Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 378 | 379 | (Page 380) | 381 | 382 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Meneja Mafao wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), James Oigo akitoa mada wakati wa kongamano la HRSTA Panorama lililowashirikisha Wakurugenzi, Mameneja na Maafisa Rasilimali Watu kutoka taasisi mbalimbali lililofanyika kwenye Hotel ya Double Tree Hilton jijini Dar es Salaam.
  Meneja Mafao wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), James Oigo akitoa mada wakati wa kongamano la HRSTA Panorama lililowashirikisha Wakurugenzi, Mameneja na Maafisa Rasilimali Watu kutoka taasisi mbalimbali lililofanyika kwenye Hotel ya Double Tree Hilton jijini Dar es Salaam.
  Meneja Mafao wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), James Oigo akitoa mada wakati wa kongamano la HRSTA Panorama lililowashirikisha Wakurugenzi, Mameneja na Maafisa Rasilimali Watu kutoka taasisi mbalimbali lililofanyika kwenye Hotel ya Double Tree Hilton jijini Dar es Salaam.
  Ofisa Mafao Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Julieth Chalamira akifafanua jambo kwa washiriki wa kongamano la HRSTA Panorama kuhusu faida za kujiunga na NSSF.
  Ofisa Uhusiano wa NSSF, Kiamba Rajabu (kushoto), akitoa maelezo ya huduma za NSSF kwa washiriki wa kongamano la HRSTA Panorama lililofanyika jijini Dar es Salaam.
  Ofisa Mafao Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Julieth Chalamira akifafanua jambo kwa washiriki wa kongamano la HRSTA Panorama kuhusu faida za kujiunga na NSSF.
  Washiriki wa kongamano hilo wakichukua vipeperushi vyenye taarifa zinazohusu mafao yanayotolewa na NSSF. Kushoto ni Ofisa Uhusiano wa NSSF, Kiamba Rajabu.
  Ofisa Uhusiano wa NSSF, Kiamba Rajabu (kushoto), akitoa maelezo ya huduma za NSSF kwa washiriki wa kongamano la HRSTA Panorama lililofanyika jijini Dar es Salaam.
  Meneja Mafao wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Meneja wa Mafao, James Oigo akitoa mada wakati wa kongamano la HRSTA Panorama lililowashirikisha Wakurugenzi, Mameneja na Maafisa Rasilimali kutoka taasisi mbalimbali na kwenye Hotel ya Double Tree Hilton jijini Dar es Salaam.
  Washiriki wa mkutano huo.
  Mmoja wa washiriki wa kongamano hilo akiuliza swali.
  Meneja Mafao wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Meneja wa Mafao, James Oigo akitoa mada wakati wa kongamano la HRSTA Panorama lililowashirikisha Wakurugenzi, Mameneja na Maafisa Rasilimali Watu kutoka taasisi mbalimbali lililofanyika kwenye Hotel ya Double Tree Hilton jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mercy Shumbusho na Gordon Oito.

  Na Mwandishi Wetu

  Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) yadhamini na kushiriki kongamano la kila mwaka lijulikanalo kama HRSTA Panorama ambalo limefanyika kwenye Hotel ya Double Tree Hilton jijini Dar es Salaam.

  Kongamano hilo ambalo hushirikisha Wakurugenzi, Mameneja na Maafisa Rasilimali Watu kutoka taasisi mbalimbali nchini lilikuwa na sehemu mbili, moja ikiwa ni maonesho yaliyofanywa na mifuko ya Hifadhi ya Jamii ikiwemo NSSF na pili ikiwa ni mijadala juu ya maendeleo na mabadiliko kwenye Hifadhi ya Jamii Tanzania.

  NSSF iliwakilishwa na Meneja wa Mafao, James Oigo kwenye mijadala iliyokuwa ikifanyika kwenye kongamano hilo.

  Katika maonesho yaliyokuwa yakiendelea NSSF iliweza kuto elimu kwa washiriki waliotembelea kwenye banda lao juu ya Mafao yatolewayo na NSSF pamoja na mipango mipya ya Hiari Scheme, Wakulima Scheme na Madini Scheme.

  0 0

   Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akifafanua jambo kwa washiriki (hawapo pichani),wa semina ya Fursa iliyofanyika mapema leo ndani ya ukumbi wa hoteli ya KBH,iliyoko nje kidogo ya mji wa Singida,ambapo watu mbalimbali wakiwemo wanavyuo walishiriki.
   Mmoja wa washiriki wa Semina ya Fursa akiuliza swali kwa Meza kuu ya watoa mada kuhusiana na mradi wa ufugaji wa kuku.
   Mwakilishi kutoka Shirika la Taifa la hifadhi ya Jamii (NSSF),Bwa.Ally Mkulemba akizungumza faida mbalimbali za kujiunga na shirika hilo la NSSF,alisema kuwa vijana wanapaswa kuamka kwa sasa na kuanza kuzichangamkia fursa zitokanazo na shirika hilo,ikiwemo mikopo,bima ya Aya na mengine kwa maendeleo na ujenzi wa maisha bora.
   Baadhi ya Washiriki wa Semina ya Kamata Fursa,Jitathimini,Jiamini,Jiongeze wakimsikiliza Msanii mahiri wa Mashairi pichani,Mrisho Mpoto,alipokuwa akizungumza ndani ya moja ya ukumbi wa hoteli ya KBH,ilioko nje kidogo ya mji wa Singida.Semina ya Fursa 2014 inaandaliwa na Waandaaji wa Tamasha la Fiesta 2014 linalotarajiwa kufanyika leo usiku ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida.
   Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya kutoka kundi la Hip hop lijulikanalo kwa jina la WEUSI,Niki wa Pili akizungumza mbele ya mamia ya washiriki wa semina ya fursa iliyofanyika katika hoteli ya KBH nje kidogo ya mjini wa Singida,Niki amewataka vijana mbalimbali kuhakikisha ndoto zao haziishii njiani na badala yake wazifanyiekazi ili kujiletea maendeleo katika maisha yao ya kila siku,pia amewataka kuitumia vyema fursa wanayoipata katika njia mbalimbali.v
   Mmoja wa washiriki wa semina ya Fursa,akiulaza swali na pia kuielezea fursa aliyonayo katika harakati za kutafuta maendeleo.
  Mkurugenzi wa kampuni ya  Automobile Garage,Joseph Msuya akifafanua jambo kuhusiana na namna alivyoaianzisha kampuni yake na kufikia hapo alipo,akitumia teknolojia za kisasa kabisa katika suala zima la ufundi wa magari,utengenezaji Viyoyozi vya magari na mambo mengine mbalimbali.
   Baadhi ya Washiriki wa Semina ya Kamata Fursa,Jitathimini,Jiamini,Jiongeze wakiwa ndani ya ukumbi wa hoteli ya KBH,iliyoko nje kidogo ya mji wa Singida wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikizungumzwa.Semina ya Fursa 2014 inaandaliwa na Waandaaji wa Tamasha la Fiesta 2014 linalotarajiwa kufanyika leo usiku ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida. 

  0 0

  MARYAM HIMID /ALI ISSA-HABARI MAELEZO.   03/10/2014.

   Vyombo vya habari nchini vimetakiwa kupiga Muziki wa Nyimbo za asili za Wasanii wa kongwe waliopita ili kuziwezesha Nyimbo hizo kukumbukwa na kutoa burudani kwa kizazi cha sasa. 

  Hayo yalisemwa leo huko Forodhani na Mkurugenzi wa Idara ya habari Maelezo Zanzibar Rafii Haji Makame wakati alipokuwa akikabidhiwa CD ya Mwana Muziki Mkongwe Nchini Salum Bend ilio tamba miaka 50 iliyopita.

   Alisema Msanii huyo alitamba sana enzi za Uhai wake hivyo kupigwa Nyimbo zake katika Vyombo vya habari ni burdani tosha kwa kizazi cha leo ambapo Vijana wataweza kujifunza hali  halisi ya muziki wake.

  “inasemekana Mwana muziki huyu alikuwa na uwezo mkubwa wakupuliza Tarumbeta na kuisikia masafa ya mbali sana kitu ambacho kilipendwa sana na watu wengi wa wakati huo”alisema Rafii.

   Aidha wakati  akipokea CD hiyo kutoka kwa Mkurugenzi wa chuo cha Music Bi Fatuma Mohamed Kiluwa, Rafii aliahidi kuisambaza CD hiyo kwenye Makumbusho na na Vituo vya Televisheni na Radio nchini. 
   
   Nae Mkuu wa Taaluma wa Chuo cha Music Profesa Mitchel Strumpf alisema chuo kimeona haja ya kutoa elimu ya muziki ili Watu waweze kujifunza, kusoma, kusikiliza na kujua tamaduni zao zikiwemo za Vyakula na Mavazi.

  ‘’Historia ya muziki ni muhimu sana kujulikanwa ili kuweza kuhifadhi kumbu kumbu za wasani wakogwe wa muziki huo kama tulivyofanya leo’ alisema Mitchel.

   Alisema ni muhimu kwa Zanzibar kuwa na Taasisi ya Muziki ambayo italeta faida kubwa kwa wanamuziki wa Zanzibar na kwa vizazi vilivyopo na vijavyo.

  CD ya Mwanamuziki huyo Mkongwe Salum Bend ilitayarishwa Afrika Kusini na kukabidhiwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar ili afanye jukumu la kuihifadhi na kuisambaza katika Vyombo vya habari nchini.

  0 0

   Afisa Mkuu Mtendaji wa Benki ya Exim Tanzania Bw. Dinesh Arora (kulia) akizungumza na uongozi wa benki hiyo (haupo pichani) wakati wa kikao cha kimkakati cha ndani kilichofanyika katika Hoteli ya Hyatt hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
   Afisa Mkuu Mtendaji wa Benki ya Exim Tanzania Bw. Dinesh Arora (katikati) akizungumza na uongozi wa benki hiyo (haupo pichani) wakati wa kikao cha kimkakati cha ndani kilichofanyika katika Hoteli ya Hyatt hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Mkuu wa Fedha Bw. Issa Hamis na Mkuu wa Matawi Bi. Agness Kaganda (kulia).
    Afisa Mkuu Mtendaji wa Benki ya Exim Tanzania Bw. Dinesh Arora (kulia) akizungumza machache na mmoja wa wafanyakazi wa benki hiyo wakati wa kikao cha kimkakati cha ndani kilichofanyika katika Hoteli ya Hyatt hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
   Afisa Mkuu Mtendaji wa Benki ya Exim Tanzania Bw. Dinesh Arora (kushoto) akizungumza machache na Mkuu wa Hazina wa benki hiyo Bw. George Shumbusho (kulia) wakati wa kikao cha kimkakati cha ndani kilichofanyika katika Hoteli ya Hyatt hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkuu wa Matawi Bi. Agness Kaganda.
   Meneja Rasilimali Watu wa Benki ya Exim Tanzania Bw. Frederick Kanga (kushoto) akizungumza na uongozi wa juu wa benki hiyo wakati wa kikao cha kimkakati cha ndani kilichofanyika katika Hoteli ya Hyatt hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

  0 0  Baadhi ya washiriki wa warsha ya kujengewa uelewa wa mpango wa kunusureu kaya maskini  unaoratibiwa na TASAF wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa TASAF kwenye ukumbi wa TEC mjini DSM.


  Mkurugenzi wa Uratibu wa TASAF,Bw. Alphonce Kyariga (aliyesimama) akifungua warsha ya kuwajengea uelewa kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga maafisa ufuatiliaji TA  wa mamlaka za utekelezaji  PAAs kwa pya kwenye ukumbi wa TEC mjini DSM.
    Baadhi ya washiriki wa warsha ya kujengewa uelewa wa mpango wa kunusureu kaya maskini  unaoratibiwa na TASAF wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa TASAF kwenye ukumbi wa TEC mjini DSM.

   Washiriki wa warsha ya siku mbili ya kujengewa uelewa wa Mpango wa  kunusuru kaya maskini  unaoratibiowa na TASAF wakiwa katika ukumbi wa TEC mjini DSM  kupata maelezo ya mpango huo kabla ya kwenye katika maeneo ya utekelezaji  katika mikoa ya Morogoro, Tanga, Mwanza, Shinyanga Na Simiyu.

   Mmoja wa wawezeshaji wa warsha ya kujen gewa uelewa maafisa ufuatiliaji wapya wa mpango wa kunusuru kaya maskini  PSSN  Bi.Woisso  kwenye ukumbi wa TEC mjini DSM .

  Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF unaanza awamu ya nne (wave 4) ya zoezi la kubaini  kaya maskini katika mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Simiyu, Morogoro, Tanga na Pwani Oktoba 6 Mwaka huu.

  Katika maandalizi hayo TASAF imeanza warsha kwa ajili ya wawezeshaji wa Kitaifa, wataalamu wa ufuatiliaji TAs na watumishi wa makao makuu (TMU) ambao watakwenda kufanya kazi kwenye maeneo ya utekelezaji wa Mradi katika mikoa hiyo.

  Akifungua warsha  hiyo kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa TASAF  Ladislaus Mwamanga, Mkurugenzi wa uratibu wa TASAF  Bw. Alphonce Kyariga amesema kazi ya utambuzi wa kaya maskini ni nyeti na inayotakiwa kufanywa kwa umakini mkubwa ili kupunguza uwezekano wa kutozibaini kaya za walengwa.

  Amessistiza kuwa miongozo na taratibu zilizowekwa na TASAF zinapaswa kufuatwa  ili hatimaye zoezi hilo liwe la mafanikio makubwa kama inavyotarajiwa.

  0 0

  Wasaniiwa muziki wa asili wakitoa burudani katika tamasha la Jambo festival.
  Mwenyekitiwa Tamasha la sanaa na utamaduni Arusha  maarufu kama JamboFerstival   Augustine Michael Namfua

  Jiji la Arusha litatikiswa na tamasha la sanaa  na utamaduni la
  kimataifa maarufu kama Jambo festival litakalojumuisha ngoma za asili,mavazi ya asili ,muziki wa asili,mavazi na vyakula  ,tamasha hilo litatikisa viunga vya jiji la Arusha ambalo ni kitovu cha utalii.

  Takribani watu 3000 kutoka sehemu mbali mbali nchini na nje ya nchi
  wanatarajia kuhudhuria tamasha hilo ambalo hutoa burudani isiyo kifani
  na lenye kila aina ya ubunifu .

  Wageni kutoka nchi za Afrika Mashariki Kenya,Rwanda,Burundi,Nchi za
  Ulaya,Marekani na Asia wanatarajia kuhudhuria huku wenyeji wao wakiwa
  ni wakazi wa Arusha.

  Mwenyekiti wa Tamasha  la Jambo Festival , Augustine Michael Namfua
  anaeleza kuwa tamasha hilo limekua likifanyika miaka 2 mfulululizo na
  kwa sasa  linasubiriwa kwa hamu kubwa na wadau wa sanaa na utamaduni.
  Augustine anaeleza kuwa kila mwaka wamekuwa wakifanya tamasha hilo
  lengo ni kuonyesha kazi za sanaa hususani tamaduni.

  Tamasha hili limekua likiwaunganisha kwa pamoja wapenzi wa sanaa na
  utamaduni wa Watu wa Arusha,Tanzania  na Afrika  kwa ujumla hasa
  ukizingatia kuwa Arusha ni makao makuu ya jumuiya ya Afrika Mashariki
  na ni mji wa utalii.


  "Katika matamasha yetu kumekuwa na uwepo wa jamii ya kimataifa ambao
  wamekuwa wakifuatilia kwa karibu matamasha kwa njia ya mtandao na hata
  kushiriki kwa wingi pia wapo wanaotuunga mkono" Alisema
  Augustine

  Mwenyekiti huyo anaeleza kuwa lengo la tamasha hilo kukuza sanaa na
  utamaduni,kukuza uchumi wa Arusha mathalani katika kipindi cha tamasha
  watu kutoka kona mbali mbali za dunia watakuja na kulala,kula na
  kununua bidhaa zinazotokana na utamaduni.
  Vikundi mbali mbali vya ngoma vitatoa burudani ya kukata na shoka
  katika tamasha hilo la aina yake.

  Wasanii kutoka nchi za Afrika Mashariki watapanda jukwaani na
  kutumbuiza mziki wa live utakaokonga nyoyo za mashabiki na wapenzi
  watakaojitokeza katika tamasha hilo ambapo kundi la Jambo Squard
  wanaotamba na nyimbo ya Mamong'o watatoa burudani.

  Wasanii wengine ni kama Santuri DJs CAB (kutoka Ufaransa), Damian
  Soul, Christian Bella,DJ Kahlil, Msafiri Zawose, Jambo Squad, Maia Von
  Lekow, Warriors from The East,Aqua Sound Band, Hisia,Jhikoman &
  Afrikabisa Band, Heart Band, G Nako kutoka WEUSI,Nash MC,
  Chaba,Shamsila.


  Pia kutakua na maonyesho ya mavazi ya kitamaduni ambapo yataandaliwa

  na wabunifu mashuhuri ambao watakuwepo ikiwamo  Ally Rehmtullah, Diana

  Magesa,Salim Ally,Martin Kadinda,Nahuja Nuhu,Neema Meena,Zakia Ally.

  Vile vile Kutakuwa na vyakula vya asili kutoka makabila mbali mbali ya

  Tanzania na Afrika Mashariki pamoja na nchi washiriki bila kusahau

  Nyama choma.
  "Arusha ni mji unaosifika kwa nyama choma katika tamasha hili
  tumejiandaa vyema watu wafike wapate nyama choma nzuri na vinywaji
  huku wakifurahia mziki wa asili unaopigwa live" Alisema
  Kwa upande wa kiingilio ni bure kwa nyakati za mchana na baada ya hapo
  jioni watatakiwa kulipa shilingi 5000 kama kiingilio  ambacho
  kinasaidia tamasha kuendesha shughuli zake.kutakuwa na sehemu mbili
  mchana na usiku.

  Tamasha la Jambo Festival litafanyika jijini Arusha katika viwanja vya
  Nane Nane vilivyopo eneo la Njiro jijini Arusha ,  litaanza siku ya
  ijumaa tarehe 3 hadi 5 octoba mwaka huu.Watu wote wanakaribishwa
  kufurahia sanaa na utamaduni ambayo ni burudani isiyo na kifani.
  Jambo Festival itapambwa na ngoma za utamaduni,muziki wa
  jukwaani,vyakula vya asili,soko za sanaa za mikono pamoja na michezo
  ya watoto.

  Tamasha hilo limedhaminiwa na Ubalozi wa Ufaransa,Kituo cha Utamaduni
  cha Ufaransa na wadhamini wengine na kuandaliwa na shirika la Idea
  Afrika.habari picha kwa hisani ya woindeshizza blog

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika majadiliano kuhusu utengamano wa Afrika na Fursa za biashara na Uwekezaji Katibu  na Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Richard Sezibera, wakati wakihojiwa na Mwandishi wa habari wa Kimataifa na Mkurugenzi wa Kampuni ya ‘Eddo Media’, Mark Eddo (kushoto).

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika majadiliano kuhusu utengamano wa Afrika na Fursa za biashara na Uwekezaji, na baadhi ya viongozi, Katibu Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Richard Sezibera (katika) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Ghana, Hanna Tetteh, wakati wakihojiwa na Mwandishi wa habari wa Kimataifa na Mkurugenzi wa Kampuni ya ‘Eddo Media’, Mark Eddo (kushoto).

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (wa nne kutoka kulia) akijumuika na baadhi ya viongozi wakati alipohudhuria Mkutano wa GBF, uliofanyika kwenye Hoteli ya Atlantis jijini Dubai.

   Baadhi ya Washiriki wa kongamano hilo kutoka Tanzania, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Nehemiah Mchechu (wa tatu kutoka kulia) akijadiliana jambo na Prof. Ahmada Ktahib kutoka Tume ya Utalii Zanzibar wakati walipohudhuria mkutano huo uliofanyika katika Hoteli ya Atlantis nchini Dubai. Picha na OMR  ======== ========= =========
  MAKAMU WA RAIS AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA KONGAMANO LA PILI LA KIMATAIFA LA BIASHARA KWA NCHI ZA AFRIKA JIJINI DUBAI
  OKTOBA 03, 2014.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Oktoba Mosi, 2014 ameiwakilisha Tanzania katika kongamano la pili la Kimataifa la Biashara kwa nchi za Afrika lililofanyika katika jiji la Dubai, Farme za Kiarabu. 

  Kongamano hili limehudhuriwa na washiriki wapatao 800 kutoka nchi mbalimbali duniani na limelenga katika kukuza uwekezaji katika nchi za Farme za Kiarabu na kufungua fursa za kibiashara barani Afrika. Kongamano la kwanza la namna hii lilifanyika pia jijini hapa  mwaka jana na kushirikisha  washiriki wapatao 3000 kutoka nchi mbalimbali duniani. 

  Baadhi ya Viongozi wa Afrika waliohudhuria kongamano hilo ni pamoja na Rais Paul Kagame wa Rwanda, Rais John Dramani Mahama wa Ghana na Rais Mulatu Teshone Watu wa Ethiopia.
   Viongozi hawa kwa nyakati tofauti walizungumzia umuhimu wa utengamano barani Afrika na wakaeleza kuwa hiyo ndiyo fimbo pekee ya kukuza uwekezaji wenye tija Afrika. 

  Pia walizungumzia mabadiliko makubwa ya Afrika huku wakiwakumbusha wawekezaji na wafanyabiashara waliohudhuria kongamano hilo kuwa Afrika ya sasa siyo bara la giza na kwamba ni bara linalokuwa kimaendeleo kwa kasi huku likiwa na fursa ya kukuza maendeleo yake kwa haraka. 


  Kongamano hili pia lilihudhuriwa na Mfalme Sheikh Mohammed Bin Rashid Al-Makhtoum ambaye alialikwa na wenyeji wa kongamano hili yaani Kituo cha Biashara cha Dubai. Sambamba na hao pia kulikuwa na wafanyabiashara wakubwa akiwemo Aliko Dangote, ambaye sambamba na kuwa na uwekezaji mkubwa katika Afrika pia anawekeza mkoani Mtwara katika ujenzi wa kiwanda kikubwa cha simenti kuliko vyote Afrika Mashariki. 

  Mfanyabiashara huyo mara baada ya mijadala ya ufunguzi wa kongamano hilo, pia alipata nafasi ya kukutana na mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Bilal na kubadilishana naye mawazo kuhusu uwekezaji wake Tanzania ambapo aligusia nia ya kutumia mkaa wa mawe uliopo Mbinga katika uzalishaji wa nishati kiwandani kwake pamoja na kutanua sekta ya usafirishaji ili kumudu kusafirisha saruji kwa matumizi ya nje ya nchi. 

  Mfanyabiashara huyo alifafanua kuwa, katika sekta ya usafirishaji pekee anatarajia kuchangia ajira zipatazo 3000 na pia anakusudia kuwapa mafunzo wafanyakazi wa kiwanda chake nchini Nigeria ili waendane na teknolojia ya sasa katika uzalishaji. 

  Uwekezaji wa Aliko Dangote katika Tanzania unatokana na nchi yetu kuwa na sera nzuri za uwekezaji na anafafanua kuwa maendeleo ya ujenzi wa kiwanda chake yanakwenda kama alivyopanga na ujenzi utakapokamilika na uzalishaji kuanza, ni wazi eneo la Kusini mwa Tanzania litaanza kubadilika kiuchumi kufuatia uwekezaji huo mkubwa.

  Mheshimiwa Makamu wa Rais akichangia katika mjadala ambao pia ulimshirikisha Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Richard Sezibera, alisema nchi za Afrika na hususani Tanzania zimepiga hatua katika kuweka mazingira ya uwekezaji licha ya kuwa changamoto ya uduni wa miundombinu na urasimu. 

  Mheshimiwa Makamu wa Rais alisema, Tanzania imeunganika katika mtandao wa barabara hivyo kwa wawekezaji ni rahisi kwao kuwekeza huku pia nchi yetu inategemea kuwa na ziada ya umeme katika miaka michache ijayo hali itakayohakikishia uhakika katika uzalishaji hasa wa viwanda vikubwa vinavyohitaji nishati kubwa ya umeme ili kuzalisha.

  Pia alisisitiza kuhusu umuhimu wa nchi za Afrika kuungana ili kurahisisha matumizi ya miundombinu sambamba na kutanua masoko katika nchi za Afrika na akaeleza kuwa Tanzania iko mstari wa mbele kuhakikisha inachangia uwezo wake katika kuhamasisha nchi kuungana kwa lengo la kukuza mahusiano, kuimarisha amani na kutanua fursa za uwekezaji.

   “Sisi Tanzania tupo katika uhusiano na nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki sambamba na zile za Kusini mwa Afrika. Ushiriki wetu katika jumuiya hizi unasaidia pia hasa sasa ambapo tunazungumzia kuweka mashirikiano na nchi za Magharibi ya Afrika na hivyo kuwa na mfumo mmoja wa biashara barani Afrika,” Mheshimiwa Makamu wa Rais anasisitiza.

  Katika hatua nyingine Mheshimiwa Makamu wa Rais alikutana na Makamu wa Rais wa Sychelles Mheshimiwa Danny Faure ambaye alimuelezea Mheshimiwa Dkt Bilal kuwa, Sychelles inakusudia kuanza safari ya ndege zake kuleta watalii Tanzania sambamba na kununua mazao ya kilimo na ufugaji na hivyo kuwa fursa mpya kwa wakulima wa mbogamboga, vitunguu na wafugaji wa ng’ombe. 

  Mheshimiwa Faure alimueleza Mheshimiwa Makamu wa Rais kuwa, uhusiano baina ya Tanzania ni Sychelles ni mkubwa na hivyo ili kuuwekea msingi imara upo umuhimu wa kushirikiana katika biashara hasa kwa bidhaa ambazo hazipatikani Sychellles. 

  Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Bilal alipokea taarifa hiyo na kumueleza Makamu wa Rais Faure kuwa, Tanzania itatoa taarifa kwa wafanyabiashara wake ili waweze kuchangamkia fursa hiyo kupitia Bodi ya Biashara za Nje (Tantrade).
  Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
  Oktoba 3, 2014 Dubai, UAE

  0 0

  Mahakama ya hakimu mkazi Kinondoni jijini Dar es Salaam imezuia kufanyika kwa tamasha lililopewa jina ‘Bang Bang Bear Fest’ lililokuwa linatarajiwa kufanyika Jumamosi hii.

  Uamuzi wa mahakama hiyo umetokana na malalamiko yaliyotolewa na Bongo5 Media Group ambao wanamiliki wazo halisi la tamasha la aina hiyo liitwalo Dar es Salaam Bear Fest.

  Kwa hali hiyo mahakama hiyo imetoa amri ya kusitishwa mara moja kwa ‘Bang Bang Bear Fest’ lililokuwa lifanyike October 4 kwenye viwanja vya Posta Kijitonyama, Dar es Salaam pamoja na kulipa hasara yoyote iliyotokana na kuingiliwa kwa haki miliki hiyo.

  0 0

  Miss Universe Tanzania 2011 Nelly Kamwelu is in New York and has started her studied in acting at the New York Film Academy . New York Film Academy-School of Film and Acting (NYFA) is a for-profit film school and acting school based in New York City. Nelly’s enrollment is part of her scholarship to the institution that she was awarded when she won the Miss Universe Tanzania title.

  Nelly Kamwelu won the Miss Universe Tanzania and Miss Southern Africa International titles in 2011. She represented Tanzania in Miss Universe 2011 in São Paulo, Brazil, Miss International 2011 in China, Miss Earth 2011 in Manila, Philippines, and Miss Tourism Queen International in China. 

  Nelly is the only beauty queen who has competed in four Grand Slam Pagents (Miss Universe, Miss International, Miss Earth and Miss Tourism Queen International) in a single year. Nelly has featured in Music Videos of Tanzanian Musicians and also recorded a song Say it to my face before her departure for Miss Universe 2011. The song was released on YouTube while she was participating in the beauty contest in São Paulo, Brazil 2011.

  New York Film Academy's programs include film directing, film producing, screenwriting, cinematography, film editing, documentary filmmaking and courses in acting. Since 2010, Miss Universe Tanzania has been sponsored by NYFA and all winners (Hellen Dausen, Nelly Kamwelu and Winfrida Dominic) have attended the Academy.

   Betty Omara, Miss Universe Tanzania 2013 will get her chance to attend the Academy once she hands over her crown this October.

  0 0

  Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kama msimamizi na mratibu wa sekta ya Sanaa nchini linapenda kutoa pongezi za dhati kwa Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nassib Abdul maarufu kama Diamond kwa kushinda tuzo ya Msanii bora wa mwezi wa kituo cha televisheni cha MTV Base kinachorusha matangazo yake kutoka Afrika Kusini na kuyafikia maeneo mengi duniani.

  Aidha, Baraza linampongeza msanii huyu na wenzake Peter Msechu na Vannessa Mdee kwa kuchaguliwa kushindania tuzo mbalimbali katika tuzo za “All Africa Music” (Afrima) ambapo nyimbo zaidi ya 2025 kutoka kwa wasanii mbalimbali barani Afrika zinatarajiwa kushindanishwa na washindi kupatikana.

  Kuteuliwa na kushinda kwa Wasanii wa Tanzania katika tuzo mbalimbali za Afrika na duniani ni ishara kwamba muziki wetu unakubalika ndani na nje ya Tanzania.

  Baraza linatoa wito kwa wasanii na wadau wote wa muziki kuzidisha ubunifu, bidii na weledi katika kazi wanazozifanya ili wasanii wengi zaidi waweze kuchomoza katika tuzo na majukwaa mbalimbali ya kimataifa kwa lengo la kulitangaza na kukuza soko la kazi zao kimataifa.

  Ni matumaini ya Baraza kwamba wasanii wataendelea kutambua umuhimu wa kufuata sheria, kanuni na taratibu za kutambuliwa na Serikali.

  Sanaa ni kazi, tuipende na kuithamini

  Godfrey Mngereza
  KAIMU KATIBU MTENDAJI

  0 0

  Kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya Viwanda na Biashara, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa Gregory Teu na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi (kulia) wakizinduwa madarasa na ofisi ya walimu katika Shule ya Msingi Msenjelele.Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa ambaye pia ni Naibu Waziri Wizara ya Viwanda na Biashara, Gregory Teu pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi (wa kwanza kulia) wakishirikiana kuzinduwa vyumba vya madarasa pamoja na ofisi za walimu katika Shule ya Msingi Msenjelele. Majengo hayo yamejengwa kwa msaada na Benki ya Posta Tanzania.Naibu Waziri Wizara ya Viwanda na Biashara, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa Gregory Teu (kushoto) akimkabidhi cheti maalum cha shukrani Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi (kulia) mara baada ya kukabidhi madarasa na ofisi ya walimu iliyojengwa kwa msaada na benki yake (TPB).Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Msingi Msenjelele walioshiriki katika hafla ya uzinduzi wa madarasa yao wakiwa katika picha ya pamoja. Nyuma yao ni sehemu ya jengo la madarasa na ofisi za walimu zilizojengwa na TPB kwa msaada.Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi (kulia) akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Shule ya Msingi Msenjelele katika hafla ya uzinduzi wa vyumba vya madarasa pamoja na ofisi Shule ya Msingi Msenjelele.Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi (wa tatu kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa, Gregory Teu (wa nne kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na wageni na wanafunzi walioshiriki hafla hiyo ya kukabidhiwa ofisi na madarasa.Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi (wa tatu kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa, Gregory Teu (wa nne kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na wageni na wanafunzi walioshiriki hafla hiyo ya kukabidhiwa ofisi na madarasa.

  0 0

  Vitabu viwili vya Eric Shigongo alivyozindua nchini Marekani juzi.
  Eric Shigongo akihojiwa na Shaka Ssali (kulia) katika kipindi cha Straight Talk Africa kabla ya uzinduzi huo.
  MKURUGENZI Mtendaji wa Global Publishers, Eric James Shigongo amezindua vitabu vyake viwili vipya vya namna ya kuondokana umaskini vyenye majina ya 10 Laws-How to Move From Poverty to Prosperity na 26 Secrets- How to Defeat From Enemies and Make Millions of Dollars.
  10 Laws-How to Move From Poverty to Prosperity.
  Shigongo alizindua vitabu hivyo vya ujasiriamali alipokuwa akihojiwa na Kituo cha Runinga cha Voice of America (Voa) kwenye Kipindi cha Straight Talk of Africa nchini Marekani juzi.
  26 Secrets- How to Defeat From Enemies and Make Millions of Dollars.
  Kwa mujibu wa Shigongo vitabu hivyo vitakuwa vikiuzwa duniani kote ili kuikomboa jamii kwenye wimbi la umaskini.

  0 0

  Kaimu Meneja Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa, Sophia Mwema akifafanua jambo kwenye mkutano maalumu ulioandaliwa na Shirika la Nyumba la Taifa wa uendelezaji mawasiliano baina ya NHC na Benki iliyoingia nazo mkataba wa kutoa mikopo ya nyumba. Mkutano huo umefanyika leo New Africa Hotel. (Picha kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii cha Shirika la Nyumba la Taifa)
   Maafisa Mawasiliano na wateja wa mabenki tofauti waliofika kwenye mkutano maalumu ulioandaliwa na Shirika la Nyumba la Taifa wa uendelezaji mawasiliano baina ya NHC na Benki iliyoingia nazo mkataba wa kutoa mikopo ya nyumba, wakifuatilia jambo.
   Watendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa wakifuatilia mkutano huo maalumu ulioandaliwa na Shirika la Nyumba la Taifa wa uendelezaji mawasiliano baina ya NHC na Benki iliyoingia nazo mkataba wa kutoa mikopo ya nyumba.
  Maafisa Mawasiliano na wateja wa mabenki tofauti waliofika kwenye mkutano maalumu ulioandaliwa na Shirika la Nyumba la Taifa wa uendelezaji mawasiliano baina ya NHC na Benki iliyoingia nazo mkataba wa kutoa mikopo ya nyumba, wakifuatilia jambo.

  Maafisa Mawasiliano na wateja wa mabenki tofauti waliofika kwenye mkutano maalumu ulioandaliwa na Shirika la Nyumba la Taifa wa uendelezaji mawasiliano baina ya NHC na Benki iliyoingia nazo mkataba wa kutoa mikopo ya nyumba, wakifuatilia jambo.
  Maafisa Mawasiliano na wateja wa mabenki wakiwasili kwenye mkutano maalumu ulioandaliwa na Shirika la Nyumba la Taifa wa uendelezaji mawasiliano baina ya NHC na Benki iliyoingia nazo mkataba wa kutoa mikopo ya nyumba, wakifuatilia jambo.
   Maafisa Mawasiliano na wateja wa mabenki tofauti waliofika kwenye mkutano maalumu ulioandaliwa na Shirika la Nyumba la Taifa wa uendelezaji mawasiliano baina ya NHC na Benki iliyoingia nazo mkataba wa kutoa mikopo ya nyumba, wakifuatilia jambo.
  Maafisa Mawasiliano na wateja wa mabenki tofauti waliofika kwenye mkutano maalumu ulioandaliwa na Shirika la Nyumba la Taifa wa uendelezaji mawasiliano baina ya NHC na Benki iliyoingia nazo mkataba wa kutoa mikopo ya nyumba, wakifuatilia jambo.
  Kaimu Meneja Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa, Sophia Mwema akifafanua jambo kwenye mkutano maalumu ulioandaliwa na Shirika la Nyumba la Taifa wa uendelezaji mawasiliano baina ya NHC na Benki iliyoingia nazo mkataba wa kutoa mikopo ya nyumba.
  Timu ya maofisa mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa kutoka kulia ni Narindwa Norbert, Olivia,, Bhoke Wambura na Salma Mwinyi, wakijadili jambo kabla ya mkutano huo kuanza.
  Maafisa Mawasiliano na wateja wa mabenki tofauti waliofika kwenye mkutano maalumu ulioandaliwa na Shirika la Nyumba la Taifa wa uendelezaji mawasiliano baina ya NHC na Benki iliyoingia nazo mkataba wa kutoa mikopo ya nyumba, wakifuatilia jambo.

  0 0

  Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), Mhandisi Kipalo Kisamfu(aliyevaa koti la kaki), na Balozi wa heshima wa Tanzania nchini Marekani na mmiliki wa Kampuni ya M/s Shumoja kutoka nchini Marekani, Robert Shumake wakisaini Mkataba wa awali wa mradi wa treni za kisasa zitakazohudumia abiria kutoka stesheni ya Dar es Salaam mpaka Pugu kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, leo asubuhi katika ofisi za Wizara ya Uchukuzi. Wanaoshuhudia na Waziri wa Uchukuzi, Dkt Harrison Mwakyembe (wan ne kutoka kulia), na wa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Shaaban Mwinjaka ( wa tatu kutoka kushoto) pamoja na wawakilishi kutoka kwa Mwanansheria Mkuu wa Serikali, Mwenyekiti wa Bodi ya TRL.
  Balozi wa heshima wa Tanzania Nchini Marekani na mmiliki wa Kampuni ya M/s Shumoja , Robert Shumake, akiwaelezea waandishi wa habari(hawapo pichani), namna treni ya mwendo kasi itakavyotengezwa baada ya utiaji saini wa Mkataba wa maelewano wa mradi wa treni za kisasa zitakazohudumia abiria kutoka stesheni ya Dar es Salaam mpaka Pugu kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, leo asubuhi katika ofisi za Wizara ya Uchukuzi.
  Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) , akisisitiza jambo wakati akiongea na Balozi wa Heshima wa Tanzania Nchini Marekani na na mmiliki wa Kampuni ya M/s Shumoja, Robert Shumake, ofisini kwake kabla ya kusaini Mkataba wa awali wa mradi wa treni za kisasa zijulikanazo kama Diesel Multiple Unit(DMU) zitakazohudumia abiria kutoka stesheni ya Dar es Salaam mpaka Pugu kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), leo asubuhi.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka (mwenye tai nyekundu), akisisitiza jambo kabla ya utiaji saini Mkataba wa awali wa mradi wa treni za kisasa zitakazohudumia abiria kutoka stesheni ya Dar es Salaam mpaka Pugu kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, leo asubuhi katika ofisi za Wizara ya Uchukuzi.
  Balozi wa heshima wa Tanzania nchini Marekani na mfanyabiashara nchini Marekani na mmiliki wa Kampuni ya M/s Shumoja, Robert Shumake akimueleza Mkurugenzi wa Huduma za Uchukuzi, Wizara ya Uchukuzi, Peter Lupatu namna treni ya mwendo kasi itakavyofanya kazi, kabla ya utiaji saini wa Mkataba wa awali wa mradi wa treni za kisasa zitakazohudumia abiria kutoka stesheni ya Dar es Salaam mpaka Pugu kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, katika ofisi za Wizara ya Uchukuzi, leo asubuhi. Treni hiyo itabeba abiria 800 mpaka 1000. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)

  0 0

   Wanachama wa Chama cha Wananchi CUF wakiwa katika msafara wa mapokezi ya Mwenyekiti wa chama hicho,Prof Ibrahim Lipumba
  Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF,Prof Ibrahim Lipumba mwenye shati jekundu na kofia nyekundu akiwapungia mkono wanachama wa chama cha CUF mara tu baada ya kufika katika ofisi za CUF Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma
   Polisi wakiwa katika ulinzi wa Prof Ibrahim Lipumba
  Naibu Mkurugenzi wa Oganaizesheni Uchaguzi na Bunge wa Chama Cha Wananchi CUF – Shaweji Mketo akiwahutubia  wakazi wa wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma,kutokufanya makosa  wakati  wauchaguzi wa serikali  za mitaa uliotangazwa  kufanyika Disemba 14 mwaka huu wahakikishe wanakipigia Chama cha Wananchi CUF
  Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF,Prof Ibrahim Lipumba akiwahutubia maelfu ya wananchi waTunduru waliojitokeza kumsikiliza katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja baraza  la Iddi Tunduru mjini. Picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0
 • 10/03/14--12:00: KINANA AWASILI TANGA MJINI
 •  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivuka na kivuko cha MV.Pangani kuelekea Wilaya ya Tanga mjini ambapo anatazamiwa kukagua miradi mbali mbali na kushiriki ujenzi wa maendeleo,wengine pichani ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (kushoto) na Mwenyekiti wa CCM Pangani Ndugu Hamis Mnegero.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi wa Pangani baada ya kuvuka na MV.Pangani
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi waliojitokeza kumuaga wakati akielekea Tanga mjni.
    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kata ya Kigombe ,Pangani ambapo  aliwaeleza lazima kuwa makini katika kuchagua viongozi wa kijiji kwani wengi wamekuwa wakiuza ardhi ya wananchi kiholela na kusababisha matatizo makubwa ya ardhi.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Tanga mjini Mh.Omari Nundu wakati wa mapokezi katika kata ya Marungu wilaya ya Tanga mjini.

   Wananchi wa kata ya Marungu wakifurahia ujio wa Katibu Mkuu wa CCM kwenye kata yao.


   Wasanii wa Tanga All Star wakionyesha ujuzi wa kuimba na kucheza wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia wakazi wa kata ya Marungu
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea kadi za wanachama wa CUF na Chadema wa kata ya Marungu walioamua kurudi CCM,zaidi ya wanachama 60 wa kata ya Marungu kutoka upinzani wamejiunga CCM .
    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi za wanachama wa CUF na Chadema wa kata ya Marungu walioamua kurudi CCM,zaidi ya wanachama 60
   Bibi Saumu Ngoma mama mzazi wa Diwani wa kata ya Marungu Ndugu Bakari Mambeya akirudisha kadi ya CUF kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  na kujiunga na  CCM.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuezeka ofisi ya CCM kata ya Marungu.
   Wazee wa kijiji cha Machui kata ya Tangasisi wakiwa kwenye mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambapo alishiriki kutoa kadi za mfuko wa afya ya jamii na kushiriki ujenzi wa nyumba ya mganga.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akiwasalimu wakazi wa kijiji cha Machui kata ya Tangasisi wilaya ya Tangamjini.
    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa nyumba ya mganga wa kijiji cha Machui katika kata ya Tangasisi
   Katibu Mkuu wa CCM akisalimiana na Wazee waasisi wa CCM Tanga mjini kwenye mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Tanga mjini.
  Mzee Athumani Makalo (wa kwanza kulia) akiwa na wazee waasisi nadi ya ukumbi wa mkutano ambapo Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Tanga mjini.

  0 0
 • 10/03/14--12:00: TAARIFA YA KIFO
 • UKOO WA MWEMA NA NKYA UNASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MAMA/DADA YAO MPENDWA BI SOPHIA RAJAB NKYA KILICHOTOKEA JANA 3/10/2014 SAA 2.45 USIKU  KATIKA HOSPITALI YA KCMC MOSHI.MAZISHI YATAFANYIKA LEO TAREHE 4/10/2014 SAA KUMI ALASIRI KATIKA MAKABURI YA MOSHI MJINI.HABARI  ZIWAFIKIE NDUGU,JAMAA NA MARAFIKI WALIOPO NDANI NA NJE YA NCHI.

  0 0

   Ilikuwa ni shangwe tu ndani ya uwanja wa Namfua wakati tamasha la Fiesta likiendelea.
   Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nyumba ya vipaji ya THT,Rachael akiwaimbisha mashabiki wake (hawapo pichani),wakati wa tamasha la Fiesta likendelea ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida hapo jana.
   Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya,Dully Sykes anaetamba na wimbo wake wa Togola akiwaimbisha mashabiki wake,kwenye tamasha la Fiesta ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida hapo jana.
   Msanii Mwana-FA na Linah wakiimba kwa pamoja wimbo wao wa Yalaiti jukwaani,huku miluzi na makelele ya mashabiki yakiwa yametawala kila kona ya uwanja wakati wa tamasha la Fiesta likiendelea.
   Wasanii mahiri wa muziki wa Bongofleva,Ney wa Mitego na Stamina wakilishambulia jukwaa kwa pamoja kupitia wimbo wao unajojulikana kwa jina la Huko kweni Vipi,ndani ya tamasha la Fiesta usiku wa kuamkia leo ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida.
   Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka kampuni ya No Fake Zone,Lina Sanga ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Oletemba,akiimba jukwaani mbele ya umati wa watu wakati wa tamasha la Fiesta lililofanyika jana katika uwanja wa Namfua,kulia ni mmoja wa wacheza shoo wake akiwajibika jukwaani.
   Kundi mahiri la muziki wa kizazi kipya litambulikalo kwa jina la Makomando wakilishambulia jukwaa la Fiesta hapo jana ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida.
   Sehemu ya umati wa watu wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye jukwaa la Fiesta ndani ya Uwanja wa Namfua hapo jana mjini Singida.


  0 0

  10311052_1940774076061511_5395068416549286320_n
  Pichani ni Zuhura Matata mgonjwa mwenye uhitaji wa upasuaji utakaofanyika nchini India.

  Kipindi cha “Mimi na Tanzania” kinachoongozwa na mrembo aliyewahi kushika taji Miss Tanzania mwaka 1999 Hoyce Temu, kinatoa shukrani kwa watanzania wote walioguswa na kufanikisha michango ya matibabu ya Zuhura Matata mwenye tatizo la kuvimba mguu ambao unahitaji Oparesheni nchini India.

  Kupitia Akaunti yake ya mtandao wa kijamii Facebook muongozaji wa kipindi hicho Hoyce Temu ameandikia ujumbe wa kuwashukuru watanzania. Soma hapa chini.
  Untitled
  Zuhura Matata ambaye tulimuombea msaada wa kwenda India kupitia kipindi cha Mimi na Tanzania, amefanikiwa kupata pesa zote shilingi milioni 15 sawa na dola elfu kumi. Ataondoka tarehe 21 Oktoba kuelekea India na kuanza Matibabu! Usikose kutazama kipindi cha Mimi na Tanzania, Jumapili, Chanel Ten kuanzia saa tatu na nusu usiku. Mimi Hoyce Temu natangaza rasmi kufunga michango kuanzia sasa kwani pesa tulizoomba tumepata zote! Asanteni Tanzania!
  10639696_1940773056061613_8215664022486093041_n
  Pichani ni Mtangazaji wa Kipindi cha "Mimi na Tanzania" Hoyce Temu alipomtembelea Zuhura Matata kwa ajili ya mahojiano.

  0 0

  KAMPUNI inayokwenda kwa jina la Wait & Watch Film Company Ltd, ipo mbioni kukamilisha filamu yake ya kwanza itakayojulikana kama ‘Lifti’ inayotengenezwa kwa umakini wa hali ya juu.
  Adam Mchomvu, mmoja  ya wasanii walioshiriki katika filamu ijulikanayo kwa jina la Lifti.

  Filamu hiyo itakuwa ya kwanza tangu kampuni hiyo iliposajiliwa kwa ajili ya kujihusisha na kazi mbalimbali za sanaa, ikiwamo filamu hapa nchini, huku ikiwa na mipango lukuki. Akizungumza leo asubuhi, jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Athuman Kilo, maarufu kama 'Dr Kilo' alisema kuwa wamejipanga imara kuteka soko la filamu hapa nchini.

  Alisema mashabiki wa filamu watapata burudani kamili pamoja na kujifunza kutoka kwenye filamu hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa inaandaliwa kwa utulivu wa hali ya juu.“Hii ni kazi ya kwanza ambayo tunaamini itaanza vyema kwasababu vichwa vimetulia na kuangalia namna gani akili zetu zinafanikisha kutoa kazi nzuri.

  “Naomba wadau wote wakae mkao wa kula kuisubiri filamu hii ambayo kwa sasa ipo katika hatua za mwisho kabisa kukamilika na itakuwa moto wa kuotea mbali,” alisema Dr Kilo. Baadhi ya watu walioshiriki katika filamu hiyo ni pamoja na Adam Mchomvu, Khamis Said, Sudi Ally ‘Akui’, Sadiki Manyeko, Jazzmin, Tatu Kingwande, Mzee Jengua na wengineo.

older | 1 | .... | 378 | 379 | (Page 380) | 381 | 382 | .... | 1897 | newer