Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 351 | 352 | (Page 353) | 354 | 355 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Meneja msaidizi  wa bia ya castle lite Victoria Kimaro kushoto akizungungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam alipokuwa akiwatangaza washindi sita wa wiki ya kwanza katika shindano la promosheni ya Castle lite Yacht Party ambapo baadae watapatikana washindi watakaojishindia zawadi kubwa ya kushiriki katika burudani itakayofanyika katika kisiwa kwenye Bahari ya Hindi na kulia kwake ni meneja wa bia hiyo Geoffray Makau.
  Sehemu ya waandishi mbalimbali wa vyombo vya habari wakiwa katika mkutano wa waandishi wa habari kwenye kutangazwa kwa washindi sita wawiki ya kwanza ambao walishiriki katika shindano kubwa la promosheni ya Castle lite Yachy Party jijini Dar Es Salaam.

  0 0

   wasanii wa bendi ya fm Academia wakiwa jukwaani wanaimba wapili kulia ni Rais wa bendi Nyoshi
  Rapa wa bendi  ya Fm Academia akiwa anashambulia jukwaa wakati wa shoo.
  wanenguaji wa bendi ya Fm wakiwa kazini  wote hawa watakuwepo katika  uzinduzi huu wa Albamu ya Chuki ya nini usikose ni balaa
  Fm  Academia baada ya kukaa kwa muda wa miaka 4 (minne) yaani kuanzia mwaka 2010 mpaka 2013 sasa wanatarajia kuzindua rasmi  album mpya kabisa inayojulikana kwa jina la Chuki ya nini ndani ya jiji la Arusha na vitongoji vyake .

   Album ya chuki ya nini imebeba nyimbo kumi ndani yake,nazo ni:-Chuki ya nini, Fataki ,Otilia ,Ndoa ya kisasa,Neema,Dai chako  ulaumiwe,Maisha,Madudu,Miraessa.album ya chuki ya nini ni album yenye kiwango cha kimataifa ambapo nyimbo hizi zote zitazinduliwa rasmi septembar tano mwaka huu ndani ya viwanja vya  ukumbi wa Triple A jijini Arusha

  Akizungumza na waandishi  wa habari jijini hapa mkurugenzi wa SB Intamenti Seif Manyota alisema kuwa bendi hiyo inatarajia kutua jijini Arusha kwa kishindo kwa ajili ya uzinduzi huu wa albamu mpya ambapo alibainisha kua tukio hilo litakuwa la kihistoria.

  Alisema kuwa  hii ni mara ya kwanza kwa bendi hii  kuzindua albamu  nje ya mkoa wa dar es salaam na kwa hivyo wameamua kuwapa heshima kubwa wapenzi wa bendi hiyo wa mkoa wa Arusha  pamoja na mikoa ya kanda ya kaskazini kwa ujumla hii ikiwa ni heshima ya kipekee.

  "uzinduzi huu wa  albamu sio tu tunazindua  nyimbo mpya bali tunazindua pia vyombo vipya na staili mpya za kuicheza gwasuma kama vile mnavyojua bendi ya fm  ni wazee wa pamba wazee wa kushambulia jukwaa"alisema Manyota

  Aidha alibainisha kuwa kwa mkoa wa Arusha wameamua kuwapa kipaumbele na pia kwakuwa kunawapenzi wengi wa ngwasuma wameamua kufanya shoo hii nje ambapo ,kutafugwa jukwaa la kisasa  kabisa.

  Alitaja baadhi ya nyimbo ambazo zipo katika albamu ambayo inazinduliwa kuwa ni pamoja na Chuki ya nini,ndoa ya kisasa fataki  pamoja na nyinginezo.

  Aidha kwa upande  mungine alisema uzinduzi huu autaishia Arusha tu bali wakazi wa Moshi na Tanga nao watapata burudani hii na kuzitambua staili mpya pamoja na nyimbo mpya zilizopo kwenye albamu hii.

  Alisema kua pia kutakuwa na CD na DVD za albamu hiyo mpya iliyozinduliwa huku akisema kuwa kwa upande wa Arusha kiingili    akuwa 20000 na unapatiwa CD moja buru mlangoni.

  kwa upande wa Rais wa bendi hiyo Nyoshi alisema kuwa timu  yake yote imejipanga vyema kuwapa burudani ya nguvu wakazi wa Arusha  na kuwapa staili mpya ikiwemo ile ya vundesa  ambapo alisema kuwa wameiboresha na imekuwa ya kiufasaha  zaidi  na ina vinjonjo vingi zaidi ,staili tamu  pamoja na maneno matamu.
  Alisema kuwa lengola kubwa la kuzindua albaimu hii apa jijini Arusha ni pamoja na kuwaelewesha wapenzi wao nyimbo mpya na kuakikisha wapenzi wao wanajua staili zao zote za  nyimbo hizo na  sio ivyo tu pia alisema kuwa kwa kipindi  hiki wanataka kuwa wakazi wa arusha zawadi ya kuwaletea wasanii wote wa bendi hiyo ambapo alisema wapo 32  na wote watafika jijini Arusha

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Bukoba,Mh. Zipora Pangani akikata utepe kuashiria ufunguzi wa duka jipya la Airtel mkoani Bukoba jana, anaefuata ni Mkurugenzi wa huduma kwa wateja Bi Adriana Lyamba (suti nyeusi) na watoa huduma wa duka hilo mkoani hapo wakishudia, duka hilo litakalohudumia wakazi wa mkoa wa Kagera .
  Mkuu wa Wilaya ya Bukoba,Mh. Zipora Pangani akiongea na wananchi na wanahabari waliohudhuria uzinduzi wa duka jipya la Airtel mkoani Bukoba jana, kulia ni Mkurugenzi wa huduma kwa wateja Bi Adriana Lyamba (suti nyeusi) pamoja na watoa huduma wa duka hilo mkoani hapo wakishudia, duka hilo litakalohudumia wakazi wa mkoa wa Kagera .
  Mkurugenzi wa huduma kwa wateja Bi Adriana Lyamba (kushoto) akimuelezwa jambo Mkuu wa Wilaya ya Bukoba,Mh. Zipora Pangani mara baada ya ufunguzi wa duka jipya la Airtel mkoani Bukoba jana.
  Mkuu wa Wilaya ya Bukoba,Mh. Zipora Pangani (kati) akikata keki maalum iliyoandaliwa na wafanyakazi wa Airtel huduma kwa wateja Bukoba kwaajili ya hafla ya kusheherekea ufunguzi wa duka jipya la Airtel mkoani hapo. Wakwanza kushoto akishuhudia ni Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa Airtel Tanzania Bi Adriana Lyamba na meneja wa duka hilo bukoba bi Anna Mapunda, duka hilo litakalohudumia wakazi wa mkoa wa Kagera .
  Picha ya pamoja.

  =======  ======  =========
  MKUU wa Wilaya ya Bukoba, Mkoani Kagera Bi. Zipora Pangani ameipongeza Kampuni ya Simu za Mkononi Airtel kwa kufungua duka kubwa, ambalo litatoa huduma mbalimbali kwa wateja ikiwemo kutuma na kutoa fedha ya (AIRTEL MONEY).

  Akifungua duka hilo lililopo eneo la Mtaa wa Kawawa Mjini Bukoba, alisema litakuwani chachu ya maendeleo, kwa wakazi wa mkoani Kagera ambapo litarahisisha huduma kwa wananachi.

  “Ufunguzi wa hili duka hapa kwetu litakuwa ni chachu ya maendeleo kwa wateja wa Air tel na wananchi kwa ujumla hasa kwenye matumizi ya huu mfumo wa air tell money” Alisema Mkuu huyo wa Wilaya.

  Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka wakazi wa kagera na maeneo jirani kuhakikisha kwamba wanaitumia hiyo fursa vizuri ili kuhakikisha wanakuza uchumi wao katika ngazi ya familia na taifa kwa ujumla.

  Naye Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel Tanzania alisema ufunguzi wa duka hilo ni mwendelezo wa ufunguzi wa maduka mengine nchi nzima ili kutoa huduma bora kwa wateja wake.

  “ Kampuni yetu ya Airtel tuna mpango madhubuti wakuhakikisha maduka yetu yote yanakuwa na mwonekano sawa na kutoa huduma bora zenye kiwango cha hali ya juu kwa wateja wetu kutokana na mahitaji yao” Aliongeza

  “ Dhamira yetu ni kuhakikisha tunaendeana na kasi ya uhutaji kwa wateja wetu kwenye mawasiliano ya kisasa na teknolojia, ya hali ya juu” Alisema Mkurugenzi huyo.

  Kwa Upande wao wateja wa kampuni hiyo waliojitambulisha kwa majina ya Joseph Kamuntu na Eradius Ernest wakizungumza mara baada ya kufunguliwa kwa duka hilo waliishikuru kampuni hiyo na kwa kuwasogezea huduma hiyo.

  “ Tunawashukuru sana hawa watu jamani yaani binafsi nimefurahi sana kupata hii huduma karibu sasa hivi wamefungua nimeingia mara moja nimehudumiwa ni mfano wa kuigwa na makampuni mengine,” Alisema Kamuntu.

  Aliyaomba Mkampuni mengine ya simu kuiga mfano wa kampuni ya Airtel kwa kutoa huduma bora ambazo zinamjali mteja ili kuhakikisha maendeleo yanakuwa kwa pande zote.

  Kampuni ya Simu za Mkononi Airtel hadi sasa imefungua maduka 11 hapa nchini katika mikoa ya Dar es salaam, Kagera, Dodoma ,Morogoro, Mtwara, Mbeya, lengo likiw ani kuhakikisha wananachi wanapata huduma bora na kwa wakati.


  0 0
 • 08/28/14--03:19: JIMMY MSAKI OBTUARY
 • Our dear sweet beloved father, son, brother, uncle and friend – JIMMY DIXON RAMMA MSAKI, Three years since you have passed away on August 28, 2011, after a brave difficult fight.

  Our thoughts are ever with you, though you have passed away, and those who loved you dearly are thinking of you today.

  Death separates our bodies, but our hearts remain the same Even after you have left our sight in our thoughts your light shines bright until we meet again.

  “Do not be anxious about anything, but in every situation, by prayer and petition, with thanksgiving, present your requests to God. And the peace of God, which transcends all understanding, will guard your hearts and your minds in Christ Jesus.” Philippians 4:6-7

  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mh. Magreth Malenga akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Gari la Wagonjwa walilokabidhiwa na kampuni ya Biolands , akisaidiwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dkt. Seif Mhina 
   Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mh. Magreth Ester Malenga  akifungua Mlango wa Gari la Wagonjwa Kuashiria Uzinduzi 
  Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mh. Magreth Ester Malenga akiwasha Gari la wagonjwa .
   Meneja wa Biolands Tawi la Kyela Erasto Kilongo akisoma  Risala kwa Mgeni Rasmi kabla ya Makabidhiano ya Gari ya wagonjwa 
   Mwenyekiti wa Bodi ya uhamasishaji wa kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya (HIMSO) Dkt. Charles Mbwanji akitoa salamu za shirika lake katika sherehe za makabidhiano ya Gari 
   Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dkt Seif Mhina akizungumza wakati wa Sherehe za Makabidhiano ya Gari la wagonjwa
   Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Clemence Kasongo akitoa Shukurani kwa niaba ya watumishi wa Halmashauri Baada ya kukabidhiwa msaada wa Gari 
   Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mh. Magreth Ester Malenga akitoa Hotuba yake kwa wageni waalikwa na wananchi wa Wilaya ya Kyela Baada ya Kukabidhiwa msaada wa Gari ya Wagonjwa na Biolands
   Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Gabriel Kipija akitoa shukurani za Halmashauri kwa kampuni ya Bioland baada ya kukabidhiwa Msaada wa Gari la Wagonjwa.
   Meneja Mkuu Msaidizi wa Biolands Felix Mtawa akitoa neno la utangulizi kabla ya Kukabidhi Msaada wa Gari ya Wagonjwa wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela


  Wananchi na Wageni mbalimbali waliohudhuria Sherehe za makabidhiano ya Gari la wagonjwa wakifuatilia kwa makini tukio hilo.
  Jukwaa ambapo sherehe ya Makabidhiano ilifanyika
  Gari la Kubebea wagonjwa likiwa linaingia kwa ajili ya Makabidhiano
  Meza kuu


   Meneja Mkuu msaidizi wa Biolands(Kulia) akimkabidhi na kupongezana  na Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mh. Magreth Ester Malenga ufunguo wa Gari la Wagonjwa katika Sherehe zilizofanyika kwenye viwanja vya Halmashauri ya Wilaya Kyela.


  *****************


  KAMPUNI ya Biolands International Ltd imetoa msaada wa gari ya kubebea wagonjwa (Ambulance) aina ya Nissan Patrol kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela lenye thamani ya shilingi zaidi ya Milion 76.


  Hafla ya makabidhiano ya gari hilo imefanyika  katika viwanja vya Halmashauri hiyo baina ya Mkuu wa Wilaya ya Kyela Magreth Esther Malenga, Meneja wa Bioland Felix Mtawa na Mwenyekiti wa uhamasishaji wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya Afya, Dk.Charles Mbwaji wakishuhudiwa na mganga mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dk. Seif Mhina.


  Katika Risala ya Bioland iliyosomwa na Meneja wa Tawi, Erasto Kilongo, alisema lengo la msaada huo ni kutambua mchango wa wananchi katika maeneo wanayofanya kazi.


  Alisema Bioland ni Kampuni Binafsi inayojishughulisha na ununuzi wa Kakao katika Wilaya za Kyela na Rungwe ambapo   inafanya kazi na na wakulima zaidi ya 20,000 katika vituo 137 vilivyopo katika wilaya hizo mbili.


  Alisema Kampuni hiyo inafanya kazi moja kwa moja na wakulima katika kufanikisha shughuli za vyeti mbalimbali ambavyo vinasaidia kuwepo kwa uhakika wa soko la kakao, vyeti kama vile kilimo hai (organic farming), Kilimo endelevu (Rain forest Allience),na  Usawa wa kibiashara katika jamii (social and Fare Trade).


  Alisema katika sekta ya Afya na usalama wa wazalishaji, Kampuni  imenuia kuhakikisha afya za wakulima na familia zao zinaendelea kuimarika wakati wote na kupata huduma za afya kwa gharama nafuu kupitia mradi wa Bima ya afya ya jamii.


  Alisema  katika kufanikisha mradi huo, Kampuni  ilikubali kutenga kiasi cha dolla 60,000 za kimarekani kwa kipindi cha miaka 5 toka 2010 hadi 2014 kwa ajili ya kutoa ruzuku kwa wakulima wanaojiunga na bima ya afya ya jamii.


  Aliongeza kuwa  Kutokana na umuhimu huu wa kuhakikasha afya za wakulima na familia zao zinaimarika pia Biolands imefadhili ununuzi wa gari la wagonjwa (Ambulance)  lenye thamani  Shilingi Milioni 76,140,000/=, ambalo  limekabidhiwa kwa Halmashauri kwa niaba ya CHIF, HIMSO, CIDR na wananchi wa Kyela.


  Awali akitoa salamu kwa niaba ya HIMSO, Dk. Charles Mwanji, alisema kazi ya HIMSO ambalo ni shirika lisilokuwa la kiserikali ni kuhakikisha wananchi wanajiunga na mfuko wa jamii na kupata huduma ipasavyo.


  Alisema moja ya majukumu yao ilikuwa ni kuwahamasisha Bioland kununua gari la wagonjwa kutokana na umuhimu kwa Wananchi wa Kyela ili waweze kupata huduma za mfuko wa bima kiufasaha.


  Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dk. Seif Mhina, alisema Kazi ya Bioland na HIMSO ilikuwa ni kutoa gari hivyo Halmashauri ihakikishe gari linatumika katika shughuli iliyokusudiwa.


  Alisema ili hayo yakamilike ni bora gari hilo likawa linashindwa kwenye Hospitali ya Wilaya ya Kyela ili kuepuka matumizi tofauti ya gari kama ilivyowahi kutokea kwa magari mengine.


  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kyela ikishukuru kwa niaba ya Wananchi wa Wilaya ya Kyela, alisema Kampuni hiyo imemaliza kilio cha Wananchi wa Kyela cha kutaka gari la wagonjwa kilichokuwepo muda mrefu.


  Alisema kupitia hamasa walioonesha Bioland Wilaya yake itaanza kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya afya ili kuhakikisha kila mwananchi anatumia kadi kwenye matibabu.


  Aidha alitoa wito kwa watumishi wa vituo vya Afya na Mahospitali kutoa kipaumbele kwa wagonjwa wenye kadi kuliko wenye fedha mkononi ili wapate tiba kama serikali ilivyoagiza.

  0 0

   Spika wa Bunge la Tanzania Anne Makinda akihutubia Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) la kwanza kufanyika Dar es Salaam, tangu utaratibu wa kufanyika kwa bunge hilo kwa mzunguko kwa kila nchi mwanachama wa Jumuiya.
   Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Margaret Zziwa akizungumza kwenye ufunguzi wa bunge hilo.
   Spika wa Bunge la Tanzania Anne Makinda (kushoto) akiwa na Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Margaret Zziwa wakati wa ufunguzi wa vikao vya bunge hilo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
   Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Dkt. Abdullah Juma Saadala (wa pili kushoto), akifuatilia ufunguzi wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki.Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki, Phyllis Kandie  (Waziri kutoka Kenya) Shem Bagaine (Waziri kutoka Uganda), Leontine Nzeyimana (Waziri kutoka Burundi), Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Richard Sezibera na kushoto ni Mwanasheria Mkuu wa Jumuiya hiyo  Wilbert Kaahwa.
   Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika  Mashariki (EALA) wakiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge hilo Dkt. Margaret Zziwa (wa nne kutoka kulia waliokaa) na Spika wa Bunge la Tanzania Anne Makinda, mara baada ya ufunguzi wa bunge hilo.
   Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Abdullah Jumaa Saadala akizungumza na waandishi wa habari baada ya ufunguzi wa bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki leo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
  Wabunge wa Tanzania wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki wakifuatilia hutuba ya Spika wa bunge hilo (hayupo pichani) kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo.

  0 0


  0 0

  Na Mwene Said wa Blogu ya Jamii 

   Aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Nchini (TBS), Charles Ekelege amehukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwenda jela miaka mitatu na kuilipa serikali Dola 42,543 za Kimarekani, baada ya kupatikana na hatia ya makosa matatu ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka kwa kutoa asilimia 50.

  Kadhalika, Ekelege anadaiwa kutoa asilimi hiyo ya  punguzo la tozo ya utawala kwa Kampuni mbili  Kampuni ya Jaffar Mohamed Ali Garage na Kampuni Quality Motors na kulisababishia shirika hilo hasara ya dola hizo.

  Hukumu hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi  Augustina Mmbando baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili na mahakama yake kumuona mshtakiwa bila kuacha shaka ana hatia.

  Hakimu alisema ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri ulieleza mahakama kwamba mshtakiwa kupitia wadhifa wake alifanya maamuzi bila kinyume na sheria za TBS zinazomwelekeza kuwasilisha masuala yote ya kiutendaji kwenye Bodi ya Wakurugenzi.

  Alisema kitendo cha kutoa msamaha kwa kampuni hizo bila kuacha shaka moja kwa moja mahakama imeona alitumia madaraka yake vibaya.

  “Kwa upande wa  shitaka la pili, kiongozi yeyote katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anapokuwa madarakani ni kwa ajili ya maslahi ya taifa, lakini mshtakiwa alikosa uzalendo na kutumia madaraka yake vibaya kuhujumu uchumi” alifafanua hakimu kuhusu ushahidi wa Jamhuri.

   “Mahakama inamuona mshtakiwa ana hatia katika kosa hili la pili la kujumu uchumi … pia mshtakiwa amesababisha watanzania waliompa dhamana kukosa kula keki ya taifa lao kwa kujinufaisha yeye binafsi” alisema hakimu huyo na kuongeza kuwa.

  “Katika ushahidi uliotolewa na mshtakiwa alikiri kufanya maamuzi bila kupata baraka na kibali cha Bodi ya Wakurugenzi na kwamba aliidanyanya mahakama” alisema Hakimu Mmbando.

  0 0

   Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje akiwasilisha mada kuhusu Sekta ya Madini – Tanzania kwa Waziri wa Nishati na Migodi wa Burundi, Mhe. Côme Manirakiza (wa kwanza kulia) na Ujumbe wake (Kulia kwake) waliofika Makao Makuu ya Wizara – Dar es Salaam, Agosti 26, 2014 kujifunza namna Sekta za Nishati na Madini zinavyofanya kazi. Upande wa kushoto ni Wataalamu mbalimbali wa Wizara na Taasisi zilizo chini yake.
   Waziri wa Nishati na Migodi wa Burundi Mhe. Côme Manirakiza (aliyeinua mkono), akiomba kupewa ufafanuzi kuhusu sekta ya madini hapa nchini, baada ya uwasilishwaji mada zilizohusu sekta za nishati na madini za Tanzania. Waziri Manirakiza na Ujumbe wake walitembelea Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini -  Dar es Salaam, Agosti 26, 2014 kwa lengo la kujifunza namna sekta husika zinavyofanya kazi. Wengine pichani ni Wataalamu wa Wizara ya Nishati na Madini - Tanzania (kushoto) na Ujumbe ulioongozana na Waziri (Kulia).
   Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), Profesa Abdulkarim Mruma (aliyeinua mikono), akitoa ufafanuzi kuhusu GST kwa Waziri wa Nishati na Migodi wa Burundi, Mhe. Côme Manirakiza (Wa kwanza Kulia) na Ujumbe wake waliofika Makao Makuu ya Wizara - Dar es Salaam, Agosti 26 kujifunza namna Sekta za Nishati na Madini zinavyofanya kazi.
  Mtendaji Mkuu wa Jiolojia na Migodi (Geology and Mines) wa Burundi, Emmanuela Ngenzebihoro (mwenye kilemba) akiuliza swali kwa Wataalamu wa Wizara ya Nishati na Madini – Tanzania (Walioketi Kushoto), wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati na Migodi wa Burundi, Mhe. Côme Manirakiza (Wa kwanza Kulia) na Ujumbe wake Makao Makuu ya Wizara - Dar es Salaam, Agosti 26, 2014. Waziri Manirakiza na Ujumbe wake walifika wizarani kujifunza namna Sekta za Nishati na Madini zinavyofanya kazi.

  ===========  ============  ==========


  Na Veronica Simba
  Waziri wa Nishati na Migodi wa Burundi, Mhe. Côme Manirakiza na Ujumbe wake wako katika ziara ya siku tano (24 – 28 Agosti, 2014) hapa nchini kwa lengo la kujifunza namna Sekta za Nishati na Madini zinavyofanya kazi.

  Katika ziara yake, Waziri Manirakiza ametembelea Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini – Dar es Salaam na kukutana na Wataalamu mbalimbali wa Wizara na Taasisi zilizo chini yake wakiongozwa na Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje.
  Wakiwa Wizarani, Waziri na Ujumbe wake walipata fursa ya kusikiliza mada zinazohusu Sekta za Nishati na Madini zilizowasilishwa na Wataalamu wa Wizara.

  Ujumbe huo pia umepata nafasi kutembelea Taasisi na Mashirika mbalimbali yaliyo chini ya Wizara na yale yenye uhusiano na Wizara ikiwemo Mpango wa Uwazi na Uwajibikaji katika Tasnia ya Uziduaji Tanzania (Tanzania Extractive Industry Transparency Initiative – TEITI), Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasimali Madini (SMMRP) na Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA).

  0 0


  Marais wa Tanzania na Burundi wamewatoa hofu wakazi wa maeneo ya mpakani mwa Tanzania na Burundi kuwa zoezi Uimarishaji wa mpaka wa kimataifa kati ya nchi hizo linalofanywa na wataalam wa upimaji na ramani katika maeneo ya  mipaka ya nchi hizo halilengi kuleta mgawanyiko miongoni mwao bali kuweka utaratibu mzuri wa utambuzi wa alama za mipaka ya kimataifa  na kuwawezesha wananchi wa pande zote kuwa na uhakika wa uhalali wa maeneo wanayoishi.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa kijiji cha Mugikomero wilayani Ngara kwa upande wa Tanzania na Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa uzinduzi wa zoezi uimarishaji wa mpaka kati ya Tanzania na Burundi viongozi hao wamesema kuwa Serikali za nchi zote zimeamua kufanya zoezi hilo kufuatia mabadiliko mbalimbali yaliyojitokeza katika maeneo ya mipaka  ikiwemo alama za  kwanza zilizowekwa na wakoloni mwaka 1924 kuchakaa na nyingine kung’olewa na wananchi kutokana na sababu mbalimbali, ongezeko la watu, shughuli za kiuchumi na baadhi ya maeneo ya mito iliyokuwa ikitenganisha nchi hizo kukauka.

   Rais wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Kikwete akizungumza na wananchi wa vijiji hivyo amesema kuwa kufanyika kwa zoezi hilo kunatokana na agizo la Umoja wa Nchi za Afrika (AU) lilotolewa mwezi June 2007 katika kikao cha wakuu wa nchini za Afrika kilichofanyika Accra, Ghana ambacho kilizitaka nchi zote za Afrika  kuhuisha upya mipaka ifikapo mwaka 2017 ili kuondoa migogoro ya mipaka inayojitokeza.

  Amesema baadhi ya nchi za Afrika zimekuwa katika malumbano na machafuko ya mipaka kutokana na kutokuwa makini katika kuhakiki maeneo ya mipaka na kuongeza kuwa Serikali ya Tanzania itahakikisha kuwa zoezi hilo linaendeshwa kwa ufanisi mkubwa katika maeneo mengine yaliyobaki.

  “ Sisi na Burundi ni ndugu wa damu tumechagua njia ya mazungumzo na kalamu, Marafiki huchora mipaka kwa mazungumzo na kalamu, maadui huchora mipaka kwa nguvu na kwa wino wa damu, mipaka ya kalamu hudumu na hustawisha jamii wakati ile ya damu huleta chuki, hujuma ,dhuluma na kisasi” Amesisitiza.

  Amesema kuwa serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Burundi itahakikisha kuwa eneo lote la mpaka kati ya Tanzania na Burundi lenye urefu wa kilometa 450 katika mikoa ya Kagera na Kigoma linafikiwa licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali na gharama kubwa za kufanikisha zoezi hilo.

  “Maeneo mengi yako msituni, yako kwenye mabonde, mito na ni vigumu kuyafikia,tumeamua kuyagharamia na kufanya wenyewe kwa fedha zetu wenyewe kuonyesha dhamira na utashi wetu kulikamilisha zoezi hilo kabla ya muda uliowekwa ili kuondoa sintofahamu iliyokuwepo” Amesisitiza.

  Amesema kuwa serikali itahakikisha kuwa inatenga fedha za kutosha kukamilisha  zoezi la uwekaji wa alama za mipaka  ili kuwezesha serikali za nchi mbili kuwa na mkataba mpya ambao utafuta mkataba uliowekwa na wakoloni.

  Amewataka wakazi wa maeneo hayo kuwa walinzi wa alama za mipaka na kuepuka kuhujumu zoezi hilo, kulima katika maeneo ya hifadhi kutokana na umuhimu wa alama hizo kimataifa na kwa wakazi wa maeneo husika kwa kuwa zoezi hilo baada ya kukamilika litaondoa mashaka kuhusu uhalali wa maeneo wanayoyamiliki, huduma, shughuli za biashara na ujenzi wa makazi.

  Kwa upande wake Rais wa Burundi Mh. Pierre Nakurunzinza ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kushirikiana na serikali ya Burundi katika kutekeleza majukumu na masuala mbalimbali yenye manufaa kwa wananchi.

  Amesema ushirikiano katika zoezi hilo unaonyesha wazi kuwa Serikali za nchi zote mbili zinafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na kuongeza kuwa kuanza kwa zoezi hilo ni uthibitisho tosha kuwa waafrika wanaweza kufanya mambo yao wenyewe kwa ufanisi mkubwa.

  Amefafanua kuwa Tanzania imefanya mambo mengi sana kwa serikali ya Burundi na hilo linathibitisha dhamira safi na ushirikiano mkubwa tokea wakati wa machafuko na vita iliyotokea nchini Burundi.

  “Serikali ya Tanzania imekuwa bega kwa bega na serikali yetu ya burundi,Tanzania imefanya mambo mengi sana kwa wananchi wa Burundi, iliwahifadhi wananchi wa Burundi wakati wa machafuko,iliwalisha iliwatunza na kuwathamini na zoezi tunalolifanya sasa la kuhakiki mipaka ni dogo sana ikilinganishwa na undugu na umoja wetu” Amesisitiza.

  Amewataka wakazi wa pande zote mbili kuhakikisha kuwa wanatoa ushirikiano kwa wataalamu wa upimaji na ramani wa nchi zote mbili na kuongeza kuwa wananchi wote watakaoathiriwa na zoezi hilo kutokana na kupoteza maeneo yao watalipwa fidia na kutafutiwa maeneo mengine.

  Kwa upande wao mawaziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi wa nchi hizo Prof. Anna Tibaijuka wa Tanzania na Jean Claude Nduwayo wa Burundi wameeleza kuwa zoezi la uhakiki wa mpaka  wenye urefu wa kilometa 450 na alama 58 zilizoanzia Pwani ya Mashariki ya Ziwa Tanganyika hadi Kusini mashariki mwa mto Mwibu lina manufaa makubwa kwa wananchi wan chi zote mbili.

  Wamesema Tanzania na Burundi zimefanya kazi kwa ushirikiano kupitia kamati ya Pamoja ya Ufundi ya Mipaka ya Kimataifa (JTC) amabayo ilitoa maamuzi muhimu ya ufanikishaji wa zoezi hilo ikiwemo uamuzi wa upana wa eneo la wazi la mpakani (buffer zone) kuwa mita 12.5 kila upande wa mpaka, Kuanza kwa kazi ya uimarishaji wa mpaka mwezi Machi mwaka huu pamoja na uratibu wa shughuli ya uzinduzi wa shughuli ya uimarishaji wa mipaka.

  Wamefafanua kuwa uamuzi wa kuimarisha mpaka umetokana na kuwepo kwa ongezeko kubwa la shughuli za kiuchumi katika maeneo ya mpakani, hali ya mabonde na milima iliyopo ya mabonde na milima katika sehemu kubwa ya mipaka inayofanya utambuzi wa mpaka kuwa mgumu kwa wananchi wa kawaida.

  . Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
  28/8/2014, Ngara, Kagera.

   

  0 0

   Ofisa mauzo wa Isere Sports, Rasul Nkusa akionesha aina ya mpira na raba mpya zilizowasili nchini
  Hizi ni baadhi ya truck Suits zilizowasili Isere Sports
  Meneja Masoko wa Isere Sports, Abas Isere akionesha skafu na kofia za bendera ya taifa zilizowasili nchini
  Hizi ni baadhi ya jezi zilizowasili kwa ajili ya kuusambaza kwa wadau wa michezo Tanzania na nje ya nchi kulia ni Ofisa Masoko Msaidizi, Ismail Bura.
   
  ========    ========  =====

  KAMPUNI ya Isere Sports inayoagiza na kuuza vifaa vya michezo nchini imepokea shehena kubwa ya mali mpya ya vifaa vya michezo kutoka Dubai na China.
  Mkurugenzi wa Michezo wa Isere Sports, Abas Isere alisema jana kuwa vifaa hivyo vyenye ubora unaokubalika vimewasili na tayari vimeanza kusambazwa kwenye ofisi zao zilizopo mtaa wa Mchikichi na Living Stone, Karikaoo na jingine la Dodoma.
  Alisema vifaa vilivyowasili ni truck suits za rangi mbalimbali, jezi za mpira wa miguu, netiboli, wavu, basketi ambavyo vyote vinauzwa kwa bei nafuu na kutoa wito kwa maofisa kutoka taasisi mbalimbali za Serikali kutoa oda zao mapema.
  Vifaa vingine vilivyowasili ni matufe, mikuki, visahani, vikombe, mipira ya michezo yote, raba za michezo, viatu vya mpira na vingine vingi ambavyo vinafaa kutumika kwenye mashindano mbalimbali nchini.
   
  Kwa mawasiliano zahusiana na vifaa vya michezo mbalimbali wasiliana na 0713241470

  0 0

  Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Klabu ya Simba, Hans Pope (kulia), akiwa na mshambuliaji raia wa Uganda, Emmanuel Okwi aliyejiunga na klabu hiyo akitokea katika timu ya Yanga baada ya kuvunjwa mkataba wake. Hata hivyo Yanga imemshtaki Okwi kwa Shirikisho la Soka Tanzania.
   Emmanuel Okwi akiwa ameshika jezi namba 25 wakati akitambulishwa kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, jezi hiyo alikuwa akiitumia wakati akiichezea timu hiyo kabla ya kuuzwa kwa klabu ya Etloile Du Sahel ya Tunisia.

  0 0


  0 0

  Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta akiongea na waandishi wa Habari huku akiwaasa kuacha chuki katika masuala yanayohusu mchakato wa Katiba.
  Mjumbe wa Kamati Namba Nne ya Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Christopher Ole Sendeka akiongea na wandishi wa Habari kuhusu kazi na majukumu ya Kamati yake leo 28 Agosti, 2014.
  Mjumbe wa Kamati Namba Tatu ya Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Dkt. Francis Michael akiongea na wandishi wa Habari kuhusu kazi na majukumu ya Kamati yake leo 28 Agosti, 2014.
  Mjumbe wa Kamati Namba Moja ya Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Ummy Mwalimu Ally akiongea na wandishi wa Habari kuhusu kazi na majukumu ya Kamati yake leo 28 Agosti, 2014.
  Mjumbe wa Kamati Namba Kumi na Moja, Mhe. Hamad Massauni akiongea na wandishi wa Habari kuhusu kazi na majukumu ya Kamati yake leo 28 Agosti, 2014. (Picha zote na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma).

  0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais –Mazingira Mh. Dk. Eng. Binilith Satano Mahenge, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam, kuhusu mkutano wa Mawaziri wa Mazingira na Mawaziri wa Mambo ya Nje kutoka nchi za kamati ya wakuu wa nchi utakaofanyika jijini Dar-es -salaam katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere Tarehe 29 Agosti 2014.
   Sehemu ya waandishi wa habari wakisikiliza hotuba inayotolewa na Mheshimiwa Dk. Eng. Binilith Satano Mahenge (hayupo pichani).
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais –Mazingira Mh. Dk. Eng. Binilith Satano Mahenge (kushoto), akiwa pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya makamu wa Rais, Bwana Sazi Saula wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano utakaofanyika jijini Dar es Salaam Tarehe 29 Agosti 2014 .
    =======  =======  =======

  Mheshimiwa Dk. Binilith Mahenge Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira  ametoa rai  kwa Wananchi wa Tanzania na Afrika kwa ujumla kuweka juhudi katika kupambana na changamoto za mabadiliko ya Tabia Nchi..
  Alitoa rai  hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar-es-salaam  kuhusu mkutano wa Mawaziri wa Mazingira na Mambo ya Nje kutoka nchi za kamati ya wakuu wa nchi za Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika jijini Dar-es -salaam katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere Tarehe 29 Agosti 2014.
    Alisema kuwa Tanzania imeandaa mkutano wa Mawaziri wa Mazingira na mambo ya nje kutoka nchi za kamati ya wakuu wa nchi za Afrika kuhusu tabia nchi lengo likiwa ni kutoa mwongozo wa namna ya kushughulikia changamoto na mabadikiko ya tabianchi na namna ambavyo nchi za Afrika zitavyoweza kunufaika na rasilimali zinazotolewa na nchi zilizoendelea ili kukabiliana na mabadiliko hayo.
  Mkutano huo ambao utakuwa ni mwendelezo wa juhudi za viongozi wa Afrika katika kushughulikia na kutoa mwongozo wa namna ya kukabiliana na athari za Mabadiliko ya tabia nchi ambazo zimeendelea kuliathiri Bara la Afrika na Dunia kwa ujumla.
  Anasema kuwa joto la dunia limeongezeka kutokana na kuongezeka kwa gesi joto kama vile hewa ukaa ambayo inatokana na shughuli mbalimbali za uzalishaji na matumizi ya nishati, viwanda na usafirishaji.
  "Mabadiliko haya ya tabianchi yanaathiri zaidi watu ambao ni maskini zaidi na wengi ni wale waishio bara la Afrika.Hivyo basi nchi za Afrika zinahitaji rasilimali fedha za kutosha ili kukabiliana na madhara hayo ambayo yanatokana na Mabadiliko ya tabianchi" Alisema Dk.Mahenge.
  Aliongeza kuwa mkutano huo utajadili zaidi mambo yanayoathiri kwa kiasi kikubwa Mazingira , hivyo utapendekeza masuala muhimu kwa bara la Afrika hasa upatikanaji wa fedha na tekinolojia katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko hayo barani Afrika.

  0 0

  Hivi ndivyo ambavyo Daladala hiyo ilivyojibamiza muda mchache uliopita 
  Askari wa usalama wa Barabarani akiwa anatazama na kuchunguza zaidi ajali hiyo
  Eneo ambalo Daladala hiyo iliyofumuka 

  Viti vikiwa vimeharibika baada ya ajali kutokea 

  Hivi ndivyo Daladala hiyo iliyokuwa ikitoka Mwanjelwa kuja Mbalizi ilivyo  Haribika Baada ya ajali hiyo
  Mashuhuda wakiwa wamelizunguka daladala hiyo kushuhudia kllichotokea 
   Hapa ndipo eneo ambapo ajali imetokea , Askari wa usalama wa barabarani wakiendelea kufuatilia ajali hiyo
   Ilikuwa ni Ajali mbaya 

  Eneo hili la ubavuni ndipo eneo ambalo Daladala hiyo iliingia na Kujigonga 
  Gari hilo aina ya Tata likiwa limepaki pembeni Muda mchache baada ya kupata ajali hiyo
  Mashuhuda 
  Baadhi ya Majeruhi wakiwa wanatolewa katika Hospitali ya Ifisi kuelekea Hospitali ya Rufaa Mbeya 

  WATU kumi wakiwemo watoto wawili wamefariki dunia papo hapo na wengine saba wamejeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha magari mawili.
  Ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa nne asubuhi ikihusisha gari ndogo ya abiria maarufu daladala lenye namba za usajili T 237 BFB aina Toyota Hiace  na gari kubwa aina ya Fuso lenye namba za usajili T 158 CSV.
  Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wamesema ajali hiyo ilitokea maeneo ya Mbalizi baada ya Hiace iliyokuwa ikitokea Mbeya mjini kuelekea Mbalizi kulivaa Fuso ilikuwa ikiingia barabarani.
  Walisema inasemekana dereva wa Hiace gari yake ilimshinda kutokana na kutelemka mlima mkali wa Mbalizi inagawa pia walimtupia lawama dereva wa Fuso ambaye alikuwa akiingia barabarani bila kuchukua tahadhari.
  Muuguzi Mkuu wa Hospitali teule ya Ifisi Mbalizi, Sikitu Mbilinyi, ambako Majeruhi na marehemu walikimbizwa hapo alithibitisha kupokea majeruhi 7 ambapo alisema kati yao ni wanawake 3 na wanaume 4.
  Alisema kati ya majeruhi hao wawili wamepewa rufaa kwenda hospitali ya Rufaa Mbeya kutokana na kuhitaji msaada zaidi huklu wengine wakiendelea kupatiwa msaada wa haraka ili kunusuru hali zao.
  Mbilinyi aliongeza kuwa pia wamepokea miili ya marehemu 10 wakiwemo watoto wawili na Wanawake wanne na Wanaume wanne.
  Hata hivyo majina ya majeruhi na marehemu hayajaweza kupatikana mara moja kutokana na kuwa katika hali mbaya ambapo Dereva wa Fuso akitokomea mara baada ya tukio.
  NA MBEYA YETU BLOG


  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki Mkombozi Commercial, Edwina Lupembe akiongea na waandishi wa habari waliofika katika hafla ya benki hiyo kufikisha miaka mitano tokea imeanzishwa. Aliongeza kuwa benki hiyo ilianzishwa kwa lengo la kutoa huduma za kibenki sanjari na kushughulika na matatizo ya kiuchumi kwa jamii katika nyanja mbalimbali.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Edwina Lupembe akikazi msisitizo mbaye ya waandishi wa habari.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki Mkombozi Commercial, Edwina Lupembe akiwatambulisha mbele ya wageni waalikwa na wafanyakazi, watoto wanaosomeshwa na benki hiyo.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakwanza kushoto akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi pamoja na Mbunge wa Kongwa ambaye pia ni Naibu Spika Job Ndugai wakifurahia mara baada ya Rais kuweka jiwe la Msingi Ujenzi wa Barabara ya Mbande-Kongwa 16.5Km .
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi, Mbunge wa Kongwa ambaye pia ni Naibu Spika Job Ndugai, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Profesa Juma Kapuya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe, akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa barabara ya Mbande-Kongwa 16.5Km.
  Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma pamoja na kikundi cha ngoma za asili cha Kibaigwa kabla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuhutubia mamia ya Wakazi wa Kibaigwa.
  Sehemu ya barabara Mbande-Kongwa 16.5Km ambayo ujenzi wake umewekwa jiwe la Msingi.
  Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kulia akizungumza na Mbunge wa Kibakwe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa George Simbachawene huku Mbunge wa Kongwa ambaye pia ni Naibu Spika Job Ndugai akishuhudia kushoto.
  Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katikati akizungumza na Mbunge wa Kongwa ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Profesa Juma Kapuya(kulia) kabla ya uzinduzi wa barabara ya Mbande-Kongwa 16.5Km.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya uzinduzi na ufunguzi wa barabara ya Mbande-Kongwa 16.5Km.
  Viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Ujenzi pamoja na Taasisi zake wakimsubiri Rais Dkt. Jakaya Kikwete kuzindua rasmi mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Mbande-Kongwa 16.5Km. Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa semina ya siku moja kwa watumishi wa serikali na taasisi zake iliyofanyika jana Agosti 29, 2014 mjini Bagamoyo, mkoa wa Pwani.
   Constatina Martin Meneja Masoko, na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Constatina Martin, akizungumza kwenye semina ya siku moja ya watumishi wa serikali na taasisi zake iliyoandaliwa na Mduko huo mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani, Ijumaa Agosti 29, 2014.
   Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Utumishi, George Yambesi(Wanne kulia waliokaa), na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, (Wanne kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa waandamizi wa Mfuko huo na wafanyakazi wa serikali na taasisi zake, wanaohudhuria semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo ili kuelezea huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko wa PSPFT.
   Mwanaasemina akipitia utaratibu wa semina ya siku moja ya watumishi wa serikali na taasisi zake iliyoandaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani, Agosti 29, 2014.
   Constatina_Kuwite_Muro Mkurugenzi wa Operesheni wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Neema Muro, (Kulia), Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko huo, Constatina Martin ,Katikati) na Meneja Utawala, Neema Kuwite, wakibadilishana mawazo muda mfupi kabla ya mkuanza semina ya siku moja kwa watumishi wa serikali na taasisi zake iliyoandaliwa na Mfuko huo mjini Bagamoyo, mkoa wa Pwani Ijumaa Agosti 29, 2014
   Constantina_Mayingu_Yambesi Meneja Masoko, na Mawasiliano, wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Constatina Martin, (Kushoto), akiwaongoza Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Utumishi, George Yambesi, (Kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Adam Mayingu, kuelekea ukumnbi wa semina ya watumishi wa serikali na taasisi zake mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani, Ijumaa Agosti 29, 2014.


   Mayingu_Yambesi Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi, George Yambesi, (Kulia), akiongozana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, wakati akiwasili kufungua semina ya siku moja ya watumishi wa serikali na taasisi zake mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani Ijumaa Agosti 29, 2014

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Tuguluvala Simbachawene na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, Waziri wa Ujenzi Dk John Pombe Magufuli na Mbunge wa Afrika Mashariki Adam Kimbisa.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishuhudia jiwe la msingi mara baada ya kufungua mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma wanaoshuhudia ni pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Tuguluvala Simbachawene na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu. 

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza wakati akitembelea mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma. Mradi huo una jumla ya nyumba 44.
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza katika hafla hiyo jana
  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai akizungumza katika hafla hiyo jana
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu wakati akitembelea mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma. Mradi huo una jumla ya nyumba 44..

  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Tuguluvala Simbachawene akizungumza wakati akitembelea mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma. Mradi huo una jumla ya nyumba 44.
  Wageni waliokuwapo katika hafla hiyo
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoka ndani ya nyumba ya mfano baada ya kufungua nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma akiwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu, Waziri wa Ujenzi Dk John Pombe Magufuli na Mbunge wa Afrika Mashariki Adam Kimbisa.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Tuguluvala Simbachawene na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, Waziri wa Ujenzi Dk John Pombe Magufuli na Mbunge wa Afrika Mashariki Adam Kimbisa.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa kuashiria ufunguzi mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma wanaoshuhudia ni pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Tuguluvala Simbachawene na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Meneja wa NHC mkoa wa Dodoma Itandula Gambalagi wakati wa ufunguzi wa nyumba hizo za gharama nafuu.
  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Tuguluvala Simbachawene akizungumza na Meneja wa NHC Dodoma Itandula Gambalagi wakati akitembelea mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma. Mradi huo una jumla ya nyumba 44.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na viongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa katika mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma, wakati wa uzinduzi wa mradi huo uliofanyika jjana.
  Msafara wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ukiwasilia katika eneo la tukio.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa katika mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma. (Picha zote kwa hisani ya Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii cha Shirika la Nyumba la Taifa)
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Abdulkarim Shah.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa katika mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikaribishwa katika mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambo na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Tuguluvala Simbachawene katika mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma

  • Imeandikwa tarehe 29 Agosti 2014
  Na Sifa Lubasi, Kongwa


  HALMASHAURI nchini zimetakiwa kununua nyumba za bei nafuu zinazojengwa na Shirika la Nyumba (NHC) ili kuwapangisha watumishi wake.
  Kauli hiyo ilitolewa jana na Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akifungua mradi wa nyumba nafuu katika eneo la Mnyakongo wilayani Kongwa mkoani Dodoma.
  Alisema kumekuwa na tabia ya baadhi ya maeneo watumishi wa halmashauri kukaa mbali na sehemu zao za kazi kwa visingizio vya kukosa makazi.

  Alisema sababu hiyo sasa haina msingi katika maeneo ambayo NHC imejenga nyumba zao kwani halmashauri inaweza kununua nyumba hizo na kuwapangisha watumishi wake. ‘’ Hawa NHC wana utaratibu kwa kupitia mabenki wanayoshirikana nayo hivyo kwa kutumia utaratibu huo halmashuri mnaweza kwenda katika hizo benki na kuingia mkataba na kukopa nyumba hizo na kisa kuwapangisha watumishi…’’ alisema.

  Aidha Rais Kikwete alisema shirika hilo linafanya kazi nzuri katika ujenzi wa nyumba hizo za bei nafuu huku akilitaka kuongeza zaidi idadi ya nyumba. Alisema ni vyema sasa halmashuri zikaongeza maeneo ya kujenga nyumba hizo ili wananchi wengi zaidi waweze kuishi katika nyumba bora.

  Akizungumza katika ufunguzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa NHC Nehemia Mchechu alisema mradi huo ni utekelezaji wa mpango wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu. Alisema mradi huo wenye nyumba 44 hadi kukamilika utakuwa umegharimu Shilingi bilioni 1.2.Alisema nyumba hizo zinauzwa kwa gharama kati ya Sh milioni 35 hadi 40 kulingana na ukubwa wa nyumba husika.

  Hata hivyo alisema bado kuna tatizo la kodi katika uuzaji wa nyumba hizo na ndio kinachofanya kuuzwa kwa bei kubwa. Alimuomba Rais kusaidia katika kusukuma nia ya kushusha kodi ili nyumba hizo ziuzwe kwa bei nafuu na kila mwananchi aweze kununua.

older | 1 | .... | 351 | 352 | (Page 353) | 354 | 355 | .... | 1897 | newer