Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 342 | 343 | (Page 344) | 345 | 346 | .... | 1897 | newer

  0 0


  0 0

  Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa (Kulia) akiwa kwenye mazungumzo na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Stephen Masele ofisini kwake Upanga jijini Dar es Salaam.
  Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa (kulia) akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Stephen Masele (Kushoto) aliyemtembelea ofisini kwake

  0 0


  Na Rose Masaka-MAELEZO
  UKAWA waombwa kukubali maoni ya watanzania walio wengi ya kuheshimu pesa za walipa kodi kwa kurudi bungeni na kupingana kwa hoja kwani hoja zao zikiwa za huakika hazitapingwa bali kanuni na taratibu zinazoendesha bunge zitafuatwa badala ya kuendelea kulalamika katika majukwaa ya kisiasa. 

  Kauli hiyo imetolewa na balozi wa amani Tanzania Risasi Mwaulanga alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa habari maelezo leo jijijni Dar es Salaam.

  “Nawaomba UKAWA warudi bungeni ili tuweze kupata katiba mpya itayoyokidhi changamoto za watanzania wote na sio masuala ya vyama vya kisiasa na maslahi binafsi kwani vyama hiyvo vinaweza kutoweka wakati wowote na nchi ikabaki palepale”.Alisema Mwaulanga.

  Aidha Mwaulanga anaiomba iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya jaji Warioba, viongozi wa dini, na asasi za kiraia kuendelea na jitihada za kuitaka UKAWA kurejea Bungeni ili kurahisisisha upatikanaji wa Katiba mpya yenye maslahi mapana kwa ummma kuliko ya kisiasa.

  Balozi huyo wa amani amesema kuwa kauli za vitisho na uvunjifu wa amani unapaswa kupigiwa kelele na kulaniwa na kila mwanademokrasia duniani katika kipindi hiki cha kuandaa Katiba mpya ili wajumbe waweze kuwa huru wakati wa kutoa maoni.

  Tanzania ni nchi ya amani,umoja, upendo na maelewano na siyo nchi ya vita,chuki na mafarakano hivyo watanzania tunapaswa kutambua ni Katiba gani tunayoitaka na kuwa na mtazamo sahihi na maamuzi bora.


  0 0

  DSC_0534
  Diwani wa kata ya Ololosokwani na Mkurugenzi wa Irkiramat Foundation (RAMAT) Bw. Yannick Ikayo Ndoinyo akiangalia kitanda cha kujifungulia wakimama kwenye Zahanati ya Sero ambayo kwa siku inatibu wagonjwa 50 na zaidi ikiwa na daktari mmoja huku wakazi wanaofuata huduma hiyo kutoka kata hiyo na ya jirani Soitosambu kutembea umbali mrefu kwa Kilometa 7-15 kupata huduma ya afya.(Picha Zainul Mzige wa MOblog)


  Wakazi wa vijiji vya Ololosokwan, Soit-Sambu, Njoroi na Loipir kata za Ololosokwana na Soit-Sambu wilayani Ngorongoro wanakabiliwa na changamoto kubwa ya huduma ya Afya kwa kutembea umbali mrefu kufuata huduma hizo kwenye kijiji cha Sero huku waathirika wakubwa ni kinamama na watoto.

  Umbali wa zahanati hizo imekuwa sababu kubwa ya vifo hususani kwa akina mama wajawazito wanaotaka kwenda kujifungua na watoto halikadhalika wanapozidiwa hufia njiani kutokana na umbali wa zahanati kutoka kijiji kimoja kwenda kingine wanapotakiwa kuwahishwa hospitalini hali inayowafanya kutembea umbali mrefu kilometa 15 hadi kuipata huduma ya zahanati .

  Akizungumza na waandishi wa habari Diwani wa kata ya Ololosokwani na Mkurugenzi wa Irkiramat Foundation (RAMAT) Yannick Ikayo Ndoinyo waliotembelea miradi inayofadhiliwa na Shirika la Elimu na Sayansi (UNESCO) wilayani humo alisema serikali haina budi kutimiza ahadi yake ya kujenga Zahanati kwa kila kata nchini Tanzania kuwapunguzia wagonjwa hususan akina mama waja wazito na watoto adha ya kutembea au kusafiri mwendo mrefu kutafuta huduma za afya.

  Ndoinyo alisema kuwa tatizo kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma ya afya lipo na kwamba vifo ya wamama na watoto na kutopata huduma zinazotakiwa kwa wakati. Wananchi hupata huduma za afya kutoka Sero ambayo ina umbali mrefu kutoka Ololosokwang au wakati mwingine mgonjwa hupata rufaa rufaa hadi Hospitali ya wilaya ya Waso na iwapo mgonjwa atakuwa katika hali mbaya ni tatizo.
  DSC_0532
  Gari la wagonjwa lilitolewa na serikali likiwa limeharibika kutoka na miundo mbinu ya barabara na kushindwa kufanyiwa matengezo kwa muda mrefu hali inayomfanya daktari wa Zahanati hiyo kuwafuata majumbani wagonjwa mahututi kwenda kuwapatia huduma za afya.


  “Utakuta wagonjwa inabidi watembee umbali mrefu kwenda kupata huduma za afya kwenye zahanati ya Sero hili ni tatizo tunaiomba serikali yetu kuliangalia ili kuokoa vifo vya mama na mtoto”alisema diwani.

  Ndoinyo alisema kuwa pamoja na daktari kuwatembelea akina mama na watoto ili kutoa huduma za afya majumbani kwao kumekuwa na changamoto mbalimbali hususan vifaa vya vipimo vya kupima magonjwa mbalimbali.

  Nae Mkunga wa jadi Mama Naani alisema mtihani mkubwa unakuja pale wakati mama mjamzito anapotaka kujifungua na anahitaji huduma ya ziada, hakuna vifaa na kumlazimu mgonjwa au mama mjamzito kuembea umbali mrefu kupata huduma hiyo hospitalini.

  Madhumuni ya ziara hiyo inayowashirikisha wawakilishi kutoka Kampuni ya Samsung na mwakilishi kutoka ubalozi wa Uswiss hapa nchini ni kujionea miradi mbalimbali inayoendeshwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) inayotekelezwa na redio ya Jamii Loliondo wilayani Ngorongoro.

  Miongoni mwa miradi inayofadhiliwa wilayani humo ni pamoja na Redio Loliondo ambayo pia inafadhiliwa na kampuni ya simu za mikononi ya Airtel kwa kurusha matangazo yake kupitia mnara wa kampuni hiyo na Mradi wa Maktaba unaolenga kuwapatia wanafunzi uelewa wa mambo mbalimbali yanayohusu masomo ya sayansi.
  DSC_0540
  Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph, akishanga kitanda cha kujifungulia wakinamama kwenye zahanati hiyo ambayo ina uhaba wa vifaa mbalimbali vya matibabu huku halmashauri ikishindwa kumalizia majengo ya wodi kwa ajili ya kulaza wagonjwa ambapo imeonyesha wakina mama na watoto wamekuwa wakifia njiani kutokana na kutembelea umbali mrefu kufuata matibabu.
  DSC_0544
  Vifaa vinavyotumika kwenye zahanati hiyo wakati wakinamama wanapojifungua, jingine ni Friji kwa ajili ya kuhifadhia chanjo mbalimbali za watoto na kinamama linalotumia umeme wa jua.
  DSC_0559
  Daktari wa Zahanati ya Sero kata ya Ololosokwani Dkt. Veronika Nyoni (katikati) akielezea changamoto mbalimbali anazokumbana nazo katika kutoa huduma ikiwemo Umeme na kupelekea kutumia tochi wakati wakinamama wanapojifungua ambapo ameiomba serikali kupitia wafadhili mbalimbali kuwasogezea hata huduma ya umeme jua ili kukabiliana na changamoto hizo.Kulia ni Mwanahabari wa gazeti la Zanzibar leo, Mahmoud Ahmad na kushoto ni Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph wakimsilikiliza kwa makini Dkt. Nyoni.
  DSC_0583
  Diwani wa kata ya Ololosokwani na mkurugenzi wa Irkiramat Foundation (RAMAT) Bw. Yannick Ikayo Ndoinyo akiwa na wadau wa maendelo wakiongozwa na UNESCO waliofanya ziara katika kata ya Ololosokwani wilayani Ngorongoro. Katikati ni Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph na kulia ni Meneja Mauzo wa Kampuni ya Samsung tawi la Tanzania, Bw. Slyvester Nteere.
  DSC_0585
  Nyumba ya Daktari Mstaafu aliyekuwa akitoa huduma katika zahanati ya Sero zaidi ya miaka 25 kama inavyoonekana ikiwa na Umeme wa jua pamoja na Dish ikiwa ni maendeleo katika eneo hilo lililopo karibu na pori tengefu la Loliondo.

  0 0

   Rais wa Vijana Wanasayansi Duniani Bw. Meng Wang (kulia) akimkabidhi kinyago cha tembo Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhe. Stephen Masele wakati wa kufunga Kongamano la Tatu la Wanasayansi Vijana Duniani lililofanyika Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
   Rais wa Vijana Wanasayansi Duniani Bw. Meng Wang (kulia) akimkabidhi zawadi ya Kipepeo Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhe. Stephen Masele wakati wa kufunga Kongamano la Tatu la Wanasayansi Vijana Duniani lililofanyika Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.

  Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhe. Stephen Masele (aliyesimama kulia) akimkabidhi ramani ya Afrika iliyochongwa kwa mti Rais wa Wajiolojia Afrika Profesa Aberra Mogessie wakati wa kufunga Kongamano la Tatu la Wanasayansi Vijana Duniani lililofanyika Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.

   Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhe. Stephen Masele (kulia) akimkabidhi zawadi Kijana Mwanasayansi Duniani toka nchini India wakati wa kufunga Kongamano la Tatu la Wanasayansi Vijana Duniani lililofanyika Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
   Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhe. Stephen Masele (kushoto) akimkabidhi zawadi Kijana Mwanasayansi Duniani toka nchini Botswana wakati wa kufunga Kongamano la Tatu la Wanasayansi Vijana Duniani lililofanyika Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
   Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhe. Stephen Masele (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Vijana Wanasayansi Duniani wakati wa kufunga Kongamano la Tatu la Wanasayansi Vijana Duniani lililofanyika Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere. Wa kwanza kulia ni Makamu Mwenyekiti na Mwakilishi wa Vijana Wanasayansi Duniani (YES) na anaemfuatia ni Rais wa YES Bw. Meng Wang. Wa kwanza toka kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania, Profesa Abdulkarim Mruma akifuatiwa na Rais wa Wajiolojia Afrika Profesa Aberra Mogessie.PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO.   Rais wa Vijana Wanasayansi Duniani Bw. Meng Wang akitoa maelezo machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kwa ajili ya kufunga Kongamano la Tatu la Wanasayansi Vijana Duniani lililofanyika Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
   Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania, Profesa Abdulkarim Mruma akitoa nasaha zake mbele ya Vijana Wanasayansi Duniani (hawapo pichani) wakati wa kufunga Kongamano la Tatu la Wanasayansi Vijana Duniani lililofanyika Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
   Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhe. Stephen Masele akiwahutubia Vijana Wanasayansi Duniani wakati alipokuwa akifunga Kongamano la Tatu la Wanasayansi Vijana Duniani lililofanyika Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
   Meza Kuu ambapo katikati ni Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhe. Stephen Masele, kulia ni Rais wa Vijana Wanasayansi Duniania Bw. Meng Wang na kushoto ni Rais wa Wajiolojia Afrika Profesa Aberra Mogessie.
   Baadhi ya Vijana Wanasayansi Duniani waliohudhuria siku ya ufungaji Kongamano wakifuatilia kwa makini hotuba ikiyotolewa na mgeni rasmi wakati wa kufunga Kongamano la Tatu la Wanasayansi Vijana Duniani lililofanyika Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.

   Rais wa Vijana Wanasayansi Duniani (YES), Bi. Elyvin Nkhonjera kutoka nchini Malawi akikaribisha wageni waalikwa wakati wa kufunga Kongamano la Tatu la Wanasayansi Vijana Duniani lililofanyika Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
  NAIBU WAZIRI MASELE AWATAKA VIJANA KUJIKITA KATIKA MAMBO YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA.
  Na Benedict Liwenga-MAELEZO.
  14/08/2014.
  NAIBU Waziri wa Nishati na Madini Stephen Masele amewataka vijana nchini kupenda kujikita katika masomo ya sayansi na teknolojia kama mihimili yenye kuleta maendeleo kwa haraka ulimwenguni ili waweze kupata ujuzi na mitazamo katika sekta ya gesi ambayo inakuwa kwa kasi kubwa nchini.
  Mhe. Masele ameyasema hayo jana wakati alipokuwa akifunga Kongamano la Tatu la Vijana Wanasayansi Duniani lililofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere, kongamano ambalo liliwakutanisha vijana toka nchi zaidi ya 46 ulimwenguni zikiwemo baadhi ya nchi za Afrika ambapo Tanzania ilikuwa mwenyeji wa Kongamano hilo.
  Mhe. Masele ameeleza kuwa sayansi na teknolojia ndiyo mihimili mikubwa ya sasa katika kuleta maendeleo ya haraka katika nyanja mbalimbali kwani mambo mengi hivi sasa hutegemea sayansi na teknolojia.
  Aidha, Mhe. Masele amezitaja baadhi ya changamoto zinazozikabili baadhi ya nchi za Afrika katika kupata maendeleo ni pamoja na kutowekeza katika sayansi na teknolojia hali inayopelekea baadhi ya nchi nyingi kukosa wataalam wa kutosha katika mambo ya sayansi na teknolojia, hivyo amezitaka nchi za Afrika kuwekeza katika sayansi ili kuweza ili kubadilisha uchumi wa Afrika.
  “Sayansi na teknolojia huleta maendeleo makubwa hivyo nawapa moyo vijana muendelee kufanya kazi kwa bidii na kujituma katika mambo ya sayansi na teknolojia ili muweze kuleta uchumui endelevu”. Alisema Masele.
  Akizungumzia kwa upande wa Serikali ya Tanzania, Mhe. Masele amesema kuwa serikali ya Tanzania imewekeza nguvu zake kwa sasa katika kuendeleza sayansi ya afya kwa kuanzisha Vyuo mbalimbali na kuwasomesha watanzania nchi mbalimbali za nje ili waweze kwenda kupata ujuzi na kuwa wataalam na wakaguzi katika sekta ya gesi pamoja na mafuta kwa lengo la kuja kuisaidia nchi yao.
  “Wajibu wetu kama Serikali tumeamua kwa makusudi kusomesha vijana katika nchi mbalimbali ili wakaweze kupata elimu juu ya sayansi na teknolojia hasa katika masuala ya gesi ili kupata wataalam na wakaguzi wa kutosha nchini ambao watalisaidia taifa kuinua uchumi wake na hivi sasa serikali imeanzisha vyuo mbalimbali nchini, program mbalimbali za mafunzo kwa watanzania, imetoa ufadhili wa masomo kwa watanzania na imedhamini makongamano ya vijana ili wapate fursa ya kujiendeleza.” Alisisitiza Masele.
  Mhe. Masele amempongeza Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Prof. Sospeter Muhongo kwa kazi kubwa anayoifanya katika Wizara yake na pia amewapongeza vijana waliohudhuria katika kongamano hilo pamoja kuyapongeza Makampuni wadhamini wa kongamano hilo na kuyataka makampuni hayo kuendelea kuwekeza pamoja na kulipa kodi ili serikali iweze kukusanya mapato na wananchi wapate kunufaika na mapato hayo.
  Naye Rais wa Vijana Wanasayansi Duniani (YES) Bw. Meng Wang amemshukuru Makamu wa Rais wa Tanzania, Waziri wa Nishati na Madini pamoja na Naibu Waziri steven Masele kwa kuwaunga mkono vijana waliohudhuria kongamano hilo na kuonesha hali nzuri ya ushirikiano baina ya serikali na vijana na amewaasa vijana kujikita katika sayansi na teknolojia kama mihimili mikuu ya maendeleo duniani.
  “Naishukuru sana Tanzania pamoja na ujio wa Mawaziri wake katika kufanikisha kongamano hili la vijana wanasayansi, nawashukuru pia wadhamini wa makampuni mbalimbali wa kongamano hili pamoja na vijana kwa ujumla toka nchi mbalimbali duniani”. Alisema Wang.

  0 0


   Mratibu wa shindano la Redd's miss Kinondoni 2014 Innocent Melleck katikati akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar Es Salaam juu ya shindano la kanda ya kinondoni litakalofanyika katika ukumbi wa Escape One ijumaa kwa kiingilio cha 10,000 kwa viti vya kawaida na 30,000 kwa VIP huku burudani za Malaika Bend chini ya Chirstian bella na Young Suma na tayari tiketi zipo mtaani. Baadhi ya warembo wa shoto ni matroni wa kambi hiyo Husna Maulid na kulia ni Mkuu wa itifaki wa kamati ya Miss Tanzania Albert Makoye

  0 0   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua Mkutano wa Diaspora katika ukumbi wa hoteli ya Serena leo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua mkutano wa kwanza wa Diaspora katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Agosti 14, 2014.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibonyeza kitufe kuzindua tovuti rasmi ya Diaspora wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa Diaspora katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Agosti 14, 2014.Pamoja naye ni Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda, Mwenyekiti wa Taasisi ya Diaspora Bw. Emmanuel Mwachullah (wa pili kulia), Mwana-Diaspora Dennis Londa (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Diaspora Bi. Rose Jairo.PICHA NA IKULU.

   Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda akimkaribisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuhutubia na kufungua rasmi Mkutano wa Diaspora.
  Mratibu wa Diaspora katika Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Suzan Mzee akitoa muhtasari wa mkutano wa Diaspora kabla ya kufunguliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika ukumbi wa Serena Hotel leo Agosti 14, 2014. Anayeangalia mabango ni mjumbe wa kamati ya maandalizi Bw. Constantine Magavilla.
   Sehemu ya wageni waalikwa akiwemo Balozi Mwanaidi Maajar ambaye anasifika kwa kusimamia mambo ya Diaspora
  Mratibu wa  Diaspora Zanzibar pamoja na wadau kutoka ughaibuni wakifuatilia


  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Watumishi Housing Company, Dkt. Fred Msemwa akitoa mada kuhusu mkopo wa ujenzi wa nyumba bora za kisasa kwa watumishi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakati wa warsha ya siku moja iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari Jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Agosti 14, 2014.
   Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakifuatia uwasilishaji wa mada kuhusu mkopo wa nyumba bora za watumishi wa umma wakati wa warsha iliyotolewa na Taasisi ya Watumishi wa Housing Company leo Alhamisi Jijini Dar es Salaam.PICHA NA BENJAMIN SAWE- MAELEZO.
   

  TAASISI ya Watumishi Housing Company imetenga kiasi cha Tsh. Bilioni 400 kwa ajili ya ujenzi za watumishi wa Serikali katika mikoa 13 nchini.

  Ujenzi wa nyumba hizo unatarajia kuanza mwezi oktoba mwaka huu, ambapo katika awamu ya kwanza, taasisi hiyo imepanga kujenga jumla ya nyumba 2500 katika kipindi cha mwaka wa fedha 2014/15 na Mikoa itayonufaika na ujenzi wa nyumba hizo ni Mtwara, Rukwa,Mbeya, Morogoro, Dodoma, Pwani, na Dar es Salaam.

  Mikoa mingine ni pamoja na Tanga, Arusha, Mwanza, Shinyanga, Kigoma na Kilimanjaro, na jumla ya nyumba 50,000 zinatarajiwa kujengwa na taasisi hiyo hadi kufikia mwaka 2019. Akizungumza katika warsha ya siku moja kwa Watumishi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Dkt. Fred Msemwa alisema mara baada ya kukamilika nyumba zinatarajia kuuzwa kiasi cha Tsh. Milioni 19 hadi Milioni 119.

  Dkt. Msemwa alisema mpaka sasa Ofisi imeanza utaratibu wa kuuza vipande vitavyowekezwa katika ardhi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Mfuko wa Pensheni wa mashirika ya Umma (PPF), mfuko wa pensheni wa watumishi wa umma (PSPF), na mfuko wa taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF), 

  Mifuko mingine ni pamoja na mfuko wa pensheni wa watumishi wa Serikali za Mitaa ( LAPF), mfuko wa Taifa wa Bima ya afya (NHIF), pamoja na Shirika la Nyumba la Taifa, ambapo waombaji watapaswa kupitisha maombi yao kupitia kwa waajiri wao.

  Aliongeza kuwa tayari ofisi yake imekwishapata maelekezo kutoka katika Benki Kuu ya Tanzania (BOT), ambapo moja ya masharti ni pamoja na makato ya riba yasiyozidi aslimia 10, na mtumishi atatakiwa kutumia kipindi cha miaka 5 hadi 25 ili kurejesha mkopo katika taasisi hiyo.

  Akifafanua zaidi Dkt. Msemwa alisema Nyumba hizo zitakuwa ni za kisasa zaidi kwani maeneo yote yaliyojengwa nyumba hizo yamepimwa na kutakuwa na miundombinu bora zaidi ikiwemo barabara, maji na umeme, hivyo aliwataka  watumishi wa umma kujitokeza kwa wingi ili waweze kujipatia nyumba hizo.

  Kwa mujibu wa Dkt. Msemwa mpaka sasa wamepokea jumla ya maombi 500 kutoka kwa watumishi wa Serikali na ofisi yake imeanza mchakato wa kupitia maombi hayo na kuangalia kama wamekamilisha vigezo vya kimsingi ikiwemo masharti ya kuwa mwajiriwa katika sekta ya umma pamoja na kuwa mwanachama wa mfumo wowote wa pansheni.

  “Leo hii watumushi wengi wa Serikali wameshindwa kununua nyumba kutoka katika taasisi mbalimbali, utakuta nyumba ya Tsh. Milioni 30,000,000 mtumishi anatakiwa kukatwa asilimia 10 ya mshahara wake ambayo ni Tsh. 3,000,000, hivyo wengi wao wamejikuta wakishindwa” alisema.

   
  Na Ismail Ngayonga
  MAELEZO
  Dar es Salaam
  14.08.2014

  0 0


  Jumla ya Dola za Marekani  milioni 53.8  zilipatikana kutokana na mauzo ya vito mbalimbali ndani ya nchi  kwa mwaka wa fedha 2013/2014.
  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha  Uchambuzi na Uthamini wa Madini ya Almasi na Vito, (TANSORT) kilichopo chini ya Wizara  ya Nishati na Madini   Archard Kalugendo kwenye semina  iliyoshirikisha Makamishna Wasaidizi wa Madini wa Kanda,  Afisa Madini Wakazi na  Wataalamu wa Wizara ya Nishati na Madini inayoendelea Bagamoyo  yenye lengo la  kujadili  utendaji na  uboreshaji wa  shughuli za uthaminishaji wa madini ya almasi na  vito nchini.
  Kalugendo alisema kuwa  mauzo hayo  yanatokana na usimamizi mzuri wa Kitengo hicho  katika kuthaminisha  almasi na vito kwa ajili ya kukokotoa mrabaha wa Serikali; Kutayarisha miongozo ya bei (Price Guides)  ya almasi na madini ya  vito inayotumika kukokotoa mrabaha na  Kutoa huduma za kijemolojia (Gemmological Services) kwa wachimbaji wadogo na wa kati na Kusimamia mauzo na kufuatilia mwenendo wa masoko ya almasi na  madini ya vito.
    Kutokana na  usimamizi mzuri wa  mauzo na kufuatilia mwenendo wa masoko ya almasi na  mad  ini ya vito, ulipelekea wastani wa bei ya almasi za Tanzania katika soko la dunia kupanda hadi  dola za Marekani 286 kwa karati   ikiwa ni ongezeko la  asilimia 13, alisisitiza Kalugendo
  Alisema  masoko saba ya kimataifa yalifatiishwa ili kutambua mwenendo wa bei na masoko ya madini ya vito na almasi duniani ambayo ni  Bangkok, Antwerp, Basel, London, Changsha, Las Vegas na Arusha.

  Kalugendo aliongeza  kuwa  mafanikio yaliyopatikana kutokana na usimamizi mzuri wa shughuli za uthamini wa almasi na madini ya  vito  ni pamoja na  mauzo ya Tanzanite kuliingizia  Shirika la Madini la  Taifa (Kalugendo aliainisha mafanikio mengine yaliyopatikana kuwa ni pamoja na Kilo 818, gramu 269,211 na carat 40,599 za Tanzanite kuthaminiwa na kuuzwa na mgodi wa TanzaniteOne Minerals Limited (TML) wa Arusha.
  Akielezea changamoto za TANSORT  Kalugendo alisema ni pamoja na kada ya  Wajemolojia kutokuwa katika muundo wa Kada za Utumishi wa Umma , kutokuwepo kwa kituo  maalum  cha kufanyia biashara ya almasi na vito nchini na kuendelea kwa vitendo vya wizi, udanganyifu, utapeli na utoroshwaji wa madini ya almasi na vito nchini.
   Kalugendo aliendelea kueleza kuwa  kumekuwepo a  ukwepaji wa kodi na tozo za Serikali miongoni mwa wazalishaji na wafanyabiashara wadogo wa almasi na vito hali inayopelekea taifa kukosa mapato yake stahiki.
  Akielezea mikakati katika utatuzi wa changamoto hizo Kalugendo alisema  rasimu ya Kada ya Wajemolojia imekamilika kwa ajili  ya taratibu  zinazofuata pamoja na matayarisho kwa ajili ya  soko rasmi la kuuzia madini ya thamani kubwa hapa nchini  kuendelea kufanyiwa kazi na Wizara.
  Alisema  hatua mbalimbali  zinazoendelea ni pamoja na kufanya tathmini za mapato, kutafuta uwekezaji katika jengo hilo, kutathmini namna bora ya kuendesha soko hilo na kujifunza kutoka nchi nyingine juu ya uendeshaji bora wa masoko ya jinsi hiyo.
  Aidha, aliongeza kuwa TANSORT imejipanga kuendelea kutoa elimu  juu ya athari za vitendo vya udanganyifu, wizi, ukwepaji kodi, na utoroshaji wa madini ya vito.
  TANSORT ni Kitengo cha Uchambuzi na Uthamini wa Madini ya Almasi na Vito cha Wizara ya Nishati na Madini ambapo uthamini unalenga ukokotoaji sahihi wa mrabaha wa Serikali kama ilivyoelekezwa na Sheria ya Madini ya Mwaka 2010, Vifungu vya 87, 88 na 89.  Kitengo hiki kilichoanzishwa mwaka 1966 kina ofisi tano  sehemu tofauti tofauti ikiwa ni pamoja na Antwerp nchini Ubeljiji,  Kanda ya Mashariki (Dar es Salaam) Kanda ya  Kati- Magharibi (Shinyanga) Kanda ya Kaskazini (Arusha) Kanda ya Kusini (Songea).

  0 0

   Afande Sele, Prof J, kareem Omary na wakazi wengine wa Mjini Morogoro.Prof Jay amemshika mtoto mdogo wa Mfalme Sele Ahsante sanaa. Mamia ya wakazi wa mjini Morogoro leo, wameungana na mfalme wa Rhymes Tanzania Afande Sele katika mazishi ya mzazi mwenzie mama  Tunda aliyefariki usiku wa jana.  Katika mazishi hayo yaliyofanyika majira ya saa tisa alasiri Mwanamuziki Professor Jaya aliungana pia na swahiba wake wa miaka mingi katika kipindi hiki  kigumu wakiwemo ndugu jamaa na marafiki.
  MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMEN
   

  0 0

  DSC_0323
  Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph, akifafanua jambo kwa Diwani wa kata ya Ololosokwani ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika lisiolo la kiserikali la RAMAT inayomiliki Redio Loliondo FM, Bw. Yannick Ndoinyo (kushoto) wakati wa ziara ya kukagua miradi inayofadhiliwa na UNESCO. Bw. Al Amin aliambatana na wadau wa maendeleo Meneja Mauzo wa Samsung tawi la Tanzania, Bw. Sylvester Nteere (wa pili kushoto) na Mwakilishi wa Ubalozi wa Uswiss nchini, Bw. Erick Kalunga (hayupo pichani). Kulia ni Afisa Miradi kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO, Myoung Su Ko. wengine wakinamama wakikundi cha kimasaia waliofika kupokea ugeni huo.

  Na Mwandishi wetu
  Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni duniani (UNESCO) limezitaka redio za jamii kuendelea kutoa elimu kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii hususan ukeketaji kwa akina mama kwa kuelezea athari zitokanazo na ukeketaji ili kuisaidia jamii yenye mila hizo kuachana nazo kabisa.

  Hayo yamebainishwa na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph wakati wa ziara ya kutembelea miradi kwenye vijiji vya Ololosokwani wilayani Ngorongoro na kuzitaka redio za kijamii kuwa sehemu ya kutoka elimu ya katiba ili kuiwezesha jamii kufahamu wajibu wao kama raia ili wakati unapofika waweze kufanya maamuzi sahihi ya maendeleo.
  Al Amin alisema kuwa vipindi vya elimu ya Afya na masuala ya kijamii yahusuyo serikali na jamii kwa ujumla yanapaswa kupewa kipaumbele na redio hizi katika masuala ya huduma za kijamii hususan ndoa za utotoni, ukeketaji na ajira za utotoni ili ziweze kukomeshwa katika jamii kwani zinarudisha maendeleo ya mtoto hasa wa kike.
  DSC_0353
  Sehemu maalum ya anayotumia mtoa huduma wa maktaba hiyo inayofadhiliwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ambapo kutokana na shida ya umeme katika eneo hilo Kompyuta hiyo inatumia umeme wa jua (solar).

  “Kwa sasa hapa nchini kumekuwa na mjadala wa Katiba Mpya mchakato unaoendeshwa na Bunge la Katiba linaloendelea na vikao vyake mjini Dodoma. Wananchi wana haki ya kujua kila kinachoendelea, kushiriki katika mijadala mbalimbali itakayosaidia kupanua uelewa wao ili mwisho wa siku wanajamii waweze kuwa na maamuzi sahihi na hilo ndio lengo la redio” alisema Al Amin.

  Alisema kuwa japo matangazo yamekuwa ya muda mfupi redio Loliondo imekuwa faraja na imetoa mchango mkubwa katika kusaidia jamii kupata uelewa kwenye masuala mbali mbali ya kijamii hususan wizi wa mifugo na utunzaji wa mazingira ya kiikolojia kwenye maeneo husika kwenye uwanda wa eneo la pori tengefu la Loliondo.

  Nae Mkurugenzi wa RAMAT Yannick Ikayo ambayo inaendesha mradi wa redio ya kijamii ya Loliondo FM alisema kuwa redio hiyo imekuwa mkombozi kwa kutoa elimu kwa jamii na imesaidia kuongeza uelewa na madhara mbali mbali kwenye masuala ya kijamii hususan ukeketaji na utunzaji wa mazingira ya kijamii.
  DSC_0300
  Jengo la Maktaba inayofadhiliwa na UNESCO iliyopo kwenye kijiji cha Ololosokwani wilayani Ngorongoro kwa uangalizi wa Shirika lisiolo la kiserikali la RAMAT.

  Loliondo FM Redio ilianzishwa mwaka Oktoba 2013 pamoja na Maktaba na Ujenzi wa Kituo cha Utamaduni ambavyo lengo ni kusogeza elimu kwa jamii ya kifugaji na kupata uelewa wa masuala mbali mbali yanayowazunguka ikiwemo utunzaji wa mazingira.

  “Migogoro ya kijamii imekuwa ikipatiwa ufumbuzi hali inayoifanya jamii ya kifugaji kufaidika na redio hii kwani imekuwa na msaada mkubwa kwa jamii yetu na wilaya kwa ujumla hivyo tunaiomba jamii kuipa ushirikiano na kuamini kuwa redio hiyo ni mkombozi wao na kiunganishi kati yao na watawala”, amehitimisha Ikayo.

  Wilaya ya Ngorongoro imeonekana kuwa na changamoto katika elimu hasa vijana wa kike kuacha masomo kwa ajili ya kuolewa na wengine kukimbia kukeketwa hali inayohitaji serikali kutoa elimu kubwa kwa jamii ya kifugaji kuachana na mila potofu ikiwemo ukeketaji ulioshamiri.
  Wanahabari walitembelea wilayani humo waliwashudiwa wasichana kutoka kabila la kifugaji wakiwa tayari wamekeketwa kwa kuvalishwa mavazi maalum yanaonyesha kutoka kwenye tohara huku wakimshuhudia msichana aliyeshindwa kwenda kujiunga na kidato cha kwanza akiuza mkaa kwa kisingizio cha kukosa ada.
  DSC_0283
  Mkurugenzi wa Shirika lisiolo la kiserikali la RAMAT inayomiliki Redio Loliondo FM, Bw. Yannick Ndoinyo (wa pili kushoto) akielezea maendeleo ya miradi mbalimbali inayosimamiwa na Shirika lake ikiwa chini ya ufadhili wa UNESCO kwa ugeni ulioambatana na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (katikati) wakati wa ziara ya kukagua miradi hiyo.
  DSC_0959
  Baadhi watoto wa jamii za kifugaji wa kijiji cha Ololosokwani ambao wanastahili kupata elimu ya awali lakini wazazi huwaamuru kwenda kuchunga mifugo kama walivyokutwa na mpiga picha wetu kwenye maeneo ya kijiji hicho.

  0 0

  Ndugu zangu,

  Leo alfajiri niliongoza mjadala kwenye redio za Kwanza Jamii na Nuru FM kuhusiana na kongamano linaloendelea Dar la Watanzania wa Diaspora wanaokutana nyumbani, Tanzania. Ni kwa nini tuna hofu na Watanzania wenzetu walio ughaibuni? Hofu hii ni ya kihistoria. 

  Kwanini kongamano hili la kwanza kufanyika lisiwe la mwisho kufanyika katika sura yake hii, kwamba maudhui ya kongamano yenyewe kuwa ni ; connect, engage, inform and ivest nako kunakosekana dhana integration kwa maana ya kujumuisha.

  Hoja kubwa kwa sasa ni kwa namna gani tunawajumuisha wenzetu walio ughaibuni kupitia uraia pacha. Kwamba wakati umefika wa kubadilika na kuona kuwa uraia pacha una maanufaa makubwa kwetu kama taifa. Haipaswi kuendelea kuwachukulia wenzetu walio diaspora kama ' Ng'ombe wa Maziwa'- Fuatilia mjadala huu...

  0 0


   Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri Baharini Bw. Ahmed Shehe, akizungumza katika Mkuta wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Kusini Unguja, Manahodha na wamiliki wa vyombo vidogo vya usafiri baharini katika Ukumbi wa SUZA Tunguu. (kuli) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Idrissa Muslim Hija na (kusho) Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri Baharini Bi. Sheikha A. Mohammed.
   Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Idrissa Muslim Hija akifungua Mkutano wa siku moja wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kusini pamoja na masheha, manahodha na wamiliki wa vyombo vidogo vya usafiri baharini uliandaliwa na Mamlaka ya Usafiri Baharini huko Tunguu. 
   Mwanasheria wa Mamlaka ya Usafiri Baharini Nd. Rashid J. Mohammed akiwasilisha mada kuhusu sheria za usafiri wa baharini.
   Sehemu ya washiri wa Mkutano huo.
   Kamanda wa KMKM Kamandi ya Kusini Unguja CDR. Moh’d Mussa (Mkobani) akitoa mchango katika Mkutano huo. 
  Sheha wa Unguja Ukuu Tindini Mzee Jecha Ali akitoa mchango wake katika Mkutano huo. (Picha na Makame Mshenga- Maelezo Zanzibar).


  =========== ========== =========
  Na Miza Othman Mkame  Maelezo –Zanzibar    

  Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Idrissa Muslim Hija amewataka wananchi wanaotumia  Bandari za Mkoa wa Kusini kuwa na Umoja na Ushirikiano kwa lengo la kulinda  usalama ndani ya  Mkoa huo. 

  Ameyaeleza hayo wakati alipokuwa akizungumza na wakuu wa kamati za ulinzi na usalama,  Masheha, Manahodha na wamiliki wa vyombo vidogo vidogo vya  usafiri wa baharini pamoja na wananchi wa Mkoa huo katika  Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibnar (SUZA)  Tunguu.

  Amesema  Masheha  wanajukumu kubwa katika kulinda na  kusimamia  usalama wa bandari zote zilizomo ndani ya Mkoa huo ili kuhakikisha sheria zilizowekwa zinafuatwa.

  “Mamlaka ya Usafiri Baharini (ZMA) imeundwa kusimamia Manahodha wa vyombo vya Baharini na kila mmoja anahaki ya kulinda na kuzuia uhalifu usiweze kutokea”, alisema Idrisa Muslim Hija.

  Mkurugenzi wa usajili na vyeti Sheikha Juma amesema  sheria za kulinda usalama wa bandari  zimeshaanzishwa tangu mwaka 2010 kwa hivyo kila raiya  analazimika kuzifuate ili kuondosha migogoro isiyo ya lazima.

   Amesema hadi hivi sasa wameshaanza kusajili vyombo vidogo vidogo vyenye urefu wa ziraa  nane au urefu wa mita nne kwani kufanya hivyo kutapelekea kurahisisha upatikanaji  wa chombo cha muhusika wakati anapotokewa na tatizo ikiwemo kupotea, kuungua na hata kuibiwa kwa chombo chenyewe.

  “Nilazima raiya atekeleze  sheria zilizopo ili kujiepusha  na majanga na panapotokea ajali  muhusika aweze kulipwa fidia”, alisema Sheikha Juma Mohammed. Aidha amesema nilazima Manahodha wawe mstari wa mbele  kutekeleze sheria za bandari zilizopo  kwa lengo la kusaidia Serikali kuipatia mapato ili iweze kujiimarisha kiuchumi.

  IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR             

  0 0

   Makamu Mwenyekiti wa TAHLISO Abdi Mahmoud Abdi akizungumza na Waandishi wa habari leo Mjini Idara ya Habari maelezo Zanzibar kuhusu kukanusha Taarifa ya Maandamano yaliyopangwa kufanyika hapo kesho. Picha na Makame Mshenga

  Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar.

  Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu TAHLISO limekanusha Taarifa zilizosambazwa katika Vyombo vya habari na Mitandao ya Kijamii juu ya kuwepo wa maandamano ya Wanafunzi wa Vyuo vikuu yanayotarajiwa kufanyika hapo kesho Ijumaa.Shirikisho hilo pia limesema Taarifa za kuwepo kwa maandamano hayo hazijatolewa na TAHLISO na kuwaomba Wanafunzi kutojaribu kushiriki katika Maandamano hayo.

  Akizungumza na Waandishi wa habari leo Mjini Zanzibar Makamu Mwenyekiti wa TAHLISO Abdi Mahmoud Abdi amesema aliyesambaza Taarifa za Maandamano hayo ni Mtu ambaye alishavuliwa Nyadhifa za Uongozi wa TAHLISO na kwamba anachokifanya ni Upotoshaji na kujipalilia kisiasa.

  “Anayejiita Mwenyekiti wa TAHLISO Musa Mdede SI MWENYEKITI HALALI kwasababu vikao halali vya Shirikisho vilivyofanyika May 3,4,2014 katika Chuo cha kodi vilimwondoa madarakani na kwa mujibu wa Katiba nafasi yake ilikaimiwa na Makamu wake ” Alisema Abdi.

  Amesema sababu ya Msingi ya kumuondoa katika nafasi yake ilitokana na kwenda kinyume na Katiba kwa kujiingiza katika Siasa ambapo aligombea na kuangushwa katika kura za maoni kupitia CHADEMA. Amedai kuwa anachokifanya Mdede kwa sasa ni upotoshaji kwa TAHLISO ambapo anajitangaza kwa malengo ya kugombea uchaguzi mkuu unaokuja wa mwaka 2015. 

  Amefahamisha kuwa licha ya kuwepo na Taarifa ya Baadhi ya Vyuo kutokupata Pesa kwa ajili ya Mafunzo ya Vitendo TAHLISO imekuwa bega kwa bega kuhakikisha suala hilo linapatiwa majibu ya haraka.

  Amesema BODI ya Mikopo inaendelea kuchukua hatua za haraka katika kuhakikisha Vyuo husika Vinapatiwa fedha na kwamba siku ya Leo Bodi itatoa Fedha kwa Chuo kikuu Kishiriki  cha kumbukumbu ya Stephano Moshi (SMUCCO)  na Chuo kikuu cha Jordan Morogoro.

  “Chuoni siyo sehemu ya kufanya Siasa bali ni sehemu ya kusoma, Maandamano siyo suluhu njia pekee ni mazungumzo na tunaendelea kuyafanya” Alifafanua Abdi.

  Aidha Makamu Abdi amesema taratibu zinazohitajika zinaendelea kuchukuliwa ili Vyuo vingine vilivyobakia viweze kupata fedha hizo.
  Vyuo ambavyo havijapata Fedha za Mafunzo kwa Vitendo ni pamoja na Chuo kikuu cha Mtakatifu Augustino(SAUT) Mwanza na Tabora, Chuo cha Usimamizi wa Fedha(IFM), Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji Mbeya na Chuo kikuu cha Tumaini Makumira-Iringa.

  Katika taarifa zilizosambaa kwenye Vyombo vya habari na Mitandao ya kijamii inadaiwa kesho Ijumaa kutafanyika Maandamano ya amani ya Wanafunzi wa Vyuo vikuu kuelekea Ofisi za Waziri Mkuu kushinikiza Serikali kutoa Shiligi Bilioni 6.6 kwa ajili ya mafunzo ya Vitendo kwa wanafunzi hao.

  Makamu huyo ambaye anashika nafasi ya Uenyekiti kwa sasa amewaomba Wanafunzi ambao hawajapata fedha zao kuwa watulivu wakati wakisubiri kupata fedha zao huku hatua za haraka zikichukuliwa.
  IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR

  0 0

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Mhe. Stephen Masele akizungumza wakati akifunga Mkutano wa Tatu wa Vijana Wanasayansi Duniani, jijiji Dar es Salaam.

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Mhe. mStephen Masele akimpa zawadi ya kinyago iliyotolewa na mtandao wa Vijana Wanasayansi Duniani (YES), Rais wa Wajilojia barani Afrika Profesa Aberra Mogessie.

   Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Mhe Stephen Masele, katika picha ya pamoja na baadhi  ya Wanasayansi Vijana Duniani waliohudhuria mkutano tatu nchini Tanzania. Wengine katika picha waliokaa kutoka kushoto ni Mtendaji Mkuu Wakala wa Jiolojia Tanzania, Profesa   Abdulkarim Mruma, Rais wa Wajilojia Barani Afrika Profesa Aberra Mogessie, Rais wa  Vijana Wanasayansi Duniani Meng Wang na Mwenyekiti wa Vijana Wanasayansi, Tanzania Steven Nyagonda.

  ==========   ========  =========
  Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam .
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Stephen Masele amesema kuwa bara la Afrika linahitaji taaluma ya sayansi kutokana na umuhimu wake kwa maendeleo na ukuaji wa uchumi. Masele ameyasema hayo jijini Dare es Salaam wakati akifunga Mkutano wa Tatu wa Vijana Wanasayansi Duniani (YES), na kuongeza kuwa, Afrika inahitaji sayansi kwa ajili ya kufanya ugunduzi na tafiti ambazo zitachangia katika kuchochea maendeleo barani Afrika. 
  Aliongeza kuwa, kutokana na umuhimu huo, Wizara ya Nishati na Madini imedhamiria kuwekeza kwa vijana katika tasnia ya sayansi ikiwemo kuhamasisha Vyuo Vikuu nchini, kuanzisha masomo ya sayansi hususan katika sekta ndogo ya gesi na mafuta jambo ambalo litawezesha kuzalisha wataalam wengi zaidi watakaosaidia kuendeleza taaluma hiyo na rasilimali zilizopo nchini. 
  Kutokana na umuhimu huo, aliutaka Mtandao wa Vijana Wanasayansi Duniani (YES), kuhakakikisha unasaidia kuwezesha vijana kuona umuhimu wa kuingia katika taaluma ya sayansi hususan jiolojia ili kuwezesha bara la Afrika kuwa na wataalamu wengi watakaosaidia kuharakisha maendeleo kupitia rasilimali asilia.
   “Mtandao wa vijana mna jukumu la kuchochea taaluma ya sayansi kwa vijana. Afrika inahitaji wanasayansi wakutosha, kwa kuwa, uwepo wao utasaidia kuchochea ukuaji wa viwanda na teknolojia barani Afrika,” alisisitiza Masele. 
  Aidha, alieleza kuwa, Afrika inahitaji wataalamu wanasayansi hivyo, alitoa wito kwa kuwashirikisha vijana katika masuala ya kitaaluma ikiwemo kufanya maamuzi.
  “Nikiwa kiongozi kijana, nawataka vijana kuona umuhimu wa taaluma hii, hivyo, nawatanguliza ninyi katika hili, nendeni mkawafundishe na kuwahamasisha wenzenu waone umuhimu wa sayansi kwa dunia na kwa Afrika,”alibainisha Masele. 
  Aidha, aliongeza kuwa, kama kiongozi kijana, atatumia nafasi yake, kusaidia uwepo wa sera nzuri ambazo zitahamasisha ukuaji wa taaluma ya sayansi na kuwezesha vijana kisayansi. 
  Kwa upande wake, Rais wa Vijana Wanasayansi Duniani, Meng Wang alieleza kuwa, mkutano huo wa tatu umeacha historia kwa Tanzania na Afrika kutokana na kupata nafasi ya kukutana, kujadili na wanasayansi wakubwa waliobobea katika masuala ya Jiolojia Afrika na Duniani jambo ambalo litasaidia kuchochea ari ya vijana kuendeleza taaluma hiyo ikiwa ni pamoja na kuhamasisha vijana wengi zaidi kuingia katika sekta hiyo.

  0 0  0 0


  Na Eleuteri Mangi- MAELEZO

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda amewatoa Watanzania hofu kuhusu suala la wageni kumiliki ardhi nchini. 

  Waziri Mkuu Pinda alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es salaam wakati akifungua mkutano wa pili wa majadiliano ya pamoja kati ya Serikali ya Mitaa ya China na Tanzania ambapo walishirikiana pia na sekta ya biashara kutoka nchi hizo.

  “Hofu ni halali na ni lazima kwa Watanzania katika masuala ya umiliki wa ardhi maana ni vema tuifikishe nchi mahali pazuri” alisema Pinda. Waziri Mkuu Pinda alisema kuwa Tanzania ni nchi inayolinda ardhi yake tofauti na nchi nyingine ambapo ardhi yote ni mali ya umma na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndio mwenye dhamana na mamlaka na ardhi ya Tanzania kwa niaba ya Watanzania.

  Akifafanua Waziri Mkuu alisema kuwa suala la mwananchi au mwekezaji kumiliki ardhi hutolewa kwa kipindi kwa maalumu kwa minajili ya kutoa huduma mbalimbali za kijamii ambapo mwekezaji anapewa umiliki wa ardhi kwa muda tofauti kulingana na huduma anayotoa. Waziri Mkuu Pinda alisema kuwa Watanzania ni lazima wajipange vizuri ili kuifikisha nchi mahali pazuri katika masuala ya uwekezaji ambapo nchi haiwezi kuendelea bila kuwa na wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

  “Ushirikiano tunaoufungua na rafiki zetu kutoka China ni hatua kubwa ya kutambua na kusimamia  dira yetu kati ya Tanzania na China ambayo ni kielelezo cha malengo makubwa ya mataifa haya mawili kwa kuzingatia uwekezaji unaojali usalama wa mazingira na kuboresha maisha ya watu” alisema Pinda.

  Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia akimkaribisha Waziri Mkuu alisema kuwa sekta binafsi na uwekezaji nchini na China zinasaidia kuongeza fursa za biashara na uwekezaji baina ya nchi hizo mbili na zitasaidia kukuza kipato cha wananchi na nchi kwa ujumla.

  Kwa upande wake Katibu Mkuu TAMISEMI Jumanne Sagini akitoa mada juu ya fursa za uwekezaji alisema kuwa Tanzania ina maeneo mengi yenye fursa za kiuwekezaji. Sagini aliyataja maeneo hayo kuwa ni mikoa 8 ikijumuisha Tanga, Dar es salaam, Pwani, Morogoro, Mtwara, Lindi, Katavi na Singida.

  0 0

    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya utoaji Tuzo kwa Wanasayansi wachanga kutoka shule mbalimbali za Sekondari za Tanzania, iliyofanyika jana Agosti 13, 2014 kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Lumumba ya mjini Zanzibar, Dhariha Amour (kulia) na Salma Khalfan (wa pili kulia) wakati wakimuelezea jinsi walivyoweza kufanya utafiti  wa kutumia Karafuu na Limao kutengeneza dawa ya kufukuza Inzi , wakati Makamu alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonesho ya Wanasayansi wachanga, yaliyofanyika jana Agosti 13, 2014 sambamba na utoaji tuzo za washindi wa maonesho hayo, katika ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwakabidhi Tuzo washindi wa jumla wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Lumumba ya mjini Zanzibar, Dhariha Amour (wa pili kushoto) na Salma Khalfan (wa tatu kulia) baada ya kutangazwa kuwa  washindi wa jumla katika maonesho ya Wanasayansi wachanga  kwa  kufanya utafiti  wa kutumia Karafuu na Limao kutengeneza dawa ya kufukuza Inzi , wakati  wa halfa ya utoaji Tuzo hizo wa wanasayansi wachanga iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam jana Agosti 13, 2014.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea mabanda ya maonesho.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia jambo baada ya kuwakabidhi Tuzo washindi wa jumla wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Lumumba ya mjini Zanzibar, Dhariha Amour (wa pili kushoto) na Salma Khalfan (wa tatu kulia) baada ya kutangazwa kuwa  washindi wa jumla katika maonesho ya Wanasayansi wachanga  kwa  kufanya utafiti  wa kutumia Karafuu na Limao kutengeneza dawa ya kufukuza Inzi , wakati  wa halfa ya utoaji Tuzo hizo wa wanasayansi wachanga iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam jana Agosti 13, 2014.

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ilongero, John Andrea (wa pili kulia) na Thobias Clement, wakati wakimuelezea jinsi walivyoweza kufanya utafiti  na kugundua matumizi ya Kinyesi cha wanyama kuzalisha Umeme, wakati Makamu alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonesho ya Wanasayansi wachanga, yaliyofanyika jana Agosti 13, 2014 sambamba na utoaji tuzo za washindi wa maonesho hayo, katika ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijum uika na baadhi ya viongozi kushuhudia zoezi la utoaji tuzo za wanasayansi Wachanga lililofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jana . P_icha na OMR

  0 0  Happy-Siana Appia Kirenga

  19.12.1966 - 5.07.2014


  Familia ya Marehemu Mzee Appia Thomas Kirenga wa Machame Kisiki Moshi inayo heshima kubwa kutoa shukrani za dhati kabisa kwa ndugu, jamaa na marafiki ambao walishiriki kwa namna moja ama nyingine kufanikisha msiba, mazishi na hatimaye matanga ya mtoto/Dada yao mpendwa, Happy-Siana Appia Kirenga aliyefariki dunia usiku wa  Jumamosi  ya July 5 kwenye Hospitali ya Taifa  ya Muhimbili na kuzikwa jirani na alipopumzishwa baba yake mzazi, nyumbani, Alhamisi ya July 10, 2014.

  Kwa vile walivyotuunga mkono na kutufariji wakati wa kipindi hiki kigumu cha msiba huu mkubwa ni wengi na ni vigumu kuwataja wote kwa majina, Familia, inapenda kwa heshima na taadhima nyingi kutoa shukrani za jumla ikiwaomba wote mkubali kuzipokea kwa moyo ule ule kama mlivyotuunga mkono. Mmetufariji sana, mmekesha nasi, mmeshinda nasi, nyote mmekuwa kimbilio salama kwetu wakati wa kipindi hiki kigumu. 

  Mmeonesha upendo wa kweli kweli kwetu kama Familia na kwa mwanetu dada yetu ambaye angerejea kwenye uzima tena, naye bila shaka yoyote angetoa shukrani za dhati ya moyo wake.

                          Hata hivyo, tunapenda kutoa shukurani kwa makundi machache ya marafiki ambao mchango wao utabakia kwenye nyoyo za wazazi na familia yetu  tukianza na majirani na marafiki wa karibu wa Familia walioko Dar es Salaam, Moshi, Arusha, Morogoro, Dodoma, Manyara, Kagera, Mbeya na kwingineko Tanzania, Kenya na nje ya Afrika Mashariki, ambao michango yao kamwe haitasahaulika.

  Familia pia inapenda kuwashukuru wanajumuia wa Sayuni Mtaa wa Neema Usharika wa Mbezi Makabe Dar Es Salaam, Uongozi na Washarika wa Makongo Juu Dar es Salaam, uongozi na Washarika wa Kalali Machame Moshi na Watumishi Wengine wa Mungu kutoka sharika mbalimbali wakiongozwa na Askofu Mstaafu Dk Erasto, N. Kweka  kwa huduma kubwa za kiroho wakati wa msiba huo mkubwa uliotufika.

  Familia vile vile inapenda kutoa shukrani za dhati kabisa kwa Dr Ayoub Pamba, na kwa Wauguzi na Madaktari wa Hospitali za Tumbi Kibaha na Muhimbili Dar es Salaam kwa juhudi zao za dhati za kutaka kuokoa maisha ya Dada yetu

  Aidha, tunatoa shukrani kwa wafanyakazi na uongozi wa Super Sky Aviation,  Regional Air Limited, Wafanyakazi marubani wakiongozwa na Kapten Tatiya Tukero Naikuni, na mfanyakazi mmoja mmoja kwa jumla michango yenu, ilitufariji na tutaendelea kukumbuka ukarimu wenu daima. 

              Vile vile, Familia inawashukuru sana wanakijiji cha Wari, Kata ya Machame, Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro, kwa kuupokea vizuri na kuushughulikia kwa heshima zote msiba wa mtoto wao Happy-Siana Appia Kirenga.


  Mwisho Tunawashukuru nyote mlioweza kufika nyumbani Machame Kisiki kumhifadhi Dada Happy.  Hatuna cha kuwalipa, Mungu atawalipa.

  “Mathayo 5: 8 :- Heri wenye moyo safi;  Maana  hao watamwona Bwana”

  0 0

   Idara ya Uhamiaji Nchini, imewakamata Raia wa nane (8) wa kigeni wakati wakiingia nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Nyerere, wakiwa na pasipoti bandia za kusafiria za Mataifa tofauti ya Ulaya. Wageni hao walikuwa wakijaribu kuingia nchini leo tarehe 15.08.2014 majira ya saa nane na nusu usiku kwa ndege ya shirika la Ndege la Uturuki yenye Namba TK 603,  wakitokea Uturuki na kujitambulisha kuwa Raia wa Sweden na Belgium.

    Maofisa Uhamiaji katika kituo hicho baada ya kuwatilia mashaka na kuwafanyia ukaguzi wa kina, waligundua kuwa wageni hao ni Raia wa Iraq wakijaribu kuingia nchini Tanzania na pasipoti za bandia.      

  kukamatwa kwa wageni hao ni jitihada za Idara ya Uhamiaji kupambana na Uhamiaji haramu nchini ambapo suala la zima la Udhibiti wa Mipaka linapewa kipaumbele. akizungumzia tukio hilo, Kaimu Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Tatu Burhan, anasema, kwa kutumia ujuzi na weledi walionao Maofisa Uhamiaji wanaendelea kufanyakazi usiku na machana kuhakikisha Sheria na Taratibu za Uhamiaji zinafuatwa. "Idara ya Uhamiaji, iko macho hatulali kuhakikisha Ulinzi na Usalama wa nchi ikiwa ndio jukumu letu namba moja unaimarika. kwahivyo, kila mtu awe Raia wa kigeni na Watanzania wanapaswa kufuata Sheria na Taratibu zilizopo za kuingia na kutoka nchini"   .

     Hadi sasa, Wageni hao wamezuiliwa kuingia nchini na wanaendelea kushikiliwa na Maofisa wa Idara ya Uhamiaji kituoni hapo huku wakisubiri kurudishwa walikotoka.  Hili ni wimbi lilioibuika hivi karibuni kwa baadhi ya Raia wa nchi za Iraq, Iran, Syria kujaribu kuingia nchini isivyo halali huku ikisemekana lengo lao kubwa ni kuingia Tanzania na baadae kutoka kuelekea Mataifa ya Ulaya.

  Majina ya Wageni hao na Pasipoti bandia walizokuwa wakitumia pamoja na Majina halisi na Pasipoti zao za Iraq zilizogunduliwa baada ya upekuzi kwenye mabano ni kama ifuatavyo;

  1. ADEL SHAALAN MOHAN - SWEDISH, PPT. NO. EI282207 ( ADEL SHAALAN MOHAN Pasipoti Nam. G1489664)
  2. SAMER HELMI KAMIT    -  SWEDISH, PPT. NO. 87187804 ( LAZIM MOSA HITEET, PPT. Namba, A 13466001)
  3. MOHAMMED JAFAR AL MOSAWI - SWEDISH, PPT.NO. 87168871 (ALI HUSSEIN OLEIWI, PPT. NO. G 1111623)
  4. DAVID GABRIEL POBLETE    - SWEDISH PPT.NO. 86867751 (AYAD SAMI MAKTTOOF, PPT NO. A 4910203)
  5. SADDAM ALKHAMERI AREF   - SWEDISH, PPT NO. 81640513 (SAIF ALDAN FALIH HASAN, PPT. NO. G 1489664)
  6. ALI MOHAMMED ABDULLAH - IRAQ, PPT. NO. A 5931725
  7. OSAMAH ZAID GHAEB AL-OBAIDI    - IRAQ, PPT. NO. A 6175951
  8. ALI HUSSEIN OLEIWI      - IRAQ, PPT. NO. G 1111623 

     

older | 1 | .... | 342 | 343 | (Page 344) | 345 | 346 | .... | 1897 | newer