Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 366 | 367 | (Page 368) | 369 | 370 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Kutoka juu ni Uwanja wa Nyamagana mahala ambako fainali ya Michuano ya Pepsi Kombe la Meya 2014 kati ya Mkolani Fc v/s Mirongo utachezwa.
  Kikosi cha Mkolani Fc kilichoshuka dimbani jana kukiputa na Mnadani Fc, matokeo kikaibuka na ushindi wa bao 2-1, hivyo kusonga mbele katika hatua ya fainali ya Michuano ya Pepsi Kombe la Meya 2014, itakayochezwa jumamosi hii kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
  Kikosi cha Mnadani Fc, kilichoshuka dimbani jana kucheza na Mkolani Fc matokeo kikakamuliwa bao 2-1, hivyo kucheza mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu dhidi ya Sokoni katika Michuano ya Pepsi Kombe la Meya 2014, mchezo utakaochezwa kabla mchana kabla ya fainali jumamosi hii kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
  Wadau wa Michezo waliofurika katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza kushuhudia mchezo wa nusu fainali kati ya Mkolani v/s Mnadani Fc.
  Pepsi Kombe la Meya ni michuano iliyoasisiwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mkolani Mhe. Stanslaus Mabula, ikisimamiwa na Kampuni ya May way Entertainment.
  Mashabiki .
  Diwani wa kata ya Mirongo Mhe. Mkama (mwenye tracksuit ya blue) juzi alikuwepo uwanja wa Nyamagana pindi timu toka kata yake Mirongo Fc iliposhuka dimbani katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza dhidi ya Sokoni, ambapo timu yake iliibuka na ushindi wa bao 2-1.
  Wanahabari dimbani.
  Diwani wa kata ya Mirongo Mhe. Mkama (mwenye tracksuit ya blue) juzi alikuwepo uwanja wa Nyamagana pindi timu toka kata yake Mirongo Fc iliposhuka dimbani katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza dhidi ya Sokoni, ambapo timu yake iliibuka na ushindi wa bao 2-1. hapa akishangilia ushindi.
  Diwani wa kata ya Mirongo Mhe. Mkama (mwenye tracksuit ya blue) na shangwe za kutinga fainali ambapo timu ya mirongo itashuka dimbani kukiputa na Mkolani jumamosi hii.(20/09/2014)
  Waamuzi toka kituo cha elimu na michezo Alliance Academy Mwanza ndiyo wanaosimamia michuano  hii ya Pepsi kombe la Meya 2014.
  Nahodha wa Mkolani Fc akizungumza na vyombo vya habari.
  NA ALBERT G. SENGO: MWANZA
  Imeshafahamika kwamba timu ya soka ya Mkolani fc na Mirongo ndizo zitakazo kutana katika fainali ya kutafuta bingwa wa Michuano ya PEPSI Kombe la Meya 2014 Mkoa wa Mwanza, mchezo unaotaraji kutimua vumbi jumamosi hii ya tarehe 20 sept katika uwanja wa Nyamagana jijini humo.

  Mchezo huo wa fainali utatanguliwa na mchezo wa kusaka mshindi wa tatu baina ya Mnadani Fc na Sokoni. (ZAIDI BOFYA PLAY KUSIKILIZA TAARIFA)

  ZAWADI KWA MICHUANO HIYO NI KAMA IFUATAVYO:-
  - Mfungaji bora wa mashindano kuondoka na kitita cha shilingi laki mbili.
  - Timu yenye nidhamu itaondoka na kitita cha shilingi laki mbili.
  - Refa bora wa mashindano shilingi laki mbili, ile hali mshindi wa tatu atalitwaa kombe, medali ya shaba na kitita cha shilingi milioni moja. 
  - Mshindi wa pili wa michuano hiyo ataondoka na kombe, medali ya fedha na kitita cha shilingi milioni mbili.
  - Bingwa atakabidhiwa Kombe, medali ya dhahabu na bajaji ya kisasa ya mizigo yenye uwezo wa kubeba pia watu wanne yenye thamani ya shilingi milioni 4.5, 

  0 0

  Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
   
  Serikali imeagiza watumishi wote wa umma walipwe mishahara moja kwa moja kupitia akaunti zao sahihi za benki ambazo zitatumika kupitishia mihahara yao.

  Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ofisi za Hazina leo jijini Dar es salaam.“Mishahara ya Watumishi wote wa Serikali, wakala na taasisi za umma italipwa moja kwa moja kupitia akaunti zao za banki” alisema Mwigulu.

  Ili kufanikisha adhima hiyo ya Serikali, Mwigulu aliwaagiza waajiri wote wa sekta ya umma kuwa wawe na akaunti namba za benki za watumishi wao wote waliochini ya fungu husika ambazo zina taarifa sahihi na wakizingatia mfumo sahihi wa taarifa za kiutumishi.

  Mwigulu alionya kuwa mtumishi asiye na akaunti benki asilipwe mshahara wake dirishani ambapo amewahimiza waajiri kuwasisitiza watumishi walio chini yao kufungua akaunti sahihi ya benki kwenye mfumo ambayo itatumika kulipa mshahara husika kupitia orodha ya malipo ya mshahara (payroll) inayotolewa na Hazina.

  Aidha, Mwigulu amasema kuwa kila ifikapo tarehe 10 ya kila mwezi  waajiri wote wawe wamewasilisha maombi ya fedha za kulipa mishahara kwa mwezi unaohusika wakiambatisha orodha ya malipo ya  watumishi ya kuthibitisha kiasi kinachoombwa.

  “Waajiri watakaoshindwa kutoa ‘Payroll’ watasababisha watumishi wanaowaongoza kushindwa kupata mishahara yao kwa mwezi husika jambo ambalo sio nia ya Serikali” alisisitiza Mwigulu.

  Utaratibu huu wa kulipa mishahara utakuwa endelevu na umedhihirisha kuwa na tija kwa matumizi ya fedha za umma kwani umeonesha mafanikio ambayo kwa mwezi wa saba na wa nane hakuna mtumishi, Wakala za Serikali wala Taasisi iliyolalamika kukosa mishahara.

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (katikati) akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Maneromango leo wakati wa ziara yake wilayani Kisarawe, Pwani ya  kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kuata Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho pamoja na kusikiliza kero za wananchi kwa lengo la kuzipatia ufumbuzi.PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
   Wananchi wa Kata ya Maneromango wakisikiliza kwa makini hotuba ya Kinana katika mkutano huo. ambapo aliwananga wapinzani kuwa wapo kwa ajili ya kupanga maandamano, kutukana, kutoa manaeneo machafu klwa Serikali wakati CCM ipo kiutendaji zaidi katika masuala ya maendeleo ya wananchi.
   Kinana akihutubia baada yakuweka jiwe la msingi katika jengo la Zahanati ya Palaka Kata ya Malumbo wakati wa ziara yake wilayani Kisarawe leo. Kinana na Nape wakitoka kufungua ujenzzi wa jengo la kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe.
   Kinana akiangalia wauguzi wakimtibia mtoto katika hospitali hiyo
   Kinana akisaidia kujenga marumaru katika jengo jipya la wodi ya wazazi katika hospitali ya Kisarawe.
   Jengo la zamani la kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Kisarawe.
   Kinana akifunua pazia alipokuwa akiweka jiwe la msingi katika jengo jipya la Zahanati ya Palaka, Kata ya Malumbo, Kisarawe
   Mganga Mkuu wa Hospitali ya Kisarawe, Dk. Happiness Ndosi akimuelekeza Kinana kuhusu maendeleo ya ujenzi wa zahanati hiyo.
   Wananchi wa Kijiji cha Palaka, wakimshangilia Kinana alipokuwa akihutubia baada ya kuweka jiwe la msingi katika zahanati Palaka.
   Wananchi wakiwa katika hafla ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa zahanati hiyo pa Palaka
   Kinana akisaidia kufyatua matofali ya kujengea maabara katika Shule ya Sekondari ya Gongoni, katika Kata ya Gongoni, wialyani Kisarawe.Matofali hayo yanafyatuliwa na wanakikundi cha vijana chas wajasiriamali.
   Kinana akiondoa tofali alilolifyatua katika mradfi huo wa matofali wa vijana.
   Katibu Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Maneromango.
  Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Suleiman Jaffo akielezea kwa wananchi jinsi miradi mingi iliyokamilika ujenzi wake kwa kuata Ialani ya Uchaguzi ya CCM.

  0 0

  Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick (wa tatu kushoto), wakiwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam leo. Daraja hilo linajengwa kwa  ufadhili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF). Wa nne kushoto ni Meneja Mradi ujenzi wa daraja hilo, Mhandisi John Msemo. (Picha na Francis Dande)
  Taarifa za ujenzi.
   Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick (kulia), wakiwasili katika eneo la Mradi wa Ujenzi wa daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam.
  Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni Mhandisi John Msemo (kulia), akipeana mkono na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick mara baada ya kuwasili katika eneo la mradi huo.
   Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam wakimsikiliza Menja Mradi Ujenzi wa Daraja la Kigamboni Mhandisi, John Msemo.
   Taarifa za ujenzi.
   Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, ramadhani Madabida akifafanua jambo baada ya kupata maelezo ya ujenzi wa daraja la Kigamboni.
   Mkuu wa Mkoa akifafanua jambo.
  Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge akiuliza swali kuhusu mradi huo.
  Mhandisi John Msemo akitoa ufafanuzi wa ujenzi wa Daraja la Kigamboni kwa  Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaa walipofanya ziara ya kuangalia maeledelo ya ujenzi wa daraja hilo.
  Mhandisi John Msemo akitoa ufafanuzi kuhusu ujenzi wa Daraja la Kigamboni kwa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaa walipofanya ziara ya kuangalia maeledeleo ya ujenzi wa daraja hilo.
   Msimamizi wa mradi huo Mhandisi Karim Mataka akielekea katika eneo la ujenzi wa daraja.
   Mwebnyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida akiwa katika ziara hiyo.
   Mhandisi John Msemo.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick
  Wajumbe wakikagua maendeleo ya ujenzi.
   Wajumbe wakikagua maendeleo ya ujenzi.
   Eneo la ujenzi wa Daraja la Kigamboni.
    Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick akiwa na Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja hilo, Mhandisi John Msemo wakati wa kuangalia maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo linalojengwa na NSSF kwa kushirikiana na Serikali.
   Mhandisi Msemwa akitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
   Moja ya nguzo za Daraja hilo.
   Ufafnuzi ukitolewa na Msimamizi wa Ujenzi wa Daraja hilo Mhandisi Karim Mataka.
   Mhandisi John Msemo akitoa maelezo kwa Wajumbe hao.
   Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick (wa pili kushoto), wakiwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam leo. Daraja hilo linajengwa kwa  ufadhili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF). Wa tatu kushoto ni Meneja Mradi ujenzi wa daraja hilo, Mhandisi John Msemo.
   Wajumbe wakiwa katika ziara hiyo.
   Baadhi ya barabara za kuingia katika daraja hilo.
   Mhandisi John Msemo kutoka NSSF akitoa ufafanuzi kuhusu ujenzi wa Daraja hilo kwa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akizungumza katika eneo la Ujenzi wa Daraja la Kigamboni.
   Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Salum Madenge akizungumza baada ya kukagua ujenzi wa Daraja la Kigamboni.
   Meneja Mradi Daraja Kigamboni Mhandisi John Msemo (wa pili kushoto) akiagana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Salum Madenge.
   Msimamizi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Mhandisi Karim Mataka akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick.

  0 0


    wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein wakisalimaiana na Makamu wa Pili Balozi Seif Idd  mara baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Amani Abeid Karume akitokea Visiwa vya Comoro baada ya kumaliza ziara yake ya siku nne.
   Waandishi wa Habari wakifanya mahojiano na Rais wa Zanzibar (hayupo pichani)   baada ya kuwasili akitokea ziara katika visiwa vya Comoro.

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Muhamed Shein akijibu maswali ya Waandishi wa Habari kwenye Uwanja wa ndege wa Zanzibar. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).   
  Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar 18/09/2014

  Baadhi ya nchi za Visiwa ikiwemo Zanzibar zimeunda umoja ujulikanao kama “Vanilla Islands” ikiwa ni mkakati wa kuimarisha mashirikiano ya kuendeleza Utalii katika nchi husika.


  Nchi hizo ni pamoja na Panama, Seychelles, Comoro na Zanzibar ambazo zitafanya kazi kwa pamoja katika kuendeleza Sekta hiyo muhimu kwa nchi hizo. Hayo yamesemwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein wakati alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari Uwanja wa Abeid Aman Karume mara baada ya kuwasili kutoka ziara yake nchini Komoro.


  Aidha Dkt shein amesema nchi hizo pia zimefanya Makubaliano ya Awali (Memorandum of understanding) yaliyotiwa Saini nchini Komoro ambayo yatawapa uthubutu nchi wanachama kutekeleza yale waliyoazimia katika kuendeleza Sekta ya Utalii.


  Katika hatua nyingine Dkt Shein amesema ili kukabiliana na mabadiliko ya Tabia Nchi, Umoja huo wa Vanilla Island umekubaliana pia kutiliana saini makubaliano ya awali ili kukabiliana na tatizo hilo.Amesema wamelazimika kufanya makubaliano hayo kutokana na nchi za Visiwa kukabiliwa na hatari ya kupata majanga ambayo yanatokana na mabadiliko hayo.


  Amefahamisha kuwa Umoja huo utafanya kazi zake kwa mujibu wa Sheria uliojiwekea ili kukabiliana na Ongezeko la Joto ambalo linazidi kukuwa duniani kadiri siku zinavyoenda mbele. Katika hatua nyingine Dkt Shein amewataka Waandishi kuwafahamisha wananchi yale ambayo Serikali imefanikiwa kuyafanya badala ya kuandika mambo ambayo hayana faida kwao.


   Amesema inashangaza kuona Waandishi wanashabikia kuandika mambo ambayo si yakimaendeleo na kushindwa kuwaonesha yale ambayo Serikali imeyafanya katika kipindi cha kuwepo madarakani kwake.


  Ametoa mfano wa namna ambavyo Awamu ya saba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilivyoweza kufanikiwa kuongeza makusanyo ya Kodi, kuzuia mfumuko wa bei nchini na kurekebisha mishahara mara mbili katika kipindi cha miaka mitatu mambo ambayo wananchi wanapaswa kujulishwa.


  “Inashangaza kwanini hamuandiki habari za maendeleo ambayo wageni kutoka nchi za nje wanakuja kuiga badala yake mnataka kujua habari zisizokuwa na msingi…Hayo na ukawa kawafuateni wenyewe” Alisema Dk Shein.


  Katika ziara hiyo ya siku nne Dkt Sheni mbali na kuzungumzia Sekta ya Utalii pia alizungumzia Sekta ya Elimu, Kilimo na Biashara ambapo Zanzibar na Comoro zitashirikiana kwa karibu ili kuleta maendeleo kwa nchi husika.

  IMETOLEWA NA MAELEZO ZNZ

  0 0

   Kikosi cha zima moto kikifanya juhudi za kuzima moto huo.
  MSIKITI wa madhehebu ya Wahindu uliopo maeneo ya Mtaa wa Kibasila karibu na shule ya Olimpia jijini Dar es Salaam, umeteketea kwa moto leo asubuhi ambapo baadhi ya mali zimeungua na mtu mmoja kukimbizwa hospitali kutokana na mshituko.
   Sehemu ya chumba cha msikiti kilichoungua.
  Akizungumza na mtandao huu, shuhuda mmoja alisema moto huo umesababishwa na hitilafu ya umeme iliyoanzia kwenye mashine ya luku ambapo baadhi ya waumini walikuwa wakijiandaa  kuupamba msikiti huo.
   Wananchi wakiwa katika eneo la tukio wakisaidia kuokoa baadhi ya mali zilizopo ndani ya msikiti.
   Gari la kikosi cha zima moto likiwa eneo la tukio kuuzima moto.
  Baadhi ya waumini wakiwa eneo la tukio.
  Baadhi ya mali zilizookolewa.

  0 0
 • 09/19/14--00:31: Article 12


 • 0 0

   Warembo wanaoshiriki shindano la Redd's Miss Tanzania 2014 wametembelea hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) na kujifunza mambo mengi kuhusiana na hifadhi hiyo ya mlima kilamanjaro. Pichani ni warembo hao wakipiga picha na mdau mkubwa wa masuala ya urembo mkoani Kilimajaro, Athena Mawalla wa mgahawa wa Meku's Bistro wakati warembo hao walipomtembelea wakiwa njiani kwenda KINAPA.
   Warembo wakiwa katika gari njiani kuelekea KINAPA. 
   Afisa Habari wa Kamati ya Miss Tanzania, Hidan Rico (kulia) akitoa maelekezo baada ya kufika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimajaro.
   Warembo wakipanda kuelekea geti kuu la kupandia Mlima Kilimanjaro.
   Viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja.
   Eliud Bemba ambaye anaongoza timu ya utayarishaji Vipindi maalum vya warembo hao kutoka True Vision akichapa picha na walimbwende.
  Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro, Erastus Lufungulo akitoa maelezo ya mlima huo kwa warembo wa Miss Tanzania. 

  0 0

  Mmiliki wa Jossekazi Auto garage ambao ndiyo waandaaji wa tamasha akizungumza na waandishi wa habari juu ya tamasha la kwanza la Magari la aina yake, linalojulikana kwa jina la Automobile Clinic, ambalo linatarajiwa kufanyika kwa siku mbili Septemba 27 na 28, 2014 katika viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam.

   Ambapo alisema kuwa tamasha hilo limelenga katika kutoa huduma ya kitaalamu ya kiufundi kwa wenye magari (Checkup and Fix) kutoka kwa mafundi stadi ambao wamebobea katika fani ya ufundi wa makenika katika aina tofauti tofauti za magari. Pembeni kulia ni Mkurugenzi wa Jast Tanzania Limited, Jahu Mohammed Kessy, Mratibu wa Tamasha hilo na Mwakilishi toka Mwambi Lube Distributor, Jonathan Mwanayongo.
   
  Kampuni ya Jast Tanzania Limited kwa kushirikiana na Jossekazi Auto Garage and General supplier wameandaa tamasha la kwanza la Magari la aina yake, linalojulikana kwa jina la Automobile Clinic, ambalo linatarajiwa kufanyika kwa siku mbili mfululizo katika viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam.Tamasha hilo limelenga katika kutoa huduma ya kitaalamu ya kiufundi kwa wenye magari (Checkup and Fix) kutoka kwa mafundi stadi ambao wamebobea katika fani ya ufundi wa makenika katika aina tofauti tofauti za magari.
  Akizungumza na vyombo vya habari, kwenye ukumbi wa habari Maelezo, Joseph Mgaya mmiliki wa Jossekazi Auto garage amesema tamasha hili lina lengo kuwakutanisha mafundi stadi na wenye magari, kwa gharama nafuu sana ya shillingi elfu ishirini tu.
  Mkurugenzi wa Jast Tanzania Limited, Jahu Mohammed Kessy, Mratibu wa Tamasha hilo akielezea machache juu ya tamasha hilo.
   
  Mgaya alisema huduma hizo ambazo zilipaswa kugharimu kiasi kikubwa sana cha pesa kwa wenye magari, kitatolewa kwa bei nafuu ili kwa makusudi tu ya kukutanisha mafundi hao na wenye magari.
  Alisema pamoja na Wateja kutengenezewa Air condition na kujaziwa gesi, kufanyiwa Electronical scan diagnosis, Kuchekiwa Matairi, kuchekiwa Battery, na kupata ushauri wa kiufundi kuhusu gari zao, pia tamasha hilo litakuwa ni sehemu ya kukutanisha watu na kupata burudani.
  Mgaya alisema, Mafundi wapatao 50 waliobobea katika fani ya ufundi magari, wamepatikana baada ya kufanyiwa usaili wa kina na kupitia mchujo na semina elekezi ili kuweza kuhudumia magari yanayokadiriwa kufika zaidi ya 6000 kwa siku hizo mbili.Pamoja na hayo, Mgaya alisema “ Tumeandaa warsha maalum kwa kina dada, tunatambua kuwa asilimia kubwa ya waendesha magari barabarani hivi sasa ni kina dada, tunataka waelewe ni nini cha kufanya pindi atakapopatwa na hitilafu kwenye gari mabarabarani. 
  Elimu hii ambayo wameiita ‘Auto First Aid’, alisema itasaidia kupunguza uharibifu zaidi kwenye magari yao, alisema wakati mwingine kwenye dashboard ya gari kuna kuwa na alama za hatari, lakini kwa kuwa gari inatembea wanawake wengi wamekua wakipuuzia alama hizo na matokeo yake wanasababisha hasara kubwa zaidi.
  Afisa Mkuu wa Fedha wa Milembe Insurance, Dioniz Diocles (wa kwanza kulia) akiongea mbele ya waandishi wa habari kuelezea jinsi walivyoona umuhimu wa kudhamini tamasha hilo. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Jast Tanzania Limited, Jahu Mohammed Kessy, Mratibu wa Tamasha hilo, Mmiliki wa Jossekazi Auto garage ambao ndiyo waandaaji wa tamasha, Mwakilishi toka Mwambi Lube Distributor, Jonathan Mwanayongo. Picha/Video na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.

  “Pamoja na kuwafundisha alama za hatari na nini cha kufanya pindi waonapo alama hizo pia Tutawafundisha kubadilisha matairi, na nini chakufanya na kuwa nacho ikitokea gari limewaharibikia njiani. “ alisema Mgaya. 
  Mgaya ambaye amefanikiwa sana katika ufundi wa AC za magari, Ndege, na Meli, aliongeza kuwa fani ya ufundi makenika ni kazi ya kuheshimika kama zilivyo kazi nyingine, na kuongeza kuwa anaiona fursa kubwa kwa vijana wanaomaliza elimu ya juu.
  “Siku hizi magari yote kuanzia Mwaka 2005 kwenda juu yanatumia vifaa maalum vya computer na internet, pamoja na kuwa maelezo yanakuja kwa lugha ya kingereza, ufundi spana wa kurithishwa hivi sasa hauna nafasi,”alisema.
  “Tofauti na zamani ukifeli form 4, unapelekwa kwenye ufundi hali hivi sasa imebadiliilka fani hii inahitaji wasomi na watu wanaoweza kubadilika na kurudi shuleni kila mara, kama computer matoleo ya magari kila mwaka yanakuja na vitu tofauti, hivi sasa break hazina annoying sound, break zikiisha utaona kwenye dashboard, kutengeneza lazima useme user manual ya kingereza na u download soft ware kwenye internet,” alisema Mgaya na kusistiza vijana waingie kwenye fani hii. 
  Aidha Mkurugenzi wa Jast Tanzania Limited, Jahu Mohammed Kessy, Mratibu wa Tamasha hilo walisema kuwa, Automobile Clinic litakuwa zaidi ya Tamasha.
  “Katika kuhakikisha tunautumia muda wa wateja wetu vizuri, wakati gari inafanyiwa ufundi, kutakuwa na huduma nyingine za ziada zitakazo patikana siku hizo mbili, kutakuwa na vinywaji, vyakula kama nyama choma, na michezo ya watoto, kutakuwa na huduma ya kulipia ya kuoshewa magari, kusafishiwa taa, na baadhi ya vifaa kama Fire extinguisher, manukato ya gari, Triangle na kadhalika vitauzwa hapo uwanjani,”
  Jahu alisema Tiketi zitauza kabla, na kwamba tiketi hizo zitakuwa katika mfano wa sticker ya kubandika kwenye magari, na zitapatikana katika vituo vyote vya kuweka mafuta vya TSN, Supermarket zote za TSN, Kwenye ofisi za Millembe insurance, Bon to shine, BM hair cutting salon, na Mlimani City.
  “Hakutakuwa na Kiingilio kwa watu, lakini badala yake kwa magari, magari yenye sticker pekee ndiyo yatakayoruhusiwa kuingia na kupata huduma hizo, tunashauri wenye kununua sticker wafike mapema kwani watakao fika kwanza ndio watakao hudumiwa,”Jahu alisema katika kurudisha kwa jamamii, mafundi hao hamsini baada ya Tamasha watatembelea kwenye hospitali ya CCBRT kusaidia wakina mama wenye matatizo ya fistula.
  Tamasha hilo limedhaminiwa na Milembe insurance, Wambi lube oil distributor, TSN, Binslum tires company Limited, I view, Cocacola, Dreams Limited, Hugo Domingo, Olduvai Bay Wash, 0-60 autogarage, Meku Auto spear part, Dick Sound, Brand Tiger, Clouds FM, Auto Beats, Neh Catering, Pamoja na Lim Painting and decorating.

  0 0

  Neema  Herbalist  &  Nutritional  Foods  Clinic  ni  wauzaji  wa  dawa  mbalimbali  za  asili. Tunapenda  kuwatangazia  wateja  wetu  kuwa  tunayo  dawa nzuri  ya  asili  inatibu na  kuponyesha  kabisa  tatizo  la  ukosefu  na  upungufu  wa  nguvu  za  kiume. Dawa  hii  iitwayo  JIKO  ni  ya  asili  kabisa  (PURE  HERBAL) na  inaponyesha  na  kumaliza  kabisa  tatizo  la  nguvu  za  kiume  ndani  ya  siku  thelathini.

  JINSI   DAWA  YA  JIKO  INAVYO  FANYA  KAZI.
  Dawa ya JIKO inasadia katika mambo makuu yafuatayo:
  i. Inasaidia kuimarisha mishipa ya uume ulio legea na hivyo kuufanya uume uwe na uwezo wa kusimama barabara kama msumari wakati wa tendo la ndoa.

  ii. Inasaidia kusafisha mishipa ya kwenye uume na hivyo kusaidia katika kuongeza kasi ya msukumo wa damu kwenye mishipa ya kwenye uume.
  iii. Husaidia kuongeza msukumo (pressure) wa damu kwenye mishipa ya uume na hivyo kuufanya uume kuwa na nguvu za ajabu.

  iv. Husaidia kurelax mind na hivyo kumfanya mtu awe na uwezo wa kuconcentrate wakati wa tendo la ndoa bila kuathiriwa na msongo wa mawazo.

  v. Humfanya mwanaume awe na uwezo wa kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara moja bila kuchoka.
  vi. Husaidia kuongeza hamu ya tendo la ndoa.
  vii. Husaidia kuurudisha nje uume ulio ingia ndani.
  viii. Husaidia kutibu side effects za punyeto na matumizi ya muda mrefu ya dawa kali za (za kizungu ) za kuongeza nguvu za kiume.
  ix. Husaidia kutibu chango la kiume.
  x. Inakuwa uwezo  wa  kukaa  kifuani  kwa  muda  mrefu
  xi. Pia   kurutubisha  mbegu  za  kiume
  xii.. Dawa hii huwasaidia hata wanawake wanao sumbuliwa na tatizo la ukosefu wa hamu ya tendo la ndoa.

  BEI  YA  DAWA : Bei  ya  Dawa hii  ni  shilingi  ELFU  THEMANINI.
  JINSI YA KUIPATA DAWA : Unaweza kuja kuichukua ofisini kwetu au kwa wasio weza kufika ofisini kwetu tunatoa huduma ya kuwapelekea dawa mahali walipo.

  ( DELIVERY ).
  KWA WATEJA WA MIKOANI : Kwa wateja wa mikoani tunawatumia dawa kwa njia ya magari na wale wa Zanzibar tunawatumia dawa kwa njia ya meli.
  KWA WATEJA WA NCHI JIRANI : Kenya, Uganda, Rwanda & Burundi tunawatumia dawa kwa njia ya mabasi.
  Kwa wateja wa nje ya Afrika : Kwa wateja wa nje ya Afrika tunawatumia dawa kwa njia ya posta au DHL.
  Kwa wateja wa SOUTH AFRIKA NA BOTSWANA.
  Kwa wateja wetu waliopo South Afrika na Botswana tunawatumia dawa kwa njia ya mabasi au posta.
  MAWASILIANO : Wasiliana nasi kwa simu namba 0766538384.
  Tunapatikana  katika  eneo  la CHANGANYIKENI  karibu  na  CHUO CHA  TAKWIMU.
  Kwa  maelezo  zaidi  kuhusu  tatizo  la ukosefu  wa nguvu  za  kiume, tembelea http://neemaherbalist.blogspot.com/2014/04/maajabu-ya-korodani-za-mbuzi-korodani.html
  Na  kwa  taarifa  zaidi kuhusu  huduma  zetu  tembelea www.neemaherbalist.blogspot.com

  0 0

  Balozi wa Tanzania Nchini Malawi Mh. Patrick Tsere Akizungumza na waandishi wa Habari kutoka Mbeya walipotembelea Ofisi za ubalozi Nchini Malawi 
  Baadhi ya Waandishi wakimsikiliza Balozi 
   Baadhi ya Waandishi wa Habari Kutoka Mkoani Mbeya wakimsikiliza Balozi kwa Makini
   Balozi wa Tanzania Nchini Malawi Mh. Patrick Tsere akipokea Taarifa kutoka kwa waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mbeya 
   Balozi wa Tanzania Nchini Malawi Mh. Patrick Tsere akijibu Taarifa ya waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mbeya .
  Waziri wa Habari , Utalii na Utamaduni Nchini Malawi Mh. Kondwani Nankumwa akiongea na waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mbeya Ofisini kwake.
   Baadhi ya Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mbeya wakifuatilia Hotuba ya Waziri wa Habari, Utalii na Utamaduni Mh. Kondwani Nankumwa
   Wa kwanza Kulia ni Afisa Habari wa Waziri wa Habari, Utalii na Utamaduni akifuatilia Mkutano huo
   Waandishi wa Habari wakiendelea kufuatilia Kikao hicho
  Francis Phiri wa kwanza Kulia ambaye ni Mratibu wa ziara hiyo Nchini Malawi na Muasisi wa Nyika Press Club ya Malawi akiwa katika Mkutano huo.
  Kikao kikiwa Kinaendelea 
  Waziri wa Habari, Utalii na Utamaduni Nchini Malawi  Mh. Kondwani Nankumwa wa pili kutoka kushoto waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na Waandishi wa Habari Kutoka Mkoa wa Mbeya nje ya Ofisi yake Jijini Lilongwe.

  Waziri wa Habari,Utalii na Utamaduni nchini Malawi Mheshimiwa Kondwani Nankhumwa alisema kuwa Serikali ya Malawi haina mgogoro na Serikali ya Tanzania kuhusiana na mpaka wa ziwa Nyasa.


  Aliyasema hayo baada ya kukutana na Jopo la Waandishi Habari wa Mkoa wa Mbeya waliotembelea ofisini kwake katika mfululizo wa ziara ya waandishi waliofanya ziara ya juma moja nchini humo katika ziara ya kubadishana uzoefu baina ya Waandishi wa Nchi hizo.


  Waziri Nankhumwa alisema  kuwa Mtoto wa Rais  wa Malawi Profesa Ather Muthalikana  anasoma Dar es Salaam naye Rais amekuwa Muhadhiri wa chuo kikuu na kwamba Watanzania wengi wanaishi na kufanya biashara nchini Malawi hivyo hakuna sababu za kuwepo kwa tofauti za aina  yoyote ile itayowapelekea kuwagawa wananchi wa pande hizo.


  Aidha alisema kuwa ili kuonesha hakuna tofauti baina ya wananchi wa pande hizo Marais wa nchi hizo watapaswa kuchukua ndoano na kuvua samaki pamoja katika ziwa hilo ili kuionesha Dunia kuwa wananchi wa pande hizo ni wamoja na kuna mwingiliano wa makabila.


  Kauli hiyo iliungwa mkono na Balozi wa Tanzania nchini Malawi Patrick Tsere ambaye alisema kuwa hakuna mgogoro wa mpaka katika Ziwa Nyasa baina ya Tanzania na Malawi.


  Aliyasema hayo alipotembelewa na waandishi wa Habari wa Mkoa Mbeya walipotembelea ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Malawi katika mfulizo wa ziara ya waandishi hao nchini Malawi ili kubadilishana mawazo na changamoto mbalimbali zikiwemo za mazingira,utalii na Elimu juu ya Ukimwi ambazo zinafanana katika nchi hizo.


  Balozi Tsere alisema hivi sasa si wakati wa marumbano kwani inahitajika subira katika mzungumzo yaliyonza baina ya viongozi wa nchi hizo na kwamba si wakati wa kuupeleka mgogoro huo katika mahakama ya  kimataifa ambapo utazigharimu fedha nyingi nchi hizo katika utatuzi wa mgogro huo.


  Hata hivyo Waandi wa Habari wa nchi hizo walifanya makubaliano ambayo yatasaidia kuzitangaza nchi hizo kimataifa ikiwa ni pamoja na mbuga za wanyama zilizopo  Malawi na Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Songwe ili utumiwe na wananchi hizo ili kukuza uchumi wan chi hizo.


  Katika ziara hiyo Waandishi  wa vyombo mbalimbali walishiriki ikiwa ni pamoja na Tone Multimedia Group, Mbeya yetu Blog,Chanel Ten,Mwananchi,Jambo leo,Bomba Fm,Majira na Raia Mwema.  Vingine na Tanzania Daima,Baraka FM na Mwandishi Rais mstaafu Ulimboka Mwakilili ambaye alikuwa Mwenyekiti wa safari na Mhandisi wa Ujenzi Claudio  Lusimbi ambaye ni Mlezi Katika Safari hiyo


  Na Mbeya Yetu Blog , Lilongwe Malawi.

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameongozana na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa La Guardia jijini Washington DC tayari kwa kushiriki katika mikutano mbalimbali na pia katika hafla ya "USIKU WA JAKAYA" leo jioni
   Rais Kikwete akilakiwa na maafisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Marekani baada ya kuwasili hoteli aliyofikia
   Karibu Washington DC Mheshimiwa
   Rais akiendelea kusalimia na na wafanyakazi wa ubalozini
   Mapokezi yakiendelea
   Rais Kikwete akisalimiana na Bw. Lucas Mkama wa Vijimambo Blog
  Karibu sana Mzee...

  0 0

   Ndugu zangu,
  LEO ni Septemba 19, ni Siku ya Kuzaliwa Mtandao wa Mjengwablog.
  Kwa mwanadamu, hakupaswi kuwapo na ukomo wa kujitahidi kufanya yalo mema kwa jamii yako.

  Na katika kujitahidi kuyafanya yalo mema, basi, mwanadamu uwe tayari kukumbana na changamoto nyingi. Na kama ilivyo kwa maji ya mto, yanapokutana na mwamba, basi, kasi yake huongezeka maradufu.

  Leo blogu yako hii ya Mjengwablog imetimiza miaka minane. Miaka minane si haba. Kwa mtoto, aweza kuwa darasa la Pili. Na kwetu wa Mjengwablog ni miaka minane ya kujifunza, kukosea, kujifunza kutokana na makosa, na kisha kusonga mbele.

  Kwa niaba ya timu nzima ya Mjengwablog nachukua fursa hii kuwashukuru, kwanza kabisa, mke wangu mpenzi, Mia, ambaye, bila yeye, kazi hii yangu ya kuitumikia jamii ingelikuwa ngumu sana. Pili, niwashukuru kwa dhati wanangu wanne, Olle, John, Manfred na Gustav. Wanawangu hawa wamekuwa na mchango mkubwa pia, ikiwamo kufanya utani na mimi baba yao, ilimradi niwe na wakati wa kucheka, hata pale nilipoona kazi ni ngumu na kukutana na vikwazo.

  Na kwa dhati kabisa, naishukuru timu nzima ya Mjengwablog. Nawashukuru kwa upekee kabisa Wanafamilia wote wa Mjengwablog, ukiwamo wewe unayesoma maandiko haya sasa, maana, bila nyinyi, kusingekuwa na maana ya kuifanya kazi hii. Mmekuwa nasi katika hali zote. Hivyo basi, kutuunga mkono.Naam, ni miaka minane ya kuwa mtandaoni karibu katika kila siku inayotujia na kupita. Ni miaka minane ya mapambano magumu ya kuitumikia jamii na kuhakikisha kuwa tunabaki hai.

  Maana, unapoamua kuitumikia jamii bila kuegemea upande, basi, ina maana pia ya kujiweka katika mazingira ya hatari sana. Yumkini kuna maua mengi ya upendo yanaweza kurushwa kwako, lakini, kuna mishale michache ya sumu ambayo pia itarushwa kwako. Kwamba kuna maadui pia.

  Na ukimwona nyani ametimiza miaka minane , basi, ujue kuna mishale kadhaa ameikwepa. Lakini, na anavyozidi kuendelea kuishi, yumkini kuna mishale mingine inaandaliwa. Na nyani hatakiwi kuishi kwa kuogopa mishale ya wanadamu. Vinginevyo, ajitundike mtini, afe. Lililo jema na kutia faraja ni kutambua, kuwa kuna walio wengi wenye kufaidika na kazi hii ya kijamii ambayo Mjengwablog inaifanya. Ni hawa ndio wenye kututia nguvu ya kuendelea kuifanya kazi hii pamoja na changamoto zake nyingi.

  Ndugu zangu,
  Ilikuwa ni Jumanne, Septemba 19, 2006. Ni siku hiyo ndipo kwa mara ya kwanza niliingiza picha ya kwanza kwenye mjengwablog na kuashiria uzinduzi wa blogu. Ni picha hiyo inayoonekana hapo juu. Niliipiga eneo la Kinondoni Shamba. Tangu siku ya kwanza, niliweka wazi kwenye fikra zangu, kuwa Mjengwablog iwe jukwaa litakalomtanguliza mtu wa kawaida. Iwe sauti ya wale ambao sauti zao hazisikiki.

  Na Mjengwablog ikawa chachu ya kuanzishwa kwa gazeti la michezo na burudani la ’ Gozi Spoti’, ikawa chachu pia ya kuanzishwa gazeti la ’ Kwanza Jamii’.Na kuna miongoni mwetu wenye kufikiri, kuwa mwenye kumiliki gazeti ni lazima awe Mhindi au Mtanzania ’ mweusi’ Mfanyabiashara tajiri.

   Nakumbuka kuna hata ambao hawakuwa tayari kuchangia kiuandishi kwenye ’ Gozi Spoti’ na ’ Kwanza Jamii’ kwa vile linamilikiwa na ’ Mswahili mwenzao!’Na hata kupata matangazo kukawa na ugumu mkubwa. Gozi Spoti lilisimama kuchapwa baada ya mwaka mmoja mitaani. Kwanza Jamii, nalo likasimama kuchapwa. Likarudi tena baada ya kuingia ubia na Shirika la Daraja. Baada ya miaka miwili na baada ya aliyepelekea kuingia ubia kuondoka nchini na kurudi kwao Uingereza, basi, Kwanza Jamii nalo ’ likaandaliwa’ mazingira ya kuondoka mitaani.

  Hata hivyo, Kwanza Jamii, gazeti dogo, ambalo naamini ni muhimu kwa jamii, limerudi tena kwa kutolewa bure kanda ya Nyanda za Juu Kusini na kwa kupitia mtandaoni. Mipango iko mbioni kuliimarisha zaidi katika siku zijazo.

  Ndugu zangu,Changamoto zipo ili tukabiliane nazo, na si kukata tamaa. Mjengwablog inatimiza miaka minane leo kwa vile tulishaamua, kuwa tutapambana hadi risasi ya mwisho. Hivyo pia, tutapambana hadi pumzi ya mwisho.

  Maana, tunaamini kuwa kazi tuifanyayo ni yenye manufaa kwa jamii pana. Na tuna haki ya kuifanya. Tunavumilia sauti zenye kutushutumu na kutukosoa. Kuna tunayojifunza kutoka kwa wakosoaji wetu. Tunawashukuru sana na tunawaomba waendelee kutukosoa kila wanapoziona kasoro.

  Chini hapa ni maoni ya kwanza kabisa kutumwa na mtembeleaji. Na anachoandika mtembeleaji huyu kutoka India kinaakisi dhamira niliyokuwa nayo.

  Bwana huyu anasema; { fakir005 } at: Tue Sep 19, 06:32:00 PM EAT said... This looks like an African blog. Once the TV showed an African milk his cow. The cow had so stretched tits. I've never seen so much stretching. The african as really stretching further to twice the original length to get any drop of milk he could get. It was obvious the cow was dry because it was too long after the birth of her calf and needed to be inseminated again.The cow just stood there while the African worked the Tits. The picture does not show anycows. But the man in the picture and the house remind me of the TV scene in the gone years."
  Maggid,
  Mwenyekiti Mtendaji.
  Mjengwablog.com

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kama ishala ya kuzindua rasmi mpango wa Utambuzi wa ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi wa mafunzo, kwa ajili ya kutathimini na kutambua ujuzi na elimu ua ufundi Stadi kwa Vijana waliojifunza fani mbalimbali, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika leo Septemba 19, 2014 kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Kazi, na Ajira, Gaudensia Kabaka (kushoto) ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Dkt. Shukuru Kawambwa.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, mmoja kati ya wahitimu 30, wa mafunzo hayo, Charles Gwambassa, wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa mpango wa Utambuzi wa ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi wa mafunzo, kwa ajili ya kutathimini na kutambua ujuzi na elimu ua ufundi Stadi kwa Vijana waliojifunza fani mbalimbali. Hafla hiyo ilifanyika leo Septemba 19, 2014 kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach, jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, mmoja kati ya wahitimu 30, wa mafunzo hayo, Mwajuma Massoud, wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa mpango wa Utambuzi wa ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi wa mafunzo, kwa ajili ya kutathimini na kutambua ujuzi na elimu ua ufundi Stadi kwa Vijana waliojifunza fani mbalimbali Hafla hiyo ilifanyika leo Septemba 19, 2014 kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach, jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Prof. Betria Mapunda ambae amemwakilisha Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar Es salaam akifungua semina iliyoandaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PPF kwa Waajiri kwa lengo la Kutoa elimu juu ya huduma zitolewazo na mfuko huo wa Pensheni wa PPF katika ukumbi wa Seaescape, Uliopo Mbezi Beach Jijini Dar Es Salaam.
  Meneja wa Kanda ya Kinondoni wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Zahara Kayugwa akitoa mada wakati wa semina iliyoandaliwa na Mfuko wa Penhsheni wa PPF kwaa Waajiri wa Makampuni na mashirika mbalimbali iliyofanyika katika ukumbi wa Seaescape, Mbezi Beach Jijini Dar Es Salaam leo.
  Majaliwa E Mkinga, Mchambuzi na Mtengenezaji wa Mifumo ya Teknolojia ya habari na mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF akielezea jinsi PPF ilivyotengeneza mfumo wa kupata taarifa za wanachama kupitia simu aina za Smartphone na kuutaja mfumo huo kuwa ni PPF TAARIFA App ambayo mteja ataweza kuiweka katika simu yake ya mkononi.
  Baadhi ya waajiri wakielekeza kuhusu jinsi ya kuweka mfumo wa PPF Taarifa katika simu zao za Smartphone leo katika semina iliyofanyika katika Ukumbi wa Seascape hotel Mbezi beach Jijini Dar Es Salaam.

  0 0

  Mkurugenzi wa Kitengo cha Uthaminishaji wa Madini ya Almasi na Vito cha Wizara ya Nishati na Madini (TANSORT), Archard Kalugendo (mwenye shati la batiki), akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Taasisi ya Wafanyabiashara wa Madini ya Vito wa Thailand, walipotembelea Banda la Tanzania katika Maonesho ya 54 ya Vito na Usonara ya Bangkok, yaliyofanyika Septemba 9 hadi 13 mwaka huu.
  Makamu wa kwanza wa Rais wa Taasisi ya Wafanyabiashara wa Madini ya Vito na Usonara wa Thailand, Bw. Sutipong Dumrongsakul, akimkabidhi zawadi maalumu Mkuu wa Ujumbe kutoka Tanzania ulioshiriki maonesho ya vito ya Bangkok, Archard Kalugendo, mara baada ya kikao kati ya Ujumbe huo na Viongozi wa Taasisi hiyo ya Wafanyabiashara wa Thailand.
  Wateja mbalimbali wakihudumiwa katika Banda la Tanzania kwenye maonesho ya vito na usonara ya Bangkok yaliyofanyika hivi karibuni nchini   Thailand.

  0 0

  Haya ni MAHOJIANO na Ahmed Mngazija a.k.a (Pongonyongo) jinsi alivyojiingiza bila ya kutegemea katika janga la madawa ya kulevya.Ahmed azungumzia mengi juu ya maisha ya wengi walioathirika na mihadarati kisiwani Zanzibar .Sikujua wala sikutambua lakini nilipomsikiliza kwa makini ndipo nilipofunguka na kuelewa zaidi juu ya ndugu zetu waliotumbukia bila ya kutegemea katika uvutaji wa madawa ya kelevya, na kwa kweli wanahitaji kupewa msaada mkubwa wa kuwaponyesha na majanga haya.Jiunge nasi kwa kumsikiliza mwanzo hadi mwisho ili na wewe upate kujua nini kimejiri kwa Ahmed Mngazija.! Karibu kusikiliza nasi

  0 0
 • 09/19/14--09:51: Article 1
 • JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
  TAARIFA KWA UMMA

  MAADHIMISHO YA SIKU YA UTALII 2014


  Wizara ya Maliasili na Utalii  kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa  Mkoa wa Arusha  pamoja na Wadau wa Sekta ya Utalii nchini wanayofuraha ya kuwakaribisha   Wananchi wote  na Wadau mbalimbali  katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani   kwa mwaka 2014  ambayo  Kitaifa yatafanyika  Mkoani Arusha kwenye viwanja vya  Nane Nane (TASO) kuanzia tarehe 20 hadi 28 Septemba, 2014.
  Siku ya Utalii Duniani huadhimishwa tarehe 27 Septemba ya kila mwaka ambapo kila nchi  mwanachama wa Shirika  la Utalii Duniani (UNWTO) husherekea siku hii, kwa lengo la kuweka uelewa kwa Jamii kuhusu umuhimu wa utalii na thamani yake, kijamii, kisiasa, kitamaduni na kiuchumi.
  Kauli Mbiu ya Mwaka huu ni “Utalii na Maendeleo ya Jamii’’ (Tourism and Community Development) kwa kuzingatia Kauli Mbiu hii,  tunawajulisha wadau wote katika nyanja mbalimbali za Utalii, Maliasili na Uhifadhi, vikundi vya jamii na wajasiriamali, viongozi na wataalamu kwa pamoja kushiriki kikamilifu katika  Maadhimisho ya  Siku ya Utalii Duniani kwa nia ya kujifunza na kutambua fursa za kiuchumi zilizopo katika Sekta ya Utalii na kutumia fursa hizo kujikomboa katika umaskini.
  Shughuli zitakazofanyika ni pamoja na kuwasilisha na kuonesha na kwa vitendo juu ya tafsiri ya Kauli Mbiu kwa kufanya kongamano la  ushirikishwaji wa jamii kwenye sekta ya Utalii kwa ajili ya kujiletea maendeleo, mashindano ya Uchoraji wa picha kuhusiana na kauli mbiu, michezo na burudani mbalimbali.
  Vilevile kutakuwa na maonesho ya utalii, malikale, misitu na masuala ya uhifadhi kwa ujumla na bila kusahau ziara ya kutembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na  Hifadhi ya Taifa ya  Arusha  kwa nia ya kuhamasisha wananchi kushiriki kwenye shughuli za utalii wa ndani.
  Wito unatolewa kwa kuwaalika wadau wote wa utalii na jamii husika kuja kwa pamoja na kuadhimisha siku hii kama ishara ya jitihada za pamoja za kufanya utalii nguzo ya kweli ya maendeleo ya Jamii nchini.

  Imetolewa na:
  Katibu Mkuu
  Wizara ya Maliasili na Utalii.

  0 0

   Naibu Waziri wa Fedha –Sera, Mhe. Mwigulu Nchemba akifungua mafunzo ya wiki tatu ya wakufunzi, wasimamizi na wadadisi kutoka Tanzania Bara  na  Zanzibar  watakaoendesha utafiti wa kufuatilia hali ya umasikini katika kaya mwaka 2014/15.
   Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Joel Bendera akiwakaribisha washiriki wa mafunzo ya wiki 3 ya utafiti wa kufuatilia hali ya umasikini katika kaya mwaka 2014/15 mkoani Morogoro.
   Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akizungumzia  umuhimu wa matumizi ya takwimu sahihi wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wakufunzi, wasimamizi na wadadisi kutoka Tanzania Bara  na  Zanzibar  watakaoendesha utafiti wa kufuatilia hali ya umasikini katika kaya nchini mwaka 2014/15.
   Washiriki wa mafunzo ya wiki tatu ya wakufunzi, wasimamizi na wadadisi kutoka Tanzania Bara  na  Zanzibar  watakaoendesha utafiti wa kufuatilia hali ya umasikini katika kaya nchini mwaka 2014/15 yanayofanyika mkoani Morogoro wakifuatilia masuala mbalimbali .
   Naibu Waziri wa Fedha –Sera, Mhe. Mwigulu Nchemba akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mhe. Joel Bendera wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wiki tatu ya wakufunzi, wasimamizi na wadadisi kutoka Tanzania Bara  na  Zanzibar  watakaoendesha utafiti wa kufuatilia hali ya umasikini katika kaya mwaka 2014/15 mkoani Morogoro.
  =========  ==========
  WANANCHI WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KWA WATAALAM WA UTAFITI WA HALI YA UMASIKINI WA KAYA TANZANIA.
  Na. Mwandishi wetu – Morogoro.
  19/9/2014.

  Serikali imewataka wananchi na viongozi wa maeneo mbalimbali nchini kuhakikisha kuwa wanatoa ushirikiano kwa wadadisi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu watakaoendesha  zoezi la utafiti wa ukusanyaji  wa takwimu za kufuatilia hali ya umasikini katika  kaya kwa mwaka 2014/2015, utaokaofanyika  kuanzia Oktoba mwaka huu.

  Kauli hiyo imetolewa jana mkoani Morogoro na Naibu Waziri wa Fedha –Sera, Mhe. Mwigulu Nchemba wakati akifungua mafunzo ya wiki tatu ya wakufunzi, Wasimamizi na wadadisi watakaoendesha utafiti huo kutoka Tanzania Bara  na  Zanzibar.

  Amesema serikali  kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa upande wa Bara na ile ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar  imeamua  kufanya utafiti huo ili kupata takwimu bora na sahihi zitakazoiwezesha kujitathmini na kupima juhudi zake katika kuwaletea wananchi maendeleo, kukuza uchumi na kupunguza umasikini wa kipato.

  Amesema utafiti huo  pamoja na tafiti zilizopita utaiwezesha serikali kuchambua kiundani sababu zinazofanya kaya nyingi nchini kuendelea kubaki kwenye umasikini,  baadhi kutoka kwenye  umasikini na nyingine kuingia kwenye umasikini.

  “Kufanyika kwa utafiti huu kutatuwezesha kufahamu namna na sababu zinazofanya kaya kuendelea kubakia kwenye umasikini , baadhi ya kaya kutoka kwenye umasikini na nyingine  kuingia kwenye umasikini” Amesema.

  Ameongeza kuwa kukamilika kwa utafiti huo kutaiwezesha serikali kuelewa kwa kina changamoto zinazoikabili katika utekelezaji wa Sera, mikakati na programu mbalimbali za maendeleo kwa wananchi.

  Mhe. Mwigulu amefafanua kuwa Serikali itaendelea kuiwezesha Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kuijengea uwezo ili iweze kukamilisha tafiti mbalimbali zinazoendelea kufanyika nchini kwa kufikisha matokeo ya tafiti hizo katika ngazi zote za utawala.

  “Nia yetu ni kuhakikisha kuwa mipango ya maendeleo ya wananchi inapangwa kwa kutumia takwimu rasmi, kwa upande wetu serikali takwimu rasmi ni masikio  na macho katika utendaji wa kazi za kilia siku” Amesisitiza Mh. Mwigulu.

  Aidha, amewataka wakufunzi, wasimamizi na wadadisi watakaoendesha zoezi hilo walio kwenye mafunzo hayo kutoa elimu kwa wananchi katika maeneo yote watakayopita kuhusiana na umuhimu wa zoezi hilo kwa taifa  na kusisitiza kuwa serikali haitawavumilia wadadisi watakaokiuka maadili katika utekelezaji wa majukumu yao.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo amesema  kuwa washiriki wa mafunzo hayo watakaofaulu wataruhusiwa kushiriki katika utafiti huo.

  Amesema kuwa utafiti huo hufanyika  kila baada ya miaka 2  kwa kuzipitia kaya binafsi ambazo huhojiwa kwa vipindi tofafuti ili kupata ufahamu wa namna ambavyo kaya zinaingia na kutoka kwenye hali ya umasikini wa kipato na sababu zinazochangia hali hiyo.

  Ameeleza kuwa kwa mwaka huu utafiti huo utakuwa wa nne  kufanyika hapa nchini ukitanguliwa na zile zilizofanyika mwaka 2008/09, 2010/11 na 2012/13.

  Amefafanua kuwa madodoso ya utafiti huo yatafuatilia na kukusanya taarifa muhimu za sekta nyingine muhimu ambazo zinaweza kuchambuliwa kwa  kuhusishwa  na hali ya umasikini zikiwemo kilimo, uvuvi, mifugo, Afya, Ajira na Upatikanaji wa huduma za maji, umeme, afya na elimu.

  Amesema Ofisi ya Taifa ya Takwimu itahakikisha  takwimu hizo zinasambazwa katika ngazi zote za utawala kwa ajili ya kutumika  kupanga mipango ya maendeleo ya wananchi. 

  Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera awali akizungumza wakati wa kuwakaribisha washiriki wa mafunzo hayo mkoani Morogoro amesema kuwa bila takwimu sahihi hakuna mipango ya maendeleo inayoweza kufanyika.

  Amesema kuwa kukamilika kwa utafiti huo  kutatoa picha halisi ya nini kifanyike katika kuwaletea maendeleo wananchi.

  0 0

  Today, I held a meeting with U.S -based Senegalese musician, Akon, who paid me a courtesy call at State House, Nairobi. Akon affirmed his commitment to supportGovernment’s initiative to light up Kibera and other selected parts of rural Kenya. This is part of his Lighting Africa project that aims to provide electricity to a million households across the continent by the end of the year. It is good to see that discussions on scaling up supply of power to Kenyans that we started during last month’s U.S – Africa Leaders’ Summit in Washington, DC are bearing fruits. I commend Akon for being a role model to African youths and I would like to encourage others to emulate him by investing back in their mother countries. We welcome this initiative and we will give him all the support he needs.older | 1 | .... | 366 | 367 | (Page 368) | 369 | 370 | .... | 1897 | newer