Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

KINANA , NAPE WAITEKA KIBAHA

$
0
0

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiwasalimia wakazi wa Kibaha mjini wakati wakiwasili kwenye uwanja wa mkutano .
 Kikundi cha ngoma cha Kisamamwe kikitumbuiza ngoma ya Afrika kabla ya kuanza kwa mkutano wa hadhara ambapo Katibu Mkuu wa CCM alihutubia wananchi wa Kibaha mjini.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Kibaha mjini ambapo aliwaambia wapinzani wamekosa hoja ya msingi kiasi cha kuamua kufanya maandamano ya kuleta vurugu nchini.
 Sehemu ya Umati wa watu wakisikiliza mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Wana CCM wakiwa kwenye mkutano
 Mbunge wa Kibaha mjini Silvestry Francis Koka akihutubia wakazi wake na kuwaambia kuwa pamoja na jitihada zote anazofanya maji bado ni donda sugu ila ufumbuzi upo njiani.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Kibaha mjini wakati wa mkutano wa hadhara ambapo aliwaambia viongozi wa halmashauri hawana budi kukaa na wafanya biashara ndogo ndogo kujadili kodi kabla ya kuwapangia kuona kama wana uwezo wa kulipa ama hapana hii itasaidia kupunguza lawama na mikingamo baina ya wafanya biashara na halmashauri.

PRESIDENT KIKWETE ADDRESSES THE USAID FORUM ON “FRONTIERS IN DEVELOPMENT: ENDING EXTREME POVERTY”, 19TH SEPTEMBER, 2014, WASHINGTON, D.C

$
0
0
 President Kikwete deliveres a keynote speech at  the USAID Frontiers in Development Forum: Ending Extreme Poverty at the Reagen Building in Washington  DC.
  President Kikwete deliveres a keynote speech at  the USAID Frontiers in Development Forum: Ending Extreme Poverty at the Reagen Building in Washington  DC
  President Kikwete in a souvenir photo with the US Secretary of State Mr John Kerry  and the USAID Administrator Dr Rajiv Shah  before the start of  the USAID Frontiers in Development Forum: Ending Extreme overty at the Reagan Building in Washington  DC.
STATE HOUSE PHOTOS.

TANZIA

$
0
0
Familia ya aliekua mwanamuziki wa bendi za super matimila na tanzania one theatre TOT Fredy Mwalasha inasikitika kutangaza cha baba yaompendwa Fredy Mwalasha kilichotokea saa 5 asubuhi ya leo tarehe 19/9/2014,mazishi yanatarajia kufanyika mkoani morogoro mara baada ya mwili kuwasili...

BONDIA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' AKIZIPIGA NA YUSUPH MNYETO KATIKA KAMBI YA ILALA AMANA

$
0
0
 Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akioneshana umwamba na Yusuph Mnyeto wakati wa mazoezi yanayo endelea katika kambi ya Ilala Amana CCM Dar es salaam jana .
 Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akioneshana umwamba na Yusuph Mnyeto wakati wa mazoezi yanayo endelea katika kambi ya Ilala Amana CCM Dar es salaam jana.
 Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akioneshana umwamba na Yusuph Mnyeto wakati wa mazoezi yanayo endelea katika kambi ya Ilala Amana CCM Dar es salaam jana .
Bondia Yusuph Mnyeto kushoto akitunishiana misuli na Ibrahimu Class ' King Class Mawe' baada ya kumaliza kupigana katika mazoezi yanayoendelea kwenye kambi ya Ilala Dar es salaam jana picha picha na SUPER D BLOG
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' katikati akijazwa katika fomu uku akiulizwa maswali mbalimbali kuhusu upimaji VVU UKIMWI wakati wa kuamasisha wakazi wa magomeni kagera kupima kwa hiali jana


Bondia Ibrahimu Class' King Class Mawe' baada ya kupima vvu ukimwi wakati wa kuamasisha wakazi wa magomeni kagera kupima afya zao jana

Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwa na bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kulia na Mikidadi Boika  wakati wa kampeni ya kupima vvu ukimwi iliyokuwa ikifanyika magomeni kagera Dar es salaam jana Super D na king class walipima kwa ajili ya kuamasisha wakazi wa kagera kutambua afya zao picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

SHIRIKA LA NYUMBA LATOA MASHINE 28 ZA KUFYATULIA MATOFALI KWA VIJANA MKOANI PWANI

$
0
0

 Meneja wa Shirika la Nyumba mkoa wa Pwani Pauline Mrango akisoma Hotuba ya makabidhiano ya mashine 28 za kufyatulia matofali kwa vikundi vya vijana katika halmashauri zote za mkoa wa Pwani.

Shirika la Nyumba la Taifa limetoa mashine hizo zenye gharama ya zaidi ya shilingi milioni 12 pamoja na mafunzo kwa vijana ya wiki mbili ambapo baada ya kumaliza mafunzo Shirika litatoa msaada wa shilingi laki tano kwa kila kikundi kama mtaji .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimpa mkono wa pongezi Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa pwani Pauline Mrango kwa kutoa mashine 28 za kuwasaidia vijana.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kuashiria makabidhiano ya mashine za kufyatulia matofali zilizotolewa na shirika la nyumba la Taifa kwenda kwenye halmashauri zote za mkoa wa Pwani.
Mashine 28 zitawasaidia vijana mkoa wa Pwani kuondokana na tatizo la ajira, pili litasaidia sana katika utunzaji wa mazingira,zitasaidia wananchi kujenga nyumba za kisasa na kwa bei nafuu.(Adam Mzee)







UJUMBE WA CHAMA CHA FRELIMO CHA MSUMBIJI CHAKUTANA NA BAADHI YA WAJUMBE WA CHAMA CHA MAPINDUZI ZANZIBAR.

$
0
0
 Mjumbe wa Kamati ya CCM Taifa Bi. Khadija Hassan Aboud akimkaribisha Mbunge ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha FRELIMO cha Msumbiji Bi. Nyeleti Mondlane Ofisi kuu ya CCM Zanzibar.
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha FRELIMO cha Msumbiji Bi. Nyeleti Mondlane akisaini kitabu cha wageni alipofika Ofisi kuu ya CCM Zanzibar (kulia) Katibu wa FRELIMO Zanzibar Bw. Agostino Andrea.
 Kiongozi wa Ujumbe wa Chama cha FRELIMO Bi. Nyeleti Mondlane (watatu kushoto) akibadilishana mawazo na wenyeji wake wajumbe wa Chama cha Mapinduzi katika Ofisi Kuu Kisiwandui Zanzibar ikiwa ni mkakati wa kuimarisha Uhusiano wa Vyama vyao na kuzindua Kampeni ya Uchaguzi Mkuu Nchini Msumbiji.
 Picha ya pamoja ya Ujumbe wa Chama cha FRELIMO na baadhi ya wajumbe wa Chama cha Mapinduzi CCM wakiongozwa na Mjumbe wa Kamati ya CCM Taifa Bi. Khadija Hassan Aboud wakatikati.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

=========  ========  ========
CHAMA cha FRELIMO kimesema Wananchi wa Msumbiji wataendelea kukumbuka na kuthamini juhudi mbali mbali zilizochukuliwa na Watanzania wakati wa harakati za ukombozi na kuwafanya kuwa watu huru.

Kauli hiyo imetolewa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha FRELIMO Bibi Nyeleti Mondlane, alipokuwa na mazungumzo maalum na Uongozi wa CCM Zanzibar, hapo Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandui.

Amesema Wananchi wa Msumbiji wana kila sababu ya kuwapongeza Watanzania kutokana na misaada yao ya hali na mali, jambo lililosaidia kwa kiasi kikubwa wananchi wa Msumbiji kujikomboa na kuishi wakiwa watu huru ndani ya nchi yao huru.

Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya FRELIMO na pia ni Mbunge, amesema nchi hiyo imo katika amani na utulivu mkubwa, hali inayotoa fursa kwa Serikali ya FRELIMO  kuweza kufanikisha shughuli za kimaendeleo kwa maslahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Ametumia kikao hicho kutoa wito kwa Wana FRELIMO wanaoishi Zanzibar kuendeleza mashirikiano ya karibu na wananchi wa Tanzania, CCM na Serikali zake, ili umoja na maendeleo kwa wananchi wa pande zote mbili.

Naye Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya CCM Mhe. Khadija Hassan Aboud, amemuhakikishia Bibi Mondlane kuwa Chama Cha Mapinduzi kitafanya kila linalowezekana kuhakikisha uhusiano wa kihistoria baina ya CCM na FRELIKO unaendelezwa kwa nguvu zote.

Amesema Vyama vya CCM mrithi wa ASP na FRELIMO, vina undugu wa kihistoria uliodumu kwa miaka mingi na kumesisitiza haja kwa Viongozi wa Vyama hivyo wanapaswa kuuendeleza na kuudumisha kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizo.

Bibi Mondlane yupo Visiwani Zanzibar kwa ziara ya kikazi ya kichama, ambapo katika mazungumzo hayo aliongoza Ujumbe wa watu watano, akiwemo Balozi Mdogo wa Msumbiji nchini Zanzibar Bwana Jorge Augusto Menezes.

RAIS KIKWETE AHUDHURIA HAFLA YA KUMPONGEZA KWA UONGOZI MZURI YA USIKU WA JAKAYA JIJINI WASHINGTON DC

$
0
0
Rais Jakaya Kikwete akiwa na mtoto wa miaka minane aliejitambulisha kwa jina la Brian ambaye alitoa burudani ya kupiga kinanda wakati wa wimbo wa Taifa na nyimbo nyinginezo katika hafla ya USIKU WA JAKAYA uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya JW Mariott jijini Washington
Rais Jakaya Kikwete akiongea na Dkt Seche Malecela baada ya kupokea risala ya pongezi kwa uongozi wake nchini Tanzania  katika hafla ya USIKU WA JAKAYA uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya JW Mariott jijini Washington
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipokea makombe toka kwa Balozi wa Heshima wa Tanzania huko California Mhe Ahmed Issa kama pongezi kwa uongozi uliotukuka Rais Jakaya Kikwete akiwa na mtoto wa miaka minane Brian ambaye alitoa burudani ya kupiga kinanda wakati wa wimbo wa Taifa na nyimbo nyinginezo katika hafla ya USIKU WA JAKAYA uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya JW Mariott jijini Washington
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipokea zawadi toka Watanzania kutoka Atlanta  kama pongezi kwa uongozi uliotukuka Rais Jakaya Kikwete akiwa na mtoto wa miaka minane Brian ambaye alitoa burudani ya kupiga kinanda wakati wa wimbo wa Taifa na nyimbo nyinginezo katika hafla ya USIKU WA JAKAYA uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya JW Mariott jijini Washington.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika hafla ya USIKU WA JAKAYA uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya JW Mariott jijini Washington.

WAKAZI WA IRINGA WABURUDIKA NA UJIO WA TAMASHA LA FIESTA 2014 NDANI YA UWANJA WA SAMORA.

$
0
0
 Wasanii wa muziki wa Bongofleva Ommy Dimpo na Vanessa Mdee a.k.a Vmoney wakilishambulia jukwaa kwa pamoja mbele ya umati wa mashabiki wa tamasha la Fiesta 2014  lililofanyika jana ndani ya uwanja wa Samora mkoani Iringa,huku miluzi na shangwe zikisikika kila kona ya uwanja.Tamasha la Fiesta linatarajiwa kufanyika kesho mjini Morogoro katika uwanja wa Jamuhuri ambapo wasanii mbalimbali wa bongofleva watatumbuiza.
Baadhi ya Mashabiki wakishangqweka.
 Msanii Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongofleva,Selemani Msindi a.k.a Afande Sele Mfalme wa Rhymes,akiimba kwa hisia kubwa juu ya jukwaa la tamasha la Fiesta 2014 lililofanyika jana ndani ya uwanja wa Samora mkoani Iringa.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Linah Sanga akionesha mumahiri wake kucheza jukwaani akiwa sambamba na mmoja wa madansa wake mahiri katika tamasha la burudani la fiesta lililofanyika jana ndani ya uwanja wa samora mkoani Iringa.
Sehemu ya umati wa watu waliojitokeza kwenye tamasha hilo la Fiesta 2014 ndani ya Samora mjini Iringa hapo jana.
Anajiita Rais wa Manzese,jina lake la kisanii anajiita Madee kutoka kundi la TIP TOP CONECTIONs,akiimba mbele ya umati wa wakazi wa mji wa Iringa waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Fiesta ndani ya uwanja wa Samora hapo jana.Tamasha la Fiesta kesho linatarajiwa kufanyika ndani ya uwanja wa jamuhuri mkoani Morogoro.
Wakazi wa mji wa Iringa waliojitokeza ndani ya tamasha la Fiesta wakishangweka kwa raha zao.

MISS TANZANIA WATOA MSAADA HOSPITALI YA KILEMA NA MARANGU MOSHI

$
0
0
Washiriki wa Shindano la Redds Miss Tanzania 2014 walitoa misaada ya kijamii katika Hospitali za Misheni Kilema na ile ya K.K.K.T Marangu baada ya kutembelea Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro.


 Mwakilishi wa Kanda ya Ziwa katika Shindano la Redds Miss Tanzania 2014 Dorine Robert akimpa zawadi ya chandarua mgonjwa Jamila Msafiri aliyelazwa katika Hospitali ya Kilema Wilaya ya Moshi Vijijini Mkoani Kilimanjaro jana ambapo warembo 30 wa Miss Tanzania walitoa msaaada mbalimbali ya kijamii hospitalini hapo.
 Warembo waiangalia watoto

 picha ya pamoja ya warembo na wenyeji Hospitali ya Kilema Moshi.
 Hapa ni Hospitali ya KKKT Marangu.
 Mpigapicha wa True Vision John Lymo akiwajibika kwa kuakama taswira za warembo.






Baada ya hapo warembo na viongozi walishirikki chakula cha mchana nyumbani kwa Naibu Kamanda wa UVCCM Moshi Vijijini, Innocent Shirima Melleck.

CCM KUANZA KUWATIMUA VIONGOZI WAVIVU,WASIO NA KAZI NA WALA RUSHWA

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Mlandizi, Kibaha Vijijini, ambapo alisema kua CCM itaanza kuwafukuza viongozi wabovu na wala rushwa. Kinana yupo mkoani Pwani kuimarisha uhai wa chama, kuhimiza, na kusukuma utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia kaaikia wananchi kuhusu tika mkutano wa hadhara Mlandizi, Kibaha Vijijini, ambapo aliwananga wapinzania kwamba wanahangaika na maandamano wakati CCM wanawahangaikia mandeleo ya wananchi.
 Katibu Mkuu wa CCM, Kinana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani, Mwinshehe Mlao wakiondoka baada ya kufungua jengo la CCM Wilaya Kibaha Vijijini
 Kinana akisaidia kupaka rangi alipokagua jengo la Baraza la Ardhi la Kata ya Mlandizi iliyojengwa kwa msaada wa Diwani wa Kata hiyo, Euphresia Kadala (kushoto)
 Kinana akihutubia baada ya kufungua jengo la Baraza la Ardhi la Kata ya Mlandizi
 Kinana akipanda mti wa kumbukumbu alipotembelea Kituo cha Afya cha Mlandizi
 Kinana akizungumza baada ya kushiriki ujenzi wa jengo la kuhifadhia maiti katika Kituo cha Afya cha Mlandizi
 Kinana akipandisha bendera wakati wa uzinduzi wa shina la wakereketwa wa Kikundi cha Mshikamano Mlandizi Mjini
 Nape akimbusu mtoto Ashrafu Waziri wa mkazi wa Mlandizi wakati wa ziara kuimarisha uhai wa chama Kibaha Vijijini
 Wafuasi wa CCM, wakisikiliza kwa makini wakati Kinana akihutubia wakati wa uzinduzi wa shina la vijana la mshikamano Kibaha Vijijini. Kutoka kulia ni Flaviana Juma, Moureen Willfred na Fadhila Jumanne
 Kinana akikagua mradi wa maji katika Kijiji cha Bokomnemela Kibaha Vijijini
 Kinana akiagana na Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Dk. Hashim Mohamed baada ya kukagua mradi wa maji katika Kijiji cha Bokomnemela.
 Katibu wa CCM Mkoa wa Pwani, Joyce Masunga akihutubia katika mkutano huo
 Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini, Hamoud Jumaa akielezea kuhusu miradi mbalimbali iliyotekelezwa katika jimbo hilo kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
 Mkazi wa Mlandizi akiuliza swali katika mahakama ya wazi ya Kinana katika kutano huo
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza akijibu swali la mwananchi aliyelalamikia kitendo cha waalimu kuwafukuza wanafunzi waliokosa kutoa michango shuleni ambapo Kinana alikemea vitendo hivyo.
 Baadhi ya wanachama wa Chadema wakionesha kadi baada ya kujiunga na CCM katika mizikutano uliofanyika Kibaha Mlandizi
Wanachama wapya wakila kiapo baada ya kukabidhiwa kadi za chama  hicho

WAREMBO MISS TANZANIA WASHUHUDIA UPIMAJI WAGONJWA WA EBOLA UWANJA WA NDEGE WA KIA

$
0
0
 Washiriki wa Shindano la Redd's Miss Tanzania 2014, wakimsikiliza Afisa Mfawidhi, Nisalile Mwangoka aliyekuwa akiwapa maelezo juu ya upimaji wa wageni wanao ingia nchini kupitia viwanja vya ndege unavyofanyika kutumia mashine maalum iitwayo 'Walk Through Thermoscaner', iliyopo uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) wakati warembo 30 wanaowania taji la Miss Tanzania walipotembelea uwanja huo na kujifunza mambo mbalimbali . Warembo hao wapo katika ziara ya kuhamasisha utalii wa ndani kwa kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii nchini.
 Mashine hiyo ikionekana kufungwa juu kuelekea usawa wa kuingilia abiria wanaowasili tka nje ya nchi.
 Namna inavyoonekana baada ya kipimo kuchukuliwa
 Nisalile Mwangoka akionesha kifaa cha zamani cha upimaji ugonjwa wa Ebola ambacho kimeelezwa kuwa licha ya ufanisi lakini kilikuwa kinaweka foleni kwa abiria tofauti na hicho kipya.
 Meneja wa Usalama katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), Kisusi Makomondi akiwapa maelezo washiriki hao wa shindano la Miss Tanzaniua 2014 juu ya shughuli mbalimbali za uwanja huo.
 Warembo wakianza ziara
 Camera man wa True Vision John Lymo akiwajibika uwanjani KIA.
 Warembo pia walipata fursa ya kutembelea kikosi cha zima moto uwanjani hapo.
 Warembo hao baada ya kutembelea Uwanja wa Ndege KIA waliwasili mkoani Arusha na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru.
Mkuu wa Wilaya (DC) wa Arumeru, Nyirembe Munassa Sabi,akiwa na warembo baada ya kuwapokea ambapo walitarajiwa kufanya ziara ya kutembelea vivutio vya utalii hifadhi ya Arusha na Namanga katika mpaka wa Tanzania na Kenya.

Maoni ya Kinana juu ya muungano baada ya wananchi wa scotland kupiga kura

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Mtongani alitoa maoni yake juu ya kura iliyopigwa na wananchi wa Scotland kuunga mkono Muungano dhidi ya wale waliotaka kujitenga.

Kinana alisema amekuwa akipigiwa simu siku nzima na waandishi wa habari kutaka kusikia maoni yake juu ya kura iliyopigwa Scotland.

Wananchi wa Scotland wamepiga kura na kuunga mkono muungano wa miaka 307 baina ya nchi hiyo na Uingereza katika kura ya maoni ya kihistoria iliyokuwa ikisubiriwa kuamua iwapo Scotland itajitenga.

“Watu wa Scotland wamezungumza. Tumechagua umoja dhidi ya mgawanyiko na mabadiliko chanya kuliko mgawanyiko usio na maana”.

SERIKALI HAITATAIFISHA SHULE WALA HOSPITALI - WAZIRI MKUU

$
0
0
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali haitataifisha shule, zahanati, hospitali wala Vyuo Vikuu vinavyoendeshwa na taasisi za kidini na amewahimiza wajenge zaidi na zaidi ili kuisaidia jamii kubwa ya Watanzania.

Ametoa wito huo wakati akizungumza na walimu, wazazi na wahitimu wa kidato cha nne wa shule ya sekondari Magnificat iliyoko Sanya Juu, wilayani Siha mkoani Kilimanjaro.

Waziri Mkuu ambaye aliwasili Sanya Juu jana asubuhi (Jumamosi, Septemba 20, 2014) akitokea Dodoma, alisema huko nyuma Serikali ilitaifisha shule na vyuo lakini kwa kiasi fulani ilishindwa kuviendesha ikaamua kuvirudisha kwa wamiliki wake ambao ni taasisi za kidini.

“Ni kweli huko nyuma tulikuwa navyo, lakini tumevirudisha kwenu tunataka na ninyi ni washirika katika kuleta maendeleo kwa wananchi walio wengi,” alisema Waziri Mkuu.

“Nilishawahi kusema huko nyuma na leo nasisitiza tena kwamba hatutaifisha shule, zahanati, hospitali wala Chuo Kikuu chochote cha taasisi ya kidini. Ninawasihi mjenge zaidi na zaidi,” aliongeza.

Waziri Mkuu ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa shule hiyo iliyoanzishwa Januari 15, 2011, aliwakabidhi vyeti wanafunzi 42 wa kidato cha nne wanaotarajia kufanya mtihani wa kidato cha nne Novemba, mwaka huu ikiwa ni mara ya kwanza kwa shule ya sekondari ya Magnificat kufanya mtihani huo.

Waziri Mkuu aliwapongeza wanafunzi hao kwa kushika nafasi ya kwanzawilayani Siha kwenye mitihani ya utamirifu (yaani mock) katika kidato cha nne. “Vilevile, shule hii imekuwa ya 12 kati ya shule 316 za Mkoa wa Kilimanjaro na ya 16 kati ya shule 564 kwa Kanda ya Kaskazini Mashariki zilizofanya mtihani huo. Mimi napata imani kuwa watafanya vizuri kwenye mtihani wao wa kidato cha nne Novemba 2014,” aliongeza.

Mapema,Mkuu wa Shirika la Masista la Kazi ya Roho Mtakatifu na Meneja wa Shule hiyo, Sista Inviolata Kessy alisema shule hiuo ilianzishwa kwa lengo la kutoa elimu bora na kuwashawishi watoto wa kike wa Kimasai waone umuhimu wa elimu na hivyo kuwaepusha na ndoa za utotoni. Vile vile, kuwapa msingi mzuri wa elimu kama sehemu ya maandalizi yao ya kupata elimu ya juu.

Alisema shule hiyo ambayo ni ya mchanganyiko na ya mchepuo wa sayansi na biashara, imefanikiwa kujenga maabara tatu za kemia, fizikia na baiolojia pamoja na chumba cha kompyuta.

Akisomarisalakwa niaba ya wahitimu, Anastazia Kimaro alisema shule hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo ukosefu wa jengo la utawala pamoja na basi la shule la kuwapeleka wananfunzi kwenye ziara za mafunzo.

Aliomba pia wawe wanapelekewa magazeti ya kila siku na kila wiki ili wanafunzi wa shule waweze kupata taarifa mbalimbali za mambo yanayojiri nchini na duniani.

Elimu ya awali yaendeshwa bila vitabu Tunduru

$
0
0
Wanafunzi wa darasa la awali Shule ya Msingi Nakayaya wakiwa darasani. Hata hivyo shule hii haina chumba cha darasa la awali chumba hiki kimejengwa kwa matumizi mengine na kwa sasa kinatumika kwa muda kwa kuwa kipo katika ujenzi. Wanafunzi wa darasa la awali Shule ya Msingi Nakayaya wakiwa darasani. Hata hivyo shule hii haina chumba cha darasa la awali chumba hiki kimejengwa kwa matumizi mengine na kwa sasa kinatumika kwa muda kwa kuwa kipo katika ujenzi.Mwalimu Christina Komba (kulia) wa darasa la awali Shule ya Msingi Tunduru Mchanganyiko akiwa darasani. Mwalimu Christina Komba (kulia) wa darasa la awali Shule ya Msingi Tunduru Mchanganyiko akiwa darasani.Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Majengo, Madina Mkali. Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Majengo, Madina Mkali akizungumza na mwandishi wa habari hizi (hayupo pichani) ofisini kwakeMwalimu wa muda wa darasa la awali, Shule ya Msingi Nakayaya, Teckla Milanzi akionesha baadhi ya nakala za vitabu walivyonavyo. Mwalimu wa muda wa darasa la awali, Shule ya Msingi Nakayaya, Teckla Milanzi akionesha baadhi ya nakala za vitabu walivyonavyo.[/caption]  

TunduruSHULE nyingi za msingi zenye madarasa ya awali Wilayani Tunduru zimekuwa zikiendeshwa kwa changamoto mbalimbali ikiwemo ya kutokuwa na vitabu vya baadhi ya masomo kabisa huku zikiwa na upungufu mkubwa wa vitabu kwa masomo mengine. 

Hali hiyo imebainika hivi karibuni katika uchunguzi uliofanywa kwa baadhi ya Shule za Msingi za Wilaya ya Tunduru, Mkoani Ruvuma huku walimu wa madarasa hayo wakielezea jitihada binafsi wanazozifanya kukabiliana na changamoto hiyo. Mwalimu Christina Komba wa darasa la awali Shule ya Msingi Tunduru Mchanganyiko akizungumzia hali hiyo alisema darasa lake halina vitabu vya masomo kama ya sanaa, Haiba na Michezo na wala miongozo ya namna ya ufundishaji hivyo kila mwalimu anayefundisha darasa hilo hubuni nini afundishe katika masomo hayo.

 “Madarasa ya elimu ya awali hayana vitabu, hayana miongozo…huwa tunaazima au ukipata hela yako wewe binafsi unaenda kununua kitabu kimoja au viwili ili uweze kuwasaidia watoto. Na baadhi ya masomo hayana vitabu kabisa hata ukienda madukani katika Wilaya yetu vitabu kama Haiba na Michezo, pamoja na Sanaa hazipo kabisa madukani," alisema Bi. Komba. Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nanjoka, Batadhari Mkwela akizungumzia shule yake alisema licha ya usajili wa wanafunzi wa awali kuongezeka kila mwaka upatikanaji wa bajeti ya kuendesha elimu hiyo ni changamoto kubwa huku uchangiaji kwa wazazi ikiwa wa kusuasua. 

“…Darasa la awali linahitaji vitendea kazi lakini havipo, hatuna vifaa kama vitabu vya kutosha, nyenzo za kufundishia, hakuna bajeti hata ya vifaa hivi toka Serikalini, hatuna hata madawati maalum kwa ajili ya wanafunzi wa darasa hili,” alisema Mkwela. Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Majengo, Madina Mkali alisema uendeshaji wa darasa la awali shuleni hapo ni wa kusuasua kutokana na kutokuwa na bajeti inayoletwa kusaidia elimu hiyo, isipokuwa kwa baadhi ya mwaka kuletwa madawati kumi kwa ajili ya wanafunzi wa awali. “…Uendeshaji elimu ya awali hapa ni wa wastani kwa kweli kutokana na changamoto zinazotukabili, kwanza vifaa vya kuwafundishia watoto hawa ni tatizo na wazazi kwa eneo hili wamekuwa hawana mwamko wa elimu hii kabisa. 

Kwanza hawachangii michango ya chakula kama inavyotakiwa ili mtoto apate chochote awapo shuleni,” anasema mwalimu Mkali. Kwa upande wake mwalimu wa darasa la awali, Shule ya Msingi Nakayaya, Teckla Milanzi akitolea mfano shuleni hapo alisema vitabu vya Kiswahili, Kiingereza, Sayansi na Hisabati kuna nakala moja moja tu kwa kila somo, ambazo huzitumia yeye mwenyewe. Aidha mwalimu Milanzi aliongeza kuwa darasa hilo licha ya kuwa na changamoto kedekede hata kwenye mgao wa fedha zinazoletwa shuleni kila mara halimo jambo ambalo husababisha hali kuendelea kuwa mbaya zaidi. 

Hata hivyo mwalimu wa darasa la awali Shule ya Msingi Majengo, Hadija Makamla alisema anavyo baadhi tu ya vitabu vinavyoitajika katika darasa hilo, nakala ambazo pia ni chache ukilinganisha na ukubwa wa darasa lake. “…Ninazo nakala chache kwa ajili ya mwalimu tu ila wanafunzi hawana hata kimoja…lakini kuna masomo mengine sina vitabu kabisa kama vile Sanaa na Haiba ya Michezo sina kabisa hata mimi,” anasema mwalimu Makamla. *Imeandaliwa na www.thehabari.com kwa ushirikiano na HakiElimu

RUFIJI UTETE- Video clip ya maswali na majibu katika mikutano ya Kinana


MKUU WA WILAYA YA HAI AWAASA WANANCHI KUACHANA NA TABIA YA UNYWAJI POME ULIOKITHIRI.

$
0
0
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO

Serikali wilayani Hai imewaasa wananchi kuachana na tabia ya unywaji wa pombe uliokithiri ambao unaathiri nguvu kazi pamoja na maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.

Hayo yamesemwa hivi karibuni na Mkuu wa Wilaya ya Hai Novatus Makunga kufuatia habari iliyochapishwa na gazeti la Habari Leo toleo Na. 02830 la Ijumaa Septemba mwaka huu yenye kichwa cha habari “Ulevi kwa wanafunzi wa Hai wamtisha DC”.

“Si kweli, hakuna kitu kama hicho wala hakuna taarifa za wanafunzi kunywa pombe hizo hali inayopelekea kuwa tishio katika wilaya yetu” alisema Makunga.

Akiongea kwa njia ya simu kutoka wilayani Hai Makunga alisema kuwa alichosema wakati wa mazishi ya aliyewahi kuwa Shehe wa mkoa wa Kilimanjaro Ally Lema alisema wazazi ndio wanaokunywa pombe aina ya gongo na viroba na sio wanafunzi wa shule za msingi wala sekondari.

Akifafanua juu ya suala hilo, Makunga alisema kuwa wazazi pamoja na vijana wengi wanaokaa vijiweni wakiowemo madereva wa “bodaboda” ndio kundi linalosadikiwa kukithiri katika unywaji wa pombe aina ya gongo na viroba ambavyo vinatishia kuathiri mfumo wa uzazi.

DC Makunga aliongeza kuwa pombe hizo ni kali, sio salama na hazina kiwango ndio maana zinapelekea kupunguza nguvu za uzazi ambapo hata Wachungaji wa dini mbalimbali wamesema idadi ya watoto wa ubarikio katika makanisa yao  pia imepungua.

Vilevile wilaya ya nchi nzima inaweza kukosa nguvu kazi kutokana na vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa kupungua au waliopo kutokuwa na nguvu ya kufanya kazi inavyopaswa kutokana na hali yao ya unywaji wa pombe hizo zisizo salama.

Katika kukabiliana na hali hiyo, Makunga alisema kuwa tayari wilaya yake ipo katika hatua za mwisho kukamilisha sheria sheria ndogo ndogo inayopiga marufuku unywaji wa pombe wakati wa saa za kazi wilayani humo.

Makunga alisema kuwa kwa sasa Sheria kuu ya Serikali kuhusu unywaji pombe ndiyo inayotumika ambapo inabainisha kuwa muda wa kunywa pombe siku za kazi yaani Jumatatu hadi Ijumaa ni kuanzia saa 9: 00 mchana hadi saa 4:00 usiku na siku za Jumamosi, Jumapili na siku za siku kuu ni kuanzia saa 6:00 mchana hadi saa 5:00 usiku ambapo atakayebainika kukiuka utaratibu huo atachukuliwa hatua za kisheria.

Sheria hiyo inataja kuwa anayekunywa pombe saa za kazi atapelekwa mahakamani na kupigwa faini au kifungo cha miezi sita jela au adhabu zote kwa pamoja.

Asasi za kiraia zafanya matembezi huru kusisitizia tamko lao juu ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi

$
0
0
Katika kuweka msisitizo juu ya tamko lao juu ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika huko New York-Marekani tarehe 23/09/2014, umoja wa Asasi Nne zisizo za kiserikali zinazojishughulisha na kupambana na mabadiliko ya tabianchi nchini ForumCC, CAN, YouthCAN na Oxfam Tanzania zimefanya matembezi huru kwenye eneo la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Maandamano hayo yamewahusisha pia wanafunzi wa shule za sekondari za Jitegemee, Kinyamwezi, Ilala, Chanika na Maji ya Chai.
 Picha ya pamoja ya wanafunzi na viongozi wa asasi za kiraia walioshiriki matembezi hayo huru ili kuweka msisitizo juu ya tamko juu ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika huko New York-Marekani tarehe 23/09/2014
 Afisa Miradi wa Forum CC, Fazal Issa aliyeshika kipasa sauti akifafanua jambo kwa wanafunzi walioshiriki matembezi hayo

 Matembezi huru yakiendelea
 Msimamizi wa idara ya Habari ya YouthCAN, Dickson Daniel akizungumza na wanafunzi walioshiriki matembezi huru ya kuunga mkono na kusisitizia tamko la asasi za kiraia juu ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika huko New York-Marekani tarehe 23/09/2014
Meneja Ushawishi wa Oxfam, Eluka Kibona akizungumza na wanafunzi walioshiriki matembezi huru ya kuunga mkono na kusisitiza tamko la asasi za kiraia kuhusu Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika huko New York-Marekani Septemba 23, 2014
 Mratibu wa CAN Tanzania, Sixbert Mwanga akifafanua jambo wakati wa matembezi huru ya kuunga mkono na kusisitiza tamko la asasi za kiraia kuhusu Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika huko New York-Marekani Septemba 23, 2014
 Wanafunzi wa Jitegemee katika picha ya pamoja
 
Mwanafunzi wa kidato cha pili shule ya sekondari Ilala, Mwanaidi Ibrahim akiimbisha wimbo wa mazingira wakati wa matembezi huru ya kuunga mkono na kusisitiza tamko la asasi za kiraia kuhusu Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika huko New York-Marekani Septemba 23, 2014, pembeni yake ni Afisa Miradi wa ForumCC, Fazal Issa

Picha zote na Tabianchi Blog

AFANDE SELE AWAASA WASANII KUUNGANA NA KUWA KITU KIMOJA,AWATAKA KUACHA TABIA YA KUBAGUANA.

$
0
0
  Afande Sele akiwa na watoto wake wawili alioachiwa na Marehemu Mama Tunda,ambao ni Tunda na Asante Sanaa wakiwa wamepozi mbele ya Camera ya Globu ya jamii mapema leo mchana,Walipokwenda kwenye Arobaini iliyoanyika mtaa wa Amani mjini Morogoro.
 Msanii Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya,Mkali wa Rhymes Afande Sele akiushukuru Uongozi wa Clouds Media Group sambamba na kuwashukuru Wasanii hao waliofika kutoa mkono wa pole kwa familia ya Mama mzazi wa marehemu Mama Tunda (aliyekuwa mke wa Msanii Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya,Afande Sele),mtaa wa Amani mjini Morogoro mapema leo mchana,ambapo Marehemu Mama Tunda leo anatimiza siku arobaini tangu kufariki kwake.
 Afande Sele akizungumza kwa kuwataka wasanii kuungana na kuwa kitu kimoja katika shida na raha,kuacha tabia ya kubaguana na kujengeana chuki ambako kumekuwa ni sehemu ya kuufanya muziki wao na mambo yao mengi yasifanikiwe ipasavyo,Hivyo amewashauri wasanii kuwa na roho ya kupendana na kufanya kazi zao kwa kujituma na ubunifu ili tasnia ya muziki iweze kufika mbali zaidi.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Mo Music anaetamba na wimbo wake wa Basi nenda unaofanya vyema katika vituo mbalimbali vya redio hapa nchini,akitoa mkono wa pole kwa Mama mzazi wa marehemu Mama Tunda (aliyekuwa mke wa Msanii Mkongwe Afande Sele),mtaa wa Amani mjini Morogoro mapema leo mchana.
 Mtoto wa kwanza wa Afande Sele,aitwaye Tunda akisalimiana na baadhi ya wasanii waliofika kutoa mkono wa pole kwa familia ya Mama mzazi wa marehemu Mama Tunda (aliyekuwa mke wa Msanii Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya,Afande Sele),mtaa wa Amani mjini Morogoro mapema leo mchana,ambapo Marehemu Mama Tunda leo anatimiza siku arobaini tangu kufariki kwake.
 Baadhi ya Wasanii wanaotarajiwa kutumbuiza jioni ya leo kwenye tamasha la Fiesta 2014,ndani ya uwanja wa Jamhuri,wakiwa na baadhi ya ndugu jamaa na marafiki wa Familia ya marehemu Mama Tunda,ambapo leo inafanyika arobaini yake,mtaa wa Amani mjini Morogoro.
PICHA NA MICHUZI JR-MOROGORO

Shule ya Sekondari Lilasia yafanya mahafali ya 6.

$
0
0
Beatha Shembilu (1)Wahitimu wa kidato cha nne, Shule ya Sekondari Lilasia, iliyopo eneo la Kitunda kwa Kibeberu, Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa shule hiyo, kwenye sherehe ya mahafali ya sita iliyofanyika Dar es Salaam jana.Mwanafunzi  wa Shule ya Sekondari Lilasia, iliyopo eneo la Kitunda kwa Kibeberu, Dar es Salaam, Beatha Shembilu, akipokea cheti cha kuhitimu kidato cha nne kutoka kwa mgeni rasmi, Samwel Lyimo, katika sherehe za mahafali ya sita ya shule hiyo, zilizofanyika Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkurugenzi wa Shule hiyo, Christina Lyimo, na Mkuu wa Shule, Silas Kamando. Wanafunzi wa Kidato cha Nne nchini kote wanatarajia kuanza mitihani yao ya Taifa ifikapo Novemba 3 mwaka huu. Beatha Shembilu (2)Mwanafunzi  wa Shule ya Sekondari Lilasia, iliyopo eneo la Kitunda kwa Kibeberu, Dar es Salaam, Flora Jeremiah, akipokea cheti cha kuhitimu kidato cha nne kutoka kwa mgeni rasmi, Samwel Lyimo, katika sherehe za mahafali ya sita ya shule hiyo, zilizofanyika Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkurugenzi wa Shule hiyo, Christina Lyimo, na Mkuu wa Shule, Silas Kamando. Wanafunzi wa Kidato cha Nne nchini kote wanatarajia kuanza mitihani yao ya Taifa ifikapo Novemba 3 mwaka huu. Peter Nyaikobe (1)(1)Mwanafunzi  wa Shule ya Sekondari Lilasia, iliyopo eneo la Kitunda kwa Kibeberu, Dar es Salaam, Peter Nyaikobe, akipokea cheti cha kuhitimu kidato cha nne kutoka kwa mgeni rasmi, Samwel Lyimo, katika sherehe za mahafali ya sita ya shule hiyo, zilizofanyika Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkurugenzi wa Shule hiyo, Christina Lyimo, na Mkuu wa Shule, Silas Kamando. Wanafunzi wa Kidato cha Nne nchini kote wanatarajia kuanza mitihani yao ya Taifa ifikapo Novemba 3 mwaka huu. Peter Nyaikobe (2)Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari Lilasia, Christina Lyimo.
Shule ya Sekondari Lilasia yafanya mahafali ya 6.
 
*Wataka kuwe na lugha maalum mashuleni
NA ANDREW CHALE.
 
NJIA nyepesi ya kukabiliana na tatizo kubwa la ajira kwa vijana nchini ni kuongeza kasi ya uwekezaji kwenye viwanda, sanjari na kuutazama upya mtaala wa kufundishia kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu, hususan kwenye eneo la lugha, imeelezwa.
 
Akizungumza kwenye mahafali ya 6, ya Shule ya Sekondari Lilasia, iliyopo Kitunda, Dar es Salaam jana septemba 20, Mkurugenzi wa shule hiyo, Christina Lyimo, alisema kupitia viwanda vijana kwa maelfu yao wataajirika na kujiajiri kwa mtiririko wa fursa zitakazokuwepo, huku pato la taifa likizidi kukua.
 
“Sina shaka sana na rasilimali tulizonazo..zinatosheleza, tuna uchumi mkubwa, hebu kama serikali itanisikia niombe sasa tuwekeze nguvu kwenye viwanda, tupeleke surveyors wakapime maeneo, sababu tuna nguvu kazi kubwa, tuna rasilimali..tuanzie hapo,” alisema Lyimo.
 
Aidha, Lyimo, ambaye kitaaluma ni mwalimu anayehudumu kazi hiyo kwa zaidi ya miaka 25 sasa, ameshauri yafanyike mabadiliko ya mtaala hususan kwenye lugha ya kufundishia, huku akisisitiza ni wakati mwafaka sasa kwa taifa kuamua ni lugha ipi itumike kufundishia kama ni Kiingereza au Kiswahili, tofauti na ilivyo sasa kuchanganya changanya.
 
“Watoto wengi wanababaika kwenye mitihani kwa sababu ya Lugha..watoto wengine wanafeli kwa kushindwa kujieleza kwa lugha za kigeni!..shule ya msingi Kiswahili miaka saba..sekondari kiingereza kwa kweli inachanganya, tuamue basi kubadilisha kama ni medium basi ziwe kuanzia awali hadi vyuo vikuu, na kadhalika kama Kiswahili iwe hivyo,” alisema
 
Hata hivyo, katika hatua nyingine, aliwaomba wafadhili kujitokeza kuchangia shule hiyo kwenye eneo la upatikanaji wa maabara ya kisasa, ikizingatiwa shule kwa sasa pamoja na mambo mengine inasomesha watoto yatima bure na kusaidia kwa kiasi utoaji wa elimu bora kwa watoto wa Kitunda na kwingineko nchini.
 
“Tunaomba pia serikali igeuzie macho kwenye shule hii, tuna watoto yatima hapa, itusukume kwenye kupata ruzuku sababu tunasaidia taifa na hata ada tunazopokea ni ndogo mno,” alisema.
 
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Lilasia, Silas Kamando alisema katika mahafali hayo jumla ya wanafunzi 36 wakiwemo wanaume 17 na wasichana 19 wamehitimu kidato cha nne mwaka huu, na kwa sasa wanajiandaa na mtihani wao wa taifa unaotarajia kufanyika Novemba 3 mwaka huu, nchini kote.

KAMPUNI YA SAMSUNG TANZANIA YAZINDUA RASMI DUKA JIPYA NA KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA JIJINI ARUSHA

$
0
0
samsung 1
Meneja Mkuu wa kampuni ya kielektroniki ya Samsung Tanzania na Mr Nawaz Ladha Mkurugenzi wa  Kampuni ya Freedom Elektronics moja ya kati ya wasmbazaji wa  Samsung Tanzania akikata utepe kuzindua rasmi duka jipya na kituo cha huduma kwa wateja jijini Arusha
IMG_2349
Meneja Mkuu wa Samsung Mr Mike Seo akiwahutubia wanahabari(hawapo kwenye poicha) katika uzinduzi rasmi wa duka la kielektroniki la Samsung na kituo cha huduma kwa wateja mjini Arusha.
SAM_9217
Meneja Mkuu wa Samsung Mr Mike Seo akiwahutubia wateja wa Samsung katika uzinduzi rasmi wa duka la kielektroniki la Samsung na kituo cha huduma kwa wateja mjini Arusha.

  IMG_2410
Meneja wa Usambazaji wa Samsung Sylvester Manyara akitoa maelezo kwa wateja na waandishi wa habari. 

IMG_2435
Meneja  wa huduma Samsung Mr Mubarak Mikidad akiwahutubia wanahabari katika uzinduzi rasmi wa duka la kielektroniki la Samsung na kituo cha huduma kwa wateja mjini Arusha.(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images