Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live

WAREMBO MISS TANZANIA 2014 WAWASILI KAMBINI, KANDA YA ZIWA WAENDESHA GARI YAO HADI DAR

$
0
0
Na Father Kidevu Blog
Wanyange 30 wanao wanbia taji la Redd's Miss Tanzania 2014 leo wameingia kambini tayari kwa safari ya fainali za Miss Tanzania 2014 zitakazo fanyikia mapema mwezi Oktoba jiji Dar es Salaam.

Warembo hao waliowasdili kwa muda tofauti kuanzaia saa 12 alfajiri ya leo na kupokelewa na waandaaji wa Miss Tanzania katika hoteli ya JB Belmont iliyopo katikati ya jiji la maraha la Dar. 

Warembo kutoka Kanda ya Ziwa walitia fora pale warembo hao walipowasili kambini hapo wakiwa ndani ya gari ya Mshindi wa Kanda ya Ziwa ambayo alizawadiwa hivi kjaribuni katika shindano lao.
 Warembo wakiwasili kambini
 Warembo wa Kanda ya Ziwa wakiteremka katika gari lao baada ya kuwasili na inaelezwa waliendesha kutoka jijini Mwanza.
 Warembo wa KJanmda ya Ziwa wakijiandikisha baada ya kuwasili kambini.
 Warembo wakielekea chumba cha mkutano.
 Warembo wakiwa katika chumba cha semina ambapo maelezo mbalimbali ya ka,mbi yao yalitolewa.
 
  Warembo wakiwa katika chumba cha semina ambapo maelezo mbalimbali ya ka,mbi yao yalitolewa.
 Wadhamini wakijitambulisha kwa warembo na wanahabari.
 Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga 'Anko' (kushoto) akiteta jambo na Katibu wake Bosco Majaliwa 'Mshua'.
Chakula cha mchana kwa warembo.

TANGAZO LA MSIBA WA MZEE IDRISA KILANGI

$
0
0
Bwana Mfaume Kilangi wa Tuangoma Marela-Kigamboni Jijini Dar es Salaam anasikitika kutanga kifo cha baba yake mnzazi MZEE IDRISA KILANGI  (pichani) kilichotokea alfajiri ya kuamkia leo jijini Dar es Salaam. Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa mtoto wa Marehemu, Mfaume Kilangi Marela Tuangoma jirani na Nyumba za NSSF.

Mwili wa marehemu unataraji kusafirishwa kesho asubuhi saa 3:00 kwenda Iringa mjini kwa Mazishi.

Habari ziwafiukie Ndugu Jamaa na Marafiki wote wa Familia ya Mzee Kilangi, popte pale alipo. 

Enzi za Uhai wake Marehemu alikuwa Mkurunzi Mkuu wa Agrofocus, Mjumbe wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC) pia amewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wasindikaji Korosho Tanzania (CPAT), Rais wa Mpito wa African Cashew Alliance (ACA). 

MHE. LAZARO NYALANDO, CASSIM MGANGA WAWASILI KUHUDHURIA TAMASHA LA UTALII NA MIAKA 4 YA VIJIMAMBO

$
0
0
Mhe. Lazaro Nyalandu, Waziri wa Maliasili na Utalii akipokewa na Afisa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Suleiman Saleh mara tu alipowasili katika uwanja wa kimataifa wa Dulles kwa ajili ya kuhudhulia tamasha la Utalii na miaka 4 ya Blog ya Vijimambo litakalo fanyika Jumamosi Sept 13, 2014. Kushoto ni msaidizi wa Waziri Bwn. Iman Nkuwi.
 
Msanii wa kizazi kipya Cassim Mganga akipiga picha na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu walipokutana kwenye jengo la Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani ulipo jijini Washington, DC.
 Msanii wa kizazi kipya Cassim Mganga akipata picha za kumbukumbu nje ya mjengo wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani
 Cassim Mganga akipata picha ya pamoja na Afisa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Bwn. Swele.
 Msanii wa Bongo Flava Cassim Mganga akipata picha ya pamoja na wadau wanao tangaza Utalii wa Tanzania nchini Marekani.
 Cassim Mganga akisalimiana na Mhe. Liberata Mulamula Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani.
 Mwanamuziki wa kizazi kipya Cassim Mganga akipata picha ya kumbukumbu na Mwambata wa jeshi Ubalozi wa Tanzani nchini Marekani na Canada, Kanali Adolph Mutta.
 Mwanamuziki wa kizazi kipya Cassim Mganga akipata picha ya kumbukumbu na Aunty Mercy Dachi.

WAWILI WADAIWA KUPOTEZA MAISHA AJALI YA BASI LA RUKSA LIKITOKEA KIGOMA KWENDA KAHAMA

$
0
0
Basi la Ruksa aina ya Scania lenye namba za usajili  T 273 ACX llililokuwa likItokea mkoani Kigoma kwenda wilayani Kahama mkoani Shinyang'a likiwa limepata ajali katika kijiji cha Kanyonza wilayani Kakonko,mkoani Kigoma ambapo watu Wawili walipoteza maisha papo hapo na wengine 65 kujeruhiwa katika Ajali hiyo ya Septemba 08,2014,majira ya saa Sita mchana
Pichani juu na chini ni Jeshi la polisi wilaya ya Kakonko lilifika eneo hilo na kuwachukuwa waliojeruhiwa  na kuwapeleka katika hospitali ya wilaya  kwa ajili ya matibabu.


Taswira ya Basi hilo la Ruksa likiwa eneo la Ajali ambapo mashuhuda wanasema chanzo cha ajali kilisababishwa na mwendo kasi.

Pichani ni Baadhi ya Majeruhi wa ajali hiyo wakiwa wodini  katika hospitali ya wilaya ya Kakonko kwa ajili ya matibabu.

KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AANZA ZIARA YAKE MIKOA YA PWANI,TANGA NA IRINGA

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Kata ya Kimanzichana leo wakati alipoanza Ziara yake ya mikoa ya Pwani ,Tanga na Iringa Ikiwa ni kuimarisha Chama na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2010 huku akihimiza wananchi kushiriki katika shughuli za kujiletea maendeleo katika maeneo yao, Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa Itikadi na Uenezi na leo amefanya shughuli mbalimbali katika ziara hiyo. (PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MKURANGA -PWANI)2 
Mbunge wa jimbo la Mkuruanga na Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi Mh. Adama Malima akizungumza na wananchi katika kijiji cha Mkuranga wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata hiyo leo.3 
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mh. Mercy Silla akwahutubia wananchi wa kata ya Kimanzichana kwenye mkutano wa hadhara leo.5 
8 
Baadhi ya wakuu wa wilaya za mkoa wa Pwani kutoka Katikati ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Mh. Ahmed Kipozi16 
Mmoja wa viongozi wa CCM wilaya ya Mkuranga Bi Agricola akiwa katika mkutano huo

NSSF YADHAMINI PAMBANO LA SIMBA NA NDANDA FC

$
0
0
NSSF  kupitia mpango wake wa Wakulima Scheme yadhamini mechi ya kujipima nguvu kati ya Simba ya Dar es Salaam na Ndanda FC ya Mtwara  kwenye uwanja wa CCM  wa Nangwanda Sijaona na kuhudhuriwa na maelfu ya washabiki wa soka mkoani Mtwara.

Mchezo huo pia ulikuwa ni sehemu ya sherehe  za Ndanda Day ulihudhuriwa na viongozi mbali mbali wakiwemo wa Serikali uliisha kwa matokeo ya timu hizo kutoka suluhu.

NSSF kupitia mpango maalum wa wakulima schemes wenye lengo la kuandikisha na kuhudumia wakulima kwenye mfuko ya hifadhi ya jamii nchini ili kuwawezesha wakulima wote nchini wawe kwenye mfuko wa huo  kupata pensheni ya uzeeni pindi watakapo fikisha umri wa miaka 55 na kuendelea wakulima  hao wataweza kulipwa penshion zao hadi watakapo fariki.

Mpangu huu unamwezesha mkulima kupitia chama cha wakulima AMCOS kuweza kupata mkopo na taarifa muhimu kuhusu wakulima,wakulima wanachama wa NSSF wanajiunga bure na kuchangia kuazia shilingi 20,000 na kuendelea.

Aidha mpangu huu unampa mkulima nafasi pekee ya kulipa kwa msimu wa mavuno yaani msimu wa mavuno anaweza kulipia kwa mwaka mzima, miezi anayoweza lipia, lakini pia wakulima wanaweza lipia baada miezi iliyopitilizia bila malipo msimu wa mavuno.

NSSF likiwa ni shirika pekee lenye kuwapa huduma ya afya  bure wanachama na kuwawezesha wanachama kutoyumba kiuchumi kwa sababu za gharama za matibabu kwenye familia.

NSSF linawahudumia familia ya mwanachama kwa kuwapa matibabu bure watoto wanne mwanachama na  mwenza.matibabu haya wanapata pia wakulima wanaojiandikisha kwenye mpango huu wa SHIB wa  NSSF na kuwawezesha kuokoa vipato vyao ambavyo vingetumia kwenye matibabu.

NSSF mkoa wa mtwara unampango wa kuandikisha wanachama 63,000 kutoka kwa wakulima wa vijiji na wilaya zote mkoani mtwara ambazo ni Tandahimba,Nanyumbu,Masasi ,Nachingwea,Newala,Mtwara Vijijini ambao wengi ni wakulima wa  zao korosho.

Pia kwa akina mama wanapata mafao ya uzazi,kabla na baada ya kujifungua.aidha wakuliwa wataweza kupata mikopo kupitia SACCOS zao na kuwawezesha kununua mbolea,madawa ya kuulia wadudu,pembejeo,dhana mbali mbali za kilimo ili kujiinia kiuchumi kupitia NSSF SACCOS Loans.

Ofisi ya NSSF Mkoa wa Mtwara umeshatoa jumla ya shilingi Bilion  1.75 kwa SACCOS zilizokidhi vigezo na kuwainua kimaisha wajasiriamali, wakulima na wafanyakazi.
 Wachezaji  wa  Simba na Ndanda FC wakiingia Uwanjani wakati wa mchezo wa maalum wa kusherehekea Ndanda Day uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara  na kudhaminiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kupitia mpango wake wa Wakulima Scheme. Timu hizo zilitoka suluhu. (Na Mpiga Picha Wetu)
 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali mstaafu Joseph Simbakalia akisalimia na timu ya Ndanda FC kabla ya mchezo wao na timu ya Simba uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali mstaafu Joseph Simbakalia akikagua timu ya Simba wakati wa mchezo wa kirafiki na timu ya Ndanda FC uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Kikosi kamili cha timu ya Simba kilichopambana na Ndanda FC.
Kikosi cha Ndanda FC kikiwa klatika picha ya pamoja kabla ya pambano lao na Simba.
Wachezazaji wa Simba na Ndanda wakichuana katika uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Mashabiki wa soka wakifuatilia pambano la Simba na Danda FC.

WASHINDI TUZO ZA HABARI ZA TANAPA 2013 WAENDELEA KUJIFUNZA MAENEO YA UTALII AFRIKA KUSINI

$
0
0
 Washindi wa Tuzo za Habari za TANAPA 2013 waliweza kufika hadi katika Hifadhi ya Taifa ya Pilanesberg ili kujionea wanyama mbalimbali. Kutoka Kushoto ni Mtanzania Peter Masika anayeishi Johannesburg, Vedasto Msungu (ITV), Pascal Shelutete(Meneja Mawasiliano TANAPA) na Gerald Kitabu wa The Guardian.
 Mwanahabari Vedasto Msungu wa ITV (kushoto) na David Rwenyagira (Radio 5) walikuwa miongoni mwa wanahabari waliofika nje ya Jengo la Mahakama Kuu ya Pretoria ambapo ilikuwa siku muhimu ya utoaji hukumu kwa mwanariadha Oscar Pistorius aliyeshitakiwa kwa makosa ya kumuua mpenzi wake kwa silaha. Unayoyaona hapo nyuma ni magari maalum ya urushaji tukio hilo moja kwa moja katika vyombo mbalimbali vya habari duniani(OB Van) na mahema meupe ni Kambi iliyopigwa na wanahabari hao kwa ajili ya kufuatilia tukio hilo muhimu.
Wanahabari Vedasto Msungu na David Rwenyagira walipata nafasi ya kumhoji raia huyu wa Afrika Kusini juu ya maoni yake kwa hukumu iliyotarajiwa kutolewa.


WAZIRI MKUU ATOA SULUHU KIWANDA CHA CHAI MPONDE

$
0
0
WAZIRI MKUU ATOA SULUHU KIWANDA CHA CHAI MPONDE
*Ataka iundwe timu ya watu wachache kusimamia kiwanda
*Amtaka mwekezaji kukubali kufanya kazi na timu ya Serikali
*Asema dawa ni CAG kufanya ukaguzi ili kupata picha halisi


WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewataka Wakala wa Wakulima Wadogo wa Chai pamoja na Bodi ya Chai nchini waangalie uwezekano wa kuunda timu ya watu wawili au watatu itakayosimamia mwenendo wa kiwanda cha chai Mponde, kilichopo wilayani Lushoto mkoani Tanga.

Waziri Mkuu ambaye aliwasili jijini Tanga jana asubuhi (Jumamosi, Septemba 13, 2014) akitokea Dodoma, alipokea taarifa fupi ya mgogoro wa kiwanda hicho kabla ya kuzungumza na wakulima, wadau wa zao la chai na viongozi wa mkoa na wizara kadhaa kwenye mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga.

“Wakala wa Wakulima pamoja na Bodi ya Chai itabidi watusaidie kuunda timu kwa sababu tunahitaji kuwa na jicho la Serikali ndani ya kiwanda... tunahitaji watu wenye uzoefu mkubwa na mambo ya chai ili wasimamie uendeshaji wa kiwanda pindi kitakapoanza kazi,” alisema.

“Vilevile mwekezaji itabidi akubali kufanya kazi na timu ya Serikali ili tuweze kujua kwa leo kiwanda kiko katika hali gani na tukitaka kukifungua ni lazima tufanye nini,” aliongeza.

Waziri Mkuu alisema timu hiyo kwa kushirikiana na mwekezaji hawana budi kuandaa mpango-kazi wa miaka miwili hadi mitatu wa kufufua kiwanda ili uzalishaji wa chai ufikie pazuri. “Kiwanda wakati kinabinafsishwa kilikuwa na uwezo wa kusindika kilo 20,000 za majani ya chai lakini kilikarabatiwa na kufikisha uwezo wa kusindika kilo 120,000 kwa siku. Sasa tuangalie uwezekano wa kuongeza uzalishaji kwani hapo tutaweza pia kuongeza mavuno kwa wakulima wetu,” alisema.

Alisema ili kuweza kusonga mbele, itabidi Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) aende kufanya ukaguzi kwenye kiwanda hicho ili kuweza kutoa picha halisi ya kiwanda hicho kwa sababu Serikali ina hisa.

Kiwanda cha Chai cha Mponde kinamilikiwa na Chama cha Wakulima wa Chai cha UTEGA (Usambara Tea Growers Association) ambacho kilitafuta mwekezaji ambayo ni Kampuni ya Chai ya Lushoto (Lushoto Tea Company). Wakulima wa Chai walikifungia kiwanda hicho kisifanye kazi kwa madai kuwa walikuwa hawalipwi walipo kwa wakati, wamiliki kutumia lugha chafu,

Baada ya kusikiliza pande zote, Waziri Mkuu alikubaliana na rai iliyotolewa na pande hizo kwamba kuna haja ya kufungua kiwanda hicho ambacho kilifungwa tangu Mei 26, 2013 ili kuwasadia wakulima wapate soko la chai lakini pia waweze kujikimu mahitaji yao.

Mapema, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Bibi Chiku Gallawa alisema mkoa wa Tanga ulijipanga kukuza kiwango cha ukusanyaji mapato ili kuendana na mpango wa Serikali wa matokeo makubwa sasa lakini kufungwa kwa kiwanda hicho, kumeshusha pato la mtu mmoja mmoja, pato la mkoa na pato la Taifa kwa ujumla.

“Changamoto kubwa ambayo tumekabiliana nayo kwa kipindi chote hiki ambacho kiwanda kilikuwa kimefungwa, ni kwa wananchi kushindwa kuuza chai yao,” aliongeza.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Bw. Majjid Mwanga akitoa taarifa mbele ya Waziri Mkuu alisema kiwanda cha Mponde kilikuwa na uwezo wa kusindika kilo 70,000 za majani mabichi ya chai kwa siku lakini hadi kinafungwa uwezo huo ulishuka na kufikia kilo 25,000 kwa siku.

Alisema idadi ya wakulima walioathirika kutokana na kufungwa kwa kiwanda hicho ni 3,908 ambao walikuwa wakilima hekta 1,951. “Bei ya kilo moja ya chai ilikuwa ni sh. 225/- wakati wastani wa pato la mkulima kwa nusu hekta ilikuwa ni sh. 180,000/- kwa mwezi lakini kwa sasa limeshuka na kufikia sh. 90,000/- kwa mwezi kwa nusu hekta hiyo hiyo,” alisema.

Alisema zaidi ya tani 1,800 zimeshindikana kusindikwa na hivyo kuikosesha Halmashauri yao kiasi cha sh. milioni 21.6/- ambazo zilikuwa zikilipwa kama ushuru kwa kila kilo moja iliyokuwa ikiuzwa. “Wakulima kwa ujumla wao wamepata hasara ya sh. milioni 370.8/-” alisema.

Mkutano huo pia ulihudhuriwa pia na Mawaziri wa OWM-TAMISEMI; Kilimo, Chakula na Ushirika; Viwanda na Biashara, Wabunge wa Mlalo, Bumbuli na Lushoto; viongozi wa Mkoa na Halmashauri za Korogwe, Lushoto na Bumbuli, viongozi wa UTEGA na mwekezaji, ambaye ni mmiliki wa kiwanda cha Lushoto Tea Company.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
S. L. P. 3021,
DAR ES SALAAM.
JUMAPILI, SEPTEMBA 14, 2014

Wabunge wanawake wasisitiza ajenda ya hamsini kwa hamsini kutokakwepeka katika Katiba Mpya ijayo.

$
0
0
 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Margareth Sitta akifungua semina ya Wanawake iliyohusu kuwawezesha wanawake katika masuala ya uongozi, utatuzi wa migogoro pamoja na harakati za uchaguzi iliyofanyika leo 13 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Pindi Chana akiwahutubia baadhi ya wanawake na wanaume waliohudhuria semina maalum iliyohusu kuwawezesha wanawake katika masuala ya uongozi, utatuzi wa migogoro pamoja na harakati za uchaguzi iliyofanyika leo 13 Septemba, 2014 mjini Dodoma.

Mwakilishi wa Shirika la Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) akichangia mada wakati wa semina ya wanawake iliyofanyika leo 13 Septemba, 2014 ambayo ikihusu iliyohusu kuwawezesha wanawake katika masuala ya uongozi, utatuzi wa migogoro pamoja na harakati za uchaguzi iliyofanyika leo 13 Septemba, 2014 mjini Dodoma.


Baadhi ya wajumbe wanawake wa Bunge Maalum la Katiba wakifuatilia uwasilishwaji wa mada toka kwa viongozi wakati wa semina hiyo. (Picha zote na Edwin Mujwahuzi)
 
Na Benedict Liwenga, MAELEZO-Dodoma.
Katika juhudi za kuleta usawa wa kijinsia na kuinua hadhi ya wanawake, Serikali imefanya jitihada kubwa katika masuala ya kiuchumi, kisiasa na kijamii licha ya kuwepo na changamoto mbalimbali katika jitihada hizo
Hayo yamesemwa 13 Septemba, 2014 na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Pindi Chana wakati wa semina iliyohusu masuala ya kuwapa nyenzo ama uwezo wananawake waweze kushiriki vizuri katika maeneo mbalimbali yanayowakilisha wanawake huku wakiungwa mkono na wanaume.
Mhe. Chana amesema kuwa baadhi ya watu nchini wamekuwa na dhana tofauti huku wakiona wakipotezewa muda pindi mambo yoyote yanayowahusu wanawake yanapozungumzwa wakisahau kuwa ili taifa liweze kufika mahali pazuri na kuwa na maisha bora kwa kila Mtanzania hakunabudi kulitazama kundi hilo la wanawake ambalo ni muhimu.
Mhe. Chana ameeleza kuwa asilimia 51% ya Watanzania ni wanawake ambao wanachangia nguvu kazi kwa upande wa kilimo kwa asilimia 45 ya pato la Taifa, pia asilimia 25 wako katika ajira iliyo rasmi lakini wengi wako katika sekta isiyo rasmi.
“Asilimia 34% pia ya wanavyuo kutokana na takwimu inaonyesha kwamba ni wanawake, kwahiyo ajenda ya wanawake haikwepeki”, alisema Mhe. Chana.
Akizungumzia kuhusiana na masuala ya mchakato wa kusaka Katiba Mpya, Mhe. Chana amesema kuwa katika majadiliano yanayohusu Katiba, ajenda ya wanawake pia haikwepeki.
Mhe. Chana aliongeza kuwa endapo wanawake nchini watawezeshwa basi taifa zima litakuwa limewezeshwa kwani watu wengi waliopata mafanikio ni kutokana na wanawake kutoa malezi bora katika kulea watoto pindi wanapozaliwa hadi kupata elimu.
Aidha, Mhe. Chana amesisitiza juu ya wanawake kushirikishwa katika vyombo vya maamuzi ili kuongeza hali ya uchumi kwa wanawake, hali ya kijamii ya wanawake na ya kisiasa kwa wanawake hao.
“Lazima tuwepo kwenye vyombo vya maamuzi kwani ndiko tunapopata haki zetu kwani huko pia ndiko tunapoweka bajeti ya serikali kuu, bajeti ya serikali za mitaa, kwahiyo tunaanza na vyombo vya maamuzi”, alisisitiza Mhe. Chana.
Naye Mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Bi. Usu Mallya amesema kuwa Tanzania ina wanawake wenye sifa, na uwezo na maarifa kwenye maeneo yote kuanzia, udaktari, uhasibu, Wahandisi yakiwemo na maeneo mengine.
Ameongeza kuwa, ajenda ya kufikia hamsini kwa hamsini kwa wanawake haina mjadala, hivyo wanawake wana haki ya kuhusishwa katika masuala ya ungozi kama ilivyo kwa wanaume.
“Mwanamke kwenye uongozi ni lazima aweze kuliko mwanaume, anatakiwa ajiwekee mikakati yake mwenyewe ya kujihudumia (selfcare) ili kuwa na muda wetu wenyewe”, alisema Bi. Mallya.
Bi. Mallya aliongeza kuwa wanawake wanapaswa kutambua kuwa ajenda inayohusu mapambano ni ajenda ya muda mrefu ndani ya maeneo yao ya uongozi.
Bi Mally alisisitiza kuwa, wanawake wajitahidi kuwa wanasiasa kwenye vyama vya siasa, wawe wabunge pia wawe viongozi kwenye taasisi za umma na binafsi ili kufanikisha suala lao la hamsini kwa hamsini.

KINANA AZIDI KUELIMISHA WANANCHI UMUHIMU WA MPANGO WA AFYA YA JAMII

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Kimnzichana Kusini ambapo alisisitiza kuwa kila familia yapaswa kujiandikisha katika mpango wa afya ya jamii kwani itasaida sana kupunguza gharama za matibabu.(Picha na Adam Mzee).

RAIS KIKWETE APOKEA UJUMBE TOKA KWA RAIS WA SUDANI YA KUSINI MHE SALVAR KIIR JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete amepokea ujumbe maalumu toka kwa Rais Salvar Kiir Mayardit wa Sudani Kusini ulioletwa na mjumbe malumu Jenerali James Kok Ruea Jumamosi September 14, Ikulu jijini Dar es salaam. Mjumbe huyo aliongozana pia naMkuu wa Kituo cha Martti Ahtisari (Martti Ahtisari Centre) kwa nchi za Afrika chini ya Jangwa la Sahara, Bw. Itonde Kakoma.Picha na IKULU

CANADIAN PRIME MINISTER STEPHEN HARPER AND AGA KHAN OPEN THE ISMAILI CENTRE TORONTO AND AGA KHAN MUSEUM

$
0
0
11 DSC_0460 (PM Harper and HH the Aga Khan waving to crowds outside the Ismaili Centre, Toronto - AKDN Zahur Ramji)
PM Harper of Canada and HH the Aga Khan waving to crowds outside the Ismaili Centre, Toronto - AKDN / Zahur Ramji).

The Right Honourable Stephen Harper, Prime Minister of Canada, and His Highness the Aga Khan formally opened the Ismaili Centre Toronto and Aga Khan Museum today. These projects, which are initiatives of the Aga Khan, the 49th hereditary Imam of the Shia Ismaili Muslims and founder and Chairman of the Aga Khan Development Network, are intended to foster knowledge and understanding both within Muslim societies and between these societies and other cultures.

Speaking at the opening ceremony of the Ismaili Centre, His Highness the Aga Khan saluted the many leaders, volunteers and staff who have made possible the completion of these new institutions, including the Prime Minister, and many members of government at the federal, provincial and municipal levels. These spaces “will be filled with sounds of enrichment, dialogue and warm human rapport, as Ismailis and non-Ismailis share their lives in a healthy gregarious spirit," he remarked.

Prime Minister Harper commented that the site will be “a source of inspiration, spiritual renewal and cultural awareness,” not only for Torontonians, but for all visitors. The Prime Minister paid a special tribute to the Aga Khan’s vision of Islam, which “stresses its social traditions of peace, tolerance and pluralism."

“The decision to establish this significant initiative in Canada reflects the deep and longstanding partnership between the Imamat and Canada,” said the Prime Minister. 
09 ZR4_0113 (PM Harper and HH the Aga Khan at the Ismaili Centre, Toronto - AKDN Zahur Ramji)
PM Harper of Canada and HH the Aga Khan at the Ismaili Centre, Toronto - photo:AKDN/Zahur Ramji).

Following the ceremony, Prime Minister Harper and His Highness the Aga Khan, as well as Prince Amyn Aga Khan, Vice-Chair of the Museum’s Board of Directors, and the Honourable Shelly Glover, Minister of Canadian Heritage and Official Languages, officiated over the opening ceremony of the Aga Khan Museum.

“I believe strongly that art and culture can have a profound impact in healing misunderstanding and in fostering trust even across great divides," said Prince Amyn. “This is the extraordinary purpose, the special mandate, to which this Museum is dedicated. In its role to reveal and to stimulate dialogue between different cultures, the Aga Khan Museum will continue a long history of cultural sharing between Islam and the West.”


 
The Ismaili Centre and the Aga Khan Museum are situated within the 6.8-hectare landscaped park designed by Vladimir Djurovic of Lebanon. This beautiful new green space for the public, which will be known as the Aga Khan Park, is expected to open next year. Japanese architect Fumihiko Maki designed the Aga Khan Museum, while Indian architect Charles Correa designed the Ismaili Centre. The Canadian firm Moriyama & Teshima are the architects of record and are responsible for integrating all aspects of the project.
05 GOT_6307 (HH the Aga Khan and PM Harper unveil a plaque at the opening of the Aga Khan Museum as Prince Amyn Aga Khan and Minister Glover look on  - AKDN Gary Otte)
HH the Aga Khan and PM Harper unveil a plaque at the opening of the Aga Khan Museum as Prince Amyn Aga Khan and Minister Glover look on - AKDN / Gary Otte).

The Aga Khan Museum is the first museum in North America dedicated to the arts of Muslim civilisations. Through its Permanent Collection, performing arts and educational programmes and roster of temporary exhibitions, it will welcome the full spectrum of public engagement and serve as a vibrant educational institution.

The Ismaili Centre incorporates spaces for social and cultural gatherings, intellectual engagement, and spiritual reflection. Together, these global institutions will contribute to a better understanding among different communities and cultures. The establishment of these institutions in Toronto reflects the Aga Khan’s longstanding relationship with Canada and his appreciation for the country’s commitment to pluralism and cultural diversity.

The Aga Khan Museum will be opened to the public on 18 September 2014. It is dedicated to presenting an overview of the artistic, intellectual, and scientific contributions that Muslim civilisations have made to world heritage. Housed in a unique building designed by Pritzker Laureate Fumihiko Maki, the Museum's Permanent Collection of over 1,000 objects includes masterpieces that reflect a broad range of artistic styles and materials. These portraits, textiles, manuscripts, manuscript paintings, ceramics, tiles, medical texts, books and musical instruments represent more than ten centuries of human history and a geographic area stretching from the Iberian Peninsula to China.

For more information, please visit www.agakhanmuseum.org
The Ismaili Centre Toronto, designed by renowned Indian architect Charles Correa, is part of a network of Centres – located in Vancouver, London, Lisbon, Dubai and Dushanbe – which host programmes that stimulate the intellect, encourage dialogue and celebrate cultural diversity. For more information, please visit www.theismaili.org/ismailicentres

08 DSC_0240 (HH the Aga Khan shows artefacts at the Aga Khan Musem to Minister Shelly Glover - AKDN Zahur Ramji)
HH the Aga Khan shows artefacts at the Aga Khan Museum to Minister Shelly Glover - AKDN Zahur Ramji).
Untitled 1
His Highness the Aga Khan and Prime Minister Harper on the terrace of the Ismaili Centre with the new Aga Khan Museum in the background - AKDN Gary Otte.
 

WAREMBO MISS TANZANIA WAJIFUA GYM KUIWEKA MIILI YAO SAFI

$
0
0
 Warembo wanaoshiriki shindano la Redd's Miss Tanzania 2014 leo wameingia siku ya pili ya kambi yao jijini Dar es Salaam na baada ya semina asubuhi na mapumziko ya mchana jioni hii wamefanya mazoezi katika chumba maalum cha mazoezi 'Gym', ungana na mpigapicha wa Father Kidevu Blog katika picha mbalimbali za warembo hao katika kambi yao.

YANGA YAIKAMUA AZAM FC 3-0

$
0
0
Mshambuliaji wa Yanga Mrisho Ngasa, kushoto akimtoka  beki wa Azam FC, Erasto Nyoni katika mchezo wa Ngao ya Hisani uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanya imeshinda 3-0.
 
Kikosi kamili cha Yanga kilichoifunga Azam FC 3-0 katika mchezo wa Ngao ya Hisani leo.
Kikosi cha Azam FC.

TASWA FC SAFARINI IRINGA, ARUSHA, TANGA NA MTWARA

$
0
0
Yafuatayo ni majina yaliyotangazwa na bench la ufundi la timu ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini (Taswa FC) ambayo itafanya ziara mkoani Iringa kuanzia Oktoba 3. Majina hayo yamepitishwa na kikao cha uongozi wa timu na kuamua kuyaweka hadharani kwa sababu mbalimbali.
MAJINA YA WACHEZAJI
1.       Mwarami Seif
2.       Mbozi Katala
3.       Edward Mbaga
4.       Elius Kambili
5.       Wilbert Molandi
6.       Eddo Kumwembe
7.       Faustine Felician
8.       Julius Kihampa
9.       Zahoro Mlanzi
10.   Fred “Chuji” Mbembela
11.   Deogratius “Super Deo” Maganga
12.   Athumani  Jabiri
13.   Sweetbert Lukonge
14.   Martin Peter
15.   Muhidin Sufiani
16.   Gulle Mandago
17.   Saleh Ally
18.   Mohamed Akida
19.   Peter Mchome
20.   Deus Saleh
21.   Ally
22.   Hussein Omary
 
WAKUU WA BECNCHI LA UFUNDI:
 
23.   Ally Mkongwe
24.   Saidi Seif
               UONGOZI:
25.   Majuto Omary-Mwenyekiti-Mkuu wa Msafara
26.   Salum Jaba-Makamu

Serikali kuanza zoezi la kuhakiki vyama vya kijamii

$
0
0
Frank Mvungi.
Serikali imedhamiria kuanza zoezi la kuhakiki vyama  vya kijamii ili kuboresha huduma zinazotolewa na vyama hivyo hapa nchini tangu kuanzishwa kwake.Hayo ya mesemwa leo Jijini Dar es salaam na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi Bw. Isack Nantanga wakati wa mkutano na waandishi wa habari .
 
“Katika  kuboresha huduma na usimamizi wa vyama vya kijamii, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imeandaa zoezi maalumu litakalowezesha kuhakiki upya vyama vya kijamii vilivyopo hapa nchini.” Alisema Nantanga.
 
Akifafanua Nantanga amesema pamoja na mambo mengine, zoezi hilo ambalo litaanza rasmi mwezi  Oktoba 2014, linalenga kuvifuta kutoka katika daftari la Msajili vya Vyama vya Kijamii vyama ambavyo havina  tena sifa ya  kuendelea kuwa katika daftari hilo.
 
Akizungumzia sababu zinazoweza kupelekea chama kufutwa kutoka katika Daftari la Msajili wa Vyama vya Kijamii  Nantanga alisema ni pamoja na kutolipa ada za mwaka kwa wakati na kutowasilisha kwa Msajili taarifa za kila mwaka za utendaji kazi  wa chama.
 
Sababu nyingine  ni chama kufanya shughuli tofauti na zile zilizoandikishwa katika katiba ya chama husika.
 
Ili kuvishirikisha vyama husika, Wizara wakati wa kuanza zoezi hili itachapicha katika baadhi ya magazeti majina ya vyama vyote vya kijamii vilivyopo katika kumbukumbu za daftari la Msajili wa Vyama vya Kijamii.
 
Baada ya kutangaza majina hayo,Nantanga alisema kila chama cha kijamii kitatakiwa kuhakikisha kuwa kinatekeleza matakwa ya kisheria ya kulipa ada  ya mwaka na kuwasilisha kwa Msajili wa Vyama vya Kijamii taarifa kuhusu utendaji na mapato na matumizi ya fedha ya chama husika kama Sheria inavyotamka.
 
Baada ya  kipindi cha miezi mitatu tangu kutangazwa kwa tangazo hilo, Wizara itaanza kuchukua hatua za kisheria, ikiwa ni pamoja na kukifuta katika daftari la Msajili chama cha kijamii ambacho kitakuwa hakijatekeleza maelekezo hayo.Pamoja na taarifa zitakazopatikana katika zoezi  la uhakiki Nantanga alisema zitawezesha kuanzishwa kwa Kanzi Data ya kisasa ya vyama vya kijamii ambayo itasaidia kuboresha mawasiliano kati ya Msajili Vyama na vyama hivyo.
 
Aidha, baada ya kukamilika kwa zoezi hili, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi itaendelea na zoezi lingine la kukagua vyama vya kijamii katika maeneo mbalimbali ya nchi ili kupata taarifa zaidi kuhusu vyama hivyo.
 
Hadi sasa Daftari la Msajili wa Vyama vya Kijamii linaonyesha kuwepo kwa vyama vya kijamii 9,554 kote nchini,Kati ya hivyo, vyama vya kidini ni 956 na vyama vingine 8,598.
 
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ndiyo yenye jukumu la kusajili na kusimamia uendeshaji wa Vyama vya Kijamii (Civil Societies) hapa nchini kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Kijamii SURA 337 (Societies Act Cap. 337) iliyofanyiwa mapitio mwaka 2002.
 
Vyama vinavyosajiliwa chini ya Sheria hii ni pamoja na vyama vya kidini, vyama vya kitaaluma  na vyama vya starehe na burudani.

KITCHEN PARTY YA DR.HAIKA MHANDO YAFUNIKA DAR

$
0
0
IMG_0794Bi. harusi mtarajiwa Dr.Haika Mhando akiwa tayari kuingia ukumbini katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Banora jijini Daressalaam Jumapili Septemba 13,2014. IMG_0643IMG_0643Mama mzaa chema. IMG_0723 - CopyDada wa bi.harusi Neema Mhando. IMG_0625Dada wa bi harusi Dr.Nandera Mhando. IMG_0729 - CopyDada wa bi.harusi Mchungaji Rebecca Mhando. IMG_0731 - CopyDada wa bi.harusi Netiwe Mhando. IMG_0703Dada wa bi.harusi Empress Elinita Mhando. IMG_0645Mc wa shughuli Mary Mwanyato. IMG_0786Mambo ya wanakamati.

BENKI YA DUNIA NA SERIKALI IKISHIRIKIANA NA WAWEKEZAJI WAKUBWA WA MADINI NCHINI WAZINDUA MRADI WA UCHIMBAJI MADINI KWA WACHIMBAJI WADOGO WADOGO MKOANI GEITA.

$
0
0
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mh,Stephen Masele akizungumza kwenye uzinduzi huo uliovuta hisia za wanakijiji wengi.Naibu Waziri wa Nishati na Madini akizungumza na Wananchi Mkurugenzi Mtendaji wa Geita Gold Mine,Michael Van Anen Mwakilishi Mwandamizi kutoka Benki ya Dunia ambaye pia ni mtaalamu wa madini kutoka idara ya nishati endelevu nchini Marekani,Bwa.Mamadou Barry akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi mkubwa wa uchimbaji madini kwa wachimbaji wadogo wadogo katika kijiji cha Lwamgasa mkoani Geita,hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Nishati na Madini,Mh Stephen Masele.Mradi huo Umefadhiliwa na Benki ya Dunia na Serikali kwa kushirikiana na Wawekezaji wakubwa wakiwemo Geita Gold Mine na African Barrick Gold Mkuu wa Wilaya ya Geita ,Mh.Omary Mangochie akiwakaribisha wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye uzinduzi huo.

Article 19

TAMASHA LA FIESTA 2014 LAPOKELEWA VYEMA NA WAKAZI WA TABORA

$
0
0
Msanii mwingine anaekuja vyema kwenye anga ya muziki wa Bongofleva aitwaye Kadja ambaye anatamba na wimbo wake wa Maumivu niache akiimba pamoja na Linah.
Mkali wa Bongo Hip Hop Farid Kubanda a.k.a Fid Q akikamua vilivyo juu ya jukwaa na la Fiesta.
Msanii wa Bongofleva,Kadja akiimba wimbo wake wa Maumivu niache mbele ya maelfu ya wakazi wa Tabora (hawapo pichani) waliofika kwenye tamasha la Fiesta usiku wa kuamkia leo.
 Ilikuwa buruuudani ya kusambaza upendo wa kweli kwa wakazi wa Tabora ndani ya tamasha la Fiesta
Palikuwa hapatoshi usiku wa kuamkia leo ndani ya uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mjini Tabora,ambapo tamasha la Fiesta lilirindima.
Wasanii chipukizi kutoka Tabora nao walionesha umahiri wao jukwaani
Sehemu ya umati mkubwa wa watu waliofika kulishuhudia tamasha la Fiesta lililofanyika usiku wa kuamkia leo ndani ya uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live


Latest Images