Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 34 | 35 | (Page 36) | 37 | 38 | .... | 1898 | newer

  0 0


  Na Khadija Khamis –Maelezo      Zanzibar     23/2/2013 .

  Mwenyekiti wa Sahara Media Group ambae pia ni mwenyekiti wa CCM Mkoani Mwanza Antony Dialo amewataka wahitimu wa fani ya Habari pamoja na fani ya Afya kuzingatia Maadili ya kazi zao ambayo yatawajengea sifa kwa jamii.

  Alisema kuwa miongoni mwa maadili ya kazi ni  uaminifu pamoja na kutunza siri . Aliyasema hayo leo huko katika Chuo cha Mwenge Community Centre (MCC) wakati  wa Mahafali ya nne ya chuo hicho.

  Akizungumzia suala la Ajira kwa wahitimu hao alisema kuwa ajira zinazidi kupungua Duniani kote, mbinu ambayo hutumika katika nchi za wenzetu ni kujaribu kutafuta kazi zaidi ya moja ambayo huengeza kipato.

  Mwenyekiti huyo aliwataka nesi hao kuepukana na mfumo wa kizamani wa kuwakaripia wagonjwa, wakiwa kazini mwao  na  ni vizuri kufanya urafiki. 
  Aidha aliwaomba wazazi na walezi kuendelea kuwasomesha watoto wao kwani ni jukumu lao . Antony aliahidi kuwaletea Mtambo mdogo wa kurushia  matangazo katika Chuo hicho ili wakifanya majaribio wanafunzi waweze kusikika hewani.

  Nao Mjumbe wa Bodi wa Chuo  hicho Abdalla Pandu aliwataka wanafunzi kudumisha mashirikiano  na kukubaliana na matukio,  wafanye kile ambacho wamekusudia  kwani kazi ya kutafuta taaluma si nyepesi unahitaji ujasiri wa hali ya juu.

  Pia alisema kuwa ushindani wa  soko la ajira halina urafiki na mtu yeyote ambae hana ujuzi . Nao wahitimu hao wakitoa changamoto katika risala yao walisema kuwa wamekabiliwa na ukosefu wa kamera, vifaa vya umeme,  komputa pamoja na vitendea kazi mbali mbali ..

  Jumla ya wahitimu 50 walitunukiwa vyeti vyao ikiwa 21 ni fani ya Habari na 29 ni fani ya Wauguzi . Chuo cha MCC kiliazishwa mwaka 2003 na hivi sasa kinasomesha kada tano tofauti ikiwemo Afya Habari Umeme Ushoni pamoja na Komputa 

  0 0

  12
  Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF),Emmanuel Humba akizungumza katika hafla iliyoandaliwa kwa ajili ya kujipongezana na kupata chakula cha jioni kwenye ukumbi wa Makonde mjini Mtwara,baada ya kumalizika kwa Kongamano la Nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),lililomalizika jana kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani humo. 2Maofisa wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) kutoka kulia ni Grace Michael na Dr. Ahena Mramba Rose Gabriel wakiwa katika hafla hiyo.
  4Mkurugenzi wa Tathmini na Uhai wa Mfuko na Takwimu NHIF , Bw. Michael Mhando akifurahia jambo na Grace Michael Ofisa Masoko wa mfuko huo wakati wa hafla hiyo kulia ni ni Angela Mziray
  5
  Baadhi ya Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika hafla hiyo kutoka kushoto ni Mgaya Kingoba wa Habari Leo na wenzake 7Steven Mhina kulia akiwa na Angel Akilimali kushoto wote kutoka Radio Uhuru
  8Wanahabari mbalimbali kutoka mikoa mbalimbali nchini wakiwa katika hafla hiyo
  10Ofisa wa Masoko wa NHIF Grace Michael wa tatu kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na wanahabari.


  11Kutoka kulia ni Catherin Sungura kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Grace Michael na Faraja Kihongole kutoka Chaenl Ten
  14Hawa jamaa walikonga nyoyo za wanahabari kwa vichekesho vyao.
  15Gladness Mboma wa pili kutoka kulia na wanahabari wenzake wakiwa kaatika hafla hiyo.
  17Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Moshi Chang'a akishukuru baada ya kupokea cheti chake kutokana na mchango wake wa NHIF katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF),Emmanuel Humba na kushoto ni Salome Manyama meneja wa tawi la NHIF makao makuu
  16
  Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Moshi Chang'a akipokea cheti chake kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF),Emmanuel Humba na kushoto ni Salome Manyama meneja wa tawi la NHIF makao makuu18Hapa ikiwa ni burudani kwa kwenda mbele
  20Wanahabari wakacheza kwaito kama wanavyoonekana.
  21Mchora Katuni King Kinya akitoa burudani jukwaani huku mpiga gitaa Yahya Mkango aliyewahi kufanya kazi na bendi ya African Stars ya jijini Dar es salaam.

  0 0


  Na Denis Mlowe,Iringa

  ZAIDI ya watoto 30 wanaoishi katika mazingira magumu na yatima wamepelekwa shule za sekondari mbalimbali mjini hapa na Asasi isiyo ya Kiserikali ya TCDA  ya mjini Iringa kupitia udhamini wa Fredrick Mwakalebela aliyekuwa mgombea ubunge mwaka 2010.

   
  Akizungumza na Tanzania Daima Msemaji na Mwanasheria wa Asasi hiyo Daniel Kibiki alisema kwamba Mwakalebela amejitolea kuwasomesha wanafunzi hao walikuwa katika mazingira magumu na yatima walioko katika halmashauri ya manispaa na nje ya mkoa.

  Kibiki alisema kwamba malipo ya awali ya shilingi milioni 13.6 zimeshatumika katika malipo ya awali kwa wanafunzi hao katika shule wanazosoma kama malipo ya ada, sare za shule, na matumizi ya kawaida kwa wanafunzi hiyo.

  Aidha Kibiki alitoa wito kwa wanafunzi hao mbalimbali kuweza kujitokeza katika asasi hiyo kuweza kupata msaada zaidi wa kimasomo kuliko kuendelea kuzurura mitaani bila kazi na kuongeza kwamba wanafunzi waliopata msaada huo watasomeshwa hadi kidato cha sita kama wakifanya vizuri katkika mitihani yao ya kidato cha nne.

  Naye mfadhili wa wanafunzi hao Fredrick Mwakalebela aliwataka wadau mbalimbali kuweza kujitokeza kuwasaidia watoto yatima na wanaoshi katika mazingira magumu kuliko kuendekeza starehe. “naomba sana mashirika mbalimbali na watu wenye uwezo kujitokeza kuwasaidia watoto hawa kwani kwa sasa wamezidi sana mkoani kwetu”

  Mwakalebela alisema kuwa kila mwaka ataongeza idadi ya wanafunzi hasa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kwa kupitia asasi ya TCDA." nitajitahidi kuongeza kila mwaka wanafunzi wenye uhitaji wa elimu ya sekondari na nitawasomesha hadi kidato cha sita hasa kama wakifanya vizuri katika kidato cha nne".

  0 0


   WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameunda Tume maalum itakayofanya uchunguzi wa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne ambayo yalitangazwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa Februari 18, mwaka huu.

  Katika matokeo hayo yaliyotangazwa Jumatatu wiki hii, asilimia 60 ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne Oktoba, 2012 walifeli.
  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Peniel Lyimo amesema Tume hiyo ambayo inatarajiwa kuanza kazi wakati wowote wiki ijayo inajumuisha wadau kutoka Chama cha Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi (Tanzania Association of Managers and Owners of Non-Government Schools/Colleges (TAMONGSCO), Taasisi za Dini zinazotoa huduma ya elimu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Asasi zisizo za Kiserikali (NGOs) zinazoshughulikia masuala ya elimu.
   
  Wadau wengine watatoka Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii na Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA).
   
  Amesema Serikali inawaomba wadau wa elimu, wazazi, walezi na wananchi wote kwa ujumla watoe ushirikiano kwa Tume ili iweze kufanya kazi yake kwa ufanisi.

  0 0


  SIKU MOJA baada ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) kuwatembezea wadau na wanachama wake katika nyumba za mradi wa nyumba za makazi ambazo zimejengwa na Shirika hilo eneo la Buyuni kata ya Majohe Chanika Wilayani Ilala nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam,  Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene nae ametembelea na kujionea nyumba hizo na kuumwagia sifa Mfuko huo kwa ubunifu na kuwajali wananchama wake.


  Mbene pia alitembelea Ujenzi wa jingo la Kitegauchumi la Ghorofa 35 linalojengwa na Mfuko huo katikati ya jiji la Dar es Salaam.

  Pichani ni Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene akiangalia mchoro wa Jengo la Kitega Uchumi cha Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) ambalo linajengwa katika ti ya jiji la Dar es Salaam na litakuwa na Ghorofa 35. Ndani ya jingo hilo la kutakuwa na Ofisi, maduka na nyumba za kulala.


  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Bwana Adam Mayingu akimpa maelezo Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene juu ya muundo kamili wa Jengo hilo la ghorofa 35 ambalo linajengwa na PSPF jijini Dar es Salaam na litakuwa na maduka, makazi na Ofisi.

  Meneja Mradi wa Ujenzi wa Jengo hilo la PSPF Tower, Ghazi Al Shamali (kushoto) akitoa maelezo kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Bwana Adam Mayingu juu ya hatua zilizofikiwa hadi sasa katika ujenzi huo.
  Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene akiangalia thamani za ndani katika moja ya vyumba katika nyumba zilizopo ndani ya jengo hilo la PSPF Tower ambalo ujenzi wake bado unaendelea na pindi zitakapo kamilika zitauzwa  kwa watumishi wa Serikali pamoja na Wanachama wa Mfuko huo.

  Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Bwana Adam Mayingu wakiongozana kuteremka ngazi zilizopo katika moja ya nyumba (apartment) zilizopo katika jingo hilo la PSPF Tower ambalo linaendelea kujengwa.


  Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene akitembezwa  ndani ya jengo hilo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Bwana Adam Mayingu.

   Watumishi wa PSPF wakizungumza  jambo ndani ya Jengo hilo.

  Awali Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene alipata fursa ya kutembelea mradi wa ujenzi wa nyumba 491 za Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) zinazojengwa Buyuni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na ambazo zimekamilika ujenzi wake na kuanza kuuzwa kwa Wanachama wa mfukjo huo. Pichani mbele kutoka kushoto ni Gabriel Silayo, Mkurugenzi wa Uwekezaji wa PSPF, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene na Mkurugenzi wa Fedha wa PSPF, Masha Mshomba wakimtembeza Kiongozi huyo katika nyumba hizo.


  Nyumba hizo zikiwa zimekamilika ujenzi wake na kusubiri wateja tu.

  Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene akiwa na Mkurugenzi wa Fedha wa PSPF, Masha Mshomba akimtembeza ndani ya moja ya nyumba hizo.

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene nje ya moja ya nyumba ambazo zimejengwa na PSPF, kwaajili ya kuwauzia wanachama wake kwa gharama nafuu.

  0 0

  drc1
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maal: umu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini  Addis Ababa, Ethiopia, leo Februari 24, 2013
  drc7
  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe Shamsi Vuai Nahodha pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Mahadhi Juma Maalim na wajumbe wengine wa ujumbe wa Tanzania wakati wa uwekaji akiweka saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maalumu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini  Addis Ababa, Ethiopia, leo Februari 4, 2013.drc8
  Rais Joseph Kabila wa DRC na Rais Paul Kagame wa Rwanda wakibadilishana mawazo kwa furaha huku Rais wa Jamhuri ya Kongo (Brazaville) Mhe Denis Sassou Nguesso akiwa kati yao baada ya wote kweka saini  katika Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maalumu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini  Addis Ababa, Ethiopia, leo Februari 4, 2013
  drc10
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon kwa kuwa mmoja wa viongozi wa bara la Afrika walio mstari wa mbele kusimamia amani baada uwekaji akiweka saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maalumu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini  Addis Ababa, Ethiopia, leo Februari 4, 2013.drc11
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipongezana na Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe. Hailemariam Desalegn baada uwekaji akiweka saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maalumu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini  Addis Ababa, Ethiopia, leo Februari 4, 2013. Katikati ni Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa Dkt  Nkosazana Clarice Dlamini-Zuma. PICHA NA IKULU

  =========  ======    =======

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo Februari 24, 2013 ameungana na Wakuu wenzake wa Nchi za  Ukanda wa Maziwa Makuu  kutia saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) mjini Addis Ababa, Ethiopia.
  Mhe. Rais Kikwete alisema mara baada ya utiwaji saini wa Mpango huo kwamba: “Hii ni siku kubwa na ya kihistoria kwa watu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, jirani zake na Ukanda wote wa Maziwa Makuu. Ni siku ya kukumbukwa kwa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Afrika, Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa na Jumuiya yote ya Kimataifa.
  “Watu wa Kongo wameteseka kwa muda mrefu sana. Wanastahili kupumua sasa. Wanastahili kuishi maisha bora; maisha ambayo usalama wao umehakikishiwa na kuthibitishwa; maisha ambayo yatawafanya waendeshe maisha yao kwa kufanya mambo ya maana zaidi katika kuboresha  maisha yao ya kila siku.
  “Saini tulizotia kwa Mpango huo leo ni kielelezo cha dhati na ahadi ya utekelezwaji wa yale yanayotarajiwa na watu wa Kongo na Ukanda wa Maziwa Makuu kwa ajili ya Amani, Usalama na Ushirikiano.
  “Kwa niaba ya Serikali na Watu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania naahidi kwamba sisi tutatekeleza kwa dhati yale yote yanayotarajiwa kwa upande wetu”, alisema.
  Mpango huo umetiwa saini na viongozi kutoka  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Jamhuri ya Uganda, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Angola, Jamhuri ya Burundi, Jamhuri ya Kongo (Brazaville), Jamhuri ya Zambia, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Jamhuri ya Afrika Kusini.
  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mhe. Ban Ki-moon, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa, Dkt. Nkosazana Dlamini-Zuma, pamoja na wenyeviti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) wametia saini Mpango huo kama mashahidi na wadhamini.
  Mpango huo una nia ya kuchangia juhudi ambazo zimefanywa na ICGLR na SADC katika kutafuta amani Mashariki ya Kongo na ukanda wote wa Maziwa Makuu kwa ujumla.  Mpango huo pia umetilia maanani mapendekezo muhimu yaliyokubalika baada ya mashauriano kati ya wakuu wa nchi za ICGLR na SADCna Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
  Mapendekezo ya mpango huo ni pamoja na kuboresha sekta ya Ulinzi na usalama, hususan jeshi la polisi, Kuimarisha mamlaka ya nchi hasa mashariki ya Kongo; na kuendeleza ajenda kuhusu maelewano, kuvumiliana na kudumisha demokrasia nchini humo.
  Vile vile, nchi za Kanda zimetakiwa kutoingilia mambo ya ndani ya nchi jirani, kututoa msaada wowote wa vikundi vya waasi, kuheshimu utawala na maeneo ya nchi jirani na kuimarisha mahusiano ya Kanda.
  Hali kadhalika, Jumuiya ya Kimataifa imetakiwa kuisaidia DRC na Kanda yote ya Maziwa Makuu kwa ujumla katika utekelezaji wa miradi muhimu pamoja na mkataba wa Amani, Usalama na Maendeleo katika Ukanda wa Maziwa Makuu.
  Aidha, Mpango huo unapendekeza kuwepo kwa chombo cha usimamizi (Oversight Mechanism) ambacho kitaundwa na viongozi wote wa nchi 11 pamoja na Umoja wa Mataifa, SADC na ICGLR.
      Imetolewa na:
  Muhidin Issa Michuzi,
  Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,
  Addis Ababa,
  ETHIOPIA.
  24 Februari, 2013

  0 0


  Mshindi wa pili wa DStv Rewards, Juliet Naivasha, akifurahia zawadi yake ya kitita cha Tshs Milioni 5 kama inavyoonekana katika mfano wa hundi aliyoishikilia.

  Kwa wiki ya pili mfululizo, wateja wa DStv wanaolipia akaunti zao kila mwezi kabla hazijakatwa na hivyo kuingia katika droo maalumu inayochezeshwa kila wiki na kutoa nafasi kwa wateja kujishindia mamilioni ya fedha imeendelea tena kwa kumpata mshindi wake wa pili. Kupitia kampeni hiyo ambayo imepewa jina la DStv Rewards, Juliet Naivasha, mfanyakazi wa National Bank Of Commerce (NBC), amekuwa mshindi wa pili na kujishindia kitita cha Tshs 5,000,000 (Milioni 5).
  Mshindi wa pili wa DStv Rewards, Juliet Naivasha ( wa pili kutoka kushoto), akiwa na wafanyakazi wa MultiChoice Tanzania (Ronald Shelukindo na Furaha Samalu) pamoja na Mama yake mzazi, Hilder Lawrence Nyambo (anayemfuatia katika picha) pamoja na mdogo wake Lisa (kulia)

  DStv Rewards ni sehemu ya kampeni maalum ya kampuni ya MultiChoice Tanzania kuwashukuru wateja wao kutokana na ushirikiano mkubwa inaoupata kutoka kwao. Akiongelea DStv Rewards, Meneja Masoko wa kampuni ya MultiChoice Tanzania, Furaha Samalu, amesema DStv Rewards ipo wazi kwa kila mteja na hivyo amewashauri waendeleee tu kulipia akaunti zao kabla hazijakatwa ili wapate nafasi ya kuibuka washindi. 

  Wakati huo huo: Mteja wa DStv, Bwana John Komakoma,ameibuka mshindi katika droo nyingine ambayo imepewa jina la Spot The Rewards Box ambapo pindi mteja akiwa anatizama televisheni na kufanikiwa kuona kibox fulani chenye nembo ya DStv, anatakiwa kutuma SMS yenye majina yake yote mawili na namba yake ya simu kwenda katika namba +27 711 745 622 ndani ya dakika tano tangu alipokiona "kibox". Kwa ushindi huo Bwana John Komakoma ameshinda Subscription ya mwaka mzima (miezi 12) ya DStv.Kwa maana hiyo, Bw.John ataendelea kufaidi DStv bila malipo yoyote kwa kipindi cha mwaka mzima!
  Mshindi wa droo ya Spot The Rewards Box, Bw. John Komakoma (katikati) akipongwezwa na Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania, Baraka R.Shelukindo huku Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania, Furaha Samalu akishuhudia. Bw. John Komakoma amesema yeye ni shabiki wa Liverpool wa kutupwa! Kampuni ya MultiChoice Tanzania kupitia DStv inawapongeza washindi wote.

  0 0

   The Azania Bank Principal Business Development Officer Othman Jibrea (left) hands over a 10m/- cheque to the Mahege Secondary School Head Teacher Faulu Maeda (right) being part of the bank’s contribution to the school’s dining construction project.
   The Mahege Secondary School Head Teacher Faulu Maeda (right) displays a 10m/- cheque handed over by the Azania Bank Principal Business Development Officer Othman Jibrea (left) being part of the bank’s contribution to the school’s dining construction project
   The Azania Bank Principal Business Development Officer Othman Jibrea (left) hands over a dummy cheque to the Mahege Secondary School Head Teacher Faulu Maeda (right) being part of the bank’s contribution to the school’s dining construction project.

  The Mahege Secondary School Head Teacher Faulu Maeda (centre) receives a 10m/- cheque from the Azania Bank Principal Business Development Officer Othman Jibrea as part of the bank’s donation to the school’s dining construction project in the back ground. 

   The Azania Bank Principal Business Development Officer Othman Jibrea (centre) poses for a gropu photo with a cross section of Mahege Secondary School students shortly after handing over the bank’s contribution to the school’s dining construction project
   A cross section of Mahege Secondary School students having their lunch outside the school’s premises. 
   The Mahege Secondary School Head Teacher Faulu Maeda (right) shows the Azania Bank Principal Business Development Officer Othman Jibrea (left) the school’s dining construction project


  0 0


  Na Freddy Macha

  Waziri wa Nishati na Umeme, Profesa Sospeter Muhongo amewasili Uingereza leo jumapili tarehe 24.2.13 kwa ziara ya siku nne. Waziri alipokewa na Balozi wetu mheshimiwa Peter Kallaghe na anatazamiwa kukutana na viongozi mbalimbali wa serikali ya Uingereza na wataalamu wanaohusiana na shughuli za madini, maendeleo ya kimataifa.

  Miongoni mwa maofisa anaotazamiwa kukutana nao kesho Jumatatu  ni pamoja na Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Kiafrika, Jumuiya ya Madola na nchi za Kigeni, Bwana Mark Simmonds;  Naibu Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa Uingereza, Bi Lynne Featherstone na Mbunge wa Stratford chama cha Conservative, Jeremy Leffroy  ambaye pia ni mwenyekiti wa kundi la Wabunge wa Uingereza wanaoshughulikia Tanzania (APPG).

  Jumanne saa kumi na moja jioni Waziri ambaye pia ni Mbunge wa kuteuliwa amepanga kuongea na Watanzania wanaoishi Uingereza ukumbi wa Ubalozi wetu London. Ukumbi uko 3 Stratford Place, London W1C 1AS. Stratford Place iliyojishika na barabara kuu  ya Bond- ni sekunde chache tu mbele ya kituo cha magari moshi na mabasi cha Bond Street.

  Waziri ambaye pia ni Mbunge wa kuteuliwa anaongozana na Dk Athanas Macheyeki wa Ukaguzi wa Madini Tanzania, Seleman Hatibu Chombo wa idara ya Nishati katika Wizara ya Madini na Nishati na Bwana Sosthenes Masau Bigambo Massola, katibu wake muhtasi.

   Waziri Muhongo ni msomi aliyebobea ndani ya masuala ya kisayansi na taaluma ya mawe na madini. Mbali na kuwa profesa na mhariri wa jarida la  “Journal of African Journal Sciences” ni vile vile mwanachama wa  jumuiya mbalimbali za madini na sayansi za kimataifa. Jumuiya hizo ni “Geological Society of London,” “Geological Society of America,” “Chinese Academy of Geological Sciences” na “Tanzania Academy of Sciences.”

   Kiongozi huyu ni  Makamu Rais wa Tume ya Tume ya Ramani ya Madini duniani iliyoundwa 1881  Ufaransa. Lengo la tume hii ni kuendeleza masuala ya mazingira, madini na hali ya hewa ya ulimwengu  na Rais wake ni Philippe Rossi.

  Mshindi wa tuzo kadhaa za kielimu na kisayansi, Profesa Muhongo alizaliwa Musoma mwaka 1954 akamaliza masomo yake vyuo vya Dar es Salaam na Ujerumani. Mwaka juzi alizawadiwa “Ordre des Palmes Academiques” ya serikali ya Ufaransa – inayotolewa kwa wataalamu waliochangia masuala ya kielimu na kitamaduni toka lipoanzishwa na Mfalme maarufu Napoelon karne ya 19.

  Mwaka 2007 kiongozi huyu alipewa tuzo la heshima (“Honours Award”) na Jumuiya ya Madini ya Afrika Kusini na 2004 akatunukiwa tuzo la “Robert Shackleton” la  Jumuiya ya Madini Afrika. Robert Shackleton aliyefariki 2001 ni Mwingereza aliyeendeleza uchimbaji madini Afrika Mashariki.

  Nchini Tanzania Waziri Muhongo amepata zawadi ya Makamu wa chuo kikuu (1977), zawadi ya Gondwana (1979) na tuzo la kitaifa la utafiti wa kisayansi na teknolojia (NARST) linalotolewa na Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania(2006). Tovuti: www.freddymacha.com

  0 0  Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Profesa Joram M. Biswaro akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda Balozi Naimi Aziz (kati) na Afisa ubalozi Samwel Shelukindo wakipungia kumuaga Rais Kikwete wakati ndege yake ikiondoka uwanjani hapo leo jioni ya  Februari 24, 2013 .PICHA NA IKULU.

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na  maafisa mbalimbali wa ubalozi wa Tanzania Nchini Ethiopia katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bole jijini Addis Ababa leo jioni ya Februari 24, 2013 baada ya kuhudhuria hafla ya Utiaji saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Rais Kikwete, kabla ya kurejea Dar es salaam leo, alikwenda Uganda kuhudhuria mazishi ya baba mzazi wa Rais Yoweri Kaguta Museveni, Mzee Amos Kaguta, aliyefariki siku ya Ijumaa na kuzikwa kijijini kwake Rwakitura.

  0 0


  Rais wa TALISS Swimming Club Bi. Najat Saleh Ahmed (mwenye miwani nyeusi) akizungumza na washiriki pamoja na wageni waalikwa wakati wa ufunguzi wa mashindano ya kuogelea yaliyoshirikisha Club mbalimbali na kwa rika tofauti yaliyodhaminiwa na Kampuni ya CFAO Motors wauzaji wa magari ya kisasa hapa nchini yaliyofanyika katika bwawa la kuogelea la shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST).

  Amesema Mashindano hayo hufanyika kila mwaka na kushirikisha vilabu na watu binafsi wenye ujuzi wa kuogelea unaofikia kiwango cha kushiriki mashindano. Aidha Bi. Najat Ahmed ameomba wadau zaidi kujitokeza kudhamini mashindano hayo na kuiomba Serikali ijitokeze na kujenga mabwawa yanayohitajika kwa ajili ya watu kujifunza kuogelea ili kuweza kujiokoa katika ajali za majini.
  Pichani juu na chini washiriki wa club mbalimbali za kuogelea wakipita mbele wazazi na makocha kwa ajili ya utambulisho.
  Official wakijipanga tayari kuanza mashindano hayo yaliyohusisha Clubs mbalimbali kutoka sehemu tofauti.
  Pichani juu na chini ni washiriki wajitosa kwenye bwawa hilo kuchuana katika mashindano ya kuogelea yaliyoratibiwa na TALISS Swim Club na kudhaminiwa na kampuni ya CFAO Motors ya jijini Dar.
  Picha juu na chini Sehemu ya watazamaji wakishuhudia mashindano hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam katika shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST).
  Picha juu na chini Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed akiwavalisha medali washindi wa mashindano hayo katika kategori mbalimbali. CFAO Motors imeamua kudhamini mashindano hayo baada ya kuona umuhimu wa vijana kujua kuogelea ili kuweza kujiokoa katika majanga yanayohusiha ajali za majini zinazopelekea vifo vya watoto ikiwa ndio lengo la TALISS.
  Rais wa TALISS Swimming Club Bi. Najat Saleh Ahmed akikabidhi medali kwa mmoja wa washindi wa mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Kampuni ya CFAO Motors.
  Picha juu na chini ni Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni ya CFAO Motors Wayne Mcintosh ambaye pia alikuwa MC katika mashindano hayo akikabidhi vikombe kwa washindi wa jumla walioshiriki TALISS Swimming Championships 2013.
  Umati wa watu wakiwemo wazazi, ndugu na jamaa pamoja makocha waliohudhuria kushuhudia mashindano ya kuogelea ya TALISS yaliyohusisha vilabu kutoka sehemu mbalimbali.
  Pichani juu na chini baadhi ya wageni waliohudhuria kutazama mashindano ya kuogelea katika shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) wakikagua gari mpya aina ya Nissan Y62 inayosambazwa na Kampuni ya CFAO Motors.

  0 0


  Na Thehabari.com

  SERIKALI imeingilia suala la uchaguzi wa Shirikisho la  Michezo nchini Tanzania (TFF) na kuamua kuifuta katiba  ya shirikisho hilo inayotumiza hivi sasa ambayo  ilirekebishwa mwaka jana (2012) pamoja na kuagiza  zifuatwe katiba ya awali ya mwaka 2006.

  Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Habari, Vijana,  Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara  akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam na  
  kuitaka TFF iitishe Mkutano Mkuu kama inataka kufanya  marekebisho ya Katiba yake.

  Katika ufafanuzi wake Dk. Mukangara ameagiza TFF  kufuata sheria na Kanuni za Baraza la Michezo Tanzania  (BMT) ikiwa inataka kufanya marekebisho ya katiba  yake. "Naelekeza na ifahamike kuwa hakuna chama chochote cha  michezo nchini kilicho juu ya BMT. TFF wafanye  uchaguzi wa viongozi kwa mujibu wa Katiba ya TFF ya  mwaka 2006 kwa kuzingatia sheria na kanuni za baraza  la michezo la Taifa," alisema Dk. Mukangara.

  Akifafanua zaidi Dk. Mukangara alisema baada ya wataala kupewa kazi yakuangalia mchakato wa mabadiliko ya katiba ya TFF na mgogoro wa uchaguzi unaoendelea, wizara imebaini; sheria Na. 12 ya BMT na marekebisho yake Na. 6 ya mwaka 1971, pamoja na kanuni za BMT za usajili Na. 442 za mwaka 1999 zimekiukwa.

  "...Ha kanuni ya BMT Na. 11(1) inayoeleza wazi utaratibu wa marekebisho ya katiba; 'haukufuatwa'. Kimsingi TFF walitakiwa wajaze fomu Na. 6, 7, 8 na 9 kwa mujibu wa sheria na kanuni za BMT. Sasa TFF hawakufuata taratibu nilizozielekeza kwa mujibu wa sheria na kanuni za BMT," alisema Waziri huyo mwenye dhamana ya Michezo Tanzania.

  Aidha Serikali imeitaka TFF na Msajili wa Michezo Tanzania kuwajulisha FIFA ambao walikuwa wameingilia mgogoro huo uamuzi uliofikiwa na Serikali ili nao wajue kinachoendelea kwa sasa.

  *Imeandaliwa na www.thehabari.com

  0 0


  Mahakama ya hakimu mkazi ya wilaya ya Musoma mkoani Mara imewahukumu maafisa wawili wa mamlaka ya mapato (TRA) kifungo cha miaka kumi na moja kila mmoja baada ya kupatikana na kosa la kushambulia.

  Moja kati ya madhara waliyofanya watumishi hao.

  Maafisa hao wawili mmoja andaiwa kuwani ni mdogo wa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Meck Sadick.


  Akisoma huku hiyo mwishoni mwa wiki hakimu Richard Maganga aliwahukumu maafisa hao ambao ni Sadick Salum na Mussa Msangi, kufuatia kukiri kosa la kujeruhi, kudhuru mwili na shambulio la kawaida ambalo walitenda novemba 10/2012 katika hoteli ya Sentavin mjini hapa.


  Maganga alisema kuwa watuhumiwa walifanya kosa hilo kinyume na kifungu namba 225 sambamba na kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka2002.


  Alifafanua makosa matatu waliyofanya kwa pamoja kuwa kosa la kwanza ni kujeruhi ambalo adhabu yake ni miaka mitano kila mmoja , kosa la pili ni kudhuru mwili ambalo nalo pia adhabu yake ni miaka mitano kwa kila mmoja  na kosa la tatu ni shambulio la kawaida ambalo adhabu yake alisema ni mwaka mmoja kila mmoja hivyo adhabu hizo zikwenda sambamba kwa kutumikia miaka sita jela kila mmoja. Hakimu alisema kuwa washitakiwa hao wote wawili watatumikia kifungo hicho ili liwe fundisho kwa watu wenye tabia za aina hiyo mkoani hapa.

  Kwa upande wake mwendesha mashitaka wa polisi Fransisi alisema kuwa washitakiwa hao kwa pamoja waliowashambulia na kuwajeruhi  Edgar Mapande, Witness Leonard  na Doris Mayuki katika hoteli ya Sentavin  Novemba 10 mwaka huu.


  Baada kutolewa kwa adhabu hiyo ambayo ilivuta mamamia ya wananchi wa Manispaa ya Musoma kutokana na watuhumiwa hao kutamba mitaani kuwa kuwa kamwe mahakama hiyo haiwezi kuwafunga kwa uwezo wao wa fedha na mahusiano ya kindugu na baadhi ya viongozi serikalini, Sadick akimgombeza hakimu kwanini aliuamua kumkomoa kwa kupata kifungo hicho.


  “Umeamua kunikomoa kama haonijui eti haya tutaona lazima nitatoka hapa si mwisho wa maisha yangu” alisikika Sadick akimwambia hakimu huku akiwa ameshika mikono mfukoni.


  NJE YA MAHAKAMA.
  Baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo baadhi ya ndugu wa watu walijeruhiwa na wananchi waliokuwa wakishuhudia baadhi ya vitendo vya kinyama na kibabe  vilivyokuwa vikifanywa na maafisa hao walisikika wakisema kuwa mahakama hiyo imetenda haki kwani licha ya kuwa ni masikini lakini haikuangalia uwezo wa watumiwa kifedha na kutoa adhabu kulingana na sheria.
  Ni sehemu tu ya majeraha yaliyosababishwa na maafisa hao kwa tukio la November 10.
  Siku nzima mjini Musoma vinywa vya watu wa mji huo vilikuwa vikizungumzia juu ya tukio hilo, baadhi ya viunga vya burudani wahudumu na baadhi ya wamiliki wengi wao walisikika wakisema "Sasa tuko huru" wakimaanisha kushoshwa na manyanyaso waliyokuwa wakifanywa na maafisa hao, ikiwa ni pamoja na kupigwa hata kuumizwa, huku maafisa hao wakidai kuwa wao ndiyo Dar es salaam,  na wao ndio Serikali hivyo hakuna mtu anayeweza kuwagusa.Na Ripota wetu: Musoma. 


  0 0
  Kuna tetesi kuwa msanii wa Bongo flava maarufu kwa jina la Timbulo, ambaye amepata umaarufu mkubwa kutokana na umahiri wa kuimba katika nyimbo zake kadhaa kama  Domo Langu, Waleo Wakesho, Samson na Delilah, amekamatwa mjini Bujumbura kwa tuhuma za kukutwa na madawa ya kulevya. Timbulo alikuwa huko katika kufanya mipango ya kufanya maonyesho kadhaa nchini Burundi mwezi April mwaka huu.Habari kwa hisani ya http://musicintanzania.blogspot.com

  0 0  0 0  0 0


  Kuna hekaheka nyingi kwenye jiji la Accra, nchini Ghana wakati wa pambano la kugombea ubingwa wa dunia kati ya bondia marufu Joseph Agbeko kutoka Ghana na Luis Mendenez bondia anayetoka katika nchi ya Amerika ya Kusini ya Columbia watakapokutana siku ya jumamosi tarehe 8 Machi.

  Kati ya mapambano ya utangulizi bondia anayeinukia kwa kasi Richard Commey atakutana na bondia mwenzake wa Ghana Bilal Mohammed kugombea mkanda wa IBF Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati (IBF AMEPG) katika uzito mwepesi (Lightweight).

  Wawili hao wanatoka katika kambi mbili zinazohasimiana kwa siku nyingi na mpambano wao unategemea kuwa wa kasi, ufundi na wenye kusisimua katika raundi zote 12.

  Mpambano wa Richard Commey (khttp://www.youtube.com/watch?v=IBG5a9LtIhU) na Bilal Muhammed umekuwa gumzo kubwa katika jiji la Accra pamoja na majiji mengine katika Afrika ya Magharibi. Hii inatokana na umaarufu wa promota na meneja wa Ruchard Commey Mghana Michael Amoo Bediako anayeishi barani Ulaya akiwa na makazi yake nchini Uingereza kuwa mtu aneyeshughulika na mabondia wenye vipaji vya hali ya juu.

  Richard Commey atapenda kuwadhihirishia wapenzi wake kuwa yeye ndiye Mfalme wa Afrika katika uzito wa mwepesi (Lightweight) na hakuka atakayeweza kumzuia katika mipango yake ya kupanda ngazi. Naye Bilal Muhammad atapenda kuudhihirisia ulimwengu kuwa sio bondia anayeweza kusukumwa sukumwa na kwamba ubingwa wa IBF AMEPG katika uzito wa Lightweight na wake.

  Imetolewa na:
   
  ISSUED BY:
  INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA)
  DAR-ES-SALAAM, TANZANIA

  0 0

                                                               TAARIFA KWA WADAU
  Leo tarehe 25 Februari mwaka 2013 ndio ilikuwa iwe siku nyingine ya kihistoria katika medani ya muziki wa kizazi kipya.

  Kwa siku kadhaa sasa tumekuwa tukitangaza kwamba wimbo mpya wa MwanaFA ulio katika mahadhi ya Hip Hop uitwao “Kama Zamani” aliowashirikisha Man'dojo, Domokaya na The Kilimanjaro Band (Wana Njenje) ungeanza kuuzwa kupitia njia mbalimbali kama ‘iTunes’, ‘Amazon’ na kupitia katika simu za mkononi. Pia ndio tarehe ambayo Kama Zamani ingeanza kusikika katika vituo vya redio Tanzania na nchi za jirani.
   
  Lifeline Music Inc. ndiyo inayosimamia muziki wa MwanaFA kwa sasa, ikiwa ni kampuni ambayo inafanya kazi za muziki, kuangalia na kuhakikisha kwamba wasanii inaowasimamia wananufaika kwa kiasi kikubwa kutokana na kazi zao; na kwamba muziki unaofanyika kwa sasa unafuata kanuni zote zinazosimamia makubaliano ya biashara.

  Kama mjuavyo, biashara yoyote ina pande mbili na mafanikio yake yanategemea zaidi maridhiano baina ya pande hizo na utimizaji wa vipengele tofauti ndani ya mikataba ya biashara. Katika kuboresha maslahi ya wanamuziki husika na wimbo huu,pia kuboresha zaidi njia zitakazotumika kuhakikisha ya kwamba burudani hii itawafikia washabiki wengi zaidi wa muziki unaofanywa na MwanaFA, Kilimanjaro Band(Wana Njenje) na Man’Dojo na Domokaya, tumefikia uamuzi wa kusubiri na kusogeza mbele siku ya kuachia wimbo wa Kama  Zamani kama ilivyopangwa hapo awali.

  Tunachukua nafasi hii kuwaomba radhi mashabiki ambao mmekuwa mnasubiri kwa hamu kusikia ni nini muungano huu wa muziki wa kizazi kipya na moja ya bendi kongwe kabisa za muziki yenye miaka zaidi ya 40 katika tasnia ya muziki Tanzania umewaandalia.

  Kwa niaba ya MwanaFA, uongozi wa Lifeline Music Inc. unaomba uvumilivu na subira toka kwenu mashabiki na wapenzi wa muziki. Tunaamini kwamba subira huvuta heri na mambo mazuri hayahitaji haraka.
   
  Tunawashukuru kwa dhati kwa ushirikiano wenu.

  Henry Mdimu
  PR Strategist
  Lifeline Music Inc

  0 0

   Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA,Mama Salma Kikwete,akiongea na baadhi ya wakazi wa Nyamisati wilaya Rufiji Mkoa wa Pwani wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya msaada wa vifaa vya tiba na dawa wenye thamani ya shilingi Mil 20 katika Zahanati ya Nyamisati, iliyopo wilayani humo vilivyotolewa na Vodacom Foundation hapo jana.
    Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA,Mama Salma Kikwete(katikati) pamoja na Mganga Mkuu wa Zahanati ya Nyamisati, iliyopo wilaya Rufiji Mkoa wa Pwani Bw.Haruna Mhina,wakipokea msaada wa vifaa vya tiba na dawa wenye thamani ya shilingi Mil 20 kutoka kwa Mkuu wa Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule.

    Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA,Mama Salma Kikwete akipokelewa na Mkuu wa Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule,kwenye Zahanati ya Nyamisati , iliyopo wilaya Rufiji Mkoa wa Pwani akiwa ni  Mgeni rasmi kwenye hafla fupi ya  makabidhiano ya msaada wa vifaa vya tiba na dawa wenye thamani ya shilingi Mil 20 kutoka Vodacom Foundation kwa ajili ya wakazi wa eneo hilo.
   Baadhi ya wakazi wa Nyamisati wilaya Rufiji Mkoa wa Pwani wakimsikiliza Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA,Mama Salma Kikwete,akiongea nao wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya msaada wa vifaa vya tiba na dawa wenye thamani ya shilingi Mil 20 katika Zahanati ya Nyamisati, iliyopo wilayani humo vilivyotolewa na Vodacom Foundation hapo jana.
   Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,mara baada ya makabidhiano ya msaada wa vifaa vya tiba na dawa wenye thamani ya shilingi Mil 20 kutoka Vodacom Foundation kwa ajili ya wakazi wa eneo Nyamisati  iliyopo wilaya Rufiji Mkoa wa Pwani.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwa wamebeba mabox yenye vifaa tiba na dawa vyenye thamani ya shilingi Mil 20 kwa ajili ya kutoa msaada katika Zahanati ya Nyamisati, iliyopo wilayani Rufiji vilivyotolewa na Vodacom Foundation hapo juzi.

  0 0


  Akhil Gupta, Deputy Group CEO & Managing Director, Bharti Enterprises Segun Ogunsanya, CEO, Airtel Nigeria, Manoj Kohli, MD & CEO International, Bharti Airtel, Sunil Bharti Mittal, Chairman, Bharti Airtel with H.E. Omobola Johnson, Hon. Minister of Communication Technology, Government of Nigeria at the inauguration of the Airtel Pavilion at the Mobile World Congress 2013

older | 1 | .... | 34 | 35 | (Page 36) | 37 | 38 | .... | 1898 | newer