Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 374 | 375 | (Page 376) | 377 | 378 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Yameanza vema mashindano ya Shirikisho la Michezo ya watumishi Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) kwa kuendeleza ushindi na kung’ara katika mashindano hayo yanayoendelea mjini Morogoro.
  Mfungaji mahiri wa magoli wa timu ya mpira wa pete Ikulu aliyecheza nafasi ya (G.S) Monica Kassy akiwania mpira dhidi ya wapinzani wao RAS Morogoro wakati wa mechi ya ufunguzi ambapo Ikulu walishinda kwa magoli 62 kwa11 dhidi ya wapinzani wao.
  Baadhi ya wachezaji wa timu ya Ikulu wakifuatilia mchezo wa mpira wa pete wanawake kati ya timu yao na wa wapinzani wao RAS Morogoro. 

  Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakiwa kwenye maandamano siku ya ufunguzi wa mashindano ya SHIMIWI taifa yanayoendelea mjini Morogoro.
  Baadhi ya wachezaji wa Timu ya Ikulu wakimsikiliza Mgeni Rasmi (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mashindano ya SHIMIWI taifa yanayoendelea mjini Morogoro..(Picha zote na Eleuteri Mangi MAELEZO)

  0 0


  0 0
 • 09/28/14--13:08: Article 1
 • WASANII WANAOTAKA KUSHIRIKI TAMASHA LA KONGAMANO LA WASANII WA TANZANIA ,UJERUMANI WAJIANDIKISHE 

  Tamasha litafanyika mjini Koloni,Ujerumani 8 November 2014

  Wasanii wanaotaka kushiriki katika katamasha la kongamano la wasanii wa Tanzania na afrika mashariki linalotarajiwa kufanyika mjini Kolon,Ujermani siku ya 8 November 2014 mnaombwa mjiandikishe kwa kuwasiliana katika namba ya simu  +49(0)15778645623 .
   
  Tamasha hili linania ya kutangaza sanaa za maonyesho za Tanzania nchini ujerumani,wasanii wa ngoma za asili,Sarakasi,Maigizo, Muziki n.k mnakaribishwa kujiandikisha kushiriki Tamasha hili ,Wasanii mnaombwa mtumie nafasi hii kuonyesha vipaji vyenu katika uwanja wa kimataifa ili kujitangaza zaidi.


  0 0

    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa kata ya Sunga.Kinana ni Katibu Mkuu wa kwanza wa CCM kufika kata ya Sunga,jimbo la Mlalo wilaya ya Lushoto mkoani Tanga.
    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Sunga ambapo alisisitiza kuwa matatizo mengi yanayowakabili wananchi hayo yapo kwenye uwezo wao na wilaya kwani majibu yapo hapo hapo na kuwaambia wananchi hao kuchagua viongozi waadilifu.
   wananchi wakifuatilia kwa umakini mkutano wa hadhara wa CCM Jimbo la Mlalo ambapo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alihutubia umati wa watu.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Sunga .

    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Ndugu Twaha Amir Hamza aliyekuwa akiuliza maswali juu ya matatizo ya mipaka kati ya kijiji cha Sunga na Kwentungi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kata ya Sunga.Katibu Mkuu wa CCM ameanzisha utaratibu wa kuwasikiliza wananchi kwenye mikutano yake ya hadhara ambapo amekuwa akipata maswali, ushauri au maoni ambayo pia hupatiwa majibu na Viongozi husika.
   Umati wa wakazi wa Sunga uliofurika kwenye mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
  Wasanii wa kata ya Sunga wakifanya igizo lao baada ya Viongozi kumaliza hotuba, wasanii hao wasanaa ya vichekesho wanafahamika kwa jina la K Square Komedi.

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wakazi wa kijiji cha Kwekangaga ikiwa siku ya pili ya ziara yake katika wilaya Lushoto ambapo alishiriki ujenzi wa ofisi ya tawi la CCM.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisoma taarifa ya ujenzi wa jengo la ofisi ya tawi la  Kwekangaga ambayo imesema ujenzi wa ofisi hiyo ungegharimu shilingi milioni 45 za kitanzania ,Katibu Mkuu aliigomea taaraifa hiyo baada ya kupata ukweli kuwa ofisi hiyo ingegharimu shilingi milioni nne na nusu tu.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya CCM  tawi la Kwekangaga.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (katikati) akisikiliza kwa makini baadhi ya maswali kutoka kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa jimbo la Mlalo,Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Lushoto Balozi Abdi Hassan Mshangamana mwisho kulia ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe waliohudhuria mkutano mkuu wa jimbo la Mlalo uliofanyika kwenye kata ya Lukozi wilayani Lushoto mkoa wa Tanga.
    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kata ya Lukozi wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa maabara ya shule ya sekondari Mtumbi ambapo aliwaambia ni muhimu sana wananchi kushiriki katika maendeleo yao kwani hakuna mtu kutoka nje anaweza kuwaletea maendeleo.
    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimia Wazee wa kijiji cha Sunga
    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwapungia wananchi mkono wakati akiwasili kwenye eneo la mkutano wa hadhara kijiji cha Sunga.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kulia) Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Lushoto Balozi Abdi Hassan Mshangama (katikati) na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiwa eneo la mkutano Sunga.
   Wananchi wa Sunga wakifuatilia mkutano wa Kinana.
   Nape Nnauye akiwa jukwaani kwenye mkutano wa hadhara kata ya Sunga.
    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kusomba kifusi  wakati wa ujenzi wa maabara wa shule ya sekondari Mtumbi.

  0 0

  Mshambuliaji wa Yanga, Andrey Coutinho akitafuta mbinu za kuwatoka wachezaji wa Tanzania Prisons, Lauvian Mpalile (kushoto) na Jeremia Juma wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga imeshinda 2-1. (Picha na Francis Dande)
  Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngasa akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Tanzania Prisons, Lauvian Mpalile.
  Jaja akimtoka beki wa Prisons, Nurdin.
   Jaja akimtoka beki wa Prisons, Nurdin.
   Beki wa Yanga, Juma Abdul akichuana na beki wa Prisons.
  Mshambuliaji wa Yanga, Andrey Coutinho akiwania mpira na beki wa Prisons, Jumanne Elifadhil
   Mrisho Ngasa akiwatoka mabeki wa Prisons.
   Haruna Niyonzima akiwatoka walinzi wa Prisons.
  Kocha wa Yanga, Marcio Maximo akiwapungia mkono mashabiki wa Yanga.
  WQachezaji wakiingia Uwanjani.
   Wachezaji wa Prisons wakisalimiana na wenzao wa Yanga.
  Kocha wa Yanga, Marcio Maximo akisalimiana na kocha wa Prisons.
   Kikosi cha Prisons kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wao na Yanga.
   Kikosi cha Yanga kikiwa katika picha ya pamoja.
  Kocha wa Yanga, Marcio Maximo akishuhudia mchezo huo.
   Mashabiki wa Yanga wakiishangilia timu yao.
   Mashabiki wa Yanga wakiishangilia timu yao.
   Mashabiki wa Yanga wakiishangilia timu yao.
  Jaja (katikati) akiwa amezungukwa na wachezaji wa Prisons.
  Mrisho Ngasa akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Prisons.
  Abdul Juma wa Yanga akipiga mpira huku beki wa Prisons akijaribu kumzuia.
  Ngasa akiambaa na mpira.
   Kipa wa Prisons, Mohamed Omari akiruka juu kuokoa hatari langoni mwake.
  Kipa wa Prisons, Mohamed Omari akiruka juu kuokoa hatari langoni mwake.
   Kipa wa Prisons, Mohamed Omari akiruka juu kuokoa hatari langoni mwake.
   Kipa wa Prisons, Mohamed Omari akiruka juu kuokoa hatari langoni mwake.
   Kipa wa Prisons, Mohamed Omari akiruka juu kuokoa hatari langoni mwake.
   Kipa wa Prisons, Mohamed Omari akiruka juu kuokoa hatari langoni mwake.
   Kipa wa Prisons, Mohamed Omari.

  Mshambuliaji wa Yanga, Andrey Coutinho akishangilia bao la kwanza aliloifungia timu yake.

   Mshambuliaji wa Yanga, Andrey Coutinho akishangilia bao la kwanza aliloifungia timu yake.
   Mshambuliaji wa Yanga, Andrey Coutinho akishangilia bao la kwanza aliloifungia timu yake.
  Andrey Coutinho akishangilia kwa staili ya kupiga magoti baada ya kufunga.
  Wachezaji na viongozi wa Yanga wakishangilia bao la kwanza la timu hiyo.
  Mashabiki wa Yanga wakipagawa kwa furaha.
  Mohamedi Omari kipa wa Prisons akipata matibabu baada ya kuumia.

   Wachezaji wa Yanga wakibadilishana mawazo wakati wakienda mapumziko.
  Mashabiki wa Yanga.
   Wachezaji wa Prisons wakitoka mapumziko.
   Mashabiki wa Yanga wakionyesha alama za vidole 3 kama ishara ya ushindi wa magoli 3.
  Mashabiki wa Yanga wakionyesha alama za vidole 3 kama ishara ya ushindi wa magoli 3.

  0 0

  Mkurugenzi  wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege (kushoto) akiwakaribisha wageni waalikwa na waandishi wa habari waliofika kweye mkutano wao uliofanyika Jana kwenye ofisi za MISA Tanzania  zilizopo jijini Dar es Salaam kulia ni  Mkurugenzi msaidi wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Andrew.

  Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Jana imekutana na waandishi wa habari na wadau tofauti katika kuadhimisha Siku ya haki ya kupata taarifa kimataifa amabayo huadhimishwa kila mwaka Septemba 28.09.2014 katika ofisi zao zilizopo kinondoni Mkwajuni Jijini Dar es salaam.
   Mkurugenzi msaidi wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Andrew Marawiti (kulia) akizungumza jambo mbele ya waandishi wa habari(hawapo pichani) kwenye siku ya kimataifa ya haki za kupata taarifa zinazoadhmishwa septemba 28 kwa kila mwaka.
   Mkurugenzi  wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege  (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wagene waalikwa (hawapo pichani) kwenye siku ya kimataifa ya haki za kupata taarifa zinazoadhmishwa septemba 28 kwa kila mwaka. kwenye ofisi za MISA Tanzania  zilizopo jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi  wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege (kushoto) akikata utepe wakati wa uzinduzi rasmi wa chapicho la ripoti ya matumizi bora ya utoaji wa habari katika sekta za umma hapa nchini.
   Mkurugenzi  wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege akiwaonesha waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa kitabu cha ripoti ya haki ya kupata taarifa halali katika sekta za umma.
    Mkurugenzi  wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege akitangaza taasisi iliyochukua tuzo ya Kofuli la Dhahabu kwa kubana sana taarifa kwa mwaka 2014.
    Mkurugenzi  wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege akionesha tuzo ya Kufuli la Dhahabu kwa kubana sana taarifa kwa mwaka 2014 iliyokwenda kwenye Idara ya Mahakama.
     Mkurugenzi  wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege akitangaza taasisi iliyochukua tuzo ya Ufunguo wa Dhahabu kwa mwaka 2014 kwa kutoa taarifa bila kificho kwa mwaka 2014
   Mkurugenzi  wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege (kulia) akimkabidhi tuzo ya Ufunguo wa Dhahabu Kaimu Mkurugenzi wa Shighuli za Takiwimu ofisi ya Taifa ya Takimu Bi. Aldegunda Komba(kushoto) kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya haki ya kupata taarifa jana jijini Dar es Salaam
   Kaimu Mkurugenzi wa Shighuli za Takiwimu ofisi ya Taifa ya Takimu Bi. Aldegunda Komba akionesha tuzo hiyo kwa waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa waliofika kwenye ofisi za Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) zilizopo eneo la Mkwajuni, Kinondoni jijini Dar es Salaam.
   Kaimu Mkurugenzi wa Shighuli za Takiwimu ofisi ya Taifa ya Takimu Bi. Aldegunda Komba akizungumza na vyombo vya habari baada ya taasisi yaokutwaa tuzo ya Ufungu wa Dhahabu.
   Afisa utafiti na maelezo wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Sengiyumva Gasirigwa akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kwenye siku ya kimataifa ya haki ya kupata taarifa ambayo uadhimishwa septemba 28 kwa kila mwaka.
   Baadhi ya wageni waalikwa pamoja na waandhishi wa habari wakifuatilia shughuli zima iliyokuwa inaendelea kwenye ofisi za Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) zilizopo jijini Dar es Salaam.
  Siku Ya Kimataifa Ya Haki Ya Kupata Taarifa 
  TANZANIA_Most Open and Most Secret Survey(1) 

  0 0

   Mgeni Rasmi katika hafla ya Chakula cha jioni cha kuchangia Mfuko wa Bonnah Education Trust Fund,Mwenyekiti wa CCM Mkoawa Dar es Salaam,Ndg. Ramadhan Madabida akitoa hotuba yake kabla ya kuanza kuendesha harambee hiyo,iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.Zaidi ya sh. Milioni 100 zilipatikana katika harambee hiyo.
   Mwenyekiti Mwanzilishi wa Bonnah Education Trust Fund,Bonnah Kaluwa akitoa hotuba yake kwa wageni wa mbali mbali (hawapo pichani) waliohudhulia hafla ya Chakula cha jioni cha kuchangia Mfuko wa Bonnah Education Trust Fund,iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.Zaidi ya sh. Milioni 100 zilipatikana katika harambee hiyo.Picha zote na Othman Michuzi.
   Katibu wa Bonnah Education Trust Fund,Mary Muwasa akizungumza machache ikiwa ni pamoja kuwatambulisha wadhamini mbali mbali waliojitolea ili kufanikisha harambee hiyo,iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
    Mgeni Rasmi katika hafla ya Chakula cha jioni cha kuchangia Mfuko wa Bonnah Education Trust Fund,Mwenyekiti wa CCM Mkoawa Dar es Salaam,Ndg. Ramadhan Madabida (kushoto) akipokea mfano wa hundi ya Dola za Marekani Elfu 8 kutoka kwa Mwenyekiti wa GCUT Group Tanzania,Lucy Jeremiar Gilya.Katikati ni Mwenyekiti Mwanzilishi wa Bonnah Education Trust Fund,Bonnah Kaluwa.
  Mgeni Rasmi katika hafla hiyo,Ndg. Ramadhan Madabida akipokea mfano wa hundi ya Dola za Marekani Elfu 15 kutoka kwa Meneja wa Miles Networks International nchini Tanzania,Diana Paul (kulia).Katikati ni Mwenyekiti Mwanzilishi wa Bonnah Education Trust Fund,Bonnah Kaluwa.
  Mgeni Rasmi katika hafla hiyo,Ndg. Ramadhan Madabida akipokea mfano wa hundi ya Sh. Mil. 4.4 kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Kampuni ya Resolution Insurance,Angela Tungaraza (kulia).Katikati ni Mwenyekiti Mwanzilishi wa Bonnah Education Trust Fund,Bonnah Kaluwa.
  Mgeni Rasmi katika hafla hiyo,Ndg. Ramadhan Madabida akipokea mfano wa hundi ya Sh. Mil. 9.8 kutoka kwa Meneja Uajiri wa Kampuni ya Aramex Tanzania,Jane Stella Njagi (kulia).Katikati ni Mwenyekiti Mwanzilishi wa Bonnah Education Trust Fund,Bonnah Kaluwa.
   Mgeni Rasmi katika hafla hiyo,Ndg. Ramadhan Madabida akiendelea kutoa hotuba yake.
   Meza Kuu.
   Mshehereshaji katika hafla hiyo,alikuwa si mwingine bali Mdau Ephrahim Kibonde.
  Baadhi ya wageni waliohudhulia hafla ya ya Chakula cha jioni cha kuchangia Mfuko wa Bonnah Education Trust Fund wakifatilia kwa makini harambee hiyo,iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.

  0 0

  DSC_0009
  Meneja wa Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Redio Sengerema mkoani Mwanza Bw. Felician Ncheye, akiutambulisha ujumbe wa wageni kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini kwa Wenyeviti wa bodi na mameneja wa redio za jamii nchini waliohudhuria warsha ya siku tano ya kuwajengea uwezo katika kuboresha masoko kwenye vituo vyao iliyofadhiliwa na shirika la maendeleo la Sweden (SIDA) na kuratibiwa na UNESCO.

  Na Ripota Wetu, Sengerema

  OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kupitia Mradi wa kuimarisha Demokrasia na Amani (DEP) itaanza kutoa elimu inayohusu sheria ya vyama vya siasa na sheria ya gharama za uchaguzi kupitia redio za jamii ili kuwawezesha wananchi kutambua wajibu wao katika kulinda amani ya taifa kuelekea katika uchaguzi na wakati wa uchaguzi.

  Kauli hiyo imetolewa na Mratibu wa Mradi wa kuimarisha Demokrasia na Amani (DEP) kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini, Beatrice Stephano wakati akizungumza na mameneja wa redio hizo katika warsha yao ya siku 5 iliyomalizika mwishoni mwa wiki mjini Sengerema.

  Beatrice alikuwa akizungumzia mradi anaousimamia ambao umedhaminiwa na UNDP kupitia UNESCO kwa ajili ya kuelimisha umma wa watanzania kupitia redio za jamii katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi 2015.
  Alisema uamuzi wa kutumia redio za jamii unatokana na redio hizo kuwafikia wananchi wengi zaidi, hali ambayo wadau katika masuala ya demokrasia wameona kwamba inaweza kutumika kuboresha zaidi uelewa wananchi.
  DSC_0013
  Meza kuu: Kutoka kushoto ni Afisa Sheria kutoka Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kanda ya ziwa mkoani Mwanza, Bw. Isaya Makoko, Mratibu wa Mradi wa kuimarisha Demokrasia na Amani (DEP) kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini, Bi. Beatrice Stephano, Mwenyekiti wa Warsha hiyo kutoka Orkonerei Radio Service Simanjiro Manyara, Bw.Baraka Ole Maika (katikati), Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (wa pili kulia) pamoja na Afisa Mfawidhi Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kanda ya ziwa Mwanza, Bw. Ludovick Ringia (kulia).
   
  Uelewa huo upo katika sheria za uchaguzi, gharama na kuona wajibu wao wa kumsaidia Msajili wa Vyama vya Siasa kukabiliana na mazingira hatarishi ya amani kabla, wakati na baada ya uchaguzi.
  Alisema ni kazi ya Ofisi Msajili wa Vyama vya Siasa kusimamia sheria ya vyama namba tano ya mwaka 1992 ya kusajili vyama na kuviangalia na ile ya namba sita ya mnwaka 2010 ambayo inagusia gharama za uchaguzi.
  Mratibu huiyo amesema kwamba timu kutoka Ofisi ya Msajili itafika kwenye redio hizo za jamii na kuzungumza na wananchi kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu mustakabali wao katika siasa na kuimariuka kwa demokrasia.
  Aidha elimu hiyo inatarajiwa kuwasaidia wananchi kutambua kwamba wana wajibu katika kuhakikisha kwamba menejimenti za uchaguzi zinawajibika pamoja na muuingiliano wake ili kuwa na michakato salama ya cuhaguzi na uchaguzi wenyewe.
  DSC_0081
  Mratibu wa Mradi wa kuimarisha Demokrasia na Amani (DEP) kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini, Bi. Beatrice Stephano (wa pili kushoto) akizungumza na mameneja wa redio za jamii nchini wanaohudhuria warsha ya siku tano inayofanyika kwenye kituo cha Habari na Mawasiliano cha Sengerema Telecentre mkoani Mwanza kuhusiana na ofisi yake kufanya kazi kwa pamoja na redio za jamii nchini katika kutoa elimu kwa umma.
  Naye Afisa mfawidhi ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kanda ya ziwa mkoani Mwanza, Ludovick Ringia akizungumzia sheria mbili za vyama vya siasa alisema kwamba ni wajibu wao kuwaeleza wananchi kuhusu maadili na kanuni katika sheria zinazogusa ukuzaji wa amani katika duru za siasa na demokrasia.
  Alisema mradi huo wa kuelimisha wananchi ambao unafanyika kwa udhamini wa Unesco kupitia ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) ni moja ya njia za kufanikisha amani katika kipindi chote kuanzia uchaguzi wa mwisho hadi mwingine.
  Alisema wanatumia redio za jamii kwa kuwa redio za kibiashara zimekuwa kikwazo hasa bajeti inapouma kidogo.
  Alisema mradi huo ambao unafanyika kwa mwaka mmoja ni sehemu ya juhudi za taasisi hiyo za kuliwezesha taifa kuendelea kuwa na utulivu.
  DSC_0073
  fisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (wa pili kulia), akielezea uwezo wa redio za jamii zinavyoweza kufikia jamii kubwa zaidi nchini wakati ujumbe kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa ulipofanya mazungumzo na Wenyeviti wa Bodi na Mameneja wa redio za jamii nchini waliohudhuria warsha ya siku tano iliyofadhiliwa na shirika maendeleo la Sweden (SIDA) na kuratibiwa na UNESCO iliyofanyika kwenye kituo cha habari na mawasiliano cha Redio Sengerema mkoani Mwanza.
  Wenyeviti wa bodi na mameneja hao katika warsha hiyo walielemishwa uboreshaji wa masoko na umuhimu wa redio za jamii juu ya matumizi ya Tehama kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa kazi na kushirikisha zaidi wananchi.
  Aidha Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Al Amin Yusuph akizungumzia mafunzo hayo alisema kwamba mradi huo umekuja wakati muafaka ili kutoa elimu kwa umma, kwani kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanywa takribani asilimia 70 ya wananchi wanaoishi vijijini wanasikiliza redio huku asilimia 5 tu ndio wanaangalia runinga.
  DSC_0119
  Afisa Mfawidhi Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kanda ya ziwa Mwanza, Bw. Ludovick Ringia (kulia) akielezea ufanyaji kazi wa sheria mbili za vyama vya siasa kwa wenyeviti wa bodi na mameneja wa redio za jamii nchini wakati wa warsha ya siku tano iliyofadhiliwa na SIDA na kuratibu na UNESCO ambayo imefanyika kwenye kituo cha Redio Sengerema mkoani Mwanza.
  DSC_0034
  Afisa Sheria kutoka Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kanda ya ziwa mkoani Mwanza, Bw. Isaya Makoko akiwasilimia wenyeviti wa bodi na mameneja wa redio za jamii nchini (hawapo pichani).
  DSC_0135
  Mmoja wa washiriki wa warsha hiyo akihoji swali kwa ujumbe uliotoka kwenye ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini.
  DSC_0126
  Pichani juu na chini ni baadhi ya wenyeviti wa bodi na mameneja wa redio za jamii nchini waliohudhuria warsha ya siku tano iliyomalizika mwishoni mwa juma kwenye kituo cha Redio Sengerema mkoani Mwanza kwa ufadhili wa SIDA na uratibu wa UNESCO.
  DSC_0085

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimpa mkono wa pongezi Ndugu Ismail Semkunde aliyekuwa Mwenyekiti wa Jimbo la Mlalo Chadema na kuamua kurejea CCM.
   Mzee Julius Kavurai aliyekuwa Katibu wa Jimbo la Mlalo Chadema akiwapungia mkono wananchi kwenye mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye yupo kwenye ziara wilayani Lushoto ya kujenga na kukiimarisha chama pamoja na kuangalia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2010 inavyoendelea.
   Mzee Charles Kagonji akiwasalimia wananchi na kutamka rasmi kurejea CCM yeye pamoja na wafuasi wake aliokuwa nao Chadema.
  Katika mkutano huu wengine waliorudi CCM kutoka Chadema ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Jimbo Ismail Semkunde,aliyekuwa Katibu wa Jimbo Mzee Julius Kavurai na aliyekuwa mgombea wa udiwani kwa tiketi ya Chadema Ndugu Ally Gaha
   Wananchi wakinyoosha mikono juu kama ishara ya kumkaribisha CCM Mzee Charles Kagonji.
   Umati wa watu waliohudhuria mkutano.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimkabidhi kadi ya CCM Mzee Charles Kagonji kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Sunga jimbo la Mlalo wilayani Lushoto.

  0 0

   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka (kulia) na Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Azania Bw. Rukwaro Senkoro (kushoto) kwa pamoja wakionyesha hundi ya shilingi milioni mia moja iliyotolewa kwa wakazi wa kata Mvuleni, Manzese mkoani Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kupitia asasi ya Tanzania Financial Services for Underserved Settlement (TAFSUS) ili kuboresha makazi yao
   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni mia moja kwa wakazi wa kata Mvuleni, Manzese ikiwa ni mkopo uliyotolewa kwa wakazi hao ili kuboresha makazi yao. Mkopo huo ulitolewa na Benki ya Azania kupitia asasi ya Tanzania Financial Services for Underserved Settlement (TAFSUS). Kutoka kulia ni Mwakilishi toka UN HABITAT Bw,   Phillemon Mutashubirwa, Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Azania Bw. Rukwaro Senkoro, na Mkurugenzi wa Bodi ya wakurugenzi ya TAFSUS Bw. John Ulanga.
   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni mia moja kwa wakazi wa kata Mvuleni, Manzese ikiwa ni mkopo uliyotolewa kwa wakazi hao ili kuboresha makazi yao. Mkopo huo ulitolewa na Benki ya Azania kupitia asasi ya Tanzania Financial Services for Underserved Settlement (TAFSUS). Wa kwa kulia ni Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Azania Bw. Rukwaro Senkoro, na Mkurugenzi wa Bodi ya wakurugenzi ya  TAFSUS Bw. John Ulanga (wa pili kulia) na wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mvuleni, Manzese Bw. Muhidini Lyomeko.
  Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Azania Bw. Rukwaro Senkoro, akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni mia moja kwa wakazi wa kata Mvuleni, Manzese ikiwa ni mkopo uliyotolewa kwa wakazi hao ili kuboresha makazi yao. Mkopo huo ulitolewa na Benki ya Azania kupitia asasi ya Tanzania Financial Services for Underserved Settlement (TAFSUS) ili kuboresha makazi ya wakazi hao. Wapili kulia ni Mkurugenzi wa Bodi ya wakurugenzi ya  TAFSUS Bw. John Ulanga, mgeni rasmi wa hafla hiyo Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka (wapili kushoto) na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mvuleni, Manzese Bw. Muhidini Lyomeko (wa kwanza kushoto)  Wakazi wa kata ya Manzese na mtaa wa Mvuleni iliyopo Jijini Dar es Salaam wamepokea zaidi ya shilingi milioni 100 kutoka benki ya Azania kwa ajili ya kuboresha makazi yao duni.

  Fedha hizo zinazotolewa kwa udhamini wa asasi inayoshughulikia na uboreshwaji wa makazi duni nchini Tanzaia ya Tanzania Financial Services for Underserved Settlement (TAFSUS) itatolewa kama mikopo ya kati ya shilingi milioni 1.5 mpaka milioni 9 kwa kila kaya.

  Akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika katika kata ya Mvuleni mwishoni mwa wiki, Waziri wa Ardhi, Nyumba, na Maendeleo ya Makazi, Mh. Prof. Anna Tibaijuka alisema mradi wa kuboresha nyumba Manzese Mvuleni umeonyesha mafanikio makubwa na kuboresha maisha ya wakazi hao.

  “Ninafurahi kuwepo katika uzinduzi huu wa awamu ya pili na tatu  ya mradi huu, kwani hii ni moja ya juhudi ambazo Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ingependa kuziona kote nchini katika  kuboresha makazi ya  Watanzania.

  “Kama unavyofahamu, namna bora ya kuboresha maisha ya mwanadamu ni kwanza kuboresha makazi yake.  Ukishakuwa na makazi bora, basi hata afya yako itakuwa bora zaidi, watoto wako wataishi na kukua katika mazingira bora zaidi, watajisomea katika mazingira bora zaidi, na mambo mengine mengi yatakuwa bora zaidi,” alisema Prof. Tibaijuka.

  Naye mkurugenzi wa bodi ya wakurugenzi ya TAFSUS Bw. John Ulanga alisema TAFSUS ni chombo cha Kitaifa kinachotoa huduma za udhamini wa kifedha ili kusaidia kuboresha makazi hapa Tanzania hasa katika maeneo ambayo yana changamoto ya ubora wa makazi na ufinyu wa huduma mbalimbali.

  “Lengo la msingi la TAFSUS ni kuhamasisha na kuwezesha taasisi za fedha kutoa mikopo ya kuboresha makazi pale ambapo kwa taratibu za kawaida, mikopo hiyo isingetolewa. Mikopo hiyo hutolewa kuboresha makazi yakiwemo yale yasiyo rasmi na kuziwezesha jamii zenye kipato cha chini kuwa na maisha bora,” alisema Bw. Ulanga.

  Aliongeza kuwa lengo ni kufikia kaya 2000 na kutekeleza  miradi yenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 3.58  kufikia mwishoni mwa  mwaka 2015.

  “Ili kutimiza malengo haya, TAFSUS ilipokea dola za kimarekani zipatazo million moja na laki mbili kutoka UN-Habitat, kwa ajili ya kuwezesha miradi ya Jamii kupata mikopo ya uboreshaji makazi,” Bw. Ulanga alisema.

  Bw. Ulanga aliongeza kuwa TAFSUS imetenga fungu la fedha la mikopo yenye thamani ya shilingi  250,000,000 kwa ajili ya kuboresha nyumba za Mvuleni, takwimu zikionyesha kwamba mtaa huo wa Manzese Mvuleni una jumla ya kaya 2180 na makadirio ya jumla ya wakazi ni 10,645. 

  Ningependa kusema kuwa sisi kama TAFSUS tunajipanga vizuri zaidi kuhakikisha huduma zetu zinakuwa bora zaidi na tunawakifikia watu wengi zaidi, ikiwemo kubuni miradi itayosaidia kuboresha makazi ya Jiji letu na majiji mengine hapa Tanzania, na kuchangia katika kuboresha maisha ya Watanzania hasa wenye kipato cha chini,” Bw. Ulanga aliongeza.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Azania Bw. Rukwaro Senkoro alisema benki hiyo iliitikia wito wa kutoa mikopo ya riba na masharti nafuu kwa ajili ya kuunga mkoni mradi huo wa kuboresha makazi ya watu, wakitambua kwamba wateja wao wanatokana na jamii, na hivyo kuwasaidia kuboresha maisha yao ni fahari ya benki hiyo.

  Wakazi wa Manzese Mvuleni walishauriwa na Waziri Tibaijuka kutumia Ushiriki wa Nyumba (Housing Cooperative) waliyoianzisha kukusanya hela za kutosha na kuchukua mikopo kutoka kwenye mabenki au kushirikiana na wawekezaji wengine kujenga majengo ya vitega uchumi kwenye eneo hilo.

  0 0

  KIKUNDI cha ngoma cha selo kilichopo katika kijiji cha Kweingoma, wilayani Handeni, mkoani Tanga, kimesema kimepania vikali Desemba 13 mwaka huu kufanya balaa katika tamasha la Handeni Kwetu 2014, litakalofanyika wilayani hapa.

  Shauku ya kikundi hicho imetolewa na Kiongozi wao Zaina Selemani, alipozungumzia umuhimu wa tamasha hilo, ambalo mwaka jana walishindwa kushiriki kutokana na wasanii wake wengi kukabiliwa na mambo ya kifamilia, ikiwamo kuugua na kuuguliwa.

  Akizungumza kwa furaha kubwa, Zaina alisema ngoma ya selo ni nzuri inayoshawishi kuangalia wasanii wanapokuwa jukwaani, hivyo mashabiki na wadau wote watapata burudani nzuri.

  “Mwaka huu tutashiriki kwa nguvu zote kwasababu ni tamasha lililoanza vizuri kwa mkoa huu wa Tanga, maana vikundi vingi kutoka sehemu mbalimbali za Handeni na mkoa wa Tanga vinashiriki,” alisema.

  Naye Mratibu Mkuu wa tamasha hilo, Kambi Mbwana, alisema kuwa kwa siku kadhaa walikuwa wakifanya ziara kadhaa katika vijiji ambavyo vina vikundi vya ngoma za asili ili vishiriki, hususan vile ambavyo mwaka jana havikushiriki.

  “Tunataka kuongeza wigo wa vikundi kutoka ndani ya Tanga na nje pia, ukizingatia kuwa tunahitaji tamasha lenye nguvu na mguso pia ili kukuza sekta ya utamaduni na uchumi wa nchi yetu,” alisema Mbwana.

  Tamasha la Handeni Kwetu lililopangwa kufanyika Desemba 13 katika Uwanja wa Azimio (Kigoda Stadium), ni moja ya matukio makubwa mkoani Tanga yanayokutanisha mamia ya watu kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania.


  0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji na Uwezeshaji Dkk. Mary Nagu akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 65 tangu kuanzishwa Jamhuri ya Watu wa China jana jijini Dar es Salaam.
   : Balozi wa China nchini Tanzania Balozi Lui Youqing akigonga glasi ya mvinyo wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 65 tangu kuanzishwa Jamhuri ya Watu wa China jana jijini Dar es Salaam.
   Picha ya Keki kwa ajili ya hafla ya maadhimisho ya miaka 65 tokea kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China hafla hiyo imefanyika jana jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Uwekezaji na Uwezeshaji) Dkt. Mary Nagu  na Balozi wa China nchini Tanzania Balozi Lui Youqing wakikata Keki  wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 65 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China jana jijini Dar es Salaam.
   Balozi wa China nchini Tanzania Balozi Lui Youqing (katikati) akiteta jambo na baadhi ya wageni waalikwa katika hafla ya kuadhimisha miaka 65 tokea kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan Rugimbana na Afisa anayeshughulikia masuala ya Menejimenti na Programu wa Aga Khana Development Network Bw. Navroz Lakhani.,

   Msanii wa Jamhuri ya Watu wa China akicheza mchezo wa Wushu wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 65 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China jana jijini Dar es Salaam.
   Baadhi ya wageni wakisoma vitabu wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 65 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China jana jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wageni wakifuatilia michezo mbalimbali kutoka kwa wasanii wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 65 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China jana jijini Dar es Salaam. Picha na Frank Shija, WHVUM.
  ========  ========  =======
  Tanzania yaendelea kunufaika na uhusiano mwema ulipo baina yake na Taifa la China.

  Na; Daud Manongi,    WHVUM.

  Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2013 China imetoa msaada wa zaidi ya dola za Kimarekani bilioni 1.943 kwa ajili ya kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania, ushirikiano wa kibiashara  dola bilioni 3.7 na uwekezaji dola bilioni 2.5 na jumla ya makampuni 500 yamewekeza nchini Tanzania.

  Haya yamebainishwa na Waziri wa Nci ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji na Uwezeshaji Dkt. Mary Nagu aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla ya miaka 65 ya toka kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China jana jijini Dar es Salaam.

  Dkt Nagu amesema kuwa msaada huo utasaidia katika kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwema Bandari ya Bagamoyo, mradi wa EPZ, usambazaji wa umeme ukanda wa Kaskazini – Mashariki, Elimu kwa njia ya mtandao,Serikali Mtandao kwa ajili ya Zanzibar na Umeme wa upepo katika mkoa wa Singida. Aliongeza kuwa kukamilika kwa miradi hiyo kutafungua njia za uchumi na kusababisha Tanzania kuwa na uchumi imara na endelevu.

  “Najisikia faraja kusema kuwama pamoja na mafanikia chanya tunayopata Tanzania bado ina miradi mingi ambayo inahitaji msaada wa kifedha na kitaalam kutoka kwa Jamhuri ya Watu wa China na ni imani kuwa wataendelea kutoa ushirikiano katika kufanikisha miradi hiyo” Alisema Dkt. Nagu.

  Kwa upande wake Balozi wa China hapa nchini Balozi Lui Youqing amesema kuwa nchi yake itaendelea kuisaidi Tanzania kwa kuwa kumekuwa na mahusiano mazuri nay a muda mrefu baina ya nchi hizi mbili.

  Balozi Youqing ameongeza kuwa Tanzania inavutia wakezaji kwa kuwa na mazingira salama ya kisiasa na kijamii ambapo anashawishika kuunganisha wawekezaji wa China kushirikiana na wawekezaji wengine katika kupunguza umasikini na kuleta maendeleo akitolea mfano ushirikiano katika sekta ya majengo.

  “Tanzania ni nchi kubwa yenye maono na inayovutia zaidi kimataifa kutokana na uimara wake katika Nyanja za siasa na uchumi jamii, imekuwa na ushawishi wa hali ya juu katika anga za kikanda na kimataifa, hali inafanya wawekezaji kutoka sehemu kama EU, US, Japana na kwingineko waongeze uwekezaji, ata mimi binafsi nashawishika kuwashawishi wawekezaji wa China kuwekeza zaidi katika nchi hii” Alisema Balozi Youqing.

  China inasherehekea miaka 65 toke kuanzishwa kwake mnamo mwaka 1949, wkati huo huo ni miaka 50 sasa tokea Taifa kuanzisha mahusiano ya kidiplomasia kati yake na Tanzania uhusiano ambao umeasisiwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Mao Zedong.
  Mwisho.


  0 0

   Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, akiongea wakati wa kikao cha Wataalamu kutoka nchi za Zambia, Kenya na Tanzania Kujadili Utekelezaji wa Mradi wa Kuunganisha Mtandao wa Umeme katika Gridi za nchi hizo. Wengine kutoka kushoto ni Balozi wa Zambia nchini Judith Kapijimpanga, Katibu Mkuu Wizara ya  Migodi, Nishati na Maendeleo ya Maji Zambia, Charity Mwansa, Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya  Nishati Petroli Kenya, Mhandisi Richard Mwiru na Katibu Mkuu Msaidizi  wa Jumuiya ya Soko  la pamoja la nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika anayeshughulikia miradi (COMESA), Dkt. Kipyego Cheluges.
   Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya  Nishati Petroli Kenya, Mhandisi Richard Mwiru (wa pili kulia) akiongea jambo wakati wa kikao hicho, ambapo ameeleza utayari wa nchi ya Kenya katika utekelezaji wa mradi huo.
   Sehemu ya Wataalamu kutoka nchi za Zambia, Kenya na Tanzania wakifuatilia kikao chaKujadili Utekelezaji wa Mradi wa Kuunganisha Mtandao wa Umeme katika Gridi za nchi hizo.
  Mtaalamu Mwelekezi kutoka nchi ya Zambia Siyanga Zomba, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji na hatua mbalimbali zilizofikiwa katika utekelezaji wa mradi wa kuunganisha Mtandao wa Umeme katika Gridi kwa nchi za Zambia, Kenya na Tanzania.


  Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam.

  Wataalamu kutoka nchi za Zambia, Kenya na Tanzania kutoka Wizara zinazoshughulika na masuala ya nishati wameanza majadiliano ya Utekelezaji wa Mradi wa Kuunganisha Mtandao wa Umeme katika Gridi za nchi hizo.   Kikao cha Majadiliano hayo kiliongozwa na Makatibu Wakuu kutoka katika nchi husika na kitafuatiwa na mkutano wa Mawaziri utakaofanyika tarehe 30 Septemba, 2014 jijini Dar es Salaam.
  Akizungumza katika kikao hicho Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi amezitaka nchi hizo kuunga mkono jitihada za utekelezaji wa mradi huo kutokana na umuhimu wake kiuchumi ikiwemo kuhakikisha nchi hizo zinakuwa na nishati ya umeme ya kutosha.

  Aidha, ameongeza kuwa, tayari Tanzania imeanza kufanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha inaanza utekelezaji wa mradi huo ambao umechukua kipindi kirefu kuanza kutekelezwa na kuongeza kuwa, Tanzania iko tayari kushiriki katika utekelezaji wa mradi huo ikiwemo kuhakikisha kwamba mradi huo unafanikiwa.

  Kwa upande wake mwakilishi wa Katibu Mkuu  Wizara ya Nishati na Petroli Kenya  Mhandisi Richard Mwiru, ameeleza kuwa, kuna matokeo bora yatakayotokana na utekelezaji wa mradi huo, matokeo ambayo yatasaidia biashara ya umeme na upatikanaji wa umeme rahisi kwa   nchi hizo. Aidha, ameongeza kuwa, nchi ya Kenya iko tayari kushiriki katika utekelezaji wa mradi huo.

  Naye Katibu Mkuu Wizara ya Migodi,Nishati na Maendeleo ya Maji  wa Zambia, Charity Mwansa, ameeleza kuwa, anatarajia mkutano huo utatoa fursa zitakazosaidia utekelezaji wa mradi huo kuendelea kutoka mahali ulipofikia ili kuweza kutoa matokeo chanya yatakayokuwa na manufaa kwa nchi hizo  ukizingatiwa kuwa, nchi hizo zimebahatika kuwa na rasilimali asilia za kutosha.

  Aidha, Katibu Mkuu Msaidizi  wa Jumuiya ya Soko  la pamoja la nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika anayeshughulikia miradi (COMESA), Dkt. Kipyego Cheluges amezitaka nchi hizo kuhakikisha kwamba mradi huo unatekelezwa  kutokana na manufaa ambayo nchi hizo zitayapata ikiwemo bara la Afrika na kuongeza kuwa, COMESA itashirikiana kwa karibu na nchi hizo kuhakikisha kwamba, mradi unatekelezwa kama ulivyopangwa.
   


  0 0

  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (Meza Kuu-Katikati), akizungumza na wawakilishi wa Kampuni mbalimbali zinazohusika kusambaza umeme vijijini kutoka India, China na Sri Lanka zinazofanya kazi katika Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kuhusu utekelezaji wa miradi husika.
  Wawakilishi wa Kampuni mbalimbali zinazohusika kusambaza umeme vijijini kutoka India, China na Sri Lanka zinazofanya kazi katika Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi pamoja na baadhi ya Mameneja wa Tanesco wa Mikoa husika, wakitoa mrejesho kwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (Meza Kuu – Katikati), kuhusu hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Miradi husika. Kulia kwa Waziri Muhongo ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Charles Kitwanga na kushoto kwa Waziri ni Kamishna Msaidizi wa Nishati sehemu ya Umeme, Mhandisi Innocent Luoga.
   Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA), Dk. Lutengano Mwakahesya akizungumza katika mkutano baina ya Waziri wa Nishati na Madini na kampuni zinazosambaza umeme vijijini kwa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini. Mwakahesya aliahidi kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kwa kiwango kinachotakiwa.
   
  ========  ======  ========
  WAKANDARASI UMEME WASIOWAJIBIKA KUNYANG’ANYWA TENDA
  Na Veronica Simba.

  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amezitaka Kampuni zilizopewa tenda kusambaza umeme vijijini kukamilisha kazi hiyo kwa wakati na kwa kiwango kinachotakiwa vinginevyo watanyang’anywa tenda hizo.

  Aliyasema hayo mwishoni mwa wiki mjini Dodoma katika Mkutano baina yake na wawakilishi wa Kampuni husika kutoka India, China na Sri Lanka zinazofanya kazi katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi pamoja na Mameneja wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) wa mikoa hiyo na Wakala wa Umeme Vijijini (REA).

  Profesa Muhongo aliitisha Mkutano huo kwa lengo la kupokea taarifa kutoka kwa Watendaji wa Kampuni hizo kuhusu hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini kabla ya kutembelea miradi hiyo kwa mara nyingine kama ambavyo amekuwa akifanya mara kwa mara kujiridhisha na maendeleo yake.

  Akizungumza katika Mkutano huo mara baada ya kupokea taarifa za utekelezaji kutoka pande zote, Waziri Muhongo alimwagiza Mkurugenzi Mkuu wa REA, Dk. Lutengano Mwakahesya kuhakikisha utekelezaji wa miradi hiyo unafuatiliwa kwa ukaribu na kusitisha tenda mara moja kwa kampuni zitakazobainika kutotimiza makubaliano ya mkataba walioingia.

  “Fuateni utaratibu wa kisheria kwa kutumia vifungu vilivyomo kwenye mkataba vinavyoelekeza kuchukua hatua stahiki kwa kampuni isiyotekeleza wajibu wake ipasavyo,” alisisitiza Muhongo.

  Aliongeza kuwa Serikali imedhamiria kuhakikisha inatimiza ahadi yake ya kuwapatia Watanzania umeme ili wajikwamue katika lindi la umaskini kwa kukuza kipato chao na cha Taifa kwa ujumla hali itakayofanya Tanzania kufikia uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.

  “Yeyote atakayetukwamisha au kuturudisha nyuma katika kufikia malengo yetu ya kuwaondolea Watanzania umaskini, tutapambana naye na kamwe hatutampa nafasi,” alisema Muhongo.

  Vilevile, aliwataka Mameneja na watendaji wengine wa Tanesco kuachana na utamaduni wa kukaa ofisini na kusubiri ripoti za utekelezaji wa miradi badala yake watembelee miradi wanayosimamia na kuhakikisha kazi inafanyika kama inavyotakiwa.

  Aidha, Waziri Muhongo aliwataka wakandarasi waliopewa tenda husika kuwa wakweli na waaminifu na kuachana na tamaa hususan wanapopewa kazi ambayo wanajua hawana uwezo wa kuitekeleza ipasavyo ili kuwapa nafasi wengine wenye uwezo huo.

  Alisema ni bora kwa Mkandarasi kukubali kazi anayoimudu ili aifanye kwa ubora unaotakiwa na hivyo kujiongezea sifa za kupewa kazi nyingine kuliko kuomba kazi kubwa asiyoweza kuitekeleza kikamilifu na matokeo yake anaharibu na kupoteza sifa ya kufikiriwa kupewa kazi nyingine.

  Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Charles Kitwanga aliwataka wote wanaohusika na utekelezaji na usimamizi wa miradi hiyo ya kusambaza umeme vijijini kutimiza wajibu wao kwa vitendo.

  “Achaneni na maneno maneno, mimi nataka kuona vitendo, nataka kuona matokeo,” alisisitiza na kuongeza kwamba hakuna sababu ya Wakandarasi kusuasua katika utekelezaji wa miradi hiyo kwani walioomba wenyewe wakijinadi kuwa wanaweza.

  Naye Kamishna Msaidizi wa Nishati Sehemu ya Umeme, Mhandisi Innocent Luoga aliwataka Wakandarasi hao kujituma na kufanya kazi inavyostahili pasipo kusubiri kufuatwa-fuatwa na kuhimizwa kwa suala ambalo ni wajibu wao.

  Wakichangia mawazo katika Mkutano huo, Mwenyekiti wa Bodi ya REA, Edmund Mkwawa na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala huo, Dk. Mwakahesya waliahidi kufanya kazi bega kwa bega na wadau mbalimbali wa sekta hiyo ili kuhakikisha Watanzania hususan walioko vijijini wanapatiwa nishati ya umeme kama Serikali ilivyodhamiria na kuahidi.

   


  0 0


  0 0

    Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama mbaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASAT) akizungumza katika tamasha la Uimbaji na Uchangiaji wa Ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Segerea jijini Dar es Salaam na kuahidi kutoa sh. milioni 6 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa kanisa hilo. Msama alikuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo akimwakilisha Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Miochezo, Dk. Fenela Mukangala.
   Mchungaji Emmanuel Masanja 'Masanja Mkandamizaji' aliguswa na kutoa ahadi ya shilingi milioni 1 katika hafla hiyo.
  "Mimi na familia yangu tutatoa milioni 1".
   Familia mbalimbali ziliguswa na kutoa ahadi za kuchangia ujenzi wa kanisa hilo.
   Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la KKKT Usharika wa Tabata Matumbi, Mchungaji Christosiler Kalata akimkabidhi Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama sehemu ya mchango walioahidi katika tamasha la Uimbaji na Uchangiaji wa Ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Segerea jijini Dar es Salaam. Usharika huo ulitoa ahadi ya sh. laki 7.
   Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akipokea mchango wa Usharikia wa Kanisa la KKKT Usharika wa Tabata Matumbi kutoka kwa Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo Christosiler Kalata .
   Familia mbalimbali ziliguswa na kutoa ahadi za kuchangia ujenzi wa Kanisa hilo.
   Watu mbalimbali waliahidi kutoa michango yao kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa Kanisa hilo.
  Mwimbaji wa nyimbo za injili, Edson Mwasabwite alichangia kiasi cha sh. laki moja.
   

  MJUMBE wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Alex Msama ametoa kitita cha sh. mil 6 katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika Segerea.  Msama ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, alitoa kiasi hicho katika harambee hiyo ya kufanikisha ujenzi huo, iliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubelee jijini Dar es Salaam, huku akitoa na ushuhuda wa maisha yake mpaka kufikia hatua aliyofikia sasa.


  Akizungumzia ushuhuda huo, Msama aliwataka waumini kuiga mfano wake kwa kujitolea bila ya kugeuka nyuma, kwani ana imani Mungu yupo na anatenda muujiza kama alioutenda kwake.

  "Unajua mimi katika maisha yangu hakuna ninayemwamini zaidi ya Bwana Yesu, kwa kuwa bila ya yeye mie nisingekuwa hapa nilipo, kwa taarifa yenu wapendwa mimi nilishakuwa dereva taxi, nilishakuwa kondakta wa daladala, lakini Mungu ni mwema na anatenda muujiza mpaka mimi kuwa hivi," alisema Msama.

  Msama ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, aliongeza kuwa hata hivi karibuni katika ajali aliyoipata akienda Dodoma licha ya kupinduka gari mara nne lakini alitoka akiwa hai.

  Harambee hiyo iliyoenda sambamba na mnada, ilihudhuriwa na wasanii mbalimbali wa muziki wa Injili kama Masanja Mkandamizaji, Edson Mwasabwite aliyeimba wimbo wa Ni kwa neema tu.

  Mbali ya kiasi hicho alichotoa, Msama pia alichangia katika mnada uliofanyika katika tamasha hilo na kununua mtungi wa gesi kwa sh. laki 5.

  0 0

  Na Miza Othman Maelezo-Zanzibar                       
  Wazazi na Walezi hasa akinababa wametakiwa kuwafuatilia watoto wao wakati wanapokuwa Skuli na nyumbani kwa lengo la  kuwawezesha  watoto hao  kupatia elimu iliyobora ndani ya maisha yao.
  Hayo yameelezwa leo huko Skuli ya Sekondari Tumekuja na Afisa Elimu Sekondari Zanzibar Khalifa Rashid Said  wakati alipokuwa akiwazawadia wanafunzi waliofaulu vyema katika mitihani ya majaribio ya kidato cha nne (Form iv) Septemba 2014.
  Amesema  watoto wengi wanakosa kupata elimu iliyobora kutokana na kukosa ushauri na kutokuwa  karibu kwa wazazi  wao jambo ambalo linarudisha nyuma  maendeleo yao ya elimu.
  “Lazima wazazi wawe  karibu na watoto wao kwa lengo la kuwashauri ili kufanikiwa katika masomo yao na kujiletea maendeleo katika maisha yao” alisema Khalifa Rashid Said”.
  Aidha amewataka walimu kuwashajihisha wanafunzi kusoma masomo ya Sayansi kwani hivi sasa yamepewa  kipaumbeli kwani kumekuwa na uhaba wa walimu wa masomo hayo katika skuli mbali mbali za Unguja na Pemba.
  Katibu wa Kamati ya  Skuli ya Tumekuja na  Hurumzi (TUMEHURU)   Khamis Hamad amesema katika kuyandaa  mitihani hiyo Tume hiyo iliweza kujitahidi kufanyakazi ili kuhakikisha mitihani hiyo inafanyika bila kutumia udanganyifu.

  Amesema lengo kuu la kufanya majaribio hayo ni kukuza uhusiano kati ya Skuli hizo mbili na kujua changomoto zilizowakabili  katika mitihani hiyo  ikiwemo uhaba wa fedha pamoja na uhaba wa vifaa vya  maabara  katika masomo ya Sayansi.
  Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Hurumzi Said Ahmed  Nassor  amesisitiza umuhiu wa mashirikiano kati ya walimu wazazi na wanafunzi wa skuli hizo mbili  na kuwataka wanafunzi kuacha tabia ya utoro.   
   Mwanafunzi Ruhayla Omar Gulam kutoka Skuli ya Sekondari ya Tumekuja kwaniaba ya wanafunzi wezake waliopata zawadi amewataka wanafunzi ambao hawakufanya vizuri katika majaribio hayo  kutovunjika moyo na kuzidisha juhudi katika masomo yao kwa lengo la kufanikiwa katika mitihani  ya taifa. 
  Majaribio hayo yalijumuisha wanafunzi 235  na kati yao wanafunzi 13 waliofanya vizuri zaidi  walipata zawadiwa  mbalimbali ikiwemo vifaa vya kusomea pamoja na fedha tasilimu.

  0 0

   Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt. Mohd Dahoma, akifungua warsha ya kupitia sheria ya kudhibiti matumizi ya tumbaku Zanzibar iliyofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resourt Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
   Mshauri wa Ufundi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kanda ya Afrika William Onzivu akizungumza na washiriki wa warsha  hiyo (hawapo pichani) katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resourt.
   Afisa kutoka Bodi ya Mapato Tanzania (TRA) akitoa mchango katika warsha ya kupitia sheria ya matumizi ya tumbako iliyofanyika Hotelini hapo. Kulia Mwenyekiti wa warsha hiyo Dkt Mohd Dahoma.
  Wajumbe wa warsha  ya kupitia sheria ya kudhibiti matumizi ya tumbaku  wakifuatilia  sheria hiyo ilipowasilishwa  na Mwanasheria wa Wizara ya Afya Amina Jabir (hayupo picha).(Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

  0 0

   Wafanyakazi wa kampuni ya Airtel Tanzania (kutoka kushoto), Kema Mabango, Abdallah Gunda na Jackson Mmbando wakishiriki katika shindano la kukuna nazi wakati wa Siku ya Wanafamilia ya Airtel, iliyofanyika katika viunga vya Fun City Kigamboni jijini Dar es salaam jana.
  Washindi wa shindano la kukuna nazi wakishow love. Kutoka
  (kushoto), Mshindi wa Kwanza, Abdallah Gunda, Mshindi wa Pili, Jackson
  Mmbando na Mshindi wa Tatu, Kema Mabango.
   Watoto wa wafanyakazi wa kampuni ya Airtel Tanzania wakiogelea wakati wa Siku ya Wanafamilia ya Airtel, iliyofanyika katika viunga vya Fun City Kigamboni jijini Dar es salaam jana.
   Watoto wa wafanyakazi wa kampuni ya Airtel Tanzania wakishiriki katika michezo  wakati wa Siku ya Wanafamilia ya Airtel, iliyofanyika katika viunga vya Fun City Kigamboni jijini Dar es salaam jana.
   Wafanyakazi wa Airtel na familia zao wakijisevia maakuli.
   Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (kulia) akiwahudumia chakula wafanyakazi wa Airtel na familia zao.

   

  •       Airtel Family day yalenga kuongeza hamasa kwa wafanyakazi kujituma
  katika kazi zao
  Imeelezwa kuwa ufanisi wa watumishi katika ngazi mbali mbali za
  kiutendaji unaweza ukaongezeka pindi wafanyakazi wanapokutana pamoja
  na kubadilishana mawazo na viongozi wao katika hali ya kiurafiki.

  Akizungumza katika tamasha la siku ya familia ya kampuni ya simu za
  mkononi ya airtel, Meneja Rasilimali Watu wa kampuni hiyo SOPHIA
  MELAMALI, amesema kuwaweka wafanyakazi katika eneo moja na familia zao kunadumisha mshikamano baina ya wafanyakazi  na familia zao kitendo
  kinachoongeza ufanisi katika eneo la kazi.

  “Airtel tumejipanga kuwa na muundo mzuri wa kufurahia matunda ya kazi
  yetu na falilia yetu kwa kuwa hii inasaidia sana kuwafanya wafanyakazi
  wetu kukutana, kufahamiana na kufurahi na familia zao  na hatimae
  kupunguza msongo wa mawazo ya kawaida ili kuendelea kufanya kazi ya
  kuhudumia wateja wetu vyema” alisema SOPHIA MELAMALI Meneja Rasilimali Watu Airtel.

  Nao baadhi ya wafanyakazi wa airtel wamepongeza kitendo cha kampuni
  hiyo kuandaa tamasha hilo na kubainisha kwamba ni sehemu ya
  kuwawezesha wafanyakazi kufahamiana.

  Wamesema tukio hilo linawawezesha wafanyakazi kupumzika na familia zao
  pamoja na wafanyakazi wenzao katika mazingira tulivu na a kirafiki
  ADRIANA LIAMBA Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja Airtel sisi wafanyakazi wa Airtel  tumefarijika sana na jinsi ambavyo leo uongozi na kampuni  yetu ilivyotukutanisha na familia zetu zote ili tuweze kufurahia,  hii
  pia inatupa moyo wakuendelea kuwahudumia wateja ipaswavyo na pia
  kushiki katika mambo ya kijamii zaidi kwa kuziona fulsa zilizomo leo
  na baadae”

  “Mfano familia zetu tumekutana watu wa aina tofauti zikiwa na
  wafanyakazi wa baadhi ya mashirika mengine nchini, hii pia ni fulsa
  kwetu kuendelea kutengeneza wateja tutakaowahudumia kwa sasa au
  kuwekeza kwa watoto wetu ili waje kuwa wateja wa baadae,  kwa kweli
  family day party ni nzuri” alimaliza kwa kusema Bi Lyamba.

  Baadhi ya watoto walioshiriki katika tamasha hilo ANTHONY NABOLI na
  FRANCIS ALEXANDER hawakusita kuonyesha hisia zao baada ya kucheza
  michezo ya aina mbali mbali kwa kuwashuru sana wazazi wao kwa
  kuwawezesha wao kushiriki michezo mingi katika viwanja vya FUN CITY
  pamoja na kupewa zawadi nyingi.

  Nae afisa rasilimali watu wa Airtel na mratibu wa Family party hiyo
  Bw, Mubaraka Kibarabara alisema “tamasha letu la familia mwaka huu
  limekuwa na mafanikio makubwa hasa kwa kuwapa nafasi wafanyakazi siku
  nzima wakicheza michezo mbalimbali na kufurahi ikiwemo ile ya kuvuta
  Kamba, kuimba karioke, kuogelea, kubembea katika mashine za kisasa, na
  kuwepo kwa shindano la kipekee kabisa lililovuta hisia za wengi la
  wanaume kushindana kukuna nazi

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za ufunguzi wa barabara ya Mwenge –Tegeta yenye urefu wa kilometa 12.9 katika eneo la Lugalo, jijini Dar es salaam. 

  Taarifa iliyotolewa leo jijini Dar esalaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Muhandisi  Musa Iyombe imeeleza kuwa sherehe za ufunguzi wa barabara hiyo zitafanyika tarehe 1, Oktoba ,2014 katika eneo la Lugalo njia panda ya Kawe kuanzia saa nne asubuhi.

  Taarifa  hiyo imeeleza kuwa kukamilika kwa upanuzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 12.9 ni sehemu ya mkakati wa serikali wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es salaam.

  Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
   

older | 1 | .... | 374 | 375 | (Page 376) | 377 | 378 | .... | 1898 | newer