Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

MFUMO DUME NA MAWAZO MGANDO: KIKWAZO USHIRIKI WA MWANAMKE KATIKA UONGOZI

0
0
20140924_085545
Mkurugenzi Mtendaji wa Uvinza FM Radio, Nuru Kalufya akisimamia usajili wa washiriki wa mafunzo ya Maadili, Jinsia na Kuandika Habari za Migogoro yaliyoanza katika kijiji cha Uvinza, wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma tarehe 24 Septemba hadi 01 Oktoba 2014.
Na Mwandishi wetu, Uvinza.

Imethibitishwa kwamba mfumo dume ulioota mizizi katika jamii kwa kisingizio cha mila, desturi na dini unachangia kwa kiasi kikubwa katika unyanyasaji wa mtoto wa kike na mwanamke nchini.

Hayo yalithibitishwa na washiriki wa mafunzo ya maadili na jinsia yanayofanyika katika kijiji cha Uvinza mkoani Kigoma wakati wakichangia mada ya Jinsia na Vyombo vya Habari iliyowasilishwa na mkufunzi kutoka Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi Rose Haji Mwalimu.

Mshiriki kutoka Loliondo Joseph Munga ambae alizungumzia jinsi gani mfumo dume mgando unavyonyima haki za mtoto wa kike wa Kimasai, alisema kwamba mtoto wa kike hapaswi kwenda shule, kuna kiwango cha juu cha shinikizo la ndoa za utotoni, ukeketaji na wanawake kutokuwa na mamlaka ya kufanya maamuzi.

“Ubaguzi unaanza katika familia, mtoto wa kike hana haki ya kuchagua mume anayemtaka au lini aolewe. Mtoto huyo huyo ni lazima akeketwe kwa sababu mtoto wa kike asiyekeketwa anaonekana ni laana katika familia na hawezi kupata mume. Kutokana na sababu hizo watoto wa kike huridhia kukeketwa ili waondoe laana hiyo lakini pia kwa kushinikizwa na wazazi wa kike.”

Hadi leo haijathibitishwa ni laana gani huwapata wasichana wasiokeketwa kwa maana kuna baadhi yao ambao hawakukeketwa, wameolewa na wanaendelea na maisha ya kawaida.

20140924_085927
Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Uvinza FM Radio Bi. Nuru Kalufya wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Maadili, Jinsia na Kuandika Habari za Migogoro katika maandalizi ya uchaguzi mkuu 2015.

Akizungumzia kuhusu uwakilishi kufikia 50/50 ifikapo mwaka 2015, Munga alisema kwamba bado kuna changamoto kubwa kwa mwanamke wa Kimasai kusimama na kugombea nafasi za uongozi kutokana na wanawake kutopewa nafasi ya kutoa maamuzi katika jamii ya Kimasai. Mathalani, moja ya tabia za mfumo dume mgando katika jamii hiyo ni mila na tamaduni za Kimasai ambapo mwanamke haruhusiwi kushiriki katika uongozi wa rika “laigwanang” kwa sababu jamii ya kimasaia inamlinganisha mwanamke na kumchukulia kama mtoto mdogo “nagara, ngara au ngarai”.

“Nafasi ambazo mwanamke anaweza kufaidika nazo ni zile za kuteuliwa tu basi,” alifafanua Munga. Naye mshiriki kutoka kisiwani Tumbatu Ali Khamis alisema kwamba katika jamii yao mwanamke hana haki ya kutoa maamuzi katika ngazi ya familia na haruhusiwi kuhudhuria vikao vya harusi na misiba. Katika uongozi hali pia hairidhishi.

“Katika kisiwa cha Tumbatu viongozi wote wa ngazi za juu katika siasa ni wanaume. Ukianzia Afisa Tawala, masheha na madiwani ni wanaume, yupo mwanamke mmoja tu ambae ni wa kuteuliwa,” alisema Khamis.
Pemba ina majimbo 18 lakini hakuna mwanamke wa kuchaguliwa kisiasa wakati huo huo kisiwa cha Unguja ambacho kina majimbo 32 kuna wanawake watatu tu wa kuchaguliwa.
DSC_0036
Mshauri na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO akisisitiza jambo katika mafunzo yanayowashirikisha waandishi wa habari na watangazaji kutoka redio jamii nane nchini.
Mshiriki mwingine kutoka Uvinza mkoani Kigoma Leah Kalokoza alisema kwamba unyanyasaji kijinsia ni wa kiwango cha juu katika jamii inayouzunguka mji huo. Alisema kuwa mgawanyo wa kazi katika familia hauna uwiano kati ya mwanamke na mwanaume maneno ambayo pia yalithibitishwa na Balozi wa Barabara ya Kasulu Bi. Tabu Ramadhani.
“Wanawake ndio wanaotafuta riziki hususan kuvuna chumvi kazi ambayo ni ngumu sana, kulima na kulea watoto. Wanaume kazi yao ni kuuza chumvi hiyo, kukaa magengeni na kula hotelini wakati watoto nyumbani hawana chakula, kwa kweli wanatunyanyasa waume zetu.”
Tegemeo kubwa la kipato cha Uvinza ni chumvi pamoja na kwamba kwa kiasi kikubwa kipato hicho kimeshuka baada ya kiwanda hicho kubinafsishwa na mwekezaji mwenye asili ya Kiasia.
Akizungumzia uhuru wa kujieleza, Leah Kalokaza alisema kwamba wanawake hawaruhusiwi kuwasiliana na vyombo vya habari bila idhini ya waume zao. Tamko la Dunia la Haki za Binadamu kuwa na Haki ya Uhuru wa Kujieleza Ibara ya 19, linasisitiza uhuru wa kujieleza ni haki ya kila mtu, awe mwanamke au mwanamume.
Kutoka Mpanda mkoani Rukwa wanawake wananyanyaswa kwa kunyimwa elimu, kutokuwa na haki ya kumiliki kama ilivyo katika jamii nyingine na pia utu wao hudhalilishwa pale mabango katika nyumba za kulala wageni huwa yanakuwa na picha au ujumbe dhahiri wa mfumo dume.
DSC_0022
Mambo mengine yanayochangia udhalilishaji wa wanawake ni nyimbo mbalimbali ambazo humsifu mwanamume na kumkashifu mwanamke hususan sehemu za Usukumani.
“Kwa mfano, kuna Wimbo unaosema, ‘kuzaa mtoto wa kiume jamii yote inafurahia, kuzaa mtoto wa kike ni maandalizi ya sherehe. Hii inaonyesha ni kwa namna gani mwanamke katika tamaduni za Kisukuma hana hadhi hata mbele ya mtoto aliyemzaa mwenyewe,” alisema Anatory John.
Mkoa wa Shinyanga umekumbwa na wimbi kubwa la mauaji ya vikongwe wanawake kwa tuhuma za uchawi, lakini ikija kwenye uganga wa jadi hawatambuliki.
“Waganga wengi wa Kisukuma ni wanaume kwa imani kwamba wanawake hawana uwezo wa kuzungumza na mizimu au miungu”, alielezea Anatory.
Vyote hivyo ni viashiria vya mfumo dume au mawazo mgandoyanayoendeleza tabia ya kumwona mwanamke ni mtu duni na mwanamume ni mtu mwenye uwezo wa pekee.
DSC_0010
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakiendelea kupata darasa kutoka Mkufunzi wao Bi. Rose Haji Mwalimu Uvinza mkoani Kigoma.
Kipengele cha Vyombo vya Habari katika Itifaki ya SADC kuhusu Jinsia na maendeleo kinaazimia kuhakikisha kuwa jinsia inaingizwa katika habari, mawasiliano na sera za vyombo vya habari, mipango, vipindi, sheria na mafunzo kulingana na Itifaki ya Utamaduni, Habari na Spoti.
Azimio la Jinsia na Maendeleo lililotolewa na Viongozi wa Umoja wa Maendeleo Kusini mwa Afrika au Serikali (SADC) linasisitiza uwakilishi wa uongozi katika ngazi ya maamuzi 50/50 ifikapo mwaka 2015.
Warsha ya Maadili na Jinsia inalenga kuwapa uwezo waandishi na watangazaji wa redio za jamii nchini kuandika habari zinatoa changamoto za mfumodume/mgando na matumuzi ya Lugha nyepesi inayohusisha jinsia zote bila kubagua hasa katika kipindi hiki tunakoelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi wa raisi mwaka 2015.
Warsha hii ya siku nane ilijumuisha waandishi wa habari wa redio jamii 48 kutoka redio 8 za jamii Tanzania Bara na Visiwani.
Mradi huu unatekelezwa kwa pamoja kati ya UNESCO na Vyombo vya habari Jamii chini ya mtandao wa COMNETA na kufadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP.
DSC_0014
20140925_142505
Washiriki wa mafunzo ya Maadili na Jinsia katika vyombo vya habari wakiwa katika vikundi kazi.
DSC_0178
Mshiriki wa mafunzo kutoka Redio Loliondo FM, Joseph Munga akichangia mada ya Jinsia na vyombo vya Habari katika mafunzo ya siku nane ya kuzipa uwezo redio jamii kuandika habari chanya cha uchaguzi na migogoro.
20140926_155057
Mshiriki kutoka Tumbatu FM Radio Kisiwa cha Tumbatu, Unguja Ali Khamis akizungumzia changamoto za mfumo dume na mawazo mgando yanayodumaza maendeleo ya mwanamke.
IMAG1321
Pichani ni mshiriki na mwandishi wa habari Uvinza FM Radio, Uvinza- Kigoma Leah Karokaza akichanganua masuala yanayoendeleza unyanyasaji wa kijinsia wilayani Uvinza.
IMAG1332
Anatory John kutoka Baloha FM Radio, Kahama akichanganua baadhi ya misemo na nyimbo zinazomdhalilisha mwanamke.
IMAG1327
“Mabango yanayotundikwa katika nyumba za kulala wageni yanadhalilisha sana wanawake”, ndivyo asemavyo Sharifa Selemani kutoka Mpanda FM Radio, Mpanda mkoani Rukwa katika picha.
20140925_163431
Picha ya pamoja ya baadhi ya washiriki wa mradi wa kuzipa uwezo uwezo redio jamii katika mchakato wa uchaguzi mwaka 2015.

MLAPA NG’OSHA: KALALE PEMA (OFFICIAL VIDEO)

0
0
MSANII wa muziki wa Bongo Fleva anayekuja kwa kasi, Gabriel Samalu Ng’osha ‘Mlapa Ng’osha' ameachia video yake mpya inayokwenda kwa jina la 'Kalale Pema' aliyoelezea maisha ya mateso anayopata mama mjamzito.
Mojawapo ya picha katika video hiyo.
Video hiyo imetengenezwa chini ya prodyuza Melkiadi Oreje 'OJ' wakati audio ikifanywa na Lebo ya Audio Visual ya nchini Kenya chini ya maprodyuza Haptune & Douncher.

TBL YAPATA TUZO YA HESHIMA WIKI YA NENDA KWA USALAMA

0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Manyara,Mbwilo, akimkabidhi Cheti cha kutambua chango mkubwa uliofanywa na Kampuni ya Bia nchini (TBL) ambayo iliendesha zoezi la upimaji afya kwa madareva, Meneja wa Kiwanda cha Bia Arusha Moshi  Sarvatory Rweyemamundiye aliyepokea kwa niaba ya uongozi wa Kampuni hiyo wakati wa kufunga Wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani iliyofanyika kitaifa mkoani Arusha.
 Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Marrison Mwakyoma akipima macho yake kama sehemu ya kuhamasisha upimaji wa fya kwa madereva wa mabasi na magari ya mizigo wakati wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani zoezi hilo lilifanyika eneo la Makuyuni wilayani Monduli mkoani Arusha
Mkuu wa wilaya ya Monduli Jowika Kasunga akisisitia jambo wakati alipokuwa akipewa maelekezo ya namna wataalamu wanavyochukua vipimo vya afya kutoka kwa madereva wa mabasi na magari ya mizingo wakati wa zoezi la upimaji wa afya lililofanyika Makuyuni wilayani humo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani

Mkutano wa Mwaka wa Wadau wa Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi wafanyika jijini Dar es Salaam

0
0
ForumCC imewakutanisha wadau wa Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi kutoka Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar katika Mkutano Mkuu wa Mwaka ili kutoa ripoti ya mafanikio na kujadili changamoto zilizopo katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi
 Picha ya pamoja ya wadau wa Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi waliohudhuria Mkutano wa wadau wa mambo hayo uliofanyika British Council jijini Dar es Salaa
Mjumbe wa Bodi ya ForumCC, Vera Florida Mugittu akitoa mada wakati wa Mkutano wa Wadau wa Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika British Council jijini Dar es Salaa
Simon na Timon kutoka KAS Ujerumani na Afisa Mawasiliano wa ForumCC, Tajiel Urioh (katikati) wakifuatilia mada wakati wa Mkutano Mkuu wa Wadau wa Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika British Council jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa bodi ya ForumCC, Euster Kibona akifafanua jambo kwa washiriki wa mkutano huo
Afisa Miradi ForumCC, Fazal Issa akichangia Mada wakati wa mkutano huo uliowashirikisha wadau mbalimbali wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi kutoka Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar
Mwakilishi wa Vijana wanaofanyakazi na ForumCC, Adam Antony akichangia mada
 Wadau wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi wakifuatilia mada mbalimbali
Afisa Mazingira Idara ya Mazingira ya Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira, Juma Limbe akifafanua jambo kwa wadau wa mazingira na mabadiliko ya Tabianchi
Wadau wa Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi wakifuatilia mada mbalimbali
Balozi wa ForumCC, Fredina Said Kutoka Shinyanga akichangia mada
Marc Wegerif Mjumbe wa Bodi ya ForumCC akifafanua jambo. Picha zote na Tabianchi Blog

KINANA AWATAKA WALIOSABABISHA HASARA KUFUNGWA KIWANDA CHA CHAI MPONDE, BUMBURI WAWAJIBISHWE HARAKA

0
0
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikagua shamba la chai lililoachwa kutunzwa baada ya kiwanda cha chai cha Mponde kufungwa tangu mwaka jana
 Kinana (kulia akiwa na Mbunge wa Jimbo la Bumburi, January Makamba na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Lushoto, Balozi Abdi Mshangama wakiangalia jinsi chai ilivyoharibika baada ya kiwanda kufungwa.
 Diwani wa Kata ya Guga, Richard Mbughuni akitolewa na askari baada ya wananchi wa Bumburi kumwambia Kinana aomtoe katika mkutano huo wa hadhara, wakidai ndiye mmojawapo wa waliosababisha kiwanda hicho kifungwa mwaka jana.
  Diwani wa Kata ya Guga, Richard Mbughuni akitolewa na Katibu Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye baada ya wananchi wa Bumburi kumwambia Kinana aondoke katika mkutano huo wa hadhara, wakidai ndiye mmojawapo wa waliosababisha kiwanda hicho kifungwa mwaka jana.
 Wananchi wakishangilia wakati Kinana akiwasili kwenye mkutano huo.
 Abdulkarim Jambia aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema kata ya Vuga akionyesha juu kadi yake ya CCM baada ya kurejea rasmi CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mponde.
 Umati wa watu ulivyofurika kwenye eneo la mkutano wa hadhara.





 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kata ya Mponde ambapo aliwaambia suala lao la matatizo katika kiwanda cha chai amelichukua na atarudi kwao baada ya mwezi mmoja akiwa na majibu.
  Mbunge wa Jimbo la Bumbuli Mheshimiwa January Makamba akihutubia wananchi wa Mponde wakati wa mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akijionea namna mashamba ya chai yalivyogeuka vichaka . Katibu Mkuu ameongozana na Mbunge wa Jimbo la Bumbuli Mheshimiwa January Makamba.
 Katibu Mkuu wa CCM, akiwapungia wananchi mikono alipowasili kwenye mkutano wa hadhara katika Kata ya Mponde, Jimbo la Bunburi, ambapo aliwahakikishia wananchi kulitafutia ufumbuzi tatizo la kufungwa kwa kiwanda cha chai cha Mponde wilayani Lushoto,Mkoani Tanga.

 Kinana aliwataka viongozi wote wa CCM na Serikali waliohusika kufungwa kwa kiwanda hicho na kuwasababishia adha wananchi kuwajibika wenyewe au kuwajibishwa.

 Katibu Mkuu wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Mponde
 Kinana akihutubia katika mkutano huo

 Kinana akijadiliana jambo na Nape pamoja na January Makamba mbunge wa jimbo hilo la Bumburi.
 Mbunge wa Jimbo la Bumburi, Jamuary Makamba, akihutubia katika mkutano wa hadhara na kumuomba Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana asaidie kutafuta suluhu ya kufungwa kwa kiwanda hicho
 January Makamba akihutubia katika mkutano huo ambapo aliwaomba msamaha wanachi kwa kuendelea kuteseka kwa kufungwa kiwanda hicho.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Ufutiaji kuhusu mgogoro wa kufungwa kwa kiwanda hicho muhimu.
 Kinana akisisitiza jambo alipokuwa akihutubia katika mkutano huo
 Makamba akielezea historia ya jengo la chama katika Kijiji cha Mbuzii lililokuwa linatumiwa na viongozi wa TANU enzi za ukoloni wakati wakiwa katika harakati ya kutaka kutaka kuanzisha chama hicho na uhuru wa Tanganyika.
 Kinana akihutubia kabla ya kushiriki ujenzi wa Kata ya Mbuzii, Lushoto Tanga
 Kinana akishiriki ujenzi jengo la CCM tawi la Mbuzii huku akisaidiwa na Mbunge wa Jimbo la Bumburi, January Makamba
 Kinana na Makamba wakikagua jengo hilo hilo la zamani linalokarabatiwa na wananchama wa chama hicho.


 Kinana akimpabidhi nyaraka Kiongozi wa  waendesha pikipiki  ikiwa ni ishara ya 
Nape akiwa amepanda pikipiki katika Mji wa Bumburi
 KINANA AKIMWANGALIA MBUNGE WA BUMBURI, JANUARY AKIWA AMEPAKIWA KWENYE PIKIPIKI ILI AWAHI KWENYE
 Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, akiendesha pikipiki kuelekea Kata ya Dule ambako Kinana alizindua kikundi cha wajasiriamali cha Maisha Pluis Jimbo la Bumburi, Lushoto
 Makamba  akimtambulisho Nape

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wananchi wa kata ya Mbuzii (hawapo pichani).Katibu Mkuu leo alianza ziara yake katika kata ya Mbuzii ambapo alishiriki ujenzi wa ofisi ya chama sehemu ambayo inahistoria kwani ilitumika kwa kufanya mikutano ya harakati za kutafuta Uhuru na ni sehemu iliyojengwa ofisi ya kwanza ya Tanu wilaya ya Lushoto.

 Wananchi wa kata ya Mbuzi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi pamoja na Mbunge wa Jimbo la Bumbuli Mheshimiwa January Makamba wa ofisi ya CCM kata ya Mbuzii ,Mbuzii ndio chimbuko la TANU wilaya ya Lushoto.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiendesha bodaboda baada ya Katibu Mkuu wa CCM kumaliza kufungua shina la madereva bodaboda shina la Dule B ambapo mbunge wa jimbo la Bumbuli Mh.January Makamba alitoa pikipiki moja.
 Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mh. Majid Mganga akiendesha boda boda kuelekea kwenye uzinduzi wa shina la wajasiriamali la Maisha Plus kata ya Dule.
 Baadhi ya mazao yanayolimwa na kikundi cha ujasiriamali Maisha Plus
 Mbunge wa Jimbo la Bumbuli ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh.January Makamba akiwasalimu wajasiriamali wa Maisha Plus wakati wa ziara ya Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana .
 Wakazi wa kata ya Dule B wakisikiliza kwa makini hotuba za viongozi wao kabla ya kuzinduliwa kwa shina la wajasiriamali la Maisha Plus.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wajasiriamali wa Maisha Plus ambapo alizindua shina la CCM wajasiriamali wa Maisha Plus katika kata ya Dule B
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupasua mawe kwenye kambi ya Maisha Plus ,jimbo la Bumbuli wilaya ya Lushoto mkoani Tanga.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kufyatua matofali .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akijiandaa kuukata muwa pamoja na Mbunge wa Jimbo la Bumbuli Mheshimiwa January Makamba
 Kazi na Dawa! Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akila muwa
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimuelekeza  Mbunge wa Jimbo la Bumbuli Mheshimiwa January Makamba namna ya kupiga randa .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipandisha bendera ya chama baada ya kuzindua shina la Maisha Plus lililopo Dule B ,jimbo la Bumbuli wilaya ya Lushoto.
 Maisha Plus Bumbuli.

KUNDI LA WAMAREKANI WAJA NCHINI KUTIZAMA FURSA ZA UWEKEZAJI.

0
0
Baadhi ya Marais,Wenyeviti na Wakurugenzi wa Makampuni mbalimbali ya nchini Marekani waliokuja nchini kwa lengo la kutizama fursa za uwekezaji .
Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Washington DC,Suleiman Saleh (katikati) akibadilishana mawazo na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya kufua Umeme ya TANASI ,William Crawford.Ziara hiyo inayo ratibiwa na Ubalozi wa Tanzania,Washington DC ni ya siku ambapo wageni hao wataembelea sehemu mbalimbali kujionea fursa za uwekezaji.
Afisa Ubalozi wa Tanzaini ,washington DC ,Suleiman Saleh akizungumza juu ya ujio wa wageni hao 11 kutoka Marekani ambao wako nchini kwa ajili ya kutizama fursa ya uwekezaji.Hii ni mara ya tatu sasa Viongozi wa Makampuni mbalimbali ya  Marekani wanafika nchini ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa Rais Kikwete kutekeleza Dipromasia ya Uchumi.
Rais wa Kampuni ya Ahmed's Moving Express,Inc  ,Ahmed Issa,ambaye pia ni Balozi wa heshima akizungumza na waandishi wa habari katika hotel ya Mount Meru, jijini Arusha kuhusu ujio wa Marais,Wenyeviti na Wakurugenzi wa makampuni mbalimbali ya Marekani walioko Tanzania .Issa tayari ambaye ni ziara yake ya tatu sasa kuja Tanzania tayari ameanza uwekezaji katika sekta ya Utalii ikiwemo kufungua ofisi ya Utalii Carfonia Marekani iliyozindiliwa hivi karibuni na Rais JAkaya Kikiwete.
Mtaalamu wa Ujenzi wa nyumba za makazi ,Nishati Erick Nyaren akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujio wao Tanzania .Nyaren yuko nchini kuangalia fursa katika uwekezaji katika sekta ya Ujenzi. na Miundo mbinu.
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya kufua Umeme ya TANASI William Crawford akiwa na mjukuu wake Colin Machamsoc akizungumza na wanahabari kuhusu ziara yao ya siku sita nchini Tanzania ikiwemo kutembelea vivutio vya utalii vya ,Manyara,Serengeti na Ngorongoro.Crowford yuko nchini kutizama fursa ya uwekezaji inayopatikana katika sekta ya Kilimo.
Mhandisi wa vifaa vya matibabu,Bob Reynolds akizungumza na waandishi wa habari namna anavyofikiria kuwekeza katika sekta ya Afya hasa kwa kutizama upatikanaji wa vifaa tiba kama X Ray,Ultrasound na CT Scan.
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya kufua Umeme ya TANASI William Crawford akiwa na mjukuu wake Colin Machamsoc wakiwa katika pozi la Picha katika hotel ya Mount Meru.
Marais,Wenyeviti na Wakurugenzi wa Makampuni mbalimbali ya Marekani wakiwa katika picha ya pamoja katika hotel ya Mount Meru jijini Arusha
Na Dixon Busagaga wa Globu ya jamii kanda ya kaskazini.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo ZIARANI MUSCAT OMAN

0
0
 Mhe. Said Ali Mbarouk akiwa na mwenyeji wake Waziri wa Habari nchini Oman Sheikh Dk. abdulla  wakati  alipofanya mazungumzo katika ofisi yake tarehe 29 Septemba 2014 akiwa katika ziara rasmi ya siku nne kutembelea sekta mbali mbali za Utalii, Utamaduni na Michezo. (px 11064 -2)
 =========  ========  =========
MUSCAT, OMAN      

Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Said Ali Mbarouk ameuelezea ushirikiano baina ya Oman na Zanzibar kuwa daima utakuwepo na utaendelea kukua kutokana na kutanuka kwa maeneo mapya ya ushirikiano katika Nyanja mbali mbali za maendeleo.

Amesema ni jambo la faraja kuona kuwa hivi sasa Zanzibar na Oman zinatambua umuhimu wa kutanua maeneo hayo ya ushirikiano katika sekta za uchumi, utalii na michezo kwa lengo la  kuwanufaisha watu wa pande zote mbili.

Mhe. Saidi Ali Mbarouk ameyaeleza hayo katika nyakati tofauti wakati alipokuwa na mazungumzo na Mawaziri  wa sekta za Habari, Michezo, Utamaduni na Utalii mjini Muscat Oman leo, akiwa katika ziara yake ya siku nne ya kukutana na viongozi mbali mbali wa nchi hiyo kwa lengo la kukuza ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.

Mapema akizungumza na Waziri wa Habari wa Oman, Sheikh Dk. Abdulla Monaim Bin Mansoor Al Husani, alitoa shukrani zake kwa Serikali ya Oman kwa misaada yake kwa Zanzibar na kusifu nidhamu   ya vyombo vya habari vya nchi hiyo katika kuwaunganisha watu na kuwawezesha kujenga uchumi imara.

Alisema hatua hii ya  mfano wa kuigwa inatokana na usimamizi  madhubuti  kwa vyombo vya habari na kujali kuwajibika kwa jamii kwa vile vinatoa nafasi ya kuwapatia taarifa za kutosha juu ya harakati za kujiendeleza na kujenga ustawi na maendeleo   yao.

Ameshauri haja ya kuwepo na utaratibu wa kubadilishana wataalamu na vipindi ili kila nchi iweze kujifunza kutoka upande mwengine kwa  kutambua maendeleo yanayofikiwa na kila upande na hivyo kutoa fursa za kuwawezesha vijana na vyombo vya habari kuongeza kasi ya utekelezaji wa majukumu yao kwa pamoja hasa kwa vile ni tegemeo kubwa la taifa katika kujenga uchumi.

Katika ziara yake hiyo ya siku nne, Mheshimiwa Saidi Ali Mbarouk pia alipata fursa ya kubadilishana mawazo na Naibu Waziri wa Utamaduni na Mambo ya Kale, Sheikh Hamad Hilal Al Maamari na Waziri wa Michezo, Sheikh Shallal Saad Moh’d Al Saad na kutuwama zaidi katika masuala ya kubadilishana wataalamu wa michezo na kuyahuisha majengo ya kihistoria yenye mnasaba na Oman.

Wakati huo huo,  Mhe. Said Ali Mbarouk ameitaka Oman kufungua fursa nyengine kwa kuisaidia Zanzibar katika kuanzisha Hoteli za kitalii za Halal utaratibu ambao Oman tayari imeuanzisha na kupata mafanikio yake.

Amefahamisha kuwa utaratibu wa hoteli kama hizo za Halal ni muafaka katika visiwa vya Zanzibar kwa vile zitaongeza soko la idadi ya watalii wanaohitaji kupumzika katika maeneo yenye utulivu wa maadili ya kidini na kiutamaduni.

Katika ziara yake hiyo Waziri huyo wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo alipata fursa ya kushiriki katika  karamu rasmi iliyoandaliwa kwa ajili yake  na ujumbe  wa watu watatu aliyofuatana na Mwenyeji wake Waziri wa Habari wa Oman Sheikh Dk. Abdulla Monaim iliyofanyika katika jumba la serikali la Opera mjini Muscat.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI HABARI AMELEZO ZANZIBAR 

Mahojiano na Dr Patrick Nhigula. Mgombea u-Rais wa DICOTA

0
0
Karibu katika mahojiano kati ya Mubelwa Bandio wa Kwanza Production na Dr Patrick Nhighula, mgombea wa nafasi ya uRais wa DICOTA 2014. Mbali na kuielezea DICOTA yenyewe, pia ameeleza nia yake kugombea nafasi hiyo Karibu umsikilize

ONESHO LA S!TE KUFUNGULIWA KESHO JUMATANO MLIMANI CITY

0
0
 
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick (kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es jana juu ya kufanyika kwa maonyesho ya utalii yanayoratibiwa na  Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
 =======  ======= ==========
ONESHO la kimataifa la utalii ‘Swahili International Tourism Expo’ (SITE) linaloandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) linafunguliwa rasmi kesho Jumatano  katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City na litamalizika Jumamosi.
Tayari maandalizi yote kuelekea ufunguzi wa onesho hilo yamekamilika na kwamba watanzania wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuja kujionea vivutio adhimu wa taifa hili.
 
Shirika la Hifadhi ya Taifa (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) pamoja na Shirika la Ndege la Ethiopia ndio wadhamini wa onesho hilo linalotarajiwa kushirikisha mataifa mbalimnali ulimwenguni.
 
Wadhamini wengine ni pamoja na Zanzibar collection, Hoteli za Sea Cliff, Serena hotel, Southern Sun,NewAfrica, Hyatt Regency,Protea, Serena hotel, Bouganvillea Safari lodge, Acacia Farm lodge na Soroi Tented Camp zimedhamini huduma ya malazi kwa wageni maalumu.
 
Pamoja na washiriki wengine onesho hilo linatarajiwa kushirikisha wafanya biashara wakubwa na watalii kutoka Marekani, Uingereza, Ujerumani pamoja na wandishi wa habari wa kimataifa wanaokuja kwa ajili ya onesho hilo.
 
Wakati Wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa ikitoa udhamini wa mabasi ya kubebea washiriki wakati wa onesho hilo, benki ya CRDB imetoa udhamini wa fedha taslimu na inatarajiwa kuwa na banda ndani ya maonesho hayo ya aina yake.
 
Usafiri wa ardhini  utadhaminiwa na makapuni Zara Tours, Naeda Safaris Ltd, Wildlife Expedition Safari, huku Azam Marine wakijitokeza kudhamini usafiri wa baharini kutoka Zanzibar. Mashirika ya ndege ya Rwandair, Precision Air na Uturuki (Turkish airline) yatatoa tiketi za ndege kwa ajili ya kuwasafirisha baadhi ya wageni wakati wa onesho hilo.
 
Makampuni mengine yaliyojitokeza ni yale yanayomiliki majarida. Haya ni Event, Dar Life na 7th Floor Media kutoka hapa nchini na Go Places kutoka Kenya, ambavyo wanatangaza onesho hili kupitia majarida yao.
 
Aidha kampuni ya Montage imetoa udhamini wa kuwa mpambaji katika kumbi za mikutano. Boogie woogie pia wametoa udhamini na watakuwa na mgahawa wao wa chakula katika banda la utalii wa utamaduni ilhali wadhamini wengine Black Tomato wao watakuwa na banda la kuuza kahawa ya Tanzania.
 
‘Swahili International Tourism Expo’ litakuwa likifanyika kila mwaka mnamo mwezi wa Oktoba na kuhudhuriwa na washiriki kutoka ndani na nje ya Tanzania.

PROGRAMU MPYA YA KUJIFUNZA SOMO LA HISABATI KWA KUTUMIA SIMU ZA MIKONONI YAZINDULIWA JIJINI DAR LEO

0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Sayansi na Teknolojia,Mh.Jonh Mgodo akizungumza mapema leo mbele ya Wanahabari kuhusiana na uzinduzi wa Programu mpya ya kujifunza somo la hisabati kwa kutumia simu za mikononi.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Sayansi na Teknolojia,Mh.Jonh Mgodo akizungumza mapema leo mbele ya Wanahabari katika ukumbi wa COSTECH,Sayansi Kijitonyama,jijini Dar kuhusiana na uzinduzi wa Programu mpya ya kujifunza somo la hisabati kwa kutumia simu ya mikononi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Sayansi na Teknolojia,Mh.Jonh Mgodo (wa tatu shoto) akioneshwa na mmoja wa wataalamuwa programu hiyo mpya ya kujifunza somo la hisabati kwa kutumia simu ya mikononi,iliyozinduliwa leo inavyoweza kufanya kazi katika simu za mikononi.
 Mmoja wa Wataalamu wa mradi huo wa Programu mpya ya kujifunza somo la hisabati kwa kutumia simu za mikononi,kutoka Nokia Mobile Mathematics,Bi.Riita Vanska akifafanua jambo kwa wanahabari na wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo iliyofanyika leo katika ukumbi wa COSTECH,Sayansi Kijitonyama,jijini Dar.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia  COSTECH,Dkt.Hassan Mshinda ambao pia ni sehemu ya mafanikio ya programu hiyo,akizungumza jambo mbele ya wanahabari (hawapo pichani) kuhusiana na uzinduzi wa programu mpya ya kujifunza somo la hisabati kwa kutumia simu za mikononi. 
  Baadhi ya wageni waalikwa na wadau mbalimbali wakiwa kwenye hafla hiyo wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo.

Shirika la Nyumba la Taifa lakabidhi mashine za kufyatulia matofali ya kufungamana Kigoma

0
0
 Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa Shirika Mkoa wa Kigoma na Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa Mhe Kanali Issa Machibya.
 Meneja wa Shirika la Nyumba Ndg. Nistas Mvungi akihutubia wananchi wa Kigoma kuhusu mradi wa mashine za kufyatulia matofali ya kufungamana 32 zilizotolewa na Shirika kwa vikundi vya  vijana wa Mkoa wa Kigoma
 Mkuu wa Wilaya Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Ramadhan Maneno akikabidhi mashine za kufungamana kwa Kikundi cha Vijana Kwanza Group. Mwenyekiti wa kikundi Ndg Daniel George  na Katibu wake wakipokea mashine.

  
Picha ya pamoja ya kikundi cha vijana kwanza group na mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa. 
Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ramadhani Maneno kwa makini kuhusiana na maelekezo yake kuhusu umuhimu wa kutumia matofali ya kufungamana na kuondokana na nyumba za matope.



 Meneja wa Mkoa NHC, Nistas Mvungi akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Issa Machibya mashine 32 za kufyatulia matofali ya kufungamana.
  
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Ujiji akishukuru Shirika kwa kuwapatia vijana mashine ya hydraform.
  
Wafanyakazi wa NHC na kikundi cha Vijana Kwanza Group  na wageni waalikwa wakisubiria Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa Mhe Kanali Issa Machibya.
 Meneja wa Shirika la Nyumba Kigoma Ndg Nistas Mvungi akijadiliana na Mkuu wa Mkoa Mhe Issa Machibya jambo kuhusiana na Mashine ya matofali ya kufungamana kuhusu ufanisi wake na ajira kwa vijana.

RAIS KIKWETE KUFUNGUA BARABARA YA MWENGE-TEGETA KESHO

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika sherehe za ufunguzi wa barabara ya Mwenge- Tegeta utakaofanyika tarehe 1 Oktoba 2014.

Ufunguzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta wenye urefu wa Kilomita 12.9, utafanyika kuanzia saa nne asubuhi katika eneo la Lugalo njia panda ya Kawe.

Upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.

Taarifa hii imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini(GCU)
Wizara ya Ujenzi

MKUTANO WA SIKU MBILI JUU YA MABADILIKO YA TABIANCHI, UHAKIKA WA CHAKULA NA HAKI ZA ARDHI ULIOANDALIWA NA OXFAM PAMOJA NA FORUM CC WAANZA LEO KATIKA UKUMBI WA KARIMJEE DAR.

0
0
 Jenerali Ulimwenguambaye ndiye mwezeshaji  akiendelea kutoa Mwongozo katika mkutano wa siku mbili juu ya mabadiliko ya Tabianchi, uhakika wa Chakula na haki za Ardhi mkutano ulioandaliwa na Oxfam pamoja na Forum CC
Robert Muthami Program Support Officer kutoka Pan African Climate Justice Alliance (PACJA) akitoa ufafanuzi juu ya baadhi ya mambo yanayohusu mabadiliko ya Tabianchi.
 Meza  ya Majaji wakiwa wanasikiliza kwa makini malalamiko ya walalamikaji kutoka Loliondo juu ya kuchukuliwa ardhi pamoja na Malalamiko kutoka Wilaya ya Kishapu.
Kushoto ni mmoja wa walalamikaji kutoka Loliondo akielezea kwa uchungu jinsi Muwekezaji alivyo wanyang'anya Ardhi yao na mpaka sasa hakuna kitu ambacho kinaendelea na wanahitaji kupata Msaada wa kisheria ili wapate rudishiwa Ardhi yao.
 Kushoto ni Mama kutoka Loliondo akitoa malalamiko yake Mbele ya Mahakama ya wazi Jinsi mwekezaji alivyochukua Ardhi, kusababisha uharibifu na akina mama kuteseka pamoja na wengine kuharibu Mimba zao pia kupoteza watoto ambapo mpaka sasa kuna mtoto hajaonekana.
 Mlalamikaji Mwengine kutoka Loliondo akielezea Mbele ya Mahakama ya wazi  jinsi ya eneo lao lilivyochukulia na mwekezaji, na kutaka agizo la Mh. Waziri Mkuu lifanyiwe kazi la kwamba ardhi ile ni ya wafugaji na wanatakiwa warudishiwe
Mmoja wa walalamikaji kutoka Wilaya ya Kishapu akitoa malalamiko yake mbele ya Mahakama ya wazi juu ya walivyo chukuliwa maeneo kwa ahadi ya kuyaendeleza na kuto fanya hivyo, na kuomba eneo hilo ambalo ni mashamba warudishiwe ili waendelee na kilimo kwa kuwa eneo hilo kuna shida ya njaa.
Mchangiaji kutoka Oxfam Bwana Marc akizungumza juu ya haki za binadamu na moja ya haki hizo ni haki ya kila mwanadamu kuwa na Chakula, na kuongezea kuwa hata Umoja wa Mataifa unafahamu hilo Pia amesisitiza kuwa ni jukumu la kila mtu kujua sheria za umiliki wa Ardhi
Mjumbe wa Bodi kutoka Forum CC akizungumza jambo wakati wa Mkutano huo

 Mmoja wa wachangiaji akizungumza Jambo
Mh. Jaji Richard Mzilay Akitoa Maelezo ya kina juu ya Walalamikaji kutoka Loliondo ambao walikuwa wana malalamiko ya Ardhi na Kishapu ambapo walikuwa wanataka Eneo lao lirudishwe, Ametoa maelekezo ya yale ambayo wanatakiwa wayafuate.

 

Washiriki wa Mkutano huo
 Mama Shujaa wa Chakula 2014 akichangia maada
 Burudani Elimisha ikiendelea
 Wadau wameguswa na kujumuika kucheza
 Picha ya pamoja

Azam yadhamini maonesho makubwa ya Keki Dar

0
0
Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion Elias (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maonesho makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya SSB, Mohammed Ramadhan wazamini wa maonesho hayo. Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion Elias (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maonesho makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya SSB, Mohammed Ramadhan wazamini wa maonesho hayo.Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion Elias (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maonesho makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya SSB, Mohammed Ramadhan wazamini wa maonesho hayo. Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion Elias (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maonesho makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya SSB, Mohammed Ramadhan wazamini wa maonesho hayo.Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya SSB, Mohammed Ramadhan (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maonesho makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion Elias. Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya SSB, Mohammed Ramadhan (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maonesho makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion Elias.Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion Elias (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maonesho makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya SSB, Mohammed Ramadhan wazamini wa maonesho hayo na kulia ni Meneja Bidhaa za Azam, Abubakar Suleiman. Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion Elias (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maonesho makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya SSB, Mohammed Ramadhan wadhamini wa maonesho hayo na kulia ni Meneja Bidhaa za Azam, Abubakar Suleiman.


KAMPUNI ya Insights Productions Limited kwa udhamini wa Kampuni ya Azam Tanzania imeandaa maonesho makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha wadau mbalimbali wa uandaaji na utayarishaji wa keki. 

Maonesho hayo yatajulikana kama 'Azam World of Cakes Exhibition'. Akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion Elias alisema maonesho hayo yanatarajiwa kuwakutanisha wadau mbalimbali binafsi, makampuni na taasisi waandaaji wa keki nchini Tanzania ikiwa ni sehemu ya kubadilishana uzoefu na kujifunza ubunifu zaidi wa shughuli hizo. 

Bi. Elias alisema dhumuni la maonesho hayo ambayo yanatarajiwa kufanyika Desemba 6, 2014 jijini Dar es Salaam ni pamoja na kusherehekea taaluma ya uokaji keki kwa kuonesha ubunifu na utaalam wa utengenezaji na upambaji wa keki bidhaa inayopendwa na watu wengi na kutumika katika shughuli anuai za kijamii.

 Alisema washiriki wa tamasha hilo mbali na kushindanisha na kuonesha bidhaa zao za keki pia wanatarajia kupata semina ya mafunzo juu ya utengenezaji bora wa keki ikiwa na lengo la kuboresha zaidi taaluma zao. Alisema washiriki hao pia watafanya maonesho ya utayarishaji wa vyombo vya kutengenezea keki, utayarishaji wa unga wa ngano kwa ajili ya kupikia keki, kutambua unga bora wa keki, uchanganyaji wa unga na viungo vingine kwa ajili ya uboreshaji wa radha ya keki. 

 Alisema maonesho mengine yatakayofanywa na wadau hao wa keki ni pamoja na uhifadhi bora wa keki kwa muda mrefu bila kuharibika na washiriki kuonesha maumbo mbalimbali ya keki yenye mvuto kwa watumiaji wa keki na jamii nzima. Alisema maonesho hayo yanayodhaminiwa na Azam watengenezaji wa unga bora kwa ajili ya kutengenezea bidhaa hiyo, yatawashindanisha wadau wa uandaaji keki na pia washindi watakao tajwa na majaji wa maonesho watajipatia fedha taslimu na bidhaa mbalimbali. 

 "...Onesho hili litahusisha jamii yote inayojishughulisha na utengenezaji wa keki, upambaji wa keki, wauzaji wa keki na wanaojishughulisha na bidhaa mbalimbali zinazotumika kutengeneza keki kama vile unga wa ngano wa Azam," alisema Mkurugenzi wa Insights Productions Limited, Bi. Elias. 

Akifafanua zaidi Mkurugenzi huyo alisema onesho hilo litajumuisha bekari na hoteli mbalimbali, Vyuo vya taaluma ya hotelia toka Tanzania na majirani (Afrika Mashariki) pamoja na watengenezaji keki binafsi. Wananchi watakaotembelea maonesho hayo ambayo hayata kuwa na kiingilio watapata fursa ya kujionea aina na mitindo mbalimbali ya utengenezaji wa keki pamoja na kuonja bidhaa hiyo kwenye maonesho ambayo yatafanyika Serena Hoteli jijini Dar es Salaam. 

 Akizungumzia maonesho hayo Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya SSB, Mohammed Ramadhan alisema Azam ikiwa ni kampuni inayotengeneza unga bora wa kutengenezea keki imeamua kudhamini ikiwa ni ishara ya kutambua taaluma hiyo ya uokaji keki nje na ndani ya Tanzania.

TANZANIA KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA GIZ.

0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Michael John akitoa tamko kuhusu Siku ya Soko la Afya iliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na Shirika la GIZ , itakayofanyika Oktoba 2 katika ukumbi wa Diammond Jubelee jijini Dar es salaam.
Naibu Meneja wa Miradi ya Afya wa GIZ Bw. Christian Ptleiderer akizungumza na waandishi wa habari kutoa wito kwa mashirika mengine yanayotoa huduma za afya nchini kuendelea kusaidia na kusambaza huduma zao katika maeneo yenye changamoto ya miundombinu na uhaba wa watumishi wa afya.Kulia ni Mtaalam na Mawasiliano wa shirika la GIZ nchini Bi. Vida Mwasalla. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

 
TANZANIA KUENDELEA  KUSHIRIKIANA NA GIZ.

Na. Aron Msigwa – MAELEZO.

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imesema kuwa itaendelea kushirikiana na Shirika la Ujerumani la GIZ katika uanzishaji na uendelezaji wa programu mbalimbali za utoaji wa huduma za afya zinazolenga kupunguza vifo vya watoto walio chini ya umri wa miaka 5.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Michael John ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akitoa tamko kuhusu Siku ya Soko la Afya  nchini iliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Ujerumani la GIZ  itakayofanyika Oktoba 2,  jijini Dar es salaam.

Amesema Tanzania na GIZ zimekuwa zikishirikiana katika uboreshaji wa miradi mbalimbali ya afya kwa kusogeza huduma za afya karibu na wananchi kuanzia ngazi ya taifa, mikoa na Halimashauri za wilaya.

Ameeleza kuwa mikoa ya Lindi, Mbeya, Mtwara na Tanga imeendelea kunufaika na miradi mbalimbali ya ushirikiano  chini ya shirika hilo inayolenga kuimarisha miundombinu ya kutolea huduma za afya katika maeneo hayo, uimarishaji wa mifuko ya Afya ya Jamii na ushiriki wa moja kwa moja kusaidia upatikanaji na uendelezaji wa wataalam wa kutoa huduma za afya maeneo ya vijijini.

Ameongeza kuwa GIZ imekuwa ikishirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii katika kuhakikisha kuwa jamii inamudu huduma bora za afya kupitia Mifuko ya Hifadhi ya Afya ya Jamii iliyopo katika maeneo yao.

Aidha, amebainisha kuwa maonyesho ya siku ya Soko la Afya yatakayowahusisha wadau mbalimbali na mashirika yanayotoa huduma za afya nchini yanalenga kuwakutanisha wadau hao ili waweze  kujadili changamoto za utoaji wa huduma za afya nchni, kujifunza mafanikio yaliyopatikana katika baadhi ya maeneo na kuweka mikakati ya kuyafikia maeneo mengi zaidi.

Kwa upande wake Mtaalam na Mawasiliano wa shirika la GIZ nchini Bi. Vida Mwasalla ameeleza kuwa maonesho ya mwaka huu yazilenga Wizara, Taasisi , Washirika wa Maendeleo, Makampuni, Mashirika binafsi  na Wakala zinazojihusisha na utoaji na uendelezaji wa sekta ya afya nchini.

Amesema katika maonesho hayo GIZ kwa kushirikiana na Wizara ya Afya itaonyesha mikakati mbalimbali ya kuwaokoa watoto wadogo wenye matatizo ya afya, namna walivyofanikiwa kuwapata watumishi wa afya katika maeneo ya Lindi na Mtwara, maeneo  ambayo hapo awali walikuwa hawakai katika vituo vyao.

Ameongeza kuwa mbali na Siku ya Soko la Afya kuhusisha huduma za utoaji wa elimu, vipimo, machapisho mbalimbali inalenga kuwaweka pamoja wadau hao ili waweze kubadilishana uzoefu na kuweka  mikakati ya kuchangia maendeleo ya sekta ya afya hapa nchini.

Naye Naibu Meneja wa Miradi ya Afya wa GIZ Bw. Christian Ptleiderer ametoa wito kwa mashirika mengine yanayotoa huduma za afya nchini kuendelea kusaidia na kusambaza huduma zao katika maeneo ambayo bado yanakumbwa na changamoto mbalimbali za miundombinu na uhaba wa watumishi wa afya.

Amesema wao kama GIZ kwa kuanzia wameanza na mikoa 4, na wanaendelea kujenga uwezo wa kuyafikia maeneo mengi zaidi kwa kushirikiana na Serikali ya Ujerumani na Tanzania.

NYUSI AKUTANA NA WANAMSUMBIJI WA ZANZIBAR

0
0
 Mgombea wa Urais wa Msumbiji kupitia chama cha FRELIMO Mh.Filipe Nyusi akipokea zawadi kutoka kwa Jumuiya ya watu wa Msumbiji wanaoishi Zanzibar.
Mgombea wa Urais wa Msumbiji kupitia chama cha FRELIMO Mh.Filipe Nyusi akizungumza na Wananchi wa Msumbiji wanaoishi Tanzania ambapo alitumia fursa hiyo kuwaomba wampigie kura kwani amekuja na mikakati mizuri ya kuboresha uchumi ambapo amedhamiria kuiondoa Msumbiji kwenye orodha ya nchi masikini,pia aliahidi kuwawezesha wakina Mama wa Msumbiji.
Wananchi wa Msumbiji wanaoishi Zanzibar wakisikiliza sera za Mgombea wa Urais wa Msumbiji kupitia chama cha FRELIMO Mh.Filipe Nyusi kwenye mkutano uliofanyika katika Hotel ya Zanzibar Beach Resort.
Mgombea wa Urais wa Msumbiji kupitia chama cha FRELIMO Mh.Filipe Nyusi akiongozana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya watu wa Msumbiji wanaoishi Zanzibar Asilia Lunji baada ya kumaliza mkutano wake wa kampeni kwa wapiga kura wanaoishi Zanzibar,Nyusi aliwaambia kuwa amefanya mkutano wa kwanza nchini Tanzania kwa sababu ya mahusiano mazuri baina ya Msumbiji na Tanzania.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiagana na Mgombea wa Urais wa Msumbiji kupitia chama cha FRELIMO Mh.Filipe Nyusi mara baada ya mgombea huyo kumaliza ziara yake Zanzibar.
Mgombea wa Urais wa Msumbiji kupitia chama cha FRELIMO Mh.Filipe Nyusi akiwaaga wananchi wa Zanzibar.

RAIS KIKWETE AREJEA NCHINI KUTOKA MAREKANI KWENYE MKUTANO WA 69 WA UMOJA WA MATAIFA

0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadik  baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 30, 2014 akitokea Marekani alikohudhuria Mkutano wa 69 wa Umoja wa Mataifa.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na IGP Ernest Mangu, Mnadhimu Mkuu  wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi  Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Samuel Ndomba na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadik  baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 30, 2014 akitokea Marekani alikohudhuria Mkutano wa 69 wa Umoja wa Mataifa.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama   baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 30, 2014 akitokea Marekani alikohudhuria Mkutano wa 69 wa Umoja wa Mataifa.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mnadhimu Mkuu  wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi  Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Samuel Ndomba mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 30, 2014 akitokea Marekani alikohudhuria Mkutano wa 69 wa Umoja wa Mataifa.PICHA NA IKULU

Kundi la Orijino Komedy wajiunga na Huduma ya Bima itolewayo na CRDB Microfinance Insurance Brokers

0
0
CRDB Microfinance Insurance Brokers ambao ni wakala wa bima za aina zote ikiwemo bima ya afya, moto, nyumbani na maisha wakishirikiana na kampuni zaidi ya kumi za bima nchini Tanzania,wamefanikiwa kuwapatia huduma ya bima ya maisha,mazishi na ulemavu wa kudumu Kundi la Wasanii wa Vichekesho la Orijino Komedy Company wao na familia zao kupitia African life Assurance (Tanzania) Ltd na bima ya afya wao na familia zao kupitia Kampuni ya AAR Insurance Tanzania.

CRDB Microfinance wanayo furaha kubwa kwa kuwapatia wasani hao huduma hiyo,kwani siku zote imekuwa ikifahamika kuwa msanii ni kioo cha jamii.Wasanii hao waliofanikiwa kujiunga na huduma hizo ni pamoja na Isaya Mwakilasa ‘Wakuvwanga’, Mjuni Silvery ‘Mpoki’, Lucas Mhuvile ‘Joti’, Alex Chalamila ‘McRegan’ na Kiongozi wa kundi hilo,Sekioni David na wengine ni Herry pamoja na Jonas.

Huduma hii inawahamasisha wasanii wengine,wanahabari,wanamitindo na watanzania wote wa hali zote kutembelea ilipo CRDB Bank tawi lolote nchini Tanzania,ili waweze kupata huduma nzuri ya na haraka ya bima "ndani ya mikono salama" .
Meneja wa CRDB Microfinance Insurance Brokers,Arthur Mosha (kushoto) akimkabidhi Kadi ya huduma ya bima ya maisha,mazishi na ulemavu wa kudumu Kiongoni Mkuu wa Orijino Komedy Company,Sekioni David (kulia) wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo kwenye ofisi za CRDB Mikocheni jijini Dar.
Msanii Lucas Mhuvile ‘Joti’ akipokea kadi yake kutoka kwa Meneja wa CRDB Microfinance Insurance Brokers,Arthur Mosha.
 Msanii Isaya Mwakilasa ‘Wakuvwanga’ (kulia) akipokea kadi yake kutoka kwa Meneja wa CRDB Microfinance Insurance Brokers,Arthur Mosha.(wa pili kulia) ni Meneja Mkuu wa African Life Assurance,Nura Masoud na Kushoto ni Meneja Mkuu wa AAR Insurance,Majala Manyama.
Meneja Uhusiano wa CRDB Microfinance Insurance Brokers,Nargis Mohamed (kulia) akiwa na Msanii wa Kundi la Wasanii wa Vichekesho la Orijino Komedy Company,Mjuni Silvery ‘Mpoki’ katika hafla hiyo.
Picha ya pamoja.

Mtandao wa Wanawake na Katiba Kuelimisha Katiba Inayopendekezwa

0
0
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanawake na Katiba, Prof. Ruth Meena akizungumza katika Kongamano la Wanaharakati Kujadili masuala muhimu kwenye mchakato wa Katiba Mpya lililofanyika jijini Dar es Salaam. 
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanawake na Katiba, Prof. Ruth Meena akizungumza katika Kongamano la Wanaharakati Kujadili masuala muhimu kwenye mchakato wa Katiba Mpya lililofanyika jijini Dar es Salaam.Mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba, Usu Mallya akizungumza katika Kongamano la Wanaharakati Kujadili masuala muhimu kwenye mchakato wa Katiba Mpya lililofanyika jijini Dar es Salaam. 
Mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba, Usu Mallya akizungumza katika Kongamano la Wanaharakati Kujadili masuala muhimu kwenye mchakato wa Katiba Mpya lililofanyika jijini Dar es Salaam.Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akizungumza katika Kongamano la Wanaharakati Kujadili masuala muhimu kwenye mchakato wa Katiba Mpya lililofanyika jijini Dar es Salaam. Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akizungumza katika Kongamano la Wanaharakati Kujadili masuala muhimu kwenye mchakato wa Katiba Mpya lililofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Wanaharakati Kujadili masuala muhimu kwenye mchakato wa Katiba Mpya lililofanyika jijini Dar es Salaam wakiwa katika kongamano hilo. Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Wanaharakati Kujadili masuala muhimu kwenye mchakato wa Katiba Mpya lililofanyika jijini Dar es Salaam wakiwa katika kongamano hilo.Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Wanaharakati Kujadili masuala muhimu kwenye mchakato wa Katiba Mpya lililofanyika jijini Dar es Salaam wakiwa katika kongamano hilo. Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Wanaharakati Kujadili masuala muhimu kwenye mchakato wa Katiba Mpya lililofanyika jijini Dar es Salaam wakiwa katika kongamano hilo.Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Wanaharakati Kujadili masuala muhimu kwenye mchakato wa Katiba Mpya lililofanyika jijini Dar es Salaam wakiwa katika kongamano hilo. Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Wanaharakati Kujadili masuala muhimu kwenye mchakato wa Katiba Mpya lililofanyika jijini Dar es Salaam wakiwa katika kongamano hilo. 


Baadhi ya wakichangia mada katika Kongamano la Wanaharakati Kujadili masuala muhimu kwenye mchakato wa Katiba Mpya lililofanyika jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wakichangia mada katika Kongamano la Wanaharakati Kujadili masuala muhimu kwenye mchakato wa Katiba Mpya lililofanyika jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wanachama wa mtandao wa Wanawake na Katiba, TGNP pamoja na mashirika mengine yanayotetea haki za binadamu wakionesha mabango yenye jumbe mbalimbali juu ya mchakato wa Katiba inayopendekezwa. Baadhi ya wanachama wa mtandao wa Wanawake na Katiba, TGNP pamoja na mashirika mengine yanayotetea haki za binadamu wakionesha mabango yenye jumbe mbalimbali juu ya mchakato wa Katiba inayopendekezwa.Baadhi ya wakichangia mada katika Kongamano la Wanaharakati Kujadili masuala muhimu kwenye mchakato wa Katiba Mpya lililofanyika jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya wakichangia mada katika Kongamano la Wanaharakati Kujadili masuala muhimu kwenye mchakato wa Katiba Mpya lililofanyika jijini Dar es Salaam.

MTANDAO wa Wanawake na Katiba, TGNP pamoja na mashirika mengine yanayotetea haki za binadamu wameahidi kushirikiana kutoa elimu ya uraia na uhamasishaji juu ya Katiba inayopendekezwa baada ya kutangazwa kwa muda rasmi wa kuanza kwa zoezi hilo kwa jamii ili kuelimisha zaidi wananchi juu ya Katiba nayopendekezwa. 

Kauli hiyo imetolewa katika Kongamano la Wanaharakati Kujadili masuala muhimu kwenye mchakato wa Katiba Mpya lililofanyika jijini Dar es Salaam na kuwashirikisha wanaharakati mbalimbali. Akifafanua zaidi katika mada yake aliyoiwasilisha kwenye Kongamano hilo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi alisema endapo Bunge Maalum la Katiba Litapitisha Rasimu ya Katiba inayopendekezwa kwa kura nyingi za ndiyo kwa Wajumbe wa Bunge hilo, Rais Jakaya Kikwete atakabidhiwa rasimu hiyo na Kuwa Katiba Inayopendekezwa. 

 Alisema baada ya hapo kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba utaratibu wa utoaji wa elimu na uhamasishaji kwa Umma juu ya maudhui yaliyomo kwenye Katiba inayopendekezwa na Kampeni ya Upigaji wa Kura ya maoni utafanyika zoezi litakalofanywa na Tume husika na vyama vya siasa, vyama vya kijamii vinaruhusiwa kushiriki kutoa elimu ya uraia na uhamasishaji juu ya elimu hiyo. 

 "...Ratiba kamili ya muda wa kutoa elimu kwa umma kuhusu maudhui yaliyomo katika Katiba inayopendekezwa itatolewa kupitia Tanagazo la Gazeti la Serikali (Government Notice). Kwa madhumuni ya kuelimisha na kuhamasisha wananchi kuhusu kuipigia kura ya maoni Katiba inayopendekezwa, Tume italazimika, na vyama vya siasa na vyama vya kijamii vinaweza kutoa elimu ya uraia na uhamasishaji juu ya Katiba inayopendekezwa kwa muda usiozidi siku thelathini kuanzia siku ya kuchapishwa katika Gazeti la Serikali," alisema Bi. Liundi. 

Alisisitiza kuwa kipindi hicho ni muhimu kuwafanya wananchi wote waelewe kilichomo katika Katiba inayopendekezwa ili waweze kuona kama masuala yao ya muhimu yameingizwa katika katiba hiyo kabla ya kuipigia kura. Aidha Mkurugenzi huyo alitoa wito hasa kwa wanawake na makundi ya pembezoni kutumia kipindi hicho kuisoma na kuielewa Katiba inayopendekezwa kwani ndiyo sheria mama na itakuwepo kwa muda mrefu kwa ajili ya jamii yote na hata ya vizazi vijavyo, hivyo ni muhimu kutambua kuwa katiba hiyo ni ya wananchi wote kwa ujumla na si ya vyama vya siasa wala kundi fulani katika jamii. 

 "...TGNP Mtandao wa wanawake na katiba pamoja na mashirika mengine yanayotetea haki za binadamu tutaendelea kutumia fursa hiyo kuendelea kuelimisha na kuraghbisha wananchi kuhusu Katiba inayopendezwa. Hii itasaidia sana wakati wa kuipigia kura ya maoni juu ya Katiba inayopendekezwa wananchi wawe wana uelewa wa kutosha kuhusu yaliyomo katika katiba hiyo na hatimaye wapige kura wakiwa na maamuzi sahihi," alisema Bi. Liundi. 

Akizungumzia zoezi la kufanya mabadiliko katika katiba ya 1977, kama walivyokubaliana wajumbe wa Taasisi ya Kidemokrasia Tanzania (TCD) katika mazungumzo na Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni kwa mujibu wa vyombo vya habari, kwamba kwa kuwa Katiba Mpya haitakuwa tayari katika uchaguzi mkuu ujao yafanyike mabadiliko muhimu kwenye katiba ya mwaka 1977 ili iweze kutumika katika uchaguzi huo. 

Aliishauri serikali kutoa taarifa rasmi kutoka katika mamlaka husika za serikali kuhusu suala hili zito na nyeti kuhusu mabadiliko ya katiba ya 1977 kama sehemu ya maandalizi ya uchaguzi ujao. Aliongeza kuwa pamoja na kwamba serikali haijatoa tamko rasmi au mwongozo wa jinsi ya kuendesha zoezi hilo, baadhi ya vyama vya siasa vimesha pendekeza mabadiliko wanayotaka yafanyiwe kazi. "...Pamoja na mapungufu hayo ya taarifa rasmi, sisi Mtandao wa Wanawake na Katiba tunatoa mapendekezo yetu ya awali kuhusu mabadiliko katiba ya 1977 endapo yatalazimika kufanyika.

" Akitaja mapendekezo hayo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TGNP, alisema Mtandao wa wanawake na katiba unapendekeza uwiano wa hamsini kwa hamsini katika nafasi zote za uongozi uingizwe katika mabadiliko pamoja na uwepo wa tume huru ya uchaguzi masuala ambayo ni kilio cha muda mrefu cha wananchi. "Tunatarajia katika marekebisho ya Katiba ya 1977 suala hili la 50/50 katika ngazi za maamuzi litapewa kipau mbele. Tunadai pia katika mabadiliko ya Katiba ya 1977 sula la mgombea huru lipewe kipaumbele kwani ni wananchi wengi hususan wanawake wenye uwezo mkubwa lakini si wanachama wa chama chochote na hawana utashi wa kujiunga na chama chochote. 

Iwapo suala la mgombea huru litapitishwa wanawake na wanaume wengi watapata fursa ya kugombea nafasi mbalimbali bila kufungwa na chama cha siasa. Hii itapanua demokrasia na ushiriki katika masuala ya uongozi bila vikwazo na ubaguzi." *Imeandaliwa na www.thehabari.com

Sikiliza Audio ya Mahojiano ya Swahilivilla na Mwanamama 'Power Black Nyati 'Jike Jeuri',

0
0
Karibuni katika kusikiliza AUDIO ya Mahojiano na Mwanamama Maisara Juma Salah a.k.a Power Black Nyati 'Jike Jeuri', Kiboko wa Wanaume aeleza mengi kuhusu utumiaji wa nguvu zake, kama kuzuwia pikipiki kwa nyele, ubebaji mfuko wa saruji kwa meno, pamoja na kumbeba mwanamke kwa mkono wake mmoja ama kupasuliwa Jiwe kwenye kifua chake.
Baada ya kuwatoa 'knock out' mabaunsa wawili, ilibidi aongezeke mwingine wawe watatu lakini bado walishindwa kupeleka kidole cha Jike Jeuri' chini wakati akifanya vitu vyake ndani ya Tamasha la Usiku wa Matumaini Agost 08,2014. Picha zote kwa hisani ya mwanawamakonda.blogspot.com
Mwanamama Power Black Nyati 'Jike Jeuri' akifanya vitu vyake ndani ya Tamasha la Usiku wa Matumaini Agost 08,2014. Karibu kusikiliza Mahojiano yetu
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images