Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

WAKONGWE WA REAL MADRID WAKWEA MLIMA KILIMANJARO

$
0
0
 Wakongwe wa Klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania wakipiga picha za kikundi cha ngoma kilichokuwa kikiwatumbuiza mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro kabla ya kuelekea Mlima Kilimanjaro.
Wachezaji wakongwe wa Klabu ya Real Madrid wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa TANAPA mara baada ya kumaliza zoezi la matembezi mafupi ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
 Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Dk. Fenela Mukangara akitoa cheti cha ushiriki kwa mchezaji Ruben De La Red wa Klabu ya Real Madrid mara baada ya kumaliza zoezi la matembezi mafupi ya kupanda Mlima Kilimanjaro. 
Wakongwe wa Real Madrid wakiwa katikati ya msitu wa Mlima Kilimanjaro.

 Eneo la Maporomoko ya Maji ambapo wachezaji wakongwe wa Real Madrid walifanikiwa kufika Mlimani Kilimanjaro. 
 Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete (mwenye fulana nyeupe na miwani) akiongoza msafara wa wakongwe wa Real Madrid kukwea Mlima Kilimanjaro.

MWIGULU AMSIMIKA SALIM ASAS KUWA KAMANDA WA VIJANA RINGA

$
0
0

MFANYABIASHARA maarufu mkoani Iringa Salim Abri Asas akisimikwa kuwa Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Iringa katika kipindi cha miaka mingine mitano  na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara Mwigulu Nchemba katika sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Mwembetogwa, mjini Iringa.
Mwigulu Nchemba akizingumza na umati wa watu katika viwanja vya mwembetogwa mwishoni mwa wiki mjini Iringa
MFANYABIASHARA maarufu mkoani Iringa Salim Abri Asas akizungumza na Wananchi mwishoni mwa wiki mara baada ya kusimikwa kuwa Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Iringa katika kipindi cha miaka mingine mitano  na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara Mwigulu Nchemba katika sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Mwembetogwa, mjini Iringa.
 Salim Abri Asas akiwa na Wazee wa Kimila kabla ya kusimikwa kuwa Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Iringa katika kipindi cha miaka mingine mitano.
 Shughuli za kusimikwa zikiendelea huku wanahabari wakiendelea kurekodi tukio hilo.

Na Denis Mlowe,Iringa

MFANYABIASHARA maarufu mkoani Iringa Salim Abri Asas mwishoni mwa wiki amesimikwa kuwa Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Iringa katika kipindi cha miaka mingine mitano  na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara Mwigulu Nchemba katika sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Mwembetogwa, mjini Iringa.

 Akimuapisha Asas kuwa Kamanda wa UVCCM Mkoa wa Iringa, Nchemba ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM alisema analitumikia taifa hili akijua sehemu kubwa ya wananchi wake ni masikini na lengo kubwa ni kuwaondoa katika lindi la umaskini.


Nchemba alisema nchi inaliwa na moja ya eneo linalowaweka katika kazi kubwa ya mapambano ni fedha zinazotolewa kwenye halmashauri kwa ajili ya maendeleo ambazo hazitumiki ipasavyo na watendaji kwa kuzitumia katika miradi isiyo endelevu na kusababishia nchi kutokuwa na maendeleo.

“Kuna mambo mengi yanatokea katika halmashauri zetu kwasababu ya kukosa usimamizi unaosababisha watu wetu wakose hali ya kupata huduma zinazotakiwa kutekelezwa katika miradi ya maendeleo hivyo nitahakikisha kuwabana na kuwafuatilia kwa kila halmashauri kuleta mchanganuo wa fedha jinsi zilivyotumika na kuhakikisha mradi umekamilika na sio kusema kiasi Fulani kimetumika.”  Alisema Nchemba.
 
Aliongeza kuwa serikali inaendelea na mikakati ya kuwasaka, kuwakamata na hatimaye kuwafikisha katika vyombo vya dola watumishi wa umma wanaokula kodi za wananchi kwa mikono miwili bila kunawa.

Mwigulu alisema mambo mazuri yanakuja na serikali itaendelea kutengeneza sera  zinazojali watanzania ili keki ya taifa iliwe na watanzania wote na kudhibiti matumizi ya ovyo na fedha tutakazokuwa tunatoa hatutaruhusu zitumike kwa kazi tofauti na ile iliyokusudiwa.

Akimpongeza Asas kwa kuwa kamanda wa UVCCM, Alisema UVCCM wakitimiza wajibu wao ipasavyo watasaidia kupunguza maadui wakubwa wawili wa CCM ambao wameendelea kuwa na athari kubwa wakati wa chaguzi za serikali.

Aliwataja maadui hao kuwa ni pamoja na kujiingiza kwenye makundi ya wagombea na hila zinazosababisha baadhi ya wana CCM wasitendewe haki stahiki kwenye vikao muhimu vya chama.

Kwa upande wake Kamanda Salim Asas alisema baada ya kuapishwa kwa kipindi kingine lengo ni kuwainua vijana kiuchumi na kutaka ushirikiano katika kuleta maendeleo ya wananchi wa mkoa wa Iringa bila kujali itikadi ya vyama na dini.

MBEYA YETU BLOG WAANZA KUTEMBELEA NA KUTANGAZA VIVUTIO VYA KITALII MKOANI MBEYA , WAKIANZIA NA KIJUNGU.

$
0
0
Baada ya kuona kuwa kuna maeneo mbalimbali ya vivutio vya kitalii muhimu na ambavyo vimesahaulika kwa njia moja au nyengine na pengine hakuna pa kuvitangaza ili watanzania na Dunia kwa ujumla wapate kuvifahamu kwa ukaribu , Tone Multimedia Group kupitia mtandao wake wa Mbeya yetu Blog wameamua kuanza rasmi kuvitembelea na kutangaza kwa Jamii kwa ujumla  wapate kuvifahamu ili nao waje kuvitembelea.

Safari hiyo ambayo moja kwa moja ilianzia Mkoa wa Mbeya Wilaya ya Rungwe-Tukuyu kwenda kujionea vivutio hivyo mbalimbali kikiwepo cha kwanza kabisa ambacho ni Kijungu eneo ambalo ni la kipekee na lenye historia ya aina yake.

Hivi ndivyo safari ilivyokuwa Fuatilia hapa kwa makini.
Kwanza kabisa tulifika katika kibao hiki ambacho kimetoa maelezo ya awali ikiwa ni pamoja na Bei ambazo mtu anatakiwa kutozwa wakati anapotaka kuingia katika eneo hilo, Bei hizo zimewekwa na uongozi wa Serikali ya Kijiji ambapo fedha hizo zinasaidia katika mambo mbalimbali za kuendeleza kijiji hicho ingawa hata hivyo kuna changamoto kadha wa kadha ambazo zinawakabili ikiwa ni pamoja ni Gharama kubwa za kuingia katika eneo hilo kwa wazawa ambapo haichagui kwamba umetoka nje ya nchi au ndani  Jambo ambalo Serikali inapaswa kutazama kwa sababu ni zaidi hata ya kuingia katika Hifadhi za Taifa.
Picha hii ilipigwa kwa juu kabisa kuonesha Jinsi eneo la Kijungu linavyo onekana 
Hapa ni eneo ambalo Maji ya mto huo yanatokea katika eneo linaitwa Namba One eneo la ukanda wa juu kabisa wa eneo hilo, Majihayo pamoja na mengine mengi hata wakati wa mvua kubwa ni lazima yazunguke yanapo kwenda lakini mwisho wa siku ni lazima yaishie hapa, Pia hapa ndipo maji haya yanapoanza kutililikia moja kwa moja katika kijungu.
Maji hayo sasa huingia katika eneo hili la kijungu, Wamekiita jina la kijungi kwa sababu kubwa kuwa eneo hilo lipo kama chungu, Maji hayo hata yakiwa na kasi kiasi gani, hata yawe mengi kwa namna gani hayawezi kujaa katika Kijungu hiki, Pia kijungu hiki hakuna mtu aliyekijenga bali ni maajabu tuu ya uumbaji wa Mwenyezi Mungu, hilin eneo limeumbwa kwa miamba ya mawe yanayofanana na Chuma kigumu. Maji haya yakishafika hapa huwa si mwisho kuna eneo yanaelekea..kwa hakika ni maajabu na kama huna wazo la kutembelea ni wakati wako sasa.

Kulia ni upinde unao onekana kutokana na kasi ya maji, upinde huu ni kivutio kikubwa hasa wakati wa jua kali huonekana vizuri
Tulipo wasili katika eneo hilo la kijungu tulipata wasaa wa kuongea na Mzee mmoja wa zamani sana ambaye kwa hakika yeye alikiona kijungu zamani sana miaka yani miaka ya 1933 , mzee huyo ambaye anatambulika kwa jina la Elia Kabadhasya aliye  zaliwa mwaka 1927 alieleza kwamba alikijua kijungu hiki wakati alipokuwa akitafuta sehemu ya Kunyweshea Ng'ombe Maji ndipo aliposhuka eneo hili na kukiona Kijungu hiki, hata hivyo wakati anawanywesha maji Ng'ombe wake kwa bahati mbaya moja kati Ng'ombe hao alitumbukia ndani ya kijungu hicho na kupotea moja kwa moja. Wa kwanza kutoka kushoto ni Joseph Mwaisango Mwandishi mkuu wa Mbeya yetu Blog na wa Kwanza kutoka kulia ni Fredy Anthony Njeje kutoka Tone Multimedia group akiwa anachukua maelezo kwa makini ya Mzee Elia Kabaghasya wa kati kati.
Baada ya maji hayo yenye kasi ya ajabu kuingia katika kijungu hicho hutokea katika eneo hili ambapo yanaonekana meupe na yenye mapovu . hii ni kutokana na sababu ya kwamba yanakuja kwa kasi na kufikia hapa, baada ya kufika hapa mbele kunaonekana kwamba kuna  uwazi, uwazi huu kwa mujibu wa wanakijiji wanaotokea eneo hili wanasema kwamba maji haya huingia hapa katika uwazi ambao unakadiliwa kuwa  na urefu kwa Kilometa moja husafiri huko na baadae hutokea katika upande mwengine ambapo ukitazama vizuri katika picha hiyo kwa mbele ya haya maji kuna maji yamepoa hayana kasi hapo ndipo yanapo tokea, hakuna yanapo kutana haya maji mpaka yaingie pangoni ndio yatokee upande wa pili, hii itaonekana katika picha inayofuatia, hili ni moja ya ajabu kwa sababu waweza dhania haya maji yanakutana kumbe hayakutani hata kidogo.
Picha hii inaonesha vizuri na ni mwendelezo ya wa maelezo ya maji hayo hapa kama inavyo onekana upande wa juu ni kijungu maji ambapo yanaingilia hapo kisha yanatokea upande huo wa pili yanapoonekana meupe sana na povu kutokana na povu kisha yanaingia katika pango hilo linalokadiliwa kuwa na Kilometa moja kisha yanatokea upande wa pili hapo yanapo onekana kama yamepoa kisha kuendelea na safari , Cha ajabu maji hayo hayakutani hata kidogo.
Fredy Anthony Njeje Kutoka Tone Multimedia Group ambao ni wamiliki wa Mtandao huu wa Mbeya yetu  wa upanda wa kulia akipata maelezo zaidi ya Kina kuhisiana na Kijungu hiki kutoka kwa Mzee Elia Kabaghasya mwenye umri wa Miaka 87 sasa mzee mwenye nguvu na  ambaye anajua historia nzima ya eneo hili la kijungu alieleza kwamba hili ni eneo zuri sana la utalii ambapo aliwataka watu wengi zaidi waje kutembelea katika eneo hili na kujionea mambo mengi zaidi na Maajabu ya Mungu ya eneo hilo la kipekee ambalo kwa Tanzania hata kwa Dunia ni hapo tuu ndipo papo hivyo, Alieleza zaidi kwamba maji hayo ya mto huo hutumika zaidi kwa ajili ya kunyweshea mifugo, na kufulia tuu hayatumiki kwa kazi zengine. Alitoa wito kuwa watu wanatakiwa kuwa makini wanapokuja kutembelea eneo hilo na kuchukua tahadhali kama maeneo mengine kwa kuwa mtu anaweza teleza ingawa eneo hilo kuna wataalam na watu maalum wa kuwaongoza. alimalizia kwa kusema kuwa kuna haja ya Serikali kukiboresha Kivutio hiki cha Kijungu.
 Mmoja wa wanakijiji ambao wanaishi katika eneo hilo akipita njia kati kati ya Kijungu hicho na kusema  kwamba zamani kutokana na imani za mababu zetu ilikuwa ili upite ni lazima utumbukize kitu chini ndio upate kupita hapo, lakini kadili siku zinavyozidi kwenda na hivi miaka ya karibuni imani hiyo imetoweka na mtu anaweza kupita bila shida, pia alisema kwamba katika eneo hilo mtu anapokatiza katika mwamba huo katikati anatakiwa aanze kutanguliza mguu wa kulia kwanza ndio anaweza akavuka. Mwisho alisema kwamba ukivuka upande wa pili unatokea moja kwa moja mpaka Uporoto ingawa ni parefu hivyo mababu zetu ndio njia walikuwa wakipita enzi hizo.
Kikosi kazi cha Mbeya yetu kazini
 Mzee Elia Kabaghasya (87) akionesha eneo ambalo anaishi halipo pichani kuwa maji hayo yamefika mpaka eneo hilo nyumbani kwake.
Kutoka kushoto ni Joseph Mwaisango akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya waliofika eneohilo ambao ni Doreen, Ruby, Happy na Eric  kufanya utalii wa ndani.

******
Inawezekana umehamasika na unataka na wewe kufika katika eneo la Kijungu kujionea wewe mwenyewe kwa macho yako na haya ndio maelekezo.

Namna ya kufika
Kutoka Mbeya Mjini hadi Sehemu moja inaitwa KK Wilaya ya Rungwe-Tukuyu ni zaidi ya Kilometa 50 , Baada ya hapo kuna njia ambayo inakatiza upande wa kulia kuelekea Chuo cha Magereza, Ukifika Chuo cha Magereza ndani utapata maelekezo yote ya namna utakavyofika, Muhimu kufuata taratibu maana ni eneo la Jeshi la Magereza kuna sheria zake. 

MAONI 
Baada ya kutembelea na kujionea wenyewe tulikuwa tunaomba Serikali iangalie swala zima kwanza la Afya za hawa wanaotembelea katika Kivutio hiki cha kitalii, kwamba hakuna sehemu ya watu kijisaidia-Choo hivyo inawalazimu watu wajisadie hovyo hovyo katika vichaka jambo linalosababisha uchavuzi wa mazingira na pengine inaweza sababisha mripuko wa magonjwa, Hilo ni swala muhimu.

Pili ni swala la mapato tumejionea kwamba kwanza hakuna Risiti inayotolewa wakati watu mbalimbali wanaenda kutembelea katika kivutio hicho cha Kijungu, Kila mtu anajiwekea bei zake ingawa wameweka Bei ya kutazama pale ni Tsh 5,000 kwa mtu ambapo hicho ni kiasi kikubwa kwa wazawa na inabidi hapa paangaliwe, na kwamba mwanakijiji yoyote ambaye yupo eneo hilo ndiye anayetoza watu, utaratibu huo unatakiwa kuangaliwa na kutengenezwa vizuri na kurekebisha viwango hivyo kwani watu wanapenda kuona lakini wanashindwa, Pia mapato hayo yanaonekana hayana msaada wowote kwa wakazi wa eneo hilo.

Tatu ni Miundombinu ya eneo hilo, ambayo inatakiwa kuboreshwa zaidi hasa eneo la kuingilia hapo Serikali itazame waweke hata ngazi kuanzia eneo la kuingilia mpaka hapo katika Kijungu ili watu waweze kufika kiurahisi 

Mwisho Serikali iangalie jinsi gani wanaweza kuweka Ofisi ili hata watu wanapofika waelewe kabisa kwamba sasa wamefika katika kijungu na kupata maelekezo yote ya awali kabla ya kwenda katika eneo la tukio.

Ikiwa unapenda kujua na kuungana nasi katika mpango huu wa kutangaza vyanzo hivi muhimu wasiliana nasi kwa namba +255 754 374 408 au +255 765 056 399

Imeandaliwa na Tone Multimedia Group kupitia Mtandao wake wa Mbeya yetu Blog, Huu ni Mwanzo bado kuna Mengi sana  usikose Kujua juu ya Maporomoko ya Kaporogwe  ambapo ndipo tutawaletea hapa usikose.

Airtel yaingiza smartphone mpya sokoni ikiwa na ofa kabambe

$
0
0
Meneja Masoko wa Airtel Bi Prisca Tembo na Meneja Biashara wa Techno bw, Marco Wang wakionyesha simu mpya ya TechoH5 iliyoingizwa sokoni ikiwa na ofa kabambe itakawawezesha wateja wa Airtel kupata simu ya kisasa pamoja na vifurushi vya internet ya kudumu kwa muda wa mienzi mitatu kuanzia leo.
Afisa Mauzo wa airtel Nizar Aladawy na Afisa Mauzo wa Techno bi, Lolinda Joshman wakionyesha simu mpya ya TechoH5 iliyoingizwa sokoni ikiwa na ofa kabambe itakawawezesha wateja wa Airtel kupata simu ya kisasa pamoja na vifurushi vya internet ya kudumu kwa muda wa mienzi mitatu kuanzia leo. Meneja Masoko wa Airtel Bi Prisca Tembo na Meneja Biashara wa Techno bw, Marco Wang wakionyesha simu mpya ya TechoH5 iliyoingizwa sokoni ikiwa na ofa kabambe itakawawezesha wateja wa Airtel kupata simu ya kisasa pamoja na vifurushi vya internet ya kudumu kwa muda wa mienzi mitatu kuanzia leo.

Airtel kupitia huduma ya Switch on yazindua ofa kambabe ya simu ya Tecno H5 Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia huduma yake ya Switch on leo imezindua ofa kabambe itakayowawezesha wateja wa Airtel kupata simu ya kisasa ya TECNO H5 pamoja na vifurushi vya internet ya kudumu kwa muda wa mienzi mitatu.

Akiongea wakati wa uzinduzi, Meneja Masoko wa Airtel Bi Prisca Tembo alisema" ofa hii maalumu itawawezesha wateja kununua simu hii ya TECNO H5 na kupata simcard ya bure pamoja na kifurushi cha internet cha muda wa mienzi mitatu kitakachomuwezesha kupiga simu katika muda huu wa mienzi mitatu kwa gharama nafuu ya shillingi 1 kwa sekunde".

"TECNO H5 ina vitu vinavyovutia ndani ya simu kama vile , camera aina ya Mega pixel yenye uwezo wa kutoa picha nzuri, nafasi ya kutunza data wa kiasi cha 4GB, pamoja na memory card yenye ukubwa wa mpaka 32GB, simu hii pia inatumia technologia ya android na pia ni raisi kuibaba kwani ina ukubwa wa kati.

Simu ya TECNO H5 inapatikana katika maduka yote Tanzania kwa kiasi cha gharama ya shilingi 129,000/= "aliongeza Tembo.

TECNO H5 itawapa nafasi wateja wa Airtel kupata huduma ya internet na kuunganishwa na huduma ya SWITCH ON iliyowekwa maasusi kwa watumiaji wa huduma ya internet Tanzania, na kuwapatia internet ya kasi kwa bei nafuu. Kupata huduma hii ya SWITCH ON ni rahisi mteja anatakiwa kupiga *148*22# na kuchagua kifurushi cha internet na kisha kupata ujumbe utakao muhakikishia kuunganishwa na huduma ya SWITCH ON na kuanza kufurahia intenet bila kikomo.

Ofa hii ni kati ya ofa nyingi zinazotolewa na Airtel kwa wateja wake, sambamba na ofa hii ya TECNO H5 Airtel pia inatoa vifurushi vya YATOSHA vya kupiga simu,ujumbe mfupi , internet na pamoja na ofay a HAKATWI MTU HAPA inayowawezesha wateja wake kutuma na kupokea pesa kwa nusu gharama.

PANONE FC ILIVYOPOKEA UGENI WA REAL MADRID KILIMANJARO

$
0
0
Waziri wa Vijana,Utamaduni na Michezo Dk Fenera Mkangara akiongoza ugeni toka klabu ya Real Madrid ulipowasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA.)

Baadhi ya wachezaji wa zamani wa klabu ya Real Madrid wakiwasili katika uwanja wa Ndege wa KIA .

TOYOTA YAFANYA BONANZA MAALUMU LA KUWAPONGEZA WAFANYAKAZI WAKE, WANAUME WACHUANA KUKUNA NAZI

$
0
0
 Wafanyakazi wanaume wa Kampuni ya Toyota Tanzania, wakishindana kukuna Nazi wakati wa Bonanza maalumu la kuwapongeza wafanyakazi lililoandaliwa na Kampuni hiyo lililofanyika kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam, juzi Agosti 23, 2014. Katika Bonanza hilo timu ya Rav 4 iliibuka mshindi wa jumla katika michezo yote iliyochezwa ikifuatiwa na timu ya Hilux, VX na Prado. 
 Wafanyakazi wanaume wa Kampuni ya Toyota Tanzania, wakishindana kukuna Nazi wakati wa Bonanza maalumu la kuwapongeza wafanyakazi lililoandaliwa na Kampuni hiyo lililofanyika kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam, juzi Agosti 23, 2014. Katika Bonanza hilo timu ya Rav 4 iliibuka mshindi wa jumla katika michezo yote iliyochezwa ikifuatiwa na timu ya Hilux, VX na Prado.
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Toyota Tanzania,  Bw. Vinod Rustagi, akimkabidhi Kombe la ushindi wa jumla katika michezo yote mwakilishi wa timu ya RAV 4, Mumma Nyamhanga, wakati wa hafla ya Bonanza maalum la kuwapongeza wafanyakazi wa Kampuni hiyo lililofanyika kwenye ufukwe wa Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es salaam, mwishini mwa wiki. Kushoto ni mwamuzi wa michezo hiyo, Othman Kazi. 

RAIS KIKWETE ATUNUKU KAMISHENI TMA MONDULI

$
0
0
D92A6553
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua vikosi hkwenye  uwanja wa Paredi la kutunuku kamisheni katika chuo cha jeshi Monduli mkoani Arusha Jumamosi.
D92A6628
Maofisa Wapya wa jeshi wakipita mbele ya mgeni Rasmi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na kutoa heshima wakati wa gwaride maalumu la Kamisheni lilofanyika katika chuo cha TMA Monduli.
D92A6697
Kikosi cha Bendera kikipita  mbele ya Amiri jeshi mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete  wakati wa gwaride maalumu la Kamisheni lilofanyika katika chuo cha TMA Monduli.
D92A6761
Maofisa Wapya wa jeshi wakipita mbele ya mgeni Rasmi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete nakutoa heshima wakati wa gwaride maalumu la Kamisheni lilofanyika katika chuo cha TMA Monduli. 

D92A6430
Mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama Jenerali Davis Mwamunyange kushoto na Mkuu wa Chuo cha Jeshi (TMA) Monduli Brigedia Jenerali Paul Peter Massao(kulia) wakimsindikiza Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho kwenda uwanja wa Paredi ambapo alitunuku kamisheni kwa maofisa wapya wa jeshi katika sherehe zilizofanyika katika chuo cha jeshi(TMA) mkoani Arusha.
D92A6383
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mkuu wa majeshi wa kwanza Mzalendo Jenerali Mirisho Sarakikya muda mfupi baada ya kuwasili katika chuo cha jeshi Monduli tayari kwa kutunuku kamisheni kwa maofisa 179 wapya wa jeshi waliohitimu vyema mafunzo yao mwishoni mwa wiki.

D92A6441
Mkuu wa Chuo Cha Jeshi Monduli TMA Brigedia Jenerali Paul Peter Massao akimsindikiza Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kuingia katika viwanja vya Paredi chuoni hapo akiwa katika gari maalumu ambapo alitunuku kamisheni kwa maofisa wapya wa Jeshi.
D92A6497
Mkuu wa Chuo Cha Jeshi Monduli TMA Brigedia Jenerali Paul Peter Massao akimsindikiza Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kuingia katika viwanja vya Paredi chuoni hapo akiwa katika gari maalumu ambapo alitunuku kamisheni kwa maofisa wapya wa Jeshi.
D92A6512
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea salamu ya heshima mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Paredi kutunuku kamisheni katika chuo cha jeshi Monduli mkoani Arusha Jumamosi.

MAMA SALMA KIKWETE AKUTANA NA MAMA GRACA MACHEL KWENYE OFISI ZA WAMA .

$
0
0

IMG_9239
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mgeni wake Mama Graca Machel na wajumbe wawili wa Bodi ya WAMA. Wajumbe hao ni Mheshimiwa Sophia Simba,Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto (kulia) na Mama Hulda Kibacha (wa kwanza kushoto).
IMG_9252
Mama Garaca Machel akiweka saini kitabu cha wageni wakati alipotembelea ofisi za WAMA tarehe 25.8.2014.
IMG_9283
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Bodi ya WAMA akimkabidhi zawadi ya picha mgeni wake Mama Graca Machel aliyemtembelea ofisini kwake tarehe 25.8.2014.
IMG_9326
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na Mgeni wake Mama Graca Machel kwenye ofisi za Taasisi hiyo zilizoko karibu na Ikulu.
IMG_9344
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi baadhi ya majarida yanayochapishwa na Taasisi ya WAMA kwa Mgeni wake Mama Graca Machel.
IMG_9354
Picha ya pamoja kati ya Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na wafanyakazi wa Taasissi ya WAMA na Mama Graca Machel na ujumbe wake mara baada ya kufanya mgeni uyo kutembelea ofisi hiyo tarehe 25.8.2014.
IMG_9369
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimwaga Mgeni wake Mama Graca Machel wakati akiondoka kwenye ofisi ya WAMA baada ya viongozi hao kufanya mazungumzo.
IMG_9220
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimpokea Mama Graca Machel aliyemtembelea kwenye ofisi za WAMA tarehe 25.8.2014.
IMG_9235
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na mgeni wake Mama Graca Machel wanaonekana wakifurahia jambo kabla ya kupiga picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya WAMA.

IMG_9379
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kuagana na Mgeni wake Mama Graca Machel nje ya ofisi za WAMA tarehe 25.8.2014.
 PICHA NA JOHN  LUKUWI.

Zoezi la kumtafuta Mshindi wa Tuzo ya Rais ya Huduma za jamii kuanza kesho

$
0
0
Picha  Na 2
Mkurugenzi wa Taasisi ya Uunganishaji na Shirikishi Wadau katika Tasnia ya Uziduaji (Extractive InterStakeholders Forum, EISF) Bi. Catherine Lyombe akielezea jinsi zoezi la kumtafuta mshindi wa Tuzo ya Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji (Presidential Award on Corporate Responsibility and Empowerment –CSRE in Extractive Industry) litakavyoendeshwa katika kikao hicho
Picha Na 1
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava akizungumza na jopo la majaji na sekretarieti inayotarajia kuanza kazi ya kumtafuta mshindi wa Tuzo ya Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji (Presidential Award on Corporate Responsibility and Empowerment –CSRE in Extractive Industry)
Picha Na 3
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava akisisitiza jambo wakati wa kikao hicho.

……………………………………………………………………….
Na Greyson Mwase, Dar es Salaam
Jopo la majaji lililoundwa kwa ajili ya kumtafuta mshindi wa tuzo ya Rais ya huduma za jamii na uwezeshaji katika miradi ya madini, gesi na mafuta linatarajia kuanza kazi yake kesho, imeelezwa.
Akizungumza katika kikao na majaji watakaoshiriki katika zoezi hilo kilichofanyika kwenye ofisi za Wizara ya Nishati na Madini Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava amesema kuwa kazi hiyo inayotarajiwa kukamilika Septemba 24, 2014 itahusisha mikoa yote ambayo miradi ya madini, gesi na mafuta inaendesha shughuli zake.
Mhandisi Mwihava alisema lengo la zoezi hilo ni kushindanisha makampuni yanayoendesha shughuli za madini, mafuta na gesi katika utoaji wa huduma bora kwa jamii.
Alieleza kuwa mara baada ya jopo la majaji kumaliza kazi yake, litawasilisha ripoti kamili ya zoezi hilo ambayo itadurusiwa kabla ya kukabidhiwa rasmi kwa ajili ya maandalizi ya halfa ya utoaji tuzo inayotarajiwa kufanyika mapema Novemba mwaka huu.
“Tanzania imewaamini katika kazi hiyo, hivyo ni imani yangu kubwa mtatumia utaalamu na uzoefu wenu katika zoezi hilo pasipo kupendelea kampuni yoyote. “ Alisisitiza Mhandisi Mwihava.
Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Uunganishaji na Shirikishi Wadau katika Tasnia ya Uziduaji (Extractive InterStakeholders Forum, EISF) Bi. Catherine Lyombe aliainisha maeneo yatakayoangaliwa kama mchango wa makampuni yanayoendesha shughuli za madini, gesi na mafuta kuwa ni pamoja na elimu, maji, afya, ajira na miundombinu.
Akielezea zoezi litakavyofanyika Bi. Lyombe alieleza kuwa majaji watatembelea maeneo yote yenye makampuni yanayoendesha shughuli za madini, gesi na mafuta na kuzungumza na wahusika pamoja na kuzungumza na wananchi ili kupata picha kamili ya mchango wa makampuni husika kwa jamii
Bi. Lyombe alisisitiza kuwa mbali na kupata taarifa kutoka katika makampuni na maelezo kutoka kwa wananchi kama wataalamu watafanya ulinganisho wa maelezo yanayotolewa na wananchi na tathmini halisi ya utekelezaji wa miradi iliyotekelezwa na kampuni husika.
Aliongeza kuwa lengo la utoaji wa tuzo hizo ni mkakati wa kuhamasisha makampuni ya madini, mafuta na gesi kuboresha huduma zake kwa jamii.“ Mshindi wa tuzo ya Rais ya huduma za jamii na uwezeshaji katika miradi ya madini, mafuta na gesi anapopatikana, anatia hamasa kwa makampuni mengine kuboresha huduma zake na wananchi kuendelea kunufaika na uwepo wa makampuni hayo” alisisitiza Bi. Lyombe.
Tuzo ya Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji (Presidential Award on Corporate Responsibility and Empowerment –CSRE in Extractive Industry) katika miradi ya madini, gesi na mafuta ilizinduliwa mwaka 2012 na Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kama mkakati wa kuhamasisha makampuni ya madini, gesi na mafuta kuboresha huduma zake kwa jamii hususan katika maeneo ya elimu, maji, miundombinu, ajira na afya.

Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta awatoa wasiwasi wasanii nchini kuhusu haki miliki.

$
0
0
 Mweyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta akiwahutubia wasanii pamoja na waandishi wa habari waliohudhuria mkutano leo katika kumbi za mikutano bungeni mjini Dodoma.
 Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Samia Suluhu Hassan akito maneno ya shukuurani kwa wasanii wakati walipofanya mkutano na Mweyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta mkutano leo katika  moja ya kumbi za mikutano bungeni mjini Dodoma.

 Viongozi wa msafara walifuatana na wasanii 25 wakimsikiliza Makamamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Samia Suluhu Hassani wakati walipohudhuria mkutano leo katika moja ya kumbi za mikutano bungeni mjini Dodoma.
 Baadhi ya wasanii na waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini maelezo kutoka kwa Mweyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta wakati walipohudhuria mkutano leo katika moja ya kumbi za mikutano bungeni mjini Dodoma.
 Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzani (TAF) Bw. Simon Mwakifamba (kushoto) akimkabidhi Mweyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta ripoti ya wasanii yenye mapendekezo mbalimbali kuhususiana na Katiba mpya wakati wa mkutano leo katika moja ya kumbi za mikutano bungeni mjini Dodoma.
Mweyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasanii walifika Bungeni mjini Dodoma kwa ajili kuwasilisha mapendekezo yao kwajili ya Katiba mpya. Kushoto kwake ni Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Samia Suluhu Hassan.(Picha na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma).

BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI KUFANYA KIKAO CHAKE CHA BUNGE KARIMJEE DAR ES SALAAM, RAIS KIKWETE KUUFUNGUA

$
0
0
Spika wa Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki (EALA) Dk. Margaret Nantongo Zziwa  akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari katika ofisi za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dar es Salaam leo juu ya mkutano wa kwanza wa Bunge la tatu unaotaraji kuanza leo katika ukumbi wa Karimjee na kufunguliwa na Rais Jakaya Kikwete kesho kutwa. 
 Spika wa Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki (EALA) Dk. Margaret Nantongo Zziwa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari katika ofisi za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dar es Salaam jana juu ya mkutano wa kwanza wa Bunge la tatu unaofanyika ukumbi wa Karimjee. Wengine kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Amantius Msole, wabunge wa EALA kutoka Tanzania Twaha Taslima na Shy Rose Banji
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Wabunge kutoka Tanzania, Adam Kimbisa, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika ofisi za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dar es Salaam leo, juu ya mkutano wa kwanza wa Bunge la tatu unaofanyika ukumbi wa Karimjee. Kushoto ni Spika wa Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki (EALA) Dk. Margaret Nantongo Zziwa,wabunge wa EALA kutoka Tanzania, Twaha Taslima na Shy Rose Banji. PICHA ZAIDI --FATHER KIDEVU BLOG

RAIS KIKWETEA AZINDUA BARABARA YA DUMILA-RUDEWA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe pamoja na Makamu mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa barabara ya Dumila-Rudewa yenye urefu wa Kilomita 45 iliyojengwa kwa kiwango cha lami.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifungua jiwe la msingi kuashiria ufunguzi rasmi wa Dumila-Rudewa yenye urefu wa Kilomita 45 iliyojengwa kwa kiwango cha lami.

 Sehemu ya barabara ya Dumila-Rudewa yenye urefu wa Kilomita 45 iliyojengwa kwa kiwango cha lami.

Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na baadhi ya Watendaji kutoka Wizara ya Ujenzi ambao walikuwa wakisubiri tukio la ufunguzi wa barabara ya Dumila-Rudewa yenye urefu wa Kilomita 45 uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe kushoto akiwa pamoja na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale wakitazama ramani pamoja na picha mbalimbali za barabara ya Dumila-Rudewa yenye urefu wa Kilomita 45 iliyojengwa kwa kiwango cha lami.

Mc Mavunde kulia akiwatambulisha watendaji mbalimbali kutoka Wizara ya ujenzi kabla ya Ufunguzi rasmi wa barabara ya Dumila-Rudewa

Sehemu ya wakazi wa Dumila waliojitokeza kwa wingi wakimsiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete licha ya giza kuingia mjini Dumila.

SEKONDARI YA MAKETE GIRLS YATII MAAGIZO YA MKUU WA WILAYA

$
0
0
 Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro akizungumza na wanafunzi wa Makete Girls Sekondari (hawapo Pichani) na pia kutoa maagizo kwa uongozi wa shule.

Shule ya sekondari ya wasichana (Makete Girl's) imetii agizo la mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro la kutaka wanafunzi hao wapewe uji mara baada ya vipindi viwili vya asubuhi badala ya saa nne agizo alilolitoa Agosti 8 mwaka huu

Hali kadhalika mkuu huyo aliagiza wapewe chakula cha mchana saa saba ili kuweka uwiano mzuri wa muda wanaokula wanafunzi hao wawapo shuleni hapo

 Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi na walimu wa shule hiyo.
Mwandishi wetu aliyefika shuleni hapo ijumaa ya Agosti 22, ameshuhudia maagizo hayo yakitekelezwa jambo ambalo limepongezwa kwa kiasi kikubwa na wanafunzi hao

"Ni kweli tumeshuhudia ratiba ya chakula ikibadilika kama alivyoagiza mkuu wa wilaya aliyokuja hapa shuleni, na kweli tunaona ni afadhali na tutajisomea vizuri na limetekelezwa mara tu alivyoagiza hivyo naupongeza uongozi wa shule kwa kutekeleza hilo" alisikika akisema mwanafunzi mmoja

Katika hatua nyingine shirika la sumasesu limetoa elimu ya ujinsia kwa wanafunzi hao na kuwataka kujiepusha na vitendo vya ngono ilihali wao ni wanafunzi ili waweze kufikia malengo yao
Rai hiyo imetolewa na Bi Anifa Mwakitalima na kusema kuwa wao ni wanafunzi wa kwanza katika shule hiyo na wanategemewa kufaulu na kuweka sifa nzuri kwa wilaya, hivyo itakuwa nia aibu kubwa kwa mwanafunzi kuweka historia ya kuwa mwanafunzi wa kwanza kusoma katika shule hiyo na pia akawa wa kwanza kupata mimba na kufukuzwa shule

"Ninani anayependa awe wa kwanza kupata mimba na kuandika historia mbaya kwa shule? bila shaka hakuna, wadogo zangu nawaomba mzingatie masomo achaneni na ngono kabisa muda wenu bado, huu ni muda wa kusoma" alisema Mwakitalima
Kwa upande wake Faustine Mwenda amewataka wanafunzi hao kujitambua kuwa wamepelekwa shuleni kwa ajili ya kusoma hivyo wajisomee na watafaulu vizuri hivyo kujijenge amsingi mzuri wa maisha pasipo kupata shida

Amesema mafanikio yao yanajengwa na wao wenyewe hivyo endapo wataonesha uzembe wa kupuuzia masomo ni dhahiri kwamba wataharibu malengo yao, hivyo wanatakiwa kushika elimu na si mambo mengine yanayoweza kuwasababisha wasifikie malengo yao ikiwemo kupata ujauzito.
Makete girls ni sekondari pekee na ni mpya ya wasichana iliyoanzishwa mapema mwaka huu wilayani hapo ambapo kwa sasa ina jumla ya wanafunzi 36.Na Edwin Moshi, Makete.

ALIYEKUWA MSHINDI WA SHINDANO LA MWANAMAKUKA 2013 AFARIKI DUNIA JIJINI DAR.

$
0
0

  
Marehemu Bi Aziza enzi za uhai wake.
Kikundi cha Unity Of Women Friends,Kupitia mradi wao wa Mwanamakuka Awards  na Washirika wake,Benki ya Wanawake TWB na Clouds Media Group,Wana tangaza kwa masikitiko makubwa ya kumpoteza mshindi wa mwaka jana 2013,Bi Aziza  Mbogolume (pichani).
Bi Aziza amefarika mapema jana mchana jijini Dar es salaam,mazishi yake yanatarajiwa kufanyika leo mnamo majira ya saa 9,na msiba upo nyumbani kwake Magomeni mwembechai.Aziza alikuwa ni Mwanamke jasiri mwenye uthubutu wa kufanya biashara kupitia kipaji chake cha Kuchora .
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI  PEMA PEPONI-AMIN

http://1.bp.blogspot.com/-pWV9rBQ6zSU/UTsAJzwBYSI/AAAAAAAEMbs/wIoMPtgWHwc/s1600/03.jpg
Aziza Mbogolume (wa pili kulia) enzi za uhai wake wakati akipokea mfano wa hundi baada ya kushinda tuzo ya Mwanamakuka 2013 kutoka kwa Mke wa Makamu wa Rais, Aisha Bilal.
http://4.bp.blogspot.com/-6hZqPBN8luU/UW3H0k0LiQI/AAAAAAACIkY/j9xLijjnl2k/s640/DSC_3104.JPG
Baadhi ya viongozi waratibu wa shindano la Tuzo za Mwanakuka wakistaajabia kazi za mikono ya Aziza Mbogolume (wa pili toka kushoto) enzi za uhai wake katika maonesho ya mwaka huu yaliyofanyika Escape 1 Mikocheni jijini Dar


RAIS KIKWETE ATEMBELEA CHUO KIKUU CHA MZUMBE, MOROGORO

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua jengo la mihadhara la Chuo Kikuu cha Mzumbe Morogoro akisaidiwa na uongozi wa chuo hicho alipotembelea hapo na kuzindua ukumbi wa huo jengo la wahadhiri chuoni hapo Agosti 25, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wanafunzi, wahadhiri na wananchi katika Chuo Kikuuu cha Mzumbe Morogoro baada ya kuzindua ukumbi wa mihadhara na jengo la wahadhiri chuoni hapo Agosti 25, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi ya picha yake ya kuchorwa wakati alipotembelea Chuo Kikuu cha mzumbe ambapo walihutubia wanafunzi, wahadhiri na wananchi katika chuo hicho baada ya kuzindua ukumbi wa mihadhara na jengo la wahadhiri chuoni hapo Agosti 25, 2014.
Meza kuu ikifurahia jambo wakati Naibu Waziri wa Maji na Mbunge wa Mvomero Mhe Amos Makalla akipohutubia wanafunzi, wahadhiri na wananchi katika chuo hicho wakati Rais Kikwete alipotembelea na kuzindua ukumbi wa mihadhara na jengo la wahadhiri chuoni hapo Agosti 25, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea risala toka kwa Rais wa Serikali ya Wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Mzumbe Mhe Boniface Maiga wakati Rais Kikwete alipotembelea na kuzindua ukumbi wa mihadhara na jengo la wahadhiri chuoni hapo Agosti 25, 2014.
Rais wa Serikali ya Wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Mzumbe Mhe Boniface Maiga akisoma risala wakati Rais Kikwete alipotembelea na kuzindua ukumbi wa mihadhara na jengo la wahadhiri chuoni hapo Agosti 25, 2014.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Morogoro wakiweka kumbumbuku ujio wa Rais Kikwete alipotembelea hapo na kuzindua ukumbi wa huo jengo la wahadhiri chuoni hapo Agosti 25, 2014.
Umati wa wanafunzi, wahadhiri na wananchi wakimsikiliza Rais Kikwete akiwahutubia alipotembelea hapo na kuzindua ukumbi wa huo jengo la wahadhiri chuoni hapo Agosti 25, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa serikali ya wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Mzumbe mjini Morogoro baada ya kuwahutubia chuoni hapo Agosti 25, 2014.

BENKI YA CRDB YALETA UFANISI KATI YA WAFANYABIASHARA, WAWEKEZAJI WA CHINA NA TANZANIA

$
0
0
 Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB anayeshughulika na huduma ya China Deski, Ibrahim Masahi (kulia), akitoa ufafanuzi kuhusu huduma maalum za kibenki kwa ajili ya kusaidia wafanyabiashara na wawekezaji wa China na Tanzania, wakati wa maonyesho ya bidhaa za China yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. 
 Baadhi ya wateja wakisoma vipeperushi vyenye taarifa muhimu za Benki ya CRDB kuhusu huduma maalum ya China Deski.
 Baadhi ya watu waliofika katika banda la CRDB wakati wa maonyesho ya bidhaa za China wakisoma vipeperushi vyenye taarifa muhimu kuhusu huduma maalum ya China Deski.
 Ibrahim Masahi akitoa ufafanuzi kwa wateja waliotaka kujua huduma za China Deski.
Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB anayeshughulika na huduma ya China Deski, Ibrahim Masahi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu huduma maalum za kibenki kwa ajili ya kusaidia wafanyabiashara na wawekezaji wa China na Tanzania, wakati wa maonyesho ya bidhaa za China yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu
  
BENKI ya CRDB, imeeleza kupata faida baada ya kuanzisha deski la China kwa kuwaunganisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka China na hapa nchini.

Akizungumza jana katika maonyesho ya bidhaa za China Afrika, yanayofanyika jijini Dar es salaam, Meneja Uhusiano wa Deski hilo, Ibrahim Masahi, alisema kuwa huduma hiyo imerahisisha na kuwasaidia wafanyabiashara kupata mikopo na kufanya huduma za kibenki, kukuza wigo wa kibiashara.

Masahi alisema kuwa huduma hiyo umuwezesha mteja wa CRDB kutoa hadi kiasi cha sh milioni 40 kwa siku ikiwa atakuwa nchini China au Tanzania kwaajili ya biashara na kuwekeza.

“Tangu kuanza kwa hudyma hii benki kupitia deski la China imepata faida ya zaidi ya Bilioni 30, na imeunganisha wateja mbalimbali na wawekezaji wanaonunua bidhaa china, lakini kwa upande wa Tanzania Chnagmoto kubwa ni lugha wakiwa kule China na rate imekuwa ikibadilikabadilika,”alisema. 

Aidha aliwataka watanzania kuchangamikia fursa hiyo ambayo imeondoa madhara ambayo yangeweza kutokea na kueleza kuwa kwasasa wameingia ubia na benki zaidi ya 10 nchini China.

TBL YAKABIDHI MSAADA WA KISIMA CHA MAJI KATA YA KING'ONGO,DAR

$
0
0
 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa King'ongo, Demetrius Mapesi (kulia),akimtwisha ndoo ya maji Radhia Said baada ya kuzindua mradi wa kisima cha maji mwishoni mwa wiki kilichojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika Kata ya King'ongo, wilayani Kinondoni, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kisima hicho kimejengwa kwa msaada wa TBL. Kushoto ni Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Kinondoni, Joseph Nicholaus
 Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Kinondoni, Joseph Nicholaus (kushoto) na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa King'ongo, Demetrius Mapesi wakifunua pazia ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa kisika cha maji kiolichojengwa kwa gharama ya sh. mil. 29  kwa msaada wa TBL katika Kata ya King'ongo, wilayani Kinondoni, Dar es Salaam. Wanaopiga makofi ni wananchi wa eneo hilo wakionekana kufurahishwa na msaada huo muhimu kwani wataondokana na tatizo la maji ambapo walikuwa wakitembea zaidi ya KM 2 kununua maji ndoo moja sh. 700. Katika Kisima hicho watakuwa wananunua ndoo moja ya maji kwa sh. 50.
 Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Kinondoni, Joseph Nicholaus, akifungua maji kwenye bomba lililounganishwa kwenye kisima hicho. Kisima hicho kina uwezo wa  kutoa zaidi ya lita 5000 za maji kwa saa. PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

 Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Kinondoni, Joseph Nicholaus (kushoto), akimtwisha Cecilia Dominic ndoo ya maji baada ya kuzindua mradi wa kisima cha maji katika Kata ya King'ongo, wilayani Kinondoni, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kisima hicho kimejengwa kwa msaada wa TBL.
  Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Kinondoni, Joseph Nicholaus (kushoto), akimtwisha Rehema Mohamed  ndoo ya maji baada ya kuzindua mradi wa kisima cha maji katika Kata ya King'ongo, wilayani Kinondoni, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kisima hicho kimejengwa kwa msaada wa TBL.
 Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Kinondoni, Joseph Nicholaus (kushoto), akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa akina mama wa Kata hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya MO Resources Ltd, Onesmo Sigalla 9kushoto) akimkabidhi kufuli na funguo pamoja na nyaraka zinginezo za kisima hicho, Meneja Mauzo wa TBL, Kanda ya Kinondoni, Joseph Nicholas ambaye pia alimkabidhi Mwenyekiti Mwenyekiti wa Serikali ya Mataa wa King'ongo, Mapesi (kulia). Kampuni hiyo ndiyo iliyopewa tenda ya kujenga kisima hicho.
 Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Kinondoni, Joseph Nicholaus (wa pili kushoto), akipongezwa na mwananchi wa kata hiyo, Abdalah Mangosongo kwa msaada huo wa TBL.
Ofisa Uhusiano wa TBL, Dorris Malulu (kushoto), akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, ambapo alisema kuwa TBL, mwaka huu imetenga sh. mil. 700 kwa ajili ya kuisaidia jamii nchini kuboresha sekta ya maji.

DJ Peter Moe na Team yake Pamoja na King Kiki @ Escape One Ijumaa Hii- Afrika Bambaataa

MO AZINDUA JARIDA LA IRIS EXECUTIVE NA KUSEMA UTAJIRI HAUJI "KIRAHISI RAHISI"

$
0
0
DSC_0425
DSC_0428
|It's now official launched".....Ofisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mh. Mohammed Dewji "MO" (Mb) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Maendeleo cha IRIS Executive Development Centre ambao ndio wamiliki wa jarida la IRIS Executive, Phylisiah Mcheni wakifurahi pamoja baada ya uzinduzi rasmi wa jarida hilo.
DSC_0445
Ofisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mh. Mohammed Dewji "MO" (Mb) akikata keki maalum iliyoandaliwa kusindikiza uzinduzi huo.
DSC_0451
Mgeni rasmi Ofisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mh. Mohammed Dewji "MO" (Mb) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa jarida la IRIS Executive. Kutoka kushoto ni Ofisa uhusiano na raslimaliwatu wa IRS Exexcutive, Beatrice Silayo, Jokha Sadiki, Ofisa Mtendaji Mkuu waKituo cha Maendeleo cha IRIS Executive Development Centre ambao ndio wamiliki wa jarida la IRIS Executive, Phylisiah Mcheni, Ofisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mh. Mohammed Dewji "MO" (Mb),Mhariri Mtendaji wa jarida la IRIS Executive, Mike Mina, Meneja Masoko wa jarida la IRIS Executive, Alinda Henry na Ofisa anayeshughulikia masuala ya Fedha wa jarida la IRIS Executive Bw. George Saltai.

Mwanza cyclists shine in ABG Cycle Challenge 2014

$
0
0
 The Deputy Minister for Information, Youth, Culture and Sports, Juma Nkamia (second left) hands over a trophy to Masunga Duba (right) a cyclist from Mwanza shortly after being announced winner of the ABG Cycle Challenge during the 156.6 km men’s race. Looking on at the left is the African Barrick Gold (ABG) Vice President Corporate Affairs Deo Mwanyika and the Cycling Association of Tanzania (CAT) Chairperson Jax Mhagama (second right).
 The African Barrick Gold (ABG) Vice President Corporate Affairs Deo Mwanyika (left) shakes hands with the ABG Cycle Challenge second runner up Simon Mbaruku (second right) during the lake Zone cycling competition sponsored by his company. Looking on second left is the Deputy Minister for Information, Youth, Culture and Sports, Juma Nkamia.
 The ABG Cycle Challenge first runner up Seni Konda (second left) celebrates after receiving a trophy, medal and one million shilling cash prize during the award ceremony to climax the event. Looking on at the left is the African Barrick Gold (ABG) Vice President Corporate Affairs Deo Mwanyika and the Cycling Association of Tanzania (CAT) Chairperson Jax Mhagama (second right).
The African Barrick Gold (ABG) Executive General Manager Planning and Business Improvement Michelle Ash (second left) poses for a group photo with ABG Cycle Challenge women’s race winners shortly after presenting awards to them. Looking on at the right is the ABG Public & Communications Manager, Nector Foya. Martha Anthony (third left) a cyclist from Mwanza emerged winner of the women’s race.


 ABG Cycle Challenge 2014 winners and runners up (first row) poses for a group photo with Deputy Minister for Information, Youth, Culture and Sports, Juma Nkamia ( fourth, second row ) and other invited guests shortly after the award ceremony of the event.
 


 The Cycling Association of Tanzania (CAT) Chairperson Jax Mhagama (right) shares a light moment with the African Barrick Gold (ABG) General Manager Sustainability (left) during the ABG Cycle Challenge held in Kahama at the weekend
 The Buzwagi Gold Mine General Manager Philber Rweyemamu (left) shares a light moment with the Deputy Minister for Information, Youth, Culture and Sports, Juma Nkamia (right) during the climax of the ABG Cycle Challenge in Kahama at the weekend.
 A cross section of ABG employees and Kahama Town Council officials take part in the ABG Cycle Challenge Fun race during the ABG Cycle Challenge held in Kahama at the weekend.
 The Deputy Minister for Information, Youth, Culture and Sports, Juma Nkamia (fourth right, first row) prepares to take part in the ABG Cycle Challenge Fun Race during the climax of the Lake Zone Cycling competition held in Kahama at the weekend. Fourth at the right is the African Barrick Gold (ABG) Vice President Corporate Affairs Deo Mwanyika.
 A cross section of ABG Cycle Challenge organizing committee poses for a photo during the climax of the event in Kahama at the weekend.
 A cross section of ABG Cycle Challenge men’s 156.6 km participants take part in the cycling completion organized by the Cycling Association of Tanzania in partnership with African Barrick Gold (ABG) that brought together more that 240 cyclists from the Lake Zone areas.
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images