Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

MAELFU YAJITOKEZA KUMUAGA MWEKA HAZINA WA MANISPAA YA ILALA MAREHEMU MEDARD KABIKILE STIMA, AZIKWA JIJINI DAR

$
0
0

Pichani ni Watoto wa marehemu Medard Kabikile Stima ambaye alikuwa ni Mweka hazina wa Manispaa ya Ilala wakiwa wamebeba msalaba pamoja na picha kuongoza kuingiza mwili katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam ili kuangwa kiserikali na baadae kuelekea kanisani na kwenye makaburi ya Kinondoni ambapo leo Agosti 4, 2014 wamempumzisha katika nyumba yake ya milele.
Marehemu Stima alikufa katika ajali ya gari iliyotokea July 31, 2014 karibu na eneo la Bwawani, wakati wakielekea mjini Morogoro kwa shughuli za kikazi. Gari aina ya Landcluiser Mali ya Manispaa ya Ilala lilipasuka gurudumu la mbele hivyo likaacha njia na kugonga mti uliokuwa pembeni ya Barabara. Marehemu Stima alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Dereva anaendelea na matibabu.
Famili ya Marehemu Medard Kabikile Stima ambaye alikuwa ni Mweka hazina wa Manispaa ya Ilala akiwa na majonzi wakati wa kumuaga mpendwa wao katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Meya mpya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi akitoa heshima zake za mwisho.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia akitoa heshima zake za mwisho.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa nae alikuwa mstari wa mbele kutoa heshima zake.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh.Raymond Mushi ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Saidi Meck Sadiki akitoa heshima yake.
Waombolezaji wakitoa heshima zao za mwisho.
Kila mmoa alikuwa na sura ya majonzi.
Mwanamitindo Flaviana Matata alikuwa ni miongoni mwa waombolezaji.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Rugimbana (wa pili kulia) alikuwa ni mmoja ya waombolezaji.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia (Katikati) akiwa na viongozi wengine.

Mwanamitindo Flaviana Matata akimmfariji mke wa Marehemu Stima.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia akitoa heshima zake za mwisho.
Familia ya Marehemu Stima ikiongozwa na Mama Stima wakiwa na nyuso za majonzi.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh.Raymond Mushi ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Saidi Meck Sadiki akitoa machache.
Meya mpya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi akitoa salamu za rambirambi.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mwandisi Mussa Natty akitoa salamu za rambi rambi.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akieleza wasifu wa marehemu Stima.
Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Elizabeth Nyambibo akieleza machache.
Msemaji wa Familia akitoa shukrani zake za pekee kwa watu wote walioweza kufanikisha maziko ya ndugu yao Marehemu Stima. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.

Hotuba Ya Mhe Rais Jakaya Kikwete Kwa WaTanzania Washington DC. Aug 2, 2014

$
0
0


Karibu kusikiliza hotuba ya Mhe. Dk Jakaya M Kikwete alipozungumza na waTanzania usiku wa Agosti 2, 2014 kwenye hotel ya Marriot, jijini Washington DC nchini Marekani.

VETA KATIKA MAONESHO YA WAKULIMA NANE NANE VIWANJA VYA NGONGO MKOANI LINDI

$
0
0
 Mwanafunzi wa Uashi wa VETA, Noel Sowan akiwaonesha vijana wenzake wa Lindi namna ya ufyatuaji wa matofari ya kissa yatuamiayo udongo yanavyo fanyika.
 Huyu akijenga kwa matofali hayo na nyumba hupendeza
 Beatrice Kirati ambaye ni Mwanafunzi wa VETA akifafanua juu ya kifaa cha kisasa cha kunyeshea kuku na nyuki maji. Kifaa hicho kinaweza unganishwa na bomba au tanki la maji moja kwa moja bila kumfanya mfugaji kuwekea mifugo yake maji mara kwa mara.
 Mwanafunzi wa VETA, Jackson Range akimpa maelezo juu ya mashine ya kutotolea vifaranga iliyotengenezwa nao.
 Mtaalam wa kutathmini mafunzo ya VETA, Joyce Mwinuka akiwasikiliza maofisa wa Polisi kutoka Mkoani Lindi ambao ni Mkuu wa Kituo cha Polisi Mingoyo, Mkaguzi wa Polisi Juma Solomon (kushoto) na Mkuu wa Oparesheni wa Mkoa wa Lindi, ASP. Charles Onyango walipotembelea banda la Veta.
 Raia wa Uingereza anaefanya utalii kwa kusafiri na pikipiki kutoka nchini kwake hadi Afrika Kusini akianglia mashine ya asili ya kukeleza mbao iliyobuniwa na VETA Mtwara. Wanaompa maelezo ni Mwalimu, Juma Malibidu (kulia) na Aboubakar Maurusi.
 Raia wa Uingereza anaefanya utalii kwa kusafiri na pikipiki kutoka nchini kwake hadi Afrika Kusini akianglia mashine ya kufyatulia nishati mbada ya kupikia itokanayo na maranda ya mbao. Hii ni VETA Pekee
VETA pia ina mashine maalum za kisasa za umwagiliaji maji katika bustani yako. 
Wafanyakazi na wanafunzi wa Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA kutoka vyuo mbalimbali nchini wapo katika maonesho ya wakulima nane nane yanayofanyika Kitaifa Mkoani Lindi katika viwanja vya maonesho Ngongo kilometya 17 kutoka Lindi mjini. VETA wamesheni vitu mbalimbali na mafunzo kwa wakulima na teknolojia za kisasa. Pia kuna mgahawa wa kisasa upo kibandani kwao na unatoa huduma zote za hoteli kuanzaia chakula na vinywaji vyote. SOURCE: FATHER KIDEVU BLOG

MZEE YUSUPH AINGIA RASMI KWENYE FILAMU NA HII NDIO TRELA YA MUVI YAKE IITWAYO NITADUMU NAE

$
0
0
Itaanza Kupatikana Kuanzia Jumatatu ya tarehe 11 August 2014 katika Maduka yote Tanzania. Usikose Nakala Yako.

MBUNGE WA JIMBO LA CHALINZE AZINDUA MAKTABA YA KISASA SHULE YA SEKONDARI CHALINZE

$
0
0
1
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akikata utepe kuzindua maktaba ya shule ya sekondari ya Chalinze mjini Chalinze jana ambayo imejengwa na Kampuni ya Tanga Cement kupitia bidhaa yake ya Simba Cement kwa kushirikiana na taasisi ya Read International kwa gharama ya shilingi milioni 42 za kitanzania katika kuboresha elimu jimboni humo.

Mbunge huyo pia ameahidi kujenga jiko katika shule hiyo na kuongeza kompyuta ili wanafunzi wajengewe mzingira mazuri zaidi ya kujisomea lakini pia ameahidi kushughulikia tatizo la wanafunzi 10 ambao wamefauru kwenda kidato cha tano na sita, lakini hawakupata nafasi ya kuchaguliwa, hivyo ameueleza uongozi wa shule hiyo pamoja na wazazi kwamba wanafunzi hao lazima watafutiwe nafasi ya kuendelea na shule hata kama itakuwa siyo ndani ya jimbo la Chalinze.

"Muhimu wapate nafasi ya kuendelea na elimu yao ya kidato cha tano na sita" Alisema Mh. Ridhiwani Kikwete alimuomba mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Bw. Mbwana Madeni amkabidhi majina ya wanafunzi wote kumi ili yaanze kufanyiwa kazi mara moja.(PICHA NA KIKSIKAZI CHA FULLSHANGWE-CHALINZE)
2
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani Kikweteakipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa bodi ya shule ya sekondari Chalinze Bw. Mbwana Madeni kabla ya kuzindua rasmi maktaba ya shule hiyo, Katikati ni Emma Lyu kutoka taasisi ya Read International na kushoto ni Raquel Araya kutoka Taasisi ya Read International pia.
3
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani Kikwete akionyeshwa vitabu mbalimbali vilivyopo katika maktaba ya shule ya sekondari ya Chalinze na Najma Juma kutoka Chuo Kikuuu cha Dar es salaam UDSM ambaye anafanya kazi za kujitolea katika taasisi ya Read Internional.
 
4
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani Kikweteakiangalia kitabu wakati akikagua maktaba hiyo kulia kwake ni Najma Juma wa Read International.
6
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani Kikweteakiweka alama za kiganja chake kama kumbukumbu wakati alipozindua maktaba hiyo jana kwenye shule ya sekondari ya Chalinze.
7
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani Kikwete akifurahia jambo wakati Mwenyekiti wa bodi ya shule ya sekondari Chalinze Bw. Mbwana Madeni alipokuwa akisoma risala yake mbele ya mbunge huyo, kutoka kulia ni Raquel Araya kutoa taasisi ya Read International na mkuu wa ituo cha polisi cha Chalinze Afande J.S Magomi.
8
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani Kikwetea akizungumza na wanafunzi wa sule ya sekondari ya Chalinze pamoja na walimu mara baada ya kuzindua maktaba katika shule hiyo jana kushoto ni Mbwana Madeni mwenyekiti wa bodi ya shule, na kutoka kulia ni Raquel Araya kutoka Read International na mkuu wa ituo cha polisi cha Chalinze Afande J.S Magomi.
9
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani Kikwetea akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua maktaba hiyo kushoto ni mdau wa masuala ya habari Dk Fadhil Kabujanta wa Fadhaget Sanitarium Clinic ya Mbezi Africana jijini dar es salaam.
11
Meneja masoko wa Simba Cement Yasin Hussein akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Maktaba ya shule hiyo iliyojengwa na Kampuni hiyo gharama yake ikiwa ni shilingi milioni 42 za kitanzania.

TAMASHA LA USIKU WA MATUMAINI 2014 FULL BURUDANI

SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA LAKABIDHI MASHINE ZA HYDRAFORM MKOA WA DODOMA

$
0
0
1
Meneja wa NHC Mkoa wa Dodoma Bw. Itandula Gambalagi akikabidhi mashine 28 kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk Rehema Nchimbi katika hafla iliyofanyika katika ofisi za mkuu wa wilaya ya Chamwino.
2
Mkufunzi kutoka VETA akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa jinsi mashine hizo zinavyofanya kazi
3
Mkuu wa mkoa Dr Rehema Nchimbi akikabidhi mashine kwa wakuu wa wilaya za Chamwino na Kongwa kwa niaba ya wakuu wa wilaya zote za mkoa wa Dodoma. (Picha kwa hisani ya kittengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii cha Shirika la Nyumba la Taifa)

Mkuu wa mkoa wa Mbeya,Mh Abbas Kandoro afungua mashindano ya Airtel Rising Stars Mbeya

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya  Mh. Abbas Kandoro  akisalimiana na wachezaji wa Timu ya Mbaspo wakati akifungua rasmi mashindano ya Airtel Rising Stars.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya  Mh. Abbas Kandoro  akisalimiana na wachezaji wa Timu ya Mbozi wakati akifungua rasmi mashindano ya Airtel Rising Stars.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akipiga mpira kuashiria ufunguzi wa mashindano ya Airtel Rising Stars Mbeya 



Kandoro afagilia mashindano ya vijana.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro amefungua rasmi mashindano ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars mkoa wa Mbeya na kusisitiza umuhimu kwa wadau wote wa soka kutilia maanani programu za vijana. Ufunguzi huo ulifanyika kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya juzi Jumatatu. 

“Hii ndio njia pekee ambayo inaweza kutuletea maendeelo ya soka na kuiwezesha nchi yetu kuondokana na matokeo mabaya katika mashindano mbali mbali ya kimataifa”, alisema. Aliishukuru kampuni ya Airtel Tanzania kwa kubuni programu hii ambayo imekuwa ikiwapa vijana fursa ya kuonyesha na kuviendeleza vipaji vyao.

Aliwataka vijana kucheza kwa kujituma na kuwataka wafahamu kwamba hatma ya mchezo wa soka kwa siku za usoni iko mikononi mwao “Miamba yote ya soka ambayo tunaihusudu na kuishabikia hivi leo imepata mafanikio hayo makubwa baada ya kuwekeza na kutilia manani soka la vijana na naamini kwamba kwa mwendo huu na sisi tutapata mafanikio ya kuridhisha. Ni suala la muda tu”, alisema.

Amewataka viongozi wa chama cha soka mkoa wa Mbeya (MREFA) kuyatumia vizuri mashindano ya Airtel Rising Stars ngazi ya mkoa na kuchagua vijana nyota watakaounda timu ya mkoa kushiriki kwenye fainali za Taifa za Airtel Rising Stars zinazotarajiwa kuanza kutimua vumbi kuanzia Agosti 10 hadi 17.

Fainali za Taifa zitashirikisha timu za wavulana na wasichana kutoka mikoa ya kisoka ya Ilala, Temeke na Kinondoni. Timu nyingine zitatoka Morogoro, Mwanza, Mbeya na Zanzibar. Alisema mbali na kutumika kubaini vipaji vya soka, programu ya Airtel Rising Stars pia inatoa fursa kwa vijana kushiriki mazoezi hivyo kuwafanya kuwa na afya njema.

Kalenda ya mwaka ya Airtel Rising Stars inatarajiwa kufikia tamati mwishoni mwa mwezi huu ambapo zaidi ya nchi 20 za Afrika zitachuana kwenye mashindano ya kimataifa yaliyopangwa kufanyika nchini Gabon. Katika kindumbwendumbwe hicho Tanzania itawakilishwa na timu za wavulana na wasichana zenye wachezaji 16 kila moja. Wawakilishi hao watachaguliwa wakati wa fainali za Taifa jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake Katibu mkuu wa MREFA Juma Killa ameishukuru kampuni ya Airtel kwa kubuni programu hii ili kutumika kama jukwaa linatotumika kubaini vipaji vya wanasoka chipukizi. Alisema kuwa mashindano ya Airtel Rising stars yameifanya kazi yao ya kutafuta vipaji vya soka kuwa rahisi zaidi.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Meneja wa Airtel Tanzania Kanda ya Mbeya Straton Mushi amewashukuru wadau wote wa soka kwa kuyaunga mkono mashindano ya Airtel Rising Stars na kuyapa umuhimu yanaostahili.


NEWS ALERT:KUPOTEA KWA MTOTO FAITH CHARLES RUHEMBE

$
0
0
Taarifa ya kupotelewa kwa mtoto Faith Charles Ruhembe. Amepotea tangu 31.07.2014 saa saba mchana, eneo la makumbusho usalama. Ni binti wa miaka tisa (9) na anasoma shule ya msingi Martin Luther Dodoma.

Usalama ni kwa shangazi yake Catherine Ruhembe, ambaye ni shemeji yangu na dada wa mke wangu Carolyne Ruhembe. Tumeshatoa taarifa vituo vya polisi na TV pia.

Pamoja na ujumbe huu, naambatanisha picha yake  kwa ufafanusi zaidi. Kwenye picha ni huyo binti. Ikiwa ufafanuzi zaidi ya huu utahitajika, basi napatikana kwa number hii 0715 119893.
Asanteni

PPF YASHIRIKI MAONYESHO YA WAKULIMA NANE NANE LINDI

$
0
0
 Afisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, (Kushoto), akiwahudumia wananchi waliotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonyesho ya wakulima Nane Nane, mkoani Lindi juzi. Kilele cha maonyesho hayo yaliyoandaliwa kwa pamoja na mikoa ya Lindi na Mtwara, yatafanyika Agosti nane mkoani Lindi.
 Afisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, (Kuli), akiwahudumia wananchi waliotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonyesho ya wakulima Nane Nane, mkoani Lindi juzi. Kilele cha maonyesho hayo yaliyoandaliwa kwa pamoja na mikoa ya Lindi na Mtwara, yatafanyika Agosti nane mkoani Lindi

 Mkulima huyu akionyesha furaha wakati akihudumiwa na Mfanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, alipotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonyesho ya wakulima 88 mkoni Lindi juzi.
 Maafisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, (Kulia), wakiwasikiliza wananchi hawa waliotembelea banda la Mfuko huo, kwenye maonyesho ya wakulima 88 mkoani Lindi juzi.

KITUO CHA REDIO 5 NDANI YA VIWANJA VYA 8 8 JIJINI ARUSHA

$
0
0
Taswira katika banda la Tan Communication Media  inayo miliki kituo cha  Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha katika viwanja vya nane nane njiro ,
Katikati niMeneja masoko wa Tan Communication Media  inayo miliki kituo cha  Radio5 Sarah Keiya kushoto mtangazaji wa kituo hicho Godfrey Thomas na kulia ni Dj Ibraah anayesababisha pande hizo
Dj Ibraah akifanya yake kwenye moja na mbili
Kushoto ni Goodluck Kissanga ,Godfrey Thomas watangazaji wa kituo hicho,katikati ni Meneja masoko wa Tan Communication Media  inayo miliki kituo cha  Radio5 Sarah Keiya na Dj Ibraah.
 
Kampuni ya Tan Communication Media  inayo miliki kituo cha  Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha kimeshiriki vyema katika maonyesho ya nane nane hivyo kuwataka watu mbalimbali kutembelea banda lao kujionea amna wanavyohabarisha jamii.
 
Meneja masoko wa Tan Communication Media  inayo miliki kituo cha  Radio5 Bi. Sarah Keiya anasema kuwakituo hicho kinasaidia wakulima kwa kuwaunganisha na wadau wa kilimo kupata pembejeo za kilimo
 
“Katika kituo chetu cha Redio 5 tunavipindi viwili vinavyohusu kilimo ambacho ni AMKA na FAHARI YANGU”Vipindi hivi huwasaidia wakulima alisema Keiya.Pia katika maonyesho hayo kutakuwepo na mashindano ya kuwashindanisha waimbaji ikiwa nikuwaibua vipaji vyao na mshindi kupatiwa zawadi.
 
Hata hivyo Keiya aliwataka wafanyabishara mbalimbali kutangaza biashara zao kupitia kituo hicho cha Redio 5 kwakuwa wamepunguza bei ya matangazo kwa asilimia 50% hadi tarehe 15 mwezi huu

Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) wakabidhi Msaada wa Vitabu kwa Taasisi 48 za Elimu nchini.

$
0
0
Mwenyekiti  wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa akiwa katika picha ya pamoja na wadau pamoja na wahisani wa Elimu wakati wa hafla ya kukabidhi vitabu kwa ajili ya  kusaidia  shule 45 na Vyuo 3 vya Elimu ya Juu vilivyotolewa na Books for Africa kutoka nchini  Marekani na kusafirishwa kwa hisani ya Mfuko wa Sir. Emeka Offod wa nchini Nigeria leo jijini Dar es Salaam. Picha na MAELEZO.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote(EOTF), Emmanuel  Matee akielezea historia ya mfuko huo kwa wadau mbalimbali wa elimu katika hafla ya kupokea vitabu kwa ajili ya shule za Msingi, Sekondari na Elimu ya Juu vilivyotolewa na Books for Africa kutoka Marekani leo jijini Dar es Salaam
 Mwenyekiti  wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote(EOTF), Mama Anna Mkapa akitoa neno la shukrani kwa wahisani wakati wa hafla ya kukabidhi  vitabu kwa ajili ya kusaidia  shule 45 na vyuo 3 vilivyotolewa na Books for Africa kutoka nchini  Marekani leo jijini Dar es Salaam,kushoto ni Mwakilishi kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bibi.Paulina Mkonongo na katika ni mwakilishi wa Balozi wa Nigeria nchini Bibi. Abiola Delupe.
 Mwenyekiti  wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa akimkabidhi kitabu mwakilishi wa Shule ya Sekondari Overland, iliyopo Kisarawe ndg. Allison Sila  wakati wa hafla ya kukabidhi  vitabu kwa ajili ya kusaidia  shule 45 na Vyuo 3 vya Elimu ya Juu vilivyotolewa na Books for Africa kutoka nchini  Marekani na kusafirishwa kwa hisani ya Mfuko wa Sir. Emeka Offod wa nchini Nigeria  leo jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti  wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa akimkabidhi kitabu mwakilishi wa Shule ya Msingi Little Hood, Ignas Kamuntu wakati wa hafla ya kukabidhi  vitabu kwa ajili ya kusaidia  shule 45 na Vyuo 3 vya Elimu ya Juu vilivyotolewa na Books for Africa kutoka nchini  Marekani na  kusafirishwa kwa hisani ya Mfuko wa Sir. Emeka Offod wa nchini Nigeria n  leo jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti  wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa akimkabidhi kitabu mwakilishi kutoka Chuo cha Ukutubi na Uhifadhi Nyaraka Bagamoyo, Bibi. Victoria Kessy wakati wa hafla ya kukabidhi  vitabu kwa ajili ya kusaidia  shule 45 na Vyuo 3vya Elimu ya Juu vilivyotolewa na Books for Africa kutoka nchini  Marekani  na kusafirishwa kwa hisani ya Mfuko wa Sir. Emeka Offod wa nchini Nigeria  leo jijini Dar es Salaam.
 Mwakilishi kutoka shule ya Sekondari Ujenzi iliyopo Mkuranga ndg. Karumuna Sigsmundi akitoa shukrani kwa Mwenyekiti  wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa kwa niaba ya wawakilishi wa shule zote zilizo kabidhiwa Vitabu vilivyotolewa na Books for Africa kutoka nchini  Marekani na kusafirishwa kwa hisani ya Mfuko wa Sir. Emeka Offod wa nchini Nigeria   leo jijini Dar es Salaam.
 Mwakilishi wa Balozi wa Nigeria nchini Bibi. Abiola Delupe akizungumzia umuhimu wa Vitabu vilivyotolewa na Books for Africa kutoka Marekani na kusafirishwa kwa hisani ya Mfuko wa Sir. Emeka Offod wa nchini Nigeria wakati wa hafla ya kukabidhi vitabu kwa shule 45 na Vyuo vya Elimu ya juu 3, kulia kwake ni Mwenyekiti  wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa,  Mdhamini wa Mfuko Sawa kwa Wote Bibi. Esther Mkwizu(katikati) na  Mwakilishi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bibi.Paulina Mkonongo.

FASHION WEEK ZANZIBAR - MODEL CASTING IN DAR ES SALAAM

MAONESHO YA NANE NANE MKOANI ARUSHA WANANNCHI WAFURIKA BANDA LA BALTON KUJIFUNZA KILIMO NA UFUGAJI

$
0
0
 Mtaalamu wa Kilimo wa kampuni ya Balton, Jane Remmy, (kushoto) akitoa maelezo ya jinsi ya kuotesha miche mboga mboga kwa baadhi ya wananchi, waliofika kwenye banda la maonesho ya Nane nane jijini Arusha leo. 
 Sufianimafoto naye hakuwa mbali kupata ujuzi wa kilimo katika banda hilo.
 Maelezo yakiendelea......
 Jane Remmy (kulia) akionesha jinsi wanavyootesha matango...
 Linda Byaba,akiangalia miche ya Maharage....
 Bwawa la kutengeneza la kufugia samaki ama kutumika kumwagilia bustani ya mbogamboga....
 Lango Kuu la kuingilia banda la Balton.....
 Wakazi wa arusha wakimiminika katika viwanja vya maonesho vya Themi.....
 Pia makulaji katika anga hizo kulikuwa ni hatareeeeee
 Kinamama wakiuzaasali.....
 Kilimo katika mabanda mengine viwanjani hapo.....
Banda la Wilaya na Karatu.
 Ofisa Mauzo wa Vifaa vya Kilimo wa Kampuni ya Balton Tanzania, Moses Lembris (kulia) akitoa maelezo kwa baadhi ya wananchi wa jijini Arusha, waliofika katika Banda la kampuni hiyo, kwenye maonesho na Sikukuu ya Wakulima Nane Nane, yanayoendelea kwenye Viwanja vya Themi jijini Arusha,leo. Picha na www.sufianimafoto.com

UP DATES: Mtoto aliepotea,apatikana maeneo ya Msasani jijini dar

$
0
0
Napenda kuwajulisha kwamba mtoto Faith amepatikana maeneo ya Msasani na ameshaungana na familia. Aliokotwa na Msamaria mwema ambaye nae alikuwa anafanya juhudi za kuitafuta familia yetu.

Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru sana sana kwa msaada wenu wa kurusha habari ile ya kupotea kwake. Lakini zaidi sana nawashukuru  jinsi mlivyotenda kwa haraka (act promptly) nilipotuma tu ujumbe.

Hii imeonyesha umuhimu wa mitandao hii na ni kweli ya wananchi na jamii. 

Asanteni sana na kila la heri.

PRESIDENT KIKWETE MEETS WITH IBM PRESIDENT AND NEW YORK MAYOR MICHAEL BLOOMBERG

$
0
0
President Jakaya Mrisho Kikwete shakes hands with Virginia M. Ginni Rometty, the Chairman, President and Chief Executive Officer of IBM during a dinner hosted by Mayor of New York and Chairman of the Bloomberg Philanthropies, Mr Michael Bloomberg, in Washington DC on Monday July 4, 2014. Bloomberg Philanthropies are some of the major sponsors of the US-Africa Leadership Summit.
President Jakaya Mrisho Kikwete with the Mayor of New York and Chairman of the Bloomberg Philanthropies, Mr Michael Bloomberg, during a dinner in Washington DC on Monday July 4, 2014. Bloomberg Philanthropies are part of the major sponsors of the US-Africa Leadership Summit. STATE HOUSE PHOTOS

MKUU WA MKOA WA KATAVI ATEMBELEA BANDA LA MBEYA YETU NANE NANE AMWAGA SIFA KEM KEM.

$
0
0
Banda la Mbeya yetu Blog.
Mtoa Maelezo kutoka Tone Multimedia Group kupitia Mtandao wao wa Mbeya yetu Blog Fredy Anthony Njeje wa kwanza kulia akitoa maelezo ya kina kwa   Mkuu wa Mkoa wa  katavi  Mh.Dr Rajab Lutengwe jinsi mtandao wa Mbeya yetu unavyofanya kazi pia unavyosaidia upatikanaji wa habari kwa urahisi kabisa. Pia kuekeza sababu za Kushiriki katika mashindano ya nane nane ikiwa ni pamoja na Kutoa elimu juu ya mitandao ya kijamii na faida zake hasa upande wa Blogs na matumizi sahihi.
 Fredy Anthony Njeje akijibu swali la Mkuu wa Mkoa wa Katavi  Mh.Dr Rajab Lutengwe kuwa si Mtandao wa Mbeya yetu pekeee lakini kupitia Blogs za Mikoa Tanzania ambazo zinajumuisha Blogs za mikoa yote Tanzania na hapa akimuonesha mtandao wa KATAVI YETU ambapo yeye ndipo anapotokea.
  Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh.Dr Rajab Lutengwe akiwapongeza Tone Multimedia Group kwa kuanzisha Mtandao wa Blogs za Mikoa na Mbeya yetu Blog ikiwemo ndani yake kwa ubunifu mkubwa na kazi kubwa wanayoifanya ili kufikisha taarifa kwa kila mkoa na Mtandao wake na kusisitiza kuwa ni vizuri kuendelea na moyo huo huo ili kuendelea kuhabarisha jamii kwa ujumla.
  Mkuu wa Mkoa wa Katavi  Mh.Dr Rajabu Lutengwe  wa tatu kutoka kushoto akitoa ushauri kwa Blog ya katavi yetu baada ya kuweka Mnyama Tembo awekwe mnyama Kiboko kwa sababu ndiye alama kubwa ya utalii katika Mbuga ya Wanyama ya Katavi.
 Fredy Anthony Njeje akiendelea kumpa maelezo Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr. Rajab Lutengwe juu ya kazi zengine ambazo kampuni ya Tone Multimedia Group inazifanya ikiwa ni pamoja na Radio ya Mtandaoni Tone Radio, Mtandao Maalum ambao unawahusu wanafunzi Matukio na wanavyuo, Huduma Mpya ya kupata habari kwa njia ya Simu kwa watu wenye Whatsapp Tone Mobile News, Mtandao wa watanzania waishio nje ya nchi pamoja na kazi zote za ambazo kampuni inazifanya. Wa kwanza kutoka kushoto ni Mwandishi wa Mbeya yetu Venance Matinya.
Mwandishi Mkuu wa Mbeya yetu Blog Joseph Mwaisango wa kwanza upande wa kushoto akiendelea kutia maelezo kwa baadhi ya watu waliotembelea katika banda la Mbeya yetu blog.
************
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr. Rajab Lutengwe, ameusifia mtandao wa kijamii wa Mbeya Yetu Unaomilikiwa na Tone Multimedia Group kwa kuonesha mabadaliko ya kwenda na wakati katika  teknolojia  ya  mawasiliano na habari teknolojia ya kisasa.

 Dr. Lutengwe ametoa pongezi hizo hivi wakati akitoa tathmini yake mara baada ya kutembelea mabanda mbalimbali kwenye maonesho ya wakulima  maarufu kama Nane nane yanayoendelea kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Alisema kuwa mtandao huu umeonesha chachu ya mabadaliko katika sekta ya mawasiliano kwa kukuza na kutangaza uchumi wa ndani na nje ya nchi kwa kurusha matukio mbalimbali yanayoendelea katika maonesho hayo.

“Nimewapenda sana wale vijana wa mtandao wa Mbeya Yetu  kwa kazi yao ya kurusha matukio yanayoendelea kwenye viwanja hivi, huko tunakoelekea hivi sasa katika kukuza biashara ya mazao yetu ni lazima tutangaze kupitia ‘Google’ Mbeya yetu imeonesha njia sahihihi ya kukabiliana na soko la uchumi na kama wataenedelea na kasi ile watafika mbali” alisema.

Alisema kwa kutumia mitandao ya kijamii taarifa mbalimbali zinazohusu sekta ya kilimo zinawafikia wananchi wengi kwa mara moja na kuwa ni muhimu kwa halmshauri za wilaya kuanzisha Tovuti na Blogu ili kuendana na wakati.

TANZIA

$
0
0
Bi. Hamisa Mahanyu enzi za Uhai wake.

Kanisa la Pugu Chanika SDA lapata milioni 5 kutoka IPTL/PAP kuendeleza ujenzi

$
0
0
 KANISA la Waadventista wa Sabato la Pugu Chanika lililopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam sasa linaweza kuendeleza mradi wake wa ujenzi na upanuzi wa kanisa baada ya kupata msaada wa fedha wa shilingi milioni 5 kutoka kampuni ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL). Msaada huo uliotolewa wakati wa ibada Jumamosi, umefufua jitihada la kanisa za kutanua na kumalizia ukumbi wa kanisa uliopo sasa pamoja na kumalizia ujenzi wa majengo mengine.

Mwakilishi kutoka IPTL ambayo ni kampuni tanzu ya Pan African Power Solutions Tanzania (PAP), Bw. Joseph Makandege, ambaye ni Katibu na Mwanasheria Mkuu wa kampuni hiyo, amesema msaada huo ni sehemu ya jitihada za kampuni yake kuunga mkono miradi mbali mbali yenye manufaa makubwa kwa kijamii.

“Baada ya kupokea maombi toka katika kanisa hilo ya kututaka kusaidia mradi huo wa ujenzi, Bodi ya wakurugenzi ya IPTL/PAP ikiongozwa na Mwenyekiti Mtendaji Bw. Harbinder Singh Sethi mara moja ilipitisha kiasi cha shilingi milioni 5 kwa kuwa inaamini kuwa taasisi za kidini zinasaidia kulijenga taifa lenye watu wanaomuogopa Mungu na hivyo kuifanya nchi iwe na mazingira mazuri ya kufanya biashara ambayo inasaidia kuleta maendeleo ya kiuchumi.

“Tunaamini kuwa katika makanisa, familia zilizotengana zinaunganishwa, waliuokosa matumaini wanapewa matumaini, na maisha ya watu yanabadilika. Inampendeza Mungu kusikia sauti za nyimbo zinazomtukuza, ujumbe madhubuti kutoka kwa wachungaji, ushuhuda wa kazi zitokanazo na Mungu, na sauti nzuri za watoto zisema Amina.

“Kampuni yetu isingeweza kukataa ombi hilo la kusaidia kanisa katika mradi ambao utatukuza kazi ya Mungu na maisha ya walio wengi katika jamii yetu yatabadilishwa kwa ujumla,” alisema Makandege. Aliliasa kanisa kutumia fedha hizo vizuri ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Naye, Mchungaji wa Kanisa hilo, Gallus Gido aliishukuru IPTL/PAP kwa mchango wao ambao alisema umewagusa watu wengi na utalisaidia kanisa kuweza kuwahudumia waumini wengi wanaomtukuza na kumuomba Mungu.

"Katika kitabu cha Matendo 10:1-4, kulikuwa na mtu aliyekuwa akitoa misaada/sadaka kwa jamii yake. Siku moja Mungu alimtokea na kumwambia kwamba sala na sadaka zake zimefika mbinguni. Nataka kuwaambia IPTL/PAP kwamba mchango wao wa kuendelea kusaidia taasisi mbalimbali ya kidini na jamii kwa ujumla, utawafungulia milango mbinguni kwa ajili ya baraka zaidi," alisema.

Mchungaji aliongeza kuwa mchango wa IPTL/PAP unadhihirisha upendo wa kampuni hiyo kwa Mungu na watu, na kuhaidi kuwa atafanyakazi kwa ukaribu na kamati ya ujenzi kuhakikisha kuwa fedha hizo zinatumika vizuri kwa lengo lililokusudiwa.

Kipindi cha Maswali na Majibu kati ya Rais Kikwete na waTanzania, Washington DC

$
0
0
Mhe. Rais Dk Jakaya Kikwete akijibu maswali ya waTanzania
Usiku wa Agosti 2, 2014, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk Jakaya Mrisho Kikwete alikutana na waTanzania katika hoteli ya Marriot jijini Washington DC Baada ya hotuba yake, Mhe. Rais aliruhusu maswali kutoka kwa waTanzania hao Na haya, ndiyo yaliyoulizwa kwake.
Karibu
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images