Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 379 | 380 | (Page 381) | 382 | 383 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Nicole Franklyn Sarakikya ambaye ni mwakilishi kutoka Shinyanga 2014  usiku wa kuamkia leo alifanikiwa kuwabagwa warembo wenzake 26 kati ya 30 wanao wania taji la Miss Tanzania mwaka huu na kufanikiwa kuwa mrembo wa 3 kuingia Nusu Fainali ya Mashindano hayo baada ya kutwaa taji la miss talent. Shindano hili limefanyika New Maisha Club jijini Dar es Salaam. (Picha na Pamoja Blog)
  Tano bora ilikuwa hii


   Ommy Dimpoz akiwa kwenye red carpet
   Msami akitoa burudani ya nguvu ndani ya Maisha club jijini Dar
    Mambo yalikuwa hivyo kwa baadhi ya washiriki
  Mardha John akifanya vitu vyake


   Huyu ni balaaaa
   Elizabeth Eliud akikizungusha kiuno chake
  Dorice Molel akifanya ya kwake kwenye stage
    Kwa Naomi Kisaka ilikuwa ni shidaaaaaa
   Huyu alikuja kiivi
   Sabina Thomas  alitoka kivyake vyake
    Weeeeee hii ni shida 
   Maureen Godfrey akishake kwenye stage
   Majaji wakifuatilia shindano hilo kwa makini
   Nicole Franklyn Sarakikya akiimba kwa hisia kali
   Hapa ni mwendo wa burudani tu
  Ni mwendo wa furaha tu
   Camilla John aliimba kwa hisia 
   Hii ni kikwetu kwetu
  Happy Sosy alikuja kama Beyonce 
  Queen Latifa Hamisi yeye aliamua kukata nyonga 
  Ni mwendo wa mauno
   Ni furaha tu
   Ngoma ziliamia India kwa muda
   Mc wa mashindano ya Redds  Miss Tanzania Talent, Hypeman Hk akifanya ya kwake kwenye jukwaa la New Maisha Club.
  Ommy Dimpoz akitoa burudani kwenye stage ya Tanzania Miss Talent iliyofanyika ndani ya New Maisha Club Dar es salaam.
  Kazi inaendelea hapa 

   Majaji wakijadiliana jambo
   Ilikuwa ni shidaaaaaa
   
  Ommy Dimpoz (kulia) akiimba pamoja na Christian Bella waimbo wa mama ulioleta amasa kwa mashabiki wake.
   Majaji wakiongozwa na Chief jaji Martin Kadinda wakitoa maoni juu ya washiriki walioonesha vipaji vyao
    Chief Jaji Martin Kadinda akitangaza washindi
  Baadhi ya mashabiki wakifuatilia kwa makini tukio lililokuwa likiendelea

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Tanga mjini ambapo aliwaambia muda wa kuwaambia watanzania maendeleo yapo kwenye mipango umekwisha na kutaka viongozi kutimiza wajibu wao.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwapungia mkono maelfu ya watu waliofurika kwenye mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana uliofanyika kwenye uwanja wa Tangamano.

   Maelfu ya wakazi wa Tanga wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa anahitimisha ziara yake ya siku 11 kwenye mkoa wa Tanga.
   Wananchi wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambapo pamoja na yote alizungumzia uchumi wa Tanga ambapo aliwaambia wananchi hao lazima reli na bandari zifanye kazi ili uchumi wa mkoa wa Tanga ubadilike.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisitiza jambo wakati akihutubia wakazi wa Tanga mjini.

   Katibu Mkuu wa CCM akiwa kwenye picha ya pamoja na wanachama waliojiunga na CCM kutokea chama cha CUF
   Mzee Athumani Makalo akitoa salaam za pongezi kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwa hotuba nzuri zilizobadilisha siasa ya Tanga .
   Mzee Makalo akimvisha Katibu Mkuu joho  zawadi kutoka kwa wazee wa Tanga mjini.
   Katibu Mkuu wa CCM akiagana na watu baada ya kumaliza mkutano
   Watu wakigombania kumshika mkono Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati akiondok kwenye uwanja wa mikutano
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwapungia mkono wananchi kama ishara ya kuwaaga baada ya kumaliza mkutano mkubwa mjini Tanga.
  Kila mtu alimuaga Katibu Mkuu wa CCM kwani mkutano wake wa leo aliongela masuala ya msingi yanayohusu mkoa wa Tanga.BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi waliofika kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Tangamano kata ya Tangamano wilaya ya Tanga mjini.
   Wananchi wakiwa na bango lao kwenye mkutano wa hadhara wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye uwanja wa mikutano Tangamano.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana , Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwa pamoja wakiwapungia wananchi waliofika kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya mikutano Tangamano, Tanga mjini.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipeana mkono na Mzee Athumani Makalo wakati akiwasili kwenye uwanja wa mkutano wa Tangamano.
   Wananchi wa Tanga mjini wakishangilia ujio wa Katibu Mkuu wa CCM kwenye viwanja hivyo ya mikutano.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wananchi wote waliohudhuria mkutano kwa kuwapingia mikono yote miwili.
   Wananchi nao hawakuwa nyuma kumpungia kiongozi wao.
   Mkuu wa wilaya ya Tanga mjini Mh.Halima Dendegu akiwasalimia watu waliofurika uwanjani kwenye mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
   Kila mwananchi wa tanga alikuwa na shauku ya kusikiliza mkutano huo
   Wananchi wakishangilia kwa nguvu wakati wa hotuba ya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia kwenye uwanja wa Tangamano
   Wadau wa CCM mkoa wa Tanga wakifuatilia mkutano
   Kila mtu wa Tanga alikuwepo kwenye mkutano huo.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa  Tanga mjini na kuwaambia watendaji wa serikali kutoka maofisini na kwenda kwa wananchi ambao wanamaswali ya matatizo yao na wanahitaji majibu.
  Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Tanga Mama Aisha Kigoda pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Tanga mjini Mh.Halima Dendegu wakifuatilia kwa makini hotuba za viongozi kwenye mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana uliofanyika kwenye viwanja vya Tangamano.
   Mbunge wa Jimbo la Tanga mjini Mh.Omari Nundu akihutubia wananchi wa Tanga mjini kwenye mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.

  0 0

   Picha ya pamoja baada ya mazungumzo.

  Mfanyabiashara mwenye ukwasi mkubwa Afrika Aliko Dangote katika mazungumzo na Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal kuhusu uwekezaji wake katika kiwanda cha simenti mkoani Mtwara. Dangote alisema kazi ya ujenzi inakwenda kama ilivyopangwa na kwamba kiwanda hicho kitakuwa kikubwa kabisa kwa uzalishaji simenti katika ukanda wa Afrika Mashariki. Picha na OMR

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunga rasmi Kikao cha kazi cha viongozi wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri nchini katuika ukumbi wa Chimwaga katika Chuo Kikuu cha Dodoma mjini Dodoma.
   Mhe. Baraka Konisaga, ambaye ni Mjumbe wa Kikao cha kazi cha viongozi wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri nchini akitoa rais binafsi muda mfupi kabla Rais Jakaya Mrisho Kikwete hajafunga rasmi kikao hicho cha siku tatu kilichojumuisha wajumbe zaidi ya 900 kuzungumzia sekta ya elimu ili  kupanga mikakati na kutatua changamoto zinazoikabili, katuika ukumbi wa Chimwaga katika Cho Kikuu cha Dodoma mjini Dodoma Ijumaa Oktoba 3, 2014


   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Profesa Shaaban Mlacha na Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Idris Kikula (tai nyekundu) alipofanya ziara ya ghafla kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo ya Chuo  cha Sayansi ya  Afya na Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu cha chuo hicho mjini Dodoma Ijumaa Oktoba 3, 2014. Alikuta ujenzi umeshakamilika na kilichobaki ni uwekaji wa samani na vifaa vya kufanyia kazi ili kitovo hicho kianzi kazi rasmi hivi karibuni.
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa sehemu mbalimbali na  Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dododma Profesa Shaaban Mlacha (mbele) na Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Idris Kikula (kulia) alipofanya ziara ya ghafla kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo ya Chuo  cha Sayansi ya Afya na Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu cha chuo hicho mjini Dodoma Ijumaa Oktoba 3, 2014. Alikuta ujenzi umeshakamilika na kilichobaki ni uwekaji wa samani na vifaa vya kufanyia kazi ili kitovo hicho kianzi kazi rasmi hivi karibuni.
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa maelekezo kwa  Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Profesa Shaaban Mlacha na Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Idris Kikula (tai nyekundu) alipofanya ziara ya ghafla kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo ya Chuo  cha Sayansi ya Afya na Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu cha chuo hicho mjini Dodoma Ijumaa Oktoba 3, 2014. Alikuta ujenzi umeshakamilika na kilichobaki ni uwekaji wa samani na vifaa vya kufanyia kazi ili kitovo hicho kianzi kazi rasmi hivi karibuni.
  Jengo kuu la  Chuo  cha Afya na Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu cha Chuo Kikuu cha Dodoma  mjini Dodoma 
   Sehemu ya majengo ya Chuo  cha Sayansi ya Afya na Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu ya UDOM
   Sehemu ya barabara ya lami ya kutoka na kuelekea vyuo mbalimbali vya UDOM

  0 0

  Golikipa wa timu ya Stend United, John Mwenda akidaka mpira mbele ya mshambuliaji wa Simba, Amisi Tambwe wakati wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka  Tanzania uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Timu hizo zilitoka sare ya 1-1. (Picha na Francis Dande)   
  John Mwenda akiwapanga wachezaji wake.
  Mshambuliaji wa Simba, ibrahim Ajib akiwatoka mabeki wa Stand United.
  kipa wa timu ya Stend United, John Mwenda akiukodolea macho mpira uliopigwa na Shaban Kisiga ukiingia wavuni wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara uliofanyika Uwanja wa Taifa.
  Wachezaji wa Simba wakishangilia goli lao.
  Wachezajhi wa Stande wakitoka mapumziko.


  Wachezaji wa Stand United wakiwa katika =chumba cha waandishi wa habari wakati wa mapumziko badala ya kuingia katika chumba maalum kwa ajili ya timu hiyo.
  Kocha wa stand United akitoa maelekezo kwa wachezaji wake.
  Mashabiki wa Simba.
  Mashabiki wa Simba wakiwa vichwa chini.
  Wakifuatilia mchezo huo uku wakiwa hawana matumaini ya ushindi..
  Mshambuliaji wa Simba, Amis Tambwe akimtoka beki wa Stand United, Idd Mobby.
  Kocha wa Simba akitoa maelekezo kwa wachezaji wake.
  Okwi akitafuta mbinu za kumtoka Iddy Mobby wa Stand United.
  Amis Tambwe akipiga kichwa katikati ya mabeki wa Stand United.
  Elius Maguri akimtoka beki wa Stand United.
  Elius Maguri akiambaa na mpira.
  Maguri akiipangua ngome ya Stand United.
  Idd Mobby akimdhibiti Emmanuel Okwi.
  Beki wa Stand United akimbana Emmanuel Okwi.
  Nawatoka hivi.........
  Mwamuzi wa mchezo huo, Anthony Kayombo kutoka Rukwa akimuonyesha kadi ya njano John Mwenda.
  Kikosi cha Stand United.
  Kikosi cha Simba.
  Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Phiri akishuhudia timu yake wakati ikicheza na Stand United.

  Benchi la ufundi la Stand United.

  0 0

   Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bibi Florence Mwanri (aliyesimama) akimkaribisha mgeni rasmi Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Pwani Bibi Mwantumu Mahiza (aliyekaa kaikati). Kulia ni Katibu wa Baraza hilo Bw. Senya Robert.
   Mgeni Rasmi  wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Mwantumu Mahiza (aliyesimama) akisisitiza jambo alipokua akifungua kikao cha Baraza hilo.

    Wajumbe wa Baraza wakifuatilia kwa makini majadiliano yaliyokua yakiendelea wakati wa baraza hilo.

   Wajumbe wa Baraza la wafanyakazi Ofisi ya Rais, Tume ya Mipando kwa pamoja wakiimba wimbo wa Solidarity Forever kuonyesha mshikamano makazini.
   Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakionyesha mshikamano kwa kuimba wimbo wa Solidarity forever mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani kufungua rasmi kikao hicho.
   Picha ya pamoja
  Kabla ya kuanza majadiliano, wajumbe walimchagua Mwenyekiti Msaidizi wa Baraza la Wafanyakazi ambapo Bibi Magreth Simwela (aliyesimama) aliibuka mshindi kati ya wajumbe watatu waliokua wakigombea nafasi hiyo. Hapo Mwenyekiti Msaidizi alikua akiwashukuru wajumbe kwa kumchagua.

  ========  -====== ========

  MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA OFISI YA RAIS, TUME YA MIPANGO KATIKA UKUMBI WA HOTELI YA JD COMPLEX – KIBAHA, PWANI.

    HOTUBA YA MKUU WA MKOA WA PWANI MH. MWANTUMU BAKARI MAHIZA KATIKA UFUNGUZI WA MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA OFISI YA RAIS, TUME YA MIPANGO KATIKA UKUMBI WA HOTELI YA JD COMPLEX – KIBAHA, PWANI.

  ·                    Ndugu Mwenyekiti
  ·                    Mwakilishi wa TUGHE Taifa
  ·                    Mwakilishi TUGHE Mkoa wa Dar es salaam
  ·                    Mwenyekiti wa TUGHE ORTM
  ·                    Ndugu Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi
  ·                    Mabibi na Mabwana
  Awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia kuwepo hapa leo hii tukiwa na afya njema.  Pia, nikushukuru wewe binafsi Kaimu Katibu Mtendaji, pamoja na timu yako kwa kunipa heshima hii kubwa ya kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
  Ndugu washiriki,
  Nimearifiwa kuwa Baraza hili ni la kwanza katika mwaka 2014/15 na limewakilishwa na Wakuu wote wa Klasta, Idara na Vitengo, wajumbe wa TUGHE Taifa, TUGHE Mkoa – Dar es salaam, Halmashauri ya Tawi la TUGHE Tume ya Mipango na mjumbe mmoja mmoja kutoka kila Klasta, Idara na Vitengo.
  Aidha, napenda kutumia fursa hii kuwapongeza wajumbe wote wa mkutano huu kwa kuchaguliwa kwenu kuwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango kupitia mabadiliko ya Mkataba Mpya. Hii ni kutokana na imani kubwa waliyonayo watumishi juu yenu katika kuwawakilisha katika chombo hiki muhimu. 

  Ndugu washiriki,
  Baraza la Wafanyakazi ni kama Bunge la Taasisi yenu kwa kuwa linaundwa na wawakilishi wa wafanyakazi wote waliochaguliwa kidemokrasia.  Baraza hili ni chombo muhimu sana kilichoundwa kisheria kwa madhumuni ya kuwashirikisha watumishi katika kujadili na kufanya maamuzi kuhusu masuala yanayohusu maslahi ya ajira mahali pa kazi kwa lengo la kuleta tija. Kupitia Baraza hili mwajiri anapokea maoni ya watumishi na kuweza kufikia maamuzi sahihi ya namna ya kuboresha mazingira ya kazi na watumishi kwa ujumla.
  Wajibu wa mabaraza haya kama vyombo vya ushauri na usimamizi ni kuhakikisha kuwa waajiri na watumishi wanatambua wajibu na haki zao na wanazingatia maadili ya utumishi wao ili kuleta matokeo makubwa ya utendaji kazi yenye tija.
  Ndugu washiriki,
  Hata kama kutakuwa na sera, sheria na kanuni nzuri katika mahali pa kazi pasipokuwa na ushirikiano baina ya mwajiri na watumishi itakuwa  vigumu Taasisi kutimiza malengo yake.  Hivyo pamoja na mambo mengine Baraza hili lina wajibu wa kuishauri Tume kwa lengo la kuleta tija na mshikamano baina ya mtumishi na mwajiri. Sio vizuri kwa watumishi kutumia muda mwingi katika kudai maslahi zaidi kuliko kupima kiwango cha utekelezaji wa wajibu wao.
  Moja ya kazi za Baraza ni kuhakikisha kuwa watumishi wanatekeleza wajibu wao kwanza kabla ya kudai maslahi na wanapodai maslahi wanatakiwa kufuata misingi ya sheria na taratibu zilizopo.
  Ndugu washiriki,
  Tume ya Mipango iliundwa chini ya Ofisi ya Rais kutekeleza majukumu ya msingi ambayo ni kutoa dira ya maendeleo na mwongozo wa uchumi wa taifa, kubuni na kuishauri Serikali kuhusu sera za menejimenti ya uchumi na mikakati ya maendeleo na kufanya utafiti.
  Ndugu Mwenyekiti na washiriki;
  Napenda kutumia nafasi hii kukupongeza Mwenyekiti kwa kushirikiana na wasaidizi wako na watumishi wote kwa ujumla kwa kuweza kutekeleza majukumu mliyopewa kitaifa kwa ufanisi.  Nimeelezwa kuwa pamoja na changamoto za uhaba wa rasilimali katika mwaka wa fedha 2013/14 mmeweza kutekeleza jukumu kubwa la kutayarisha Mpango wa Maendeleo wa Taifa, 2014/15 ambao uliwasilishwa katika kikao cha Bunge cha mwezi Juni 2014, pamoja na majukumu mengine ambayo ni kufuatilia utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa mwaka 2013/14 na kufanya mapitio ya utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12 – 2015/16), kusambaza machapisho mbalimbali ya Tume ya Mipango na kuandaa Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji wa Umma (Public Investment Management Manual).
  Ndugu Mwenyekiti na washiriki;
  Ni matarajio yangu kuwa kwa kuzingatia taratibu na miongozo ya Serikali, Tume ya Mipango mmepanga malengo mbalimbali ya kutekeleza katika mwaka wa 2013/14 ambapo hatimaye mtakuwa kwenye nafasi nzuri ya kuishauri Serikali katika masuala mbalimbali ya kiuchumi, kisiasa na kijamii. Kwa kusema hivi natumaini kuwa michango yenu katika mkutano huu wa siku mbili, itatoa matokeo makubwa yatakayoliwezeshaTaifa letu kusonga mbele kiuchumi.
  Ndugu Mwenyekiti na washiriki;
  Hivyo, ni matumaini yangu kuwa kwa kutumia kikao hiki kama wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi mnayo nafasi kubwa ya kuwaelimisha wafanyakazi wenzenu kuhusu umuhimu wa kila mmoja kutimiza wajibu wake katika sehemu yake ya kazi ili kufikia malengo mliojiwekea. Njia pekee ya kufikia malengo yetu ni kila mmoja kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia maadili ya utumishi wa umma ili kulitendea haki Taifa letu. Kila mmoja wetu akemee kwa sauti watumishi wasiotimiza wajibu wao. Wakuu wa Klasta, Idara na Vitengo wasimamie kwa dhati suala la maadili katika sehemu zao za kazi. Tukumbuke kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huelekeza kuwa kila mtu apate ujira unaolingana na wajibu aliotimiza.                                                                                                                                                                                                                               
  Ndugu Mwenyekiti na washiriki;
  Nimeelezwa kwamba miongoni mwa mada zitakazowasilishwa na kujadiliwa katika mkutano huu ni mafanikio ya utekelezaji wa Bajeti kwa mwaka 2013/14 na kujadili taarifa ya fedha za mwaka, elimu kuhusu magonjwa yasiyoambukiza, umuhimu wa mawasiliano serikalini na uelewa juu ya kiwango kinachopaswa kutozwa kodi ya mapato yatokanayo na ajira (mshahara).
  Ndugu Mwenyekiti na washiriki;
  Mwisho napenda kutoa shukrani kwa kuwa Mgeni Rasmi katika mkutano huu muhimu na kuwatakia majadiliano mazuri na yenye lengo la kuimarisha uhusiano mzuri kwenye Taasisi yenu.  Nihitimishe kwa kuwatakia kikao chenye mafanikio yaliyokusudiwa.
  Baada ya kusema hayo machache, napenda kutamka kwamba Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Tume ya Mipango Umefunguliwa Rasmi’!

  ASANTENI KWA KUNISIKILIZA
   


  0 0

  Neema  Herbalist  & Nutritional  Foods  Clinic ni  wauzaji  wa   dawa  mbalimbali  za  asili.   Tunayo  dawa  nzuri  ya  asili  inayo  ondoa
  kitambi  na kulifanya  tumbo  lako  kuwa  flat  kabisa  ndani  ya  siku  kumi  na  nne.
  Dawa  ni  ya  asili  kabisa " Pure  Herbal", haijachanganywa  na  kemikali  yoyote  na  haina  side  effects  kwa  mtumiaji .

  BEI  YAKE  NI  SHILINGI  ELFU  HAMSINI  TU 
   

   ( Tshs.50,000/=)

  Tunapatikana  jijini  DAR  ES  SALAAM  katika  eneo  la  CHANGANYIKENI  karibu  na  CHUO  CHA  TAKWIMU  mbele  ya  CHUO  KIKUU  CHA  DAR  ES  SALAAM.

  Kwa  wasio weza  kufika  ofisini  kwetu tunawapelekea  dawa  mahali  walipo  ( DELIVERY )

  Kwa  wateja  wa  mikoani, tunawatumia  dawa  kwa  njia  ya  mabasi, kwa  wateja  waliopo  Zanzibar tunawatumia  dawa  kwa  njia  ya  meli na  kwa  wateja  waliopo  nje  ya  Tanzania, tunawatumia  dawa  kwa  njia  ya   posta  au  DHL.

  Tunapatikana  kwa  SIMU : 0766538384.

  Kwa  maelezo zaidi  kuhusu  huduma  zetu, tembelea :


  0 0

  In the effort to bring customer care services closer to its customers in the country, ZANTEL has opened its 19th customer care shop along Samora Avenue, Dar es Salaam.The services to be offered in the new shop include SIM cards, SIM registration, Internet activation, device sales and configuration, EzyPesa and after sales support.
   
  Speaking during the inauguration of the shop, the Chairman, ZANTEL Board, Mr. Essa Al Haddad, said that, the launch was the beginning of a new journey to open a lot more in the country. ZANTEL has several shop centers in various parts of the City and that the company will continue opening as many shops as possible so as to reduce congestion in the already existing shops.cid:image001.jpg@01CFDF19.7E1474C0
  The Chairperson, Zantel Board, Mr. Essa Al Haddad
  “We want to follow customers where they are,” he said.Some of the company’s shops in Dar es Salaam are situated at, among others, Dar Airport, Kariakoo, Buguruni, Shoppers Plaza, and ZANTEL Headquarters.
  Over the few years, Zantel has been able to transform mobile communication in Tanzania by introducing various innovative platforms which have tremendously improved lives of Tanzanians and therefore looking for ways of bringing services closer to the people so as to evade crowding and loss of time.

  Zantel’s Corporate Solutions Director, Mr. Ahmed Seif Mohamed promised customers of more innovations and quality services.cid:image008.jpg@01CFDF1E.03CEA140
  The Chairperson, Zantel Board, Mr. Essa Al Haddad (left) exchanging views with the company’s Executive Director, Mr. Pratap Ghose (center) and the Director of Sales at Zantel, Mr. Sukhwinder Bajwa (in suit) during the inauguration of a new Zantel shop along Samora Avenue in Dar es Salaam yesterday.cid:image002.jpg@01CFDF19.7E1474C0
  ZANTEL team poses for a group photo after the launch.
  cid:image003.jpg@01CFDF19.7E1474C0
  The Chairperson, Zantel Board, Mr. Essa Al Haddad (center) going around the shop with Manager, Customer Care, Ms. Yasmeen Ismael (right) and the Supervisor, Samora Shop, Mr. Yassini Makwaruzo (left) during the inauguration of a new Zantel shop along Samora Avenue in Dar es Salaam yesterday.
  cid:image011.jpg@01CFDF1E.03CEA140
  Customers as were captured at the shop yesterday being serviced.
  cid:image014.jpg@01CFDF1E.03CEA140
  The Chairperson, Zantel Board, Mr. Essa Al Haddad (center) giving a hand of applause to the Flash Mob (not in picture) during their performance. Looking on is Etisalat Group, Chief Procurement Officer, Mr. Obaid Bokisha (right) and Director, Customer Experience, Mr. Gabriel Kamukara (left)

  cid:image004.jpg@01CFDF19.7E1474C0
  cid:image005.jpg@01CFDF19.E687A720
   The two photos above are Flash Mob Dancers as shot at the inauguration ceremony of the ZANTEL Samora Shop

  0 0

  Mkuu wa Mkoa Mstaafu wa Mbeya Mh. Johm Mwakangale ambaye ndiye Mgeni Rasmi katika Mkutano wa wahitimu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE)  wanaoishi nyanda za Juu kusini waliowahi kusoma katika chuo hicho kuanzia mwaka 1965-2014 na yeye akiwa ni mmoja wa wanafunzi ambaye alisoma katika chuo hicho mwaka 1967 na ambaye pia alikuwa ni Mkufunzi katika chuo hiki na Mlezi wa Umoja wa wana CBE waishio nyanda za juu kusini.

  Akitoa hotuba yake ambapo, alikishukuru chuo cha CBE kwa kufanya mkutano huu muhimu wa kuwaalika wahitimu wote kukutana pamoja pia aliongeza kuwa CBE ni chuo cha Kuigwa kwa sababu hata Viongozi baadhi yao Tanzania wamesoma katika Chuo hicho mfano Omar Kingi Mhasibu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Stagomena Tax Katibu Mtendaji SADC, Harry Katillya aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Suzan Kaganda-RPC Tabora, Dkt. Ramadhani Dau Mkurugenzi Mtendaji NSSF na Graciano Kanzugala Mwenyekiti wa TCCIA kanda za nyanda za juu Kusini .

   Alimalizia kwa Kuzindua umoja huo wa wanafunzi na kusema CBE ni chuo ambacho kimezalisha wataalam wengi . Mwisho alizindua Rasmi Umoja wa wana CBE waishio nyanda za Juu kusini mkutano uliofanyika Tarehe 4.10.2014
   Mkuu wa Mkoa Mstaafu wa Mbeya Mh. John Mwakipesile akisaini kitabu cha wageni wakati akiingia katika Mkutano huo
  Meza kuu
   Muongozaji wa Mkutano MC Bwana Ben akiwa anatoa Muongozo wakati wa Mkutano huo 
   Mkuu  wa Chuo Cha Elimu ya Biashara Kampasi ya Mbeya Ndugu Deonise Lwanga akitoa utambulisho pamoja na Kumkaribisha Mkuu wa Vyuo vyote vya CBE Tanzania.
   Mkuu wa Vyuo vyote vya Elimu ya Biashara (CBE ) Profesa Emmanuel Mjema akitoa nasaha zake na kueleza malengo makuu ya Mkutano huo, alieleza kuwa wanafunzi waliowahi kusoma katika Chuo cha CBE kuwa ni Mabalozi wazuri ambao ndio wanaweza kukitangaza vyema chuo hicho kwa kuwa wao ndio wanajua vyema chuo hicho, aliongeza kuwa wanafunzi waliowahi kusoma katika Chuo cha CBE wanasaidia chuo kwa kutoa mrejesho wa chuo hicho,pia inasadia katika Elimu, na aliongeza kuwa Alumni ni muhimu katika maswala ya kuandaa Semina, Makongamano na mambo kama hayo, Mwisho Alimshukuru Mgeni Rasmi kwa kukubali mwaliko na kujumuika katika Mkutano huo pamoja na wanachuo wote waliowahi kusoma katika chuo cha CBE
  Makamu Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) , Mipango, Fredha na Utawala Dkt. Peter Msami akitoa Salamu za Shukurani kwa niaba ya chuo cha CBE
   Mkurugenzi wa Fedha wa Chuo cha CBE Bwana John Mwangobola akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa Mkutano huo.
  Mwenyekiti wa kwanza wa Umoja wa wana CBE waishio Nyanda za juu Kusini ambao umezinduliwa Rasmi Tarehe 04.10.2014 Bwana Boyd Faustin Mwakyusa akitoa neno la Shukurani Baada ya uteuzi huo
  Msimamizi wa Taaluma kutoka Chuo cha CBE Kampasi ya Mbeya Bwana Kayombo akizungumza jambo wakati wa Mkutano huo
   Viongozi wa kwanza wa Umoja wa wana CBE waishio nyanda za Juu Kusini wakiwa pamoja na Mlezi wao Mkuu wa Mkoa Mstaafu wa Mbeya Mh. John Mwakipesile wa nne Kutoka Kushoto Mara baada ya Uchaguzi huo
   Washiriki wakiwa wanafuatilia Mkutano kwa umakini.
  Picha ya Pamoja
  0 0

  Irene Neema Vedastous 'La Veda', Mshiriki wa Big Brother Hotshots kutoka Tanzania.

  IRENE NEEMA VEDASTOUS ni msichana mrembo wa Kitanzania, mwenye umri wa miaka 23 anayeiwakilisha Tanzania katika shindano la BIG BROTHER 2014 ‘HOTSHOTS’ nchini Afrika Kusini.
  La Veda katika pozi na baadhi ya mastaa.
  Mrembo huyu ambaye ameshawahi kuingia 10 bora ya shindano la Miss Tanzania mwaka 2012, baada ya kutwaa taji la Miss Lindi 2012, anaingia rasmi leo tarehe 5 Oktoba 2014 kwenye shindano hilo lenye mashabiki
  wengi duniani ambalo kuanzia saa 1 jioni litakua likirushwa live kupitia DSTV kwenye channel no. 198.

  Irene Neema Vedastous aka Irene La Veda ni nani?
  Irene La Veda, sio mrembo mpya kwenye jamii ya Watanzania kama wengi wanavyodhani, ni mrembo anayependa kujichanganya na watu mbalimbali. Hii hali imemuwezesha kufanya vitu mbalimbali na
  vikubwa kwenye fani mbalimbali kama filamu, muziki, urembo, mitindo, nk.
  FILAMU (BONGO MOVIES): Amecheza filamu mbalimbali ambazo nyingine zipo sokoni na nyingine bado hazijaingia mfano; KITENDAWILI, aliyofanya na msanii Rich Rich tayari ipo sokoni, LOVE IN A MESS 
  aliyocheza na Msungu. Mrembo huyo, pia amecheza filamu na magwiji kama King Majuto, Mzee Magali, Hashimu Kambi na Mzee Chilo ambapo filamu hizo walizocheza zitaingia sokoni hivi karibuni na zote
  La Veda amecheza kama mhusika mkuu ‘Main Character’.
  La Veda akiwa kazini.
  MUZIKI: Kwa upande wa muziki, La Veda ni mkali sana wa kucheza na tarumbeta. Hii ni nadra sana kukutana na mwanamuziki ambaye anauwezo wa kupiga kifaa japo kimoja cha muziki.
  Mrembo La Veda sio tu mkali wa kupuliza tarumbeta bali ameshatoa vibao mbalimbali kama UTANIMISS, SIMPLE LOVE, LET IT GO, na kibao kikali kinachotamba kwenye mitandao mbalimbali, kibao
  ambacho kinaitangaza Tanzania katika sekta ya utalii kiitwacho TWENDE TUKATALII , Video ya wimbo huu inapatikana You tube.
  Video ya wimbo wa La Veda, Twende Tukatalii.
  UCHEZAJI DANSI: Mshiriki huyo ni dansa mzuri na umahiri wake tayari ameuonyesha katika video zake alizofanya pamoja na kazi nyingine za muziki alizofanya hapa Tanzania na nje ya nchi zikiwemo Uswiss na Ufaransa.

  MITINDO NA UREMBO: Licha ya kuwa Miss Lindi 2012, La Veda ni mwanamitindo ambaye tayari ameshafanya 'events' mbalimbali za mitindo mojawapo ikienda kwa jina LA VEDA SHOW.

  Irene La Veda ambaye hasiti kusema 'Role Model' wake ni Mama yake Mzazi, moja ya mipango yake ni kuona anafika mbali kisanaa, hivyo aliamua kwenda kukaa darasani kwenye Chuo Cha Sanaa
  Bagamoyo mwaka 2012 kuongeza ujuzi na utaalamu katika fani hiyo.
  La Veda (wa kwanza kulia) akiwa na baadhi ya washiriki wa Miss Tanzania 2012.
  Mama Mzazi wa La Veda, Mecky Sebastian anasemaje kuhusu mwanaye kushiriki Big Brother Hotshots? msikie hapa;

  "Naomba akina mama wenzangu, wasanii na Watanzania wote kwa ujumla mnisaidie katika kumuunga mkono La Veda ili aweze kuiletea heshima nchi yetu na yeyote popote alipo mwenye kuitakia mema .

  Tanzania na Afrika Mashariki tumpe ‘support’ ya kutosha ili aweze kuibuka mshindi. Nawatakia Watanzania kila la kheri kwenye shughuli zao za maendeleo", alisema Mama Mzazi wa La Veda, Mecky
  Sebastian.

  0 0

   Wanamichezo wa Wizara wa Mambo ya Ndani ya Nchi wakimshangilia Alavuya Ntalima baada ya kushiriki mbio za Kilomita 32 za Baiskeli wanawake kutoka Kijiji cha Melela Mlandizi hadi Rombo mjini Morogoro. Timu 12 za Baiskeli za Shirikisho za Michezo ya Wizara na Taasisi za Serikali (SHIMIWI) zilishiriki katika mbio hizo leo. Hata hivyo, Timu za mpira wa miguu, Kamba wanaume na wanawake na Netball zimeingia katika kundi la 16 Bora huku Timu ya mchezo wa riadha mita 100 ya wizara hiyo imeingia fainali. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

   Wanamichezo wa Wizara wa Mambo ya Ndani ya Nchi wakimshangilia Alavuya Ntalima baada ya kushiriki mbio za Kilomita 32 za Baiskeli wanawake kutoka Kijiji cha Melela Mlandizi hadi Rombo mjini Morogoro. Timu 12 za Baiskeli za Shirikisho za Michezo ya Wizara na Taasisi za Serikali  (SHIMIWI) zilishiriki katika mbio hizo leo. Hata hivyo, Timu za mpira wa miguu, Kamba wanaume na wanawake na Netball zimeingia katika kundi la 16 Bora huku Timu ya mchezo wa riadha mita 100 ya wizara hiyo imeingia fainali. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

   Mshiriki wa mbio za Baiskeli wanawake, Alavuya Ntalima akishangiliwa na wanamichezo wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakati alipokuwa anawasili baada ya kushiriki mbio za Kilomita 32 za Baiskeli kutoka Kijiji cha Melela Mlandizi hadi Rombo mjini Morogoro. Timu 12 za Baiskeli za Shirikisho za Michezo ya Wizara na Taasisi za Serikali  (SHIMIWI) zilishiriki katika mbio hizo leo. Hata hivyo, Timu za mpira wa miguu, Kamba wanaume na wanawake na Netball zimeingia katika kundi la 16 Bora huku Timu ya mchezo wa riadha mita 100 ya wizara hiyo imeingia fainali. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani.
   Wanamichezo wa Wizara wa Mambo ya Ndani ya Nchi wakimshangilia Cosmas Peter (aliyevaa kofia) baada ya kushiriki mbio za Kilomita 50 za Baiskeli kundi la wanaume kutoka Kijiji cha Melela Njia Panda ya Msata hadi Rombo mjini Morogoro. Timu 19 za Baiskeli za Shirikisho za Michezo ya Wizara na Taasisi za Serikali  (SHIMIWI) zilishiriki katika mbio hizo leo. Hata hivyo, Timu za mpira wa miguu, Kamba wanaume na wanawake, Netball zimeingia katika kundi la 16 Bora huku Timu ya mchezo wa riadha mita 100 ya wizara hiyo imeingia fainali. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Wanamichezo wa Wizara wa Mambo ya Ndani ya Nchi wakimnyoosha misuli Cosmas Peter baada ya kushiriki mbio za Kilomita 50 za Baiskeli kundi la wanaume kutoka Kijiji cha Melela Njia Panda ya Msata hadi Rombo mjini Morogoro. Timu 19 za Baiskeli za Shirikisho za Michezo ya Wizara na Taasisi za Serikali (SHIMIWI) zilishiriki katika mbio hizo leo. Hata hivyo, Timu za Mpira wa Miguu, Kamba wanaume na wanawake na Netball zimeingia katika kundi la 16 Bora huku Timu ya mchezo wa riadha mita 100 ya wizara hiyo imeingia fainali. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0

  Bendi maarufu ya Muziki wa dansi Ngoma Africa Band aka FFU-Ughaibuni yenye makao yake nchini Ujerumani, inawapa mkono wa Eid El Hajj wadau na wapenzi wote wa Ngoma Africa band popote walipo.
  Ngoma Africa Band inawatakia siku kuu njema ya Eid tusherehekee sote kwa Amani na Upendo.

  Pia usikose kupata burudani kamili ya muziki at  www.ngoma-africa.com

  0 0

  Timu ya soka ya Uhamiaji kabla ya kuanza kwa mchezo dhidi yake na timu ya soka ya Ikulu (haipo pichani) katika mchezo wa mtoano wa SHIMIWI uliofanyika uwanja wa Morogoro Sec. mjini Morogoro leo.
  Timu ya soka ya Ikulu ikifanya mazoezi mepesi kabla ya kuanza kwa mechi dhidi yake na timu ya soka ya Uhamiaji (haipo pichani) katika mchezo wa mtoano wa SHIMIWI uliofanyika uwanja wa Morogoro Sec.mjini Morogoro leo.(Picha zote na Happiness Shayo)

  Na Happiness Shayo-Morogoro

  Timu ya soka ya Uhamiaji imeweka historia katika michezo ya SHIMIWI baada ya kuifunga timu ya soka ya Ikulu bao moja kwa bila katika mchezo wa mtoano uliofanyika viwanja vya Morogoro Sec. mjini Morogoro na hivyo kuitoa timu hiyo ya Ikulu katika mashindano ya SHIMIWI.

  Mchezo huo wa aina yake uliochezwa kwa vipindi viwili vya dakika thelathini ulianza kwa kasi huku timu ya Ikulu ikijitahidi kushambulia lango la Uhamiaji kupitia mshambuliaji wake Salehe Hamad bila mafanikio.

  Ikulu ambayo inaongoza kwa kunyakua kombe la soka la SHIMIWI kwa mfululizo ilishindwa kufunga bao katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo hivyo hadi timu hizo zinaenda mapumziko hakuna aliyemfunga mwenzake.

  Uhamiaji iliyokuwa imeangukia kundi la wafungwa bora kwa kupata pointi 4 katika michezo ya SHIMIWI ilijitoa kimasomaso katika kipindi cha pili cha mchezo huo baada ya mshambuaji wake Edward Dafe kufunga bao la kufuta machozi lililoiingiza timu hiyo katika 16 bora.

  Goli hilo la Uhamiaji lilileta changamoto kwa wachezaji wa Ikulu ambao mda wote walipania kunyakua ushindi na kupelekea kucheza rafu hadi kumjeruhi kipa wa Uhamiaji Josia Steven ambaye aliendelea na mchezo baada ya kupewa huduma ya kwanza.

  Akiongelea mchezo huo Katibu wa timu ya Uhamiaji Bw.Richard Mwasongwe alisema kuwa mchezo ulikuwa mgumu kwa timu yake lakini jitihada binafsi zimepelekea kuwa na matokeo mazuri. “Mchezo huu ni mgumu sana lakini timu yangu imejitahidi kadri iwezekanyavyo kufanya vizuri” alisema.

  Kwa upande wa timu ya Ikulu, ilishindwa kutoa ushirikiano wa kuelezea hali halisi ya mchezo huo na badala yake kuondoka uwanjani kwa majonzi.

  Timu za soka zilizoingia 16 bora zitaingia dimbani Oktoba 6 ambapo watakaofanikiwa kupita katika hatua hiyo wataingia robo fainali ya mashindano ya SHIMIWI.


  0 0

  *Yanahitajika madawati 99,204 kwa shule zote za msingi

  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameutaka uongozi wa mkoa wa Kagera ulichukulie suala la upungufu wa madawati kwa uzito ule ule kama ilivyo kwenye suala la ujenzi wa maabara katika shule za sekondari.

  Ametoa wito huo jana usiku (Jumamosi, Oktoba 5, 2014) wakati akizungumza na viongozi na watendaji wa Serikali wa mkoa huo mara baada ya kupokea taarifa ya mkoa huo iliyowasilishwa kwake na Mkuu wa Mkoa huo, Kanali (Mst) Fabian Massawe.

  Waziri Mkuu aliwasili Bukoba jana jioni akitokea Dodoma ili kumwakilisha Rais Jakaya Kikwete kwenye maadhimisho ya Siku ya Walimu Duniani ambayo kitaifa yanafanyika mkoani Kagera.

  “Kwenye ujenzi wa maabara naona mnafanya vizuri lakini nataka kwa uzito uleule tusimamie suala la upungufu wa madawati. Tuunganishe nguvu za wananchi wa kawaida na za Serikali za Mitaa ili kuondoa kabisa tatizo hili mkoani mwenu,” alisema.

  “RC hapa kasema kuna kata moja huko Bugandika kuna maprofesa 40. Huwezi kuwa na Maprofesa wote hao halafu kwenye shule wanakotoka maprofesa hao eti watoto wanakaa chini, haiwezekani!” alisisitiza.

  Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Katibu Tawala wa mkoa huo, mkoa wa Kagera unahitaji madawati 238,080 kwa shule zote za msingi ambapo yaliyopo ni 138,876 na upungufu ni madawati 99,204. Kwa shule za sekondari, mkoa unahitaji viti 84,344, vilivyopo ni 82,275 na pungufu ni 2,069 wakati mahitaji ya meza ni 84,344; zilizopo ni 73,615 na upungufu ni 10,729.  


  Aliwataka viongozi wa mkoa huo watafute mbinu za kukuza kipato cha wananchi wanaowaongoza kama njia mojawapo ya kuwasaidia wananchi wao kujikwamua kiuchumi. “Kwanza jiulize pato la mkoa likoje na limeongezeka kiasi gani? Je hali ya watu wangu ikoje? Nifanye nini ili niweze kuwaondoa hapo walipo na kuwafikisha katika kiwango kingine cha maendeleo?” alisisitiza.

  Alisema kama kila kiongozi atadhamiria kupambana na umaskini wa kipato wa wananchi, ni dhahiri kuwa kazi ya kuondoa maadui wengine ambao ni maradhi na ujinga itakuwa rahisi mno.

  Mapema, akiwasilisha taarifa ya mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali (Mst) Fabian Massawe alisema mkoa huo unahitaji kujenga maabara 570 ambapo zilizopo ni 136 wakati zingine 434 ziko katika hatua mbalimbali za ujenzi. Alisema mkoa unatumia maabara zinazohamishika (mobile labs) ambazo zipo 35.

  Aliosema mkoa huo pia unazo hosteli za wananfunzi 84 na unahitaji kujenga hosteli nyingine 212 ili kuwasaidia watoto wa kike waweze kuhitimu masomo yao.

  Akizungumzia hali ya ulinzi na usalama mkoani humo, Kanali Massawe alisema kati ya Desemba 2013 na Septemba 2014, jumla ya wahamiaji haramu 1,589 kutoka nchi jirani za Burundi, Rwanda Uganda na DRC wameondoshwa nchini na wengine 231 waliondoka kwa hiari ikiwa ni utekelezaji wa Operesheni Kimbunga Endelevu.

  “Katika operesheni Kimbunga ya awali wahamiaji 25,258 waliondolewa nchini ikiwa ni sawa na asilimia 48 ya wahamiaji wote 50,520 wanaokadiriwa kuwepo mkoani Kagera. Tangu wakati huo, tumeendelea na misako kwenye mabasi, maeneo ya starehe, nyumba za kulala wageni, viwandani, mashambani, taasisi za elimu, taasisi za madhehebu ya kidini, vipenyo na vijiji vya mpakani.”

  “Kuanzia Januari hadi Septemba mwaka huu, jumla ya watu 572 walikamatwa na kufikishwa mahakamani au kufukuzwa nchini (PI). Walioshtakiwa walikuwa ni 431 na kuhukumiwa vifungo ama kutozwa faini na wahamiaji 231 walifukuzwa nchini kwa PI,” alifafanua.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU
  DAR ES SALAAM.
  JUMAPILI, OKTOBA 5, 2014

  0 0
 • 10/05/14--07:51: Maafali ya 36 ya NBAA yafana
 •  Baadhi ya wahitimu wa NBAA wakiwa katika maandamano ya kitaaluma wakati wa maafali ya 36 yaliyofanyika katika kituo cha NBAA Mbweni jijini Dar es Salaam jana ambapo jumla ya wahitimu 855 walipata Degrii ya juu ya uhasibu (CPA) na wahitimu 82 walitunukiwa cheti cha utunzaji wa hesabu (ATEC.)
   Mkurugenzi wa Bodi ya NBAA Bw. Pius Maneno akitoa hotuba fupi kabla yakumkaribisha mgeni rasmi wakati wa maafali ya 36 yaliyofanyika katika kituo cha NBAA Mbweni jijini Dar es Salaam jana.
   Mgeni rasmi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Viwanda  Mhe. Janeth Mbene akiongea na wahitimu (hawapo pichani) wakati wa maafali ya 36 yaliyofanyika katika kituo cha NBAA Mbweni jijini Dar es Salaam jana.
   Baadhi ya wahitimu wa NBAA wakifuatili kwa makini matukio yaliyokua yakiendelea wakati wa maafali ya 36 yaliyofanyika katika kituo cha NBAA Mbweni jijini Dar es Salaam jana ambapo jumla ya wahitimu 855 walipata CPA na wahitimu 82 walipata cheti cha utunzaji wa hesabu.
  Kikundi cha ngoma kutoka JKT Mbweni kikitumbuiza wakati wa maafali ya 36 yaliyofanyika katika kituo cha NBAA Mbweni jijini Dar es Salaam jana.
  Picha na: Genofeva Matemu - Maelezo.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiungana na waumini wa dini ya Kiislamu katika swala ya Sikukuu ya Eid El- Hajim iliyoswaliwa katika Msikiti wa Istiqaama, jijini Dar es Salaam, leo. Wa pili (kulia) ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashid.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib  Bilal, akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu baada ya kushiriki swala ya Sikukuu ya Eid El- Hajim iliyoswaliwa katika Msikiti wa Istiqaama, jijini Dar es Salaam, leo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib  Bilal, akiagana na waumini wa dini ya Kiislamu baada ya kushiriki nao katika swala ya Sikukuu ya Eid El- Haji iliyoswaliwa katika Msikiti wa Istiqaama. Picha na OMR

  0 0


  Mashabiki wa Yanga wakifuatilia mchezo huo.

  Jaja akitafuta mbinu za kuwatoka wachezaji wa JKT Ruvu.

  Jaja akichuana na beki wa JKT RUVU, Madenge Ramadhani.

  Jaja akichuana na beki wa JKT RUVU, Madenge Ramadhani.

  Mashabiki wa Yanga wakiishangilia timu yao.   Edward Manyama akimtoka beki wa JKT Ruvu, Madenge Ramadhani.

   Kipa wa JKT Ruvu, Jackson Chove akiruka juu kuokoa hatari langoni mwake.

  Mohamed Faki akimiliki mpira mbele ya mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima.


  Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao lililofungwa na Kelvin Yondani katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)

  0 0

  Mrisho Mpoto akimkabidhi kifaa cha kupimia magari mmoja wa wakazi wa Dodoma Beatrice Chilewa (kulia), muda mfupi baada ya kujishindia moja ya swali lililoulizwa na msemaji wa GS1, Pius Mikongoti, ambalo lilikuwa likimtaka ataje nchi tatu za Kusini mwa Jangwa la Sahara zinazotoa Barcode na namba za utambulisho wa nchi hizo, wa kwanza kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa kampuni ya Josekazi Auto Garage ambaye ndiye mmiliki wa kifaa hicho cha kupimia magari.
  MKURUGENZI wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group Ruge Mutahaba,(wanne kushoto) akiongea na baaddhi ya wakazi wa Dodoma mjini (hawapo pichani) waliohudhuria Semina ya Kamata Fursa ndani ya Ukumbi wa Royal Village mapema jana,ambapo aliwaeleza wakazi hao namna ya kuwapatia mbinu mbalimbali za kujikwamua kupitia rasilimali zilizopo ndani ya mkoa huo wa Dodoma.
  Msemaji kutoka GS1, Pius Mikongoti akiwalezea wakzi wa Dodoma namna ya  kunufaika kupitia huduma zitolewazo na GS1, hasa katika mfumo wa kutumia Barcode. 
  Msanii wa kughani Mashairi Mrisho Mpoto akiwapa historia yake ya mafanikio na namna alivyoweza kutumia fursa hadi kufikia hapo alipo kwa sasa.
  Afisa Utekelezaji na mipango wa NSSF Ally Mkulemba akitoa semina kwa wakazi wa Dodoma, huku akiwapa mbinu za kutumia fursa katika kusongesha mafanikio kupitia mikopo mbalimbali itolewayo na Shirika hilo mapema jana ndani ya Ukumbi wa Royal Village.
  Sehemu ya watu waliojitokeza kwenye Semina ya Kamata Fursa iliyokuwa ikifanyika ndani ya Ukumbi wa Royal Village,mjini Dodoma hapo jana.


  0 0


  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei (wa tatu kushoto) akimkabidhi sehemu ya vifaa vya michezo Mwenyekiti wa Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum kwa ajili ya mechi ya viongozi wa Kamati ya Amani na Ushirikiano inayowaunganisha viongozi wa dini zote itakayofanyika Oktoba 12 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 

  Kutoka kulia ni Mkurugenzi waMasoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa,Katibu wa Kamati hiyo, Padri John Solomon (wa pili kulia),  Mkurugenzi wa Tawi la Benki ya Kijitonyama, Lucas Busigazi (kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mchungaji George Fupe (wa pili kushoto). 

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kushoto) akijaza fomu ya kufungua akaunti ya Junior Jumbo  kwa ajili ya mtoto Daud Stephen (6) (katikati) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Wateja wa Benki iliyoanza jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles kimei akizungumza na waandishi wa habari.
  Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj Mussa Salum akionyesha jezi namba 9 atakayoitumia katika mchezo huo.
  Dk. Kimei akifurahia jambo wakati wa makabidhiano ya vifaa vya michezo kwa viongozi wa timu ya Kamati ya Amani na ushirikiano ikiwa ni maandalizi ya mechi baina ya viongozi wa madhehebu ya dini.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akitoa ufafanuuzi kwa mteja wa Benki ya CRDB kuhusu huduma mbalimbali za benki hiyo. Dk. Kimei alijumuika na wafanyakazi wa tawi la Kijitonyama katika kuwahudumia wateja wa benki hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya wateja wa Benki hiyo inayoanza Oktoba 6.
  Baadhi yawateja wakimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei baada ya kupata huduma katika tawi la Kijitonyama.
  Baadhi yawateja wakimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei baada ya kupata huduma katika tawi la Kijitonyama.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akigonga muhuri katika cheki ya mteja.
  Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akiwa na Ofisa Uhusiano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Silvia Lupembe.
  Dk. Kimei akitoa ufafanuazi kwa mmoja wa wateja waliofika katika tawi la Benki ya CRDB Kijitonyama kupata huduma.
  Dk. Kimei akimsikiliza mteja wa Benki ya CRDB tawi la Kijitonyama.
  Wateja wakipata huduma.
  Keki iliyopambwa vizuri ikisubiri kukatwa kwa ajili wateja na wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Kijitonyama ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wateja wa Benki ya CRDB.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akikata keki ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wateja wa Benki ya CRDB.
  Mteja mdogo kuliko wote wa tawi la Kijitonyama, Daud Mwakwenda (6) akilishwa keki na Dk. Kimei wakati wa hafla hiyo.
  Mkurugenzi Mkuu wa Maxcom, Juma Rajabu akilishwa keki na Dk. Kimei.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akimkabidhi maua mteja wa Benki ya CRDB aliyefika katika tawi la Kijitonyama.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akiwa katika picha ya pamoja na wateja wa Benki ya CRDB na maofisa wa benki hiyo.

  0 0


older | 1 | .... | 379 | 380 | (Page 381) | 382 | 383 | .... | 1898 | newer