Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 365 | 366 | (Page 367) | 368 | 369 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Biashara kutoka Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Abdulla Makame Akiwaeleza waandishi wa Habari(hawapo pichani) Kuhusu Mkutano wa 29 wa Baraza la Mawaziri wa nchi  wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika Septemba 20 mwaka huu Jijini Arusha. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara hiyo Anthony Ishengoma.
  Picha na Hassan Silayo
   
  Frank Mvungi- Maelezo
  Mkutano wa 29 wa Baraza la Mawaziri wa nchi  wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki  utapokea na kuidhinisha aina mpya ya hati za kusafiria za kielektroniki, zikiwemo sampuli za hati za kusafiria za kibalozi,  za Maofisa na za kawaida.
  Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Biashara,Uwekezaji na shughuli za uzalishaji wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk. Abdulla Makame  wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
  Mkutano huo utakaofanyika Septemba 20 mwaka huu Jijini Arusha pia unatarajia kupokea na kuidhinisha taarifa mbalimbali sambamba na kutolea maamuzi masuala yanayohusu mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
  Akieleza zaidi Makame amesema mkutano huo utapokea na kuidhinisha aina mpya ya hati ya kusafiria ya kielektroniki,zikiwemo sampuli za hati za kusafiria za kibalozi,  za Maofisa na za kawaida za kusafiria.
  Aidha Mkutano huo utajadili mapendekezo na hadidu za rejea za uanzishwaji wa Dira ya maendeleo ya Afrika Mashariki ya mwaka 2050.
  Pia mkutano huo utajadili mapendekezo ya mpango mwelekeo na shughuli mbalimbali zinazolenga kuandaa katiba ya shirikisho la Afrika Mashariki na kujadili mapendekezo ya baraza la ulinzi na usalama linalopendekezwa.
  Baraza la Mawaziri katika Jumuiya ya Afrika mashariki ni chombo cha pili katika ngazi za kufanya maamuzi ndani ya Jumuiya ya  Afrika Mashariki baada ya Mkutano wa Kilele.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi mkutano wa Mashauriano kati ya Vyombo vya Habari na Vyombo vya Ulinzi, Usalama na Sheria, uliofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, leo Septemba 17, 2014. Mkutano huo uliandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT).
  Rais wa Baraza la Habari Tanzania, (MCT) Jaji Thomas Mihayo, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kufungua rasmi mkutano huo, uliofanyika leo Septemba 17, 2014 kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Baraza la Habari Tanzania, (MCT) Kajubi Mukajanga, akizungumza kabla ya mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kufungua rasmi mkutano huo, uliofanyika leo Septemba 17, 2014 kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.

  0 0

   Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene akitoa pongezi kwa Mfuko wa Pensheni wa PSPF kwa mafanikio waliopata tangu kuanzishwa kwa mfuko huo, kwenye mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bw. Adam Mayingu akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mafanikio ya mfuko huo kwa kipindi cha miaka 15 tangu ulipoanzishwa. Kushoto ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF Bw. Abdul Njaidi.
   Baadhi ya watumishi wa PSPF na waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa mfuko huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bw. Adam Mayingu akijibu maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu tofauti za malipo ya pensheni kwa wastaafu  ambapo alisema kuwa tofauti hizo zinatokana na kiwango cha mshahara na muda wa utumishi wa mwanachama.
  Wakurugenzi wakionesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) tuzo mbalimbali zilizotolewa kwa PSPF. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bw. Adam Mayingu, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Bw. Masha Mshomba, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa PSPF Bi. Neema Muro.PICHA ZOTE NA GEORGINA MISAMA (MAELEZO)

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini usiku wa jana, Jumatatu, Septemba 15, 2014, kuanza ziara ya wiki mbili katika Marekani ambapo atahutubia Mkutano wa 69 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN General Assembly) New York. Mbali na kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Rais Kikwete pia atahudhuria mikutano muhimu katika mji mkuu wa Marekani, Washington, D.C.
  Rais Kikwete akiagana na viongozi mbalimbali waliofika kumuaga katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Septemba 15, 2014. Kushoto ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali
  Rais Kikwete akiagana na viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama waliofika kumuaga katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Septemba 15, 2014. Kulia ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali
  Rais Kikwete akisindikizwa na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali wakati alipokuwa anaondoka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam kuelekea Marekani Septemba 15, 2014. 
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwasili New York, Marekani. Kulia Mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi akifuatiwa na Mama  Upendo Manongi Septemba 16, 2014
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakilakiwa na maofisa mbalimbali wa Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa baada ya kuwasili New York, Marekani, Septemba 16, 2014.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakilakiwa na maofisa mbalimbali wa Tanzania  baada ya kuwasili New York, Marekani, Septemba 16, 2014.  PICHA NA IKULU

  0 0


   Waziri wa Habari  Utamaduni Utalii na Michezo  Saidi Ali Mbarouk Mwenye Koti Jeupe akipewa Maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa uwanja wa ndege Juma Saleh.Katika ziara hiyo Waziri Mbarouk alitembelea maeneo tofauti ya Uwanja wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume.
   Baadhi ya Wageni kutoka nchi tofauti wakipata huduma kutoka Uhamiaji mara baada ya kuwasili Uwanja wa Abeid Aman Karume. Picha na Yussuf Simai-Maelezo Zanzibar.

  Maryam Himid/Saada Saleh-ZJMMC

  Waziri wa Habari  Utamaduni Utalii na Michezo  Saidi Ali Mbarouk  amezitaka Taasisi zinazosimamia kupokea Watalii Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Amani Abeid Karume kujenga mashirikiano ili kuondosha usumbufu kwa wageni wanaoingia  na kuotoka nchini. Ameyasema hayo alipofanya ziara Uwanjani hapo kwa lengo la kuangalia hali halisi ya Wageni wanaoingia na kutoka nchini.

  Waziri Mbarouk amesema  suala la Mashirikiano kwa wageni ni jambo muhimu linaloweza kuijengea sifa kubwa Zanzibar  kwa wageni ambao wanakuja ambao wataweza kusimulia watakaoporudi ziara zao. Ametoa wito kwa Taasisi husika kuhakikisha Wageni wanaoingia Zanzibar wanapata huduma stahiki na ili kuepukana na usumbufu wa aina yoyote wanapofika katika Uwanja huo wa Ndege.

  Kwa upande wake Daktari wa kituo cha Afya uwanjani hapo  Juma muhammed Juma amesema Wanaendelea kulisimamia vyema suala la kuwakagua kwa Vifaa maalumu Wageni wanaoingia kutoka Nchi zilizoathirika na Ugonjwa wa Ebola. Amezitaja Nchi hizo kuwa ni pamoja na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Liberia na Sera lion ambapo amesema kila abiria kutoka nchi hizo lazima Apimwe ili kuweka kinga ya Ugonjwa wa Ebola nchini.

  Hata hivyo Mkurugenzi wa uwanja wa ndege Juma Saleh  Juma ameelezea baadhi ya changamoto zinazowakabili uwanjani hapo kuwa ni pamoja na upungufu wa maeneo ya kukaribisha wageni,maegesho ya Magari na Uhaba wa Wafanyakazi  wanaozungumza Lunga ya Kitaliano kutokana na Wataliano hao kutumia lugha yao tu.
  Katika ziara hiyo Waziri Mbarouk alitembelea maeneo mbali mbali Uwanjani hapo ikiwemo Mapokezi, Maegesho ya Ndege na Magari na sehemu ya Mapumziko ya Abiria.

  0 0

  Mzee Shauri Timoth Nathan  (18/08/1925-18/09/2007)
    
  Sekunde, Dakika, Saa, Siku, Wiki, Mwezi, Mwaka na hatimaye mika saba sasa imetimia tangu Mzee Shauri Timoth Nathan  (18/08/1925-18/09/2007) ututangulie Mbele za haki kama ulivyotutangulia kuja duniani Tarehe 18/08/2025. 

  Nimajonzi sana kwetu hasa ukizingatia kuwa uliondoka katika tarehe ambayo kitinda mimba wako Mroki Mroki alizaliwa na ni siku kumi tu baada ya kufunga ndoa Mroki "Father Kidevu".

  Unakumbukwa na wengi sana maana ulikuwa ni mhimili mkuu katika familia, kipekee ni Mke wako Mary O Nathan na watoto wako James Nathan, Mrs Stella Kaluse, Lloyd Atenaka, Dossa Mroki,Freddrick (Kajiru) Mroki, Onesmo Nathan, Thomas Nathan, Daniel Nathan, Kyaze Nathan, Namche Mroki, Kille Nathan na Mroki Mroki na Wakwe zako wote.

  Pia unakumbukwa sana na Wajukuu zako Kidai Kaluse, Shauri Kaluse, Mfaume Kilangi, Shauri James, Mwanaamani James, Hellena James, Nuru James, Maria Kaluse, Ludao Kaluse, Kilave Atenaka, Maria Atenaka, Victoria Dossa, Doureen Atenaka, Erick Mushi, Beatrice Mroki, Timothy Tomas, Timothy Kajiru, Imanuel Kajiru, Elizabeth Kajiru, Timothy Kille, Maria Thomas, Irine Atenaka, Anjela Chistian, Glory Mroki, Nathan Kyaze, Nathan Dossa, Dinner Onesmo,Digna Onesmo, Debora Daniel na  Leonard Kyase pamoja na Vitukuu wako pia kutoka kwa Mwanaamani, Kidai na Shauri.

  Wananchi na majirani zako wa pale Kijiji cha Kipera , Kitongoji cha Kinyenze,Kata na Tarafa ya Mlali , Wilayani Mvomero mkoani Morogoro pia wanakukumbuka sana pamoja na wote wa Ugweno, Kilimanjaro.
  Tunakumbuka maneno yako ya Mwisho uliotuachia watoto wako kuwa "TUPENDANE, TUSAIDIANE na TUSHIRIKIANE," baba hakika hili linatendeka na tupo na umoja uliotujengea na tunajivunia hilo.

  Tunazidi kukuombea Baraka na pumziko jema maana sote uliotuacha tutakufata kama tulivyo kufuata hapa duniani.

  Jina la Bwana Lihimidiwe Amina.

  0 0

  Kava la Filamu ya KITENDAWILI iliyochezwa na Single Mtambalike au Rich Rich, Irene Veda na Haji Adam ambayo inasambazwa na Kampuni ya Proin Promotions Limited
  Kava la Filamu ya NETWORK iliyochezwa na MONALISA NA BRIAN ambayo inasambazwa na Kampuni ya Proin Promotions Limited.
   

  Tamasha la Arusha Film Festival ni tamasha la kimataifa ambalo linatarajiwa kufanyika kwa Mara ya Tatu mfululizo, ambapo litaanza tarehe 20 mpaka 27 Mwezi wa tisa (september) Jijini Arusha.
   

  Arusha Film Festival 2014 tayari imeshatangaza majina ya filamu  
  zilizochaguliwa kuonyeshwa katika tamasha hilo kubwa la kimataifa ambalo hujumuisha filamu toka mabara yote yaani Africa, Ulaya, Marekani na Asia. 
  Filamu zilizochaguliwa kuingia katika Tamasha hizo kutoka kampuni mahiri ya utengenezaji na usambazaji wa filamu Tanzania ya Proin Promotions Limited na ambazo zina ubora wa kimataifa huku filamu hizo kutoka Proin Promotions ltd zikiiwakilisha vyema Tanzania. 
  Filamu zilizoingia katika tamasha hilo na  zenye ubora wa Kimataifa kutoka Kampuni ya Proin Promotions Ltd ni pamoja na Kitendawili(feature), Kigodoro(Feature), Sunshine(Feature), Network(Feature).
  Filamu hizi za Kitanzania zina sehemu moja tu yaani part 1 na sio Part 1 na part 2. Kwa kuzingatia vigezo vya kimataifa vya filamu kuwa Na Sehemu Moja tu yaani Part 1 ndio sababu filamu kutoka Proin Promotions zimefanikiwa kupita mchujo ambapo Kampuni ya Proin Promotions Ltd ambayo haitaki part 1 na part 2 kwa lengo la  kukuza tasnia ya filamu nchini.
  Filamu za Tanzania zenye part 1 na part 2 zimetupwa nje sababu waandaji na wataalamu wa nje wameziona hazina ubora wa muda katika standard ya kimataifa na vigezo  vinginevyo.
  Filamu hizo za Tanzania zitaonyeshwa pamoja na filamu mbalimbali nyingine zilizopita katika mchujo huo toka mataifa mabalimbali ikiwemo Canada, Kenya, Uganda, Austalia, Rwanda, Spain, S.Africa, Guinea Bisau, Brazil, Nigeria, Switzerland, Argentina, UK, Burundi, Morocco. Ili kuona List nzima ya filamu hizo ingia hapa Selected Films Arusha Film Festival 2014.
  Vilevile kutakuwa na zoezi la utoaji wa tuzo  katika tamasha hilo la filamu kwa kazi nzuri.

  0 0

   Mwenyekiti wa Kikundi cha Tumaini Saccos, akiowanesha namna sanduku maalumu la kutunzia taarifa za kikundi chao linavyolindwa, wakati maofisa wa Kampuni ya Bia Tanzania walipokwenda hivi karibuni kukagua miradi mbalimbali ya wananchi wilayani Arumeru inayowezeshwa na Taasisi ya ACE AFRIKA kwa ufadhili wa TBL.
   Mwanachama wa Tumaini Saccos ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa kikundi hicho akionesha baadhi ya shughuli anazozifanya mbazo amewezeshwa na ACE AFRICA  chini ya ufadhili wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). Maofisa wa TBL walikwenda hivi karibuni kukagua miradi ya kikundi hicho.
   Mkulima wa bustani ya ndizi na mboga za majani, Isaya Supuk wa kijiji cha Olmotonyi, wilayani Arumeru, Arusha akiwaonesha maofisa wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) na ACE AFRICA namna shamba lake lilivyostawi wakati maofisa hao wa TBL walipokwenda hivi karibuni kukagua shughuli hizo zilizofadhiliwa na na kampuni hiyo.
  Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),  Editha Mushi akizungumza na Mkurugenzi wa ACE AFRICA (TANZANIA), Joanna Waddington ofisini kwake Arusha, hivi karibuni kuhusu ufadhili wao unaowezeshwa na taasisi hiyo kwa wananchi wa Arumeru katika shuguli mbalimbali za maendeleo..

  0 0
 • 09/17/14--22:22: KINANA AMALIZA ZIARA MAFIA
 •  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kuashiria ishara ya kuweka jiwe la msingi katika jengo la ofisi ya CCM wilaya ya Mafia.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya siasa wilaya ya Mafia.
   Hii ndio ofisi mpya ya CCM wilaya ya Mafia.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana akifanya mzaha na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye mara baada kukagua mradi wa maji,masaidia zaidi ya mradi huu wa maji  utahudumia watu zaidi ya 3000.
   Sehemu ya vifaa vya mkandarasi vikiwa kwenye eneo linapotengenezwa tuta la Banjo,ujenzi wa tuta hili utasaidia sana wakazi wa vijiji vya Banja na Jojo.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea zawadi ya mashua kutoka kwa Katibu wa CCM wilaya wa pwani
   Mafia umeme kila kona mpaka kwenye nyumba ya Udongo
   Mafia
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiwaaga wananchi wa Mafia tayari kwa safari ya kurudi Nyamisaki.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimwonyesha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman taarifa mbali mbali kutoka kwenye blogs, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza na upande wa pili kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwinshehe Mlao.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahma Kinana akiteremka kutoka kwenye mashua ambayo imewasafirisha salama kwa muda wa masaa manne.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiteremka kwenye mashua


  0 0

  Warembo 30 wanaoshiriki shindano la Redd's Miss Tanzania 2014 jana walitembelea hifadhi ya taifa ya Mikumi mkoani Morogoro kujionea vivutio mbalimbali vya utalii viliovyopo katika hifadhi hiyo ambapo waliweza kujionea wanyama wa aina mbalimbali wakiwepo, Tembo, Twiga, Swala, Viboko na Simba.
   Kaimu Mhifadhi Utalii wa Hifadhi ya Taifa Mikumi, Apaikunda Mungure akigawa vipeperushi kwa warembo.
  Warembo walibahatika kuwaona Simba zaidi ya Saba wakiwamepumzika chini ya mti.

   Warembo wa Redd's Miss Tanzania wakiongozwa na Matron wao, Gladness Chuwa mbugani Mikumi.

  Warembo wakipiga picha na watalii waliowakuta Mikumi.


   Punda milia nao walionekana kwa wingi.
   Wakisikiliza maelezo juu ya Viboko kutoka kwa Benina Mwananzila.
   Warembo wakipata maelezo katika kituo cha Mbuyu
   Muongoza watalii Ibrahim Kassim akitoa maelezo kwa washiriki wa shindano la Redd's Miss Tanzania 2014.
   Mrembo akitazamana na ngedere
   Warembo wakitembelea lodge ya Hifadhi hiyo ya Mikumi.
   Tembo nao walikuwepo.

  0 0

  Balozi Mdogo wa Tanzania Dubai Mhe Omar Mjenga (kulia) akiongozana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Nakheel ambayo ndio kampuni kubwa ya Serikali Dubai ambayo ni wawekezaji wakubwa duniani katika sekta ya uendelezaji miliki, Rashid Ahmed Lootah, kuingia kwenye chumba cha mikutano cha Ofisi za 

  Mkurugenzi Mkuu wa NHC jiji Dar es Salaam jana, nyuma yake ni Mkurugenzi Mkuu wa Ujenzi wa Miradi wa Kampuni hiyo, Masood Al Zarooni na Injinia Fawzi Al Shah ambaye ni Mkurugenzi wa Udhibiti na Mipango Miji wa Kampuni hiyo.

  Mwenyekiti huyo na ujumbe wake wakiongozwa na Balozi Mjenga walikuwa na mazungumzo na Menejimenti ya Shirika la Nyumba la Taifa kuhusiana na fursa za uwekezaji zilizopo katika Satellite Cities na Fursa za Kujenga uwezo wa masuala mbalimbali katika uendelezaji miliki.  

  Baadhi ya miradi iliyosimamiwa na kampuni hiyo ni pamoja na The Palm Dubai (the largest island Palm City in the World), Nakheel Mall, Dragon Mart na baadhi ya hotel za nyota tano Jijini Dubai. (Picha za

  0 0

   Mstahiki Jerry Silaa meya wa Ilala akimkabidhi msaada huo wa madawati mia moja (100) mwalimu mkuu wa shule ya msingi kivule 
    Mstahiki Jerry Silaa meya wa Ilala akipeana mkono wa shukrani na mratibu Bw.Mkami Sudayi
   Diwani wa kata ya kivule Bw.Nyansika Motena akitoa shukrani kwa meya mara baada ya kukabidhiwa msaada huo
   Afisa elimu wa Ilala Bi. Bi Elizabeth Thomas naye pia aliungana na wenzake kuweza kumpa mkono meya wa ilala Jerry Silaa
   Waalimu wa shule ya kivule wa kiwa katika picha ya pamoja na Mh.Jerry Silaa mara baada ya kukabidhiwa madawati hayo.

  Meza kuu ikiwa imepambwa na viongozi mbalimbali kwaajili ya kupokea msaada wa madawati.Meya wa manispaa ya  Ilala Jerry silaa akabidhi msaada wa madawati mia moja katika shule ya msingi kivule iliyopo jijini dar es salaam ikiwa ni mpango aliouanzisha na kuanza kuutekeleza kupitia (meya boll) katika mpango huo madawati hayo yamekabidhiwa kwa mwalimu mkuu wa shue hiyo pamoja na diwani wa kata ya kivule na afisa elimu wa manispaa ya ilala walikuwepo katika shuguli hiyo ya kupokea msaada huo Jana
   Bw.Nyansika G Motena ambaye ni Diwani wa kata ya kivule katika halmashauri ya ilala akiongea machache kumkaribisha mstahiki meya
   Mwalimu mkuu wa shule ya msingi kivule akisoma Risala ya shule hiyo kabla ya kukabidhiwa msaada wa madawati
   Meya wa Ilala Mstahiki Jerry Silaa akizungumza mara baada ya kupokea risala iliyo somwa na Mkuu wa shule ya kivule
   Mh.Akifurahi na wanafunzi wa shule hiyo ambapo walikuwa na furaha wa kupokea msaada huo
   Wanafunzi wakishangilia kwa furaha na meya  wakiwa wamekabidhiwa msaada huo wa dawati miamoja
   picha  Jerry Silaa meya wa Ilala akiwa na daadhi ya viongozi na wanafunzi 
    Afisa Elimu wa Manispaa ya Ilala, Bi Elizabeth Thomas akiongea maneno ya shukrani kwa meya mara baada ya shughuli ya kukabidhi kumalizika
   Mwanafunzi Frednand  chales akiongea maneno ya shukrani kwa meya mara baada ya shughuli ya kukabidhi kumalizika
   Kwenye picha ni baadhi ya madawati yaliyotolewa na Meya wa Ilala Mstahiki Jerry Silaa katika shule ya kivule iliyopo manispaa ya Ilaa jijini Dar es Salaam
   baadhi ya wanafunzi wakiwa wanaendelea kusikiliza tukio liendavyo
   Kikundi cha ngoma cha makirikiri kilichoundwa na wanafunzi kwaajiri ya kusherehesha katika sherehe hiyo ua kukabidhi madawati mkatika shule ya kivule
   Burudani ikiwa imepamba moto kwa kusherehesha wahudhuriaji  na kikundi hicho
   kauli iliyopo katika madawati hayo
   
   kundi la burudani ka kikulwa likiwa linatoa burudani wakati wa kukabidhi madawati hayo
   Mh:Jerry Silaa akiwa ameongozana wa viongozi mbalimbali walio kuwepo katika shughuli hiyo kwenda kukagua madarasa mawili mapya yaliyo jengwa hivi karibuni 
   Akizungumza na viongozi hao mara baada ya kuangalia madarasa hayo ambayo nayo ameshirika katika kuchangia wakati wa ujenzi
  haya ndiyo madarasa ya vyumba viwili mapya yaliyo jengwa hivi karibuni katika  shule ya kivule.

  Akikabidhi madawati hayo MH:Jerry Silaa amewaasa kuwa hata yeye alikuwa anasoma na anakaa chini lakini kwa kizazi cha sasa yatupasa tubadilike hiyo hatapenda kuona watoto wakiendelea kukaa chini  na kusoma katika mazingira magumu kama aliyo weza kusoma yeye  kwahiyo kwa moyo wake anarudisha fadhira kwa watanzania  kwa kushirikiana na wadau mbal;imbali kwa misaada tofautitofauti katika kipindi chake cha uongozi kwa nafasi ya meya.
  Aidha muheshimiwa aliweza kuwafafanulia baadhi ya watu walio weza kufika katika hafra ya kukabidhi madawati kwa shule ya kivule kwamba kodi za pango zinavyo kusanywa huwa haziliwi na mtu zaidi ya kutatua matatizo katika sehemu mbalimbali ya halmashauri kwahiyo aliwaomba watu wote wasiwe na imani ya kuliwa kwa fedha hizo bali watambue zinakazi nyingi na tofauti tofauti katika halmashauri husika.
  Naye mwalimu mkuu wa shule ya kivule wakati akisoma risala waliyo iandaa kwaajiri ya shughuli hiyo alisema shule ya kivule inawanafunzi wengi ambao ni takribani ya wanafunzi 2020 ambapo inakabiriwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya ukosefu wa madawati ,matundu ya vyoo,nyumba za walimu ambapo kwa sasa kuna nyumba moja tu,waalimu wa masomo mbalimbali pamoja na vifaa vya kufundishia hususani  somo la Tehama,hivyo kupelekea waalimu kutumia nguvu katika ufundishaj.
  Bw.kubilu Lupembe  Dede  ambaye ni mwalimu mkuu wa shule ya kivule ametoa shukrani za dhati kwa mstahiki meya  wa ilala Jerry Silaa ambapo ameonesha nia ya dhati katika kufanikisha elimu inasonga mbele kwa kujitoa sehemu mbalimbali  na kuwa karibu na jamii


  Pia diwani wa kata ya kivule Bw.Nyansika.G.Motena ametoa shukrani kwa niaba ya wananchi wote kwa kile anacho kifanya mheshimiwa meya wa ilala Jerry Silaa ameweza kukifany ana kusema inapaswa kuwa kiongozi wa mfano kwa wengine  


  0 0

  LEO ni siku ya kuzaliwa ya mpiganaji Mroki Mroki 'Father Kidevu' ambapo leo anaadhimisha miaka kadhaa hapa duniani. Anasema Sifa na Utukufu anazirudisha kwa Mungu maana yeye ndie ajauae sababu ya kumuacha hadi hii leo na hakuna alicho mpa. Pia anashukuru wazazi hasa mama yake, familia yake ikiongozwa na mkewe pamoja na watoto wao. 

  "Ndugu zangu mbali na hao niliowataja hapo juu, lakini ninyi marafiki zangu, Wadau wangu, ndugu na jamaa wote popote pale mlipo hapa duniani ni watu muhimu sana sana, hadi kufika hapa leo ninyi mnachango wenu wa namna moja au nyingine. Sina la zaidi ya kusema Asanteni sana na Mungu awazidishie na tukazidi kuishi kwa amani na Upendo."

  HAPPY BIRTHDAY FATHER KIDEVU!! HAPPY BIRTHDAY MROKI MROKI!!

  0 0


  Regional retailer Nakumatt Holdings has announced the scheduled late opening of all its branches across East Africa this Sunday to allow the firm observe the Westgate Shopping Mall Terror attack first anniversary memorial activities.


  One year after the tragic terror attack, Nakumatt which hitherto operated its flagship store at the Westgate Mall will this Sunday conduct interdenominational religious prayers across its network.


  Speaking when he confirmed the memorial plans ahead of the events, Nakumatt Holdings Managing Director Atul Shah disclosed that the supermarket chain will remain closed early morning for the prayers scheduled to commence at 9am on Sunday.


  The prayers will be led by respective Nakumatt branch chaplains and catechists and will be open to members of the public. All branches are expected to reopen from 10am after the memorial prayers.


  Still on Sunday, the firm will also disrupt its normal operations at 12noon to observe a minute of silence in memory of the departed souls and victims of the terror attack. The observance of the branch wide minute of silence in Kenya will be followed by the recital of the National Anthem which is also a powerful prayer to God.


  “The events on that fateful Saturdaymidmorning are still very painful and the entire Nakumatt fraternity shall be taking time off on Sunday to say our memorial prayers to seek God’s comfort, global peace, love and harmony,” Shah explained. In Nairobi, Shah, will also lead Nakumatt staffers to light a memorial candle outside the Westgate Shopping mall at 12noon on Sunday.


  One year ago, Nakumatt Holdings suffered the loss of three of its dedicated staff members the late Veronicah Wairimu, Kennedy Mogaka and John Musango Mutinda who were fatally shot at the mall. The retailer, also lost its flagship Nakumatt Westgate branch to a mysterious fire just days after the terror attack.


  Since then, Nakumatt which had a branch complement of 40 branches has managed to set off on a recovery path and recently opened its 50th branch in Arusha, Tanzania.

  0 0

  OKTOBA NI MWEZI WA KUKUZA UELEWA WA MATUMIZI SALAMA YA MITANDAO.

  Miaka 11 iliyopita Marekani ikitambua ukuaji wa matumizi mabaya ya mitandao walianzisha kampeni maalum iliyoamuliwa kufanyika kila mwezi oktoba. Kampeni hiyo maalum ilihamasisha mashule , kampuni binafsi na  serikali kutumia mwezi oktoba kuhamashisha uelewa wa matumizi salama ya mitandao.

  Kadri muda ulivyojongea Mataifa mengine yaliamua kutumia mwezi huo kuwa mwezi wa kukuza uelewa wa matumizi salama ya mitandao ambapo sasa mataifa mengi tayari yamesha kua yakiazimisha kampeni hizi. Mwaka huu wa 2014 Kama Inavyo ainishwa "HAPA" imeweza kuchanganua  kwa ufupi  maudhui na kauli mbiu ya mwaka huu, ratiba, namna ya kushiriki na mambo mengine muhimu.

  Ifahamike vizuri jitihada za kukuza uelewa wa matumizi salama ya mitandao duniani kote ni endelevu na mwezi oktoba umechukuliwa kuwa maalum ili kuonyesha umuhimu wa kampeni hizi kwa kuzingatia ukuaji wa matumizi ya mitandao unaoambatana kabisa na matumizi mapaya kwa baadhi ya watu.

  "JUMBE"  teule kwa upande wangu ni kuongeza matumizi mazuri na sahihi ya maneno ya siri ili kujiweka salama utumiapo mitandao.

  Kwa Upande mwingine Tanzania imeendelea kuwa mwenyeji wa midahalo na  warsha mbali mbali zihusianazo na maswala ya usalama mitandao ambapo ni fursa nzuri kwa watanzania kuweza kushiriki ili kukuza uelewa wa maswala haya ya ulinzi mitandao ambapo dunia ya leo yemeonekana kua na sura ya pekee.


  Mwanzoni mwa mwaka huu Nikiwa Ughaibuni, Kwenye "MKUTANO"mkuu wa mwaka katika maswala usalama mitandao na teknolojia ya habari kwa ujumla miongoni mwa mazungumzo mengi nje ya vikao yalionyesha mataifa mbali mbali kua na jitihada binafsi za kuhakiki mikutano na warsha mbali mabli zinachukua nafasi ya pekee ili kuhamasisha matumizi salama  ya teknolojia habari na mawasiliano.

  Kwa Tanzania, "MKUTANO" Unaotegemea kukamilika Hapo Kesho wa Maswala Ya Usalama Mitandao Jijini Arusha umekua ni moja ya fursa nzuri kwa watanzania kuhakiki wanatambua hali halisi kuhusiana na uhalifu mtandao na jitihada endelevu zinazoendelea kwenye taifa kwenye mapambano dhidi ya uhalifu mtandao.

  Aidha, mwezi wa Oktoba  mwaka huu Tanzania Inategemewa kuwa mwenyeji wa mkutano/ Warsha ya kimataifa ya maswala ya usalama katika mitandao ambapo wataalam kutoka mataifa mbali mbali watategemewa kujadili maswala mbali mbali. Kushiriki warsha hii muhimu,Mtanzania anapaswa kusoma na kujaza Fomu maalumu iliyo ambatanishwa hapo chini na kuirudisha COSTECH Tanzania.


  Mwezi Novemba mkutano Mwingine mkubwa wa kufunga mwaka unaotegemewa kuhusisha wataalam mbali mbali wa maswala ya uslama mitandao watakutana kuongezeana uwezo na kujadili maswala makuu manne ya jinsi ya kutambua uhalifu mtandao, Kuuzuia, Kuchukulia hatua unapotokea na jinsi ya kurudisha uslama mitandao katika hali yake ya awali baada ya kutokea.

  "MKUTANO" huu ambapo Mwenyeji wake ni Nchi ya Afrika Kusini ni fursa nyingine kwa watanzania kuhuduria ili kujua mengi katika maswala haya ya uhalifu mitandao ikizingatiwa mimi nikiwa kama Mtanzania kuteuliwa kuwa katika Paneli ya Washauri katika Mkutano huo.

  0 0

  Na Greyson Mwase, Katavi

  Makamishna wasaidizi wa madini wa kanda wametakiwa kuongeza ushirikiano  wa karibu  na  viongozi waandamizi wa mikoa na wilaya ili kukuza sekta ya madini  ili iwe na  mchango mkubwa katika uchumi wa taifa.

  Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya  ya  Mpanda Bw. Paza Mwamlima alipokutana na timu ya majaji na sekretarieti iliyomtembelea ofisini kwake  kabla ya kuendelea na zoezi lake la kumtafuta  mshindi wa  Tuzo ya Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji  katika wilaya  ya Mpanda. Timu hiyo inafanya  tathmini katika makampuni ya madini  katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo ya jamii ili  kumpata mshindi  atakayekabidhiwa tuzo na Rais mapema mwezi Novemba. Maeneo yanayoangaliwa ni pamoja na miundombinu,  maji, afya, elimu, manunuzi  ya ndani, ajira pamoja na uwezeshaji wa vikundi  vidogo   vidogo katika jamii husika.

  Bw. Mwamlima alisema kuwa ili kuhakikisha kuwa sekta ya madini inakuwa na mchango mkubwa katika uchumi wa wilaya na mkoa, ni vyema  ofisi za madini zikafanya kazi kwa karibu kwa kushirikiana na ofisi za mikoa na wilaya  katika usimamizi wa  sekta ya madini kupitia wawekezaji.

  Alisema kuwa ofisi za  madini zinapaswa kuongeza kasi ya  ushirikishaji wa taarifa zake za kijiolojia pamoja na kuwatambulisha wawekezaji kwa ofisi za mikoa na wilaya  kabla ya kuanza kwa shughuli za utafiti na uchimbaji wa madini katika  maeneo husika. Alisisitiza kuwa kupatikana kwa taarifa sahihi na kwa wakati, kunarahisisha katika usuluhishi wa migogoro kati ya wawekezaji na jamii inayozunguka migodi inayoweza kujitokeza.

  “ Tunaamini kuwa kupitia makanmishna wasaidizi wa madini, tunaweza kuwa na taarifa zote za kijiolojia,aina na idadi  ya wawekezaji  walioko  katika maeneo yetu, na hii inaturahisishia  katika usuluhishi wa migogoro kati ya  wawekezaji na jamii  inayowazunguka inayoweza kujitokeza,” Alisema Bw. Mwamlima.


  Naye mtaalamu kutoka Wizara  ya Nishati na Madini Mhandisi  Jones Mushi alisema kuwa katika Sheria ya Madini  kuna kifungu kinamtaka mwekezaji  kujitambulisha  katika ofisi ya mkoa na wilaya kabla ya kuanza kwa shughuli za utafiti na uchimbaji wa madini katika eneo husika.

  Mhandisi Mushi alisema kuwa Wizara imekuwa ikihimiza makamishna wasaidizi wa madini wa kanda  kushirikiana kwa karibu zaidi  na ofisi za mikoa na wilaya   ili kuboresha sekta hiyo ikiwa ni pamoja na kukabiliana  na changamoto zinazoweza kujitokeza.Wakati huo huo  timu ya majaji  ilitembelea mgodi wa utafiti wa madini  aina ya dhahabu wa GBN ambapo uongozi wa kampuni hiyo umesema kuwa unatarajia kuanza uzalishaji wa madini mwezi Oktoba.

  Akizungumza na  timu hiyo  kwa niaba ya mgodi huo, msimamizi wa mgodi huo Bw. Edson  Steven amesema kuwa mgodi huo unatarajia kuanza uzalishaji wa dhahabu  baada ya utafiti wake kukamilika. Alisema kuwa mgodi huo ulianza rasmi mwaka 2013 kwa kufanya utafiti wa madini ya  dhahabu na hadi  kufikia Juni mwaka huu ulikuwa umejiridhisha na kiasi cha  madini ya dhahabu kilichopo katika mgodi huo.

  Akielezea mafanikio ya mgodi huo kwa  kipindi cha mwaka  2013 Bw. Steven alisema kuwa mgodi  ulichangia   katika ujenzi wa shule ya  sekondari ya Machimboni, kompyuta kwa ajili ya ofisi ya mkuu wa polisi ya mkoa.Naye  Afisa Utawala na Fedha wa kiwanda cha kuyeyusha madini ya shaba cha TPM ambacho pia  kilitembelewa na  timu ya majaji kwa ajili ya tathmini Bw. Philip Muna, akielezea mafanikio ya kiwanda hicho alisema kuwa, katika kipindi cha mwaka 2014 kiwanda kilinunua mashine ndogo   ya kusaga mawe yenye dhahabu kwa ajili ya  kikundi cha  wachimbaji wadogo  saba kama moja ya utekelezaji wa shughuli za jamii.

  Bw. Muna alisema kuwa kiwanda kilianza na uhamasishaji kwa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu waozunguka maeneo  ya kiwanda hicho kuunda umoja ili waweze kuwapatia  mashine ndogo kwa ajili ya kusaga mawe yenye dhahabu na kuchenjua ili kujipatia kipato. Alisema kuwa mara baada ya vijana hao kuunda kikundi chao chenye jumla ya wajumbe saba, uongozi wa kiwanda hicho uliwapatia mashine hiyo ambayo imekuwa msaada mkubwa kwao.

  Akielezea mafanikio mengine Bw. Muna alieleza kuwa ni pamoja na ujenzi na ukarabati wa barabara yenye urefu wa kilomita 2.2 na transfoma  moja inayotumiwa na kampuni hiyo pamoja na wakazi wanaozunguka kiwanda hicho.

  0 0

  Afisa Habari wa Wakala wa Ajira Tanzania (TaESA) Jamilah Mbarouk akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuelezea mkakati wao wa kuanzisha mafunzo ili kuweza kuwasaidia vijana wahitimu ili wakabiliane na soko la ajira, Wakala umekuwa ukitoa mafunzo ya namna ya kushindania fursa za ajira. Mafunzo haya yamevutia watafutakazi wengi ambao tayari wako sokoni na walioko vyuoni. Aidha mafunzo haya yamewabadilisha vijana wengi waliohudhuria kuhusu suala zima la kuajiriwa na kujiajiri na kupelekea uhitaji wa mafunzo haya kuongezeka. Pembeni yake Afisa Utawala, Peter Ugata.


  0 0

  Model: 2001
  4 CYLINDER
  COLOUR: SILVER
  LEATHER SEATS
  1999-CC
  120,000 Km
  AMPLIFIER
  SUB WOOFER na CD CHANGER.
  VIDEO DVD PLAYER
  Price:11 Milion Tshs.
  Kwa mawasiliano piga +255-714-940992
  DSC_0258IMG-20140918-WA0006_1
  Muonekano wa mbele usiku.
  IMG-20140918-WA0005
  Muonekano wa ndani usiku.
  DSC_0259
  Muonekano wa ubavuni kushoto na kulia.
  DSC_0260DSC_0257
  Muonekano wa nyuma.
  IMG-20140918-WA0007_1

  0 0

   Kamishna wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (Tacaids), Daniel Machemba katikati akikata utepe kaushiria uzinduzi wa mabango ya kuelimisha Ukimwi na masuala mbalimbali ya kuwajengea uwezo vijana yatakayosambazwa katika vyuo vikuu mbalimbali na Shirika la Vijana Tayoa. Anayefuata kulia ni kamishna mwingine Diana Chilolo, Mkurugenzi wa Tayoa Peter Masika. Kulia ni Mhadhiri wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM, Emmanuel Mushi na Kamishna wa Tacaids, Faraja Kotta Nyalandu.
   Kamishna wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi, Diana Chilolo akimkabidhi zawadi Mhadhiri wa Chuo cha IFM, Emmanuel Mushi kwa chuo hicho kushirikiana na Shirika la Vijana tayoa katika mapambano dhidi ya Ukimwi. Nyuma yake ni kamishna mwingine, Faraja Kotta Nyalandu, Kamishna Daniel  Machemba na Mkurugenzi Mkazi wa Tayoa Peter Masika.
  Kamishna wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi, Diana Chilolo akimkabidhi zawadi Mhadhiri wa Chuo cha IFM, Emmanuel Mushi (mbele shati la bluu) kwa chuo hicho kushirikiana na Shirika la Vijana tayoa katika mapambano dhidi ya Ukimwi. Pembeni yake ni kamishna mwingine, Faraja Kotta Nyalandu, Kamishna Daniel  Machemba na Mkurugenzi Mkazi wa Tayoa Peter Masika.

  0 0

  Asasi Nne zisizo za kiserikali zinazojishughulisha na kupambana na mabadiliko ya tabianchi nchini ForumCC, CAN, YouthCAN na Oxfam Tanzania zimetoa tamko la pamoja kuhusiana na Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika huko New York-Marekani tarehe 23/09/2014.

  Katika tamko hilo ambalo pia limewasilishwa kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira, Dr. Eng. Binilith Mahenge, mambo matano yamependekezwa kuzingatiwa wakati wa mkutano huo ambao Rais wa Tanzania DK. Jakaya Kikwete pia atatoa hotuba yake.

  Mambo hayo ni pamoja na kupunguza utoaji wa hewa ukaa (Emission Reduction), Misaada ya Fedha za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi (Climate Finance), Kuongeza mapambano ya mabadiliko ya tabianchi kwa vitendo, Matumizi ya teknolojia na Nishati Mbadala na Kilimo.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira, Dr. Eng. Binilith Mahenge(katikati) akiwa na Viongozi wa Forum CC, kutoka kulia ni Oscar Munga, Mjumbe wa bodi ya wadhamini ya ForumCC, Vera Mugita, Afisa Miradi, Fazal Issa na Adam Anthony.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira, Dr. Eng. Binilith Mahenge wa kwanza kushoto akizungumza na Mjumbe wa bodi ya wadhamini ya ForumCC, Vera Mugita na Afisa Miradi wa ForumCC Fazal Issa
  Meneja Ushawishi wa Oxfam, Eluka Kibona wa kwanza kushoto akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika huko New York-Marekani Septemba 23, 2014Mahenge.
   Afisa Miradi wa ForumCC, Fazal Issa akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa Habari.  Waandishi wa habari wakifuatilia ufafanuzi kutoka kwa viongozi wa asasi za kiraia kuhusu Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika huko New York-Marekani Septemba 23, 2014

  Picha zote na tabianchi blog

older | 1 | .... | 365 | 366 | (Page 367) | 368 | 369 | .... | 1897 | newer