Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

Viongozi, wanaharakati wataka Katiba Mpya Imtambue mtoto na haki zake

$
0
0
Mwenyekiti wa Mtandao wa Mashirika yanayofanya kazi na Watoto Tanzania ambaye pia ni Mratibu Miradi, Kituo cha Watoto wa Mtaani cha Dogodogo Kigogo (Dogodogo Centre Street Children Trust), Sabas Masawe. 
Mwenyekiti wa Mtandao wa Mashirika yanayofanya kazi na Watoto Tanzania ambaye pia ni Mratibu Miradi, Kituo cha Watoto wa Mtaani cha Dogodogo Kigogo (Dogodogo Centre Street Children Trust), Sabas Masawe.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Fatma Mwasa akizungumza na mwandishi wa makala haya. 
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Fatma Mwasa akizungumza na mwandishi wa makala haya.

. MCHAKATO wa kujadili na kuandika Katiba Mpya unaendelea bungeni mjini Dodoma, licha ya kuwepo kwa mvutano na mgawanyiko wa makundi ya wabunge wa bunge maalumu wanaojadili Rasimu ya Pili iliyowasilishwa kwao. Wakati hayo yakiendelea viongozi, wanaharakati na wadau wa watoto wanapendekeza masuala ya haki za msingi za watoto yatambulike vizuri katika katiba ijayo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Watoto na Jinsia wa Tanzania, Anna Maembe akizungumza na mwandishi wa makala haya. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Watoto na Jinsia wa Tanzania, Anna Maembe akizungumza na mwandishi wa makala haya.
 Bi. Valerie Msoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA). Bi. Valerie Msoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA).

 Mwenyekiti wa Mtandao wa Mashirika yanayofanya kazi na Watoto Tanzania ambaye pia ni Mratibu Miradi, Kituo cha Watoto wa Mtaani cha Dogodogo Kigogo (Dogodogo Centre Street Children Trust), Sabas Masawe anashauri ibara ya 43 ambayo inataja haki za msingi za watoto iendelee kuwepo mpaka Katiba inakamilika na iboreshwe zaidi katika mchakato unaoendelea Bungeni. 

Nasema haya maana tayari kuna baadhi ya watu wameanza kuhoji kwamba kwanini hata watoto wanaingia kwenye katiba ilhali wao ni sehemu ya watu kama wazazi wao. Anasema pamoja na kuingizwa kipengele cha mtoto kwenye rasimu ya pili ya katiba bado kuna mambo ambayo wao kama wadau wangependa yaingizwe tena hivi sasa katika mchakato wa majadiliano unaoendelea. Anasema baadhi ya mambo hayo ni kama umri wa mtoto mwenyewe kutaja wazi kwamba ni kuanzia umri gani.


 "...Unaweza ukaangalia hili ni suala la msingi sana kutaja umri wa mtoto mwenyewe anayezungumziwa...kwa sisi wadau wa watoto tunashangaa sana kwa maana nyingine tunaona suala hilo ni kama linaongeza utata, kumuweka mtoto kwenye katiba ilhali umeshindwa kumtambua (kiumri) mtoto ni yupi ni sawa na vichekesho...tunashauri mtoto huyu umri utajwe wazi kuondoa utata...," anasema.

 Mfano ukisema wazee wana haki ya kutibiwa bure lazima useme huyu mzee anaanzia umri gani na kuishia wapi. Huwezi kusema wazee watibiwe bure alafu unashindwa kuainisha vitu vya muhimu kama umri wao, bila hivyo utaleta mkanganyiko wa tafsiri...ndiyo maana hata sasa mtoto anayetajwa tunataka tujue anaanzia umri gani na kuishia umri gani. Sasa hili pekee linatushangaza watu wasomi wanajadili bila kuliona hili.
 Huyu mtoto akiingia kwenye mgongano katika sheria anashughulikiwa namna gani kwasababu hili linaweza kuwa na mgongano kama pia litashindwa kutajwa kwenye katiba chombo ambacho ni sheria mama ya nchi. Masawe anasema mambo mengine ambayo yanatakiwa kuainishwa ni pamoja na kuelekeza namna ya kuwawajibisha wazazi ambao wamekuwa wakikimbia majukumu yao ya kulea watoto na kuwapeleka katika vituo vya yatima eti kwa madai wamewashinda.

 "Hapa tunataka ijulikane pia hawa wazazi ambao wamekuwa wakikwepa majukumu yao wanawajibishwa vipi...maana wengine tunawapelekea mtoto wake anatamka wazi kwamba mimi huyu mtoto amenishinda kabisa, sasa kama amekushinda nani wa kukulelea? Sasa watu kama hawa lazima ijulikane namna wanavyowajibishwa kwenye katiba au kama ni jukumu la Serikali katiba ieleze wazi ili iwe rahisi kumbana mtu kisheria," anasema Masawe.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Watoto na Jinsia wa Tanzania, Anna Maembe, anasema Serikali inawapenda watoto na ndiyo maana katika mchakato mzima wa kukusanya maoni ilizingatia kupata maoni ya kutosha kutoka kwa watoto wenyewe pamoja na wadau wengine wanaotetea haki za watoto. 

Bi. Maembe anasema Ibara ya 43 katika Rasimu ya Pili imeweka wazi haki za watoto pamoja na kufafanua zaidi. "...Ibara ya 43(1) (a) na kuendelea hadi (g) inaongelea kabisa na kufafanua kwa kina haki ya mtoto...hii ni pamoja na kulindwa, kuelimishwa, kupatiwa huduma za afya na huduma zingine zozote muhimu ambazo zitamfanya mtoto akuwe na kufikia utimilifu ambapo naye awe mzalishaji na mwananchi mwema...," anasema.

 Bi. Maembe akizungumza na mwandishi wa makala haya. Anasema katika mchakato wa kukusanya maoni wadau wamepewa nafasi ya kutosha katika kutoa maoni kwa ushirikiano na wabunge, wadau wengine wa watoto, pamoja na mabaraza ya watoto ambayo yapo kila wilaya kutoa sauti za watoto. Anasema anaamini ibara iliyopo sasa inayozungumzia haki za watoto itaboreshwa zaidi mara baada ya mchakato kufikia mwisho hivyo kutoka na mwongozo mzuri zaidi wa kutetea haki za kundi hilo la watoto. 

 "...Binafsi mi bado naamini kuwa mchakato wa katiba, mi naomba niseme hivi mchakato wa katiba ni nafasi nzuri sana ya kuweza kutetea haki za watoto wa Tanzania, kwa kuwa mtoto wa leo ndiyo mbunge wa kesho, kwa hiyo tusipoweka haki zake vizuri hata wabunge wetu wajao hawatakaa wakatimiza wajibu wao vizuri...kwa kuwa sisi wote tulianzia utotoni hadi kufikia hapa, kwa hiyo mchakato wa katiba ufanye mambo yote lakini haki za mtoto zionekane vizuri ili sheria zote za nchi ziweze kupata mwongozo kutoka kwenye katiba yetu inayokuja ambayo ni sheria mama kuweza kutoa haki kwa mtoto.

. Hata hivyo anasema mbali na haki za mtoto kuzingatiwa katika Katiba inayokuja bado watoto wanapaswa kuzingatia kuwa haki inakwenda sawa na wajibu, hivyo nao wanapaswa kutimiza wajibu yaani wasome kwa bidii, wakubali kuelekezwa na sio wafanye mambo yao kinyume kwa kuwa wanajua haki zao zimezingatiwa. Mkuu wa Mkoa wa Tabora Fatma Mwasa anaipongeza Serikali kwa kitendo cha kutoa msukumo wa kipekee kwa kuwaingiza watoto katika Katiba Mpya. 

Anaongeza kuwa Serikali ina kila sababu ya kufanya hivyo maana imeridhia mikataba ya kimataifa kulinda haki za msingi za watoto, ambapo katika mikataba hiyo imeainisha mambo ya msingi ya kuzingatia. Haki ya kuishi, haki ya kupata elimu, haki ya afya haki ya kuudumiwa na kulindwa. Anasema kikubwa ambacho tukiweza kukifanya kikapitishwa katika katiba mpya ambacho kitasaidia kuongeza hatua ambayo Serikali imefikia ni kiongeza umri wa mtoto wa kike kuolewa. 

Akifafanua zaidi Mwasa anasema suala hilo limekuwa na ajenda kwa muda mrefu hasa tunapopigania masuala ya kijinsia, usawa na haki za watoto. Anasema eneo hili la umri wa kuolewa limekuwa likizua mkanganyiko kwa wengi kwa kile upande mmoja sheria kuruhusu mtoto wa chini ya miaka 18 kuolewa, licha ya upande mwingine bado sheria nyingine inamtambua mtu chini ya umri wa miaka 18 ni mtoto. 

"...Kimsingi eneo hili limekuwa likizua utata kwa baadhi ya makundi katika jamii...hasa baadhi ya viongozi wa dini wao wanasema mtoto wa Tanzania anamaliza elimu ya msingi akiwa na miaka 14 na hapo kama hakufanikiwa kuendelea na sekondari hubaki nyumbani bila kuwa na cha kufanya, wanasema mtoto huyu anaweza kujiingiza katika mchezo mbaya kama atakaa tu akisubiri umri wa kuolewa wao wanaona kama amepata wa kumuoa ni bora akaolewa kuliko kujikuta akijiingiza katika mambo yasiofaa," anasema Mkuu wa Mkoa huyo.

 Anasema hata hivyo anaishukuru Serikali kuleta shule za kata maana idadi kubwa ya watoto sasa wanapata nafasi za kuendelea na masomo na kujikuta wakiepukana na hatari za ndoa za utotoni, lakini pamoja na hayo anasema bado kuna haja ya kujenga mfumo mzuri wa kuhakikisha suala la ndoa za utotoni linatoweka kabisa. Pamoja na hayo anabainisha kuwa kuna haja ya Katiba kutamka wazi kuwa mtoto asiruhusiwe kuolewa chini ya umri wa miaka 18.

 Akizungumzia haki kwa makundi maalum ya watoto wakiwemo walemavu, anawashauri wazazi wenye imani potofu kubadilika na kumchukulia mtoto mlemavu ana haki zote kama ilivyo kwa watoto wengine. Anasema baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwaficha watoto wenye ulemavu ili wasiweze kupata haki zao ya msingi. 

 "...Kwenye hili changamoto kubwa ilikuwa wazazi wenyewe kufikiri kuwa kuzaa mtoto mwenye ulemavu ni jambo ambalo linaleta fedheha, hii imekuwa ikisumbua sana maana wakati mwingine tunabaini watoto wenye ulemavu wakiwa wamewekwa ndani wakati mwingine kwa miaka kadhaa...sasa hili tunaamini sio haki maana mtu yeyote anaweza kuwa mlemavu wakati wowote hata mimi sasa kumbagua juu ya haki kwa kuwa yuko vile sio sawa hata kidogo," anasema Mwasa. 

Bi. Valerie Msoka ni Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA), anasema ili mabadiliko katika jamii yatokee vyombo vya habari vinahitajika sana na kwa namna yingine vinatoa mchango mkubwa. Anatolea mfano kuwa kwa sasa matukio ya ndoa za utotoni bado yanashamiri kwa baadhi ya mikoa kwa kiasi kikubwa. Anasema pamoja na vitendo hivyo kuendelea vyombo vya habari ndiyo nyenzo pekee ambayo inaweza kubadili mtazamo katika jamii na matendo hayo kukoma kabisa. 

Anasema mijadala inayoendelea kutoka kwa jamii na vyombo vya habari kuendelea kuripo inasaidia wajumbe wa Bunge la Katiba kupata taarifa za kina zaidi juu ya masuala mbalimbali wanayoyajadili hivi sasa hivyo kuendelea kuboresha zaidi. "...Mfano masuala ya ndoa za utotoni yanayozungumzwa hivi sasa, ukeketaji na masuala mengine ya unyanyasaji wanayofanyiwa watoto na vyombo vya habari kuandika yanawasaidia wabunge kuwa naufahamu zaidi wanapochangia katika kamati mbalimbali za Bunge la Katiba...kwa maana hiyo mchango wa vyombo vya habari unaitajika sana," anasema Bi. Msoka. 

 Anasema ili kuondoa utata juu ya umri wa mtoto; Katiba ijayo ingemsaidia mtoto kutamka wazi kuwa mtoto wa kike au wa kiume haruhusiwi kuoa au kuolewa akiwa chini ya miaka 18. Anasema hii ikitamkwa wazi watu wataelewa na hata utoaji elimu kwa jamii juu ya umri wa mtoto na haki zake hauta kuwa wa mkanganyiko kama ilivyo sasa.

 Anasema kwa sasa zipo baadhi ya mila zinashindwa kumlinda mtoto hasa wa kike hivyo kujikuta wanaozeshwa na kukosa haki zao za msingi ya kupata elimu, ilhali sheria zinashindwa kuwasaidia kwa kile nayo kuwa wa utata juu ya umri wa kuolewa kwa mtoto. Anasema katiba mpya ikitamka wazi masuala hayo itakuwa rahisi kuwashughulikia wanaotumia udhaifu wa sheria na kumnyanyasa mtoto. 

Hata hivyo anafafanua kuwa pamoja na kuweka sheria ya kumlinda mtoto katika hali zote za unyanyasaji bado jamii inatakiwa kupewa elimu ya kutosha juu ya kuziacha mila na desturi zilizopitwa na wakati ambazo zimekuwa zikimnyanyasa mtoto hasa wa kike. Mwanaharakati huyu ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba anashauri elimu ya kuanzia msingi hadi kidato cha nne itolewe bure na kwa watoto wote. Anasema mtoto atatakiwa kusoma hadi kidato cha nne bure kama ilivyo darasa la saba sasa kisha kuchujwa kidato cha nne. "...

Nasema hivyo nikiwa na sababu kwamba ukiangalia mtoto anayemaliza elimu ya msingi madarasa ambayo ni lazima kila mmoja apitie, wanamaliza wakiwa wadogo sana, sasa kwa hali hii mi ninashauri kuanzia msingi hadi kidato cha nne yangekuwa ni madarasa la lazima na bure ili watoto hawa wapate elimu hadi kidato cha nne angalau hapa watakuwa wameongeza kitu kichwani na miaka kusogea...," alisema. 

Anasema mtoto anayemaliza katika kidato cha nne angalau atakuwa amepata elimu kiasi, anajitambua na umri umeongezeka kidogo hivyo kama wengine wataishia katika darasa hilo wanaweza kujitegemea na hata walioolewa watajitambua hivyo kujenga familia ambazo zinajielewa kwa kiasi fulani tofauti na ilivyo kwa sasa. 

Kwa upande wake Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Watoto na Jinsia wa Tanzania, Sophia Simba anasema takwimu zinaonesha kuwa Tanzania ni kati ya nchi 20 Ulimwenguni ambazo zimekithiri kwa kuwa na ndoa za utotoni. Aidha anabainisha kuwa takwimu pia zinaeleza katika kila watoto tano, wawili kati yao wameolewa chini ya miaka 18. "...Hili ni tatizo kubwa sana, fikiria kwa kila watoto watano wasichana wawili kati yao wameolewa chini ya miaka 18, sasa ukiangalia utaona karibuni kila wakati kuna mtoto anaolewa Tanzania akiwa chini ya miaka 18. 

Hili Serikali haiwezi kukaa kimya ndiyo maana kuna programu mbalimbali zinafanywa kukabiliana na hali hii...leo tumezinduwa kampeni za kukabiliana na hali hiyo Mara tutafanya hivi maeneo mengine pia kupinga suala hili," anasema Bi. Simba. Pili Muherisens (13) ni mwanafunzi wa darasa la tano katika moja ya shule za msingi Wilayani Tarime. Binti huyu alilazimika kutoroka kwao na kukimbilia eneo lingine akikwepa kukeketwa na wanaukoo kijijini kwao. 

Mtoto huyu wala wazazi wake wote hakupenda kukeketwa baada ya kuhofia madhara ya tendo hilo lakini ukoo ulishinikiza na ukatishia kama wazazi watazuia mtoto wao kufanyiwa hivyo wangeliwatenga na mama yake kupigwa. Hapo ndipo binti alipoamua kukimbia kijiji na kwenda kwenye vituo salama. Binti huyu anaomba Serikali iwasaidie watoto kama hawa ambao hulazimishwa kukeketwa na hata kuozeshwa mapema ikiwa ni vitendo vya unyanyasaji dhidi yao. Cha kujiuliza ni watoto wangapi Tanzania ambao wanakumbana na unyanyasaji wa nguvu kama huu. *Imeandaliwa na www.thehabari.com

Buriani BETTY NDEJEMBI: Tusake #JusticeFor Betty kwa kupambana na unyanyasaji mtandaoni (Cyberbullying) pia

$
0
0
Ninaandika makala hii nikitambua bayana kuwa itamuudhi kila mtu anayeingia mtandaoni kwa minajili ya kuwanyanyasa watu wengine. Lakini siku zote ninaamini katika busara hii: kuuchukia ukweli hakuufanyi kuwa uongo. Ukweli ni ukweli na uongo ni uongo. Ukweli hauwezi kuwa uongo, na kadhalika uongo hauwezi kuwa ukweli. Kamwe asilani.

Wakati tunaomboleza kifo cha ndugu yetu Betty Ndejembi hatuwezi kukwepa ukweli kwamba siku chache kabla ya kifo chake binti huyo alinynyaswa mno kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter. Japo hadi muda huu hatuwezi kuhusisha moja kwa moja uhusiano kati ya unyanyasaji huo na kifo cha binti huyo, ukweli tu kwamba mtu akinyanyaswa masaa kadhaa kabla ya kifo chake, waweza kujenga picha flani.

Naomba ieleweke kuwa simlaumu mtu kwa sababu sina mamlaka ya kufanya hivyo bali dhima ya makala hii ni rambirambi zangu na kuzungumzia tatizo la unyanyasaji mtandaoni, sambamba na suala zima la unafiki kila kinapojiri kifo hususan cha mtu maarufu.

Tuna tatizo kubwa huko mitandaoni. Tumefika hatua ya kuwapa umaarufu watu wenye matusi ya nguoni, wazushi, wambeya, wanafiki, wanaharamu na kila aina ya binaadamu wanaostahili laana lakini twaishia kuwatukuza. Kwa Twitter, matusi imekuwa ni njia ya mkato ya kupata umaarufu. Kuna wenzetu wengi tu wenye 'umaarufu' huko Twitter, na ukidadisi chanzo cha 'umaarufu' huo, utaambiwa 'ah huyu ana matusi si mchezo!'


Kuna watu wazima na akili zao wanatumia muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii aidha kunyanyasa wenzao kama si kusherehesha unyanyasaji huo. Marehemu aliitwa majina kadhaa ya kumdhihaki kabla ya kukutana na mauti. Kuna waliomwita Di Maria na wanajifahamu. Japo sijui chanzo cha 'ugomvi na aliogombana nao' (na ndio maana sikujihusisha nao kwani haukunihusu), kuna wanafiki wengi tu waliokuwa katika nafasi nzuri ya kuzima moto huo hasa kwa vile baadhi yao walikuwa wakizifahamu pande zote mbili za 'ugomvi' husika.


La kukera zaidi ambalo ni wazi litajichomoza wakati wa maombolezo haya ni unafiki: baadhi ya watu walewale waliodiriki kumwandama marehemu wakati wa uhai wake watageuka kuwa wenye uchungu mkubwa baada ya kifo chake. Hii inanikumbusha suala ambalo nimeshawahi kulizungumzia mara kadhaa, katika hali ya utani japo wenye uweli, kwamba 'wakati mwafaka kabisa wa kutafuta vipaji vya uigizaji ni kwenye misiba: watu walewale waliokuwa wakikuchukia kwa nguvu zote watageuka wenye uchungu mkubwa kwa kifo chako.

Ukiangalia baadhi ya tweets za mwisho za marehemu ni wazi kuwa binti huyo alikuwa anahitaji msaada kutoka kwa wanaomjali




Hata pasi uelewa wa taaluma ya saikolojia, tweets za aina hii zinaashiria tatizo, na laiti 'wenye upendo wa dhati' wangeingilia kati muda huo, huenda muda huu Betty asingekuwa marehemu. 


Na hizo tweets mbili ambazo ni miongoni mwa za mwisho kabisa za marehemu ni ushuhuda tosha wa jinsi alivyokuwa akisumbuliwa na wanyanyasaji dhidi yake mtandaoni. Ndio pengine kilichomuua ni maradhi ya kawaida ya kibinadamu lakini kila mwenye ubinadamu hatoshindwa kuhusisha unyanyasaji huu na hali mbaya ya afya aliyokuwa nayo hadi anafariki.

Kuna watakaolaumu kuwa ninatumia kifo cha binti huyo kwa 'maslahi binafsi.' Hapana, sina maslahi yoyote binafsi hasa ikizingatiwa kuwa sikuwa nikifahamiana na marehemu. Hakuna anani-follow na mie sikuwa nam-follow. Labda maslahi pekee niliyonayo ni upinzani wangu mkali dhidi ya unyanyasaji wa mtandaoni. Vyovyote ilivyo, marehemu alikuwa bullied kabla hajafariki na atakayetaka kukataa ukweli huo na akatae lakini utabaki kuwa ukweli usioweza kugeuka uongo. Na kwa hakika, kila aliyeshiriki kumnyanyasa binti huyo atakuwa anasutwa na nafsi yake, hata kama atatafuta hifadhi kwenye 'huu sio wakati wa kulaumiana' au 'we failed you Betty.' 

Mara nyingi nimekuwa nikiwalaumu watu wanaodai 'Instagram imekuwa mbaya' au Twitter imeharibika siku hizi' ambapo mara zote nimewakumbusha wahusika kuwa katika hii mitandao ya kijamii, ni muhimu kuwa makini katika nani wa kum-follow. Maana yangu ni kwamba ukim-follow mtu mwenye matusi, utashuhudia matusi katika anachoandika. Ukim-follow mtu wa busara, utashuhudia busara.

Hata hivyo, katika siku za hivi karibuni kumeibuka kundi kubwa tu la watu wenye busara na elimu zao lakini wepesi wa kuvutiwa na vitu vya 'kipuuzi' - umbeya, matusi, majungu, na upuuzi mwingine, na hawasiti kushea na wanaowa-follow. Ni hivi, mtu akitweet tusi, kisha ukali-retweet, utambue kuwa unalikuza (amplify) tusi hilo. Na kimsingi, kwa kiasi kikubwa, tuna-RT vitu tunavyoviunga mkono. Uki-RT tusi maana yake unaliunga mkono. Na ni wazi mwenye kujiheshimu, na kuheshimu 'watu wa maana' wanaom-follow hawezi ku-RT upuuzi.

Tatizo kubwa sasa ni kwamba waweza kuamua kuwa-follow watu unaodhani wana busara au akili za kutosha lakini ukaishia kusoma vitu vya ajabu ajabu kwenye timeline yako kutokana na haya 'mahaba' ya ku-RT vitu vya kipuuzi. 

Binafsi, nadhani chanzo kikubwa cha mitandao ya kijamii kuwa 'sehemu za kukera, kuogopesha, kunyanyasana, nk' ni ile hali ya baadhi ya wenzetu kutokuwa na vitu muhimu vya kufanya katika maisha yao. Ni wazi kwamba ukiwa busy na maisha yako hutokuwa na muda wa kubughudhi wenzako. 

Kingine kinachopelekea social media kuwa 'dunia uwanja wa fujo' ni ugonjwa mkubwa unawasumbua baadhi ya wenzetu: kusaka sifa wasizostahili. Wanasema,. ashakum si matusi, 'lugha ya mpumbavu ni matusi,' na ndo maana baadhi ya wenzetu wasio na cha maana cha kuongea katika hadhara hukimbili matusi, unyanyasaji, maneno macha

Nitamke bayana kuwa siandiki makala hii nikitegemea kuungwa mkono na wahusika wa unyanyasaji mtandaoni. Na kwa hakika kuna uwezekano mkubwa wa makala hii kuzua 'kampeni ya chuki' dhidi yangu kutokana na makala hii. Tatizo kubwa la wenzetu hawa ni kutotaka kuambiwa kuwa 'Hapana, hili ni kosa. Na kosa ni kosa, haliwezi kuwa sahihi.' Lakini pamoja na uwezekano wa 'kuwashiwa moto' kutokana na makala hii, wito wangu kwa kila mwenye busara na akili ni kuliangalia tukio hili la kusikitisha kama 'wake up call.' Tujifunze, tujisahihishe. Tuache kusherehesha vitu vya kipuuzi mtandaoni.

Ifike mahala, ukishindwa kumkemea mtu mwenye tabia mbaya mtandaoni basi chukua option  rahisi ya kum-unfollow au ikibidi kum-block. Na ifike mahala kuwafahamisha watu wanaoendekeza utoto, majungu, umbeya, unyanyasaji na upuuzi mwingine kuwa kama hawana kitu cha maana cha kufany katika maisha yao basi isiwe sababu ya kuwasumbua wenzao wenye majukumu katika maisha yao.

Tukemee maovu badala ya kutarajia yataondoka yenyewe tu. Tuomboleze kifo cha Betty kwa kusema 'NO' kwa cyberbullies (wanyanyasaji wa mtandaoni). Tufike sehemu tuache kuwasujudia wahuni wanaodhani matusi ni sehemu ya wimbo wa taifa. Tuwakwepe waendekeza majungu, wanyanyasaji, wataka sifa za kipuuzi, na watu wasiofaa katik maisha yetu.

Wakati 'tunatafuta haki kwa marehemu Betty kutokana na unyama aliofanyiwa,' suala ambalo ni la kisheria, kilicho ndani ya uwezo wetu ni kukemea unyanyasaji mtandaoni (cyber bullying). Wakati hadi muda huu hatuwajui waliomfanyia marehemu unyama huo, takriban sote twawajua vema wanyanyasaji wa mtandaoni. Tuanze na hawa, kwani leo wamefanya kwa kwa marehemu Betty kesho itakuwa kwako.

Mwisho kabisa, ni muhimu kwetu sote kutambua kuwa tulitoka kwa udongo na tutarudi kwa udongo. Kifo ni hatma ya kila mmoja wetu.Betty ametutoka lakini nasi twaelekea huko. Visa, chuki, kunyanyasana, na vitu vingine visivyopendeza japo ni kama sehemu ya maisha yetu havipaswi kupewa nafasi katika maisha yetu haya ambayo hakuna mmoja wetu mwenye japo 'lue' ya lini yatafikia kikomo. TUPENDANE na TUHESHIMIANE.

Kwako marehemu Betty, hakuna tunaloweza kusema au kufanya sasa kurejesha uhai wako. Na hakuna neno sahihi la kuonyesha jinsi gani kifo chako kimewagusa wengi. Kubwa tunaloweza kufanya ni kukuombea kwa Mwenyezi Mungu akupatie pumziko la milele na mwanga wa milele akuangazie upumzike kwa amani. Amina.



JOPO LA MAJAJI LA KUMTAFUTA MSHINDI WA TUZO YA RAIS YA HUDUMA ZA JAMII NA UWEZESHAJI YAENDELEA NA ZOEZI LAKE JIJINI TANGA NA WILAYA YA MKINGA

$
0
0
Picha Na 6Mkurugenzi wa kampuni ya  Dawson Food Products Ltd iliyopo wilayani Mkinga mkoani Tanga Bw. Burhani Taibali (kulia) akizungumza na majaji pamoja na sekretarieti iliyotembelea  kampuni hiyo.
Picha Na 1
Majaji  Bw.  Venance Bahati (kushoto) na Bi.  Costansia Gabusa (kulia) wakijadiliana jambo wakati wa kufanya tathmini ya  mradi wa ukingo uliojengwa pembezoni mwa bahari kwa ajili ya kuzuia mmomonyoko katika eneo la  Mwarongo jijini Tanga. Ukingo huo umejengwa kwa msaada wa kampuni ya utafutaji wa mafuta na gesi ya Afren PLC.
Picha Na 2Mwalimu Mkuu  wa Shule ya Sekondari ya Tongoni Bw.  Mzihili Abeid (kushoto) akitoa maelezo mbele ya majaji waliotembelea maabara ya shule hiyo. Maabara hiyo  imejengwa na  kampuni ya utafutaji wa mafuta na gesi ya Afren PLC.
Picha Na 3Msimamizi wa kampuni ya  utafutaji  wa mafuta na gesi  ya Afren PLC Bw.  Ahmed Omar (kulia) akizungumza  na jopo la majaji na sektretarieti  kwenye maabara ya shule ya sekondari ya  Tongoni  iliyofadhiliwa na kampuni  hiyo.
Picha Na 4Jaji  Venance Bahati (katikati) akiteta jambo na msimamizi wa kampuni ya utafutaji  wa mafuta na gesi ya Afren PLC Bw. Ahmed  Omar (kulia). Kushoto ni Jaji Costansia Gabusa.
Picha Na 5Msimamizi wa kampuni ya  utafutaji  wa mafuta na gesi  ya Afren PLC Bw.  Ahmed Omar (kushoto) akizungumza na majaji  walipotembelea maabara ya  Shule ya Sekondari ya Mabokweni  jijini Tanga ambapo kwa sasa kampuni hiyo imejitolea kuwajengea maabara  ya kisasa.

MASHIRIKISHO YA SANAA NCHINI YATUA BUNGE LA KATIBA KUFUKUZIA HOJA ZAO

$
0
0

pix 1Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mh. Samuel Sitta (kulia), akisisitiza jambo kwa wawakilishi wa mashirikisho ya sanaa mjini Dodoma hivi karibuni. Mashirikisho hayo yamekuwa yakipambana kufa na kupona kuhakikisha katiba mpya inatambue wasanii kama kundi maalum na pia ilinde mali zisizoshikika yaani miliki bunifu (intellectual property). 

Maoni ya mashirikisho hayo yalishatolewa katika hatua za awali za utoaji maoni na pia kupitia mabaraza lakini kwa bahati mbaya, hayakujumuishwa katika rasimu. Waliokaa kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanamuziki Tanzania, Bw. John Kitime, Rais wa Shirikisho la Filamu, Bw. Simon Mwakifwamba na Makamu mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Bi. Samia Suluhu Hassan. (Picha zote kwa hisani ya ofisi ya Bunge la Katiba).
Makamu Mwenyekiti  wa Kamati namba tano ya Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Assumpter Mshama, akishibishwa hoja za kina kwa nini wasanii wanataka katiba mpya itambue wasanii kuwa kundi maalum na pia ilinde mali isiyoshikika au kwa lugha nyepesi miliki bunifu (intellectual property) toka kwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanamuziki Tanzania, Bw. John Kitime, mjini Dodoma hivi karibuni.
pix 9

KAMPUNI YA MATANGAZO YANAYOTEMBEA (TRIA) YAZINDULIWA RASMI TANZANIA

$
0
0
1q 
DIANA LAVENDER Meneja Mauzo na Masoko kampuni ya CONICA MINOLTA akisoma risala yake wakati wa uzinduzi wa matangazo hayo.
2q 
TRUSHAR KHETIA Mkurugenzi mtendaji wa TRIA akikata utepe wakati akizindua rasmi matangazo hayo nchini Tanzania wa pili kulia ni ZULFIKAR MOHAMED Meneja Mkuu wa kampuni ya TRANSPAPER EXPRESS na mwisho kulia ni DIANA LAVENDER Meneja Mauzo na Masoko kampuni ya CONICA MINOLTA na kushoto ni AZDA AMANI Meneja wa Huduma Shirika la ndege la PRECISION AIRLINE ambao ni wateja wakampuni ya TRIA.

.................................................................................
Kampuni ya matangazo kwa kutumia vifaa tembezi yaani matangazo yanayotembea imezinduliwa rasmi jijini Dar esSalaam.

Akiongea na waandishi wa habari pamoja na wageniwengine waliohudhuria katika hafla hiyo ya uzinduzi ulifanyika katika hanga la shirika la ndege la Precision yenye makao makuu yake eneo la uwanja wa ndege jijini Dar esSalaam, mkurugenzi mtendaji na muasisi wa TRIA bw. Trushar Khetia amesema kuwa TRIA ni kampuni ya kimataifa inayojishughulisha na matangazo yawekwayo juu, nje au ndani ya fifaa safirishi kama mabasi ya kusafiria ndani na nje ya miji, ndege na usafiri wa majini maarufu kama boti au meli.

“Tumezoea kuona ama kusikia matangazo malimbali ya kibiashara nay ale ya kijamii yaani matangazo yasiyo ya kibiashara yakifanyika kupitia kwenye TV REDIO magazeti na majarida hapa nchini lakini leo TRIA inawathibishia wafanya biashara wa Tanzania na wengine kuwa matangazo yanaweza kufanyika popote wakati wowote tena kwa gharama ndogo” alisema bwana Trushar na kuongeza kuwa TRIA ina lenga kuwainua watanzania hasa vijana wadogo na kuwafanya watambue fursa zao katika maisha sambamba na kuwaongezea matumaini makubwa wamiliki wa mabasi, ndege, daladala namakapuni ya usafirishaji katika kunufaika kutokana na biashara zao za usafirishaji.
Aidha bwana Trushar amesema kuwa kampuni yake pamoja na kwamba haitegemi kufanya biashara kwa hasara hailengi pia kutengeneza faida tu bali kuleta ufanisi na changamoto endelevu katika sekta ya masoko na matangazo ambapo vijana wadau na wateja wa huduma hiyo wataweza kupiga hatua za kimaendeleo kibiashara sambamba na kuongezeka kwa soko la ajira hususana kwa vijana wa kitanzania “TRIA Tanzania hailengi kutengeneza faida tu bali pia kuleta maendeleo yenye tija kibiashara kwa wale watakaokuwa wateja wetu na wadau kwa ujmla, lakini pia ajira kwa vijana wenye uwezo tofauti tofauti wa kufanya kazi pamoja na wale wenye utaalamu wa kuandaa na kutengeneza matangazo haya” alisema Khetia.
Kwa upande wake mwakili wa Conica katika hafla hiyo Bi Diana Lavender amesema Conoca imekuwa mteja mkubwa wa TRIA nchini Kenya na kwakutambua ubora wa kazi zinafanywa naTRIA Conica imeamua kuunga na TRIA kwakuendelea kufanya matangazo yake hapa chini “tumekuwa wateja wa hii kampuni mda mrefu sasa huko nchini Kenya na kutoka na mafanikio makubwa tumeweza kupata kupitia matangazo yetu yanayofanywa na TRIA tumeonelea kuwa ni vizuri kuja kufanya hayo matangazo hapa Tanzania hasa pale tuliposikia kwamba TRIA inaanzisha tawi hapa nchini” alisema Lavender na kuongeza kuwa kufanya matangazo kupitia mabasi, ndege, daladala, treni, vyombo vya usafiri wa majini ni sehemu ya mapambo ya mji na njia zake kwani matangazo haya hutengenezwa vizuri na kufanya kuvuta macho ya wengi kila ipitapo “ni ma mabasi yetu huko Kenya maarufu kama matatu ukipita ukiona vile inavutia lazima utafurahia na kwamba lazima unaweza kutaka kupanda hiyo basi” aliongeza.

Naye mwakilishi kutoka shirika la ndege la precision hapa nchini ambao ni moja kati ya wadau wa karibu kabisa na TRIA Bi Azda Amani amesema kuwa uwekezaji wa biashara mbalimbali hasa biashara ngeni kama hayo ni sehemu ya kuongeza na kukuza pato la taifa na kupitia kodi kwa kampuni husika lakini pia kwa wamiliki wa mabasi, ndege na vinginevyo pamoja na wale wamiliki wa matangazo yatakawekwa kwenye magari haya watalipia kodi “ni furaha kuona wawekezaji wakubwa na wadogo wakiingia kila siku hapa nchini kuwekeza kibiashara na kwakufanya hivi nchi yetu ina kuwa pia kiuchumi kupitia kodi kutoka kwa watoa huduma na wahudumiwa wa huduma hii muhimu kwa maendeleo ya uchumi na biashara nchini” alisema Amani.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Zulfikar Mohamed kutoka Transpaper ameisifia TRIA kwa hatua iliyofikia na kuwataka watanzania kuiga mfano huo muhimu na kwenda kuwekeza pia katika nchi jirani hata kimataifa “ mimi nipewa fursa ya kuzindua tawi la TRIA hapa Tanzania na kwakweli nimefurahia fursa hii.

Naomba kuwapongeza sana wahusika wote waliokaa na kuona kwamba mimi naweza kuwa mgeni rasmi wa kuzindua mradi huu muhimu lakini pia nawasifia watanzania kwa kuwa waungwana wakubwa sana kuwapokea wawekezaji kutoka pande zote za dunia bila kujali rangi kabila wa udini, kwa hili mko vizuri sana na nawapongeza sana niwaombe tu kwamba igeni huu mfano mzuri na nyinyi mkawekeze biashara zenu katika nchi nyingine kwa manufaa ya watoto wenu na watanzania wote” alisema Mohamed nakuongeza kuwa maendele ya kiuchumi katka taifa lolote huletwa na wenye nchi kupitia biashara yenye tija na inayovuka mipaka na kuleta fedha za kigeni.

WAZIRI MKUU ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI IRELAND

$
0
0
* Asaini kitabu cha maombolezo ya Waziri Mkuu wa zamani

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ametumua salamu za rambirambi kwa Serikali ya Ireland kufuatia kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo, Bw. Albert Reynolds.

Hayati Reynolds ambaye amefariki akiwa na miaka 81, alikuwa Waziri Mkuu wa nane wa nchi hiyo kwa miaka mitatu kuanzia mwaka 1992. Atakumbukwa kwa kuanzisha mchakato wa kuleta amani Ireland Kaskazini dhidi ya kundi la IRA.

Waziri Mkuu Pinda ambaye aliwasili jana (Alhamisi, Agosti 28, 2014) jijini Dar es Salaam akitokea Dodoma, alikwenda moja kwa moja ubalozi wa Ireland na kusaini kitabu cha maombolezo cha kiongozi huyo.

Katika salamu za rambirambi, Waziri Mkuu amemwelezea Bw. Reynolds kuwa ni kiongozi atakayekumbukwa kwa kuleta amani duniani na misaada ya kimaendeleo nchini Tanzania.

“Kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, ninawapa pole sana kwa kufiwa na Kaka yetu na ndugu yetu, Waziri Mkuu wa zamani wa Ireland, Albert Reynolds. Tunashirikiana nanyi katika kipindi hiki cha majonzi. Tutaendelea kumkumbuka kwa kazi nzuri alizofanya kwa nchi yetu na duniani. POLENI SANA KWA MSIBA HUU MKUBWA,” inasomeka sehemu ya salamu za rambirambi alizotoa Waziri Mkuu.

Akipokea salamu hizo, Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Bibi Fionnuala Gilsenan alimshukuru Waziri Mkuu Pinda kwa kufika ubalozini hapo na kuwapa pole kwa kifo cha Waziri Mkuu wao wa zamani.

“Tutamkumbuka kiongozi wetu kwa mambo mengi aliyoifanyia nchi yetu… Tunafarijika kwa salamu hizi za rambirambi. Tutafikisha kitabu hiki cha salamu za rambirambi kwa familia yake, naamini nao watafarijika sana,” alisema Balozi Gilsenan.

Balozi Gilsenan alimweleza Waziri Mkuu kwamba kitabu cha maombolezo kitafungwa leo.
(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
DAR ES SALAAM.
IJUMAA, AGOSTI 29, 2014.

BONDIA THOMAS MASHALI KUMKABILA HENRY WANDERA WA KENYA NOVEMBA 4 TANDALE

$
0
0

 Bondia Thomas Mashali katikati akisaini mkataba wa kucheza na Henry Wandera kutoka Kenya Novemba 4 katika ukumbi wa New Madiba 'Korini' uliopo Tandale Dar es salaam wanaoshudia kushoto ni Raisi wa oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO, Yassini Abdallah 'Ostadhi' na promota wa mpambano huo Khamis Ally picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
 Rais wa TPBO Yassin Abdala akiandika mkataba wa bondia Thomas Mashali katikati atakaepambana na mkenya Henry Wandera Novemba 4 katika ukumbi wa New Madiba 'Korini' uliopo Tandale Dar es salaam kulia ni  promota wa mpambano huo Khamis Ally picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Thomas Mashali katikati akisaini mkataba wa kucheza na Henry Wandera kutoka Kenya Novemba 4 katika ukumbi wa New Madiba 'Korini' uliopo Tandale Dar es salaam wanaoshudia kushoto ni Raisi wa oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO, Yassini Abdallah 'Ostadhi' na promota wa mpambano huo Khamis Ally picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Na Mwandishi Wetu

BONDIA Thomas Mashali 'Simba asiyefugika' anatarajia kupanda uringoni tena novemba 4 mwaka huu kumvaa mkenya Henry Wandera mpambano utakaofanyika katika ukumbi wa New Madiba zamani Korini

Mashali anapigana uku akiwa na historia ya kupoteza mpambano wake wa mwisho zidi ya bondia Mada Maugo ambapo walicheza katika uwanja wa taifa na kupoteza kwa point mpambano huo

akizungumzia mpambano huo Mashali amesema atokubali kupoteza tena mchezo huuo ukizingatia anachezea nyumbani kwao alopozaliwa na ndipo alipoanzia ngumi maeneo ya Tandale hivyo sito kubali niaibike mbele ya ndugu zangu hivyo nawambia wapenzi waje kwa wingi kuangalia mashali anavyofanya kazi yake ya mchezo wa masumbwi

nae promota wa mpambano huo Khamis Ally amewahakikishia kuwa sehemu ya parkingi ni kubwa na ulinzi ni wa kutosha kifupi katika ulinzi tumejipanga vizuri pia siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine mazuri ya utangulizi ambapo mabondia wengi wamejitokeza kucheza siku hiyo

siku hiyo pia kutakuwa na huuzwaji wa 
DVD ambazo zinatoa mwanga kwa mchezaji kujua mchezo na kufahamu zaidi mbinu mpya zitumiwazo na mataifa mbali mbali Duniani.

Wakiwemo mabondia bingwa wa dunia kama Manny Paquaio,Floyd Maywether,Amir Khani, Mohamed Ali ,Mike Tayson na wengine wengi wanaotamba na waliotamba katika mchezo huo wa masumbwi Duniani.
 
kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ametoa wito kwa makampuni mbalimbali kujitokeza kutoa sapoti ya mchezo wa masumbwi kwani ndio mchezo pekee unaoweza kututoa kimasomaso watanzania tukafurahi

AFRIKA INACHANGIA ASILIMIA 3 TU YA HEWA CHAFU DUNIANI - WAZIRI MKUU

$
0
0

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema tatizo la mabadilko ya tabianchi ni kubwa sana na kama hazitachukuliwa hatua stahiki Dunia itaisha.

Ametoa kauli hiyo leo (Ijumaa, Agosti 29, 2014) wakati akifungua mkutano wa pamoja wa Mawaziri wa Mambo ya Nje na Mazingira ambao ni wajumbe wa Kamati ya Wakuu wa Nchi Barani Afrika inayosimamia Mabadiliko ya Tabianchi (Committee of African Heads of States and Governments on Climate Change-CAHOSCC) wanaokutana kwenye ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Alisema tatizo la mabadiliko ya tabianchi linachangiwa kwa kiasi kikubwa na hewa chafu ambayo inazalishwa viwandani kutokana na matumizi makubwaya nishati.

"Kuna vyanzo vya nishati ambavyo si rafiki na kimojawapo ni makaa ya mawe. Ili uweze kupata nishati yakeni lazima uyaunguze nakwa kufanya hivyo unatoa hewa ukaa nyingi sana. Viko viwanda vinatumia mafuta mazito, vinginedizeli kwa wingi sana. Yote haya yanachangia hewa chafuambayo inafanya utando unaozuia hewa ya joto kurudi kwenye mfumo wa sayari na kutumika tena,"alisema.

Akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari,  Waziri Mkuu alisema kiwango kikubwa cha hewa chafu inayozalishwa viwandani kutokanana matumizi ya nishati kinatoka nchi zilizoendelea wakati Bara la Afrika linazalisha asilimia tatu tu ya hewa hiyo.

"Sisi Afrika tunapaswa tusifiwekwa kupunguza kasi ya ongezeko la jotoduniani.Nchi tajiri zinapaswa kutupongeza kwa sababu bado tuna misitu ambayo inasaidia kunyonya hiyo hewa chafu,"aliongeza.

Waziri Mkuu alisema mkutano huo ni muhimu kwa sababu unaandaa kauli kwa ajili ya Wakuu wa Nchi watakayokwenda kuiwasilisha kwenye Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Kujadili masuala ya Tabianchi utakaofanyika New York, Marekani mwezi ujao.

"Ninatumaini Mawaziri wote watatoka na kauli moja itayowawezesha Wakuu wa Nchi zetu waende na kauli moja. Natumaini watafanikiwa,"alisisitiza Waziri Mkuu.

Akizungumza na washiriki wa mkutano huo kutoka nchi za Algeria,  Jamhuri ya Congo,  Misri, Kenya, Uganda,  Sudan,  Msumbiji, Ethiopia,  Ghana, Mauritania na wenyeji Tanzania,  Waziri Mkuu alisema suala la mabadiliko ya tabianchi yanaziathiri nchi zote duniani bila kujali kipato, umri, mahali nchi ilipo, matabakawala kazi za wananchi.

"Nchi za Afrika ambazo kazi za uchumi wa wananchi wake zinategemea zaidi hali ya hewa, ndizo zinaathirika maradufu zikichangiwa zaidi na kukosekana kwa mbinu za kujihami pamoja na misingi dhaifu ya kiuchumi,"alisema.

Alisema taarifa za hivi karibuni kutoka Intergovernmental Panel on ClimateChange zinaonyesha kwamba kiwango cha utoaji wa hewa chafu kila mwaka kimeongezeka kwa asilimia 2.2huku hewa chafu kutoka viwandani ikiongoza kwa kuchangia asilimia 80 ya hewa hiyo kwenye nchi zilizoendelea.

Mapema, Kamishna wa Umoja wa Afrika anayesimamia Kilimo na Uchumi wa Vijijini, Bibi Rhoda Tumusiime alisema bara la Afrika linapaswa lijipange vizuri na kutoa matamko mazito kwenye mikutano ya kimataifa ili kukemea matumizi matumkzi makubwa ya nishati yanayochangia uharibifu wa mazingira.

"Afrika lazima iendelee kutetea nafasi yake kwenye mikutano hii mikubwa. Lazima itoa kauli nzito kwani kuharibiwa kwa mazingira kunaathiri pia sektanyingine za utalii, maji, nishati na kadhalika,"alisema.

  NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
DAR ES SALAAM.
IJUMAA, AGOSTI29, 2014.

Waziri Mkuu Pinda afungua Mkutano wa mawaziri wa mazingira na mambo ya nje

$
0
0

 Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Peter Pinda (wa pili kulia waliokaa)akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri wa Mazingira na Mambo ya Nje kutoka  Nchi za kamati ya Wakuu wa Nchi za Afrika wakati wa ufunguzi wa mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Peter Pinda( wa pili kulia waliokaa)akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi kutoka  Nchi za kamati ya Wakuu wa Nchi za Afrika wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Mawaziri wa Mazingira na Mambo ya Nje kutoka  Nchi za kamati ya Wakuu wa Nchi za Afrika wenye lengo la  kujadili changamoto za mabadiliko ya tabianchi kwa nchi hizo leo jijini Dar es Salaam.( Picha na Lorietha Laurence-Maelezo)

 Kamishna wa Umoja wa Afrika anayeshughulikia Uchumi Vijijini na Kilimo Roda Tumusiime  akizungumza na wajumbe ambao ni Mawaziri wa Mazingira na Mambo ya Nje kutoka Nchi za kamati ya Wakuu wa Nchi za Afrika wakati wa ufunguzi wa mkutano huo jijini Dar es Salaam   kujadili changamoto za mabadiliko ya tabianchi kwa nchi za Afrika. 
 Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Peter Pinda  ambaye pia ni mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano wa Mawaziri wa Mazingira na Mambo ya Nje kutoka Nchi za kamati ya Wakuu wa Nchi za Afrika akisoma risala ya ufunguzi wa  mkutano huo jijini Dar es Salaam wenye lengo la kupata muongozo wa kujadili changamoto za mabadiliko ya tabianchi kwa nchi za Afrika ili kuwasilisha maazimio hayo katika mkutano unaotarajiwa kufanyika Septemba 23,2014 nchini Marekani.
 Wajumbe wa mkutano wa Mawaziri wa Mazingira na Mambo ya Nje kutoka Nchi za kamati ya Wakuu wa Nchi za Afrika wakifuatilia hotuba zilizokuwa zikitolewa katika mkutano huo leo  jijini Dar es Salaam.

 Waziri wa Maji na Mazingira wa Uganda  Eprahim Kamuntu akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi leo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi rasmi wa mkutano wa siku moja wa Mawaziri wa Mazingira na Mambo ya Nje kutoka Nchi za kamati ya Wakuu wa Nchi za Afrika.
 Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Peter Pinda (katikati) ambaye pia ni mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano wa Mawaziri wa Mazingira na Mambo ya Nje kutoka Nchi za kamati ya Wakuu wa Nchi za Afrika  akifuatilia hotuba zilizokuwa zikitolewa katika mkutano huo leo  jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Kamishna wa Umoja wa Afrikaanayeshughulika  Uchumi wa Vijijini na Kilimo Roda Tumusiime na kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais mazingira Dkt.Bilinilith Mahenge.

TANZANIA YAGUNDUA GESI ASILIA YENYE UJAZO WA TRILIONI 50.5

$
0
0
Na Anitha Jonas – Maelezo.
 
Tanzania imegundua gesi asilia katika maeneo 19  ya mwambao na kina kirefu cha maji baharini ambayo ina ujazo wa trilioni 50.5.

Kati ya maeneo hayo  19 yaligundulika gesi  hiyo ,matano yanapatikana katika mwambao na 14 yapo katika kina kirefu cha maji baharini .

Hata hivyo gesi iliyogundulika katika maeneo ya mwambao kama Songo songo na Mnazi Bay kwa sasa inatumika kufua umeme na pia kwa ajili ya matumizi ya viwandani,majumbani na kwenye magari.

Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa   Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro  wakati akifungua kongamano la wadau wa mafuta na gesi linalofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa huyo amewataka wadau hao watumie muda wao kutoa maoni yatakayosaidia kuwa Sera ya Mafuta na Gesi asilia itakayowanufaisha watanzania pindi itakapoanza kutumika.

Kandoro ameongeza kuwa ni vema Sera hiyo ikasaidia Serikali kupata mapato yake yatakayotokana na Mafuta na Gesi asilia kwa ajili ya kuleata maendeleo mbalimbali kwa manufaa ya wananchi wake.

“Uandaaji wa sera hii ulipitia marejeo ya  nyaraka mbalimbali  ikiwemo sera ya petroli za nchi zilizogundua nishati ya  mafuta na gesi asilia zikiwemo Uganda,Ghana,Sierra Leone na Pakistani”.

Mpaka Oktoba mwaka jana (2013) Serikali ilikuwa imekamilisha sera ya gesi asilia ,hii ni kwa ajili ya kutoa muongozo wa kusimamia na kuendesha biashara ya gesi  asilia katika uchakataji,usafirishaji  na usambazaji”, alisema Kandoro.

Amesema  kuwa  Sera hiyo itazingatia na kuangalia kwa ukaribu suala la udhibiti wa mazingira ukomo wa uzalishaji wa rasilimali hiyo pale utakapoanza.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Jiolojia kutoka  Wizara ya Nishati na Madini Adam  Zuberi amesema lengo la sera hiyo ni kuhakikisha rasilimali ya gesi asilia inawanufaisha watanzania wote kwa  mapato yatakayopatikana katika maeneo husika  kwani asilimia 3 itabaki Halmashauri kwa  matumizi ya wananchi.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF),Prof. Ibrahim Lipumba  ameishauri Serikali kuwa makini katika makubaliano na makampuni yatakayochimba gesi katika mgawanyo wa mapato kama inavyoonyesha katika sera kuwa asilimia 60 ya mapato itapelekwa  Serikalini. Pia  umakini na uangalifu wa hali ya juu unahitajika kwenye makubaliano hayo.

Mkutano huo wa wa siku moja uliandaliwa na wizara ya Nishati na Madini na kujumuisha  wataalam mbalimbali waliobobea katika masuala ya mafuta ,wawakilishi wa ofisi za ubalozi zilizopo nchini ,Vyama vya siasa , viongozi wa dini, Wakuu wa Mikoa  na asasi za kiraia .

RAIS KIKWETE ATEMBELEA SOKO LA NAFAKA LA KIMATAIFA LA KIBAIGWA, DODOMA

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembelea soko la nafaka la kimataifa la Kibaigwa mkoani Dodoma katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani humo Agosti 28, 2014 , ambapo alijionea shehena kubwa sana ya mahindi iliyoletwa kutoka mashambani na kusafirishwa kila pembe ya nchi. Mwaka huu, kama ilivyokuwa mwaka jana, mavuno ya mahindi yamekuwa makubwa kiasi hata cha kupatikana kwa mavuno ya ziada yanayolemea maghala yaliyopo, ikiwa ni muendelezo wa mafanikio ya sera ya kilimo kwanza ambayo imekuwa ikileta matokeo mazuri kila mwaka.PICHA NA IKULU.
 

NSSF YASHIRIKI MAONYESHO YA WAJASIRIAMALI KANDA YA KATI

$
0
0
Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Kigoma, Josephat Komba akimuelezea Mgeni Rasmi, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene huduma mbalimbali zitolewazo na NSSF kwenye banda lao wakati wa maonesho ya wajasiriamali Kanda ya Kati.
 Banda la NSSF linavyooneka kwenye maonesho ya Wajasiriamali wa Kanda ya Kati yanayofanyika 
 Maofisa wa NSSF walioshiriki Kwenye Maonesho ya wajasiriamali kanda ya Kati wakiwa na Meneja wa 
Daktari wa NSSF akimpima Shinikizo la Damu Afisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF ,Theopista Muheta wakati wa maonesho ya wajasiriamali kanda ya kati.
Mmoja ya Washiriki wa Maonesho ya Wajasiliamali Kanda ya kati akipima uzito tayari kupewa Ushauri juu ya uwiano wa uzito wake na urefu (BMI) na Daktari wa NSSF.
 Wakazi wa Mkoa wa Kigoma wakipata maelekezo ya Mafao yatolewayo na NSSF kwa wanachama wa Hiari na wasio wa Hiari.

Bodi ya ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) yatembelea Eneo la Mradi wa Ujenzi wa Bwawa la Maji Kidunda

$
0
0

 
Meneja Usimamizi, Uendeshaji na Mazingira toka Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) Bi.Modesta Mushi akiwaonesha wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) ramani ya maeneo yatakayoguswa na Ujenzi wa Mradi wa Bwawa la Kidunda lenye ujazo wa Mita milioni 190, wakati wa Ziara ya Bodi hiyo katika eneo la Mradi Mkoani Morogoro.
Mkuu wa Msafara wa Timu ya Ulipaji fidia kwa Wakazi walio katika Eneo la Mradi Mhandisi John Kirecha akitoa maelezo kwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) (Hawapo pichani)kuhusu kukamilika kwa taratibu za ulipaji fidia kwa wakazi waliopisha ujenzi wa mradi wa bwana la Kidunda litakaloweza kutoka huduma kwa mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro, wakati wa Ziara ya Bodi hiyo katika eneo la Mradi Mkoani Morogoro.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) Alhaji Said El-Maamry akimueleza jambo Mkuu wa Msafara wa Timu ya Ulipaji fidia kwa Wakazi walio katika Eneo la Mradi Mhandisi John Kirecha ikiwemo kuhakikisha taratibu hizo haziathiri maendeleo ya ujenzi wa mradi huo,ikiwamo kuwataka wakazi wenye matatizo ya Mirathi kuyamaliza ndipo waweze kupatiwa fidia zao.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) Bw. Archard Mtalemwa (katikati mwenye shati jeupe)  akiwaonesha Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) Ramani ya Viwanja 1000 vilivyopimwa  vya Makazi mapya eneo la Bwira juu kwa wakazi 2068 waliopisha Mradi wa  ujenzi wa Bwawa la Kidunda, wakati wa Ziara ya Bodi hiyo katika eneo la Mradi huo Mkoani Morogoro.
Msimamizi wa  Kitengo cha Usimamizi na Upimaji Ramani wa Wilaya Mkoani Morogoro Bw. Kitomaga Francis(aliyevaa Kaunda suti)  akiwaeleza Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) mgawanyiko wa matumizi wa viwanja hivyo ikiwamo kwa ujenzi wa shule, makazi, Hospitali, Polisi, Ofisi na huduma nyingine muhimu za jamii, wakati wa Ziara ya Bodi hiyo katika eneo la Mradi huo Mkoani Morogoro.
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) wakiondoka eneo la Bwira Juu , eneo lililotegwa kwa ajili ya makazi mapya kwa wananchi waliopisha ujenzi wa Mradi wa Bwawa la Kidunga, wakati wa Ziara ya Bodi hiyo katika eneo la Mradi huo Mkoani Morogoro.
 (Picha na Hassan Silayo)

RAIS KIKWETE AZINDUA UJENZI WA DARAJA LA GULWE MPWAPWA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakwanza kushoto  akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Mbunge wa Mpwapwa Mheshimiwa Gregory Teu pamoja na Mbunge wa Kibakwe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa George Simbachawene, akiweka jiwe la msingi kama ishara ya kuzindua rasmi ujenzi wa Daraja la Mto Gulwe lenye urefu wa mita 170 litakalo unganisha kati ya Wilaya ya Mpwapwa na Kibakwe.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglicana Tanzania Jacob Chimeleja, Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi, Mbunge wa Mpwapwa Mheshimiwa Gregory Teu, Mbunge wa Kibakwe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa George Simbachawene pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe,  akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi ujenzi wa Daraja la Mto Gulwe lenye urefu wa mita 170.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete  akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wakiwa katika picha ya  pamoja na Mkandarasi,viongozi wa dini na kitaifa mara baada ya Rais kuzindua rasmi ujenzi wa daraja la Gulwe.
 Daraja la Gulwe linalotumika sasa kama linavyoonekana hali iliyopelekea Serikali ya awamu ya nne kupitia Wizara ya Ujenzi kuanza kujenga daraja kubwa na la kisasa la Gulwe litakalokuwa na mita 170 mara baada ya kukamilika kwake.


 Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo wakati akipita mbele ya Mitambo itakayotumika katika ujenzi wa Daraja la Gulwe lenye urefu wa Mita 170.
 Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wapili kutoka kulia akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe wakwanza kulia, Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi ERB Profesa Ninatubu Lema watatu kutoka kulia pamoja na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale wakifatilia ngoma za asili kabla ya uzinduzi rasmi wa Daraja la Gulwe
 Ujenzi wa Makalvati yatakayosaidia Daraja kupitisha maji katika mto Gulwe kama yanavyoonekana. Jumla ya Makalvati tisa yatajengwa katika daraja hilo la mita 170.
 Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ili kuweka jiwe la msingi kuashiria uzinduzi rasmi ujenzi wa Daraja la Gulwe lenye urefu wa mita 170.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) akizungumza na Mbunge wa zamani wa Mpwapwa George Malima Lubeleje kabla ya uzinduzi rasmi wa ujenzi wa Daraja la Gulwe lenye urefu wa mita 170.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe wakwanza kulia akiwatambulisha Wakurugenzi, Wenyeviti, Wakuu wa Taasisi zilizochini ya Wizara ya Ujenzi kabla ya uzinduzi rasmi wa ujenzi wa Daraja la Gulwe litakalokuwa na mita 170.
=====  ========

Jiwe la msingi daraja la Gulwe-Wilayani Mpwapwa.

Rais Jakaya Kikwete amesisitiza kuwa ujenzi wa daraja la Gulwe katika mto Sinyasungwi ni mwanzo wa ujenzi wa barabara ya Mbande-Kongwa-Mpwapwa-Kibakwe yenye urefu wa kilomita 101, kwa kiwango cha lami.

Akiweka jiwe la msingi na kuzindua ujenzi wa daraja hilo lenye urefu wa mita 170 na uwezo wa kupitisha tani 150 rais kikwete amesema daraja hilo licha ya kuunganisha jimbo la Mpwapwa na Kibakwe pia litamaliza kero ya muda mrefu iliyokuwa ikiathiri barabara na reli katika eneo la Gulwe na Godegode wilayani Mpwapwa.

“Kukamilika kwa daraja hili itakuwa jawabu la kudumu kwa reli na barabara katika eneo la Gulwe na hivyo kazi yenu sasa ni kutunza mazingira ili maji yafuate mkondo na hivyo kutoathiri miundombinu na mashamba ili kukuza shughuli za kilimo”,amesisitiza Rais Kikwete.

Naye Waziri wa ujenzi Dkt. John Magufuli amezungumzia umuhimu wa halmashauri nchini ikiwemo ya Mpwapwa kutumia fedha za mfuko wa barabara kujenga barabara zake kwa kiwango cha lami ili kuboresha miundombinu ya miji na kuwataka wananchi kuacha kuchimba mchanga karibu na madaraja na barabara ili kulinda miundombinu hiyo na kuiwezesha kudumu kwa muda mrefu.

Dkt. Magufuli amesema ujenzi wa barabara ya Mbande-Kongwa-Mpwapwa-Kibakwe hadi Chipogoro yenye urefu wa kilomita 120, utafanyika kwa awamu tatu ambazo ni Mbande-Kongwa-Mpwapwa, Mpwapwa-Kibakwe na Kibakwe-Chipogoro ili kuiunganisha barabara hiyo na ile ya tanzam na hivyo kuiunganisha wilaya ya Mpwapwa na kupunguza magari yaendayo Morogoro na Dare s salaam kupitia Dodoma.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa barabara nchini (TANROADS), mhandisi Patrick Mfugale amesema ujenzi wa daraja la Gulwe lenye urefu wa mita 170 utahusisha ujenzi wa makalvati 9 yatakayosaidiana na daraja kupitisha maji na barabara ya kilomita 1.5 kila upande wa daraja na linatarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi bilioni 3.3 litakapokamilika na litakuwa na uwezo wa kubeba tani 150 kwa wakati mmoja.
 


RAIS KIKWETE AHITIMISHA ZIARA YA MKOA WA MOROGORO, AFANYA MAJUMUISHO

$
0
0
Rais Kikwete akiongoza kikao cha majumuisho baada ya kutembekea Mkoa wa Morogoro
Rais Kikwete akiongea kwenye kikao hicho. Kulia ni Mbunge wa Mvomero na Naibu Waziri wa Maji Mhe Amos Makalla akifuatiwa na Mbunge wa Morogoro kusini ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo Mh Innocent Kalogeris.
Watendaji wa kada mbalimbali wa mkoa wa Morogoro katika kikao hicho cha majumuisho.
Sehemu ya Wabunge wa mkoa wa Morogoro kwenye kikao hicho
Wabunge wa mkoa wa Morogoro kikaoni hapo
Watendaji wa mkoa wa Morogoro wakiwa kikaoni
Mmoja wa wajumbe wa kikao akielezea jambo 
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Joel Bendera akimshukuru Rais Kikwete kwa kufanya ziara mkoani mwake
Mkuu wa Mkoa wa Mororogo akielezwa jambo na Katibu Tawala wa Mkoa huo Mhe  Eliya Ntandu
Rais Kikwete akimsikiliza Mbunge wa Mvomero Mhe. Amos Makalla wakati wa kikao hicho. Katikati ni Mbunge wa Morogoro kusini ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo Mh Innocent Kalogeris

Rais Kikwete akiongea na  Mbunge wa Mvomero Mhe. Amos Makalla

Rais Kikwete akitoka nje ya ukumbi baada ya kuhitimisha kikao cha majumuisho
Rais Kikwete akiagana na Mbunge wa Mvomero Mhe. Amos Makalla
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mbunge wa Morogoro kusini ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo Mh Innocent Kalogeris  alipowasili katika ukumbi wa shule ya msingi Gairo ya kwenye kikao cha majumuisho na watendaji wa mkoa huo baada ya kuhitimisha ziara yake ya mkoa wa Morogoro
Rais Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Mvomero na Naibu Waziri wa Maji Mhe Amos Makalla
Rais Kikwete akiwashukuru wafadhili wa miradi ya afya ya mama na mtoto mkoani Morogoro.

UJENZI NA UPANUZI WA BARABARA ENEO LA KOROGWE-MOMBO UKIENDELEA KWA KASI.

Mwanahabari Salum Mwalim ajitosa uchaguzi Chadema, Atangaza kugombea ujumbe wa kamati kuu kupitia Zanzibar

$
0
0
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la CHADEMA Zanzibar Bi Maryam Ahmed Omar akimkabidhi fomu Salum Mwalim fomu ya kugombea nafasi ya Ujumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho kundi la Zanzibar katika hafla fupi iliyofanyika ofisi Kuu za Chadema kisiwani humo.  
Mmoja wa wachama wa CHADEMA Zanzibar Bikwao Khamis akitia saini ya fomu ya udhamini wa Salum Mwalim (aliyesimama wa kwanza kushoto) anaegombea nafasi ya Ujumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho kundi la Zanzibar. Mwalim alichukua na kurudisha fomu hiyo Jumamosi Agosti 30, 2014 katika Ofisi za Chadema Zanzibar. (Picha zote na Martin Kabemba).
Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar Jumbe Idrisa akitia saini ya fomu ya udhamini wa Salum Mwalim (aliyesimama wa kwanza kushoto) anaegombea nafasi ya Ujumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho kundi la Zanzibar. Mwalim alichukua na kurudisha fomu hiyoJumamosiAgosti 30, 2014 katika Ofisi za Chadema Zanzibar.
Mbunge wa CAHDEMA viti Maalum wa CHADEMA Mwanamrisho Abama akimdhamini Mgombe Ujumbe wa Kamati Kuu wa Chama hicho Salum Mwalim katika ofisi za chama Zanzaibar. Mwalim alichukua na kurudisha fomu hiyo Jumamosi Agosti 30, 2014 katika Ofisiza Chadema Zanzibar.
Salum Mwalim anaewania nafasi ya ujumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA kundi la Zanzibar akitia saini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi Kuu za chama hicho Zanzibar kwa lengo la kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo.

Na Martin Kabemba, Zanzibar

Mmoja wa wanahabari na mtangazaji mahiri wa wakati huu Salum Mwalim ameomba kuchaguliwa kuwa mjumbe wa kamati kuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupitia nafasi za Zanzibar,

Uamuzi huo wa Mwalim ambae kwa sasa ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Kampuni ya Vodacom tayari umeibua mjadala Zanzibar na kwamba unatarajiwa kubadili upepo wa uchaguzi wa Chadema Visiwani humo kutokana na ushawishi na mvuto alionao utakaomfanya kukubalika na kuaminika huku akifanya joto la uchaguzi kupanda.

Kwa sasa joto la uchaguzi ndani ya Chadema linaonekana kuwa juu zaidi Tanzania Bara.


Akichukua fomu ya kuomba kugombea kuingia kwenye chombo hicho kikuu cha maamuzi ndani ya Chadema, Mwalim amesema baada ya kushawishiwa na watu wa rika na wa aina mbalimbali kushauriana na makundi mbalimbali amejipima na kuona kuwa anatosha katika nafasi hiyo.

Mwalim amesema wakati wote wa maisha yake amekuwa akitembea na uzanzibari wake na kwamba alitambua kuwa siku moja atakuja kuwatumikia wazanzibar na hivyo kutoa mchango wake katika maendeleo ya visiwa hivyo ambako ndiko asili yake ilipo.

Mwalim amechukulia fomu hiyo mapema leo (Jumamosi Agosti 30) katika ofisi kuu za Chadema Zanzibar na kuirudisha majira ya mchana ikiwa leo ndio siku ya mwisho ya uchukuaji wa fomu na urejeshaji kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho,

"Nimechukua fomu na sasa nairudisha, kwa kuwa wakati wa kampeni bado sitoweza kuzungumza wala kujinadi naomba niheshimu taratibu na miongozo ya uchaguzi ya chama lakini nataka kuwaambia kuwa Zanzibar na U-zanzibari wangu ni jambo ninalojivunia kuliko kitu kingine chochote maishani mwangu."Alisema Mwalim 


"Ni uamuzi mgumu sana kuwahi kufanya katika maisha yangu lakini nimeufanya kwa kuzingatia masilahi mapana ya chama ninachokiamini na kwa nchi yangu ya Zanzibar na watanzania kwa ujumla,ninamuomba Mwenyezi Mungu anisimamie anipe nguvu,afya,hekima,busara, unyenyekevu na uadilifu katika safari hii ya siasa ninayoianza." Aliongeza Mwalim

Akiongea kwa kujiamini na kwa umakini mkubwa, amesema ana imani kubwa kuwa ataungwa mkono na kushinda nafasi hiyo kwa kuwa pande zote mbili za Visiwani na Bara wanamfahamu vizuri sana na wanatambua mchango wake kwa Chadema na kwa nchi kwa ujumla.

Mwalim ambae ni msomi wa masuala ya uandishi wa habari na mwenye shahada ya uzamii katika usimamizi wa Biashara ni mmoja wa vijana waliotokea kujizolea umashuhuri mkubwa nchini kutoka na uwezo wake na uchapaji kazi wake akiwa mtu mwenye misimamo na kukubalika hasa na vijana nchini.

Kamati kuu ya Chadema ndicho chombo kikuu cha maamuzi ndani ya Chama hicho, na iwapo Mwalim atafanikiwa kushinda na kuingia kwenye chombo hicho anatabiriwa kuwa atabadili upepo wa Chadema katika siasa za Zanzibar kutokana na Mwanahabari huyo kukubalika katika jamii na upya wake katika siasa unamfanya kuingia katika siasa pasi na kuwa na makundi hali itakayomwezesha kupewa ushirikiano na kila mtu ndani na nje ya Zanzibar.
Akimkabidhi fomu hiyo Makamu Mwenyekiti wa Zanzibar wa Baraza la Wazee La Chadema Bi Maryam Ahmed Omar amempongeza Mwalim kwa uamuzi wake huo na kumtakia kila la kheri katika uchaguzi huo.

Bi Omar amesema Chadema ya sasa imeimarika kwa kiwango cha juu na kwamba uamuzi wa Mwalim ambae ni kijana mzaliwa wa visiwani humo wa kuamua kugombea nafasi hiyo utasaidia kuongeza nguvu ya kukiimarisha chama.

Tukio la uchukuaji wa Fomu wa Mwalim limehudhuriwa pia na Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Mjini Magharibi Idrisa Jumbe, mbunge wa wa viti maalum wa chama hicho Mwanamrisho Abama miongoni mwa viongozi na makada mbalimbali wa chama hicho 

WAFANYE WATABASAMU NA UJUMBE MUHIMU

NI LEO FAINALI YA TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT) NDANI YA MLIMANI CITY + MWALIKO KWENU WADAU

WAZIRI MKUU PINDA ASISITIZA UMOJA KWA MAJESHI YA EAC.

$
0
0
*Afunga michezo ya majeshi Afrika Mashariki

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema majeshi ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki hayana budi kuendeleza umoja na mshikamano ili kukuza udugu uliopo.

Ametoa kauli hiyo jana usiku (Ijumaa, Agosti 29, 2014) wakati akifunga mashindano ya Michezo ya Majeshi ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwenye Uwanja wa Amaan, mjini Zanzibar.

Waziri Mkuu ambaye kabla ya kuhutubia umati ulioshiriki hafla hiyo, alikabidhi kombe kwa washindi wa soka, ambao ni timu ya Jeshi la Ulinzi la Kenya, alisema amefarijika kwa jinsi alivyoshuhudia mechi kati ya Tanzania na Uganda ikichezwa kwa staha bila vurugu zozote. Katika mechi hiyo, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 na kuifanya Tanzania iibuke mshindi wa pili kwenye mchezo wa soka na Uganda kushika nafasi ya tatu.

“Michezo siyo chuki bali hujenga uelewano na mshikamano. Ni fursa ya kujenga mahusiano ya baadaye kwani hakuna ajuaye, huenda tukawa na jeshi moja la Jumuiya huko mbele,” alisema.

Alisema kutokana na ustadi ulioonyeshwa na wachezaji, wakuu wa majeshi waangalie uwezekano wa kutafuta mechi na jumuiya nyingine za Afrika Magharibi ama Afrika Kaskazini ili kujipima kwa kiwango kikubwa zaidi badala ya wao kwa wao. “Tujaribu kwenda nje ya Jumuiya yetu tukashindane nao kwa sababu nimeona uwezo mnao,” alisema.

Katika mashindano hayo yaliyoanza Agosti 19, 2014, Kenya iliibuka mshindi katika soka, Tanzania iliibuka mshindi kwenye Netiboli, Uganda kwenye mpira wa vikapu na Kenya ikashinda tena kwenye mpira wa mikono. Katika riadha, Tanzania ilishinda upande wa wanaume na Kenya ilishinda upande wa wanawake.

Michuano hiyo ambayo imefanyika kwa miaka minane mfululizo katika nchi wanachama, mwaka kesho, imepangwa kufanyika nchini Uganda.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3012,
DAR ES SALAAM.
JUMAMOSI, AGOSTI 30, 2014.
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live


Latest Images