Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

wakazi wa jiji la dar waupongeza mkoa huo kuwa wa kwanza tamasha la pasaka.

$
0
0
Muimbaji mahiri wa nyimbo za kiroho,kutoka nchini DRC-Kongo,Solomoni Mukubwa akiwasalimia mashabiki wake waliofika kwenye uwanja wa Taifa,kushiriki pamoja tamasha la pasaka lililofanyika mwaka jana,ambapo pia mwaka huu limepangwa kufanyika uwanjani hapo mnamo Machi 31.
=======  =====  =======
 WAKAZI wa jijini Dar es Salaam wamepongeza mkoa wao kuwa wa kwanza kuchaguliwa kupata nafasi ya kuandaa tamasha la mwaka huu kwa sababu limezingatia matakwa ya mashabiki ya tamasha hilo. Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wakazi hao walisema mfumo wa upigaji kura kwa njia ya sms unaofanyika kwa sasa unasaidia wadau kupigia kura mikoa yao.

Eunice Muhandia alisema inaonyesha Dar es Salaam kuwa na wakazi wengi hali ambayo imesababisha kupata nafasi ya kwanza, ingawa hata Mwanza na Arusha kuna idadi ya wakazi inayokaribiana na Dar es Salaam, hivyo mikoa mingine iongeze kasi ya upigaji kura ili wapate fursa ya kuandaa tamasha hilo.


Muhandia alisema kwa mfumo ulioanza mwaka huu, utaliimarisha zaidi kutokana na kuwashirikisha wadau ambao ndio wenye tamasha lao. Naye Janeth Christopher ambaye ni muimbaji wa injili chipukizi alisema fursa ya kuwapata waimbaji watakaoshiriki itawasaidia kwa sababu walikuwa hawana namna ya kuweza kupata nafasi ya kushiriki.


Janeth alisema awali walidhani kwamba, tamasha linaendeshwa kwa mfumo wa mtu mmoja ambaye ni Alex Msama kumbe linatushirikisha hata sisi wadau, jambo ambalo anaipongeza kamati ya maandalizi kwa kuwaona.


Aidha wakati taratibu za maandalizi ya tamasha hilo zikiendelea, wadau wanatakiwa kupiga kura katika mikoa yao ili kukamilisha mikoa takribani saba ambayo inategemewa kufikiwa na tamasha hilo, wadau wanatakiwa kupiga kura kwa kuandika neno gospo halafu jina la mkoa unaotaka lifanyike na utume kupitia namba 15522.   


Wakati zoezi hilo likifanyika, litakalofuata ni zoezi la kuwapata waimbaji washiriki  ambao nao watapatikana kwa kuandika neno gospo, jina la mwimbaji, kikundi au kwaya na kuituma kwenda namba 15678.  



TAMKO LA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOA WA MBEYA KUHUSU UCHOCHEZI WA KIDINI

$
0
0

Kwanza kabisa tungependa kutoa pongezi kwa Viongozi na Waumini wa Dini na Madhehebu mbalimbali hapo Mkoa Mbeya kuendeleza utamaduni wetu wa kuishi na kushirikiana katika shughuli mbalimbali za kijamii. Bila kuweka hisia za udini. Tunawashukuru kwa kuendelea kuvumiliana. Pamoja na kuendelea katika hali hii, kumejitokeza viashiria mbalimbali vyenye kuonyesha dalili za kumomonyoka kwa maadili, katika Mkoa wetu.

    2.   Kumejitokeza baadhi ya viongozi wa dini ambao wamekuwa   

Wakuzitumia nyumba zetu takatifu za Ibada kuhubiri mambo  ambayohayahusiani kabisa na mambo yanayohusu Mwenyezi Mungu na mafundisho yake, kwa kuhubiri mambo ya siasa za chuki kwa dhamira ya kupandikiza chukidhidi ya Serikali au dini na madhehebumengine. Baadhi yao wamediriki kuyasema hayo hadharani kwenye miadhara yao au mikusanyiko ya waumini wao.


   Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mbeya inaona hali hii haina  

   afya njema kwa mustakabali wa amani na utulivu wa Mkoa wetu na    

   Nchi kwa ujumla.


3.               Pamoja na mahubiri hayo pia kumekuwepo nyaraka mbalimbali za kimaandishi za sauti katika kanda, CD zenye kuhubiri chuki, uchochezi dhidi ya dini au dhehebu lingine. Kumekuwepo na video katika kanda, CD au DVD zenye kuhubiri chuki, uchochezi, dharau na kebehi dhidi ya dini nyingine au Serikali na baadhi ya kanda hizo zimediriki kuhamasisha waumini wake vurugu na hata kuua jambo ambalo Kamti ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mbeya inaamini hakuna dini ya aina yoyote dunianiinayohimiza waumini wote kutumia kwa jambo lolote lile.

4.               Baada ya kutafakari, Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa  Mbeya imeamua yafuatayo:- inapiga marufuku:


(i)               Kuuza, kusambaza au kuonyesha, Kanda za sauti CD za sauti, Kanda   

za Video, CD, DVD, nyaraka na maandiko yoyte yenye uchochezi wa aina yoyote ile au kukashifu dini yeyote katika Mkoa wa Mbeya.


(ii)             Chombo chochote cha Habari kilichopo Mkoani Mbeya kiepuke   

           kuandika makala, kunakili au kurusha hewani hotuba, mahubiri au   

           kuonyesha video zenye kuchochea, kudharau, kuhubiri au kukashifu 

           dini yoyote ile 

 

 
5.       Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa inawaasa viongozi wa dini

 Mbalimbali kutohubiri siasa kwenye majumba ya Ibada kwani kwa   

 kufanya hivyo watakuwa wanakiuka sheria za nchi. Mtawagawa       

 waumini wenu kwa sababu waumini wanaelewa hayo si maagizo ya 

 Mungu, na hayamo kwenye vitabu vitakatifu.


6.       Waandishi wa Habari epukeni kushabikia matamko ya Viongozi wa   
          Dini au Siasa yenye kulenga kuleta mgawanyiko katika taifa hili kwa  

          Misingi ya kidini au kisiasa kwa kisingizio cha Uhuru wa Habari,  

          kumbukeni Amani Umoja na Mshikamano wa Mkoa na Taifa

          utategemea mchango wenu katika kushabikia au kukemea kauli hizo

          bila kujali zimetolewa na kiongozi gain.


Mwisho, Serikali itamchukulia hatua za kisheria mtu yeyote atakayekwenda kinyume na haya, bila kujali itikadi yake, dini yake au wadhifa wake. Wananchi wanaaswa kuzikabidhi nyaraka, kanda CD na DVD kwa ofisi za Serikali ngazi ya Vijiji, kata Wilaya na Mkoa au kituo chochote cha Polisi. Endapo watakabidhi kwa hiyari hawatachukuliwa hatua.


Imetolewa na:


MWENYEKITI

KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOA-MBEYA

Ophir yamwaga sembe na saruji ya Sh. Mil. 13 Mtwara

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bw Wilman Kipenjam Ndile akitoa shukrani kwa kampuni ya Ophir Energy plc mara baada ya kupokea msaada wa chakula na saruji vyote vikiwa na thamani ya Sh Mil 13.2, kwa ajili ya wahanga wa mafuriko wilayani humo.Wengine pichani ni Meneja Uhusiano wa Kampuni hiyo Bw Fidelis Lekule(kushoto) na mwakilishi wa wahanga hao mlemavu wa macho Bw Mohammed Omari.(Picha ya Executive Solutions). 
Mkuu wa wilaya ya Mtwara Bw. Wilman Kipenjama Ndile(kulia) akipokea msaada  unga na simenti kutoka kampuni ya Ophir Energy Plc vyote vikiwa na thamani ya Sh Mil 13 kwa ajili ya waahanga wa mafuriko wilayani humo. Msaada huo ulikabidhiwa na Meneja Uhusiano wa Kampuni hiyo Bw Fidelis Lekule(kushoto).
======  =======  =========

Ophir yamwaga sembe na saruji ya Sh. Mil. 13 Mtwara

Na Ripota Wetu,Mtwara.

KAMPUNI ya kimataifa ya utafiti wa mafuta na gesi nchini Tanzania, yenye visima uwepo mkubwa mkoani Mtwara, Ophir Energy plc jana imekabidhi msaada wa sembe na saruji vyenye thamani ya Sh Mil 13.2m, kwa ajili ya wahanga wa mafuriko yaliyoikumba wilaya hiyo hivi karibuni.

Akikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Meneja wa Uhusiano Fidelis Lekule alisema kampuni ayke imeguswa na janga lililowapata wana-Mtwara ndiyo maana wameamua kutoa msaada huo. “Ukweli ni kwamba Ophir Energy inafanya kazi Mtwara pamoja na sehemu nyingine duniani, hivyo matatizo na mafanikio ya wilaya hii yanaigusa kampuni kwa namna moja au nyingine,” alisema Bw Lekule.

Kwa mujibu wa Lekule, msaada huo unajumuisha magunia 280 ya unga wa sembe ili kuwapa chakula wahanga hao wa mafuriko ambao chakula chao kilisombwa na maji ya mvua na pia mifuko 300 ya saruji kwa ajili ya kukarabati miundombinu iliyoharibiwa ikiwa ni pamoja na makalivati na mfumo wa mifereji ya maji katika manispaa hiyo. Akipokea msaada huo, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Wilman Kapenjama Ndile, aliishukuru kampuni ya Ophir Energy kwa msaada huo na kusema umekuja wakati muafaka ili kusaidia wananchi wenye shida wilayani Mtwara.

Akizungumzia ukubwa wa tatizo, Mkuu wa Wilaya alisema kuwa mafuriko hayo kumbukumbu zinaonyesha kuwa hayajawahi kutokea Mtwara katika miaka 30 iliyopita, yalisababishwa na mvua kubwa iliyonyesha katikati ya Januari mwaka huu.

Alisema: “Takwimu zinaonyesha kuwa mafuriko hayo yaliathiri zaidi ya watu 7,000, nyumba 210 zilibomolewa na zingine 385 ziliharibiwa kwa njia moja au nyingine. Ndile alisema kuwa ofisi yake iko mbioni kutengeneza vyeti vya shukrani vitavyotumika kuwatambua watu waliojitokeza kusaidia wananchi wa Mtwara ikiwa ni pamoja na kampuni ya Ophir, wakati wa kipindi hicho cha matatizo.

Mkazi mmoja wa Mtwara mwenye ulemavu wa kutoona ambaye aliwawakilisha wahanga wengine wa mafuriko hayo katika hafla hiyo fupi ya kupokea msaada, Mohammed Omari, alishukuru kampni ya Ophir kwa msaada huo ambao umekuja katika kipindi muafaka na kupitia ofisi ya Mkuu wa Wilaya, “Nyumba yangu ilikumbwa na mafuriko. Chakula changu na mali zingine za thamani  zilizokuwemo ndani ya nyumba viliharibiwa kabisa,” alilalamika mlemavu huyo kwa masikitiko makubwa. 

Mbeya yapewa mikoba Tamasha la Pasaka

$
0
0
MKOA wa Mbeya nao umechaguliwa kubeba jahazi la kufanyika Tamasha la Pasaka Aprili mosi mwaka huu.

Mapema wiki hii waandaaji wa tamasha hilo walisema kuwa siku yenyewe ya sikukuu ya Pasaka, Machi 31 litafanyika jijini Dar es Salaam na kwamba walikuwa wakihangaika kutafuta mahali litakapofanyika siku inayofuata. 

“Tumekubaliana kuwa Jumatatu ya Pasaka, ambayo itakuwa Aprili mosi, tamasha letu lifanyike mkoani Mbeya. Hivyo tayari tumepata mikoa miwili ambayo tamasha litafanyika bado mingine mitano.

“Mkoa wa Mbeya umechukua jukumu la kufanyika Jumatatu ya Pasaka kutokana na idadi kubwa ya mashabiki waliokuwa wameomba awali siku yenyewe ya tamasha ifanyike mkoani  humo, lakini kwa kuwa Dar es Salaam iliongoza tukaamua Mbeya iliyoshika nafasi ya pili basi ipewe jukumu la kuandaa Jumatatu ya Pasaka,” alisema Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo,Bwa. Alex Msama.

Alisema kamati yake ilikuwa ikiendesha kura za maoni kwa mashabiki wao wa eneo lipi tamasha hilo lifanyike na kwamba Dar es Salaam na Mbeya ndizo zimeshika nafasi za juu.

Alisema dhamira yao mwaka huu ni kufanya matamasha katika mikoa saba tofauti, hivyo bado wanajipanga kuona maeneo mengine ambapo tamasha hilo linaweza kutumbuiza.

IN THE MEMORY OF OUR BELOVED MUM ESTHER NYIMBO BADI

$
0
0


IN THE MEMORY OF OUR BELOVED MUM ESTHER NYIMBO BADI

It is exactly one year today since the fateful Wednesday, 22nd February 2012 at 6.30 p.m when you left us without a word of "kwaheri". We continue to celebrate your life  our beloved mother Esther Nyimbo Badi. The pain of loosing you, Mum, still remains fresh in our hearts. Mum, no words are sufficient to describe the significant role you played in our lives; your discipline and leadership qualities greatly influenced the lives of all  children who passed through your hands. You were a great pillar in our family.

Days may break and night may fall; seasons may start and seasons may end; years may come and years may go; but your memory lives in our hearts, perpetuated by the destiny of time.

You are profondly remembered and cherished by your children Blandina, Bertha, Stella, Joseph, Lilian, John and Upendo; your in-laws Cashmir, Modest, James, Ken and Afro; your grand children  Kim, Abraham, Faith, Jeff, Deborah, Larry, Caleb, Karen, Sarah,  Brandon, Dillan, Esther and Suzana.

Mum in God’s hands  rest in peace, in our hearts you live forever.
May the Lord shower you with favor until we meet again. 

Psalm 103: 1  ‘Bless the Lord o my soul, and that all that is within me, bless His holy name’.

Montage Charity Ball kufanyika leo jioni serena hotel

$
0
0
Pichani ni baadhi ya Wasanii watakao tumbuiza kwenye tafrija ya Montage Charity Ball itakayofanyika jioni ya leo ndani ya Serena Hotel,jijini Dar.Kutoka kushoto ni Peter Msechu,Kidumu kutoka Kenya,Barnaba pamoja na Deo Mwanambilimbi ambaye ni kiongozi wa Kulunde Band.
Pichani shoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Montage,Teddy Mapunda (katikati) akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea kufanyika kwa tafrija maalum ya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wanawake wenye matatizo ya afya hapa nchini kupitia mfuko wa Montage Charity Ball,itakayofanyika jioni ya leo, Februari 22 kwenye Hoteli ya Serena,jijini Dar es Salaam


Aidha Teddy ameeleza kuwa malengo hasa ni kukusanya kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 100 kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Wanawake wenye matatizo mbali mbali.Mgeni rasmi katika Tafrija hiyo anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA),Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.Kulia kwake ni baadhi ya Wasanii watakaotumbuiza kwenye tafrija hiyo ambao ni Kidumu kutoka Kenya,Barnaba pamoja na Deo Mwanambilimbi ambaye ni kiongozi wa Kulunde Band na Peter Msechu ambaye hayupo pichani.

WADAU WA PSPF WAONESHWA NYUMBA ZA MKOPO ZILIZOPO BUYUNI CHANIKA

$
0
0


Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) umekamilisha awamu ya kwanza ya ujenzi wa nyumba 641 katika mikoa mitano ambazo zilianza kuuzwa tangu Novemba mwaka 2012. Mradi huo unalenga kutatua tatizo la makazi kwa wanachama wake na jamii kwa ujumla.

Mikoa iliyojengwa nyumba hizo na idadi ya nyumba katika mabano ni Dar es salaam – Buyuni (491), Morogoro – Lukobe (25), Shinyanga – Ibadakuli (50), Tabora – Usule (25) na Mkoa wa Mtwara – Mang’amba (50).

Aidha kwa Mujibu wa maelezo ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bwana Adam Mayingu amewaambia wanandishi wa habari na viongozi mbalimbali waliotembelea eneo la mradi huo Mkoa wa Dar es Salaam kuwa Shirika lake limejenga nyumba za aina nne ambazo ni za nyumba viwili, Vyumba vitatu, Nyumba za vyumba vitatu kimoja ikiwa ni Master na Nyumba ya vymba vine kimoja kikiwa ni Master.

Gharama ya ununuzi wa nyumba hizo ambazo zinauzwa kwa wanachama wa Mfuko huo ni kati ya Shilingi Milioni 64 hadi milioni 94 gharama zikijumlishwa na Kodi ya ongezejo la Thamani.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) Adam Mayingu (katikati) akiwaonesha maofisa wa Jeshi la Polisi moja ya nyumba 491 zilizopo katika mradi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu ambazo zitkopeshwa kwa wanachgama wa mfuko huo. Nyumba hizo zipo katika eneo la Kigezi Kata ya Majohe wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) Adam Mayingu (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa ziara hiyo ya kuakagua makazi hayo. Kulia ni  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Hery Mohamed Kessy Nyumba hizo zipo katika eneo la Kigezi Kata ya Majohe wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.
 Wadau mbalimbali wakitembelea nyumba hizo hii leo.

 Ziara ikiendelea katika nyumba hizo zipatazo 491

<!--[if gte mso 9]>

GLORIOUS WORSHIP TEAM KUADHIMISHA MIAKA 2 J'PILI HII ATRIUMS HOTEL

$
0
0
HTML
Mmoja wa kiongozi wa kundi la 'Glorious Worship Team akiongea jambo na Wandishi wa habari hawapo pichani
Kundi la 'Glorious Worship Team, wakiimba nyimbo.
WASANII wa kundi la nyimbo za injili nchini 'Glorious Worship Team' keshokutwa Jumapili, Februari 24 mwaka huu wataadhimisha sherehe ya kutimiza miaka miwili ya kueneza injili ndani ya Ukumbi wa Hoteli ya The Atrium, iliyopo Sinza Afrika Sana. Kiingilio katika hafla hiyo ni shilingi 5,000/= na wote mnakaribishwa.

SEMINA YA MAFUNZO UNESCO yafungwa rasmi leo zanzibar

$
0
0


Mkurugenzi wa Habari Maelezo Zanzibar Omar Yussuf Chunda amesema njia pekee ya kuwawezesha Wanahabari kufanya majukumu yao kwa ufanisi mkubwa ni kupatiwa mafunzo ya mara kwa mara ya kuwajengea uwezo katika fani yao.

Amesema mafunzo ndio njia muhimu ya kuwafahamisha Wanahabari mabadiliko na mbinu muhimu zinazotumika katika uandishi wa kisasa wenye lengo la kuhudumia jamii kikamilifu.

Mkurugenzi Chunda ameyasema hayo alipokuwa akifunga Semina ya siku tano ya kuwajengea uwezo Waandishi wa Idara yake katika Ukumbi wa Wizara ya Habari Kikwajuni mjini Zanzibar

Amesema fani ya habari  hubadilika katika mifumo tofauti ya kiuandishi na kwamba ujuzi huo unahitajika ili kuwawezesha Waandishi kufanya kazi kwa ari na kasi kubwa. Mkurugenzi Chunda ameongeza kuwa Idara yake pia inatarajia kuwapatia mafunzo Wanahabari mwezi April mwaka huu kupitia ufadhili wa Ubalozi wa Uingereza Nchini.

Aidha Chunda amewataka Washiriki wa Semina hiyo kuyatumia vizuri mafunzo waliyoyapata ili yaweze kuwasaidia katika kufanya majukumu yao ya kila siku. Mapema Mkufunzi wa Mafunzo hayo Salim Said Salim aliwataka waandishi hao kufichua maovu yanayotokea katika jamii sambamba na kuzingatia maadili ya kazi zao.

Amesema Zanzibar kuna maovu mbalimbali ambayo hutendeka na kwamba Waandishi ndio watu muhimu wa kuyafichua ili kuilinda jamii na matatizo hayo. Ameongeza kuwa Ufisadi unaofanywa na baadhi ya watu haupaswi kufumbiwa mamcho kwani kufanya hivyo ni kusaliti maslahi ya taifa.

“Nakuombeni fanyeni uchunguzi wa kubaini ufisadi na maovu yanayofanyika ili kuinusuru Zanzibar na maovu hayo kinyume na hivyo nanyie mtakuwa mnahusika kuchochea maovu hayo” Alisisitiza Salim .Salim amewasisitiza Waandishi hao kujitolea kufanya habari za kiuchunguzi bila kuegemea upande wowote na kuwataka wazingatie maslahi ya Taifa badala ya maslahi binafsi.

Semina hiyo ya Siku tano iliyofadhiliwa na Shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO ilikuwa na lengo la kuwajengea uwezo waandishi wa Idara ya Habari Maelezo.

IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

WASHIRIKI WA MISS UTALII TANZANIA 2012/13 KUZINDUA SAFARI YA WANAVYUO TANZANIA

$
0
0
Jumla ya Washiriki 40 wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 ambao wapo Kambini Ikindoleo Lodge Hoteli ya kitalii, Kesho wataungana na wanavyuo mbalimbali Tanzania katika safari yao kwenda Bagamoyo kutangaza  vivutio vya Utalii wa Ndani ya nchi, Safari hiyo ambayo inakwenda kwa jina la Tanzania Journalism Endorses Domestic Tour, Washiriki hao wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 ndio ambao watazindua Rasmi safari hizo ambazo zitaanzia Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) na kisha kuwa wageni Rasmi katika Safari hiyo huko Bagamoyo.


Akizungumza na waandaaji wa Safari hiyo Rais wa Miss Utalii Tanzania Ndugu Gideon Erasto Chipungahelo  alisema fainali za Miss Utalii Tanzania kwa mwaka 2012/13 zitafanyika hivi karibuni. Pia amesema kwamba Miss Tourism Organisation wanatambua sana mchango wa wanafunzi wa vyuo mbalimbali Tanzania pamoja na waandishi wa Habari kwa hiyo  imetoa sapoti kubwa kwa kuwaleta Warembo wote 40 kushiriki na wanafunzi hao katika Safari hiyo.

Katika safari hiyo ambapo wanafunzi wa vyuo vya DSJ,UDSM, TIA, IFM, TSJ, KIU, CBE, Open University Pamoja na vyuo vinginevyo watakuwepo.

Baadhi ya Maeneo watakayo tembelea kesho ni pamoja na Kaole Ruins, Mamba Ranch, Stone Town na Kanisani.

mama salma kikwete aongoza hafla ya kuchangia wanawake wenye matatizo ya afya,zaidi ya mil 142 zapatikana.

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Montage (iliyoandaa hafla hiyo),Teddy Mapunda akimpa zawadi ya heshima Mgeni Rasmi,Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete mara baada ya kuifanikisha vyema tafrija hiyo maalum ya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wanawake wenye matatizo ya afya hapa nchini kupitia mfuko wa Montage Charity Ball,iliyofanyika usiku wa kuamkia leo Serena Hotel,jijini Dar es Salaam,aidha katika tafrija hiyo iliyofana sana kiasi cha shilingi milioni 142 na laki tano zimepatikana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Montage (iliyoandaa hafla hiyo),Teddy Mapunda pichani kushoto akizungumza machache mbele ya meza kuu kabla ya kumpa zawadi ya heshima Mgeni Rasmi,Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete mara baada ya kuifanikisha vyema tafrija hiyo maalum ya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wanawake wenye matatizo ya afya hapa nchini kupitia mfuko wa Montage Charity Ball,iliyofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye Hoteli ya Serena,jijini Dar es Salaam,aidha katika tafrija hiyo iliyofana sana kiasi cha shilingi milioni 142 na laki tano zimepatikana.Kulia ni  Mke wa Makamu wa Rais,Mama Asha Bilal.

Mgeni Rasmi,Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akimkabidhi Bwa.Charles Stith ambaye aliwahi kuwa balozi wa Marekani nchini Tanzania cheti chake cha heshima ,mara baada ya kuchangia  $ 10,000 kwenye hafla ya kukusanya kiasi cha fedha zaidi ya shilingi milioni 100 kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Wanawake wenye matatizo mbali mbali,Anaeshuhudia pichani kulia ni Mke wa Makamu wa Rais,Mama Asha Bilal,aidha katika tafrija hiyo iliyofana sana kiasi cha shilingi milioni 142 na laki tano zimepatikana usiku huu,ndani ya hoteli ya Serena,jijini Dar.
Mgeni Rasmi,Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akimkabidhi Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BOT),Bwa.Benno Ndulu cheti chake cha heshima ,mara baada ya kuchangia  Milioni Kumi kwenye hafla ya kukusanya kiasi cha fedha zaidi ya shilingi milioni 100 kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Wanawake wenye matatizo mbali mbali,Anaeshuhudia pichani kulia ni Mke wa Makamu wa Rais,Mama Asha Bilal,aidha katika tafrija hiyo iliyofana sana kiasi cha shilingi milioni 142 na laki tano zimepatikana usiku huu,ndani ya hoteli ya Serena,jijini Dar. 
 Mke wa Makamu wa Rais,Mama Asha Bilal pichani kulia akizungumza machache,ambaye pia alichangia kiasi cha shilingi Milioni mbili katika hafla hiyo. 
Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete wakipeana mkono wa pongezi na  Mke wa Makamu wa Rais,Mama Asha Bilal kwa kuchangia kwake.
Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete wakipeana mkono wa pongezi na kumkabidhi cheti cha heshima Mke wa Makamu wa Rais,Mama Asha Bilal kwa kuchangia kwake
Mgeni Rasmi,Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akimkabidhi cheti cha heshim mmoja wa watangazaji wa kipindi cha Powerbreakfast kutoka Clouds FM,Said Bonge a.k.a Bonge Barabarani ambaye pia alichangia kiasi cha shilingi laki tisa.
 Makofi  ya pongezi na shukurani kwa Bonge Barabarani yakipigwa.
Mama Salma Kikwete akimkabidhi mmoja wa Wakilishi wa Kampuni ya ndege ya Flight Link cheti chake cha heshima ,mara baada ya kuchangia kiasi cha fedha kwenye hafla hiyo.
Mama Salma Kikwete akimkabidhi cheti cha heshima Meneja mahusiano wa PPF,Lulu Mengele ,mara baada ya kuchangia kiasi cha fedha kwenye hafla hiyo,kulia kwake akishuhudia ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal..

 Mgeni Rasmi,Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza machache mbele ya wageni waalikwa (hawapo pichani) mara baada ya kuifanikisha hafla hiyo kwa kiasi kikubwa.
Mmoja wa Waratibu wa hafla ya  Montage Charity Ball,Barbra  Hassan akiwakaribisha baadhi ya viongozi mbalimbali wa kiserikali,mabalozi na wageni waalikwa wengine waliofika kwenye hafla hiyo ndani ya hotel ya Serena jijini Dar.
 
 Pichani juu ni wageni waalikwa kutoka makampuni mbalimbali wakishuhudia yaliyokuwa yakijiri kwenye hafla hiyo,ambapo mgeni rasmi alikuwa Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete.
 Kalunde Band wakitumbuiza jukwaani
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Barnaba akipewa kampani na baadhi ya wanamuziki wenzake jukwaani,wakitumbuiza mbele ya wageni waalikwa (hawapo pichani),ndani ya hotel ya Serena jijini Dar.
 Baadhi ya Wafanyakazi wa kampuni ya bia ya Serengeti wakiongozwa na MKurugenzi wao Mtendani (wa tatu kulia),Steve Gannon wakiwa katika picha ya pamoja,aidha kampuni hiyo pamoja na kudhamini hafla hiyo pia ilichangia kiasi cha shilingi milioni tano 
Baadhi ya magauni yakinadiwa kwa staili ya kipekee kabisa,kwa ajili ya kuchangia mfuko huo wa kuwasiadia wanawake wenye matatizo ya afya hapa nchini kupitia mfuko wa Montage Charity Ball.

tbc na vita foam wakabidhi msaada wa magodoro wenye thamani ya sh.mil. 3 shule ya msingi uhuru mchanganyiko jijini dar

$
0
0


 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC), Clement Mshana akikabidhi moja ya mashine inayotumiwa na watoto walemavu wa macho kuandikia kwa Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Anna Mang'enya wakati TBC kwa kushirikiana na kampuni ya magodoro ya Vita Foam (T) ltd walipokwenda kutoa msaada wa magodoro 100 yenye thamani ya sh milioni 3, Dar es Salaam leo. 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC), Clement Mshana akikabidhi sehemu ya magodoro 100 yenye thamani ya shilingi milioni 3 kwa Mratibu wa Elimu Kata ya Gerezani, Seraphina Mdamu kwa ajili ya matumizi ya wanafunzi walemavu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko wakati shirika hilo kwa kushirikiana na kampuni ya magodoro ya Vita Foam (T) Limited walipokwenda kutoa msaada huo shuleni hapo, Dar es Salaam leo. Wengine ni Mkuu wa Shule 

 Mkutubi msaidizi wa Maktaba ya Watoto wenye ulemavu katika shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, joyce Nyamuhokwa (katikat) akimwelezea Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC), Clement Mshana kuhusu maktaba hiyo wakati shirika hilo kwa kushirikiana na kampuni ya magodoro ya Vita Foam (T) ltd walipokwenda kutoa msaada wa magodoro 100 yenye thamani ya sh milioni 3, Dar es Salaam leo. Wengine ni Mkuu wa Shule hiyo, Anna Mang'enya (wa pili kushoto), Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Vitafoam, Justine Mwakalinga (wa tatu kushoto) na wafanyakazi wengine wa Vita Foam, TBC na walimu wa shule hiyo.
 Mkutubi msaidizi wa Maktaba ya Watoto wenye ulemavu katika shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Joyce Nyamuhokwa akimuonesha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC), Clement Mshana (kushoto) moja ya nyenzo zinazotumiwa na wanafunzi walemavu kuandikia wakati TBC kwa kushirikiana na kampuni ya magodoro ya Vita Foam (T) ltd walipokwenda kutoa msaada wa magodoro 100 yenye thamani ya sh milioni 3, Dar es Salaam leo. 
 Mkutubi msaidizi wa Maktaba ya Watoto wenye ulemavu katika shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Joyce Nyamuhokwa (kulia) akimuonesha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC), Clement Mshana (kushoto) moja ya kompyuta zinazotumiwa na wanafunzi walemavu kusomea wakati TBC kwa kushirikiana na kampuni ya magodoro ya Vita Foam (T) ltd walipokwenda kutoa msaada wa magodoro 100 yenye thamani ya sh milioni 3, Dar es Salaam leo. 

Mkutubi msaidizi wa Maktaba ya Watoto wenye ulemavu katika shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Joyce Nyamuhokwa (kulia) akimuonesha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC), Clement Mshana sehemu ya vitabu vya Maktaba ya watoto hao walemavu wakati TBC kwa kushirikiana na kampuni ya magodoro ya Vita Foam (T) ltd walipokwenda kutoa msaada wa magodoro 100 yenye thamani ya sh milioni 3, Dar es Salaam leo. Wa pili kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Vitafoam, Justine Mwakalinga.hiyo, Anna Mang'enya na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Vitafoam, Justine Mwakalinga (wa pili kulia).

Mstahiki Meya Jerry Silaa akabidhi vyeti kwa wahitimu wa kidato cha sita katika shule ya St. Anthony jijini Dar

$
0
0

Mgeni rasmi katika mahafali ya 20 ya Kidato cha Sita ya Shule ya Sekondari St. Anthony Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akizungumza na uongozi wa shule hiyo kabla ya kuanza rasmi kwa sherehe hizo.
Padri akiendesha ibada wakati wa mahafali hayo.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa akifuatilia ibada hiyo kubariki mahafali ya 20 ya kidato cha sita ya Shule ya Sekondari St. Anthony. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Shule hiyo Sylvester John na Mkuu wa shule hiyo Bro. Ismail Edward ( wa pili kulia).
Baadhi ya Wahitimu wa Kidato cha Sita shule ya St. Anthony wakisikiliza mahaburi wakati wa ibada hiyo.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa akishiriki kwenye sala maalum wakati wa ibada hiyo.
Baadhi ya wahitimu wa kidato cha sita wakisoma sala za mtu mmoja kuombea mambo tofauti ikiwemo Amani kwa Taifa.
Baadhi ya wahitimu wa Kidato cha Sita shule ya Sekondari St. Anthony wakimwogoza mgeni rasmi kwa madoido ya aina yake wakati wa mahafali hayo.

Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa akiwasili katika viwanja vya shule ya Sekondari St. Anthony akiwa ameambatana na viongozi wa shule hiyo tayari kuanza rasmi sherehe za mahafali hayo.
Baadhi ya wahitimu wa kidato cha sita wakishiriki kuimba wimbo wa shule.
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha tano wakiimba wimbo wa kuwaaga dada zao na kaka zao mbele ya mgeni rasmi wakati wa mahafali hayo.
Wanafunzi wa shule ya sekondari St. Anthony wakifanya igizo la Dr. Livingstone lililowavunja mbavu wazazi na mgeni rasmi.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa akiwa hoi kwa kucheka kutokana na igizo la Dr. Livingstone. Kushoto ni Makamu Mkuu wa pili wa Shule hiyo Rempta Adams akifuatiwa na Mkuu wa Shule hiyo Bro. Ismail Edward.
Makamu Mkuu wa pili wa Shule ya sekondari St. Anthony Rempta Adams akisoma taarifa ya shule hiyo mbele ya mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala ambapo amezungumzia changamoto mbalimbali zinazoikabili shule hiyo ikiwa ni pamoja na uhaba wa vifaa vya kufundishia na kujifunza, mabadiliko ya mara kwa mara ya Mitaala na matamko juu ya Elimu, tabia ya wanafunzi kuiga tamaduni za Ughaibuni na Ukosefu/kukatika kwa nishati ya Umeme.
Sehemu ya wazazi na walezi waliohudhuria mahafali hayo.
Makamu Mkuu wa pili wa Shule ya sekondari St. Anthony Rempta Adams akikabidhi taarifa ya shule yake kwa mgeni rasmi.
Makamu wa Rais wa Wanafunzi wa St. Anthony Jacqueline Ndunguru akisoma risala ya wanafunzi wa kidato cha sita mbele ya mgeni rasmi.
Makamu wa Rais wa Wanafunzi wa St. Anthony Jacqueline Ndunguru akimkabidhi mgeni rasmi risala hiyo.
Mwanfunzi Samwel Mwanzini akionyesha kipaji chake cha kuimba na kupiga kinanda ambapo alishangaza wengi kwa uwezo aliokuwa nao.
Mwanfunzi Tracy Raymond Ndanshau wa kidato cha tano PCM akiimba sambamba na Mwl. Nikiza Bwenge katika mahafali ya 20 ya kidato cha sita.
Makamu Mkuu wa Shule hiyo Sylvester John (kulia) akisoma risala fupi ya kukabidhi wahitimu kidato cha sita 2013 kwa wazazi rasmi Bw. na Bibi Amos Bujiku wakati wa mahafali hayo.
Wazazi rasmi rasmi Bw. na Bibi Bujiku wakiwapokea rasmi wanafunzi Mary Bujiku na Edward Mugyabuso kwa niaba ya wahitimu wa kidato cha sita kwenda kuwalea kiroho.
Mkuu wa Shule ya sekondari St. Anthony Bro. Ismail Edward akisoma risala kwenye mahafali ya 20 ya kidato cha sita ambapo amewasihi wanafunzi wanaohitimu waendelee kutunza kumbukumbu ya shule hiyo na kuwa mabalozi wazuri wa St. Anthony kwa kuwa wazalendo wa kweli waliotayari kulijenga na kulilinda taifa letu na kukabiliana na changamoto za dunia ya leo hususani gonjwa hatari la Ukimwi na matatizo mengine yanayoikumba Tanzania.
Meza kuu ipitia risala ya Mkuu wa shule hiyo.
Picha juu na chini Mgeni rasmi Mstahi Meya Jerry Silaa akizungumza wakati wa mahafali ya 20 ya kidato cha sita ya St. Anthony ambapo ametoa pongezi kwa walimu na wanafunzi wa shule hiyo na kuongeza kuwa kwa sisi Watanzania Elimu ni nyenzo muhimu sana hasa katika mbio zetu za kupambana na maadui watatu; ujinga, maradhi na umaskini ambayo ni Silaha pekee ya kuwashinda maadui hao wote watatu.
Sehemu ya wahitimu wa kidato cha sita wakimsikiliza mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa.
Wahitimu wa kidato cha sita wakielekea kukabidhi zawadi kwa mgeni rasmi Mstahiki Meya.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akipokea zawadi hiyo.
Mgeni rasmi akifingua zawadi hiyo mbele ya wahitimu hao.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akionyesha zawadi aliyokabidhiwa na wahitimu wa kidato cha sita ambapo walimtaka kuiweka ofisini kwake ili aendelee kuwakumbuka.
Picha Juu na Chini Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa akikabidhi vyeti na zawadi kwa wahitimu wa kidato cha sita wa St. Anthony katika sherehe za mahafali ya 20 shuleni hapo.
Mstahi Meya Jerry Silaa akishow love na mmoja wa wanafunzi wanaohitimu aliyesoma kombi kama aliyosoma Mstahiki.
Mhitimu wa Kidato cha Sita Yvonne Laurent Mganga akipongezwa na familia yake baada ya kuhitimu kidato cha Sita.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya St. Anthony Bi. Fides Challe (wa tatu kushoto waliokaa), wageni waalikwa pamoja na uongozi wa shule hiyo.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya burudani wa shuleni hapo.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa akiwa na MC wa mahafali hayo ambaye ni Katibu wa wanafunzi Shuleni hapo Kennedy Mlawa.
Picha Juu na Chini wanafunzi wa St. Anthony ambao Mstahiki Meya Jerry Silaa ni Role Model wao wakionyesha upendo.
Bw. na Bibi Amos Bujiku na binti yao katika picha ya pamoja na mgeni rasmi na Uongozi wa shule hiyo.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA RASMI MRADI WA UPANUZI WA BARABARA YA KILWA, MBAGALA RANGI TATU

$
0
0

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada, wakifunua kitambaa kwa pamoja ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa mradi wa Upanuzi wa Barabara ya Kilwa, eneo la Mbagala Rangi tatu leo. Kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (kushoto) wakishiriki kwa pamoja kukata utepe ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa mradi wa Upanuzi wa Barabara ya Kilwa, eneo la Mbagala Rangi tatu leo.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada, wakati alipowasili katika hafla ya ufunguzi wa mradi wa Upanuzi wa Barabara ya Kilwa, eneo la Mbagala Rangi tatu leo. Katikati ni Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza jambo na kumpongeza Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada, mara baada ya balozi huyo kumaliza kusoma hotuba yake iliyochanganywa na Kiswahili, wakati wa hafla ya ufunguzi wa mradi wa Upanuzi wa Barabara ya Kilwa, eneo la Mbagala Rangi tatu leo. Kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli.
 Balozi wa Japan Nchini Tanzania, Masaki Okada, akishiriki kucheza sebene la bendi ya Msondo Ngoma na Vijana wa kikundi cha uhamasishaji cha Temeke, wakati wa hafla hiyo.
 Baadhi ya wanamuziki wa bendi ya Msondo Ngoma, wakishambulia jukwaa kutoa burudani wakati wa halfa hiyo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya Wazee wastaafu wa CCM, mara baada ya kumaliza kupiga nao picha ya pamoja ya kumbukumbu wakati wa hafla ya ufunguzi wa mradi wa Upanuzi wa Barabara ya Kilwa, eneo la Mbagala Rangi tatu leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya viongozi kutembea na kukagua sehemu ya Barabara ya Kilwa eneo la Mbagala Rangi tatu, baada ya kufungua rasmi barabara hiyo iliyokamilika kwa Upanuzi na ukarabati. Hafla hiyo ya ufunguzi imefanyika leo. .Picha na OMR

Rais Kikwete awasili jijini Addis Ababa kuhudhuria utiwaji saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole jijini Addis Ababa, Ethiopia, leo Februari 23, 2013 kuhudhuria utiwaji saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). PICHA NA IKULUU


Oman's Foreign Minister in Dar for a two-day Joint Permanent Commission of Cooperation meeting

$
0
0


Hon. Bernard K. Membe (MP), Minister for Foreign Affairs and International Co-operation, welcomes H.E. Yousuf bin Alawi bin Abdullah, Minister Responsible for Foreign Affairs of the Sultanate of Oman.
H.E. Abdullah is in the country attending a two-day Joint Permanent Commission of Cooperation between Tanzania and Oman (JPC) which is set to kick start on February 24 to 25, 2013 at Hyatt Regency (Kilimanjaro) Hotel in Dar es Salaam.
Hon. Membe hugs and welcomes H.E. Abdullah to Tanzania upon his arrival today at the Julius Nyerere International Airport in Dar es Salaam.
H.E. Ali Ahmed Saleh, Ambassador of the United Republic of Tanzania to Oman welcomes H.E. Abdullah.
Ambassador Simba Yahya, Director of the Department of Middle East in the Ministry of Foreign Affairs in Tanzania welcomes H.E. Abdullah. All photos by Tagie Daisy Mwakawago of the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation.

TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM YA MWAKA 2005-2012 YA MKOA WA RUKWA

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akisoma taarifa hiyo kwa vyombo vya habari mapema hii leo. Taarifa hiyo hiyo iliyodumu kwa zaidi ya saa moja na nusu ilirushwa moja kwa moja (LIVE) na Radio Chemchem FM ya Hapa mjini Sumbawanga.
NA HAMZA TEMBA - OFISI YA MKUU WA MKOA RUKWA...rukwareview.blogspot.com

MANENO OSWARD ATAMBA KUMCHAKAZA KASEBA MARCH 2

$
0
0

Bondia Maneno Osward akijifua kwa ajili ya mpambano wake wa ubingwa dhidi ya Japhert Kaseba March 2 katika ukumbi wa DDC Madomeni Kondoa Dar es salaam .
Bondia Maneno Osward 'Mtambo wa Gongo' akifanya mazoezi ya kukaza misuli ya tumbo kwa ajili ya mpambano wake wa ubingwa dhidi ya Japhert Kaseba March 2 katika ukumbi wa DDC Madomeni Kondoa Dar es salaam.
Mabondia Maneno Osward kushoto na Japhert Kaseba walipokutana kwa ajili ya kuzungumzia mpambano wao utakaofanyika March 2 katika ukumbi wa DDC Magomeni Kondoa Dar es salaam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Na Mwandishi Wetu

BONDIA Maneno Osward ametamba kumchakaza mpinzani wake Japhert Kaseba kunako raundi za awali akizungumza na mwandishi wa habari hizi maneno maarufu kwa jina la Mtambo wa Gongo amesema yeye yupo fiti na anasubili hiyo March 2 katika ukumbi wa DDC Magomeni kondoa apate kumshikisha adabu 

Kaseba ni bondia mchanga sana kwangu nilimkaribisha katika masumbwi na sasa nitamstafisha masumbwi mimi mwenyewe kwa kipigo nitakacho mpa na atajua kwa nini nimepewa jina la mtambo wa Gongo


Katika mpambano huo kutakuwa na mpambano wa uzito wa juu kati ya Josefu Marwa na Alphonce Mchumiatumbo mpambano unaosubiliwa kwa hamu na mashabiki na wapenzi wa ngumi za uzito wa juu nchini .

UCHAGUZI SHINA LA PAMBA ROAD.

$
0
0
Picha ya pamoja ya wanachama n awajumbe wa mkutano wa Uchaguzi wa Viongozi wa Shina la Pamba.

 Wajumbe wa mkutano wa uchaguzi wa Shina la Pamba road wakiwa wamesimama kumlaki mgeni mwalikwa kwenye Mkutano wa Uchaguzi waViongozi waShina Hilo uliofanyika leo tarehe 22 February 2013 katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam.
 Moja ya wagombea wanafasi ya Mwenyekiti, Ndugu Hamis Nshimba akijieleza mbele ya wajumbe waliojitokeza katika Uchaguzi wa Viongozi wa Shina Hilo uliofanyika leo tarehe 22 February 2013 katika Ukumbi wa Karimjee  ijini Dar es salaam.
Wajumbe wa Mkutano wa Uchaguzi Shina la Pamba Road wakiwa wanasikiliza kwa makini Hoja za Mmoja w aMgombea katika Uchaguzi wa Viongozi waS hina Hilo uliofanyika leo tarehe 22 February 2013 katika Ukumbiwa KarimjeeJijini Dar es salaamba Road uliofanyika leo katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam
.
 Mwenyekiti w aMuda na Msimamizi wa Uchaguzi wa Shina la pamba Road Ndugu Augustino Matefu akiwa Meza Kuu katika Uchaguzi wa Viongozi wa Shina Hilo uliofanyika leo tarehe 22 February 2013 katika Ukumbi w aKarimjee Jijini Dar es salaam.
MGENI MWALIKWA KATIKA MKUTANO WA UCHAGUZI WA SHINA LA PAMBA ROAD, LILILOPO POSTA JIJINI DAR ES SAAAM, NDUGU RIDHWAN J. KIKWETE AKIWASILI KATIKA UKUMBI WA KARIMJEE ULIPOFANYIKA MKUTANO HUO, AKIONGOZANA NA MWENYEKITI MSTAAFU WA SHINA HILO NDUGU SAID SALUM MASANGA (WA KWANZA KULIA) RIDHWAN (MWENYE SHATI YA KIJANI) ABDALAH MALEMA-KATIBU WA TAWI LA KIVUKONI NA SALEHE KISAUTI (MJUMBE)

Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro yashirikiana na Green Waste Pro kusafisha fukwe za Kivukoni Front

$
0
0

Picha juu na chini ni Wafanyakazi wa Hoteli ya Hyatt Regency wakishirikiana na Kampuni ya usafi ya Green Waste Pro kusafisha fukwe za Kivukoni Front jijini Dar zilizopo mbele ya hoteli hiyo ikiwa ni utaratibu wa hoteli hiyo kufanya zoezi hilo mara moja kwa mwezi ili kutunza mazingira.
Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro imeamua kuialika kampuni ya usafi ya Green Waste Pro baada ya kuona juhudi zao za kuweka Manispaa ya Ilala safi na mabadiliko yanaonekana ndipo wakaamua kushirikiana nao katika zoezi la kusafisha fukwe hizo.
Wafanyakazi wa Hoteli ya Hyatt Regency wakishirikiana na Kampuni ya usafi ya Green Waste Pro kusafisha fukwe za Kivukoni Front jijini Dar zilizopo mbele ya hoteli hiyo ikiwa ni utaratibu wa hoteli hiyo iliyojipangia kufanya zoezi hilo mara moja kwa mwezi ili kutunza mazingira.


Meneja Msaidizi wa Kampuni ya Usafi ya Green Waste Pro ltd Bw. Abdallah Mbena (kushoto) akishiriki zoezi la kufanya usafi katika fukwe za Kivukoni Front baada ya kupata mwaliko kutoka Hoteli ya Hyatt Regency wa kushiriki katika kusafisha fukwe hizo.
Mwananchi asiyefahamika akiwa amechapa usingizi huku akiwa amejifunika gunia chafu na kulifanya kuwa shuka katika kichaka cha fukwe za Kivukoni Front wakati zoezi la usafi likiendelea.WADAU huyu jamaa hatuna uhakika kama naye ni sehemu ya uchafu au ndio nyumbani?? Tembea uone.
Picha juu na chini ni Baadhi ya Wafanyakazi wa Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro wakiwa wamebeba mafurushi ya lundo la uchafu uliokusanywa kutoka kwenye fukwe za Kivukoni Front zilizopo karibu na Hoteli hiyo.
Moja ya magari ya kukusanya uchafu ya kampuni ya Green Waste Pro likiwa limesheheni lundo la uchafu uliokusanywa toka kwenye Fukwe za Kivukoni Front baada ya kusafishwa na Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro kwa kushirikiana na kampuni ya usafi ya Green Waste Pro.
Wafanyakazi wa Hoteli ya Hyatt Regency na wafanyakazi wa kampuni ya usafi ya Green Waste Pro ltd wakibadilishana mawazo baada ya kuhitimisha zoezi la kusafisha fukwe za Kivukoni Front na kuishukuru kampuni ya Green Waste Pro kwa kuitikia wito.
Picha ya pamoja ya Wafanyakazi wa Hyatt Regency na kampuni ya Green Waste Pro baada ya zoezi la usafi.
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images