Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 353 | 354 | (Page 355) | 356 | 357 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Mwenyekiti wa Umoja wa Wabunge Wanawake Tanzania (TWPG), Mhe. Anna Abdallah akifungua Semina iliyoandaliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwaajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum kuhusu masuala ya Jinsia na Katiba iliyofanyika leo 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
   Katibu wa Umoja wa Wanawake Wabunge Tanzania (TWPG), Mhe. Angellah Kairuki (MB) akizungumzia masuala mbalimbali ya kijinsia katika Semina iliyoandaliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwaajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum kuhusu masuala ya Jinsia na Katiba iliyofanyika leo 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
   Mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Bi. Usu Mallya akitoa mada kuhusiana na suala la kijinsia katika Katiba, wakati wa Semina iliyoandaliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwaajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum kuhusu masuala ya Jinsia na Katiba iliyofanyika leo 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
   Mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba, Profesa Ruth Meena akitoa mada juu ya masuala muhimu ya Jinsia ya kuzingatiwa katika Katiba Mpya wakati wa Semina iliyoandaliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwaajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum kuhusu masuala ya Jinsia na Katiba iliyofanyika leo 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.

   Mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Bi. Stella Gailos akitoa mada akitoa mada juu ya masuala muhimu ya Jinsia ya kuzingatiwa katika Katiba Mpya wakati wa Semina iliyoandaliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwaajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum kuhusu masuala ya Jinsia na Katiba iliyofanyika leo 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
   Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akifafanua juu ya masuala mbalimbali ya kijinsia wakati Semina iliyoandaliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwaajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum kuhusu masuala ya Jinsia na Katiba iliyofanyika leo 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
   Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Sophia Simba akichangia mada wakati Semina iliyoandaliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwaajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum kuhusu masuala ya Jinsia na Katiba iliyofanyika leo 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
   Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Hamad Rashid akifafanua jambo wakati Semina iliyoandaliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwaajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum kuhusu masuala ya Jinsia na Katiba iliyofanyika leo 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.


   Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Fami Dovutwa akifafanua jambo wakati Semina iliyoandaliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwaajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum kuhusu masuala ya Jinsia na Katiba iliyofanyika leo 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
   Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba wa Kundi la 201 upande wa Wakulima, Mhe. Agnes Senyagwa akizungumzia kuhusu utoaji elimu kwaajili ya kuongeza nafasi za uwakilishi wa wanawake katika ngazi mbalimbali maeneo ya vijijini, wakati Semina iliyoandaliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwaajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum kuhusu masuala ya Jinsia na Katiba iliyofanyika leo 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
   Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Faustina Urassa akifafanua jambo wakati Semina iliyoandaliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwaajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum kuhusu masuala ya Jinsia na Katiba iliyofanyika leo 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
   Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakifuatilia Semina iliyoandaliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwaajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum kuhusu masuala ya Jinsia na Katiba iliyofanyika leo 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
   Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakifuatilia Semina iliyoandaliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwaajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum kuhusu masuala ya Jinsia na Katiba iliyofanyika leo 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Mjini Dodoma
   Viongozi wa Meza Kuu wakiiimba kwa pamoja wimbo wa kuhamasisha wanawake kupigania haki zao wakati wa Semina iliyoandaliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwaajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum kuhusu masuala ya Jinsia na Katiba iliyofanyika leo 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (MB) akitoa neno la sukrani kwa watoa mada na wajumbe wa Semina iliyoandaliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwaajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum kuhusu masuala ya Jinsia na Katiba iliyofanyika leo 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
   Mwenyekiti wa Umoja wa Wabunge Wanawake Tanzania (TWPG), Mhe. Anna Abdallah (kulia) akifanya mahojiano na Mwandishi wa Habari wa Shirika la Habari Tanzania (TBC) mara baada ya kumalizika kwa na Semina iliyoandaliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwaajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum kuhusu masuala ya Jinsia na Katiba iliyofanyika leo 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
  Picha ya pamoja ya baadhi ya Wajumbe wa Semina hiyo iliyoandaliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwaajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum kuhusu masuala ya Jinsia na Katiba iliyofanyika leo 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.

  0 0

  PG4A3943 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Hirotaka Ishihara baada ya kukutana naye Ofisini kwake jijini Dar es salaam August 30, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   ………………………………………………..
  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema umefika wakati wa Japan kuhamia barani Afrika na na kuwekeza kwa nguvu hasa kwenye ukanda wa Afrika Mashariki.

  Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumamosi, Agosti 30, 2014) wakati alipokutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Bw. Hirotaka Ishihara na wafanyabiashara kutoka Japan kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu. Bw. Ishihara anaongoza ujumbe wa wafanyabiashara 70 kutoka makampuni makubwa 14 ya Japan.

  Akizungumza na Bw. Ishihara na baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria mkutano huo, Waziri Mkuu alisema ni ukweli usiopingika kwamba Japan ni nchi yenye uchumi imara na kwamba licha ya kuwepo kwa mikutano ya TICAD ambayo hutoa fursa kwa Japan kushirikiana na nchi za kiafrika, bado kuna haja ya wao kuelekeza macho yao Afrika kipekee.

  “Mikutano ya TICAD imekuwa ikifanyika kwa zaidi ya miaka 20 sasa lakini nchi za Afrika na hasa Afrika Mashariki tumefumba macho… tumeshindwa kutumia kwa kiasi kikubwa fursa zilizopo na kuchota utaalamu wa kiteknolojia kutoka Japan,” alisema.

  Waziri Mkuu alisema Afrika Mashariki ni soko la uhakika kwa mtu yeyote anayetaka kuwekeza barani Afrika. “Kama nchi wanachama wa Jumuiya siyo soko la kutisha, lakini kutokana na mahali nchi zetu zilipo, tuna fursa kubwa ya kufungua milango ya soko kwa nchi zote jirani zinazotuzunguka na hiyo ni fursa kubwa kwa mwekezaji yoyote,” alisisitiza.

  Kuhusu uwekezaji, Waziri Mkuu alisema Japan inaweza kuwekeza kwenye viwanda vya nguo na kusokota nyuzi, kuna fursa kwenye viwanda vya kusindika samaki kwani kuna aina nyingi za samaki waliopo katika bahari ya Hindi. Pia alisema amefarijika kusikia kwamba wameonana na wahusika kutoka Shirikisho la Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

  Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan ambaye ndiye kiongozi wa msafara huo alimweleza Waziri Mkuu kuridhishwa kwake na mahusiano yaliyopo baina ya nchi hizo mbili na kwamba katika kipindi cha miaka miwili kumekuwa na ongezeko la ziara za viongozi baina ya nchi hizi mbili.

  “Nina furaha kuzuru Tanzania kwa mara ya pili nikiongoza Kamati ya Pamoja ya Umma na Sekta Binafsi ya Kukuza Biashara na Uwekezaji nchini Tanzania… tumevutiwa na kasi ya ukuaji uchumi wa Tanzania, ndiyo maana makampuni ya Kijapani yameonyesha nia ya kuja kuwekeza nchini Tanzania,” alisema Bw. Ishihara. Bw. Ishihara na msafara wake wamemaliza ziara yao ya siku ya tatu hapa nchini na wanaondoka Tanzania kurejea Japan leo jioni.

  0 0

   Wananchi wa Mwanagati-Kitunda jijini Dar es Salaam  na maeneo jirani wamelilalamikia shirika la TANESCO  kwa kukatiwa umeme kwa siku tatu mfululizo,bila taarifa yoyote kutolewa kwa wakazi hao.''hatuna umeme kwa siku 3 mfululizo usiku na mchana mpaka sasa na hakuna taarifa zozote toka shirika la umeme Tanesco kuelezea hali hii inayoendelea mpaka sasa'',alilalama mmoja wa wakazi  wa eneo hilo.


  Wakielezea kwa masikitiko makubwa juu ya tatizo hilo,Wananchi hao wamesema kuwa hawakupata taarifa yoyote ile toka Tanesco, na mpaka sasa wengi wao wamepata hasara kubwa kibiashara kutokana na tatizo hilo la kukosekana kwa umeme.


  Mbali na matatizo hayo, Mji huo mpya ambao una chanzo chao cha kipekee kikubwa cha maji,kinachotegemea umeme katika uzalishaji wa maji na kufanya wananchi hao kukosa maji pia kwa siku 3 mfululizo na kufanya maisha yao kuwa magumu zaidi.

  Tunaliomba shirika la TANESCO lisikilize kilio chetu haraka iwezekanavyo,na kuhakikisha tatizo la umeme linatatuliwa kwa wakati ili kutuepusha na adha tunayoipata sisi wakazi wa Managati-Kitunda


  Juhudi za kuweza kuwapata wahusika toka shirika la umeme Tanesco ili kuelezea tatizo ili kwa wananchi wa Mwanagati - Kitunda zilishindikana mpaka tunapotoa habari hii.

  0 0

  Mwanaafa Mwinzago (katikati) akiwa katika picha ya Pamoja na wazazi wake na timu ya wafanyakazi wa TMT na washiriki wenzie mara baada ya kukabidhiwa mfano wa Hundi ya Shilingi Milioni 50 za Kitanzania Mara baada ya Kuwabwaga Washiriki wenzie tisa na Kuibuka Mshindi wa Kitita Cha Milioni 50 za Kitanzania katika Fainali ya Kusaka Vipaji Vya Kuigiza Nchini lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents (TMT) ambalo limefikia Ukingoni Jana Katika Ukumbi wa Mlimani City.
  Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar waliojitokeza kushuhudia fainali ya TMT ambayo ilikua ikirushwa live kupitia ITV

  Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin, Bw Johnson Lukaza akitoa neno kwa wadau waliojitokeza kushuhudia fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) lililokuwa pia likirushwa live kupitia Kituo Cha Runinga cha ITV
  Mwanaafa Mwinzago (katikati) akishangilia Mara baada ya kutangazwa Mshindi wa Kitita Cha Milioni 50 za Kitanzania katika Fainali ya Kumsaka Mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa Mlimani City na Kuhudhuriwa na Mamia ya Watanzania.

  Washiriki wa Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 waliofanikiwa kuingia Kumi Bora wakiwa wanasubiri mshindi atangazwe 
  Host Wa TMT 2014 Joti akimpongeza Baba wa Mwanaafa Mwizago kwa Mwanae kuibuka Mshindi wa Fainali ya Tanzania Movie Talents (TMT) na kuibuka na kitita cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania

  Mwanaafa Akiwa amembeba Mdogo wake mara baada ya kutangazwa Mshindi wa Fainali ya Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 na kuibuka na kitita cha Shilingi milioni 50.
  Lulu akionyesha Bahasha iliyokuwa na JIna la Mshindi wa Tanzania Movie Talents (TMT) ambae ni Mwanaafa Mwinzago na Kumfanya kujishindia Shilingi Milioni 50 za Kitanzania.
  Malaika Band wakitoa Burudani wakati wa fainali ya TMT 2014 katika Ukumbi wa Mlimani City Usiku wa Kuamkia leo.
  Christian Bella Akitoa burudani kwa kuimba wimbo wa Nani kama Mama ambao uliamsha Shamra Shamra katika Ukumbi wa Mlimani City Usiku wa Kuamkia leo na Mwanaafa Mwinzago Kuibuka Mshindi.
  Majaji wa Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 
  Joti akitoa Suprize ya ukweli haswa katika fainali ya Tanzania Movie Talents (TMT) katika ukumbi wa Mlimani City usiku wa Kuamkia Leo
   Mkurugenzi wa Kampuni ya Proin Promotions, Geofrey Lukaza akiwa na Mkewe katika Red Carpet Kabla ya Show Kuanza katika Ukumbi wa Mlimani City usiku wa Kuamkia leo
   Mc Pilipili Akifanya Yake
   Wadau wa Kampuni ya Proin Promotions Limited wakiwa katika Picha ya Pamoja mara baada ya MShindi wa Tanzania Movie Talents (TMT) kupatikana na kila Mmoja kusherehekea Ushindi huo.

  0 0

  AOTTL Managing Director Mr.  Mark Mason
  Part of the 28 million kgs of Flue Cured Tobacco in Mororogo.
  =========  =========
  The tobacco buying season which began in Tanzania during May 2014, resulted in Alliance One Tobacco Tanzania Limited (AOTTL) purchasing 28 million kgs of Flue Cured Tobacco by third week of August 2014. 

  The Flue cured tobacco (FCV) was valued at 61.7million USD (Tshs 101.805 Billion) at an average price of 2.20 USD per kilo. Dark Fire cured tobacco (DFC) purchases stood at 0. 225 million Kgs valued at 0.278 million USD (Tshs 458.7 million) at an average price of 1.23 USD per kg. 
   AOTTL buys tobacco from 182 contracted Primary Societies with over 35,000 farmer members. 

   “The targets set at the beginning of the season stand at 35 million Kgs of Flue Cured Tobacco and 0.5 million kgs of Dark Fired Tobacco,” said AOTTL MD Mark Mason, from Morogoro on Friday. 

  “At present the bought tobacco is at 80% of the target for FCV. I am happy to report that analyzing the current buying trends it is likely that the targets will be met by the end of the buying season in October 2014 and quality has been as expected,” concluded Mason. 

  Purchased tobacco is transported to Alliance One factory in Morogoro for processing and selling to domestic and export customers. Purchases amounting to 15.177 million kgs of tobacco have already been received at the factory. 

  The processing stage for the tobacco began in June 2014, and is scheduled to go up to December 2014. AOTTL’s 50 Million USD factory employs 300 permanent staff and provides jobs for over 2000 seasonal employees at the peak of the season. 

   Tanzania Tobacco Board (TTB), the regulatory authority of the Tobacco industry in Tanzania, estimates total production in the country this season to be 104 million kgs of Flue cured tobacco valued at 219 million USD (Tshs 362 Billion) at an estimated average price of USD 2.11 per kg and 1.074 million kgs of Dark Fired Tobacco valued at 1.6 million USD (Tshs 2.640 Billion) at an average price of 1.48 USD per kg. 

  Tobacco is the leading foreign exchange earner among Tanzania’s traditional export crops earning the Country more than 300 million USD annually. 
  Alliance One Tobacco Tanzania Ltd (AOTTL) with its headquarters in Morogoro municipality at Kingolwira township is a subsidiary company of Alliance One International (AOI) of the USA, with its headquarters in North Carolina.

   It is one of the three tobacco buying companies in Tanzania buying more than 35 million kgs of tobacco from 182 Primary Cooperative Societies with more than 39,800 farmers in Tabora, Urambo, Kahama, Manyoni, Iringa, Kasulu, Songea and Mara.


  0 0

  Mshindi wa Miss Lake Zone 2014 Rachael Clavery (katikati) akila pozi katika picha ya ukumbusho na mshindi wa pili Mary Emanuel( kulia) na Mshindi wa tatu Nikole Sarakikya ( kushoto). 

  Rachael amejinyakulia zawadi nono ya Gari la millioni 10 katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza usiku huu. Shindano hilo lilikuwa na Walimbwende 18 wote wakichuana vikali na kila mmoja akitaka ashinde kabla ya Rachael Clavery kuwafunika wenzake na kuibuka na ushindi. 
  Gari aliloshinda Miss Lake Zone 2014 Rachael Clavery usiku huu.
  Warembo wote 18 jukwaani
  Vazi la ufunguzi..warembo wote 18 walipanda jukwaani
  Warembo waliopanda jukwaani ni Mikoa yao kwenye mabano ni Moshy Shaban: Doreen Robert; Christina Jilulu (Mwanza): Nikole Sarakikya, Mary Emanuel na Rachael Julika (Shinyanga).
  Wengine ni Faudhia Haruna, Jackline Kimambo na Christina John (Kagera), huku Nyangi Warioba: Cecilia Kibada na Everlyn Charles (Simiyu). Wamo pia Martina John: Elinaja Nnko, Winfrida Nashon (Mara)huku Rose Msuya, Rachael Clavery na Faridha Ramadhani wakiwakilisha mkoa wa Geita.

  0 0

  Rais Kikwete akizungumza  na wajumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania alipokutana nao Ikulu Ndogo Mjini Dodoma leo
   Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania baada ya kukutana nao Ikulu Ndogo Mjini Dodoma leo
   Rais Kikwete akiagana na wajumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania baada ya kukutana nao Ikulu Ndogo Mjini Dodoma leo
   Rais Kikwete akiagana nna wajumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania baada ya kukutana nao Ikulu Ndogo Mjini Dodoma leo.
  Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) Mhe John Cheyo (kushoto) akiongea na Makamu Mwenyekiti wa TCD Mhe Philip Mangula, Katibu Mkuu wa CCM Ndg. ABdulrahman Kinana na Mhe Isack Cheyo walipowasili Ikulu ndogo mjini Dodoma kukutana na Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo. Nyuma yao ni Mwenyekiti wa TLP Mhe Augustine Lyatonga Mrema na Mwenyekiti wa UPDP Mhe Fahmi Dovutwa leo.TCD inaundwa na vyama vyenye uwakilishi bungeni, ambavyo ni CCM, CUF, CHADEMA, TLP, NCCR-Mageuzi na UDP.
  Mwenyekiti wa NCCR-MAGEUZI Mhe Joseph Mbatia, Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt Wilbroad Slaa wakiwasili Ikulu Ndogo mjini Dodoma leo


  0 0

   Spika wa Bunge la Jumuiya ya AfrikaMashariki (EALA) Mhe. Margareth Zziwa (Kulia) akikabidhi kitabu cha mpango mkakati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe Ahmed Chipozi jana wilayani Bagamoyo wakati wa ziara ya Wabunge wa Afrika Mashariki katika taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSuBa). Anayeshuhudia katikati ni Waziriwa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB).
   Spika wa Bunge la Jumuiya ya AfrikaMashariki (EALA) Mhe. Margareth Zziwa (Kushoto)  na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB).wakiwa na baadhi ya Wabunge wa Afrika Mashariki wakipata maelezo kuhusu muelekeo na malengo ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa)  kutoka Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo Bw. Michael Kadinde jana wakati wa ziara ya wabunge hao.
   Kikundi cha Sanaa kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSuBa)wakifanaya sanaa za maonyesho kwa mchezo aina ya Akrobati mbele ya wageni ambao ni wabunge wa Afrika Mashariki wakiongozwa na Spika wa Bunge hilo Mhe. Margareth Zziwa (Hawapo picha) walipotembelea taasisi hiyo jana mjini Bagamoyo.
   Kikundi cha Sanaa kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSuBa)wakichezo ngoma yenye asili ya kabila la Kisukuma ijulikanayo kama Gobogobo mbele ya wageni ambao ni wabunge wa Afrika Mashariki wakiongozwa na Spika wa Bunge hilo Mhe. Margareth Zziwa (Hawapo picha) walipotembelea taasisi hiyo jana mjini Bagamoyo.

  0 0

   Gari ya Polili ilioibuka kumuokoa Diambond kufuatia sakata la mashabiki wake kupandwa na jazba
  Sehemu ya ukumbi ulioharibiwa vibaya na washabiki mjini stuttgart,ujerumani
  UJERUMANI SI SHWARI KIMENUKA !!

  POLISI UJERUMANI WAMUOKOA DIAMOND KUTOKA KWA WASHABIKI WENYE HASIRA ! KASHINDWA KUWIKA STUTTGART KISA ?

  KAFIKA UKUMBINI SAA 10 ALFAJIRI ! WASHABIKI WANASURI SHOW TANGU SAA 4 USIKU

  PROMOTA MNAIJERIA AINGIA MITINI ,DJ APATA KISAGO HETI VYOMBO VIBOVU ! HAIBU

  Stuttgart,Ujerumani,
  Usiku wa Jumamosi ya Tarehe  30.Augost 2014, majira ya saa 10 alfajiri
  Mwanamuziki nyota wa Bongo Flaver  Nasib Abdul aka Diamond Platnumz alijikuta katika hali ya hatari hadi kuokolewa na Polisi mjini Stuttgart,ujerumani,baada ya washabiki waliokuwa na hasira kuchoka kusubiri show,washabiki hao waliokuwa wamelipa ticket euro 25 kwa kiingilio walihadiwa kuwa show ingeanza saa 4.00 usiku,lakini walijukuta wakisubiri hadi majira ya saa10 usiku au alfajiri ndipo mwanamuziki Diamond alipoletwa jukwaani na promota wake raia wa Nigeria anajiita kama Britts Event.
  Hapo ndipo washabiki walipoona kuwa hawakutendewa haki walianza kurusha chupa na kutaka kumvamia mwanamuziki  Diamond na promota wake,Kilichowakera zaidi washabiki ni pamoja na vyombo vibovu vilivyofungwa katika ukumbi huo kitu ambacho kiliwafanya washabiki kuvunja hadi vyombo vya muzikima-Djs walishambuliwa na wapo Hosptalini kwa sasa.
  Mmoja wa Djs hao alipoteza Lap top yake ,mwanadada DJ  Flor alipatwa shock mstuko wa moyo na kukimbizwa hosptali, washabiki hao walimpa kipigo  DJ Drazee naye yupo hoi hospatal. Polisi nchini ujerumani wanamesema tukio hili la haibu alijawahi kutokea,kuwa msanii kuchelewa kufika jukwaani kwa ujerumani ni kitu cha hatari kwani washabiki wa ujerumani wanaheshimu sana muda wao.
  mpaka sasa polisi wanamsaka mwandaaji wa onyesho hilo na wamesema kuwawanachunguza thamani ya hasara hiliyosababishwa na ghasia hizo na pia itamfungulia mashataka promoter huyo raia wa Nigeria,ambaye pia anachunguzwa kwa kusemekana anajihusisha na mtandao fulani wa biashara.

  Magazeti ya Stuttgart; yameandika "Washabiki wa hasira nawe DIAMOND" link:


  0 0

  DSC_0018

  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akisoma risala ya kufungwa kwa mradi huo ambao uliojulikana kama Micro Science Kits (MSKs) kwa wadau wa elimu, wakuu wa shule mbalimbali, maafisa elimu na maofisa wa serikali kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za shirika hilo jijini Dar.

  MRADI wa miaka minne wa kusaidia ufundishaji wa masomo ya sayansi kwa kufanikisha majaribio ya maabara uliokuwa ukifadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu na sayansi na utamaduni (UNESCO) na kuendeshwa na wizara ya elimu nchini katika shule 180 zilizopo katika wilaya 34 umemalizika kwa mafanikio huku wito ukitolewa kutafutwa njia ya kuendeleza mradi huo.

  Tangu awali mradi huo haukuelezwa kinaga ubaga unakuaje endelevu kama utaonekana kuwa na manufaa kwa taifa.Akitoa maelezo ya kufungwa kwa mradi huo ambao uliojulikana kama Micro Science Kits (MSKs) kwa wadau wa elimu,wataalamu na maofisa wa serikali, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues aliwataka wadau hao kuzingatia mafanikio yaliyokuwapo,kuangalia changamoto zake na kuona namna ya kuendeleza mazuri ya mradi.

  Mradi huo wa majaribio ulifanyika katika shule za mikoa ya Mbeya, Kilimanjaro, Mwanza, Shinyanga, Dodoma, Kagera, Morogoro, Kigoma na Tanga kwa upande wa Tanzania Bara.

  Aidha ilielezwa katika kikao hicho kilichofanyika ofisi za Unesco kwa lengo la kuufunga rasmi pamoja na malengo yake ya kuboresha elimu Tanzania kwa kuhakikisha masomo ya sayansi yanafundishwa kwa namna inavyotakiwa, tathmini ilionesha udhaifu wa kutokuwepo na mpango madhubuti wa kuendelezwa kwake.
  DSC_0015
  Mradi huu wa majaribio wa MSK ulilenga kukuza uwezo wa kufundisha masomo ya sayansi (baiolojia,kemia na fizikia) kwa shule ambazo hazina maabara kwakuzipatia visanduku vya majaribio pia uliendesha warsha mbalimbali ili kukuza uwezo wa matumizi ya zana zilizo katika mradi wa MSK pamoja na vitabu vya kufundishia.

  Aidha mradi huo ulizingatia pia kuongeza upendo wa masomo ya sayansi kwa jamii na kuwafanya wanafunzi wapende na wawe na hamu na masomo ya sayansi. Mradi huo ambao umefanyika kwa kuzingatia pia mahitaji ya taifa na kimataifa chini ya dhana ya kuendeleza masomo ya sayansi duniani unaendeshwa na UNESCO kwa kujenga uwezo wa shule za sekondari na msingi kufanya mazoezi ya utambuzi wa nadharia mbalimbali kimaabara hutoa masanduku maalumu ambayo yanakuwa ni kama maabara ndogo zinazotembea.

  Maabara hizi hutoa uwezo wa kufanyika kwa majaribio ya msingi na yale makubwa kwa kuzingatia madaraja mbalimbali ya mafunzo kuanzia ngazi za chini kati na juu. Katika ufungaji wa mradi huo uliofanyika mwishoni mwa mwezi Agosti washiriki walielezwa maendeleo ya mradi hadi mwisho wake na changamoto zilizokuwa zinakabiliwa.

  Unesco imesema kutanuka kwa kasi kwa elimu ya msingi kumesababisha changamoto za ubora wa elimu katika mfumo wa elimu nchini na mradi wa majaribio ulionesha kwamba ubora unaweza kurejeshwa kwa kuwa na mpango kama MSKs.
  DSC_0021 
  Pichani juu na chini ni baadhi ya wadau wa elimu, wakuu wa shule mbalimbali, maafisa elimu na maofisa wa serikali waliohudhuria mkutano huo uliofanyika mwishoni mwa juma. Kutokana na changamoto za raslimali kushindwa kuhakikisha kwamba kila darasa, mwalimu na mwanafunzi wanakuwa na zana zinazotakiwa kufundisha na kujifunza,walimu na wanafunzi walielemewa na hivyo kuathiri ufundishaji wa masomo ya sayansi ya baiolojia, kemia na fizikia.

  Mathalani matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2011 wastani wa matokeo ya masomo ya sayansi kitaifa uliporomnoka chini ya asilimia 50. Fizikia ilikuwa aislimia 43.2, kemia 43.3 na baiolojia 43.4 na katika takwimu hizo zilionesha kwamba wasichana walifanya vibaya zaidi.
  Utafiti ulionesha wazi kwamba udhaifu huo umetokana na kukosekana kwa maabara, vifaa vya kufundishia na upungufu mkubwa wa walimu wa sayansi.

  Pamoja na kuwepo kwa changamoto za uhaba wa masanduku haya ya maabara, tathmini iliyiofanywa ilionesha kwamba mradi ungeliweza kuunganishwa na miradi kama ya JICA na pia kutengenezewa mfumoi wa wa kuweza kuwa endelevu kutokana na umuhimu wake na ufanisi.

  Changamoto kama za masanduku machache kuliko yalivyokusudiwa katika mradi , muda mfupi wa kufunza walimu na pia kutekeleza yote yaliyopangwa na suala la ukaguzi bado mradi huu kutokana na asili yake ungelikuwa na maana zaidi kuendelezwa ili kufikia zaidi shule zilizo pembezoni.
  DSC_0009
  Aidha ili kuendelea na mradi huo tathmini iliyofanywa na kuelezwa na Ellen Binagi katika kikao cha wadau ilishauriwa serikali kufikiria kuanzisha vituo na taasisi za kutengeneza maabara hizo ndogo nchini badala ya kuagiza kutoka nje kutokana na gharama zake na hasa ikizingatiwa kwamba Tanzania ni nchi kubwa na yenye shule nyingi.Binagi alisema kwamba kuanzishwa kwa mtindo huo kumeleta muonekano mpya katika upenzi wa masomo ya sayansi na katika shule za majaribio ufanisi wake ulikuwa mkubwa na ipo haja ya kuangalia namna ya kuendeleza.

  Mtathmini huyo pia amesema ipo haja kwa UNESCO na serikali ya Tanzania pamoja na mradi kumalizika kuona namna ya kuuendeleza na kuondoa changamoto zilizoonekana wakati wa utekelezaji wake.
  DSC_0012

  0 0

   Mmoja wa mashabiki wa tamasha la Fiesta 2014 pichani akitazama kwa makini yaliyokuwa yakijiri kwenye jukwaa la tamasha hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki mjini Moshi.
   Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka THT,Rachael akiimba kwa hisia jukwaani.
   Mashabikii wakishangilia jambo wakati wasanii mbalimbali wa tamasha la Fiesta 2014 wakiendelea kutumbuiza jukwaani.
   Mwanadada Feza Kessy akiimba jukwaani wakati wa tamasha la Fiesta 2014 lililofanyka mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Majengo mjini Moshi.
   Sehemu ya umati wa watu waliofika kushuhudia tamasha la Fiesta 2014 lililofanyika mwishoni mwa wiki mjini Moshi.
   MKali wa kusugua ngoma,kutoka Clouds FM,Dj Zero akiwa kwenye mashine yake ya kazi
   Mashabiki wakisambaza upendo wa kutosha kabisa kwa wasanii wao waliokuwa wakitumbuiza jukwaani.
   Sehemu ya umati wa mashabiki wa tamasha la fiesta wakiwa wamemezwa vilivyo na jicho la samaki
   Wakazi wa jiji la Moshi walisambaza upendo wa kutosha ndani ya tamasha hilo ambalo hukusanyisha watu kutoka vitongoji mbalimbali ndani na nje ya mji wa Moshi.
   Mkali mwingine wa muziki wa Bongofleva,Ali Kiba akiwaimbisha mashabiki wake jukwaani.PICHA NA MICHUZIJR-FIESTA MOSHI

  0 0

  TAMASHA kubwa la umataduni linalojulikana kama 'Handeni Kwetu' limepangwa kufanyika Desemba 13 mwaka huu, katika Uwanja wa Azimio, wilayani Handeni, mkoani Tanga.
  Mratibu Mkuu wa Tamasha la Handeni Kwetu, Kambi Mbwana, akizungumza jambo katika tamasha la mwaka lililofanyika Desemba 14. Mwaka huu tamasha hilo litafanyika Desemba 13, Siku ya Jumamosi, katika Uwanja wa Azimio, wilayani Handeni, mkoani Tanga. Picha na Maktaba Yetu.
  Wasanii wa kundi la ngoma za asili la Mgambo JKT, wilayani Handeni, mkoani Tanga, wakitoa burudani katika tamasha hilo mwaka jana. Mwaka huu litafanyika Desemba 13, Siku ya Jumamosi, katika Uwanja wa Azimio, wilayani Handeni, mkoani Tanga. Picha na Maktaba Yetu.
  Mkuu wa Wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu (katikati), akifurahia katika tamasha hilo mwaka jana lililofanyika Desemba 14. Mwaka huu litafanyika Desemba 13, Siku ya Jumamosi, katika Uwanja wa Azimio, wilayani Handeni, mkoani Tanga. Kulia kwake ni Afisa Utawala wa wilaya ya Handeni, Upendo Magashi. Picha na Maktaba Yetu.

  Katika tamasha hilo linalofanyika kwa mara pili, burudani mbalimbali za ngoma za asili zinatarajiwa kuonekana jukwaani, ambapo pia vikundi kutoka nje ya Handeni, mkoani Tanga navyo vitaalikwa kwa ajili ya kwenda kutoa burudani wilayani humo.

  Akizungumzia hilo, jijini Dar es Salaam, Mratibu Mkuu wa tamasha hilo, Kambi Mbwana, alisema kuwa maandalizi ya tamasha hilo yanawekwa ili kuliweka katika kilele cha ubora na kuchangia maendeleo ya sanaa na uchumi kwa ujumla.

  Alisema kuwa mwaka jana tamasha hilo lilianza kwa mafanikio makubwa, ambapo wageni mbalimbali walifika wilayani humo, jambo lililochangia pia kuitangaza Handeni na mkoa mzima wa Tanga.

  “Mwaka huu tumeweka mikakati kabambe ya kuhakikisha kuwa tamasha letu linaendelea kukua kwa kasi baada ya kuanzishwa kwa mafanikio makubwa mwaka jana.“Naamini kuwa haya ni matunda ya kushirikiana kwa pamoja na wadau wote, ikiwamo serikali kwa kupitia ofisi zote za wilaya ya Handeni, hivyo watu wajiandae mambo mazuri na makubwa kutoka kwenye tamasha hili,” alisema Mbwana.

  Tamasha la utamaduni la Handeni, linalojulikana kama Handeni Kwetu, ni miongoni mwa matamasha yenye mchango mkubwa, ambapo kwa mwaka jana Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ndio waliokuwa wadhamini wakuu na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kuliweka katika mguso wa aina yake.

  0 0

  DSC_0140
  Mratibu wa mradi wa PREPARE ambaye pia ni Mwanasaikolojia wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi cha Muhimbili, Kitengo cha magonjwa na afya ya akili, Lusajo Kajula (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukamilisha SAMPULI tathmini ya matokeo ya mradi wa PREPARE uliokuwa na lengo la kuangalia uwezekano wa vijana kupunguza ngono mwishoni mwa wiki kwenye kituo cha maelezo ya afya Muhimbili katika idara ya magonjwa ya akili. Kulia ni Mtathmini kiongozi wa mradi huo, Mrema Kilonzo.

   ==========  =========  =======

  SAMPULI tathmini ya matokeo ya mradi wa PREPARE uliokuwa na lengo la kuangalia uwezekano wa vijana kupunguza ngono, imebainisha haja ya elimu ya afya ya uzazi kukabili hali ya sasa ya tabia hatarishi zinazowakabili vijana wadogo.Matokeo ya awali ya mradi yalionesha kuwa asilimia 10 ya vijana wenye umri wa miaka 12 mpaka 14 ambao ni darasa la tano na sita waliofanyiwa utafiti walikuwa wameshawahi kufanya ngono na asilimia kubwa ikiwa ni kwa kutumia njia ya haja kubwa.

  Kauli hiyo imetolewa na mmoja wa watafiti wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi cha Muhimbili,Kitengo cha magonjwa na afya ya akili, Lusajo Kajula. “Vijana wengi walionekana wakifanya ngono ya uke na ya mdomo ikifuatiwa na ngono ya njia ya haja kubwa Kwa wale ambao wameshawahi kufanya ngono, asilimia 6.3 wamefanya ngono ya njia ya haja kubwa wakati asilimia 93.7 hawajawahi.”

  Aidha alisema utumiaji wa kondomu ulionekana kuwa mdogo kwa vijana wadogo ambao wameanza kufanya ngono. “Asilimia 68 ya wale walioanza kufanya ngono hawajawai kutumia kondomu kabisa wakati asilimia 32 wamewahi kutumia kondomu.” Alisema utafiti huo ni sehemu ya utafiti wa miaka minne ulioshirikisha Vyuo Vikuu vya Makerere cha Uganda, Cape Town na Limpopo vya Afrika Kusini, Bergen na Oslo vya Norway, Maastricht cha Uholanzi na Sussex cha nchini Uingereza.

  DSC_0154
  Mtathmini kiongozi wa mradi huo, Mrema Kilonzo akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) uliofanyika jijini Dar es Salaam.

  Alisema utafiti umeonesha haja ya kutolewa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana wadogo ambao bado hawajaanza ngono ili kuchelewesha kuanza ngono kwa mfumo wa kisaikolojia ili waweze kujitambua na kuacha kufuata nadharia za kisayansi pekee ambazo ndizo zinazotumika katika shule mbalimbali kuwaeleza mabadiliko ya miili yao.

  Katika utekelezaji wa utafiti huo idadi ya wanafunzi 5,099 walichaguliwa mwanzoni mwa mradi kufanyiwa utafiti huo ambapo wanafunzi 4783 (asilimia 93.9) walifuatiliwa kwa miezi 6 na wengine 4370 (asilimia 85.8) walifuatiliwa kwa miezi 12. Utafiti ulionesha elimu inayojishughulisha na masuala ya ujinsia na afya ya uzazi kwa vijana wadogo itumie mtazamo mpana utakaoleta mabadiliko ya msingi kwenye misingi ya virekebisho vya mabadiliko ya tabia.

  Mradi huo wa PREPARE ulitekelezwa kwenye shule 38 kutoka manispaa ya Kinondoni zilizochaguliwa kwa kutumia taratibu sampuli mtawanyiko zilizopangwa katika makundi mawili ya shule za mwingilio yaani ilikotolewa elimu hiyo zilizokuwa 19 na za kulinganisha zilizokuwa 19.Ili kuweza kupata matokeo yaliyokusudiwa mradi ulitoa mafunzo kwa walimu watano wakufunzi wa wakufunzi; ulitoa mafunzo kwa walimu watekelezaji 76, na waelimishaji rika wanafunzi 132 na kuelekeza watoa huduma 8 wa afya katika kliniki za huduma rafiki kwa vijana ili kutekeleza muingiliano.

  Tathmini iliyotoa majibu ya jinsi utendaji unavyoendelea na ya matokeo ilihusisha shule zote na wanafunzi zaidi ya 6,000 waliowekwa kwenye muingiliano, huku uchambuzi wa tathmini ukihusisha wanafunzi wenye umri wa miaka 12-14, wenye kujua kusoma na kuandika.
  Matokeo yaliyotathminiwa ni Mabadiliko katika masuala ya ngono (kuanza ngono) na Kutumia kondomu wakati wa kujamiiana kwa wale waliokwisha anza ngono.
  Kwa wastani mradi uliona kwamba mwingilio wa PREPARE ulipunguza uwezekano wa vijana wadogo (wavulana na wasichana) kuanza ngono na kuongeza uwezekanao wa kutumia kondomu kwa wale walioanza.
  DSC_0148
  Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo. Kushoto ni mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi, Vicky Kimaro akiuliza swali kwenye mkutano huo.

  Hata hivyo, katika utekelezaji wa mradi mabadiliko katika uchukuaji wa hatua yalionekana zaidi miongoni mwa wasichana waliopata mwingilio ukilinganisha na wale ambao hawakupata mwingilio. Uchukuaji wa hatua ulisababisha tabia ya kutumia kondomu miongoni mwa wanafunzi wa kiume lakini siyo miongoni mwa wanafunzi wa kike.

  “Kimsingi tunataka kuwaambia wanahabari kuwa miongoni mwa mafanikio makubwa ya mradi wa PREPARE ni kuchelewesha kuanza ngono miongoni mwa wanafunzi wa kiume na wa kike wenye umri wa miaka 12-14 katika mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania; “Kuongeza uchukuaji wa hatua ulio chanya katika kutumia kondomu kwa jinsia zote na taarifa za ongezeko la utumiaji wa kondomu miongoni mwa vijana wa kiume. “

  Mradi huu uliofadhiliwa na Umoja wa Nchi za Ulaya, Programu ya utafiti wa afya umelenga kuangalia mwingilio ulio katika misingi ya utamaduni na jinsia, endelevu, kijamii ili kukuza ujinsia na afya ya uzazi miongoni mwa vijana wenye umri kati ya miaka 12-14 kwa kutumia shule kama njia ya kufundishia.

  0 0

   Dar es Salaam. ENOC Africa, a Tanzanian oil company, has won a tender to import fuel under the Petroleum Bulk Procurement System (BPS) for the month of October this year.

  The tender, which attracted six oil companies including five foreign and international companies, was awarded to ENOC Africa after offering the lowest Weighted Average Premium per Metric Ton of $ 45.771 per MT. Other companies (all international) that participated in the tender include Addax Energy SA which quoted $ 49.18 per MT, Augusta Energy SA ($ 48.854 per MT) and Gapco (K) Ltd ($ 47.543 per MT).

  Speaking about the tender results over the weekend of which the company will import 299,872 Metric Tons of fuel, Petroleum Importation Coordinator (PIC) General Manager, Michael Mjinja said ENOC Africa was pronounced the winner after meeting all the tender requirements and proving that its offer would most benefit the country, traders and consumers.
    
  “Among the six oil companies, only four returned the tender documents and finally the winner (ENOC Africa) was picked.  ENOC Africa is the only a locally registered company and the consignment it will import will be enough to serve the country for a period of one month and two weeks,” he said.

  Mr. Mjinja said it was delighting to see local companies like ENOC Africa coming up to pose a challenge to giant foreign international oil companies which had previously dominated the sector by frequently winning such tenders.

  “BPS is the most transparent way of public procurement where the winning bidder is decided in the open before representatives of all bidders, everyone endorses the winning bidder,” said Mr. Mjinja. ENOC Africa will import 156,863 MT of Automotive Gas & Oils (AGO), 115,490MT of Premium Motor Spirit (PMS – gasoline), 26,269MT of Jet A1 and 1,250MT of Kerosene.

  “With the transparent manner in which the winning bidder is picked, oil marketing companies are satisfied with the process. They do accept decisions made openly and unanimously in picking the winning bidder,” said Mr. Minja.

  When contacted via phone yesterday, the Energy and Water Utilities Regulatory Authority (Ewura) Head of Communication and Public Relations, Titus Kaguo said that BPS has proved to be a system which both consumers and suppliers are happy with and has helped lowered pump prices for fuel, increased government revenue and restored some sanity in the oil trading business.

  “The system has helped in improving quality of petroleum products, stabilized cup prices, improved taxation and has helped to reduce demurrages at the port. Apart from transparency and increasing government revenue, the BPS has also assisted the country to save foreign currency used to purchase petroleum products,” he said.

  ENOC Africa, which recently expressed its intention to heavily invest in storage facilities in Tanzania and neighbouring countries, has proved its ability to ensure sustainability in oil supply in Tanzania by winning the tender for the third time.   Tanzania consumes about 1.54 million cubic meters per annum of petroleum products.

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Fatma S. Ally alipowasili wilayani humo kukagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na wananchi.
   Rais Kikwete akisalimiana na viongozi mbalimbali wilayani humo.
    Rais Kikwete akisalimiana na viongozi mbalimbali wilayani humo
   Rais Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Mtera Mhe Livingstone Lusinde "Kibajaji".

  0 0

  Bondia Imani Daud kushoto akipambana na Hamaduu Mwalimu wakati wa mchezo wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita tandika Dar es salaam Daud alishinda kwa pointi katika mpambano huo wa raundi sita.
  Bondia Hamaduu Mwalimu akimrushia konde Imani Daud wakati wa mchezo wao uliofanyika Tandika Dar es salaa Daud alishinda kwa point .
   


  Bondia Nobel Syrvesta kushoto akipambana na Bakari Dunda wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Nobel alishinda kwa point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

  0 0

  Mkuu wa wilaya songea Joseph Mkirikiti akikata utepe kuasiria ufunguzi wa mnara wa Airtel uliopo Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma mipakakani mwa Msumbiji na Tanzania ili kuboresha  mawasiliano katika mkoa Ruvuma na jirani, anaeshudia ni meneja wa kanda ya Kusini wa Airtel Bw Straton Mushi (wakwanza kulia) na meneja masoko wa kanda hiyo wa Airtel Bw Jonas Mbaga (kati) mwishoni mwa wiki, mawasiliano hayo yatazaidia vijiji vya Muhukulu, Lalia, Magwamila, Nakwale, Nambendo, Mkenda, Makwaya, Miputa  vyote vya Mkoani Ruvuma

  wananci wakisangili mara baada ya Mkuu wa wilaya ya
  Songea Joseph Mkirikiti kukata utepe kuashiria ufunguzi wa mnara wa
  Airtel Mkoani Ruvuma mpakani mwa Tanzania na msumbiji kwa lengo la
  kuboresha mawasiliano mwishoni mwa wiki,wawasiliano haya yatasaidia
  vijiji vya Muhukulu, Lalia, Magwamila, Nakwale, Nambendo, Mkenda,
  Makwaya, Miputa  vyote vya Mkoani Ruvuma
   Mkuu wa Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma Joseph Joseph  Mkirikiti
  amezindua mitambo ya mawasiliano (minara) katikaka kijiji cha Muhukulu
  na kuwataka raia wa Tanzania wa vijiji vya Muhukulu, Lalia, Magwamila,
  Nakwale, Nambendo, Mkenda, Makwaya, Miputa  vyote vya Mkoani Ruvuma na wale wote wanaoishi mipakakani mwa Msumbiji na Tanzania kuwa Walinzi kwa mitambo ya Airtel inayowekwa kwa ajili ya mawasiliano isiharibiwe na watu wasiopenda maendeleo.

  Mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Joseph Mkirikiti ameyasema hayo
  mwishoni mwa wiki wakati akizindua Minara hiyo ya ya mawasiliano ya
  Simu iliojengwa katika kata ya Mhukuru Mpakani mwa Msumbiji na
  Tanzania.

  Mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Joseph Mkirikiti alisema “juhudi
  zinazofanywa na Serekari kwa kushirikiana na Makapuni ya Simu ikwemo
  kampuni ya Airtel ni kumpa mwananchi fulsa ya  kuwasiliana na
  watukatika mambo ya  kiuchumi,afya,na elimu  na mawasiliano ya kijami”

  Amesema pia katika kutatua kero mbali mbali za wananchi, pamoja na
  mawasiliano ndiyo maana baada ya ziara ya Rais wa Jamuhuri ya Mungano
  wa Tanzania wananchi walipotoa kero zao kwa Rais ufumbuzi umefanywa
  wakuiomba Airtel kujenga Mnara .

  …”sasa ni juu ya Wananchi kuutumia kwa lengo lililo wekwa ili
  kutowakatisha tamaa wawekezaji aliongeza kwa kusema Mkirikiti!
  Meneja wa kanda ya kusini wa Airtel kutoka mbeya Straton Afrikan Mushi
  amewataka wananchi kutumia mtandao wa Airtel hasa huduma za kibenki
  ili kuepukana na uporaji wa fedha wanaposafili,  pia amewaomba kuwa
  walinzi wa Minara ya Airtel ‘naomba mfahamu huu mtambo hapa ni
  kwaajili yenu wote hivyo changamkieni huduma zetu nafuu Zaidi hasa ile
  ya Airtel Money ambayo itaondoa na kupunguza changamoto nyingi za
  upatikanaji wa huduma za kibenk katika vijiji na miji ya karibu na
  mkoa wetu huu” aliongeza Straton

  Wananchi wa Mkoani Ruvuma wameishukuru serikali kwa kuweza
  kushirikiana na Kampuni ya Airtel kupata mawasilino ya uhakika huku
  injinia wa Airtel  Saidi Hanga akiwaahidi  wananchi kuto katika kwa
  mawasiliano

  Mnara wa Simu wa Kampuni ya Airtel umekuwa mkombozi pekee kwa wananchi  wa Mpakani mwa Msumbiji na Tanzania ambao walikuwa wakisafiri kwa muda mrefu zaidi ya kilometa 40 kutafuta sehemu yenye kushika mawasiliano kwa kupanda kwenye kilele cha mlima, pia wamesema
  mawasiliano ya nchi jirani ya msumbiji ukiyapata yalikuwa yatoza fedha
  pande zote mbili bila kujali nani kapiga simu nani amepokea simu.

  0 0

  THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

  Telephone: 255-22-2114512, 2116898
  Website : www.ikulu.go.tz              

  Fax: 255-22-2113425  PRESIDENT’S OFFICE,
        STATE HOUSE,
                1 BARACK OBAMA ROAD,  
  11400 DAR ES SALAAM.
  Tanzania.
   

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mheshimiwa Abbas Kandoro kuomboleza vifo vya watu 10 vilivyotokea Mbalizi, Mkoani Mbeya tarehe 29 Agosti, 2014 baada ya basi dogo la abiria aina ya Toyota Hiace maarufu kama Daladala Na. T 237 BFB kugongana na lori aina ya Tata Na. T 158 CSV.   Katika ajali hiyo, watu saba wengine walijeruhiwa na kukimbizwa hospitali kwa matibabu.

  “Nimesikitishwa na kuhuzunishwa mno na taarifa za vifo vya watu 10 na wengine saba kujeruhiwa katika ajali hii iliyotokea siku chache baada ya ajali nyingine kutokea Mkoani Tabora iliyoua watu 19 na wengine 81 kujeruhiwa”, amesema Rais katika salamu zake.

  Rais Kikwete amesema mfululizo wa ajali hizi unaonyesha dhahiri kuendelea kuwepo kwa tatizo la ukosefu wa umakini miongoni mwa madereva, hivyo jitihada zaidi zinatakiwa kufanywa kusimamia kikamilifu Sheria ya Usalama Barabarani na kufuatiliwa kwa karibu kwa mienendo ya wanaoendesha vyombo vya moto, ili ajali hizi ziweze kupunguzwa na hata kudhibitiwa kabisa katika barabara zetu.

  “Naomba upokee  salamu zangu za rambirambi  kutoka dhati ya moyo wangu kutokana na ajali hiyo, na kupitia kwako naomba unifikishie salamu zangu za pole kwa wafiwa wote kwa kupotelewa ghafla na wapendwa wao”Ameongeza.

  Rais Kikwete amesema anatambua machungu waliyo nayo wanafamilia, ndugu na jamaa wa watu waliopoteza maisha yao kwenye ajali hiyo, lakini anawaomba wote wawe wavumilivu na wenye subira wakati huu wanapoomboleza vifo vya ndugu na jamaa zao.

  “Ninawaombea kwa Mola majeruhi wote wa ajali hiyo waweze kupona haraka na kurejea katika hali zao za kawaida ili waweze  kuungana tena na familia, ndugu na jamaa zao”, amemalizia kusema Rais Kikwete katika salamu zake. 


  Imetolewa na;
  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu – Dar es Salaam.
  31 Agosti,2014  0 0


   Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa kwenye maonyesho Katika Uwanja wa Taifa.Picha na Maktaba.
  Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa mazoezini.
  Na Josephat Lukaza - Lukaza Blog. 

  Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) leo limetimiza Miaka 50 toka Kuanzishwa kwake mnamo tarehe 1/09/1964. JWTZ ni moja ya Jeshi lililotajwa na Mtandao mmoja hivi karibuni kuwa Ni Jeshi lenye weredi wa hali juu Duniani kutokana na Operesheni ambazo wamewahi kuzifanya na linalotumia Silaha za Kisasa. Baadhi ya Operesheni zilizowahi kufanywa na Jeshi la Wananchi Wa Tanzania (JWTZ) ni Ile ya Kuwasambaratisha Waasi Wa M23 nchini Congo, Operesheni ya Comoro, Operesheni nyingine ni Ile ya Kulinda Amani Sudan wakiwa wameungana na Majeshi Mengine Kutoka Umoja wa Mataifa (UN).

  Jeshi la Wananchi Wa Tanzania (JWTZ) limejipatia Umaarufu na sifa kutokana na Kuwa na Askari wenye Nidhamu ya Hali ya Juu na Kuwachukulia Hatua kwa Haraka Askari wake ambao wameonyesha utovu wa Nidhamu kwa Wananchi na Jamii kwa Ujumla lakini Pia Sifa Hiyo Kubwa Imekuja Kutokana na uwezo mkubwa wa Kivita na Kuweza Kuwasambaratisha Waasi wa Kikundi cha M23 nchini Congo.

  Jukumu kubwa la Kazi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania ni Kulinda Mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dhidi ya Wavamizi na Vile vile Kushiriki katika kulinda Amani Katika Ngazi ya Kimataifa lakini Pia Pamoja na Majukumu hayo vilevile Jeshi la Wanannchi wa Tanzania (JWTZ) limekuwa Mstari wa Mbele katika Kujitoa kwenye shughuli za Kijamii kama Vile Matibabu, Elimu nk na Wamekuwa Mstari wa Mbele katika Kusaidia Jamii katika shughuli mbalimbali kama Vile za Uokoaji katika Maafa yanayotokea Nchini.

  Kwa kifupi Sahivi Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limekuwa jeshi la Kisasa na wasomi ambao wanalisaidia Jeshi katika Kufanikisha Malengo yake kama Kulinda Mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kujitoa katika shughuli nyingine za kijamii. Hongera ya Kutimiza Miaka 50 Tokea Kuanzishwa

  0 0

  Mtaalamu wa masuala ya lishe wa wilaya ya Njombe,Bi Bertha Nyigu, akijibu maswali ya wanavijiji mbalimbali waliofika kupata elimu ya masuala ya lishe na uongozeji virutubishi kwenye chakula.Kampeni za lishe bora na virutubishi zinaendelea kufanyika katika wilaya mbalimbali hapa nchini chini ya usimamizi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
   Afisa lishe wa Wilaya ya Njombe akitoa mada kwenye semina ya maafisa watendajji wa kata na viongozi wa vijiji wakati wa semina kuhusu kuongeza virutubishi kwenye vyakula iliyofanyika wilayani humo katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Njombe leo.Kampeni za matumizi ya vyakula vyenye virutubishi zinaendelea katika wilaya mbalimbali nchini.
   Wanakijiji cha Ngalanga wilayani Njombe wakisikiliza mtaalamu wa lishe wa wilaya Bi Bertha Nyigu wakati wa semina juu ya matumizi ya vyakula vilivyoongezewa virutubishi iliyofanyika katika viwanja vya halmashauri ya wilaya ya Njombe.Kampeni za matumizi ya vyakula vyenye virutubishi zinaendelea katika wilaya mbalimbali chini ya usimamizi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii na wadau wengine wa masuala ya afya.


older | 1 | .... | 353 | 354 | (Page 355) | 356 | 357 | .... | 1897 | newer