Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 332 | 333 | (Page 334) | 335 | 336 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Balozi wa Norway nchini anayemaliza muda wake Mhe. Ingunn Klepsvik wakati balozi huyo alipokwenda kumuaga ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Norway nchini anayemaliza muda wake Mhe. Ingunn Klepsvik wakati balozi huyo alipokwenda kumuaga ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Balozi wa Norway nchini anayemaliza muda wake Mhe. Ingunn Klepsvik wakati balozi huyo akimuaga ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi (picha na Freddy Maro)

  0 0

   Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Nassor Ahmed Mazrui akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa maonyesho ya biashara ya Eid El Fitri katika viwanja vya Maisara, wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Sabetha Mwambenja na katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi. Anna Bulondo.
   Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Nassor Ahmed Mazrui akiangalia bidhaa za wajasiriamali kwenye maonyesho ya Biashara ya Eid El Fitri yanayofanyika katika viwanja vya Maisara, pamoja nae katika picha kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi. Anna Bulondo, na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Thawabay Kisasi.
  Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko wa Zanzibar Nassor Mazrui akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Sabetha Mwambenja wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbali mbali wa serikali na TanTrade punde baada ya kufungua Maonesho ya Eid El Fitri visiwani humo.


  (Picha: Maelezo Zanzibar)
  TanTrade yapongezwa kwa kuboresha Muungano Kibiashara

  Waziri wa Viwanda, Masoko na Biashara wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Nassor Ahmed Mazrui ameipongeza Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania, (Tantrade) kwa kuwa na utendaji unaozingatia Usawa kati ya Bara na Visiwani Zanzibar na kuboresha biashara pande zote.

  Waziri Mazrui amesema hayo wakati wa Hafla ya Uzinduzi wa Maonesho ya Biashara ya Idd El Fitri yanayofanyika kwa siku nane Visiwani Zanzibar.

  “Mimi kama waziri mwenye dhamana ya kusimamia masuala ya masoko viwanda na biashara katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, nimeshuhudia utendaji mzuri ndani ya TanTrade unaozingatia usawa wa kibiashara kati ya Bara na Visiwani” alisema na kuongeza.

  “Kupitia TanTrade wafanyabiashara wa hapa Zanzibar wanapata fursa ya kushiriki katika maonesho mbalimbali ya ndani na nje ya nchi ambayo yanaandaliwa na Mamlaka hii bila ya kujali upande ambako maonesho haya yanaandaliwa, hili ni jambo jema na ni lakupongezwa kwani linakuza Uchumi wan chi na kutoa fursa sawa kwa wafanyabiashara, alisema Mazrui.

  Waziri huyo aliongeza kwa kutoa wito kwa Wafanya Biashara wa ndani kuboresha bidhaa zao na kutumia fursa wanayo ipata katika maonesho mbalimbali wanayoshiriki kwa kujenga mahusiano ya kibiashara na mtandao utakao weza kuwaongezea mauzo ndani na nje ya nchi.

  Kwa Upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Sabetha Mwambenja amesema kuwa Tantrade itaendelea kuwaunga mkono wafanyabiashara wa Tanzania na kuhakikisha Ubora na viwango vya bidhaa za Tanzania unaboresheka, huku akitanabaisha kuwa Mamlaka hiyo iko katika hatua za mwisho za kukamilisha Ofisi za kuduma Visiwai Zanzibar.

   “Tunatambua umuhimu wa kuboresha na kupanua huduma zetu, hivyo tuliomba serikali itusaidie kupata jengo ambalo tungeweza kulitumia kama Ofisi za kudumu na tukapatiwa jengo hilo, na sasa tuko katika hatua za mwisho za kukamilisha ofisi zetu Visiwani Zanzibar” alisema.

  “Ninaipongeza Serikali kwa namna ambavyo imekuwa ikiunga mkono jitihada zetu za kukuza biashara na uchumi wa Taifa kwa ujumla, tunawaahidi wafanyabiashara wote na Watanzania kwa ujumla kuwa TanTrade tutasimamia na kutoa fursa sawa kadri inavyowezekana.

  Awali, Kaimu Mkurugenzi wa TanTrade Bi. Anna Bulondo, pamoja na kutoa wito kwa Watanzania kujitokeza katika maonesho hayo ametoa wito kwa, taasisi za Serikali, mashirika binafsi na jumuiya ya wafanyabiashara kufanya maandalizi ya Maonesho ya Mapinduzi ya Zanzibar mapema ambayo yatafanyika kwa mara ya pili mjini Zanzibar.

  “Naomba nitoe wito kwa taasisi mbalimbali za serikali, mashirika binafsi na wafanyabiashara kufanya maandalizi mapema ya maonesho ya Mapinduzi ambayo yatafanyika kwa mara ya pili visiwani Zanzibar baada ya kufanyika kwa mafanikio Makubwa mwaka jana wakati wa sherehe za Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

  0 0
 • 07/31/14--05:18: Article 6


 • TANGAZO
  WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO MHE.DKT.FENELLA MUKANGARA ATAKUWA MGENI RASMI KATIKA UZINDUZI WA MAFUNZO YA MAKOCHA WA MPIRA WA MIGUU YATAKAYOFANYIKA KATIKA UWANJWA WA KARUME  KESHO TAREHE 01 AGOSTI 2014 SAA 4:00 ASUBUHI. MAFUNZO HAYO YATAENDESHWA NA WATAALAM  KUTOKA BARCELONA NCHINI HISPANIA

  WAANDISHI WA HABARI MNAKARIBISHWA

  IMETOLEWA NA
  KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
  WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO

  0 0
  THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

  Telephone:255-22-2114512, 2116898
  Website : www.ikulu.go.tz              

  Fax: 255-22-2113425  PRESIDENT’S OFFICE,
        STATE HOUSE,
                1 BARACK OBAMA ROAD,  
  11400 DAR ES SALAAM.
  Tanzania.
   

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi kufuatia ajali iliyotokea tarehe 30 Julai, 2014 katika eneo la Pandambili, Wilayani Kongwa na kuua watu wapatao 18.

  Katika ajali hiyo, watu 13 walifariki katika eneo la ajali, na majeruhi wapatao 56 walifikishwa hospitalini. Kati ya majeruhi hao hadi sasa waliolazwa ni 30 na wengine wameruhusiwa baada ya kupata matibabu.

  Rais amemuomba Dkt. Nchimbi kumfikishia rambirambi zake za dhati kwa ndugu na jamaa waliopoteza wapendwa wao katika ajali hiyo, na kuwapa pole majeruhi wote na kuwatakia kupona haraka ili warejee kwenye shughuli zao za kila siku.

  “ Natoa Pole za dhati kwa wale wote walioondokewa na wapendwa wao katika ajali hii na pia kuchukua nafasi hii kuwapa pole majeruhi wote na kuwaombea kupona haraka na kurudi katika shughuli zao za kila siku”.  Rais amesema katika salamu zake kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

  “Hakika ni jambo la kusikitisha sana kuondokewa na wananchi wetu katika ajali , natoa wito wangu kwa madereva wote na wote wanaotumia vyombo vya moto kuwa makini wanapokuwa barabarani “.  Rais amesema na kuongeza kuwa;  

  “Kila dereva anaetumia chombo cha moto,  ana wajibu wa kulinda maisha yake na ya watumiaji wengine kwa kuwa makini na muangalifu awapo barabarani, kwani ajali hizi zinarudisha nyuma maendeleo ya taifa na ya wananchi kwa ujumla” Rais amesema na kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama barabarani kutolegeza kamba katika kuwachukulia hatua madereva wasio makini na wazembe wakati wote”.Rais amesisitiza.


  Taarifa kutoka Mkoani Dodoma zinasema ajali hiyo ya jana (30 Julai, 2014) ilisababishwa na Lori  ambalo lilitaka kupita lori jingine na hivyo kwenda kugongana uso kwa uso na Basi la Moro Best lililokuwa likitokea Mpwapwa kuelekea Dar es Salaam.

  ……Mwisho……

  Imetolewa na;
  Premi Kibanga,
  Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
  Ikulu – Dar es Salaam.
  30 Julai, 2014

  0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira Mh. Dkt. Eng Binilith Satano Mahenge akizindua rasmi tovuti ya mabadiliko ya tabianchi itakayotumika kutoa taarifa mbalimbali za utunzaji wa Mazingira.
   
  Mheshimiwa      Eng  Dkt. Binirithi S.  Mahenge  (mbunge)  Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa  Rais (mazingira) azindua tovuti ya mabadiliko ya tabia  nchi. Katika hotuba yake fupi ya uzinduzi wa tovuti hiyo, aliyoandaliwa kwa ufadhili wa serikali ya Denmark Mh. Binirithi  Mhenge amesema kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi huangaliwa kwa muda wa miaka 30 hivyo kwa kipindi hiki chote kumekuwa na madhara mengi yatokanayo na athari za mabadiliko ya tabia Nchi ikiwa ongezeko la joto, kina cha bahari kuongezeka pamoja na ongezeko la majanga ya mvua zisizo na viwango,  kutoka na shughuli za binadamu katika uzalishaji hasa viwanda vikubwa

  Alisema kwa tovuti inayozinduliwa ina umuhimu mkubwa kwani inaelezea maeneo ya hali ya mabadiliko ya tabia  nchi na juhudi za serikali katika kukabiliana na athari zinazoletwa na mabadiliko hayo.

  “ziko sababu za kuungana na wenzetu ili kuondoa      tatizo hili la mabadiliko ya nchi ambapo tovuti hii WWW.climatechange.go.tzinatuunganisha na tovuti mbali mbali katika kupunguza gesi joto hapanchini pia inaelezea fursa zilizopo katika miradi na program mbali mbali. Alisisitiza”

  Alibaini kuwa tovuti hii itachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza uelewa na weledi kuhusu mabadiliko ya tabia  nchi nchini kwa wananchi na wadau kwa ujumla.

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira Mh. Dkt. Eng Binilith Satano Mahenge (wa kwanza kushoto) akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) katika ukumbi wa mkutano wa  Ofisi ya Makamu wa Rais leo jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa "tovuti ya mabadiliko ya tabianchi" huku akieleza malengo ya tovuti hiyo. kushoto ni Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Julius Ningu.
   sehemu ya wadau waliyoudhulia katika mkutano huo kushuhudia makubaliano ya mkataba huo.
   Mkuu Msaidizi wa Chuo cha kilimo SUA Prof. Gerald Monella (aliyesimama) akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wadau mbalimbali kuhusu mkataba huo unaofanyika baina ya Ofisi ya Makamu wa Rais na chuo cha SUA.
   Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sazi Salula (wa kwanza kushoto) na Mkuu Msaidizi wa Chuo cha SUA Prof. Gerald Monella wakisaini mkataba wa uwanzishwaji wa kituo cha Taifa cha kukusanya na kuratibu takwimu za hewa ukaa  uliofanyika katika ukumbi wa mkutano Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dar es Salaam.
   Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sazi Salula wakipeana Mkataba na mkuu msaidizi wa wa chuo cha kilimo SUA Prof. Gerald Monella baada ya kusaini.
   Sehemu ya waandishi wa habari waliyoudhulia katika uzinduzi huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  1a
  Marais wastaafu Thabo Mbeki wa Afrika Kusini na Festus Mogae wa Botswana wakiigia kwenye chumba cha Mkutano katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo wakati wa mkutano wa mwaka wa Africa Readership Forum ulioandaliwa na Taasisi ya Uongozi Institute jijini Dar es salaam ambao ulikuwa unajadili changamoto mbalimbali zinazozikabili nchi za Afrika na kuangalia masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na hatua za kushughulikia changamoto hizo.
  2a
  Rais mstaafu wa wa Afrika Kusin Thabo Mbeki akizungumza katika mkutano huo uliojumuisha viongozi mbalimbali wa afrika na taasisi mbalimbali kweye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo.
  3a
  Marais wastaafu Thabo Mbeki wa Afrika Kusini katikati ,Festus Mogae wa Botswana kushoo na Rais Mstaafu wa Tanzania Mh. Benjamin William Mkapa wakiwa wakiongoza mkutano huo.
  4a
  Baadhi ya viongozi kutoka taasisi mbalimbali waliohudhuria katika mkutano huo.
  5a
  Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh. Zitto Kabwe katikati ni mmoja wa viongozi waliohudhuria katik mkutano huo uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
  6a
  Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Fredrick Sumaye kulia ni Mh. Balozi Ali Karume walikuwa ni miogoni wa viongozi waliohudhuria katika mkutano huo pia.

  0 0

  Jeshi la Polisi likiimarisha ulinzi Mahakamani.


  Baadhi ya watuhumiwa wakiingizwa mahakamani wiki chache zilizopita

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

  JESHI LA POLISI TANZANIA

   

     TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU WATUHUMIWA WALIOKAMATWA WAKIHUSISHWA NA MATUKIO YA MILIPUKO YA MABOMU NA TINDIKALI MKOANI ARUSHA

   

  NDUGU WANAHABARI, MTAKUMBUKA KUWA WIKI MOJA ILIYOPITA JESHI LA POLISI LILITOA TAARIFA KWA UMMA JUU YA WATUHUMIWA SITA WALIOKAMATWA NA KUFIKISHWA MAHAKAMANI KUHUSIANA NA TUKIO LA MLIPUKO WA BOMU ULIOTOKEA TAREHE 07/07/2014 KATIKA MGAHAWA WA VAMA ULIOPO MAENEO YA VIWANJA VYA GYMKANA JIJINI ARUSHA.  TAARIFA HIYO ILIZUNGUMZIA PIA TUKIO LA KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA MMOJA AMBAYE BAADA YA KUPEKULIWA NYUMBANI KWAKE ALIKUTWA NA MABOMU SABA YA KURUSHA KWA MKONO, RISASI SITA ZA BUNDUKI AINA YA SHOT-GUN PAMOJA NA UNGA WA BARUTI. TULIELEZA PIA KUWA OPERESHENI YA KUKAMATA WATUHUMIWA WENGINE KUHUSIANA NA MATUKIO YA MILIPUKO YA MABOMU NA TINDIKALI ILIKUWA IKIENDELEA, NA KWAMBA WATUHUMIWA KADHAA WALIKUWA CHINI YA ULINZI WA POLISI KUHUSIANA NA MATUKIO HAYO.  KUTOKANA NA OPERESHENI HIYO ENDELEVU, WATUHUMIWA WENGINE KADHAA WAMEKWISHA KAMATWA NA KUHOJIWA, AMBAPO USHAHIDI ULIOKUSANYWA UMEBAINI KUWA  KATI YAO  WATUHUMIWA ISHIRINI NA MOJA (21) WANAHUSIKA KATIKA MATUKIO MBALIMBALI YA ULIPUAJI MABOMU NA KUMWAGIA WATU TINDIKALI HAPA JIJINI ARUSHA KATIKA KIPINDI CHA KUANZIA MWAKA 2012 HADI YALE YALIYOTOKEA KATIKA KIPINDI CHA HIVI KARIBUNI. WATUHUMIWA HAO WANATAZAMIWA KUFIKISHWA MAHAKAMANI TAREHE 01/08/2014 KUUNGANA NA WENZAO WALIOKWISHA TANGULIA ILI KUJIBU MASHITAKA YANAYOWAKABILI. UFAFANUZI WA WATUHUMIWA WALIOKAMATWA NA MATUKIO WALIYOHUSIKA NAYO NI KAMA IFUATAVYO:

   

   

  I.             TUKIO LA MLIPUKO WA BOMU NYUMBANI KWA SHEKH ABDULKARIM JONJO  TAREHE 25/10/2012

  WATAKAOFIKISHWA MAHAKAMANI:

  1.    YUSUPH S/O HUSEIN ALLY HUTA, MRANGI, MIAKA 30, MKAZI WA NGUSERO

   

  2.    KASSIM S/O IDRISA RAMADHAN, MRANGI, MIAKA 34, MKAZI WA NGUSERO BANDA MBILI, DEREVA BODABODA FRIENDS CORNERLL

   

  3.    MUSTAPHA S/O MOHAMED KIAGO, MZIGUA, MIAKA 49, MKAZI WA KALOLENI, NI SHEKH MSIKITI MKUU WA IJUMA

   

  4.    ABDUL-AZIZ S/O MOHAMED, MCHAGA, MIAKA 49, MKAZI WA ENEO LA FAYA, ALIKUWA IMAMU WA MSIKITI MKUU WA IJUMAA

   

  II.          TUKIO LA MLIPUKO WA BOMU KANISA LA ST. JOSEPH MFANYAKAZI OLASITI LA TAREHE 05/05/2013

  WATAKAOFIKISHWA MAHAKAMANI:

  1.    YUSUPH S/O HUSEIN ALLY HUTA, MRANGI, MIAKA 30, MKAZI WA NGUSERO.

   

  2.    RAMADHAN S/O HAMAD WAZIRI, MRANGI, MIAKA 28, MKAZI WA KWA MOROMBO.

   

  3.    ABDUL S/O MOHAMED HUMUD @ WAGOBA, MMANYEMA, MIAKA 30, MKAZI WA MURIET, WAKALA WA MABASI YA MOHAMED TRANS (AMEKWISHAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUHUSISHWA NA TUKIO LA BOMU MGAHAWA WA VAMA)

   

  4.    JAFAR S/O LEMA, MCHAGA, MIAKA 38, MKAZI WA NGULELO, ALIKUWA IMAMU WA MSIKITI WA QUBA (AMEKWISHA FIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUHUSISHWA NA TUKIO LA BOMU MGAHAWA WA VAMA)

   

  5.    SAID S/O  MICHAEL TEMBA, MCHAGA, MIAKA 42, MKAZI WA SINONI- UNGA LTD, MFANYABIASHARA SOKO LA KILOMBERO (AMEKWISHAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUHUSISHWA NA TUKIO LA BOMU MGAHAWA WA VAMA)

   

  6.    KASSIM S/O IDRISA RAMADHAN, MRANGI, MIAKA 34, MKAZI WA NGUSERO BANDA MBILI, DEREVA BODABODA FRIENDS CORNER

  7.    ABASHAR S/O HASSAN OMAR, MRANGI, MIAKA 24, MKAZI WA NGUSERO MWISHO WA HIACE, DEREVA BODABODA STAND KUU ARUSHA

   

  8.    ABDULRAHAMAN S/O JUMANNE HASSAN, MBONDEI, MIAKA 41, MKAZI WA SINONI, MFANYAKAZI WA STANBIC BANK ARUSHA

   

  9.    MORRIS S/O JOHN MUZI, MUHA, MIAKA 44, MKAZI WA KALINZI MKOANI KIGOMA

   

  10.NIGANYA S/O HAMISI NIGANYA, MUHA, MIAKA 28, MKAZI WA BUSINDE UJIJI MKOANI KIGOMA

   

  11.BARAKA S/O NTEMBO BILANGO, MUHA, MIAKA 40, MKAZI WA KALINZI MKOANI KIGOMA

   

  12.HASSAN S/O ABDALLAH OMAR, MNYATURU, MIAKA 40, MKAZI WA ILONGERO MKOANI SINGIDA

   

   

  III.        TUKIO LA MLIPUKO WA BOMU VIWANJA VYA SOWETO KWENYE MKUTANO WA CHADEMA TAREHE 15/06/2013

  WATAKAOFIKISHWA MAHAKAMANI:

  1.    YUSUPH S/O HUSEIN ALLY HUTA, MRANGI, MIAKA 30, MKAZI WA NGUSERO

   

  2.    ABDUL S/O MOHAMED HUMUD @ WAGOBA, MMANYEMA, MIAKA 30, MKAZI WA MURIET, WAKALA WA MABASI YA MOHAMED TRANS (AMEKWISHAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUHUSISHWA NA TUKIO LA BOMU MGAHAWA WA VAMA)

   

  3.    JAFAR S/O LEMA, MCHAGA, MIAKA 38, MKAZI WA NGULELO, ALIKUWA IMAMU WA MSIKITI WA QUBA (AMEKWISHA FIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUHUSISHWA NA TUKIO LA BOMU MGAHAWA WA VAMA)

   

  4.    SAID S/O  MICHAEL TEMBA, MCHAGA, MIAKA 42, MKAZI WA SINONI- UNGA LTD, MFANYABIASHARA SOKO LA KILOMBERO (AMEKWISHAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUHUSISHWA NA TUKIO LA BOMU MGAHAWA WA VAMA)

  5.    KASSIM S/O IDRISSA RAMADHAN, MRANGI, MIAKA 34, MKAZI WA NGUSERO BANDA MBILI, DEREVA BODABODA FRIENDS CORNER

   

  6.    RAMADHAN S/O HAMAD WAZIRI, MRANGI, MIAKA 28, MKAZI WA KWA MOROMBO

   

  7.    ABASHAR S/O HASSAN OMAR, MRANGI, MIAKA 24, MKAZI WA NGUSERO MWISHO WA HIACE, DEREVA BODABODA STAND KUU ARUSHA

   

  8.    ABDULRAHAMAN S/O JUMANNE HASSAN, MBONDEI, MIAKA 41, MKAZI WA SINONI, MFANYAKAZI WA STANBIC BANK ARUSHA

  9.    MORRIS S/O JOHN MUZI, MUHA, MIAKA 44, MKAZI WA KALINZI MKOANI KIGOMA

   

  10.NIGANYA S/O HAMISI NIGANYA, MUHA, MIAKA 28, MKAZI WA BUSINDE UJIJI MKOANI KIGOMA

  11.BARAKA S/O NTEMBO BILANGO, MUHA, MIAKA 40, MKAZI WA KALINZI MKOANI KIGOMA

   

  12.HASSAN S/O ABDALLAH OMAR, MNYATURU, MIAKA 40, MKAZI WA ILONGERO MKOANI SINGIDA

   

  IV.          TUKIO LA KUMWAGIWA TINDIKALI SHEKH SAID JUMA MAKAMBA WA MSIKITI WA KWA MOROMBO TAREHE 11/07/2013

  WATAKAOFIKISHWA MAHAKAMANI:

  1.    YUSUPH S/O HUSEIN ALLY HUTA, MRANGI, MIAKA 30, MKAZI WA NGUSERO

   

  2.    RAMADHAN S/O HAMAD WAZIRI, MRANGI, MIAKA 28, MKAZI WA KWA MOROMBO.

   

  3.    KASSIM S/O IDRISA RAMADHAN, MRANGI, MIAKA 34, MKAZI WA NGUSERO BANDA MBILI, DEREVA BODABODA FRIENDS CORNER

   

  4.    JAFAR S/O LEMA, MCHAGA, MIAKA 38, MKAZI WA NGULELO, ALIKUWA IMAMU WA MSIKITI WA QUBA (AMEKWISHA FIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUHUSISHWA NA TUKIO LA BOMU MGAHAWA WA VAMA)

   

  V.           TUKIO LA KUMWAGIWA TINDIKALI SHEKH MUSTAPHA KIAGO WA MSIKITI MKUU LA TAREHE 28/02/2014

  WATAKAOFIKISHWA MAHAKAMANI:

  1.    YUSUPH S/O HUSEIN ALLY HUTA, MRANGI, MIAKA 30, MKAZI WA NGUSERO

   

  2.    KASSIM S/O IDRISSA RAMADHAN, MRANGI, MIAKA 34, MKAZI WA NGUSERO BANDA MBILI, DEREVA BODABODA FRIENDS CORNER

   

  3.    JAFAR S/O LEMA, MCHAGA, MIAKA 38, MKAZI WA NGULELO, ALIKUWA IMAMU WA MSIKITI WA QUBA (AMEKWISHA FIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUHUSISHWA NA TUKIO LA BOMU MGAHAWA WA VAMA)

   

  4.    HASSAN S/O ALLY MFINANGA, MPARE, MIAKA 57, MKAZI WA MAKAO MAPYA, BIASHARA

   

  VI.          TUKIO LA BOMU ARUSHA NIGHT PARK (MTK) LA TAREHE 13/04/2014

  WATAKAOFIKISHWA MAHAKAMANI:

  1.    JAFAR S/O LEMA, MCHAGA, MIAKA 38, MKAZI WA NGULELO, ALIKUWA IMAMU WA MSIKITI WA QUBA (AMEKWISHA FIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUHUSISHWA NA TUKIO LA BOMU MGAHAWA WA VAMA)

   

  2.    IBRAHIM S/O LENARD @ SHEKH ABUU ISMAIL, MSUKUMA, MIAKA 37, MKAZI WA MABATINI MKOANI MWANZA.

   

  VII.      TUKIO LA BOMU NYUMBANI KWA SHEKH SUDI ALLY SUDI LA TAREHE 03/07/2014

  WATAKAOFIKISHWA MAHAKAMANI:

  1.    YAHAYA S/O TWALIB TWAHIR @ MPEMBA, MSAMBAA, MIAKA 37, MKAZI WA MTAA WA JALUO, MFANYABIASHARA YA DUKA MTAA WA BONDENI

   

  2.    IDD S/O RAMADHAN YUSUPH, MSAMBAA, MIAKA 23, MKAZI WA MTAA WA JALUO.

   

  3.    SAID S/O  MICHAEL TEMBA, MCHAGA, MIAKA 42, MKAZI WA SINONI- UNGA LTD, MFANYABIASHARA SOKO LA KILOMBERO (AMEKWISHAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUHUSISHWA NA TUKIO LA BOMU MGAHAWAWA VAMA)

   

  4.    ANWAR S/O NASHER HAYEL, MNYAMWEZI, MIAKA 29, MKAZI WA  NGULELO, MFANYABIASHARA

   

  5.    JAFAR S/O LEMA, MCHAGA, MIAKA 38, MKAZI WA NGULELO, ALIKUWA IMAMU WA MSIKITI WA QUBA (AMEKWISHA FIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUHUSISHWA NA TUKIO LA BOMU MGAHAWA WA VAMA)

  6.    HASSAN S/O ALLY MFINANGA, MPARE, MIAKA 57, MKAZI WA MAKAO MAPYA, BIASHARA

   

  7.    YUSUPH S/O ALLY RAADHAN @ SEFU, MPARE, MIAKA 23, MKAZI WA NGUSERO

   

  8.    ABASHAR S/O HASSAN OMAR, MRANGI, MIAKA 24, MKAZI WA NGUSERO MWISHO WA HIACE, DEREVA BODABODA STAND KUU ARUSHA

   

  VIII.    TUKIO LA KUPATIKANA NA MABOMU LA TAREHE 21/07/2014

  WATAKAOFIKISHWA MAHAKAMANI:

  1.    YUSUPH S/O HUSEIN ALLY HUTA, MRANGI, MIAKA 30, MKAZI WA NGUSERO

   

  2.    SUMAIYA W/O YUSUPH HUSEIN ALLY, MWASI, MIAKA 19, MKAZI WA NGUSERO.

   

  3.    RAMADHAN S/O HAMAD WAZIRI, MRANGI, MIAKA 28, MKAZI WA KWA MOROMBO.

   

  4.    HASSAN S/O ALLY MFINANGA, MPARE, MIAKA 57, MKAZI WA MAKAO MAPYA, BIASHARA

   

  5.    ABASHAR S/O HASSAN OMAR, MRANGI, MIAKA 24, MKAZI WA NGUSERO MWISHO WA HIACE, DEREVA BODABODA STAND KUU ARUSHA

   

  6.    KIMORO S/O ISSA MCHANA @  OMAR @ ABUU TWALIB, MRANGI, 25YRS, MKAZI WA ITOLWA KONDOA

   

  7.    HASSAN S/O ABDALLAH OMAR, MNYATURU, MIAKA 40, MKAZI WA ILONGERO MKOANI SINGIDA.

   

  8.    MORRIS S/O JOHN MUZI, MUHA, MIAKA 44, MKAZI WA KALINZI MKOANI KIGOMA

   

  9.    NIGANYA S/O HAMISI NIGANYA, MUHA, MIAKA 28, MKAZI WA BUSINDE UJIJI MKOANI KIGOMA

   

  10.BARAKA S/O NTEMBO BILANGO, MUHA, MIAKA 40, MKAZI WA KALINZI MKOANI KIGOMA

   

  IX.          KOSA LA KUHAMASISHA VITENDO VYA KIGAIDI KUPITIA MTANDAO WA KIJAMII

  WATAKAOFIKISHWA MAHAKAMANI:

  1.    IBRAHIM S/O LENARD @ SHEKH ABUU ISMAIL, MSUKUMA, MIAKA 37, MKAZI WA MABATINI MKOANI MWANZA.

   

  2.    ANWAR S/O NASHER HAYEL, MNYAMWEZI, MIAKA 29, MKAZI WA  NGULELO, MFANYABIASHARA

   

  3.    YASINI S/O MOHAMED SHABAN @ YAKI, MCHAGA, MIAKA 20, MKAZI WA KALOLENI MITA 200

  OPERESHENI YA  KUWATAFUTA WATUHUMIWA WENGINE WA MATUKIO HAYA INAENDELEA NCHI NZIMA, NA TAYARI TUNAYO MAJINA YA WATUHUMIWA KADHAA AMBAO WAMETOWEKA ARUSHA NA KUELEKEA MAENEO MBALIMBALI YA NDANI NA NJE YA NCHI. MTUHUMIWA MMOJAWAPO ANAYETAFUTWA SANA NA POLISI KUHUSIANA NA MATUKIO HAYA NI YAHAYA HASSAN HELLA @ SENSEI, KABILA NI MRANGI, MZALIWA WA KIJIJI CHA CHEMCHEM WILAYA YA KONDOA.

  IMEBAINIKA KUWA MTUHUMIWA HUYO NDIYE KINARA WA MATUKIO YA MILIPUKO YA MABOMU NA TINDIKALI HAPA JIJINI ARUSHA KWA KUSHIRIKIANA NA WENZAKE WALIOKAMATWA, NA AMBAO BADO WANAENDELEA KUTAFUTWA. JESHI LA POLISI  LINAFANYA KILA JITIHADA KUWEZA KUWAKAMATA WATUHUMIWA WOTE WALIOTOROKA NA KUHAKIKISHA KUWA SHERIA INACHUKUA MKONDO WAKE.

  ASANTENI KWA KUNISIKILIZA.

  0 0

   Naibu Waziri wa Maji,Mh.  Amos Makalla (kulia), akipata maelezo kutoka kwa kiongozi wa Mafundi wa Kampuni ya CDM Smith, John Donoherth, kuhusu ujenzi wa kisima kilichopo Mkwalia Mkuranga ambacho ni moja kati ya visima 8 vinavyofanyiwa utafiti maji wilayani humo. Makalla alifanya ziara ya kukagua miradi ya maji wilayani Mkuranga mkoani Pwani leo. Pia alikagua mradi wa  kisima cha maji cha Nyamato chenye uwezo wa kutoa maji lita 26,000 kwa saa kitakachohudumia wakazi wa vijiji vya  Mvuleni, Nyamato na Kilimahewa. 
  Naibu Waziri wa Maji, Mh. Amos Makalla akiangalia mradi wa kisima cha Mkwalia ambacho kinafanyiwa utafiti
   Maji yakitiririka kwenye kisima hicho
  Naibu Waziri wa Maji, Mh. Amos Makalla akijadiliana jambo na Mkandarasi wa kisima hicho,John Donoherth


  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Kigamboni,Dk Faustine Ndugulile, akikata utepe kuashiria tendo la kukabidhi madawati 650 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 60, kwa shule 12 za sekondari katika tarafa ya Mbagala, makabidhiano yaliyofanyika jana.
  Mbunge wa Jimbo Kigamboni,Dk Faustine Ndugulile, (Katikati),akiwa na baadhi ya watendaji wa halmashauri ya manispaa ya Temeke idara ya elimu, mara baada ya kukabidhi madawati 650 kwa shule 12 za sekondari katika tarafa ya Mbagala jijini Dar esSalaam.
  Mbunge wa Jimbo la Kigamboni,Dk Faustine Ndugulile, aakiwahutubia wazazi na wanafunzi wanaotoka katika shule 12 za sekondari katika tarafa ya Mbagala kabla ya kuzikabidhi shule hizo jumla ya madawati 650 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 69,makabidhiano yaliyofanyika katika shule ya sekondari Mbagala.


  0 0  Mtuhumiwa  wa kesi ya Mauaji, Conrad Leo (33)akiwa chini ya ulinzi wa polisi mara baada ya kuachiwa na kukamatwa tena katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam jana.Mtuhumiwa huyo anashitakiwa kwa kosa la kumuua kwa kutumia silaha Ayubu Mlai.
  Mtuhumiwa  wa kesi ya Mauaji, Conrad Leo (33)akiwa ndani ya gari ya polisi akipelekwa Mahabusu baada ya kuachiwa na kukamatwa tena katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam .Mtuhumiwa huyo anashitakiwa kwa kosa la kumuua kwa kutumia silaha Ayubu Mlai 
  Mtuhumiwa  wa kesi ya Mauaji, Conrad Leo (33)akizibitiwa na Polisi

  0 0

  IDADI ya watu waliokufa katika ajali ya Dodoma imeongezeka baada ya mtu mwingine kufa .
   
  Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi David Misime amesema tukio hilo la Pandambili Wilayani Kongwa katika barabara ya Dodoma – Morogoro limesababisha vifo vya watu 18 wanaume watu wazima 11 na mtoto mmoja wa kiume na Wanawake watu wazima 5 na mtoto 1 wa kike.
   
   Majina ya Marehemu hao ambao wametambuliwa na ndugu zao na kusafirishwa kwenda makwao kwa maziko ni:-
   1.   Christina d/o Dickson, Miaka 35, Mgogo, Mkulima, Mkazi wa Mpwapwa
   2.   Omari s/o Mkubwa, Miaka 32, Muhaya, Kondakta wa bus, Mkazi wa Morogoro
   3.   Malick s/o Masawe, Miaka 42, Mfanyabiashara, Mkazi wa Mpwapwa
   4.   Wilson s/o Paul @ Suda, Miaka 63, Mgogo, Mstaafu  Red Cross, Mkazi wa Mpwapwa.
   5.   Said s/o Lusogo, Miaka 44, mluguru, dereva wa bus, Mkazi wa Kihonda Morogoro.
   6.   Gabriel s/o Meja @ Chiwipe, Miaka 50, Mgogo, Mkazi wa Mpwapwa
   7.   Gilbert s/o Lemanya, Miaka 53, Mgogo, dereva wa Lori, Mkazi wa Makole Dodoma
   8.   Mikidadi s/o Zuberi @ Omari Miaka 22, Mbondei, Tingo wa Lori, Mkazi wa Morogoro/Ilala Dar es Salaam.
  9.   Justine s/o Makasi, Miaka 24, Mgogo, Mkulima wa Mpwapwa
  10.       Alice d/o Masingisa, Miaka 24, Mgogo, Mkazi wa Mpwapwa
  11.       Merina d/o Doto @ Marcel, Mgogo, Miaka wa Mji mpya  Mpwapwa
  12.       Nasibu s/oSeif, Miaka 48, Mkazi wa Morogoro
  13.       Nicholaus s/o Raymond Kileo Miaka 51, Mkazi wa Mpwapwa
  14.       Stella d/o Mdako, Miaka 60, Mkazi wa Mpwapwa
  15.       Erick s/o Lucas,Miaka 10, Mkazi wa Morogoro
  16.       Nazaret s/o Deremsi @ Kasuga, Miaka 45, Mhehe,  Mfanyabiashara, Mkazi wa     Kibakwe Mpwapwa.
  17.       DArini d/o Dickson, Miaka 2, Mgogo, Mkazi wa Mpwapwa
  18.       Magreth d/o Nyanzi, Miaka 35, Mgogo, Mfanyabiashara, Mkazi    wa Mwananyamala Dar es Salaam.
           Aidha majeruhi waliokuwa wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Kongwa wametibiwa na kuruhusiwa na wengine kuhamishiwa katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma.
   
  Waliobaki katika Hospitali ya Mkoa wakiendelea na matibabu ni 32 na wanaendelea vizuri isipokuwa walio katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa karibu wa madaktari (ICU)  ambao ni George s/o Mjelwa, Miaka 40, Daktari wa Wilaya ya Mpwapwa na mke wake aitwaye Getrudar s/o Kombe, Miaka 37, Mfamasia wa Hospitali ya Wilaya ya Kondoa.
   
  Jana kamanda alisema ajali hiyo baada ya uchunguzi zaidi inaonyesha kusababishwa na madereva wote wawili kwa maana ya dereva aliyekuwa anaendesha lori namba T 820 CKU/T390 CKT GILBERT S/O LEMANYA kwa kupita gari lingine bila kuwa mwangalifu na magari yaliyokuwa yanatokea mbele yake na kuwa katika mwendo kasi.
   
  Dereva wa bus namba T 858 AUH SAID S/O LUSOGO kulingana na mashuhuda hasa abiria wanaeleza alikuwa mwendo kasi na ndiyo maana ajali hii imeleta madhara makubwa kiasi hicho kwani kama angelikuwa kwenye mwendo wa kawaida unaotakiwa madhara yangekuwa siyo makubwa kiasi hicho pamoja na dereva wa lori kufanya aliyofanya.
   
  Wito kwa madereva na watumia barabara wengine waache mwendo kasi na ushabiki wa ushindani kwani kulingana na ushahidi uliokusanywa unaonyesha dereva wa Moro best alikuwa akiendesha kwa mwendo kasi kutaka kwenda kulipita bus la AL-SAEDY lililokuwa limeondoka mbele yake kwa kigezo kuwa dereva wa bus hilo ni mwanafunzi wake hivyo hawezi kufika Morogoro kabla yake.
   
  Wamiliki wa Ma bus na magari mengine wawaonye madereva wao kuhusiana na mwendo kasi na kuwataka wazingatie sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali mbaya kama hii.
   
   Aidha abiria wasiwe wanakaa kimya kama walivyofanya wa bus la Moro best wanapoona dereva anaendesha kwa mwendao wa kasi watoe taarifa Polisi ili wakamatwe na kuepusha madhara kama yaliyotokea. 

  Imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.

  0 0

  Mpendwa Baba yetu, Joseph Mturi Mahemba
  Hatimaye siku, Miezi imepita hadi hii leo ambapo imetimia Miaka miwili (2) tangu ulipotutoka ghafla usiku ule wa siku ya jumatano ya tarehe moja ya Mwezi Agosti, 2012 na kutuachia huzuni kubwa.

   Japokuwa haupo nasi hapa duniani lakini tupo nawe kiroho kwa kuendeleza mema yote uliyotufundisha na kutuasa.
  Tunakukumbuka kwa Upole, Upendo, Busara na Ukarimu uliokuwa nao kwa familia na Marafiki. Mwongozo na matendo yako yataendelea kuwa dira kwetu.

  Daima unakumbukwa sana na Mkeo Rose Joseph, dada  zako Theresia, Karaghita, Wankuru na Mnaga, wanao wapendwa Michael, Mkami, Niwa, Sagana, Mary, Geofrey, Nyakaho, Lecardia na Pricilla, na wajukuu zako wote.

  Ibada Maalum ya Maombi itafanyika tarehe 03/08/2014 Saa 2.00 asubuhi kwenye kanisa katoliki la Mt Maurus Kurasini, Dar es Salaam.
  Bwana ametoa, Bwana ametwaa jina lake libalikiwe.

  0 0
 • 07/31/14--22:11: ni shiiiidaaaaah..!

 • 0 0

  Kikwete na mtangazaji wa Cloud FM Mbwiga MbwigukeRais Dkt. Jakaya Kikwete akipozi katika picha na Mbwiga wa Mbwiguke wa Clouds fm (kulia)

  Na Maregesi Paul

  SIKU moja nilikuwa katika mkutano wa Jukwaa la Wahariri ambao mgeni rasmi alikuwa Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Reginard Mengi.Katika mazungumzo yake, Mengi aligusia historia ya maisha yake ambapo alisema alikulia katika familia masikini.Kwa mujibu wa Mengi, nyumba aliyokulia ilikuwa na panya wengi pamoja na mende na kwamba kila walipokuwa wakilala usiku, wapita njia walikuwa wakiwaona kwa sababu nyumba ilikuwa imejaa matobo.

  Pamoja na mazingira hayo, Mengi kwa sasa ni kati ya matajiri wakubwa wanaoheshimika ndani na nje ya nchi na suala la umasikini aliokulia, limebaki kuwa historia.Hivyo hivyo, hata mimi niliyeandika makala haya, niliwahi kuvua dagaa na sangara kwa kutumia nyavu haramu ziitwazo makokoro. Lakini sasa mimi ni mhariri wa gazeti hili na suala la uvuvi, limebaki katika historia.

  Wakati hayo yakitokea, katika Radio Clouds kuna watangazaji wengi wanaovuta masikio na hisia za wasikilizaji kutokana na lugha na vichekesho wanavyovitumia pindi wanapokuwa studio.
  Miongoni mwao ni Said Seleman maarufu kwa jina la Mbwiga wa Mbwiguke.

  Kama ilivyo kawaida kwa watu kuwa na historia tofauti tofauti kama nilivyoeleza hapo awali, wakati wa mahojiano maalum na MTANZANIA Jumatatu, Mbwiga anaeleza kwa kirefu ni wapi alikotokea hadi akawa mmoja wa watangazaji maarufu katika radio hiyo maarufu nchini.

  “Kwanza nianze na maana ya jina Mbwiga. Mbwiga ni neno la kizaramo ambalo maana yake ni rafiki. Kwa hiyo mimi ni rafiki wa kila mmoja kwa sababu huwa napenda sana kuwachekesha watu.
  “Lakini pia, maisha ni mzunguko na kamwe hakuna binadamu anayezaliwa na kujua maisha yake yatakuwaje kwa siku zijazo.

  “Kwa maana hiyo, hiki nitakachokieleza ndivyo kilivyo kwa sababu hapa nilipo sikutarajia kama itatokea siku nikawa mmoja wa watu wanaoungwa mkono na mamilioni ya Watanzania.“Kwanza kabisa niseme tu kwamba, mtu aliyenifikisha hapa ni mtangazaji mwenzangu aitwaye Shafii Dauda. Huyu ndiye aliyenileta Clouds baada ya kuniona naweza kuwa na mchango fulani fulani katika redio yetu hii.
  “Sikumbuki ni mwaka gani, lakini nakumbuka ni kama miaka mitatu iliyopita, siku moja usiku nilikuwa pale Muhimbili Shule ya Msingi kwenye mazoezi ya mpira unaowahusisha wachezaji wakongwe kama akina Akida Makunda, Mohamed Binda, Idd Moshi, Ally Mayai, Crement Kahabuka, Dua Said na wengineo wengi .

  “Siku hiyo nilikuwa sichezi bali nilikuwa shabiki tu nikiwashangilia wenzagu, kwa hiyo, mazoezi yalipomalizika, Shafii Dauda alikuja mahali nilipokuwa na akina Ally Mayai na alitukuta tunacheka,” anasema Mbwiga na kuongeza.“Alipoona tunacheka, akauliza tunacheka nini, Ally Mayai akamwambia huyu jamaa anatuchekesha, hebu mchukue umtumie kwenye kipindi chako kile cha michezo cha saa tatu usiku atakusaidia sana,” anasema Mbwiga.

  Kwa mujibu wa Mbwiga, Shafii alikubali na hapo ndipo ukawa mwanzo wa safari yake kujiunga na Radio Clouds.Anasimulia kwamba, baada ya kukubaliwa, Shafii akawa anampigia simu ili aripoti matukio mbalimbali ya michezo na kwamba taarifa hizo alikuwa akiziripoti katika mazingira magumu.
   
  “Wakati mwingine nilipokuwa nikiripoti, kuna wakati Shafii alikuwa akinipigia simu nikiwa kwenye daladala, kwa hiyo, nilikuwa nikilazimika kushuka ili nitafute sehemu nzuri iliyotulia ili nirekodi kipindi.
  Mtangaaji wa Clouds Fm, Mbwiga wa Mbwiguke (kushoto) akipozi na shabiki wake Imani Ntila.

  “Jambo la kuwaeleza wapenzi wa Radio Clouds ni kwamba, wakati ule nilipokuwa nikirekodi kipindi na Shafii, nilikuwa nikifanya kazi pale Uwanja wa Azamu kule Chamazi. Kule Azam nilikuwa nikisafisha uwanja kwa kuokota vyuma na chupa za maji zilizokuwa zikitupwa wakati wa ujenzi na zilizokuwa zikitupwa na wachezaji walipokuwa wakifanya mazoezi.

  “Lakini kumbuka kwamba, pale Azam nilikwenda kuomba kazi za uselemala, nilipokosa hiyo kazi, nikaangukia katika kusafisha uwanja kama nilivyokwambia.“Kwa maana hiyo, kuna wakati nilipokuwa nikitakiwa kurekodi kipindi na Shafii, nilikuwa nikijificha kwenye majukwaa chini kabisa kwa sababu kule pametulia kweli kweli.“Nilipokuwa nikifanya hivyo, wenzagu niliokuwa nikifanya nao usafi walikuwa wakilalamika kweli kwa sababu waliamini nategea kazi, kumbe mwenzao nilikuwa naandaa maisha,” anafafanua Mbwiga.
  Mbwiga Mbwiguke akiwatuliza wanachama wa Yanga waliojitokeza kwenye mkutano mkuu wa klabu hiyo mwaka huu.

  Baada ya kufanya kazi hiyo kwa miezi kama mitatu hivi, anasema baadaye Shafii aliamua kumpeleka ofisini kwao Mikocheni Dar es Salaam ambako alianza kutangaza akiwa studio.Alipofika ofisini hapo, anasema alikutana na mmiliki wa radio hiyo, Joseph Kusaga ambaye alisoma naye Shule ya Msingi Forodhani (zamani St Joseph).

  “Siku moja baada ya kuanza kutangaza, ilifanyika sherehe ya wafanyakazi wote ambapo MC alinipa fursa ya kuzungumza. Hapo nilimshukuru bosi Kusaga kwa kumwambia amenipa nyavu badala ya samaki, hivyo ni wajibu wangu kuendelea kuvua,” anasema Mbwiga.

  MAISHA YAKE KAZINI
  Mbwiga anasema baada ya kuanza kazi rasmi, anasema alikutana na changamoto nyingi ambazo ni pamoja na kutakiwa kujua mambo mengi yanayotokea duniani.

  Pia anasema kwa kiasi fulani amefanikiwa kufikia malengo kwa kuwa pamoja na kutangaza katika kipindi cha michezo cha saa tatu usiku, hivi sasa anashiriki katika kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa kila siku asubuhi.

  “Nashukuru kwa sababu sasa niko katika vipindi viwili, yaani kile cha usiku na cha asubuhi na nadhani wakubwa wangu wameniongezea majukumu baada ya kuona nina msaada fulani kiofisi.
  “Jambo la kushangaza ni kwamba, wakati naanza kutangaza Power Breakfast, moyo uliuma sana, yaani niliogopa kwa sababu sikujua kama ningeweza kufanikiwa.

  “Lakini Jerad Hando alinitoa hofu, akaniambia usiogope, hakuna kitu kipya, nikamuelewa na mwishowe nikawa nimefanikiwa,” anasema.
  EX6Mbwiga wa Mbwiguke (kuli) akipozi na Shaffih Dauda kwenye moja ya mechi iliyoihusisha timu ya mpira ya Clouds Media Group maarufu kama ‘The Dream Team’
   
  Mbwiga Mbwiguke (kulia) akiwa na mdau wa michezo

  MAISHA YAKE KWA SASA
  Mbwiga anasema kwa sasa anaonekana mtu wa maana mtaani kwake anaokoishi Magomeni Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla tofauti na alivyokuwa mwanzo.

  “Maisha yangu yamebadilika sana mtaani kwetu na jambo jingine ninaloshukuru ni kwamba, nina marafiki wengi na nafahamika kila mahali.

  “Yaani hata Rais Kikwete ananifahamu kwa jina kwa sababu mwaka jana nilifuturu naye Ikulu tukiwa naye meza moja.

  “Hata hivi karibuni tulikutana naye kwenye tamasha la wasanii kule Dodoma na aliponiona, aliniita kwa jina akaniambia, Mbwiga hujambo, nilimjibu, sijambo mheshimiwa, msimu wa embe nyani hakondi, halafu akacheka,” anaeleza.

  HISTORIA KIFAMILIA
  Anasema yeye ni mtoto wa pili kuzaliwa katika familia yao akitanguliwa na kaka yake aitwaye Nassor Fadhir anayeishi jijini Cologne, nchini Ujerumani.

  MALENGO YAKE
  Mbwiga ambaye anapenda kujitambulisha kuwa ni mzaramo, anasema ana mpango wa kujiendeleza kielimu ili aweze kuitumikia vizuri kazi yake.

  “Elimu yangu siyo kubwa sana ila nimesoma pale VETA Chang’ombe kwa miaka miwili na kutunukiwa cheti cha ujenzi wa barabara.

  “Baadaye nilijiingiza katika masuala ya ufundi selemala, kwa hiyo, naweza kusema mimi ni fundi selemala mzuri wa fenicha zote za ndani.

  “Ili niweze kwenda na wakati, niko katika mikakati ya kujiendeleza kielimu kwa sababu hata wafanyakazi wenzangu wamekuwa wakinihimiza juu ya hilo,” anasema.

  Katika mazungumzo yake, anawashukuru wafanyakazi wenzake wote na kuwataja baadhi kwa majina kuwa ni Joseph Kusaga, Ruge Mutahaba, Joyce Shebe, Shafii Dauda, Gerad Hando, Maestro, Alex Luambano, Bonge, PJ na Simalenga.

  “Nimewataja hao, lakini lazima umuweke Babra Hassan, yaani usipomtaja huyo, ataninunia mpaka basi,” anatania Mbwiga.

  0 0

  Maadhimisho ya siku ya Mwanamke wa Afrika yaliyo ratibiwa na Women in Law and Development in Africa-WiLDAF yafana jijini Dar es salaam. Ni siku ya Mwanamke wa Afrika na husheherekewa kila mwaka tarehe 31 July toka ilipotamkwa rasmi mwaka 1963 July 31 na wanawake wa Pan African waliokutana Dar es Salaam kwa wakati huo.Mada mbalimbali zilitolewa ikiwemo mchakato mzima wa katiba mpya na changamoto zake. Kulikuwa na watoa mada mbalimbali wakiwemo Dr Khoti Kamanga na Mh. Getrude Mongela.


  0 0

  Mbunge wa Ilala Mh. Mussa Zungu ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa Uzinduzi wa Maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) akikata utepe kuashiria uzindunzi wa maadhimisho ya chuo hicho kutimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake katika hafla iliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
  Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) wakiangalia moja ya picha ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyopigwa wakati akifungua Chuo hicho Januari, 1965. Kutoka kushoto ni Mkuu wa chuo hicho Prof. Emanuel Mjema, Mh. Musa Zungu (Mb) jimbo la Ilala,Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda,Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho Prof. Mathew Luhanga na Prof.Eliuta Mwageni Makamu Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha.
  Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) wakiwa katika picha ya pamoja wakiongozwa na Mbunge wa Ilala Mh. Mussa Zungu na Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda (katikati). Nyuma ni bango lenye picha ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyopigwa wakati akifungua Chuo hicho mwaka 1965.
  Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Tunu Pinda kwa niaba ya wanafunzi waliosoma katika chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam akizungumza na wadau na wanajumuiya wa Chuo hicho wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo hicho jijini Dar es salaam.


  0 0


  Taasisi  ya  RafikiElimu  FOUNDATION  kupitia  MRADI  WA  ELIMU  YA  UJASIRIAMALI  MIJINI  NA  VIJIJINJI  inatangaza  nafasi  za   MAFUNZO  YA  UTENGENEZAJI  WA  MASHINE  ZA  KUTOTOLEA  VIFARANGA  WA  KUKU.

  Mashine   zitakazo fundishwa  kutengeneza  ni  INCUBATOR   ( MANUAL & AUTOMATIC) ZENYE  UWEZO  WA  KUTUNZA  JOTO  KWA  SAA  48 PAMOJA  NA  KUTOTORESHA  MAYAI   KUANZIA  240  HADI  5000.
  Vile  vile  yatatolewa  mafunzo  ya   UTENGENEZAJI  WA  MAJIKO  SANIFU  NA  NISHATI  MBADALA.
  ADA   YA   MAFUNZO   :
  Ada  ya  mafunzo  haya  ni  SHILINGI  ELFU  ISHIRINI  NA  TANO  TU. (Tshs.25,000/=)
  TAREHE  YA  KUANZA  KWA  MAFUNZO
  Mafunzo  haya  yatafanyika  kwa  muda  wa  siku  tano  kuanzia  tarehe    01  SEPTEMBA  2014  hadi  tarehe  05 SEPTEMBA  2014
  FOMU   ZA   KUJIUNGA   NA   MAFUNZO :
  Fomu  za  kujiunga  na  mafunzo  haya  zinapatikana  ofisini  kwetu  kwa  gharama  ya  SHILINGI  ELFU  KUMI  NA  TANO  TU  ( Tshs.15,000/=).
  MWISHO  WA  KUCHUKUA  FOMU  :
  Mwisho  wa  kuchukua  fomu  ni  tarehe   28  AGOSTI 2014.
  Ofisi  zetu  zinapatikana  katika  eneo  la  CHANGANYIKENI  karibu  na  CHUO  CHA  TAKWIMU.
  JINSI   YA   KUFIKA   OFISINI   KWETU:
  Kufika  ofisini  kwetu, panda  daladala za  UBUNGO- CHANGANYIKENI  kisha  shuka  kituo  cha  TAKWIMU  halafu  tembea  hatua  ishirini  mbele  kisha  tazama  upande  wako  wa  kulia utaona  ofisi  imeandikwa   RAEFO  TANZANIA.
  Kwa  maelezo  zaidi wasiliana  nasi  kwa  simu 0784406508.
  Kwa  taarifa  zaidi  kuhusu  mafunzo  ya  utengenezaji  wa  mashine  za  kutotolea  vifaranga, tembelea :
  www.rafikielimu.blogspot.com

  0 0

  Mchekeshaji Mahiri kutoka nchini Uganda,Anne Kansiime (wa pili kulia) akifafanua jambo mbele ya Wanahabari kuhusiana na burudani kubwa ya uchekeshaji atakayoionyesha kwa mashabiki wake hapo kesho Agosti 2,2014  katika ukumbi wa Golden Tulip,jijini Dar,Kulia kwake ni mchekeshaji mwingine kutoka nchini Kenya,Fred Omondi.
   Mmoja wa wachekeshaji mahiri kutoka nchini Tanzania,atambulikae kwa jina la kisanii Mc Pili Pili akielezea jambo kwenye mkutano wa Wanahabari uliofanyika mapema leo jijini Dar,wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Radio 5, Robert Francis,ambao ndio waandaaji wa Onesho hilo la vichekesho.
   Baadhi ya Wanahabari walioshiriki mkutano huo wa wasanii wa vichekesho uliofanyika mapema leo jijini Dar

  ========  ======  ====== 

  Mchekeshaji Anne Kansiime anatarajiwa kutoa burudani kubwa siku ya Jumamosi kwa mashabiki wake katika ukumbi wa Golden Tulip.

  Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Sports Lounge, mkali huyo wa kuchekesha na sanaa za majukwaani amesema mashabiki wake watarajie mambo makubwa hapo Jumamosi.

  ‘Hii ni mara yangu ya kwanza kuja Tanzania, hivyo mashabiki wangu watarajie burudani ambayo itaacha mbavu zao hoi, lakini pia watapata nafasi ya kujifunza vitu vingi kupitia vichekesho vyangu’ alisema Anne.

  Kwa upande wake, mchekeshaji mwingine kutoka Kenya atayetoa burudani, Fred Omondi, amesema watanzania watarajie burudani kali kama lilivyo jina la burudani yenyewe, Cheka Kwa Nguvu.

  ‘Usiku wa Jumamosi utawakutanisha moja ya wachekeshaji mahiri barani Afrika, hivyo watanzania waje kwa wingi kushuhudia burudani hii’ alisema Fred.

  Naye mchekeshaji Pilipili kutoka Tanzania amesema usiku wa leo utakuwa usiku wa kukumbukwa hasa kwa vichekesho alivyowaandalia mashabiki wake.Usiku wa Cheka Kwa Nguvu unaandaliwa na kituo cha Radio 5 na pia utaambatana na burudani ya muziki kutoka ODAMA Band.

  Akizungumzia tukio hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Radio 5, Robert Francis amewataka wapenzi wa burudani ya vichekesho kuhudhuria kwa wingi ili wafurahie burudani waliyowaandalia.  ‘Usiku huo utakuwa ni maalumu kwa watanzania kufurahia Utanzania wao, kwani kucheka ni sehemu muhimu kwa maisha ya mwanadamu’ alisema Robert.

  Kansiime amejipatia umaarufu kupitia mitandao ya kijamiii ambako alianza kwa kuweka vipande vya video akiigiza kama mwanamke wa kiafrika anayekutana na changamoto mbalimbali za maisha.

  Mchekeshaji huyo wa kike, ambaye pia huendesha kipindi cha “Don’t Mess With Kansiime” kwenye kituo cha Citizen TV, anatajwa kuwa mwanamke mwenye kipaji cha pekee nchini Uganda na Afrika Mashariki kwa ujumla.

  0 0


  *Asema malumbano ya viongozi hayawasaidii wananchi

  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ametoa saa 30 na kutaka kupatiwa majibu ni kwa nini maelekezo aliyotoa kuhusu kiwanda cha kusindika nyama cha Mbeya hayajafanyiwa kazi.

  Ametoa kauli hiyo leo mchana (Ijumaa, Agosti Mosi, 2014) wakati akizindua Kongamano la siku tatu la Uwekezaji la Mikoa ya Iringa, Njombe na Mbeya la mwaka 2014 ambalo limeanza leo kwenye ukumbi wa Benjamini Mkapa jijini Mbeya.

  “Mbeya inaweza kuwa na fursa kubwa ya viwanda vya usindikaji nyama, unga wa mahindi ili kuongeza thamani ya mazao mnayozalisha katika mkoa wenu. Nilipokuwa hapa ziara yangu ya mwisho 2012, niliagiza kiwanda hiki kitafutiwe mwekezaji ili kianze uzalishaji. Jana nimeuliza kiwanda cha nyama kimefikia wapi, naambiwa watu bado wanaongea. Wanaongea nini?,” alihoji.

  “Mtu akija kusikia habari ya kiwanda hiki atatuona ni wajinga tena ni wajinga wa kujitakia, kisa watu bado wanazungumza… hiki kiwanda cha nyama ni cha Mbeya na manuafaa yake ni kwa ajili ya wana Mbeya. Hivi wahusika ni kwani hamuioni hiyo fursa?” alisema.

  “Dk. Mary Nagu watafute watu wa CHC waje hapa kujieleza ni kwa nini suala hili limechukua muda mrefu. Kabla sijaondoka hapa Mbeya kesho nataka nipate majibu kuhusu jambo hili,” aliagiza.

  Katika hotuba yake ya ufunguzi, Waziri Mkuu alisisitiza suala la watendaji wa mikoa na wilaya kuchukulia kwa umakini suala la uwekezaji kwani wasipofanya hivyo wao ndiyo watageuka kikwazo na kukwamisha maendeleo ya wananchi wanaowaongoza.

  “Ndugu zangu wa Serikali za mitaa msiwe vikwazo, kuwezi wawezeshaji. Ninyi si watawala bali ni waleta maendeleo kwa jamii. Natoa wito mshirikiane na wafanyabiashara kuharakisha maendeleo ya wananchi mliokabidhiwa kuwaongoza. Acheni kudai hongo, kwani badala ya kuwasadia jamii, mtajikuta ninyi ndo mnakuwa vikwazo vya maendeleo,” alionya.

  Alisema Serikali za Mitaa zinapaswa kuwa wawezeshaji na siyo wakwamishaji wa masuala ya maendeleo na ili kufanikisha hilo aliwataka wakuu wa mikoa waanzishe one-stop centre katika ngazi ya mkoa na Halmashauri ili wawekezaji wanapofika katika mikoa yao wasizungushwe na kukatishwa tamaa kwa sababu ya mlolongo wa taasisi zilizopo.

  “Uzoefu unaonyesha kuwa baada ya kufanya makongamano kama haya, wawekezaji wengi wanajitokeza lakini katika ngazi ya Mkoa na Halmashauri wanakosa mahali ambapo wanaweza kushughulikiwa na kupata huduma bora kwa pamoja “One Stop Centre”. Hali hiyo huwafanya wakate tamaa.”

  “Ninashauri kila Mkoa na kila Halmashauri iweke mfumo mzuri wa kuwapokea wawekezaji hususan kuwa na Mratibu (Focal Point) wa masuala ya uwekezaji ambaye ndiye atakuwa “One Stop Centre” wa kushughulikia wawekezaji wanaojitokeza na kuwahudumia kwa ufanisi bila urasimu. Ni imani yangu kuwa tukifanya hivyo, tutawezesha Kanda hii kuwa kitovu kikubwa cha uwekezaji katika nchi yetu,” aliongeza.

  Alisema kila mmoja hana budi kuendelea amani na utulivu wa nchi ili uwekezaji uweze kufanikiwa na kushamiri. “Hakuna uwekezaji endelevu na wenye tija katikati ya fujo na migogoro, na uwekezaji utashamiri pale tu penye amani na utulivu,” alisisitiza.
  Mapema, Waziri wa Nchi (OWM-Uwezeshaji na Uwekezaji), Dk. Mary Nagu alisema ili uwekezaji uweze kuwanufaisha wananchi, ni lazima rasilmali za nchi zigeuzwe kuwa bidhaa. “Ukiangalia chuma cha Liganga kipo pale miaka mingi, bila kukigeuza kuwa bidhaa, bado hakiwezi kuwanufaisha wananchi wetu,” alisema. Alisema bila uwekezaji hakuna uchumi, na bila uchumi hakuna maendeleo na bila maendeleo hakuna maisha bora kwa kila Mtanzania.

  Katika hatua nyingine, Wakuu wa mikoa ya Mbeya, Iringa na Njombe walipewa nafasi ya kuzungumza na washiriki wa kongamano hilo ikiwa ni pamoja na kuelezea fursa mahsusi zilizomo kwenye mikoa yao.

  Mada zitakazowasilisha katika kongamano hilo ambalo kaulimbiu yake ni “Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii katika Nyanda za Juu Kusini” zinahusu fursa za uwekezaji katika sekta za uchumi na miundombinu katika kanda hiyo, fursa za uwekezaji katika sekta za huduma za jamii katika kanda hiyo, fursa za uwekezaji katika kilimo cha mazao ya bustani (matunda, mboga, maua na viungo) na mchango wa taasisi za fedha katika uwekezaji.

  Nyingine ni mchango wa sekta binafsi katika uwekezaji, na nafasi ya MKURABITA katika kukuza mitaji ya uwekezaji.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  IJUMAA, AGOSTI MOSI, 2014

  0 0

    Mbunge wa jimbo la Ukonga Eugen Mwaiposa akimkabidhi kombe la ubingwa nahodha wa timu ya Ilala Academy Maisala Adam baada ya timu hiyo kuibuka mabingwa wa Airtel Rising Stars mkoa wa kisoka wa Ilala juzi.
   Mbunge wa jimbo la Ukonga Eugen Mwaiposa akimkabidhi kombe la ubingwa nahodha wa timu ya Temeke All Stars Maulid Jamal baada ya timu hiyo kuibuka mabingwa wa Airtel Rising Stars mkoa wa kisoka wa Temeke juzi.
   Mbunge wa jimbo la Ukonga Eugen Mwaiposa akimkabidhi kombe la ubingwa nahodha wa timu ya Kinondoni Academy Jafali Said baada ya timu hiyo kuibuka mabingwa wa Airtel Rising Stars mkoa wa kisoka wa Kinondoni juzi.


older | 1 | .... | 332 | 333 | (Page 334) | 335 | 336 | .... | 1897 | newer