Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

Padri Evaristus Gabriel Mushi azikwa leo zanzibar

$
0
0



ASkofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Muadham Policup Kadinari Pengo,kwa pamoja na maaskofu wengine wakichomeka Msalaba katika kaburi la marehemu  Padri Evaristus Gabriel Mushi,aliyezikwa leo  katika viwanja vya kanisa Katoliki la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja,ambae alifariki Jumapili Iliyopita kwa kupigwa risasi na watu wasiojukanwa



Rais wa Zanbzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Mohamed Shein,(katikati) akiweka shada la mauwa katika kaburi la Marehemu  Padri Evaristus Gabriel  Mushi,wakati wa mazishi yake yaliyofanyika leo  katika viwanja vya kanisa la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja.


Rais wa Zanbzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Mohamed Shein,(katikati) akitia udongo  katika kaburi  la Marehemu  Padri Evaristus Gabriel  Mushi,wakati wa mazishi yake yaliyofanyika leo  katika viwanja vya kanisa la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja.


 Waziri  wa  Mambo ya Ndani ya Nchi Emanuel Nchimbi ,akitia udongo  katika kaburi la Marehemu  Padri Evaristus Gabriel Mushi,wakati wa mazishi yake yaliyofanyika leo  katika viwanja vya kanisa la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja.


Askofu wa Kanisa  Katoliki Jimbo la Zanzibar Augustino Shao, akitia udongo katika kaburi la Marehemu Padri Evaristus Gabriel  Mushi,aliyezikwa leo  katika viwanja vya kanisa Katoliki la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja. 


Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Tanga Antony Banzi,akiongoza  sala  wakati wa mazishi ya  Marehemu  Padri Evaristus Gabriel  Mushi,aliyekufa kwa kupigwa risasi Jumapili Iliyopita na kuzikwa leo katika viwanja vya kanisa la Kitope,Wilaya ya kaskazini B Unguja leo.

 Vijana waumini wa Dini ya Kikiristo wakiteremsha jeneza lenye mwili wa marehemu  Padri Evaristus Gabriel  Mushi,katika kaburi  alilozikwa  leo katika viwanja vya kanisa la Katoliki la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja,marehemu alifariki kwa kupigwa risasi Jumapili iliyopita na watu wasiojulikana.


 Baadhi ya waumini wa kanisa katoliki  wakiwa katika mazishi ya marehemu  Padri Evaristus Gabriel  Mushi,aliyezikwa leo  katika viwanja vya kanisa Katoliki la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja,ambae alifariki Jumapili Iliyopita kwa kupigwa risasi na watu wasiojukana.


 Waumini wa Dini ya Kikiristo wa Kanisa katoliki na wananchi wakifukia udongo katika kaburi la marehemu  Padri Evaristus Gabriel  Mushi,aliyezikwa leo  katika viwanja vya kanisa Katoliki la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja,ambae alifariki Jumapili Iliyopita kwa kupigwa risasi na watu wasiojukana.


 Rais wa Zanbzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Mohamed Shein,(katikati) akifuatana na Askofu wa Kanisa  Katoliki Jimbo la Zanzibar Augustino Shao, wakielekea katika Mazishi ya Padri Evaristus Gabriel  Mushi,aliyezikwa katika viwanja vya kanisa la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja.[Picha na Ramadhan Othman,IKULU.]



========  ========  =========  =======
Na Maelezo Zanzibar   
   
      20/02/2013

Mamia ya Wananchi wa Zanzibar leo wameshiriki Mazishi ya Padri Evaristus Mushi aliyeuwa kwa kupigwa Risasi na Watu wasiojulikana ambayo yamefanyika katika kijiji cha Kitope Wilaya ya Kaskazini B,Unguja.

Katika mazishi hayo Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Shariff Hamad,Viongozi wa Serikali na Vyama vya siasa walihudhuria.

Akitoa salamu za Serikali katika Mazishi hayo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohammed alisema Serikali imeguswa sana na kifo cha Padri huyo na kuongeza kuwa itahakikisha waliohusika na tukio la mauji hayo wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria. Kwa upande wake Askofu wa Kanisa la Anglikacana Michael hafidh amewataka Waamini wa dini ya kikristo kuwa watulivu bila kulipiza kisasi bali waiachie Serikali kufanya kazi yake ili kuwabaini waliopoteza Uhai wa Marehemu huyo.

Awali Mazishi hayo yalitanguliwa na Misa takatifu ya kumuombea Marehemu iliyoendeshwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo kuu la Dar es Salaam Muadhama Policarp Kadinali Pengo katika Kanisa la Minara Miwili Mjini Zanzibar. Padri Mushi alifariki dunia Februari 17 baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana wakati akielekea Kanisani kuendesha Misa ya Asubuhi katika Kigangwe cha Mtakatifu Teresia eneo la Beit El Raas mjini Unguja.

Enzi za uhai wake Padri Mushi alikuwa Msomi wa Shahada ya Uzamivu ya Elimu ya Ushauri nasaha aliyoipata nchini Marekani ambapo umauti ulimkuta akiwa anaelekea kuendesha Ibada ya Jumapili ya kwanza ya Kwarezma. Padri Evarist Mushi wa Kanisa la Minara Miwili mjini Zanzibar alizaliwa June 15, 1957 Mkoa wa Kilimanjaro akiwa ni mtoto wa nne katika familia ya watoto sita ya Mzee Mushi.

 IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR

siku ya wanawake duniani,wanaume tuwapunguzie mzigo wanawake.!

Rais Kibaki awasili nchini kwa Ziara ya Kiserikali ya siku Mbili

$
0
0


Rais Mwai kibaki wa Kenya akikaribishwa  kwa maua na Mwanafunzi Tazmina Rasul(6) muda mfupi baada ya kuwasili nchini kwa ziara ya kiserikali (State Visit) ya siku mbili huku mwenyeji wake Rais Dkt.Jakaya Kikwete akiangalia. (Picha na Freddy Maro).

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Mwai Kibaki wa Kenya muda mfupi baaada ya kuwasili katika uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kwa ziara ya kiserikali (State Visit) ya siku mbili.


 Rais wa Jamhuri ya Kenya Emilio Mwai Kibaki akiwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere leo jijini Dar es salaam kwa ziara ya siku mbili na kupokewa na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete.

 Rais wa Jamhuri ya Kenya Emilio Mwai Kibaki akiwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete mara baada ya kuwasili  leo jijini Dar es salaam.
 Sehemu ya askari wa JWTZ walioshiriki katika mapokezi ya Rais wa Jamhuri ya Kenya leo jijini Dar es salaam. 

Rais wa Jamhuri ya Kenya Emilio Mwai Kibaki akipata ukaribisho wa burudani ya vikundi mbalimbali wakati wa mapokezi yake jijini Dar es salaam.Picha na Aron Msigwa -MAELEZO.

WITO KWA MABLOGA WETU KUWA WABUNIFU BADALA YA KUIBA AU KUNUKUU TU KAZI NA PICHA ZA WENZAO BILA IDHINI

$
0
0
Ukingoni mwa Ziwa Nyasa- Revo Meza
Ndesanjo Macha
Ukingoni mwa Ziwa Tanganyika- picha ya Revocatus Meza, Desemba 2012. Wimbi la “blogging” liliikumba dunia kati ya 1995 hadi 1998 na kuanza kumea kwetu Tanzania kupitia mwanahabari Ndesanjo Macha miaka kumi iliyopita. Wakati Ndesanjo anaanza kublogu si wengi tuliomwelewa. Nakumbuka alivyokua akiniongelea juu ya fani hii kwa hamasa kwenye 2002. Baadaye kidogo aliendesha Jikomboe, blogu lililokua na taswira ya majani mabichi ya ukoka. Enzi hizo hakukua na hata senti moja aliyoichuma. 

Ndesanjo Macha- mwasisi wa blogu Tanzania Ndesanjo alikua akisema blogu ni dunia ya kesho ya mawasiliano. Wakati huo vyombo vikubwa vya habari nchi zilizoendelea vilianza kuona umuhimu wa blogu vikaanza kuunda idara pembezoni mwa tovuti zake mama. Kwetu wenye magazeti wengi hawakupenda wanablogu;waliwaona washindani. Mwaka ambapo wanablogu wetu walianza kuchomoza ilikua 2006 baada ya kifo cha wapenzi wawili wa Kitanzania waliouliwa kinyama Marekani. 

Blogu la Michuzi (ambalo halikua maarufu kama leo) na Radio Butiama (inayojulikana kwa jina Podcast) zilisimama dede kutangaza habari hizo. Hapo ndipo miye binafsi nilipoanza kuona namna wanablogu walivyokuwa na mwendo mkali - zaidi ya vyombo vya habari vya kijadi. Niliingia rasmi uwanjani mwaka 2007- nikisaidiwa na Ndesanjo na wanabloga wengine walionitangulia; akina Simon Kitururu, Jeff Msangi (Bongo Celebrity) mathalan. Nilichogundua siku za mwanzo ni kwamba Blogaz husaidiana sana. “Ukiwa mbinafsi huendelei kama Bloga” alisisitiza Ndesanjo. Goats feeding on rubbish Mbuzi wetu Bongo wakila kila aina ya takataka mitaani. Nyama yake tamu. Lakini je, ina nini kinachotudhuru tusichokijua? Nilipiga picha hii, Zanzibar, mwaka 2011. Leo Jikomboe na ule ukoka havipo tena. Ndesanjo, mwasisi wa blog za Kiswahili duniani, anafanya kazi shirika la habari- Global Voices. Kati ya mamia ya waandishi wa shirika hilo la kimataifa, Mtanzania huyu anaongoza kwa habari asilia za uchambuzi zaidi ya 4,200 . Tofauti ya mtu kama Ndesanjo na baadhi ya blogaz ni kwamba yeye kiasilia ni mwanahabari hivyo anachanganya ujuzi na mitindo hii miwili ya kusanifu matukio. Si ajabu mwaka jana Ndesanjo alishinda tuzo la Mwanablog bora wa Afrika.

Lugha ya blogaz na vyombo asilia vya habari zi tofauti. Wanahabari lakini ni watu waliosemea sawasawa kazi zao na kufuata utaratibu wa lugha, kusahihisha na kuhariri kazi. Bloga ni mtu yeyote tu mitaani au kijijini anayetaka kuelezea jambo. Kuhe -samaki- by Revo Meza Samaki aitwaye Kuhe katika Ziwa Tanganyika. Picha nimeletewa na mwandishi Revocatus Meza. Mvua ya blogaz Tanzania imejaza bahari safi tena ya faraja. Blogaz ni wengi tena wa kila rangi na jinsia; wanatupasha matukio kila sekunde! Wakati tukianza, wanawake hawakua wengi. Mwaka jana mshindi wa Blogaz bora Bongo alikuwa Mwanamke na Nyumba. Nyingine zimekuwa makutano au baraza la maoni na malumbano muhimu- mfano Jamii Forums, iliyoundwa 2006. Zipo zenye mafunzo mazito- angalia Al Hidaaya inayofunza masuala ya Kiislamu na Korani tutaelewana n’na maana gani. Zile zenye kurasa moja (kama zangu) zimegeuzwa viwanda vidogo; mathalan ya Maggid Mjengwa ambayo ni kijigazeti cha ajira. Ajira zinazowahudumia na kuwafariji wanahabari wake. Mara nyingine zina maudhi maana hata kuzifungua zinakua shida maana matangazo yamejazana pale juu kiasi ambacho si tena habari bali duka. Ama kweli mtandao umekuwa biashara. Uzuri upo ndiyo; ubaya tuuseme pia! Msukuma Mkokoteni-Magomeni 2009-pic by F Macha Msukuma mikokoteni akitotwa jasho saa za alasiri, mitaa ya Magomeni Mapipa. Niliipiga picha hii mwaka 2009, Dar es Salaam. Watanzania tunakwenda na wakati si uongo. Maana ukitazama wenzetu nchi zilizoendelea wanaelekeza kila jicho katika mtandao na inteneti. Maduka makubwa makubwa asilia nchi magharibi yanapata hasara na kufunga virago vyake. Mwishoni mwa mwaka jana asilimia 25 ya biashara zote nchi zilizoendelea zilitokana na makampuni yenye mauzo ya mitandaoni – yakaingiza dola bilioni 1.7! Linaloongoza sasa hivi ni Amazon inayouza kila kitu bei rahisi na kwa ufanisi zaidi kuliko maduka asilia. Makisio ya faida ya Amazon mwaka jana yalikuwa dola bilioni 63. Uingereza duka maarufu la muziki, sinema na vitabu- HMV- lilipunguza wafanyakazi mwezi jana na tetesi ni kuwa wameshafifia kibiashara. Ama kweli mtandao ndiyo soko mzazi wa biashara leo na kesho (kama alivyosema Ndesanjo) na wanabloga wetu wanakwenda na wakati. Mwandishi gwiji wa Kiswahili Ebrahim Hussenaliwahi kuandika “wakati ukuta ukipigana nao utaumia.” Ndiyo maana wafanya biashara wanatangaza bidhaa kupitia blogu. Ndiyo hali halisi ilivyo. [caption id="attachment_1655" align="aligncenter" width="500"]Kitabu kipya cha Prof Said Ahmed Kitabu kipya cha Prof Said Ahmed[/caption] Kitabu kipya cha Mwandishi nguli, Profesa Said Ahmed- Mhanga Nafsi Yangu- ambacho kinamwangalia mwanamke wa Kibongo anayekwenda kusoma ughaibuni. Kimetolewa na Sasa Sema (Longhorn) wa Kenya,2012. Ila tutathmini zaidi hilo... Blogu zilibuniwa kutangaza mambo na kadhia ambazo hazipo ndani ya vyombo habari mama na runinga. Zilibuniwa kumfaidisha mwananchi yeyote wa kawaida akibeba kamera na simu yake mkononi akaeleza habari za pale anapoishi. Hicho ndicho chanzo... Kama hukua na nafasi kuna Twitter ambayo ni fupi zaidi (maneno 30 tu!). Zana hizi ni muhimu sana kwa jamii ya leo. Hizi ni “habari za raia wa kawaida” . Umuhimu wa Blog, Twitter na You Tube umeonekana pale yalipotokea machafuko na harakati mbalimbali duniani kama Tunisia, Misri, Libya na Mashariki ya Kati nzima miaka miwili iliyopita. Dhoruba za mauaji ya mwanahabari Daudi Mwangosi zilisambaa dunia nzima haraka kutokana na uwezo huu muadhama. Nguzo zake ndizo hizo. Google ambaye hulipa matangazo ya biashara kutokana na “maudhui ya habari” husisitiza wanablogu na waandishi kuwa wa kweli na kutochezea kazi za wenzao. Kwetu Bongo hapana. Miaka ya karibuni makampuni makubwa makubwa na mabenki kama National Microfinance (NMB) yanasaidia kuwekezea wajisiria mali wadogo wadogo (yaani Blogaz). Mara nyingi makampuni haya hayaangalii kama wanablog hawa wananukuu kazi za wenzao, wanaandika mambo yao wenyewe au wanakopi tu na kubandika. Logo- Sema Ndiyo-2 Nembo ya kutetea haki za wanyama pori wanaouliwa ovyo. Kampeni hii inaongozwa na Kidon Mkuu Ngoille Mkuu, wa Arusha. Dili zinapatikana kwa kujuana juana, mathalan. Bahati mbaya kumezuka mtindo wa wanablogu wengi kutwaa kazi na picha za wenzao bila kuandika zimetoka wapi. Ukilinganisha sasa hivi Blogu zetu Tanzania ni tofauti sana na za nchi nyingine maana wengi hatuandiki vitu tulivyovibuni au tunavyoviona. Mmoja akishaandika tu basi wengine wote tunakopi na kubandika tu bila kuangalia sana kazi ikoje. Siku Google na mashirika miliki ya hizi blogu wakifahamu yatakua mengine. Kwa sasa tunajificha ficha tu. Saria akikochi vijana Dodoma Mwanamichezo na mwanahabari Israel Saria akiwa kazini na vijana Dodoma miaka ile ya Themanini. Niliongea na Israel Saria, anayeendesha blogu-tovuti la Michezo Tanzania (Tanzania Sports) tokea London karibuni. Saria ameendesha shughuli hii toka 2005 na anafadhiliwa na NMB. Mbali ya kuwa mtangazaji wa michezo BBC, Saria ni mwalimu rasmi wa mchezo wa mpira wa nyavu aliyekuwa kocha miaka mingi Tanzania. Alipendekeza wawekezaji kuangalia thamani ya blog mbalimbali kabla ya kuzipachikia matangazo: “Hebu linganisha blogu zetu na za majirani wa Kenya. Wakenya wengi huandika mambo wanayobuni. Sisi tunakosa ubunifu na uhalisia. Mwenzetu akiandika habari- baada ya dakika tano –mabloga wengine wote tunainukuu na kuitangaza ikiwa imejazana makosa. Tunalipua tu. Hatuna hata muda wa kuichunguza au kuihariri. Tunadhani kublogu ni suala la umaarufu na kuonekana kwamba na mimi nipo; eti sitaki nionekane kwamba nimekosa ile habari iliyotangazwa na mwenzangu!” Saria anaongeza kusema kwamba wengi wetu tunashindwa kutambua kwamba Google huwa wanajua na kuangalia kazi asilia. “Ukishatundika tu kazi yako, baada ya dakika chache tayari inasajiliwa kama ni mali yako. Yeyote anayeinukuu au kuitumia hatambuliwi kama mwenye hiyo kazi.” Mabloga wengi Bongo basi wanarudia rudia tu kazi za wenzao kwa kuzitapika na kuzitafuna kama ambavyo ng’ombe wanavyofanya baada ya kula majani. Matokeo baadhi ya blogu leo zimegeuka mabango ya matangazo badala ya kazi muhimu za kifasihi. Zipo blogu nyingi zinazobuni mambo- lakini pia zipo ambazo zinacheza tu. Maandazi Picha ya Maandazi toka tovuti la Taste of Tanzania. Picha ya Miriam Rose Kinunda... Miriam Rose Kinunda anayeendesha tovuti-blogu ya mapishi (Taste of Tanzania) amekuwa akisanifu blogu na kusaidia wenzake kuzijenga toka 2004. Anasema ni mara nyingi sana ambapo kazi na picha zake zimetumiwa bila idhini. “Awali nilikua nikiblogu Kiswahili na Kiingereza, lakini kutokana na huu wizi wa kazi, nimeondoa kabisa kitengo cha Kiswahili nikabakisha Kiingereza kwa wasomaji wa kimataifa.” Miriam ambaye karibuni atatoka na kitabu chake cha mapishi anataja mfano ambapo tovuti moja maarufu ya Kenya iliiba kazi na picha zake. Akaamua kuwapigia simu. “Baada tu ya dakika tano, jamaa walinitumia barua pepe kunitaka radhi. Walionyesha namna walivyo waungwana.” Miriam Rose Kitunda Miriam Rose Kinunda Je nini kifanyike? Saria na Bi Kinunda wanashauri wawekezaji (mathalan benki inayowafariji wanablogu kama NMB) kufadhili na kusaidia tu wale wanaokua wabunifu na wanaofuata kanuni za fani hii muhimu katika jamii. Kigoda Kigoda nyumbani kwa mpigania utamaduni wetu na mfanyabiashara mashuhuri wa Dar es Salaam, Mwafrika Merinyo anayeendesha shughuli za Afrika Sana. Nilipiga picha Novemba 2011. Makala hii iliandikwa pia kwa Kiingereza katika safu ya Mwandishi gazeti la Citizen mwezi jana

KIPIMO CHA UTU WETU: UMESHAWAHI KUMUONA MTU HUYU?

$
0
0
Kama unaishi jijini Dar-es-salaam na hususani kama unatumia njia inayojulikana kama “Mbezi ya Chini” naamini kwamba umeshawahi kumuona mtu huyo anayeonekana katika picha hapo juu. Kwa muda mrefu sasa (yaweza kuwa miaka sasa) makazi yake yamekuwa hapo pembeni tu mwa daraja la Mlalakuwa karibu kabisa na yalipo makao makuu ya Jeshi La Kujenga Taifa(JKT) na pia karibu na yalipo mashirika mbalimbali yenye mlengo wa kijamii kama vile Red Cross nk.

Kutokana na jinsi eneo hilo lilivyo maarufu kwa foleni takribani kila jicho linalopita pale linamuona. Hujawahi kumuona? Kweli? Askari Polisi(wa traffic police na wa kawaida) wanaokuwepo eneo lile mara kwa mara wanamuona na wakati mwingine hata kupiga naye story mbili tatu. Nimewahi kushuhudia lundo la askari polisi wakisimamisha magari na pikipiki pale pale huku jamaa akiwa kakaa tu pale kimya akiangalia zoezi linaloendelea bila kuwabughudhi.

Njia ya Mbezi ya Chini hutumiwa pia na lundo la “viongozi” wa nchi hii wanaoishi maeneo ya Mbezi wanapita pale na kumuona. Wao pia, kama mimi na wewe, wanamuona.Wanapotupa jicho pale wanamtizama na kuendelea na safari zao.

Wahusika wa masuala ya afya, haki sawa, ustawi wa jamii nk. wanapita pale asubuhi wakielekea kwenye “ofisi” zao zinazoshughulikia masuala hayo na jioni wanarejea kutoka katika “ofisi” hizo na wanapita pale kuelekea majumbani mwao na kumuacha pale pale!

Mahali pale ambapo mtu huyu ambaye ni wazi anaonekana kuwa na matatizo ya akili(mental health issues) ameamua kuishi ni jalalani. Ni pachafu na pasipotamanika. Kimsingi mazingira anayoishi huyu bwana hayafai kwa mwanadamu kuishi. Isitoshe, pembeni yake tu, kuna mto ambao umegeuzwa kuwa dampo la takataka. Karibuni kutwa nzima huyu bwana hushinda amelala au ameketi katika kijigodoro kidogo na chakavu ambacho nimeambiwa alitupiwa na watu waliokuwa wamelitumia kumpeleka mgonjwa fulani hospitalini.

Sasa nimewahi kusoma na kusikia mahali kadhaa kwamba ukitaka kujua undani wa jamii fulani tizama jinsi inavyowashughulikia watu hawa katika jamii zao; wanawake, watoto na watu wenye matatizo ya akili(mental health issues). Sote tunajua jinsi gani jamii yetu inashughulikia au kutoshughulikia masuala ya wanawake. Tunatambua fika jinsi tunavyojali au kutowajali watoto(ajira kwa watoto, watoto wa mitaani nk vinaweza kukupa majibu ya haraka). Pia sasa,na mfano ulio mbele yetu, twaweza tambua ni jinsi gani tunawajali au kutowajali wenzetu wanaokumbwa na matatizo ya akili. Picha ya jamii yetu?

Sina uhakika na sera yetu ya taifa ya namna ya kushughulikia watu wenye matatizo kama anayoonekana kuwa nayo huyu bwana lakini ni wazi kwamba hastahili kuwa pale. Mbaya zaidi ni kwamba huyu yupo mahali pa wazi. Mahali ambapo kama nilivyogusia hapo juu, naamini wahusika wa moja kwa moja wanamuona kila siku na kuamua kwa makusudi kumpotezea tu. Vipi kuhusu wale ambao wapo huko walipo na ambao hawaonekani?

Unaweza kujiuliza kwamba ndugu mwandishi, mbona wewe huendi basi na kumuondoa pale? Ni kweli na swali lako litakuwa na mantiki. Pamoja na hayo, utetezi wangu utakuwa kwamba sina utaalamu wowote wa kushughulikia watu wenye matatizo ya akili(naamini kwa dhati kwamba huyu mwenzetu ana matatizo hayo). Wapo wataalamu waliosomea na wenye uwezo zaidi wa kumsaidia.

Nimeandika hapa kama kutoa wito. Nipo tayari kusaidiana na yeyote mwenye utaalamu zaidi au wahusika wa moja kwa moja ambao naamini ni Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii. Mtu huyu ni sehemu ya jamii yetu. Kumsaidia ni kuwajibika na kuonyesha utu wetu. Kumuacha mtanzania mwenzetu (na watanzania wengine wengi) katika hali kama ile sio sawa. Kama jamii tunawajibika. Nakaribisha maoni na ushauri. Unaweza kutuma maoni hapa kwenye post hii au kutumia bongocelebrity at gmail dot com. Asante.

Tigo yabadili viwango vya huduma ya tigo pesa

$
0
0

 Dar es Es Salaam Tanzania, Tigo Tanzania imetangaza kubadili  bei za huduma zake za Tigo pesa kuanzia sasa.

Meneja wa Tigo Pesa Bi. Catherine Rutenge Alisema “dhumuni kuu la kubadili bei na kuweka viwango vipya ni kuhakikisha kuwa wateja wa vipato vyote hususan wenye vipato vya chini wanaweza pia  kunufaika na huduma zetu",

Kampuni ya Tigo pia imedhihirisha kuwa imepunguza bei za kutuma pesa kutoka kwa wateja waliosajiliwa na Tigo Pesa kwenda kwa wateja wasiosajiliwa na wale wa mitandao mingine, hivyo kurahisisha zoezi la utumaji hili na kulifanya la bei nafuu kabisa.  

Pamoja na mabadiliko ya bei, Tigo Pesa imezindua promosheni ya ulipaji bili ambapo wateja waliosajiliwa na Tigo Pesa wanapolipa bili zao za Luku, Star-times, Zuku, Dawasco,  au DSTV, wanazawadiwa kiwango cha Tshs 1,000 cha salio la kupiga simu siku inayofuata. Nyongeza hii inaweza kutumika ndani ya siku mbili kwenye kutuma SMS kutoka Tigo kwenda Tigo, au kutoka Tigo kwenda mitandao mingine yote hapa nchini.

Vilevile sasa unaweza kutuma kiasi cha fedha kuanzia shilingi  mia mbili (200) mpaka shilingi milioni  moja (1,000,000) kupitia Tigo Pesa.

“Tigo inataka kuhakikisha kuwa wateja wake wana nafasi ya kuchagua huduma na bidhaa mbalimbali . Tunataka kuwajumuisha watu wa aina zote kwenye kutumia huduma zetu. Tunaona jinsi watumiaji wa simu wanavyotegemea simu zao za mkononi kwa utatuzi wa mambo mbalimbali na hivyo basi tunahakikisha kuwa tuko mstari wa mbele kuwapa huduma bora zaidi na zenye unafuu.”  Alimalizia Ndg. William Mpinga, meneja wa chapa ya Tigo.

Tibaijuka azindua hoteli ya Nyota tano jijini Arusha

$
0
0

Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Profesa Anna Tibaijuka akikata utepe wakati wa uzinduzi wa hoteli mpya yenye hadhi ya nyota 4 ya palace jijini Arusha jana.Wanaoshuhudia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mh. Lazaro Nyalandu,Mkurugenzi Mkuu wa NHC,Bw. Nehemia Mchechu na kulia mmiliki wa hoteli hiyo Dr.Hans Macha.
waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka akiangalia jiwe la msingi baada ya uzinduzi wa hotel yenye hadhi ya nyota 4 Palace hoteli iliyopo katikati ya jiji la Arusha.
WAZIRI wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka akikata keki yenye taswira ya jengo la hotel ya palace pamoja na mke wa mkurugenzi mkuu wa Palace hotel Bibi Vaileth ,Macha wakati wa uzindizi rasmi wa hoteli hiyo.
WAZIRI wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka,naibu waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyalandu,Waheshimiwa Wabunge wa Majimbo ya Arusha na Arumeru Mashariki,Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Nyumba na Mkutugenzi Mkuu wa Hoteli hiyo waliongozana kuingia ndani ya jengo la hoteli hiyo.
Watu mbalimbali wakati wa kufungua hoteli wakishuhudia. 

WAJASIRIAMALI nchini, wametakiwa kujitokeza katika ujenzi wa hoteli za kitalii nchini, ili kukabiliana na tatizo kubwa la uhaba wa vitanda katika hoteli za kitalii ambao unalikabili Taifa. Naibu waziri wa Maliasilia na Utalii, Lazaro Nyarandu, alitoa wito huo jana wakati wa uzinduzi wa hoteli ya kitalii ya Palace Hoteli, ambayo imejengwa kwa ubia na Shirika la nyumba nchini(NHC). 

 Lazaro alisema uwekezaji huo utasadia kuongeza idadi kubwa ya watalii na mapato,”mwaka jana tulipata watalii 800,000 ukilinganisha na nchi ya Rwanda na udogo wake ilipata wageni 600,000 tatizo kubwa la nchi yetu ni upungufu wa vyumba vya kulala wageni”alisema. 

Alisema mkakati huo utaufanya mkoa wa Arusha ambao ni kitovu cha utalii kuzidi kuongeza idadi ya vitanda vya kisasa kulala wageni ambapo kwa sasa ina vitanda 2,800 tu nyuma ya mkoa wa Dar es salaam wenye vitanda 3,800 na kuzidi mkoa wa Mwanza wenye vitanda 900 licha ya ukubwa wake. 

 “Tunaomba shirika la nyumba lijitanue hadi maeneo hasa ujenzi wa hoteli za kisasa za kitalii…na sisi wizara tunahitaji wawekezaji wa ndani na nje kujitokeza kujenga katika maeneo ya wazi na ndani ya hifadhi zetu panapofaa…na tumejipanga kukabiliana na watumishi wenye urasimu wanaokwamisha watu wenye nia njema”alisisitiza.

 Awali Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu alisema ujenzi wa hoteli hiyo yenye hadhi ya nyota nne, umegharimu kiasi cha sh 16 bilioni ambapo NHC imetoa ardhi n ash 9 bilioni huku kiasi kingine kikitolewa na Palace Hoteli. 

 Alisema mradi wa hoteli hiyo ni moja ya miradi ambayo imekuwa na manufaa makubwa, kutokana na uwazi katika uendeshwaji wake na hivyo kuingiza mapato kwa pande zote NHC na Mbia. “binafsi nampongeza sana Mkurugenzi wa Palace hoteli, Dk Hans Macha kwa uwazi katika uendeshwaji wa mradi huu na tunamkaribisha katika miradi mingine aje tushirikiane”alisema Mchechu. 

Naye Dk Ha Macha alisema mradi huo hadi sasa imetoa ajira ya wafanyakazi 120 na unatoa huduma nyingine kadhaa, ikiwepo huduma za kibenki na utachangia kwa kiasi kikubwa kikuza uchumi wa mkoa wa Arusha na Taifa. 

 “hoteli hii tunatumia malighafi za hapa Arusha toka kwa wajasiriamali ikiwa ni njia ya kuongeza ajira na kipato na pia tumekuwa na miradi mbali mbali ikiwepo na utunzwaji wa mazingira”alisema Macha.

 Akifungua mradi huo rasmi, Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alipongeza mradi huo na kutoa wito kwa wajasiriamali wengine kujitokeza na kuingia ubia na NHC katika kutekeleza miradi mbali mbali. Alisema mradi huo unakwenda vizuri na umeongeza mapato ya NHC kwani katika eneo hilo, kabla ya ujenzi wa hoteli walikuwa wakipata kwa mwaka kiasi cha sh 31 milioni pekee lakini sasa wanapata 151 milioni. 

 “natoa agizo rasmi kwa wabia wengine walioingia mikataba na NHC kama huu, kama hawajatekeleza hadi sasa basi mikataba yao ifutwe kwani ni hasara kwa shirika la Taifa”alisema Profesa Tibaijuka.

Mradi wa “Airtel shule yetu” kuleta ufanisi katika masomo ya Sayansi

$
0
0
 Meneja huduma kwa wateja wa Airtel Hawa Bayumi akimkabithi Afisa elimu wa mkoa wa Mwanza Hamisi Maulidi msaada wa vitabu kwa shule tatu za sekondari za Kalebezo, Buhongwa, and Kabuhoro zilizopo mkoani Mwanza. wakishuhudia kulia ni Meneja Mauzo wa Kanda Ally Maswanya na Meneja huduma ya Airtel money wa Kanda Galus Mgawe.
Afisa elimu wa mkoa wa Mwanza Hamisi Maulidi  akipokea msaada wa vitabu kutoka kwa Meneja huduma kwa wateja wa Airtel Hawa Bayumi zilivyokabithiwa  na Airtel chini ya mradi wake wa Shule yetu, shule 3 za sekondari za  Kalebezo, Buhongwa na  Kabuhoro za mkoani Mwanza zilifaidika na Msaada huo.
 =======  ======= ====== 
Mradi wa “Airtel shule yetu” kuleta ufanisi katika masomo ya Sayansi
·         Airtel yachangi vitabu vya sayansi kwa shule 3 za sekondari mkoani Mwanza
Wakati Tanzania ikikabiliwa na uhaba wa wataalamu wa fani ya sayansi,wanafunzi wametakiwa kutohofia masomo ya sayansi na kukimbilia kusoma masomo mengine kwa lengo la kulifanya taifa liwe na wataalamu wengi wa fani mbalimbali.Kauli hiyo imetolewa jijini Mwanza na Afisa Elimu wa Mkoa wa Mwanza Hamis Maulid wakati akikabidhi vitabu kwa shule nne za sekondari za mkoa huo vilivyotelewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel.
Afisa Elimu wa mkoa wa mwanza ameendelea kwa kusema elimu ni urithi endelevu na kusoma masomo ya sayansi kunamwezesha mwanafunzi kuwa katika nafasi nzuri ya kulisaidia taifa katika Nyanja ya kitaalamu. mataifa mengi duniani yamepiga hatua kutokana na wanafunzi kupewa msukumo wa kusoma masomo ya mchepuo wa sayansi.
Akiongea katika halfa ya makabithiano ya vitabu mkoani Mwanza, Meneja wa huduma kwa jamii wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Hawa Bayumi amesema Airtel imeguswa na tatizo la ukosefu wa vitabu mashuleni na kusababisha kiwango cha ufaulu kushuka hasa katika masomo ya sayansi. Na leo tunayofuraha kutoa msaada wa vitabu kwa shule za sekondari  za mkoa wa mwanza zikiwemo: Kalebezo  sekondari iliyopo wilayani Sengerema, shule ya sekondari ya Buhongwa na Kabuhoro sekondari.
Tunaamini mchango huu wa vitabu mashule utakuwa chachu ya maendeleo ya elimu nchini na kuongeza kiwango cha ufaulu nchini. Tunaahidi kuendelea kushirikiana na serikali chini ya wizara ya elimu katika kuhakikisha tunafikia malengo waliojiwekea. Aliongeza Bayumi.
 Naye Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Kalebezo iliyopo wilayani Sengerema Thomas Muswaga na mwanafuzi Julieth John wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Buhongwa wanazungumzia changamoto mbalimbali zikiwemo uhaba wa vitabu na kushukuru Airtel kwa msaada wa vitabu walioutoa katika shule hizo za mkoa wa Mwanza
Airtel chini ya mpango wake wa shule yetu imeendelea kutoa msaada wa vitabu kwa shule za sekondari mbalimbali nchini. kwa mwaka huu shule 93 za sekondari  tangu kuanzishwa kwa mradi huo shule zaidi  ya shule za sekondari 900 zimekabithiwa

wananchi watakiwa kwenda kutibiwa hospitali na siyo kwa waganga wa jadi

$
0
0

Na Anna Nkinda, 
Maelezo  Lindi
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Mama Salma Kikwete amewataka wakazi wa wilaya ya Lindi mjini  kujenga mazoea ya kwenda hospitali kupima afya zao mara kwa  mara na kuachana na tabia ya kwenda kutibiwa kwa waganga wa jadi na kushikana uchawi kutokana na maradhi yanayowasumbua.
Mama Kikwete ambaye pia ni Mke wa Rais alitoa rai hiyo  jana alipokuwa  akiongea kwa nyakati tofauti na wakazi wa kata za Matopeni na Wailesi zilizopo wilaya ya Lindi mjini wakati wa ziara yake ya kichama ya siku saba katika wilaya ya Lindi mjini ya kuwashukuru wanachama wa CCM kwa kumchagua kuwa mjumbe wa NEC.
Aliwasihi watu wenye tabia ya kutopenda kupima afya zao wakati wanaumwa na wale wenye tabia za kukimbilia kwa waganga wa jadi huku wakijua fika kuwa ni wagonjwa waache kwani wanaweza kupoteza maisha kwa magonjwa ambayo wangeweza kutibiwa katika vituo vya afya na kupona.
“Hakuna mtu asiyejua kuwa kuna Ugonjwa wa Ukimwi, muache suala la kushikana uchawi katika hili kwani ugonjwa huu haupatikani kwa kurogwa. Mtu mwenye virusi vya ukimwi  anapimwa  kinga za mwili za kupambana na magonjwa ( CD4) kama zipo chini atapewa dawa za kuongeza na akitumia dawa atakuwa na nguvu na kuweza kufanya kazi zake kama zamani jambo la muhimu asipitishe muda wa kuzitumia” , alisema Mama Kikwete.


Aidha Mjumbe huyo wa NEC alisema kuwa jamii nzima inahusika katika ulezi wa watoto lakini jambo la kusikitisha ni kuwa hivi sasa watu wamebadilisha mienendo ya maisha kila mtu anahangaika kulea mwanawe. Na kuwasihi wakazi wa Lindi kufuata maadili ya  zamani ya kuwalea watoto  kwani mtoto wa mwenzako ni wako .
“Ni jukumu la jamii nzima kuwalea watoto wao kwa kufuata  mila za kitanzania , wazazi ambao wakiambiwa kuwa watoto wao wanamienondo mibaya na kuja juu badala ya kuzifanyia kazi taarifa hizo waache tabia hiyo kwani watoto wakilelewa vizuri hata shuleni watakuwa na maadili mazuri na kuweza kufanya vizuri katika masomo yao”, alisema.
Kuhusu ufanyaji kazi kwa ushirikiano Mama Kikwete aliwataka wananchi hao kuachana na  mambo ya siasa kwani uchaguzi umeshapita hivyo basi wafanye kazi za maendeleo kwa na kujenga tabia ya kujitolea kufanya kazi.
Mama Kikwete alihoji,  “Hawa wazungu manaowaona wanakuja Lindi kufanya kazi wamekuja kujitolea ni jambo la muhimu kujitolea kufanya kazi za maendeleo, ukiambiwa kuna ujenzi wa shule, Zahanati wewe nenda ukajitolee usiseme ile si kazi ya Serikali sasa Serikali ni nani kama si wewe mwananchi?”.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi 2010 – 2015 Diwani wa kata ya Matopeni Suleiman Namkoma alisema kuwa idadi ya watoto wanaoanza darasa la kwanza imeongezeka kutoka 45 hadi 60, kuongezeka kwa ufaulu wa wanafunzi wanaofanya mtihani wa darasa la saba kutoka 20 hadi 43, kuongezeka kwa barabara zinazopitika kipindi cha masika na kiangazi na kuimarika kwa miundombinu na barabara za mifereji.
Namkoma alisema, “Tunakabiliwa na changamoto za uchache wa wataalam wa kada mbalimbali ngazi ya kata na jamii kukosa wataaluma wa huduma stahiki, ukosefu wa uwajibikaji kwa baadhi ya watumishi wa ngazi ya kata, ukosefu wa huduma ya maji safi na salama, kuchelewa kwa ruzuku ya Serikali kuu na makusanyo madogo ya Halmashauri na upungufu wa walimu wa shule ya msingi”.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Mikumbi Zahara Suleiman alisema kuwa katika kata hiyo kuna vikundi vingi vya maendeleo lakini kwa mwaka 2010/2013 hakuna vikundi vilivyokopeshwa na Seambavyo ni  Ayayoli na Mafundi Seremali.
Suleiman alisema, “Tunawashukuru wafadhili waliovikopeshwa baadhi ya vikundi vyetu vya maendeleo kwani  kikundi cha Mwambao Fishing Group kilipewa na Mama Salma Kikwete boti na vifaa vya kuvulia vyenye thamani ya shilini milioni 57  na kikundi cha Uganda kilipewa pesa kutoka MACEP  shilingi milioni 15”.
Katika mkutano wa kata ya Mikumbi   Mjumbe huyo wa NEC aliwapokea vijana 18  waliokuwa wanachama wa CUF na kujiunga  na CCM. Akiwa katika kata za Matopeni, Wailesi  na Mikumbi alikabidhi  kadi  kwa wanachama  wapya wa CCM 43 , Umoja wa vijana 60, Umoja wa Wanawake  22 na Jumuia ya Wazazi  59.

KAMA UNA TATIZO LA CHUNUSI BASI HAPA NDIO KIGOMA MWISHO WA RELI

$
0
0
 BLACK OPAL MAXIMUM STRENGTH ACNE SYSTEM.KATIKA SET HII UTAKUTANA NA CLEANSER,TONER NA ANTI-ACNE LOTION: MCHANGANYIKO HUU HUSAIDIA KUTOA UCHAFU NA MAFUTA KATIKA NGOZI,KUFUNGUA NJIA ZA MFUMO A KUPUMULIA  WA NGOZI NA HII HUSAIDIA KUTOTOKEA MLIPUKO WA HARARA ZITOKANAZO KUFUNGWA KWA NJIA HIZO!
 NEUTROGENA  COMPLETE ACNE THERAPY SYSTEM,KATIKA SET HII UTAKUTANA NA ACNE CLEANSER,SUNBLOCK LOTION NA ACNE CONTROL LOTION,MARA BAADA YA KUANZA KUTUMIA SET HII SIKU 4 ZA KWANZA HUPOTEZA ULE MLIPUKO A HARARA ZISAMBAAZO USO MZIMA!!BAADA YA HAPO KADRI UNAVYOITUMIA NDIO MABADILIKO YANAVYOANZA KUTOKEA!!
HII NI ACNE GONE SOAP IMETHIBITIKA KUFANYA VIZURI TENA SANA HATA INAPOSIMAMA PEKE YAKE,WATU WENGI WALIOIJARIBU WAMEIKUBALI!!
=========   ======  =====
KWA WALE AMBAO WAMEKUWA WAKISUMBULIWA NA TATIZO LA CHUNUSI KWA MUDA MREFU,SASA WANAWEZA KWENDA AK CLASSIC COSMETICS KWANI BAADA YA RESEARCH YA KINA WAMEJIRIDHISHA KUWA TATIZO LENU LINAWEZA KUPUNGUZWA HATA KUMALIZWA KABISA NA BLACK OPAL,NEUTROGENA AU ACNE GONE...MAELEZO YA MOJA MOJA NA JINSI GANI INAWEZA KUKUSAIDIA,TEMBELEA BLOG YAO www.akclassic.blogspot.com AU WAPIGIE 0713468393/0753482909.

UNESCO NA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WA HABARI

$
0
0

Na Miza Kona- Maelezo Zanzibar  
20/02/2013

Waandishi wa habari wametakiwa kubadilika katika fani yao kwa kuandika habari zenye maslahi kwa jamii badala ya kuandika habari za viongozi wa kisiasa na watu maarufu pekee.

Wito huo umetolewa na Mwandishi mwandamizi na Mkufunzi wa Fani ya Uandishi wa habari Salim Said Salim wakati alipokuwa akifungua mafunzo ya siku tano ya kuwajengea uwezo Waandishi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar katika ukumbi wa Wizara ya habari Kikwajuni mjini Zanzibar.

Amesema fani ya Uandishi wa habari inaendana na wakati hivyo waandishi wanapaswa kujifunza zaidi kila wanapopata nafasi ili kukabiliana na mabadiliko yanayotokea katika tasnia ya habari.

Salim amesema miongoni mwa mabadiliko muhimu yanayopaswa kupewa kipao mbele katika uandishi ni kuandika habari zinazohusu matatizo ya vijijini ili jamii iweze kuyafahamu badala ya kuandika habari za mijini pekee.

Aidha amewasisitiza Waandishi kufanya uchunguzi wa kina bila kuegemea upande wowote katika kuandika habari zao ili kuondoa sintofahamau zinazoweza kujitokeza.

“Andikeni habari za uhakika na mnapoandika habari zenye pande mbili hakikisheni kila upande mnaupa haki sawa dhidi ya upande mwingine, kama mtu mmoja mkimpa paragrafu nne na mwingine apewe hizo hizo” alisisitiza Salim.

Awali akifungua Mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na UNESCO Mkurugenzi Sera Mipango na Utafiti wa Wizara ya habari, Mwita Mashengo Hassan amesema kwa kufahamu umuhimu wa kujiendeleza Wizara imeamua kuwajengea uwezo waandishi wa Idara hiyo ili waweze kukabiliana na mabadiliko ya kiuandishi.

Mkurugenzi Mwita amesema uandishi wa habari ni kipaji hivyo Wanahabari wanapaswa waendelee kujifunza fani hiyo ili kukuza vipaji vyao na kuweza kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi mkubwa.

Aidha amewataka waandishi hao kuwa makini katika mafunzo hayo ikiwa ni pamoja na kusikiliza maagizo yote yatakayotolewa na Mwalimu wao.

Mafuzo hayo ya siku tano ya kuwajengea uwezo Waandishi wa Idara ya habari Maelezo Zanzíbar yamefadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO

IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR .

Diageo Africa Business Reporting Awards 2013 celebrate 10 years of best in business journalism on Africa

RAIS WA KENYA AZINDUA BARABARA YA MWAI KIBAKI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0


 Rais Mwai Kibaki wa Kenya akikata utepe, akishuhudiwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli na Meya wa Kinondoni Mstahiki Yusuph Mwenda kuzindua rasmi  jina la Barabara ya Mwai Kibaki linalochukua nafasi ya jiba la barabara ya Old Bagamoyo leo kwenye makutano ya barabara ya Bagamoyo na Rashid Kawawa na iliyokuwa Old Bagamoyo leo Februari 21, 2013.

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Mwai Kibaki wa Kenya wakiongozwa na Meya wa Kinondoni Mstahiki Yusuph  Mwenda kutembea hatua chache kabla ya kuzindua rasmi jina la Barabara ya Mwai Kibaki linalochukua nafasi ya jiba la barabara ya Old Bagamoyo leo kwenye makutano ya barabara ya Bagamoyo na Rashid Kawawa na iliyokuwa Old Bagamoyo leo Februari 21, 2013.
 Rais Mwai Kibaki wa Kenya akifunua pazia, akishuhudiwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli na Meya wa Kinondoni Mstahiki Yusuph Mwenda akizindua rasmi  jina la Barabara ya Mwai Kibaki linalochukua nafasi ya jiba la barabara ya Old Bagamoyo leo kwenye makutano ya barabara ya Bagamoyo na Rashid Kawawa na iliyokuwa Old Bagamoyo leo Februari 21, 2013.




  Madiwani wa kinondoni
 Bendi ya Vijana Jazz ikitumbuiza wakati wa uzinduzi rasmi  jina la Barabara ya Mwai Kibaki linalochukua nafasi ya jiba la barabara ya Old Bagamoyo leo kwenye makutano ya barabara ya Bagamoyo na Rashid Kawawa na iliyokuwa Old Bagamoyo leo Februari 21, 2013. 
 MC Ephraim Kibonde akiwa kazini katika uzinduzi  rasmi wa  jina la Barabara ya Mwai Kibaki linalochukua nafasi ya jiba la barabara ya Old Bagamoyo leo kwenye makutano ya barabara ya Bagamoyo na Rashid Kawawa na iliyokuwa Old Bagamoyo leo Februari 21, 2013.
 Sehemu ya barabara iliyopewa  rasmi  jina la Barabara ya Mwai Kibaki linalochukua nafasi ya jiba la barabara ya Old Bagamoyo leo kwenye makutano ya barabara ya Bagamoyo na Rashid Kawawa na iliyokuwa Old Bagamoyo leo Februari 21, 2013.
  Meya wa Kinondoni Mstahiki Yusuph Mwenda akimkaribisha Rais Mwai kibaka na Mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika uzinduzi  rasmi wa  jina la Barabara ya Mwai Kibaki linalochukua nafasi ya jiba la barabara ya Old Bagamoyo leo kwenye makutano ya barabara ya Bagamoyo na Rashid Kawawa na iliyokuwa Old Bagamoyo leo Februari 21, 2013. 
    Meya wa Kinondoni Mstahiki Yusuph Mwenda akimkabidhi zawadi ya kasha la Zanzibar Rais Mwai kibaka huku  Mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishuhudia katika uzinduzi  rasmi wa  jina la Barabara ya Mwai Kibaki linalochukua nafasi ya jiba la barabara ya Old Bagamoyo leo kwenye makutano ya barabara ya Bagamoyo na Rashid Kawawa na iliyokuwa Old Bagamoyo leo Februari 21, 2013. PICHA NA IKULU.

KAMPUNI YA DELOITTE YAFANYA UTAFITI WA TEKNOLOJIA NA MAWASILIANO KWA MIEZI 18-24 IJAYO

$
0
0
Mkurugenzi wa Kampuni ya Deloitte nchini Kenya, Bw. Nikhil Hira akiongea katika mkutano na wadau wa teknolojia na mawasiliano leo ambapo alisema kuwa kwa utafiti mdogo ambao wameuanza unaonyesha kuwa watu wengi wamekuwa wakitizama TV kwa kutumia kompyuta. Mkutano huo ulifanyika  hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Deloitte nchini Uholanzi, Bw. Jean Diop akisisitiza jambo katika mkutano na wadau wa teknolojia na mawasiliano leo hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Wadau wa teknolojia na mawasiliano waliohuduria katika mkutano huo.
Mmoja ya wadau wa teknolojia na mawasiliano akiuliza swali.

kongamano la nane la Wanahabari na Wadau wa NHIF lafunguliwa leo Mkoani Mtwara

$
0
0
 Mgeni Rasmi katika Kongamano la Nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Dkt. Seif Rashid akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Kongamano hilo linalofanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara.Kauli mbiu ya Kongamano hilo kwa mwaka huu ni “Matumizi Sahihi ya Fedha za Uchangiaji Katika Halmashauri ili kuboresha huduma katika vituo vya matibabu”.


Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Mh. Joseph Simbakalia akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni Rasmi kuhutubia na kufungua Kongamano hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ambaye ni Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa yote Nchini,Mh. Abbas Kandoro akitoa salamu kwa Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wanaoshiriki Kongamano hilo.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Emmanuel Humba akitoa taarifa fupi ya Mfuko wa Bima ya Afya kutokana tafiti mbali mbali zilizofanywa na baadhi ya Wanahabari katika Halmashauri 26 hapa nchini.

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara mjini,Mh. Wilman Kapenjama Ndile akisalimia.

Wakijadiliana jambo.

Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri wa vyombo vya Habari hapa nchini,Nevile Meena akizungumza machache wakati wa Kongamano hilo la nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya,linaloendelea hivi sasa kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara.


Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Raphael Mwamotto akitoa muongozo na utambulisho kwa baadhi ya viongozi kutoka sehemu mbali mbali wanaohudhulia Kongamano hilo.


 Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Eugin Mikongoti akiwasilisha mada yake kwenye Kongamano la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

Wadau wakifatilia Mada zinazotolewa kwenye Kongamano hilo.


Wadau.

Mkuu wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF),Athuman Rehani akiweka sawa mambo kabla ya kuwasilisha mada yake.





Baadhi ya Wanahabari kutoka Vyombo mbali mbali vya Habari wakifatilia kwa makini Kongamano hilo la nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),linalofanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara.Picha na Othman Michuzi

lowassa afunguka live kuhusiana na sakata la elimu na uvunjifu wa amani hapa nchini

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh Edward Lowassa leo amezungumza mambo kadhaa ambayo kimsingi yameitikisa na kuishtua jamii kwa kiasi kikubwa,amezungumzia suala la Elimu na mustakabali wake unavyokwenda hapa nchini,kama vile haitoshi akazungumzia suala la  baadhi ya watu kuleta mitafaruku ndani ya jamii kiasi hata kupelekea uvunjifu wa amani katika nchi yetu,Bofya video hizo juu na chini kumsikiliza Mh Lowassa alivofunguka kwa kina mapema leo kwenye moja ya ofisi zake zilizopo Mikocheni,Jijini Dar.

BENDI YA SKYLIGHT YATAMBULISHA WIMBO WAO MPYA

$
0
0
Meneja wa bendi ya Skylight, Anneth Kushaba a.k.a AK 47 akiongea na waandishi wa habari wakati wakitambulisha wimbo wao mpya uitwao 'Nasaka Dhoughs'. Pembeni ni mwimbaji mwenzake Joniko flower. Utambulisho huo ulifanyika leo katika kiota cha Thai Village jijini Dar es Salaam.
 Meneja wa bendi ya Skylight, Anneth Kushaba a.k.a AK 47 akisisitiza jambo. Bendi yetu iko katika hatua za mwisho za kumalizia Album yetu yenye nyimbo nane na zote kali. Kwa sasa wameshatoa nyimbo mbili: Wivu na Carolina na leo wametambulisha wimbo wao wa tatu uitwao 'Nasaka Dhoughs'.
Waimbaji wa bendi ya Skylight wakiwasha moto mbele ya waandishi wa habari wakati wakifanya utambulisho wa wimbo wao mpya uitwao 'Nasaka Dhoughs'.

BALOZI SEFUE AKUTANA NA MKUU WA PEMANDU TOKA MALAYSIA DKT IDRIS JALA

$
0
0
 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiongea na Dkt Idris Jala wa kitengo cha usimamizi na utekelezaji kiitwacho PEMANDU (Performance Management and Delivery Unit) cha Malaysia na ujumbe wake ofisini kwake jijini Dar es salaam leo Februari 21, 2013. Katikati ni Dkt Philip Mpango, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango. PICHA NA IKULU.

RAIS KIBAKI AHITIMISHA ZIARA YAKE YA KISERIKALI YA SIKU MBILI NCHINI

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Emilio Mwai Kibaki wa Kenya anayehitimisha leo Februari 21, 2013 ziara yake ya Kiserikali nchini, wakisikiliza taarifa ya pamoja ikisomwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Vikundi mbalimbali vya ngoma vikitumbuiza wakati Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza mgeni wake Rais Emilio Mwai Kibaki wa Kenya anayehitimisha leo Februari 21, 2013 ziara yake ya Kiserikali nchini katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam. 
 Rais Emilio Mwai Kibaki wa Kenya anayehitimisha leo Februari 21, 2013 ziara yake ya Kiserikali nchini akiagana na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali aliye pamoja na Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda pamoja na viongozi wengine katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza mgeni wake Rais Emilio Mwai Kibaki wa Kenya anayehitimisha leo Februari 21, 2013 ziara yake ya Kiserikali nchini katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Emilio Mwai Kibaki wa Kenya anayehitimisha leo Februari 21, 2013 ziara yake ya Kiserikali nchini wakisimama kupokea heshima wakati nyimbo za taifa zikipigwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.PICHA NA IKULU

MAKOCHA WA MCHEZO WA NGUMI WAHITIMU KOZI YA AWALI LEO

$
0
0

Meja Charles Mbuge wa pili kushoto akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya Hawari ya ukocha wa mchezo wa masumbwi,Charles Muhilu wakati wa kumalizika kwa kozi hiyo Dar es salaam leo kushoto ni mjumbe wa BFT, Koba Kimanga na Rais wa shirikisho hili, Michael Changalawe..
Baadhi ya makocha wa mchezo wa masumbwi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuhitimu mafunzo ya awali yaliyomalizika Dar es salaam.
Meja Charles Mbuge akihojiwa na wana habari wakati wa kufunga mafunzo hayo leo
Mmoja ya wakufunzi Kulwa Kindondi akiojiwa na wandishi wa habari
kocha Charles Muhilu kushoto akihojiwa kuhusu kozi hiyo
Mmoja ya wakufunzi Kulwa Kindondi kushoto akiwa na Patric Nyembela wa EATV picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images