoria ya nchi kwani hatua ambayo imesalia hivi sasa ni ile ya wananchi kwenda kuipigia kura za maoni Katiba hiyo ili waweze kufanya uamuzi kuhusiana na Katiba hiyo na endapo wananchi hao wataikubali basi Tanzania itakuwa imejipatia Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
   
  “Sina budi Kumshurkuru Mwenyezi Mungu kwa hapa tulipofikia na sina budi kumshukuru Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel John Sitta, Makamu wake Mama Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya, nawashukuru pia Wenyeviti wa Kamati mbalimbali za Bunge Maalum kwa uongozi waa makini, natoa pia shukurani za pekee kwa Wajumbe wote wa Bunge Maalum la Katiba kwa kukamilisha kazi hii tena mmeikamilisha kazi hii kwa kiwango cha juu sana cha ubora”, alisema Mhe. Dkt. Kikwete.    
   
  “Shukurani zangu pia ziende kwa Katibu wa Bunge Maalum na Naibu Katibu pamoja na Wasaidizi wao wote kwa kazi nzuri walioifanya na kuiwezesha Bunge Maalum la Katiba kukamilisha kazi yake kwani haikuwa kazi rahisi hata kidogo”, aliongeza Mhe. Dkt. Kikwete.
   
  Naye Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein alimpongeza Rais wa Tanzania Bara, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuanzisha mchakato huo wa kupata Katiba mpya na alitoa pongezi zake kwa Mwenyekiti wa lililokuwa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samule Sitta pamoja na Makamu wake Mhe. Samia Suluhu ikiwemo pongezi pia kwa Wajumbe wote walioshiriki katika mchakato huo.
   
  Katika Hotuba yake, Mhe. Dkt. Shein alisema kuwa katika mchakato mzima wa kutafuta Katiba hiyo, Zanzibar ilishirikishwa kikamilifu kwani hakuna hata hatua moja ambayo haikushiriki.
   
  “Nataka leo nisisitize kuwa Zanzibar ibaki sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kila hatua ya mchakato huu imeshirikishwa na kushiriki kikamilifu hadi hivi leo tulipofikia”, alisema Dkt. Shein.
   
  Naye aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi wa lililokuwa Bunge Maalum la Katiba. Mhe. Andrew Chenge alisema kuwa ndani ya Katiba hiyo katika eneo la Uongozi, kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania imeweka Ukomo wa idadi ya Mawaziri pamoja na Naibu Mawaziri ambapo kwa mapendekezo hayo, idadi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri haitazidi 40.
   
  Mhe. Chenge alifafanua kuwa idadi hiyo ya Mawaziri na Naibu Mawaziri itaisadia Serikali na Wananchi kupunguza gharama kwa ujumla na pia katika suala hilo hilo la uongozi aliongeza kuwa Rais wa Zanzibar anapokuwa Makamu wa Rais ni ishara ya Muungano, hivyo itaisadia Serikali ya Jamhuri ya Muungano kudumisha Muungano uliopo.
   
  Aidha, Katika masuala yanayohusu Bunge, Chenge ameeleza kuwa Katiba inayopendekezwa inapendekeza mambo mawili ya msingi ambayo ni Uwiano wa Wabunge pamoja na Ukomo wa Idadi yao.“Kuhusu Uwiano wa Wabunge, inapendekezwa kuwepo na uwiano ulio sawa kati ya Wabunge Wanaume na Wabunge Wanawake uwe asilimia hamsini kwa hamsini”, alisema Chenge.
   
  Akiongea kuhusu suala la ukomo wa Wabunge hao, wote wa kuchaguliwa na wale wa kuteuliwa, Mhe. Chenge alibainisha kuwa idadi hiyo haitapungua 340 na haitazidi 390.“Mhe. Rais, Katiba hii Inayopendekezwa imesheheni malengo muhimu, ya Kiuchumi, ya Kisiasa, kijamii, ya kiutamaduni na kimazingira”, alisema Chenge.
   
  Aliongeza kuwa katika malengo ya Taifa na kijamii yameboreshwa zaidi kwa kuweka mazingira yatakayowezesha Wasanii pamoja na Wanamichezo kukuza na kuendeleza vipaji vyao na kuleta mabadiliko ya kiuchumi katika jamii.

  0 0

  Bondia Hamza Mchanjo akinolewa na kocha Saidi Chaku katika GYM ya Gongolamboto Dar es salaam jana Mchanjo anajiandaa na mpambano wake na Juma Fundi utakaofanyika Oktoba 25 katika ukumbi wa Frends Corne Manzese .
  Bondia Hamza Mchanjo akinolewa na kocha Saidi Chaku katika GYM ya Gongolamboto Dar es salaam jana Mchanjo anajiandaa na mpambano wake na Juma Fundi utakaofanyika Oktoba 25 katika ukumbi wa Frends Corne Manzese.
  Bondia Hamza Mchanjo kushoto akizipiga na Hassan Hoza wakati wa mazoezi yao yaliyofanyika katika GYM ya Gongolamboto makaburi ya Kichina Dar es salaam Mchanjo anajianaa na mpambano wake na Juma Fundi utakaofanyika October 25 katika ukumbi wa frends corner manzese Picha na SUPER D BLOG
  Bondia Hamza Mchanjo kushoto akizipiga na Hassan Hoza wakati wa mazoezi yao yaliyofanyika katika GYM ya Gongolamboto makaburi ya Kichina Dar es salaam Mchanjo anajianaa na mpambano wake na Juma Fundi utakaofanyika

  October 25 katika ukumbi wa frends corner manzese Picha na SUPER D BLOG

  RATIBA YA MABONDIA WATAKAOCHEZA SIKU HIYO YA TAREHE 25/7/2014

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Fatma Mwassa akizungumza na wananchi jana wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Vijana yanayofanyika katika viwanja vya Ali Hassan Mwinyi Mkoani Tabora.
   Katibu Mkuu wa Wizaraya Habari.Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga akisalimia wananchi jana wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Vijana yanayofanyika katika viwanja vya Ali Hassan Mwinyi Mkoani Tabora.
   Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Kudra Mwinyimvua akisalimia wananchi jana wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Vijana yanayofanyika katika viwanja vya Ali Hassan Mwinyi Mkoani Tabora
   Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Fatma Mwassa akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa maadhimisho ya wiki ya Vijana jana mkoani Tabora.Kushoto ni ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga,Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Bibi. Kudra Mwinyimvua na wa mwisho kulia ni Mwakilishi wa UNFPA Tausi Hassan.

   Baadhi ya Vikundi vya Burudani wakitumbuiza wakati wa hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Vijana jana mkoani Tabora.
   Baadhi ya wadau wa wiki ya Vijana wakifuatilia Burudani kutoka kwa Kikundi cha JKT hakipo pichani jana mkoani Tabora wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Vijana ambayo kitaifa inafanyika mkoani hapa.


   Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Fatma Mwassa akielezea jambo alipotembelea banda la Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo jana mkoa Tabora mara baada ya kuzindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Vijana.Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga na mwisho kushoto ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo.
   Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Fatma Mwassa akisikiliza maelezo kuhusu mfumo wa kuwajengea uwezo Vijana kujitengenezea makampuni yao na kumiliki Biashara  alipotembelea banda la Kampuni ya GODTEC jana mkoa Tabora mara baada ya kuzindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Vijana.
   Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Fatma Mwassa akiweka saini katika kitabu cha wageni katika banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) jana mkoa Tabora mara baada ya kuzindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Vijana.
  Baadhi ya wananchi wakipata huduma ya upimaji wa afya zao katika banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya jana mkoani Tabora ambapo maadhimisho ya wiki ya Vijana yanaenedele.


  Na Jonas Kamaleki - MAELEZO

  Serikali yaweka Mkakati kupunguza changamoto ya ajira kwa Vijana
  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka mkakati kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana kwa kutenga fedha katika halmashauri mbali mbali nchini kwa lengo la kusaidia miradi ya vijana.

  Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Bibi Fatma Mwassa wakati wa sherehe za uzinduzi wa Wiki ya Vijana mjini Tabora leo (jana). Bibi Fatuma amesema kuwa Mkoa wa Tabora umetenga jumla ya shilingi 1.8 kwa ajili ya kusaidia miradi ya vijana.

  “Serikali inatambua changamoto zinazo wakabili vijana ikiwemo ukosefu wa ajira ata hivyo tumekuwa tukijitahidi kukabiliana nazo ikiwemo kwa kutenga fedha kwa ajili ya kusaidia vijana ambapo hapa mkoani kwetu jumla ya shilingi bilioni 1.8 zimetengwa katiak halmashauri zote.” Alisema Bibi. Fatma. Aidha Bibi Fatma aliongeza kuwa Serikali ipo tayari kusaidia Vijana katika kuendeleza shughuli zao na kuwataka kuwa wabunifu na wenye dhamira ya kweli katika kutekeleza miradi ya maendeleo.

  Mkuu huyo wa Mkoa amewataka vijana wasitumiwe tu na watu wasioitakia mema nchi bali wajitambue ili waweze kufanya shughuli za uzalishaji mali na kuacha tabia ya kukaa vijiweni. Pia amewaasa vijana kutojihusisha na mada ya kulevya. “Msitumike katika kubeba madawa hayo matumboni mwenu au kuyauza reja reja,kataeni kutumikishwa,” alisisitiza Bibi Fatma Mwassa. 

  Amewataka vijana watumie fursa zilizopo ili waweze kujiendeleza badala ya kulalamika. Amewaasa watumie ujana wao vizuri kama alivyoutumia Baba wa Taifa, Hayati Julius Kambarage Nyerere ambaye tunaadhimisha miaka 15 ya kifo chake. Alisema Mwalimu aliutumia ujana wake vizuri katika shughuli za kisiasa na kujipatia heshima kubwa.

  Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga amesema kuwa Wiki ya Vijana imekuwa jukwaa muhimu kwa Vijana wengi hapa nchini kwani upata fursa ya kukutana na kujifunza kupitia maonyesho yanayoambatanana maadhimisho hayo.

  Bibi. Sihaba aliongeza kuwa kumekuwapo na matokeo chanya yanayotokana na maadhimisho hayo ambapo baadhi ya vijana wenye dhamira wemepata kuwa wajasiriamali kupitia wa kubwa na wakati kupitia maadhimisho hayo.

  Wiki ya Vijana inaadhimishwa ikiwa inatimizwa umri wa miaka 15 tokea ilipoanzishwa mnamo mwaka 2000 Mkoani Kilimanjaro. Katika Wiki hii Vijana mbalimbali ujumuika pamoja katika maadhimisho hayo ambayo kwa mwaka huu yanafanyoika mkoani Tabora na yatafikia kilele chake tarehe 14 Oktoba ambayo ni siku ya Kumbukumbu ya Baba wa Taifa na kilele cha mbio za Mwenge.
   


  0 0

  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiwasili kwenye Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Washington, DC nchini Marekani alikokaribishwa chakula cha jioni wakiwemo viongozi mbalimbali wa Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya Tanzania. Mhe. Ombeni Sefue ndiye aliyewezesha ununuzi wa jengo hilo la Ubalozi wakati alipokua Balozi wa Tanzania nchini Marekani mwaka 2007
  Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akimpokea Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue siku ya Jumatano Oct 8, 2014 siku Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani ulipomkaribisha chakula cha jioni wakiwemo viongozi mbalimbali wa Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya Tanzania.
  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiongea mawili matatu na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dr. Servacius Likwelile.
  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akisalimiana na Naibu Gavana Dr. Natu Mwamba.
  Mkuu wa Utawala na Fedha Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mama Lily Munanka akiongea machche na baadae kumkaribisha Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula.

  0 0

  Vijana katika biashara ya uuzaji samaki. Vijana katika biashara ya uuzaji samaki.Vijana katika biashara ya uuzaji mapambo mbalimbali 
  Vijana katika biashara ya uuzaji mapambo mbalimbaliVijana katika biashara ya uuzaji samaki. 
  Vijana katika biashara ya uuzaji samaki.Vijana katika biashara ya ukaangaji na uuzaji samaki. 
  Vijana katika biashara ya ukaangaji na uuzaji samaki.

  WAKATI siku ya mwisho ya urejeshaji wa fomu kwa vijana watakao shiriki Shindano la Mashujaa wa Kesho ukiwadia na dirisha la upokeaji fomu hizo kutarajiwa kufungwa hapo kesho majira ya saa nane idadi ya vijana waliorejesha fomu hizo imeendelea kupanda. 

  Akizungumzia zoezi hilo jana mchana, Ofisa Mawasiliano wa Kampuni ya Statoil Tanzania, Erick Mchome aliwataka vijana waliochukua fomu zao kuzirejesha mapema ili kujipatia fursa ya kushiriki katika shindano hilo ambale linaweza kuwakwamua vijana kiuchumi. 

   Akifafanua zaidi, Erick Mchome alisema dirisha la kupokea fomu za Shindano la Mashujaa wa Kesho linatarajiwa kufungwa rasmi kesho, Oktoba 10, 2014 majira ya saa nane za mchana na kuwataka vijana wachangamke kabla ya muda huo kufungwa. Alisema bado kuna idadi kubwa ya fomu ambazo hazijarejeshwa na vijana waliochukua fomu hizo na kuwataka kufanya hivyo kabla ya muda wa zoezi hilo kufungwa hapo kesho. “Vijana waliorejesha fomu mpaka leo (jana) ni takribani vijana 200. 

  Waliochukua fomu tangu siku ya uzinduzi Septemba 3, 2014 ni zaidi ya vijana 1000. Hivyo natoa wito kwa vijana ambao bado hawajarejesha na wanataka kuingia kwenye ushindani huu kurejesha fomu zao kwa wakati,” alisema Mchome. Zoezi zima la urejeshaji fomu litafikia tamati siku ya Ijumaa Oktoba 10, 2014 kabla ya saa nane mchana na baadaye kufanyika mchujo wa kupata vijana 40 watakaoingia hatua ya pili kabla ya kutangazwa washindi watano ifikapo mwezi wa 12. 

   Aidha alivitaja vituo vya kurejesha fomu mkoani Mtwara kuwa ni pamoja na Naliendele Agricultural Institute, Tanzania Institute of Accountancy, VETA, Chuo cha Utumishi, Chuo cha Stella Maris Pamojana Pride FM. Naye Mhadhiri wa Chuo cha Stella Maris ambaye pia ni Mratibu wa shindano hilo kituo cha chuo hicho, Justin Lusasi aliwataka vijana kutokata tamaa katika ushiriki kwani kitendo cha kushiriki pekee katika shindano hilo na kuingia hatua ya pili ni faida kubwa kwao kwa kuwa watapata fursa ya kujifunza jinsi ya kuaanda mipango ya biashara. 

   “Napenda kuwasihi vijana wote warejeshe fomu zao, wala wasikate tamaa kwani kwa kila atakayefanikiwa kuwa miongoni mwa washiriki 40 watakaoingia katika hatua ya pili, atapata faida kubwa...watapata nafasi ya kujifunza masuala ya biashara kama vile namna ya kuandika mipango ya biashara, utekelezaji na usimamizi wa biashara,” alisema Lusasi. 

  Shindano la Mashujaa wa Kesho linaloendeshwa mkoani Mtwara linalenga kuendeleza ujasiriamali kwa vijana mkoani Mtwara linaratibiwa na kampuni ya uchimbaji gesi ya Statoil Tanzania. Washindi watano watapatikana ambapo mshindi wa kwanza atajishindia kitita cha dola za Kimarekani 5,000 na dola 1,000 kwa washindi wengine wanne. Washindi wanatarajia kutangazwa Desemba, 2014.

  0 0

  Meneja Uhusiano Mwandamizi wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) Noves Moses akikabidhi jezi za mpira wa miguu zenye thamani ya sh. 1,800,000/= kwa Mwenyekiti wa TASWA SC Majuto Omary. 
  Meneja Uhusiano Mwandamizi wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) Noves Moses akikabidhi jezi za mpira wa miguu zenye thamani ya sh. 1,800,000/= kwa Mwenyekiti wa TASWA SC Majuto Omary.[/caption] TANZANIA Sports Writers Association Sports Club (TASWA SC) received sports gears worth Tzs 1,800,000/= from Tanzania Postal Bank (TPB). Chief Manager, Corporate Affairs of the bank Noves Moses said her bank has decided to support the team as a gesture for active recreation activity besides reporting. 

  Noves said TASWA SC has done that for more than 20 years and win various honors. She said TPB is very proud to be part and parcel of sports development in the country. This is the second time TPB supporting TASWA SC, before the banks handed over Tzs. 2 million to the club for their sports tours. TASWA SC Chairman Majuto Omary thanked TPB for the support and called other sports stakeholders to emulate their footsteps. Majuto said their club is facing a pile of challenges in its operations that TPBs boost has come at the right time for right purpose and in the right way.

  0 0

   Meja Jenerali  Mstaafu Muhiddin Kimario.

  Mwili wa aliyekuwa Waziri mwandamizi kwenye serikali ya awamu ya kwanza na pili Meja Jenerali (mstaafu) Muhiddin Mfaume Kimario umewasili leo mchana kwa ndege ya shirika la Ethiopia kutoka nchini India alikokuwa akipata matibabu tayari kwa mazishi siku ya Jumamosi mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.

  Mwili wa Meja Jenerali Kimario uliwasili jana saa saba mchana kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (JKNIA) na kupokelewa na maafisa wa Jeshi, Serikali na wanafamilia.

  Ijumaa tarehe 10 Oktoba, 2014 Jenerali Kimario ataagwa kwa heshima za mwisho kwenye kambi ya Jeshi Lugalo. Watu wote wanaotaka kushiriki kuaga mwili wanakaribishwa. Tukio hilo la dakika 90 linatarajia kuanza saa 4 na kukamilika saa 5:30asubuhi.

  Baada ya hapo mwili utapelekwa Msikiti wa Maamur ulioko Upanga kwa ajili ya kuswaliwa wakati wa sala ya Ijumaa na baada ya kukamilika kwa sala hiyo mwili utapelekwa uwanja wa JKNIA kwa ajili ya kwenda Moshi, Kilimanjaro kwa ajili ya maziko siku ya Jumamosi.

  Mazishi yake yatafanyika saa 10 jioni kwenye makaburi ya Moshi mjini baada ya kuswaliwa kwenye Msikiti wa Riadha.

  Marehemu Meja Jenerali Kimario atakumbukwa kama moja ya Maafisa wa kwanza walioanzisha JWTZ, Kamanda wa vita aliyefanikisha kung’olewa kwa nduli Iddi Amin, mwanasiasa shupavu aliyeshika nyadhifa mbalimbali kama Waziri wa Ulinzi na Mambo ya Ndani pamoja na ukuu wa Mkoa kwa mikoa ya Mwanza na Dar-es-salaam na Mkurugenzi wa CDA.

  0 0


   Mganga Mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Mufindi Dk.Boaz Mnenegwa  akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipotembelea wodi ya kina mama hospitalini hapo.
   Sehemu ya Wodi ya akina mama katika hospitali ya wilaya ya Mufindi.
   Meneja wa Shamba la SAO Hill Ndugu Salehe Beleku akizungumza mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipotembelea  ofisi ya SAO Hill Mufindi
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitazama mti uliopandwa mwezi wa kumi mwaka 1980 kwenye viwanja vya SAO Hill na Baba wa Taifa Mwl.Julius Kambarage Nyerere
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda mti wa kumbukumbu baada ya kutembelea ofisi za SAO Hill wilayani Mufindi mkoa wa Iringa.

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka udongo baada ya kupanda mti wa kumbukumbu baada ya kutembelea ofisi za SAO Hill wilayani Mufindi mkoa wa Iringa
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye  akipanda mti wa kumbukumbu nje ya ofisi ya SAO Hill wilaya ya Mafinga
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akikusanya baadhi ya mabango kutoka kwa wananchi wa Mafinga waliotaka ujumbe wao ufike kwa Katibu Mkuu wa CCM
  Katibu Mkuu wa CCM akiangalia namna mbao zinavyotayarishwa kwenye kiwanda cha mbao cha Emmanuel kinachomilikiwa na Ndugu Charles Emmanuel Akyoo

older | 1 | .... | 382 | 383 | (Page 384) | 385 | 386 | .... | 1897 | newer