Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 359 | 360 | (Page 361) | 362 | 363 | .... | 1898 | newer

  0 0

  The Cyber Defense East Africa 2014 will take place on 16th to 19th September next week with the MAIN theme “Fighting against Financial and Data privacy crime. The guest of honor in this event will be the Minister of Home Affairs, Hon Mathias Chikawe. Speakers from BOT, TCRA, Police Cyber Crime unit, Legal Sector Reform and international experts in forensic science and defense in depth from Europe will attend the event.   To get your ticket call +255719233037 or send email to registration@nrd.no 

  0 0

   Mbunge wa Jimbo la Morogoro kusini Mh Innocent Kalogeris (kulia) Ahimkabidhi Pikipiki 11 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Vijijini Mh Jazar Ikiwa Ni ahadi yake aliyoitoa ya Kukusaidia chama cha Mapinduzi Kujitegemea Kiuchumi.Mh Kalogeris Amekabidhi pikipiki hizo akiwa na Lengo Kila kata Kuwa na Pikipiki MMoja uwe Mradi wa Chama ili kuwezesha Kila kata Kuendesha Shuguli za Chama Bila kuwa wategemezi .Mbunge Kalogeris amehadi kuhakikisha kata zote za jimbo hilo zinapatiwa Pikipiki.Mh Kalogeris amesisitiza Pikipiki hizo ni mali ya CCM Wilaya ya Morogoro Vijijini na si mali ya watu binafsi. 
   Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mh Innocent Kalogeris  Akitoa hotuba yake Namna atakavyoshirikiana na Wanachama na Viongoizi wa Jimbo la Morogoro Kusini bega kwa bega ili chama hicho kiweze kujitegemea kiuchumi kwajili ya kutekeleza Majukumu yake ya Kila siku Ikiwemo Kushinda kwa kishindo Uchaguzi wa serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu mwaka 2O15.
  Mwenyekiti wa CCM Morogoro Vijijini Mh Jazar akisisitiza jambo wakati akitoa neno la Shukrani mara Baada ya Kupokea Msaada ikiwa ni Utekelezaji wa Ahadi ya Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini  Mh Kalogeris aaliyoitoa kwajili ya kukifanya Chama cha Mapinduzi Kujitegemea Kiuchumi.
   Wanachama na wapenzi wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Morogoro vijijini waliojitokeza wakati wa Kupokea Msaada huo.    Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Vijijini Mh Jazar (Kulia) Akikabidi Pikipiki kwa Mmoja wa Mwakilishi wa kata zinazounda Wilaya ya Morogoro mjini Ikiwa kama mrdi wa kukiwezesha chama hicho kujitegemea

  0 0


  Barclays Africa Group announces the appointment of Mizinga Melu as Chief Executive of Barclays Africa Regional Management. Effective from 1 October 2014, Mizinga will be responsible for the group’s businesses outside of South Africa.

  Commenting on the appointment, Barclays Africa Group Chief Executive Maria Ramos said: “I am excited that we were able to appoint someone with such breadth of skills and experience into this role. Her appointment will be instrumental in executing our strategy on the continent.”
   
  Mizinga joined the then Absa Group in March 2013 as Managing Director of NBC Tanzania, where she built a strong team who are transforming that business. She is leaving the business in a much stronger position from where the team will continue to build. Previously Mizinga held a number of roles at Standard Chartered including: CEO of Standard Chartered Zambia, Global Head of Development Organisations in the UK, and Africa Regional Head of Financial Institutions in both South Africa and Kenya. 

  With an MBA from Henley Management School and deep experience across many countries in Africa, Mizinga brings a wealth of expertise and experience to the role.

  The country Managing Directors of all Barclays Africa’s businesses outside South Africa will report to Mizinga, who will co-ordinate integrated planning and ensure the development of product-led and country-specific strategies, as well as support their execution. In addition, Mizinga will oversee the development of stakeholder relationships with governments, regulators, the Boards and customers in the countries.
  Mizinga will report to David Hodnett, Deputy CEO of Barclays Africa Group.

  0 0

    Gari inauzwa kwa bei nzuri tu na ipo Dar kwa atakayeipenda tuwasiliane kupitia mawasiliano hapo chini
  SPECIFICATIONS ZA GARI HIYO NI
  MAKER: TOYOTA
  MODEL: VEROSSA
  YoM:      2001
  CC:       1980
  Odo:   65,944KM
  Color : BURGUNDY
  KWA MAWASILIANO
  0713327106/0756673327.
   

  0 0


  JAJI  Mstaafu wa Tanzania,Agustino Ramadhani amechaguliwa kuwa rais wa  Mahakama ya Haki za Binadamu ya Afrika(AfCHPR) , kwa kipindi cha
  miaka miwili hadi  mwaka 2016.


  Pia katika  jopo la majaji hao   Elsie Thomposon kutoka Nijeria  naye
  ameibuka kidedea kwenye uchaguzi huo uliofanyika juzi katika   viwanja vya
  mahakama hiyo na kushika nafasi ya kuwa makamu wa Rais wa mahakama
  hiyo.


  Akiongea na waandishi wa habari mara baada ya uchaguzi huo kuisha,
  Jaji Mstaafu Ramadhani alishukuru kwa majaji wenzake kumchagua
  kuiongoza mahakama hiyo kwa kipindi hicho.


  Aidha alisema kuwa katika  nafasi aliyoipata ni sifa kubwa kwa nchi ya Tanzania na nchi za Afrika kwani  kwa Tanzania nafasi hiyo ni  changamoto ya
  kuhakikisha haki za binadamu zinalindwa na kuheshimiwa na kila mtu.


  “Nawashukuru wenzangu kwakuniichagua na pia hii ni sifa kwa nchi yangu
  na  wenzetu wakiona tunafaa kuongoza  tunaweza  tena mara baada ya
  kumaliza  nafasi zetu mwaka 2016 , hivyo hii ni heshima kwa Taifa
  letu”.


  Jaji Ramadhani amepata nafasi hiyo mara baada ya  aliyekuwa Rais wa
  mahakama hiyo,  Jaji Sophia  na  Akkufo  kumaliza muda wake.

  Awali kulitanguliwa na kuwaapisha majaji wengine wapya watatu ambao ni
   Jaji Rafaa Achour kutoka Jaji Solomy Basa ,  pamoja na Jaji  Angelo
  Mahesa  ambao wameapishwa jana kuziba nafasi zilizoachwa wazi na
  majaji wengine watatu waliomaliza muda wao akiwemo Akuffo .


  Halfya ya kuapishwa kwa  majaji hao pia ilihudhuriwa na viongozi wa
  dini kutoka mahehebu mbalimbali pamoja na viongozi wa serikali.

  Mara baada ya kuapishwa kwa majaji hao na uchaguzi  kumalizika  Rais
  wa mahakama hiyo, Jaji mstaafu   Ramadhani alisema kuwa kazi ya
  mahakama hiyo ni kusimamia haki za binadamu pamoja na kuhakikisha
  inatoa maamuzi katika kesi mbalimbali zilizofikishwa mahakamani hapo .

  HABARI KWA HISANI ya  woindeshizza blog

  0 0

  Je wewe ni mrembo, mrefu mwembaba unayejiamini? Usisite kuchukua forms za kujiunga na Miss Universe Tanzania 2014 katika mikoa ifuatayo MWANZA (LULU SANGA- 0715471412); IRINGAna MBEYA ( VERONICA KILEMILE- 0782488030); ARUSHA (GADIOLA0715643633/0784643633) na DAR ES SALAAM waone au wasiliana na  (SEIF KABELELE/MWANAKOMBO SALIM - 0655441165/0713302075) Ukiona tangazo hili mjulishe na mwenzio.
   RATIBA YA USAILI.
  Yale mashindano ya kumsaka mwakilishi katika mashindano makubwa kabisa ya ulimbwende ulimwenguni Miss Universe Tanzania 2014 yameanza rasmi, Kama wewe ni mrembo mwenye vigezo vyote usisite kutimiza ndoto yako na ratiba ya usaili ni kama Ifuatavyo:- MWANZA tutakua Gold Crest tarehe 14 /09/2014 saa 4 asubuhi mpaka saa 9 alasiri. ARUSHA Tarehe 12/09/2014MBEYA NA IRINGA Tarehe 16/09/2014 na DAR ES SALAAM itakua tarehe 19/09/2014 Ukumbi na muda mtatangaziwa punde. Kwa maelezo zaidi piga namba 0655441165/0713302075

  0 0

  Na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma

  BUNGE Maalum la Katiba leo tarehe 9 Septemba, 2014 limeanza kazi yake ya kusoma na kujadili taarifa za Kamati mbalimbali zikiwemo Kamati namba Kumi na Mbili, Kamati namba Mbili, Kamati namba Moja, Kamati namba Nne, Kamati namba Nane, Kamati namba Tano, Kamati namba Tisa, Kamati namba Tatu, Kamati namba Sita pamoja na Kamati namba Kumi na Moja.

  Baadhi ya mambo yaliyojadiliwa katika Bunge hilo ni pamoja suala la baadhi ya viongozi kumiliki akaunti zao za fedha nje ya nchi, haki za makundi mbalimbali nchini, haki za binadamu, masuala ya ndoa ya jinsia moja, haki za wafanyakazi na ajira, wajibu wa Waajiri nchini, haki za uzazi kwa wanawake, haki ya kuishi na sheria ya kunyonga, pia mambo yanayohusu Muundo wa Baraza la Usalama la Taifa.

  Akizungumza wakati wa mjadala huo katika Bunge hilo, mjumbe wa Kamati namba Sita, Mhe. Charles Mwijage amesema kuwa si vema kwa viongozi nchini kujenga tabia ya kufungua akaunti na kuweka fedha zao nje ya nchi kwani kunakaribisha masuala ya wizi wa fedha toka ndani ya nchi kwenda nje ya nchi.

  “Ni vema kiongozi yoyote anayetaka kumiliki fedha nje ya nchi aeleze ni wapi anamiliki hizo akaunti na nini anamiliki”, alisema Mhe. Mwijage.


  0 0

  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango), Bi Joyce Mkinga (Kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati alipokuwa akitoa taarifa ya kufanyika kwa Mkutano wa Maafisa Mipango unaotarajiwa kufanyika Mwezi wa Oktoba mwaka huu. Kulia ni Mchumi Mkuu (Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango), Bw. Omary Juma.


  0 0

  Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Mhe. John Cheyo akitoa tamko kuhusu mchakato wa Katiba na Uchaguzi Mkuu wa 2015 leo 9 Septemba, 2014 katika Ukumbi wa Idara ya Habari Bungeni mjini Dodoma.
  Picha na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma
  ----------------------------
  VIONGOZI Wakuu wa Vyama vya siasa vyenye Wabunge vinavyounda Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) wamekuwa katika mashauriano ya zaidi ya mwezi mmoja tangu tarehe 2 Agosti mwaka huu huku wakishauriana juu ya mwenendo wa mchakato wa Katiba Mpya na jinsi ya kuwa na uchaguzi ulio huru na wa haki hapo mwakani. 

  Akiongea kwa niaba ya viongozi wengine wa kituo hicho, Mhe. John Cheyo amesema kuwa Katika mashauriano hayo yaliyochukua sura ya Kamati ya Makatibu Wakuu, Kamati ya Wenyeviti wa Vyama vya CCM, CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi katika hatua tofauti.

  Mhe. Cheyo ameeleza kuwa kamati zote zilitoa taarifa zao kwenye vikao vya Viongozi Wakuu wa Vyama (Summit) ya TCD ambayo wajumbe wake ni Wenyeviti, Makamu Wenyeviti na Makatibu Wakuu wa Vyama wanachama.
  Mhe. Cheyo aliongeza kuwa katika kutafuta maridhiano, Wenyeviti na Makatibu Wakuu wa Vyama walifanya mashauriano na Mhe. Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete siku ya Agosti 31 na tena Nane Septemba 8, 2014 hapa Ikulu ndogo mjini Dodoma. 

  “Pamoja na kazi ya msingi inayofanywa na Bunge Maalum la Katiba, mchakato wa Katiba unaoendelea sasa hauwezi kutupa Katiba itakayotumika katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwa kuwa muda hautoshi kukamilisha mchakato na kufanya mabadiliko yatakayohitajika ya Sheria, Kanuni na Taasisi mbalimbali zitakazohitajika”, alisema Mhe. Cheyo.
  Mhe. Cheyo aliendelea kwa kusema kuwa, kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba mwisho wa mchakato ni kura ya maoni itakayofanyika mwezi Aprili 2015.

  “Kama itabidi kura irudiwe kwa mujibu wa Sheria iliyotajwa, kura itarudiwa mwezi Juni au Julai 2015, muda ambao Bunge la Jamhuri ya Muungano linatakiwa livunjwe kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba 2015 na ili Katiba Mpya itumike katika uchaguzi Mkuu utakaokuja, itabidi uhai wa Bunge na Serikali uongezwe zaidi ya 2015, jambo ambalo hatuliungi mkono”, alisisitiza Mhe. Cheyo.

   Mhe. Cheyo amesema kuwa Bunge Maalum la Katiba kwa sasa linafanya kazi kwa mujibu wa Tangazo la Serikali (Government Notice) Na 254 lililotolewa na Mhe. Rais Kikwete tarehe 1 Agosti, 2014.

  “Tangazo hilo litatumika hadi tarehe 4 Oktoba, 2014 ambapo Katiba inayopendekezwa inategemewa kupatikana, Wajumbe walikubaliana hatua hii iachwe ifikiwe”, alisema Mhe. Cheyo.Kuhusiana na Kura ya maoni, Mhe. Cheyo ameeleza kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba baada ya Bunge hilo kumaliza kutunga Katiba, ingefuata hatua ya kura maoni kuthibitisha Katiba.

  “Kwa kutambua kuwa hatua ya kura ya maoni italazimisha uchaguzi mkuu 2015 kuahirishwa, basi hatua hii iahilishwe, na mchakato wa Katiba uendelee baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2015”, alisema Mhe. Cheyo.
  Sambamba na hayo, Mhe. Cheyo ameishauri Serikali kuchukua hatua za kisheria ili matayarisho kwa ajili ya Uchaguzi wa Vijiji, Vitongoji na Mitaa, yaanze haraka iwezekanavyo ili uchaguzi ufanyike mapema hapo mwakani.

  Aidha, amegusia kuhusu Mabadiliko ya 15 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 akasema kuwa, kwa vile Uchaguzi Mkuu wa 2015 utafanyika kwa kutumia Katiba ya 1977, kuna umuhimu kufanya mabadiliko kidogo (minimum reforms) katika Katiba pamoja na sheria ya Uchaguzi yatayowezesha nchi kufanya uchaguzi huru na wa haki.

  “Tayari mambo yafuatayo yamekubaliwa, kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi kusimamia uchaguzi, Mshindi wa Uchaguzi wa Rais ashinde kwa zaidi ya asilimia 50% (50%+1)”, alisema Mhe. Cheyo.Viongozi hao Wakuu wa Vyama wamempongeza Mhe. Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa ujasiri wake na imani yake katika kuimarisha demokrasia nchini na kuanzisha mchakato wa kuandika Katiba Mpya ya nchi. 

  “Tunampongeza kwa kukubali kukutana na kushauriana nasi kuhusu mambo ya muhimu kwa mustakabali wa taifa letu kwa lengo la kudumisha amani, upendo na mshikamano ili nchi yetu iende kwenye uchaguzi ikiwa ni nchi ya kujivunia yenye amani, mshikamano na itakayokuwa na Uchaguzi Huru na wa haki, lakini pia tunajipongeza sisi wenyewe Wakuu wa Vyama kwa kuwa tumetoka mbali na misimamo yetu, lakini utaifa umetufanya tukubaliane katika mambo ya msingi wa Taifa letu”, alipongeza Mhe. Cheyo.

  0 0

  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewataka wanasheria kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki waweke mbele maslahi ya wananchi wa kawaida wakati wanapoingia mikataba na wawekezaji kwenye sekta ya madini.

  Ametoa wito huo leo mchana (Jumanne, Septemba 9, 2014) wakati akifungua semina ya siku tano juuya mafunzo ya kuingia makubaliano na mikataba kwenye sekta ya madini kwa wanasheria wa sekta ya umma kutoka nchi wanachama wa Jumuiya hiyo ulioanza leo kwenye hoteli ya Whitesands jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza na washirki wa mkutano huo kutoka Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Tanzania, Waziri Mkuu Pinda alisema wanapaswa wawajali sana wananchi walio maskini kwa sababu wao hawana fursa ya kuingia kwenye vikao kama vyao na kutoa sauti juu ya kile wanachokitaka.

  “Muwapo ofisini kwenu au kwenye miji yenu mikuu, mnapojadiliana na wawekezaji na kufikia makubaliano kuhusu rasilmali za nchi, siku zote muwafikirie hawa watu wa chini, walio maskini ambao ni wengi na wako nje ya majengo yenu.”

  “Wao ndiyo wadau wakuu lakini hawana uwezo wa kuingia kwenye vikao kama hivi, sote tunatambua kwamba wameishi na hizo rasilmali kwa vizazi vingi tu. Licha ya umaskini wao, wanaishi juu ya ardhi ambayo chini yake kuna utajiri tele wa madini na rasilmali nyingine.  Ninawasihi sana muwafikirie watu hawa kabla ya kufanya maamuzi yoyote,” alisisitiza Waziri Mkuu.

  Alisema ili jambo hilo liweze kufanikiwa ni lazima, wanasheria kama wadau wa mwanzo kabisa, wakubali kukataa pokea fedha chafu na vishawishi kutoka kwa wawekezaji na siku zote waweke uzalendo mbele kwa maslahi ya nchi zao.

  “Rasilmali za bara la Afrika hazijaleta maendeleo kwa wakazi wakazi wa bara hili kwa sababu wanaofaidika ni makampuni makubwa kutoka nje na watu wachache sana wenye nafasi huku walio wengi wakiambulia patupu. Ni theluthi moja tu ya mikataba ya uchimbaji madini inayolifaidisha bara zima la Afrika ikilinganishwa na faida ambayo bara la Amerika Kusini inanufaika nalo.”
   
  Ili kuepukana na hali hiyo, Waziri Mkuu alisema umefika wakati wa kukataa kutoa misamaha ya kodi kwa makampuni ya kimataifa na kuhakikisha kuwa makampuni hayo yanalipa kodi katika kila nchi husika ya Afrika Mashariki. “Natumaini hii semina itasaidia kutufungua macho katika maeneo ambayo mikataba yetu na sheria zetu zilikuwa zinalegalega, ili kuanzia sasa tuweze kunufaika na rasilmali zetu,” alisema.

  Alisema umefika wakati wa kuhakikisha Serikali za nchi husika zinaweka sera madhubuti na miongozo ya kisheria itakayohakikisha mikataba inayoandaliwa kwa ajili ya utafutaji na uendelezaji wa madini na rasilmali zake inazinufaisha nchi kwanza.

  Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano huo, Waziri Mkuu alisema semina hiyo ni muhimu kwa sababu wanaolengwa ni wanasheria kutoka Afrika Mashariki na Afrika ndilo eneo pekee lenye rasilmali ambazo bado hazijaendelezwa.

  “Semina hii imelenga kuwafunua macho wanasheria wetu ili rasilmali zetu ziweze kuwanufaisha wananchi… ndani ya mikataba tunayoingia kuna mapungufu makubwa kwa maana ya kuwanufaisha wananchi.”

  “Inawataka watambue kwamba mfanyabiashara yeyote akija ni lazima anatafuta faida. Na ukilala tu, yeye anapata faida kubwa sana. Wakienda kusaini mikataba hawa wanasheria wanapaswa kuangalia sheria za nchi husika lakini pia wanapaswa kuweka uzalendo mbele na kuacha tamaa. Wanatakiwa wafanye maamuzi kwa niaba ya wananchi,” alisema.

  Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu, Naibu Waziri wa Fedha, Bw. Mwigulu Nchemba alisema sekta ya madini ni mojawapo ya sekta zinazokua kwa haraka sana hapa nchini lakini inachangia chini ya asilimia moja ya ajira zote nchini.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU
  S. L. P. 3021,
  DAR ES SALAAM.

  0 0

  NA ANDREW CHALE
  TIMU ya Daraja la Kwanza ya Villa Squad ya Magomeni,  Dar es Salaam, siku ya Jumatano Septemba 10 inatarajia kushuka dimbani kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Ashanti United ‘Wauza mitumba, ya Ilala mchezo utakaochezwa uwanja wa Mwananyamala shule.
  Kwa mujibu wa  Katibu wa Villa, Mbarouk Kasanda  mchezo huo utakuwa ni mahususi kwa ajili ya kukipa makali kikosi chao hicho kinachotarajia kujiwinda kurejea ligi kuu msimu ujao.
  Kasanda aliwaomba  marafiki wa Villa na wadau wa soka Kinondoni kujitokeza kwa wingi  uwanja wa shule ya Msingi Mwananyamala kushuhudia timu hiyo yenye wachezaji mbalimbali wakiwemo walioachwa na timu kubwa zikiwemo za Simba, Yanga, Azam, Mtibwa na Coastal Union. 
  Mcheazo huo unatarajiwa kuwa mkali kwa timu zote mbili, kutokana na kukamiana kila wanapokutana, ikiwemo zilipokuwa ligi kuu misimu iliyopita. Kiingilio cha mchezo  huo kinatarajiwa kuwa sh 1,000.
  Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Villa, Idd Godgod alisema wameamua kujipanga kuakikisha wanarejea ligi kuu ndio maana wamesajili wachezaji wakongwe na wazoefu sambamba na kuchanganya damu changa.

  Godgod aliwataja baadhi ya wachezaji waliowasajili  chini ya ufadhili wa mdau wa soka, Nassoro Binslum, ni pamoja na Ramadhani Chombo ‘Redondo’ aliyeachwa na Simba, Ibrahim Mwaipopo kutoka Azam FC na Ally Mohamed ‘Gaucho’ (Mtibwa Sugar)  ya Morogoro.
   Wengine ni Nurdin Bakari, Godfrey Taita, Pius Kasambale,Jamal Magulu, Rashid Roshuwa na wengine wengi ambao kwa sasa bado wanasubiria hatua ya mwisho kuwaweka wazi.
  Pia timu hiyo inatarajia kuendelea na mazoezi yake uwanja wa Muhimbili chini ya kocha wao, Kamba Lufu ambapo wadau mbalimbali wameombwa kujitokeza kuipa sapoti timu hiyo.

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wauguzi waliovalia mavazi maalumu tayari kutoa huduma kwa  abiria  atayekutwa na ugonjwa wa ebola  mara atapowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2014 mara alipowasili kutokea Dodoma.
    Baadhi ya wahudumu waliovalia mavazi maalumu wa  wodi maalumu iliyotengwa kwa ajili ya wagonjwa wa ebola iliyoko katika eneo la hospitali ya Temeke  jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2014 mara alipowasili kutokea Dodoma.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid jinsi Tanzania ilivyojipanga kupambana na ugonjwa hatari wa ebola baada ya kukagua wodi maalumu iliyotengwa kwa ajili ya wagonjwa wa ebola iliyoko katika eneo la hospitali ya Temeke  jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2014 mara alipowasili kutokea Dodoma.
   Baadhi ya wahudumu waliovalia mavazi maalumu wa  wodi maalumu iliyotengwa kwa ajili ya wagonjwa wa ebola iliyoko katika eneo la hospitali ya Temeke  jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2014 mara alipowasili kutokea Dodoma.
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwaangalia wahudumu waliopata mafunzo maalumu ya kumhudumia mgonjwa wa ebola wakati alipokagua wodi maalumu iliyotengwa kwa ajili ya wagonjwa wa ebola iliyoko katika eneo la hospitali ya Temeke  jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2014 mara alipowasili kutokea Dodoma. PICHA NA IKULU
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwaangalia wahudumu waliopata mafunzo maalumu ya kumhudumia mgonjwa wa ebola wakati alipokagua wodi maalumu iliyotengwa kwa ajili ya wagonjwa wa ebola iliyoko katika eneo la hospitali ya Temeke  jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2014 mara alipowasili kutokea Dodoma.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya jinsi vifaa maalumu vinavyofanya kazi ya kutambua wagonjwa wa ebola mara watapowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2014 mara alipowasili kutokea Dodoma.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa maelekezo ya namna ya kuhudumia abiria wakati wa ukaguzi wa wagonjwa wa ebola mara watapowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2014 mara alipowasili kutokea Dodoma.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya jinsi madakrai na wauguzi walivyo jiandaa kufanya ukaguzi wa abiria na kutambua wagonjwa wa ebola mara watapowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jueb4: lius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2014 mara alipowasili kutokea Dodoma.
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo wakati alipokagua wodi maalumu iliyotengwa kwa ajili ya wagonjwa wa ebola iliyoko katika eneo la hospitali ya Temeke  jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2014 mara alipowasili kutokea Dodoma.

  0 0

   Mkurugenzi wa Idara ya Hospitali ya Mnazimmoja Dkt. Jamala Adam  Taib akimueleza Waziri wa Afya Mh. Rashid Seif kazi zinazofanywa na Idara hiyo alipofika ofisini kwake kuanza ziara ya kutembelea Hospitali hiyo.
   Waziri wa Afya Mh. Rashid Seif akiongozana na Naibu  wake Mh. Mahmoud Thabit Kombo wakitembelea eneo la Hospitali ya  Mnzammoja katika ziara yake ya kutembelea Hospitali hiyo.
   Mkuu wa kitengo cha maradhi ya kisukari katika Hospitali kuu ya Mnazimmoja Dkt Miskia Ali akitowa maelezo kwa Waziri wa Afya juu kadhia ya maradhi hayo.
  Waziri wa Afya akipata maelezo  ya shughuli za Maabara kutoka kwa  mtaalamu wa Maabara wa Hospitali Kuu ya Mnazimmoja Dkt. Marijani.Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar.
  =======  =====  =======

  RAMADHANI  ALI – MAELEZO ZANZIBAR .
                        
  Mkurugenzi wa Idara ya Hospitali ya Mnazimmoja  inayojumuisha Hospitali tatu, Hospitali ya Rufaa ya Mnazimmoja, Hospitali ya wagonjwa wa akili Kidongo chekundu na Hospitali ya Wazazi ya Muembeladu Dkt. Jamala Adam Taib amesema kazi kubwa inayofanywa na Idara hiyo katika kipindi cha miaka mitano kuanzia 2010 ni kuimarisha Hospitali ya Mnazimmoja ifikie kiwango cha Hospitali ya rufaa. Amesema hatua zinazochukuliwa na Idara  ni Kuimarisha miundo mbinu, kusomesha wataalamu wa fani tofauti za afya, kuimarisha uchunguzi wa maradhi na kuhakikisha madawa yanapatikana katika Hospitali hiyo.

  Dkt. Jamala amemueleza Waziri mpya wa Wizara ya Afya Rashijd Seif Suleiman alipofanya ziara ya kutembelea Hospitali hiyo kuangalia utendaji wa kazi na changamoto zinazoikabili Hospitali hiyo. Amesema majukumu yote waliyopangiwa katika  kuimarisha Hospitali Kuu ya mnazimmoja wamefikia hatua nzuri na hivi sasa wananchi wamejenga matumaini makubwa kutokana na huduma zake.

  Dkt. Jamala  amesema Idara ya Hospitali ya Mnazimmoja  inawafanyakazi 800 wakiwemo madaktari bingwa 14 na   Serikali inaendelea kusomesha wataalamu wa fani mbali mbali ambapo wanafunzi 200  wa fani ya udaktari wapo vyuoni . Pamoja na mafanikio makubwa yaliyofikiwa na Hospitali Kuu ya Mnazimmoja, Dkt. Jamala amesema bado inakabiliwa na ufinyu  mkubwa wa bajeti na mageuzi yanayoendelea ya kuifanya   Hospitali hiyo  iwe inajitegemea.

  “Changamoto hizi hata hivyo haziathiri malengo yetu ya kuwapa wananchi matumaini ya kupata huduma  bora katika Hospitali hii,” Dkt Jamala alimueleza Waziri wa Afya. Msaidizi Mganga Mkuu wa Hospitali Kuu ya Mnazimmoja Dkt. Muhidini Abdalla Muhamed amemueleza Waziri wa Afya ambae alifuatana na Naibu wake Mahmoud Thabit Kombo kwamba kliniki  ya meno ya Hospitali hiyo inavifaa  vya kisasa kutoka Shirika la MCW la Marekani na kuifanya kuwa kliniki bora zaidi  kuliko hospitali nyengine za Zanzibar.

  Amewahakikishia wananchi kwamba huduma za matatizo  yote ya meno zinapatikana kwenye kliniki hiyo na kuwataka wananchi kutokuwa na wasi wasi na waendelee  kuitumia.

  Katika kitengo cha maradhi ya kisukari daktari msaidizi wa maradhi hayo Dkt. Miskia Ali Mohd alimueleza Waziri  kwamba maradhi hayo yanaongezeka kwa kasi na kumekuwa na upungufu mkubwa wa dawa za maradhi hayo. Amesema tatizo jengine linalokabili kitengo hicho ni upungufu wa chakula cha wagonjwa wa kisukari wanaolazwa katika Hospitali hiyo ambacho kinatakiwa kiliwe sambamba na matatibabu wanayopatiwa ili dawa  wanazotumia zifanyekazi  kwa ufanisi.

  “Naiomba wizara ifanye juhudi za  kuhakikisha dawa za  maradhi ya kisukari  na chakula maalum cha wagonwa wanaolazwa  vinapatikana kwani  maradhi haya  yamekuwa hatari zaidi hata kwa watoto wadogo, ”alisisitiza Dkt. Miskia. Waziri wa Afya kwa upande wake amewataka viongozi  wa Idara hiyo kuimarisha umoja na  mshikamano  na watendaji  wao ili kufanikisha malengo yaliyowekwa  ya kuwahudumia wananchi na kuwapa huduma nzuri.

  Ameupongeza uongozi wa Hospitali hiyo kwa kuanzisha utaratibu maalum wa kuangalia wagonjwa waliolazwa ambao umepunguza msongamano wa watu katika mazingira ya sehemu hiyo.  
  IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akisaini hati za kiapo cha Balozi mpya wa Tanzania nchini Rwanda, Balozi Ally Iddi Siwa Ikulu jijini Dar es salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akimkabidhi mwongozo wa kazi anayekwenda kuwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Rwanda, Balozi Ally Iddi Siwa leo Ikulu jijini Dar es salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akipokea hati za utambulisha wa Balozi mpya wa Norway nchini Tanzania,Balozi Hanne Maria Kaarstad leo Ikulu jijini Dar es salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (katikati) akimtambulisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Benard Membe kwa Balozi mpya wa Norway nchini Tanzania, Balozi Hanne Maria Kaarstad Ikulu jijini Dar es salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (kulia) akizungumza jambo na  Balozi mpya wa Norway nchini Tanzania,Balozi Hanne Maria Kaarstad leo Ikulu jijini Dar es salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akimwapisha Balozi mpya wa Tanzania nchini Rwanda, Balozi Ally Iddi Siwa leo Ikulu jijini Dar es salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (kulia) akiwa katika picha ya pamoja Balozi mpya wa Rwanda nchini Tanzania,Balozi Eugene Segore Kayihura mara baada ya kuwasilisha hati za utambulisho leo, Ikulu jijini Dar es salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akizungumza (kulia) na  Balozi mpya wa Rwanda nchini Tanzania,Balozi Eugene Segore Kayihura mara baada ya kuwasilisha hati za utambulisho leo Ikulu jijini Dar es salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akimkaribisha rasmi Balozi mpya wa Rwanda nchini Tanzania,Balozi Eugene Segore Kayihura mara baada ya kupokea  hati zake za utambulisho leo Ikulu jijini Dar es salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (kushoto) akimkaribisha rasmi Balozi mpya wa Rwanda nchini Tanzania,Balozi Eugene Segore Kayihura alipowasilisha hati za utambulisho leo Ikulu jijini Dar es salaam.

  0 0

  Mara baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Mtwara, Mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 Mwanaafa Mwinzago akitoa Maneno ya Shukrani kwa Wakazi wa Mtwara waliojitokeza kuja Kumpokea uwanja wa Ndege wa Mtwara mapema Leo. Vilevile alitoa Shukrani zake zote kwa Watanzania Wote kwa Kuweza umpigia Kura na Kumfanya aibuke mshindi wa Milioni 50 za Tanzania katika fainali ya Shindano la  Kusaka vipaji vya Kuigiza lijulikanalo Kama Tanzania Movie Talents (TMT).
  Wapenzi, Mashabiki na wana Mtwara wakiwa Nje ya Uwanja wa Ndege wa Mtwara wakisubiri Kumpokea Mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 Mwanaafa Mwinzago kwaajili ya Kumpongeza kwa Kuibuka MShindi wa SHilingi Milioni 50 za Kitanzania katika Fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT)lililofanyika Mwisho wa Mwezi wa nane katika Ukumbi wa Mlimani City, Jijini Dar Es Salaam.
  Wakazi wa Mkoa wa Mtwara wakimpongeza Mshindi wa TMT 2014 Mwanaafa Mwinzago ambaye amewasili Mkoani Mtwara ambapo ndio Nyumbani Kwao akitokea Dar Es Salaam mara baada ya Kuibuka Mshindi na Kujinyakulia Kitita Cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania.
  Ndugu, Jamaa na Marafiki wa Mshindi wa TMT 2014 Mwanaafa Mwinzago wakipiga picha ya Pamoja mara baada ya Kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mtwara akitokea Dar Es Salaam.

  Shangwe na Ndelemo zilitawala katika Viunga Vya Uwanja wa Ndege wa Mtwara kabla na Baada ya Mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2014, Mwanaafa Mwinzago kutua katika Uwanja wa Ndege wa Mtwara akitokea Dar Es Salaam ambapo fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) lilifanyika katika Ukumbi wa Mlimani City.
  Msafara wa Kuelekea Nyumbani Kwa MShindi wa TMT 2014 , Mwanaafa Mwinzago Ukitoka katika Uwanja wa Ndege wa Mtwara.
  Msafara Ukielekea Nyumbani kwa Mshindi wa TMT 2014 Mwanaafa Mwinzago,
   Wazee kwa Vijana wakimpongeza Mwanaafa Mwinzago wakati alipokuwa akipelekwa Nyumbani Kwao kwa Msafara wakati akitokea Uwanja wa Ndege
   Vijana nao wakimpongeza Mshindi wa TMT 2014 Mwanaafa MwinzagoBOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI»
  Wakazi wa Mtwara wakimpongeza Mshindi wa TMT 2014 Mwanaafa Mwinzago wakati alipokuwa akipita na masafara uliompokea uwanja wa Ndege wa Mtwara na kumsindikiza Hadi Nyumbani kwao Magomeni Mkoani Mtwara mapema leo Asubuhi
   Wanafunzi wa Shule ya Msingi wakimpongeza Mwanaafa Mwinzago wakati alipokuwa akipita na msafara kutoka Uwanja wa Ndege wa Mtwara akielekea Nyumbani kwaajili ya Kujiandaa kwenda Shule leo asubuhi wakati alipowasili kutokea Mkoani Dar Es Salaam.
  Majirani, Ndugu, Marafiki na Wakazi wa Mtwara wakimshangilia Mshindi wa TMT 2014 Mwanaafa Mwinzago wakati alipowasili Nyumbani Kwao Eneo la Magomeni , Manispaa ya Mtwara Mikindani akitokea Uwanja wa Ndege wa Mtwara.Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

  0 0

  FREE WRISTBANDS AD2


  0 0

  DSC_0002
  Mkurugenzi Mkazi wa ASASI isiyo ya kiserikali ya kupiga vita umaskini Actionaid Tanzania (AATZ), Yaekob Metena akifungua kongamano la siku tatu kwa asasi zisizo za kiserikali, wawakilishi kutoka makundi ya vijana na waandishi wa habari juu ya masuala ya haki kwenye kodi linaloendelea kwenye hoteli ya Seascape jijini Dar.(Picha na Zainul Mzige wa MOblog)
  Na Mwandishi wetu.

  MAMLAKA mbalimbali ambazo zinawajibika kwa namna moja au nyingine katika kuwezesha mizigo mbalimbali inayoingia nchini kutolewa bandarini zitaunganishwa na mfumo mpya wa kisasa wa kutumia mtandao wa kompyuta wa Tanzania Customer Integrated System (TANCIS) kwa lengo la kuharakisha uondoaji wa mizigo hiyo.

  Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa elimu kwa walipa kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Diana Masalla wakati akitoa mada katika kongamano lililoandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali inayoendeshwa bila faida ikiwa na lengo la kupiga vita umaskini Actionaid Tanzania (AATZ) ikishirikiana na Kikundi cha haki kwenye kodi (Tanzania Tax justice Group).

  Kongamano hilo ambalo linahusu haki kwenye kodi ni sehemu ya mpango wa asasi ya Action Aid Tanzania kuleta uelewa na weledi katika masuala ya kodi miongoni mwa watanzania na walipa kodi ili kufanikisha ukusanyaji wa raslimali zinazowezesha serikali kutoa huduma za msingi na pia kutengeneza fursa za wananchi kujiendesha kiuchumi.

  Masalla alisema mfumo huo mpya ambao utamfanya mwenye mzigo kutoa maelezo ya mzigo wake kidigitali na maofisa forodha nao kushughulika na mzigo wake bila kukutana naye ana kwa ana, umeonesha ufanisi mkubwa hasa wa ufuatiliaji wa hatua kwa hatua tangu mzigo umeingia nchini hadi unamfikia mhusika. Aidha mfumo huo umebana uchepushaji wa mizigo hiyo kutokana na ufuatiliaji wa kidigitali unaofanywa na mfumo huo.

  DSC_0008
  Meneja uratibu na mahusiano wa Action Aid Tanzania Bibi Jovina Nawenzake akielezea historia fupi ya ActionAid Tanzania na kazi wanazozifanya.

  Alisema ingawa kumekuwepo na kilio kikubwa cha ucheleweshaji wa mizigo na kusukumiwa lawama hizo TRA, lakini kiukweli kuna mambo ambayo yanaingiliana na mamlaka zingine na mzigo hauwezi kutolewa mpaka mamlaka hizo ziseme na kwa mfumo wa zamani ilikuwa inachukua muda kuhangaika ofisi moja hadi nyingine.

  Alisema mathalani kwa bidhaa za pembejeo , dawa na mazao mengine yenye sheria za kimataifa, mizigo yake haiwezi kuingia mpaka TBS au TFDA au wizara husika iidhinishe. Alisema kuundwa kwa mamlaka na taasisi hizo katika mfumo mpya kutasaidia kila kitu kwenda kigitali na hivyo kuharakisha kasi ya uondoaji mizigo bandarini kutokana na kuongezeka kwa kasi ya utoaji wa vibali na ulipaji wa kodi.

  Akiwasilisha mada ya uelewa wa misingi ya kodi na uchambuzi wa misingi ya sera ya kodi nchini Tanzania, Masalla alisema kwamba mfumo huo pamoja na kunung’unikiwa Julai mwaka huu baada ya kuzinduliwa Oktoba mwaka jana, maboresho makubwa yamefanyika ili kuufanya ujibu mahitaji ya wananchi na walipa kodi.
  Miongoni mwa maboresho hayo ni kuweka kompyuta takribani 20 katika chama cha mawakala wa utoaji mizigo nchini TAFFA ambapo zinatumiwa na watumishi wa TRA kuingiza takwimu na kusaidia kujibu hoja za watumishi wa TRA kwa njia za mfumo wa kompyuta.
  DSC_0116
  Meneja wa elimu kwa walipa kodi kutoka mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), Diana Masalla, akiwasilisha mada ya uelewa wa misingi ya kodi na uchambuzi wa misingi ya sera ya kodi nchini wakati wa kongamano hilo.

  Masalla alisema kwamba mfumo mpya unaleta makampuni na mamlaka zote husika katika mwavuli mmoja na hivyo kurahisisha utoaji huduma na kudhibiti upotevu wa mapato ya serikali.

  Akifungua kongamano hilo Mkurugenzi mkazi wa Action Aid Yaekob Metena alisema kwamba ni lengo lao kuhakikisha kwamba kila mtanzania anajua misingi ya kodi na kwamba bila kodi serikali haiwezi kufanya majukumu yake ya msingi kama ukusanyaji wa rasilimali kwa ajili ya kuzitumia katika kazi nyingine.

  Alisema kutokana na kukosekana kwa haki katika kodi kumefanya serikali kupoteza fedha nyingi ambazo zingeliweza kutumika kwa ajili ya kufungua fursa za ajira na pia kuhudumia shughuli za afya.

  Mkurugenzi huyo alisema lengo kuu la kongamano hilo kutambua misingi ya kodi na sababu zake na pia kuelewa kwamba kuna haki ya kodi ambayo inamtaka kila mwananchi na mfanyakazi iwe wa umma au watu binafsi kutambua ushiriki wake katika kuiwezesha serikali kuwa na makusanyo makubwa ya kodi kwa maendeleo ya taifa.

  Metena alisema: kama hakuna uelewa wa haki ya kodi na wahusika nao wakasababisha kodi isikatwe serikali itakuwa inapoteza fedha nyingi.
  “Kama hakuna haki katika kodi, serikali haitaweza kukusanya mahitaji yake ambayo yanasubiriwa na watu wake”
  DSC_0004
  Pichani juu na chini ni baadhi ya washiriki wanaohudhuria kongamano la haki kwenye kodi lililoandaliwa na shirika la Actionaid Tanzania.
  Amesema mfumo wa kodi unaposhindwa kuwafanya watu wote kushiriki katika kuitendea haki serikali kwa kulipa kodi ambayo ndiyo msingi wa mapato yanayochangia maendeleo na ustawi wa jamii.

  Kongamano hilo la Actionaid Tanzania linafanyika katika hoteli ya Seascape iliyopo jijini Dare s salaam, lengo kuu likiwa kuhamasisha watu kutambua misingi ya kodi, sababu na serikali yenye makusanyo mazuri ya kodi inavyoweza kutengeneza fursa nyingi za kiuchumi ili wananchi wake waweze kuzitumia.

  Lengo la kongamano hilo ikiwa kutanua uelewa na weledi wa washiriki ambao wengi wao ni kutoka asasi zisizo za kiserikali na waandishi wa habari wanaotakiwa kujua masuala ya kodi, baada ya mada mbalimbali, ofisa wa TRA aliulizwa kuhusu misamaha ya kodi.
  DSC_0128
  Katika kongamano hilo pia waandishi wa walijifunza utendaji wa serikali na pamoja na kuitaka serikali kuhakikisha kwamba wadau wenye fedha wanaotoa michango yao kwa ajili ya bajeti ya taifa na kuboresha huduma za msingi kwa wakati kwa Tanzania.
  Aidha washiriki wengi katika kongamano hilo walihoji kisa cha serikali kung’ang’ania Pay as you earn (PAYE) kwa wafanyakazi na kuacha vyanzo vingine huku misamaha ya kodi ikiendelea kuitafuna.
  Wakati huo huo katika mazungumzo na waandishi wa habari Masalla amewataka waandishi wa habari/jamii kufichua wakwepa kodi.
  Aidha alisema kwamba sheria mpya ya VAT itaondoa misamaha mingi na hivyo kuisaidia serikali.
  Pia amesisitiza wateja wanapofanya manunuzi kudai risiti.
  DSC_0135
  Mkufunzi wa kongamano la siku tatu la haki kwenye kodi, Bwana Mosses Kulaba kutoka kituo cha uendeshaji uchumi na sera za biashara, akiwasilisha mada inayohusu mfumo wa kodi nchini Tanzania na changamoto zake katika ukusanyaji kodi.
  DSC_0099
  Mmoja wa washiriki katika semina hiyo aliyeibua hoja ya kuwepo kwa jitihada za makusudi kwa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), kujikita katika kutafuta vyanzo vipya vya mapato kuliko kujikita katika kodi zilizozoeleka kama PAYE inayolenga kukusanya kodi zaidi kutoka kwa wafanyakazi na wafanyabiashara wadogo wadogo.
  DSC_0088
  Ndugu Anwar Mkama mwakilishi kutoka vyombo vya habari akiuliza swali kwa meneja elimu kwa walipa kodi juu ya changamoto za mfumo wa kodi nchini ni namna gani wanazishughulikia ili kuboresha ukusanyaji wa mapato na kupunguza urasimu.

  0 0

   ·        Wadai fidia ya shilingi bilioni 500

  Kampuni ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na wadai wengine wawili wamefungua kesi ya madai katika Mahakama Kuu dhidi ya Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe na wengine wawili wakitaka kulipwa fidia ya Shilingi bilioni 500 kwa kashfa alizotoa kimaandishi dhidi yao.

  Mbali na IPTL,  wengine waliofungua kesi hiyo mnamo tarehe 4, Septemba kupitia wakili Melchisedeck Lutema wa Asyla Attorneys na  Kay Felician Mwesiga wa Bulwark Associates Advocates, ni kampuni ya Pan Africa Power Solutions Tanzania Limited (PAP) na Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni hayo mawili, Bw. Harbinder Sing Seth.

  Wadai hao watatu, miongoni mwa mambo mengine wanahitaji malipo ya fedha kutoka kwa Bw. Kabwe na washtakiwa wengine watatu ambao ni mhariri wa gazeti la Raia Mwema, Kampuni ya Raia Mwema na kampuni ya Flint Graphics, kuwa kama fidia itokanayo na makala ya kuwachafua iliyochapishwa kwenye gazeti hilo, iliyosababishwa na washitakiwa hao.

  Pamoja na hayo, pia wanahitaji tamko rasmi toka mahakamani kwamba makala iliyokuwa na kichwa cha habari "Fedha za IPTL ni Mali Ya Umma" iliyochapishwa katika kurasa wa 7 na 14 za gazeti la tarehe 13 Agosti, 2014 ilikuwa ni ya kupotosha na kuchafua kwa kudhamiria na kuhitaji washitakiwa kuomba radhi kwa kuandika na kuchapisha katika kurasa za mbele kichwa cha habari ya kuomba msamaha katika matoleo mawili mfululizo ya gazeti hilo.


  Zaidi ya hayo, wadai waliiomba mahakama kuweka vizuizi vya kudumu kwa washitakiwa, watumishi wao, wafanyakazi, washirika, wawakilishi au watu wengine wowote wanaofanya kazi chini ya washitakiwa kwa uchapishaji, kuchapisha au kusababisha kuandika na kuchapishwa kwa makala yoyote ya kuwachafua.

  Wadai walisema kuwa, IPTL waliingia mkataba na Shirika la Usambazaji Umeme Tanzania (Tanesco) kuwa umeme unaozalishwa na mdai utakuwa ukinunuliwa na kusambazwa na TANESCO kwa bei waliyokubaliana.

  Inadaiwa kwamba, katika kurasa namba 7 na 14 za gazeti la Raia Mwema la mwezi Agosti 13, 2014, Mbunge wa Kigoma Kaskazini aliandika, wakati mshtakiwa wa pili,  wa tatu na wa nne walihariri, kuchapa na kusambaza makala ambayo ilikuwa ni ya uongo na yakuwachafua wadai.

  Katika hati ya mashtaka, wadai walisema kuwa makala hiyo ilikuwa na maneno yafuatayo yaliyokuwa si ya ukweli na ya kuwachafua wanaodai; “Kwa mara nyingine, serikali kupitia viongozi wake akiwamo Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), wamedai kwamba kiasi cha Dola za Marekani milioni 250 zilizopaswa kuendelea kuwapo katika “Tegeta Escrow Account’ si mali ya serikali na hivyo si mali ya umma. Akaunti hiyo ilifunguliwa na serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) pamoja na kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL).”
    
  Ilidaiwa kuwa pasingekuwa na nia ya dhati ya kumchafua  mdai, mdaiwa hasingechapisha, na kusambaza maneno yaliyonukuliwa kama angefanya juhudi za kuthibitisha ukweli kutoka upande wa pili (kwa mdai) au kutoka kwa maafisa husika wa serikali ambao wangethibitisha kwamba:

  “kiasi cha fedha kilichowekwa kwenye akaunti ya Escrow ilikuwa ni dola za kimarekani 122,000,000.00 na siyo dola za kimarekani 250,000,000.00 kama ilivyodaiwa na mshtakiwa,” ilisomeka sehemu ya hati ya madai.

  Kwa mujibu wa wadai, Tanesco kamwe haikuwa sehemu ya makubaliano ya Escrow kama  ilivyodaiwa na washtakiwa.  “Fedha ziliwekwa katika makubaliano ya Escrow na siyo kama fedha za umma lakini ni kwa kutokana na mgogoro wa malipo yaliyotakiwa kufanywa na Tanesco kwa IPTL.
  “Madai kuwa fedha hizo ziliwekwa kama fedha za umma ni za uongo za kuupotosha umma na kuwachafua wadai kuwa ni wabadhilifu wa fedha za umma”, sehemu ya hati ya madai ilisomeka.

  0 0

  Mgodi wa Geita waleta mabadiliko katika mji wa Geita
  Maji, Afya, Elimu kuwa  ya uhakika

  Na Greyson Mwase, Geita.
  Mji  wa Geita  umeendelea kupiga hatua katika ukuaji wa uchumi wake baada ya  huduma muhimu za jamii kupatikana kwa uhakika kutokana na  mchango wa mgodi wa dhahabu wa Geita (Geita Gold Mine) , imeelezwa.

  Hayo yameelezwa na Mshauri wa Mkurugenzi Mtendaji wa Geita Gold Mine katika masuala ya   serikali na  jamii Bw. Clement Msalangi  mbele  ya   timu ya majaji  na  sekretarieti iliyofanya ziara katika mgodi huo kwa lengo la kumtafuta mshindi wa  Tuzo ya Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji.

  Akizungumzia mafanikio katika  sekta ya maji Bw. Msalangi alisema  kuwa ili kuhakikisha kuwa mji wa Geita unaondokana na tatizo la uhaba wa maji  mgodi wa Geita umeanza utekelezaji wa mradi wa maji  kwa  kujenga kisima chenye uwezo wa kusambaza maji kwa wakazi 100,000 wa mji huo.


  Aliongeza kuwa  hatua inayosubiriwa kwa sasa ni kukamilika kwa miundombinu kwa ajili ya kuchukua maji kutoka bwawa la  Nyankanga na kusafishwa kabla ya kupelekwa katika kisima kikubwa cha maji kitakachokuwa na uwezo wa kusambaza maji katika mji mzima wa Geita.
  Bw. Msalangi alisisitiza kuwa mradi huo  ambao hadi sasa umegharimu Dola za Marekani 212,000 utawanufaisha wakazi wa mji wa Geita pamoja na vitongoji vyake. 

  Akizungumzia changamoto  katika mradi huo  Bw. Msalangi alisema kuwa kumekuwepo na  uharibifu wa miundombinu  ya maji hali inayopelekea mgodi  huo kuingia  katika gharama kubwa ya ukarabati. Akizungumzia suala  la makazi kwa ajili ya wananchi waliopisha shughuli za mgodi huo Bw. Msalangi alisema kuwa mgodi ulijenga nyumba 18 ambazo ziko katika hatua za mwisho za ukamilishwaji wake kabla ya kukabidhiwa kwa wakazi hao.
   
  Aliongeza kuwa pia mgodi ulijenga jengo jipya kwa ajili ya kituo cha watoto  yatima cha Moyo wa Huruma ambapo ujenzi wake mpaka sasa pamoja na uendeshaji wa kituo hicho umegharimu Dola za Marekani 475,077. Kuhusiana na suala la elimu Bw. Msalangi alisema kuwa mgodi ulifanikiwa kujenga shule ya wasichana ya Nyankumbu ambayo kwa sasa ujenzi wake upo katika awamu ya nne.

  Alisema lengo la shule hiyo ni kuhimiza watoto wa kike katika mkoa wa Geita kujiunga na elimu ya sekondari katika shule ambayo ni bora ili kuzalisha wataalamu wa kike  zaidi katika masuala ya sayansi  ili waweze kufanya kazi kwenye migodi.Alisisitiza kuwa shule hiyo hiyo inajumuisha madarasa 21, nyumba 11 za walimu, ukumbi wa mikutano, mabweni sita, maabara  tatu, pamoja na darasa maalumu la kompyuta.

  Akizungumzia mafanikio ya mgodi huo katika sekta ya afya Bw. Msalangi alisema kuwa tangu mwaka  2006 mgodi ulifadhili  wagonjwa 600 kwa ajili ya upasuaji mdogo katika Kanda ya Ziwa kwa kushirikiana na Taasisi ya Rafiki Mission of the  Australia Tanzania Society.

  Aliongeza kuwa kwa sasa mgodi pia upo mbioni kwa ajili ya ukamilishwaji wa kituo cha kupima virusi  vya Ukimwi pamoja na utoaji wa ushauri nasaha cha  Geita na kusisitiza kuwa kituo hicho ni mkakati wa mgodi katika  kupunguza kuenea kwa maambukizi ya  virusi vya  Ukimwi kwa kupima  afya pamoja na kutoa ushauri nasaha.

  0 0

  Waziri wa Ujenzi  Dkt. John Magufuli  akiongea na wajumbe mbalimbali waliofika katika  uzinduzi wa kivuko cha kigamboni  leo jijini Dar es  Salaam kinachofanyiwa matenganezo  na Jeshi la Wanamaji maeneo ya kurasini ,ambacho kinatarajiwa kuanza kutumika rasmi alhamisi wiki hii.
   Mtendaji  Mkuu  Temesa Injinia  Marceline Magesa akitoa neno la shukrani  kwa Jeshi la Wanamaji waliwezesha matengenezo ya Mv Kigamboni  leo jijini Dar es Salaam ambapo kinatarajiwa kuanza kutumiwa na wananchi wiki hii.
   Kivuko cha Mv Kigamboni kinavyoonekana kwa ndani, kinatarajiwa kuanza kutumika siku ya alhamisi baada ya matengenezo yalifanywa na Jeshi la Wanamaji  kwa mda wa wiki tatu tangu kilipoaacha kufanya kazi Agosti 14 mwaka huu.
   Waziri wa Ujenzi  Dkt. John Magufuli ( kushoto) na Katibu Mkuu wa Ujenzi  Injinia Mussa Iyombe(kulia) wakisikiliza kwa makini maelekezo yaliyokuwa yakitolewa katika ufunguzi wa kivuko cha Mv Kigamboni leo jijini Dar es Salaam kinachofanyiwa matenganezo  na Jeshi la Wanamaji maeneo ya kurasini  na kinatarajiwa kuanza kutumika wiki hii.
   Waziri wa Ujenzi  Dkt. John Magufuli ( katikati mwenye suti nyeusi) akielekea katika eneo  ambalo kivuko cha MV Kigamboni  kilipo kwa ajili ya ukaguzi wa kazi iliyofanywa na wahandisi wa Jeshi la Wanamaji leo jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Ujenzi  Dkt. John Magufuli ( katikati) akipata maelekezo kutoka kwa  Msimamizi wa matengenezo  Luten Kanali Abel Gwanafyo (Kulia), kushoto  ni  Mkuu wa Jeshi la Maji Brigadia Jenerali Rostian Laswai wakati wa ufunguzi wa kivuko hicho leo jijini Dar es Salaam ,amabapo  kinatarajiwa kuanza kutumika wiki  kurahisisha usafiri kwa watu wa  Kigamboni.
   Waziri wa Ujenzi  Dkt. John Magufuli ( katikati) akipata maelekezo kutoka kwa  Msimamizi wa matengenezo  Luten Kanali Abel Gwanafyo (Kushoto), kulia  ni  Mkuu wa Jeshi nla Maji Brigadia Jenerali Rostian Laswai wakati wa ufunguzi wa kivuko hicho leo jijini Dar es Salaam ,amabapo  kinatarajiwa kuanza kutumika wiki hii kurahisisha usafiri kwa watu wa  Kigamboni.
   Kivuko cha Mv Kigamboni kinavyoonekana  upande wa mbele na ubavuni , kikiwa katika hatua za mwisho tayari kwa kuanza  kutumiwa na wananchi siku ya alhamisi baada ya matengenezo yaliofanywa na Jeshi la Wanamaji  kwa mda wa wiki tatu tangu kilipoaacha kufanya kazi Agosti 14 mwaka huu.( Picha na Lorietha Laurenc eMaelezo).

older | 1 | .... | 359 | 360 | (Page 361) | 362 | 363 | .... | 1898 | newer