Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 364 | 365 | (Page 366) | 367 | 368 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Washiriki wa Mkutano wa Wadau wa Maendeleo, maafisa wa serikali na TASAF wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa mkutano huo kwenye ukmbi wa miktrano wa Mwalim Nyerere jijini DSM.
   Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw Ladislaus Mwamanga akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa Mkutano wa pamoja baina ya wadau wa maendeleo,Maafisa wa serikali na watendaji wa TASAF kwenye Ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini DSM leo.
   Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Bwana Peter Ilomo akifungua mkutano wa wadau wa Maendeleo ,maafisa wa Serikali na watendaji wa TASAF uliofanya mapitio ya Mpango wa kunusuru kaya maskini uliofanyika kwenye Ukumbi kimataifa wa  Nyerere Jijini DSM.
   Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Peter Ilomo (aliyeketi katikati) akiwa na viongozi wengine Katika meza kuu wakifuatilia maelezo ya Mkurgenzi Mtendaji wa TASAF ,Bw. Ladislaus Mwamanga (hayupo pichani) wakati wa ufungzi wa Mkutano wa mapitio ya Mpango wa Kunusuru kaya maskini uliofanyika jijini DSM.
   Wakurugenzi wa TASAF Bw.Amedeus Kamagenge wa kwanza mbele na  Fariji Mishael wa pili wakifuatilia mjadala wa mapitio ya Mpango wa Kunusuru kaya maskini kati ya wadau wa maendeleo ,maafisa wa serikali na watendaji wa TASAF kwenye ukumbi wa kimataifa wa MWL jk Nyerere jijini DSM.
   Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abass Kandoro katikati akifuatilia mada kwenye mkutano wa wadau wa maendeleo ,maafisa wa serikali na watendaji wa TASAF ambao mefanya mapitio ya Mpango wa knusuru kaya maskini kwenye ukmbi wa Kimataifa wa JK Nyerere jijini DSM.
   Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa wadao wa maendeleo na wale wa serikali na TASAF wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa mkutano uliojadili maendeleo ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru kaya maskini PSSN.
   Mmoja wa walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini Kong’enza Mfunda Chanzi  mkazi wa Mwanabwito  wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani akitoa ushuhuda wa namna alivyonufaika na Mpango wa kunusuru kaya maskini kwenye mkutano wa wadau wa maendeleo,maafisa wa serikali na watendaji wa TASAF.

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya maji mama mmoja  wa Kijiji cha Muyuyu, katika Jimbo la Kibiti, alipozindua mradi wa maji katika Kijiji cha Muyuyu, wakati wa ziara yake  ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya  maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM mkoani Pwani.
   Katibu wa Ityikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, akihutubia katika Kijiji cha Mchukwi ambapo Kinana alikwenda kuzindua kikundi cha Akina mama cha kutengeneza batiki.
  Kinana akisaidia kutengeza batiki katika kijiji cha Mchukwi

  0 0

   Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti Majanga wa Benki ya Exim, Bw. David Lusala (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano kutangaza kuingia ubia na kampuni ya Hymans Robertson ya London ikishirikiana na  StraitsBridge Advisors (SBA) ya Singapore katika utoaji wa huduma kwenye masuala ya UdhibitI Majanga ijulikanayo kama Enterprise-Wide Risk Management (ERM). Wakishuhudia wa kwanza kulia ni Mwakilishi toka Hymans Robertson Bw. Maurice Kilavuka na Bw. Laurent Chauvet (wa kwanza kushoto).
   Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti Majanga wa Benki ya Exim, Bw. David Lusala (watatu kulia) akibadilishana hati na Mwakilishi toka Hymans Robertson Bw. Maurice Kilavuka (wapili kulia) wakati benki hiyo ilipoingia ubia na kampuni ya Hymans Robertson ya London ikishirikiana na  StraitsBridge Advisors (SBA) ya Singapore katika utoaji wa huduma kwenye masuala ya UdhibitI Majanga ijulikanayo kama Enterprise-Wide Risk Management (ERM). Wakishuhudia wa kwanza kulia ni Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu wa Ndani, Bw. Goerge Binde na Mwakilishi toka Hymans Robertson Bw. Laurent Chauvet (wa kwanza kushoto).
   Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti Majanga wa Benki ya Exim, Bw. David Lusala (kushoto) akibadilishana hati na Mwakilishi toka Hymans Robertson Bw. Maurice Kilavuka (kulia) wakati benki hiyo ilipoingia ubia na kampuni ya Hymans Robertson ya London ikishirikiana na  StraitsBridge Advisors (SBA) ya Singapore katika utoaji wa huduma kwenye masuala ya UdhibitI Majanga ijulikanayo kama Enterprise-Wide Risk Management (ERM)
  Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti Majanga wa Benki ya Exim, Bw. David Lusala (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano kutangaza kuingia ubia na kampuni ya Hymans Robertson ya London ikishirikiana na  StraitsBridge Advisors (SBA) ya Singapore katika utoaji wa huduma kwenye masuala ya UdhibitI Majanga ijulikanayo kama Enterprise-Wide Risk Management (ERM). Wakishuhudia wa kwanza kulia ni Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu wa Ndani, Bw. Goerge Binde, Mwakilishi toka Hymans Robertson Bw. Maurice Kilavuka (wapili kulia), Mkuu wa Kitengo cha Hazina wa Benki ya Exim, Bw. George Shumbusho (wakwanza kushoto) na Mwakilishi toka Hymans Robertson  Bw. Laurent Chauvet (wa kwanza kushoto)

  BENKI ya Exim Tanzania imeingia ubia na kampuni ya StraitsBridge Advisors (SBA) ya nchini Singapore, kampuni itoayo huduma za kifedha kwa ajili ya kutoa huduma ya kitaalam katika masuala ya udhibiti wa majanga ijulikanayo kama Enterprise – Wide Risk Management (ERM), itakayoiwezesha benki hiyo kuongeza ufanisi katika udhibiti wa majanga. 

  Akizungumza katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti Majanga wa Benki ya Exim, Bw. David Lusala alisema, ili Benki ya Exim iongeze ufanisi katika eneo la udhibiti wa majanga imesaini makubaliano na kampuni ya SBA ambayo itashirikiana na kampuni ya Hymans Robertson (H&R) ya London kuipa benki ujuzi mkubwa dhidi ya majanga inayokutanayo na kutumia fursa mbali mbali zinazojitokeza kibiashara.

  Alisema kuwa ikiwa inazaidi ya miaka 92 ya uzoefu katika utoaji huduma hizo, Hymans Robertson ikishirikiana na SBA itaisaidia benki kuongeza ufanisi wake katika eneo la udhibiti wa majanga yaani Enterprise-Wide Risk Management (ERM).

  “ERM inatoa muongozo katika masuala ya udhibiti wa majanga, ambayo moja kwa moja inahusisha matukio yanayoiusisha benki (majanga na fursa), kuyachunguza kwa kuyaangalia na kujua ukubwa wa athari zake na kufuatilia uendeleaji wake.

  “Kwa kutambua na kwa umakini kuangalia na kufanyia kazi majanga na fursa, muongozo bora wa ERM utailinda benki na kuwajengea thamani wamiliki, wafanyakazi, wateja na wadhibiti,” alisema Bw. Lusala.

  Alibainisha kuwa, mafanikio ya benki yoyote yanatokana na uwezo wa benki hiyo kuweza kufanya uwiano katika ya majanga yanayolandana na shughuli zake za kibiashara dhidi ya gharama za kudhibiti majanga mbali mbali.

  "Kwa hiyo,benki yetu inatarajiwakuutekeleza utaratibu huo wa ERM, ikiwa ni pamoja kuangalia maendeleo yake na utumiaji wa profaili ya benki ya majanga ili iweze kutuongoza katika ufanyaji wa maamuzi katika masuala yote ya kimkakati na yasiyokimakakati.

  "ERM itahakikisha kuwamatokeo yatokanayo na jitihada za benki hayapotei kwahasarazinazoweza epukika, au majanga," aliongeza.

  Kwa upande wake,Mwakilishi kutoka Hymans&Robertson (H&R) Bw. MauriceKilavukaalisema kampuni yake inafuraha kupata fursa ya kufanyakazi na Benki ya Eximkatikasafariyake ya kufikiaubora zaidi hususani katika masuala ya udhibiti wa majanga.

  "Tunayofuraha kubwa kupata fursa hii ya kufanyakazi na Benki ya Exim ikiwa katikasafariyake ya kufikiaubora zaidi hususani katika masuala ya udhibiti wa majanga. Ushirikiano huu unadhihirisha uelewa walionao Benki ya Eximjuu utaalamu unaopatikana toka kwa wataalam wa StraitsBridge&HymansRobertson. Tutafanya jitihada kubwa na kuiwezesha benki kuwa na mfumo bora duniani katika masuala ya udhibiti wa majanga yaani Enterprise Risk Management (ERM).

  StraitsBridgeAdvisorspamoja naHymansRobertson,imekuja mifumo mbali mbali madhubuti ya jinsi gani ya kudhibiti majanga ikiwa ni pamoja na majanga katika masoko, majanga katika mikopo, ALM, uwekaji bei katika utumaji fedha, Usimamizi na Upangaji wa Mtaji, na Usimamizi wa Fedha. Hii bila Bila ya shaka itakuwa ni nyenzo ya benki kuweza kujengamfumo madhubuti wa udhibiti majanga,” Bw. Kilavukaalisema.

  0 0

   Mkurugenzi wa Idara ya Habari- Maelezo, Bw Assah Mwambene akizungumza jambo wakati wa mkutano wa waandishi wa habari na Viongozi wa Mfuko wa Hifadhi wa Pensheni wa PSPF mapema leo katika Ukumbi wa JB Belmonte, Jijini Dar Es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa pensheni wa PSPF, Bw Adam Mayingu akizungumzia mafanikio ya mfuko wa PSPF katika kipindi cha Miaka 15 tokea kuanzishwa kwake katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo katika Ukumbi wa JB Belmonte Jijini Dar.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Mh Adam Mayingu (kushoto) akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari-Maelezo, Mh Assah Mwambene leo katika Mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo wakati Mkurugenzi mkuu wa PSPF alipokuwa akizungumzia mafanikio ya PSPF ndani ya miaka 15 tokea kuanzishwa Kwake.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF na wanahabari waliohudhuria mkutano kati ya Waandishi wa habari na Mfuko wa Pensheni wa PSPF uliolenga kuelezea mafanikio ya mfuko huo ndani ya Miaka 15 tokea kuanzishwa kwake.
  Mmoja wa Waandishi wa Habari akiuliza swali wakati wa Mkutano kati ya Mfuko wa Pensheni wa PSPF na waandishi wa habari uliofanyika leo Katika ukumbi wa JB Belmonte, Jijini Dar Es salaam, Mkutano huo ulilenga kueleza mafanikio yaliyopatikana kwa Kipindi cha Miaka 15 tokea kuanzishwa kwa mfuko huo wa PSPF.Picha na Josephat Lukaza - Lukaza Blog

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini usiku wa jana, Jumatatu, Septemba 15, 2014, kuanza ziara ya wiki mbili katika Marekani ambapo atahutubia Mkutano wa 69 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN General Assembly) New York.

  Mbali na kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Rais Kikwete pia atahudhuria mikutano muhimu katika mji mkuu wa Marekani, Washington, D.C.

  Mjini New York, Rais Kikwete atashiriki katika mikutano mikubwa zaidi ya 10 ikiwa ni pamoja na kuhutubia Baraza Kuu wakati wa Majadiliano ya Jumla ( General Debate) yaliyopangwa kufanyika Septemba 24 hadi 27 na Septemba 29 hadi Oktoba Mosi, mwaka huu, 2014.

  Rais Kikwete amepangwa kuwa kiongozi wa 12 duniani kuhutubia Baraza hilo mchana wa Alhamisi ijayo, Septemba 25, 2014. Mkutano wa 69 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa utaanza Septemba 16 hadi Desemba 24, mwaka huu, Miongoni mwa mikutano mingine muhimu ambayo Rais Kikwete atashiriki ni pamoja na kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) Kuhusu Mazingira (CAHOSC) na Mkutano wa Wakuu wa Nchi Kuhusu Mazingira ulioitishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Mheshimiwa Ban Ki Moon.

  Imetolewa na;
  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu – Dar es Salaam.
  16 Septemba , 2014.

  0 0

  Na Benedict Liwenga, MAELEZO-DSM.

  TEHAMA ni moja kati ya Sekta zinazokua kwa kasi hapa nchini na duniani kote na imekuwa ikichangia kikamilifu katika maendeleo ya Taifa na pia imekuwa ikiwezesha sekta nyingine kukua na kuboresha maisha ya wananchi na huduma za jamii kwa ujumla.
   
  Kutokana na ukuaji wa Sekta hii, jitihada za makusudi zinahitajika katika kusimamia na kuratibu shughuli za TEHAMA ili nchi iweze kunufaika zaidi kwani mchango wa sekta hiyo unaweza kuwa mkubwa kama TEHAMA na matumizi yake yataratibiwa, kusimamiwa na kuendelezwa vyema zaidi kuliko hali ilivyo sasa.
   
  Katika kuhakikisha masuala ya TEHAMA nchini yanaratibiwa, kusimamiwa na kuendelezwa vyema, Serikali iliona ni vema ikaundwa Tume ya TEHAMA (ICT Commission).
   
  Tarakilishi “Computer” katika lugha ya Kiswahili ni kifaa ambacho kimebadilisha mfumo wa maisha ya binadamu katika miongo takribani sita iliyopita.Kutokana na kuwepo kwa kifaa hiko dunia imejikuta katika maendeleo makubwa kabisa kuliko kipindi chochote kile katika historia ya kuwapo kwake. 
   
   Bila shaka kila mwanadamu katika dunia hii anafahamu ukuaji mkubwa na uwezo wa mawasiliano ambao umeleta mapinduzi makubwa katika ukuaji wa chumi za nchi na mwingiliano wa jamii moja kutoka jamii nyingine.
   
  Ni maendeleo haya ya kiteknolojia ambayo yamesababisha utandawazi ambao hakika umeifanya dunia kuonekana kama kijiji kidogo kilicho na jamii nyingi zenye taratibu, maendeleo, mila na desturi na siasa tofauti.
   
  Kwa kimombo Teknolojia ya Habari na Mawasiliano inafahamika kama Information Technology au IT kwa kifupi na Kwa Kiswahili teknolojia hiyo inafahamika kama TEKNOHAMA.
   
  TEHAMA duniani imeanza kupiga hatua ya kasi sana toka mwishoni mwa Karne ya ishirini na imeleta mabadiliko makubwa katika nyanja za mawasiliano, uchumi, tafiti na ukusanyaji wa takwimu mbalimbali.
   
  Pamoja na uwepo wa sheria ya 1974 iliyokuwa ikipinga uagizwaji wa vifaa vya tarakilishi zenyewe na seti za runinga, mfumo wa mabadiliko mbalimbali ndio uliopelekea Tanzania kupiga hatua ya kutosha katika kuboresha mfumo wa habari.
   
  Sera ya Taifa ya TEHAMA ya mwaka 2003 inaelekeza kuundwa kwa chombo cha TEHAMA ikiwemo juhudi na programu mbalimbali zinazoendelea hapa nchini zinazohitaji utaratibu wenye ufanisi.
   
  Jitihada za kuanzisha Tume zililenga kutekeleza Sera ya Taifa ya TEHAMA pamoja na maazimio mbalimbali ya kitaifa na kimataifa ikiwemo maagizo ya Mkutano wa Dunia wa Jamii Habari (World Summit on Information Society).
   
  Aidha, jitihada mbalimbali zimefanywa na Serikali katika kuhakikisha Sekta ya TEHAMA inakua nchini na miongoni mwa jitihada hizo ni pamoja na uanzishwaji wa vituo vya Mawasiliano vya Jamii (Community Telecentres), ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (National ICT Broadband Backbone-NICTBB), Uanzishwaji wa Wakala wa Serikali wa Mtandao, Uanzishwaji wa Vituo vya Kutunzia kumbukumbu za TEHAMA (Data centres), na Mradi wa Anwani za Makazi na Simbo za Posta.
   
  Tume hii inalenga kutambua na kuvutia fursa za uwekezaji katika TEHAMA, kutoa ushauri, kuendeleza rasilimali watu kitaifa kwenye sekta ya TEHAMA, kuendeleza program za kitaifa za TEHAMA na kushiriki katika kuendeleza miundombinu mbalimbali ya TEHAMA yenye sura ya kitaifa kwa kushirikisha wadau wa sekta zote.
   
  Kwa sasa, Idara za Serikali, Mashirika, na Asasi za aina zote zimejitahidi kuwa na tovuti zao, ili wananchi wapate habari za vyombo hivyo kupitia mtandao huo wa kompyuta.
   
  Serikali imeanzisha uhamasishaji na uendelezaji wa wataalam wa TEHAMA (ICT Professionals) katika taasisi za Serikali na sekta binafsi ili kujenga rasilimali watu nchini itakayowezesha kutumia fursa na rasilimali za TEHAMA vizuri na kwa manufaa zaidi.
  Kwa upande wa Serikali, Wizara kwa kushirikiana na wadau wengine wa TEHAMA imekamilisha Muundo wa Utumishi wa teknohama ambao tunaamini utatoa fursa mahsusi katika kuendeleza watumishi wa fani hiyo ambao ina jukumu kubwa sana katika maendeleo ya nchi yetu katika zama hizi za TEHAMA.
   
  Mafanikio katika jitihada hizo yamekabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kutokuwepo kwa chombo mahususi kinachoratibu, kusimamia na kuendeleza TEHAMA nchini.
   
  Ni dhahiri kuwa sekta ya Mawasiliano inakuwa kwa kasi kubwa sana duniani kote na hapa nchini kwetu, na hivyo kufanya baadhi ya mambo kuwa na changamoto katika utekelezaji wake hususan kutokuwepo na uratibu wa kitaifa katika miradi na program zenye sura ya kitaifa.
   
  Kukosekana kwa mpango wa Kitaifa wa usimamizi wa kuhakikisha kuwa mifumo ya TEHAMA inawasiliana na hatimaye kuepuka upotevu wa rasilimali unaotokana na taasisi mbalimbali kufanya kitu kile kile.
   
  Changamoto nyingine ni kutokuwapo na usimamizi, usajili wa kitaifa wa kuendeleza weledi kwa wataalamu wa TEHAMA na kuhakikisha utoshelevu wa rasilimali watu utakaokidhi mahitaji ya maendeleo ya TEHAMA, pia kutokuwepo chombo mahususi chenye majukumu ya kisheria.
   
  Tume ya Teknolojia, Habari na Mawasiliano itasaidia kukuza uchumi wa Taifa kutokana na kukua kwa sekta ya TEHAMA na kuchochea uzalishaji, ukuaji wa sekta zingine kiuchumi na usambazaji wa huduma za jamii; kuwa na taifa la jamii habari, lenye wataalam wanaotambulika kitaifa na Kimataifa, na wajasiriamali katika Nyanja mbalimbali za TEHAMA kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia duniani; kuwa na uhakika wa usalama katika matumizi ya TEHAMA na kuwepo na mfumo unaoainisha na kuendeleza uwekezaji katika sekta ya TEHAMA kitaifa.
   
  Tume hii inatarajia kuondoa changamoto nyingi na kujenga mfumo utakaowezesha uwekezaji wa kushirikisha sekta binafsi katika ujenzi wa miundombinu ya mawasiliano na TEHAMA yenye sura ya kitaifa; Kuwepo mfumo utakaowezesha wabunifu na wajasiriamali kuendeleza sekta ya TEHAMA; na kuweka utaratibu na miongozo ya namna bora ya kuhifadhi vifaa chakavu vya TEHAMA (e-waste management).
   
  “Miongoni mwa mambo muhimu na ya msingi katika kuratibu sekta ya TEHAMA nchini, tume ya TEHAMA inatakiwa ihakikishe inaunda Bodi ya Wataalamu wa TEHAMA ambao watasajiliwa na kufahamika kisheria ili kulinda weledi na maadili ya usambazaji na ubora wa huduma za TEHAMA zinazotolewa kwa jamii”, alisema Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mhe. January Makamba alisema
   
  Kwa namna hiyo, tume itakuwa imesaidia kuwa na Taifa Habari lenye wataalam waliounganishwa na chombo kimoja na hivyo basi kuongeza wigo na dhamana ya uwajibikaji kwa huduma zitolewazo kwa jamii.
   
  Mhe. Makamba aliongeza kuwa Tume ya Teknnolojia ya Habari na Mawasiliano pamoja na mambo mengine itatakiwa iendelee kuleta  mabadiliko na maboresho katika nyanja ya mawasiliano na habari kwa kuhakikisha inafuta na kuondoa uwepo wa vyuo visivyo na hadhi (feki) vinavyotoa elimu ya sayansi na teknolojia isiyokidhi viwango vinavyotakiwa katika kuboresha sekta ya TEHAMA.
   
  Tatizo la kuwepo na uanzishwaji wa vyuo vya masuala ya habari ambavyo kimsingi havina ubora na havifuati Sera ya Habari na Mawasiliano iliyoanzishwa 2003 na hivyo basi kutengeneza wataalamu wasioweza kuendana na kasi ya mabadiliko katika nyanja ya mawasiliano nchini.
   
  Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia ilikabidhiwa  dhamana ya kuhakikisha kwamba Teknolojia ya Habari  na Mawasiliano, Sayansi,  Teknolojia na Ubunifu vinachangia kikamilifu katika maendeleo ya nchi yetu.
   
  Pamoja na  jukumu hilo, Wizara hii imepewa dhamana ya kusimamia Taasisi, Mashirika, Tume na  Kampuni ambazo zinachangia juhudi za Wizara katika  kuyafikia malengo na matarajio ya  wananchi. Taasisi hizo ni: Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT); Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Mbeya (MIST),Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela - Arusha (NM-AIST); Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC); Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH); Shirika la Posta Tanzania (TPC); Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL); Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA); na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCAF).
   
  Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara hiyo, Serikali imeendelea kujenga Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, ujenzi ambao ulianza rasmi mwezi Februari 2009. Awamu ya Kwanza ya ujenzi wa mkongo wa mawasiliano imekamilika na huduma za mawasiliano zimeanza kutolewa. Katika awamu hii, jumla ya kilometa 4,300 za Mkongo katika Mikoa 16 zimejengwa. Mikoa hiyo ni: Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Iringa, Mbeya, Dodoma, Singida, Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga, Shinyanga, Mwanza, Tabora, Mara na Kagera.
   
  Taarifa zilisema kuwa, kabla ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kuwepo na kabla ya Mikongo ya Baharini kuunganishwa na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, gharama za simu kwa sekunde moja zilikuwa kati ya shilingi 2.50 na shilingi 3.00.  
  Aidha, gharama za mtandao wa intaneti zilikuwa shilingi 12,400,000 kwa kiwango cha sita (6) mega bits/sec dedicated internet bandwidth ambapo hivi sasa, gharama ya simu na matumizi ya mtandao zimepungua.
   
  Serikali kupitia wizara husika imekamilisha tathmini ya uanzishwaji wa Mtandao wa Elimu na Utafiti (National Education and Research Network-NREN) utakaounganisha vyuo vikuu na vituo vya utafiti 27 katika Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kupitia Mradi wa Sayansi Teknolojia na Elimu ya Juu unaofadhiliwa na Benki ya Dunia  katika jitihada za Serikali kupeleka huduma za mawasiliano hadi vijijini, Serikali imeanzisha Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCAF).
   
  Madhumuni ya Mfuko huu ni kusaidia juhudi za upelekaji mawasiliano ikiwa ni pamoja na kutoa ruzuku kwa wawekezaji watakaokuwa tayari kupeleka huduma za mawasiliano maeneo ya vijijini na baadhi ya maeneo ya mjini yasiyokuwa na mvuto kibiashara.
   
  Hadi sasa Mfuko umeainisha vijiji 239 katika mikoa 17 ambayo ni Dodoma, Arusha, Tanga, Morogoro, Pwani, Lindi, Ruvuma, Iringa, Mbeya, Singida, Tabora, Rukwa, Shinyanga, Kagera, Mara, Manyara na Kigoma (Kiambatisho Na.10). Aidha, vijiji 139 vimechaguliwa kwa ajili ya mradi wa majaribio (pilot project). Uhakiki wa maeneo mengine unaendelea.
   
  Mabadiliko na maboresho katika teknologia ya habari na mawasiliano Tanzania yametokana juhudi madhubuti zilizofanywa na serikali sambamba na hitaji na malengo ya millenium na Dira yake ni  kuhakikisha maisha bora kwa kila Mtanzania katika nyanja mbali mbali yanafikiwa ifikapo 2025.

  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi mkutano mkuu wa tatu wa Afrika kuhusu masuala ya usimamizi wakodi uliofanyika kwenye Hoteli ya Double Tree, jijini Dar es Salaam, leo Septemba 16, 2014.
  Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kufungua rasmi mkutano mkuu wa tatu wa Afrika kuhusu masuala ya usimamizi wakodi uliofanyika kwenye Hoteli ya Double Tree, jijini Dar es Salaam, leo Septemba 16, 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati) Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba (wa pili kulia) wakiwa meza kuu na baadhi ya viongozi wa TRA wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa tatu wa Afrika kuhusu masuala ya usimamizi wakodi uliofanyika kwenye Hoteli ya Double Tree, jijini Dar es Salaam, leo Septemba 16, 2014.
  Baadhi ya washiriki wa mkutano huo kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika, waliohudhuria mkutano huo, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo, uliofanyika kwenye Hoteli ya Double Tree, jijini Dar es Salaam, leo Septemba 16, 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa TRA, baada ya kufungua mkutano mkuu wa wa tatu wa Afrika kuhusu masuala ya usimamizi wakodi uliofanyika kwenye Hoteli ya Double Tree, jijini Dar es Salaam, leo Septemba 16, 2014. Picha na OMR

  0 0
 • 09/16/14--13:30: TBS KUAJIRI WATUMISHI 200
 •  

  Kaimu Mkurugenzi Udhibiti Ubora wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bi. Mary Meela akiwaeleza waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu Mikakati wanayoweka ya kuendelea kudhibiti ubora wa bidhaa nchini ikiwemo kuimarisha ukaguzi kwenye vituo vya mipakani mwa nchi,Kulia ni Afisa Habari Wa Idara ya Habari Bw. Frank Mvungi. 

  Afisa Uhusiano wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bi. Roida Andusamile akitoa wito kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuendelea kuelemisha umma kuhusu madhara ya matumizi ya nguo za mdani za mtumba. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Udhibiti Ubora wa Shirika hilo Bi. Mary Meela
  =======  ===== =====          
  Frank Mvungi-Maelezo
  Shirika la viwango Tanzania (TBS) linatarajia kuajiri watumishi 200 katika harakati za kuimarisha utendaji wa shirika hilo.
  Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa udhibiti ubora wa shirika hilo Bi Mary Meela wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
  Akifafanua Meela amesema watumishi watakaoajiriwa watasaidia kuimarisha utendaji kazi wa shirika hilo hasa katika kufanya ukaguzi na kuhakisha tatizo la bidhaa hafifu linapungua au kuondolewa kabisa.
  Aidha Bi. Meela alisema kuwa Shirika limeweza kuweka wakaguzi kwenye vituo 5 ambavyo ni Sirari, Namanga, Taveta, Horohoro, Bandari za Tanga na Dar es salaam na kuweka wakaguzi kwenye vituo vya bandari kavu (ICD).
  Akizungumzia kuhusu utumiaji wa nguo za ndani za Mtumba Bi. Meela amewataka watanzania kuwa mstari wa mbele kupinga matumizi ya nguo hizo kwani zina madhara kiafya kwa watumiaji na wataendelea kufanya ukaguzi wa nguo hizo na kuziteketeza pindi zinapopatikana.
  Shirika la viwango lilianzishwa kwa Sheria ya Bunge Na. 3 ya mwaka 1975, kasha kuundwa upya mwaka 2009 sheria ambayo imelipa shirika uwezo mkubwa zaidi wa utayarishaji viwango na kusimamia utekelezaji wake.

  0 0

  Suitable for both office and residential purposes
  ? Four (4) Total Bedroom(s)
  ? Twin master's bed room
  ? Independent balconies for the three up-per floor bed rooms
  ? Ample office space
  ? 2 sitting rooms
  ? Kitchen, Dining Room, Pantry, Store room, Study room
  ? Brick wall fencing, metal sliding gate
  ? Plot area 1448 square meters

  The property has a potential to be easily transformed into hotel / hostel / school.

  The house is 150m from the Indian ocean / beach the area is well developed with supermarkets and entertainment centers, restaurants, clubs, hotels etc.

  Please call 0713 274 535 for further information


  0 0

   Mkurugenzi wa Angels Moments inayoendesha Kampeni ya Mwanamke na Uchumi, Naima Malima akitoa hotuba ya ufunguzi wa kampeni hiyo iliyofanyika mkoani mwanza hivi karibuni. Kampeni hiyo yenye lengo la kuwawezesha kiuchumi wanawake wajasiriamali ambapo kampeni hiyo itafanyika mkoani Tanga Mwezi Oktoba. Picha na Angels Moments.
   Mshairi maarufu bibi sauda akitoa burudani ya mashairi yake adhimu kwa lugha ya kufurahisha na burudani kwa wanawake wajasiliamali katika kampeni ya mwanamke na uchumi jijini mwanza.
   Mkuu wa Wilaya ya Ilemela ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Kampeni ya Mwanamke na Uchumi iliyofanyika Mwanza, Mh. Amina Masenza akifurahia mashairi ya Bi. Sauda (hayupo pichani) katika kughani mashairi yake kwa lugha ya kiswahili.
  Mtoa mada maarufu Emiliani Busara akitoa mada na kufundisha biashara bora kwa wajasiliamali jijini mwanza katika kampeni ya mwanamke na uchumi zilizofanyika jijini mwanza hivi karibuni.
   Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mh. Amina Masenza akihutubia wanawake wajasiliamali katika ufunguzi wa semina za kampeni ya mwanamke na uchumi jijini mwanza hivi karibuni.
  mjasiliamali mwenye ulemavu wa macho akiuliza swali kutoka kwa watoa mada katika kampeni ya mwanamke na uchumi mkoani mwanza.
  Mkuu wa Wilaya ya ilemela Mh: Amina Masenza  bidhaa za wajasiliamali katika moja ya mabanda ya wanawake
  walioshiriki katika kampeni ya mwanamke na uchumi katika viwanja vya magomeni kirumba jijini mwanza.
  Huduma za upimaji Afya zilitolewa  kwenye kampeni ya mwanamke na uchumi inayotolewa na kampuni ya Angels Moments jijini mwanza hivi karibuni.
  Balozi wa kampeni ya mwanamke na uchumi, Linah Sanga akitoa burudani katika ufunguzi wa kampeni ya mwanamke na uchumi mkoani mwanza.
  Picha ya pamoja.   Baada ya kutoa  elimu juu ya mafanikio na ujuzi wa biashara na ujasiriamali kwa wanawake wajasiriamali mkoani Mwanza, kampeni ya mwanamke na uchumi inahamia mkoani Tanga ambapo wanawake na vijana zaidi ya 600 wanategemea kupata elimu ya msingi juu ya ujasiliamali na fursa zilizopo na nidhamu ya matumizi katika kuhifadhi fedha na mikopo.  “Sasa tunahamia mkoa wa Tanga ambapo sasa mafanikio ya kampeni ya mwanamke na uchumi tunayapeleka kwa wanawake wajasiliamali na vijana ambapo pamoja na mambo mengine,tumefanya tathimini ya mkoa wa Mwanza imeonesha mafanikio makubwa kwani mrejesho ni mkubwa na hamasa ni ya kutosha ambapo wajasiriamali wanatuomba turudi tena, na hili ni jambo la kutia moyo”Anasema Naima Malima Mkurugenzi wa Angels Moment waratibu wa kampeni ya mwanamke na uchumi kwa wanawake wajasiriamali nchini.  “Unajua mkoa wa Tanga unafursa nyingi sana,na jambo la kufurahisha ni kwamba viongozi wengi wa mkoa huu ni wanawake kama mimi, ukianzia mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya wote ni wanawake na wanajitahidi kuhakikisha wajasiliamali wanasonga mbele ambapo pamoja na mambo mengine masuala haya yatajadiliwa na kufundishwa na wataalamu na watoa mada hivyo elimu ya ujasiliamali na fursa zilizopo, usimamizi binafsi wa fedha na uwekaji akiba, afya bora na uchumi kwa akina mama na mwisho ni mwanamke na rslimali ardhi tunategemea mada hizi zitafundishwa kwa usitaadi wa hali ya juu na wakufunzi wetu” anasisitiza Mkurugenzi huyo.


  Kampeni ya mwanamke na uchumi mkoani Tanga inatazamiwa kuhudhuliwa na wawezeshaji na wakufunzi maarufu kama ndugu Emiliani Busara na Bi. Tabu Likoko kutoka taasisi ya WAMA ya jijini Dar es Salaam. Elimu sahihi juu ya mada tajwa hapo juu zitatolewa ambapo wanawake wajasiriamali kutoka wilaya za Tanga, Muheza, Mkinga na Pangani zitashiriki.

  Kampeni hii ni ya pili kufanyika katika mkoa wa Tanga,baada ya awali kufanyika mkoani Mwanza ambapo itapambwa na Balozi wa kampeni ya mwanamke na uchumi Mwanamziki LINAH SANGA ambaye ataburudisha na kutoa elimu kupitia mziki wake na wimbo maalumu wa kampeni ya mwanamke na uchumi ambapo imepanga kufanyika terehe 10 na 11 mwezi ujao jijini Tanga.

  0 0  0 0

   Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba toka Kamati namba Tano, Mhe. Dkt. Asha-Rose Migiro akisoma taarifa wakati wa mjadala wa jioni bungeni hapo jana 15 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
  =======   =======   ========
  HOJA ya kusitisha Bunge Maalum la Katiba imehitimishwa rasmi Kisheria kwa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutamka kwamba bunge hilo linaweza kuendelea na shughuli zake.
   
  Taarifa hiyo imetolewa jana 15 Septemba, 2014 na Mjumbe wa Kamati namba Tano, Mhe. Dkt. Asha-Rose-Migiro wakati wa mjadala wa jioni bungeni hapo.
   
  Akisoma taarifa hiyo, Dkt. Migiro amesema kuwa mjadala wa kusitisha bunge umefungwa rasmi hapo jana licha ya kuwepo kwa madai kuwa bunge hilo halina uhalali wa kisiasa.
   
  “Kwaajili ya kuondoa shaka yoyote ningependa kuwaambieni takwimu tulizonazo hivi sasa, bunge hili lina jumla ya Wajumbe 630, kati ya hao waliotoka ni wajumbe 130 ambao ni sawa na asilimia 21% tu ya wajumbe wote, wajumbe waliobaki ndani ya bunge ni 500 hii ni sawa na asilimia 79% ya wajumbe wote na tukizichambua takwimu hizi, ningeomba kutambua wingi wa Kundi la 201”, alisema Dkt. Migiro.
   
  Akikanusha juu ya kuwepo kwa dhana iliyojitokeza ya kwamba wajumbe waliobaki ndani ya bunge hilo ni wa aina moja, Dkt. Migiro alisema kuwa taarifa hizo si za kweli, kwani kati ya wajumbe 500 walioko ndani ya bunge hilo wajumbe wanaotokana na kundi la 201 ni wajumbe 189 ambapo wajumbe wanaotoka Tanzania bara jumla yao ni 348 na kati ya hao, 125 ni wajumbe wanaotoka katika kundi hilo la 201.
   
  “Ukitazama takwimu hizi kwa jicho lolote lile basi wajumbe wa 201 ni sehemu kubwa na ni sehemu muhimu ya wajumbe hawa waliobaki”, alisema Dkt. Migiro.
   
  Akizungumzia juu ya wajumbe toka upande wa Zanzibar, Dkt. Migiro alisema kuwa wajumbe waliobaki ni 152 na kati ya hao wajumbe 64 wanatokana na kundi la 201.
   
  “Tunasisitiza takwimu hizi kwa wajumbe wa 201 kwasababu wajumbe hawa ndiyo wajumbe ambao kwa wingi wao kitakwimu lakini pia kwa wingi wao kimakundi wanawakilisha sura zote Kitaifa, hivyo ni dhairi kwamba kwa namna yoyote ile waliobaki ndani ni wengi, ni idadi kubwa, ni idadi wakilishi na tukiangalia kwa takwimu hizi, wajumbe walioamua kususia bunge kwa pande zote mbili hizi hawafikii hata theluthi moja ya wajumbe waliobaki”, alisisitiza Dkt. Migiro.
   
  Kwa kuzingatia matakwa ya kisheria, Dkt. Migiro alieleza kwamba uamuzi upatikane kwa maridhiano, kwa majadiliano na kwa kushawishiana kwa hoja wajumbe waliobaki na walio wengi wanaweza wakatumia wingi wao na wana uhalali wa kisiasa na wa kisheria.
   
  Dkt. Migiro aliendelea kusema kuwa, wajumbe waliotoka hawakuona kuwa utaratibu huo ungekuwa na manufaa kwao licha ya kuwepo na maridhiano katika bunge hilo, pia kupitia wadau mbalimbali Vyama vya siasa vyote vimekuwa vinazungumza nje ya bunge kupitia Msajili wa Vyama vya siasa, kupitia Kituo cha Demokrasia (TCD) na kupitia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
   

  0 0
 • 09/16/14--22:28: SIGOMBEI URAIS 2015 NKAMIA
 • GEDSC DIGITAL CAMERA
  Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia ambaye pia ni   Mbunge wa Kondoa Kusini ,akiongea na waandishi wa habari leo  jijini Arusha katika studio za redio 5 zenye makao yake makuu njiro ambapo alisema kuwa hana mpango wowote wakugombea nafasi ya Urais 2015
  GEDSC DIGITAL CAMERA
  Baadhi ya waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwa wanafanya mahojiano na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia leo jijini Arusha katika studio za redio 5 
  GEDSC DIGITAL CAMERA
  Mkurugenzi wa Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha  Bw Robert Francis akiwa anamsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia wakati akizungumza na waandishi wa habari kulia ni mwandishi wa chanel Ten Jamilah Omary.
  GEDSC DIGITAL CAMERA
  Mtangazaji wa redio 5 Mwangaza Jumanne akifanya mahojiano live na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia.
  GEDSC DIGITAL CAMERA
  Kulia Mwanaisha Suleiman akiwa anafanya yake ndani ya studio za redio 5 mara baada Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia alipofanya ziara kituoni hapo
  GEDSC DIGITAL CAMERA
  Muonekano wa studio ya Redio 5 wakati Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia akifanyiwa mahojiano hewani na mtangazaji wa kituo hicho Mwangaza Jumanne
  GEDSC DIGITAL CAMERA
  Meneja masoko wa Tan Communication media Bi.Sarah Keiya akiwa anasalimiana na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia 
  GEDSC DIGITAL CAMERA
  Mkurugenzi  wa Radio 5  Bw Robert Francis akiwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia ofisini kwake mda mfupi kabla ya kuingia studio za redio hiyo
  GEDSC DIGITAL CAMERA
  GEDSC DIGITAL CAMERA
  Katibu wa waziri Juma Nkamia Bw.Francis Songoro
  GEDSC DIGITAL CAMERA
  Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia akiongea na baadhi ya uongozi wa kituo hicho ambapo aliwapongeza kwa kazi nzuri ya utangazaji katika kuburudisha na hata kuelimisha jamii kupitia vipindi vyao mbalimbali
  GEDSC DIGITAL CAMERA
  Meneja mbunifu wa redio 5 Vicky Mwokoyo wakiwa wanabadilishana mawazo na mtangazaji wa kituo cha Redio 5 Ashura Mohamed
  GEDSC DIGITAL CAMERA
  John Mhala wa gazeti la Habari leo akiwa na mwandishi mwenzake wa mwananchi Happy Lazaro wakiwa wanabadilishana mawazo ndani ya jengo la Redio 
  GEDSC DIGITAL CAMERA
  Waandishi wa habari pamoja na mkurugenzi wa kituo cha redio 5 Bw.Robert Francis  katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia,kulia ni mmiliki wa mtandao wa Jamiiblog Pamela Mollel.
   
  Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia ambaye pia ni , Mbunge wa Kondoa Kusini amesema kuwa hana mpango wowote wa kugombea nafasi ya urais 2015 kama viongozi wengine wanavyotangaza nia huku akidai kuwa kazi yake kubwa nikuhakikisha wananchi katika jimbo lake wanapata maendeleo kupitia nafasi yake ya  ubunge.
   
  Waziri Nkamia aliyasema hayo leo mara baada ya kufanya ziara fupi katika kampuni ya Tan Communication Media inayomiliki kituo cha Redio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha,ambapo alisema kuwa hajawa na ndoto ya kuwa Rais 2015.Alisema kuwa kiongozi anayestahili kuwa rais ni lazima awe na uwezo wa kuongoza na anayekubalika na watanzania na vigezo isiwe umri wa mtu.
   
  ''Pamoja na umri nilionao 42 sina mpango wowote wa kugombea nafasi ya Urais 2015 na umri usiwe kigezo cha kugombea uwezo wa kiongozi ni muhimu sana''alisema Nkamia.
   
  Pia Waziri huyo aliipongeza kituo hicho cha redio kwa kazi nzuri ya kuburudisha na kuelimisha jamii kupitianvipindi vyake mbalimbali huku akiwataka kuandaa vipindi ambavyo vitawashirikisha wachezaji wazamani hali itakayosaidia kukuza na kuibua changamoto katika michezo(Habari Picha Pamala Mollel)

  0 0

  WALE MABINGWA WA COSMETICS ZA UKWELI KUTOKA USA, @AK CLASSIC COSMETICS SAFARI HII WAMEKULETEA BIDHAA ULIZOKUWA UNAZIMISS KUZIPATA HAPA BONGO.JAMANI NGOZI ZETU KWA SABABU MBALI MBALI ZIMEKUWA ZIKIBADILIKA IWE NI UJAUZITO= MARA MIWANI>,MARA NGOZI INAFUBAAA!!>HUKU MWILI MZIMA UKITOKWA NA MICHIRIZI!!>HUKU TUMBO LINAGOMA KURUDI!! SASA UNAHANGAIKA UMESHATUMIA VITU KIBAO BILA SULUHISHO!!HAYA MATATIZO HAYAWAHUSU WALIOJIFUNGUA PEKE YAO TUKO WENGI....

  EM TUPITIE HAPA ..
  KWA MAELEZO YA KINA KWA KILA BIDHAA NA TATIZO HUSIKA NA PICHA ZAIDI WATEMBELEE BLOGUNI
  www.akclassic.blogspot.com
   KUWEKA ODA NA KUFIKISHIWA BIDHAA MPAKA ULIPO PIGA  0753-482909/0713-468393.
  WAPO KINONDONI KWA MANYANYA NA SINZA KUMEKUCHA.

  Pata uhondo wao insta@ak_classic_cosmetics.
   KATI YA BIDHAA CHACHE SANA ZA NWELE AMBAZO UKIZITUMIA..LAZIMA USEME WOW!!YAANI HUTOJUTA HATA KIDOGO!!CANTU HUYU BWANA SIJUI NIMSEMEJE ILA UKITAKA UNYWELE USIMAME FULL KUNG"AA HUYU NDIEE,T444Z HII HABARE YA MUJINI KILA MTU ANAMJUA.SASA HUYU JAMAICAN BLACK CASTRO OIL NADHANI NDIO ANAKUJA KUFUNIKA OMG..YEYE ANAENDA DEEP MPAKA KUKUZA KOPE NA NYUSI...DAH EM NJOO #AKCLASSIC HARAKA UNAPITWA UJUE!!

   HIZI CHIPS MAYAI BALAA SANA..YAANI VITAMBO DAH!ANYWAY CORSET ITAKUSAIDIA KURUDISHA TUMBO KADRI UNAVOIVAA NDIVYO LINAVYORUDI..AS LNAKUKUWA INAKUSAIDIA KUCONTROL CHAKULA NA VITU KAMA IVYO..AYA SASA NI WAKATI WA KURUDISHA MVUTO WAKO!!WALE TULIOTOKA KUJIFUNGUA HAO HATA NISIPOSEMA NYIE NDIO NO. 1 WAHANGA!!SIZE ZOTE ZIPO!!
   NANI ASIYEJUA BALAA LA CARROT KWENYE SUALA ZIMA LA NGOZI!!WENGI HUWA TUNATUMIA VITU NUSU NUSU...YAANI UNAKUTA UNA LOTION TU AMA SABUNI TU!!NI SAWA ILA KAMA UNATAKA KUPATA MATOKEO MAZURI SHURTI UPATE SET!!NDIO MAANA UNAKUTA MTU ANANG'AA SAWA LAKINI NGOZI NGUMUUUU!!UKIIPIGA MBAO RANGI MBAO BILA KUANZA NA MSASA UNATEGEMEA NINI?NADHANI IMEELEWEKA UMUHIMU WA KUWA NA SABUNI,SERUM,CREME NA LOTION!!HATA RANGI YA CHUNGWA HIYO!
   MAMA MIO HII NI KIBOKO YA MICHIRIZI!HASA HASA  MICHIRIZI AMBAYO HAIJAKAA MUDA MREFU NA HASA ILE YA UZAZI....IMETHIBIKA KUFANYA KAZI KWA KIWANGO CHA HALI YA JUU..WATU WENGI WALIOTUMIA MAMA MIO WAMEZIKUBALI.. ZITUMIE KWA PAMOJA AMA KWA HAKIKA HUTOJUTA!! ..NAJUA MPO WENGI MLIOKATA TAMAA LAKINI KWA HII ITARUDISHA SMILE LENU!!NJOO DUKANI UPATE VITU TOFAUTI UTAKUBALI!!
   KUNA WAKATI UNATUMIA CREME INAFANYA VIZURI LAKINI KUNA SEHEMU ZINAGOMA,MARA NGOZI INAUNGUA,MARA MIWANI,MARA SHINGO NYEUSI,MARA KWAPA JEUSI WALE MLIOTOKA KUJIFUNGUA MNANIELEWA ZAIDI KUHUSU HII!!LAKINI HATA SIE WENGINE...SASA HII IMEKUJA KUFUTA VILIO VYETU!!HII KITU IKO SET KAMILI UKIJA DUKANI TUTAKUELEZEA JINSI GANI UTAFANYA!!

  0 0

  Aliyekuwa miss Kigamboni mwaka 2013, Miss Magdalena Olotu amepata nafasi ya kuipeperusha bendera ya Tanzania katika anga za kimataifa, baada ya kuchaguliwa kwenye shindano la umtafuta Super modal wa  Afrika shindano hilo linaitwa "Next Africa Supermodel Ultimate Search 2014" litakalofanyika Afrika ya Kusini. Shindano hili linawashilikisha wanamitindo mbalimbali kutoka nchi nne za Afrika.

  Sasa unaweza kumpigia kura yako kwa Kulike na Kucomment kwenye picha yake iliyoko kwenye ukurasa wa facebook uitwao "Supermodel Search Africa" au bofya ili jina lake MAGDALENA OLOTU ili kumpigia kura.

  WATANZANIA TUONYESHE UZALENDO KWA KUMPIGIA KURA SASA

  0 0

   Umati wa wananchi wa Mafia wakimsikiliza mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akiwahutubia wananchi hao.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa wilaya ya Mafia ambapo aliwataka Viongozi wa CCM waache mkorogano badala yake wafanye shughuli za maendeleo kwanza.

   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mafia kwenye uwanja wa Mkunguni stendi ya Mabasi mjini Mafia.
  Naibu Waziri Nishati Charles Kitwanga akihutubia wakazi wa Mafia ambapo aliwaambia Mafia ndio wilaya pekee itakayopata Umeme kwa asilimia 100%.

  0 0

   Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mbulu Joseph Geheri akikata  utepe wakati wa uzinduzi wa Mnara wa  huduma za Mawasiliano  katika kijiji cha Aicho wilayani Mbulu Mkoani Manyara ambapo sasa wakazi wa kijiji hicho na jijini vya jirani wameunganishwa na huduma za simu za  mkononi za Airtel. Akishuhudia ni Meneja Mauzo wa Airtel Kanda ya Kaskazini Brightone Majwala   pamoja na wakazi wa Kijiji  hicho
  Meneja Mauzo wa Airtel Kanda ya Kaskazini Brightone Majwala  akiwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mbulu Joseph Geheri wakati wa uzinduzi wa Mnara wa  huduma za Mawasiliano  katika kijiji cha Aicho
  wilayani Mbulu Mkoani Manyara. Pichani ni wakazi wa Kijiji  hicho

  Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel imewawezesha wakazi wa kijiji cha
  Aicho  na vijiji vya jirani kupata huduma za mawasiliano kufatia
  uzinduzi wa mnara wa mawasiliano katika kijiji cha Aicho kata ya
  Marang wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara

  Uzinduzi huo ni mwendelezo wa dhamira ya Airtel katika kuboresha
  upatikanaji wa mawasiliano na kuwawezesha wakazi wa maeneo ya
  pembezoni mwa nchi kupata huduma ya mawasiliano ya simu za Mkononi

  Akiongea wakati wa uzinduzi uliofanyika mkoani Manyara Meneja Mauzo
  kanda ya kaskazini wa Airtel Bwana Brighton Majwala alisema “ Airtel
  Tunatambua kuwa mawasiliano ni kichocheo kikuu cha uchumi katika
  nchini na jamiii yoyote ile, ndio maaana tumeona ni vyema kufikisha
  mawasiliano katika maeneo yenye changamoto za mawasiliano hususani ya
  vijijini. Na leo tunazindua huduma za mawasiliano katika kijiji  cha
  Aiko na kuwawezesha wakazi wa hapa na maeneo ya jirani kupata huduma
  mbalimbali ikiwemo za kifedha za kutuma na kupokea pesa, kufanya
  malipo kwa njia rahisi, salama wakiwa  mahali popote  kwa kupitia
  huduma ya Airtel Money”.

  “Airtel tumejipanga na tutaendelea kutekeleza  dhamira yetu ya kutoa
  huduma bora za kibunifu na za bei nafuu na huku tukiendelea kuboresha
  upatikanaji wa mawasiliano katika maeno mbalimbali ya pembezoni
  nchini”  aliongeza Majwala

  Kwa upande wake mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya
  Mbulu Joseph Geheri alisema” Tunashukuru sana Airtel kwa kuendelea
  kuboresha mawasiliano na kuwapa vijana wetu kufaidika na kupata Ajira
  kwa kupitia huduma hizi zilizosheheni hapa wilayani Mbulu.Kadhalika
  mawasiliano haya yamewawezesha wanafunzi kupata taarifa za matokeo yao  ya mtihani ya kuhitimu kwa kupitia simu za mkononi mahali popote pale  walipo.

  Vilevile tunafurahi kuona jinsi gani Airtel imerahisha mawasiliano
  haya kijiji hapa na kuwezesha upatikanaji wa taarifa muhimu kwa wakati
  na kirahisi zaidi, kwa wafanyabiashara,  wakulima pamoja na wafugaji
  mawasiliano haya yatawawezesha kuendesha shughuli zao za kiuchumi kwa
  ufanisi zaidi na kupata masoko katika sehemu mbalimbali za nchi
  kupitia mtandao huu wa simu za mkononi wa Airtel.  Nachukua nafasi hii
  kuwaasa wakazi wa hapa kuyatumia mawasiliano haya kwa faida ya
  maendeleo yao na ya jamii kwa ujumla Aliongeza Geheri

  Airtel inaendelea kupanua wigo  wa mawasilano nchini ambapo wiki
  zilizopita Airtel ilizindua mnara wa mawasiliano katika mkoa wa
  Sigunga Kigoma na Muhukuru  Songea , huku ikiwa na  mpango mkakati wa
  kuzindua huduma za mawasiliano katika maeneo mengi zaidi nchini. Sasa
  wakazi wa sigunga, Mahukuru na Aicho wanafurahia huduma mbalimbali za
  Airtel ikiwemo ya kifedha ya Airtel Money Hatoki Mtu hapa, Switch on
  huduma ya internet  na  vifurushi vya Airtel yatosha na vingine vingi.


  0 0   Aunty akitia saini kitabu cha wageni alipotembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani siku ya Jumanne Sept 16, 2014.
   Aunty Ezekiel akipata picha ndani ya mjengo wa Ubalozi wa Tanzania Washington, DC
   Aunty akipata picha nje ya mjengo wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
   Aunty na Cassim Mganga wakipata menu ndani ya jiji la Washington, DC
   Cassim Mganga akipata picha nje ya mjengo mweupe wa Obama
   Aunty Ezekiel akipata picha nje ya mjengo wa Obama
   Shabiki akipata picha na wasanii Aunty na Cassim Mganga
    Shabiki akipata picha na wasanii Aunty na Cassim Mganga
    Shabiki akipata picha na wasanii Aunty na Cassim Mganga


  0 0

      Mwanafunzi wa Chuo kikuu huria cha Tanzania Bw. Mussa Omari (katikati) akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu tamko la kulaani kauli za mwenyekiti wa chadema taifa za kuhamasisha uasi kwa njia ya maandamano, wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
   Mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Bw. Gulatone Masiga akitoa wito kwa wananchi kuudumisha muungano wetu na kuacha kupelekwa na wanasiasa wasio na misingi ya kidemokrasia.Kulia ni Mwanafunzi wa Chuo kikuu huria cha Tanzania Bw. Mussa Omari.
    Mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Theodora Malata akiwaeleza jambo waandishi wa habari leo wakati wa Mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.
   
  =======  =======  ========
     UMOJA WA VIJANA WAZALENDO WA VYUO VYA ELIMU YA JUU DAR ES SALAAM

  TAMKO LA KULAANI KAULI ZA MWENYEKITI WA CHADEMA TAIFA ZA KUHAMASISHA UASI KWA NJIA YA MAANDAMANO.

  Sisi ni vijana  wasomi wazalendo  kutoka vyuo vikuu mbalimbali vilivyoko Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM); Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU); Dar es Salaam University College of Education (DUCE); USTAWI WA JAMII; Chuo Kikuu cha Mtakatifu John (St. John); Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM); Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT); Kampala International University (KIU); Dar es Salaam Institute of Technology (DIT); Institute of Adult Education (IAE); Tanzania School of Journalism (TSJ); College of Business Education (CBE), Chuo cha Uhasibu (TIA) na Chuo cha kumbukumbu ya Mwl JK Nyerere. 

  Tunachukua fursa hii  kulaani vikali kauli zilizotolewa na Mh. Freeman Mbowe ambae ni Mwenyekiti wa CHADEMA ya kutaka kuitisha maandamano ya nchi nzima bila kikomo pamoja na kuhamasisha asasi nyingine za kiraia kufanya na kuratibu maandamano kama hayo ya CHADEMA kwa ajili tu ya kupinga kuendelea kwa Bunge Maalumu la Katiba. 

  Tunawaambia watanzania wenzetu kuwa tumekerwa na kusononeshwa sana na kauli ya kibabe ya kiongozi huyu wa CHADEMA ya kuhamasisha vurugu ambazo tumezishuhudia zikisambaratisha umoja wa nchi nyingi na kuwa chanzo cha vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo huwa haviishi  na hatimaye kuendelea kulipakazia Bara la Afrika kuwa halijastaarabika na siasa za kidemokrasia. Tulimsikia akiahidi maandamano bila kikomo kwa kibali cha polisi au bila kibali cha polisi mbele ya wajumbe ambao wengine sio watanzania. Ndugu watanzania wenzetu, kauli kama hii haiwezi kusemwa hata na Rais yeyote ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu anaeongoza kwa kufuata misingi ya sheria na utawala bora, je Mh. Mbowe anapata wapi uhalali na ujasiri huo?

   Maana Rais na Amiri Jeshi Mkuu ambae ni dikteta anaweza kusema lakini yule anaetawala kwa misingi ya sheria, katiba na utawala bora kamwe hawezi kusema kauli kama hizo. Maneno aliyoyasema Mh. Mbowe amejivalisha madaraka zaidi hata ya yale ya Rais wetu ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama. Lakini kwa mtazamo wetu ni kuwa Mh. Mbowe amejivalisha UDIKTETA ambao unatakiwa kulaaniwa na kila mtanzania aliyeko ndani na nje ya nchi hii. Uzito wa kauli zake haubebeki na mtu yeyote kwenye taifa hili. Hatuna shaka kuwa ametoa kauli mbaya sana kuliko zote za kisiasa ambazo zimewahi kusemwa majukwaani. 

  Watanzania kwa ujumla wetu na makundi yetu tukikaa kimya bila ya kuzilaani na kuzikemea vikali kauli zake, tutakuwa hatujitendei haki sisi wenyewe na pia hatutavitendea haki vizazi vijavyo vya nchi yetu. 

  Ndugu zetu watanzania, kama ambavyo yeye mwenyewe alisema kabla ya kutoa amri kwa watu kuandamana kuwa anaamini watanzania wapo tayari kufanya mageuzi ili chama chake kingie IKULU ya Magogoni. Hayo yatafanikiwa endapo tu vijana wataacha uoga, maneno ambayo yanaashiria kutaka kuchukua uongozi kwa nguvu bila kufuata misingi ya kidemokrasia inayosimamiwa na serikali iliyo madarakani.   

  Sisi umoja wa vijana wazalendo wa vyuo vya elimu ya juu Dar es Salaam tunasema kuwa uzito na ubaya wa kauli hizi unaonesha wazi kuwa Mh. Freeman Mbowe hafai kupewa dhamana ya kuwa Rais wa nchi na Amiri Jeshi Mkuu wa vikosi vya ulinzi na usalama na pia amedhihirisha kuwa CHADEMA haina sifa ya kuiongoza nchi hii kwa sasa kwa kufuata misingi ya demokrasia na kudumisha amani, utulivu na mshikamano wa watanzania kwa lengo la kudumisha umoja, na muungano wetu.Tunaomba watanzania mkumbuke na mtilie maanani kuwa, Mh. Freeman Mbowe katoa kauli hizi akiwa raia tu wa kawaida. 

  Je itakuwaje akiwa Rais wa nchi na Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vyetu vya Ulinzi na Usalama wa nchi hii?  Kwa maoni yetu ni kuwa kwa upeo na mtazamo wa akili yake hakuna atakaebaki salama ndani ya nchi hii kwa kuwa atatuingiza kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe na pia atatuingiza kwenye vita na nchi majirani. Hafai, hafai, hafai hata mara moja kuwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu. Ndugu watanzaia, hivi ni mtu gani anaeweza kuishi kwa amani na viongozi kama Mbowe na wenzake wanaotumia ubabe kwenye maisha ya kawaida ya kila siku?

   Na hapa ndipo wanatuthibitishia kuwa Mh. Freeman Mbowe na Kikundi cha viongozi wa chama chake wote karibu wameshindwa kuzichunga na kuziweka pamoja familia zao na hatimaye zimesambaratika kwa ubabe huo huo, hivyo hawataweza kutuongoza na kutuweka pamoja watanzania ili tuishi kwa amani.

  Ndugu watanzania wenzetu tumebaini kuwa Mh. Freeman Mbowe na viongozi wenzake wa CHADEMA wanatumia maandamano na damu za watanzania kutafuta fedha kwa wafadhili wao ambao hawaitakii mema nchi yetu. Wakiaandaa maandamano, wanapiga picha na kuwapelekea wafadhili wao,  wanapata fedha, wanajenga majumba na kununua magari ya kifahari na kusafiri ulaya, marekani na familia zisizo rasmi kwa kujificha kwenye pazia la DEMOKRASIA huku watanzania wakiendelea kuathirika na maandamano. Hapo ndugu watanzania hakuna DEMOKRASIA bali tunaona DOMO-KRASIA na BONGO-KRASIA, yaani  wanatumia ulimi na akili ndogo za kitoto kujinufaisha na familia zisizo rasmi kwa siasa za ulaghai, ghilba, fitina, majungu, choyo, chuki, usanii wa kisiasa na uhaini alioutangaza Mh. Mbowe.

  Ndugu zetu watanzania, fahamuni kuwa Mh. Freeman Mbowe, Dk. Wilbroad Slaa, Tundu Lissu, Godless Lema, Mchungaji Peter Msigwa, Hezekiah Wenje na wengine wana familia. Swali je mmeshawahi kuwaona wake, watoto, na ndugu zao wa karibu kwenye maandamano yoyote yale waliyowahi kuyaandaa? Siku zote huwaambia watu wao hao bakini majumbani mtadhurika. 

  Pale damu za watanzania zinapomwagika kwenye maandamano baadae huwa wanajifungia na kushangilia ushindi mkubwa wa kuvuna mabilioni ya fedha za kigeni, kwa kuwa huwa wanapiga  picha matukio hayo na kwenda kuonesha wafadhili wao kwa taswira kwamba demokrasia inanyanyaswa. Wanakinga mabilioni ya fedha za kigeni wanatia kwenye akaunti zao, wanagawana, na mambo yao yanaenda sawasawa, huku watanzania wengine wakiwa wana vilio vya kupoteza ndugu na baba zao, waume, wake, wapenzi/wachumba, na watoto wao na kadhalika. Swali kwa nini hawaoni umuhimu wa kujali utu, ubinadamu na uhai wa watanzania wengine? 

  Sisi umoja wa vijana wazalendo wa vyuo vya elimu ya juu Dar es Salaam tunapenda kuwahakikishia kuwa thamani ya maisha ya watanzania wote au hata kwa mtanzania mmoja ni kubwa sana kuliko hiyo katiba mpya wanayoidai. Tunawaomba watanzania wenzetu msikubali kufanywa kama mbuzi wa kafara na watu wenye tamaa, pupa, ulevi, na uroho wa madaraka kama hawa akina Mbowe na kundi lake. 

  Tusijiendee tu kama kuku aliekatwa kichwa halafu akaachiwa atembee, na tusishikiwe akili zetu kama za mbayuwayu kwani “Akili za Kushikiwa, ongeza na zako”. Tuwakataeni wanasiasa uchwara waliofilisika kihoja na kutaka kuwatumia ili kujinufaisha. Wanataka kutupeleka wapi? Ni dhambi isiyosameheka kulitumbukiza taifa hili katika machafuko yenye majuto makubwa kama ya Misri, Syria, Afrika ya kati, Libya, Sudan ya Kusini na kwingineko. Tusikubali watupeleke huko, waacheni waende wenyewe kama wanaweza. kwani nchi yetu ina mgogoro wa kisiasa?!!!!! Waulizeni wanataka nini?

  Ndugu watanzania wenzetu, tunaomba mjue kwenye nchi hizo hizo zenye demokrasia pevu watu wa aina ya Mh. Freeman Mbowe (hasa kwa kauli zake alizozitoa juzi tarehe 14.09.2014) wanaotaka kuvuruga na kuvunja misingi mikuu ya utaifa wao (core values) kama vile amani, usalama na umoja huwa hawavumiliwi hata kidogo. 

  Sisi umoja wa vijana wazalendo wa vyuo vya elimu ya juu Dar es Salaam  tunaviomba vyombo vyetu vya dola visizivumilie kauli kama hizi zilizotolewa na Mh. Freeman Mbowe hata mara moja. Kwani vyombo vya dola vina dhamana ya kulinda, kutunza na kuendeleza amani na utulivu wa nchi yetu. Umoja wetu,  kwa heshima na taadhima kubwa, tunaviomba vyombo hivi kumchukulia hatua kali za kisheria Mh. Mbowe kwa kauli hii ya kutishia uvunjifu wa amani kabla hajaiingiza nchi yetu kwenye machafuko ya kisiasa. 

  Sisi umoja wa vijana wazalendo wa vyuo vya elimu ya juu Dar es Salaam hatutaki kuona vijana wenzetu na watanzania wote kwa ujumla wakiathirika kwa ujinga huo wa maandamano yanayofanywa mradi wa kutafuta fedha. Kwani maandamano hayo yatawaathiri wana vyuo wa Dar es Salaam pamoja na kuathiri shughuli nyingine za kiuchumi, na kijamii za wananchi wa kawaida. 

  Kwa nini shughuli zetu na za wananchi zisimame kwa sababu tu ya machafuko ili  Mh. Mbowe apate picha za kwenda kuuza huko kwa wafadhili wao? Sisi umoja wa vijana wazalendo wa vyuo vya elimu ya juu Dar es Salaam tulisikiliza na kutazama hotuba ile kwa umakini wa hali ya juu, tunapenda kuwathibitishia kuwa hotuba ile haikuwa ya kisomi, ilikuwa haijengi chama chake wala ilikuwa haijengi nchi yetu isipokuwa ilikuwa ya kibabe, ilikuwa ya kejeli,  ilikuwa ya kichochezi iliyolenga  kuvunja misingi ya amani na utulivu wa nchi yetu. Ni matumaini yetu kuwa hata kwa mwanafunzi wa shule ya msingi hawezi kujifunza kitu chochote cha maana kutoka kwenye hotuba ile. Hotuba ya Mh. Mbowe haiwezi kutusaidia kujenga taifa lenye dira kwa vizazi vijavyo. 

  Mwisho, Sisi kama umoja wa vijana wazalendo wa vyuo vya elimu ya juu Dar es Salaam, tunawataka watanzania wenzetu mzipime na kuzitafakari kwa makini kauli za Mh. Mbowe,  na kujiuliza je anafaa kuwa kiongozi wa nchi hii?
  Asanteni kwa kutusikiliza,
  Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika
  Imesomwa na Mussa Omari, Mwanafunzi OUT, kwa niaba ya umoja wa vijana wazalendo wa Vyuo vya elimu ya juu Dar es Salaam
  Tarehe 17.09.2014                        Sahihi……………………….Simu 0715632681
   

  0 0

   Sehemu ya Watoto yatima wanaolelewa na Kituo cha Tanzania Mitindo Houshe chini yake Mwanamitindo nguli hapa nchini,Khadija Mwanamboka wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wasimamizi wao wakati wa sherehe ya kuadhimisha miaka 7 ya kituo hicho iliyofanyika mwishoni mwa wiki,Msasani jijini Dar es Salaam.
  Mlezi wa Tanzania Mitindo House,Mwanamitindo,Khadija Mwanamboka akikata keki pamoja na Watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho.

   Sehemu ya watoto hao wakifurahia kwa pamoja michezo mbali mbali iliyokuwepo.
   Taswira ya mtoto akiwa kachora uso wake.


older | 1 | .... | 364 | 365 | (Page 366) | 367 | 368 | .... | 1897 | newer