Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46317 articles
Browse latest View live

Naibu Waziri Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii azindua Mfumo wa Uboreshaji wa Upatikanaji wa Dawa na Vifaa tiba mjini Dodoma.

$
0
0
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Mhe. Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akiwahutubia wadau mbalimbali waliohudhuria sherehe ya Uzinduzi Uboreshaji wa Mfumo wa Upatikanaji wa Dawa na Vifaa Tiba kupitia Mzabuni mmoja mkoa wa Dodoma, leo tarehe 11 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Mhe. Balozi Oliver Chave akitoa hotuba yake mbele ya wadau mbalimbali waliohudhuria katika sherehe ya Uzinduzi Uboreshaji wa Mfumo wa Upatikanaji wa Dawa na Vifaa Tiba kupitia Mzabuni mmoja mkoa wa Dodoma, leo tarehe 11 Septemba, 2014 mjini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Rehema Nchimbi akitoa maelezo mazuri kuhusiana na faida ya Uzinduzi Uzinduzi Uboreshaji wa Mfumo wa Upatikanaji wa Dawa na Vifaa Tiba kupitia Mzabuni mmoja mkoa wa Dodoma, leo tarehe 11 Septemba, 2014 mjini Dodoma.

Dkt. Karin ambaye pia ni mdau wa Mfumo wa upatikanaji wa dawa na Vifaa Tiba kupitia Mzabuni mmoja mkoa wa Dodoma akitoa shukurani zake za dhati kwa wadau mbalimbali waliohudhuria sherehe za Uzinduzi wa Mfumo huo leo tarehe 11 Septemba, 2014 mjini Dodoma.

Baadhi ya wadau toka sehemu mikoa mbalimbali wakifuatilia hotuba zikizowasilishwa na viongozi katika sherehe ya Uzinduzi Uboreshaji wa Mfumo wa Upatikanaji wa Dawa na Vifaa Tiba kupitia Mzabuni mmoja mkoa wa Dodoma, leo tarehe 11 Septemba, 2014 mjini Dodoma.


Kikundi cha Ngoma cha mjini Dodoma kikitumbuiza mbele ya mgeni rasmi wakati wa sherehe ya Uzinduzi Uboreshaji wa Mfumo wa Upatikanaji wa Dawa na Vifaa Tiba kupitia Mzabuni mmoja mkoa wa Dodoma, leo tarehe 11 Septemba, 2014 mjini Dodoma.

Baadhi ya Waandishi wa habari wakichukua matukio wakati wa sherehe ya Uzinduzi Uboreshaji wa Mfumo wa Upatikanaji wa Dawa na Vifaa Tiba kupitia Mzabuni mmoja mkoa wa Dodoma, leo tarehe 11 Septemba, 2014 mjini Dodoma.

Wadau wa Mfumo wa upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kupitia mzabuni mmoja mkoa wa Dodoma wakitiliana saini makubaliano wakati wa sherehe ya Uzinduzi Uboreshaji wa Mfumo wa Upatikanaji wa Dawa na Vifaa Tiba kupitia Mzabuni mmoja mkoa wa Dodoma, leo tarehe 11 Septemba, 2014 mjini Dodoma.

(Picha zote na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma)



Jux aachia ‘Sisikii’ redioni

$
0
0
 
Na Andrew Chale
MWANAMUZIKI nyota anayefanya vizuri katika tasnia ya muziki nchini, Juma Mussa ‘Jux’ anayetamba zaidi  na vibao vya ‘Uzuri wako’ na ‘Nitasubiri’, ameachia rasmi wimbo wake mpya wa ‘Sisikii’ katika stesheni mbalimbali za redio. 
 
Akizungumza jijini Dar es Salaam , Jux alisema wimbo huo wa ‘Sisikii’ ameutengeneza kwa Mtayarishaji  Maneke wa AM rekodi, ambao ni zawadi nyingine kwa mashabiki wake wote duniani.
Jux aliwataka kuupokea kwa mikono miwili na wasubiri video ambayo itakuwa ya kiwango cha hali ya juu.
 
“Septemba 9, nimeachia rasmi wimbo wa ‘Sisikii’ katika redio hapa nchini na wadau wangu waoupokee kwa mikono miwili kama nyimbo nyingine ninazotoa, pia wakae mkao wa kuona video ya wimbo huu muda si mrefu,”alisema Jux.
 
Awali Jux amekuwa akiwonjesha mashabiki wake kwenye shoo mbalimbali zinazoendelea nchini kupitia ziara za muziki wa Serengeti Fiesta mwaka huu.

SEKTA ZA MADINI ,UMEME NA KILIMO ZAKUZA PATO LA TAIFA.

$
0
0
 Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bw. Morrice Oyuke (katikati) akizungumza  na waandishi wa habari kuhusu ukuaji wa Pato la Taifa kwa bei ya Soko leo jijini Dar es salaam. Wengine ni Bw. Oswald Ruboha (kulia) Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Sera na Mipango, Wizara ya Kilimo na Dkt. Stephen Kirama (kushoto), Mhadhiri wa Uchumi, Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
 
========  ======  =======
SEKTA ZA MADINI ,UMEME NA KILIMO ZAKUZA PATO LA TAIFA.
Na. Aron Msigwa – MAELEZO
11/9/2014. Dar es salaam.

Sekta ya Kilimo,Uvuvi,  Viwanda , Nishati na Madini zimeelezwa kuwa miongoni mwa sekta muhimu zinazoongoza zaidi katika kuchangia kukua kwa pato la Taifa hadi asilimia 7.4 katika robo ya kwanza ya mwaka 2014.

Kwa mujibu wa taarifa zilizokusanywa kutoka katika vyanzo mbalimbali vya uzalishaji nchini na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kutumia kanuni za kimataifa kukokotoa pato la Taifa zinaonyesha kuwa sekta hizo zimetoa mchango mkubwa wa kukua kwa pato la Taifa  kwa asilimia 7.4 kuanzia mwezi Januari hadi  Machi, 2014 ikilinganishwa na asilimia 7.1 za mwaka 2013.

Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bw. Morrice Oyuke akizungumzia ukuaji wa Pato la Taifa kwa bei ya Soko leo jijini Dar es salaam amesema kuwa Pato la Taifa katika robo ya mwaka 2014 kuanzia Januari hadi Machi limekua kwa asilimia 7.4 kutokana na kukua kwa sekta za Kilimo, Uvuvi, Viwanda, Ujenzi, Umeme na  utoaji wa huduma.

Amesema sekta zilizofanya vizuri katika ukuaji huo ni pamoja na sekta ya uchimbaji wa Madini, mawe na kokoto ambayo imekua kwa asilimia 8.7 ikilinganishwa na asilimia 1.7 za mwaka uliopita kutokana na kukua kwa masoko ya uuzaji ya nje ya nchi.

Ameongeza kuwa sekta uzalishaji wa bidhaa za viwandani imekua kwa asilimia 8.5 kutoka 8.3 huku shughuli za utoaji wa huduma na uchumi zikiwemo za ukarabati wa magari, pikipiki na vifaa vingine vya majumbani zikikua kwa asilimia 8.0 kwa robo ya mwaka 2014.

Bw. Oyuke ameeleza kuwa shughuli za uchukuzi na mawasiliano zimefikia kasi ya ukuaji wa asilimia 16.5 katika kipindi hicho na kuongeza kuwa huduma za hoteli na migahawa zimefikia kasi ya ukuaji wa asilimia 3.0, huku shughuli za uendeshaji wa Serikali zikifikia asilimia 5.1, Elimu asilimia 5.2, huduma za Sfya na  shughuli nyingine zikikua kwa asilimia 4.5.

Aidha, amefafanua kuwa sekta ya umeme katika robo ya mwaka 2014 imekua kwa asilimia 12.6 ikilinganishwa na asilimia 6 ya mwaka uliopita kutokana na kupatikana kwa vyanzo mbadala vya kuzalisha umeme hususan ugunduzi wa gesi nchini ambao umeondoa tatizo la utegemezi wa umeme wa maji katika kuzalisha umeme.

“Kwa kipindi kirefu sekta ya umeme imekuwa na mawimbi kwa kiasi kikubwa , umeme wetu umekuwa wa kutegemea maji ya mvua, baada ya juhudi za Serikali na kugundulika kwa nishati ya Gesi nchini na kupatikana chanzo mbadala cha nishati tatizo hili limeshghulikiwa sasa sekta hii imeimarika” Amesisitiza.

Amesema Tanzania sasa inafanya vizuri kiuchumi katika nchi za Afrika ya Mashariki kwa kuwa ya pili ikifuatiwa na Uganda, Rwanda na Burundi na kuongeza kuwa hali ya amani na utulivu iliyopo nchini inaiweka Tanzania katika nafasi nzuri ya kukua zaidi kiuchumi.

Kwa upande wake mtaalam wa wa Uchumi kutoka Benki Kuu ya Taifa (BOT) Bw. Davidi Kwimbere akifafanua kuhusu hali iliyopo ya ukuaji wa uchumi amesema kuwa imechangiwa na kuongezeka kwa shughuli za uzalishaji .

Amesema sekta ya Kilimo na uzalishaji wa mazao imekua kutokana na matumizi ya mbolea, zana bora za kilimo, mbegu bora, madawa na kufafanua kuwa endapo juhudi zaidi zitaendelea kufanywa na wananchi kwa kuingia katika shughuli mbalimbali za uzalishaji uchumi utaendendelea kuonekana kwa mtu mmoja mmoja.

Amefafanua kuwa maendeleo katika nchi yoyote  yanachukua muda na kutoa wito kwa nchi za Afrika kuendelea kujifunza  na kufafanua kuwa nchi zote zilizopiga hatua kimaendeleo mpaka kufikia asilimia 15 ikiwemo China iliwachukua miaka 20 kuondoa umasikini.

Amesema Tanzania inayo nafasi nzuri kukua kiuchumi kutokana na kuendelea kuimarika kwa miundombinu  na ukuaji wa sekta za ujenzi, Nishati, madini, Viwanda, umeme , kilimo na uvuvi hali inayochangia kuongezeka kwa uwekezaji.

USIMAMIZI WA MAADILI CHUO CHA ELIMU YA BIASHARA (CBE) DAR ES SALAAM WAONGEZA UFAULU

$
0
0
Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) Prof. Emanuel Mjema akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu maadhimisho miaka 50 ya chuo hicho yanayoendelea jijini Dar es salaam.

Na. Aron Msigwa –MAELEZO.

Hatua iliyochukuliwa na uongozi wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) kuendelea kuweka msisitizo katika usimamizi wa maadili kwa wanafunzi imeanza kuzaa matunda kufuatia kuogezeka kwa ufaulu wa masomo kwa wanafunzi wanaosoma chuoni hapo. 

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es salaam na mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) Prof. Emanuel Mjema wakati akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu maadhimisho yanayoendelea ya chuo hicho kutimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake Januari, 1965.

TOVUTI MPYA YA HABARI ZA KIELIMU TANZANIA YAANZISHWA

RAIS ATAKA MSAADA ESRF KUONDOA UMASKINI KWENYE UCHUMI UNAOKUA KWA KASI KUBWA

$
0
0
DSC_0389
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifungua rasmi mkutano mkubwa wa tatu wa ESRF unaozungumzia ukuaji wa uchumi kwa kutumia fursa zilizopo na maendeleo yanayogusa jamii uliofanyika jana jijini Dar katika hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro.
DSC_0251
Meza kuu, Katikati ni mgeni rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya fedha, Prof. Adolf Mkenda, Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez ( wapili kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya ESRF, Philemon Luhanjo (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Hoseana Lunogelo (wa pili kushoto).
DSC_0280
Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Hoseana Lunogelo akisoma taarifa ya taasisi yake mbele ya mgeni rasmi wakati wa mkutano mkubwa wa tatu wa ESRF unaozungumzia ukuaji wa uchumi kwa kutumia fursa zilizopo na maendeleo yanayogusa jamii sambamba na kutimiza miaka 20 ya tasisi hiyo tangu kuanzishwa kwake uliofanyika jana jijini Dar katika hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro.
DSC_0295
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa mkono wa pongezi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Hoseana Lunogelo mara baada ya kusikiliza taarifa ya maendeleo ya ESRF.
DSC_0301
Mwenyekiti wa Bodi ya ESRF Philemon Luhanjo, akizungumza neno fupi kabla ya kumrabisha mgeni rasmi Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufungua rasmi mkutano huo.

DSC_0257
Pichani juu na chini ni Baadhi ya wawakilishi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, mabalozi, taasisi mbalimbali za serikali waliohudhuria mkutano huo uliofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro jijini Dar.


DSC_0349
DSC_0455
Mkurugenzi wa Programu wa ESRF ambaye pia ni Mratibu wa Mradi wa taarifa ya maendeleo ya watu nchini Tanzania (THDR), Dr. Tausi Kida akifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa mkutano huo.
DSC_0393
Mjumbe wa Bodi ya wadhamini ESRF, Prof. Sylvia Temu akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi.
DSC_0444
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza kwa niaba ya Umoja wa Mataifa wakati wa mkutano huo. Kulia ni Gelase Mutahaba kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Kushoto ni Prof. Bertil Tungodden kutoka nchini Norway na Mjumbe wa Bodi ya wadhamini ESRF, Prof. Sylvia Temu (wa pili kushoto).
DSC_0265
DSC_0259
DSC_0267
Kwa picha zaidi MOblog
DSC_0039
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Hoseana Lunogelo akisalimiana na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini , Alvaro Rodriguez nje ya ukumbi wa mikutano kabla ya mgeni rasmi kuwasili kwenye mkutano mkubwa wa tatu wa ESRF unaozungumzia ukuaji wa uchumi kwa kutumia fursa zilizopo na maendeleo yanayogusa jamii uliofanyika jana jijini Dar katika hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro.(Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog)

Na Mwandishi wetu
RAIS Jakaya Kikwete amewataka nguli wa masuala ya uchumi na maendeleo ya binadamu kuisaidia serikali kufanikisha azma yake ya maendeleo kwa wananchi hasa ikizingatiwa kwamba zipo raslimali za kutosha, uchumi unakua lakini umaskini haupungui.

Rais alisema hayo jana wakati akifungua mkutano mkubwa wa tatu wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) unaozungumzia ukuaji wa uchumi kwa kutumia fursa zilizopo na maendeleo yanayogusa jamii uliofanyika hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro.
Katika hotuba yake kwa wataalamu nguli hao ambao wanaangalia athari za kisera na kutoa ushauri katika masuala ya maendeleo yenye kulenga kunufaisha jamii, alisema katika miaka 10 iliyopita uchumi wetu umekua ukikua kwa kasi lakini hali hiyo haikuweza kusaidia kupunguza umaskini kama ulivyolengwa na serikali.

Alisema moja ya malengo ya millennia yalikuwa ifikapo mwaka wa kesho hali ya umaskini ipunguzwe angalua nusu yake, kwa kuongeza pato la mtu binafsi lakini hali sivyo ilivyo.
Rais ambaye alitumia muda mwingi kueleza maendeleo ya kiuchumi yaliyofikiwa katika hatua ya kuifikisha nchi hii miongoni mwa mataifa yenye kipato cha kati ifikapo mwaka 2025, alisema zinatakiwa juhudi kubwa ili kuondoa umaskini wa kipato kwa mtu mmoja mmoja.
DSC_0047
Mwenyekiti wa Bodi ya ESRF, Philemon Luhanjo (kushoto) akiteta jambo na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez nje ya ukumbi wa mikutano kwenye hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro.

“Pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika ustawi wa jamii kama uandikishaji wa watoto shule, uzazi na upunguzaji wa vifo vya watoto, taifa bado linakabiliwa na changamoto kubwa ya ubora wa elimu, upunguzaji wa vifo kwa wanawake wazazi na utapiamlo” alisema Rais Kikwete.

Alisema kwa kuangalia takwimu hizo katika jamii na ukuaji wa uchumi ni dhahiri kwamba taifa letu ili kufikia malengo yake kuna mambo mengi yanatakiwa kufanyiwa kazi na kuamini kwamba wataalamu hao katika mada zao mbalimbali watakazojadiliana watatoka na kitu cha maana kuisaidia serikali kupata mwelekeo sahihi wa kufikia taifa lenye kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.

Dira ya maendeleo ya mwaka 2025 ambayo inayotaka kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati yenye maisha bora, utawala bora na uchumi wenye ushindani miongoni mwa mambo machache yenye upeo wa juu yaliyomo katika dira hiyo ndiyo yanayotumika kujadili na hatimaye kuipa serikali majawabu ya mambo muhimu yanayotikisa safari ya kuelekea huko.

Ili kufika huko kwa mujibu wa Rais Kikwete viashiria kadhaa vitaonekana ikiwa ni pamoja na kushuka kwa mchango wa kilimo kwa pato la taifa na ajira, kukua kwa sekta ya kisasa ya viwanda na huduma kwa uchumi, kukua kwa miji na mabadiliko katika vizazi na vifo ambapo taifa linaondoka katika vifo na uzazi wa fujo na kuwa na vizazi vidogo na vifo kidogo kutokana na kukua kwa elimu na huduma za afya.
DSC_0064
Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF Dk. Hoseana Lunogelo (kushoto) akiongozana na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini , Alvaro Rodriguez kuelekea kwenye ukumbi wa mkutano.

Alisema mpango wa muda mrefu umelenga ifikapo mwaka 2025 mchango wa kilimo kwa pato la taifa utapungua kutoka asilimia 27.8 kufikia 20.7, mchango wa viwanda kupanda kutoka 24.4 hadi 30.7 na mchango wa huduma utapanda kutoka asilimia 47.8 ya mwaka 2010 hadi 48.6.

“Ni matumaini yangu kwamba wastani wa idadi ya watu ikipungua kutokana na elimu na huduma safi za afya au ukuaji wa kasi wa pato la taifa kuliko ongezeko la watu na hivyo kipato kitaongezeka na umaskini utapungua” Miaka 10 iliyopita mchango wa kilimo katika pato la taifa umekuwa mkubwa huku vizazi na vifo vikiwa ni vingi.

Mkutano huo ambao unajadili mabadiliko ya kiuchumi kwa ajili ya maendeleo ya jamii unatokana na ripoti ya mradi wa maendeleo ya jamii (THDR) iliyofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
DSC_0025
Wageni waalikwa wakipitia ripoti mbalimbali zilizoandaliwa na ESRF nje ya ukumbi wa mikutano kabla ya kuwasili kwa mgeni rasmi.

Naye Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini , Alvaro Rodriguez akizungumza kwa niaba ya Umoja wa Mataifa katika mkutano huo amesema Umoja wa Mataifa utaendelea kuisaidia Tanzania kutengeneza ustawi kwa wananchi wake.

Alisema pamoja na kuwapongeza ESRF kwa kuandaa mkutano huo muhimu wa kuipatia serikali fikira za namna ya kuboresha hali za wananchi wake. Alisema amefurahishwa kwa ESRF kusaidia kutafuta mustakabali wa maendeleo kwa minajili ya kuendeleza wananchi kwani maendeleo ya kweli ni yale yanayoboresha maisha ya wananchi.

Aidha alivitaja vigezo muhimu vya maendeleo ya jamii katika hali ya uchumi unaokua ambavyo ni kuhakikisha kwamba kuna usawa katika ukuaji wa uchumi na maisha ya wananchi, kuongeza uwezo wa kuhami maendeleo yaliyofikiwa dhidi ya haki zisizotabirika zinazovuruga ustawi,Kuhakikisha maendeleo endelevu ya wananchi na nchi na kuendelea kuwasaidia wanaume kwa wanawake kushiriki kikamilifu katika mchakato wa maendeleo iwe kiuchumi, kijamii na kisiasa na kugawana kwa usawa matunda ya maendeleo.
DSC_0068
Mratibu wa Programu kutoka ESRF, Yasser Manu (kulia) akibadilishana mawazo na baadhi ya wafanyakazi wenzake nje ya ukumbi wa mikutano kabla ya kuwasili kwa mgeni rasmi.
Amesema Mratibu huyo wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini kwamba amefurahishwa na taarifa kwamba mkutano huo utajadili mada mbalimbali na kutolea ushauri kwa kuzingatia taarifa ya THDR.

Awali akimkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya ESRF Philemon Luhanjo, kumkaribisha rais Jakaya Kikwete Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF Dk Hoseana Lunogelo alisema wakati taasisi hiyo inaadhimisha miaka 20 ya uwepo wake, katika mkutano wake wa 3 wa kitaifa wanatarajia wanazuoni kuchambua mada mbalimbali na kuandika kitu kitakachosaidia serikali katika kuhakikisha maendeleo ya kiuchumi yanakwenda sanjari na ustawi wa jamii kwa maana ya kuondokana na umaskini katika ngazi ya mtu mmoja mmoja. Mada zinazochambuliwa zinatoka kwa wataalamu waliobobea kutoka Tanzania,Ethiopia, Uingereza, Norway na India.
DSC_0195
Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Hoseana Lunogelo akibadilishana mawazo na Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Masaki Okada wakati wakimsubiri mgeni rasmi kuwasili ukumbini hapo.
DSC_0203
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya ESRF, Philemon Luhanjo mara baada ya kuwasili kwenye hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro kufungua mkutano mkubwa wa tatu wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) unaozungumzia ukuaji wa uchumi kwa kutumia fursa zilizopo na maendeleo yanayogusa jamii.
DSC_0204
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
DSC_0209
Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Hoseana Lunogelo (kushoto) akiongozana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya ESRF, Philemon Luhanjo (katikati) kuelekea ukumbi wa mikutano.
DSC_0233
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili ukumbini kufungua mkutano mkubwa wa tatu wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) unaozungumzia ukuaji wa uchumi kwa kutumia fursa zilizopo na maendeleo yanayogusa jamii. Katikati ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.

WAKALA WA TAIFA WA HIFADHI YA CHAKULA (NFRA) KANDA YA DODOMA INAKABILIWA NA UFINYU WA ENEO LA KUHIFADHIA MAZAO MSIMU HUU WA UNUNUZI WA MAZAO

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akikagua shughuli za ufungashaji mahindi na Mtama kwenye magunia tayari kwa kuhifadhiwa kwenye maghala  wakati alipotembelea kituo cha NFRA Kanda ya Dodoma.
 Wakinamama kwenye kituo cha Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Dodoma wakipeta mahindi na kuyaondoa uchafu tayari kwa ajili ya kuyafungasha kwenye magunia na kuyahifadhi ghalani, mahindi hayo yananunuliwa kutoka kwa wakulima na wafanyabiashara mbalimbali.

 Moja ya maghala ya NFRA Kanda ya Dodoma ambayo yamejaa mahindi na Mtama na hivyo kuhitaji maeneo/maghala mengine zaidi ya kuhifadhia mazao.
 Gari iliyobeba mahindi ikipima uzito ili kupeleka mahindi hayo kuhifadhiwa kwenye maghala kwenye kituo cha Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Dodoma, changamoto kubwa kituoni hapo ni uchache wa maghala ya kuhifadhia mazao hayo.
 Baadhi ya Magari ya mizigo yakipakua mahindi na mtama kwenye kituo cha (NFRA) Kanda ya Dodoma.
 Magari yaliyobeba mahindi na mtama yakiwa kwenye foleni nje ya kituo cha Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Dodoma wakisubiri kuuza mazao hayo kwa wakala huyo wa serikali kama walivyokutwa kituoni hapo jana.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akiwa kwenye picha ya pamoja naC baadhi ya wanachama wa vyama mbalimbali vya ushirika vya kilimo vilivyoleta mazao kuuza kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Dodoma, mapema jana wakati ukaguzi wa zoezi la ununuzi wa mazao kituoni hapo.

Na John Banda

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi ameitaka Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Dodoma kuhakikisha inatafuta suluhisho la haraka la changamoto ya maghala na mifumo ya kuhifadhia mazao inayoikabili taasisi hiyo wakati huu wa msimu wa kununua mazao.

Vilevile Dr. Nchimbi ameelekeza ukarabati wa Maghala ya hifadhi ya “National Milling” yaliyopo eneo la Makole ambayo uwezo wake ni kuhifadhi takribani tani elfu 10 kwa ghala uwekewe mkakati ili kusaidia kuletasuluhisho la haraka la ukosefu wa maeneo ya kuhifadhia mazao yanayoendelea kununuliwa hivi sasa.

Alitoa maelekezo hayo jana alipotembelea kituo cha NFRA Dodoma kukagua maendeleo ya zoezi la ununuzi na uhifadhi wa mahindi na Mtama ambapo alijionea maghala yaliyopo kwa ajili ya kuhifadhia mazao yamejaa na foleni kubwa ya magari yaliyoleta mahindi na mtama kutoka kwa wakulima yakiwa yanasubiri kushusha mazao huku changamoto kubwa ikiwa sehemu ya kuyahifadhi mazao hayo.

Meneja wa NFRA Kanda ya Dodoma Ndg. Mambali alisema kuwa kwa sasa NFRA inanunua mahindi na Mtama kutoka kwa walulima, na kwa mwaka huu, NFRA Kanda ya Dodoma imepanga kununua tani elfu 15 na mpaka sasa tani elfu tatu tu ndio zimeshanunuliwa ambapo tani elfu moja ndio zimefanikiwa kuhifadhiwakwenye maghala hivyo kunahitajika suluhisho la haraka la sehemu ya kuhifadhi mazao ili zoezi la ununuzi lifanyike kama lilivyopangwa.

Katika hatua nyingine Dr. Nchimbi amepongeza NFRA kwa kutoa kipaumbele kwa vyama vya ushirika vya wakulima kwa kununua mazao yao kwa bei maalumu tofauti na inavyonunua kwa wafanyabiashara wengine ambapo bei inayonunua kwa vyama vya ushirika vya wakulima kwa kilo moja ya mahindi ni shilingi 530 wakati kwa wafanyabiashara wengine inanunua kwa shilingi 500.

Akiwasilisha ombi la vyama vya ushirika vya wakulima kuongezewa kiwango cha tani wanazoruhusiwa kuuza kwa NFRA, Mwenyekiti wa kikundi cha wakulima cha Matumaini Kongwa Ndg. Stanley Machakala amemuomba Mkuu wa Mkoa Dodoma kuwasaidia waongezewe tani zaidi za kuiuzia NFRA kwani huko vijijini bado wakulima wamebakiza mahindi mengi yanayohitajika kuuzwa.

Akitoa ufafanuzi juu ya ombi hilo, Dr. Nchimbi ameahidi kuwasaidia vyama hivyo vya ushirika vya wakulima kulifikisha suala hilo ngazi husika na kusimamia hadi watakapoongezewa kiwango cha mahindi na mtama
wanachorususiwa kuiuzia NFRA.



HALIMA MDEE AWA MWENYEKITI MPYA BAWACHA

$
0
0
Wajumbe wa mkutano Mkuu wa Baraza la Wanawake Chadema Taifa (Bawacha), wakifungua shampeni kusherehekea ushindi wa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema Taifa, Halima Mdee (kushoto) baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi huo. (Picha na Francis Dande)
 Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bara), Hawa Mwaifunga akilia kwa furaha baada ya kushinda nafasi hiyo katika uchaguzi uliofanyika juzi.
 Wajumbe wa mkutano Mkuu wa Baraza la Wanawake wa Chadema wakiwa katika mkutano huo.
 Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema Taifa, Halima Mdee (kulia) akipongezwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa Baraza la Wanawake wa Chadema. Wa pili kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bara), Hawa Mwaifunga.
 Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema Taifa, Halima Mdee (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wake (Bara), Hawa Mwaifunga (kushoto) na  Makamu Mwenyekiti (Zanzibar), Hamida Abdallah.
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema, Halima Mdee akizungumza baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa Baraza hilo.

WAANDISHI WA HABARI WANAOENDA NCHINI MALAWI WAAGWA RASMI.

$
0
0
 Baadhi ya waandishi wa habari wanaosafiri kwenda Malawi wakiwa wanamsikiliza Katibu tawala msaidizi wakati wa kuagana.
 Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Mbeya, Leonard Magacha akizungumza na waandishi wa Habari wanaotarajia kusafiri.
 Mwenyekiti wa safari ya Malawi, Ulimboka Mwakilili, akitoa ufafanuzi wakati wa kuagana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
 Mwandishi Christopher Nyenyembe, mmoja wa Waandishi wanaosafiri akifafanua jambo.
 Katibu tawala Msaidizi akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya.

Kaimu Mkurugenzi wa Jiji Akiongea na Waandishi wa Habari wanaokwenda Safarini Malawi


 Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Dk. Samwel Lazaro, akiwasikiliza waandishi wa habari walipoenda kumuaga ofisini kwake.

 baadhi ya Waandishi wa Habari wakiwa ofisini kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya wakimsikiliza kwa makini walipoenda kumuaga tayari kwa safari ya Malawi.
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Dk. Samwel Lazaro akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari wanaotarajia kusafiri baada ya kuagana.


BAADHI ya  Waandishi wa habari Mkoa wa Mbeya wanaotarajia kufanya ziara ya kimafunzo nchini Malawi na Zambia wameagwa rasmi na viongozi wa Serikali.
Waandishi hao wapatao 15 wanatarajia kuanza safari Septemba 14, Mwaka huu hivyo kabla ya kuondoka wameagana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na Halmashauri ya Jiji la Mbeya.
Maagano hayo yamefanyika leo kwa nyakati tofauti na kupata Baraka zote kutoka kwa wawakilishi wa Ofisi hizo na kuwataka waandishi kuuwakilisha vema Mkoa wa Mbeya na Taifa kwa ujumla.
Katibu Tawala Msaidizi, idara ya Utawala na rasilimali watu, Leonard Magacha, kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja, alisema matarajio ya Mkoa ni kupata mrejesho kutoka kwa waandishi baada ya kurudi kutoka safarini.
Alisema hiyo ni fursa pekee ambayo waandishi wanaitumia kuvitangaza vivutio mbali mbali vilivyopo katika Mkoa wa Mbeya kwa watu wa Malawi ili waweze kutembelea pamoja na fursa zilizopo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Dk. Samwel Lazaro, amewataka waandishi wa habari kutumia nafasi hiyo kuitangaza timu ya Mbeya City kimataifa zaidi.
Alisema hivi sasa Halmashauri imekuwa na mahusiano mazuri na wananchi kutokana na uwepo wa timu ya mpira wa miguu ambayo hivi sasa inajulikana nchi nzima hivyo ni fursa iliyotokea ya kuitangaza nchi za Nje ili ijulikane kimataifa zaidi.
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Msafara wa Waandishi wa Habari kwenda nchini Malawi, Ulimboka Mwakilili, ametoa shukrani kwa wadau mbali mbali waliowezesha safari hiyo kwa hali na mali.
Alisema mbali na kila mwandishi kuchangia gharama za kwenda na kurudi lakini kuna wadau walioweza kuchangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya safari hiyo.
Aliwataja baadhi ya wadau kuwa ni Mkurugenzi wa Hifadhi ya wanyama pori(Ifisi Zoo), Leirner, WYCS, Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Ofisi ya Katibu tawala Mkoa wa Mbeya, Faraja nursing na Maridadi Shop.
Aliongeza kuwa wadau wengine wanakaribishwa kuchangia safari hiyo kutokana na umuhimu wake katika kutangaza fursa ambazo zinapatikana katika Mkoa wa Mbeya kwa wafanyabiashara na wananchi wa Nchi ya Malawi.
Naye Mratibu wa Safari hiyo, Venance Matinya, alisema maandalizi ya safari yamekamilika kwa asilimia kubwa hivyo kinachosubiriwa ni tarehe ya kuondoka.
Alisema waandishi wa habari wameshaajiandaa kwa mahitaji yote ya safari za nje ya nchi ikiwa ni pamoja na kukata Hati za kudumu za kusafiria pamoja na cheti cha chanjo ya ugonjwa wa manjano kwa mujibu wa sheria.

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA UONGOZI WA NEC-JAPAN IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Rais wa Shirika la NEC Corporation la Japan, Dkt. Nobuhiro Endo, wakati alipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Septemba 12, 2014 akiwa ameongozana na ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Uongozi wa Shirika la NEC Corporation la Japan, wakiongozwa na Rais wao Dkt. Nobuhiro Endo, wakati walipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Septemba 12, 2014 kwa ajili ya mazungumzo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwakatika picha ya pamoja na Rais wa Shirika la NEC Corporation la Japan, Dkt. Nobuhiro Endo (kushoto) na Balozi wa Japan Nchini Tanzania, Masaki Okada, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Septemba 12, 2014. Picha na OMR
 ========  ========  ========

Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal leo amekutana na Uongozi wa Kampuni ya NEC yenye makao yake makuu jijini Tokyo nchini Japan. Ujumbe wa NEC-Japan umeongozwa na Rais wa Kampuni hiyo inayojishughulisha na masuala ya Mawasiliano na Teknolojia, Dkt. Nobuhiro Endo.

Ujio wa Kampuni hii nchini Tanzania unatokana na mwaliko wa Tanzania kwa makampuni ya Japan kufuatia ziara ya kikazi aliyoifanya Mheshimiwa Makamu wa Rais nchini Japan, mwezi wa Mei mwaka huu. Mheshimiwa Makamu wa Rais alitembelea Makao Makuu ya Kampuni hiyo wakati za ziara hiyo.

Katika mazungumzo na uongozi wa NEC Mheshimiwa Makamu wa Rais aliwaeleza wageni wake nia ya Tanzania kuona inatanua mawasiliano na teknolojia nchini ili kuinua uchumi na akafafanua kuwa teknolojia yoyote kutoka NEC inakaribishwa hapa nchini ili kusaidia Tanzania kupiga hatua. 

Uongozi wa NEC nao ulimueleza Mheshimiwa Makamu wa Rais kuwa, NEC inaushirikiano wa karibu na Shirika la Simu Tanzania (TTCL) na kwamba wanatarajia kukutana na uongozi wa wizara ya Mambo ya Ndani kwa lengo la kutazama fursa za kusaidia teknolojia katika ulinzi.

Imetolewa na:              Ofisi ya Makamu wa Rais
Ikulu Dar es Salaam Septemba 12, 2014


Kituo cha uwekezaji Tanzania chasajili (TIC) chasajili miradi 885

$
0
0
Frank Mvungi-Maelezo
Kituo cha uwekezaji Tanzania chasajili (TIC) chasajili miradi 885 ambayo inategemea kuzalisha ajira 198,573   yenye thamani ya dola za Marekani milioni 88134.92
Haya yamesemwa leo na Meneja Uhusiano wa kituo hicho Bi Pendo gondwe  wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
“TIC inajivunia huduma inazotoa kwa Wawekezaji kupitia dirisha la huduma (One Stop Centre) ambalo linasaidia kuleta tija katika kuwahudumiawawekezaji  ”alisema Pendo.
Akifafanua zaidi Pendo amesema kwa upande wa kodi tuliweza kushughulikia  masuala 3461, Kutoa hati za Ardhi ( Dervarative rights21) Usajili wa Makampuni 23 na kutoa leseni zipatazo 84, na upande wa vibali vya Class A 387 na Vibali vya Class B 1966.
Pia Pendo alitoa wito kwa Watanzania wote kutumia huduma zinazotolewa na Kituo cha Uwekezaji ikiwemo Kusajili miradi, Kuandikisha Kampuni, Kujisajili na VAT, TIN, Leseni mbalimbali, Hati za ukazi daraja ‘B”, endapo utahitaji kumwajiri mgeni,Ushauri kuhusu kodi,Usaidizi wa kupata ardhi kwa ajili ya uwekezaji na vivutio vya uwekezaji.
Huduma nyingine ni Kuwaunganisha wawekezaji wa nje  na wandani kwa ajili ya ubia na Usaidizi wa kutafuta masoko kupitia ziara za nje za wafanyabiashara wa Tanzania.
Kituo cha Uwekezaji (TIC) kwa muda mrefu tumekuwa tukihamasisha watanzania washiriki kwa kuanzisha miradi ya Uwekezaji katika sekta mbalimbali nchini. Kutokana na juhudi za Kituo cha uwekezaji pamoja na Taasisi mbalimbali za Serikali, tumeweza kuwavutia wawekzaji wengi ambao ni wafanya biashara kuweza kuanzisha miradi ya uwekezaji kwenye sekta kama vile Viwanda, Utalii, Usafirishaji, Majengo ya biashara.

WASHINDI TUZO ZA HABARI TANAPA WATEMBELEA MAENEO YA KIHISTORIA AFRIKA KUSINI

$
0
0
Washindi wa Tuzo za Habari za TANAPA 2013 kutoka kushoto David Rwenyagira (Radio Five), Vedasto Msungu (ITV), Mtanzania Peter Masika wa Johannesburg na Gerald Kitabu (The Guardian) wakiwa nje ya nyumba ya Rais wa Kwanza wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
Washindi wa Tuzo za Habari za TANAPA 2013 wakiwa ya Jumba la Makumbusho ya Ubaguzi wa Rangi.
Picha ya Mzee Nelson Mandela inayopatikana katika Jengo hilo la Makumbusho ya Ubaguzi wa Rangi.
Washindi wa Tuzo za Habari za TANAPA 2013 wakiwa nje ya ‘Union Building’ ambapo ndipo yalipo Makazi ya Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini, jijini Pretoria.
Mbele ya sanamu ya Mzee Nelson Mandela.
Washindi wa Tuzo za Habari za TANAPA 2013 katika picha ya pamoja na watalii mbalimbali jijini Johannesburg.
Washindi wa Tuzo za Habari za TANAPA 2013 wakiwa katika eneo la Makumbusho la Hector Pieterson, kijana aliyeuwawa wakati wa Harakati za Kupinga Ubaguzi wa Rangi nchini Afrika Kusini mwaka 1976.

TBL YATOA MSAADA WA SH. MIL.24.6 WIKI YA NENDA KWA USALAMA. ZITASAIDIA UPIMAJI AFYA ZA MADEREVA

$
0
0
 Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve  Kilindo (kulia), akimkabidhi Mganga Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, SSP Charles Msenga mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil. 24.6 kwa ajili ya Wiki ya Nenda kwa Usalama inayotarajia kuanza hivi karibuni. Anayeshuhudia makabidhiano hayo yaliyofanyika Dar es Salaam jana, ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani, Naibu Kamishna Mohamed Mpinga.
 Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve  Kilindo (kulia), akimkabidhi Mganga Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, SSP Charles Msenga (wa pili kushoto) mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil. 24.6 kwa ajili ya Wiki ya Nenda kwa Usalama inayotarajia kuanza hivi karibuni. Wanaoshuhudia makabidhiano hayo yaliyofanyika Dar es Salaam jana, ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu  Kamishna Mohamed Mpinga (wa pili kulia) na Mjumbe wa Kamati ya Usalama Barabarani, Henry Bantu.
 Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve  Kilindo (kushoto) na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu  Kamishna Mohamed Mpinga wakionesha moja ya fulana zilizotolewa msaada na TBL kwa ajili ya Wiki ya Nenda kwa Usalama katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana. TBL ilikabidhi pia hundi yenye thamani ya sh. mil. 24.6 kwa ajili hiyo.

 Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve  Kilindo (kushoto) na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu  Kamishna Mohamed Mpinga wakionesha moja ya fulana zilizotolewa msaada na TBL kwa ajili ya Wiki ya Nenda kwa Usalama katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana. TBL ilikabidhi pia hundi yenye thamani ya sh. mil. 24.6 kwa ajili hiyo. Fedha hizo pia zitasaidia upimaji wa afya za madereva. (PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG0
 Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve  Kilindo (kulia) akimkabidhi  moja ya fulana na cheti Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu  Kamishna Mohamed Mpinga kwa ajili ya Wiki ya Nenda kwa Usalama katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana. TBL ilikabidhi pia hundi yenye thamani ya sh. mil. 24.6 kwa ajili hiyo. Kushoto ni  Mganga Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, SSP Charles Msenga

Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve  Kilindo (kulia) akimkabidhi  moja ya fulana na cheti Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu  Kamishna Mohamed Mpinga kwa ajili ya Wiki ya Nenda kwa Usalama katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana. TBL ilikabidhi pia hundi yenye thamani ya sh. mil. 24.6 kwa ajili hiyo.
 Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve  Kilindo (kulia) akimkabidhi  moja ya fulana na cheti Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu  Kamishna Mohamed Mpinga kwa ajili ya Wiki ya Nenda kwa Usalama katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana. TBL ilikabidhi pia hundi yenye thamani ya sh. mil. 24.6 kwa ajili hiyo.
 Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve  Kilindo (kulia) akimkabidhi  moja ya fulana na cheti Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu  Kamishna Mohamed Mpinga kwa ajili ya Wiki ya Nenda kwa Usalama katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana. TBL ilikabidhi pia hundi yenye thamani ya sh. mil. 24.6 kwa ajili hiyo.

 Baadhi ya maofisa wa Kikosi cha Usalama Barabarani wakishuhudia makabidhiano hayo
 Kamanda Mpinga akitoa shukrani kwa TBL kwa msaada huo muhimu utakaosaidia pia kupima afya za madereva
 Baadhi ya kofia zilizokabidhiwa
 Baadhi ya fulana zilizokabidhiwa
 Baadhi ya maofisa wa kikosi cha usalama barabarani wakiwa katika hafla hiyo
 Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, Naibu Kamishna Mohamed Mpinga
Kamanda Mpinga akimshukuru Kilindo

WANAWAKE VAENI NGUO SASA, KAMA KUVUA MUMESHAVUA IMETOSHA

$
0
0

MOJA ya sifa ya mwandishi ni kusoma, na katika kusoma huko na kupekua pekua hapa na pale unaweza kujifunza na kupata la kuandika kupitia maandiko ya watu wengine na kutoa elimu kwa umma. Leo nimepita pita katika kurasa za marafiki zangu huko katika uso wa kitabu ‘Facebook nikakutana na nasaha ya ndugu yangu Victory Richard, juu ya kuwasihi wanawake kwamba  sasa wavae nguo.

Ndugu yangu yule amechoshwa na tabia za dada zetu, wake zetu na hata mama zetu wakati mwingine wanavyotembea uchi, ndio! utavaaje nguo fupiii au skintight halafu useme umevaa nguo?. Binafsi naomba radhi kama nitakuwa nimemkwaza mtu hasa hao mama zetu, Ah! Lakini potelea mbali Anko Kidevu sijali kitu si wamejitakia.

Hivi akina mama na dada zetu kweli jamani katika yooote ambayo mnalilia usawa na sisi tunakubali kuwa sawa, hili la kutembea uchi au kuvaa mavazi nusu uchi mbona mnapitiliza?

Ndio mmepitiliza Anko nimebaini kuwa mmetupita maana sisi tukivaa sana ni kaptura au bichkoma na kawosh au singlendi lakini sasa naona mmepita katika sketi na sasa mna vimini na kuacha vifua wazi.

Ni nani awezaye kuona aibu yenu zaidi yangu mimi Anko Kidevu na kaka yenu Victor Richard, tafadhalini tunawasihi, hebu vaeni nguo sasa na jamii itawaheshimu maana hakuna heshima kwa mwanamke hata kidogo. Na kama mnahisi mnaheshimika kwa hilo ni bure kabisa. SOMA ZAIDI FATHER KIDEVU BLOG

WAKAZI WA SHINYANGA WAKUNWA NA UJIO WA TAMASHA LA FIESTA,LEO KUSAMBAZA UPENDO KWA WAKAZI WA GEITA

$
0
0
Pichani kati msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka THT,Rachael akiwa na madansa wake wakilishambulia jukwaa kwa namna ya kipekee usiku huu kwenye tamasha la Fiesta ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage mjini Shinyanga.
Mmoja wa wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,atambulikae kwa jina la kisanii Ommy Dimpo akiwaimbisha mashabiki huku akisherehekea siku yake ya kuzaliwa na wakazi wa mji huo usiku katika tamasha la Fiesta ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage
Mmoja wa wasanii wa Bongofleva anaefanya vyema katika muziki huo atambulikae kwa jina la Young Killer a.k.a Msodoki akiimba jukwaani usiku huu kwenye tamasha la Fiesta ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage mjini Shinyanga.
Pichani juu na chini ni umati wa wakazi wa mji wa Shinyanga waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Fiesta ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage,usiku huu.
Wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Ney Wa Mitego (pichani kulia) na Stamina wakilishambulia jukwaa kwa wimbo wao wa Huko Kwenu vipi,huku makele ya shangwe yakiwa yametawala kila kona ya uwanja mdogo wa Kambarage mjini Shinyanga usiku huu.
Sehemu ya mashabiki wa Fiesta wakishangilia yaliyokuwa yakijiri kwenye jukwaa la Fiesta 2014 ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage mjini Shinyanga.
 Mwanadada Linah akionesha umahiri wake wa kucheza wimbo wake wa Ole Temba juu ya jukwaa la Fiesta 2014 usiku huu kwenye tamasha la Fiesta ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage.
Ukipenda muite Mr Blue,msanii wa muziki wa kizazi kipya juu ya jukwaa la Fiesta 2014 usiku huu ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage mjini Shinyanga.
Mmoja wa wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,atambulikae kwa jina la kisanii Ommy Dimpo akiimba mbele ya mashabiki wimbo wake wa ani kama mama usiku huu katika tamasha la Fiesta ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage
Wanajiita Wakata Mkaa kutoka kundi la Wanaume TMK,Chege na Temba kwa pamoja wakilishambulia jukwa la fiesta mbele ya umati wa watu (hawapo pichani) ndani ya tamasha la Fiesta lililofanyika usiku huu ndani ya uwanja mdodog wa Kambarage mjini Shinyanga.
Wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya Khadija anaetamba na wimbo wake wa maumivu akiwa sambamba na mwanadada Rachael anaetamba na wimbo wake wa Ole temba,kwa pamoja wakilishambulia jukwaa la Fiesta usiku huu ndani ya uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Mmoja wa wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,atambulikae kwa jina la kisanii Ommy Dimpo akiwaimbisha mashabiki wimbo wake wa nani kama mamaa,usiku huu kwenye tamasha la Fiesta ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage
Sehemu ya umati wa watu wakishangweka na na Fiesta usiku huu.
Mmoja wa wakali wa kukamua mangona kutoka Clouds FM,Dj Zero akikamua  ngoma jukwaani mbele ya umati wa wakazi wa Shinyanga kwenye tamasha la Fiesta ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage
Sehemu ya umati wa wakazi wa mji wa Shinyanga wakiwa ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage,wakishuhudia tamasha la Fiesta 2014 likifanyika usiku huu.
Sehemu ya umati wa wakazi wa mji wa Shinyanga wakiwa ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage,wakishuhudia tamasha la Fiesta 2014 likifanyika usiku huu.

TPDC, KAMPUNI ZA WENTWORTH, MAUREL & PROM WASAINI MKATABA WA KUUZIANA GESI

$
0
0
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (wa nne kushoto) akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya WENTWORTH inayochimba gesi katika eneo la Mnazi Bay Mkoani Mtwara , Robert MacBean (wa tatu kushoto) mara baada ya kusaini Makubaliano ya Mkataba wa Kuuziana Gesi kati yake na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC). Wengine katika picha ni baadhi wa Watendaji Wakuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la maendeleo ya Petroli Tanzania TPDC na wawakilishi wa kampuni za WENTWORTH na MAUREL & PROM.
Wajumbe waliohudhuria kikao cha Kusaini Mkataba wa Kuuziana Gesi kati ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), na Kampuni zinazochimba gesi katika eneo la Mnazi Bay Mkoani Mtwara za WENTWORTH Resources Limited na MAUREL & PROM wakisaini MKataba huo. Anayeshuhudia mbele ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo pamoja na wawakilishi wengine kutoka kampuni hizo, TPDC, Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) James Andilile (wa kwanza kulia) wakipitia Mkataba kwa pamoja na mmoja wa wawakilishi wa Kampuni hizo wakati wa kusaini Mkataba huo. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya MAUREL & PROM, Michael Hochard na wa kwanza ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya WENTWORTH Robert MacBean.

PRESIDENT KIKWETE LAUNCHES World bank's report on Productive Jobs Necessary for Tanzania’s Fast-Growing Workforce

$
0
0
 President Jakaya Mrisho Kikwete  and the   Managing Director of the World Bank Ms Sri Mulyani Indrawati present 13-year-old Chanda Atulinda Lwansa, for emerging winner of the world Bank Children's Art Contest. Chanda, a form one student at Feza girl's Secondary shool, beat 150 other entries to emerge winner and grab the One Million Tanzania shillings award. Her work, which is on the cover of the report, depicts men and women engaged in different occupations as surgeons, pilots, chemists, business people, gardeners and teachers.  
  President Jakaya Mrisho Kikwete  presents  a certificate to 13-year-old Sakina Khuzema Adamali for emerging 1st runner up of the world Bank Children's Art Contest, as  Managing Director of the World Bank Ms Sri Mulyani Indrawati sakina loons oon. Sakina an eighth grade student at the Aga Khan Mzizima Secondary school, received 650,000/.  Her piece shows children living in below par conditions but with dreams of attaining a university degree and a better life.
   President Jakaya Mrisho Kikwete  sand the   Managing Director of the World Bank Ms Sri Mulyani Indrawati present a certificate to seven-year-old Ibrahim Habhi Redemtus Bugalama  for emerging 2nd runner up of the world Bank Children's Art Contest. sakina, an eighth grade student at the Aga Khan Mzizima Secondary school, received 650,000/.  
    President Jakaya Mrisho Kikwete  sand the   Managing Director of the World Bank Ms Sri Mulyani Indrawati pose with winners of the  world Bank Children's Art Contest.
  President Jakaya Mrisho Kikwete  and the   Managing Director of the World Bank Ms Sri Mulyani Indrawati listen to 13-year-old Chanda Atulinda Lwansa,  the  winner of the world Bank Children's Art Contest. Chanda, a form one student at Feza girl's Secondary shool, beat 150 other entries to emerge winner and grab the One Million Tanzania shillings award. Her work, which is on the cover of the report, depicts men and women engaged in different occupations as surgeons, pilots, chemists, business people, gardeners and teachers.  
President Jakaya Mrisho Kikwete  makes his speech at the launch of the bank's report on Productive Jobs Necessary for Tanzania’s Fast-Growing Workforce today at the Hyatt Regency Kilimanjaro hotel in Dar es salaam.

 President Jakaya Mrisho Kikwete greets Managing Director of the World Bank Ms Sri Mulyani Indrawati as he arrives  at the launch of the bank's report on Productive Jobs Necessary for Tanzania’s Fast-Growing Workforce today at the Hyatt Regency Kilimanjaro hotel in Dar es salaam. Looking on is Mr Philippe Dongier. Country Director for Burundi, Tanzania and Uganda. Ms Mulyani Indrawati is responsible for the institution's global operations.
President Kikwete greets Philippe Dongier. World bank's Country Director for Burundi, Tanzania and Uganda, as Managing Director of the World Bank Ms Sri Mulyani
 President Kikwete greets IPP Chairman Dr Reginald Mengi as he arrives  at the launch of the bank's report on Productive Jobs Necessary for Tanzania’s Fast-Growing Workforce today at the Hyatt Regency Kilimanjaro hotel in Dar es salaam. Looking on is Mr Philippe Dongier. Country Director for Burundi, Tanzania and Uganda. 
 President Kikwete greets  Mr. Omari Issa,  CEO of the Presidential Delivery Bureau on the 'Big Results Now' initiative.
 President Jakaya Mrisho Kikwete  is escorted to the meeting room by  Managing Director of the World Bank Ms Sri Mulyani Indrawati as he arrives  at the launch of the bank's report on Productive Jobs Necessary for Tanzania’s Fast-Growing Workforce today at the Hyatt Regency Kilimanjaro hotel in Dar es salaam. Right is Mr Philippe Dongier. Country Director for Burundi, Tanzania and Uganda.

WATANZANIA WATAKIWA KUTODANGANYWA KUHUSU MCHAKATO WA KATIBA

$
0
0
 Na Benedict Liwenga, MAELEZO-Dodoma.

 
MJUMBE wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Mwenyekiti wa TCD Mhe. John Cheyo amewataka Watanzania kutodanganywa kuhusiana na mchakato mzima wa kusaka Katiba Mpya.
 
Kauli hiyo imetolewa leo na Mhe. Cheyo wakati alipokuwa akifanya mahojiano katika kipindi cha asubuhi cha Jambo kinachorushwa na Televisheni ya Shirika la Habari Tanzania (TBC).
 
Mhe. Cheyo amesema kuwa ni vema viongozi kuacha kusema uwogo na kuwa waungwana katika mchakato wa kutafuta Katiba Mpya kwani si vema kuitakia Tanzania mabaya bali ni kutaka mchakato huo wa Katiba uendelee kwa amani.
 
Ameongeza kuwa Taifa la Tanzania linahitaji kuwa Taifa lenye nguvu kwani amani haiwezu kuwekewa thamani kwa vurugu, hivyo ametaka amani iliyopo nchini ilindwe na kuepuka kudanganywa na baadhi ya watu wasiokuwa na nia njema na nchi.
 
Mhe. Cheyo ameshangazwa kwa kitendo cha viongozi wa UKAWA kutoweka ajenda ya kurudi ndani ya Bunge hilo wala kuzungumzia kuhusu suala hilo la kurudi ndani, bali wamekuwa wakitaka wajumbe wengine walioko ndani watoke kwa kusema kuwa bunge hilo sio halali.
 
“Nawashangaa UKAWA kwa kutoweka ajenda ya kurudi ndani ya Bunge hili Maalum la Katiba na badala yake wao wanaweka ajenda ya kutoka ndani ya bunge hili tena kwa nguvu”, alisema Mhe. Cheyo.
 
Aidha, Mhe. Cheyo amewataka vijana nchini wawe na mshikamano na kuepuka kudanganywa na viongozi kwa kuambiwa mambo yenye uwongo huku akisisitiza kuwa Rais aliyeko sasa hivi ana nia njema ya kuipatia nchi Katiba iliyo bora na yenye kumfaa kila Mtanzania.
 
“Vijana achene kuvunjika miguu yenu bure, achene kukimbia kimbia barabarani huku mkilishwa maneno yenye uongo kuhusiana na mchakato huu wa Katiba, vunjikeni miguu kwa kufanya kazi kwa bidiii na sio kusikiliza uwongo”, alisema Mhe. Cheyo.
Akizungumzia kuhusu TCD, Mhe. Cheyo amefafanua kuwa TCD ni Jukwaa la majadiliano kwa ajili ya maridhiano na mapatano pale panapokuwa na tofauti kati ya vyama vya siasa.
 
“TCD ni Jukwaa kwa ajili ya kufanya majadiliano na si vinginevyo, hii ni meza ya maridhiano na nawaambia kuwa huko mnapokwenda ni kuchepuka, rudini ndani kwenye njia kuu”, alisisitiza Mhe. Cheyo.
 
Naye mjumbe wa Kamati namba Sita ya Bunge Malaam la Katiba Mhe. Steven Wasira amewaasa Watanzania kwa kusema kuwa, watu wanaosema kuwa Bunge limenyofoa baadhi ya mambo muhimu yanayohusu wananchi ni waongo na wenye nia ya kupotosha Umma wa Tanzania.
 
“Kuna watu wanasema kuwa Bunge Maalum la Katiba limenyofoa baadhi ya mambo muhimu yanayohusu wananchi huo ni uwongo, ni mambo gani hayo yaliyonyofolewa? kwasababu kuna mambo mengi yameongezwa na kuboreshwa katika mapendekezo kwa ajili ya makundi mbalimbali ndani ya hiyo Rasimu”, alisema Mhe. Wasira.
 
Mhe. Wasira ameongeza kuwa katika Bunge hilo kuna Ibara ya Rasimu ya Katiba na sio ibara za CCM, amewataka Watanzania nchini wafanya uchunguzi na kusikiliza kwa kuchambua ili kupata ukweli wa hayo.
 
“Sisi tuko tayari kuvaana na viopngozi wowote kwani tunataka Watanzania wote waamini shughuli zifanywazo ndani ya bunge hili na waepuke kudanganywa”, alisema Mhe. Wasira.

Article 3

Sitta awapa somo Viongozi wanaojiita UKAWA.

$
0
0
 Na Benedict Liwenga, MAELEZO-Dodoma.
 
MWENYEKITI wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta amewaadaa baadhi ya viongozi wanaojiita UKAWA kwa taarifa yao ya kutaka kumfikisha Mahakama ya Uhalifu wa Kimataifa kwa kuendeleza mchakato huo wa Katiba.
 
Kauli hiyo imetolewa jana Septemba, 2014 mjini Dodoma na Mhe. Sitta kufuatia baadhi ya viongozi hao, kudai kuwa watampeleka katika mahakama hiyo.
 
Mhe. Sitta ameeleza kuwa baadhi ya viongozi wa kundi hilo kuwa wanakipaji kikubwa cha uigizaji huku akifafanua kuwa wakati walipokuwa Bungeni wakati wa mchakato wa kupiga kura za siri, viongozi wa kundi hilo walizifanya kura hizo kuwa wazi na baadaye kuja na kauli kuwa Bunge Maalum la Katiba linaloendelea sasa sio halali lihairishwe.
 
“Juzi Mhe. Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amekutana nao mara mbili kwa muda wa saa Saba na katika kukutana huko wakafikia maafikiano, lakini siku moja baadaye wao wamekana yote waliyokubaliana hapa mjini Dodoma, kwa hiyo ni vyema wananchi wakawapima hawa watu”, alisema Mhe. Sitta.
 
Aidha, Mhe. Sitta aliasa kwa kusema kuwa wananchi na viongozi wanatakiwa kujua kuwa mchakato wa bunge Maalum la Katiba sio jambo la mzaha na wao hawapo hapo bungeni kwa mzaha mzaha.
 
“Mimi nawaambia kuwa hapo mwakani watakaposhindwa uchaguzi basi warejee katika fani zao ambazo Mwenyezi Mungu kawajalia”, alisema Mhe. Sitta.
Viewing all 46317 articles
Browse latest View live




Latest Images