Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live

KINANA AKUTANA NA VIONGOZI WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI TANZANIA

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania ( TUCTA )Nicholaus Mgaya akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipowasili kwenye Makao Makuu ya TUCTA kwa mazungumzo na Viongozi wa vyama vya wafanyakazi.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Wanawake,Jinsia na Watoto (TUCTA) Siham Ahmed kabla ya kuanza kwa mazungumzo baina ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi.
  Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania ( TUCTA )Nicholaus Mgaya akizungumza wakati wa kikao cha Viongozi wa vyama vya Wafanyakazi na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye ukumbi wa mikutano TUCTA.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumzwa kwenye kikao na Viongozi wa Vyama Vya Wafanyakazi Tanzania.
 Sehemu ya Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi Tanzania wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (TRAWU) Erasto Kihwele akichangia jambo wakati wa kikao hicho.
(Picha na Adam H.Mzee)


Kampuni ya Drive Dentsu yafungua ofisi zake Dar es Salaam.

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Drive Dentsu, Mr Cheriff Tabet (kushoto)akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ofisi yao Dar es Salaam. Kulia kwake ni Meneja Uendelezaji wa Biashara na Masoko Mapya, Rami El Khalil.

Mkurugenzi Mkuu wa Drive Dentsu, Mr Cheriff Tabet (katikati)akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ofisi yao Dar es Salaam. Kulia kwake ni Meneja Uendelezaji wa Biashara na Masoko Mapya, Rami El Khalil, na kushoto ni Meneja Mkuu wa Drive Dentsu Tanzania, Terry Greenwood.


========  ========  ========= 
             
Dar es Salaam, 26-August, 2014: Kampuni ya Drive Dentsu, imefungua ofisi zake mpya jijini Dar es Salaam katika jitihada za kusogeza huduma zake kwa wateja wake katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Ikiwa ni kampuni iliyotanda nchi zaidi ya 110, Drive Dentsu ni sehemu ya muunganiko wa kimataifa wenye zaidi ya wafanyakazi 37000 na ofisi 160 duniani kote, muunganiko ambao unaleta pamoja ujuzi, maarifa na vitendea kazi vyenye kuhakikisha inawapa wateja wake huduma zenye ubora wa hali ya juu.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Bw. Cheriff Tabet, Mkurugenzi Mkuu wa Drive Dentsu, amesema ufunguzi wa ofisi mpya ya Drive Dentsu jijini Dar unalenga kutoa suluhisho la ubunifu kwa makampuni na bidhaa za kitanzania.

Bw. Tabet amesema pamoja na kuwekeza nchini Tanzania, Drive Dentsu imelenga kujipanua katika masoko mengine katika ukanda huu ili kuhakikisha wanakidhi mahitaji yao kwa kutoa suluhu kwa changamoto zote za kibiashara.

 “Katika ukanda wa Afrika Mashariki, uchumi wa Tanzania umekua ukikua kwa kasi kubwa pamoja na ongezeko la uzalishaji wa bidhaa nyingi jambo ambalo linakuza mazingira yenye ushindani hivyo kufanya kuwepo na uhitaji mkubwa wa ubunifu katika kuwafikia wateja’  anasema Bwana Tabet.

Tabet pia anasema kuwa Drive Dentsu inaleta uzoefu wake mkubwa, nchini Tanzania, ambao umewawezesha kutwaa tuzo 17  za kimataifa na kitaifa katika tasnia ya ubunifu wa matangazo. Naye Bw. Rami El Khalil, Meneja Mkuu wa Masoko na Maendeleo ya Biashara wa Drive Dentsu anasema Tanzania ni nchi yenye fursa nyingi kutokana na uchumi wake kuwa imara hivyo ni sehemu nzuri kuwekeza.

‘Drive Dentsu itaweka muhimili mpya katika tasnia hii ikiwa na mtazamo mpya wenye kusaidia chapa kujidhihirisha na kutambulika kwa watumiaji wake’ anasema Bw. Rami. Pia Drive Dentsu wamewekeza katika wataalam mahiri walioko nchini, hili linajidhirisha walipomteua Terry Greenwood kuwa Meneja Mkuu wa kampuni hiyo nchini Tanzania.

Terry mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 41 katika tasnia ya mawasiliano, amepata uzoefu huo katika makampuni mbalimbali huko Amerika, China na Mashariki ya Kati. Pia kwa miaka saba sasa amekuwa akifanya kazi na Drive Dentsu.

Kwa uzoefu wake na ushirikiano kutoka kwa mtandao wa Drive Dentsu kimataifa tunaamini ataleta mapinduzi katika tasnia ya utengenezaji matangazo. Wateja wa Drive Dentsu kwa sasa ni kama Zantel, Moov, Moneygram, Radisson Royal Hotel, Daihatsu, Hitachi, Jammal Trust Bank, Toshiba, Lexus, Bridgestone, Jumeirah dot Shabaka, Toyota, Virgin, Abdul Latif Jameel na Vitaene C.

‘Ofisi zetu nchini Tanzania zitakuwa ni sehemu ya kuimarisha muunganiko wetu kimataifa, pia itaiwezesha Drive Dentsu kuwasaidia wateja wetu kukabiliana na mabadiliko ya kila siku katika biashara’ anamaliza Bwana Rami.

Watoto 984 waozeshwa kwa nguvu Tarime, 1,628 wakeketwa

$
0
0
Mjane wa Hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust (GMT), Bi. Graca Michel (kulia) akizungumza kabla ya kuzindua rasmi kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara. Mjane wa Hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust (GMT), Bi. Graca Michel (kulia) akizungumza kabla ya kuzindua rasmi kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara.
Viongozi mbalimbali wastaafu wa Serikali, viongozi wa dini Mkoa wa Mara, wawakilishi wa wanafunzi Mkoa wa Mara wakiwa katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara. Viongozi mbalimbali wastaafu wa Serikali, viongozi wa dini Mkoa wa Mara, wawakilishi wa wanafunzi Mkoa wa Mara wakiwa katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara
Baadhi ya washiriki katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara. Uzinduzi huo umefanywa na mjane wa hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust, Bi. Graca Michel leo jijini Dar es Salaam. Baadhi ya washiriki katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara. Uzinduzi huo umefanywa na mjane wa hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust, Bi. Graca Michel leo jijini Dar es Salaam.Mjane wa Hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust (GMT), Bi. Graca Michel (kulia) akishangilia baada ya kutuma ujumbe mfupi kwa njia ya simu za viganjani kwa simu zote zilizosajiliwa nchini Tanzania ikiwa ni ishara ya uzinduzi kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara. Mjane wa Hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust (GMT), Bi. Graca Michel (kulia) akishangilia baada ya kutuma ujumbe mfupi kwa njia ya simu za viganjani kwa simu zote zilizosajiliwa nchini Tanzania ikiwa ni ishara ya uzinduzi kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara.
Baadhi ya viongozi wa mashirika mbalimbali walioshiriki hafla ya uzinduzi wa kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara. Uzinduzi huo umefanywa na mjane wa hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust, Bi. Graca Michel leo jijini Dar es Salaam. Baadhi ya viongozi wa mashirika mbalimbali walioshiriki hafla ya uzinduzi wa kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara. Uzinduzi huo umefanywa na mjane wa hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust, Bi. Graca Michel leo jijini Dar es Salaam 


Mjane wa Hayati Nelson Mandela na Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust (GMT), Bi. Graca Michel akimbusu mmoja ya watoto wa kike kutoka Mkoa wa Mara kuonesha ishara ya upendo katika uzinduzi huo. Mjane wa Hayati Nelson Mandela na Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust (GMT), Bi. Graca Michel akimbusu mmoja ya watoto wa kike kutoka Mkoa wa Mara kuonesha ishara ya upendo katika uzinduzi huo.Mjane wa Hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust (GMT), Bi. Graca Michel akisalimiana na baadhi ya viongozi mbalimbali kutoka mkoani Mara. Mjane wa Hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust (GMT), Bi. Graca Michel akisalimiana na baadhi ya viongozi mbalimbali kutoka mkoani Mara.Baadhi ya watoto wa kike kutoka Mkoa wa Mara wakizungumzia namna walivyonusurika kufanyiwa vitendo vya kikatili (kukeketwa). Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Nsoka akiwasikiliza. Baadhi ya watoto wa kike kutoka Mkoa wa Mara wakizungumzia namna walivyonusurika kufanyiwa vitendo vya kikatili (kukeketwa). Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Nsoka akiwasikiliza.
Baadhi ya wanafunzi wakiangalia ujumbe mfupi uliotumwa kwa simu zote zilizosajiliwa kwa njia ya simu za kiganjani na Mjane wa Hayati Nelson Mandela, Bi. Graca Michel kwa kushirikiana na Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Bi. Sophia Simba kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike. Baadhi ya wanafunzi wakiangalia ujumbe mfupi uliotumwa kwa simu zote zilizosajiliwa kwa njia ya simu za kiganjani na Mjane wa Hayati Nelson Mandela, Bi. Graca Michel kwa kushirikiana na Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Bi. Sophia Simba kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kikeBaadhi ya wanafunzi wakitumbuiza katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike. Baadhi ya wanafunzi wakitumbuiza katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike.Moja ya kikundi cha maigizo kikionesha igizo namna mtoto wa kike anavyokabiliana na changamoto za unyanyasaji kutoka kwa jamii katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike Moja ya kikundi cha maigizo kikionesha igizo namna mtoto wa kike anavyokabiliana na changamoto za unyanyasaji kutoka kwa jamii katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike

 JUMLA ya wasichana wenye umri mdogo wapatao 984 wameolewa na kukatishwa masomo huku wasichana wengine 1,628 wakikeketwa wilayani Tarime, Mkoa wa Mara ikiwa ni miongoni mwa vitendo vya kikatili ambavyo amekuwa akifanyiwa mtoto wa kike baadhi ya maeneo nchini Tanzania. Takwimu hizo za vitendo vya kikatili dhidi ya mtoto wa kike wilayani Tarime zimetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Wilaya ya Tarime, John Henjewele kwa niaba ya Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mara kwenye hafla ya uzinduzi rasmi wa kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara.

 Akizungumza kabla ya uzinduzi wa kampeni hiyo, Henjewele alisema takwimu hizo zavitendo vya kikatili Mkoani Mara ni za kuanzia mwaka 2013 hadi Juni 2014. Alisema baadhi ya familia eneo hilo wanamchukulia mtoto wa kike kama kitega uchumi hivyo wamekuwa wakiwaozesha mapema ili kupata mali (yaani ng'ombe) jambo ambalo bado uongozi wa mkoa huo kwa kushirikiana na wadau anuai wamekuwa wakipinga na kupambana na ukatili huo. 

"...Matukio ya vitendo vya unyanyasaji kwa mtoto wa kike kwa mwaka 2013 hadi Juni 2014 ni kama ifuatavyo; watoto wa kike wapatao 984 waliozeshwa, wasichana 1,628 walikeketwa, jumla ya wanafunzi wa kike 4,134 walipewa mimba na kukatishwa masomo yao huku wasichana 1,912 wakifanyiwa ukatili wa vipigo kwenye familia ama kwenye ndoa na jumla ya watoto 11 walibakwa...," alisema Henjewele. 

Aidha alisema vitendo hivyo vya kikatili kwa mtoto wa kike vinachangiwa na baadhi ya jamii mkoani humo kuendeleza mila na desturi zilizopitwa na wakati, migogoro ya koo, mwamko duni wa elimu kwa jamii na usiri mkubwa wa kutokubali mabadiliko dhidi ya vitendo vya kikatili kwa jamii hiyo. Akizungumzia jitihada zinazofanywa na viongozi wilayani hapo kukabiliana na vitendo hivyo, alisema wamekuwa wakiendesha semina na vikao mbalimbali na wazee wa kimila, mangariba na jamii kwa ujumla kwa lengo la kutokomeza vitendo vya Ukatili wa kijinsia, ukeketaji pamoja na mila na desturi zilizopitwa na wakati. 

 Kwa Upande wake mjane wa hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust, Bi. Graca Michel akizungumza kabla ya kuzindua rasmi kapeni hizo alisema viongozi kwa kushirikiana na wanajamii mkoani Mara wakiamua kwa dhati wanaweza kukabiliana na ndoa za utotoni na vitendo vingine vya kikatili eneo hilo. Akizungumzia kwa ujumla alisema jamii nyingi ya kiafrika bado zinamthamini mtoto wa kiume zaidi ya yule wa kike ilhali watoto wote wanapaswa kuwa na haki sawa. Aliwataka wazazi wenye mawazo kama hayo kubadilika na kutoa haki sawa kwa watoto bila ubaguzi. Alishauri suala la uamuzi dhidi ya maisha ya mtoto lifanywe kwa ushirikiano kwa familia nzima pamoja na kushirikishwa mtoto.

 "...Lazima tukubali kubadilika, umefika wakati suala la uamuzi wa wakati gani wa kuolewa kwa mtoto wa kike ufanywe kwa ushirikiano kati ya wazazi wote pamoja na mtoto mwenyewe tena kwa wakati muafaka...lazima turejeshe maamuzi pia kwa mtoto mwenyewe si kutumia nguvu kwa kila kitu," alisema Bi. Michel. Aliongeza hata hivyo ipo haja ya kuwa na asasi za ushauri ngazi ya familia ambazo zitakuwa zikitoa ushauri juu ya masuala ya familia kwa kuzingatia sheria na taratibu zinazotambulika. 

Alisisitiza katika kampeni za sasa juhudi na elimu ya kutosha itolewe kwa jamii mkoani Mara ili baadaye ifanyike tathmini kwa eneo hilo jambo ambalo linaweza kusaidia mapambano maeneo mengine hapo baadaye. Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Nsoka akifafanua juu ya shughuli za kampeni hizo alibainisha kuwa zitaambatana na utoaji elimu kwa makundi mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, watendaji wa vyombo vinavyosimamia sheria, viongozi wa jamii na jamii kwa ujumla juu ya mapambano ya kampeni hizo. 

Kampeni hizo baadaye zitaendelea katika maeneo mengine ya Tanzania. Programu ya kampeni hiyo imefanikishwa kwa kushirikiana na Serikali, Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA), Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA), Shirika lisilo la Kiserikali la Children's Dignity Forum (CDF), Graca Machel Trust (GMT), asasi za mkoani Mara na uongozi wa mkoa. *Imeandaliwa na www.thehabari.com

FAINALI YA TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT) KUFANYIKA AUGUST 30 2014 MLIMANI CITY

$
0
0
 Mc Pilipili Akiongea mbele ya Waandishi wa habari wakati wa Mkutano na Waandishi wa habari kuhusiana na fainali kubwa ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) litakalofanyika tarehe 30 August 2014 katika Ukumbi wa Mlimani City kuanzia Mida ya Saa 7:30 PM (Usiku) huku viingilio vikiwa ni Elfu Hamsini (50,000/=) kwa V.I.P na Elfu thelethini (30,000/=) kwa Kawaida. Wapili Kushoto ni Meneja Mradi TMT Joshua Moshi, Julieth Samson "Kemmy" ambae ni Mwalimu wa Nidhamu na Afisa Uhusiano TMT, Josephat Lukaza.
 Washiriki kumi bora Ambao wameingia kwenye fainali ya Kuwania Shilingi Milioni 50 za kitanzania ambayo fainali itafanyika tarehe 30 August 2014 katika Ukumbi wa Mlimani City  huku viingilio vikiwa ni Elfu Hamsini (50,000/=) kwa V.I.P na Elfu thelethini (30,000/=) kwa Kawaida.
 Mmoja wa washiriki walioingia Kwenye fainali ya TMT, Mwanaafa Mwinzago akiongea na waandishi wa habari leo wakati wa mkutano uliofanyika katika Ofisi za Proin zilizopo Mikocheni.
Baadhi ya washiriki na waandishi wa habari waliofika katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo katika ofisi za Proin zilizopo Mikocheni.
BAADA ya mchakato wa kuzunguka mikoani kwa ajili ya kusaka wasanii wenye vipaji vya uigizaji, hatimaye fainali za Tanzania Movie Talents  ( TMT) zitafanyika  Jumamosi ya Agosti 30 mwaka huu  katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mshindi wa shindano hilo atajinyakulia kitita cha shilingi milioni 50 wakati burudani itadondondoshwa  na Christian Bella na mchekeshaji MC Pilipili.

RAIS JAKAYA KIKWETE KUZINDUA PROGRAMU YA UIMARISHAJI WA MIPAKA YA KIMATAIFA MKOANI KAGERA.

$
0
0

 Kaimu Katibu Tawala wa wilaya ya Ngara Bw. Hussein Seif akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa maandalizi ya shughuli ya uzinduzi wa Programu ya uimarishaji wa mipaka ya Kimataifa wa wilaya ya Ngara itakayozinduliwa na Rais Jakaya Kikwete eneo la Mugikomero mpakani mwa Tanzania na Burundi. Wanaoonekana nyuma ni raia wa Burundi waishio mpakani.
 Raia wa Burundi wakiwa nyuma ya alama ya mpaka  inayotenganisha Tanzania na Burundi. Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inaendelea na zoezi la kuhuisha mipaka hiyo ya kimataifa.
 Moja ya Shamba la ndizi lililopandwa katikati ya eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi ambalo kwa sheria za kimataifa haliruhusiwi kufanyiwa shughuli yoyote.

 Bw. Israel Paul akipaka rangi moja ya alama ya mpaka unaotenganisha Tanzania na Burundi eneo la Mugikomero, wilayani Ngara kufuatia Programu inayoendelea ya uhuishaji wa mipaka ya kimataifa.
 Viongozi wa wilaya ya Halimashauri ya Wilaya ya Ngara wakikagua moja ya eneo la mpaka wa Kabanga unaotenganisha Tanzania na Burundi ambapo Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania atampokea Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza.
 Moja ya alama ya mpaka unaotenganisha Tanzania na Burundi ikiwa imekamilika katika eneo la Mugikomero, wilayani Ngara kufuatia Programu inayoendelea ya uhuishaji wa mipaka ya kimataifa.


Na. Aron Msigwa – MAELEZO
26/8/2014. Ngara, Kagera.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete anatarajia kuwa mgeni rasmi katika  uzinduzi wa programu ya  uimarishaji wa mipaka ya kimataifa kwa lengo la kuhuisha alama zilizopo na kuweka mpya katika maeneo ya  mipaka ya Tanzania ambayo awali yalikuwa yametengwa na mito na baadaye mito hiyo kukauka .

Programu hiyo inayofanywa na wataalam wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi itazinduliwa rasmi Agosti 28, katika eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare  kwa upande wa Burundi.

 Aidha, itahusisha ujenzi na uwekaji wa vigingi vya mipaka, Marais wa nchi za Burundi na Tanzania kutembelea baadhi ya maeneo yenye alama za mipaka na kisha kuzungumza na wananchi waishio mpakani.
 
Katika tukio hilo Rais Jakaya Kikwete anatarajia kumpokea mwenzake wa Burundi, Rais Pierre Nkurunziza atakayewasili nchini Tanzania kushuhudia zoezi hilo akitokea nchini Burundi kupitia mpaka wa Kabanga ulioko wilayani Ngara.

Kaimu Katibu Tawala wa wilaya ya Ngara Bw. Hussein Seif akizungumzia maandalizi ya shughuli hiyo amesema kuwa wilaya hiyo imejipanga kuhakikisha kuwa programu hiyo inatekelezwa kwa ufanisi katika maeneo yote ya wilaya ya Ngara yanayopakana na nchi ya Burundi.

Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Topographia na Giodosia wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. James Mtamakaya akizungumzia zoezi hilo amesema kuwa tayari maeneo mbalimbali ya mipaka ya Tanzania yameshapitiwa na zoezi hilo likiwemo eneo la mpaka kati ya Tanzania na Uganda.

Ameyataja maeneo mengine kuwa ni eneo la Tanzania na Rwanda ambalo bado linatenganishwa na mto Kagera, eneo la mpaka kati ya Tanzania na Msumbiji, Tanzania na Kenya pamoja na zoezi la uimarishaji wa mpaka kati ya Burundi na Tanzania ambalo linaendelea kufanyika.

MAMEYA NA WAKURUGENZI WA TANZANIA WATEMBELEA NYUMBA ZILIZOJENGWA KWA MBAO FINLAND

$
0
0
 Baadhi ya viongozi kutoka majiji sita ya Tanzania wakipata maelezo kuhusu mfumo wa ukusanyaji wa taka na uchujaji wa maji machafu katika jiji la LAHTI, kutoka kushoto ni mratibu wa mtandao wa majiji Tanzania, ( Tanzania Cities Network) Philoteus Mbogoro, Meya wa jiji la Tanga Omary Guledi, Lissa Tervo wa taasisi ya Uongozi ya Tanzania, Johanna Palamoki ambae ni mtaalam wa mipangomiji katika jiji la LAHTI, Mkurugenzi wajiji la Lahti Kari Porra na Meya wa jiji la Mbeya Athanas Kapunga ( picha zote na Vedasto Msungu wa ITV)
 Mkurugenzi wa jiji la LAHTI, Kari Porra akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa nyumba hizo za mbao kwa mratibu wa ziara hiyo Godfrey Nyamrunda kutoka taasisi ya Uongozi ya Tanzania, nyuma yao ni Meya wa jiji la Dar Esa Salaam Dk Didas Masaburi
Badhi ya nyumba za ghorofa zilizojengwa kutumia mbao katika jiji la LAHTI nchini Finland ambazo zilitembelewa na madiwani wa majiji sita ya Tanzania waliokuwa katika ziara ya mafunzo nchini humo iliyoratibiwa na taasisi ya Uongozi ya Tanzania. Finland ni miongoni mwa nchi zenye maeneo makubwa ya misitu ya kupandwa dunaini, zaidi ya asilimia 80 ya eneo la nchi hiyo ni misitu na wenyewe wanasema nyumba zinazojengwa kwa kutumia mbao zina gharama nafuu kuliko kujenga kwa matofali au mawe.
 Viongozi kutoka majiji sita ya Tanzania wakiwa kando kando ya ziwa Maji ambako mkondo wa maji machafu kutoka majumbani huingia ziwani baada ya kuchujwa, viongozi hawa kutoka kushoto ni Stanslaus Mabula ambaye ni Meya wa jiji la Mwanza, Athanas Kapunga ambae ni meya wa jiji la Mbeya, Mussa Zungiza,mkurugenzi mtendaji wa jiji la Mbeya na Philoteus Mbogoro ambae ni mratibu wa mtandao wa majiji Tanzania TACIN
Badhi ya nyumba za ghorofa zilizojengwa kutumia mbao katika jiji la LAHTI nchini Finland ambazo zilitembelewa na madiwani wa majiji sita ya Tanzania waliokuwa katika ziara ya mafunzo nchini humo iliyoratibiwa na taasisi ya Uongozi ya Tanzania. Finland ni miongoni mwa nchi zenye maeneo makubwa ya misitu ya kupandwa dunaini, zaidi ya asilimia 80 ya eneo la nchi hiyo ni misitu na wenyewe wanasema nyumba zinazojengwa kwa kutumia mbao zina gharama nafuu kuliko kujenga kwa matofali au mawe.

Serikali yapokea gari na pikipiki kukabiliana na ugonjwa wa kifua kikuu na ukoma nchini

$
0
0
   Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashidi (kulia) akipokea ufunguo wa moja ya gari kutoka kwa mwakilishi wa shirika la GLRA nchini Burchard Rwamtoga (kushoto) ikiwa ni ishara ya kukabidhi msaada wa gari 4 na pikipiki 20 vyenye thamani ya Tsh. Milioni 261 leo jijini Dar es salaam.

    Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashidi akiwasha moja ya kati ya magari manne  aliyoyapokea kutoka kwa mwakilishi wa shirika la GLRA la Ujerumani nchini Burchard Rwamtoga leo jijini Dar es salaam.

 Mwakilishi wa shirika la GLRA nchini Burchard Rwamtoga (kushoto) akimkabidhi Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashidi (kulia) ufunguo wa moja kati ya pikipiki 20 zilizotolewa na shirika la hilo leo jijini Dar es salaam.

   Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashidi (kulia) akimkabidhi Mratibu wa huduma za kifua kikuu na ukoma mkoa wa Kigoma Dkt. Deus Leonard (kushoto) moja kati ya magari manne  yaliyokabidhiwa kwa Serikali kutoka kwa  shirika la GLRA la Ujerumani nchini leo jijini Dar es salaam.



Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashidi (kulia) akisalimiana na Mratibu wa huduma za kifua kikuu na ukoma mkoa wa Ilala baada ya mkabidhi moja kati ya magari manne  yaliyokabidhiwa kwa Serikali kutoka kwa  shirika la GLRA la Ujerumani nchini leo jijini Dar es salaam.(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO).

Umoja wa Machifu Tanzania (UMT) wawasilisha mapendekezo yao kuhusiana na Rasimu ya Katiba Mpya.

$
0
0
 Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samia Suluhu akiwaeleza jambo Wawakilishi wa Umoja wa Machifu Tanzania (UMT) kuhusu mapendekezo yao waliyoyawasilisha kwake kwaajili ya Katiba Mpya.
 Chifu John Nyanza (aliyekaa katikati) wa kutoka Magu akimueleza jambo Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samia Suluhu (kulia) juu ya uwasilishaji wa mapendekezo yao kwa ajili ya Katiba Mpya alipokutana naye leo kwenye Ofisi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum.
 Chifu Agnes Ndaturu (kushoto) wa kutoka Ntuzu, Bariadi akimueleza jambo Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samia Suluhu (kulia) juu ya uwasilishaji wa mapendekezo yao kwa ajili ya Katiba Mpya alipokutana naye leo kwenye Ofisi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum.
 Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samia Suluhu (kulia) akipokea mapendekezo ya maoni toka kwa Chifu John Nyanza alieuwakilisha Umoja wa Machifu wa Tanzania (UMT) leo kwenye Ofisi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum.
Baadhi ya Waandishi wa Habari walikifuatilia uwasilishwaji wa mapendekezo toka kwa Machifu waliouwakilisha Umoja wa Machifu wa Tanzania (UMT) leo kwenye Ofisi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum.
 



 
 
Na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma.
26/08/2014.
UMOJA wa Machifu wa Tanzania (UMT) kupitia wawakilishi wake, leo umewasilisha nyongeza ya mapendekezo yake kuhusu Katiba Mpya kwa Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Akiuwakilisha Umoja wa Machifu Tanzani (UMT), Chifu kutoka Magu John Nyanza amemueleza Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba kuwa wanaishauri Serikali kutayarisha mkakati wa Kitaifa wa Utamaduni kwa kuwashirikisha wadau wakuu wa masuala ya Utamaduni ili mpango mkakati huo uwe na Dira ya Utamaduni itakayobainisha cha kufanya ili kujenga, kuhamasisha na kuendeleza Utamduni katika maeneo yote nchini.

“Chifu kutoka Magu, John Nyanza amesema kuwa lengo la kuwasilisha mapendekezo hayo kwaajili ya kusisitiza masuala mazuri ya Utamduni kuendelea ili kuweza kudumisha madili kwa nia nzuri ya kudumisha amni na ushirikiano”. Alisema Chifu Nyanza.

Naye Chifu kutoka Ntuzu, Bariadi Chifu Agnes Ndaturu ameeleza kuwa mapendekezo yao yatasaidia kuweza kuwatambua waganga wa Jadi ambapo hapo zamani , mganga wa Jadi alikuwa anatambulika na kufanya kazi katika eneo husika analotoka, lakini hivi sasa waganga wengi wa jadi wamekuwa na tabia ya kufanya kazi zao bila mipaka.

 ”Mapendekezo haya yatasaidia viongozi wa waganga wa jadi nchini kuwatambua wale waganga wanaokiuka maadili ya shughuli zao mfano mauaji ya Albino, kwakuwa kila kiongozi atakuwa anawatambua waganga wa eneo lake husika”. Alisema Chifu Ndaturu.

Aidha, Machifu hao wameongeza kuwa, Wajumbe wenzao waliowatuma kuwawakilisha wanasisitiza juu ya umuhimu wa Utamaduni kupewa nafasi rasmi katika Katiba mpya na Serikali ili pawepo na kipaumbele katika utekelezaji wake nchini.

Wakizungumza kwa kauli moja Umoja wa Machifu wa Tanzania wamesema kuwa suala la Utamaduni katika Rasimu ya Pili ya Katiba lifanyiwe marekebisho kwa kuzingatia mapendekezo yaliyoibainishwa huku msisitizo wao ukiwa katika Katiba kueleza wazi kuwa sera na Sheria mpya zitakazotungwa  zihakikishe kuwa Tume ya Taifa ya Utamaduni inaanzishwa kisheria ili kusimamia masuala ya Utamaduni.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewatotoa wasiwasi wawakilishi wa Umoja wa Machifu hao wa Tanzania aliokutana nao kwa kuwaeleza kuwa atayawasilisha katika Uongozi wa Kamati ya Bunge ambapo Kamati Ndogo ya Uongozi inatarajiwa kukutana leo jioni ili kuweza kuyajadili.

“Nimeyapokea mapendekezo yenu, kwakuwa Kamati zinaendelea na kazi ambapo wiki hii kamati zitakuwa zimemaliza kazi zake na hakutakuwa na nafasi tena ya kuyapokea mapendekezo na maoni mengine”. Alisema Samia.

Hivi karibuni, makundi mbalimbali yaliwasilisha mapendekezo yao ambapo baadhi ya makundi hayo yakiwemo Wafugaji, Wasanii na Wanahabari yaliwasilisha.

Kocha wa Zanzibar Cosmos Seif Mbuzi Aongeza Juhudi ya kunyanyua Kiwango cha Mpira wa Miguu Zenj.

$
0
0
Hii ni Taswira ya Vijana wa Zanzibar Cosmos wakiwa na Kocha wao mkuu Seif Mbuzi kwenye mazoezi ya Jioni katika viwanja vya Mnazi mmoja ikiwa ni Jitihada yake Seif Mbuzi Katika kunyanyua Kiwango cha Mpira Visiwani Zanzibar
Kocha wa timu ya Zanzibar Cosmos Seif Mbuzi akiwa na vijana wake katika Mazoezi ya kawaida kwenye viwanja vya mpira wa Miguu Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar siku ya Jumanne Aug 26,2014. (Picha na http://swahilivilla.blogspot.com/)
Kocha wa timu ya Zanzibar Cosmos Seif  Mbuzi akiwafundisha na vijana wake jinsi ya kufunga magoli ya mbali katika Mazoezi kwenye viwanja vya mpira wa Miguu Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar siku ya Jumanne Aug 26,2014.
Kocha wa timu ya Zanzibar Cosmos, Seif Mbuzi akipata picha ya pamoja na timu yake mara tu baada ya mazoezi  siku ya Jumanne Aug 26, 2014 ndani ya wanja wa Malindi uliopo mnazi mmoja Zanzibar

CAMERA ACCESSORIES ZA AINA ZOTE TUNALETA KWA SPECIAL ORDER.

$
0
0
Tunachukua order ya vitu vyote vya camera accesories iwe lens na kadhalika kwa special order,vilevile kwa wale wanaohitaji used camera's aina zote,used Plotter's,used cd printer's na mengineyo.Kwa mawasiliano unaweza wasiliana nasi kwa 0767410763/0715770033 ama kwa email add:macamaca97@outlook.com



MAELFU YA WANANCHI WAMLAKI RAIS KIKWETE GAIRO, KATIKA ZIARA YAKE YA MKOA WA MOROGORO

$
0
0
 Rais Jakaya Kikwete akilakiwa na maelfu ya wananchi alipowasili kwenye uwanja wa mkutano wa mji wa Gairo mkoani Morogoro  kuhutubia mkutano wa hadhara Agosti 26, 2014. 
 Mbunge wa Gairo Mhe. Ahmed Mabhut Shabiby akimkaribisha Rais Kikwete kwenye uwanja wa mkutano wa mji wa Gairo mkoani Morogoro  kuhutubia mkutano wa hadhara Agosti 26, 2014.
 Sehemu ya maelfu ya wananchi waliofurika kwenye uwanja wa mkutano wa mji wa Gairo mkoani Morogoro  kumsikiliza Rais Kikwete alipowahutubia kwenye mkutano wa hadhara Agosti 26, 2014
  Mmoja wa wananchi waliofurika kwenye uwanja wa mkutano wa mji wa Gairo mkoani Morogoro akichukua kumbukumbu wakati wa  kumsikiliza Rais Kikwete alipowahutubia kwenye mkutano wa hadhara Agosti 26, 2014
 Rais Kikwete akihutubia umati wa maelfu ya wananchi waliojitokeza  kumsikiliza  kwenye uwanja wa mkutano wa mji wa Gairo mkoani Morogoro  alipowahutubia kwenye mkutano wa hadhara Agosti 26, 2014.
 Rais Kikwete akipata picha ya kumbukumbu na wazee wa mji wa gairo waliojitokeza  kumsikiliza  kwenye uwanja wa mkutano wa mji wa Gairo mkoani Morogoro  alipowahutubia kwenye mkutano wa hadhara Agosti 26, 2014
  Rais Kikwete akiagana na baadhi ya wananchi  waliojitokeza  kumsikiliza  kwenye uwanja wa mkutano wa mji wa Gairo mkoani Morogoro  alipowahutubia kwenye mkutano wa hadhara Agosti 26, 2014
Rais Kikwete akiawaaga wananchi waliojitokeza  kumsikiliza  kwenye  mkutano wa mji wa Gairo mkoani Morogoro  alipowahutubia kwenye mkutano wa hadhara Agosti 26, 2014

VIONGOZI WA TAKUKURU WAKUTANA KILIMANJARO .

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka wa viongozi wa TAKUKURU unaofanyika katika ukumbi wa Kuringe.
Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Dk Edward Hosea akizummza wakati wa Mkutano wa mkuu wa mwaka wa viongozi wa TAKUKURU .
Mkurugenzi wa idara ya elimu TAKUKURU ,Marry Mosha akitoa neno la shukurani mara baada ya mgeni rasmi kufungua mkutano huo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama akiteta jambo na Mkurugenzi wa TAKUKURU Dk Edward Hosea.
Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa wa Kilimanjaro pia walikuwa waalikwa katika mkutano huo.
Baadhi ya washiriki katika mkutano huo.
Dk Hosea akitoa zawadi kwa mgeni rasmi RC ,Gama.
Makundi mbalimbali yakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano huo.Na Dixon Busagaga wa Globu ya jamii kanda ya kaskazini.

Exclusive: Mtanzania DABO ametajwa kuwania tuzo za reggae za kimataifa na muziki wa dunia 2014 (IRAWMA)

$
0
0
10349153_841207622565532_7288991937464718532_n
Unaweza kuwa humfahamu kwa vile hana kelele nyingi....TUONYESHE UZALENDO KWA KUMPIGIA KURA SASA.

Msanii bora wa muziki wa Reggae Tanzania, DABO (Pichani) amepata nafasi ya kuipeperusha bendera ya Tanzania katika anga za kimataifa, baada ya kuchaguliwa kuwania tuzo kubwa kabisa za reggae za kimataifa na muziki wa dunia 2014 (International Reggae and World Music Awards (IRAWMA).
DABO anawania tuzo hizi katika kipengele cha Mtumbuizaji Mpya Bora, akikabiliwa na ushindani kutoka kwa wasanii MC Norman kutoka Uganda, Alkaline na Kranium kutoka Jamaica na Shatta Wale kutoka Ghana.
196441_588093307897900_104541301_n
Zoezi la kuwapigia kura wasanii hawa kuwawezesha kushinda linaendelea sasa mtandaoni. Link ya kumpigia kura ni: http://www.irawma.com/irawma_vote2014
DABO ametajwa kuwania kipengele cha Best New Entertainer
Kwenye kipengele hicho, DABO anachuana na
* Daniel Bambatta Marley - Jamaica
* MC Norman - Uganda, Africa
* Alkaline - Jamaica
* Kranium - Jamaica
* Shatta Wale – Ghana
Asante kwa Kuunga mkono zoezi zima ndio kama linaanza!

Meet the African base in Germany Female Boxer Bintou Yawa Schmill a.k.a " The Voice"

$
0
0

Female Boxer Bintou Schmill "The VOICE" will fight on the ring on
26.September 2014 ,time 18.00 hour in Stadthalle/ Saalbau Frankfurt-Nied, in Germany

 African ladies are otherwise known for other things than Boxing, except for this one who is changing and making the story looks different.Ms.Bintou Yawa Schmill, 29 years young, a totally black African breed  1.71m, Togo born and based in Germany, started her boxing career at a tender age. Something she did as an Amature has become a success story. She wickedly punched competitors, messlessly and won 24 fights ,and 2 draw in the category welterweight -64Kg.
Her fingerprint show her since 2007, to have been a professional boxer with unbeatable record of 4 fights, 4wins in a package including 3 K. O.Her case study is exceptional, she has not only broken the gender rule, she’s representing the African continent in a Boxing ring , punching evil out the brains of her competitors, Bintou is the Lioness that roars and the Lions make a way. Now she´s back on stage, live and ready for a face2face catch, one on one.
Any brave hearted out there to sponsor and make a name with Bintou? Bintou needs you to make it happen… a man is a man because of another man –UBUNTU
For more information write to
 Africans support your children and make them proud NOW! http://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=iEmjbWJr


JUKATA WAMBEBESHA LAWAMA SITTA, WASEMA KATIBA MPYA NI NDOTO KUPATIKANA

$
0
0
 Kaimu mwenyekiti wa Uukwaa la Katiba Tanzania Hebron Mwakagenda akizungumza na wanandishi wa habari leo Agosti 27, 2014 juu ya mwenendo wa bunge la katiba.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Wakati mchakato wa katiba Tanzania ukiwa ni kama kitendawili kisicho na majibu sahihi kutokana na mchakato huo kuvurugika na kukosa mwelekeo, nao Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA) wazidi kumtupia lawama zote za kuvurugika bunge hilo mwenyekiti wa bunge hilo mheshimiwa Samweli Sitta na kudai kuwa ndiye aneyeuvuruga mchakato huo baada ya kugeuza Bunge hilo kama kikao cha Chama cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza na wanahabari muda huu jijini Dar es salaam kaimu mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania Hebron Mwakagenda amesema kuwa JUKATA wamekuwa wakifuatilia mchakato huu wa bunge ka katiba kwa wiki mbili hizi na kubaini mapungufu makubwa sana ambayo yanatokea jambo ambalo linaonyesha wazi kuwa mwenyeikiti wa bunge hilo hana nia wala dhamira ya kulipatia taifa katiba mpya ya watanzania.
Wanahabari mbalimbali wakiwa wanamsikiliza kiongozi huyo wakati wa mkutano Bw Mwakadenga amesema kuwa swala la mahudhurio ya wabunge wanaoshiriki katika kamati mbalimbali za bunge hilo yamekuwa madogo sana na yasiyo ya kuridhisha ikiwa ni pamoja na wabunge wengi kutokuhudhuria katika kamati hizo pamoja na kusaini kulipwa posho za siku jambo ambalo amesema kuwa ni wizi mpya kwa
watanzania,
 “Kwanza bunge la katiba linaonyesha kuwa wajumbe 441 wamehidhuria lakini uchunguzi wetu unaonyesha kuwa hawa ni wale wote ambao wamewahi kufika na kusaini kwenye kitabu cha mahudhurio wengine wao takribani 100 tuligundua kuwa hawapo bungeni wakiwemo mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na serikali ya mapinduzi Zanzibar pamoja na baadhi ya viongozi wa kamati”amesema Mwakagenda.
Ameongeza kuwa mambo mengine ambayo yanalifanya bunge hilo kuvurugika ni pamoja na kukosekana kwa muafaka na maridhiano ya kitaifa, matumizi mabaya fedha ikiwa ni pamoja na Wajumbe kulipwa bila kuhudhuria bungeni, kukosekana kwa theluthi mbili toka Zanzibar ili kupitisha katiba,pamoja na uondoaji wa vifungu muhimu kwenye rasimu mambo ambayo amesema kuwa mwenyekiti Samweli Sitta ameyafumbia macho na kijifanya kama hayaoni huku akiwa anajua wazi kuwa anauzika mchakato huo.
“Huyu mzee hatujamwelewa kabisa, sisi tumekaa tumezungumza naye tukamuuliza atueleze swala la theluthi mbili hawa wajumbe watapatikana wapi hajatupa jibu la kuridhisha na ukimwona ni kama mtu ambayeameshachanganyikiwa, anapambana na kila anayekuja mbele yake, iwe mwandishi, mwanaharakati, mbunge, yeye amekaa kujihami tu, sasa hali hii sio nzuri kwa mchakato muhimu kama huu”alisema kiongozi huyo wa JUKATA.
Katika hatua nyingine JUKATA wamemwomba raisi Kikwete kiusimamisha mchakato huu wa katiba hadi kipindi kingine kutokana na kuonekana wazi kuwa hauwezekani na kusema Tanzania imekuwa na michakato mingi ambayo sisi kama taifa hatuwezi kuiendesha kwa wakati mmoja na kupata katiba bora, 

“Kusema ukweli taifa sasa lina michakati mingi sana mfano mchakato wa vitambulisho vya taifa, uchaguzi wa serikali za mitaa, daftari la kudumu la kupiga kura na michakato mingine mikubwa, hii haitaki usome sana ndo uelewe ni kutumia busara tu kwamba huu mchakato wa katiba hautawezekana tena, sisi tunamwomba mheshimiwa Rais Kikwete awasikilize watanzania na kuusimamisha mchakato huu wa katiba ili tujipange upya kuanza
tena.
Mchakato wa katiba umekuwa ukiendelea jijini Dodoma bila ya mariano na wajumbe waliotoka wa UKAWA huku kukiwa na taarifa kuwa rais amekubali kukutana nao wiki hii kwa ajili ya mazungumzo ya kuunasua mchakato huu.

ENOC Africa sets for major expansion drive

$
0
0
  
Dar es Salaam. ENOC Africa is planning a major expansion program in Tanzania in the coming few months as a strategy to tap the booming local as well as regional market.

ENOC Africa, a Tanzanian oil company is a joint venture between Petro (T) Limited and Dubai’s ENOC Supply and Trading LLC (ESTC), a subsidiary of Emirates National Oil Company (ENOC) owned by the Government of Dubai.

 “We are planning to invest heavily in Tanzania and the East African countries, beyond between now and next year”, ENOC Africa Managing Director, Mr. Arshid Esmail said.
Under the planned expansion drive, the company, which is actively participating in the Bulk Procurement System (BPS) tenders of white petroleum products through the Petroleum Importation Coordinator (PIC) in Tanzania, will now enter into terminalling and storage facilities while spreading the horizon of their activities in East Africa.

ENOC Africa take note of the steadily increasing trend of economic development of Tanzania and East African region in the next few years, and recognizes the need for state-of-the-art storage facilities, at industry affordable costs for the wholesalers, in the region. 

This dynamic move from ENOC Africa is meant to make sure that Tanzania and its neighbouring landlocked countries have enough reserves even during times of uncertainties in global supply of the products, which will support the country and the wholesale businesses significantly. 

“Our storage facilities will be built across Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi, DRC, Zambia and Malawi as we remain a trusted partner in the response to any urgent crises in fuel shortage while remaining firm on quality assurance of our products,” he said.

ENOC Africa is the first Tanzanian company which has won two competitive tenders in February and July under the bulk procurement system, this year. He said the company relies on its state-of-the-art refinery and International Standard Quality Testing Laboratory (ISQTL) to ensure supplies meet the quality requirements of Tanzania and neighboring countries”, he said, adding: 

“Being an advocate of the BPS initiative, ENOC Africa believes it has what it takes to play an increasingly important role in sustaining Tanzania’s Strategic Petroleum Reserves (SPR) which helps the country during times of supply crises”, he said.  He added that ENOC Africa has the right products and infrastructure to respond to any urgent crisis in fuel shortage situations.

Apart from winning two BPS tenders, ENOC Africa also prides itself for being a company that operates with a team of oil and gas professionals. With such capabilities and rich exposure over decades, ENOC Africa is determined to provide accelerated support to the growing quality conscious product requirements of wholesalers and retailers, while providing guiding role as responsible partners to all the stakeholders in Oil and Gas industry in Tanzania and East Africa.

Real Madrid kujenga Soka Akademi Tanzania

Birthday Wishes to Ankal from Mrs Ankal

$
0
0
Happy birthday to you my better half, my friend, perfect father/daddy to our kids‎. Wish you happiness, wish you success and  contentment in your life. I wish to be there with you but " kazi hizi" I am always thankful to God for you and for every opportunity and everything he has favoured us. His blessings are ever in abundance. I love and  cherish you and will forever do so, in a very special way. Happy birthday.

Mrs Ankal.

RAIS KIKWETE KATIKA SHEREHE ZA UZINDUZI WA PROGRAMU YA UIMARISHAJI WA MIPAKA YA KIMATAIFA MKOANI KAGERA

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakipokea nyimbo za Taifa za nchi zao eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wananchi wa Tanzania na Burundi katika eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakiangalia moja ya alama katika eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014. Kushoto kwa Rais Kikwete ni Waziri wa Ardhi na Maendeleo na Makazi, Profesa Anna Tibaijuka.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakizindua kwa pamoja eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.

ZAIDI YA WANAWAKE 600 KUNUFAISHWA NA ELIMU YA UJASILIAMALI MKOANI MWANZA

$
0
0
Afisa Uhusiano wa TBS, Roida Andusamile akielezea jukumu la TBS katika kuwaelimisha wanawake wajasiriamali wa Kitanzania watakaoshiriki katika kampeni ya Mwanamke na Uchumi juu ya ubora na viwango katika bidhaa wanazoandaa.
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Angels Moment, Naima Malima akizungumza na na waandishi wa habari kuhusu Kampeni ya Mwanamke na Akiba inayotarajiwa kufanyika Mkoani Mwanza kuanzia Septemba 4-5, ambapo zaidi ya wanawake wajasiriamali 600 wanatarajiwa kufaidika na mafunzo hayo. 

Afisa Uhusiano wa TBS, Roida Andusamile pamoja na Meneja wa Kanda ya ziwa wa PPF Bwana Meshach Bandawe wakifuatilia mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mapema leo katika ukumbi wa Gold Crest kuwahabarisha kuhusu kampeni ya Mwanamke ya Uchumi itakayofanyika jijini Mwanza tarehe 4-5 Septemba, 2014 katika viwanja vya Mwaloni Kirumba Jijini Mwanza.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Angels Moment, Naima Malima akizungumza na na waandishi wa habari kuhusu Kampeni ya Mwanamke na Akiba inayotarajiwa kufanyika Mkoani Mwanza kuanzia Septemba 4-5, ambapo zaidi ya wanawake wajasiriamali 600 wanatarajiwa kufaidika na mafunzo hayo. 
Afisa Uhusiano wa TBS, Roida Andusamile akielezea jukumu la TBS katika kuwaelimisha wanawake wajasiriamali wa Kitanzania watakaoshiriki katika kampeni ya Mwanamke na Uchumi juu ya ubora na viwango katika bidhaa wanazoandaa.
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live




Latest Images