Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 360 | 361 | (Page 362) | 363 | 364 | .... | 1896 | newer

  0 0

  Bw. Julius Mziray mkaguzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) akizungumza na waandishi wa habari katika hospitali ya Regency ya jijini Dar es salaam. Baada ya kumkamata mtu mmoja anayetuhumiwa kutumia kadi ya bima ya afya yenye namba 02-HCTP1801 ambayo inamilikiwa na Bw. Terry J. Maona kinyume na utaratibu.

  Mtu huyo alikamatwa jana katika hospitali hiyo wakati akitaka kufanya vipimo vya (CityScan), ndipo mmoja wa wafanyakazi wa hospitali hiyo alipogundua na kupiga simu makao makuu ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuwataarifu kuhusiana na tukio hilo, ambapo maofisa walifika na kukamata nyaraka hizo huku mgonjwa akitokomea kusikojulikana baada ya kugundulika, Bw. Julius Mziray amewaasa wamiliki wa kadi za Bima ya Afya kutozitumia watu tofauti badala yake zitumie kwa wahusika walioorodheshwa katika bima hiyo tu Jambo ambalo kuwaigiza katika mikono ya sheria na kupata adhabu kali. 2Bw. Julius Mziray mkaguzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF akiwasomea waandishi wa habari maelezo yaliomo katika nyaraka hizo 3 
  Baadhi ya wgonjwa mbalimbali wakisubiri huduma katika hospitali hiyo4 

  0 0
 • 09/10/14--02:20: Article 4


 • 0 0


  BIA ya Kibo Gold Lager imechaguliwa kuwa mshindi wa medali ya dhahabu kwa ubora duniani inayotolewa na ‘Monde Selection’. Kibo ilipokea utambulisho huo wa kimataifa wakati wa sherehe za 53 za kila mwaka zilizofanyika huko Bordeaux, Ufaransa.  

  ‘Monde Selection’ ni tuzo zinazotolewa kila mwaka tangu mwaka 1961, kwa ajili ya bidhaa za vinywaji na chakula. Huendeshwa na kampuni ya Biashara ijulikanayo kama ‘International Institute for Quality Selections’ ya Brussels, Ubelgiji. Bidhaa hizo huonjwa na kujaribiwa ili ziweze kupewa alama ya ubora.

  Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries Ltd (SBL), Bw. Steve Ganon, alisema: “Kama familia ya SBL, tumefarijika sana kusikia habari hii kubwa inayoihusu bidhaa yetu, kitu kama hiki huwa hakitokei hivi hivi; tumekifanya kitokee... Kwa hiyo ninaipongeza timu nzima ya SBL kwa juhudi zao za kujenga imani kwa watumiaji.” 

  Bia ya Kibo Gold ilizinduliwa miaka 15 iliyopita chini ya Kibo Breweries. Kwa bahati mbaya, bidhaa hiyo haikudumu sana sokoni kutokana na kufungwa kwa kampuni ya Kibo Breweries. Nembo hiyo ilichukuliwa na Serengeti Breweries Ltd na kuzinduliwa upya Juni 2012 katika kiwanda cha SBL kilichopo Moshi Brewery ambako ndiko huzalishwa na kusambazwa sehemukubwa ya kaskazini mwa Tanzania katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Tanga na Manyara, kati ya mingine mingi.

  Lengo la bia ya Kibo Gold ni kutanua wigo wa vinywaji vya Serengeti Breweries Ltd na kuwashika watumiaji wa daraja la kati katika soko la kaskazini mwa nchi.  Agosti 2013, Kibo Gold ilibadilishwa na kuwekwa katika chupa yenye shingo ndefu maarufu kama ‘mwanamke nyonga’ ili kwenda na wakati na matakwa ya soko la kisasa.  

  Sasa Kibo ipo katika chupa yenye shingo ndefu ya milimita 500 ikiwa na asilima 5.5 ya kileo inayodumu kwa kipindi cha miezi sita. Kauli mbiu ya Kibo ni ‘Yaone maisha katika mwanga bora.’Bia hii kwa sasa inauzwa rejareja kwa Sh 1,800.

  0 0

  NBC Tanzania announces the appointment of Pius Tibazarwa as Interim Managing Director of NBC Tanzania. Effective 1 October 2014, Pius will succeed Mizinga Melu, who has been appointed Chief Executive of Barclays Africa Regional Management. NBC Tanzania is a subsidiary of Johannesburg listed Barclays Africa Group Limited (BAGL).
  Pius is currently the Treasurer for NBC Tanzania and has recently been on secondment to BAGL in Johannesburg.  Previously he was Head of Global Markets, Head of Trading and Head of Global Markets Sales for Standard Chartered Bank Tanzania.

  In his banking career, Pius has pioneered the introduction of several new products into the Tanzanian market including FX Options, Structured Deposits and Interest Rate Derivatives.

  He holds a Bachelor of Science in Engineering Degree from the University of Dar es Salaam and is a member of the ACI Tanzania Association.

  NBC Board Chairman Dr Mussa Assad said: “As Managing Director of NBC Tanzania, Mizinga has built a strong team which is truly transforming our business. She is leaving the business in a much stronger position from where the team will continue to build on under Pius’s leadership. I wish Pius and Mizinga both well in their new endeavours.”
  Pius will report to Mizinga in her new role as Chief Executive of Barclays Africa Regional Management, as will the country Managing Directors of all BAGL’s businesses outside South Africa.

  0 0

  Mbunge wa  jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa  (kulia) akikabidhi ahadi ya bati 100 alizokuwa ameziahidi mbunge aliyepita marehemu Dr  Wiliam Mgimwa kwa  viongozi wa kijiji cha Mangalali kwa ajili ya ujenzi  wa vyumba vya madarasa  shule ya msingi Lukwambe hadi  sasa ni asilimia 90 ya ahadi binafsi za mbunge aliyefariki  zimetekelezwa jimbo la Kalenga na mbunge Mgimwa.


  Mbunge wa  jimbo la Kalenga Bw Godfrey Mgimwa kulia akikabidhi mchango wake wa Tsh 250,000 kwa ajili ya kusaidia kazi ndogo ndogo  za ujenzi wa zanahati ya kijiji cha Mangalali 
  mbunge wa Kalenga Godfrey Mgimwa akiongoza viongozi kutembelea  ujenzi wa zahanati kijiji cha Mangalali 
  Diwani wa kata ya Ulanda kulia  akitoa ufafanuzi kwa mbunge wa  jimbo la Kalenga Bw Mgimwa  kuhusu maendeleo ya ujenzi wa zahanati kijiji cha Mangalali 
  Katibu  wa mbunge Mgimwa kulia Bw Martine Simangwa  kulia akiteta jambo na mbunge Mgimwa.
  Mwananchi  wa kijiji cha Mangalali akisalimia na mbunge wa jimbo la Kalenga  Bw Godfrey Mgimwa
  Mbunge Mgimwa akidua sanjari na  wananchi wa kijiji cha Mangalali 
  Mmoja kati ya  wananchi wa kijiji cha Mangalali akimpongeza mbunge Godfrey Mgimwa kwa  utendaji kazi mzuri 
  Katibu wa Mgimwa akiwaonya  wana CCM wanaojipitisha  jimboni kwa  sasa 
  Baadhi ya Wananchi wa  kijiji  cha Mangalali  wakiwa katika mkutano wa mbunge wao Bw Mgimwa

   .......................................................................................................
  Na Matukiodaima.co.tz
  MBUNGE   wa  jimbo  wa  jimbo la  Kalenga  Godfrey  Mgimwa  ajipongeza kutumia kiasi cha  zaidi ya Tsh milioni 68 kwa ajili ya  kufanikisha  utekelezaji wa ahadi  zilizotolewa na mbunge  aliyefariki Dr  Wiliam Mgimwa  kwa  asilimia 90 kwa  muda  wa  miezi mitatu pekee .

  Akizungumza na  wananchi  wa  kijiji  cha Mangalali   baada ya  kukamilisha ahadi ya bati 100 kwa ajili ya ujenzi wa  vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Lukwambe , mbunge Mgimwa  alisema  kuwa alianza  kutekeleza  ahadi hizo hata kabla ya  kuapishwa   bungeni na  hadi sasa  bado asilimia 10 pekee ya utekelezaji wa ahadi zilizoachwa na mbunge  aliyefariki  dunia mwanzoni mwa mwaka  huu marehemu Dr Mgimwa ambae alikuwa ni babake mzazi.

  " Ni jambo la kumshukuru  mwenyezi Mungu  kwani ahadi  zilizokuwa  zimetolewa na  mbunge  aliyefariki  dunia marehemu Dr  wiliam Mgimwa  zilikuwa ni asilimia 100 na hadi mnanichangua  kuwa  mbunge ahadi  hizo  zilikuwa  bado kutekelezwa na ndio  sababu ya mimi   katika kampeni kutoahidi  ahadi mpya  zaidi ya  kuzipokea  zile  zilizoachwa na baba ambazo  kimsingi nilizipokea .......ila kwa sasa ahadi  hizo nimetekeleza kwa asilimia 90  bado asilimia 10 pekee ambazo hadi mwakani  nitakuwa nimezimaliza kikubwa naomba mzidi kuniombea  uzima" alisema  mbunge Mgimwa.

  Alisema  kuwa hakuweza  kuahidi ahadi mpya  wakati wa kampeni  hizo za uchaguzi mdogo  jimboni humo kutokana na kuwepo kwa ahadi nyingi ambazo  zilikuwa zimetolewa na mbunge  aliyepita na zilikuwa bado  kutekelezwa na muda  wa   utekelezaji  ulikuwa bado  hivyo aliamua  kuzichukua  zote kama  zilivyo na kuanza  kuzifanyia kazi moja baada  ya nyingine .

  Mbunge Mgimwa alisema  kuwa ahadi  hizo  zinazotekelezwa  ni  zile ahadi  binafsi ambazo mbunge  aliyepita alikuwa amezitoa ila  zipo ahadi mbali mbali ambazo zimo katika ilani ya  CCM ambazo pia  zimeendelea  kutekelezwa  kwa  nguvu  kubwa .

  Hata  hivyo  alisema kuwa ahadi ambazo  zimetekelezwa kwa asilimia 90 ambazo zilikuwa ni ahadi binafsi ni pamoja  na elimu ,afya na  uchangiaji wa  vikundi  vya Vicoba pamoja na uanzishwaji wa  vikundi  hivyo pia katika  sekta ya  michezo na huduma  nyingine  za kijamii kama  upelekaji wa umeme katika maeneo ya kata ya Mgama  na Magulilwa zoezi hilo  linaendelea ambayo   ahadi  hiyo ya umeme  ipo katika ilani ya CCM pamoja na zile za  huduma za maji vijijini ambazo baadhi ya maeneo mradi kata ya Maboga  na kata ya Lumuli wa maji  unatekelezwa .

  Pia  alisema  kuwa bado  anautamani  ubunge wa  jimbo  hilo la Kalenga kwa mwaka 2015 -2020   hivyo kamwe hatawaangusha  wana Kalenga kwa  kipindi  hiki  cha miaka miwili alichopewa  hadi 2010.

  " Ndugu  zangu hii nafasi ya  ubunge  mimi  nimeipata mwishoni ila sikutaka  kuwaangusha  nilitaka kuwaonyesha  utendaji  wangu na kamwe  sitakuwa mbali na ninyi  wananchi  wangu  nitakuwa  bega kwa  bega  kuhakikisha jimbo la Kalenga linapata maendeleo na linakuwa ni  jimbo la mfano katika maendeleo  kule  bungeni kutokana na umri  wangu  wabunge  wananiita bwana mdogo ila  kiutendaji kweli  ni bwana mkubwa kwani kati ya wabunge zaidi ya 300 bungeni  mimi ni mmoja kati ya  wabunge  tuliochanguliwa  kuingia katika kamati ya bunge ya bajeti ya  serikali " alisema mbunge Mgimwa .

  Awali katibu  wa mbunge huyo  Martine Simangwa  aliwaonya  wana CCM ambao  wameendelea  kujipitisha katika  jimbo  hilo na kuwa kwa kufanya hivyo ni kutowatendea haki  wananchi wa  jimbo la Kalenga ambao kwa  sasa wameshikamana na  wapo tayari kuona  maendeleo na sio kampeni za  uchaguzi wa mwaka 2010.

  " wapo  baadhi ya  wana CCM bila haya  wameendelea  kujipitisha kwa wananchi na  kuponda utendaji huu mzuri wa mbunge Godfrey Mgimwa ....sasa  wananchi  nawaombeni  sana msidanganyike na  watu hao kwa sasa mbunge ni Godfrey Mgimwa wakija na kuwapa  pesa chukueni ila msikubali kugawanywa kwa misingi ya pesa kubalini  kuungana katika misingi ya kimaendeleo"

  Kwa upande  wao  wananchi hao  walieleza  kufurahishwa na utendaji mzuri wa mbunge  wao Mgimwa na  kuwa kamwe hawatakubali kudanganyika na kuwa  wamejipanga  kumchukulia  fomu mwakani  ili kuwaongoza vipindi  vingine viwili zaidi baada ya  kuona utendaji  wake mzuri.

  MWISHO 

  0 0

   Rais wa Uganda Yoweri Museveni akiteremka katika ndege iliyomleta leo jijini dar es Salaam kwa ajili ya  ziara yake ya siku moja nchini Tanzania .
   Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akikagua Gwaride la Maaskari pamoja na Mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni baada ya kuwasili  leo jijini  katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Mwalimu Julius Nyerere kwa ajili ya ziara ya siku moja.
   Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete (Kulia) pamoja na mgeni wake Rais wa  Uganda Yoweri Museveni (kushoto) wakiangalia ngoma za utamaduni baada ya kuwasili  katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa  Mwalimu Julius  Nyerere Leo jijini Dar es Salaam ,kwa ajili ya ziara ya siku moja hapa nchini.
  Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete (Katikati)akipata maelekezo kutoka kwa mwongoza msafara na kushoto ni  Rais wa  Uganda Yoweri Museveni  ambaye amewasili nchini leo  kwa ajili ya ziara ya siku moja . ( Picha na Lorietha Laurence-Maelezo).
   Ndege iliyomleta Rais wa Uganda Yoweri Museveni ikiwa imetua katika Kiwanja cha Ndege cha  Kimataifa  Mwalimu Julius Nyerere tayari kwa ziara yake ya kikazi ya siku moja ambapo alipokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete leo jijini Dar es Salaam.


  0 0

   
   Mratibu wa Rock City Marathon  kutoka kampuni ya Capital Plus International Ltd, Bi Grace Sanga (wa kwanza kulia) akipongezwa na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Bw. Dioniz Malinzi (Wa nne kulia) ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika uzinduzi  wa Rock City Marathon 2014, jana jijini Dar es Salaam jana. Mbio hizo zitafanyika tarehe 26 Oktoba katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
   Baadhi ya wawakilishi wa wadhamini wa mbio za Rock City Marathon 2014 pamoja na viongozi wa chama cha mchezo wa riadha Tanzania, wakifuatilia yanayojiri wakati wa uzinduzi wa mbio hizo jana iliyofanyika Jijini Dar es Salaam. Mbio hizo zitafanyika tarehe 26 Oktoba katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
   Msemaji wa Kampuni ya Capital Plus International, ambao ni waandaaji wa mbio za Rock City Marathon, Bw. Mathew Kasonta, akizungumuza na wageni waalikwa katika uzinduzi wa mbio hizo jana iliyofanyika Jijini Dar es Salaam. Mbio hizo zitafanyika tarehe 26 Oktoba katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
   Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF ) Bw. Jumanne Mbepo, ambao ndo wadhamini wakuu wa mbio za Rock City Marathon 2014, akizungumza machache wakati wa uzinduzi wa mbio hizo iliyofanyika Jijini Dar es Salaam jana. Mbio hizo zitafanyika tarehe 26 Oktoba katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
   Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Suleiman Nyambui akizungumza machache wakati wa uzinduzi wa mbio hizo iliyofanyika Jijini Dar es Salaam jana. Mbio hizo zitafanyika tarehe 26 Oktoba katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
  Afisa Uhusiano na mawasiliano wa TSN Group Koiya Kibanga, ambao ni moja wa  wadhamini wakuu wa mbio za Rock City Marathon 2014, akizungumza machache wakati wa uzinduzi wa mbio hizo iliyofanyika Jijini Dar es Salaam jana. Mbio hizo zitafanyika tarehe 26 Oktoba katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.


  ======  =======  ======
  Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Bw. Dioniz Malinzi, amezindua rasmi mbio za Rock City Marathon, zitakazofanyika Oktoba 26 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
  Akizungumza katika uzinduzi huo jana jijini Dar es Salaam, Malinzi alisema mbio hizo zimeweza kuwa ni moja ya mbio zinazoheshimika nchini Tanzania na kuiweka kanda ya ziwa katika kalenda ya michezo kila mwaka. 

  Malinzi aliipongeza kampuni ya Capital Plus International (CPI) kwa kuendelea kujidhatiti katika maandalizi ya mbio hizo na kuziboresha kila mwaka licha ya changamoto nyingi zinazoukabili mchezo huo wa riadha nchini. 

   “Ni kweli kwamba makampuni na hata watu binafsi wamekuwa wakisaidia kukuza mchezo wa riadha hapa nchini, lakini bado mchezo huu unachangamoto nyingi.

  “Jitihada za pamoja zinahitajika baina ya serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, sisi Baraza la Michezo la Taifa (BMT), vyama vya michezo, mashirika na wadau wengine, ili kurejesha heshima iliyopotea miongoni mwa michezo na wanamichezo wa Tanzania, hususani riadha,” alisema Bw. Malinzi. 

  Bw. Malinzi alibainisha kuwa na kuwepo kwa changamoto mbali mbali CPI imekuwa ikijitahidi kuboresha mbio hizo zifanyikazo kila mwaka.
  “Tumeshuhudia viwango vya mbio hizi vikipanda kila mwaka, ambapo ni kielelezo cha maandalizi mazuri yanayofanywa kwa kuzingatia viwango na sheria zilizo wekwa,” aliongeza  Bw. Malinzi. 

  Hata hivyo, Mwenyekiti huyo wa BMT alisisitiza kuwa vyama vya michezo pia vinapaswa kujiimarisha katika kuwaandaa wachezaji kabla ya kuwapeleka kushiriki katika mashindano ya kimataifa ambapo wachezaji hao wanabeba jina la nchi ya Tanzania.

  “Hatunabudi kuimarisha msingi wetu katika kila aina ya michezo hapa nchini, kama bado tunayo ndoto ya kuirudisha ramani ya Tanzania katika ulimwengu wa michezo kama ilivyokuwa zamani,” alisisitiza. 

  Tukio hilo limewavutia wadau wengi wa michezo nchini, ikiwa ni pamoja na makampuni makubwa kama Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Kampuni ya TSN Group Ltd, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), African Barrick Gold, Nyanza Bottlers, Mfuko wa Pensions (PPF), Sahara Communication, ATCL, New Mwanza Hotel, na New Africa Hotel ambao wamejitokeza kudhamini mbio hizo. 

  Kwa upande wake Mwakilishi wa kampuni ya Capital Plus International, Bw. Mathew Kasonta, alisema mbio za mwaka huu zitahusisha mbio za nusu Marathon za kilomita 21, mbio za kujifurahisha maarufu kama Corporate Race za kilomita 5, mbio za watu wenye ulemavu wa ngozi za kilomita 3, mbio za watu wazima za kilomita 3 na mbio za watoto kuanzia miaka saba hadi 10 ambazo ni za kilomita 2.

  Bw. Kasonta alisema kuwa mbio hizo zinaenda sambamba na kuhamasisha Utalii wa ndani kupitia sekta ya michezo, ambapo washiriki watakua ni kutoka kanda ya ziwa Victoria na nchi jirani kama Kenya, Uganda, Afrika Kusini na baadhi yao wakiwa na uzoefu wa kucheza mashindano ya kimataifa ili kutoa ushindani zaidi. 

  “Ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa wafadhili mbalimbali wanaoshirikiana nasi ili kuyafanikisha mashindano haya, kwa niaba ya Capital Plus International, ningependa kuwahakikishia kuwa mashindano ya mwaka huu yataboreshwa zaidi na hivyo yataweza kutupatia wanariadha bora watakaoiwakilisha nchi yetu kikamirifu katika mashindano ya kimataifa,” alisema Bw. Kasonta.

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa  mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu Gold Mine Bw. Peter Burger ( wa kwanza kushoto) akizungumza na jopo la  majajaji na sekretarieti  iliyotembelea mgodi huo  kwa ajili ya kumtafuta mshindi wa  Tuzo ya Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji
   Mwalimu Mkuu wa  Shule ya Msingi ya Ibanza Bw. Dions Kagiye (katikati) akizungumza na  baadhi ya majaji waliotembelea shule hiyo inayofadhiliwa na mgodi wa Bulyanhulu Gold Mine kwa ajili  ya kuifanyia tathmini
   Mmoja wa majaji Dkt. Yohana Mtoni (kushoto) akimsaidia mmoja wa watoto waliofika katika kisima cha maji cha Ilogi kuvuta maji. Kisima hicho kinafadhiliwa na mgodi wa Bulyanhulu
   Meneja Mahusiano wa Mgodi wa Buzwagi uliopo Kahama, Shinyanga Bi. Dorothy  Bikurakule ( wa kwanza kulia  mbele) akiongoza jopo la majaji na sekretarieti kutembelea kituo cha afya cha Mwendakulima kinachofadhiliwa na mgodi huo.
   Meneja Mahusiano wa Mgodi wa Buzwagi uliopo Kahama, Shinyanga Bi. Dorothy  Bikurakule (katikati) akielezea mchango wa mgodi huo katika  uwezeshaji wa kikundi cha vijana cha ufyatuaji wa matofali cha Mwendakulima.
  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mwendakulima Bi. Diana Kuboja akielezea mchango wa mgodi wa Buzwagi Gold Mine katika ujenzi wa shule hiyo  kwa  majaji na sekretarieti iliyotembelea shule hiyo kwa ajili ya kufanya  tathmini.

  0 0

   Washindi wa Tuzo za Habari za TANAPA 2013 wakiwa pamoja na Mhariri Mkuu wa Habari na Matukio wa  Channel  Afrika ya Shirika la Utangazaji la Afrika Kusini (SABC) Busi Chaane (wa tatu kushoto) pamoja na Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Channel Afrika ya SABC Mike Arareng (wa kwanza kulia) walipotembelea studio hizo kwa ziara ya mafunzo.
  Washindi wa Tuzo za Habari za TANAPA 2013. Kutoka kulia ni Vedasto Msungu (ITV), Gerald Kitabu (The Guardian), David Rwenyagira (Radio Five) na Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete katika picha ya pamoja katika ofisi za Shirika la Utangazaji la Afrika Kusini (SABC) jijini Johannesburg. 
   Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Wahariri nchini Afrika Kusini Mathatha Tsedu (mwenye kofia) akimsikiliza kwa makini Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete wakati wa ziara ya mafunzo kwa washindi wa Tuzo za Habari za TANAPA 2013 nchini humo. Baadhi ya washindi hao ni pamoja na Vedasto Msungu kutoka ITV (kulia) na Gerald Kitab.
  Washindi wa Tuzo za Habari za TANAPA 2013 . Kutoka kulia ni David Rwenyagira (Radio Five), Vedasto Msungu (ITV), Gerald Kitabu (The Guardian) na Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete wakiwa nje ya Ofisi za Makao Makuu ya Jukwaa la Wahariri Afrika Kusini.
  Washindi wa Tuzo za Habari za TANAPA 2013 wakifanya  mahojiano ndani ya Studio za Shirika la Utangazaji la Afrika ya Kusini  (SABC- Channel Afrika). Kutoka kushoto ni David Rwenyagira (Radio Five), Gerald Kitabu (The Guardian), Vedasto Msungu (ITV) na Mtayarishaji Vipindi  Isaack Khomo.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Wahariri Afrika Kusini Mathatha Tsedu (wa tatu kulia) akiwa pamoja na Washindi wa Tuzo za Habari za TANAPA 2013. Kutoka kushoto ni Gerald Kitabu (The Guardian), Vedasto Msungu (ITV), David Rwenyagira (Radio Five) na Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete. 

  0 0

   Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia), akikabidhi vitabu vya masomo ya sayansi vyenye thamani ya shilingi milioni 4.5/-, kupitia Mradi wa ‘Airtel Shule Yetu’ kwa Mwakilishi wa Afisa Elimu ya Sekondari Manispaa ya Temeke, Yasintha Kayoza kwa niaba ya shule tatu za sekondari za Mbagala, Mvuti na Kambangwa katika hafla iliyofanyika kwenye Shule ya Sekondari ya Mbagala jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkuu wa Shule ya Sekondari ya  Mbagala, Mwalimu Marcelina Kimario.
    Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (mwenye miwani), akiangalia moja ya vitabu vya masomo ya sayansi baada ya kuvikabidhi vitabu vyenye thamani ya milioni 4.5/-,  kupitia Mradi wa ‘Airtel Shule Yetu’ kwa shule tatu za sekondari za Mbagala, Mvuti na Kambangwa katika hafla iliyofanyika kwenye Shule ya Sekondari ya Mbagala jijini Dar es Salaam jana.
   Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia), akikabidhi vitabu vya masomo ya sayansi vyenye thamani ya milioni 1.5/-, kupitia Mradi wa ‘Airtel Shule Yetu’ kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mbagala, Mwalimu Marcelina Kimario katika hafla iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam jana. Sekondari nyingine zilizokabidhiwa vitabu hivyo ni pamoja na Mvuti na Kambangwa. Kushoto ni Mwakilishi wa Shule ya Sekondari Kambangwa, Mwalimu Sueiba
  Mfinanga.
  Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mbagala wakifurahia vitabu vya masomo ya sayansi, baada ya Kampuni ya Airtel kupitia Mradi wake wa ‘Shule Yetu’ kukabidhi vitabu hivyo vyenye thamani ya milioni 4.5/- kwa shule tatu za sekondari za Mbagala, Mvuti na Kambangwa katika hafla iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam jana.


  ==========  ========  ========
  Airtel yatoa msaada wa vitabu kwa shule za sekondari Dar
  ·         Zaidi ya shule 30 kufaidika na msaada wa vitabu kwa mwaka
  huu,  kupitia mradi wa Airtel “Shule yetu”

  Dar es Salaam, Jumanne 9 septamba 2014, Kampuni ya simu za mkononi ya
  Airtel kupitia mpango wake wa “shule yetu” umeendelea na mpango wake
  wa kuchangia katika kusaidia sekta ya elimu nchini ambapo  leo imetoa
  msaada wa vitabu kwa shule 3 za sekondari jijini Dar es saalam

  Shule zilizofaidika na msaada huo ni pamoja na Kambagwa sekondari
  iliyopo wilaya Kinondoni,  shule ya sekondari Mvuti iliyopo wilaya ya
  Ilala na shule ya sekondari Mbagala iliyopo wilaya ya Temeke ambapo
  kila shule imepata vitabu vyenye thamani ya shilingi milioni moja na
  laki tano.

  Akiongea wakati wa kukabithi vitabu hivyo, Meneja huduma kwa jamii
  Airtel Bi Hawa Bayumi alisema”  Tunayofuraha kuendelea na mpango huu
  wa “shule yetu”  kwa mwaka huu na kuwa na shule mpya zitakazofaidika
  na vitabu vya masomo ya Sayansi. Tunazo shule zaidi ya 30 ambazo
  tumezipata kwa kushirikiana na uongozi wa serikali zitakazofaidika na
  msaada huu wa vitabu kwa mwaka huu,  Na leo tumeweza  kuzifikia shule
  za Kambagwa, Mvuti na Mbagala na kuwapati  vitabu vitakavyoweza kuleta
  tija katika ufaulu na elimu kwa ujumla”.

  “Nia yetu ni kuendelea kushirikiana na Serikali chini ya wizara ya
  elimu katika kuinua sekta ya elimu nchini huku tukiwekea mkazo katika
  masomo ya sayansi kwani tuaamini ulimwengu na nchi inahitaji
  wanasayansi wengi ili kwenda na kasi ya ukuaji wa technologia. natoa
  wito kwa walimu na wanafunzi basi watumie vitabu vizuri na kuweza
  kuongeza wanafunzi wengi katika masomo ya sayansi na hatimae kuongeza
  ufaulu zaidi.aliongeza” Bayumi

  Akiongea kwa niaba ya walimu wakuu wa shule zilizopokea msaada jijini
  Dar es saalam, Mwalimu mkuu wa shule ya Mbagala Bi Marcelina  Kimaro
  alisema” Tunawashukuru sana Airtel kwa  kutufikia leo, tumekuwa
  tukiona shule nyingi zikifaidiaka na mpango huu wa “Shule yetu” na leo
  tunayofuraha kupokea msaada wa vitabu vya  Hisabati, Chemia, physikia
  na Baiologia kutoka Airtel

  Shule hii ya mbagala Sekondari ina jumla ya wanafunzi 2031 na uwiano
  wa vitabu kwa wanafunzi kwa sasa ni kati ya kitabu kimoja kwa
  wanafunzi wa 3 au 4 , kwa msaada huu leo utasaidia kupunguza
  changamoto tuliyonayo ya uhaba wa vitabu na kufanya uwiano kuwa kitabu
  kimoja kwa wanafunzi wawili. Halikadhalika msaada huu utatupatia
  urahisi katika kusoma na walimu kuandaa masomo yao.

  Kimaro aliongeza kwa kusema” Vitabu hivi vimetupa changamoto  kubwa ya
  kuongeza juhudi katika masomo kwani nyenzo sasa tunazo na tunaamini
  wanafunzi wetu wa masomo ya sayansi watasoma kirahisi na hatimaye
  kupata  idadi kubwa ya wanafunzi wanaosoma masomo ya Sayansi.
  Tunawaahidi kuvitunza na kuvitumia vitabu hivi kwa faida ya wanafunzi
  na jamii kwa ujumla”

  Chini ya mpango wa “shule yetu” Airtel imeweza kutoa msaada wa vitabu
  kwa shule za sekondari zaidi ya 1000 nchini huku mpango ukiwa ni
  kizifikia shule nyingi zaidi kila mwaka

  0 0

  Naibu waziri wa Fedha,Mwigulu Mchemba akimkabidhi Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Bodi ya Kahawa Tanzania(TCB) Astery Bitegeko tuzo na Cheti baada ya kushika nafasi ya pili uwasilishaji  michango ya wanachama wa PPF mapema kwa upande wa sekta ya Kilimo.
  Naibu waziri wa Fedha,Mwigulu Mchemba akipeana mkono na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Bodi ya Kahawa Tanzania(TCB) Astery Bitegeko mara baada ya kumkabidhi  tuzo na Cheti baada ya kushika nafasi ya pili uwasilishaji  michango ya wanachama wa PPF mapema kwa upande wa sekta ya Kilimo.
  Naibu waziri wa Fedha,Mwigulu Mchemba akimkabidhi Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa,Allan Kijazi tuzo na Cheti baada ya kushika nafasi ya kwanza kwa sekta zinazotoa huduma nyinginezo kwa uwasilishaji  michango ya wanachama wa PPF mapema kwa upande wa sekta ya Kilimo. 
  Naibu waziri wa Fedha,Mwigulu Mchemba akimkabidhi Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa,Allan Kijazi akionesha tuzo na cheti alivyokabidhiwa mara baada ya kuibuka mshindi wa kwanza kwa taasisi zinazowasilisha michango ya wananchama  wa PPF kwa wakati.
  Baadhi ya washindi wakionesha tuzo na vyeti walivyo kabidhiwa.
  Mgeni rasmi katika mkutano huo wa 24 wa wananchama na wadau wa PPF unaofanyika jijini Arusha wakiwa katika picha na baadhi ya mawaziri pamoja na viongozi wa PPF.
  Washindi wa tuzo wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.
  Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Bodi ya Kahawa Tanzania(TCB) Astery Bitegeko akionesha  tuzo na Cheti baada ya kushika nafasi ya  kwanza  uwasilishaji wa  michango ya wanachama wa PPF mapema kwa upande wa SACCOS. Na Dixon Busagaga wa Globu ya jamii kanda ya kaskazini.


  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Tanzania (kushoto)Moezz Mir akimkabidhi Mkurugenzi Mkazi wa Amref Heath Africa Tanzania Dk. Festus Ilako, hundi yenye thamani ya shilingi milioni 48. Kwa ajili ya kuwasomesha wakunga 10 ambao baada ya kupata elimu wataajiliwa katika vituo vya afya hasa vijijini ili kuwasaidia akinamama wanaohitaji huduma za uzazi.KCB na AMREF wametangaza ushirikiano katika kusaidia suala zima la Afya ya mama na motto nchini hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam, wapili kutoka kushoto ni Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki ya KCB Christina Manyenye na Meneja msimaizi wa mifuko wa jamii wa Amref Lilian Nsemwa.( fund Raising Manager)
  Mkurugenzi Mkazi wa Amref Heath Africa Tanzania Dk. Festus Ilako, akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam (hawapo pichani)wakati alipokuwa akiongelea juu ya ushirikiano wao na benki KCB Tanzania katika kusaidia suala zima la Afya ya mama na motto nchini ,wakati benki hiyo ilipokabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni 48. Kwa ajili ya kuwasomesha wakunga 10 ambao baada ya kupata elimu wataajiliwa katika vituo vya afya hasa vijijini ili kuwasaidia akinamama wanaohitaji huduma za uzazi.Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Tanzania Moezz Mir na Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki ya KCB Christina Manyenye wakimsikiza kwa makini.
  Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB Tanzania Moezz Mir akiongele juu ya ushirikiano wao na Amref Heath Africa Tanzania katika kusaidia suala zima la Afya ya mama na motto nchini ,wakati benki hiyo ilipokabidhi AMREF hundi yenye thamani ya shilingi milioni 48, kwa ajili ya kuwasomesha wakunga 10 ambao baada ya kupata elimu wataajiliwa katika vituo vya Afya hasa vijijini ili kuwasaidia akinamama wanaohitaji huduma za uzazi.Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Amref Heath Africa Tanzania Dk. Festus Ilako, na Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki ya KCB Christina Manyenye hafla ya hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Tanzania (kushoto)Moezz Mir akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkazi wa Amref Heath Africa Tanzania Dk. Festus Ilako, jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akiongerea juu ya ushirikiano wao na benki hiyo katika kusaidia suala zima la Afya ya mama na motto nchini ,benki ya KCB Tanzania imekabidhi Amref hundi yenye thamani ya shilingi milioni 48. Kwa ajili ya kuwasomesha wakunga 10 ambao baada ya kupata elimu wataajiliwa katika vituo vya afya hasa vijijini ili kuwasaidia akinamama wanaohitaji huduma za uzazi.

  0 0

   Mkuu wa matawi wa Benki ya Exim Tanzania, Bi. Agnes Kaganda (mwenye fulana nyeupe)akiwapa somo wafanyabiashara wadogo juu ya umuhimu wa kutumia huduma za kifedha na kibenki ili kukuza biashara zao wakati wa Wiki ya Huduma za Kifedha na Uwekezaji 2014 iliyoandaliwa na kampuni ya Nuebrand iliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
   Mkuu wa matawi wa Benki ya Exim Tanzania, Bi. Agnes Kaganda (mwenye fulana nyeupe)akiwapa somo wafanyabiashara wadogo juu ya umuhimu wa kutumia huduma za kifedha na kibenki ili kukuza biashara zao wakati wa Wiki ya Huduma za Kifedha na Uwekezaji 2014 iliyoandaliwa na kampuni ya Nuebrand iliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
   Mfanyakazi wa kitengo cha mauzo wa Benki ya Exim akizungumza na wateja juu ya huduma za kibenki zitolewazo na benki hiyo wakati wa Wiki ya Huduma za Kifedha na Uwekezaji 2014 iliyoandaliwa na kampuni ya Nuebrand iliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
  Wafanyakazi wa kitengo cha mauzo wa Benki ya Exim wakizungumza na wateja juu ya huduma za kibenki zitolewazo na benki hiyo wakati wa Wiki ya Huduma za Kifedha na Uwekezaji 2014 iliyoandaliwa na kampuni ya Nuebrand iliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam hivi karibuni

  0 0

   Mwezeshaji wa Taasisi ya MAYEPS Tanzania Lucas Marco (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) hivi karibuni jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa kitabu kiitwacho “NITUNZE NIKUTUNZE FAINALI UZEENI”, chenye maudhui ya kuwasaidia watu wanaofanyakazi ya kujiajiri au kuajiriwa kufanya maamuzi yaliyosahihi ili waweze kuishi maisha bora wakati wakiwa kwenye ajira na baada ya kustaafu. Katikati ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Rose Mang’enya na kushoto ni Meneja wa Taasisi hiyo John Masumba.
  1 Mwezeshaji wa Taasisi ya MAYEPS Tanzania Lucas Marco (wa pili kulia) akimpongeza Mwenyekiti wa Taasisi ya MAYEPS Tanzania Rose Mang’enya wakati wa uzinduzi wa kitabu kiitwacho “NITUNZE NIKUTUNZE FAINALI UZEENI” hivi karibuni jijini Dar es salaam. Wa kwanza kushoto ni Meneja wa Taasisi hiyo John Masumba na Afisa Habari Idara ya Habari MAELEZO Eleuteri mangi (kulia). (Picha na MAELEZO).

  Taasisi isiyo ya kiserikali ya MAYEPS Tanzania imezindua kitabu kiitwacho “NITUNZE NIKUTUNZE FAINALI UZEENI”, chenye maudhui ya kuwasaidia watu wanaofanyakazi ya kujiajiri au kuajiriwa kufanya maamuzi yaliyosahihi ili waweze kuishi maisha bora wakati wakiwa kwenye ajira na baada ya kustaafu.

  Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni jijini Dar es salaam, Meneja wa Taasisi hiyo John Masumba amesema kuwa uzoefu unaonesha kuwa wafanyakazi katika jamii ya Kitanzania hawaweki akiba kwa ajili ya kuwekeza kwa madhumuni ya kujenga uchumi. 

  Meneja Masumba amesisitiza kuwa MAYEPS imetambua kwamba ikiandaa warsha moja kwa mwezi juu wafanyakazi kufanya maamuzi yaliyo sahihi, itawafikia watu 600 kwa mwaka.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Rose Mang’enya aliwapitisha waandishi wa habari juu ya yaliyomo kwenye kitabu hicho kwa kuendesha warsha fupi iliyowafungua macho waandishi hao kuhusu namna ya kutunza fedha kuandaa maisha ya baadaye. 

  Akinukuu kauli ya mtaalamu wa uongozi John Maxwell Mwenyekiti huyo alisema kuwa “Watu wanaofanikiwa na wasiofanikiwa hawatofautiani sana kiuwezo bali wanatofautiana katika dhamira ya kufika kilele au upeo wa  uwezo wao”. Mang’enya aliongeza kuwa jukumu la kujenga maisha  binafsi   lipo kwa muhusika binafsi, hivyo, watumishi wawe na msimamo sahihi utakaowawezesha kuwa na maisha bora.

  Aidha, MAYEPS hutoa mafunzo  kwa wafanyakazi wa Umama na binafsi namna ya kupanga matumizi.  Pia hutoa  mafunzo  ambayo yatawezesha wafanyakazi kutambua kuwa fedha za mafao au pensheni hupungua thamani mwaka hadi mwaka hivyo uwekezaji wa fedha hizo ni muhimu ufanywe kwa uangalifu.


  0 0  Price for ticket for student is Tsh 300, 000 or USD 200 
   Due to number of request received from students asking for discount, the committee for preparation of CDEA14 has resolved to offer a 40% discount to student, now the price is USD 200 or Tsh 300,000 (terms and conditions  apply).

  Deadline for registration will be this Friday 12th Sept 2014
  Call us on +255 719 25 30 37 or email us on registration@nrd.no
  You can also visit us on our websites
  NRD East Africa
  3rdfloor,   Elite tower
  Azikiwe Street Dare s salaam

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea baadhi ya machapisho ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) kutoka kwa Rais wa Baraza hilo, Jaji Thomas Mihayo, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Septemba 11, 2014. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na viongozi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) wakati walipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Septemba 11, 2014 kwa ajili ya mazungumzo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Septemba 11, 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Kaimu Katibu Mtendaji na Meneja Nyaraka na Machapisho wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) John Mirenyi baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Septemba 11, 2014. Picha na OMR

  0 0

  Kampuni ya SMART CODES inayojishughulisha na teknolojia ya mtandao, imezindua huduma mpya na ya bei nafuu kuwawezesha wafanyabiashara wote duniani hususani Tanzania kuweza kuweka bishara zao kwenye mtandao (Website).
  Huduma hiyo itawezesha wafanyabiashara wakubwa na wale wadogo kusajili maji na ya biashara zao kwenye kikoa cha Tanzania DotTZ (.tz) mfano www.jinalabiasharayako.co.tz napia kukupa emails nyingi utakavyokupitia jina la biashara yako. Mifano ya email unazoweza kupata ni kama vile wewe@jinalabiasharayako.co.tz ambazo zitakuwezesha kufanya biashara kisasa zaidi. Pia kupitia huduma hiyo ya Patikana utapata Tovuti/Website ya kuanzia BURE kabisa.
  Akitoa taarifa hizo Mkurugenzi Mkuu wa SMART CODES bwana Edwin Bruno, amesema “Kwa sasa wafanyabiashara wengi wamekua wakipoteza wateja wengi wanaowatafuta mtandao nikutokana na kutokua na Website zinazo onyesha huduma wanazozitoa, hapo ndipo tulipoona ni vizuri kuwapa watanzania wote huduma hii kwa bei sawa na bure ya TSH. 199,000 Tu! Ambapo atapata Domain Name, Hosting , Emails na Tovuti ya kuanzia”
  Ili kuweza kufurahia huduma hii tembelea tovuti ya PATIKANA sasa hapa www.patikana.co.tz na ufuate maelekezo ya jinsi ya kujisajili.
  Pia unaweza kuangalia video iliyopo kwenye mtandao wa huduma za PATIKANA hapa

  Kwa maelezo zaidi wapigie simu kupitia 0658511115 au watumie barua pepe; support@patikana.co.tz

  0 0  0 0

  Wadau wa madini ya vito kutoka sehemu mbalimbali duniani, wakipatiwa huduma katika Banda la Tanzania katika Maonesho ya 54 ya Kimataifa ya Vito na Usonara – Bangkok, Thailand.
   Makamu wa Rais wa Taasisi ya Wafanyabiashara wa Madini ya Vito – Thailand, ambao ndiyo waandaaji wa Maonesho ya Vito ya Bangkok, Tony Brooks akizungumza na baadhi ya Watanzania wanaoshiriki katika Maonesho hayo nchini Thailand alipotembelea Banda la Tanzania.
   Mkuu wa Banda la Tanzania katika Maonesho ya Vito ya Bangkok ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Uthaminishaji wa Madini ya Almasi na Vito cha Wizara ya Nishati na Madini (TANSORT), Archard Kalugendo  akimweleza mdau wa madini ya vito aliyetembelea banda hilo kuhusu fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo nchini Tanzania. Mbele yao ni vinyago vilivyochongwa kutokana na miamba.
   Mfanyabiashara wa madini ya vito kutoka Tanzania, Peter Pereira akimhudumia Mteja aliyefika katika Banda la Tanzania kwenye Maonesho ya Vito ya Bangkok. Maonesho hayo ya siku tano yalianza Septemba 9 mwaka huu.

   Mfanyabiashara wa madini ya vito kutoka Tanzania, Latifah Abdallah akitoa maelezo kuhusu madini hayo kwa wadau waliotembelea Banda la Tanzania katika Maonesho ya Vito ya Bangkok.
   Baadhi ya Washiriki kutoka Tanzania katika Maonesho ya Vito ya Bangkok wakipozi kwa picha muda mfupi kabla ya kuanza  kwa siku ya tatu ya maonesho hayo. Kutoka Kushoto ni Asimwe Kafrika, Iddi Pazzi, Gregory Kibusi, Nelson Magawa, Teddy Goliama na Matiko Sanawa.

  =======  =======  ======
  WACHIMBAJI WADOGO ‘WAIFAGILIA’ SERIKALI
  ØWauza madini yao Thailand
  ØWasifu jitihada kuwainua kiuchumi
  Na Veronica Simba - Bangkok

  Wachimbaji wadogo na wafanyabiashara wa madini ya vito nchini, wameishukuru na kuipongeza Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, kwa jitihada inazofanya za kuwaendeleza na kuwainua kiuchumi.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika Maonesho ya Kimataifa ya Vito na Usonara yanayoendelea jijini Bangkok, nchini Thailand Viongozi waliowawakilisha wachimbaji wenzao katika maonesho hayo, Gregory Kibusi na Kassim Pazi walisema Serikali imewapa fursa adhimu kwa kuwawezesha kujionea na kujifunza zaidi kuhusu sekta hiyo ili waendane na viwango vya kimataifa na kumudu ushindani wa soko.

  “Hatua iliyochukuliwa na Serikali kuandaa na kuwezesha ushiriki wa wachimbaji wadogo na wafanyabiashara wa madini ya vito kuja kushiriki maonesho makubwa kama haya inastahili kupongezwa,” alisema Pazi.

  Alifafanua kuwa ushiriki wa wachimbaji na wafanyabiashara wa vito utawapa fursa kupanua mtandao na wigo wa biashara kwa kukutana na wadau wa madini hayo kutoka sehemu mbalimbali duniani na kubadilishana uzoefu katika kazi hiyo.
  Aliongeza kwamba fursa hiyo pia imewawezesha kutambua aina ya madini ya vito yaliyo katika soko ili kuwarahisishia kuzalisha madini hayo kwa wingi badala ya kuzalisha kwa kubahatisha tu hali inayopelekea kukosa soko na kupata hasara.
  “Siku za nyuma kwa mfano, kuna madini tuliyokuwa tunayatupa tu kwa kudhani hayana thamani, lakini tumeshangaa kwamba katika maonesho haya, wadau wengi wanayaulizia. Tumechukua mawasiliano yao ili tukirudi nyumbani tuwatumie,” alisema Pazi.
  Kwa upande wake, Kibusi alisema ushiriki wao katika maonesho husika umekuwa wenye tija kwa kiasi kikubwa kwani mbali na kupanua wigo wa mtandao na soko, pia wameweza kuuza shehena kubwa ya madini kwa bei nzuri.
  “Sisi kama Viongozi, tunawajibika kuhakikisha wachimbaji wenzetu waliobaki nyumbani wananufaika pia kwa namna moja au nyingine kutokana na ushiriki wetu katika maonesho haya, hivyo tutahakikisha tunaandaa semina na kuwashirikisha tuliyoyaona na kujifunza huku,” alisema Kibusi.
  Aidha, alitoa ushauri kwa Serikali kuwapatia nafasi kubwa ya ushiriki wachimbaji wadogo katika Maonesho ya Vito yanayotarajiwa kufanyika Arusha mwezi Novemba mwaka huu ili wapate fursa ya kukutana na wadau wao kutoka sehemu mbalimbali duniani na kujifunza.
  Naye Kiongozi wa Ujumbe wa Watanzania wanaoshiriki katika maonesho hayo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Uthaminishaji wa Madini ya Almasi na Vito cha Wizara ya Nishati na Madini (TANSORT), Archard Kalugendo alitoa wito kwa wachimbaji na wafanyabiashara wa madini ya vito kuyatumia maonesho hayo kuboresha kazi na biashara zao.
  Alisema, lengo la Serikali ni kuona madini ya aina zote yakiwamo ya vito na usonara yanainufaisha nchi na wananchi wake ipasavyo ndiyo sababu Serikali inatumia njia na mbinu mbalimbali kuwezesha maendeleo hayo.
  “Sisi kama Serikali, tumefungua njia kwa wachimbaji na wafanyabiashara wa madini ya vito nchini. Ni vema sasa wakaanza kusimama wenyewe taratibu ili kuendelea kujifunza na kufanya shughuli zao kwa viwango vya kimataifa waweze kumudu ushindani wa soko,” alisema Kalugendo.
  Aidha, Kalugendo aliwataka wachimbaji na wafanyabiashara waliopata fursa kushiriki maonesho ya Bangkok, kuwa mabalozi wazuri ili wawasaidie wenzao pasipo ubinafsi wala choyo.
  Alisema ni wakati sasa madini ya vito yaingize fedha nyingi katika uchumi wa nchi na hivyo alitoa changamoto kwa wachimbaji na wafanyabiashara kushirikiana na Serikali ili kuhakikisha wanatekeleza mikakati iliyowekwa ya kuhakikisha wadau mbalimbali wa madini ya vito wanakuja kwa wingi Tanzania badala ya kuwafuata wao nje ya nchi.
  “Ifike mahala tusilazimike kuleta madini yetu Bangkok, bali Wa-Thailand na mataifa mengine waone umuhimu wa kuja kwetu,” alisisitiza Kalugendo.
  Hii ni mara ya pili kwa Wizara ya Nishati na Madini kupitia TANSORT kuratibu na kuwezesha ushiriki wa Tanzania katika Maonesho ya Kimataifa ya Vito na Usonara ya Bangkok ambapo wachimbaji wadogo na wafanyabiashara wa madini hayo hushirikishwa.
  ---mwisho---
  Imeandikwa Septemba 11, 2014.
  CHUO CHA JIMOLOJIA KUKUZA MAPATO YA MADINI
  ØNi kwa kuongeza thamani madini vito
  ØMasomo kuanza Januari
  Na Veronica Simba – Bangkok
  Imeelezwa kuwa Chuo cha Mafunzo ya Jimolojia kinachotarajiwa kufunguliwa mapema mwakani jijini Arusha, kitakuza kwa kiasi kikubwa mapato yatokanayo na madini ya vito hapa nchini na hivyo kuchangia kuinua uchumi wa Taifa.
  Hayo yalielezwa jana na Mratibu wa Kituo cha Jimolojia cha Tanzania (Tanzania Gemological Centre - TGC), Mussa Shanyangi katika Maonesho ya Kimataifa ya Vito na Usonara yanayoendelea jijini Bangkok nchini Thailand.
  Shanyangi alisema miongoni mwa kozi zinazotarajiwa kufundishwa chuoni hapo ni Elimu ya Ukataji Madini ya Vito (Lapidary) ambayo inalenga kuwaandaa wanafunzi kuwa wataalamu wa fani ya uongezaji thamani madini kwa kuyakata na kuyachonga katika maumbile tofauti ya kuvutia.
  Alisema kwa sasa Tanzania ina upungufu mkubwa wa wataalamu wa kukata na kuchonga madini ya vito hali inayosababisha kuuza madini hayo yakiwa ghafi na hivyo kupunguza thamani na faida yake kuwa ndogo.

  “Wafanyabiashara wanalazimika kuajiri wataalamu kutoka nje ya nchi na kuwalipa fedha nyingi kwa madai kuwa wataalamu wazawa katika fani husika ni wachache sana. Chuo kitazalisha wataalamu wazalendo waliobobea katika fani husika na hivyo kuondoa kabisa tatizo hilo,” alisema Shanyangi. Alisema, maandalizi ya kuanza Chuo hicho yapo katika hatua nzuri ambapo tayari mitaala ilikwishatengenezwa na zoezi la kupata Walimu linaendelea.

  Shanyangi alitaja kozi nyingine zinazotarajiwa kufundishwa Chuoni hapo kuwa ni Jimolojia, Uchongaji vinyago kwa kutumia mawe ya urembo pamoja na Kozi ya utengenezaji bidhaa za mapambo.

  Akitoa maelezo zaidi kuhusu mkakati wa kukuza Kituo cha Jimolojia (TGC), Shanyangi alisema lengo hasa ni kuwa na Taasisi kubwa ambayo mbali na kuwa na Chuo husika, pia itakuwa na Maabara ya Mawe (Gem Testing Laboratory) itakayofanya kazi ya kutambua na kutoa uthibitisho (certification) wa mawe mbalimbali.

  Vilevile, alisema Taasisi hiyo itakuwa na Makumbusho ya Madini ya Vito (Gem Museum and Jewelry) itakayotumika kuhifadhi mawe ya vito ya aina mbalimbali yanayopatikana nchini na kutoka nje ya nchi.

  Alisema kuwa taasisi hiyo itakuwa na Maabara ya Jimolojia itakayotumiwa na Wanafunzi wa Chuo lakini pia na watu wengine mbalimbali wenye kuhitaji kujifunza na kuongeza uelewa kuhusu taaluma hiyo.

  Akizungumzia kuhusu ushiriki wake katika Maonesho ya Vito na Usonara ya Bangkok, Shanyangi alisema lengo ni kukitangaza Chuo hicho kipya kwa wadau na kuwapa fursa ya kuomba kujiunga na masomo katika Muhula wa kwanza wa masomo utakaoanza Januari, 2015.

  Alitaja madhumuni mengine kuwa ni kutangaza bidhaa mbalimbali zinazochongwa na vijana wa TGC kutokana na mawe mbalimbali ili kuziongezea thamani.
  ---mwisho---
  Imeandikwa Septemba 11, 2014.   

  0 0

  President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete officiates the opening of the 3rd National Conference on “Enleashing Growth Potentials in Tanzania:Economic Transformation for human Development”, held at Hyatt Regency Kilimanjaro Hotel in Dar es Salaam this morning.The Conference was organized by Economic and Social Research Foundation ESRF.Second left seated is the ESRF Chairperson of the Board of Trustees Mr.Philemon Luhanjo and third left seated is the ESRF Executive Director Dr.Hoseana Bohela Lugonelo.(photo by Freddy Maro).


older | 1 | .... | 360 | 361 | (Page 362) | 363 | 364 | .... | 1896 | newer