Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

Tamasha la 'Handeni Kwetu' lapania kuvunja rekodi

$
0
0
MRATIBU Mkuu wa Tamasha la Utamaduni Handeni, maarufu kama ‘Handeni Kwetu’, Kambi Mbwana, ameapa kuhakikisha kuwa tamasha lao msimu wa 2014 linakuwa la aina yake na kuvunja rekodi ya mwaka jana lilipofanyika kwa mara ya kwanza wilayani Handeni, mkoani Tanga.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mbwana alisema kuwa hiyo ni kutokana na kutamani kushirikisha wasanii wengi kutoka Tanga na Tanzania kwa ujumla.

Alisema kwamba mwaka jana wasanii zaidi ya 200 walionyesha uwezo wao kutoka kwa vikundi mbalimbali vya wilayani Handeni na jijini Dar es Salaam.

“Mwaka jana vikundi zaidi ya 10 vyenye wasanii wasiopungua 15 walipata nafasi ya kupanda jukwaani kuonyesha vipaji vyao, ukiacha wasanii wanaotoka kwenye Kambi ya jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wa Mgambo waliozidi 80.

“Wakati tunajivunia mafanikio haya, tunaamini msimu huu utakuwa mzuri zaidi tukiamini kuwa tutavunja rekodi ya mwaka jana, ambapo tulishuhudia burudani mbalimbali, ikiwamo hadithi zilizohusu watu wa Handeni, bila kusahau vyakula vya asili pamoja na michezo waliyokuwa wakicheza wazee wetu enzi hizo,” alisema Mbwana.

Kwa mujibu wa Mbwana, mipango ya kuboresha tamasha hilo imepamba moto ambapo kwa sasa utafiti wa ubora wa vikundi nje ya wilaya ya Handeni inafanywa ili kuhakikisha kuwa wasanii watakaopanda jukwaani wanakuwa na uwezo wa juu na kufanikisha kwa dhati kukuza sekta ya utamaduni pamoja na uchumi wa Tanzania.

NHIF YAKUTANA NA KUTETA NA WASANII BASATA

$
0
0
2Meneja wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa NHIF tawi la Ilala Bw.Christopher Mapunda akizungumza na washiriki wa semina katika ya shirika hilo na Wasanii mbalimbali iliyofanyika kwenye ukumbi wa Baraa za la Sanaa nchini BASATA ili kupata elimu juu ya huduma za afya zinazotolewa na shirika hilo kwa vikundi mbalimbali na mashirika pamoja na taasisi mbalimbali za serikali, kulia ni Mkwabi Fikirini Meneja Udhibiti na ubora na Hans Mwankenja Ofisa Mwandamizi matekelezo.
9Msanii aliyeng'ara na Kundi la Wagosi wa Kaya, Fred Maliki 'Mkoloni'akichangia mada wakwati alipokuwa akiuliza swali katika semina hiyo 10Baadi ya wanamuziki wa muziki wa dansi wakiwa katika semina hiyo. 12Mwimbaji wa muziki wa taarabu Siza Mazongela alikuwa ni mmoja wa wasanii walioshiriki katika semina hiyo.

Benki ya NBC yazindua Kampeni ya Weka Upewe awamu ya pil

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Mussa Jallow (katikati) Meneja Masoko wa Benki ya NBC, Alina Maria Kimaryo (kushoto) Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa Binafsi na Bidhaa za Kuwekeza, Andrew Massawe wakionyesha vipeperushi kuashiria uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya Weka Upewe ya benki hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Meneja Masoko wa Benki ya NBC, Alina Maria Kimaryo (kushoto) akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya Weka Upewe ya mwaka 2014 jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Mussa Jallow na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa Binafsi na Bidhaa za Kuwekeza, Andrew Massawe.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa Binafsi na Bidhaa za Kuwekeza, Andrew Massawe (kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Weka Upewe ya mwaka huu jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Meneja Masoko wa benki hiyo, Alina Maria Kimaryo na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Mussa Jallow.
Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano wa Benki ya NBC, William Kallaghe (kushoto) akizungumza katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya maofisa wa benki hiyo na waandishi wa habari waliohudhuria hafla ya uzinduzi huo jijini Dar es Salaam leo.

ICM/TAMA – Midwifery Services Gap Analysis 5 Days Workshop in Dar es Salaam from 8th to 12th September 2014 at White Sands Hotel.

FILAMU YA MSHALE WA KIFO KUINGIA SOKONI LEO JUMATATU

$
0
0
AISHA Fathi ‘Aisha Bui’ anafunguka kwa kutamba kuwa filamu yake mpya inayoingia sokoni siku ya jumatatu, itadhihiri kipaji chake katika tasnia ya filamu, kwani amewakilisha wazo lake moja kwa moja bila kupigwa alichoandika ingekuwa ni kazi ya kushirikishwa isingekuwa rahisi.

“Najua kila mtu anakuwa na uwezo wake katika filamu lakini unaweza kushindwa kufanya hivyo kwa sababu ya kukosa nafasi ndio maana mimi nimeamua kutumia kampuni yangu kutimiza ndoto zangu, wiki hii Yuneda Entertainment wanasambaza kazi yangu mtaani,”anasema Aisha Bui.

Sinema hiyo ya Mshale wa Kifo inasambazwa na kampuni ya kizalendo ya Yuneda Entertainment ya Jijini Dar es Salaam, ikiwa imetayarishwa na Aisha Bui chini ya kampuni yake ya Badgirl Entertainment filamu yake ya kwanza mwanadada huyu.

Filamu ya Mshale wa Kifo inawakutanisha wasanii nyota wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamu Bongo kama vile Ahmed Olotu ‘Mzee Chilo’, Mzee Korongo, Salim Ahmed ‘Gabo’, Aisha Bui na wasanii wengeine wakali, Aisha anasema pia anazindua kampuni yake ya Badgirl Entertainment inayotoa filamu ya Mshale wa Kifo.

INTRODUCING BRAND NEW VIDEO LONKA- BEUTIFUL SMILE (Official Video)

GREEN WASTE PRO ltd WAENDESHA KAMPENI YA WIKI TATU YA KUFANYA USAFI KATIKATI YA JIJI

$
0
0
DSC_0423
Mkuu wa wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (katikati) akizungumza na vyombo vya habari na wananchi wa Kata ya Kisutu muda mfupi kabla ya kuzindua kampeni ya chukia uchafu katika kata tatu za wilaya hiyo. Kata hizo ni Kisutu, Mchafukoge na Kivukoni. Kulia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Kheri Kessy na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya usafi iliyopewa zabuni ya kusafisha Manispaa ya Ilala Green Waste Pro Ltd. Bw. Anthony Mark Shayo.
DSC_0442
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Kheri Kessy akizungumza na waandishi wa habari ambapo alitoa rai kwa wananchi wa kata hizo kuunga mkono kampeni hiyo yenye lengo la kung'arisha vitongoji vya manispaa ya Ilala na wengine waige kutoka kwao.
DSC_0469
Meneja Msaidizi wa Kampuni ya Usafi ya Green Waste Pro ltd Bw. Abdallah Mbena akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.
DSC_0420
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya wasichana ya sekondari Kisutu na wafanyakazi wa Green Waste Pro ltd. waliojumuika na kampuni ya Green Waste Pro Ltd kuunga mkono kampeni hiyo ya iliyopewa jina na Mkuu wa wilaya ya Ilala ya "Chukia uchafu".
DSC_0413
Mkuu wa wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya usafi iliyopewa zabuni ya kusafisha Manispaa ya Ilala Green Waste Pro Ltd. Bw. Anthony Mark Shayo kwenye picha ya pamoja na watendaji wa manispaa ya Ilala na madiwani wa kata hizo tatu.

DSC_0493
Baadhi ya madiwani na wafanyakazi wa kampuni ya usafi ya Green Waste Pro Ltd. wakimwaga taka kwenye gari maalum la kampuni hiyo kwenye maeneo ya katikati ya jiji wakati wa kampeni hiyo iliyoanza mwishoni mwa juma.
DSC_0496
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya usafi iliyopewa zabuni ya kusafisha Manispaa ya Ilala Green Waste Pro Ltd. Bw. Anthony Mark Shayo (aliyebeba jiwe) akishiriki zoezi hilo.
DSC_0511
Zoezi la usafi likiendelea ikiwemo kukusanya madumu ya maji pamoja na maboksi ya wauza matunda na mboga mboga yanayozagaa maeneo ya Kata ya Kisutu kama inavyoonekana pichani.
DSC_0355
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya usafi ya Green Waste Pro Ltd. wadau na wananchi wakijipanga tayari kuanza kampeni ya wiki tatu ya kusafisha maeneo mbalimbali ya katikati ya jiji iliyozinduliwa rasmi na Mkuu wa wilaya ya Ilala, Raymond Mushi ikiwa ni awamu ya kwanza kwa mwaka huu kabla ya kuelekea kwenye kata nyingine mbili zilimo ndani ya manispaa ya Ilala wakishirikiana na wananchi.

Na Mwandishi wetu
WILAYA ya Ilala imeanzisha kampeni ya wiki tatu ya usafi katika maeneo yaliyopo katikati ya Jijini la Dar es salaam kwa lengo la kutoa elimu na kuyaweka maeneo hayo safi na salama.Kampeni hiyo ilizinduliwa mwishoni mwa juma katika eneo la Kisutu na Mkuu wa wilaya ya Ilala Raymond Mushi .
Akizundua kampeni hiyo alisema bila suala la usafi kufanyiwa kazi, wageni wataona kwamba mambo katika Jiji la Dar e s salaam ni hovyo hasa ikizingatiwa kwamba kati ya jiji ndio sebule ya Jiji. Kampeni hiyo inayosimamiwa na kampuni yenye dhamana ya usafi katika eneo hilo la kati ya Green Waste Pro Limited inashirikisha wananchi kwa lengo la kuwafanya wawe washirika wa usafi kwa kujenga utamaduni wa kuchukia uchafu.

Mkuu huyo wa wilaya pamoja na kushukuru wananchi na wanafunzi wa shule ya Kisutu waliofika katika kampeni aliwataka viongozi kujipanga kuhakikisha kampeni hiyo inakuwa endelevu na yenye mafanikio.
Kampeni hiyo inafanyika katika kata ya Kivukoni, Kisutu na Mchafukoge.
DSC_0378
Pamoja na Mkuu huyo wa wilaya kusema kwamba kampeni hiyo ni chachu kwa kata za pembezoni za kujali usafi amewataka wananchi kuwa washiriki kw akuhakikisha hawatupi uchafu hovyo.

Naye Naibu Meya na Diwani wa Kisutu Kheri Kessy alisema kazi ya usafi inakabiliwa na changamoto kubwa hasa kutokana na kuvuja kwa chemba za maji machafu na wananchi kutupa taka hovyo. Alisema wananchi na hasa wapiti njia kama wakijifunza kutupa uchafu maeneo wanayotakiwa watakuwa wamesaidia sana kujenga utamaduni wa kuchukia uchafu na pia kufanya maeneo yapendeze.

Alisema wananchi wa kata yake ya Kisutu ni waelewa tangu kuanza kwa kampeni hizo miaka miwili iliyopita lakini wapiti njia wamekuwa wakivuruga utaratibu wa usafi.Aliwataka wakazi wa dare s salaam kutimiza wajibu wao kwa kuhakikisha hawatupi taka hovyo na kuanza kuuchukia uchafu kutoka katika majumba yao hadi wanakotembea.
DSC_0361
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya usafi iliyopewa zabuni ya kusafisha Manispaa ya Ilala Green Waste Pro Ltd. Bw. Anthony Mark Shayo (wa pili kushoto) akibadilishana mawazo na baadhi ya madiwani wa kata tatu zilizomo ndani ya manispaa ya Ilala na watendaji wa halamshauri ya manispaa ya Ilala wakati wakimsubiri mgeni ramsi kuzindua kampeni ya wiki tatu ya kusafisha maeneo yanayozinguka manispaa hiyo wakianzia katikati ya jiji. Kushoto ni Meneja Msaidizi wa Kampuni ya Usafi ya Green Waste Pro ltd Bw. Abdallah Mbena.
Kampuni inayoendesha kampeni hiyo ya Green Wate kupitia kwa meneja wao Abdallah Mbena amesema kwamba kuna maendeleo makubwa katika kamepni za kuweka Jiji safi na safari hii wamewaalika wenzao kutoka Segerea na Upanga ili waone njia wanazotumia kuweka maeneo yao yenye dhamana safi na ya kupendeza.
Mbena alisema changamoto kubwa zinazokabili juhudi za kuweka maeneo safi ni upungufu wa usimamizi katika sheria kwani wengi hawakubali kuzitii.
Alisema kama wangelizitii kungelikuwa na usafi kila siku. Kwani wengine wamekuwa wakifika katika majengo yao na kuyasafisha na kutupa uchafu barabrani wakati wafagiaji wameshafanyakazi yao usiku.
DSC_0402
Mkuu wa wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (kushoto) Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya usafi iliyopewa zabuni ya kusafisha Manispaa ya Ilala Green Waste Pro Ltd. Bw. Anthony Mark Shayo (katikati) na Meneja Msaidizi wa Kampuni ya Usafi ya Green Waste Pro ltd Bw. Abdallah Mbena wakijadiliana jambo kabla ya kuzungumza na vyombo vya habari kuhusiana na kampeni hiyo.

Kwa picha zaidi ingia hapa

MWANAHARAKATI KHADIJA LIGANGA ATOA SEMINA YA UNYANYASAJI WA KIJINSIA NA UKATILI DHIDI YA WATOTO KWA VIJANA ZAIDI YA 100 JIJINI MWANZA

$
0
0
Mwanaharakati toka Shirika la Kutetea Haki za Wanawake la KIVULINI la jijini Mwanza, Bi. Khadija Liganga ametoa mafunzo ya siku moja kuhusu Unyanyasaji wa kijinsia na ukatili Dhidi ya watoto kwa vijana takribani 100 wa jiji la Mwanza ikiwa ni hatua za kuwajenga vijana katika misingi ya kuachana na mila, tamaduni na dhana potofu zinazowakandamiza wanawake na watoto katika jamii.

Semina hiyo iliyoandaliwa na Teen Club Mwanza, ililenga Kujenga uwezo wa kutambua ukatili na unyanyasaji wa kijinsia, kuelewesha na kutoa njia za namna ya kuripoti unyanyasaji na ukatili na kuwasihi vijana kutoendeleza tabia za unyanyasaji na ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Akizungumza mara baada ya kutoa mafunzo hayo Bi. Khadija Liganga alisema ni lazima jamii ichukue jukumu la makusudi kukomesha vitendo vyote vinavyowakandamiza na kuwanyanyasa wanawake na watoto kwani ni moja ya sehemu inayochangia kwa kiasi kikubwa kuleta umasikini na kurudisha nyuma gurudumu la maendeleo kwa haraka sana.

“Mwanamke akipigwa au kutukanwa hatoweza kufanyakazi zake, mtoto akiteswa na kunyanyaswa hatoweza kusoma vizuri shuleni, huwezi pata maendeleo. Ili vijana waweze kupeleka ujumbe sahihi wa masuala ya ukatili wa kijinsia wanatakiwa kujua na kufahamu masuala yanayohusiana na tofauti za kijinsia, kulingana na suala la ukatili wa kijinsia (GBV) na namna ya kuzikemea tabia hizo” alisema Bi. Khadija.

Kwa mujibu wa ripoti ya UNICEF ‘Watoto na Wanawake Tanzania’ ya mwaka 2010 inasema kuwa kuwekeza kwa watoto na wanawake ni moja ya njia bora kabisa kwa maendeleo ya Tanzania. Sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2012 inaonesha Zaidi ya asilimia 50 ni watoto, ubunifu wao na umahiri wao katika kuzalisha ndio msingi mkubwa wa kufikia malengo ya Tanzania 2025.

Bi. Khadija aliendelea kusema kuwa bado katika jamii nyingi watoto hukatazwa kusema hadharani kwamba wananyanyaswa, mila nyengine watoto hawastahili kuzizungumzia, hivyo hivyo mwanamke anaona aibu au anaogopa kuzungumzia suala la ukatili wakati mwanaume anaweza kufanya kisema mbele za watu na wakati mwingine kwa kujidai /kujigamba amempiga mkewe. Hivyo basi ushiriki wa wa vijana ni muhimu sana kuelimishwa ili kujenga familia na jamii salama isiyo na ukatili Dhidi ya wanawake na watoto.

“Ni swali la kujiuliza kama sisi watu wazima tumeshindwa kujenga miji iliyo salama, kwanini tusiwekeza nguvu nyingi kwa hawa vijana, waswahili husema ‘ashakum si matusi’ni ngumu kumfundisha mbwa mzee mbinu mpya, hivyo naomba serikali, vyombo vya habari, mashirika ya kijamii, wazazi, pamoja na wanaharakati kuwekeza katika kuwapa kundi hili la vijana elimu ya ukatili wa kijinsia na haki za watoto ili kujenga kizazi bora” alimalizia kwa kusema Bi. Khadija.

Ripoti ya “Ukatili Dhidi ya Watoto Tanzania” ya UNICEF 2011, inasema kuwa karibu wasichana 3 kati ya 10 na mvulana 1 kati ya 7 wameripoti kutendewa walau tukio moja la ukatiliwa kijinsia kabla ya kutimiza umri wa miaka 18. Huku karibu asilimia 6 ya wasichana wamelazimishwa kujamiiana kabla hawajatimiza miaka 18. Marafiki, majirani, na watu wasiowafahamu walitajwa na wasichana na wavulana kama wakosaji wa ukatili wa kijinsia.
Kundi la vijana Zaidi ya 100 toka katika klabu ya Vijana (Teen Club) jijini Mwanza wakisikiliza kwa makini mafunzo toka kwa Bi. Khadija Liganga ya jinsi gani wanaweza kukabiliana na Unyanyasaji na Ukatili wa kijinsia lakini pia jinsi ya kuripoti matukio mbalimbali ya ukatili katika vyombo husika.
Bi. Khadija Liganga, Mwanaharakati wa kupigania Haki za Wanawake wa Shirika la Kutetea Haki za Wanawake KIVULINI akitoa semina ya siku moja kuhusu unyanyasaji wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto kwa vijana Zaidi ya 100 kutoka klabu ya vijana (Teen Club) ya jijini Mwanza.

Waziri wa Viwanda ba Biashara Dr. Kigoda afunga mafunzo ya wajasiliamali zaidi ya 3500 jijini Dar es Salaam

$
0
0
 Waziri wa Viwanda na Biashara Dr. Abdallah Kigoda akiongea wakati wa kufunga mafunzo ya wiki ya huduma za kifedha na uwekezaji yaliyoshirikisha zaidi ya wajasiliamali 3500 jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Waziri wa Viwanda na Biashara Dr. Abdallah Kigoda akikabidhi kikombe kwa mwakilishi wa Exim Bank Agnes Kaganda baada ya benki hiyo kushinda nafasi ya tatu kwenye mafunzo ya wiki ya huduma za kifedha na uwekezaji yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Viwanda na Biashara Dr. Abdallah Kigoda akikabidhi kikombe kwa mwakilishi wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Badru Idd baada ya benki hiyo kushinda nafasi ya pili kwenye mafunzo ya wiki ya huduma za kifedha na uwekezaji yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda na Biashara Dr. Abdallah Kigoda akikabidhi kikombe kwa mwakilishi wa CRDB Albert Michael baada ya benki hiyo kushika nafasi ya kwanza kwenye mafunzo ya wiki ya huduma za kifedha na uwekezaji yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

========  =======  =======
Dar es Salaam. Mafunzo na Kampeni za uhamasishaji nchini Tanzania zitachangia katika kuongeza kasi ya kufanikisha azma ya kutekeleza mpango wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Kifedha.

Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda wakati akifunga Mafunzo ya Wiki ya Huduma za Kifedha na Uwekezaji katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Semina hiyo iliyoshirikisha wajasiliamali 3,500 kutoka sehemu mbali mbali nchini iliratibiwa na Kampuni ya NUEBRAND na kufadhiliwa na wizara ya viwanda na biashara, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, taasisi ya PESCODE, Tanzania Standard Newspapers, Sayona, Times FM na Kampuni ya Ulinzi ya Kiwango.

Alisema shughuli hizo zinasaidia kusogeza huduma karibu na jamii ya Watanzania ambao wote kwa viwango balimbali ni wawekezaji.
“Wengi wanafikiri wawekezaji ni wakubwa tu.Hapana. Wakulima, wajasiriamali hata wamachinga pia,” alisema Waziri Kigoda.

Alisema kuwa muhimu ni kuwa na uongozi unaoratibu shughuli hizo na kuzingatia nidhamu ya kujua uongozi uliopo.“Hali hii itapunguza matatizo mengi yanayoendelea sasa kwa wamachinga,” alisema Waziri Kigoda.

Aidha,  Dk Kigoda aliongeza akisema wafanyabiashara wote, kwa viwango vyao tofauti wanategemeana kuanzia wamachinga mpaka ngazi ya mitaji mikubwa.
Alisema ili kufikia hali hiyo, wawekezaji wa makongamano, mafunzo na kampeni husika ipo haja ya kuendelea kutumia mitandao na mifumo ya teknolojia mbalimbali katika kuelemisha namna ya kufikisha huduma za kifedha kwa wawekezaji wanaoshiriki katika minyororo ya kuongeza thamani.

“Katika thamani hizo kuna bidhaa za kilimo, ufugaji, madini, misitu, uvuvi hasa vijijini na hata sekta ya huduma inayojumuisha utii, afya na elimu,” alisema na kuongeza: “Niwaambieni na kuwafahamisha kuwa moja ya malengo ya Sayansi ni kubuni na kuunda teknolojia na utaratibu wa kufanya kazi zenu ili kutumia mali ghafi na nguvu kidogo, kupata vingi kutoka vichache, kwa manufaa ya taifa.”

Ili kuhakikisha tekinolojia inaleta ufanisi, Waziri Kigoda alisema, ni muhimu sana kujikita katika matumizi bora na fursa zinazojitokeza kupitia teknmolojia. “Wito wangu ni kwa taasisi za fedha, na zile za utafiti na sayansi kuendelea kushirikiana na serikali kuona ni jinsi gani tutaendeleza matumizi ya simu za mkononi kwa ajili ya kupata huduma za kifedha kwa watu wengi zaidi,” alisema.

Alisema takwimu zinaonesha kuwa karibu asilimia 90 ya wenye simu nchini wanatumia huduma za fedha za simu, hivyo kama kundi hili likibadilishwa na wakakubali kuwa wateja wa benki nchini, itaongeza upatikanaji wa huduma za kifedha hasa maeneo ya vijijini.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Nuebrand Events Company, Abdul Ally, akisema kuwa kumekuwa na mafanikia sana toka kampeni hii ianze kwani idadi ya makampuni washiriki yamekuwa yakiongezeka toka 1200 mwaka 2012 mpaka 3600 kwa mwaka huu. “Mafanikio ni makubwa, tumepata pia washiriki toka mikoani mfano Mbeya. Hali hii inatutia moyo,” alisema.

Alisema kuwa mwakani uhamasishaji huu utafanyika pia jijini Arusha ikiwa ni katika mkakati wa kuhakikisha mikoa mbalimbali inafikiwa na huduma hii.

NBS YATOA TAARIFA YA MFUMUKO WA BEI NCHINI

$
0
0
Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo akitoa taarifa ya mfumuko wa bei nchini kwa mwezi Agosti, 2014 leo jijini Dar es salaam.

Na Aron Msigwa-MAELEZO.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Agosti, 2014 umeongezeka hadi kufikia asilimia 6.7 kutoka asilimia 6.5 iliyokuwepo mwezi Julai kutokana na kuendelea kupanda kwa bei ya baadhi ya bidhaa na huduma katika maeneo mbalimbali nchini.

Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii Bw. Ephraim Kwesigabo akitoa taarifa ya ongezeko hilo leo jijini Dar es salaam, amesema kuwa bidhaa zisizo za vyakula zikiwemo Bia, Sare za shule, mkaa, samani za nyumbani na bidhaa za vitambaa kwa matumizi ya nyumbani zimechangia kuwepo kwa ongezeko dogo la mfumuko wa bei nchini.

Ameongeza kuwa kuwepo kwa ongezeko la gharama kwenye huduma ya meno, huduma za vyakula kwenye migahawa na zile za kulala hotelini katika maeneo mbalimbali nchini pia zime kumechangia mfumuko wa bei.

Aidha, Bw. Kwesigabo amebainisha kuwa kuongezeka kwa Fahirisi za bei kwa maana ya kipimo kinachotumika kupima mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma mbalimbali zinazotumiwa na sampuli wakilishi ya kaya binafsi nchini hadi 149.31 kwa mwezi Agosti 2014 kutoka 149.16 za mwezi Julai kumechangiwa na kupanda kwa gharama ya bidhaa zisizo za vyakula.

Kuhusu mfumuko wa bei unaopimwa kwa kipimo cha mwezi kwa mwezi Agosti amesema kuwa umeongezeka kwa asilimia 0.1 huku uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma za jamii kwa mwezi Agosti, 2014 ukipungua na kufikia shilingi 66 na senti 97.

“ Kuongezeka kwa bei ya baadhi ya bidhaa na huduma katika maeneo mbalimbali kuna athari kwa fedha yetu, hii inamaanisha kwamba, uwezo wa fedha yetu katika kununua huduma na bidhaa za mlaji unapungua, mfumuko wa bei unapopanda thamani ya shilingi nayo inashuka”

Kwa upande wa ulinganifu wa mfumuko wa bei wa Tanzania na baadhi ya nchi za Afrika Mashariki Bw. Kwesigabo ameeleza kuwa una mwelekeo unaofanana na kuongeza kuwa mfumuko wa bei nchini Kenya kwa mwezi Agosti umefikia asilimia 8.36 ikilinganishwa na 7.67 za mwezi Julai huku Uganda ikiwa na mfumuko wa bei wa asilimia 2.8 mwezi Agosti ikilinganishwa na asilimia 4.3 za mwezi Julai.

Serikali yatoa usajili kwa makampuni 51 ya wakala Binafsi wa Huduma za ajira nchini

$
0
0
Serikali yatoa usajili kwa makampuni 51 ya wakala Binafsi wa Huduma za ajira nchini kati ya 87 yaliyowasilisha maombi yake kwa Kamishna wa kazi.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na Msemaji  wa Wizara ya Kazi na Ajira Bw. Ridhiwan Wema wakati wa mkutano na waansishi wa habari.
Makampuni yaliyosalia 36 hayakupata usajili kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutokidhi vigezo na kukosa nyaraka muhimu. Alisema wema
Akitaja baadhi ya makampuni yaliyopewa usajili baada ya kukidhi vigezo kuwa ni PA Ppospect Africa,Delloitte,KPMG Advisory Ltd, People Ltd, HR-Solutions na AGP Consultants.
Akifafanua wema amesema kuwa Kampuni au wakala yoyote ambaye hajapata usajili hatoruhusiwa kufanya kazi ya uwakala binafsi wa huduma za ajira hapa nchini.
Katika Kushughulikia suala la usajili Wema amesema kuwa Wizara imeandaa kanuni chini ya sheria ya ukuzaji wa huduma za ajira Na.9 ya mwaka 1999 na kutangazwa kupitia tangazo la Serikali Na. 232 la tarehe 11 Julai 2014.
Aidha Wema alitoa wito Makampuni au mtu yeyote anayetaka kufanya shughuli za huduma za ajira kuzingatia taratibu na kanuni chini ya Sheria ya kukuza Huduma za ajira Na. 9 ya Mwaka 1999.
Katika hatua nyingine Wema amesema kwamba ukodishaji wa Huduma (outsourcing of Services) haujapigwa marufuku bali kilichopigwa marufuku ni ukodishwaji wa watu (outsourcing of persons) hivyo ni marufuku kwa wakala wa huduma za ajira kuajira na kukodisha wafanyakazi au kuajiri kwa niaba ya kampuni nyingine na wakala hao kuwa sehemu ya mahusiano ya ajira yanayoweza kujitokeza baina ya watafuta kazi na waajiri.
Tarehe 27/1/2014,Waziri wa Kazi na Ajira,Bibi Gaudensia Kabaka alitoa tamko la Serikali kuhusu uendeshaji wa wakala binafsi wa huduma za ajira nchini, hii inatokana na Wizara hiyo kupokea malalamiko toka kwa wadau mbalimbali kuhusu utaratibu wa udalali wa kukodisha wafanyakazi katika makampuni unaofanywa na baadhi ya wakala binafsi wa huduma za ajira nchini.

UJUMBE MZITO KWA LADY JAY DEE

$
0
0
UJUMBE MZITO KWA LADY JAY DEE by Nathan Mpangala TV

RAIS KIKWETE AHITIMISHA MAZUNGUMZO YAKE NA UJUMBE WA KITUO CHA DEMOKRASIA IKULU NDOGO DODOMA LEO

$
0
0

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na ujumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) baada ya kumalizika kwa  awamu ya pili ya mazungumzo nao Ikulu Ndogo mjini Dodoma leo

PICHA NA IKULU.


LAPF YAZINDUA HUDUMA MPYA YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU KWA WANACHAMA WAKE

$
0
0
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu -Tamisemi, Mh. Hawa A. Ghasia, akitoa neno kwa wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya mkopo wa elimu ya juu(‘Piga Kitabu na LAPF’)
 Uzinduzi rasmi wa Piga Kitabu na LAPF ulipambwa na shamrashamra za aina yake.
 Waziri Wa Nchi, Ofisi Ya Waziri Mkuu -Tamisemi, Mh. Hawa A. Ghasia, akimkabidhi mfano wa hundi Bwana Rolland Lyamuya mmoja wa wanachama wa mfuko wa pensheni wa LAPF ambaye amenufaika na huduma mpya ya mkopo wa elimu ya juu(‘Piga Kitabu na LAPF’)  iliyozinduliwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
  Mgeni rasmi wa hafla ya uzinduzi wa Piga Kitabu na LAPF Mh. Hawa A. Ghasia akipokea zawadi ya kitabu cha Nelson Mandela kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa  Pensheni wa LAPF. 
 Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi huo.
  Baadhi ya wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya uzinduzi wa ‘Piga Kitabu na LAPF’ Mkopo wa elimu ya juu kwa wanachama wa LAPF iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
  Vijana kutoka Kigamboni Community Centre wakitoa burudani ya ngoma wakati wa hafla ya uzinduzi wa ‘Piga Kitabu na LAPF’ huduma mpya ya mikopo ya eilimu ya juu kwa wanachama wa LAPF, iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. 
Kalunde Band wakitoa burudani wakati wa uzinduzi huo

TAARIFA RASMI KUTOKA JESHI LA MAGEREZA KUHUSU TAARIFA ZA UZUSHI ZINAZOZAGAA KUWA BABU SEYA NA MAWAE WAMEACHIWA HURU

$
0
0
Hivi sasa kuna taarifa zimesambaa kupitia Ujumbe mfupi wa simu (SMS) na mitandao ya kijamii zikihusisha kuachiliwa huru kwa wafungwa wawili wanaotumikia Kifungo cha Maisha gerezani. Wafungwa hao wanaotajwa ni Nguza Vicking(Maarufu kwa jina Babu Seya) na Johnson Nguza(Maarufu kwa jina la Papii Kocha).

Napenda kuufahamisha Umma wa Watanzania kuwa taarifa hizo zote zilizotolewa kupitia njia hizo ni za Uongo na uzushi mkubwa na zinalenga kuipotosha jamii kwani wafungwa hao wapo gerezani na wanaendelea kutumikia adhabu ya kifungo cha Maisha gerezani kwa mujibu wa Sheria.

Jeshi la Magereza nchini linatoa onyo kali kwa watu kujiepusha na uhalifu huo na linawataka wale wote wanaotumiwa ujumbe wa aina hiyo waepuke kuusambaza ujumbe huo kwa wengine bali waufute, kwani kuendelea kuusambaza ni kosa kisheria.

Aidha, Jeshi la Magereza linaendelea na uchunguzi wa kina ili kuwabaini wanaosambaza ujumbe huo likishirikiana na Vyombo vingine muhimu kwa lengo la kuwakamata wahalifu hao ili mkondo wa Sheria uchukue nafasi yake.

Imetolewa na;
Lucas Mboje, Mkaguzi wa Magereza,
Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
DAR ES SALAAM.
Septemba 8, 2014.

short courses

FIGHT AGAINST FINANCIAL AND DATA PRIVACY CRIME

TASAF NA WADAU WA MAENDELEO WAKUTANA JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0

 Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF na wadau wa Maendeleo kutoka ndani na nje ya nchi wameanza Mkutano wa kupitia mafanikio na changamoto za utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini,PSSN unaoratibiwa na Mfuko huo nchini. 


Mapitio ya Utekelezaji wa Mpango huo unaowahusisha wataalamu mbalimbali kutoka Taasisi za Fedha na mashirika ya misaada ya kimataifa utawawezesha pia wataalamu hao kutembelea maeneo kadhaa ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru kaya maskini  katika mikoa y Dodoma, Lindi na Zanzibar.


Akitoa tathmini ya utekelezaji wa Mpango  wa kunusuru kaya maskini Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga amesema tayari kiasi cha zaidi ya shilingi Bilioni 13 kimetumika katika kutoka ruzuku kwa walengwa wa Mpango huo na kuwa katika maeneo ambako ruzuku hiyo imetolewa kumekuwa na mafanikio makubwa ya uboreshaji wa maisha ya kwalengwa wa  mpango huo.


Kwa Upande wao wadau wa Maendeleo kutoka BENKI YA DUNIA , UNICEF,ILO, UNPF,na  DFID,,wameonyesha kuridhishwa kwao na namna TASAF inavyotekeleza Mpango wa kunusuru kaya maskini na kuonyesha kuwa kazi hiyo itakamilimka kwa mafanikio makubwa .

 Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF bwana Ladislaus Mwamanga akiongoza Mkutano wa wadau wa maendeleo na maafisa wa TASAF juu ya utekelezaji wa mpango wa kunusuru Kaya maskini nchini ,PSSN ulioanza leo Jijini DSM.
 Baadhi ya wadau wa Maendeleo wakiwa katika mkutano wa kutathmini  utekelezaji wa shughuli za Mpango wa kunusuru Kaya Maskini, unaoratibiwa na TASAF.
 Baadhi ya wadau wa maendeleo  na watendaji wa TASAF wakiwa katika mkutano wa kutathimini utekelezaji wa mpango wa Kunusuru kaya maskini PSSN.
Baadhi ya wadau wa maendeleo wakiongozwa na mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, aliyevaa tai  walipotembelea chumba cha kurekodi takwimu za walengwa wa mpango wa kunusuru kaya maskini  ambacho kimefungwa zaidi ya kompyuta 100.



VIJANA WEKENI MSISITIZO MASOMO YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA ILI MUWE WAJUZI NA KULETA MAENDELEO NCHINI

$
0
0
 Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu, Mhe. Benjamini Wiliam Mkapa akiwahutubia Wajumbe waliohudhuria mkutano wa Jiolojia uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa J.K Nyerere Jijini Dar es Salaam.
 Baadhi wa Wajumbe waliohudhuria mkutano wa Jiolojia wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa ikitolewa na mgeni rasmi katika Ukumbi wa Kimataifa wa J.K Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Wanasayansi Vijana wakifuatilia mada wakati wa mkutano wa tatu wa Wanasayansi Vijana Duniani wenye lengo la kuhakikisha kuwa vijana wanashiriki vyema katika rasilimali za duniani kwa ajili ya maendeleo na ukuaji wa uchumi thabiti. (Picha na Makala na Benedict Liwenga, Maelezo-DSM)

 ========  ======  ========
Na Benedict Liwenga, Maelezo-DSM.
 
Vijana nchini hawanabudi kupenda kujifunza masomo ya Sayansi na teknolojia ili waweze kupata ujuzi na mitazamo katika sekta ya gesi ambayo inakuwa kwa kasi kubwa hapa nchini na Duniani kwa ujumla.
 
Kiukweli sayansi na teknolojia inasadikiwa kuwa mihimili mikubwa ya sasa katika kuleta maendeleo katika nyanja mbalimbali kwani mambo mengi yenye kuhitaji haraka hutegemea sayansi na teknolojia kwa kiasi kikubwa.
 
Licha ya kuwepo kwa changamoto zinazozikabili baadhi ya nchi nyingi za Afrika katika kupata maendeleo ikiwa ni pamoja na kutowekeza katika sayansi na teknolojia, hali inayopelekea baadhi ya nchi nyingi kukosa Wataalam wa kutosha katika mambo ya sayansi na teknolojia, hivyo nchi za Afrika zinahitaji kujikwamua na changamoto hiyo kwa kuhakikisha kuwa zinawekeza katika sayansi ili kubadilisha uchumi wa Afrika.
 
Sayansi na teknolojia hapa duniani huleta maendeleo makubwa hivyo Vijana wanatakiwa kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kujituma katika mambo ya sayansi na teknolojia ili kuweza kuleta uchumi endelevu.
 
Sambamba na hilo, katika Kongamano liloandaliwa hivi karibuni na Wizara ya Nishati na Madini nchini Tanzania ambao ulifunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt Mohammed Gharib Bilal ambao ulikuwa ni mkutano wa tatu wa Wanasayansi Vijana Duniani wenye lengo la kuhakikisha kuwa vijana wanashiriki vyema katika rasilimali za duniani kwa ajili ya maendeleo na ukuaji wa uchumi thabiti, Wakala wa Jiolojia nchini, Profesa Mruma alisema kuwa Mkutano huo una lengo la kurithisha taaluma ya jiolojia inayohusisha madini, rasilimali, gesi na mafuta kutoka kizazi kimoja hadi kizazi kingine.
 
Kongamano hilo la Vijana liliwakutanisha vijana toka nchi zaidi ya 42 zikiwemo baadhi ya nchi za Afrika Tanzania ikiwemo na ambaye ndiyo alikuwa mwenyeji wa Kongamano hilo.
 
Katika kongamano hilo, Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na madini, Mhe. Masele alisema kuwa Serikali ya Tanzania imewekeza nguvu zake kwa katika kuendeleza sayansi ya mambo ya gesi na mafuta pamoja na afya kwa kuanzisha Vyuo mbalimbali na kuwapeleka baadhi ya Watanzania kwenda kusoma nje ya nchi ili waweze kupata ujuzi na kuwa wataalam na wakaguzi katika sekta ya gesi, mafuta na afya kwa lengo la kuja kuisaidia nchi.
 
Aidha, Mhe. Masele alisisitiza kuwa wajibu wa Serikali kuamua kwa makusudi kusomesha vijana katika nchi mbalimbali ni kuwawezesha vijana waweze kupata elimu juu ya sayansi na teknolojia hasa katika masuala ya gesi ili kupata wataalam na wakaguzi wa kutosha nchini ambao watalisaidia taifa kuinua uchumi wake.
 
“Hivi sasa Serikali imeanzisha vyuo mbalimbali nchini, programu mbalimbali za mafunzo kwa watanzania, imetoa ufadhili wa masomo kwa watanzania na imedhamini makongamano ya vijana ili wapate fursa ya kujiendeleza’, alisema Masele.
 
Mhe. Masele pia aliyataka Makampuni ambayo ndiyo yalikuwa Wadhamini wa kongamano hilo kuendelea kuwekeza nchini pamoja na kuendelea kulipa kodi ili serikali iweze kukusanya mapato na wananchi wapate kunufaika na mapato hayo.
 
Halikadharika, katika mkutano mwingine uliohusiana na mambo ya Jiolojia uliowakutanisha Wataalam mbalimbali wa mambo ya jiolojia ulimwenguni jijini Dar es Salaam, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe. Benjamini William Mkapa ambaye alikuwa ndiye mgeni rasmi wa mkutano huo aliziasa jamii hizo za Kiafrika kuwa na uelewa wa kutosha kuhusiana na mambo ya sayansi na teknolojia ili ziweze kujikwamua kimaendeleo.
 
Mhe. Mkapa alisema kuwa jamii nyingi za kiafrika hazijaelewa mchango mkubwa wa sayansi na teknolojia katika kuleta maendeleo licha ya ukweli wa kwamba maendeleo daima yanatokana na rasilimaliwatu iliyopo juu ya ardhi na chini ya ardhi, mchango wake huo hauthaminiwi na wengi lakini wanaoweza kufanya hivyo ni Wanasayansi.
 
“Serikali licha ya kudhamini mafunzo mbalimbali na masomo kwa vijana nje na ndani ya nchi, fedha za kutosha bado zinahitajika katika kuhakikisha kuwa kazi hiyo inakuwa endelevu”, alisema Mhe. Mkapa.
 
Bila shaka kuna haja ya kizazi kilichopo na kijacho kurithishwa uelewa mzuri kuhusiana na mambo ya jiolojia ya jamii, jiolojia ya madini, mazingira na mabadiliko ya tabianchi, vyanzo vya nishati, matatizo yanayotokana na milipuko kama jiolojia na kuunganisha elimu ya Tehama na jiolojia kwani hii itawasaidia vijana wengi kuelimika vya kutosha kuhusiana na mambo ya jiolojia na pamoja na maendeleo kwa manufaa yao wenyewe.
 
Naye Mwenyekiti wa Mtandao huo kwa upande wa Tanzania Bw. Stephen Joseph Nyagonde alitaja kauli mbiu ya mkutano huo kuwa ni ”Kuhakikisha ushiriki wa vijana katika rasilimali za duniani kwa ajili ya maendeleo endelevu na ukuaji wa uchumi imara”.
 
Katika mikutano hii yote, wadau mbalimbali wakiwemo Wanasayansi Vijana walipata fursa ya kujadiliana kwa kina na kutoa mapendekezo ya kisayansi ya namna ya dunia inavyotakiwa kupiga hatua za kimaendeleo na kuboresha maisha ya wakazi.
 
Jamii nyingi za Kiafrika kiuhalisia hazina uelewa wa kutosha kuhusiana na mchango wa sayansi na teknolojia katika kuleta maendeleo nchini hali inayopelekea kuzorota kwa maendeleo ya nchi nyingi za Kiafrika.
 
Hivyo Wanasayansi ulimwenguni wanatakiwa kujenga utamaduni wa kukutana mara kwa mara na kujadili mambo yanayohusu Sayansi na teknolojia ili kuondoa changamoto mbalimbali zilizopo katika jamii hizo.
 
Endapo vijana nao wakichangamkia fursa mbalimbali za masomo yanayohusiana na mambo ya rasilimali zipatikanazo nchini mwao kama vile gesi asilia, mafuta na madini mengine wataweza kutatua kitendawili cha umasikini Barani Afrika na nchini mwao, hasa vijana wa kike kujenga utamaduni wa kujikita katika masomo ya sayansi ili waweze kuwa wabunifu na kujikwamua na maisha yao.
 

WADAU WA SANAA NA WAMILIKI WA KUMBI WATAKIWA KUSAJILI NA KUPEWA VIBALI

Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images