Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 333 | 334 | (Page 335) | 336 | 337 | .... | 1897 | newer

  0 0


  0 0

   Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Pudenciana Kisaka akizungumza wakati wa kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi Siasa ni Kilimo, kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Steven Mhapa.
   Baadhi ya madiwani wakifuatilia majadiliano katika kikao hicho yakiendelea katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Iringa katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo.
   Baadhi ya wakuu wa idara wa halmshauri ya wilaya ya Iringa wakifuatilia majadiliano katika kikao hicho yakiendelea katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Iringa katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo(picha na Denis Mlowe)
   Madiwani wakichangia majadiliano


  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya maafisa waliofika kumpokea wakati akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dulles tayari kwa Mkutano wa Viongozi wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Amerika na Africa (US-Africa Leaders summit) uliondaliwa na Rais Barack Obama wa unaotaraji kuanza Agosti 4-hadi 6, 2014, ambao utatanguliwa na mikutano mingine ya maendeleo ya sekta mbalimbali na uwekezaji (2-3 Agosti, 2014) jijini Washington DC. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani,Balozi Liberata Mulamula.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakisalimiana na baadhi ya maafisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani wakati walipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dulles.PICHA NA IKULU.

  0 0


  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari (wa pili toka shoto) akiwa ni miongoni mwa wawasishaji wa mada katika mdahalo maalumu uliofanyika Makao Makuu ya Benki ya Dunia.
  Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari (katikati) akichangia mada iliyosema "The Fundamental Role of Education and Skills ,addressing the Challenge of Youth Education " katika mdahalo maalumu uliofanyika Makao Makuu ya Benki ya Dunia ambapo Mh Nassari alikuwa ni miongoni mwa wawasilishaji wa mada. Wengine ni Waziri Msaatfu wa Mambo ya nje wa Liberia na baadhi ya maofisa wa Benki ya Dunia ambapo Nassari pia alipata fursa ya kukutana na rais wa Benki ya Dunia kwa maswala ya Afrika.

  0 0

                Marehemu Gabriel Makalla

  Naibu Waziri wa Maji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla anasikitika kutangaza kifo cha babake mzazi, Gabriel Makalla kilichotokea usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam.

  Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa waziri Palm Residence Ocean Road namba 18E Dar es Salaam, Mwili utaagwa Jumapili katika Kanisa la Azania Front saa 6 mchana.

  Baada ya hapo mwili utasafirishwa kwenda Mvomero kwa mazishi yatakayofanyika Jumatatu saa 7 mchana. 

  Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi,  amina.

  0 0


  0 0

  UPAKO! Zikiwa zimesalia siku chache kuelekea katika Tamasha la Matumaini litakalofanyika katika Uwanja wa Taifa, Agosti 8, mwaka huu, pamoja na burudani mbalimbali, waimbaji wa muziki wa Injili watakuwepo kulipamba tamasha hilo.
  Mwimbaji wa nyimbo za injili Bongo, Martha Mwaipaja.
  Akizungumza na Mikito Nusunusu, mratibu wa tamasha hilo, Luqman Maloto alisema kila kitu kimekwenda kwenye mstari na kinachosubiriwa ni muda ufike, Watanzania wajumuike kwa pamoja uwanjani kushuhudia burudani zisizo na mfano.

  Kwenye muziki wa Injili, Maloto alisema  mkongwe wa nyimbo za Injili, Upendo Nkone ataliongoza jukwaa kwa kuporomosha nyimbo kama Haleluya Usifiwe, Mwambie Yesu, Unastahili Kuabudiwa, Usinipite Bwana na nyingine nyingi.

  Kama hiyo haitoshi, watakuwepo Martha Mwaipaja anayetamba na wimbo wa Tusikate Tamaa na Ombi Langu, pia katika kundi hilo wapo Ambwene Mwasongwe, Angela na Paul Clement. Katika kuleta raha zaidi, Maloto alisema mgeni rasmi safari hii atakuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Gharib Bilal. “Dk. Bilal ndiye atakayepuliza kipyenga kuanza kwa mechi kati ya Wabunge Mashabiki wa Simba dhidi ya wenzao wa Yanga.”
  Mwimbaji wa nyimbo za injili Bongo,Ambwene Mwasongwe.
  Kwa upande wa Wabunge wa Yanga imefanya usajili wa nguvu kwa kumchukuwa, Mbunge wa Chalinze,  Ridhiwani Jakaya Kikwete wakati Simba  wamefanikiwa kumsajili,  Mbunge wa Kalenga, Godfrey Mgimwa

  Pia viongozi mbalimbali wa kitaifa, wakiwemo mawaziri na mabalozi wanaowakilisha nchi mbalimbali hapa nchini, wanatarajiwa kuhudhuria tamasha hilo na kuandika historia kwa pamoja.
  Maloto amesema kutakuwa na mpambano mkali kati ya bondia anayeshikilia mkanda wa UBO, Thomas Mashali dhidi ya Mada Maugo ambaye hajawahi kumpiga mwenzake huyo katika pambano lao lilofanyika mara ya mwisho.

  “Mashabiki wajitokeze kwa wingi kuja kumuona mkali wa muziki wa dansi, Khalid Chokoraa akizichapa dhidi ya Said Memba huku mastaa wa Bongo Movie Jacob Steven ‘JB’ akizitwanga na Cloud 112.” Ndondi nyingine za kukata na shoka ni pale Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba atakapozichapa ulingoni na Mbunge wa Nzega, Dk. Hamis Kigwangala.
  Mwimbaji wa nyimbo za injili Bongo,Upendo Nkone.
  Maloto aliongeza kuwa kutakuwa na mechi kali za mpira wa miguu ambapo Azam FC itaumana vikali na Mtibwa Sugar.Kama hiyo haitoshi, Bongo Movie watakipiga na Bongo Fleva. Akasema burudani haitaishia hapo, kwani mastaa kibao wa Bongo Fleva watakuwepo kupiga shoo baab’kubwa.

  “Tutakuwa na mfalme wa Bongo Fleva, Ali Kiba. Mashabiki wategemee kusikia nyimbo zake zote kali sambamba na hizi mpya za Kimasomaso na Mwana.”Mastaa wengine watakaolipamba jukwaa siku hiyo ni pamoja na Madee, Meninah, Scorpion Girls, R.O.M.A, Nyandu Tozi, Navy Kenzo, P-Plan, Shilole, Juma Nature na kundi zima la TMK Wanaume Halisi.

  Tamasha la Usiku wa Matumaini limedhaminiwa na Vodacom, Pepsi, PSI, Benki ya Posta, GEPF, Azam TV, E.FM (93.7), Gazeti la Championi, Times FM (100.5), SYSCORP na Clouds FM/TV.

  0 0


  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
  Mnamo mwezi wa Machi 2014 Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ilipokea taarifa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu ugonjwa wa Ebola katika nchi za Afrika Magharibi ambao ulianzia katika ya Guinea na kusambaa katika nchi za Siera Leone, Liberia na Nigeria. Hadi tarehe 31 Julai, 2014 idadi ya wagonjwa ilikuwa 1323 na vifo 729.

  Ugonjwa wa Ebola husababishwa na virusi vya Ebola. Dalili zake ni homa kali ya ghafla, kulegea mwili, maumivu ya misuli, kuuma kichwa, na vidonda kooni. Mara nyingi dalili hizo hufuatiwa na kutapika, kuharisha, vipele vya ngozi, figo na ini kushindwa kufanya kazi na kwa baadhi ya wagonjwa kutokwa damu ndani na nje mwilini. Kipindi cha kuonekana kwa dalili za ugonjwa ni kati ya siku 2 hadi 21 baada ya kupata maambukizi.

  Ugonjwa wa Ebola unaambukiza kwa kasi na unaenea kati ya mtu na mtu kwa:
  o   kugusa damu na majimaji kutoka mwilini mwa mtu aliyeambukizwa ugonjwa huo
  o   kugusa maiti wakati ya mtu aliyekufa kwa ugonjwa huu.
  o   kugusa wanyama walioambukizwa Mizoga na wazima kama vile sokwe na swala wa msitu.

  Aidha Ugonjwa wa Ebola hauna tiba wala chanjo.

  Hadi sasa hapa nchini Tanzania hakuna mgonjwa yoyote aliyehisiwa au kuthibitishwa kuwa virusi vya Ebola.

  Wizara ya Afya na ustawi wa Jamii imeandaa mikakati ya  kuzuia ugojnwa huu usiingie hapa nchini na ikiwa utaiingia uweze kudhibitiwa kabla haujasambaa. Mikakati hiyo ni pamoja  na:

  o   Kuunda kikosi kazi (Task Force) kinachohusisha  wajumbe mbalimbali wakiwemo wadau wa maendeleo ikiwa ni pamoja na WHO, UNICEF, USAID na CDC  kwa ajili ya kuweka mikakati ya kukabiliana na ugonjwa huu ikwa ni pamoja na kusimamia utekelezaji wa mpango wa dharura wa kukabiliana na Ebola ambao tayari umeandaliwa.

  o   Kutoa taarifa ya tahadhari ya ugonjwa huu kupitia kwa Makatibu Tawala na Waganga Wakuu wote wa Mikoa. Aidha taarifa hii pia imejumuisha namna mgonjwa anavyoweza kutambuliwa (Ainisho la Ugonjwa),  “Fact sheet” ya ugonjwa, Mwongozo kwa watumishi wa afya wa namna ya kuchukua sampuli, na na namna ya kuwahudumia wagonjwa.    

  o   Kuboresha ufuatiliaji na utambuzi wa ugonjwa katika maeneo ya viwanja vya ndege na mipakani ili kuweza kubaini wasafiri watakaoonyesha dalili za ugonjwa au wenye viashiria hatari. .

  o   Miongozo ya utoaji elimu imeandaliwa ikiwemo Vipeperushi. Aidha watalaamu wa Afya wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu dalili za ugonjwa huu kupitia vyombo mbalimbali vya habari ili endapo ugonjwa huo ukitokea uweze kutolewa taarifa mapema


  o   Vifaa kinga (Personal Protective Gears) vipo vya kutosha na Wizara imeanza kuvisambaza kutoka bohari za kanda za MSD na kuzipeleka kwenye vituo vya kutoa huduma za afya ili watumishi wa afya waweze kutumia iwapo mgonjwa atajitokeza. Aidha idadi itaongezwa kadiri ya mahitaji yatakavyojitokeza.

  o   Wizara imebainisha vituo vya kutolea huduma kwa mikoa yote iwapo endapo ugonjwa huu utatokea hapa nchini. Aidha katika vituo hivi, vifaa kinga pamoja na madawa vimeshaandaliwa.

  o   Kuwasiliana na wadau mbalimbali ikiwemo wadau wa maendeleo ili kuweza kupata msaada wa mahitaji mbalimbali kama yalivyoainishwa kwenye mpango wa dharura wa kukabliana na Ebola ulioandaliwa.

  Hitimisho

  Wananchi wanashauriwa kutokuwa na hofu ila kuendelea kuchukua tahadhari za kujikinga na ugonjwa huu. Ugonjwa wa Ebola unaweza kuzuilika. Njia kuu za kujikinga na ugonjwa huu ni:-
  o   Kuepuka kugusa au kuingiwa na mate, damu, mkojo, jasho, kinyesi, machozi  na majimaji mengine yanayotoka  mwilini mwa mwenye dalili za ugonjwa  wa Ebola
  o   Wananchi wanatahadharishwa kuepuka  kushughulikia maiti ya mtu aliyekufa akiwa na dalili za Ebola; badala yake watoe taarifa kwa uongozi wa kituo cha huduma za Afya kwa ushauri.
  o   Wananchi waepuke mila na desturi  zinazoweza kuchelewesha kupata huduma muhimu na kuzidi kueneza ugonjwa wa Ebola.
  o   Zingatia       usafi  wa     mwili  tabia  na      kiroho.
  o   Kutoa taarifa mapema kwa viongozi wa  Serikali na wa huduma za Afya katika ngazi zote pale anapotokea mtu mwenye  dalili za Ebola.
  o   Kuwahi katika vituo vya huduma za  Afya pale mtu anapoona dalili za  ugonjwa huu.

  Wizara itaendelea kushirikiana na sekta mbalimbali kuimarisha ufuatiliaji ili kudhibiti ugonjwa huu usiingie nchini.

  Charles A. Pallangyo
  Katibu Mkuu
  01 Augus,t 2014

  0 0

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda akisalimiana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Adam Misana alipotembelea banda la Halmashauri ya Wilaya hiyo leo tarehe 02/08/2014 katika maonyesho ya wakulima Nanenane nyanda za juu kusini Jijini Mbeya ambapo alipokelewa na viongozi waandamizi wa Serikali ya Mkoa wa Rukwa wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Eng. Stella Manyanya (Pichani Kulia).

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda (aliyeshika boga kushoto) akisikiliza maelezo ya kilimo bora cha maboga alipotembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga leo tarehe 02/08/2014 katika maonyesho ya wakulima Nanenane nyanda za juu kusini Jijini Mbeya. Kulia kwake ni Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Dkt. Merry Nagu na pichani kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya.

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda akipokea maelezo kutoka kwa mjasiriamali kuhusu kilimo cha Uyoga alipotembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga leo 02/08/2014 katika maonyesho ya wakulima Nanenane nyanda za juu kusini Jijini Mbeya.  Wa pili kushoto ni mwanasiasa nguli nchini na Mbunge wa zamani wa jimbo la Kwela Dkt. Chrissant Mzindakaya.

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda wa pili kushoto akiangalia mbegu ya uyoga alipotembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga leo tarehe 02/08/2014 katika maonyesho ya wakulima Nanenane nyanda za juu kusini Jijini Mbeya. Wa kwanza kushoto ni mwanasiasa nguli nchini na Mbunge wa zamani wa Jimbo la Kwela Dkt. Chrissant Mzindakaya na wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya.

  Kilimo cha uyoga ni rahisi kwani sio lazima uwe na shamba, kama unavyoonekana pichani.

  Picha ya pamoja kati ya Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda, viongozi wa serikali mkoani Rukwa na wajasiriamali wadogowadogo mara baada ya kutembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga leo tarehe 02/08/2014 katika maonyesho ya wakulima Nanenane nyanda za juu kusini Jijini Mbeya. Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)

  0 0

       Chama Cha Mapinduzi kimewastukia Ukawa na kusema wanachofanya ni Usanii usiokuwa na tija mbele ya mambo ya msingi kwa Taifa la Tanzania, akizungumza na mwaandishi wa habari hizi Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye alisema hoja zote zinazotolewa na UKAWA zina majibu kwenye Sheria na Kanuni zinazoendesha Bunge la Katiba ,CCM pia imewashukia  UKAWA kwa kuwatukana na kuwadhalilisha viongozi wa dini ambao wamekuwa wakisisitiza UKAWA kurudi Bungeni.

       CCM yawaomba wabunge wa bunge la Katiba wanaotaka Katiba mpya waendelee na bunge  litakapoitishwa tarehe 5/8/2014.

  Kwa taarifa za ndani ya kikao hicho ,kikao kimeisha kwa kukubalina kutokubaliana ,pande mbili hizi zimekutana zaidi ya mara nne pamoja na kikao cha leo kilichoanza tangia asubuhi saa nne mpaka jioni lakini hakuna hata pande mmoja uliokubalina na mwenzake.

  Kwa mujibu wa taarifa za ndani Msajili wa vyama vya Siasa  nchi anatarajiwa kuzungumza na waandishi wa habari kesho jijini Dar es Salaam.

  0 0

   Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, wakiwa kwenye Jengo la mapokezi ya wagonjwa (OPD) ambalo linajengwa katika eneo la Mabwepande, likiwa ni sehemu ya Hospitali ya Jimbo la Kawe katika Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam, walipotembelea kiradi mbalimbali ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2010-2015 katika jimbo la Kawe.
   Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yussuf Mwenda, akizungumza na watumishi wa Manispaa hiyo yeye na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Kinondoni walipofika kwenye mradi wa Ujenzi wa Hospitali ya Jimbo la Kawe unaofanyika Mambwepande, jana.
   Mwenda (wapili kushoto) akikagua ujenzi wa jengo la kupokea wagonjwa (OPD) la hospitali ya Jimbo la Kawe inayojengwa Mabwepande, Dar es Salaam.
   Mwenda akiingia ndani ya chumba cha mapokezi cha jengo hilo la mapokezi ya wagonjwa (OPD) wakati wa ziara hiyo.
   Katibu wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Mohammed Cholage akiwaonyesha wenzake eneo aliloona kuwa ni kama kasoro kwenye ujenzi wa jengo la kupokea wagonjwa (OPD) kwenye hospitali hiyo.
   Mwenda akifanya majumuisho na wajumbe baada ya kutembelea jengo la kupokea wagonjwa (OPD) kwenye Hospitali ya jimbo la Kawe inayojengwa mabwepande.

  UJENZI WODI YA KINA MAMA NA NYUMBA YA MGANGA ZAHANATI YA NDUMBWI
   Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yussuf Mwenda akiongozwa jana na Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Ndumbwi, Sophia Kasubi, kuingia kwenye jengo la wodi ya Kina mama ambalo ujenzi wake umekamilika kwa ajili ya zahanati hiyo.
   Mwenda akisaini kitabu cha mapokezi kwenye jengo hilo wodi ya Kina mama kwenye zahanati ya Ndumbwi baada ya kuingia yeye na wageni wenzake.
   Mwenda akiongozana na Katibu wa CCM wilaya ya Kinondoni Athumani Sheshe baada ya kukagua nyumba ya mganga kwenye zahanati ya Ndumbwi.
   Mwenda akiagana na watumishi wa zahanati ya Ndumbwi
   Baadhi ya watumishi katika zahanati ya Ndumbwi

  UJENZI SHULE YA SEKONDARI KATIKA ENEO LA MIKOCHENI
   Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda akiongoza msafara kukagua ujenzi wa shule ya sekondari ambayo inajengwa na Manispaa hiyo katika eneo la Mikocheni.
   Mwenda akishiriki ujenzi wa shule hiyo ya sekondari kwa kuchanganya mchanga na saruji wakati wa ziara hiyo.
   Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Kinondoni Pili Chande akishiriki ujenzi Shule ya Sekondari inayojengwa Mikocheni, jana. Kushoto ni Mwenda akishuhudia na aliyesimama kulia ni Katibu wa Itikadi na uenezi Kata ya Kawe, Eddy Mlaponi
   Mwenda akizungumza na wajumbe kufanya majumuisho baada ya kukagua shule hiyo ya sekondari Mikocheni na kuridhika kwamba ni mradi mzuri unaopaswa kupigiwa mfano katika utekelezaji wa ilani ya CCM

  UJENZI SOKO BUNJU 'B'
   Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuf Mwenda akiongoza msafara kukagua ujenzi wa soko katika eneo la Bunju B jana.
   Mmoja wa wajumbe akilazimika kwenda kukagua hali ya choo kwa ajili ya soko hiyo ipoje kwa ajili ya matumizi ya binadamu?
  UJENZI DARAJA MIKOCHENZI FEZA
   Wajumbe wakikagua daraja lililojengwa katika utekelezaji wa ilani ya CCM katika eneo la Mikochezi-FEZA.
  Wajumbe wakiwa wameshuka kwenye basi kukagua ujenzi wa barabara ya Maandaazi eneo la Msasani ambayo pia imeboreshwa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya CCM. (Picha zote na Bashir Nkoromo-theNkoromo Blog)


  *Yatekeleza agizo la Rais Kikwete
  *Ni la jimbo kuwa na hospitali kubwa
   NA BASHIR NKOROMO
  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeshuhudia makubwa yaliyofanywa na Manispaa ya wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, katika utekelezaji wa Ilani ya CCM ndani ya jimbo la Kawe.

  Miongoni mwa miradi ambayo chama kililazimika kumpongeza Meya wa Manispaa hiyo ya Kinondoni, Yussuf Mwenda, ni utekelezaji wa agizo la Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete ya ujenzi wa Hospitali kubwa katika jimbo la Kawe yenye hadhi kama zilivyo za Mwananyamala, 
  Amana na Temeke.

  Katika uteekelezaji agizo hilo la Rais Kikwete ambayo haikuwemo katika ilani, tayari Manispaa ya Kinondoni imeshaanza ujenzi wa hospitali hiyo katika eneo la Mabwepande, kwa jengo la kupokea wagonjwa (OPD), linalotarajiwa kukamilika mwaka huu, ambapo imeelezwa hadi mwishogharama yake itakuwa sh. milioni 288 ambazo kati yake sh. milioni Sh.153 zimeshalipwa kwa mkandarasi.

  Wakiwa katika ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa chini ya Ilani ya CCM ya mwaka 2010-2015 katika jimbo la Kawe, Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Kinondoni, waliokuwa kwenye ziara hiyo jana, walielezwa kwamba, baada ya kukamilika ujenzi wa jengo hilo la kupokea wagonjwa, utaanza ujenzi wa wodi ya kina mama.

  "Ndugu wajumbe, wakati Rais Kikwete akiwa katika kampeni zake katika uchaguzi mkuu uliopita, aliagiza kwamba kila jimbo latika mkoa wa Dar es Salaam, lazima liwe na hospitali yenye hadhi kubwa. Sasa ukiangalia agizo hilo ni kama lilikuwa linatulenga sisi wa jimbo la Kawe, maana Jimbo la Kinondoni ipo ya Mwananyamala, Ilala ipo Amana na Temeke pia ipo, ndiyo  sababu tumefanya kila jijitahada kuhakikisha sisi Manispaa tunajenga hospitali hii.", alisema Mwenda.

  Wajumbe hao wa Halmashauri Kuu ya CCM, wakiendelea na ziara hiyo, pia walishuhudia mradi mkubwa wa ujenzi wa Shule ya sekondari unaoendelea katika eneo la Mikocheni, unaotekelezwa kwa gharama ya sh. bilioni 1.5 kwenye awamu ya kwanza.

  Mwenda alisema, kukamilika kwa shule hiyo kutasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa adha ambayo imekuwa ikiwapata wananchi wa jimbo hilo kwa watoto wao kwenda maeneo ya mbali wanapojiunga na shule ya sekondari baada ya mitihani ya darasa la saba.

  Alisema, ujenzi wa shule hiyo ambao sasa upo kwenye hatua ya orofa ya kwanza, unatarajiwa kukamilika mapema na marajio ni kuwezesha watoto watakaomaliza darasa la saba mwaka huu, kuanza kidato cha kwanza kwenye shule hiyo.

  Wajumbe hao pia walitembelea mradi wa ujenzi wa soko la kisasa katika eneo la Bunju B, ambalo ujenzi wake unafanyika ili kuwahamishia wafanyabishara ambao wamekuwa wakifanya shughuli zao pembezoni mwa barabara ya Bagamoyo katika eneo hilo la Bunju B na hivyo kuhatarisha maisha yao na pia kuharibu mandhari ya mji.

  Ujenzi wa soko hilo umekamilika kwa asilimia 90, na taratibu za kuanza kuwahamishia hapo wafanyabiashara zinaendelea kufanywa na mamlaka zinazohusika.

  Baadhi ya miradi mingine ambayo wajumbe hao waliikagua na kuonyesha kuwasisimua, ni ujenzi wa wodi na kina mama na nyumba ya mganga ambavyo vimekamilika, katika zahanati ya Ndumbwi  kwenye jimbo hilo la Kawe.

  Pia alikagua na kuridhiwa na hatua iliyopigwa na Manispaa ya Kinondoni katika ujenzi wa barabara za Maandazi iliyopo Masasani, na barabara ya Jourunalism iliyopo eneo la Feza, Mikocheni.


  0 0

   Waendeshaji wa Show ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) Joti na Lulu wakiwa kwa steji, tayari kwa kuendelea na show hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Mkaumbusho ya Taifa Jijini Dar Es Salaam.
   Mshiriki Ally Kiwendo ambae alikuwa ni mmoja kati ya washindi watatu kutoka kanda ya Kusini mkoani Mtwara akitoa maneno ya shukrani kwa Kampuni ya Proin Promoitons ambao ndio waandaaji na waendeshaji wa Shindano la TMT mara baada ya kutangazwa kuaga shindano hilo kutokana na Kura kuwa chache, huku pia akiwashukuru watazamaji na wote waliompigia kura
   Joyce Kalinga Mshiriki wa Shindano la TMT ambae apia alikua mshindi kutoka Kanda ya Kati Mkoani Dodoma akitoa maneno yake ya shukrani na pia kuwashukuru wadau, Kampuni ya Proin Promotions na watazamaji na waliompigia kura japokuwa bahati haikuwa yake kutokana na kutolewa kwenye kinyanganyiro hiko kutokana na uchache wa kura kutoka kwa watazamaji
   Lulu na Joti wakitoa maelekezo kwa washiriki wawili wa Shindano la TMT ambao waliweza kutolewa katika kinyanganyiro hiko kutokana na kupata kura chache kutoka kwa watazamaji wa Kipindi cha TMT kinachorushwa Kila Jumamosi saa Nne usiku.
  Baadhi ya washiriki wakiwa na nyuso za simanzi kutokana na Washiriki wenzao wawili kuaga mashindano hayo.Picha zote na Josephat Lukaza
  Na Josephat Lukaza - Proin Promotions Limited - Dar Es Salaam.
  Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) Linaelekea Ukingoni ambapo mwisho wa Mwezi huu wa nane Mshindi mmoja wa shindano hilo la TMT ataondoka na kitita cha Shilingi Milioni 50 za kitanzania katika fainali kubwa.
   
   Shindano la TMT ni shindano ambalo limekuwa likiteka hisia za washiriki pamoja na wadau na watazamaji wa kipindi hiko cha TMT ambacho kimejizolea umaarufu nchini na nje ya Nchini kutokana na Umahiri wake.

  Awali shindano hilo lilianza kanda ya ziwa Mkoani Mwanza kwaajili ya kusaka vipaji vya kweli vya kuigiza ambapo baadae safari ilielekea katika kanda nyingine za Tanzania ambapo washindi watatu kutoka kila kanda waliweza Kupatikana na hatimaye kufanya jumla ya washiriki ishirini kutokana kanda sita za Tanzania Kuwasili Jijini Dar Es Salaam, Mwishoni mwa Mwezi wa Sita ambapo waliweka kambi na kuanza kupewa mafunzo na Mwalimu Kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam aitwaye Dk Mona Mwakalinga akisaidia na Mwl Issa.
  Washiriki Hao 20 waliweza pia kupata fursa ya kufanya filamu fupi ambazo ziliweza kupima uwezo wao wa kuigiza mara baada ya kutoka darasani na hatimaye kupelekea watazamaji kuweza kuwapigia kura huku wakisaidiana na majaji wa Shindano hilo. Majaji wa shindano hilo ni Roy Sarungi, Vyonne Cherry na SIngle Mtambalike.
  Mpaka sasa Jumla ya Washiriki 7 wameshatoka kwenye kinyanganyiro na kupelekea kubaki na washiriki wengine 13 ambapo washiriki watatu wanatakiwa kutoka na kubaki washiriki 10 huku kumi hao wakiwa wameingia fainali sasa ya kuzisaka zile Milioni hamsini ambazo Mshindi mmoja atajinyakulia siku ya Fainali inayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa Mwezi wa 8.
  Ili kuweza kumbakiza mshiriki wako unachotakiwa kufanya ni Kumpigia Kura kwa wingi kupitia Simu yako ya mkononi kwa kuandika Neno "TMT" acha nafasi namba ya Mshiriki halafu tuma kwenda 15678. Mfano "TMT" 00 halafu tuma kwenda 15678 au Pia unaweza kumpigia kura mshiriki umpendae kupitia ukurasa wetu wa facebook kwa kutembelea anuani ifuatayo https://www.facebook.com/tztmt.
  Washiriki Kumi watakaoingia Kwenye Fainali ya Kusaka Milioni 50 watakuwa chini ya Kampuni mahiri ya Utengenezaji na Usamabazaji wa filamu za Kitanzania ya Proin Promotions ambao ndio waandaaji na waendeshaji wa Shindano la Tanzania Movie Talents, Shindano Bora na kubwa Tanzania na la Kwanza kufanyika Afrika Mashariki na Kati 

  0 0

  MKUU wa Mkoa wa Tanga, Chiku Gallawa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa taasisi ya Handeni Kwetu Foundation, utakaofanyika Jumanne ya Agosti 5, katika Ukumbi wa Vijana Social Hall, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

  Tukio hilo la uzinduzi wa taasisi hiyo limepangwa kuanza saa 10 za jioni ambapo wamealikwa wageni mbalimbali kwa ajili ya kuitambulisha kabla ya kuanza kazi zake rasmi nchini Tanzania.

  Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa taasisi hiyo, Kambi Mbwana, alisema kuwa wameona wamualike RC Gallawa kuwa mgeni rasmi kwakuwa ni miongoni mwa viongozi makini na wenye kiu ya maendeleo hapa nchini.

  Alisema kuwa kitendo cha kuzinduliwa na Mkuu wa Mkoa Tanga, kinaonyesha namna gani viongozi wa serikali wanashirikiana na wadau wote kwa ajili ya kufanikisha mipango ya kimaendeleo.

  “Tanzania imejaliwa kuwa na viongozi makini mno, hivyo taasisi imemualika Mheshimiwa Gallawa kuwa mgeni wake rasmi ili ashirikiane na wageni waalikwa kuitambulisha taasisi.

  “Tunaamini kwa pamoja tutafanikisha kuitambulisha taasisi kwa wadau wote, hususan Watanzania kwa kupitia Handeni Kwetu Foundation, ukizingatia kuwa imesajiliwa kufanya kazi zake nchini nzima,” alisema.

  Kwa mujibu wa Mbwana, sera na mikakati ya taasisi hiyo itaanikwa katika utambulisho huo utakaokuwa na malengo mahususi ya kujikwamua kiuchumi na kuhamasisha masuala ya utawala bora.

  0 0

  Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva akifafanua jambo wakati wa mkutano maalum wa wananchama wa klabu hiyo uliofanyika kwenye Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
  Baadhi ya wanachama wa Simba wakiwa katika mkutano maalum wa klabu hiyo jijini Dar es Salaam 
  Baadhi ya wanachama wa Simba wakihakiki kadi zao kabla ya kuingia katika ukumbi wa mkutano.
  Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassan Dalali akipitia nyaraka za klabu hiyo wakati akiingia katika ukumbi wa mkutano maalum wa Simba uliofanyika katika Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.
   Wanachama wa Simba wakiwa katika mkutano huo.

  Wanachama wa Simba wakipitia nyaraka mbalimbali wakati wa mkutano huo.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba, Damasi Ndumabaro akizungumza wakati wa mkutano huo.

  0 0

    President Jakaya Mrisho Kikwete with Reasearch fellow and Senior Lecturer at the Muhimbili University of Health Sciences, Dr Julie Makani (left) and Prof. Mwaikambo during his familiarisation tour of the National Institutes of Health (NIH) in Washington DC July 2, 2014
    President Jakaya Mrisho Kikwete enjoys a light moment with  President Dennis Sassou Nguesso of the Republic of Congo, during their familiarisation tour of the National Institutes of Health (NIH) in Washington DC July 2, 2014.
     President Jakaya Mrisho Kikwete speaks with members of the National Institutes of Health (NIH) in Washington DC during a familiarisation tour of the NIH, reputedly the largest hospital and reasearch facility in the world July 2, 2014.
    President Jakaya Mrisho Kikwete and  President Dennis Sassou Nguesso of the Republic of Congo, in a group photo with members of  the National Institutes of Health (NIH) in Washington DC July 2, 2014
    President Jakaya Mrisho Kikwete to  President Dennis Sassou Nguesso of the Republic of Congo, Tanzania's Ambassador to the US Hon,. Liberata Mulamula at the end of their familiarisation tour of the National Institutes of Health (NIH) in Washington DC July 2, 2014.
   President Jakaya Mrisho Kikwete and President Dennis Sassou Nguesso of the Republic of Congo, being briefed on the operations of the National Institutes of Health (NIH) when they toured tha institution in Washington DC July 2, 2014.STATE HOUSE PHOTO.

  0 0

   
  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameutaka uongozi wa Jiji la Mbeya uongeze mapato yake ya ndani kwa kuweka mifumo ya kisasa ya ukusanyaji mapato.
   
  Ametoa agizo hilo jana (Jumamosi, Agosti 2, 2014) wakati akizindua stendi ya kisasa ya mabasi katika eneo la Nane Nane nje kidogo ya Jiji la Mbeya.
   
  “Nikuombe Meya Kapunga, wewe na watu wako ongezeni mapato ya ndani ya Jiji la Mbeya. Wekeni mifumo ya kisasa ya makusanyo inayotumia teknolojia ya habari na mawasiliano, acheni kutumia risiti za kuandika wa mikono,” alisema.
   
  Akizungumzia mradi wa stendi mpya ya mabasi, Waziri Mkuu alisema ujenzi wa stendi hiyo ni miongoni mwa kazi zilizo kwenye mradi mkubwa unaohusisha uboreshaji wa huduma na miundombinu kwenye miji na majiji saba hapa nchini (Tanzania Strategic Cities Programme).
   
  Alisema mradi huo uliibuliwa na Serikali tangu mwaka 2006 kwa kushirikiana na Benki ya Dunia. Miji na majiji mengine yanayohusika na mradi huo ni Mwanza, Arusha, Tanga, Kigoma, Mtwara na Dodoma.
   
  “Utekelezaji wa miradi katika miji na majiji haya saba, umetuwezesha kupata ufadhili katika awamu ya pili ya mradi huu ambayo itajumuisha miji 17. Tusingekubaliwa kuingia awamu ya pili kama ninyi madiwani msingesimamia vizuri miradi hii,” alisema.
  Akisoma taarifa ya mradi huo, Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, Bw. Mussa Zungiza alisema ujenzi wa stendi hiyo yenye ukubwa wa mita za mraba 30,000 utasaidia kupunguza msongamano wa magari kwenye barabara kuu ya TANZAM ambako mabasi ya mikoani yalikuwa yakisimama na kupakia ama kushusha abiria.
   
  Alisema mradi huo wa stendi ya Nane Nane uliogharimu sh. Bilioni 2.9/- ni sehemu tu ya mradi mzima ambao thamani yake ni sh. Bilioni 31.4 ambazo zimetumika kujenga barabara za kiwango cha lami zenye urefu wa kilometa 23.1, daraja moja na dampo la kisasa la kutupia taka (sanitary land fill) katika kata ya Nsalaga.
   
  “Hata hivyo, mradi huo uko chini ya uangalizi wa mkandarasi hadi Desemba 4, 2014 utakapokabidhiwa rasmi kwa Halmashauri ya Jiji, “ alisema Bw. Zungiza.
   
  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Pinda ameutaka uongozi wa Jiji la Mbeya kuhakikisha unatengeneza kwanza miundombinu ya maji na vyoo katika eneo jipya lililopo jirani na stendi mpya ya Nane Nane ambalo limetengwa mahsusi kwa ajili ya wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama ‘wamachinga’.
   
  “Ni vema Jiji litenge kiasi cha fedha kwa ajili ya kuboresha huduma za muhimu kama maji na vyoo badala kukimbilia kuwalundika mahali hapa. Wafanye biashara zao, na hata mtu akitoka stendi akaja kununua bidhaa zao, kama na shida apate mahali pa kujihifadhi,” alisema huku akishangiliwa na umati uliohudhuria uzinduzi huo.
   
  Aliwataka wawapangie maeneo ya mabanda yao, na ikibidi watafute mwekezaji anayeweza kufanya kazi hiyo. “Tusifanye kosa la kuja kuwalundika tu. Ni heri kugharimika kidogo lakini pawe pazuri. Tengenezeni eneo hili ili kituo chenu kiwe cha mfano na wengine waje waige,” aliongeza.
   
  Uzinduzi huo ulihudhuriwa na Waziri wa Nchi (OWM – Uwekezaji na Uwezeshaji), Dk. Mary Nagu, Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Bw. George Owuor, Kaimu Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Bibi Nora Katabarwa, Wakuu wa Mikoa ya Rukwa, Iringa, Njombe na Katavi ambao walikuwa jijini Mbeya kuhudhuria kongamano la Uwekezaji na wanahudhuria maonyesho ya Nane Nane Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.
   
   IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  S. L. P. 3021,
  DAR ES SALAAM
  JUMAPILI, AGOSTI 3, 2014

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu (wa tatu kushoto) akisaini hati za makubaliano ya mkopo wa shs bilioni 100 na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya Mohamed Enterprises Ltd (METL), Mohamed Dewji kwa ajili ya kampuni dada ya METL ya Star Oils inayoshughulika na biashara ya uagizaji na usambazaji mafuta. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni baadhi ya watendaji wakuu wa NBC, METL na Star Oils.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu (kushoto) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa METL, Mohamed Dewji wakionyesha mikataba muda mfupi baada ya kusaini  hati za makubaliano ya mkopo wa shs bilioni 100  kwa ajili ya kampuni dada ya METL ya Star Oils inayoshughulika na biashara ya uagizaji na usambazaji mafuta. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
   Ofisa Mtendaji Mkuu wa METL, Mohamed Dewji (kulia) akibadilishana mawazo na baadhi ya maofisa wa benki ya NBC katika hafla hiyo.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Bi Mizinga Melu akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini makubaliano ya kuipatia kampuni ya Star  Oils mkopo wa takribani sh bilioni 100 ili kuAongeza ufanisi katika kampuni hiyo ya uagizaji na usambazaji wa mafuta nchini.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu (wa nne kushoto), Ofisa Mtendaji Mkuu wa METL, Mohamed Dewji (wa nne kulia), watendaji wakuu wa NBC, METL na Star Oils wakipozi kwa picha ya kumbukumbu mara baada ya utiaji saini makubaliano hayo.

  0 0

  Ndugu zangu,

  Msafara wa tembo huwa na kawaida ya kutokurudi nyuma,ndio maana porini huzioni nyayo za tembo zenye kwenda mbele na kurudi nyuma.

  Ni ukweli, kuwa tembo ndiye mnyama mkubwa porini, na ni mfalme wa pori. Lakini tembo hufika mahali akasumbuliwa na siafu kiasi cha kuweweseka na hata kutamani kulihama pori. Ni kwa kosa la tembo kukanyaga kichuguu cha siafu. Naam, siafu mia tano ni wengi kuliko tembo mmoja, pamoja na ukubwa wa tembo.

  Na adili ya jambo hilo ni ukweli kuwa duniani hapa mkubwa anapaswa kumuheshimu mdogo, na mdogo pia kumuheshimu mkubwa.Hivyo, wanadamu tunapaswa kuheshimiana.

  Kwenye hili la hofu ya mkwamo wa mchakato wa Katiba nayaona mapungufu mawili kwa pande zinazohusika; KUTOHESHIMIANA na KUTOAMINIANA.

  Kwenye awamu ya kwanza ya Bunge Maalum la Katiba mawili hayo yalijidhihiri. Hakika UKAWA na CCM kwa pamoja wamebeba dhamana kubwa ya hatma ya nchi yetu. Kuna makosa yameshafanyika tangu kuanza kwa mchakato huu. Hatupaswi kama taifa kuwa kama tembo kwenye msafara wao, kwamba hawarudi nyuma.

  Kabla ya kuendelea na mchakato huu wa Katiba, kama taifa, na kwa kupitia viongozi wakuu wa UKAWA na CCM. Viongozi hao, kwa namna yeyote ile, wana lazima ya kujiandalia au kuandaliwa mazingira ya kukaa meza moja kama Watanzania. Kuendelea kufanya vikao vya siri na kuyapitia mapungufu yaliyojitokeza kwenye Awamu ya kwanza, kisha watoke kwa pamoja na kwa kauli moja ya namna ya kwenda mbele.

  Wakishindwa kukaa meza moja,basi,ni heri mchakato mzima ukahairishwa kusubiri wakati muafaka, kuliko kusonga mbele kwa staili ya msafara wa tembo, maana, huko njiani kutakuwa na vichuguu vingi vya siafu vitakavyokanyagwa, na tembo pamoja ukubwa wao, wataweweseka sana porini, na hata kusababisha pori lichafuke. Pori kukosa amani.

  RAI YANGU: Kinachoonekana kwa sasa ni kwamba CCM hawako tayari kwa Serikali Tatu, kuna mengine basi, ya muhimu kwa nchi, ambayo CCM wako tayari nayo. Na UKAWA nao hawako tayari kurudi bungeni kwa kujadili Serikali Mbili, kuna mengine pia UKAWA wako tayari nayo na muhimu sana kwa taifa. Na katika dunia hii, si yote anayotaka mwanadamu anayapata katika wakati huo huo anapoonyesha kuyataka, mengine husubiri.

  Na kubaki kuelekeza lawama kwa Rais wa nchi na hata kumtaka aombe radhi kwa wananchi hilo nalo haliwezekani na ni kuendelea kupoteza muda. Pamoja na kuwa Urais ni taasisi, lakini, Rais naye ni mwanadamu kama wengine, si malaika, na ni MwanaCCM pia, si Mwana UKAWA.

  Na katika dunia tunayoishi, yumkini kuna UKAWA ndani ya CCM na CCM ndani ya UKAWA. Hivyo,yawezekana haya tunayoyashuhudia si mepesi sana. Si mepesi maana hata kuamini kuwa Bunge liendelea na UKAWA warudi Bungeni ina maana ya kuendelea kwa malumbano na ushindani wa CCM na UKAWA. Ni kwa vile itakuwa na tafsiri ya kuendelea kuwepo Bungeni kwa wajumbe wa ' Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi' dhidi ya ' CCM'. Nao watakuwa wakitetea Katiba ya nani? Ni mazungumzo tu ya pande mbili katika mazingira ya kuheshimiana na kuaminiana ndiyo yanapaswa kuandaa mazingira ya wajumbe wa Barazala Katiba kurudi Bungeni kwa maslahi ya taifa na si makundi yao.

  Na zaidi, tumwamini Rais wetu katika dhamira yake ya kuanzisha mchakato wa kupata Katiba Mpya. Tumsaidie pia, maana, yumkini, Katiba Mpya ni moja ya mambo anayotaka kuyaacha nyuma yake na akumbukwe nayo-legacy.

  Hivyo, tulikofikia ni mahali ambapo kila mzalendo wa nchi hii anapaswa kujisikia huzuni na hata kujutia. Tulikofikia hakuna mshindi, sote tumeshindwa, kama taifa. Maana, tumetumia rasilimali nyingi kama taifa, muda na fedha . Mchakato huu kukwamia hapa ni aibu kwa taifa. Na wahenga walisema; majuto ni mjukuu, na kwamba yaliyopita si ndwele, tugange yajayo.

  Kongamano la Kitaifa la Katiba lililoandaliwa na Baraza la Vyama Vya siasa, liwe ni fursa ya kutukwamua kutoka tulikokwama, hivyo, kusonga mbele kwa KUHESHIMIANA na KUAMINIANA. Ndio,kongamano hilo litoke na ' AZIMIO LA DODOMA' la kusonga mbele kama taifa.

  Ni Neno La Leo.

  0 0

  Miss Redd's Kagera 2014 Jackline Kimambo kwenye pozi ya picha baada ya Kutangazwa Mshindi usiku wa kuamkia leoMshindi wa Taji la Redd's Miss Kagera Jackline Kimambo(katikati) kwenye picha ya pamoja na mshindi wa  pili na watatu ambapo mshindi wa pili ni Nyangi Warioba na watatu ni Faudhia Haruna(kushoto).Babylove Kalala (kulia) akimvisha taji Miss Redd's Kagera 2014 Jacline Kimambo(katikati) shindano lililofanyika usiku huu katika Ukumbi wa Lina's Night Club Bukoba Mjini.
  Mshindi wa Miss Redd's mwaka 2012 Babylove Kalala ndie aliyemvalisha Taji Miss Redd's Kagera 2014
  Picha za Pamoja zilipigwa za washindi
  Jackline Kimambo(katikati) Mshindi wa Redd's Miss Kagera 2014, kulia ni mshindi wa pili Nyangi Warioba na (kushoto) ni Faudhia Haruna kwenye picha ya pamoja.
  Warembo walipokuwa wakitoa burudani ya ufunguzi.
  Jumla ya warembo nane walichuana
  Warembo wakitoa Burudani yao ya Onesho la Ufunguzi Jukwaani.
   Mgeni Rasmi (kushoto) Bw. Amimu Kangezi-Mwenezi wa Chama cha mapinduzi Mkoa Kagera na (kulia) ni Kiongozi wa Utamaduni hapa Kagera
  Warembo wakitoa Burudani ya Ufunguzi
  Sharobaro Wakihaya kutoka kundi la Futuhi la (Star Tv) akipagawisha Wahaya wenzake katika Usiku wa Redd's Miss Kagera 2014
  Ilikuwa Balaa sana!! Tajiri wa Kigoma nae alikuwepo!Kwa kuchekeshaa tuu!! Huu ndio mtambo wa kuchomoa mbavu na kuanika 32 nje!!
  Vazi la Ufukweni
  Mshiriki Miss Redd's Kagera 2014 Tete Augustine
  Warembo wakionesha VaziUbunifu
  Furaha kwa Mashabiki wao! TabasamuChief Judge alimtangaza Miss Redd's Talent 2014 Jackline Kimambo na kuvishwa taji!Miss Redd's Talent 2014, Jackline akiwa kwenye hali ya kushangaa baada ya kutajwa!
  Baadhi ya Wapenzi wa Miss Redd's wakifuatilia kwa karibu Mchuano huu wa kmpata Mwakilishi wa Mkoa wa Kagera 2014
  Majaji wakiumiza kichwa kutafuta tano bora, kutoka kushoto ni Jaji Abera Kamala, Mr. Jay Buberwa na kulia ni Jaji Lilian PeterWarembo wa Miss Redd's Kagera 2014 waliobahatika kuingia Tano Bora-"Top 5"
  Baadhi ya Dadaz wakifuatilia nao kwa karibu wadogo zao wanavyo chuana jukwaaniWakina Dada wa Kundi la Dreams Girls kutoka Nchini Uganda walikuwepo kutoa Burudani naoKundi hili linataba sana na nyimbo mablimbali zikiwemo za Wine, Weekiend, Dance overnight, Wandekangawo na nyingine kibao.Hatari lakini salama!Kibao cha jigy jigy kikishambuliwa na wenyewe jukwaani!! Wadau wa Miss redd's wakichukua na Kumbukumbu na wengine furaha zipo 120, Vunjika mbavu!! Kutoka kwa Mwanahutuhi!
  Walioshindwa kujizuia waliwafuata jukwaani!! Dreams Girls na Mashabiki wao wakifanya yao stejini
  Hakika Dreamz Girls walishusha Burudani ya nguvuUnaweza ukajizuia kuona hata kucheka!! Macho yoote ylikuwa mbele!Junior Mwemezi akichukua kumbukumbu za Video kwenye Ukumbi wa Lina's Night Club, Usiku wa Redd's Miss Kagera 2014.Picha ya Pamoja na Mgeni Rasmi (kushoto) Bw. Amimu Kangezi-Mwenezi wa Chama cha mapinduzi Mkoa Kagera.

older | 1 | .... | 333 | 334 | (Page 335) | 336 | 337 | .... | 1897 | newer