Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46371 articles
Browse latest View live

BENKI YA CRDB YAZINDUA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

$
0
0

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka (kulia), Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay (kushoto) wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyu (kulia) akiwa na maofisa wa Benki hiyo kabla ya kuanza kwa mkutano.
Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akimkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei kuzungumza na waandishi wa habari kjuhusu Wiki ya Wateja wa Benki ya CRDB.
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya wiki ya Wateja wa Benki ya CRDB itakayoanza Oktoba 6-11.
 Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
-----------------------------------------------
WATANZANIA wametakiwa kutumia huduma za kibenki katika kukuza na kujiongezea uchumi wa maisha yao.

Rai hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei katika mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu wiki ya wateja wa benki hiyo itakayoanza Oktob 6,hadi 11,mwaka huu.Alisema wiki hiyo ni maalum kwa ajili ya kusikiliza kero mbalimbali za wateja ikiwemo kuwashukuru kwa mchango wao mkubwa.

"Azma kubwa ya maazimisho hayo ni kuwasikiliza wateja na kutimiza mahitaji yao kwa wakati ...lengo la CRDB ni kuboresha na kuinua uchumi wa kila mtanzania kupitia mikopo, kutunza na kukuza amana pamoja na kutoa ajira kwa vijana na misaada kwa jamii"alisema Dk. Kimei.

Akifafanua zaidi alisema kwa kutambua umuhimu na mchango mkubwa wa watanzania kwa CRDB, wanatumia wiki hiyo kutoa huduma bora na kusikiliza kero zao.

ERIC SHIGONGO SPEAKS ON VOA'S STRAIGHT TALK AFRICA

$
0
0
According to the Tanzanian Proverb, "A wise person will always find a way"... and so did our Straight Talk Africa Studio Guest! Tanzanian icon Eric James Shigongo, Author, Motivator, and Founder & CEO of Global Publishers & General Enterprises Ltd along with host Shaka Ssali and VOA Social Media Reporter, Mariama Diallo along with TV to Africa Producers, Paul Sisco (L) and Paul Ndiho (R).
Host Shaka Ssali and his studio guest, Eric James Shigongo. Author, Motivator, and Founder & CEO of Global Publishers & General Enterprises Ltd examine contemporary literary trends and new perspectives of publishing in Africa.

UZINDUZI WA REDIO JAMII UVINZA: MKUU WA MKOA AHIMIZA WELEDI, UADILIFU NA AMANI

$
0
0
DSC_0177
Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mwalimu Hadijah Nyembo (kulia) akitoa nasaha zake kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya (wa pili kulia) kuzungumza na wakazi wa wilaya ya Uvinza kwenye sherehe za uzinduzi wa kituo cha redio jamii Uvinza FM mkoani Kigoma. Kutoka kushoto ni Meneja wa huduma za kijamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi, Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ambao ndio wadhamini wakuu wa redio Uvinza FM, Bi. Rose Haji Mwalimu na Mkurugenzi Mtendaji wa Uvinza FM Radio Bi. Nuru Kalufya.(Picha na Zainul Mzige wa MOblog).
 
Na Mwandishi wetu, Uvinza - Kigoma
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya amesisitiza uadilifu katika vyombo vya habari jamii kwa kutangaza habari zisizoumiza hisia kwa wananchi wengine na kuepuka migogoro.
Akizindua kituo cha redio jamii cha Uvinza FM, Luteni Kanali Mstaafu Machibya alisema kuwa vyombo vina wakati mgumu hasa katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2015.

“Changamoto hii inaweza kuepukika kwa kuhakikisha habari zinazotolewa zinalenga kuendeleza utamaduni wa amani, upendo, utulivu na uvumilivu na kuepuka viashiria vinavyoweza kusambaza chuki kwa lengo la kufanikisha chaguzi salama.

Mkuu wa Mkoa huyo amesisitiza umuhimu wa kuutumia uhuru wa kutoa na kupata habari vizuri kwa kusema kwamba uhuru huo usitumike kutoa habari zinazopendelea upande mmoja na kukandamiza mwingine kwa kuwa hali kama hiyo husababisha machafuko.

“Kwa mujibu wa Ibara ya 18 (b) ya Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, kila mtu anayo haki ya kutafuta, kupokea na kutoa habari bila ya kujali mipaka ya nchi, lakini haki hiyo iende sambamba kwa kuzingatia Sheria za nchi na kuhakikisha habari hizo haziumizi hisia za wananchi wengine,”
DSC_0206
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya akisoma risala wakati wa uzinduzi wa kituo cha redio jamii Uvinza FM ambapo alilipongeza shirika la UNESCO kwa juhudi kuwaweka karibu wananchi na serikali kupitia mawasiliano ya redio.

Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya ameitaka redio jamii Uvinza kuonyesha uwezo wao ili waweze kujitangaza na kujijengea imani kwa wanajamii wao kuwa wanaweza. “Ni kwa hali hiyo tu mtaweza kujulikana, kutambulika na kupata udhamini na matangazo ya kutosha.”
Amewataka wanajamii kukitumia vyema kituo chao cha redio ili kiwe chachu ya kuleta na kukuza maendeleo katika vijiji, wilaya, mkoa na taifa kwa ujumla.

Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa ameitaka redio jamii ya Uvinza kutangaza habari zenye kuonyesha madhara ya mila potofu na kujenga uelewa wa jamii kuhusu mila hizo hususan mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), kufichua wagonjwa wanaohofia kuwa na dalili za ugonjwa wa ebola na uharibifu wa mazingira.

Amelipongeza shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kutoa msaada wa vifaa vya kituo hicho na kuendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo wanahabari jamii, Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kuruhusu matangazo ya Uvinza FM Redio yarushwe kupitia mnara wake na waanzilishi wa kituo hicho.
DSC_0120
Mwalikishi wa Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ambaye pia ni mshauri na mkufunzi wa redio jamii, Bi. Rose Haji Mwalimu akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues kwenye sherehe za uzinduzi wa kituo hicho cha redio jamii Uvinza FM uliofanyika wilayani Uvinza mkoani Kigoma.
“Ninayapongeza mashirika hayo ya Umoja wa Mataifa na Airtel kwa ufadhili wao, Ruchugi Salt Works na Asasi za kiraia (EHENA) kwa ushirikiano wao kwa jambo hili”.
 
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mwalimu Hadijah Nyembo amewakumbusha waandishi wa habari kuepuka kutangaza habari zinazoleta hofu katika jamii kwa kutangaza habari zinazotoa maelezo ya ufafanuzi kutoka chombo husika.

Amekemea matumizi ya lugha isiyo sahihi na kutoeleweka kwa wasikilizaji kwa kusema kwamba redio inalenga makundi yote ya umri kwa hiyo Matangazo yalenge wananchi wote.

“Redio Uvinza isiwe chombo cha propaganda, zingatieni mojawapo ya madhumuni ya kuanzishwa kwa redio zenu ambayo yanalenga kuhamasisha mshikamano, Amani, upendo, utulivu, umoja na utaifa, alisema Mwalimu Nyembo.”

Chombo cha habari jamii Uvinza FM Redio ni cha kwanza kuanzishwa mkoani Kigoma katika halmashauri mpya ya Uvinza.
DSC_0153
"Hongereni sana UNESCO serikali inatambua mchango wenu",...... Ni maneno ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya akimpongeza Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ambao ndio wadhamini wakuu wa redio jamii Uvinza FM, Bi. Rose Haji Mwalimu kwa niaba ya UNESCO. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Uvinza FM Radio Bi. Nuru Kalufya.
Chombo hicho kimetakiwa kutumika kuwaunganisha wanajamii, kuepuka kutangaza hisia au uvumi kwa kueleza ukweli na kuwatunzia heshima wasikilizaji wao kwa kuwa wana haki ya kuheshimiwa na kutoumbuliwa masuala yao binafsi.
Uzinduzi huo umeshuhudiwa pia na Mkuu wa wilaya ya Uvinza Mheshimiwa Mwalimu Hadijah Nyembo, viongozi wa chama na serikali, viongozi wa dini, Shirika la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Kampuni ya simu za mkononi AIRTEL, wanakijiji na wananchi wa halmashauri ya Uvinza.
Wengine ni wanahabari 30 wanaohudhuria mafunzo ya maadili, jinsia na habari za migogoro kijijini Uvinza, kutoka redio jamii za wilaya 8 ambazo ni Karagwe, Bunda, Mwanza, Kahama, Sengerema, Maswa, Simanjiro, Loliondo, Mpanda, Ngara. Kutoka Zanzibar ni Unguja North, na Southern Pemba (Pemba).
DSC_0082
Meneja wa huduma za kijamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi, akitoa salamu kwa wakazi wa wilaya ya Uvinza kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Airtel ambao wametoa udhamini wa mnara wao kurusha matangazo ya kituo cha redio jamii Uvinza FM ili kupanua wigo wa usikivu kwa redio hiyo.
DSC_0257
Mkurugenzi Mtendaji wa Uvinza FM Radio Bi. Nuru Kalufya akitoa neno la shukrani kwa mkuu wa mkoa na wadhamini wa kituo hicho cha redio jamii Uvinza FM.
DSC_0054
Meneja wa huduma za kijamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi akishiriki kutoa burudani na kikundi cha wakinamama wachimba chumvi Uvinza.
DSC_0164
Baadhi ya viongozi wa dini na jeshi la polisi waliohudhiria uzinduzi huo...Kutoka kulia ni Sheikh Mkuu wa wilaya ya Uvinza Hassan Hamisi, OCD wa Wilaya ya Uvinza S.P Nobert Mahala, Mchungaji wa SDA, Pius Mutani, Mchungaji wa EAG Uvinza, Daniel Magunge na Diwani wa kata ya Ngumka, Abdallah Masanga.
DSC_0333
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali za jamii waliokuwa wakihudhuria warsha ya siku nane iliyokuwa ikiendelea kwenye kituo cha redio jamii Uvinza FM na wakazi wa wilaya hiyo waliohdhuria sherehe za uzinduzi wa kituo hicho.
DSC_0231
DSC_0226
DSC_0264
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kituo cha redio jamii Uvinza FM chini ya ufadhili wa Shirika la UNESCO na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania. Wanaoshuhudia tukio hilo kutoka kulia ni Meneja wa huduma za kijamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi, Mwalikishi wa Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ambaye pia ni mshauri na mkufunzi wa redio jamii Bi Rose Haji Mwalimu pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Uvinza FM Radio Bi. Nuru Kalufya.
DSC_0267
Sasa kimezinduliwa rasmi.
DSC_0285
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya akifanyiwa mahojiano mafupi ndani ya studio za redio jamii Uvinza FM na Mtangazaji wa kituo hicho, Kadisilaus Simon mara baada ya kuzindua rasmi redio hiyo.
DSC_0304
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya akisaini kitabi cha wageni ndani ya studio za redio jamii Uvinza FM.
DSC_0308
Mtangazaji wa kituo cha redio jamii Uvinza FM, Kadisilaus Simon akitekeleza majukumu yake kwa furaha kabisa mara baada ya kupewa baraka na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya.

Mahakama yaiamuru SCBHK, TANESCO kutokuwabugudhi wamiliki wa IPTL

$
0
0
Katibu na Mwanasheria mkuu wa kampuni ya ufuaji umeme ya IPTL, Bw. Joseph Makandege akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) nakala ya hukumu iliyotolewa na mahakama kuu ya Tanzania ikizuia benki ya Standard Chartered ya Hong Kong na Tanesco kuendelea kuwabugudhi wamiliki wa IPTL na kuingilia uendeshaji wa mitambo yake. Kushoto ni Meneja Rasilimali watu wa IPTL Bw. Aidan Kaude. 

·         Yasema Bw. Sethi kuendelea kusimamia mitambo ya ufuaji umeme ya Tegeta.

Mahakama Kuu ya Tanzania imeiamuru Benki ya Standard Chartered ya Hong Kong na Shirika la Usambazaji Umeme Tanzania (TANESCO) kuacha kuingilia utulivu,umiliki,usimamizi na utawala wa Mitambo ya ufuaji umeme ya Bw. HarbinderSinghSethi iliyopo Tegeta, na kusubiri uamuzi wa mwisho wakesiyao ya msingi.

Kampuni ya IndependentPowerTanzaniaLimited (IPTL) na Pan AfricanPowerSolutionsLimited(PAP)zilifungua kesi kwa kuhoji uhalali wamaamuzi yaKituo cha Kimataifa chaKutatua Migogoro ya Uwekezaji(ICSID) dhidi ya Benki ya Standard Chartered ya HongKong(SCB-HK) na MarthaRenju (anaedaiwa kuwa msimamizi wa mali zake), ijulikanayo kama"Decision on Jurisdiction and liability" iliyotolewa katika kesi yaICSDnamba ARB/ 10/20.

Katika hukumu hiyo yenye kurasa 16 iliyoandikwa na Mhe.Dk.FauzTwaib(Jaji) na kusomwa kwa niaba yakena Mhe.AmriMsumiHamisi(Jaji), mahakama kuu janailiwazuiaSCBHKna / auTanescokuendelea kuwabugudhi IPTLnaPAP -zinazomilikiwa na Bw. Sethi –mpaka pale uamuzi wa mwisho wakesi yao ya msingi itakapo amuliwa.

Katika hukumu hiyo iliyotolewa na mahakama mbele ya Bw. Sethi  (mmiliki wa IPTL /PAP)naKierenDay (Mkurugenzi wa SCB-HK), Mhe. DkTwaibaliamuruTanescokutofanya biashara yoyote na SCB-HK au MarthaRenju kwa niaba ya IPTL/PAP bila ya idhini ya kimaandishi kutokaIPTL/PAP.
 
"Wadaiwa kwa pamoja wanazuiliwa kufanya utekelezaji wamaamuzi iliyotolewa katika chombo cha kimataifa yaICSDyenye namba ARB/ 10/20 na kusambazwa kwa wahusika mnamo tarehe  12 mwezi Februari mwaka 2014,kwa namna yoyoteile,na kusubiri uamuzi wa mwisho wa kesi yao ya mdai, "inasomeka sehemu ya hukumu hiyo.

Tanescoambayo iliwakilishwa naWakiliwake Bw. Urassa, pia imezuiwa kutolipakwaSCB-HK naMarthaRenjumalipo yoyote wanayostahili IPTL/PAP bila ya idhiniya maandishi kutoka kwaIPTL/PAP.
Mahakama pia imeizuia Tanescokutotekeleza aukukubaliana naaukuyatekeleza maamuzi ya ICSID, na kusubiri uamuzi wa mwisho wa kesi yao ya msingi.

JajiMhe.DkTwaibalitupilia mbali hoja ya mwanasheria wa SCB-HK,Bw.CharlesMorrison, ambaye alisema kuwa mahakama kuu ya Tanzaniahaipaswikusikiliza na kutoa maamuzi juu ya ombi hilo sababuTanzaniani mwanachama waKituo cha Kimataifa chaKutatua Migogoro ya Uwekezaji(ICSID) ambayo pia inajulikana kama Washington Convention auICSID.


Kwa mujibu wa hakimu Dr. Twaib,WakiliMorrisonalionya kuwa kamaTanzaniaaitotii wajibu huo, itajiweka sehemu mbaya katikanyanja ya kimataifa.

"Kwaheshima kubwa, nashindwa kuonamantikiya utetezi wa Bw.Morrisonnajinsi gani litaathiri mamlaka ya Mahakamahiilakuikubali ombi hili. Japokuwa Bw. Morrison amekwepa kusema moja kwa moja,maoniyake yamelenga kusema kwambamahakamahii hainamamlakaya kutoaamri husika.

"Ninashindwa kuelewa ni jinsi gani serikali ya Tanzania, ambayo si sehemu ya kesi hii, itakuwa imevunjaMkataba wa Washingtonkwa sababu tu ya wananchi wake wawili ambao ni wafanyabishara binafsi,wametafutaamriyakuzuiautekelezaji wauamuziwa ICSIDkwa misingi yaudanganyifu.Sionini jinsi gani,kwa kutumiamamlaka yakekatikakutoamaagizo hayo, mahakama hii itakuwa inaingilia majukumu ya kimataifayaTanzaniachini ya Mkataba waWashington," inasomeka hukumu ya JajiTwaib.

Sababu ya pili ya Bw. Morrison ya kuoma mahakama isikubali ombi hilo ilikuwa kwamba madai hayo yanaweza kuwa yametolewa “miaka mingi iliyopita” wakati kesi ya ICSIDilipoanzana kubainisha kuwahii ni kesi iliyokufa (tort case), ingekuwa imefanyiwa kazi ndani yamiaka mitatu yatarehe ile.

JajiTwaibalitupilia mbali hoja hiyokwa kusema, "Kwa heshima kuba kwa Bw. Morrison, hoja hii haina nguvu ya kisheria.Kamailivyosemwa na mwanasheria wawaombaji(Bw.JosephMakandegena Bw.MelkzedekLutema), madai hayo yanatoa changamotokwa uamuzi wa ICSIDambayo ulitolewa mwezi Februari,2014. Madai, hayo baada ya kushindwaAprili2014, haiwezi ukasema imepitwa na wakati. Nitaitupilia mbali pingamizi hilo.”

Kuhusu ombi kuwa shauri hilo lisikilizwe katika mahakama ya Hong Kong na fedha zote zipelekwe hiko, wanasheria wote Bw. Makandegena Bw.Lutemawalisema kuwa litakuwa sio kutenda haki kwa mteja wao, sababu kunakiasi kikubwa cha fedhakinahusika,ambayo itakuwa vigumu kuirejesha na kuwa itakuwa vigumu kwa IPTL/PAP kurejea katika hali yakekwa sababuSCB-HK niya nje na hainamalizozote kubwaTanzania.
Hii inampa Bw.Sethiushindi kwa mara nyingine miongoni mwa kesi kadhaaambazo zimekuwa zikianzishwa naSCB-HK dhidi ya IPTL/PAP.

RAIS KIKWETE AFUNGUA MAONYESHO YA KIMATAIFA YA UTALII JIJINI DAR LEO

$
0
0
 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akishirikiana na viongozi mbali mbali kukata utepe ikiwa ni ishara ya Ufunguzi wa Maonyesho ya Kimataifa ya Utalii "Swahili International Tourism Expo (SITE)" kwenye Ukumbi wa Mlimani City,Jijini Dar es Salaam leo Oktoba 2,2014.
 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa Ufunguzi wa Maonyesho ya Kimataifa ya Utalii "Swahili International Tourism Expo (SITE)" kwenye Ukumbi wa Mlimani City,Jijini Dar es Salaam leo Oktoba 2,2014.
  Sehemu ya Wageni kutoka nchi mbali mbali wakifuatilia kwa makini hotuba ya Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete  wakati wa Ufunguzi wa Maonyesho ya Kimataifa ya Utalii "Swahili International Tourism Expo (SITE)" kwenye Ukumbi wa Mlimani City,Jijini Dar es Salaam leo Oktoba 2,2014.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na viongozi wengine wakiwa kwenye picha ya pamoja baadhi Wafanyakazi wa Bodi ya Utalii Tanzania,ambao ndio waratibu wakuu wa Maonyesho hayo ya  Kimataifa ya Utalii "Swahili International Tourism Expo (SITE)" kwenye Ukumbi wa Mlimani City,Jijini Dar es Salaam leo Oktoba 2,2014. PICHA NA IKULU

GARI ZINAUZWA

$
0
0
Gari ya mwaka 2004, Honda Accord 2.0 i-VTEC Executive 4dr, automatic na manual (tiptronic), Engine Size 1998CC, Low Mileage, Silver.

Gari ya mwaka 2008 Nissan Navara, Manual, Diesel, greyish black, mileage 65,660 AC, 6 CD Changer, passenger airbag, roof bars, electric mirrors, Four wheel drive, Full Service History, Immobiliser, Navigation system, Power Assisted Steering, Trailer coupling.

Kwa mawasiliano piga simu namba 0787 622 761

MATUKIO BUNGE MAALUM LA KATIBA LEO MJINI DODOMA.

$
0
0
1
2Wajumbe wa Bunge Maalum la katiba wakishangilia leo mjini Dodoma mara baada ya matokeo ya upigaji kura kuonyesha kuwa Theluthi mbili ya Zanzibar imepatikana.
3 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Anne Makinda akitoa neno la shukurani kwa wajumbe wa Bunge la Katiba na uongozi wao pamoja na uongozi wa nchi kabla ya bunge hilo kuvunjwa rasmi leo mjini Dodoma.
4 
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, mhe. John Shibuda akitoa neno la shukurani kwa wajumbe wa Bunge la Katiba na uongozi wao pamoja na uongozi wa nchi kabla ya bunge hilo kuvunjwa rasmi leo mjini Dodoma.
5 
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. John Cheyo akitoa neno la shukurani kwa wajumbe wa Bunge la Katiba na uongozi wao pamoja na uongozi wa nchi kabla ya bunge hilo kuvunjwa rasmi leo mjini Dodoma.
6 
Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar  ambaye pia ni mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Pandu Ameir Kificho akitoa neno la shukurani kwa wajumbe wa Bunge la Katiba na uongozi wao pamoja na uongozi wa nchi kabla ya bunge hilo kuvunjwa rasmi leo mjini Dodoma.
7 
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Selemani Nchambi akitoa neno la shukurani kwa wajumbe wa Bunge la Katiba na uongozi wao pamoja na uongozi wa nchi kabla ya bunge hilo kuvunjwa rasmi leo mjini Dodoma.
8 
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Mzee Kingunge Ngombale Mwiru akitoa neno la shukurani kwa wajumbe wa Bunge la Katiba na uongozi wao pamoja na uongozi wa nchi kabla ya bunge hilo kuvunjwa rasmi leo mjini Dodoma.
10 (1)Makamu wa Pili wa Zanzibar ambaye pia alikuwa ni mjumbe wa Buge Maalum la Katiba, Mhe. Balozi Seif Ali Idd akitoa neno la shukurani kwa wajumbe wa Bunge la Katiba na uongozi wao pamoja na uongozi wa nchi kabla ya bunge hilo kuvunjwa rasmi leo mjini Dodoma.
11Aliyekuwa Makamu wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza bunge hilo mjini Dodoma wakati wa ufungaji wa bunge hilo leo 2 Septemba, 2014.
13Waziri Mkuu wa Tanzania ambaye pia alikuwa mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Mizengo Pinda akitoa akitoa neno la shukurani kwa wajumbe wa Bunge la Katiba na uongozi wao pamoja na uongozi wa nchi kabla ya bunge hilo kuvunjwa rasmi leo mjini Dodoma.
15Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta akiwashukuru wajumbe na Watanzania kabla ya kuvunja bunge hilo rsmi leo 2 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
17 (1)Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakitoa maneno ya shukurani kwa wajumbe na Watanzania kabla ya kuvunja bunge hilo rsmi leo 2 Septemba, 2014 mjini Dodoma.

USIKU WA WAKALI DAR LIVE, IDD EL HAJI


TAASISI YA COOPERATION FOR ASSISTING HANDCAPPED PEOPLE YAHITAJI TSH. BILIONI 5 KUJENGA MABWENI YA SHULE ZA KATA

$
0
0
TAASISI ya Co-Operation For Assisting Handcapped People Tanzania imepanga kukusanya kiasi cha Tsh. Bilioni 5 kwa ajili ya kufanikisha mpango wa taasisi hiyo ya kujenga mabweni ya wanafunzi wa kike na Kiume katika Shule za Sekondari za Kata Nchini.
Wilaya ya Temeke inatajwa kuwa Halmashauri ya kwanza itayoweza kunufaika na mpango huo kutokana  na ukubwa na idadi ya shule zilizopo katika eneo hilo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Alhamisi (Okt 2, 2014) Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Mhina Shengena alisema fedha hizo zitaweza kukusanywa kupitia harambee mbalimbali zitakazofanywa na Ofisi yake ndani na nje ya nchi.
Kwa  mujibu wa Shengena alisema taasisi hiyo imepanga kukusanya kiasi cha Tsh. 2400 kwa mwezi kutoka kwa kila Mtanzania pamoja na kupitia kwa waajiri na taasisi mbalimbali na mara baada ya kufanikiwa kukusanya fedha hizo, ujenzi wa makazi ya wanafunzi hao unatarajiwa kuanza mara moja.
“Wanafunzi wetu hususani wa kike wanaishi katika mazingira hatarishi sana, wapo baadhi wamepanga katika makazi ya watu mara kwa  mara tumekuwa tukisikia  matukio ya wao kubakwa na kupewa mimba, hii yote inatokana na ukosefu wa makazi ya kudumu” alisema Shengena.
Aidha Shengena aliipongeza Serikali kupitia Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa pamoja na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa msaada na ushirikiano wa karibu wanaonyesha kwao katika kufanikisha malengo ya Taasisi hiyo.
Aliongeza kuwa Ofisi yake tayari imekwishafanya mawasiliano na Watanzania mbalimbali waliopo nje ya Nchi ambao baadhi yao wameonyesha nia ya dhati ya kusaidia harambee ya ujenzi huo, ikiwemo Watanzania wanaoishi nchini Uingereza.
Akifafanua zaidi Shengena alisema kwa Watanzania walioopo nchini wanaweza kutuma michango yao katika Benki ya Posta Tanzania (TPB) katika akaunti na. 016-002156 Tawi la Kijitonyama Jijini Dar esa Salaam na kwa wale waliopo nje ya nchi watume michango hiyo katika benki ya CRDB kwa akaunti na. 01j2070153800.
Shengena alisema suluhu ya elimu bora kwa mtoto wa kike na kiume Tanzania ni ujenzi wa mabweni, na hivyo aliwataka Watanzania wote waguswe na kilio cha watoto hao ambao ni taifa la kesho.
Taasisi ya Co-Operation For Assisting Handcapped People Tanzania, ni taasisi isiyo ya kiserikali iliyoanzishwa mwaka 1998 na inajishughulisha katika kusaidia makundi ya watu wasiojiweza ikiwemo yatima, walemavu na watoto wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi.

Na Beatrice Lyimo
Maelezo
Dar es Salaam
02.Oktoba, 2014

TAMISEMI YAINYUKA WIZARA YA UJENZI 1-0 MASHINDANO YA SHIMIWI

$
0
0

Mchezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Maji (jezi ya kijani) wakipambana na mchezaji wa timu ya mpira wa miguu ya TAMISEMI (jezi ya orange) katika mashindano ya SHIMIWI yanayoendelea mkoani Morogoro.TAMISEMI iliibuka mshindi kwa bao 1-0.(Picha na Happiness Shayo-Morogoro).

KAMPENI YA HAKI YA UCHUMI KATIKA MASWALA YA KILIMO YAENDESHA MDAHALO WA KUHAMASISHA WAKULIMA WADOGO WADOGO HUSUSANI WANAWAKE.

$
0
0

 Meneja wa Kampeni haki ya Uchumi kutoka Oxfam Eluka Kibona akifungua Mdahalo huo na mafunzo juu ya Kujenga hoja ya upatikanaji wa Chakula na haki ya chakula, Kufuatilia upatikanaji wa haki kwenye Rasilimali za Ardhi na matumizi yake,na kuhamasisha uwekezaji kwa wakilima wadogo wadogo Hususani wanawake kwenye Muktadha wa mabadiliko ya Tabia nchi, katika kampeni ya GROW .
Mmoja wa washiriki wa Semina hiyo akielezea matarajio yake akiwa kama Mama shujaa wa Chakula na Mkulima mwanamke Jinsi ambavyo wameweza kusaidiwa na Oxfam kufikia malengo yao katika kilimo na kuwa wakulima Bora wenye mfano wa Kuigwa
Mshindi wa Maisha Plus 2012 Bernick Kimiro akitoa mchango wake Jinsi kilimo kinavyo weza kumsaidia mwanamke na kufikia Malengo yake.
Mshindi wa Mama shujaa wa Chakula 2014 , akiendelea kuchukua Maoni mbalimbali , Mchango na mawazo ya watu mbalimbali katika Mdahalo huo.
Oscar Munga kutoka Forum CC akitoa ufafanuzi wa kina juu ya mahusiano ya kilimo na mabadiliko ya Tabianchi, Pia alizungumzia ni namna gani watu wanaweza kujikomboka katika kilimo na kuendana na Mabadiliko ya Tabianchi.
Balozi wa Oxfam kupitia kampeni ya GROW Khadija Mwanamboka akielezea umuhimu wa kilimo bora na uwezeshaji wa wanawake katika kupata haki za Ardhi lakini pia jinsi gani Mwanamke anaweza kujikomboa katika kilimo na kuwa wanawake wanahaki sawa katika swala zima la kumiliki Ardhi.
Wa kwanza kulia ni mmoja wa aliyekuwa mshiriki wa Mama Shujaa wa Chakula 2014 kutoka Zanzibar akitoa Mchango wake kuhusu Umiliki wa Ardhi na kuelezea jinsi gani wanawake wasivyo na haki ya Ardhi hiyo, na kuomba kwamba nao ni binadamu na wanahaki sawa ya kumiliki ardhi hiyo
Wakili Joseph Chiobola ambaye ni Afisa Programu kutoka Haki Ardhi akitoa ufafanuzi wa kina juu ya haki za watu kumiliki Ardhi, pia alieleza kwa kina sababu za watu mbalimbali kugombania Ardhi na kueleza namna gani Migogoro ya Ardhi inatokea na Njia za kuimaliza Migogoro hiyo.
Mkamiti Mgawe kutoka Oxfam Akichangia Jambo katika Mdahalo huo
Afisa Ushawishi wa Ardhi kutoka Oxfam Naomi Shadrack akiendelea kutoa muongozo katika mdahalo huo.
Mchoraji Maarufu wa Katuni Muhidini Msamba akitoa mchango wake juu ya mada ambayo ilikuwa inahusu mazao kuto kuwa na thamani kuwa ndio moja ya chanzo cha wakulima waliowengi kutoka Tanzania kukosa  Masoko katika mazao yao, aliongeza ushauri kuwa kunahitajika nguvu ya ziada ili kujikwamua katika swala hilo kwa ujumla
 Mama Shujaa wa Chakula 2012 akitoa ushuhuda wake jinsi Kampeni ya Grow inayoendeshwa na Oxfam Jinsi walivyo weza kumpa Shamba ambalo mpaka sasa Linamsaidia yeye pia watu wengine kupitia elimu anayoitoa ya Shamba Darasa kwa wakazi wa eneo analoishi huko Morogoro. na kusisitiza kuwa na matumizi Bora ya Ardhi.
 Mmoja wa Washiriki Akichangia Mada juu ya rushwa kuwa ni kikwazo kikubwa sana kwa wakulima na kuwa kuna Baadhi yao wanamazao mazuri lakini kutokana na kuwa mkulima mdogo anashindwa kuuza mazao yake na badala yake anayeuza mazao hayo ni Mkulima mkubwa ambaye huweza kutoa hongo na Mazao yake kununuliwa kirahisi
Mshindi wa Shindano la Maisha Plus 2014 Boniface akitoa maelezo na kuchangia katika Mdahalo huo
Tajiel Urioh kutoka Forum CC akihitimisha Mdahalo huo
Washiriki wakiendelea kufuatilia kwa makini Mdahalo huo
 Kila mmoja akiwa makini kuhakikisha anapata Somo na kulielewa ili apate kwenda wafundisha na wengine.
 Washiriki wakiwa katika Mdahalo huo


RAIS KIKWETE AHUTUBIA KIKAO CHA KAZI KWA VIONGOZI WA MIKOA< WILAYA NA HALMASHAURI MJINI DODOMA LEO

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubuia Kikao cha KAzi kwa Viongozi wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri katika ukumbi wa Chimwaga Chuo Kikuu cha Dodoma leo Oktoba 2, 2014.
PICHA NA IKULU.

DJ STEVE JUNIOR KUTOKA KENYA ATINGA TZ KUKISANUKISHA KESHO IJUMAA VILLA PARK JIJINI MWANZA

$
0
0
Dj Maarufu wa muziki wa Reggae kutoka nchini Kenya Dj Steve Junior akitizama maadhari ya jiji la Mwanza baada ya kuwasili leo mchana kwaajili ya Tamasha la REGGAE BRING BACK LOVE litakalo fanyika kesho Ijumaa (3/oct/2014) Villa Park Mwanza.
Dj Maarufu wa muziki wa Reggae kutoka nchini Kenya Dj Steve Junior (katikati) akifanya mahojiano na G. Sengo (kushoto) katika hoteli ya JB Belmonte baada ya kuwasili leo mchana kwaajili ya Tamasha la REGGAE BRING BACK LOVE litakalo fanyika kesho Ijumaa (3/oct/2014) Villa Park Mwanza. Kulia ni Meneja wa Dj Huyo.
WAFANYABIASHARA wanao miliki vituo vya radio, television pamoja na kumbi za burudani nchini wameaswa kuwekeza katika muziki wa reggae kwa kuanzisha vituo maalum vya kupiga muziki huo na kumbi maalum za muziki huo kwani ni sekta ambayo ni fursa iliyo wazi kwa kuwa soko lake lipo si kwa vijana tu bali hata kwa watu wazima.

Hayo yamesemwa na Dj Maarufu wa muziki wa Reggae kutoka nchini Kenya Dj Steve Junior ambaye yuko jijini Mwanza katika ziara yake ya kuzitembelea nchi kadhaa barani Afrika akitoa burudani ya muziki huo na kuutambulisha uzuri wake kwa jamii kizazi na kizazi ambapo kesho (Ijumaa) kwa mara ya kwanza atakutana na mashabiki wake pale Villa Park kwenye Tamasha lake linalojulikana kama REGGAE BRING BACK LOVE.

Dj Steve Junior anasema kuwa ni kwa takribani miaka kumi sasa amewekeza katika muziki huo akiburudisha na kuufanya muziki huo kuwa sehemu ya kuendesha maisha yake, familia na jamii yake. ZAIDI BOFYA PLAY KUSIKILIZA MAHOJIANO.
Dj Maarufu wa muziki wa Reggae kutoka nchini Kenya Dj Steve Junior (katikati), Kutoka Clouds Fm G. Sengo (kushoto) katika hoteli ya JB Belmonte baada ya kumaliza mahojiano leo mchana ikiwa ni matayarisho kwaajili ya Tamasha la REGGAE BRING BACK LOVE litakalo fanyika kesho Ijumaa (3/oct/2014) Villa Park Mwanza. Kulia ni Meneja wa Dj Huyo.
Dj Maarufu wa muziki wa Reggae kutoka nchini Kenya Dj Steve Junior amefurahia sana mapokezi aliyoyapata toka kwa watanzania wakarimu.
Ni wakati wa ku-Enjoy mazingira safi na tulivu ya jiji la Mwanza yanayo nakshiwa na muonekano wa ziwa Victoria. 
100 usikose Tamasha la REGGAE BRING BACK LOVE litakalo fanyika kesho Ijumaa (3/oct/2014) Villa Park Mwanza. 
Swimming pool iliyo juu ya ghorofa...
With FrendZ...!!
Mpango mzima wa Ijumaa hii tarehe 3/oct/2014

Article 7

KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AENDELEA NA ZIARA YAKE WILAYANI PANGANII MKOANI TANGA

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikinga maji wakati wa kuzindua mradi wa maji wa kata ya Mkalamo wilaya ya Pangani mkoani Tanga.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimtwisha dumu la maji mmoja wa wakazi wa kata ya Mkalamo
 Wananchi wa Kata ya Mkalamo  wakichota maji safi na salama kwenye mradi wa maji ya kisima kilichogharimu zaidi ya shilingi milioni 29 ambacho kimefadhiliwa na hifadhi ya Taifa ya Saadani.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuchimba mtaro wa bomba la maji  wa kata ya Mkalamo wilaya ya Pangani mkoani Tanga.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua matofali ya ujenzi wa ofisi yaCCM kata ya Mkwaja.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akibeba tofali kata ya Mkwaja,Pangani mkoani Tanga.

 Popoo zikiwa zimeanikwa
 Katibu wa NEC Itkadi na Uenezi Nape Nnauye akichambua Popoo katika kijiji cha Mseko,Pangani mkoani Tanga.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kulia) akishiriki kumenya popoo pamoja na viongozi wa CCM wilaya ya Pangani
 Wahamasishaji wa Pangani wakiwa wamependeza na sare yao ya CCM

 Katibu Mkuu wa CCm Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya CCM tawi la Mseko
 Tanga ni mkoa maarufu kwa kilimo cha katani
 Sehemu ya kuanikia katatani
 Wananchi wakifuatilia mkutano wa hadhara uliofanyika Mwera
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa pangani na kuwaambia kuwa saa za kuisha kwa upinzani zimeshafika
 Kila mtu alifika uwanjani kumsikiliza Katibu Mku wa CCM Ndugu Abdulrahman  Kinana
 Viongozi wa Dini wa wilaya ya Pangani wakifuatlilia mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
 Fulana za kumkaribisha Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman  Kinana
 Mbunge wa Pangani Mh.Salehe Ahmed Pamba akihutubia wakazi wa Mwera na kuwaambia hatua walizofikia katika Jimbo la Pangani kimaendeleo,
 Muuza machungwa akiuza machungwa kwenye mkutano wa Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana
 Kamanda wa Matukio Ndugu Richard Mwaikenda akiwa  kazini kuhakikisha mikutano inapata picha
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Pangani kwenye kiwanja ch mikutano Mwera
 Wananchi wakifuatlia mkutano

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Mwera Pangani ambapo aliwaambia wasiuze ardhi kiolela kwani kuna matapeli wa ardhi
 Mwinyimkuu Nasoro Sultan akiuliza swali juu ya malipo ya mafao ya kustaafu
 Diwani wa Kata ya Ubangaya akijibu moja ya maswali kutoka wananchi

 Wachezaji walioongoza  michuano ya Mbuzi
 Beberu akiwa amebebwa juu juu
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi ya CUF iliyorudishwa na Bw. Mohamed ambaye amejiunga na CCM
 Bw. Mohamed ambaye amejiunga na CCM kutokea chama cha CUF akizungumza mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  kwenye uwanja wa mikutano Mwera wilaya ya Pangani.
Wananchi wa Mwera wakimpa mkono wa pongezi Ramadhani Rashidi aliyerejea CCM akitokea chama cha CUF

DSTV Tanzania yazindua kifurushi kipya

$
0
0
3
Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo (kulia), akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa kifurushi kipya cha DSTV Bomba.(katikati), Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania Barbara Kambogi, na kushoto ni Meneja Masoko wa Multichoice, Furaha Samalu.

KAMPUNI ya Multichoice Tanzania kupitia huduma ya DSTV imewataka wasanii kupeleka kazi zao ili waweze kutambulika nje na ndani ya nchi. Kauli hiyo imetolewa Dar es Salaam leo na Meneja Masoko wa kampuni hiyo Furaha Samalu wakati wa uzinduzi wa kifurushi kipya cha DSTV Bomba .

Alisema kifurushi hicho mahususi kwa watanzania chenye chanieli zaidi ya 65 za kitaifa na kimataifa zikiwemo za Maisha Magic Swahili inayoonesha filamu za Kiswahili, chaneli ya telemundo, chaneli ya nickelodeoni na Disney junior zinazoonesha vipindi vya watoto.
Alitaja chaneli nyingine zitakazopatikana kwenye kifurushi hicho ni Afrika magic Epic Movie, Discovery world, CBS Action, CBS reality na CBS drama pamoja na Select sport 1 na 2 kwa vipindi vya michezo.
1
Meneja Masoko wa Multichoice, Furaha Samalu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Octoba 1,2014 jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kifurushi kipya cha DSTV Bomba.

“Uzinduzi wa kifurushi hichi ni jambo la furaha na msisimko sana kwetu kuona kuwa sasawatanzania wanaweza kupata kifurushi kinachokidhi mahitaji yao.
“Kila wakati multichoice inafanya jitihada za kudumu namna ya kuwapa wateja wetu uwanja mpana wa burudani kwa uwepo wa filamu , makala, habari, vipindi vya watoto, muziki, vipindi vya dini na michezo,” alisema.

Aliongeza kuwa kifurushi hicho kitagharimu kiasi cha shilingi 17,000 kwa mwezi ambapo watakao jiunga watapata DSTV ikiwemo na gharama ya ufundi kwa shilingi 99,000 kwa kipindi maalum. Alifafanua kuwa kifurushi hicho pia kitawapa fursa watanzania kuangalia Chaneli za Super Sport select1 na 2 ambayo inatonesha ligi kuu ya Uingereza, kombe la klabu bingwa ulaya, ligi kuu ya Hispania, ligi kuu ya Ujerumani pamoja na riadha na ngumi.
2
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania Barbara Kambogi akitoa ufafanuzi kuhusiana na kifurushi hicho.
5
Waandishi wa habari wakiwa kwenye uzinduzi huo.(PICHA NA PHILEMON SOLOMON).

TWANGA PEPETA WAFANYA SHOO YA NGUVU CLUB YA MAISHA JIJINI DAR

$
0
0
  Waimbaji wa Twanga Pepeta wakitoa burudani kwenye shoo yao iliyofanyika club ya Maisha jijini Dar usiku wa kuamkia leo.
  Kiongozi na mwimbaji  wa bendi ya 'Twanga Pepeta, Luiza Mbutu akiimba  moja ya nyimbo zao kwenye shoo hiyo iliyofanyika club maisha jijini Dar.
 Mwimbaji wa bendi ya 'Twanga Pepeta, Msafiri Diouf akitoa burudani ya nguvu kwenye shoo iliyofanyika club maisha jijini dar.
Wacheza shoo wa Twanga Pepeta wakifanya ya kwao kwenye club ya Maisha jijini Dar.

WAFANYAKAZI WA UNFPA, TUSHIKAME PAMOJA FOUNDATION NA PROJECKT INSPIRE WAONYESHA UPENDO KWA WAZEE MSIMBAZI CENTRE

$
0
0
IMG_2579
Wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) hapa nchini, wadau wa Tushikamane Pamoja Foundation pamoja madaktari vijana wanaounda kundi la Projeckt Inspire chini ya mradi wa Inspire Healthy kwenye picha ya pamoja na mmoja wa wazee wanaoishi kituoni hapo.
IMG_2450
Daktari kijana Brian Mushi wa Projeckt Inspire akionyesha upendo kwa mmoja wa wazee wanaoishi kwenye kituo hicho kilichopo Msimbazi Centre mara baada ya kumpima Presha wakati wa maadhimisho ya siku ya wazee duniani.

WAZEE wanaoshi katika makazi ya Msimbazi Centre Jijini Dar es salaam karibu na kanisa la Mtakatifu Maria wa Fatma, Msimbazi walipata faraja kubwa baada ya kutembelewa na makundi matatu ya jamii.

Makundi hayo ni pamoja na wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) hapa nchini, Tushikamane Pamoja Foundation na madaktari vijana wanaounda kundi la Projeckt Inspire chini ya mradi wa Inspire Healthy. Makundi hayo yalifika katika kituo hicho katika kuadhimisha siku ya wazee duniani.

Wakiwa na lengo kuu la kuwafariji, kukagua afya zao na kuheshimu uwepo wao, makundi hayo pia yaliwapa zawadi za vyandarua, sabuni za kufulia na kuogea, pampers, Thermos Flask, vikombe vya chai, sahani za kulia, vijiko, sukari, njugu mawe, Tshirts, viatu, nguo, vyombo vya kufanyia usafi .
Pia walipiga picha za pamoja za ukumbusho.

Siku ya Wazee Duniani imetengwa kwa ajili ya kuweaenzi na pia kuwakumbuka kwa mambo waliyofanya kuendeleza kizazi cha wanadamu.
IMG_2514
Dr. Brian Mushi wa Projeckt Inspire akimpima presha mmoja wa wazee wanaoishi kwenye kituo hicho.
IMG_2523
Dr. Brian Mushi wa Projeckt Inspire akichukua vipimo vya damu kwa ajili ya kupima sukari kwa mmoja wa wazee wanaolelewa kwenye kituo hicho wakati wa maadhimisho ya siku ya wazee duniani.


IMG_2330
Wafanyakazi wa UNFPA kutoka kushoto ni Clementina Njau, Mike Mwakuvila na mdau kutoka Tushikamane Pamoja Foundation wakionyesha upendo kwa mmoja wa wazeee wanaoishi kwenye kituo hicho wakati wa maadhimisho ya siku ya wazee duniani.
IMG_2351
Dr. Majaliwa Marwa kutoka UNFPA akikabidhi moja ya vyandarua walivyovitoa kwenye kituo hicho kinacholelea wazee Msimbazi Centre wakati wa maadhimisho ya siku ya wazee duniani.
IMG_2383
Sehemu ya msaada uliotolewa na makundi hayo.
IMG_2371
IMG_2364
Wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) hapa nchini wakiongozwa na mtaalam wa mawasiliano kutoka UNFPA, Sawiche Wamunza(kushoto), wadau wa Tushikamane Pamoja Foundation pamoja madaktari vijana wanaounda kundi la Projeckt Inspire chini ya mradi wa Inspire Healthy wakiwa kwenye picha ya pamoja na masista wanaowahudumia wazee hao kwenye kituo hicho.
IMG_2574
Wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) hapa nchini wakiongozwa na mtaalam wa mawasiliano kutoka UNFPA, Sawiche Wamunza(wa nne kushoto), wadau wa Tushikamane Pamoja Foundation pamoja madaktari vijana wanaounda kundi la Projeckt Inspire chini ya mradi wa Inspire Healthy kwenye picha ya pamoja.


PIGA KURA UBORESHE MAISHA YA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI

$
0
0
a href="http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2014/10/Untitled.jpg">Untitled
Shirika linalojibidisha na kutetea na kulinda watu wenye ulemavu wa ngozi nchini Under the Same Sun, (UTSS) limeteuliwa kushindania Tuzo ya Haki za Binadamu ijulikanayo kama "Tulip" itolewayo nchini Uholanzi. Iwapo UTSS watashinda tuzo hiyo, ni dhahiri kwamba kutakuwa na mapinduzi makubwa katika uboreshaji wa maisha ya watu wenye ulemavu wa ngozi. 

 Shiriki kwa kupiga kura ili UTSS washinde Tuzo hii na kulinda ndugu zetu wenye Ulemavu wa Ngozi Tanzania kwa kupiga kura hapa chini na kusambambaza tarifa hizi kwa taasisi na watu mbalimbali.
Kwa kupiga kura hiyo bofya hapa

BALOZI LUMBANGA AFUNGUA RASMI MKUTANO WA MAAFISA MIPANGO

$
0
0
 Mgeni Rasmi wa mkutano wa mwaka wa wachumi na maafisa mipango, Balozi Dkt. Matern Lumbanga akizungumza na washiriki wa Mkutano huo kabla ya kuufungua rasmi.
 Baadhi ya viongozi wa wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakimsikiliza kwa makini Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Hayupo pichani). Kutoka Kushoto ni Naibu Katibu Mtendaji (Uchumi Jumla), Prof. Longinus Rutasitara, anayemfuatia ni Bw. Paul Sangawe (Naibu Katibu Mtendaji anayeshughulikia Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Kiuchumi) na Kulia ni Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu) Bibi Florence Mwanri.
 Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango akisoma hotuba wakati wa mkutano wa mwaka wa wachumi na maafisa mipango unaofanyika jijini Dar es Salaam.

Washiriki wa mkutano wa mwaka wa wachumi na maafisa mipango wakimsikiliza Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Hayupo pichani).

 Washiriki wa mkutano wa mwaka wa wachumi na maafisa mipango wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi Balozi Dkt. Matern Lumbanga (katikati waliokaa) pamoja na viongozi waandamizi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.


 Washiriki wa mkutano wa mwaka wa wachumi na maafisa mipango wakimsikiliza Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Hayupo pichani).
 Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kulia) akimpongeza na kumshukuru Mgeni Rasmi wa mkutano wa mwaka wa wachumi na maafisa mipango, Balozi Dkt. Matern Lumbanga mara baada ya kuufungua rasmi mkutano huo.
 picha ya pamoja.
Picha na SAIDI MKABAKULI
==========  =======  ===========
Mkutano wa kitaalamu ambao unawakutanisha wataalamu mbalimbali kutoka tasnia za mipango, uchumi, takwimu na maendeleo, wenye wajibu wa kusimamia uchumi na mipango umefunguliwa rasmi na Balozi (Mstaafu) Dkt. Matern Lumbanga. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Balozi (Mstaafu) Dkt. Lumbanga alisema kuwa wachumi na maafisa mipango wana wajibu mkubwa katika kuishauri serikali juu ya njia bora na madhubuti za kupambana na umaskini na kuharakisha maendeleo kwa jamii ya Watanzania.
 
“Muna dhima kubwa katika kushauri kitaalamu juu ya namna nzuri za kupunguza tatizo sugu la umaskini miongoni mwa Watanzania,” alisema.Balozi (Mstaafu) Dkt. Lumbanga aliwasihi washiriki kutumia fursa hiyo kujadili kwa kina na kubadilishana uzoefu juu ya sera, mipango na kujenga mtandao wa masuala ya maendeleo ya kitaaluma.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo, Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango alisema kuwa lengo kuu la mkutano huo ni kutoa fursa ya kuwakutanisha kwa pamoja wataalamu hao na kujenga uelewa wa pamoja juu ya uendeshaji wa shughuli mbalimbali za Serikali. Aliongeza kuwa Mkutano huo, unatoa fursa za kujadiliana kwa pamoja juu ya mafanikio na njia za kukabiliana na changamoto kwa kubadilishana uzoefu na ujuzi kwenye masuala hayo. 

“Mkutano huu ni muhimu katika kuimarisha utendaji kazi wa kada hizi kwa minajili ya kusukuma gurudumu la maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini,” alisema Dkt. Mpango. Kwa mujibu wa ratiba ya mkutano huo, Mada mbalimbali zinawasilishwa kwa kutilia mkazo masuala mbalimbali ya kimaendeleo yanayojitokeza hivi sasa, ambapo mkutano huo unajadili masuala ya Maendeleo ya Tasnia ya Wapanga Mipango (wachumi, maafisa mipango na watakwimu) na Maandalizi ya Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2015/16 – 2020/2021).

Mada nyingine ni pamoja na Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji katika Sekta ya Umma ambao una lengo likiwa kuimarisha utendaji, ufanisi na uwajibikaji katika matumizi ya rasilimali za umma zilizotengwa kwa ajili ya miradi na program za maendeleo. Pamoja na mada ya Namna bora ya kujiandaa na Uchumi wa Gesi. 

Washiriki wa mkutano huu ni pamoja na wakurugenzi wa sera na mipango, maafisa mipango kutoka kwenye wizara, Serikali za Mitaa, idara na wakala wa Serikali, pamoja na taasisi za kitaaluma na watafiti wanaojishughulisha na masuala ya maendeleo na uchumi.
Viewing all 46371 articles
Browse latest View live




Latest Images