Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

Swala ya Eid El Fitr kitaifa yaswaliwa kwenye viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar leo

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal (katikati),Sheikh Mkuu,Issa Shaaban Simba,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Sheikh Mussa Salum wakijumuika na Waumini wengine wa Dini ya Kiislam kwenye Swala ya Eid El Fitr iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja,Jijini Dar es Salaam leo.Picha zote na Othman Michuzi.
Sehemu ya Waumini wa Dini ya Kiislam wakiwa kwenye Ibada ya Eid el Fitr katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
 Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam,Sheikh Mussa Salum akitoa Khotuba katika Idada ya Swala ya Eid El Fitr iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja,Jijini Dar es Salaam leo.
 Mawaidha yakiendelea mara baada ya Swala ya Eid el Fitr.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal akitoa salamu za Eid el Fitr leo mara baada ya Swala iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja,Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Ulinzi,Dkt. Hussein Mwinyi (katikati) akijumuika pamoja na Waumini wenzake wa Kiislam katika Swala ya Eid El Fitr iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja,Jijini Dar es Salaam leo.


MPIGIE KURA MSHIRIKI UMPENDAYE TMT

MABONDIA WAPIMA UZITO KUPIGANA IDDI PILI MANYARA PARK

$
0
0
Bondia Peter Mbowe akioneshana umwamba wa kutunishiana misuli na Ibrahimu Tamba baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao yutakaofanyika katika ukumbi wa Manyara Park Tandale CCM siku ya Iddi pili.
Bondia Karim Ramadhani akipima uzito
Bondia Karim Ramadhani kushoto akitunishiana misuli na bondia Stevin Kobelo baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika siku ya iddi pili katika ukumbi wa Manyara Park manzese CCM wa pili kushoto ni bondia Nassibu Ramadhani na Kocha Jafari Ndame.
Mjumbe wa kamati ya utendaji wa chama cha ngumi za kulipwa nchini Ally Bakari ' Champion' akiwakumbusha mabondia na wasaidizi wao sheria mbalimbali za mchezo wa ngumi kabla ya mpambano wao.
 
Rais wa TPBO cHAUREMBO pALASA AKISISITIZA JAMBO
Bondia Peter Mbowe akioneshana umwamba wa kutunishiana misuli na Ibrahimu Tamba baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao yutakaofanyika katika ukumbi wa Manyara Park Tandale CCM siku ya Iddi pili picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

GLOBAL PUBLISHERS INAWATAKIA EID NJEMA

Rais Kikwete katika Swala ya Iddi jijini Dar es Salaaam leo

$
0
0
 Baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu wakiswali sala ya Iddi El Fitr katika masjid Maamur Upanga jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu muda mfupi baada ya kuswali sala ya Iddi El Fitr katika mshikiti wa Maamur Upanga jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
 "...Eid Mubarak....Eid Mubarak..."
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mlemavu mara baada ya kumalizika kwa swala ya Iddi katika masjid Maamur Upanga jijini Dar es Salaam leo asubuhi.

TAMASHA LA USIKU WA MATUMAINI 2014 WABUNGE SIMBA NA YANGA FULL KUKANYAGANA UWANJA WA TAIFA

$
0
0
Makala na Nassor GalluSIKU ya Agosti 8, mwaka huu kutakuwa na bonge la mechi litakalopigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar ambapo wabunge wanaoshabikia Yanga, watakuwa dimbani kupepetana na wenzao wa Simba.
Wabunge wa timu ya Simba wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Hebu jaribu kuvuta picha katika ubongo wako, waheshimiwa wabunge watakapoweka kando masuala ya ‘Ukawa’ na ‘Tanzania Kwanza’, kisha kukutana katika uwanja kuonyeshana umwamba kwa kusakata gozi la ng’ombe katika  mchezo huu wa kihistoria.

Kila timu tayari imeingia mafichoni kujiwinda na mchezo huo ili kuhakikisha inaibuka kidedea na kujenga heshima mbele ya watani wao huku Simba wakiahidi kulipiza kisago cha bao 1-0 walichokipata mwaka jana kutoka kwa Yanga. “Tayari tumeingia kambini kujiwinda na mchezo huu ili kuziba midomo na kelele za Yanga ambao wamekuwa wakitamba tangu watubahatishe mwaka jana,” alijinasibu Hamis Kigwangala ambaye ndiye nahodha wa Simba.

Kwa upande wa mlezi wa Yanga ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abassi Mtemvu, alijigamba kuwa ni lazima waendeleze moto wa ushindi kwa kuwa wapo na kikosi imara na tayari wameshaingia kambini kwa kuwa mchezo huu ni siriazi kwao.

“Kwa kweli mchezo huu tumeuchukulia kwa mtazamo wa juu kabisa na lazima tuwapige kwa kuwa tuna damu changa nyingi, hatuna masihara, maana wakitufunga hatutakaa bungeni. “Tupo katika maandalizi ya mwisho kwa sasa ingawa tulipoweka kambi yetu itabaki kuwa  siri,” alisema Mtemvu kwa kujiamini.

Baadhi ya wabunge wanaounda timu ya Yanga ni pamoja na Abassi Mtemvu, Ridhiwani Kikwete, Freeman Mbowe na  Mwigulu Nchemba, huku kikosi cha Simba kikiundwa na wakali kama Zitto Kabwe, Hamisi Kigwangalla, Wiliam Ngeleja, Juma Nkamia, Amos Makalla na Ismail Aden Rage. Mbali na mchezo huo ambao utakuwa kivutio kikubwa kwa wadau wa soka, pia kutakuwa na mchezo mwingine wa kusisimua pale Bongo Fleva chini ya mkali wao, Peter Manyika itakapopepetana na Bongo Movie FC chini ya Jacob Steven JB.

Mkurugenzi wa Ufundi wa Bongo Movie, Fatuma Makongoro ‘Bi Mwenda’, tayari ameanika wachezaji wake huku akisema kuwa hahofii kwani kikosi chake kipo kamiligado kuelekea mchezo huo ambao wameuchukulia kwa umakini mkubwa.
 *
“Sisi tumeuchukulia ‘serious’ sana mchezo huu kwa kuwa mashabiki wetu watakuja wengi na hatutakubali kuwaangusha.“Wachezaji waliopo kambini mpaka sasa ni Mzee Majuto, Kingwendu, Bambo, JB, Steve Nyerere, Dk Cheni, Ray, Mtitu, Cloud pamoja na Muhogo Mchungu,” alisema Bi Mwenda.
Wabunge wa timu ya Yanga wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Akijibu mapigo ya wapinzani wao, kocha wa Bongo Fleva ambaye pia anakinoa kikosi cha Yanga, Juma Pondamali ‘Mensah’, alisema Bongo Movie wajiandae kupata kipigo cha mshangao kwa kuwa wao hawatakwenda kuigiza uwanjani.
 
“Hawa waigizaji wajiandae na kipigo cha ‘sapraizi’, maana pale sisi hatuendi kuigiza, tunaenda kupiga kazi kwa kuwa mpira hauigizwi, unachezwa kila mmoja anaona, sasa acha wapige domo wataona kitakachowakuta,” alisema Pondamali. Baadhi ya mastaa wanaounda kikosi cha Bongo Fleva ni pamoja na Peter Manyika, H-Baba, Ali Kiba, Rich One, Kalapina na wengineo.

Ukiachana na soka, pia kutakuwa na burudani mbalimbali ambapo mastaa kibao kutoka ndani na nje ya nchi watakuwepo kulipamba jukwaa la Usiku wa Matumaini. Baadhi ya mastaa hao ni pamoja na Yemi Alade kutoka Nigeria, Madee, Ali Kiba, Roma Mkatoliki, Shilole, Menninah, Juma Nature na kundi zima la TMK Wanaume Halisi.

Mgeni rasmi katika tamasha hili atakuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Mohammed Gharib Bilal.Tamasha la Usiku wa Matumaini limedhaminiwa na Clouds FM (88.5),  Times Fm (100.5), Vodacom, Pepsi, Azam TV pamoja na Syscorp.
JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS

Diamond Platnumz arejea nchini na tuzo yake

$
0
0
 Diamond Platnumz  akionesha tuzo yake aliyoshinda kwa baadhi ya vyombo vya habari  na mashabiki waliofika kumlaki,mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere leo asubuhi (30.7.2014) kutokea Marekani ambako alishinda zawadi ya Mwanamuziki bora wa kiume wa Afrika Mashariki 2014.
 Mwanamuziki nyota wa miondoko ya Bongo Fleva Diamond Platnumz akiwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere leo asubuhi (30.7.2014) kutokea Marekani ambako alishinda zawadi ya Mwanamuziki bora wa kiume wa Afrika Mashariki 2014.Pichani akilakiwa na Mama yake Mzazi na baadhi ya washabiki na wapenzi wa muziki huo.
 Diamond Platnumz akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere leo asubuhi (30.7.2014) kutokea Marekani ambako alishinda zawadi ya Mwanamuziki bora wa kiume wa Afrika Mashariki 2014.


Mbeki, Mogae, Obasanjo to grace regional leadership forum in Dar

$
0
0
Obasanjo
Former Presidents Thabo Mbeki from South Africa, Olusegun Obasanjo of Nigeria and Festus Mogae of Botswana are set to arrive in Dar today to attend the African Leadership Forum to be held on July 31st, 2014.
The forum, which has been convened by H.E. Benjamin William Mkapa, former President of the United Republic of Tanzania and coordinated by UONGOZI Institute will be kick started with a plenary session with H.E. Thabo Mbeki as the keynote speaker. 
Mbeki
Mogae
The plenary will also feature a panel discussion including Mr. Carlos Lopes, Executive Secretary of the United Nations Economic Commission for Africa, Ms. Wendy Luhabe, founder of The Women Private Equity Fund of South Africa, and Mr. Omari Issa, CEO of the Presidential Delivery Bureau in Tanzania. 
According to a statement issued this week by UONGOZI Institute, the Forum, which will gather more than 150 participants from Tanzania and across Africa will discuss the challenges of meeting Africa’s transformation.
Mkapa

“The forum will provide a platform to reflect on the journey thus far, take stock of the challenges and opportunities and forecast prospects for Africa’s future,” said the statement.
The African Leadership Forum will bring together selected number of key influential leaders and thinkers across the continent, including former heads of state or government, as well as leaders from the business sector, government, civil society and academia.


ROSE MUHANDO KUIZINDUA ALBAMU YAKE YA KAMATA PINDO LA YESU DIAMOND JUBILEE JIJINI DAR

$
0
0
MWIMBAJI mahiri wa muziki wa Injili, Rose Muhando amelalamika kuwa albamu yake ya Kamata Pindo la Yesu Albamu anayotarajia kuizindua Jumapili wiki hii imeingizwa mtaani na wezi wa kazi za wasanii, hivyo kuonya wananchi wawe makini kwani albamu yake halisi itatoka Jumapili.
 
Taarifa kwa vyombo vya habari aliyoitoa Muhando jana, ilieleza kuwa albamu yake halisi bado haijaingia mtaani na kwamba hiyo wanayoiona wananchi sasa ni bandia na mtu atakayewauzia wamripoti polisi.
 
“Albamu ya Kamata Pindo la Yesu itaanza kuingia mtaani baada ya uzinduzi wangu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Jumapili wiki hii. Albamu yangu ina nembo ya TRA (Mamlaka ya Kodi ya Mapato nchini).
 
“Hizi CD zinazouzwa hivi sasa si zangu, hao ni matapeli na nawaomba wananchi tushirikiane kudhibiti wizi. Hao ni maharamia wa kazi za wasanii wanataka kunyonyajasho langu, naomba sana wananchi mnisaidie.“Nasisitiza albamu yangu sijaiachia sokoni bado mpaka uzinduzi ukamilike, Watanzania wenzangu na mashabiki wangu kote duniani mnielewe na naomba tusaidiane katika hili maana CD feki zimezagaa,” alisema Muhando na kuongez akuwa tayari ameripoti taarifa hiyo kwa vyombo vya dola.
 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions inayoratibu uzinduzi huo, Alex msama naye katika taarifa hiyo ya pamoja alionya wote watakaobanika kuwa CD za albamu ya Rose Muhando watakumbana na mkono wa sheria.
 
“Inasikitisha sana kuona baadhi ya watu wanataka kutumia jasho la wengine kujinufaisha. Watanzania kuweni macho, msubiri albamu yenyewe ya Rose Muhando Jumapili pale ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam,” alisema Msama.
 
Albamu hiyo ya Muhando itakayozinduliwa Jumapili ina nyimbo za Bwana Niongoze, Wewe Waweza, Usiniache, Nibariki, Muongo, Kwema, Kamata Pindo la Yesu na Facebook.
 
Hivi sasa Rose anatamba na albamu yake ya Utamu wa Yesu, ambapo pia amewahi kutamba na albamu za Uwe Macho, Nyota ya Ajabu (Zawadi ya Krismasi), Jipange Sawasawa, Kitimutimu, Mungu Anacheka na Wololo.

MWENGE WAWASILI ZANZIBAR KUTOKEA DAR ES SALAM NA KUKABIDHIWA MKUU WA MKOA WA MJINI MAGHARIBI.

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadiki akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi Khamis, makabidhiano hayo yamefanyika uwanja wa ndege mkongwe Kiembesamaki leo.
 Vijana wa Chipkizi wakiimba nyimbo ya Mwenge.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Ikulu na Utawala Bora Dkt. Mwinyihaji Makame akishika mwenge wa Uhuru ulipowasili Zanzibar.

 Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Hamza Ibrahim kutoka Mjini Magharibi na maaskari wakiukimbiza Mwenge.
  Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi Khamis akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Magharibi Hasan Mussa Takrima kwa ajili ya kuukimbiza katika Wilaya yake.
Mkuu wa Wilaya ya Magharibi Hasan Mussa Takrima akikimbiza Mwenge wa Uhuru mara baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini tayari kuanza ziara yake.(Picha na Makame Mshenga- Maelezo Zanzibar).
 Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Getrudi Mpaka akitoa salam za Mkoa huo kabla ya kuukabizi Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Mjini Magharibi leo july 30.

MEMBE ASEMA DINI NDIKO KWENYE CHIMBUKO LA AMANI NA UTULIVU, ACHANGIA KITABU CHA MUFTI

$
0
0
 
HABARI KATIKA PICHA KUHUSU BARAZA HILO LA EID
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Kamilius Membe, akizungumza jambo na Waziri Mkuu Mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim, huku waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye (kulia) akifuatilia mazungumzo hayo kwa pembeni, wakati wakiwa kwenye hafla ya Baraza la Idd El Fitr, leo, Julai 29, 2014, kwenye Viwanja vya Kariamjee, Jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi kwenye Baraza la Eid ElFitr, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akiingia kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, akisindikizwa na  Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Kassim.
 Pinda akimsalimia Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi baada ya kuwasili ukumbini
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimsalimia Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu, Shaaban Issa Simba baada ya kuwasili ukumbini.
 Pinda akimtazama kwa furaha wakati Mwinyi akizindua kitabu kwa furaha ambacho kimeandikwa na Sheikh Mkuu, Shaaba Issa Simba, kitabu hicho chenye jina la Al Muhtaswar ni makusanyo mbalimbali ambayo sheikh Mkuu huyo ameyakusanya na kisha kutengeneza kitambu kwa ajili ya kukisambaza nchini kote kusaidia waislam kuzingatia vyema dini hiyo. Pamoja na wadau kadhaa, Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe amechangia kuwezesha uchapishaji wa kitabu hicho.
 Mtoto  wa jijini Dar es Salaam, Arafat Msham akiduusu kitabu hicho
 Membe, Dk. Salim na Sumaye wakisoma kitabu cha Sheikh Mkuu Shaaban Issa Simba
Pinda akitoa hotuba yake kwenye Baraza hilo la Idd
 Kinamama kwenye Baraza hilo la Eid ElFitr
 Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (kulia) akiwa na Mama Shamim Khan kwenye Baraza hilo la Eid 
 Mwanazuoni akighani kaswida maalum kwenye Baraza hilo la Idd
Wanazuoni wakitumbuiza kaswida kwenye Baraza la Idd
 Ustaadhi Mroki Mroki wa Habari leo akifuatilia kwa makini shughuli za hafla hiyo ya Baraza la Eid
 Baadhi ya Wasanii maafurufu wa Bongo Movie akiwemo Steve Nyerere  nao walihudhuria Baraza hilo
Membe akiagana na wadau baada ya shughuli za Maulid. Picha zote na Bashir Nkoromo-theNkoromo Blog

Rais Kikwete atunukiwa Tuzo nyingine ya kimataifa, safari hii ni la kuwa Nyota wa Demokrasia Afrika

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 
Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete 

IPTL, Al-Madinah washerehekea sikukuu ya Eid na mayatima 500

$
0
0

Meneja rasilimali watu wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL Bw. Aidan Kaune (mwenye suti ya kijivu) akijumuika pamoja na baadhi ya watoto 500 mayatima kusherehekea sikukuu ya Eid wakati wa karamu ya chakula iliyoandaliwa na taasisi ya Al-Madina na kufadhiliwa na IPTL. Kulia ni meneja maswala ya kampuni ya IPTL (Company Affairs Manager) Bw. Kulwinder Singh Jheeta na wa tatu kulia ni Mkurugenzi wa taasisi ya Al-Madinah Sheikh Ally Mubarak. 
 Meneja rasilimali watu wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL Bw. Aidan Kaune (kulia) na Meneja maswakla ya kampuni wa IPTL (Company Affairs Manager) Bw. Kulwinder Singh Jheeta (katikati) wakikabidhi sehemu ya bidhaa zilizonunuliwa wakati wa karamu ya chakula kwa watoto yatima wapatao 500 kutoka vituo mbali mbali Dar es Salaam na Wilaya ya Kondoa, kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Eid al-Fitr. Kushoto ni Mkurugenzi wa taasisi ya Al-Madinah Sheikh Ally Mubarak, ambao waliandaa karamu hiyo baada ya kufadhiliwa na IPTL. 
 Meneja rasilimali watu wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL Bw. Aidan Kaune (mwenye suti ya kijivu) akijumuika pamoja na baadhi ya watoto 500 mayatima kusherehekea sikukuu ya Eid wakati wa karamu ya chakula iliyoandaliwa na taasisi ya Al-Madina na kufadhiliwa na IPTL. Kulia ni meneja maswala ya kampuni ya IPTL (Company Affairs Manager) Bw. Kulwinder Singh Jheeta.
Meneja maswala ya kampuni ya kufua umeme ya IPTL (Company Affairs Manager) Bw. Kulwinder Singh Jheeta akijumuika pamoja na baadhi ya watoto 500 mayatima kutoka vituo mbalimbali Dar es Salaam na Wilaya ya Kondoa kusherehekea sikukuu ya Eid wakati wa karamu ya chakula iliyoandaliwa na taasisi ya Al-Madina na kufadhiliwa na IPTL.

ZAIDI ya watoto 500 wasio katika mazingira magumu na mayatima jijini Dar es Salaam na Wilayani Kondoa wameungana na waislam wengine duniani siku ya Jumanne kusheherekea sikukuu ya Eid, sikukuu inayoashiria kuisha kwa mwezi wa mfungo wa Ramadhani.

Watoto hao kutoka katika vituo mbali mbali vya watoto yatima, walipata fursa ya kula na kufurahia pamoja na wengine wakati wa karamu ya chakula cha watoto yatima ililoandaliwa na taasisi ya Ai-Madinah Social Service Trust na kudhaminiwa na kampuni ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL).

Bw. Aidan Kaude, Meneja Rasilimali Watu wa IPTL aliejumuika na watoto hao jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe hizo alisema kampuni yake imeona haja ya kuisaidia Al-Madinah katika kuhakikisha kuwa watoto hao wanaohitaji msaada pia wanapata haki ya kusheherekea wakati huu muhimu katika maisha ya waislam wote dunia mzima.

"Tulipopata maombi toka Al-Madinah ili kusaidia kufanikisa karamu hii, Mwenyekiti wetu mtendaji Bw. Harbinder Singh Sethi aliidhinisha haraka ombi hilo na kusema kuwa ni jambo la kheri sababu watoto hao walengwa ni mayatima na wanahitaji msaada toka kwa kila mtu ili waweze kuishi maisha ya kawaida kama wengine wanavyoishi licha ya kupoteza wazazi wao," alisema.

Mkurugenzi wa Al-Madinah Social Service Trust, Sheikh Ally Mubarakí aliyeandaa tukio hilo alisema kuwa baada ya kufanyakazi karibu na kwa muda mrefu na makundi mengi na taasisi mbali mbali za kiislam, taasisi yake imegundua kuwa mayatima wengi wanakumbwa na changamoto nyingi ambazo ni pamoja na ukosefu wa mahitaji ya msingi kama vile chakula, mavazi na malazi. 

Alisema taasisi yake iliomba msaada wa kifedha toka IPTL ili nao kuwapatia msaada wale watoto wenye maisha magumu, nafasi ya kusheherekea na waislam wenzao. Waislam walianza kusheherekea sikukuu ya Eid Jumatatu kwa dhehebu la Sunni na Jumanne kwa wengine, baada ya mwezi kuonekana na kuonesha mwanzo wa Shawwal, mwezi wa kumi wa Kalenda ya mwezi wa kiislama. 

Kuonyesha mwanzo wa Eid na kutoa Sunnah, kwa kuyafanya yake yaliyoganya na Mtume Muhammad, waislam wengi waliamka mapema kusali sala ya Asubuhi ya Sarat ul-Falr. 

Waslam wanasheherekea sikukuu kwa kukusanyika pamoja na marafiki na familia, na kuandaa vyakula vizuri , nguo nzuri kupeana zawadi na kupamba nyumba zao. Salaam ya kawaida wakati wa sikukuu hii ya Eid Madhubuti ya "Eid Mubarak" ikimaanisha "uwe na Eid iliyo na upendo."

UDA yatoa msaada wa shilingi milioni 15 kwa kanisa la Mt. Rita

$
0
0
   Mkurugenzi Mtendaji wa Shirila la Usafiri (UDA) Bw. Simon Bulenganija (kushoto) akisisitiza jambo kwa Paroko Msaidizi wa Kigango cha Kanisa la Mavurunza, Padri Xavery Kassase kabla ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 15 kwa Kigango cha Kanisa la Mtakatifu Rita kusaidia mradi wa ujenzi wa nyumba ya mapadri wakati wa harambee iliyofanyika kanisani hapo hivi karibuni.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirila la Usafiri (UDA) Bw. Simon Bulenganija (kushoto) akikabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni 15 kwa Paroko Msaidizi wa Kigango cha kanisa la Mavurunza, Padri Xavery Kassase (kulia) kusaidia mradi wa ujenzi wa nyumba ya mapadri wakati wa harambee iliyofanyika katika Kigango cha Kanisa la Mtakatifu Rita hivi karibuni
Paroko Msaidizi wa Kigango cha Kanisa la Mavurunza, Padri Xavery Kassase(kulia) akionyesha hundi ya shilingi milioni 15 zilizotolewa na  Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) kwa kigango cha Kanisa la Mtakatifu Rita jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Mchango huo wa kampuni ulitolewa kusaidia ujenzi wa nyumba ya mapadri kanisani hapo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirila la Usafiri (UDA) Bw. Simon Bulenganija.

MAENDELEO ya kijamii na kiuchumi yataweza kupatikana endapo tu kila mtu ataweza kutoa mchango wake kuwasaidia wale wanaohitaji msaada ili kubadilisha maisha yao na kuwa wachangiaji wakubwa katika ukuaji wa uchumi wa taifa. Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), Bw. Simon Bulenganija wakati wa harambee ya kusaidia ujenzi wa nyumba ya mapadri katika Kigango cha kanisa la Mtakatifu Rita lililopo Kimara jijini Dar es Salaam, ambapo UDA ilichangia shilingi milioni 15.

“Watanzania wasisubiri mpaka makampuni makubwa yajitokeze na kutusaidia kubadilisha hali zetu za kiuchumi na mfumo wetu wa maisha. Mabadiliko yataweza kufikiwa tu endapo kila mmoja wetu ataweza kuchangia kwa nafasi yake kikamilifu. Makampuni yote makubwa na madogo na watu binafsi wenye uwezo wa kusaidia, wawashike mkono wale wanaohitaji msaada ili tuweze kuendelea pamoja,” alisema. Bw. Simon Bulenganija alisema kuwa kampuni yake imekuwa ikijihusisha na shughuli mbali mbali za kijamii ikiwa ni jitihada madhubuti zinazolenga katika upatikanaji wa maendeleo miongoni mwa watanzania wote.

Alisema kuwa shilingi milioni 15 zilizotolewa na UDA zitasaidia kwa kiasi kikubwa kupiga jeki maendeleo ya kanisa hilo hususani katika ujenzi wa nyumba ya mapadri na baadae kuendelea na mradi wa ujenzi wa kanisa jipya.“Japokuwa bado kampuni yetu ni kampuni changa ya kitanzania, tumeunda programu yetu ya shughuli za kijamii katika namna ya kwamba shughuli tunazojihusisha nazo, zitasaidia katika kutekeleza ajenda yetu yenye kaulimbiu “ukuaji wa kampuni yetu uwe sambamba na ukuaji wa kiuchumi wa jamii yetu”. Hii pia ni njia pekee ya kurudisha sehemu ya pato letu kwa jamii,” alisema Bw. Bulenganija.

Naye, Bw. Frederick Msumali, Mwenyekiti wa Kigango cha Mtakatifu Rita, aliipongeza kampuni hiyo kwa mchango wake na ushiriki wa Mkurugenzi wa UDA wakati wa shughuli hiyo ya harambee ambayo iliwezesha kanisa hilo kukusanya zaidi ya shilingi milioni 60 zitakazotumika katika mradi huo.

“Tungependa kwa kiasi kikubwa kutoa shukrani zetu kwa mchango uliotolewa na UDA.  Msaada huu kwa kiasi kikubwa utasaidia kupiga jeki mradi wetu wa ujenzi wa nyumba ya mapadri na baadae kuendelea na ujenzi wa kanisa jipya utakaofanyika karibu na kanisa hili la sasa. “Lakini pia, tunaishukuru UDA kama kampuni na Bw. Bulenganija mwenyewe kwa kuwa mgeni wetu rasmi. Mfano huu unahitaji kuigwa na makampuni mengine nchini,” alisema Bw. Msumali.

HOYCE TEMU AHAMASISHA WATANZANIA KUMPIGIA KURA MISS TANZANIA USA 2014 KWENYE KINYANG'ANYIRO CHA MISS AFRICA USA

$
0
0
IMG-20140727-WA0011
Pichani ni Miss Tanzania USA 2014, Joy Kalemera katika pozi kabla ya mahojiano na Mtangazaji wa kipindi cha "Mimi na Tanzania" Hoyce Temu nchin Marekani.

Mpigie Kura Miss Tanzania USA, Joy Kalemera anayeshiriki kinyang'ayiro cha kumtafuta Miss Africa USA. Mtangazaji wa Mimi Na Tanzania Hoyce Temu ambaye pia ni Miss Tanzania 1999 yupo nchini Marekani na amefanya mahojiano na mrembo huyo.

Usikose kuangalia marudio ya mahojiano hayo kwenye kipindi cha "Mimi na Tanzania" Jumamosi ya tarehe 2 August ,2014 Saa saba mchana katika kituo cha Televisheni cha Channel Ten.
IMG-20140727-WA0013
Miss Tanzania 1999 ambaye pia ni Mtangazaji wa kipindi cha "Mimi na Tanzania" Hoyce Temu akipata ukodak na Miss Tanzania USA, Joy Kelemera baada ya mahojiano maalum nchini Marekani.
Joy Kelemera
Namna ya kushiriki kumpigia kura moja kwa moja kwenye profile yake Bonyeza hapa utakuwa umeingia kwenye profile ya Joy Kalemera na bonyeza kitufe chenye alama ya mkono (sehemu iliyozungushiwa duara na wino mweusi) na moja kwa moja utakuwa umempigia kura Mtanzania mwenzetu anayeiwakilisha vyema nchini yetu kwenye kinyan'ganyito hicho.
NOTE: Unaweza kupiga kura mara nyingi uwezavyo kila baada ya dakika mbili kwa kubofya sehemu ile ile. Let us all wish her all the best! Ushindi wake ni wa Nchi! Piga Kura Sasa!
IMG-20140727-WA0014
Pichani ni Hoyce Temu, Joy Kalemera na camera crew/IskaJojo studios (katikati) aliyefanikisha kukerokodi maojiano hayo.
IMG-20140727-WA0015
Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu na Miss Tanzania USA 2014, Joy Kalemera katika pozi za madaha.

NGUMI ZILIVYOPIGWA MANZESE SIKU YA IDDI PILI

$
0
0


Kocha mkongwe wa mchezo wa masumbwi nchini Habibu Kinyogoli 'Masta' kulia akimvisha mkanda wa ubingwa bondia ramadhani Kumbele baada ya kumdunda Julius Kisalawe kwa point kushoto ni Refarii Ally Bakari.
Bondia Sadick Nuru kushoto akioneshana umwamba na Baraka Mchonge wakati wa mpambano wao ulifanyika Mazese Dar es salaam wakati wa sikukuu ya iddi pili Nuru alishinda kwa point mpambano huo .
Bondia Stevin Kobelo kushoto akirusha ngumi kumpiga Karim Ramadhani wakati wa mpambano wao uliofanyika siku ya iddi pili katika ukumbi wa Manyara park manzese Dar es salaam mpambano huo walitoka droo ya kufungana point.
Mabondia Joseph Gili kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Ibrahimu Tamba wakati wa mpambano wao uliofanyika siku ya Iddi pili katika ukumbi wa manyara park manzese Dar es salaam Tamba aklishinda kwa T.K.O  ya raundi ya nne.
Bondia Julius Kisalawe kushoto akipambana na Ramadhani Kumbele wajkati wa mpambano wao wa ubingwa wa TPBC uliofanyika siku ya Iddi pili katika ukumbi wa Manyara Park Manzese Dar es salaam Kumbele alishinda kwa point na kufanikiwa kuchukua ubingwa picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com.

TAMASHA LA MATUMAINI 2014, MASTAA WAELEZA WATAKAVYOKAMUA TAIFA

$
0
0
Stori: Centre Spread
ITAKUWA balaa! Siku chache kuelekea kwenye Tamasha la Matumaini, Agosti 8, mwaka huu, mastaa kibao watakaolipamba jukwaa litakalofungwa ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar, wameeleza jinsi gani
Diva wa muziki kutoka pande za Nigeria, Yemi Alade.
Yemi Alade
Diva wa muziki kutoka pande za Nigeria ambaye huwa habahatishi, amesema: “Nitawapagawisha mashabiki kwa kupiga nyimbo zangu zote kali ikiwemo iliyojizolea umaarufu kila kona ya Afrika, Johhny. Mashabiki wategemee kumuona Yemi akimaliza. Kati ya nyimbo ambazo nitazipiga ni Tangerine, Johnny, Bamboo, Birthday, Ghen Ghen Love na nyingine kibao.”
Mzee wa Dushelele, The Single Boy, Ali kiba akipozi.
Ali Kiba
“Kwa mara ya kwanza, nitapanda jukwaa la Uwanja wa Taifa kuweka historia mpya. Mashabiki wengi ‘wamenimiss’, Agosti 8 itakuwa maalum kwa ajili yao. Wategemee ngoma kali kibao kutoka kwa mfalme wa Bongo Fleva niliyerudi kupangusa kiti changu na kukikalia,
“Nitagonga kali kama Dushelele, Single Boy, Run Dunia na mpya zinazobamba kwa sasa ambazo ni Mwana na Kimasomaso.”
 
Malkia wa 'Chuna Buzi', Shilole.
Shilole
“Mashabiki wategemee kuona shoo ya nguvu, hakuna anayebisha kwamba najua kuimba na kukitumia vyema kiuno changu. Nitazipiga Chuna Buzi, Paka la Baa, Nakomaa na Jiji, Lawama na hii mpya ya Namchukuwa.”watakavyolishambulia jukwaa.
Mkali wa Hip Hop Bongo, R.O.M.A mkatoliki ndani ya ofisi za Global.
R.O.M.A
“Huwa sibahatishi katika shoo zangu, nitawainua mashabiki kwa kunyoosha kidole cha mwisho juu kwa kupiga ngoma kali kibao kama Tanzania, Mechi za Ugenini, Pastor, Mr. President pamoja na hii mpya ya Karibu Kwenye Karamu (KKK).
Navy Kenzo.
Navy Kenzo
“Tutawapagawisha mashabiki kwa staili ya Bokodo iliyotokea kujizolea umaarufu mkubwa. Ngoma kama Cheza Kizembe, Usinibwage, Chelewa (Bokodo) na hii mpya ya Aiyola ndizo zitakazosisimua zaidi siku hiyo.”
Mkali wa Bongo Fleva, Juma Nature akipozi.
Juma Nature
“Huwa ushindi kwetu ni lazima, tutakamua Tatu Bila, Fitina, Nyama pamoja na ngoma mpya niliyomshirikisha Lady Jay Dee, Kama Jana.”
Scorpion Girls, Isabela Mpanda(kushoto) na Jini Kabula wakipozi.
Scorpion Girls
“Sisi huwa hatubahatishi, unapomuona sehemu Isabela na Jini Kabula ujue timu nzima ya Scorpion Girls imetimia. Tutacheza na kuwaimbia nyimbo zetu kama Tanzania, Watuache na nyingine kibao.”
Mzee wa Tema Mate Tuwachape, Madee ndani ya ofisi za Global.
Madee
“Pale taifa nitakwenda kudhihirisha urais wangu wa Manzese, nitazipiga zote kali ikiwemo Pombe Yangu, Tema Mate Tuwachape na hii mpya ya Ni Shidaa, noma saaana!”
'La Diva', Meninah zao la Bongo Star Search akipozi.
Meninah
“Nitawapagawisha kwa ngoma zangu kali kama Dream Tonight, Kacopy Kapaste na mpya ya sasa ambayo ni Pipi ya Kijiti. Tukutane pale taifa, Agosti 8 mwaka huu.”

Waziri wa mambo ya ndani Mh. Mathias Chikawe kuwa mgeni rasmi katika kongamano la Usalama wa mitandao (Cyber Defence East Africa 2014).

$
0
0




 Waziri wa Mambo ya Ndani, Mh Mathias Chikawe atakuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa kangamano la usalama wa mitandao (Cyber Defense East Africa 2014) tar 16-19 Septemba.

Wadau mbalimbali wa sekta ya ulinzi na usalama wa mitandao wakiwemo wanasheria, wakaguzi wa kifedha na wale wa mitandao, wataalamu wa utunzaji mifumo ya kopyuta na mitando yake, wakuu wa vitengo vya TEHAMA wanatarajiwa kuhudhuria kongamano hilo. 

Mkutano wa ulinzi na usalama wa mitandao hufanyika kila mwaka hapa Tanzania na kuwavutia wadau wa ndani nan je ya nchi kwa ujumla. Mwaka huu wataalumu kutoka nchi za ulaya waliobobea katika masuala ya “digital forensic, cyber security, governance and cyber laws” watakuwepo. Watakuwepo pia jeshi la polisi kitengo cha uhalifu wa mitandao (Cyber-crime unit), TCRA and Legal Sector Reform”
Nafasi ni chache. 

Kujisajili Tuma barua pepe kwenda registration@nrd.no  or piga simu namba +255719253037
Nyote Mnakaribishwa

Alikiba new songs and profile

USIKU WA MNYAMA NA WANYAMA WATIKISA DAR LIVE SIKUKUU YA IDD PILI

$
0
0
Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Khalid Mohammed 'TID Mnyama' akizikonga nyoyo za mashabiki wa Dar Live katika Usiku wa Mnyama na Wanyama.
Mnyama TID akijiachia kwa mashabiki wake wa Dar Live.
Mwanamuziki Jafarai akipagawisha mashabiki waliofurika katika Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live.
Jay Moe akifanya makamuzi katika steji ya kupanda na kushuka ya Dar Live.
Inspector Haroun akiwapa hi mashabiki wake ndani ya Dar Live.
 
Mwanadada Naaziz kutoka Kenya akilishambulia jukwaa la Dar Live.
Masai Sharo akifanya vitu vyake stejini.
Mashabiki wakijiachia kijanja ndani ya Dar Live.
TID akitunzwa Cheni na shabiki wake.
TID akifanya manjonjo yake mbele ya Naaziz.
Nyomi ikifuatilia burudani za Idd Pili ndani ya Dar Live.
(PICHA NA RICHARD BUKOS NA GABRIEL NG'OSHA / GPL)
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>