Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 376 | 377 | (Page 378) | 379 | 380 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa na viongozi, waandishi wa habari pamoja na wananchi wakiendesha baiskeli kwenda Kata ya Mg'aro katika mteremko wa milima ya Usambara, akitokea Lushoto kwenda Wilaya ya Mkinga,  mkoani Tanga jana kuendelea na ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM pamoja na  kusikiliza kero za wananchi na kutafutia ufumbuzi.
  Nape akihutubia wananchi katika Kata ya Mg'aro mpakani mwa wilaya za Lushoto na Mkinga
  Wananchi wakishangilia huku mmoja wapo akiwa na bango la kuisifia CCM katika mkutano huo wa hadhara.
  Kinana akihutubia katika mkutano huo wa hadhara katika Uwanja wa Maforoni, Duga.

  0 0

   Mawaziri wanaoshughulikia Nishati kutoka nchi za Zambia, Tanzania na Kenya wakisaini Mkataba wa Makubaliano kuonesha dhamira ya Serikali ya nchi hizo kujenga miundombinu ya pamoja ya kusafirisha umeme na kufanya biashara ya kuuziana umeme wa ziada baina ya nchi hizo. Mkataba huo umesainiwa jijini Dar es Salaam leo na Waziri wa Nishati na Madini Tanzania, Profesa Sospeter Muhongo (katikati), Waziri wa Wizara ya   Migodi, Nishati na Maendeleo ya Maji  wa Zambia , Christopher Yaruma (kushoto)  na  Waziri wa Nishati na Petroli Kenya , Davis Chirchir (kulia) . Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Migodi , Nishati na Maendeleo ya Maji Zambia, Charity Mwansa, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini , Tanzania , Eliakim Maswi na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Petroli Kenya,  Mhandisi Joseph Njoroge.
   1.      Mawaziri wanaoshughulikia Nishati kutoka nchi za Zambia, Tanzania na Kenya , Waziri wa Wizara ya   Migodi, Nishati na Maendeleo ya Maji  wa Zambia , Christopher Yaruma (kushoto) Waziri wa Nishati na Madini , Profesa Sospeter Muhongo Tanzania (katikati) na Waziri wa Nishati na Petroli Kenya, Davis Chirchir (kulia) wakibadilishana Mkataba wa Makubaliano kuonesha dhamira ya Serikali ya nchi hizo kujenga miundombinu ya pamoja ya kusafirisha umeme na kufanya biashara ya kuuziana umeme wa ziada baina ya nchi hizo mara baada ya kusaini.
   1.     Mawaziri wa wanaoshughulikia Nishati kutoka nchi za Zambia, Tanzania na Kenya , Waziri wa Wizara ya   Migodi, Nishati na Maendeleo ya Maji  wa Zambia , Christopher Yaruma (kushoto) Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo  Tanzania (katikati) na Waziri wa Nishati na Petroli Kenya, Davis Chirchir (kulia) wakionesha Mkataba wa Makubaliano mara baada ya kusaini.
  1.     Sehemu wa wadau waliohudhuria hafla ya kusaini Mkataba  wa Makubaliano kuonesha dhamira ya Serikali ya nchi za Zambia, Tanzania na Kenya kujenga miundombinu ya pamoja ya kusafirisha umeme na kufanya biashara ya kuuziana umeme wa ziada baina ya nchi hizo. Mbali na Wataalamu kutoka katika nchi hizo, hafla hiyo imehudhuriwa uwakilishi wa COMESA,  Mashirika ya Umeme kutoka nchi hizo na  baadhi ya washirika wa Maendeleo wakiwemo Benki ya Dunia, Umoja wa Ulaya, Ubalozi wa Norway, Shirika la Maendeleo la Japani (JICA), African Development Bank (AfDB), Ubalozi wa Ufaransa.


  Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam
   Nchi za Zambia, Tanzania na Kenya zimesaini Mkataba wa Makubaliano kuonesha dhamira ya Serikali ya nchi hizo kujenga miundombinu ya pamoja ya kusafirisha umeme (ZTK) na kufanya biashara ya kuuziana umeme wa ziada baina ya nchi hizo na nchi nyingine barani Afrika. 

  Akiongea katika hafla hiyo Waziri wa Nishati na Madini, Tanzania Profesa Sospeter Muhongo ameeleza kuwa, mradi huo wa pamoja unalenga kuondoa tatizo la upungufu wa nishati ya umeme baina ya nchi hizo na nchi nyingine barani Afrika jambo ambalo litachangia katika kukuza uchumi wa mataifa hayo. 

  Waziri wa Migodi, Nishati na Maendeleo ya Maji wa Zambia , Christopher Yaruma ameeleza kuwa, utekelezaji wa mradi huo sio tu utaziwezesha nchi hizo kufanya biashara bali pia utafungua fursa za uwekezaji na kusaidia katika kuondoa umaskini miongoni mwa nchi wanachama kutokana kuzitumia fursa mbalimbali zinazotokana na nishati ya umeme. 

  Kwa upande wake Waziri wa Nishati na Petroli Kenya, Davis Chirchir amewataka washirika wa maendeleo kusaidia katika kuwezesha utekelezaji wa mradi huo wa kujenga miundombinu ya pamoja ya kusafirisha umeme baina ya nchi hizo kutokana na manufaa yake kwa bara la Afrika na kuongeza kuwa, kutokana na uwepo wa rasilimali asilia za kutosha katika nchi hizo hakuna sababu ya kuwepo tatizo la nishati katika nchi hizo na barani Afrika.

   Naye Katibu Mkuu Msaidizi wa Jumuiya ya Soko la pamoja la nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika anayeshughulikia miradi (COMESA), Dkt. Kipyego Cheluget amezipongeza nchi hizo kwa kuuendeleza utekelezaji wa mradi huo ambao umechukua kipindi kirefu na kuueleza kuwa, ni miongoni mwa miradi 16 ya kipaumbele na kimaendeleo kwa Afrika. 

  Aidha, kwa upande wao Washirika wa maendeleo waliohudhuria hafla hiyo, wameonesha kufurahishwa kwao na dhamira ya nchi hizo na kuahidi kushirikana na nchi hizo kuhakikisha mradi huo unatekelezwa. Miongoni mwa washirika wa maendeleo waliohudhuria ni pamoja na uwakilishi wa Umoja wa Ulaya, Benki ya Dunia, Ubalozi wa Norway, Shirika la Maendeleo la Japani (JICA), African Development Bank(AfDB) na Ubalozi wa Ufaransa.


  0 0

   Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Mohamed Mpinga pamoja na Mkuu wa wilaya ya Monduli Jowika Kasunga na mafisa wa TBL wakifurahia baada ya kujionea namna zoezi la upimaji wa afya kwa madereva katika eneo la Makuyuni wilayani Monduli lililovyofanikiwa wakati wa wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani lililofanyika kitaifa mkoani Arusha.
   Mganga Mkuu wa Jeshi la Polisi Makao Makuu Dar  es Salaam Dk. Charles Msenga akizungumzia juu ya mafanikio waliyopata wakati wa zoezi la kupima afya za madereva takribani 800 mkoani Arusha, katika eneo la Makuyuni wilayani Monduli, pembeni yake ni Mkuu wa wilaya hiyo Jowika Kasunga.
   Mkuu wa wilaya ya Monduli Jowika Kasunga akizungumza mara baada ya kutembelea mabanda na kujionea jinsi zoezi la upimaji afya kwa madereva lilivyokuwa likifanyika wakati wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani, ambapo zoezi hilo lilifanyika katika eneo la Makyuni wilayani Monduli. Pembeni yake mwenye kofia ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani nchini Mohamed Mpiga na Meneja wa Mauzo Kanda ya Kaskazini Davis Degratius.
   Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani nchini Mohamed Mpinga akizungumzia juu ya mafanikio ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani yaliyofadahiliwa na Kampuni ya BIA TBL wakati wa zoezi la upimaji wa afya kwa madereva lililofanyika Makyuni wilayani Monduli, Arusha kulia kwake ni Meneja wa Kiwanda cha Arusha Salvatory Rweyemamu na kushoto kwake ni Mkuu wa wilaya ya Monduli Jowika Kasunga.
   Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Arusha ... Mwakyoma akiunga mkono zoezi la upimaji wa afya kwa madereva wakati wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani lililofanyika Makuyuni, wilayani Monduli mkoani Arusha kwa kutoa damu kwa ajili ya kupima vipimo vya sukari mwilini.
   Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Marrison Mwakyoma akipima macho yake kama sehemu ya kuhamasisha upimaji wa fya kwa madereva wa mabasi na magari ya mizigo wakati wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani zoezi hilo lilifanyika eneo la Makuyuni wilayani Monduli mkoani Arusha.
   Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Marrison Mwakyoma akipima macho yake kama sehemu ya kuhamasisha upimaji wa fya kwa madereva wa mabasi na magari ya mizigo wakati wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani zoezi hilo lilifanyika eneo la Makuyuni wilayani Monduli mkoani Arusha.
   Mkuu wa wilaya ya Monduli Jowika Kasunga akisisitia jambo wakati alipokuwa akipewa maelekezo ya namna wataalamu wanavyochukua vipimo vya afya kutoka kwa madereva wa mabasi na magari ya mizingo wakati wa zoezi la upimaji wa afya lililofanyika Makuyuni wilayani humo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA.  TAARIFA KWA UMMA

  KUHUSU UTARATIBU MPYA WA USHURU WA FORODHA KATIKA JUMUIYA YA ULAYA IFIKAPO TAREHE 1 OKTOBA, 2014.

  WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA  INAPENDA KUWATAARIFU WATANZANIA NA WAUZAJI BIDHAA KATIKA SOKO LA NCHI ZA JUMUIYA YA ULAYA KUWA IFIKAPO TAREHE 1 OKTOBA, 2014 BIDHAA ZOTE KUTOKA TANZANIA ZITAKUWA ZINATUMIA UTARATIBU WA “UZA KILA KITU ISIPOKUWA SILAHA” (EVERYTHING BUT ARMS-EBA). UTARATIBU HUU MPYA UTATUMIKA BADALA YA UTARATIBU WA “KANUNI 1528 YA JUMUIYA YA ULAYA YA FURSA ZA MASOKO” (EU MARKET ACCESS REGULATION 1528).

  UTARATIBU WA AWALI ULIOKUWA UNAWATAKA WAUZAJI BIDHAA KATIKA SOKO HILO KUJAZA FOMU IJULIKANAYO KAMA “EUR1” UTAFIKIA UKOMO IFIKAPO TAREHE 30 SEPTEMBA, 2014. KATIKA UTARATIBU UTAKAOANZA KUTUMIKA KUANZIA TAREHE 1 OKTOBA, 2014 WAUZAJI WATATAKIWA KUJAZA FOMU MPYA ZINAZOITWA “GSP FORM A” ILI KUWEZESHA BIDHAA ZAKO KUINGIA KATIKA SOKO LA ULAYA BILA YA KUTOZWA KODI WALA KUWEKEWA UKOMO WA IDADI ISIPOKUWA SILAHA. 

  AIDHA, KATIKA UTARATIBU HUU MPYA WA EBA, VIGEZO VYA UASILI WA BIDHAA (RULES OF ORIGIN) VITABADILIKA. MAELEZO YA ZIADA KUHUSU MABADILIKO HAYO YANAPATIKANA KUPITIA anuani http://ec.europa.eu/taxation customs/customs duties/rules origin/preferential/article 839 en.htm na http://exporthelp.europa.eu/thdapp/index.htm
  TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA
   BW. ULEDI A. MUSSA
  KATIBU MKUU WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA

  0 0

  Patric Kajale. Mmoja wa waandaaji wa Tamasha hilo.
  PHOTO CREDITS DMK Blog 
  Karibu katika mahojiano kati ya Mubelwa Bandio na waandaaji wa SWAHILI FESTIVAL iliyofanyika Sept 21 jijini Bladensburg, jimbo la Maryland nchini Marekani Karibu

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Sadick Meck Sadick akimkabidhi madawati 1000 Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke. Madawati hayo ni msaada uliotolewa na kampuni ya mafuta ya TOTAL Tanzania Limited wakishirikiana na shirika la SATF(Social Action Trust Fund). Msaada huo uliratibiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA)

   Wanafunzi wa shule ya msingi Chamazi wakishangilia msaada wa madawati uliotolewa na Kamuni ya TOTAL Tanzania Limited na SATF. Katika picha, mkuu wa mkoa Sadick Meck Sadick (Katikati) akiwa amekaa na mkrugenzi mkuu wa kampuni ya TOTAL Tanzania Limited(Kushoto) na Muwakilishi wa SATF (Kulia)
  Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, akiwa amekaa na Mkurugenzi mkuu wa TEA, na mkurugenzi mkuu wa TOTAL katika moja ya madawati ya msaada kutoka TOTAL Tanzania Limited na SATF.

  0 0

   Meneja masoko wa kinywaji cha GrandMalt Tanzania Fimbo Buttala akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Kebbys Hotel juu ya uzinduzi wa Tamasha la Filamu jijini Tanga kuanzaia jumamosi ya Tarehe 04/10/2014 hadi 08/10/2014 kushoto ni Sinle Mtambalike, Ray Kigosi na kulia ni Rose Ndauka,Shamsa Ford.

   Msanii Rose ndauka akizungumza na waandishi wa habari juu ya ushiriki wao kwenye tamasha kubwa la filamu litakalofanyika jijini Tanga jumamosi ya wiki hii na kuwashirikisha wasanii wote wa kundi la Bongo Muvie kuliani shamsa ford na wasanii wengine.

  ======  =======  =======
  TAMASHA la wazi la filamu Tanzania “Grand Malt Film Festival 2014” sasa litafanyika kuanzia Oktoba 4hadi 8 mwaka huu kwenye viwanja vya Tangamano jijinia Tanga imeelezwa.
  Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Fimbo Butallah, alisema kuwa maandalizi ya tamasha hili yamekamilisha na uzinduzi rasmi utafanyika Jumamosi Oktoba 4 na mgeni rasmi ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Halima Dendegu.
  Butallah alisema kuwa tamasha hilo ni la wazi na hakuna kiingilio kwa wadau wa Sanaa hiyo ya filamu na uzinduzi utafanyika kuanzia saa tisa mchana.
  Alisema kuwa kabla ya uzinduzi wa tamasha hilo, wasanii mbalimbali nyota ambao wanatarajia kushirikishi tamasha hilo watafanya kazi ya jamii kwa kutembelea kituo cha watoto wenye matatizo ya ngozi.
  Aliongeza kuwa kupitia tamasha hili Grand Malt inasaidia kuinua na kutangaza kazi za wasanii wa hapa nchini na kuwapa nafasi ya kuwakutanisha na wadau na mashabiki wao.
  Naye Kaimu Mwenyekiti wa Bongo Movie, Single Mtambalike, aliishukuru Grand Malt, kwa kufanikisha tamasha hili kwa mwaka wa tatu mfululizo.
  Mtambalike alisema kuwa Sanaa ya filamu inasaidia kuwapatia ajira watu mbalimbali hapa nchini na kutaja katika maandalizi ya filamu moja, Zaidi ya wasanii 50 wanatumika kucheza filamu hiyo.
  “Tunaashukuru sana Grand Malt na Sophia Records kwa kufanikisha tamasha hili ambalo linathibitisha wazi kuwa tasnia hii ni biashara kubwa”, alisema Mtambalike.
  Rose Ndauka, ambaye naye ni msanii ya filamu aliwataka wadau wote kujitokeza na kutaja moja ya vitu watakavyotoa kwa watoto watakaowatembelea ni magodoro 60.
  Awali tamasha hilo lilipangwa kufanyika mapema mwezi Agosti mwaka huu mkoani Mtwara.

  0 0

   Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dk. Florens Turuka (wa pili kulia) akifurahia jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA, Prof. Samuel Wangwe (kulia) wakati wa mkutano wa Taasisi ya Maafisa Wakuu Watendaji (CEOs Round Table) katika semina kuhusu umuhimu wa kutumia utaratibu huo wa KAIZEN kuchochea maendeleo Jumanne jijini Dar es Salaam.  Wa pili kushoto ni Katibu Mkuu, Wizara ya Biashara na Viwanda, Bw. Uledi Musa na Muwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Japan (JICA) Tanzania, Bw. Yasunori Onishi (kushoto). 
  Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dk. Florens Turuka (katikati) akifuatilia jambo wakati wa mkutano wa Taasisi ya Maafisa Wakuu Watendaji (CEOs Round Table) katika semina kuhusu umuhimu wa kutumia utaratibu huo wa KAIZEN kuchochea maendeleo Jumanne jijini Dar es Salaam.  Kulia ni Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada na Katibu Mkuu, Wizara ya Biashara na Viwanda, Bw. Uledi Musa.

  Watanzania wameshauriwa kujifunza na kuutumia mfumo wa KAIZEN ambao unalenga  kuongeza tija katika utendaji kazi, kuleta ufanisi wa uzalishaji na ubora ili kuchochea maendeleo nchini.

  Wito huo ulitolewa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dk. Florence Turuka wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mara tu baada ya kufungua mkutano wa Taasisi ya Maafisa Wakuu Watendaji (CEOs Round Table) katika semina kuhusu umuhimu wa kutumia utaratibu huo wa KAIZEN kuchochea maendeleo. “Utaratibu huu unalenga kuleta mabadiliko ya kifikra na ujuzi sehemu za kazi na kuongeza ubora wa huduma zinazotolewa na kampuni au taasisi zetu hapa nchini,”alisema Dk. Turuka aliyemuwakilisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

  KAIZEN ni dhana iliyoanzia na kutumika nchini Japan na kuaminika kuleta mapinduzi makubwa ya maendeleo katika nchi hiyo ikilenga kufikiwa kwa mapinduzi ya viwanda. Kimsingi, mfumo huo unalenga kuongeza thamani na uzalishaji kwa kuwawezesha wananchi mbinu mbinu bora za kazi na usimamizi katika maeneo yao ya kazi. “Utaratibu huu ni wa mabadiliko ya fikra kwa wafanyakazi na waajiri wao sehemu za kazi na kutumia fursa hiyo kuwawezesha wafanyakazi kupata ujuzi zaidi na vitendea kazi bora kutoa huduma bora,”alisema.

  Dk. Turuka alisema utaratibu huo haulengi tu sekta binafsi, bali pia sekta ya umma ambayo inatakiwa kushirikiana na sekta hiyo ili kufikia malengo ya nchi. Balozi wa Japani nchini, Bw. Masaki Okanda alisema utaratibu huo ni wa kubadili fikra kwa kampuni au taasisi katika uendeshaji kwa nia  ya kuleta tija na ubora wa uzalishaji. “Japani imefanikiwa sana katika utendaji na ubora huduma kupitia utaratibu huu wa KAIZEN na mnaweza kuutumia mpate mafanikio,” alisema.

  Alisema Tanzania ina rasilimali nyingi na kuna kampuni na taasisi nyingi lakini inatakiwa kuimarisha utaratibu wa kujenga ujuzi kwa ajili ya kuongeza tija na ubora wa huduma. Alisema panahitajika kuwawezesha wafanyakazi sehemu za kazi na kuweza kuleta mabadiliko ya uzalishaji bora na kuwa kichocho katika kuleta mabadiliko ya maendeleo.

  Naye, Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Japan (JICA) Tanzania, Bw. Yasunori Onishi aliipongeza Wizara ya Viwanda na Biashara na Tanzania KAIZEN Unit katika jitihada inazozifanya kwa kushirikiana na shirika lao katika kuimarisha swala hilo. Alisema utaratibu huo uliasisiwa Japan na kuwapatia mafanikio makubwa ambao  unalenga zaidi ushirikishwaji wa watu wa chini.

  Mfumo huo sasa unatumika kama njia ya kuleta mabadiliko na tayari mataifa mbalimbali duniani wanautumia zikiwemo nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara kama Ghana, Kenya na Zambia. Mhandishi wa Kampuni ya TAPCO, Shabbier Khataw ambae kampuni yake inatumia mfumo huo alisema umewaletea mafanikio makubwa katika utendaji, uzalishaji na ubora wa huduma wanazotoa.

  Hadi sasa kuna kampuni 32 Tanzania ambazo zinatumia mfumo huu kwa majaribio. “Utaratibu huu ni muhimu kama tunataka kuendelea katika sekta ya viwanda...ni viwanda pekee ndivyo vitalikwamua taifa hili,”alisema.
  Mkutano huo wa majadiliano uliandaliwa na Wizara ya Viwanda na Biashara, Tanzania KAIZEN Unit Kwa kushirikiana na Shirika la kimataifa la Japani la JICA.

  0 0

  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha (katikati) akizungumza na ujumbe wa wafanyabiashara na Mabalozi wa Heshima wa Tanzania nchini Marekani uliokuja kumtembelea Ofisini kwake. Ujumbe huo uliongozwa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya TANAS Energy Group ya Marekani, Bw. William Crawford wa kwanza kulia kwa Kaimu Katibu Mkuu upo nchini kwa madhumuni ya kuangalia fursa za uwekezaji na vivutio vya utalii.
  Ujumbe wa Marekani ukimsikiliza kwa makini Kaimu Katibu Mkuu hayupo pichani. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya TANAS Energy Group ya Marekani, Bw. William Crawford, Balozi wa Heshima wa Tanzania, California, Bw. Ahmed Issa; Rais wa Automated Transmission Rebuilding California, Bw. Steve Horgan; Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Seafarers inc, Bibi Deborah Owens; na Rais na Mwanzilishi wa Shirika la Women Empowered to Achieve the Impossible (WETATI), Bibi Margret Dureke,
  Ujumbe mwingine ukifuatilia mazungumzo hayo. Kutoka kulia ni Mhandisi wa Tiba, San Francisco, California, Bw. Robert Reynolds; Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Bw. Suleiman Saleh; Bw. Andy Math na Balozi wa Heshima wa Tanzania, Michigan, Bw. Robert Shumake.
  Kaimu Katibu Mkuu, Balozi Gamaha akiagana na Kiongozi wa Msafara, Bw. William Crawford.
  Picha ya pamoja

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Peter Pinda amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuendana na kasi ya Mpango wa MATOKEO Makubwa Sasa (BRN) katika utendaji wao hasa katika eneo la ufuatiliaji na uadilifu.

  Waziri Mkuu Pinda ameyasema hayo leo (Jumatano) mjini hapa wakati wa hotuba yake fupi ya ufunguzi wa Mkutano wa siku tatu wa watendaji hao kujitathmini katika utekelezaji wa miradi ikiwemo miradi ya elimu iliyoko chini ya BRN. Mkutano huo umeandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI.

  BRN ni Mpango ulioasisiwa na Serikali ya Tanzania na kuanza kazi Julai mosi, 2013 ukiwa na malengo ya kuleta mfumo mpya wa kuweka vipaumbele, kutekeleza miradi kwa wakati na watendaji kuacha kufanyakazi kwa mazoea.

  Sekta sita za awali zilizoingizwa katika vipaumbele vya BRN ni elimu, maji, kilimo, nishati, uchukuzi na ukusanyaji wa mapato. Sekta za uboreshaji wa mazingira ya biashara na afya ziko mbioni kuingia katika BRN. Utekelezaji wa BRN unasimamiwa na Kitengo kipya cha Rais cha Usimamizi wa Miradi (PDB).

  Bw. Pinda alitumia muda huo kusisitizia kuwa BRN imeleta kasi nzuri katika utekelezaji wa miradi kwa kusisitizia uwajibikaji na malengo. Aliwahamaisha viongozi hao kushirikiana na wataalamu mbali mbali wanaofanya kazi zao katika maeneo ya mikoa na wilaya ili kufanikisha maendeleo ya Taifa.

  Akifafanua zaidi utendaji kazi chini ya BRN, Waziri Mkuu alisema Mpango huo unawalazimu watendaji hao kuwajibika ipasavyo katika ushirikishaji, usimamizi makini na ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi mbali mbali ya Serikari.

  Alitumia pia fursa hiyo kuwataka viongozi hao waandamizi kuhakikisha kuwa katika utekeleaji huo wa miradi unakuwepo ushirikiano na wakandarasi wenye sifa kwani ubadhirifu na upendeleo katika utoaji wa miradi umekuwa ukirudisha nyuma maendeleo na kuwakwaza wananchi. 

  Kwa upande wake Mratibu wa Masuala ya Utawala Serikalini kutoka Ikulu, Francis Mang’ila siri ya nchi kupata maendeleo ni kwa watendaji wote ngazi za mikoa na wilaya, kutatua malalamiko mbali mbali yanayowafikia kwa kuzingatia wakati badala ya kuacha wananchi wakilalamika.

  Alisema hali iliyopo sasa inapaswa kubadilika ambapo badala ya wananchi kuwasilisha zaidi matarajio wamekuwa wakiwasilisha malalamiko kutokana na watendaji waandamizi wa mikoa na wilaya kushindwa kufanyiakazi kero zao mapema.

  0 0

   Meneja Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya UAP Insurance, Raymond Komanga akifafanua jambo wakati wa akitangaza mashindano ya gofu yaliyoandaliwa na kampuni hiyo yatakayofanyika Oktoba 4 jijini Arusha. Kushoto ni Meneja Mkuu wa Uendeshaji wa UAP Insurance, Michael Kiruti na Meneja Uandikishaji Bima,  Ally Athuman. (Picha na Francis Dande)

  xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx


  Mashindano ya wazi ya gofu ya Arusha gofu championships yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi Oktoba 4 mwaka huu katika uwanja wa Gymkhana jijini Arusha.

  UAP ambao ni kampuni la huduma ya utoaji Bima, uwekezaji na utawala, uwekezaji wa vitega uchumi na maendeleo, pamoja na kuwa washauri katika mambo ya fedha na ulinzi wa mali, ndio waandaaji wa mchuano huu.

  Akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam meneja biashara wa kampuni ya UAP Insurance Tanzania inayoratibu michuano hiyo Raymond Komanga alisema wanatarajia kushirikisha wachezaji wa gofu wa rika zote kutoka jijini humo na hata maeneo mengine ya jirani

  Komanga alisema lengo la michuano hiyo ni pamoja na kuwashukuru wakazi wa jiji la Arusha kutokana na ushirkiano wao na kampuni hiyo.

  Wachezaji watakaojitokeza kushiriki katika mashindano haya watanufaika kutokana na kwamba watakuza vipaji vyao, kujenga afya pamoja na kukuza wigo wao wa washiriki wa kibiashara kupitia mchezo wa gofu, hivyo tunaomba wachezaji gofu wajitokeze siku hiyo.

  Kwa sasa UAP inafanya kazi katika nchi 6 Afrikazikiwemo Kenya, Uganda, South Sudan, Rwanda, DRC na Tanzania. Baadhi ya bidhaa na huduma za UAP ni pamoja na Bima ya mazao , Bima Mifugo , Bima ya magari, Bima ya mabasi na lori , Bima ya Ndani, bima ya matibabu, bima shule , dhima ya umma , bima ya ajali ya makundi au binafsi , bima yamoto na hatarizingine na mengine zaidi.

  Komanga alisema lengo lingine ni kutaka kuona michuano hiyo inapata washiriki wengi ili kutoa ushindani na kwamba huo ni mwanzo kwani bado watandaa michuano mingine.

  Tutahakikisha  tunaandaa michezo  mbalimbali  ikiwemo huu wa gofu na ipo lingine  la kuandaa jijini Arusha ni kuhakikisha inakuwa na wachezji wengi wazuri  mchezo huo ambao baadaye wataweza kuichezea timu ya taifa na klabu mbalimbali8 alisema.

  Alisema mshindi wa kwanza katika michuano hiyo atapata zawadi ya kulipiwa bima ya nyumba anayoishi pamoja na watu wawili anaoishi nao pili atalipiwa bima ya gofu kwa mwaka mmoja wakati mshindi wa tatu atalipiwa bima ya ajali ya aina yoyote ndani ya mwaka.

  0 0


  Wataalamu wa sekta ya mawsiliano wakiwa katika majadiliano katika mkutano wa masuala ya TEHAMA ‘Connect-to-Connect Summit’ unaofanyika jijini Dar es Salaam. Wataalamu wa sekta ya mawsiliano wakiwa katika majadiliano katika mkutano wa masuala ya TEHAMA ‘Connect-to-Connect Summit’ unaofanyika jijini Dar es Salaam.Wataalamu wa sekta ya mawsiliano wakiwa katika majadiliano katika mkutano wa masuala ya TEHAMA ‘Connect-to-Connect Summit’ unaofanyika jijini Dar es Salaam. Wataalamu wa sekta ya mawsiliano wakiwa katika majadiliano katika mkutano wa masuala ya TEHAMA ‘Connect-to-Connect Summit’ unaofanyika jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Prof. John Nkoma (kushoto) akiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura wakiwa katika mkutano huo. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Prof. John Nkoma (kushoto) akiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura wakiwa katika mkutano huo.Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kushoto) akiwa na Mkuu wa Kitengo cha Ufundi cha TTCL, Senzige Kisenge (kulia) wakifuatilia mada anuai zinazowasilishwa katika mkutano huo unaofanyika jijini Dar es Salaam. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kushoto) akiwa na Mkuu wa Kitengo cha Ufundi cha TTCL, Senzige Kisenge (kulia) wakifuatilia mada anuai zinazowasilishwa katika mkutano huo unaofanyika jijini Dar es Salaam.Wa pili kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura, akizungumza na Waziri wa Mawasiliano na Huduma za Posta wa Sudan Kusini, Rebecca Okaci (wa tatu kulia) viongozi hao pamoja na maofisa kutoka sekta hiyo walikutana kimazungumzo ya kuangalia namna ya kushirikiana katika utendaji kazi. Mkutano huo umeandaliwa na TTCL kwa kushirikiana na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia. Wa pili kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura, akizungumza na Waziri wa Mawasiliano na Huduma za Posta wa Sudan Kusini, Rebecca Okaci (wa tatu kulia) viongozi hao pamoja na maofisa kutoka sekta hiyo walikutana kimazungumzo ya kuangalia namna ya kushirikiana katika utendaji kazi. Mkutano huo umeandaliwa na TTCL kwa kushirikiana na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (katikati) akijadiliana jambo na Waziri wa Mawasiliano na Huduma za Posta wa Sudan Kusini, Rebecca Okaci (wa pili kulia). Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Ufundi cha TTCL, Senzige Kisenge. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (katikati) akijadiliana jambo na Waziri wa Mawasiliano na Huduma za Posta wa Sudan Kusini, Rebecca Okaci (wa pili kulia). Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Ufundi cha TTCL, Senzige Kisenge.Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kushoto) akijadiliana jambo na Waziri wa Mawasiliano na Huduma za Posta wa Sudan Kusini, Rebecca Okaci (katikati). Wa kwanza kulia Mkuu wa Kitengo cha Ufundi cha TTCL, Senzige Kisenge. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kushoto) akijadiliana jambo na Waziri wa Mawasiliano na Huduma za Posta wa Sudan Kusini, Rebecca Okaci (katikati). Wa kwanza kulia Mkuu wa Kitengo cha Ufundi cha TTCL, Senzige Kisenge.Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura na Waziri wa Mawasiliano na Huduma za Posta wa Sudan Kusini, Rebecca Okaci (mwanamama pichani) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mazungumzo yao juu ya ushirikiano kikazi. Wengine ni maofisa waandamizi kutoka pande zote wa sekta ya mawasiliano. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura na Waziri wa Mawasiliano na Huduma za Posta wa Sudan Kusini, Rebecca Okaci (mwanamama pichani) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mazungumzo yao juu ya ushirikiano kikazi. Wengine ni maofisa waandamizi kutoka pande zote wa sekta ya mawasilianoBaadhi ya washiriki katika mkutano wa masuala ya TEHAMA ‘Connect-to-Connect Summit’ wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa leo ikiwa ni siku ya pili ya mkutano huo unaofanyika jijini Dar es Salaam. Baadhi ya washiriki katika mkutano wa masuala ya TEHAMA ‘Connect-to-Connect Summit’ wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa leo ikiwa ni siku ya pili ya mkutano huo unaofanyika jijini Dar es SalaamBaadhi ya washiriki katika mkutano wa masuala ya TEHAMA ‘Connect-to-Connect Summit’ wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa leo ikiwa ni siku ya pili ya mkutano huo unaofanyika jijini Dar es Salaam. Baadhi ya washiriki katika mkutano wa masuala ya TEHAMA ‘Connect-to-Connect Summit’ wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa leo ikiwa ni siku ya pili ya mkutano huo unaofanyika jijini Dar es Salaam.Baadhi ya washiriki katika mkutano wa masuala ya TEHAMA ‘Connect-to-Connect Summit’ wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa leo ikiwa ni siku ya pili ya mkutano huo unaofanyika jijini Dar es Salaam. Baadhi ya washiriki katika mkutano wa masuala ya TEHAMA ‘Connect-to-Connect Summit’ wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa leo ikiwa ni siku ya pili ya mkutano huo unaofanyika jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Harbinder Sigh Seth (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 20 kwa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Juma Pinto (wapili kulia) ikiwa ni mchango wa IPTL kusaidia maandalizi ya Tuzo za wanamichezo bora nchini. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni ni Makamu Mweyekiti wa TASWA, Egbert Mkoko, Katibu Mkuu, Amir Mhando na Mwanasheria na Mshauri Mkuu wa IPTL,Joseph Makandege na kulia ni Mjumbe wa TASWA, Rehure Richard Nyaulawa
   Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto akizungumza na wanahabari baada ya kupokea fedha hizo.
   Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Harbinder Sigh Seth akiwaeleza wanahabari furaha yake ya kuisaidia TASWA kitita hicho cha fedha kusaidia wanamichezo ambapo nae alikiri kuwa ni miongoni mwa wanamichezo na amewahi kuwa Mshindi wa tatu wa Mbio za Magari Afrika.
   Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Harbinder Sigh Seth (katikati) akiwaongoza wanahabari kuangalia mitambo ya Kampuni hiyo ambayo inazalisha umeme. Kulia ni Katibu mkuu wa TASWA, Amir Mhando na Kushoto ni Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto.
  Waandishi wa habari wakiingia kuangalia uzalishaji wa umeme katika mitambo ya IPTL.

  0 0

  Chumba cha kompyuta cha washiriki wa Shindano la Mashujaa wa Kesho. Chumba cha kompyuta cha washiriki wa Shindano la Mashujaa wa Kesho.Baadhi ya washiriki wa Shindano la Mashujaa wa Kesho wakipitia fomu zao. Baadhi ya washiriki wa Shindano la Mashujaa wa Kesho wakipitia fomu zao.

  ZOEZI la uchukuaji fomu kwa ajili ya vijana mbalimbali kushiriki katika Shindano la Mashujaa wa Kesho la Statoil limeendelea kushika kasi huku idadi kubwa ya vijana wakiendelea kurejesha fomu kwa lengo la kushiriki katika kinyang’anyiro hicho. 

  Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Ofisa Mawasiliano wa Statoil Tanzania, Erick Mchome alisema hadi sasa zaidi ya vijana 150 wamerejesha fomu zao tayari kwa kuyashindanisha mawazo anuai ya miradi yao walioiwasilisha kwa ajili ya kushiriki katika shindano hilo. Mchome alisema vijana hao wamejaza fomu kwa ajili ya kushiriki katika shindano hilo kuwania kitita cha hadi Dola 5,000 kwa mshindi wa kwanza. 

   “Kimsingi zoezi hili la shindano la Mashujaa wa Kesho limepokelewa vizuri na linaendelea vizuri sana vijana wengi wa Mtwara wamejitokeza kuchukua fomu na baadhi wameanza kuzirejesha fomu zao…zaidi ya vijana 150 tayari wamerejesha fomu,” alisema Mchome. Hata hivyo kiongozi huyo aliwataka vijana ambao wamechukua fomu kuzirejesha fomu zao kwa wakati kwenye vituo walivyoelekezwa ili hatua zingine za utaratibu wa shindano hilo ziweze kuendelea. 

  “Ningependa kuwakumbusha washiriki kuwa mwisho wa kurejesha fomu ni Oktoba 10, 2014 saa nane kamili kwenye vyuo vya Naliendele Agricultural Institute, Tanzania Institute of Accountancy, VETA, Chuo cha Utumishi na Chuo cha Stella Maris Pamoja na Pride FM,” alisisitiza Mchome. Akifafanua zaidi, Mchome alisema mchujo wa kupata washiriki 40 watakaoingia hatua ya pili utafanyika mara baada ya zoezi la urejeshwaji fomu kukamilika na kutakuwa na mchujo wa tatu ambao ni wa mwisho na kuwatoa washindi watano watakao wania dola 5,000 kwa mshindi wa kwanza na dola 1,000 kwa wa shindi wa pili, tatu, nne na tano . 

  Shindano hilo la vijana linalojulikana kama Mashujaa wa Kesho lenye lengo la kuhamasisha ujasiriamali lilizinduliwa rasmi Septemba 3, 2014 na kampuni ya Statoil na linatarajiwa kumalizika Desemba 12 mwaka huu.

  0 0

    Picha ya pamoja ya timu ya kuvuta kamba wanawake kabla ya mechi ya kuvuta kamba na timu ya Hazina  ambapo walishinda kwa kuwavuta kwa 2-0
   Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu wa timu ya Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wao na timu ya Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii leo mjini Morogoro.

   Wachezaji wa mpira wa pete timu ya Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo wakiwa katika pozi kabla ya kuanza mechi yao na timu ya Jeshi la Ulinzi
   Timu ya kuvuta kamba ya wanaume ya Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo iliyowatoa jasho timu ya Hazina kwa kuwavuta kwa 2-0 wakati wa mashindano ya SHIMIWI mjini Morogoro.
  Timu ya kuvuta kamba ya wanawake ya Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo ikionesha umahiri wao wakati wa mashindano ya SHIMIWI mjini Morogoro ambapo walishinda timu ya Hazina kwa kuwavuta kwa 2-0.


  ========  =======  ========
   Na Eleuteri Mangi-MAELEZO 
  Mji wa Morogoro na viunga vyake imepambwa kwa shamra shamra za mashindano ya Shirikisho la Michezo ya watumishi Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) yanayoendelea katika viwanja mbalimbali mjini hapo. 
  Kwa kipindi cha wiki mbili, watumishi wamekuwa wakionesha vipaji vyao katika michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, kuvuta kamba, riadha, mbio za baiskeli, mpira wa pete na michezo ya ndani. 
  Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ambayo ndio Wizara yenye dhamana ya michezo imedhihirisha ukakakamavu wake katika mashindano hayo leo mjini Morogoro. Ikiwa na timu mahiri, wizara hiyi imeibuka kidedea katika mchezo wa kuvuta kamba kwa timu ya wanawake na ya wanaume dhidi ya wapinzani wao Hazina kwa kuwavuta kwa mizunguko yote miwili kwa timu zote mbili. 
  Kazi ya kuvuta kamba haikuwa ngumu kwa timu za Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwani hikuwachukua muda mrefu kuwavuta wapinzani wao hata kabla ya filimbi ya mwisho ya mchezo huo. Ikumbukwe kuwa michezo ya SHIMIWI imekuwa ni sehemu ya wafanyakazi ambao ni watumishi wa umma kupata fursa ya kujenga afya zao kwa kuwa michezi ni afya kwa maendeleo ya mtumishi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. 
  Zaidi ya hayo, michezo ya SHIMIWI imekuwa desturi ya kujenga udugu, amani upendo na mshikamano kati ya wachezaji na viongozi wa michezo husika katika jamii. Aidha, katika mpira wa pete, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imetoka suluhu kwa kutoa sare na timu ya Ulinzi kwa kufungana kwa magoli 18 kabla ya mechi za mwisho za hatua ya makundi ambayo inatarajiwa kumalizika siku ya Alhamisi Oktoba 2 mwaka huu. 
  Mashindano hayo yanayoendelea mjini Morogoro yanafanyika katika viwanja vya Jamhuri, Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA), Mazimbu na chuo cha Ujenzi ili kutoa mwanya wa michezo mingi kufanyika kwa mara moja.


  0 0

   
  Jaji Mh. Richard Mziray Akitoa Hukumu katika Mahakama ya wazi  katika Kesi zote Mbili ya Kiteto na Kilosa ,ambapo katika Kesi ya Wilaya ya Kiteto alitoa Maamuzi kwamba kulikuwa na umuhimu wa utekelezeji wa Amri ya Mahakama na kuheshimu Amri za Mahakama kuwa Mahakama ilisha tamka kuwa ile ni Hifadhi hivyo inatakiwa kulindwa na kuheshimiwa na ameongeza kuwa kama kungekuwa na kuzingatiwa kwa Sera za Ardhi basi kusingekuwa na Migogoro yote hiyo ametolea mfano pia maeneo ambayo yanatakiwa kulindwa ni pamoja na Bahari na Hifadhi.Katika kesi ya Kiteto alimalizia kuwa Maamuzi ya Mahakama yangeheshimiwa basi kungekuwa hakuna hii Migogoro yote.

  Katika Kesi ya Kilosa Mh. Jaji Richard alisema kwamba Mgogoro uliopo ni juu ya Maji katika Mto wa Mkondoa na Muyombo ambao unagombaniwa wa wafugaji pamoja na wakulima na kwamba katika mgogolo huu Serikali inapendelea zaidi Wakulima na kuwaacha wafugaji alisema kwamba ikiwa wafugaji wangekuwa wanasababisha uharibifu wa Mazingira basi wasinge Ruhusiwa kutumia mito hiyo na hakuna sehemu inaonesha wafugaji wanaharibu Mazingira. 

  Hivyo wafugaji wanahaki ya kutumia mto huo.
  Mwisho katika kesi zote Mbili Mh. Jaji  Richard Mziray alitoa Tamko lifuatalo kuwa Wafugaji wanahaki sawa ya kutumia mito hiyo, pia wafugaji wanahaki ya kushiriki katika maamuzi ya wakulima , Wanao lazimisha mkondo wa mito hiyo uende sehemu ambayo sio yake hawana mamlaka ya kufanya hivyo Mwisho ameshauri kwamba ili migogoro hii isiweze kuendelea kuna umuhimu wa upendo kwanza Baina ya pande zote Mbili wakilima na Wafugaji, wakifanya hivyo kutakuwa hakuna migogoro kulipo kungoja Amri za Mahakama.
   Majaji wakiwa wanasikiliza Kesi kwa Makini juu ya migogoro ya Ardhi na wafugaji, Wawekezaji wanachukua maeneo ya wanavijiji, Unyang'anyi wa ardhi na Mazingira kwa ujumla  Kutoka kushoto ni Mh. Jaji msaidizi Jonas, wa katikati ni Mh. Jaji Richard Mziray, na Mh.Jaji Msaidizi Emma Lukumai
   Muwezeshaji wa Mkutano huu Jenerali Ulimwengu akiendelea kutoa Mwongozo
  Mlalamikaji wa Kesi ya matukio makubwa katika hifadhi za Murtangos na Sulendo Wilayani Kiteto Bwana Lembulu Ole Kosyamlos  kushoto akitoma malalamiko juu ya hifadhi ya E-Murtangos iliyoundwa na vijiji saba ambavyo ni Kimana,Ndirkishi, Emarti,Nhati, Engusero,O-sidan na Loltepesi ambapo walianza mchakato huo mwaka 1996 na kurasimishwa rasmi Mwaka 2002 na hifadhi hiyo inaukubwa wa Hekta za Mraba 133,33.15, alieleza changamoto za wafugaji na wakulima ambapo watu wengi walipoteza maisha,Wavamizi kuingia bila utaratibu na kuharibu mazingira, na wimbi la uvamizi kuendelea siku hadi siku mpaka kufikia mwaka 2013. Pia katika Mashitaka hayo ameiomba mahakama ya wazi iwasaidie kutatua tatizo lao na Serikali iangalie upya eneo hilo Kisheria na zisiingizwe Sheria katika Jambo Hilo.
  Mh. Diwani lairumbe Mollel ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto akitoa Malalamiko yao Mbele ya Mahakama ya wazi juu ya Hifadhi ya Msitu wa Vijiji Lusendo ambapo alieleza kuwa hifadhi hiyo ilianzishwa mnamo mwaka 1994/1995 ambapo vijiji 9 viliungana na kutengeneza hifadhi hiyo aliongeza baada ya kuanzisha hifadhi hiyo walipata mafanikio ikiwa ni pamoja na kujipatia fedha kupitia uvunaji wa miti , mkaa endelevu na asali , pia walifanikiwa kupata Gari moja aina ya Land Cruzer Pick up na pikipiki . Alimalizia kwa kuleta malalamiko yake katika Mahakama ya wazi kuwa kuna uvamizi uliokithiri kwa maeneo ya Misitu Hususani Maeneo yote yanayozunguka mipaka ya Wilaya za Kilindi na Kiteto na Kuiomba Serikari wapate kurejeshewa maeneo yao.
  Bwana Henry Parmeo akitoa mashitaka yake Mbele ya Mahakama ya wazi  juu ya mgogolo uliopo Kilosa kati ya wafugaji na wakulima hasa katika eneo la maji, na muwekezaji ambaye yeye amebadilisha Mkondo wa Maji kutoka katika eneo lake husika na kwenda katika Mashamba, Katika kesi hiyo amedai kwamba wakulima wamekuwa wakiwalaumu wafugaji hao kuwa ndio wenye makosa kwa kuwa wanaingilia wakulima kuwa Mifugo yao inakula mazao na kusahau kwamba Wakulima hao wamebadilisha mkondo huo kwenda mashambani, na aliongeza kuwa mgogoro huu huwa unajitokeza hasa wakati wa kiangazi miezi ya Nane,Tisa, Kumi, Kumi na moja na Kumi na Mbili katika mto Mkondoa na Myumbo. ameiomba Mahakama ya wazi pamoja na Serikali kumaliza Mgogoro huu.
  Mama Shujaa wa  Chakula kutoka Mkoa wa Morogoro akielezea kwa kina zaidi juu ya Mgogoro wa wakulima na wafugaji hasa katika mito miwili ambapo wote wanagombania kupata maji hasa wakati wa kiangazi na amewapongeza Oxfam kwa Juhudi zao za kusaidia kutatua matatizo ya Mgogoro huo
  Bi Vera F. Mugittu Mjumbe wa Bodi ya Forum CC akitoa maelezo ya kina zaidi Juu ya Kesi Mbili zilizotajwa Kesi ya Kilosa na Kiteto na kusema kuwa Migogoro yote ni Juu ya Lasilimali na kwamba Serikali pamoja na Mahakama wanatakiwa kujua Matatizo haya na kujua Jinsi gani wanaweza kuyatatua na kuwajengea uwezo watu wapate kujitambua ili kuepukana na migogoro hiyo, Alimalizia kwa kusema kuwa ucheleweshaji wa kusikiliza kesi ndio unao ongezea Migogoro.
  Bwana Muro Mjumbe wa Bodi ya Forum CC akitoa maelezo ya kina juu ya kesi mbili za Kilosa na Kiteto
  Baadhi ya Wachangiaji wakichangia Michango na mawazo mbalimbali wakati wa Mahakama ya Wazi iliyo andaliwa na Oxfam pamoja na Forum CC
  Mh. Emma akitoa ufafanuzi juu ya Vifungu mbalimbali vya Sheria wakati wa Hukumu hizo katika mahakama ya wazi leo
  Mh.  Jonas akitoa ufafanuzi zaidi wa maamuzi katika kesi hiyo ya Mahakama ya wazi
   Michoro ambayo inaonesha matukio mbalimbali ya Mkutano huo
   Burudani ikiendelea wakati wa mapumziko mafupi
  Baadhi ya watu wakiwa wanasikiliza kesi kwa makini katika Mahakama hiyo ya wazi ambayo iliandaliwa na Oxfam na Forum CC


  0 0
  0 0

  Now you can not only control your venue,profits or promote your brand but can also "give back" to your customers etc. Make them win anything as they attend your event etc. See the details below and feel free to call and order RN SCRATCH AND WIN

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.
   Wananchi wakifurahia hotuba ya  Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Masaki Okada  wakikata utepe  kuashiria ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam. Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadiki, Meya wa Konondoni Mhe, Mbunge wa Kawe  Mhe Halima Mdee, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Musa Iyombe na viongozi wengine
   Sehemu ya barabara  ya Mwenge-Tegeta yenye urefu wa Km 12.9, ambayo ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mbunge wa Kawe Mhe Halima Mdee  baada ya ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatano, Oktoba Mosi, 2014, amezindua rasmi Barabara ya Kisasa ya Mwenge-Tegeta ambayo ni sehemu ya Barabara ya New Bagamoyo Road, mjini Dar Es Salaam.
  Barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 12.9 imegharimu kiasi cha Sh. bilioni 77.85, fedha ambazo zimetolewa na Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo ya Kimataifa la JICA. Serikali ya Tanzania imechangia asilimia 7.64 katika gharama za ujenzi wa Barabara hiyo.
  Rais Kikwete amefanya uzinduzi huo katika eneo la Makutano ya Kambi ya Jeshi ya Lugalo na Barabara ya Kawe katika sherehe iliyoshuhudiwa na mamia ya wananchi. Alikuwa ni Rais Kikwete ambaye aliweke jiwe la msingi la ujenzi wa Barabara hiyo Aprili 4, mwaka 2011.
  Barabara hiyo ni awamu ya kwanza ya ujenzi wa Barabara itokayo Makutano ya Barabara ya Kawawa, Kinondoni hadi Tegeta. Ujenzi wa awamu ya pili wa kilomita 4.3 kati ya Mwenge na Makutano ya Barabara ya Kawawa, unatarajiwa kuanza wakati wowote baada ya mipango yote ya ujenzi huo kukamilika.
  Barabara hiyo ya Mwenge-Tegeta inalenga kupunguza msongamano wa magari katika eneo la kaskazini mwa Dar Es Salaam na pia ni sehemu ya bararaba kuu inayounganisha Jiji la Dar Es Salaam na Mkoa wa Pwani, kupitia Wilaya ya Bagamoyo, na kuunganisha mikoa hiyo na mikoa ya kaskazini mwa Tanzania.
  Akizungumza kwenye sherehe hiyo ya uzinduzi wa Barabara hiyo iliyojengwa na Kampuni ya Konoike kutoka pia Japan, Balozi wa Japan katika Tanzania, Mheshimiwa Masaki Okada amesema kuwa ujenzi wa barabara hiyo ulichelewa kukamilika mwaka jana, kama ilivyopangwa, kwa sababu ya wajenzi kukabiliwa na matatizo ya mafuriko makubwa yaliyotokea mwaka 2011.
  Mbali na kutaja misaada mingi katika sekta ya miundombinu na hasa barabara ambayo imefadhiliwa na Japan katika miaka mingi iliyopita, Mheshimiwa Okada amesema kuwa Japan sasa iko tayari kuanza ujenzi wa Barabara ya Gerezani-Bendera Tatu, Dar Es Salaam, utakaogharimu Sh. bilioni 18.5, msaada kutoka Japan.
  Aidha, Balozi huyo amewaomba radhi Watanzania kutokana na ucheleweshaji wa kuanza kwa ujenzi wa barabara ya juu kwa juu –flyover- katika eneo la TAZARA, Dar Es Salaam, ambao utagharimu Sh. bilioni 53 ambazo zinatolewa na Serikali ya Japan kupitia Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la JICA.
  Amesema kuwa ujenzi huo umechelewa kwa sababu makandarasi wa Kijapan ambao walitakiwa kujenga flyover hiyo wanakabiliwa na kazi nyingi huko nyumbani za kujenga upya miundombinu iliyoharibiwa na tetemeko na kimbunga cha Great East Japan Earthquake and Tsunami, kilichotokea Machi 2011 na kusababisha uharibifu mkubwa mno.
  Aidha, amesema kuwa wajenzi hao pia wanalazimika kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha miundombinu ya kuiwezesha Japan kuandaa Michezo ya Olimpiki ambayo imepangwa kufanyika nchini humo mwaka 2020.
  Imetolewa na;
  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu – Dar es Salaam.

  1 Oktoba, 2014.


  0 0

   Kampuni ya simu inayoongoza barani Afrika, Asia na Mashariki ya Kati, EtisalatGroup, imeongeza hisa zake katika kampuni ya simu za mkononi ya Zantel kufikia asilimia 85.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Zantel jana jijini Dar es Salaam, hatua hiyo ni ongezeko la hisa hizo kwa asilimia 20 zaidi.

  Katika miaka ya hivi karibuni, Zantel imekuwa ikifanya mapinduzi makubwa katika sekta ya simu za mkononi Tanzania kwa ubunifu ambao umekuwa ukisaidia kustawisha maisha ya watu. Baadhi ya huduma hizo ni pamoja na Z-Kilimo ambayo huwezesha wakulima hata wa vijijini kuweza kupata taarifa muhimu za jinsi ya kuongeza uzalishaji na hivyo kuendeleza sekta ya kilimo. 

  Huduma nyingine ni Islamic Portal, Discover Tanzania (Tourist Portal) na Reverse Ring Back tone (RRBT) ambazo zinawasaidia watanzania kwa namna mbalimbali.

  Pia Zantel ni moja ya kampuni za simu za mkononi nchini zilizofikia makubaliano na kampuni nyingine za simu kuwezesha wateja wao kutuma na kupokea pesa miongoni mwao. 
  Hii ni huduma ya kwanza ya aina hiyo Afrika ambapo mteja wa kampuni hiyo wa huduma ya EzyPesa anaweza kutuma na kupokea pesa kwenda mitandao mingine.

  Kwa sababu ya juhudi zake katika kuokoa maisha ya mama na motto, Zantel imeshawahi kupata tuzo inayoheshimika ya GSMA kwa mradi wa “Mobile Baby”, wakati mkakati wa “Fight Against Malaria” ulitambulika na Wizara ya Afya.

older | 1 | .... | 376 | 377 | (Page 378) | 379 | 380 | .... | 1897 | newer