Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 363 | 364 | (Page 365) | 366 | 367 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiangalia moja kati ya miti 19,270 ya korosho iliyoharibika  alipokwenda kukagua shamba la hekali 1000 katika Kijiji cha Magawa wakati wa ziara yake wilayani Mkuranga ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM.PICHA NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
   Kinana akiongoza kukagua shamba la mikorosho iliyoharibika na kuwafanya wananchi wa Kijiji cha Magawa kuwa masikini.
   Kinana akisaidia kuranda mbao baada ya kufungua Tawi la Vijana wajasriliamali la Mayuyu Mjini Utete, Wilayani Rufiji leo
   Kinana na Nape wakiangalia viti walivyozawadiwa na kikundi hicho cha vijana. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


  0 0

  IMG_0590Mdau Sunday Shomari akiwa na Ankal wakati alipotembelea ndani ya ofisi Michuzi Media Group (MMG) mara tu baada ya kuwasili jijini Dar es alaam. IMG_0594


  0 0

  Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano wa Benki ya NBC, William Kallaghe (kushoto) akizungumza huku Mkuu wa Huduma za Rejareja za Kibenki wa NBC, Mongateko Makongoro akimsikiliza katika Mkutano wa 24 wa Wadau na Wanachama wa Mfuko wa PPF uliofanyika hivi karibuni jijini Arusha.
  Mkuu wa Huduma za Rejareja za Kibenki wa NBC, Mongateko Makongoro akizungumza katika Mkutano huo.
  Kaimu Mhazini Mkuu wa Benki ya NBC Tanzania, Ivan Tarimo, (wa pili kushoto), akizungumza wakati wa tafrija ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wajumbe wa mkutano wa 24 wa wanachama na wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF jijini Arusha hivi karibuni. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PPF, Ramadhan Khija, na watatu kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, (watatu kulia), akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Benki ya NBC Limited, kwa wajumbe wa mkutano wa 24 wa wanachama na wadau wa PPF jijini Arusha. Wengine pichani kutoka kushoto ni Kaimu Mhazini Mhuu Benki ya NBC, Ivan Tarimo, Mkuu wa Huduma za Rejareja za Kibenki, Mongateko Makongoro, mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ramadhan Khija, na wafanyakazi wa NBC

  0 0

  DSCN1621
  Mfugaji wa Heifer International Tanzania Abel Mwakatumbula na mkewe wakiwa na Makamu wa Rais wa shirika hilo.
  DSCN1660
  Makamu wa Rais wa Heifer International Steve Denne, Mkurugenzi wa Heifer International Tanzania Dk. Henry Njakoi wakifurahia mafanikio ya miradi ya Heifer International.
  DSCN1799
  Makamu wa Rais wa Heifer International akigawa mtamba kwa mwana kikundi cha Faraja Wilayani Rungwe.
  DSCN1908
  Steve Denne akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Abbas Kandoro alipotembelea ofisi za Mkoa.  Steve Denne alitembelea Tanzania kwa mara kwanza wiki iliyopita kuona miradi inayoendeshwa na shirika hilo. Katika ziara hiyo, Steve Denne alitembelea ofisi za mkoa wa Mbeya akifuatana na Mkurugenzi wa Heifer International Tanzania Dk Henry Njakoi, Meneja Mradi wa EADD Tanzania Bwana Mark Tsoxo, ambapo walikutana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro. 

  Katika Mazungumzo yake na Mheshimiwa Abbas Kandoro, Bw Denne aliishukuru sana serekali ya Tanzania kwa mahusiano mazuri na ushirikiano mkubwa kwenye kutekeleza miradi ya shirika hilo nchini na hasa katika kuanzisha Mradi wa Uendelezaji Sekta ya Maziwa Afrika Mashariki (EADD). 

  Aliahidi kuwa shirika hilo kupitia mradi wa EADD na miradi mingine tarajiwa, litaendelea kuleta mabadiliko kwa kuwasaidia wafugaji wadogo kwenye mikoa wa Mbeya, Iringa na Njombe ili kuinua uchumi wao na kuwa na ufugaji wenye tija na endelevu.

  Pamoja na miradi aliyoitembelea Steve Denne, mradi wa Uendelezaji Sekta ya Maziwa Afrika Mashariki (EADD) unaoanza Mkoani Mbeya wilaya ya Rungwe kijiji cha Kyimo ambapo aligawa mtamba kwa mfugaji wa kikundi cha Faraja kama dira ya shirika hilo ya “Toa Zawadi Pia” – Pass On The Gift.
  Akiwa nchini, Makamu wa Rais wa shirika la Heifer International alikutana na wadau mbalimbali wa sekta ya maziwa nchini wakiwemo wasindikaji, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bwana Jordan Rugimbana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi Zanzibar ambapo alikutana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dr. Kassim Gharib Juma.
  DSCN1909
  Makamu wa Rais wa Shirika la Heifer International Steve Denne, Meneja Mradi wa EADD Tanzania na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro katika picha ya pamoja.
  DSCN2098
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bwana Jordan Rugimbana akiwakaribisha ofisini kwake, Makamu wa Rais wa Shirika la Heifer International Steve Denne na Mkurugenzi wa Shirika hilo Tanzania Dk. Henry Njakoi.
  DSCN2100
  Steve Denne alipomtembelea Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan Rugimbana.
  DSCN2111
  Steve Denne katika mazungumzo na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan Rugimbana.
  DSCN2320
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Zanzibar Dk. Kassim Gharib Juma (kushoto) akibadilishana mawazo na Makamu wa Rais wa Shirika la Heifer International Steve Denne na Dk. Henry Njakoi, Mkurugenzi wa Shirika hilo nchini.

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt Rehema (kati) akikatata utepe kuashiria kulizindua rasmi duka la Airtel Dodoma lililopo barabara ya Mkuu mkoani humo, anaeshuhudia wakwanza kulia ni mkurugenzi wa airtel huduma kwa wateja Bi, Adriana Lyamba na Meneja biashara wa Airtel Dodoma Bw, Stephen Akyoo wakwanza kushoto, Airtel imefanya uzinduzi wa duka hilo jana baada ya kuzindua maduka mengine katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha Mwanza Mbeya na Mtwara. Maduka mengine ya Morogoro, Bukoba na Zanzibar pia yanatarajiwa kuzindulia mwezi huu.
  Meneja mauzo wa Airtel Mkoa wa Dodoma Bw Stephen Akyoo akiwa na wafanyakazi wengine wa Airtel Dodoma akitoa maelezo mafupi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr Rehema Nchimbi kuhusiana na muonekano wa duka jipya la Airtel Dodoma lililopo barabara ya Mkuu muda mfupi kabla ya mkuu wa mkoa huyo kuzindua duka hilo jana.
  Kati kati ni Mkuuu wa mkoa wa Dodoma Dkt Rehema nchimbi akiwa na Mkurugenzia wa huduma kwa Mteja Airtel Bi Adriana Lyamba (shoto) na Meneja wa Duka hilo mkoani hapo Bi Elida kulia wakikata keki iliyoandaliwa maalum kwa ajili ya uzinduzi wa duka jipya la Airtel mtaa wa Mkuu mjini Dodoma jana.
  Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt Rehema Nchimbi akiongea na wananchi na wanahabari hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa duka jipya la Airtel mkoani Dodoma barabara ya mkuu Jana, Airtel ilizindua duka hilo kwa dhumuni la kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja wake nchini.
  Wafanyakazi wa Airtel mkoa wa Dodoma wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya Airtel kufungua Duka jipya mkoani hapo mtaa wa Mkuu jana.


  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imefungua duka lake la Dodoma kufatia ukarabati uliokuwa unafanyika wa kuliweka duka hilo kuwa la kisasa zaidi ili kuweza kuendelea kuwapatia wateja wake huduma bora zaidi. 

  Uzinduzi wa duka hilo ulifanywa na mkuu wa mkoa wa dodo dkt Rehema Nchimbi ambapo amewapongeza Airtel kwa mpango kabambe wa kuboresha maduka yake nchini pamoja na duka la Dodoma.

  Akiongea wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa wateja Bi Adriana Lyamba alisema,"Leo tunazindua rasmi duka hili lenye muundo mpya lililopo katika barabara ya Mkuu hapa Dodoma ikiwa ni moja kati ya mikakati yetu ya kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma zetu na kupunguza msururu wa wateja wanaoingia dukani hapa kupata huduma mbalimbali.

  Kwa kupitia duka hili wateja wetu watafurahia huduma zetu za pesa mkononi za Airtel Money ,internet na kuweza kununua muda wa maongezi pamoja bidhaa zikiwemo simu za mkononi na vifaa vya huduma za mawasiliano na huduma nyingine nyingi.

  Sasa wateja wetu wanauhakika wa kupata huduma bora kwa haraka zaidi kupitia duka hili. Tutaendelea kutoa huduma za kibunifu zenye uhakika na zenye ubora wakati wote kupitia mtandao wetu bora na mpana ulioenea zaidi nchini. Lengo letu ni kuhakikisha tuwapatia wateja wetu uzoefu tofauti katika huduma zetu na kufikia matarajio yao. aliongeza Lyamba.

  Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh, Dkt Rehema Nchimbi alisema" nawapongeza sana Airtel kwa juhudi hizi za kuboresha utoaji wa huduma za mawasiliano kwa watumiaji nchini. Sote tunatambua mawasiliano ni nyenzo muhimu katika kuunganisha jamii na kuendesha shughuli za kibiashara na kiuchumi nachukua fulsa hii kuwaomba wakazi wa Dodoma watumie vyema nafasi hii kupata huduma bora zitakazorahisisha uendeshaji wa Shughuli zao mbalimalbali za kila siku".

  "Serikali inaunga mkono juhudi zinazofanywa na Airtel na kuwaomba waendelee kuwekeza zaidi katika kuboresha upatikanaji wa huduma za mawasilaino nchini. tuko tayari kushirikiana Airtel katika kuhakikisha tunaweka mazingira bora ya kuendesha biashara ili kuwawezesha wananchi wetu kufaidika na huduma hizi za mawasiliano na hatimaye kuwa maisha bora."

  Airtel imeendelea kuboresha maduka yake nchini ambapo hivi karibuni imezindua maduka yake mapya katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha Mwanza Mbeya na Mtwara. Maduka mengine ya Morogoro, Bukoba na Zanzibar yanategemewa kuzinduliwa kabla ya mwisho wa mwezi huu wa septemba.


  0 0

  Muonekano wa Jengo hilo ambalo lipo Katikati ya Mji wa Dodoma, lenye Ghorofa moja linakodishwa tunapenda kuwakaribisha Mtu binafsi, makampuni, shirika au taasisi ambayo inataka kufungua ofisi au imekuwa ikihitaji jengo kwaajili ya Ofisi sasa Jengo Zuri tu lenye huduma zote muhimu lipo na Nafasi pia Zipo Karibu Kwa Mawasiliano Zaidi 
  Piga namba hii 0787 970 072
   Korido Kama inavyoonekana 
   Vyumba vyake ni Vikubwa na Unaweza kufanya Ofisi kama inavyoonekana kwenye picha.
   Sehemu ya Kupandia Kwenda kwenye ghorofa ya Kwanza
  NI Jengo la Ghorofa 1 ambalo hapo awali lilikuwa ni hotel lakini kwasasa linapagishwa kwaajili ya Makampuni, Maofisi na Mashirika mbalimbali au Watu binafsi ambao wanahitaji Ofisi Mkoani Dodoma, Jengo Hilo linapatikana Mkoani Dodoma na Lipo Katikakati ya Mjini Kabisa huku likiwa na Huduma Zote Muhimu za Kijamii.Kama Kampuni, Shirika, au Taasisi inataka kupanga au Mtu Binafsi basi asisite kuwasiliana na Sisi kupitia namba hii 0787 970 072

  0 0

  “PIGA KITABU NA LAPF”
  WANACHAMA WA LAPF KUNUFAIKA NA FAO LA ELIMU

  Bilioni 3 kutumika mwaka wa masomo 2014 – 2015 kutoka mfuko wa pensheni wa LAPF kwa wanachama wake.

  15 Septemba 2014, Dodoma: Wanachama wa mfuko wa penseni wa LAPF kunufaika na fao jipya lilozinduliwa hivi karibuni nchini kwa Baraka zake Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI Mh. Hawa Ghasia. Fao hilo lijulikanalo kama ‘Piga Kitabu na LAPF’ limelenga kuwakopesha wanachama wa LAPF mikopo ya elimu ya juu kwani ni ombi la muda mrefu kutoka kwa wanachama wa mfuko huo. Hivyo kwa kuthamini na kuona umuhimu wa elimu Mfuko wa Penseni wa LAPF umjibu kiu yao ya muda mrefu ili kumpunguzia mzigo mwajiri.

  Akiongea kutoka Dodoma, Mkurugenzi Mkuu wa LAPF Bwana Eliud Sangaalieleza kuwa  mfuko wa Pensheni wa LAPF una huduma nyingi na ambazo zimelengwa kwa ajili ya jamii na hususani zinazochangia sana kwenye maendeleo. 

  “Huduma hii mpya ya Fao la Elimu imetengewa shilingi Bilioni Tatu (3) kwa mwaka huu wa fedha ikiwa ni kianzio cha mfuko huu, tunaahidi mwaka unaofuata fao hili litatengewa bajeti kubwa zaidi kutokana na umuhimu wake katika nchi yetu, wanachama wengi wameshanufaika mpaka sasa na wengine wengi zaidi wanazidi kutuma maombi ya kupata mkopo wa elimu ya juu. Fao hili litawanufaisha wanachama maelfu na maelfu, wanachama wengi watume maombi kunufaika na huduma hii”

  “Mwanachama anatakiwa kujaza fomu ya mkopo wa elimu LAPF/LON.2, ambayo hupatikana katika ofisi zote za LAPF pamoja na ofisi za waajiri wachangiaji na pia kwenye tovuti ya LAPF www.lapf.or.tz. Baada ya kukamilisha fomu na kuambatisha vielelezo vinavyotakiwa atawasilisha fomu hiyo kwenye ofisi za LAPF au atatuma kwa njia ya posta. Fao hili la Mkopo wa Elimu kwa mwanachama utalipwa moja kwa moja chuoni kila mwaka wa masomo kwa taratibu za chuo husika na urejeshaji wake utakuwa kwa muda wa miaka mitano tangu ulipoanza kutolewa” Aliongeza Bwana Sanga.

  ‘Piga Kitabu na LAPF’ ni fao la elimu litakalotolewa kwa  mwanachama yoyote wa lapf ambaye amekidhi vigezo kama kupata kibali cha kusoma toka kwa mwajiri wake, barua (admission letter) ya kukubalika kujiunga na chuo cha hapa nchini kilichosajiliwa na nacte au tcu na awa na michango inayozidi kiasi cha mkopo unachoombwa kwa asilimia 25.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akizungumza na Mhe. Charles M. Huber (wa pili kushoto) ambaye ni Mbunge na Mjumbe wa Kamati ya Ushirikiano wa Uchumi na Maendeleo na Mambo ya Nje ya Bunge la Shirikisho la Ujerumani wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam kwa mazungumzo leo Septemba 15, 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Charles M. Huber (kulia kwa Makamu wa Rais), Stefan Reith Mwakilishi wa Konrad Adenauer Stiftung (KAS) kushoto, Naibu Balozi wa Ujeruman nchini John Reyels (wa pili kulia) na Richard Shaba baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu Dar es Salaam Septemba 15, 2014. Picha na OMR

  0 0

  Mkuu wa Rasilimali Watu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Flora Lupembe (kulia) akimwagiwa maji baridi na Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Rukia Mtingwa katika hafla ya kumwagiana maji baridi iitwayo ‘Ice Bucket Challenge’ yenye makusudi ya kuchangisha fedha kwa ajili kusaidia wanawake wanaosumbuliwa na ugonjwa wa fistula. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.
  Kaimu Mhazini Mkuu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Ivan Tarimo (kushoto) akimwagiwa maji baridi na mmoja wa mfanyakazi mwenzake katika hafla ya kumwagiana maji baridi iitwayo ‘Ice Bucket Challenge’ yenye makusudi ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wanawake wanaosumbuliwa na ugonjwa wa fistula. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Mussa Jallow (katikati) naye akimwagiwa maji baridi ili kutimiza azma ya benki hiyo katika kutafuta fedha ili kusaidia wanawake wanaosumbuliwa na tatizo la ugonjwa wa fistula nchini.


  0 0

   
  Na Benedict Liwenga, MAELEZO-Dodoma.
   
  MJUMBE wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. George Simba Chawene amesikitishwa na kauli zilizotolewa na baadhi ya Wajumbe walioko nje ya bunge hilo kuhusiana na uhalali wa bunge hilo lililoko Kisheria.
   
  Kauli hiyo ameitoa leo wakati akichangia mada katika mjadala ndani ya bunge hilo huku akisisitiza kuwa huo ni upotoshwaji mkubwa na watu hao wanapaswa kuangaliwa kuhusu uzalendo wao.
   
  Mhe. Chawene ameeleza kuwa inasikitisha zaidi hasa pale shutuma zinapoelekezwa kwa Mwenyekiti wa bunge hilo, Mhe. Samuel Sitta, kuwa bunge hilo sasa linaonekana ni mali ya Mwenyekiti wa bunge hilo wakati si kweli.“Gazeti linachukua kurasa tatu hadi nne kuzungumzia habari Sitta king’ang’anizi, hivi hili bunge lipo kama liliitishwa na Sitta ama na Rais wa nchi?, hili bunge liko kisheria”, alisema Mhe. Chawene.
   
  Aliongeza kuwa kwa niaba ya Watanzania wanafanya kazi ya bunge hilo kwa mujibu wa sheria huku akisisitiza kuwa wajumbe waliotoka nje ya bunge hilo wamevunja sheria na kwamba hawawezi kutafuta uhalali nje ya sheria.“Wanamlazimisha Rais avunje bunge hili, Rais wa kufuata utawala bora anavunja kwa mamlaka yapi? Mamlaka ya Rais yako kwa mujibu wa sheria”, alisema Mhe. Chawene.
   
  Aidha, ameeleza kuwa Sheria inayoendesha mchakato wa Katiba ni Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambayo imetungwa kutoka katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye hatua tatu zikiwemo hatua ya kukusanya maoni ambayo Tume ya Warioba ilifanya kazi hiyo na kumaliza, hatua ya Pili ni bunge hilo kujadili kwa niaba ya wananchi wa Tanzania kwa uwakilishi uliopo ndani ya bunge hilo na hatua ya tatu ni wananchi kwenda kutunga Katiba.
   
  “Sisi hapa tunatoa Katiba inayopendekezwa, inayofuata ni Watanzania kwenda kutunga Katiba kwa kutunga kwa kupiga kura ya kusema ndiyo au hapana yale tuliyoyajadili na kuletwa na Tume”, alisisitiza Mhe. Chawene.
   
  Aidha, amewataka watanzania kuwaona watu hao kuwa ni watu wabaya na wasio na nia nzuri na nchi na kuepuka kuingia barabarani kufanya maandamano ya kuipinga Katiba hiyo.

  0 0

  TIMU nane kati ya 18 zinazoshiriki mashindano ya Kombe la OG Wala Wala yanayofanyika kwenye uwanja wa Jitegemee mjini Muheza Jumatano Septemba 18 zinaingia kwenye robo fainali ya kumpata bingwa wamwaka huu.

  Msemaji wa Kombe la Wala Wala, Yusufu Shemweta maarufu kama Majisafi alisema jana kuwa kila kundi kati ya mawili ya inaingiza timu nne katika Robo fainali inayotarajiwa kuwa na mvutano ya hali ya juu.

  Alisema mshindi wa mwaka huu atazawadiwa seti mbili za jezi, mipira mitatu na sh. 100,000 taslimi pia mshindi wa pili atapata zawadi kama hiyo lakini atapata jezi seti moja na mpira miwili.

  Shemweta ambaye pia ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka Wilaya ya Muheza (TFF) alisema mshindi wa tatu atazawadiwajezi seti moja, mpira mmoja nafedhataslimu sh. 100,000 na timunyingine zilizoshiriki mashindano hayo zitazawadiwa mpira mmoja nafedhash. 100,000.

  Alizitajatimu zinazoshiriki mashindano hayo kutoka kundi A ni Kilimo FC, Mkumbi FC, Chipukizi FC< Uruguay FC, Mafundi FC, Miembeni, Muheza United, Lusanga Star na Black Fighter.

  Kutoka kundi B kuna timu za Tax Driver FC, Wabambino FC, Mkanyageni FC, Shoeshine FC,  Kwamkadala FC , Magila Star, Wakosanamba FC, Kwa Mkangala FC na Kitisa FC.

  0 0

  Mkurugenzi wa Kitengo cha Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO’s) wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Bw. Marcel Katemba akiongea na waandishi wa habari( Hawapo pichani)kuhusu juhudi zinazofanywa na serikali katika kuyajengea mazingira mazuri ya ufanyaji kazi Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO’s) ili kuongeza ushiriki na kutoa mchango wao katika kuleta maendeleo katika  jamii, Wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jiijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara hiyo Bw. Erasto Ching’oro.
      Na Jovina Bujulu-MAELEZO.

  Serikali kupitia uratibu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto imeendelea kujenga mazingira wezeshi kwa ajili ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGO’s) kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya ya jamii.
   Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Marcel Katemba leo jijini Dar es Salaam.
  Mercel alisema kuwa serikali inaendeleza jitihada za kuwezesha Mashirika hayo ikiwemo utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2001 na Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na.24 ya mwaka 2002 na marekebisho yake ya mwaka 2005.
  “Sera hii ni mwongozo mkuu kwa Taifa katika masuala ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ikiwa na lengo la kuweka mazingira wezeshi kwa Mashirika hayo kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya jamii kwa kuzingatia uwazi, uwajibikaji na ushirikano” Alisema Marcel.
  Marcel aliongeza kuwa Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali inaendelea kusimamia sekta ya mashirika hayo na kutoa ushauri kwa Waziri mwenye dhamana ya uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ili kuongeza ufanisi katika usimamizi wa sekta hiyo.
  Aidha Baraza la Taifa la NGO’s linaendelea kuratibu utekelezaji wa kanuni za maadili ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa lengo la kujitawala, kutandaa na kuboresha huduma zinazotolewa na mashirika hayo.
  Akifafanua zaidi Marcel amesema ubia na ushirikiano baina ya Serikali na NGO’s umeimarika kutokana na matamko ya kisera na elimu inayotolewa kwa wadau mbalimbali wa mashirika yasiyo yakiserikali.
  Pia Serikali imeendelea kutoa misamaha ya Kodi na ruzuku kwa Mashirika hayo ikiwa ni sehemu ya kuthamini mchango wao katika maendeleo ya Taifa.
  Juhudi za serikali za kujenga mazingira wezeshi kwa NGO’s zimepanua wigo kwa wananchi kujumuika na kushiriki katika maendeleo ya jamii ambapo zaidi ya wananchi 35,000 ni wanachama wa mashirika hayo yaliyo zaidi ya 6679 kote nchini.

  0 0

   Mjumbe wa Bunge Maalum, Mhe. Prof. Mark Mwandosya akichangia mjadala wa ndani ya Bunge Maalum kujadili taarifa za kamati za bunge hilo zilizowasilishwa wiki iliyopita kwa ajili ya kuandika Katiba inayopendekezwa.(Picha na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma)
   
  Na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma.
   
  MJUMBE wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Prof. Mark Mwandosya ameeleza kuwa mpaka ifikapo mwaka 2055 Tanzania itakuwa imeachana na umaskini katika nchi ya uchumi wa kwanza endapo kutakuwa na dhamira ya dhati hususani kuwa kuandika Katiba yenye kuleta nafuu kwa watanzania kwani kila kitu kwa Waafrika kinawezekana pasipo kuwa na Wazungu.
   
  Prof. Mwandosya alisema hayo jana wakati akichangia mjadala wa katiba ndani ya Bunge Maalum, ambapo alisisitiza umuhimu wa kuwa na katiba itakayozingatia vipaumbele ambavyo vinaweza kumkwamua mwananchi wa kawaida kuondokana na umasikini na kuliinua Taifa kiuchumi.
   
  Mhe. Mwandosya amesema kuwa kuhusu changamoto na kero zinazohusu mambo ya Muungano, katiba imejaribu kuzizingatia karibia zote, huku akieleza kuwa hali ya Muungano ni imara na itaendelea kuwa imara.
   
  Ili kufanikisha nchi inapiga hatua baada ya kuwa na Katiba bora, Mhe. Mwandosya amefafanua kuwa, watumishi wote wa Umma hawana budi kuliletea tija Taifa hili kwa kuwa misingi imewekwa ndani ya rasimu ya katiba  na kusisitiza kuwa Mtumishi wa Umma sio mtawala na mambo yanayohusu miiko na maadili ya mtumishi huyo yenye kumtumikia mwananchi serikali Katiba imeweza kuyazungumzia.
   
  “Tumezungumzia kuhusu rushwa ambaye ni adui wa haki, kwamba hili tulitambue katika Katiba ili katika Sheria likasimamiwe vilivyo na pia tumezungumzia pia wale wanaouhujumu uchumi”, alisema Mhe. Mwandosya.
   
  Kuhusu haki za vijana, Mhe. Mwandosya ameeleza kuwa katika Rasimu ya Katiba wamezungumzia juu ya haki za vijana, haki za walemavu, haki za wazee, pamoja na haki za watoto, huku akiwashangaa baadhi ya wajumbe walioko nje ya bunge hilo wanapotoa shutuma kuwa wanapoteza wakati kana kwamba hawazungumzii mambo yanayowahusu wananchi.
   
  “Nawaomba wananchi watusikilize na wayazingatie haya tunayoyasema”. Alisema Mhe. Mwandosya.
   
  Akizungumzia kuhusu Vyombo vya Usalama, amesema kuwa Katiba inawalinda na kuwatambua viongozi wa usalama, ambapo sheria inawapa haki hata baada ya kustaafu ili wakaweze kuishi maisha bora kwa kuchukua dhamana kubwa, hivyo kwa dhamana hiyo viongozi hao wanapostaafu wanatakiwa kujiepusha na masuala ya kisiasa kwasababu.
   
  “Usalama wa Taifa, Jeshi, Polisi, Magereza na Uhamiaji, hawa tunawatengezea mambo mazuri sana wanapostaafu, kwahiyo tafadhari sana mkishatoka tusaidieni, toeni ushauri lakini mkijiingiza katika siasa na mafaili yetu huku mmeyashika hamtutendei haki”, alisema Mhe. Mwandosya.
   
  Aidha, ameomba kuwepo na Randama kwani hiyo inaandikwa katika lugha ambayo mwananchi anaweza kuisoma tofauti na katiba kwani hiyo inaandikwa kwa lugha ya kisheria, kwahiyo amependekezo kuwepo na randama kwa ajili ya wananchi.
   
  Mwandosya ameongezea juu ya suala la amani kuwa ni jambo kubwa sana, amewananga watu wenye tabia ya kutaka wananchi kuandamana wakapigwe risasi hao ni watu wasioitakia mema nchi, hivyo amewaasa wananchi walipinge kwa nguvu zao zote kuhusu suala hilo.
   
  “Nina ushauri kwa viongozi wenye kutaka wananchi wakapigwe risasi na Polisi, naomba watangulie wao wajipige risasi, unapotaka kuwa Shujaa anzia kwanza wewe mwenyewe, usiwapeleke vijana ambao ni matumaini ya nchi yetu, ndugu zangu hili jambo siyo la busara hata kidogo na wananchi mnapokwenda kuandamana, vijana mseme mnaandamana kwa nini? Kwasababu gani? Na kwa misingi gani na kwasababu ya nani? Ukishajibu haya maswali kwakweli mtaona nchi yetu kuwa ni nzuri sana, nchji ya amani”, alisisitiza Mhe. Mwandosya.

  0 0

  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi George Yambesi akizungumza na watunishi wa sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu Mkoa wa Mwanza,juu ya umuhimu wa kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, kanuni na miongozo iliyopo ili kuleta tija katika ufanisi wa kazi zao.
  Sehemu ya watunishi wa sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza wakiwa kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu Mkoa wa Mwanza wakati wa mkutano wao na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi,George Yambesi 
  Picha ya pamoja.

  Na Atley Kuni- Afisa habari Mwanza.

  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi George Yambeshi, amewataka watumishi wa Umma wa Sekretarieti ya mkoa wa Mwanza kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, kanuni na miongozo iliyopo ili kuleta tija katika ufanisi wa kazi zao.

  Ameyasema hayo wakati alipokutana na watunishi wa sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mwanza hii leo alipokuwa ziarani mkoani humo kwa shughuli za kijamii na kuamua kutumia fursa hiyo kukutana na watumishi hao.

  Yambeshi amesema kama watumishi wa umma ni lazima kuzingatia miiko inayo ongoza utumishi wa umma huku akitolea mfano wa mavazi nadhifu kwa watumishi na yasiyo na utata kwa watu " kama watumishi wa ni vema kuzingatia miiko inayo tuongoza" alisema na kuongeza. kuwa suala la kuvujisha siri za serikali ni suala lisilo kubalika hivyo moja ya sifa ya mtumishi wa umma ni lazima ajue kutunza siri.

  Katika hatua nyingine Katibu Mkuu huyo ameonya watumishi wa kuacha kuchanganya mambo ya siasa mahali pa kazi" Ndugu zangu haikazwi kuwa mwanachama wa chama cha siasa lakini sio vema mtumishi kufanya masuala ya siasa mahali pa kazi kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na taratibu za utumishi wa umma.

  Mbali na masuala la siasa na uadilifu katika kazi ,pia katibu Mkuu huyo ametumia fursa hiyo, kusilikiliza kero mbali mbali za watumishi hao ikiwapo suala la kodi kubwa, mikopo kwa watumishi pamoja na kukosekana kwa baadhi ya miundo ya kada mpya za utumishi serikialini.

  Awali akimkaribusha katibu Mkuu kiongozi kuzungumza na watumishi hao wa Skretarieti ya Mkoa wa Mwanza, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Bwana Ndaro Kulwijila, alimuelezea kuhusu hali halisi ya watumishi katika mkoa wa Mwanza huku akitoa kilio chake kwa Katibu Mkuu huyu juu ya utofauti Mkubwa wa mishahara baina ya watumishi waliopo kwenye wakala wa serikali na wale wa serikali kuu.

  Hata hivyo katika majibu yake Katibu Mkuu huyo aliahidi kushughulikia changamoto zote zilizo jitokeza katika kikao hicho na kuzipatia ufumbuzi kwa kadri itakavyowezekana.

  Katibu Mkuu Utumishi ndiye mkuu wa masuala ya Utumishi wa umma katika Serikali ya jamahuri ya Muungano wa Tanzania.

  0 0

   Pichani ni Mkurugenzi wa kundi hilo, Fadhili Lugendo maarufu kama Koka Star anayecheza tumbo wazi akiwajibika.

  Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
  KUNDI la ngoma za asili lenye kupendwa na wengi jijini Dar es Salaam linalojulikana kama Naukala Ndima, limejipigia debe likisema lina hamu kubwa ya kufanya kazi ya maana katika tamasha la Handeni Kwetu, litakalofanyika Desemba 13, mwaka huu wilayani Handeni, mkoani Tanga.

  Tamasha hilo linalosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa matukio makubwa ya sanaa na burudani linafanyika kwa msimu wa pili, baada ya kuzinduliwa rasmi mwaka jana Desemba 14 na kuhudhuriwa na wengi.

  Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa kundi hilo, ambaye ni miongoni mwa wasanii wa ngoma za asili, Fadhili Lugendo, maarufu kama ‘Koka Star’, alisema kuwa wamelipania tamasha hilo kwasababu wanafahamu linavyopendwa na wengi mkoani Tanga na Tanzania kwa ujumla kutokana na kuandaliwa vizuri.

  Alisema kuwa tamasha la mwaka jana lilikuwa zuri na kuwapatia mafanikio makubwa kutokana na mikataba mingi waliyoipata, ukiwapo ule unaohusisha wao na televisheni ya CTN iliyowapa haki ya kurusha vipindi vya utamaduni wa Tanzania.

  “Baada ya kusikia waandaaji wa tamasha hilo wamejipanga tena kufanya tukio hilo mwezi Desemba mwaka huu, tunapata shauku ya kuomba na sisi tuwe miongoni mwa makundi kutoka nje ya mkoa wa Tanga tutakaoshiriki.

  “Nikiwa kama msanii wa ngoma za asili natambua matamasha makubwa kama haya ndio yanayoweza kutangaza sanaa yetu pamoja na kukuza utamaduni wa Mtanzania, hivyo endapo tutapewa mwaliko wa kuelekea Handeni, hakika tutafanya kazi ambayo haitasahaulika,” alisema.

  Naukalanda Ndima ni miongoni mwa makundi kutoka nje ya Handeni, mkoani Tanga yaliyopata fursa ya kuonyesha sanaa yao mwaka jana kwenye tamasha hilo linaloandaliwa chini ya Mratibu wake Mkuu Kambi Mbwana.

  0 0

  Mashabiki wa Mnadani Fc wakiwa wamembebe mchezaji wao Alawi Mohamed ambaye aliwanyanyua mara mbili mashabiki hao toka vitini hatimaye ushindi katika mchezo wa robo fainali ya michuano ya Pepsi kombe la Meya 214 dhidi ya timu ya Magazeti, hadi mwisho wa mchezo Mnadani Fc 2, Magazeti 1.
  Mpira wa adhabu ukipigwa kuelekea langoni mwa timu ya Magazeti Fc, katika mchezo wa robo fainali Pepsi kombe la Meya 2014, uliochezwa jana Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza,  Matokeo ya mchezo huo Mnadani Fc 2, Magazeti 1.
  'Mpira uwekwe kati' kwa mujibu wa mwamuzi wa mchezo, mara baada ya goli la kwanza la kusawazishwa na Mnadani Fc ikiwa ni dakika saba tu toka Magazeti Fc  walipopata goli la kuongoza, baadaye Mnadani Fc waliongeza bao la pili na laushindi hivyo hadi mwisho wa mchezo Mnadani Fc wakasonga mbele kwenye hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa 2-1.
  Michuano ya Pepsi Kombe la Meya 2014 imefikia patamu, sasa ni katika hatua ya nusu fainali.

  Timu zilitinga nusu fainali ya michuano hiyo ni:-
  1.Sokoni FC 
  2.Mkolani
  3.Mirongo pamoja na 
  4.Mnadani Fc.

  Michezo ya nusu fainali ya Pepsi Kombe la Meya 2014 itachezwa tarehe 17 na 18 mwezi huu ile hali fainali itakuwa jumamosi ya tarehe 20 katika Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.

  Zaidi (BOFYA PLAY KUSIKILIZA TAARIFA YA UWANJANI)

  0 0

   Waziri wan chi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira, Mhe. Mhandisi Dkt. Binilith Mahenge akiongea na waandishi wa habari kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Hifadhi ya Tabaka la Ozoni linatakalofanyika 16 Septemba, 2014.
   Baadhi ya waandishi wa habari wakifauatilia kwa makini maelezo toka kwa Mhe. Mhandisi Dkt. Binilith Mahenge yakiyohusu Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Hifadhi ya Tabaka la Ozoni linatakalofanyika 16 Septemba, 2014.(Picha zote na Benedict Liwenga, MAELEZO-Dodoma)
   
  Na Benedict Liwenga, MAELEZO-Dodoma.
   
  Tarehe 16 Septemba, mwaka huu Tanzania itaungana na Jumuiya ya Kimataifa katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Hifadhi ya Tabaka la Ozoni kama ilivyoagizwa na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika azimio lake la 49/114 la tarehe 19 Desemba, 1994.
   
  Hayo yamesemwa leo na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mhe. Mwandisi Dkt. Binilith Mahenge wakati alipofanya mkutano na waandishi wa habari 15 Septemba, 2014 kwa lengo la kuongelea juu ya Maadhimisho hayo linalofanyika tarehe 16 Septemba mwaka huu.
   
  Mwandisi Mahenge ameeleza kuwa tarehe hiyo ni kumbukumbu ya kutiwa saini Mkataba wa Montreal (Montreal Protocol-1987) kuhusu kemikali zinazomonyoa Tabaka la Ozoni kwa kudhibiti utengenezaji na matumizi ya kemikali zinazoharibu Tabaka hilo.
   
  Ameendelea kwa kusema kuwa Mkataba huo umepata mafanikio makubwa ya kupunguza zaidi ya asilimia 98% ambapo ni takribani tani milioni 1.8 ya uzalishaji na matumizi ya kemikali zinazomong’onyoa Tabaka la Hewa ya Ozoni.
   
  “Punguzo hilo limechangia katika juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwasababu baadhi ya kemikali zinamong’onyoa tabaka la ozoni pia husababisha kuongezeka kwa joto duniani”, alisema Dkt. Mahenge.
   
  Akizungumzia kuhusu mikakati ya kitaifa kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa Mkataba huo, Dkt. Mahenge alisema kuwa 1996 Serikali iliandaa na kutekeleza Programu ya Taifa ya kuondosha matumizi ya kemikali zinazomong’onyoa Tabaka la Ozoni, mikakati hiyo ni pamoja kujenga uwezo wa Taasisi zinazosimamia utekelezaji wa Mkataba, kuweka takwimu za kemikali hizo, kutoa elimu kwa wadau na kwa umma kuhusu umuhimu wa Tabaka la Ozoni na hatari zinazolikabili, kusambaza habari kuhusu kemikali na teknolojia mbadala na mikakati mingineyo.
   
  “Hatua hizi zimewezesha Tanzania kuondosha kemikali hizi kwa mujibu wa ratiba iliyowekwa na Mkataba”, alisema Mhe. Mwandisi Mahenge.
   
  Chini ya Programu ya Taifa ya kuondosha matumizi ya kemikali haribifu, serikali iliandaa Mpango wa Usimamizi wa Vipodozi yaani (Refrigerant Management Plan) na katika utekelezaji wake, mambo kadhaa yamefanyika ikiwemo kuandaa Kanuni za Usimamizi wa kemikali zinazomong’onyoa tabaka la hewa ya Ozoni ambazo zilianza kutumika tarehe 7 Desemba mwaka 2007, kusambaza kwa Vitambuzi vya kemikali hizo vipatavyo 18 kwa ajili ya vituo vilivyo mipakani mwa Tanzania, pia kusambaza mitambo na zana za kuhudumia majokofu na viyoyozi kama vile mashine za kunasa na kurejeleza gesi chakavu kwa vyuo vyote vinavyotoa mafunzo ya fani ya kuhudumia majokofu na viyoyozi hapa nchini.
   
  Aliongeza kuwa hadi sasa, Tanzania imeweza kupunguza zaidi ya tani 216 sawa na asilimia 86% ya kiasi cha matumizi ya kemikali hizo, mwaka 1999.
   
  Hapa nchini maadhimisho haya yatafanyika kwa njia ya uelimishaji umma kuhusu Tabaka la Ozoni, faida zake, madhara ya kuharibika kwa Tabaka hilo na matumizi salama ya bidhaa zenye kemikali rafiki kwa tabaka la ozone.

  0 0

  Na Benedict Liwenga, MAELEZO-Dodoma.

  15/09/2014.
   
  MUUNGANO wa Tanzania ni muungano wa damu na wa watu, ambapo Ibara ya kwanza Sura ya kwanza inaeleza kuwa msingi mkuu wa Jamhuri ya Muungano pamoja na katiba iliyopo na inayopendekezwa ni haki ya makubaliaono ya mwaka 1964.
   
  Hayo yamesemwa leo na Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Mary Nagu wakati akichangia mada katika mjadala ndani ya bunge hilo kuhusu mambo mchakato mzima wa kusaka Katiba Mpya.
   
  Mhe. Nagu amesema kuwa Hati ya Makubaliano hayo imejengeka katika misingi ya utu, udugu na kuaminiana ambapo Waasisi wa muungano huo hawakupeleka maslahi yao wenyewe binafsi wala kuzingatia suala la mali, bali walizingatia umuhimu na mahitaji  ya muungano kutokana na mambo hayo makuu matatu.
   
  Ameeleza kuwa mambo wanayoyajadili bungeni hapo kwa sasa ndiyo yatatokana na muungano ambao una mfumo bora na muundo bora.Mhe. Nagu amebainisha kuwa wale viongozi wenye kutaka muungano wenye gharama kubwa watawafanya wengine washindwe hapo baadaye.
   
  “Naomba sana tuendelee na kuona kuwa muungano huu ni muhimu nataka niwaambie kwamba Zanzibar ni lango kuu la Jamhuri ya muungano wa Tanzania na lango hili linatuhakikishia usalama wetu na ulinzi wetu kwahivyo na Wazanzibar nao wanufaike na rasilimali za Bara, kwahiyo muungano huu ni muhimu na utanufaisha pande zote mbili mimi sina wasi wasi”, alisema Mhe. Nagu.
   
  Aidha, Mhe. Nagu amegusia suala la usawa wa jinsia kupitia hamsini kwa hamsini katika uwakilishi, ajira na maeneo mengine.Mhe. Nagu ameleza kuwa usawa wa jinsia utajenga jamii nzuri ya Tanzania ikiwemo kuleta heshima pamoja na haki katika jamii hiyo kwani kwa mila na desturi za Waafrika na Watanzania, wanaume hawakupaswa kuwa wamiliki wa kila kitu.
   
  “Akina baba ni Custodians lakini  wakajigeuza wamiliki, tunachotaka waendelee kuwa Custodians na sisi watuone ni wenzao, kwahivyo suala la jinsia halina mjadala, kupitia uwakilishi teundelee na hamsini kwa hamsini na Katiba iseme wazi, mengine yatajitokeza kwenye Sheria ya uchaguzi”. Alisisitiza Mhe. Nagu.
   
  Kuhusiana na suala la ajira na uongozi Mhe. Nagu ameeleza kuwa wanawake zaidi ya asilimia 52% wangepaswa kuwa katika kila eneo lakini hawapo na suala hilo linaleta tofauti isipokuwa mashambani ambapo chakula chote kinachotoka kwa kiasi kikubwa wanaolima ni wanawake.

  0 0

  SEMINA ya Kamata Fursa Jitathimini,Jiamini,Jiongeze inayoendeshwa sambamba na burudani za Fiesta 2014, jana imeendelea kwa kuwapatia dira ya maisha na namna ya kuwafanya wajikwamue kwenye shughuli mbalimbali za kiuchumi wakazi wa Mkoa wa Tabora mjini ndani ya ukumbi wa chuo cha TEKU,kilichopo katikati ya mji wa Tabora.
  Semina hiyo ambayo imeongozwa na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba (pichani juu) ilikuwa ya aina yake, kwani baadhi ya vitu na mbinu alizowapatia wakazi wa Mkoa wa Tabora,wengi wao wameonesha kuvutiwa nayo kutokana na mafunzo,maelekezo na mbinu mbalimbali za kupambana na changamoto zinazowakabili/zitakazowakabili katika miradi yao mbalimbali wanayotarajia kuianzisha ama wamekwishaianzisha.
   Msanii muziki wa kizazi kipya kutoka kundi la Weusi,Niki wa Pili  akizungumza na vijana mbalimbali waliokuwa wamegawanywa katika makundi ili kusikiliza mipango na miradi waliyonayo na namna wanavyoiendeleza,lakini pia Washiriki hao walielezwa namna ya kujikwamua na changamoto wanazokumbana nazo katika kuendeleza miradi yao,ikiwamo na namna ya kujitafutia soko ,jambo ambalo Washiriki hao wamekiri wazi kuwa ndio changamoto yao kubwa katika shughuli zao za ujasiliamali.
    Meneja wa Maxcom Africa, ‘Max malipo’,  Bernard Munubi  akiwa katikati ya vijana akiwaeleza namna ya kufanikiwa katika shughuli zao kimaendeleo na pia kuwapatia mbinu za kupambana na changamoto na hatimae kuelekea kwenye kilele cha mafanikio .Bernad pia aliwaeleza washiriki hao kwa wale ambao wanafikiria kuanza miradi ya ujasiliamali,kwamba si vibaya wakaanza kujaribu kujitafutia maendeleo kupitia mashine za Max Malipo na kujionea wenyewe namna zinavyoweza kusaidia kuondokana na umaskini kwa kiasi kikubwa miongoni mwao.Mnubi alisema kuwa mpaka sasa mashine hizo zimewaletea mafanikio makubwa ya kiuchumi watu wengi.
   Mmoja wa Wajasiliamali kutoka mjini Tabora ,Dada Flora Zakaria ambaye amejiunga kwenye moja ya kikundi kinachofanya shughuli mbalimbali kupitia kikundi chao kiitwacho JACANA Natural Products,akionesha aina ya sabuni zilizotengenezwa na kikundi chao,ambapo pia kikundi hicho hujishughulisha na utengenezaji wa vipodozi vya asili kwa akina mama pamoja na mafuta ya aina mbalimbali.Flora alieleza kuwa wamekuwa wakijitahidi kutengeneza bidhaa mbalimbali lakini changamoto yao kubwa imekuwa ni namna ya kupata soko la kuziuza bidhaa zao.
   Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha VETA wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikichambuliwa na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji kutoka Clouds Media Group,Bwa. Ruge Mutahaba (hayupo pichani).Ambapo washiriki wa semina hiyo waliunda vikundi na kubainisha wana miradi gani ama  wanatarajia kuanza kufanya miradi gani,ili kusaidia kutatua vikwazo na kutoa miongozo kwa namna moja ama nyingine.
   Niki wa Pili akifafanua jambo kwa baadhi ya Washiriki wa Semina hiyo ya Fursa,ambayo imekuwa ikiwavutia watu wa rika mbalimbali wakiwemo vijana kwa wazee.
   Pichani juu na chini ni washiriki wakifuatilia yaliyokuwa yakijadiliwa kwenye semina ya Fursa na wengine waliweza kuandika jambo lolote waliloliona lina manufaa kwao.
   Sehemu ya Washirikiwa semina ya Fursa wakiwa ndani ya ukumbi wa Chuo cha TAKE wakifautilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo .
   Mtangazaji wa Clouds FM kupitia kipindi cha Jahazi,Mdau Mussa akizungumza na wakazi wa mjii wa Tabora waliofika kwenye semina ya Fursa,iliyofanyika kwenye ukumbi wa chuo cha TEKU mjini Tabora.
  Baadhii ya Washiriki wakitoka nje ya ukumbi baada ya semina ya Fursa kuisha.

  0 0


older | 1 | .... | 363 | 364 | (Page 365) | 366 | 367 | .... | 1897 | newer